Kesi ya Mbowe: Shahidi muhimu akiri kuwa amezoea kusema uwongo

WAKILI NASHON: Wakati ule unampigia unamuuliza ‘upo tayari, kuna kazi ya ulinzi,’ wewe moyoni ulikuwa unajua kuwa Mbowe hahitaji walinzi bali ni vijana wa kuambatana naye? SHAHIDI: Ni sahihi. WAKILI NASHON: Kwahiyo ni sahihi uliwadanganya pia watuhumiwa wa pili na watatu? SHAHIDI: Ni sahihi. WAKILI NASHON: Kwani shahidi, mwaka 2012 ulikuwa na rank (cheo) gani? SHAHIDI: Nilikuwa na rank ya Koplo. WAKILI NASHON: Ni sahihi kwamba ulipokutana na Freeman Mbowe akakudodosa kuhusu rank yako, ulimdanganya kuwa huna rank? SHAHIDI: Ni sahihi.

Kama ilivyoletwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 27 Januari 2022.

Jaji ameingia Mahakamani Muda huu.

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa Wakili wa Serikali: Robert Kidando: nipo pamoja na wakili Pius Hilla

Abdallah Chavula

Jenitreza Kitali

Nassoro Katuga

Esther Martin

Tulimanywa Majige

Ignasi Mwinuka

Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo na Shahidi: Mmoja ambaye Jana Alianza Kutoa UShahidi: Wake, Tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea

Jaji nakukumbusha kuwa Jana Ulikuwa Kiapo, na Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili Abdallah Chavula ataendelea Kumuongoza Shahidi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

Nashon: Nkungu

John Malya

Dickson Matata

Michael Mwangasa

Paul Kisabo

Seleman Matauka

Alex Massaba

Maria Mushi

Hadija Aron

Evaresta Kisanga

Michael Lugina

Sisty Aloyce. 

Wakili wa Serikali: akimuhoji shahidi: wake Dennis Urio..

Wakili wa Serikali: Jana tuliishia 12 August 2020, Je Iambie Mahakama Wewe Ulifanya nini

Shahidi: Nilipeleka Simu ambazo sikwenda nazo Kwa Inspector Swila

Wakili wa Serikali: Ulimpeleka Wapi

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Simu hizo tatu ulizo Mpelekea Inspector Swila Zilikuwa ni Mali ya nani

Shahidi: Zilikuwa ni Mali yangu

Wakili wa Serikali: Simu hizo tatu zilikuwa za aina gani

Shahidi: Techno C9, Itel na Sumsumg Ndogo ya Tochi

Wakili wa Serikali: Hebu tueleze Sasa nini Kilitokea Ulipofika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Shahidi: Baada ya Kufika Nilikutana na Inspector Swila Nikamkabidhi Simu zote, Kwa Kuni kabidhi Nyaraka ambayo Niliandika Majina yangu, Ilikuwa ina IMEI namba Baada ya Hapo a Kaandika Majina yake, nikasaini na Yeye akasaini

Wakili wa Serikali: Kwa Hiyo Jumla Nyaraka Ngapi zilizokabidhiwa

Shahidi: Jumla ni Nyaraka Nne

Wakili wa Serikali: Kwa Siku hiyo ya Tarehe 12 August 2020 ziliandaliwa Nyaraka Ngapi

Shahidi: Nyaraka Tatu

Wakili wa Serikali: Nani alizi andaa zile Nyaraka

Shahidi: Alizi andaa Inspector Swila

Alinipa nikasaini Kazi toa Kopi akanikabidhi

Wakili wa Serikali: Shahidi: Nikurejeshe Kwenye Nyaraka Iliyoandaliwa Tarehe 11 August 2020, Iliyoandaliwa na Inspector Swila

Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Kwa Majina Yangu Matatu, Denis Leo Urio, Nitaitambua Kwa Tarehe Niliyokabidhi ambayo ni Tarehe 11 August 2020, Nitaitambua Kwa Sahihi Yangu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi: Nyaraka aweze Kuitambua

Wakili wa Serikali: Shahidi: Hebu Tizama hii Karatasi kwa Makini, alafu Iambie Mahakama Kama Unaifahamu

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naitambua Nyaraka hii Kwamba Nilisaini Mimi, Kwamba ina Majina yangu Matatu, Ina IMEI namba ya Simu yangu ya Techno,

Wakili wa Serikali: Majina yako Yapo

Shahidi: Ndiyo Yapo

Wakili wa Serikali: Je Tarehe ipo

Shahidi: Tarehe ipo

Wakili wa Serikali: Ulisema Utaitambua Kwa Sahihi yako, Je Ipo.?

Shahidi: Ndiyo ipo

Wakili wa Serikali: Sasa Ungependa Mahakama Ifanye nini Juu ya hiyo Nyaraka

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Ningependa Mahakama itambue hiyo Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi: anaomba itambue Kama Kielelezo

Wakili Peter Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Shahidi: ajasema Ipokelewe Kama Kielelezo, Bali amesema Anaomba Mahakama itambue Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi ni Maafisa Wa Mahakamani tuna Wajibu wa kusaidia

Jaji Wakili Kibatala

Kibatala Mheshimiwa kama Anaomba Kwa ajili ya a Utambuzi Ibakie hivyo

Nashon: Nkungu:  Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Nyaraka Onaombwa kwa ajili ya Utambuzi Hatuna Pingamizi

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji na Mimi pia sina Pingamizi Juu ya Utambuzi

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji na Mimi Sina Pingamizi Juu ya Utambuzi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji namimi pia Sina Pingamizi Ka Nyaraka Inapokelewa kwa ajili ya Utambuzi

Nyaraka Inatoka Benchi la Utetezi Kwenda Katika Meza ya Jaji Pale Juu..

Tukio limewaacha MaWakili wa Serikali: Wakiteta na Mshangao Mkubwa, Badala ya Shahidi: Kusahau Kusema anaomba Ipokelewe Kama Kielelezo

Jaji: Naipokea Nyaraka Kamq ID namba 2

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Wakili wa Serikali: Shahidi Awali Ulieleza Mahakama Kwamba Siku ya Tarehe 11 August 2020 Ulimkabidhi Simu TECHNO CAMMO Inspector Swila

Je Simu hii Ukiona Utaweza Kuitambuaje

Shahidi: Simu yangu Techno CAMMO, Ina Cover Jeusi, na Screen Protector Imepasuka Upande Wa Kulia

Wakili wa Serikali: Kingine kitachokufanya Utambue

Shahidi: Kama Ukiwasha inatoka Picha ya Familia Yangu Kwenye Screen Saver

Wakili wa Serikali: Unaposema picha ya Familia Unamanisha Nini

Shahidi: Nime save Kwemye Screen Saver Ina Display Picha Ya Mke wangu

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Nikienda Kwenye Program ya Telegram nitakuta Mawasiliano Baina yangu Mimi na Mbowe, Mawasiliano Ya Meseji

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama itupatie Kielelezo Cha Mashitaka Namba 34

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumkabidhi Shahidi: Kielelezo hiki, Kwa ajili ya Utambuzi

Wakili wa Serikali: Shahidi: Hebu Tazama hii Simu, Jaribu Kuangalia Yale uliyokuwa Unaeleza Mahakama Kama Yapo

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Mwonekano Wa Nje hii Ndiyo Simu Yangu yenyewe

Wakili wa Serikali: Mwonekano gani Wa Nje

Shahidi: Cover Jeusi

Screen protector kupasuka Kwa Juu

Simu yenyewe ni TECHNO CAMMON

Wakili wa Serikali: Shahidi Vipi Kuhusiana na Yale Mengine

Shahidi: Mpaka niwashe Simu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Shahidi: awashe Simu

Jaji Utetezi Je

Kibatala Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji.

Shahidi: anawasha Simu akiwa amesimama Kizimbani, Vidole Vinatetemeka

Shahidi: Hii Ndiyo Picha ya Mke wangu

Wakili wa Serikali: Ionyeshe Mahakama, Mahakama ione

Jaji: Wakili Malya, Ungependa Uone Picha ya Mke wake

Wakili John Malya: Hapana Mheshimiwa Jaji, Tunateta Jambo Jingine Kabisa

Shahidi: Mawasiliano yangu ya Ujumbe Mfupi Kati yangu Mimi na Freeman Mbowe haya hapa

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano yapo Kwenye nini

Shahidi: Tulikuwa tuna wasiliana Kwa Mfumo wa Telegram

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wanaomba Kujiridhisha

SIMU Inapelekwa kwenye Benchi la Utetezi

Wakili Kibatala Anaenda Kwa Shahidi: Kizimbani Kuangalia Mawasiliano Ya Telegram Kwenye Simu

Wakili John Malya: na Yeye anaomba Kwenda Kizimbani Kwa Shahidi: Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji namimi naomba Kwenda Kujiridhisha

Matata anafika na Kukagua Simu ya Shahidi

Bado Wakili Matata Yupo Kizimbani

Wakili Nashon Nkungu Na Yeye anaenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi

Nashon Nkungu:  Mheshimiwa Jaji Asante Sana

MaWakili wa Serikali: Wanateta Kwa Pamoja

Wakili wa Serikali: Shahidi hizo Meseji Ulizo Onyesha Mahakama Unaweza Kuzisoma.?

