Usajili soka la ‘majuu’ katika dakika za lala salama

KABLA hatujaanza msimu mwingine wa soka la kulipwa barani Ulaya, kumekuwa na vuta nikivute katika dirisha la usajili hasa hizi dakika za mwisho.

Ikiwa zimebaki siku 4 tu ligi ya Uingereza kuanza, klabu mbalimbali nchini humo zimeongeza kasi zaidi ya usajili huku nchi za Uhispania, Italia, Ujerumani pamoja na Ufaransa nazo hazijabaki nyuma.

Habari iliyotikisa vichwa vingi vya burudani duniani kote ni usajili ambao haukutarajiwa ni Messi kuhama Barcelona na kwenda PSG.

Usajili huu unatarajiwa ukamilika wiki hii kwani tayari baba mzazi wa nyota huyo pamoja na mwanasheria wake walionekana Ufaransa siku tatu zilizopita wakifanya majadiliano na klabu ya Paris saint Germain ( PSG) kwaajili ya nyota huyo kujiunga.

Leo Messi alionekana kwenye ndege akiwa na mke wake wakielekea Paris na baadae walionekana Uwanja wa ndege jijini Paris’. Inaamikina staa huyu amekwenda kukamilisha usajili wake na kumwaga wino kujiunga na miamba hao wa Ufaransa.

Hakuna aliyekuwa anajua hata siku moja Messi angeweza kutoka katika klabu hiyo iliyomkuza ya Barcelona. Kama ingetokea timu yoyote kumtaka basi kiasi cha pesa ambacho kingehitajika ni kirefu sana.

Lakini huwezi amini mwamba huyo anajiunga na PSG kama mchezaji huru baada ya makubaliano kati yake na klabu yake ya Barcelona kugonga mwamba.

Messi ameondoka akiwa mfungaji bora wa Barcelona, amefunga mabao 672 akiwa na ameshinda Mataji 36.

PSG wameweka rekodi ya kusajili wachezaji huru ambao ni mastaa wa soka la kulipwa na wenye thamani sana katika soko la soka. Baadhi ya wachezaji hao ni Wijnadam kutoka Liverpool, Ramos kutoka Real Madrid na sasa Lionel Messi kutoka Barcelona.

Mastaa hao wanajiunga na mastaa wengine wakubwa wa timu hiyo kama Neymar Jr, Kyline Mbappe,Di Maria, Ramos na wengine wengi.

Klabu ya Chelsea kutoka Uingereza imekamilisha usajili wa mchezaji Romelo Lukaku kutoka Inter Milan. Lukaku alitokea Everton alipong’ara na baadae kuchukuliwa na Manchester United na kisha kuuzwa Italia kwa mabingwa wa lingi hiyo msimu uliolita Inter Milan.

Akiwa Inter Milan, Lukaku alifanikiwa kuwa mfungaji bora huku akifanikiwa kufunga magori zaidi ya 40 katika michezo 64 aliyocheza na hata kuisaidia timu hiyo kubeba ubingwa wa Italia.

Chelsea wanataka kumrudisha Lukaku klabuni hapo kwani aliwahi kuichezea klabu hiyo Ila hakuwa na makali ya kutosha na hakuweza kufua dafu hadi kupelekea Chelsea kumuuza na sasa miamba hao wa Uingereza wamemsajili tena.

Kiasi cha €120m zilitolewa na mabingwa hao wa UEFA champions league, Chelsea FC kwenda kwa Inter Milan Ili kukamilisha usajili huo.

Usajili mwingine ambao unatarajiwa kukamililika ni Tammy Abraham ambaye anaondoka Chelsea FC kujiunga na miamba wa Italia, Roma FC. Usajili huo umewagharimu Roma kitita cha €34m kumng’oa staa huyo Stanford Bridge.

Miamba wa Uingereza kutoka London, Spur wanaamini watafanikiwa kuinasa saini ya nyota wa Inter Milan na Argentina, Martinez.

Nyota huyo amekuwa aking’aa sana huko Italia akiwa na klabu yake ya Inter Milan. Spurs wanataka kuongeza makali kwani msimu uliolita haukuwa mzuri kwa miamba hao.

Like
1