SINTOFAHAMU, VILIO VYATAWALA MSOMERA

Wadau wa haki za binadamu wamesema hawaridhiki na taarifa ya ripoti ya Tume ya Rais kuhusu uhamaji wa hiari kwa madai kuwa imeficha ukweli na ukatili unaofanyika katika makazi yao Msomera.

Wakizungumza na SAUTI KUBWA juzi baada ya kongamano la wadau Jijini Arusha, baadhi ya wanakijiji wa Msomera, wamesema wamekatishwa tamaa na ripoti ya tume hiyo, kwa maelezo kuwa haikueleza hali halisi ya mateso ya wenyeji, ambao maeneo yao ya asili yalitwaliwa na kugawanywa kwa wageni waliotoka Ngorongoro.

Mmoja wa wanakijiji, Sauda Kimweri, anasema tume ilifuta maoni na ushahidi wao wa ukatili uliotolewa dhidi ya haki za binadamu. Sauda anasema waliiambia tume jinsi walivyopigwa na kunyanyaswa, kiasi cha kusababisha baadhi ya akina mama wajawazito kuharibikiwa na mimba kutokana na vipigo hivyo vya kikatili, lakini tume ilipuuza ushahidi huo.

Tume imekiri wazi jambo moja tu – kwamba wenyeji wa Msomera hawakushirikishwa kabisa wakati ardhi yao inachukuliwa.

Wananchi hao walitoa maoni yao katika mkutano wa dharura ulioshirikisha viongozi na asasi zote za kiraia kutoka wilaya za Ngorongoro, Monduli, Simanjiro, Longido, Kilindi, na Handeni. wadau mbalimbali wa haki za binadamu

Mkurugenzi wa Shirika la CILAO, ndugu Odero Charles Odero, ameeleza kuwa lengo kuu la kongamano hilo ni kupitia na kuchambua ripoti zote mbili zilizoundwa na rais, ili kuweka msimamo wa pamoja na kupaza ssautijuu ya ukweli unaofichwa kuhusu hatima ya ardhi na usalama wa wananchi hawa.

Odero Charles Odero anasema:

“Tume imekiri wazi kuwa wananchi wana imani kubwa na NGOs, ingawa pia mashirika haya yamenyooshewa kidole kwa kudaiwa kukwamisha programu za serikali za uhifadhi endelevu.

“Baada ya kuzipitia ripoti hizi, tumeona iko haja kubwa ya dharura ya kukutanisha makundi yote: Jamii husika, Serikali, NGOs, na Wataalamu, ili kuzijadili kwa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya nchi nzima. Hilo ndilo azimio kuu tulilotoka nalo.”

Wadau hao wa haki za binadamu wameitaka jamii yenyewe kukutana haraka na kujadili ripoti hizo kwa kina. Lengo ni kuchunguza namna gani ripoti hizo zimegusa masuala yao ya msingi, na kupanga mikakati thabiti ya kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na tume ya rais.

Wadau wengine wanasemaje?

1. Dkt Mosses Mereto Mollel kutoka Ngorongoro Legal Aid Centre

2. Mwarabu Seneti, mkazi wa Msomera.

3. Sauda Kimweri, mkazi wa Msomera.

4. Paulo Oleshiro Mwanakijiki wa Kitwai B wilaya ya Simanjiro

Like