DMP wanunua kesi ya Malasusa

Na Mwandishi Wetu

DAYOSISI ya Mashariki na Pwani (DMP) imetoa waraka maalumu wa kumtetea na kumlinda askofu wake, Dk. Alex Malasusa, ambaye ametengwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kulisaliti. Waraka huo utarajiwa kusoma katika sharika zote kesho Jumapili tarehe 6 Mei 2018; kwa waamini wale wale ambao Askofu Malasus alizuia kusomwa kwa waraka wa pasaka uliokuwa na salaam za maaskofu kuhusu amani.

Alifanya hivyo kwa ushawishi wa maofisa wa Ikulu na Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ambao kwa sababu wanazojua wao, waliona kuwa kusomwa kwa waraka huo kungepaka matope serikali ya awamu ya tano ambayo inalaumiwa kwa kumwaga damu nyingi ya raia, hasa wanaoipinga na wanaoikosoa, jambo ambalo linahatarisha amani na usalama wa nchi. Hatua hiyo ilisababisha Baraza Kuu la Maaskofu wa KKKT kumtenga yeye na wenzake mawili kama onyo.

Hata hivyo, kwa hatua yake kushawishi halmashauri kuu ya DPM ibebe msalaba wake na kumsafisha kwa waamini, atakuwa anatumia mbinu ya kwamba yeye akitenda kosa, ionekane kuwa dayosisi yake ndiyo imetenda kosa hilo. Baadhi ya wachungaji wake hawakubaliani na hatua yake hii.

Sakata la kutengwa kwa Askofu Malasusa limeibua mambo mengine zaidi. Mchungaji mmoja aliyehudhuria kikao cha halmashauri kuu na ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema barua aliyoandikiwa askofu Malasusa inasema wazi kuwa adhabu hii ni yake na si ya dayosisi.

“Yeye kama mjumbe wa nyumba ya maaskofu ndiye ametengwa lakini katika hali ya kulindana kuna watu wanataka ionekane dayosisi ndiyo imetengwa. Hatuwezi kukubali kubeba makosa ya mtu binafsi,” alisema mchungaji huyo, na kuongeza: “kesho ataiba, atachepuka, atatukana, kisha adai ni dayosisi.”

Katika hatua nyingine, malalamiko mapya yameibuka juu ya Askofu Malasusa kuwa amekuwa na tabia ya kuvunja ndoa za watu. Mchezo huo mchafu huufanya kwa kuwasiliana kwa siri na wana ndoa wa kike wafikao kwake kusuluhishwa.

“Mimi nimeacha kwenda kanisani baada ya askofu kunisumbua sana akitaka uhusiano wa kimapenzi baada ya mimi na mume wangu kwenda kusuluhishwa kwake,” anasema muumini mmoja wa KKKT.”

Mme wa mama huyo alilazimika kurudi kwao Afrika Magharibi baada ya kugundua askofu anamtaka mkewe kimapenzi. Hii inafanana na tuhuma zilizovuma sana siku za karibuni kuwa ana uhusiano na mchungaji wa kike ambaye ni mke wa mtu. Hivi sasa mchungaji huyo wa like anajiandaa kwenda masomoni Ujerumani, kitendo kinachotafsiriwa kuwa ni rushwa ya ngono, na wanaojua sakata hili wanaona ni njia ya askofu kumficha huko ili kupoteza ushahidi.

Habari nyingine zinasema kuwa hata waraka huu wa halmashauri hautokani na msukumo wa ndani ya kanisa, bali kuna mkono wa Ikulu nyuma yake kulinda na kutetea heshima ya Malasusa mbele ya waamini wa DMP, kwani ameingia matatani kwa sababu ya kulinda maslahi ya watawala.

SAUTI KUBWA imeweka hapa nakala halisi ya waraka huo.