Shahidi: July 2020, Kaka Wa Mtu tatu ni Muhimu sana

Yeye Bro Kuna Members Wawili Mpaka sasa, Mmoja Yupo Tunduma na Mmoja Yupo Dodoma

Security Ni Muhimu Sana, Wasije kutelekezwa

Siwezi Kuwatelekeza

Naomba Unitumie Nauli ya Kuwa Mobilise Niende nao Moro

Kwa Namba Ipi

Laki 5 inatumwa

Nashukuru Nimepata

Usiwe Unatumia Namba yako Binafsi Kutuma, Tumia Watu wengine au Wakala

Wapo Wapi Bro

Nipo nao Njiani

Mkuu Shikamoo Vipi Maendeleo ya Magonjwa wako

Wale Watu wawili nipo nao nasubiri Maelekezo yako Kaka

Nashukuru, Je and anaweza Kuja Dar

Naomba Unitumie Nauli na Dar Wapi watafikia

Wanaweza Kuja Dar na Kesho Wa kaenda Hai

Nitumie Nauli

Kwa namba ipi

Kwa namba yangu

Usitume Kwa namba yako

Nita tuma Gari ya kuwapokea Ubungo

Namba ninayo wa tumia ni Ya Dereva Wangu anaitwa Willy yeye Ndiye atakaye Wapokea

Nashukuru Nimepata

Asante Bro Hope Wameondoka

Wawili Wapo Ruvu Wawili bado

Uwe unatuma Pesa ya a Kutosha ya akuwa Mobilise

Kaka bado Nipo Kamati Kuu, Tuma Meseji

Shikamoo Kaka Vipi Magonjwa wako

Wale Wapo Tayari Kuondoka

Nilishindwa Kupokea Su yako sababu ya Deshi Deshi

Naamini umenielewa, Mwisho wa Kunukuu

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano Uliyokuwa Ukiyasoma Yalikuwa ni Baina ya nani na nani

Shahidi: Ni Baina yangu Mimi na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi: Hebu Rejea Meseji ya Kwanza Kusoma

Shahidi: Kaka wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu Sana, Siku zimekwisha

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Hao Mtu tatu au Nne Nini hasa a Kilikuwa kinazungumzwa

Shahidi: Nilikuwa Nimeongea naye hapo NYUMA kuhusu Kuwatafuta Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya na Moses Lijenje Kwamba hata hao waende Siku zinaenda

Wakili wa Serikali: Huo Ujumbe Ulikuwa Unatoka Kwa nani

Shahidi: Unatoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu.

Wakili wa Serikali: Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 14 na Sekunde 50

Shahidi: Ya Tarehe ngapi

Wakili wa Serikali: Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Mmoja Kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986

Wakili wa Serikali: Ni nani alikuwa kazaliwa Mwaka 1980

Shahidi: Ni Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Ni nani kazaliwa Mwaka 1986

Shahidi: Ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Tarehe hiyo hiyo 30 Mwezi July 2020, Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 2

Shahidi: Bro Kuna Members Wawili Mpak Saa hizi, Mmoja Yupo Tunduma anahusika na Magari ya kwenda nje na Mwingine yupo Dodoma SGR

Wakili wa Serikali: Huyo aliyepo Tunduma anafanya Kazi ya Kusafirishia Magari Kwenda Nje ni nani

Shahidi: Ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Na Mwingine anaye fanya kazi SGR Dodoma ni nani

Shahidi: Ni Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Haya Inayofuata Baada ya hiyo, Isome

Shahidi: Simu Siyo Salama, Niweze she niweze Kukutana nao

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo kwenda kwa nani

Shahidi: Niliandika Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Ulimaanisha nini Kusema Simu Siyo salama

Shahidi: Simu Siyo Salama, Kum Ensure Kuwa Hakuna Mtu wa Kututrack

Wakili wa Serikali: Soma Inayofuata

Shahidi: Kikubwa ni Security ya Shughuli zao Wanazofanya Saa hizi, Wasije Kutelekezwa baadae

Wakili wa Serikali: Meseji hiyo ni ya nani

Shahidi: Inatoka Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Hao wawili Kwaa kuanzia Siyo Mbaya, Hawawezi Kutekelezwa, Wanakuwa na Mimi Full time, Wamekwambia Wanataka nini.?

Wakili wa Serikali: Meseji hii ilikuwa Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Neno hawa Wawili Kuanzia Siyo Mbaya ni akina nani hao

Shahidi: Ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Enheeeee Meseji inayofuata

Shahidi: Sema Tuh Kaka nifanyeje

Wakili wa Serikali: Hiyo Meseji Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Meseji ainayofuata

Shahidi: Mmoja kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986

Wakili wa Serikali: akiyezaliwa Mwaka 1986 ni nani

Shahidi: Ni Moses Lijenje na Mwaka 1986 ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Soma inayofuata

Shahidi: Naomba Unitumie Nauli ni Mobilise nikutane nao Morogoro.

Wakili wa Serikali: Nani hao Uwa Mobilise, na Meseji Imetoka Kwa na nani Kwenda Kwa nani

Shahidi: Meseji Imetoka. Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe, Wakukutanao Moro ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Shahidi: naKurudisha Nyuma, Kuna a Meseji hao wawili Kuanzia Siyo Mbaya walikuwa wakina nani na Siyo Mbaya ni nini hasa

Shahidi: Alikuwa ni Moses Lijenje na Khalfani Hassan Bwire

Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata

Shahidi: Kwani Kiasi gani na Kwa Simu ipi

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji

Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Mlikuwa Mnazungumzia Kiasi cha Nini

Shahidi: Kiasi cha pesa

Wakili wa Serikali: Kwa ajili ya Shughuli gani

Wakili wa Serikali: Kwa ajili ya nauli ya Kuwa chukua Khalfani Bwire na Moses Lijenje Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Meseji ilikuwa ni ya nani na inaenda kwa nani

Shahidi: Ya Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Soma hapo

Shahidi: Laki 5, 0787 555200

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji

Shahidi: Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Sawa, Tayari kaka

Wakili wa Serikali: Meseji Imetoka Kwa nani.

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Nashukuru Nimepata broo 

Wakili wa Serikali: hii nayo imeandikwa na nani Kwenda Kwa Nani

Shahidi: Kutoka Kwangu Kwenda Kwa mbowe

Wakili wa Serikali: Tusomee Meseji ya Mwisho Kabisa

Shahidi: Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu ya Deshi Deshi Deshi naamini Umenielewa

Wakili wa Serikali: Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Shahidi: izime hiyo Simu alafu Irejeshe Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nirejeshe Kielelezo P34

Wakili wa Serikali: Shahidi: Ulimpeleka Simu Kwa Inspector Swila aina ya Techno C9 Je Simu hiyo Ukiona Kipi Kitaku fanya Utambue

Shahidi: Upande wa Kushoto Juu Housing Imepasuka, Ukiwasha haiwezi Kuwaka, Haiwezi Ku Display Kitu,

Vilevile Inarangi Nyeusi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo P28

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Ruhusa yako naomba ni Muonyeshe Shahidi: Kielelezo

Wakili wa Serikali: Shahidi: habu itizame hii Simu

Shahidi: Hii ni Simu yangu aina ya Techno C9, Sababu Nimeitambua Kwenye Housing yake Juu Kushoto imepasuka, alafu Ina Rangi Nyeusi, na Uki switch On haiwezi Kuonyesha

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Ruhusa ya Mahakama Shahidi: aweze Kuiwasha Simu

Shahidi: Haiwaki

Wakili wa Serikali: Shahidi: Ukazungumza tena Siku hiyo Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila,simu aina ya Itel, Je Utaitambuaje.

Shahidi: Mfuniko, Yani Cover ina Rangi Ya Blue Nyuma, Screen Protector Yake Mbele Juu Imepasuka, Ukiwasha itakuwa Na Picha Kwenye Screen Saver Either Mke wangu au Watoto Wangu au Wote

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tupatiwe Kielelezo namba 33

Wakili wa Serikali: Shahidi: Hebu Tizama hii Simu, Tuambie

Shahidi: Nimeitambua hii Simu aina ya Itel, Kama Nilivyosema Kuwa Ina Housing ya Blue na Juu Kwenye Screen Kipo Chake Kimebanduka

Wakili wa Serikali: Shahidi: Vilevile Unasema Siku ile ya Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila Ulikabidhi Simu aina ya Samsung Je Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Ni simu Ndogo, Samsung ya torch lakini Pia Chini Kwenye eneo la Earphone Kulia Imekatika

Wakili wa Serikali: habu Shika Simu hii, utueleze.

