Kanuni mbovu za mitandao zagonga mwamba mahakamani

TAARIFA kutoka Mtwara zinasema Mahakama Kuu imezuia zinasema serikali kutumia kanuni mpya za mtandaoni ambazo zilipangwa kutumika kuanzia tarehe 4 Mei 2018.

Hakama Kuu Kanda ya Mtwara leo imetoa zuio la muda (temporary injuction) linalozuia matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5, 2018.

Mahakama imetoa zuio hilo baada ya taasisi sita kuwasilisha mahakamani maombi ya kuzia matumizi ya Kanuni hizo April 30, mwaka huu.

Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Legal and Human Rights Cente (LHRC), Tanzania Human Rights Defenders (THRD), Media Council of Tanzania (MCT), Jamii Media, Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) na Tanzania Editors Forum (TEF).

Taasisi hizo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (judicial review) zimewashitaki Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba:-

i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake ( Ultra vires)

ii) Zinakiuka kanuni za usawa (natural justice)

iii) Kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza ( Freedom of exepression) haki ya kusikilizwa( rights to be heard) , na haki ya usiri ( Privacy rights)

Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 may 2018.

Like
6
2 Comments
  1. makaveli 6 years ago
    Reply

    Our judicial system has no credibility. It has been ifilrated and captured.The president is the law of the land ,eventually he will get his wish .

    2

    1
  2. Kakakuona 6 years ago
    Reply

    In a democracy, you need to have a strong judicial system. You need freedom of speech, you need art, and you need a free press.

    2

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.