Kesi ya Mbowe: Shahidi muhimu Urio asema ‘lengo lilishatimia’

Kama ilivyoletwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 26 Januari 2022.

Jaji kaingia mahakamani. Kesi inatajwa.

Wakili wa serikali: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili Wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na wakili

Pius Hilla

Abdallah Chavula

Jenitreza Kitali

Nassoro Katuga

Esther Martin

Tulimanywa Majige

Ignasi Mwinuka

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

Nashon Nkungu

John Mallya 

Dickson Matata

Maria Mushi

Khadija Aron

Seleman Matauka

Idd Msawanga

Michael Lugina

Jaji: Anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea

Jaji: Anakuwa Shahidi namba Ngapi

Wakili wa Serikali Robert Kidando Anakuwa Shahidi namba 12

Shahidi anakwenda kuitwa

Shahidi anaingia Mahakamani, Mrefu Mwembamba, Mweupe Kidogo

Jaji: Majina yako

Shahidi: Naitwa Luteni Denis Urio

Jaji: Umri

Shahidi: Miaka 42

Jaji: Kabila

Shahidi: Mchaga

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Jaji: Kazi yako

Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi Tanzania

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama, kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu, Mungu Nisaidie

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili Abdallah Chavula

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anasimama na Kwenda Kwa Shahidi

Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuwa nakuuliza Maswali, Ukijibu utakuwa unamjibu Mheshimiwa Jaji, Naomba Uongee kwa Sauti Ya Juu

Shahidi: Sawa

Wakili wa Serikali: Tukumbushe Majina yako

Shahidi: Naitwa Luteni Denis Leo Urio

Wakili wa Serikali: Mkazi wa Wapi

Shahidi: Mkazi wa Ngerengere Morogoro

Shahidi: Unafanya Shughuli gani

Shahidi: Ni Mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania

Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi ni wapi

Shahidi: Ni Ngerengere Morogoro

Wakili wa Serikali: Kituo Chako Kinafahamika kwa Jina gani

Shahidi: 92 KJ Ngerengere

Wakili wa Serikali: Cheo Chako ni Kipi

Shahidi: Luteni wa Jeshi

Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni Yapi

Shahidi: Ni Platoon Commander

Kuongoza Askari Walio Chini yangu

Wakili wa Serikali: Unaongoza Askari Wangapi

Shahidi: Afisa Mmoja na Askari 30

Wakili wa Serikali: Ni Askari gani wanayofanya kazi Katika Kikosi cha KJ 92

Shahidi: Ni Wanajeshi Waliopata Mafunzo Maalum, Komando

Wakili wa Serikali: tuambie Wewe Umetumikia Jeshi Kwa Miaka Mingapi

Shahidi: Miaka 18

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania Mwaka gani

Shahidi: Tarehe 16,June 2003

Wakili wa Serikali: Jeshi la Wananchi Tanzania lina Majukumu yepi

Shahidi: Lina Majukumu ya Ulinzi wa Mipaka dhidi ya Uvamizi Wa Ndani na Nje

Wakili wa Serikali: Jukumu lingine ni lipi

Shahidi: Kwenye Operation ya Ulinzi Wa Amani Kwenye Mataifa yenye Mgogoro

Wakili wa Serikali: Umesema Wewe ni Luteni wa Jeshi, Je Umekuwa Kwenye Nafasi hiyo kwa Miaka Mingapi

Shahidi: Kwa Miaka 6

Wakili wa Serikali: Umeeleza Mahakama Kwamba Miongoni Mwa Majukumu ya Jeshi ni Kuleta Amani Kwenye Mataifa Mengine, Ushiriki wako ni Vipi

Shahidi: Nimeshirriki Kulinda Amani 2011 Nchini Sudani, Na 2019 ni Sudan hiyo hiyo Jimbo la Darfur

Wakili wa Serikali: Tueleze Mahakama Kule Darfur ulipo enda Majukumu yako yalikuwa yepi

Shahidi: Kuhakikisha Wale Staff Officer (Wapatanishi) Ku Ensure Usalama wao Kwa Sababu Wao ni Unarmed Personnel

Wakili wa serikali: Kuna Mtu anafahamika Kwa Jina la Khalfani Bwire Unamfahamu Vipi

Shahidi: Nina Mfahamu Kwa Muda Mrefu, Nili Mtrain, Nikifanya naye Kazi Kituo Kimoja cha 92 KJ

Wakili wa Serikali: Umemfahamu Kuanzia Mwaka gani

Shahidi: Kuanzia 2006 Mpaka 2009

Wakili wa Serikali: Wakati Unamfahamu, yeye alikuwa ana Jukumu gani

Shahidi: alikuwa Kiongozi Mdogo, anaongoza,Ni Section Commander, alikuwa anaongoza Watu 9

Wakili wa Serikali: Cheo Chake Kilikuwa ni Kipi

Shahidi: Rank ya koplo

Wakili wa Serikali: Unaposema Ulifahamiana naye kuanzia 2006 Mpaka 2009 umamaam gani

Wakili wa Serikali: Unaposema Ulifahamiana naye kuanzia 2006 Mpaka 2019 umamaam gani

Shahidi: Ukomo wake Ulikuwa Mwaka 2019

Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mpaka I kafika Ukomo wake

Shahidi: alifukuzwa Kazi Jeshini

Wakili wa Serikali: Kwa sababu Zipi afukuzwe Kazi

Shahidi: Kwa Utovu wa Nidhamu

Wakili wa Serikali: Wakati Mwaka 2019 anafukuzwa + kazi Wewe Ulikuwa wapi

Shahidi: Kwenye Operation Ya Peace Keeping, Sudan Jimbo la Darfur

Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kazi kwa Utovu wa Nidhamu

Shahidi: Ni 2020 Mwezi March Baada ya Kutoka Darfur

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ni Mazingira Yapi Ulifahamu Kwa Yeye Kufukuzwa Kazi Jeshini

Shahidi: Nilipata Taarifa hizo kutoka Kwa Administration Officer of the Unit

Wakili wa serikali: Administration Officer ndiyo nani

Shahidi: Mtu anaye fuatilia Maisha ya Askari Wote Kikosini na Maafisa ya Jeshi, Pia ni Kiongozi

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu na Khalfani Bwire tangu 2006 Mpaka 2019 yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri tu, Ya Kiongozi na afisa wake

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu baada ya Ajira Kukoma yalikuwaje

Shahidi: Bado nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye, Mawasiliano ya Kawaida tu

Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu anaitwa Adam Hassan Kasekwa ama Jina Lingine anaitwa Adamoo

Shahidi: Nafahamiana naye toka Mwaka 2012 ndipo alipofika Kwenye Unit ya 92KJ alifika Kwenye Mafunzo, Nikam’ train, aka’ pass Maana nilimpokea Mimi

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama, Huyu Adam Kasekwa ama Adamoo alifanya kazi Jeshini Kwenye 92 KJ alifanya kazi Mpaka Lini

Shahidi: Mpaka Mwaka 2018

Wakili wa Serikali: Nini Kilimsibu Mwaka huo 2018

Shahidi: Alifukuzwa Kazi Jeshini

Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Kazi Jeshini Kwa Sababu zipi

Shahidi: Kwa Utovu Wa Nidhamu

Wakili wa Serikali: Mpaka anafukuzwa Kazi Jeshini Kwa Utovu, Je alikuwa na Cheo gani

Shahidi: alikuwa Private Soldier

Wakili wa Serikali: Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini

Shahidi: Ni Askari ambaye hana Rank inayo kuwa Displayed, Ni Askari anayekuwa Chini ya Kiongozi Wake

Wakili wa Serikali: Wakati Adam Kasekwa anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa upo wapi

Shahidi: Nilikuwa Nipo Arusha

Wakili wa Serikali: Ni wakati Gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Adam Kasekwa kafukuzwa Kazi Jeshini

Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi Kutoka Arusha Kwenye Kozi

Wakili wa Serikali: Taarifa za Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu Wewe Ulizipata Wapi

Shahidi: Administration Officer

Wakili wa Serikali: alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira gani

Shahidi: Ofisini Kwake

Wakili wa Serikali: Mazingira ya Mahusiano Baina ya Wewe na Adam Kasekwa yalikuwa Je Kipindi Kile Kabla ajafukuzwa Jeshi

Shahidi: Yalikuwa Mazuri tuh

Wakili wa Serikali: VIpi Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi na Kuondoka Jeshini yalikuwa Je

Shahidi: Yalikuwa Mazuri

Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu Naitwa Mohammed Abdilah Ling’wenya Unamfahamu Vipi

Shahidi: Namfahamu Nilifanya naye Kazi Kituo Kimoja

Wakili wa Serikali: Kituo Gani hicho

Shahidi: 92 KJ

Wakili wa Serikali: umeanza Kufanya naye Kazi huyo Mohammed Ling’wenya kuanzia Mwaka gani Mpka Mwaka gani

Shahidi: Kuanzia Mwaka 2010 Mpaka Mwaka 2017

Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mwaka 2017

Shahidi: alifukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mpaka anafukuzwa Kazi, alikuwa ana Cheo gani Katika Jeshi