Shahidi: Naitambua ndiyo Simu yangu ndogo Samsung ya Torch, nyeupe na lakini Kwenye earphone Plug ni nyeupe

Wakili wa Serikali: Shahidi: Hebu tuambie Sasa, awali wakati tunakuhoji Uliambia Mahakama Kwamba Ulifahamiana na FREEMAN MBOWE Kuanzia Mwaka 2012 Mpaka Mwaka 2020, Je ilikuwa Ina Maana Gani

Shahidi: Nilikuwa na Maana Kwamba, Baada ya Ku Hitaji Vijana Wa a kwenda Kuchukua Dola na Kuwapata alikata Mawasiliano na Mimi Kuanzia Tarehe 24 July 2020 alikata Mawasiliano na Mimi

Wakili wa Serikali: Shahidi: tuambie Mahusiano yenu Baina yako wewe na Freeman Mbowe Kiujumla yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri, lakini alikata Mawasiliano na Mimi, Wala sijui alikata Mawasiliano na Mimi

Wakili wa Serikali: Jumla ya Kiasi gani Cha Fedha Ulicho pokea Kutokana Kwa Freeman Mbowe Uliyokuwa Unapokea Kwa ajili ya Kumpelekea wale Watu

Shahidi: Jumla ni Tsh 699,000

Wakili wa Serikali: Shahidi: tuambie Umekuwa Unamtaja Freeman Mbowe Mara Nyingi Sana, Je Ulimuona Unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Sababu Ipi itakupekea kumtambua

Shahidi: Body Morphology, anapenda Kuvaa Miwani, Mnene Kiasi na Mweusi Kiasi

Wakili wa Serikali: Sasa tuambie Kama yupo Hapa Mahakamani.

Shahidi: Yule Pale Kavaa T shirt, Kavaa Miwani

Mahakama: Kichekoooooo, Maana Mbowe ajavaa Miwani Leo

Wakili wa Serikali: Shahidi eleza Basi, Unasema Ulipo pokea Ujumbe kutoka Kwa Freeman Mbowe, Ujumbe Ule wewe Ulienda Kutolea Taarifa Boazi DCI na Ramadhan Kingai, Ukiacha hao wawili Nani Mwingine uliye wahi Kumpeleka Taarifa hiyo

Shahidi: Sikuwahi Kumpa Mtu yoyote Taarifa

Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama ni Kwanini Hukwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa wako wa kazi Jeshini

Shahidi: Si kwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa zangu wa kazi Kwasababu ni Taarifa za Uhalifu, Ndiyo Maana Nilienda Moja kwa Moja Kwa DCI Kwenye Vyombo Vya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Shahidi: Iambie Mahakama Ni wakati Gani Ulipeleka Taarifa Kwa Viongozi wako

Shahidi: Nilipeka Taarifa Kwa Viongozi………..

Wakili JOHN MALYA… Mheshimiwa Jaji hiyo ni Leading Question, Hakuna Sehemu Shahidi: anasema Kuhusu Viongozi wake

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Labda alikuwa hanifuatilii, Mwanzo Nili uliza Kabla

Wakili JOHN MALYA: bado haja Jibu Hoja

Jaji: Rudia Swali

Wakili wa Serikali: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo Ulimwambia nani

Shahidi: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo nilimwambia Kiongozi wangu

Wakili wa Serikali: Unaposema Kiongozi Wako Unamaanisha nini

Shahidi: Ni Mkuu wa Kikosi ninacho fanyia Kazi cha 92KJ

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu ni hayo tuh

Wakili wa Serikali anaishia hapa sasa anaingia Wakili wa Utetezi.

Wakili wa Serikali anakaa Chini

Sasa anaingia wakili wa Utetezi Nashon: Nkungu

WAKILI WA UTETEZI NASHON NKUNGU  AKIMHOJI SHAHIDI WA SERIKALI DENNIS URIO..

Wakili Nashon: Nimesikia Mwanzo Unasema Wewe ni Mkristo

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Dhehebu gani

Shahidi: Roman Catholic

Nashon: Unasali Wapi

Shahidi: Huko Ngerengere

Nashon: Unasali Jumuiya

Shahidi: sababu Ya Majukumu siudhurii Mara kwa Mara

Nashon: Unafahamu a kwamba Baada ya Kesi hii Unaweza Kutoka Kama shujaa au Mtu asiye na Thamani Duniani

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Msemo unaosema Kuwa ni Heri Kufa Jasiri Kuliko Kuishi Katika Utumwa

Shahidi: ndio 

Nashon: Unafahamu Kwamba Kesi hii Inafuatiliwa Nchini na Duniani Kote

Shahidi: …..

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyuma ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Naomba Mheshimiwa Jaji arudie hapo

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyima ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Hata sasa Nipo Pamoja na Jeshi

Nashon: Baada ya Kueleza hayo, Naamini Umetafakari Vizuri

Nashon: tuanze hapo Unaposema Jeshi lipo na wewe, Kivipi

Shahidi: Wanafahamu Kuwa nimekuja Kutoa Ushahidi

Nashon: Nikisema Kwamba Hujatoka kazini Kwako Utakataa

Shahidi: Ndiyo Nimetoka Kazini Kwangu.

Nashon: Je Unaruhusa au Movement Order

Shahidi: Ndiyo ninayo

Nashon: Unayo hapo Mahakamani

Shahidi: Hapana Nimeiacha Hotelini

Nashon: anaitwa Nani

Shahidi: CO wangu

Nashon: Anaitwa nani

Shahidi: Siwezi Kumtaja hapa Mahakamani

Nashon: kwanini uwezi Kumtaja

Shahidi: Mpaka Nipate Maelekezo Ya Kutaja Viongozi Wa Ulinzi

Nashon: Maelekezo Kutoka kwa nani

Shahidi: Mahakama

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba apewe Ruhusa a nitajie

Jaji: Shahidi. Kwani Mahakama Imekukataza

Shahidi: Anaitwa Light Keno CJP

Nashon: Nimesikia Unasema Kwamba Kikosi Chako Cha 92 KJ, Je Kuna kikosi kingine

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Kitaje

Shahidi: Siwezi Kutaja Mambo ya Jeshi

Nashon: Kwanin

Shahidi: Kwa sababu Kesi Inafuatiliwa ndani na Nje ya Nchi na Nina Kiapo

Shahidi: Hapa Umekula Kiapo Kingine

Shahidi: Ndiyo siwezi Kutaja

Nashon: Mheshimiwa Jaji Naomba atutajie

Jaji: Naona Kasha Sema Hawezi Kusema

Nashon: Twende Sehemu Nyingine, Je Kwa Mwaka Mnatoa Makomandoo Wangapi

Shahidi: Siwezi Kusema Pia

Nashon: Uwezi Kusema kwa sababu utaki au Kiburi

Nashon: Kwa sababu ni Siri

Nashon: Tutajie Siri zingine ili tusikuulize

Shahidi: Siwezi Kusema

Nashon: Haya na wewe Kozi yako ya Mwisho Ya Ukomandoo Ulifanya lini

Shahidi: Mwaka 2010

Nashon: Kozi zipi Ulifanya

Shahidi: Siwezi Kusema

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Mahakama, Section 364 ya Sheria ya Ushahidi, Inahusu General Jurisdiction ya Mahakama

Mheshimiwa Jaji ni 264 ya CPA ambayo inasema Mahakama Kuu Itakuwa na Mamlaka, Kwa Shahidi anapo fika Shahidi aweze Kutoa Ushahidi, Na Shahidi amefika ataki Kutoa Majibu, Tunaomba Mahakama Yako itoe Mwongozo na Pia Imuonye

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Muda Kidogo tupitie

Mahakama Ipo Kimyaaa

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anasimama

Ikupendeze Mheshimiwa Jaji, Tumemsikiliza Wakili Msomi Mwenzetu Wakili Nashon Nkungu, Kwa Heshima Zote Siye hatukubaliani na Maombi yake anayo yataja kwa kuwa hayana Mashiko Kisheria.

Mheshimiwa Jaji Wakili anaomba Mahakama Imlazimishe Shahid: Kujibu swali lake la Level gani ya Mafunzo aliyo ya fanya, Shahidi: amemueleza hilo Swala la Siri Hawezi Kutamka hadharani Yeye ni Wa level gani Katika fani yake

Na Wakili kabla ya hapo amekuwa aliulizwa Maswali Kadhaa kuhusu Ikama ya Jeshi la Tanzania, Shahidi: amemueleza Kwamba awezi Kueleza Kutokana na Kiapo Chake

Ameeleza Pia Kuhusu Kifungu Cha 264 cha Criminal Procedure Act, Ambapo Wakili anasema Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi: Kupitia Kifungu hiki, Naomba Nikisome……….

Tafsiri ipo wazi Hapa, Kwamba Subject to the Provision of this Act…… Maana yake Discription Ya Mahakama Katika hili Inategemea na Sheria zingine

Mheshimiwa Jaji Maswala ya kiushahidi, Kupokelewa Kwa UShahidi: Mahakamani Kuna Sura yake Maalum ambayo ni Sura Ya 6 ya Sheria ya UShahidi: ya 2019

Na Sheria hiyo Inavifungu Mahususi Kinacho Elekeza ni Mazingira Yepi Shahidi: anaanza Kulazimishwa Na Mahakama Kujibu Swali

Mheshimiwa Jaji Kifungu Cha 158 cha Sheria hiyo kimeeeleza Ni wakati gani Mahakama, na Mazingira Yepi hasa Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi: Ajibu Swali.

