Wavuvi haramu waidindia serikali: Hawakamatiki

Naweza kukushuhudia kuwa kazi ya uvuvi haramu imeweza kuniharakishia maisha kwani nilioa, nikanunua gari na kujenga angalau nyumba ndogo…

DAWA ya kukomesha Uvuvi Haramu bado haijapatikana nchini Tanzania, licha ya kuwepo kwa doria mbalimbali zinazofanyika katika ‘Feri ya Kivukoni’ na nyingine zinazonguka Pwani ya Dar es Salaam ya Bahari ya Hindi.

Licha ya jitihada za serikali kuwapiga vita, wavuvi haramu wanaendelea na uvuvi wao, bila kujali adhabu na sheria zzilizotungwa dhidi yao, kwa maelezo kuwa uvuvi hio ndiyo unawapatia kipato chao cha kila siku.

Kwa mtazamo wa serikali, kisheria, uvuvi haramu unaojadiliwa katika uchunguzi huu ni ule wa kuvua kwa nyavu zenye matundu madogo chini ya inchi tatu na ule wa kutumia mabomu au baruti.

Sheria dhidi ya uvuvi haramu ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho mbalimbali mwaka 2020, inasema:

“Mvuvi atakayekamatwa amevua samaki kwa mabomu/baruti, samaki hao watatahifishwa na serikali pamoja na vifaa na  vya uvuvi walivyonavyo.”

Pia sheria hiyo, itamtaka kufunguliwa mashtaka makahamani na endapo mhusika atabainika kuwa na kosa atatakiwa kulipa faini ya sh milioni mbili au tano na kupewa kifungo cha miaka miwili hadi mitatu kulingana na ukubwa wa kosa.

Na wavuvi watakaokamatwa wakitumia nyavu zilizo chini ya kiwango (makokolo) adhabu yao ni kutaifisha samaki au dagaa, nyavu hizo pamoja na chombo (boti ama ngalawa).

Sheria iko wazi: “Mvuvi huyo atafikishwa mahakamani kwa ajili ya mashtaka na endapo watabainika watatakiwa kuilipa serikali sh. Milioni moja, kifungo cha mwaka mmoja na nyavu hizo kuteketezwa.”

Wavuvi haramu wasimulia wanavyofanya kazi hiyo

SAUTI KUBWA, katika uchunguzi huu, imebaini uhaba doria za mara kwa mara. Baadhi ya wavuvi haramu waliohojiwa katika Soko la Kimataifa la Samaki, Feri Kivukoni na Kunduchi wamekiri kufanya uvuvi haramu. 

Sababu kuu ya kushamiri kwa uvuvi haramu, kwa mujibu wa kauli.zao,  ni ugumu wa maisha unaowachochea kupata fedha ya haraka. Sababu ya pili ni ukosefu wa zana za kuvulia katika kina kirefu cha maji baharini.

Juma Halii (si jina lake rasmi) ni mmoja wa wavuvi hao. Anasema huu ni mwaka wa 17 tangu aanze kushiriki uvuvi huu katika ufukwe wa Kunduchi. Anatumia mtumbwi (ngalawa).

Aliianza akiwa kijana mwenye umri wa miaka 19 na sasa ana miaka 36 mwenye familia ya mke mmoja na watoto wanne.

Anasema alianza kwa kushirikiana na mwenzake mmoja katika kuvua kwa kupokeza chombo/ngalawa lakini hali ikawa mbaya ya upatikanaji wa samaki kwa kuwa ngalawa yao siyo ya kubeba mzigo mkubwa hivyo kuwalazisha kufanya uvuvi usiyokuwa na faida.

Anasema akiwa katika shughuli hizo baharini, waliamua kujadiliana na wavuvi wenzake kuanza uvuvi wa haramu ili wapate fedha za haraka na kuwanikiwa Maisha.

“Tukiwa na zaidi ya miaka ya 10 katika harakati zetu za uvuvi, hatukuweza kufanikiwa, nilipoamua kuingia katika kazi ya uvuvi haramu angalau kwa muda wa miezi sita na mambo yaliweza kuwa mazuri sana.

“Kazi hii niliifanya wenzangu watatu ambao nao watumia ngalawa kuvua samaki hivyo tunashirikiana kuandaa makokoro na tunaongozana kuingia baharini kuvua”

“Shughuli hii tulikuwa tukiifanya usiku mkubwa na kwa kuwa hatuna mitumbwi/ngalawa zisizo na uwezo wa kwenda kina kirefu… tunavua katikakina kifupi na yalipo mazalia ya samaki na kuleta sokonikuuva kwa haraka.”

