Sophia Mwakagenda atwaa tuzo kimataifa

SOPHIA Mwakagenda, mbunge wa viti maalumu (CHADEMA) – wa kwanza kushoto pichani – ametwaa tuzo ya heshima ya mwanamke bora katika muongo mmoja wa kusaidia jamii.

Sophia amekabidhiwa tuzo hiyo katika mkutano wa kimataifa ujulikanao kama Women Economic Forum uliokuwa unafanyika mjini New Delhi, India kati ya tarehe 26 Aprili na 1 Mei mwaka huu.

Akiwa pekee aliyeshinda tuzo hiyo miongoni mwa akina mama wa Afrika Mashariki na Kati, Sophia ametunukiwa heshima hiyo kutokana na harakati alizofanya kwa miaka mingi katika kusaidia wanawake na watoto waishio mazingira magumu nchini Tanzania hata kabla hajawa mbunge.

Kwa mujibu wa taarifa ya jana Jumatatu kutoka New Delhi, iliyosainiwa na Idan Jushua, ofisa ambaye hakujitambulisha cheo chake, miongoni mwa kazi alizofanya Sophia ni pamoja na kuanzisha au kufadhili vituo maalumu vya ujasiriamali kwa wanawake katika mikoa ya Mbeya , Arusha, na Dar es Salaam.

Vile vile, Sophia amesaidia wasichana walio katika mazingira magumu ili wapate elimu bora.

Like
6

Leave a Comment

Your email address will not be published.