Na si hicho tuh, lakini hata Kifungu cha 156 Cha Sheria hiyo hiyo nacho Kinatoa Mazingira Yepi,

Mheshimiwa Jaji Miye nitajielekeza Kifungu cha 155 Kifungu Kidogo Cha Kwanza……. Nanukuuu

Mheshimiwa Jaji Swali la level ya Mafunzo ya Shahidi: Ni swali ambalo halina Mahusiano na Kinacho Jadiliwa Mbele ya Mahakama au Kilichopo Mbele ya Mahakama

Mheshimiwa Jaji Maswala ya namna hii, labda yawe yanapelekea Ku Injure character ya witness basi Shahidi: anaweza Kulazimishwa Kuyajibu

Kinyume na hapo Shahidi: Awezi Kulazimishwa

Mheshimiwa Jaji, Wakili Ajaonyesha Mahakama Lengo la Swala lake la Kufahamu Mafunzo ya Shahidi Ni Ku Injure Character yake

MAHAKAMA IMEKWENDA MAPUMZIKO. WAKILI WA SERIKALI: ANAJIBU OMBI LA WAKILI WA UTETEZI NASHON: NKUNGU.

Wakili Serikali Chavula anaendeleaa….

Swala la Forces inatoa Makomandoo Wangapi, Force Inavituo Vingapi Vya Makomandoo, Ni Maoni yetu Kwamba Maswala ya Namna hiyo hayalengi Ku Distort Character Ya Shaw.

Mheshimiwa Jaji siye tunachokiona hapa Inawezekana Msomi.

ameshindwa Kimtingisha Shahidi

Anataka Kumlazimisha Shahidi: azungumze Maswala la Ikama ya Jeshi.

Wakili serikali Chavula anaendeleaa….

Mheshimiwa Jaji Samahani Ukasema Kifungu Cha 155 Sura ya 6, kina Sema “When a witness,………. “.

to test his Velacity………….

Sasa Mheshimiwa Jaji Hata Maswali Yenyewe haya haya Follow under 155, Untest Velacity Ya Shahidi: Kwa Kutaka Kufahamu Kuna Vituo Vingapi Vya Makomando, Unatest Velacity ya Shahidi: Kutaka Kujua Mafunzo yake ni ya level gani, Unatest Velacity Kwa Kutaka Kujua Makomando Wanazlishwa Kwa Mwaka Mara ngapi?

Mheshimiwa Jaji in addition to Hereny Refered to , Question ambazo Zinakuwa Refered ni zile zinazoanzia 148 Mpaka 154.

Shahidi: amekuja Mahakamani Kwa Kusema Yeye ni Askari Wa Jeshi la Wananchi, Kutoka Kikosi cha 92 KJ, Cheo Chake ni Luteni na Jukumu lake anasimama Askari Walio Chini yake 30.

Shahidi: amekuja Kutoa UShahidi: Kwa Kile Kilichopekea Kesi Hii Kuwapo Mahakamani, Katika. 

UShahidi Wake Hakuna Mahala ameeleza Kwamba Jeshi La Wananchi Tanzania lilihusika Kwa namna Yoyote Ile.

Sasa Mheshimiwa Jaji Katika Mazingira hayo, Utaona Maswala la Wakili hayana Relevance, Hata Ukiangalia Kwa Namna Yoyote Ile haya Affect Character Ya Shahidi.

Anateta tena Kidogo na Wenzie

Hata Kama angejielekeza..

Mahakama Katika Utaratibu Huu, haingefaa, Na Mahakama Haiwezi Kujiwekea Utaratibu Wake Pale ambapo Kuna Utaratibu Uliowekwa Kisheria

Wakili serikali Chavula anaendeleaa….

Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi: Yupo sahihi.

Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Hoja ya Wenzetu haina Msingi, ajielekeze Katika Maswala ambayo anaweza Kutest Velacity ya Shahidi.

Kwa namna ambayo Maswali yameulizwa Mahakama haina Mamlaka ya Kumlazimisha Shahidi: ayajibu.

Mheshimiwa Jaji naomba nimkaribishe

Mwenzangu Pius Hilla aendelee…

Wakili serikali Hilla anaanzaa..

Mh Jaji Bila Kurudia Kile ambacho amezungumza Mwenzako.

Mheshimiwa Jaji tunakazia Maneno Kwa Kiapo chake.

Mheshimiwa Jaji

Shahidi aliyepo Kizimbani aliulizwa swali Kuhusiana na level yake Ya Ukomando, Ajaieleza Mahakama Kwamba Kwa Kiapo Chake awezi Kueleza level ya Mafunzo yake.

Wakili serikali Hilla Anandeleaa:

Mheshimiwa Jaji tunakazia Maneno Kwa Kiapo chake.

Mheshimiwa Jaji Ni Kosa LA Jinai Ku Communicate Information ambayo ni Confidential.

Mheshimiwa Jaji sect 4(1) ya CAP 47 ya National Security, Inasema Ni Kosa la Jinai Ku Communicate Information.

Na hauruhusiwi Kufanya hivyo, Kwakuwa Shahidi: amesha eleza Kwa Kiapo Chake Harusiwi Ku Communicate Kwa Kiapo Chake Kusema Level ya Mafunzo ambayo amefanya.

Kuna Maswali ambayo Shahidi anaweza Kujibu.

Mheshimiwa Jaji nimalizie Kwa Kusema Kwamba Taarifa Ya Kuhusiana na Level Ya Ukomando wa Shahidi: Kwa Mujibu wa Kiapo Chake awezi Kusema.

Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama Itupilie Mbali Maombi ya wakili

Na Kwakuwa Kuna Back up Ya Sheria, Remedy siyo Kulazimishwa, Bali wakili aelekezwe Wakili Kuuliza Maswali Sahihi.

Wakili Nashon: NkunguMheshimiwa Jaji, it’s Very Interesting, Leo nimeshuhudia OBJECTION Ya Kupinga Identify ya Shahidi, Kama Nilikuwa namuuliza Shahidi: ana Elimu gani?.

Wakili wa SerikaliPius Hilla OBJECTION Mheshimiwa Jaji Samahani, Hakuna Swala la Identify ya Shahidi, Kilichopo hapa Ni Kutaja Kumlazimisha Shahidi: Kusema Mambo ambayo awezi Kusema

WAKILI WA UTETEZI NASHON NKUNGU ANAKAZIA OMBI LAKE..

Nashoni Nkungu:

Sisi tunaomba Kiapo alichokula hapa Mahakamani Kiwe Juu Ya Viapo Vingine Vyote.

Mheshimiwa Jaji, Niendelee Kwenye Submission yangu, Naomba Mahakama Kwa Wivu Mkubwa Mahakama Ilinde Mamlaka yake, Hapa Shahidi: amekula Kiapo Kimoja, la Sivyo Mwanzoni Wakati wa Kiapo angesema anakula Kiapo Lakini anakiapo Kingine kinamkaza Kusema Yeye ni nani. 

Hakuna Sheria ambayo Wametoa Kwamba Inakataza, Bali Tunaona Kwamba Ni Vifungu Vinavyoruhusu Kujua Shahidi: Ni nani Na Elimu yake ni Ipi?.

Mheshimiwa Jaji Nikienda Kwa Section Moja Moja Ka. Ambavyo imetajwa hapa, Naona Vyote ni Permissive, Vyote ni Relevant kwa Sababu Lengo lake Ni Kutaka Ku Establis Je anaujuzi Wa Kile anachokiongea, anatoka Kweli Ngerengere.

Hatuoni kwa namna Gani Swala.

Hilo lina kuwa Relevant, Mheshimiwa Jaji Kiusalama Hakuna Mambo ambayo yanakiuka, Hatuoni Shida Kusema Mtu fulani na Kusema Yeye ni nani!

We kuja Hapa Watu Wakasema Wao Nia Inspector, Wao ni MA RCO

Kwamba Hapatakiwa na Excuse Juu ya Kutoa Ushahidi.

Mheshimiwa Jaji Hizo Section ambazo wame zitaja Zina refers Kwenye Kifungu cha 151.

Kuna Msemo Mmoja unasema Mwisho uoshwa, Mahakama hii hii..

Wakili aliyesimama Abdallah Chavula Ndiye aliyesimama Kuhoji MaShahidi: Wakina Adamoo Kwamba Komando Mmoja anapiga Askari Wangapi.?

Tunahitaji accuracy, Tunahitaji Conforming, Kwa sababu Watakuja Hat Washtakiwa Watasema wao Wana Kiapo.

Hatuku Object, Tilimuacha aulize

WAKILI WA UTETEZI NASHON NKUNGU ANAMALIZIA.