Shahidi: Alikuwa ni Private Soldier

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini

Shahidi: Ni Askari Mwenye Cheo Cha Mwisho chini

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Mahusiano yenu

Shahidi: Tulikuwa na Mahusiano Mazuri

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu, Mahusiano yenu yalikuwaje

Shahidi: Yaliendelea Kuwa Kama alipokuwa Kazini

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati Mohammed Ling’wenya anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa Wapi

Shahidi: Nilikuwa Kwenye Kazi Maalum

Wakili wa Serikali: Ni Wakati Gani Ulikuja Kupata Ufahamu, kuwa Mohammed Ling’wenya amefukuzwa kazi

Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi, kutoka kwa Administration Officer

Wakili wa Serikali: Huyo Administration Officer alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira Yepi

Shahidi: Tukiwa Ofisini

Wakili wa serikali: Unasema Unamfahamu Khalfani Bwire Je akiwa Miongoni Mwetu unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa serikali: Sababu ipi itakufanya Umtambue

Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 10, lakini pia Body Morphology 

Wakili wa Serikali: Mtu huyo Yupo wapi

Shahidi: aliyepo Mbele yangu, Tunatizamana, Yupo Jirani na Magereza

Wakili wa Serikali: Pia Umemtaja Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo, Je Unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Ni sababu Zipi hasa zitafanya Umtambue

Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5 lakini pia na Body Morphology Yake

Wakili wa Serikali: Hebu tuonyeshe Mtu huyo Yupo wapi

Shahidi: Ni Wapili Kutoka Kulia Mwa Khalfani Bwire

Wakili wa serikali: tuambie Mwingine unaye Msema ni Mohammed Abdilah Ling’wenya, na Yeye Vipi Unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa serikali: Sababu Ipi Itakufanya umtambue

Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5, pia Body Morphology yake, Tatu ana Makovu Usoni na Mkononi

Wakili wa Serikali: Hapa Yupo wapi

Shahidi: Ni watatu Kutoka Upande Wa Kulia wa Bwire

Wakili wa Serikali: Shahidi isaidie Mahakama, Unasema Adam Kasekwa Na Mohamed Ling’wenya Walikuwa ni Private Soldier, Je pale Jeshini Walikuwa na Majukumu Yapi

Shahidi: Wao Ni watendaji wa Shughuli za Kijeshi

Wakili wa Serikali: Huyu Khalfani Hassan Bwire, Adam Hassan Kasekwa, Mohammed Abdilah Ling’wenya wakati wa Utumishi wao Wa Jeshi Pale 92 KJ Makazi yao yalikuwa wapi

Shahidi: Walikuwa Wa naishi huko, Khalfani Bwire Ngerengere, Adam Kasekwa alikuwa Anaishi Chalinze katika Utaratibu Wa Misbehave

Wakili wa Serikali: Hapana Usiende Huko

Shahidi: Na Mohamed Ling’wenya na Yeye Chalinze

Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Mwaka 2011 ulikuwa Darfur, Je katika Wenye Cheo Cha Private Soldier nani Uliyekuwa naye

Shahidi: Sikumbuki

Wakili wa Serikali: Unaposema Ukumbuki unamaanisha nini

Shahidi: Sina Kumbukumbu Ka Nilikuwa na Mmoja wapo

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama pale Darfur Ulipokuwa Unaishi Kwenye ile Nyumba yako Ulikuwa Unaishi na Nani

Shahidi: Tulikuwa tunaishi Viongozi Watupu

Wakili wa Serikali: Na Mwaka 2012 pale Darfur Pia Mwenye Cheo Cha Private, nani ulikuwa naye

Shahidi: Sikumbuki

Wakili wa Serikali: Mtu anaitwa Freeman Mbowe Wewe Unahusiana naye Vipi

Shahidi: Tulifahamiana naye Mwaka 2008 Mpaka 2020

Wakili wa Serikali: Unaweza Kusema ni Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kufahamiana

Shahidi: Mwaka 2008 Freeman Mbowe anilipigia Simu akaniita Kwa Majina yangu

Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Siwezi Kukumbuka hiyo Tarehe

Wakili wa Serikali: Shahidi Irejee Mahakama tena, Unasema alikupigia Simu lini

Shahidi: Mwaka 2008

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi na Mwezi gani

Shahidi: Sikumbuki Tarehe Wala Mwezi

Wakili wa serikali: alikupigia Simu, wewe si yako ilikuwa ya Namba gani

Shahidi: ilikuwa 0754612518

Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka na Yeye namba yake iliyokupogoa ilikuwa namba gani

Shahidi: Ilikuwa Mtandao Wa Airtel, ila namba Sikumbuki

Wakili wa Serikali: alikueleza nini

Shahidi: alipiga Simu akauliza Wewe ni Denis Urio, Nikamwambia Yes ndiyo Mimi, akasema ni Askari wa Jeshi la Wananchi, Nikamwambia Ndiyo, akajitambulisha, Kwa Sababu Namfahamu Nikamuamkia..

Wakili wa Serikali: Kwa Sababu Unamfahamu Ukamuamkia, Ulikuwa Unamfahamu Vipi

Shahidi: Alikuwa anaonekana Kwenye Vyombo Vya Habari, Haikuwa Jina geni, I Amana anafahamika

Wakili wa Serikali: Baada ya wewe Kumpa Salamu nini Ulifanya

Shahidi: alikuwa ana confirm Profile Yangu

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini

Shahidi: alikuwa nauliza wewe si Denis Urio Nikasema Ndiyo, ni Mtu wa Kilimanjaro basi Mimi Ndugu yako, Ndipo Uhusiano Ulianza

Wakili wa Serikali: Hebu Iambie Mahakama Namba yako ya Simu alitoa Wapi

Shahidi: Sifahamu alipoitoa

Wakili wa Serikali: Yeye alikueleza, Ni wapi ametoa Namba yako

Shahidi: aliniambia Kuwa Mbona Unafahamu, Kwa Mtu Kupata Namba ya Simu Siyo Tatizo, Usiwe na Wasiwasi

Wakili wa Serikali: Ni Kitu gani kilipelekea Mpaka Yeye Kusema Kuwa Mbona Unafahamika Sana

Shahidi: Ni pale Nilipo taka Kujua amepata wapi Namba Yangu

Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hayo Maneno ni Wakati gani alikutamkia

Shahidi: Mara ile ya Kwanza Kuwasiliana, Nikiwa natumia Mtandao Wa Voda yeye akitumia Mtandao Wa Airtel

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Baada ya Siku hiyo kuwasiliana Mawasiliano yenu yalikuwaje

Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana, Iwe Kwa Kunisalimia alikuwa ananitumia Ujumbe wa Kuni wish hata Kama Kuna Sikukuu au Event Yoyote

Wakili wa Serikali: Mlimkuta ana kwa ana Lini

Shahidi: Tukikutana Ana Kwa Ana Mwaka 2012

Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Mwaka huo 2012 Ilikuwa ni Tarehe Ngapi na Mwezi Gani

Shahidi: Siwezi Kukumbuka Tarehe Wala Mwezi

Wakili wa Serikali: Shahidi nikirudishe Nyuma, Umeeleza Awali Kwamba 2011 ulikuwa Darfur Nchi Sudan, Je Ulirejea Nchi Mwaka Gani

Shahidi: Nili rejea Mwaka 2011 Mwezi wa 10

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Siwezi Kukumbuka Siku wala Tarehe

Wakili wa Serikali: Ni Mazingira Yepi Yalipelekea Ninyi Mwaka 2012 Kukutana

Shahidi: Mwaka 2012 nikiwa Maeneo Ya Mgulani (Saba Saba) Nilipokea Simu ya Mheshimiwa Mbowe Kama Ilivyo Kawaida yake akaniambia Upo wapi, Nikamwambia Nipo Maeneo Ya Mgulani (sabasaba)

Wakili wa Serikali: alikueleza nini

Shahidi: Alini uliza nipo Wapi, Nikamuelekeza Location nilipo

Wakili wa Serikali: Location Maana yake ni nini

Shahidi: Eneo nilipo

Wakili wa Serikali: Endelea

Shahidi: aliniambia Kuwa Kuna Kitu anataka Tuongee, Je tunaweza Kuonana? Nikamuuliza Wewe Upo wapi akasema Yupo Mikocheni Cassa Motel

Jaji: Unaweza Kutaja Spelling zake

Shahidi: CASA Sikumbuki Vizuri

Wakili wa serikali: Wewe Ukamwambia Nini

Shahidi: Sijui Mikocheni Vizuri, Wala Mahala Ilipo

Wakili wa Serikali: Ulifanya Nini sasa

Shahidi: Baada ya kumwambia Siyo Mwenyeji aliambiwa niende Kituo Cha Tax Ni Mwambie Dereva Yoyote yule anipeleke CASA Motel

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupewa hayo Maelekezo, Maamuzi yako yalikuwa ni nini

Shahidi: Nilienda Kwa Dereva Tax, Nikamwambia Anipeleke CASA Motel, nikaweza Kufika CASA Motel

Wakili wa Serikali: Hicho Kituo Cha Tax Ulicho enda Kutafuta Tax ni Kituo Cha Wapi

Shahidi: Ni Saba Saba Mbele Kidogo Kama Unaenda Kwa Aziz Ally Wilaya Ya Temeke

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Hiyo Safari yako ya CASA hotel Ilikuwaje

Shahidi: Nili weza Kufika, Nikampigia Simu akapokea, akauliza nimefika Wapi, Nikamwambia Nimeshafika

Wakili wa Serikali: Taratibu Jaji anaandika..

