Askofu Malasusa kukimbia nchi kama Jerry Mngwamba?

Na Mwandishi wetu

KUTENGWA kwa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kumeleta fukuto na mjadala mkali ndani ya dayosisi hiyo juu ya hatima ya askofu huyo.

Baadhi ya wachungaji wa DMP wanasema kuna uwezekano mkubwa Askofu Malasusa akakimbia nchi kama ilivyotokea kwa Askofu Jerry Mngwamba wa kanisa hilo miaka kadhaa iliyopita.

Machi 27, 2002 kanisa hilo lilimvua Mngwamba uaskofu baada ya kuwa ametuhumiwa wizi wa Sh. 64 milioni za mfanyabiashara ya magari jijini Dar es Salaam. Naye alikuwa askofu wa DMP. Baada ya kuvuliwa uaskofu, alikimbilia Marekani ambako ilijulikana baadaye kuwa alikuwa anafanya kazi ya udereva wa teksi katika jiji la Chicago.

Kwa sakata la sasa kuhusu Askofu Malasusa, wachungaji wanadai kuwa mwenyewe amejiweka pabaya kwa kutengwa na kanisa baada ya Baraza Kuu la maaskofu wa KKKT kumtenga kwa usaliti, na kumfanya aonekane kikwazo cha imani kwa waamini wake.

Mbali na usaliti, huko nyuma amekuwa anaandamwa na tuhuma za uhusiano wa kimapenzi na Leita Ngoy, mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo, ambaye siku chache zijazo anatarajiwa kwenda Ujerumani kusoma shahada ya uzamivu, huko Bochum. Taarifa zinasema Malasusa aliipitisha skolarshipu ya Ngoy kimya kimya na kumtafutia mfadhili wa shirika la UEM. Mara zote Askofu Malasusa amekuwa anakanusha tuhuma hizi.

Taarifa zinasema baadhi ya wachungaji wake wamefurahishwa na adhabu aliyopewa “bosi” wao, kwani tangu Machi 24 2018 hawakufurahishwa na malekezo aliyowapa kutosoma waraka wa maaskofu katika sharika zao.

Kwao, kitendo cha Askofu Malasusa kukiuka makubaliano ya wenzake 25, ni utovu wa nidhamu na kinyume cha kanuni za kichungaji.

Wanasema kwa kuwa imebainika kuwa maelekezo yake ni matokeo ya “urafiki unaotia shaka” kati yake na serikali, wao wanautazama kama uchochezi mkubwa wa fikra na kiimani dhidi ya waamini wao.

Bila kufafanua zaidi, wanasema kutengwa kwa Askofu Malasusa kuna athari mbaya kwa dayosisi kwani hadi sasa inakabiliwa na madeni makubwa.

“Shule zinazosimamiwa na dayosisi – sekondari na chuo kikuu – zipo hoi. Mashirika ya umma, hasa NSSF na NHIF, yanadai dayosisi yetu pesa nyingi. Mradi pekee ulio salama ni benki,” anasema mchungaji mmoja, kwa sharti la kutotajwa jina.

Wasiwasi wa wachungaji ni kwamba kutengwa huku kwa Askofu Malasusa kutasababisha hata marafiki wa dayosisi kurudi nyuma.

Jitihada za kupata Askofu Malasusa ili azungumzie masuala haya hazikufanikiwa.

Like
31
8 Comments
  1. Mtanzania 6 years ago
    Reply

    Askofu huyo anatia mashaka. Kama kweli alithubutu kukaa na Bashite kama partner kuhadili masuala ya nyaraka. Kuna kitu kimefichika hapo!. Lakini lazima tukumbuke kuwa kama Askofu ana mambo yake ya siri mabaya( kuwa na wapenzi nje ya ndoa). Tunavyojua serikali hii ya kibashitebashite, ilimu- blackmail kifichua matendo yake hadharani. Ndiyo maana hakusoma nyaraka.

    1

    0
  2. Kirusi Dumetu 6 years ago
    Reply

    Comment*
    Wachungaji wa kondoo hawamheshimu Mungu wala kumtii ila ni wanyenyekevu na wasikivu wa mamlaka za kibinadamu.

    0

    0
  3. Kakakuona 6 years ago
    Reply

    Andoke kama wanafiki wengine

    0

    0
  4. Mkerereketwa 6 years ago
    Reply

    Nanukuu “Shule zinazosimamiwa na dayosisi – sekondari na chuo kikuu – zipo hoi. Mashirika ya umma, hasa NSSF na NHIF, yanadai dayosisi yetu pesa nyingi. Mradi pekee ulio salama ni benki,” . Mimi ni MKKKT wa DMP. Nimekuwa najiuliza 42% ya sadaka ya kila wiki kwa kila kanisa katika dayosisi inaishia wapi? Na wanakaa kutuwekeana bahasha ya ELIMU na kila MKKKT mwenye bahasha anatakiwa kuchangia 30000/= kwa mwaka 2018 kutoka 15000/= kwa mwaka 2017.Kwa maendeleo gani ya shule zetu na bado zinafanya vibaya na zimechoka mpaka majengo. Catholic hawana huu upuuzi na shule zao ndo zinazoongoza miaka yote. Kumekuwa na tetesi za ubadhirifu wa pesa za dayosisi kwa muda mrefu tena chini ya Askofu Malasusa.Tuangalie tunakosea wapi?

    1

    1
  5. Siji Haji 6 years ago
    Reply

    Napo ni lazima kuna kitu kimejificha hasa kuhusu utakatifu wa huyo Askofu wa DMP.

    0

    0
  6. Karlmarx 6 years ago
    Reply

    Askofu huyu aliyepata kuwa mkuu wa KKT amejivunjia heshima na hadhi si kwake bali na kwa kanisa. Ameamua kumtumikia mwanadamu badala YA Mungu

    0

    0
  7. May Mosi 6 years ago
    Reply

    Viongozi wa dini kama hawa hukumu yao ni kutengwa hadi pale watakapotubu na kufanya kazi kama watumishi wa Mungu.

    0

    0
  8. Ngano Ngano 6 years ago
    Reply

    Jambo la Busara ni Kwa Yeye Aksofu Malasusa Kutii Agiza la Baraza la Ma-Askofu wa KKKT. Yaaani aombe Msamaha kwa Wakristo na Wachugaji wa Dayosisi yake na Kuutambua Waraka wa Ma-Askofu na Kuruhu Usomwe Katika Dayosisi yake.

    Kama Binadamu yoyote yule Anaweza akaghafilika. Mbaya ni Kama hatakubali Kushuka Kunyeyekea na Kutubu.

    After all, Kutubu-Kuomba Msamaha ni Inshara Mojawapo Kubwa saana kwamba Mtu anamjua MUNGU.

    Biblia Takatifu inatufundisha Kuwa Afichaye Zambi Zake Hatafanikiwa Bali Yeye Aziungamaye Atapata Rehema.

    0

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.