Like
15
11 Comments
  1. Salome 6 years ago
    Reply

    Kusomea washarika waraka wa kumtetea askofu Mwalasusa ili hali kilichopelekea kutengwa ni waraka ambao haujasomwa kwa washirika sio haki kabisa na sio sahihi kabisa!!!Dayosisi ingekuwa imetengwa kwa ujumla wake labda ingelazimu Dayasisi ijitetee lakini askofu mwalasusa alifanya uamuzi bila kushauriana na washarika wake kwa nini anatetewa kiasi hcho??. Kwani washarika wa Dayosisi ya Mwalasusa hawaoni uchungu kwa mauaji na manyanyaso ya wananchi? Alikataza waraka usisomwe kwa faida ya nani? Tukumbuke Ubungo ina washarika wengi na baadhi ni kati ya waliovunjiwa nyumba bila fidia na kwa kejeli nyingi. Tundu Lisu kupigwa risasi hadharani mchana kweupeee, maiti ufukweni ndani ya viroba!!!n.k! Kanisa lilipaswa kupaaza sauti tangia kipindi kile na sio kukaa kimya. Hata waraka aliokataza usisomwe ulichelewa kwa hiyo watu waache unafiki ni kujipendekeza tu na Mwalasusa PhD yake anajua Biblia fika inaongeaje kuhusu mauaji ya wasio na hatia, uonevu, rushwa, dhuluma, ubaguzi, haki n.k

    4

    0
    • Shighadi 6 years ago
      Reply

      Huyu ni askofu wa ajabu kuliko wote ambao nimepata kuwafahamu, kashfa kubwa nyingi zinamkabili, nawashangaa wajumbe wa Halmashauri kuu ya Dayosisi wanaoendelea kumbeba, huu ni wokovu mkuu wa namna gani? Aachie ngazi tu.

      0

      0
  2. Makina 6 years ago
    Reply

    Hii ni mchezo unachezwa na system, Divide and rule?

    0

    0
  3. Mzalendo 6 years ago
    Reply

    Kuwa na Askofu wa aina hii ni hatari katika Taifa… Malasusa alaaniwe….

    1

    0
    • Elimwidimi mushi 6 years ago
      Reply

      Kama washarika wa kkkt tumesikitishwa sana na Halmashauri kuu kuiingiza DMP kwenye mgogoro wa askofu Malasusa, tumeshangazwa pia kwanini kutusomea waraka wao wakati waraka wa maaskofu wa pasaka haukusomwa kanisani? Tunafika mahali tunaanza kupoteza imani yetu na DMP

      1

      0
  4. benson msemwa 6 years ago
    Reply

    “Kila kukicha Afrika haikosi kituko”,

    Wengi wetu tumekuzwa kwenye mazingira tunayoamini kuwa viongozi wa dini huwa na roho mtakatifu na si mtakavitu

    Wenye kubeba sauti na maono ya kiMungu kwa sisi kondoo wanaotuchunga,

    Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,kama maaskofu zaidi ya 25 wote wameona kuna kosa baba Malasusa amelifanya,ni uungwana kwake kuomba msamaha na si kutengeneza huu utengano na mfarakano katika kanisa

    Yeye na mimi tutapita ila kanisa litabaki milele,kama hili ni la kweli,mpakwa mafuta wa bwana Malasusa amepoteza sifa na anapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu kwa ustawi chanya wa kanisa

    3

    0
  5. MAKIWERU 6 years ago
    Reply

    Yes

    0

    0
  6. Mtanzania 6 years ago
    Reply

    Huyu askofu kuna kitu anahofia. Angesoma waraka angekomeshwa na Bashite. Bashite angemwaga madhambi yake hadharani. Simple, ni kuwa huyu askofu siyo honest.

    0

    0
  7. MAKUSARO SIRIELI HERMANNI 6 years ago
    Reply

    Labda ushauri wangu kwa waumini na wasio waumini wa KKKT na DMP
    Tuendelee kumtii MUNGU na siyo wanadamu.
    Kwa Baba na Mama zangu HALMASHAURI KUU,hivi mlifikiri kwa akili na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU wakati mnaandaa Barua hii?NINATIA SHAKA.Nanyi tunawaombea.VIZURI TUSOME kwa makini unabii wa EZEKIELI

    0

    1
  8. Mtanzania 6 years ago
    Reply

    @Makusaro, tuache kutumia maandiko, ili kuwapa watawala fursa ya kujinufaisha wenyewe. Mimi naamini utawala huu maongozi yake ni ya kiibilisi. Hakuna mtawala anayemcha Mungu anayeweza kufunga mdomo wake huku akitazama haya maovu yakitokea.

    0

    0
  9. Jaimee 6 years ago
    Reply

    Haya mambo yananikumbusha ule mgogoro waliotengenezewa cuf ya kweli kwakupitia Lipumba.Lengo ni kunusuru mambo yao ya hovyo yaliyofanywa ktk uchaguzi.Na ndivyo ilivyo ktk hili la Malasusa,yani Malasusa +Lipumba= Usaliti na upumbavu.

    0

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.