Wakili wa serikali: endeleaaaa

Shahidi: akanielkeza Pale CASA Motel Kuna Vitu Kama Vimepangwa Kuna watu walikuwa wamekaa Mbali Mbali Ka Wanne hivj, Baada ya Kufika akaniuliza huyu anadai TSh ngapi Nikamwambia TSh 20

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumwambia Ikawaje

Shahidi: Alilipa hiyo Tsh 20

Wakili wa Serikali: Wakati yoye Haya Unayosema Kuanzia Kupigana Simu Mpaka Unafika CASA Hotel Ilikuwa ni Majira yapi

Shahidi: Ilikuwa Kuanzia Saa Saba Mchana Mpaka Alasiri

Wakili wa Serikali: Pale Mlipoliwa Mmekaa na Kukutana naye, Mwingine nani Mliye kuwa Mmekaa naye

Shahidi: Hapakuwa na Mtu Mwingine zaidi yangu Mimi na Yeye

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa, Nini Mlichozungumza Wakati Mmekutana

Shahidi: Mambo Makubwa matatu, Kutaka Kujua Mimi ni Nani, nafanya kazi gani, Nina Cheo gani

Wakili wa Serikali: Kwenye Hayo Madodoso wewe Ulimjibu nini

Shahidi: Mimi ni +Rank gami Majibu niliyompa, Nilimwambia Mimi Sina Rank

Wakili wa Serikali: Ulipomueleza Wewe huna Rank Ulikuwa Unamanisha Nini

Shahidi: Nilimwambia Mimi Sina Cheo Chochote

Wakili wa Serikali: Kwanini Ulimueleza hayo

Shahidi: Kwa sababu aliniuliza Swali

Wakili wa Serikali: Lingine lipi ulilomjibu

Shahidi: Nilimjibu nafanya kazi Mkoani Morogoro, na Nyumbani ni wapi nilimwambia Mimi Nyumbani ni Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Vijijini

Wakili wa Serikali: Kingine Kipi

Shahidi: Akitaka Kujua Msimamo Wangu dhidi ya Vyama Vya Upinzani

Wakili wa serikali: Kwenye hilo la Msimamo Wako Majibu yako Yalikuwa ni Yepi

Shahidi: Nilimwambia Kwa Mujibu wa Kazi yangu Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote

Wakili wa serikali: ukamueleza nini?

Shahidi: Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote, Ila Kwa Kiongozi aliyepo Madarakani

Wakili wa serikali: Lingine lipi mililozungumza

Shahidi: Alini uliza Juu ya Makampuni ambayo yangeweza Kufunga Mfumo Wa Mawasiliano Kwenye Ofisi zao, na Kama Jeshini Kuna Makampuni yaliyofunga Mawasiliano Jeshini

Nilipo Muuliza Kwanini anataka Kufanya kazi na Makampuni Yaliyofunga Mawasiliano Jeshini, Akajibu Kuwa anataka Kufuatilia Mawasiliano ya Viongozi Wenzie Wanaotoa Siri Nje ya Chama

Wakili wa Serikali ieleze Mahakama Baada ya Kuku uliza Juu ya Swala hilo, Majibu yako Yalikuwa ni nini

Shahidi Nilimshauri aende Kwenye Taasisi za Elimu ya Juu ndiyo atapata Suluhu ya Tatizo lake

Wakili wa Serikali Nini Kiliendelea Sasa Baada ya Hapo

Shahidi Baada ya Hapo tuliachana, Akaita Tax akamlipa Ni kaondoka zangu

Wakili wa Serikali Ilikuwa ni Fedha kiasi gani aliyolipwa

Shahidi Sijui ni fedha Kiasi gani

Wakili wa Serikali Baada ya akiwa mmeachana, Mliachana Majira gani

Shahidi: Majira ya Jioni kati ya Saa 9 Mpaka Saa 11 Jioni

Wakili wa serikali: Baada ya Wewe Kuachana naye Ulieleka Wapi

Shahidi Nilirudi Nyumbani

Wakili wa serikali: Baada ya Kikao Chenu Mawasiliano Yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa Ka Kawaida, Nanipigia Simu, ananitumia Meseji na anani’ Wish Kama ni Sikukuu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya Mwaka 2012, Je ni wakati gani Mwingine Mlikutana ana kwa ana

Shahidi: Ilikuwa ni Mwaka 2020 Mwezi Saba Tarehe za Katikati

Wakili wa Serikali: Hebu elezea Mahakama ni. Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kukutana

Shahidi: Ilikuwa Kwenye Tarehe 26 Mpaka 30 June Mwaka 2020, Niliacha Simu Kwenye Gari, Nipo rudi Nilikutana Missed Calls Nyingi. Missed Calls zaidi ya Tano Katika Simu

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Unaposema Missed Call zaidi ya Tano

Shahidi: Ni simu ambazo hazikupokelewa

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ni Namba za akina nani

Shahidi: Hazikuwa Saved, Zilikuwa ni Namba Ngeni Katika Simu yangu

Wakili wa serikali: Baada ya Kukuta namba Ngeni na Huku pokea, Ulihisi nini

Shahidi: Nili Fikiri ni Familia Yangu, Nilipiga Mwanzo Haku pokea, Nilipiga tena akapokea akasema alikuwa anakutafuta Mwenyekiti

Baadae Nilipiga Simu Nyingine, ikapokelewa akasema alikuwa anakutafuta Chairman

Basi sikupiga tena namba Nyingine

Wakili wa Serikali: Hebu elezea Mahakama ni nini Kilitokea

Shahidi: Baadae Ikipigwa Simu na namba Ngeni akasema ni Kaka Yangu wa Dodoma, Nikamwambia Mbona sina Kaka Dodoma, akasema Sikia Mimi ni Freeman Mbowe, Nikamsalimia Shikamoo Mzee

Wakili wa Serikali: Kasema nini

Shahidi: Akaniambia Kuna Mambo ya Muhimu Sana nataka Tuongee, Nikamwambia Kuwa tunaweza Kuongea tuh kwenye Simu, akasema Ni Jambo Muhimu Sana ni Lazima tuonane, Nikamwambia Kwa sasa Sina Muda,

Wakili wa Serikali: Wakati hayo Yanatokea yalikuwa ni Majira gani

Shahidi: Yalikuwa Majira ya Saa 10 Jioni

Wakili wa Serikali: Wakati hayo Yanatokea wewe Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa nipo Likizo Morogoro

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kukupa Ombi lake la Kuonana, Nini Kiliendelea

Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana tu. Baada ya Hapo Nilikuja Dar es Salaam Mwezi wa Saba 2020

Nilikuja: kwa kazi Binafsi, Ni kafanya Shughuli zangu za Kijeshi, Majira ya Saa 10 nikakummbuka Nilikuwa na appointment, Nimampigia Simu yake Mara Kadhaa hazikupokelewa, Basi Nikawa naenda Station, Kupanda Magari ya Mgulani

Wakili wa Serikali: Nini kitokea

Shahidi: Wakati Nasubiri Gari Kituoni Majira ya Saa 12 alinipigia Simu Kwa namba Nyingine, akaniambia Alikuwa yupo Bussy alishindwa Kupokea simu yangu, Kaniuliza upo wapi

Nikawa Mwambia nipo Station Najiandaa Kwenda Mgulani akaniambia Homeboy hatuwezi Kuonana

Wakili wa Serikali: Nimesikia Mara Kadhaa unatamla Homeboy, Je Tafsiri yake ni nini

Shahidi: Tafsiri yake Mimi siwezi Kujua, Ila mara Kadhaa alikuwa ananiita Homeboy

Wakili wa Serikali: Wewe Sasa Ulimjibu nini Kuhusiana na Ombi lake

Shahidi: Alini taka kama naweza Kufika Mikocheni, Nakamwambia Kuwa Mikocheni sipajui Vizuri, naweza Kupotea

Akaniambia huwezi Kupotea, akaniambia Cheki Dereva Tax au Bodaboda Karibu amuelekeze Mahali alipo

Nikampa Bodaboda Simu Pale Stand ya Station akamuelekeza, baada ya hapo Ni kaondoka na Bodaboda Kuelekea Mikocheni

Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hapo Mikocheni Mlienda Hadi sehemu gani

Shahidi: Tulienda Mpaka Kwenye Mgahawa Sipafahamu, Kuna Parking ya Magari, I kabidhi nipigie simu Haku pokea, Wakati Napiga simu, akatokea Kijana Mmoja Nyuma Yangu

Akaniuliza wewe Ndiyo Denis Urio, Nikamwambia Ndiyo Mimi, akatoa Elfu 10 akamlipa Bodaboda akaniambia Mwenyekiti Yupo huku, Tukaenda kwa Nyuma kama VIP, Basi yeye akatoka Nje

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tuambie wakati huo Unafika Pale sasa, Ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi

Shahidi: Ilikuwa Majira ya Saa Moja Kasoro, Jua lilikuwa Leshazama lakini Bado Kuna Mwanga, Kwa hiyo Kama Saa Moja Kasoro

