Salah awapumulia kisogoni Messi, Ronaldo

MOHAMED Salah, mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, ambaye timu yake itakutana na Real Madrid katika mechi ya fainali za klabu bingwa ulaya (UEFA), amesisitiza kwamba si vema watu kutazama mechi kama vile ni mchuano kati yake na Christian Ronaldo, mshambuliaji wa Madrid.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini London leo, Salah amesema hakuna mchezaji anayeweza kushinda mechi bila timu kushirikiana.

Si sahihi kusema fainali hii ni kati ya Salah na Ronaldo. Klabu yetu ni nzuri, ina wachezaji mahiri, na tumefika hatua hii kwa sababu tumeshirikiana vema,” amesema Salah.

Salah ameshafunga magoli 10, Ronaldo ameshafunga magoli 15 katika michuano ya UEFA mwaka huu. Klabu zao zinatarajiwa kucheza mechi ya fainali tarehe 26 Mei 2018 mjini Kiev, Ukraine.

Kuwaka kwa nyota ya Salah katika soka, hasa akiwa na Liverpool ya Uingereza, kumeibua mjadala mpya miongoni mwa wapenzi wa soka juu ya ushindani mpya kwenye tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Balloon d’Or,) ambayo kwa miaka 10 mfululizo imetawaliwa na Lionel Messi (Barcelona) na Ronaldo. Wote wawili wamebeba tuzo hiyo mara tano.

Katika msimu huu, Salah amefunga magoli 43 katika mashindano yote.

Like

Leave a Comment

Your email address will not be published.