Tunaomba Haki iwe pande zote Mbili

Mheshimiwa Jaji Kwenye kutumia Kifungu Sahihi au Siyo Sahihi, Ni Kifungu ambacho tunaona ni sahihi

uhusiana na Powers Kuhusu Ku Compel Shahidi, Kwa Kuweka hii Hoja Vizuri Mahakama Kwa Kutumia hici Vifungu Vya 141,156,155, 158 Vyote ni Vifungu Wezeshi ambavyo Bimaipa Mahakama Mamlaka Wajibu wa Kutoa Ushahidi

Kama Hakuna Kifungu Kinachokataza, Ni Msimamo Wetu Kwamba Shahidi: Yupo Compellable Kuweza Kujibu

Mheshimiwa Jaji Kwenye Hoja Nyingine Kwenye 158 cha Sheria ya UShahidi: Kifungu Kipo Subject kwenye Subsection Two ya 158 ya Sheria ya Ushahidi

Narudia Kumuomba Shahidi: ajibu Swali langu Ka alivyo Ulizwa

Wakili Nashon: Nkungu:  Anakaa Chini

Mahakama Ipo Kimya Kidogo

MAHAKAMA INAENDA MAPUMZIKO.

Jaji: Mme-site Sheria a Kadhaa na Vifungu Kadhaa, Ili niweze Kutoa Maamuzi Ambayo ni sahihi naomba Kupitia Kidogo hivi, Kwa Dakika 30 kisha tutarejea

Tukutane baada ya Dakika 30 

Jaji anatoka

MAAMUZI.. JAJI ANATOA MAAMUZI YA OMBI LA UTETEZI..

Jaji amerejea Mahakamani Muda huu Saa 8 na Dakika 52

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Kwa Upande wetu tupo Kama Awali na tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu tupo Kama Awali Hakuna Mabadiriko, na Tupo tayari Kupokea Uamuzi Mdogo na Cross examination

Jaji: Wakati Uliopoita Mahakama Ilitoa Hairisho la Muda Kufuatia Hoja Iliyo letwa na Wakili Nashon: Nkungu

Hoja Ilikujia baada ya Upande Wa Mashitaka Kumalizia Kumuuliza Maswali Shahidi: Ndipo Bwana Nkungu akapokea na Kuuliza Maswali

Ndipo Baada Ya Maswali Kadhaa a Shahidi: alisita Kujibu Kwa Kusema Kwamba awezi Kujibu Maswali Kadhaa

Kwamba Yupo Mtu anaye weza Kuzungumzia

Moja ya Swali ni Kikosi Vipi ambavyo Vinafunisha Makomandoo, Aeleze Mafunzo aliyofikia Level yake ya Ukomandoo

Ambapo Shahidi: alisema awezi Kujibu.

Ndipo wakili Nashon: Nkungu:  akana Mahakama Imlazimishe Shahidi: Ajibu Maswali Kwa sababu Mahakama ina Mamlaka hiyo

Upande wa Mashitaka Walipinga Hoja hiyo Kwa Kusema Kwamba Kwanza Kifungu Kilochotumiwa Kuleta Ombi hilo Kimekosewa

Wakataja Kifungu Namba 158 na 156 kwa Kueleza Vifungu ambavyo Vina eleza kwamba ni Mazingira Yap Shahidi: anaweza Kulazimishwa Kutoa Ushahidi

Kwa Mazingira haya Jambo hilo halipo

Shahidi ameulizwa Na amesha Sema Kwamba Yeye ni Komandoo na Kwamba Yeye anajukumu la Kuongoza Afisa Mmoja na Askari Kadhaa

Wakaendelea Kusema Katika Mazingira Hayo Mahakama Imkatalie Kumlazimisha Shahidi

Upande Wa Mashitaka Waliendelea Kusema Kuwa Shahidi: amesha Ulizwa ana akasema anakatazwa kwa Mujibu wa Sheria ya usalama wa Taifa na Kwamba Kwa Mujibu wa Sheria hiyo Mtu anakatazwa Kutoa Siri au Taarifa anazokatazwa

Wakasema Kuwa Shahidi: asilazimishwe

Kwamba Remedy Siyo Kumlazimisha Shahidi Bali Wakili aelekezwe Kwenda Katika Eneo Lingine.

Wakili Nashon Nkungu:  akasema Kwamba Vifungu Vyote Vya 158,155 na 156 ni Vifungu Muafaka na Kwamba akaomba Mahakama Itumie hivyo Vifungu Kujibu swali lake

Akasema Kwamba Sheria inasema Kuwa Shahidi: hatoachwa Bila Kuulizwa Swali

Na Kwamba Shahidi: amekula Kiapo hapa Mahakamani, na Hakusema Kwamba anakiapo Kingine

Na akaomba Shahidi: Ajibu swali lake

Jaji: Ni Walinakubalina na Wakili Nashon Nkungu  Kwamba Kifungu Cha 264 Kinatoa Mamlaka ya Jumla Juu ya Mahakama Juu kuendesha Shughuli zake

Kifungu hiki hakitoa Mamlaka Kwamba ni Kwa namna gani Mahakama Itamlazimisha Shahidi: Kujibu Swali lake

Kwa a Mujibu Wa Kesi Mbalimbali, Hoja Kwamba Sheria ambayo Maombi yameletwa Kwamba Sheria SIYO Muafaka basi Maombi yatupwe Siyo Muafaka, Basi Mahakama Inaendelea Kusikiliza

Wao Wenyewe Wameieleleza Mahakama Vizuri Katika Vifungu ambavyo anaweza kutumia.

Kifungu Cha 151 kina Sema Shahidi: hatoachwa Bila Kujibu swali Lolote Kama swali hilo ni Relevant Na Kesi hiyo

Mahakama Inatakiwa Kuhakikisha Shahidi anajibu Swali hilo Moja kwa Moja ambapo Swali hilo Linabishaniwa Mahakamani

Kifungu Namba 155 kina Sema Shahidi: anaweza Kuulizwa Maswali Yoyote, ambayo Yana lenga Kutest Velacity Yake, Ambapo Pia Kama Maswali ambayo siyo Relevant Kama Kutaka Kumtambua Yeye ni nani au Kutaka Kumtikisa UShahidi: wake

Kifungu 156 kina Sema Maswali yote ambayo Yana Ulizwa katika Kifungu Cha 156

Kifungu Namba 158 kinaelekeza Kwamba Maswali ambayo ya naelekeza Mahakamani yawe ni Relevant Au Maswali hayo Mahakama Italazila Kujibu kwa Msingi

Kitu Cha Msingi Ni swali Ka Lipo relevant

Jambo la Pili Kutest Velacity Yake

Jambo la Tatu Kutaka Kujua yeye Ni Nani

Na la Nne ni Kutaka Kumtikisa

Swala ambalo lipo Mahakamani Ni Swali ambalo linataka Kujua Shahidi Ni nani, Ni kweli Swali siyo Relevant Ila linalemga Kujua Shahidi: yeye ni nani

Katika Mazingira Ya Shauri hili ambalo linalemga Kutaka Kujua Shahidi: Yeye Binafsi ni nani, Basi Mahakama Inaona anaweza Kujibu

JAJI KAKUBALIANA NA UPANDE WA UTETEZI..

Kama Maswali Mengine yataendelea Nje ya a

Mipaka basi anaweza Kuzuiwa Kujibu swali

Nafahamu Kama Yapo Maswali kuhusu Jeshi Awezi Kujibu Basi Nita Elekeza kuwa Asijibu

Katika Mazingira haya basi Swali ambalo Shahidi: Unaulizwa Kuhusu Mazingira Yako unapaswa Kujibu

Lakini Kama Utaulizwa Kuhusu Mitaaka ya Mafunzo yako au Vitu ambavyo wewe Siyo Muhusika Unaweza Kusita Kujibu

Kwa Maana hiyo natoa Amri

WAKILI WA UTETEZI NASHON NKUNGU  ANAMUHOJI SHAHIDI WA SERIKALI DENIS URIO.