Wakili wa Serikali: Na Wakati una Mpigia Simu, Na Yeye akakupigia baadae, alikuwa anatumia namba gani

Shahidi: alikuwa ana tumia namba ambayo siyo ya kwake ni Namba ambayo sihifahamu

Wakili wa serikali: Iambie Mahakama wakati wewe Umefika pale ulipokutana naye, Ulimpigia Simu Kwa namba ipi

Shahidi: alikuwa na namba yake ya Airtel na Tigo, Nilipiga Airtel hakupokea na Nilipiga Tigo hakupokea pia

Wakili wa Serikali: Ukiondoa Pale Mlipokutana, Ni nani Mwingine alikuwa pale

Shahidi: Hapakuwa na mtu, Ni Mazingira ya starehe, Tulikuwa wawili tu Mimi na Yeye

Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Sasa nini Kilichotokea Sasa Pale Mlipokutana

Shahidi: Nilimkuta yupo Pekee yake anakunywa Redbul anamuita Muhudumu anisikilize na mimi nikaagiza Malta

Wakili wa serikali: Sasa Shahidi Tuambie, Ieleze Mahakama Alikueleza au Kukwambia Kitu gani alichokuitia

Shahidi: Kitu cha Kwanza tulisalimiana Salamu za Muda Mrefu, Lakini Baada ya Salamu hizo akaniambia komredi mwaka huu wa 2020 Kuna Uchaguzi Mkuu, Hivyo Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola Kwa namna na Kwa Gharama Yoyote ile

Akaniambia Wewe si Unaona Watu wa wanyonge wa hali ya Chini wanavyoishi Maisha ya Shida

Akanielekeza, komredi Tumefahamiana Muda Mrefu, Tunatoka Mkoa Mmoja, pia wewe ni Mchaga Mwenzangu, Tukichukua Dola Unafikiri Wewe Utakosa Cheo Cha Juu Jeshini?

Akaniambia hivyo Jeshini Kuna Watu Waliostaafu au Kufukuzwa Kazi ya Jeshi.. Wale ambao wamefanya Mafunzo Maalum ya Komandoo.. Homeboy naomba umitafutie Vijana hao wenye Mafunzo Maalum Ya Komando, ambao nitaambatana nao kwenye Harakati za Kuchukua Dola..

Najua Watakuwa na Uwezo wa Kunisaidia Kufanya Nchi isitawalike, Kuleta Taharuki na Kusiwe na Amani.. Tutafanya hayo Kwa Kuzua Taharuki Mheshimiwa Freeman Mbowe Alisema yalikuwa ni Kulipua Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Moto Masoko na Mikusanyiko Mkubwa Ya watu..

Kukata Miti Mikubwa iliyoota pembezoni Mwa Barabara zote, Hasa Kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro hasa Mji wa Moshi na Barabara Kuu ya Morogoro – Iringa, Kwa Kufanya Vitendo hivyo Vitatu Kutapelekea watu Kuwa na Taharuki na Kuandamana Nchi Nzima,

Mikoa Mingine Iliyobakia Itasapoti Mikoa hii niliyo highlight.. Point Nyingine ya Mwisho ni Kuwadhuru Viongozi Wengine Wa Serikali, Ni Viongozi ambao ni Vikwazo Kwa Vyama Vya Upinzani.. Hivyo Homeboy nisaidie Kuwapata hao watu Nina Haraka nao sana, MWISHO WA MAELEZO YAKE FREEMAN

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama alipokueleza yeye Hayo Makusudi yake wewe Ulifanya Jambo Gani

Shahidi: Nilitafakari nikamkubalia

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tueleze Wewe alipokueleza hayo Maneno, Ni Kipi kilikupelekea ukamkubalia

Shahidi: Kwa Experience yangu Kuna kitu kinaitwa Tactical appreciation

Wakili wa Serikali: Experience yako Kwenye Nini

Shahidi: Kwenye Ulinzi

Wakili wa Serikali: Tactical appreciation ni Kitu gani hicho

Shahidi: Kuna Binadamu, Kuna Mimi na Tanzania, lakini Mimi si kitu Kuliko Tanzania, Freeman Ni Ndugu yangu, Tayari Alishakuja na Ile Nia, Kwamba Unataka nimkatalie, lakini Mimi huenda ni Plan B au C…

Je Nikimkatalia atachukua hatua gani, Je nitakuwa ni solution matatizo yasitokee, Naweza Kumkatalia lakini kumbe ana Backup plan nitakuwa sija solve tatizo..

Wakili wa serikali: Sasa hiyo Tactical Appreciation Uliyotumia Ulitumia Kufanya nini

Shahidi: Ikaniongoza Kwamba Nimkubalie, Kwamba Nipe Muda Nikutafute hao watu

Wakili wa serikali: Sasa Shahidi Tuambie, yeye alikwambia anataka Wangapi

Shahidi: Hakuna Kikomo cha Watu, Ni wale Watakaopatikana

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Baada ya kukueleza Maneno yale nini Kilitokea

Shahidi: alimuita Kijana wake, Akaita Tax nikarudishwa nilipotolewa

Wakili wa Serikali: Wakati huo unamaliza na Wewe unarudi Mgulani ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi

Shahidi: Saa Mbili hadi Saa Tatu, Kwa sababu Taarifa ya Habari Ilikuwa imeshaanza

Wakili wa Serikali: Na Huyo Dereva Tax alikuwa amelipwa TSh ngapi

Shahidi: Sijui alikuwa amelipwa TSh ngapi

Wakili wa Serikali: Shahidi Umerudi Mgulani, Nini Sasa Ulichofanya au Hatua ulizo chukua Juu ya Ujumbe Uliopewa

Shahidi: Nilishindwa Kulimeza

Wakili wa Serikali: Kushindwa Kulimeza ndiyo nini

Shahidi: Nilishindwa kukaa nalo

Wakili wa Serikali: Kwanini Ushindwe Kukaa na Taarifa Ya siri

Shahidi: Nature ya Taarifa

Wakili wa Serikali: Taarifa Ipi

Shahidi: Ya Kuleta Taharuki

Wakili wa serikali: Baada ya Kushindwa Kueleza Ulifanya nini

Shahidi: Nilichukua Hatua Ya akimpigia DCI Afande Boazi Majura ya Saa 3 Usiku

Wakili wa Serikali: DCI ni Kitu gani?

Shahidi: Director of Criminal intelligence, Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai

Wakili wa serikali: ulipo Mpigia nini Kilitokea

Shahidi: Nilimpa Taarifa amilizopewa na Freeman Mbowe, Juu ya Uvunjifu wa Amani, Kwamba ameniambia nitafutie Watu wa Kukata Miti Barabarani na Kuchoma Masoko wakati naendelea Kusema hivyo akasema Subiri, Unaweza Kuja Kesho Ofisini Kwangu Asubuhi

Wakili wa Serikali: alikwambia nini

Shahidi: Kama naweza Kufika Ofisini Kwake Kesho Asubuhi

Wakili wa Serikali: Na shahidi Unaweza Kukumbuka namba ya Simu ya Robert Boazi (DCI) Uliyompigia

Shahidi: Sijaikariri Kichwani

Wakili wa Serikali: alikwambia Uende Ofisini Kwake wapi

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi, Jijini Dar es Salaam Mtaa wa Ohio

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Alikutaka Uende Ofisini Kwake Saa ngapi

Shahidi: Majira ya Asubuhi

Shahidi: Nilifika Makao Makuu ya Jeshi Polisi, nikajitambulisha Getini Kuwa Nina Appointment na Afande DCI, Nikaenda Pia nikamkuta Polisi nilajitambulisha Kuwa mimi ni Afande Mwenzao Nina appointment na Afande DCI, wakaniruhusu Nikaenda Ghorofa ya Saba

Wakili wa Serikali: Wewe Ulikuwa unapanda Juu Kuelekea Wapi

Shahidi: Nilikuwa napanda Juu Ofisi ya DCI Ghorofa Ya Saba

Wakili wa Serikali: kabla Ya Siku hiyo Kwemda Kwa DCI ni lini tena Ulienda Ofisi hiyo

Shahidi: Nilishafika Mara Mbili Mwaka 2017 na Mwaka 2014

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Kipi kililufahamisha Ofisi za DCI zipo Ghorofa ya Saba

Shahidi: Nilishafika Awali, ila baada ya Kufika Reception Nili Confirm kwa wale askari

Wakili wa Serikali: Ulienda Vipi Ghorofa ya saba

Shahidi: Kuna Njia Mbili Kuna Lift na Kuna Ngazi, Lift ilikuwa haifanyi kazi, nikapanda ngazi

Shahidi: Inapofika Ghorofa ya Saba Kwa Kupanda Ngazi, Pembeni yake Kuna Mlango, Nilipo Fungua Mlango Nikakuta Kuna Askari Mwanamke ambaye ni PS wake, Nikajitambulisha Kwamba Naitwa Luteni Denis Leo Urio Askari Wa Jeshi la Jeshi la Wananchi,

Wakili wa Serikali: Baada ya Kujitambulisha, Ulimwambia nini huyo PS

Shahidi: Nilimwambia Nina appointment na Afande DCI

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kumueleza hayo

Shahidi: Palikuwa na Kochi pembeni akaniambia Nikae pale pembeni afanye Mawasiliano naye

Baada ya Kufanya Mawasiliano naye, Nikaambiwa Ingia, Nikakuta tena kuna Makochi na Kuna msaidizi Wake akasema Subiri utaitwa

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukaa hapo Nini Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Muda PS Wake akaja akaniambia Fungua Mlango Niingie Kwa DCI

Wakili wa Serikali: Ulikutana na Kitu gani

Shahidi: Nilimkuta Afande DCI yupo Pekee yake, Nikamsalimia, Nikajitambulisha, Nikamkumbusha

Wakili wa Serikali: Ukajitambulishaje

Shahidi: Mimi naitwa Luten Denis Urio, Miliyekupigia simu Jana Usiku

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani Sasa ni saa Saba Kasoro Dakika Nne, Na Mimi bado Nina Maswali mengi sana, Naomba Tupate Break Kidogo

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Basi tunahairisha Kwa Muda Kupata Health Break, Kwa hiyo tutarudi Saa Saba na Dakika 45

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Jaji.. Kimasta zaidi..

