Lissu ahoji sababu ya Rais Magufuli kujitenga na misiba mikubwa kitaifa

Naomba na hili la maafa nilizungumzie kidogo kabla halijazikwa na maajabu mengine ya nchi yetu.

Nadhani Mheshimiwa Rais wetu ana tatizo kubwa na misiba ya kitaifa ambalo wanaofahamu zaidi wanabidi watueleze.

1. Walipokufa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent Arusha mwezi Mei 2017, Rais Magufuli hakuhudhuria mazishi yale, ijapokuwa alikuwepo nchini. Serikali ikawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

2. Walipokufa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi mwezi September 2016, Rais Magufuli, aliyekuwa asafiri kwenda Zambia, aliahirisha safari hiyo lakini hakuonekana kwenye mazishi ya wahanga hao. Serikali ikawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

3. Walipouawa askari polisi 7 kule Kibiti Ijumaa Kuu ya 2017, Rais Magufuli alikuwepo nchini. Hata hivyo, hakuhudhuria mazishi ya askari polisi hao, badala yake aliyeonekana ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba.

4. Mara wakauawa wanajeshi wetu wa kikosi cha kulinda amani nchi DR Congo mwezi December 2017. Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hakuonekana Uwanja wa Taifa kwenye mazishi ya wanajeshi wetu. Aliyekwenda kwa niaba ya Serikali ni Waziri Mkuu Majaliwa.

5. Sasa wamekufa zaidi ya watu 200 kwenye Janga la MV Nyerere. Rais wetu badala ya kwenda kwenye mazishi, amemtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili yeye apate wasaa wa kunywa chai Ikulu na mapolisi wa usalama barabarani.

Rais wetu una shida gani na misiba hii ya kitaifa?

Like
1

Leave a Comment

Your email address will not be published.