Wakili Nashon Nkungu:  Shahidi Unakumbuka Swali nililokuuliza

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Nakuuliza Level ya Mafunzo Yako ni Ipi

Shahidi: Kimyaaaaaaaa

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall

Jaji: Jibu swali Bila kumuathiri Mwajiri Wako Sasa

Shahidi: Nilifanya Mafunzo Ya Advanced Parachute niliopata South Africa

Shahidi: Pia Ina Certificate Of Diesel Engine

Nashon: Ulipata wapi

Shahidi: Moshi

Nashon: Ulisoma lini

Shahidi: Mwaka 2000 pale RVTCS

Nashon: Kabla ya hapo ulikuwa na Elimu gani

Shahidi: Form Four

Nashon: Unaweza Kueleza Namna Ulivyo ingia Jeshi Mpaka Ukapata Cheo Cha Luteni

Shahidi: Nimeingia Jeshi Mwaka 2003, Ni kafanya Kozi ya Basic, 2004 Basic Komando, 2005 Mpaka 2006 nikasa Advanced Komandoo, 2009 Mpaka 2010 Nikaenda Special Operation

Nashon: Unakumbuka Ulisema Mwaka 2011 kwenye Operation Sudani

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Unaweza Kukumbuka Askari Yoyote Uliyekuwa naye Huko Sudan

Shahidi: Siwezi Kukumbuka

Nashon: Je Unkumbuka Askari Yoyote Wa Tanzania aliyekuwa Sudan

Shahidi: Siwezi Kukumbuka

Nashon: Jibu lako Pia Lita kuwa hivyo Kwa Operation ya 2012 Kwamba hukumbuki Jina la Mtanzania yoyote

Shahidi: Siwezi Kukumbuka

Nashon: Mwaka 2019 Wakati Khalfani Bwire aNafukuzwa Wewe Ukwepo Ulikuwa Sudani

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na Adamoo Wakati anafukuzwa kazi Pia Hukwepo Ulikuwa Kozi Arusha

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Pia wakati Mohammed Ling’wenya Anafukuzwa Kazi Pia wewe Hukwepo

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Je Ni Kwanini Uliongelea Kuhusu Hawa Kufukuzwa Kwao Wakati wewe huya fahamu kwa sababu Ulikuwa na Nia Ovu Dhidi Ya Washitakiwa

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Lakini ni sahihi Kwamba Wewe Ufahamu Kuhusiana Kufukuzwa Kwao Jeshini, Na Tuhuma zao

Shahidi: Nafahamu Kwamba ni Utovu Wa Nidhamu.

Nashon: Ni sahihi Kwamba Utovu wa Nidhamu Lenyewe Siyo Kosa Ila Ndani yake ndiyo Kuna Kosa Sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Specifically Ujaiambia Mahakama Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kwa Kosa gani

Shahidi: Siyo Wajibu Wangu Kusema hilo, Ni Wajibu Wa Msemaji Wa Jeshi

Nashon: Kwahiyo Siyo Wajibu wako pia Kwa Mtuhumiwa Wa Pili na watatu

Shahidi: Miye Nimeishia Kusema Utovu wa Nidhamu, Mengine Ni Siri zao

Nashon: Ni sahihi hUjataja Pia Mahakama Iliyotumika kuwasikiliza na Kuwafukuza Kazi watu hawa Jeshini

Shahidi: Sijaeleza Ndiyo

Nashon: Na wala Ujaeleza Kuwa aliye Wafukuza ni Service Kamanda wao au Tribunal Court Marshall

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Na wala Ujaeleza Mahakama Tarehe Waliyo Fukuzwa

Shahidi: Ndiyo Sifahamu

Nashon: Ni kweli hukumtajia Mheshimiwa Jajo Jina la Admin officer aliyekujia Hawa Kufukuzwa Kazi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naweza Kutoa Maelezo.

Nashon: Hakuna Cha Maelezo huu Ni Muda wa Maswali Mafupi

Nashon: Ni kweli hukumtajia Mheshimiwa Jajo Jina la Admin officer aliyekujia Hawa Kufukuzwa Kazi

Shahidi: Ndiyo Sikutaja

Nashon: Na ni kweli Ujamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Huyo Admin Officer ni Mmoja au Watu tofauti

Shahidi: Umenisikia Vibaya Nilisema Nilienda Ofisini Nikapitia File

Nashon: Ni UShahidi: Wako Ulipitia File

Shahidi: Ndiyo

Nashon: ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Lilikuwa ni Faili namba Ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Ni wazi Kwamba Uwezi Kusema alifukuzwa Kazi na Chombo Kipi

Shahidi: Walifukuzwa kazi na Mwajiri Wao

Nashon: KWANI Shahidi: Unafahamu Kwamba Ili Askari afukuzwe Kazi anatakiwa apitie Procedure Zipi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Turudi Kwenye Ile Siku ambayo Ulikutana na Mheshimiwa Freeman Mbowe ambapo alikuta futa Kwa Njia ya Simu na Baadae Mkakutana Kwenye Mgahawa.

Je Unakumbuka Kwamba Baada ya Kukueleza Mipango Yake Ya Kuchukua Nchi na Ugaidi, Ukasema Ulitafakari na Ukakubali

Shahidi: Ndiyo Ni sahihi

Nashon: Je Wakati huo Ulikuwa Upo Sober na Malta Yako au Ulibadiri kinywaji

Shahidi: Ilikuwa Kwenye Mgahawa siyo Sober, Sijui Kama Palikuwa panaitwa sober

Jaji: Wakili Uliza Katika Namna Rahisi ambayo Shahidi atakuelewa

Nashon: Nakuuliza Ulikuwa Timamu Kiakili au Ulitumia Kilevi

Shahidi: Nilikuwa timamu

Nashon: Muda unaosema Ulikuwa smart Sana na Ukakubali, Si Ulikuwa Ujawasiliana na Chombo Chochote cha Ulinzi Kuhusiana na hiki Kikao

Shahidi: Ilikuwa Bado

Nashon: Nikiwambia Kwamba Kwa wewe Kukaa Kile kikao na Kuzungumzia Maswala ya Ugaidi, Utakuwa Ulikuwa Umeshiriki Kikao cha Kigaidi

Shahidi: Sitakubali

Nashon: Ulikubali Kwenda Kumtafutia Vijana, Kwa sababu Ulikuwa na Uchu wa Madaraka

Shahidi: Siyo Kweli

Nashon: Lakini Ulihaidiwa Cheo

Shahidi: Ndiyo Nilihaidiwa Cheo

Nashon: Kuna Kitu Kinaitwa Chain Of Information Jeshini

Shahidi: Ndiyo,

Shahidi: aaaahhh Kinaitwa Chain Of Command.

Nashon: Haya Elezea Kuhusu Hiyo Chain of Command

Shahidi: Ni Mtiririko Wa Amri Kutoka Mtu Wa Juu Mpaka Chini

Nashon: Ulisema Kwamba Ulitoka Mgulani na Ukarudi Mgulani

Shahidi: Ndiyo ni sahihi

Nashon: Jeshini unafahamu Mtu anaitwa Intelligence Officer

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Kikanuni Taarifa Ka hizo Ulitakiwa Kupeleka Kwa Intelligence Officer, Adimn Officer au Mkuu wa Kikosi

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba Huku pelekwa Taarifa Hizo Jeshini Kwa Sababu uwaamini

Shahidi: Hapana ni Kwa sababu, Taarifa zilikuwa zinahusika na Raia

Nashon: Kwahiyo Wewe Ulikuwa Raia

Shahidi: Ni Askari siyo Raia.

Nashon: Ni sahihi Kwamba UShahidi Wako Kuwa Uwezi Kupeleka Taarifa Hizo Kwa Intelligence Officer

Shahidi: Hapana Si Kweli, Sema Nilifanya Analysis Ya Threat

Nashon: kwahiyo wewe Ulivunja Chain of Command Kwa sababu Unaharaka

Shahidi: Sikweli

Nashon: Tukio Kubwa la wewe Kwemda kwa DCI Ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki Tarehe, Ilikuwa katikati ya Mwezi Wa Saba

Nashon: Kwa hiyo ufahamu Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe Kamili sikumbuki

Nashon: Unafahamu Kwamba Unapoenda Kwenye Ofisi za Umma Unaandikisha

Shahidi: Nilicho fanya ni Kutoa Kitambulisho Wakanitambua na Tayari Nilikuwa na Appointment na DCI

Nashon: Umeeleza Kwamba Freeman Mbowe alikueleza Kwamba Wanataka Kuchukua Dola Kwa Namna yoyote ile

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Alikwambia Watachukua bila Uchaguzi

Shahidi: Sifahamu, Hakuniambia Watachukua Kwa Namna gani

Nashon: Alikwambia Watachukua Dola Kwa kukata Miti

Shahidi: Hayo yalikuwa Matendo ya Kuleta Taharuki

Nashon: Kwa Uelewa Wako hayo Yakitokea Upinzani Wa Nachukua Nchi

Shahidi: Sifahamu sasa yeye.

Nashon: Kipi Kitaku wa sahihi Kulingana na Habari Yako, Mbowe Kuchukua Wanajeshi Ex Soldiers au Wanajeshi Ambao Wapo Kazini katika Kuchukua Nchi

Shahidi: Sijui

Wakili wa Serikali: Abdallah Mheshimiwa Jaji Pamoja na Shahidi: Katoa Majibu, lakini linataka Opinion zake

Nashon: Shahidi: Unasema Baadae Ulianza Kuwatafuta Vijana Kibao amba Freeman Mbowe anatafuta Walinzi na Kama Wapo Tayari

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Wakati Huo Wewe Ulikuwa Unafahamu Kuwa Mbowe Haitaji Vijana Wa Ulinzi Bali Vijana Wa Kufanya Ugaidi

Shahidi: Ni Vijana Wa Kuambatana naye Kufanya Ugaidi

Nashon: Wakati Ule Unampigia Unamiuliza Upo tayari Kuna kazi ya Ulinzi, wewe Moyoni Ulikuwa unajua Kuwa haitaji Walinzi Bali ni Vijana wa Kuambatana naye

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwahiyo Ni sahihi Uliwadanganya pia Watuhumiwa wa Pili na watatu

Shahidi: Ni sahihi.