Jaji anatoka

Jaji ameingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile kama awali tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia Upande wa Utetezi Quorum yetu haijabadirika

Shahidi aliingia Mahakamani aliongozana Wakili Wa Serikali Ignasi Mwinuka

Jaji Shahidi :nakukumbusha Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako Chini ya Kiapo, Na Chini ya Kiapo Utaendelea Kutoa Ushahidi

Wakili wa Serikali: Shahidi uliishia Kuwa Ulipofika Ofisini Kwa DCI Ulijitambulisha na Kumbukumbusha, Je Ulimkumbusha nini

Shahidi: Kwanza nilipofika Ofisini Kwake Kuna Conference Table Kama Nne, Kama Hizi hapa, Nilipo Kuwa Naanza Kutoa zile Taarifa Kanitaka

Wakili wa Serikali: Baada ya Kujitambulisha Ulimwambia nini

Shahidi: Kwamba Mimi ndiye niliyekupigia Simu Kuwa Nilikutana na Freeman Mbowe, akinitaka nitafutie Askari Waliopata Mafunzo Kwa ajili ya Harakati Zake za Kuchukua Dola

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumpa Maelezo hayo, Nini Kilitokea

Shahidi: Wakati huo alikuwa anafanya Mawasiliano, Akaingia Mtu, akaja akamsalimia Afande DCI

WAKILI WA SERIKALI: Unasema alikuwa anafanya Mawasiliano, Je ni Mawasiliano gani

Shahidi: Alikuwa anapiga Simu

Wakili wa serikali: Baada ya Hapo

Shahidi: Akaingia Mtu akanisalimia, Baada ya Hapo akakaa Kwenye Kiti

Wakili wa serikali: ulipita Muda gani tangu alipokuwa anafanya Mawasiliano

Shahidi: Sijui Kama Dakika 10

Wakili wa serikali: Yule Mtu aliye ingia Mkaa Kaa na Kutizamana, Siku ile ikiwa Mara ya Ngapi Kuonana

Shahidi: Mara yangu ya Kwanza

Wakili wa serikali: Iambie Mahakama sasa, Yule Mtu alipoingia Mkatazamana, Nini Kiliendelea

Shahidi: Afande Boazi alinitambulisha Kuwa Yule Mtu anaitwa ACP Ramadhan Kingai

Wakili wa serikali: Baada ya Utambulisho huo

Shahidi: DCI akanitaka tena nianze tena Upya Kusimulia

Wakili wa Serikali: Uliwaeleza nini

Shahidi: Nikiwa eleza Kwamba Jana nilipigiwa Simu na Freeman Mbowe Akinitaka Tukutane Maeneo Ya Mikocheni, Na Mimi nikafanya hivyo.. Freeman Mbowe akanieleza yafuatayo

Kwamba Mwaka huu Kuna Uchaguzi, Sisi tumedhamiria Kuchukua Dola Kwa namna yoyote ile

Na Kwa sababu Mimi Nafahamiana na wewe Kwa Muda mrefu, Wakichukua Dola nitapewa nafasi Kwa Maana Cheo Cha Juu..

Kwa Maana hiyo akaniomba Sasa, Nitafutie Askari Waliostaafu Au waliofukuzwa Kazi ambao Wamefanya Mafunzo Maalum ikiwa ana maana ni Makomandoo ili waambatane naye

Katika Harakati hizo za Kuchukua Dola Kwa Kufanya. Matukio yatakayofanya Nchi isiwe na Amani, Isitawalike, Kwa Kufanya Matendo haya, Ilikusudi Nchi isitawalike watalipua Vituo Vya Mafuta, Katika Majiji Matano Makubwa ambayo ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha na Mji wa Moshi

Vilevile Watachoma Moto Masoko Makubwa Kwenye Miji, Pomoja na Mikusanyiko ya Watu Kwenye Miji niliyotaja, Pia watakata miti Mikubwa Pembezoni kwenye Barabara Inayoingia na Kutoka, Ili Kusiwe na Mawasiliano

Matendo hayo Makubwa Matatu niliyo yataja Yakitoka Kwenye Miji niliyo taja Patatokea Taharuki, Serikali Itaonekana Imeshindwa Kujali wananchi Wake, Ili wao Watangaze Mandamano, Kwamba Serikali Imeshindwa Kuangalia Usalama Wa Watu wao..

Pia Niliendelea kueleza Kingai Na DCI Kwamba Wampanga Kuwashambulia Viongozi Wa Serikali ambao ni Vikwazo Kwa Vyama Vya Upinzani, Na hiyo ndiyo Ilikuwa Taarifa Yangu niliyompa DCI Afande Robert Boazi…

Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Mahakama Sasa Baada ya wewe Kutoa Taarifa Kwa Afande DCI Nini kiliendelea

Shahidi: DCI alimuita DCP Ramadhan Kingai Kwenye Eneo lake (kiti) wakaketi Wao Wawili, Mimi sikujua Kilichokuwa Kinaendelea

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuitama Wenyewe na Kutetea nini Kilifuata

Shahidi: DCI alimtaka DCP Ramadhan Kingai anipe Namba zake za simu na Mimi Nimpe namba zangu

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Maelekezo hayo Kilifuata nini

Shahidi: Tulibadilishana namba

Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo

Shahidi: Niendelee na Utaratibu Wa Kumtafutia Mbowe Hao Watu, Na Kila Stage na Kila Hatua niwe na report Kwa DCI na Ramadhan Kingai

Wakili wa Serikali: DCI alikupa Maelezo gani Katika Kuwatafuta hao watu

Shahidi: Nisisite Kuwatafuta hao watu, lakini Kila Hatua niwe na Report Kwake DCI na Ramadhan Kingai

Wakili wa Serikali: DCI alikwambia Uwape Maelekezo gani

John mallya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hiyo ni Leading Question. Napendekeza hilo Swali na Jibu Visiingie. Kwamba

Wanaotafutwa Wapewe Maneno Fulani, haikuwa Based kwenye Ushahidi Wa Shahidi

Wakili wa serikali: Mhe Jaji Sija Uelewa Mwenzangu Kwamba Swali Ninapo uliza ni Leading Question, na Hili swali Haki Suggest Jibu lakini pia Hakuna Kanuni za Sheria Zinazokataza Uliulize Swali ambalo Shahidi ajasema

Jaji: Rudi Swali lako

Wakili wa serikali: Sawa mheshimiwa Jaji, ukiacha maelezo hayo, Je maelekezo yapi mengine uliyapokea kutoka kwa DCI

Shahidi: aliniambia kwamba nikisha wapata watu hao, wakienda huko wakakuta matukio ya kihalifu yoyote, popote kwa Freeman Mbowe waniambie mimi

Mawakili wa serikali wanatazamana kidogo hapa, Kama wamehamaki baada ya Maelezo hayo ya ndugu shahidi (Homeboy)

wakili wa serikali: Eeeh Shahidi Baada ya Kupewa hayo Maelekezo nini Kilifuata

Shahidi: mimi niliagana na Afande DCI Nikaenda Kuendelea na Shughuli zangu, lakini Kwakuwa alishanipa Kazi niendelee Kwa Utaratibu huo huo Nikaanza Mchakato Wa Kutafuta hao Watu

Nilianza Kumtafuta Mtu anaitwa Moses Lijenje

Wakili wa serikali: Huyu Moses Lijenje ni nani

Shahidi: Naye alikuwa ni Askari Wa Jeshi la Wananchi Aliyefukuzwa Jeshi

Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Jeshi Mwaka gani

Shahidi: Mwaka 2008

Wakili wa Serikali: alikuwa Kikosi gani Cha Jeshi

Shahidi: alikuwa 92 KJ

Wakili wa Serikali: Na wewe Ulifahamiana naye Kuanzia lini

Shahidi: Nilifahamiana naye Kuanzia 2003 Mpaka 2008

Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Jeshi Kwa Sababu Zipi

Shahidi: Kwa Utovu Wa Nidhamu

Wakili Peter Kibatala: Mhe Jaji, Kanuni yetu ya Kwamba Wasiopo Mahakamani wasitajwe Majina inaendelea au Inakuwaje, Maana Mallya alizuiwa Kutaja Jina la Rais Mwinyi Hapa

Jaji Mallya: Hakuwa Shahidi

Kibatala: Kwa hiyo Mimi nikiwa nam’ cross examination Shahidi naruhusiwa

Jaji: Ndiyo

Kibatala: Sawa, pia Samahani Kwa Usumbufu

Wakili wa Serikali: Lijenje Wakati huo alikuwa wapi

Shahidi: Alikuwa anafanya Kazi YARP MAKENZIE Katika Kipande Cha SGR cha MOROGORO

Wakili wa Serikali: Ulimtafuta Kwa Njia gani

Shahidi: Kwa Njia ya Simu, Baada ya Kumpata Nikamwambia Kuna kazi ya Ulinzi Kwa Freeman Aikael Mbowe, Nikamuuliza Je Unaweza Kufanya kazi hiyo..? Akaniambia yupo tayari Kufanya kazi Kwa sababu huo alikuwa amepunguzwa Kazi kwa muda Sababu ya Corona, Kwa hiyo Yupo Tayari

Wakili wa Serikali: Shahidi Baada ya kumtamkia hayo Majibu yake ni Yepi

Shahidi: Akaniambia Yupo Tayari, Ni Mimi Nikamwambia Subiri Freeman Mbowe akisha Kuwa Tayari nitamkulisha

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umesha Pata Moses Lijenje, Nani Mwingine Ulimpata

Shahidi: Nikamtafuta Khalfani Hassan Bwire

Wakili wa Serikali: Ulimtafuta Kwa Njia gani

Shahidi: Kwa Njia ya Simu, namba yake Ilikuwa haipatikani, Nikamtafuta Kwa Messenger, akatuma namba yake ya Simu

WAKILI WA SERIKALI: Naye ulipo Mpata ulimueleza Nini

Shahidi: Nilimueleza Freeman Aikael Mbowe anahitaji Walinzi, Je Upo tayari, akaniambia Yupo Tayari

Wakili wa Serikali: Wakati huo Yupo wapi anafanya nini

Shahidi: Wakati huo aliniambia anafanya Kazi ya IT Kupeleka Magari Kupeleka Tunduma

Wakili wa Serikali: Kutokea Wapi

Shahidi: Sina Hakika Ka. NI Dar es Salaam au wapi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumpa Taarifa hizo alisemaje

Shahidi: Akaniambia Yupo Tayari Kufanya Kazi

Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Baada ya Kuwa amekukubalia wewe Ulimpa Majibu gani

Shahidi: Nilimwambia Subiri Muda Utakao Hitajika na Freeman Mbowe Nitamjulisha

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umempata Mtu wa Pili Ukafanya nini

Shahidi: Nikawa naasubiri Kama Mwemye uhitaji akiwa serious atanitafuta

Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Sasa Baina yako wewe na Freeman Aikael Mbowe

Shahidi: Nili tulia Baada ya Siku Chache, Wiki Kasoro Freeman Mbowe akanipigia Simu akaniambia Homeboy

WAKILI WA SERIKALI: Twende Taratibu

Shahidi: Akaniambia HOMEBOY Mbona Wale Watu Mpaka Saa hizi Kimya, Wale Watu Mbona hukunitafutia?

Hapo Ndiyo Nikajua sasa Yupo serious, Nikamwambia Kwamba Watu wapo Tayari, Unatakiwa kuwatumia tu nauli ili miweze Kuwa Mobilise huko walipo

Akaniuliza Gharama zote Tsh ngapi.. Nikamwambia TSh Laki 5..

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu iambie Mahakama hayo Mawasiliano Mlikuwa Mnafanya Kwa Njia gani

Shahidi: Mawasiliano Makubwa yalikuwa kwa Telegram, Kwa hiyo nampigia Kwa Telegram au WhatsApp Call

Nikimpigia Kwa simu ya Kawaida Hapokei, Lazima atumie simu ya Mtu

Wakili wa Serikali: alipoanza Kukukumbushia ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Ilikuwa Tarehe 20 July

Wakili wa Serikali: Mlikuwa Mawasiliana kwa Njia gani

Shahidi: Kwa Kupiga na Meseji Kwa Telegram

Wakili wa Serikali: Ikumbushe tena Mahakama unasema ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulipo Mwambia unahitaji TSh Laki 5 nini Kilitokea

Shahidi: aliniambia ni mtumie namba Nyingine, nikamtumia Namba yangu ya Airtel

Wakili wa Serikali: Namba yako ya Airtel ni Namba gani

Shahidi: Ni 0787 555200

Wakili wa Serikali: Ulitumia hiyo namba nini Kilitokea

Shahidi: ailituma TSh Laki Tano Kupitia Namba Yake ya Tigo

Wakili wa Serikali: Ni Namba gani hiyo ya Tigo

Shahidi: Ni 0719933386

Wakili wa Serikali: Na Fedha hiyo alikutumia Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Wakili wa Serikali: pesa hiyo ilikuwa kwa Malengo gani

Shahidi: Kwa Malengo ya Kumpelekea Watu Kwenda Kufanya Uhalifu

Mawakili wa Serikali Wanateta Tena

Mawakili wa serikali wameitana kama Jopo tena, wananong’onezana hapa kwa sauti ya chini..

Wakili wa serikali: Shahidi Iambie Mahakama Baada ya Kupokea ile TSh Laki 5 Ulifanya nini

Shahidi: Cha Kwanza Nilimpigia Ramadhan Kingai Kwamba Freeman Mbowe ameshanitumia TSh 500,000

Akaniambia We Endelea Watumie hao watu Pesa halafu waende Huko Mahali ambapo Freeman Mbowe anataka Waende

Wakili wa serikali: lipi lingine ulilofanya

Shahidi: Siku ileile niliopata Pesa Nilimpigia Moses Lijenje, Nikamwambia Kazi Ipo tayari, Waje Morogoro

Wakili wa serikali: Ulipomueleza hayo

Shahidi: akasa anakuja mara Moja, Nikampigia Khalfani Hassan Bwire akasema na Yeye anakuja, Nikakutana nao Msavu Terminal

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kufika huko Ieleze Mahakama, ulizifanyia nini

Shahidi: Nilizitoa lakini hazikutoka zote, Kama 499,000 zikatoka

Wakili wa Serikali: Iambie Sasa Mahakama Wale Watu Ulionana nao, Bwire na Lijenje, Kwamba Kuna kazi ipo Kwa Freeman Mbowe, Nikamwambia kuwa nyinyi Mnakiapo, Nyinyi Ni Askari, Kile Kiapo Chenu hakija Vunjwa

Nikamwambia Kuwa mnaenda kufanya kazi Kwa Freeman Mbowe, kazi ya ulinzi lakini mnapokuwa Kwa Mwajiri wenu huko Mnapokwenda Huko mkiona Kuna mipango ya uhalifu Mtakuwa mnaniambia, nikatoa TSh Laki 3 kutoka katika Ile laki nne na tisini na tisa nikawapa

Wakili wa Serikali: Baada ya Maelekezo hayo Ukafanya nini

Shahidi: Nilpigia Freeman Mbowe, Kuwa wale Vijam wapo tayari, akaniamba walete, akaniambia nani atawapokea akasema Dereva Wangu Willy

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano Mliyokuwa mnafanya yalikuwa ya namna gani

Shahidi: Ya Mfumo Wa Telegram, Baada ya hawa Kuondoka, Kwenda Dar es Salaam, Nika Riport kwa Ramadhan Kingai Kwamba Moses Lijenje na Khalfani Bwire Wapo Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Tuambie Sasa Umepeleka Watu wawili, Nini Kikafuata

Shahidi: Freeman Mbowe akaniambia Bado, Ongeza wengine Wawili

Wakili wa Serikali: Baada ya kukueleza hivyo wewe Ulifanyaje

Shahidi: Nikaanza Kuwatafuta Watu wawili

Wakili wa Serikali: Ambao ni nani na nani

Shahidi: Ni Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya

Wakili wa Serikali: Walipatikana Vipi hawa wawili

Shahidi: Adam Kasekwa alipatikana kwa Njia ya Simu nilimpigia Simu

Wakili wa Serikali: Na Mohamed Ling’wenya

Shahidi: Mohamed Ling’wenya ndiye niliye Mpigia Simu, Yeye akampigia Simu Adam Kasekwa Wakaja Pamoja

Nilimwambia natafuta wengine akaniambia Kuna Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Ulikutana nao wapi hawa wawili

Shahidi: Nilikutana nao Msavu Stendi

Wakili wa Serikali: Msamvu umepataja Mara Mbili, Ni wapi huko

Shahidi: Ni Morogoro Mjini Eneo la Stendi

Wakili wa Serikali: Ulipokutana nao hao watu hapo Msamvu ulizungumza nao nini na mlikubaliana nao nini

Shahidi: Nilimwambia Freeman Mbowe anatafuta makomandoo waliofuzu kwa ajili ya ulinzi….. wakasema wapo tayari..

Wakili wa serikali: Baada ya Kusema Wapo tayari?