Nashon: kwanini Uliwadanganya.?

Shahidi: sikuwadanganya, Isipokuwa….

Nashon: Huko sijafika

Nashon: Ka Uliwaambia Kitu ambacho halikuwa Kweli na Sahihi, Inawezekana Hata Leo undanganya Mahakama

Shahidi: Sivyo

Nashon: Shahidi: Ulisema Kwamba Ulikutana na Watuhumiwa Wa Kwanza na Wapili na watatu Morogoro, Ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: katika hichi Kikao Chenu Morogoro Hakutaja Ugaidi Wala Kikao Chenu Hakikuwa na Nia mbaya

Nashon: Hebu tuisaidie Mahakama, Unafahamu Muda wowote Mwingine Mtuhumiwa Wa Kwanza, Wapili, watatu na wanne Walikutana Morogoro Kwa ajili ya Kula Njama Hizo

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Kwa hiyo, Vipi Kuhusu Moshi, Unafahamu Kwamba Aishi Hotel Moshi Wakala Njama Kufanya Njama Hizo

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Unafahamu Kwamba Walikutana Arusha Waka panga Mikakati ya Kupanga Mipango ya Ugaidi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Kwani Shahidi: Mwaka 2012 ulikuwa na Rank gani

Shahidi: Nilikuwa na Rank ya Coplo.

Nashon: Ni sahihi Kwamba Ulipokutana na Freeman Mbowe aKakudodosa Kuhusu Rank yako ukamdanganya huna Rank

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Jibu ililompa lilikuwa ni Sahihi

Shahidi: Ni sahihi Kwangu

Nashon: Lilikuwa Jibu la Ukweli

Shahidi: Sijui

Nashon: Na Scenerio zinazojitokeza za wewe Kudanganya Mara Kadhaa Unataka Mahakama Ikuamini wewe ni Shahidi: Mkweli

Shahidi: Ndiyo Mimi ni Shahidi: Mkweli

Nashon: katika UShahidi: Wako Umesema Kwamba Ufaungamani na Chama Chochote Isipokuwa na Kiongozi aliyepo Madarakani, Ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na Huyo Kiongozi aliyepo Madarakani, Hukusema Kwamba ni Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya au Rais

Shahidi: Nilisema Kwamba naheshimu Mamlaka zilizopo Madarakani

Nashon: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa wewe Ukisema umaheshimu na siyo Kufungamana.

Nashon: Na Shahidi: ni sahihi Kwamba Mara zote Freeman Mbowe alipokuwa anakutafuta alikuwa anakutafuta Kwa Njia za simu

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na hata Asipo tumia namba yake Basi atatumia namba ya mtu Mwingine

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Hii Fact pia Iliwashirikisha Wapelelezi Waliokuwa Wanaopeleleza Kesi hii

Shahidi: Sijaelewa

Nashon: Ulipoenda Kwa DCI ulipewa nani awe Mpelelezi Wa Kesi yako

Shahidi: Kingai

Nashon: Je ulimueleza Swala hilo kuwa Mbowe akinitafuta lazima atatumia Namba ya Mtu Mwingine, Je Ulimwambia Kingai

Shahidi: Ndiyo Nilimwambia

Nashon: Na wewe Ulikuwa na Simu Nne, ambazo Umeziorodhesha Hapa Mahakamani

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Wewe na Mpelelezi Wako Hamkuona Umuhimu Wa Kuweka Simu Moja Chini ya Surveillance, Kuweza Kurekodi Pindi Mbowe atakapo piga

Shahidi: hapakuwa na Umuhimu

Nashon: Sasa Shahidi: Umetoa hapa Meseji, Je Unaweza Kutoa Meseji haya Moja yenye Mwelekeo Wa Kupanga Ugaidi

Shahidi: Hakuna Meseji ya Neno Gaidi

Nashon: hayo ya Kwako, Nauliza Je kuna Meseji Kwamba inaonyesha Kuna Mwelekeo Wa Ugaidi

Shahidi: kuna Meseji ya Kuwasafirisha

Nashon: Kwahiyo Meseji hiyo inamwekeo wa Ugaidi, inasemaje.

Shahidi: Wale mtu tatu Wanauharaka

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Kielelezo namba 23

Nashon: naomba Ni Kukabidhi Kielelezo hiki, Naomba unitafutie Sehemu yenye Meseji ya Kupanga Ugaidi

Shahidi: “Kaka Wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu Sana, Siku zimeisha “

Nashon: Wewe Ulivyosoma hapo Ukaona Kuna Ugaidi, Ukaona Kuna Umuhimu Sana Wa Kuleta Mahakamani

Shahidi: Kwa sababu Walikuwa wa nahitaji na Mbowe

Nashon: Soma Meseji ya Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Mmoja Yupo Tunduma anasafirisha Magari Kwenda Nje Ya Nchi na Moja yupo Dodoma kwenye SGR.

Nashon: Na Meseji ya Saa 2 na Dakika 3

Shahidi: Simu Siyo Salama Sana, Niwezeshe nikakutane nao

Nashon: Ilikuwa siyo Salama kwa nani

Shahidi: Siyo Salama Kwa sababu Hatuelewani

Nashon: Soma Meseji ya hapo Chini ya Saa 2 na Dakika 5

Shahidi: Naomba Unitumie Nauli niweze Kuwa Mobilise Tukutane Morogoro

Nashon: hiyo Meseji ya nani

Shahidi: Ya Kwangu Mimi

Nashon: kwa hiyo Wewe ulikuwa Unamobilise Magaidi

Shahidi: Hapana Siyo Mimi ni Mbowe

Nashon: Mbowe ndiyo Alikutana nao Morogoro.?

Shahidi: Hapana ni Mimi ni kutana nao

Nashon: Kwahiyo Ulienda Kukutana na Magaidi na akuwa Mobilise

Shahidi: Hapana Siyo Magaidi

*Mahakama Kichekoooooo*

Nashon: Unasema Kwamba Khalfani Bwire Alikwambia Kazi Imebadirika, Je alikuwa ni Lini

Shahidi: Asubuhi aya Tarehe 4 August 2020, Saa 2 Asubuhi

Nashon: Kwa hiyo Bwire ndiye aliye kwambia Ni lini Shughuli imebadirika

Shahidi: Hakuniambia ni Lini Imebadrika

Nashon: Kwahiyo Ni sahihi Kwamba Bwire Alikwambia Tarehe 4 August 2020 alipofahamu Shughuli Imebadirika

Shahidi: Sijui

Nashon: Je Bwire Kwakukupia Simu wewe, Je alifanya Kitu sahihi

Shahidi: Alifanya Kitu sahihi.

Nashon: Kwa Mujibu wa Bwire Ndiyo Taarifa Yake ilipelekea Wenzake Kukamatwa Rau Madukani

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Je Ulirusidha Taarifa Hizo Kuwa Kijana Wangu Bwire Ndiyo amenipatia Taarifa hizi

Shahidi: Ndiyo ni sahihi

Nashon: Baada ya pale Hata wewe Ilikushangaza Bwire kukamatwa

Shahidi: Hapana Sikushangaa

Nashon: Kwani wewe Kwa Uelewa Wako Kwenye Scenerio hii, Kosa la Bwire Lipo wapi

Shahidi: Sijui

Nashon: Kwa hiyo Ufahamu Kipande Cha Bwire wala involvement Ya Bwire Katika kupanga Matendo Ya Kigaidi

Shahidi: Miye Sijui

Nashon: Na kwamba Shahidi: Wewe Upo Nje, Na Bwire alikuwa informer Wako Yupo Gerezani, Wewe upo Nje Unakula Maisha

Shahidi: Sifahamu aliye Mkamata.