Shahidi: Laki Moja na tisini na Tisa Iliyobakia, nilimwambia Mtafanya kazi Iliyowapeleka, Lakini mkiona chochote ambacho cha uhalifu mtaniambia, Mohammed Ling’wenya Kwa Maneno yake aliniambia ASKARI HAWEZI KUWA RAIA ILA RAIA ANAWEZA KUWA ASKARI

Shahidi: Nikawaambia Chochote Kitakachotokea Wataniambia, Baada ya Hapo, Nilimpigia Freeman Mbowe akanitumia Laki Moja na Tisini na Tano, Kwa ajili ya nauli yao Kutoka Morogoro Kwenda Dar es Salaam..

Wakili wa Serikali: alituma Kwa namba ipi kwa Njia gani

Shahidi: alituma Kutoka Kwa Wakala,kuja Kwa namba yangu ya 0787 555200

Wakili wa Serikali: Nini Kilipelekea ukatumiwa Kupitia Kwa Wakala na siyo Kwa Simu yake

Shahidi: Nahisi Alimpa Mtu akaenda Kuitumia

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani Kilikufanya Utambue Kuwa Pesa hiyo Imetoka Kwa Freeman Mbowe

Shahidi: alinipigia na tulikuwa tuna Chat, Kwa hiyo Nili Cornfirm

Wakili wa Serikali: Uli Cornfirm Nini

Shahidi: Nili acknowledge Kwamba Nimepokea

Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo Ulifanya nini

Shahidi: Pesa ile niliwapa Adam kasekwa na Mohamed Ling’wenya Kwa ajili ya a nauli ya kutoka Morogoro Kwenda Dar es Salaam

Wakili wa serikali: Iambie Mahakama sasa Awali unasema Utumiwa Laki 5 ukawapa Moses Lijenje na Khalfani Bwire, na Sasa ukatumiwa hii, Pesa Nyingine Ulimpeleka Wapi

Shahidi: Niliwapa Kufidia Gharama zao, za Kutoka Walipokuwa, Sababu Walikuwa Mtwara

Wakili wa Serikali: Nani alikuwa Mtwara

Shahidi: Mohamed Ling’wenya

Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Sasa Baada ya Kuwa Umewapatia pesa nini Kiliendelea sasa

Shahidi: Walianza Safari ya Kutola Morogoro Kwenda Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Wewe Ukafanya nini Baada ya wao Kuanza Safari

Shahidi: Baada ya Kumwambia Freeman Mbowe kuwa Vijana wale wawili Wanakuja, akamwambia Khalfani Bwire kawapokeee

Wakili wa Serikali: Wewe Ulijuaje Kama alimwambia Khalfani Bwire akawapokee

Shahidi: Ni baada ya Kuwa Napiga Simu hazipokelewi, Nilimpigia Khalfani Bwire na akasema Ndiyo anaenda Kuwa pokea

Wakili wa Serikali: Shahidi niambie Wewe Uliambiwa Kuwa utafute Watu wa Kwenda Kufanya Matendo Ya Kihalifu alafu wewe Wale Watu Unawaambia Kuwa Wanaenda Kufanya Kazi ya Ulinzi, Ni Kwanini Ulifanya hivyo

Shahidi: Nilifanya hivyo Kwa Sababu za Kiusalama

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Kusema Sababu ya Ulinzi

Shahidi: hawa ni Askari, Bado Wanaviapo Vyao, Ukiwaambia Kwamba Mnaenda Kufanya Kazi ya Uhalifu wangeogopa, Na Wange’ spoil kazi Nzima, Tusingeweza Kuzuia Uhalifu

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Kuwa Umepeleka Kundi la Pili Ulifanya nini

Shahidi: Kwanza Kundi la Pili Liliondoka Tarehe 24 July 2020 Mwanzo Alikuwa Busy na Mimi, Baada ya Hapo hakuwahi Kupokea Simu yangu tena wala Kujibu Jumbe ya simu, Na Ndiyo Mara ya Mwisho Kuwasiliana na Freeman Mbowe

Shahidi: Nilipiga Simu Hapokei nikituma Jumbe hajibu

Wakili wa Serikali: Sasa tuambie Mawasiliano yako wewe na Adam Kasekwa baada ya Kuondoka yalikuwaje

Shahidi: Baada ya Wao Kuwa wameondoka Freeman Mbowe alikuwa hapokei Simu zangu

Wakili wa Serikali: hebu toka huko ushaelezaaaaaaa, Mawasiliano yako wewe na Adam Kasekwa yalikuwajeee?

Wakili wa Serikali: Mawasiliano yako wewe na Adam Kasekwa yalikuwaje

Shahidi: Sijawahi Kuwasiliana naye wala Sijawahi Kuwa na namba yake

Wakili wa serikali: Mawasiliano Yenu wewe na Mohamed Ling’wenya yalikuwaje

Shahidi: Nilikuwa nawasiliana na Mohamed Ling’wenya Kwa Njia ya WhatsApp

Baada ya Kupiga na Kuona sipokelewi Simu zangu, Nikawa namcheki WhatsApp Kwamba Kuna Mapya gani? Mmeambiwa nini?

Wakili wa Serikali: Majibu yake yalikuwa ni nini? 

Shahidi: aliniambia Kwamba Boss Wao atawaajiri na Kuwalipa Mishahara Kila Mwisho Wa Mwezi

Wakili wa Serikali: Huyo Boss Wao alikuwa ni nani

Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama sasa Mawasiliano yako wewe na Mohamed Ling’wenya yaliishia Wapi

Shahidi: Baada ya Kuniambia tuh+ Kuwa wataajiriwa yakaishia hapo, Kwa hiyo nikaendelea Kuwasiliana na Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Mawasiliano yako wewe na Khalfani Bwire yalikuwaje

Shahidi: alikuwa yupo bize Mara Nyingi, Nikataka Kujua Yupo Wapi na wanafanya nini, Bwire akaniambia Bro Tupo Dar es Salaam sasa hivi lakini tunatakiwa Kwenda Moshi Kwa Sababu Kuna kazi tunaenda Kufanya

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea

Shahidi: Nilimuuliza kazi gani akajibu sijui, Tukawa tumeishia hapo

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Kuwasiliana naye, Siku gani Nyingine Mliwasiliana

Shahidi: Baada ya Kuona Kimya, Ilibidi nipigie Simu Siku ya Tarehe 04 August 2020

Wakili wa Serikali: Ikawaje

Shahidi: Nikamsalimia, Tukasalimiana, akaniambia Bro Samahani, Sijakutafuta Kama Ulivyonielekeza Kwa sababu tumekengeuka

Jaji: Kuna Kiswahili Kingine Cha Kukengeuka

Shahidi: Kwamba Samahani Tulikuwa Tumepitiwa

Kazi Uliyotuambia temekuja Kufanya Ya Ulinzi Kwa Freeman Mbowe imebadirika siyo hiyo, Kwamba Freeman Aikael Mbowe ametushawishi Kufanya kazi Nyingine.. Ambayo hivi sasa tunavyoongea, Wale Madogo (Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya) Wapo Moshi sasa hivi

Na Lijenje Wapo Moshi Wamepewa kazi ya kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.. Na kabla ya Tarehe 07 August 2020 Wanatakiwa Wawe Wameshamaliza kazi hiyo na Kurudi Dar es Salaam,

Kwa Sababu Tarehe 12 August 2020 Kuna kazi Nyingine Wanayo kuja Kufanya Dar es Salaam Kuja Kulipua Vituo Vya Mafuta.. Hiyo ndiyo Mwisho wa Taarifa Niliyopokea Kwa Khalfani Hassan Bwire

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukupa Taarifa hiyo Ulifanya nini

Shahidi: Baada ya Kunipa Taarifa Nilimwambia aendelee Kuwasiliana na Mimi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umepokea Taarifa hiyo

Shahidi: Baada ya Kunipa Taarifa hiyo ilikuwa Saa Mbili Asubuhi Kuelelea Saa Tatu instantly Nikampigia ACP Ramadhan Kingai simu

Wakili wa Serikali: Baada ya kumpigia Simu ulimwambia Yepi?

Shahidi: Baada ya Kunipa Taarifa hiyo ilikuwa Saa Mbili Asubuhi Kuelelea Saa Tatu instantly Nikampigia ACP Ramadhan Kingai simu

Wakili wa Serikali: Baada ya kumpigia Simu ulimwambia Yepi?

Hivi sasa wote Moses Lijenje, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya wanatembelea (Kufanya Surveillance) Maeneo ambayo Mkuu wa Wilaya Ole Sabaya Anayopenda Kutembelea Mji wa Moshi na Arusha…. Mwisho wa Taarifa yangu Kwa Kingai

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Taarifa ya Kutembelea Maeneo Mbalimbali ambayo Mkuu wa Wilaya anapenda Kutembelea Wewe Ulizitoa wapi

Shahidi: Tarehe 04 August 2020 niliongea na Khalfani Bwire, Ndiye aliyenipa Taarifa hizo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umemaliza Kutoa Taarifa Kwa Ramadhan Kingai Ukafanya Nini

Shahidi: Alisema tu, Nashukuru kwa Taarifa nitafuatilia

Wakili wa Serikali: Mimi Tarehe 05 August 2020 nilimpigia Khalfani Bwire akaniambia Bwana Wale Madogo wamekamatwa

Wakili wa Serikali: Ni Madogo gani alikwambia wamekamatwa

Shahidi: aliniambia ni Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya

Wakili wa Serikali: Shahidi alikueleza Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Ling’wenya wamekamatwa na nani

Shahidi: Hakusema Wamekamatwa na nani, Nilicho Muuliza Boss wenu anafahamu?