Nashon: Kwani wewe Shahidi: Una Umaalum au unamkataba na Serikali

Shahidi: Hapana

Wakili Nashon: Nkungu:  Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia Hapa

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji nitakuwa na Maswali Machache, Jibu kwa Sauti Mteja wangu Adamoo aweze Kusikia

Nakuonyesha Kielelezo hiki Kama Meseji hizi kama zinafanama na za Kwenye simu

Shahidi: Zinafanama

Malya: Nionyeshe Hump Kwenye Meseji Sehemu aliyokuita Homeboy

Cdm mayor Ubungo

Shahidi: Hakuna

Malya: Umetutolea Sauti au uliyomrekodi Sauti ambayo Mbowe anamuita Homeboy

Shahidi: Sinaonyesha

Malya: Sababu Ya Kusema Maneno ambayo Kwenye UShahidi: Hakuna ikiwa ni Sababu Ya kujipendekeza tuh Uonekane Mtu wa karibu Wa Mbowe

Shahidi: Sina Device Ya Kumrekodi

Malya: walikuja watu wa Airtel hapa tukawaambia Kuwa wanatoa Siri za Watu 

Wakabisha, Nakuonyesha Kielelezo Namba 19

Ni sahihi hizi Taarifa ni za Kwako

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Nakuonyesha hapa Muamala umepokea TSh 199,000, Kwenye Kielelezo P 19 Tarehe 2 Mwezi July 2020

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Pamoja ni kwamba ni Kielelezo Cha Mahakama naomba Wakili awe ana Introduce

Malya: Kielelezo namba 20, inasemekana ni Mihamala ya kwako, Kwa namba 0787 555200 Je ni Namba yako

Shahidi: Ndiyo Ni namba yangu

Malya: Kwenye Ukurasa Wa Pili wa Hii Nyaraka, Kuna Mihamala Hapa, Unazungumzia 199,000

Shahidi: Ni namba Yangu

Malya: Ulipokea Kutoka Kwa Nani

Shahidi: Sikumbuki Imetoka Kwa Nani

Malya: Inaonekana Balance Yako Ilikuwa 121,000 baada ya Kupokea 199,000 Ikawa ni Tsh 302,0296

Shahidi: Ndiyo naona

Malya: Kesho Yake Ulituma TSh 190,000 Kwenda Kwa GODSON MNURU Je ni nani

Shahidi: Simfahamu

Malya: anayefuata Ukamtumia URIO

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Sisi Kwenye Nyaraka Hakuna Majina, Mheshimiwa Jaji naomba Wakili atuambie Majina anatoa wapi

Malya: Shahidi: tueleze Wew basi hizo namba Unazifahamu 0787000027

Shahidi: Namba hiyo naifahamu

Malya: Je huyo unayesema Unamfahamu, Je Mtu huyo ni Baina ya Wale Washitakiwa

Shahidi: Siyo Baina ya Wale Washitakiwa

Malya: Muhamala Wa Tarehe hiyo hiyo 20 Muhamala Wa 3 kutoka Juu

Shahidi: Ndiyo naifahamu

Malya: na Shahidi: unasema Ulitoa Cash Kuwapa TSh ngapi Khalfani Bwire na wenzake.

Shahidi: Niliwapa Cash TSh Laki 3 siyo Kutoka Kwa Wakala, Ilikuwa Mfukoni kwangu, Nilikuwa nayo Mimi

Malya: Pale usangu Mlikuwa Kidogo

Shahidi: Nisahihi

Malya: Wewe Ulikula Supu ya mbuzi na Chapati Mbili

Shahidi: Nilikula ila Sikumbuki

Malya: na Adamoo na Ling’wenya Walikuwa Supu ya Samaki na Chapati

Shahidi: Sikumbuki

Malya: Ila Unakumbuka Kuwa Mlikula

Shahidi: Ndiyo

Malya: nani alilipa Chakula

Shahidi: Nililipa Mimi

Malya: Ulitoa Wapi Pesa ya Kuwalisha Magaidi

Shahidi: Kwa Freeman Mbowe

Malya: Soma Maelezo Yako hapo Unasema Kwamba Ulitumia pesa ya na Mbowe ya Nini

Shahidi: Ya Kuwaita na na Nauli ya Kwemda Moshi

Malya: Kuna sehemu ambayo Mbowe alikwambia anakupa pesa ya Kuwapa Chakula

Malya: Ila wewe Ukaona uwalishe Magaidi

Shahidi: Hapana

Shahidi: Nilikuta Wanakula na Mimi nikajiunga kula, Kisha ni kalipa

Mahakama Kichekoooooo

Kwamba Mwanzo ulikuwa na balance ya 49,000ma Baadae ukatumiwa Tsh Laki 5 Ikawa 549,000

Shahidi: ni sahihi

Malya: Twende Kwenye Mhamala Wa TSh Laki Tano

Malya: nani alikutumia hii pesa

Shahidi: Freeman Mbowe

Malya: Hii Cash Out watu wa Simu walisema ni Kutoa Kwa Wakala

Shahidi: Upo sahihi

Malya: Ulitoa TSh 300,000

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ulielezea Mahakama Kwamba hii lako Mbili ulimpa nami

Shahidi: Nilimpa Adamoo na Ling’wenya

Malya: Kuna sehemu umesema Kwamba Ulitoa TSh ngapi

Malya: Nilikuwa na Cash Mfukoni

Shahidi: Sikuulizwa

Malya: Wakati Wa UShahidi: Wako Ulisema Kama Ulikuwa na Cash Mfukoni

Malya: haya Twende Kwenye Kielelezo Namba 26

Ni sahihi Kwamba Ulisema Baada ya Vijana Wanne Kufika Kwa Mbowe akawa akioi Mawasiliano tena Bwana Mbowe

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ni sahihi Kwamba Siku Uliyomtembelea Mbowe alikuwa anatembelea na Magongo

Shahidi: Ilikuwa Jioni sikuona

Malya: Unakumbuka Kama alikuwa Magonjwa

Shahidi: Ndiyo aliniambia Kwamba alipigwa na Wahuni.

Malya: Ulikuwa unafahamu alikuwa nauguliwa na Mtoto wake na Yeye anaitwa Denis kama wewe

Shahidi: Aliniambia Kuwa nauguliwa tuh, Hakusema ni nani

Malya: Nikikuonyesha Nyaraka ya Hospital ambayo Inaonyesha Kwamba alikuwa na P. O. P na. Kwamba alikuwa anatembelea Magongo, Ukasema Kuwa Kaka wanakuonea Sana

Shahidi: Hapana Miye sifahamu

Malya: na wakati huo nauguliwa na Mwanaye

Shahidi: Aliniambia Kuwa Bado anauguliwa

Malya: Ni sahihi Kwamba Ukasema Kuwa Kaka Wanakuonea sana Ngoja Nikutafutie Vijana

Shahidi: Hapana Sikusema

Malya: Je unafahamu kwamba Mwaka 2020 ulikuwa Mwaka Wa Uchaguzi

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Malya: Je Unafahamu kwamba Maandalizi ya Uchaguzi yalikuwa yanakaribia

Shahidi: Sifahamu

Malya: kuanzia Mwezi Wa Saba Mpaka Mwezi wa 10 Kuna angalau Miezi Miwili

Shahidi: Ndiyo

Malya: Ushawahi Kusikia Kwenye Uchaguzi Kuna Vurugu kati ya Chama Kingine na Chama Kingine

Shahidi: Ndiyo Nishawahi Kusiki.

Malya: Je ni Vibaya Mtu Kutafuta Ulinzi Kwa ajili yake

Sijui Kama Ni Kosa au Siyo Kosa

Malya: Lakini wewe Uliwatafuta Vijana Ukawaambia Waende kwa Mbowe Kufanya nini

Shahidi: Kuambatana kazi ya Ulinzi

Malya: Kwa hiyo Mtu Kuwa na Walinzi ni Kosa siyo Kosa

Shahidi: Sijui Kama Siyo Kosa

Malya: Kwahiyo wewe Umawataguta Wakina Khalfani Bwire Unawapa pesa au unawapeleka kwa Mbowe kuwa Walinzi, Ujui Kuwa Kosa siyo kosa

Shahidi: Siyo Kosa

*Mahakama Kichekoooooo*

Malya: Sasa Kutafuta hawa Vijana Wanne Kwa ajili ya Ulinzi Kuna Kosa gani

Shahidi: Shida siyo Vijana 

Inategemea Wanaenda Kufanya Kazi gani

Malya: Kwani Wewe Uliwatafuta Vijana Wanne Kwa ajili ya Nini

UShahidi: Hakuna Sehemu ambayo amesema Walinzi

Malya: Soma hapa

Shahidi: Kaka Wale Watu watatu au wanne Ni Muhimu sana

Malya: hao Vijana so Ndiyo hawa

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Unawatafuta Ulisema Kwamba Unawatafuta kwa kazi gani

Shahidi: Ya Ulinzi

Mahakama: Kichekoooooo

Malya: Sasa Wewe Umesha enda kwa DCI na DCI amekuoa Jukumu la Kutekeleza huo Mpango

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Kuna sehemu Kwenye Meseji ya Mbowe inasema Kwamba tukafanye Uhalifu au Ugaidi

Shahidi: Hakuna

Malya: Soma hapa

Shahidi: Usiwe Unatumia Namba yako Binafsi tumia namba ya Wakala au Wasaidizi wako

Malya: Umeme lekeza Mbowe Cha Kufanya, Ni sahihi akitekeleza unachosema, Haitoonekana namba yake Bali Namba yako wewe

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Mheshimiwa Jaji Sina Swali Zaidi Kwa Jioni hii, Muda siyo Rafiki naomba Hairisho Muda Umeshakimbia Naomba Kuendelea Kesho ambapo Wakili wa Mshtakiwa Wa Pili ataendelea na Maswali yake kwa Shahidi

Jaji: Kufuatia Maombi ya Wakili John Malya nahairisha Mahakama Mpaka Kesho Tarehe 28 January 2022

Shahidi ataendelea Kutoa UShahidi: Wake akiwa Kizimbani

Upande wa Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi

Jaji anatoka

Like