Wakili wa Serikali: boss wenu, Ni nani huyo

Shahidi: ambaye ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: ulipomujoji Juu ya hilo yeye alikwambia nini? 

Shahidi: aliniambia anafahamu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa wewe umezungumza naye, Nini Kiliendelea

Shahidi: Nilichukua Hatua Ya Kumpigia Freeman Aikael Mbowe, Hakupokea, Nilipiga tena na tena simu Hakupokea, Kumbuka Tangu Tarehe 24 July alikata Mawasiliano na mimi

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi Baada ya Kuwa Umempigia Simu na Hakupokea, Nini Kilifuata

Shahidi: Baadae Nilikuta Ujumbe wa Telegram Kwenye akaunti yangu ambao unasema, “Nimeshindwa Kupokea Simu ya Kawaida Kwa Sababu ya Deshi Deshi Deshi, Najua umenielewa” ilikuwa ni Tarehe 06 August 2020

Wakili wa Serikali: Hizi Deshi Deshi Deshi ni Kitu gani

Shahidi: Ni Vile Vinukta Nukta… Mbele akaniuliza Any NeWakili wa Serikali?

Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama sasa, Wewe Ulielewa nini

Shahidi: Mimi siwezi kuwa na Tafsiri sahihi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji shahidi katoa ushahidi wake unasema alikuta ujumbe unasema “najua umenielewa”, Sisi tumeuliza ameelewaje, amesema hawezi kuwa na tafsiri sahihi.. Lakini sisi tuna achana na hilo suala hatutoendelea nalo…

Wakili wa Serikali: Hebu sasa iambie Mahakama Baada ya hapo Nini Kilifutia

Shahidi: Baada ya hapo wala sikuhangaika naye, Bwire naye alinipigia simu hiyo tarehe 06 wala sikupokea

Wakili wa Serikali: Kwanini hukupokea simu ya Bwire? 

Shahidi: Ni kwa sababu lengo limeshatimia

Wakili wa Serikali: lengo gani hilo? 

Shahidi: Sababu nishajua wamekamatwa sasa naongea naye nini?

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini kiliendelea

Shahidi: Tarehe 10 August 2020 Majira ya Saa 9 au Saa 10 alinipigia DCP Ramadhan Kingai Akanitaka niende Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Shahidi: nikakutana na afisa wa Jeshi LA Polisi anaitwa Inspector Swila akanitumia na namba zake za Simu

Wakili wa Serikali: Alikwambia Uende Makao Makao Makuu ya Polisi Yaliyopo wapi?

Shahidi: Jiji la Dar es Salaam, Eneo la Posta Mapya Yaliyopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Wakili wa serikali: Wakati huo Wewe Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikwepo Morogoro

Wakili wa serikali: Wewe Ulichukua Hatua zipi

Shahidi: Nilichukua Hatua Ya Kutoka Morogoro Kuja Dar es Salaam Siku ya Tarehe 10 August 2020 nikaja Dar es Salaam kwa ajili ya Kumuona Inspector Swila Tarehe 11 August 2020

Wakili wa Serikali: Tuambie Sasa hiyo Siku ya Tarehe 11 August 2020 Ulifanya nini

Shahidi: Siku ya Tarehe 11 August 2020 Nikaenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Nika fuata Procedure ya Jeshi la Polisi

Wakili wa Serikali: Shahidi Procedure Zipi

Shahidi: Kujitambulisha, Kutoa Kitambulisho Changu na Kwamba Nimeitwa na Inspector Swila, Nilipofika Reception ya Pili alishuka Kuja Kunichukua Mpaka Ghorofa ya 8..

Wakili wa Serikali: Mlipanda Kwa Njia gani

Shahidi: Niliwapanda Kwa Ngazi Kwa Maana Lift Ilikuwa Mbovu

Wakili wa Serikali: Mlipofika Ghorofa ya Nane nini Kiliendelea

Shahidi: Kwamba amepewa Maelekezo anichukue Maelezo Ya Matukio

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukueleza hayo Wewe Ulimwambia Nini

Shahidi: Nilimueleza Kuhusu, Khalfani Bwire na Wenzie Pamoja na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Baada ya Kuwa amekuchukua maelezo nini Ulifanya

Shahidi: alinichukua Maelezo, nikasaini Maelezo akaniomba Nimuachie simu

Wakili wa Serikali: Simu gani aliyokuomba Umuachie

Shahidi: Simu nilivyokuwa nayo, aliniambia Kwa sababu ya Uchunguzi, Mawasiliano nilivyokuwa nafanya kati yangu Mimi na akina Bwire pamoja na Freeman Mbowe.

Wakili wa Serikali: Shahidi Wakati anakwambia hayo, hiyo simu ilikuwa Ipo wapi

Shahidi: Baada ya Kusema hivyo Nikamwambia Kwamba nilikuwa nafanya Mawasiliano na Simu zangu Zote, Basi akataka Nimuachie

Wakili wa serikali: Wewe Ulikuwa unatumia Simu Ngapi Kuwasiliana na Watu hawa

Shahidi: Simu Nne

Wakili wa Serikali: Unaweza Kunitajia Mahakama hizo Simu Nne uliokuwa Uliwasiliana na hao Uliowataja

Shahidi: Ya Kwanza ni TECNO CAMMO simu ya Pili ni TECNO C9, simu ya tatu ni itel na Nyingine ni Samsung ya Tochi

Wakili wa serikali: Sasa Shahidi iambie Mahakama, katika simu hizo Ulikuwa ukitumia Mitandao gani ya simu

Shahidi: Nilikuwa natumia Airtel, Vodacom, Hallotel na Tigo Kwa Tanzania

Wakili wa Serikali: Ulisema Kwa Tanzania Unamaanisha nini

Shahidi: Pia Nilikuwa na Line nilivyokuwa natumia Sudan

Wakili wa Serikali: ambazo hizo Line uliokuwa unatumia Sudan ni zipi

Shahidi: MTN na ZAIN

Wakili wa Serikali: Tuambie Sasa, ulipotakiwa Kuacha Simu zako Wewe Ulifanya Nini

Shahidi: Kitu cha Kwanza Kwa sababu sikujua Kama naenda kuacha Simu zangu, Nilitoa Line ya Voda katika Su ya Tecno CAMMON, nikaweka katika Simu Ya Tochi ya Samsung, halafu nikamwambia tarehe 12 nitaenda Kuchukua Hizo Simu zingine Kisha nitamletea

Wakili wa Serikali: Hebu Iambie Mahakama Ulipomuachia simu Yako, Taratibu gani zilifuatwa?

Shahidi: alichukua ile simu akafungua ndani akai’ register kwenye Document IMEI namba

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufanya hayo.?

Shahidi: alisaini na Mimi nikasaini, Mimi akanipa Copy

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama ile Nyaraka Unayosema Iliandikwa ukadainishana Ka Ukiiona unaweza Kuitambua

Shahidi: Naweza Kuitambua

Wakili wa Serikali: Mambo Yepi yatakufanya Utambue hiyo Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mambo Yepi yatakufanya Utambue hiyo Nyaraka

Shahidi: Ni sahihi Yangu

Wakili wa serikali: Ile Nyaraka yenyewe halisi Baada ya Kusaini Shana Ilienda wapi

Shahidi: alibakia nayo Inspector Swila

Wakili wa serikali: Baada ya Kumuachia na Kuchukua Nakala yako nini Kiliendelea

Shahidi Nilimwambia Kwamba Simu ambazo nilikuwa nafanya nazo Mawasiliano ambazo

Shahidi: ambazo sijaja nazo nitamletea Tarehe 12 August 2020

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini Kilifuata

Shahidi: Niliondoka Kurudi Morogoro Kesho yake nikamletea Simu 3

Wakili wa Serikali: Ulirudi lini Morogoro?

Shahidi: Siku hiyo hiyo

Wakili wa Serikali: Tuambie Sasa Tarehe 12 August 2020 Nini Ulifanya

Shahidi: Nilienda Kuchukua simu tatu, Tecno C9, Itel Pamoja na Samsung ya Torch

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Simu hizo Ulizochukua Kuzipeleka wapi

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, Maeneo ya Posta Mpya Kwenye Ofisi za DCI kwa Inspector Swila

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji natazama sasa ni Saa 11 Kasoro Dakika 10 na sisi Bado tuna Maswali zaidi, Lakini pia amekuja Afisa wa Magereza Kutukumbusha Sababu hiyo

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, Maeneo ya Posta Mpya Kwenye Ofisi za DCI kwa Inspector Swila

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji natazama sasa ni Saa 11 Kasoro Dakika 10 na sisi Bado tuna Maswali zaidi, Lakini pia amekuja Afisa wa Magereza Kutukumbusha Sababu hiyo

Jaji: Kufuatia maombi yaliyoletwa na Jamhuri na Kuungwa mkono na upande wa utetezi l, nahairisha shauri hili mpaka kesho tarehe 27 January 2022,

Shahidi utatakiwa kuendelea kuwa mahakamani kutoa ushahidi wako

Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho Asubuhi saa 3 kamili asubuhi 

Jaji anatoka Mahakamani

Like
1