Halii anasema baada ya kumaliza mnada wa samaki usiku saa 7 hadi 9 urudi majumbani kwao kupumzika kwa ajili ya kuingia baharini tena usiku” 

Anasema kazi ya kuandaa ngalawa zao na chambo kwa ajili ya samaki wakubwa hufanywa na vibarua ambao ulipwa kwa kazi hiyo.

“Naweza kukushuhudia kuwa kazi ya uvuvi haramu imeweza kuniharakishia maisha kwani nilioa, nikanunua gari na kujenga angalau nyumba ndogo kwa kazi hiyo.

“Si mimi tuu, hata wenzangu wote tulioshirikiliana katika jambo hili haramu tumevuka katika kimaisha ingawa ni hatari endapo kuingia mikono mwa mwa Jeshi la Polisi awakiwa katika doria yao,” anasema Halii.

Anasema baada ya kufanikiwa kimaisha aliendelea na shughuli hiyo kwa kushirikiana na haohao wenzake.

“Siku moja usiku mkubwa nikiwa na marafiki zangu katika shughuli yetu ya uvuvi … kwa mbali tuliiona boti/fiber ya polisi ikitukimbiza il tukamatwe”

Anasema kwa bahati mbaya mwenzao mmoja alishindwa kukimbia na ngalawa yake isipokuwa yeye na wenzake wawili kufanikiwa kukimbia hata kufika nchi kavu wakiwa na mzigo kigo wa samaki kwani walitaka kukamatwa wakiwa waanza kuvua.

“Kwa masikitiko makubwa mwenzetu hatumwona tena huu sasa mwaka wa pili… hatukujua kama alizama majini ama alichukuliwa na polisi wa doria… tulifatilia bila mafanikio”

“Kufuatia tukio hilo, mimi Halii niliachama na kazi ya uvuvi haramu inagwaje wenzangu bado wanaendelea ingawa hawafanyi mara kwa mara … wanaweza kwenda mara moja kwa mwezi”   

Mvuvi mwingine, Hamidu (alitaja jina moja tu la kweli) wa Soko la Kimataifa Feri – Kivukni jijini Dar es Salaam, anasema uvuvi haramu upo na unaendelea na nyavu sizizo za viwango zenye chini ya nchi tatu kutengenezwa na wataalum wa kazi hiyo hapo hapo feri. 

“Mimi baada ya kucha kazi ya uvuvi haramu, nilianza kufanya biashara ya kutengeneza makokoro ambayo yananilipa sana kuliko kuuza nyavu halali za kuvulia.

“Asikwambie mtu…. Uvuvi haramu unalipa hasa katika kipindi chenye samaki wengi, maana kazi hizi hufanyika usiku na mnada wake usiku kwa usiku.

“Katika mwambao huu Pwani ya Dar es Salaam, kazi hii hufanyika katika fukwe zisizo rasmi kama Kawe, Mbweni, Mbezi Beach, Ununio, Kigamboni na kwingineko.

“Nyavu makokoro wanazipata hapa na kwenda kuendelea na shughuli zao, kisha kuwahi mnada alfajiri hapa Feri maana ndipo lilipo soko la kimataifa la samaki.

“Wavuvi wengi wanaojishugulisha na uvuvi haramu wamefanikiwa sana kimaisha ingawaje ni hatari endapo utaingia mikono mwa polisi na maofisa doria.”

Polisi waelemewa

Ufanisi wa Jeshi la Polisi kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa Bahari ya Hindi umekwama kutokana na ukata wa bajeti yake, imefahamika.

Uchunguzi wa SAUTI KUBWA kwa miezi kadhaa katika mialo na bandari bubu zisizo rasmi za uvuvi katika Mkoa wa Dar es Salaam umebaini kushamiri kwa uvuvi haramu wa kutumia nyavu zilizo chini ya nchi tatu yaani makokolo.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Maji, Kamishna Msaidizi wa Polisi Moshi Sokoro amekiri Ugumu huo na kwamba ndiyo sababu ya polisi kushindwa  doria za mara kwa mara.

“Kwa kweli doria tunafanya mara moja kwa mwezi … hiyo inatokana na kutokuwa na fedha za doria na kwa sasa tuna boti moja tu.

“Hata hivyo, tunajitahidi kushirikiana na wadau wetu wakiwemo maofisa wa uvuvi kutoka katika halmashauri za Kinondoni na Ilala ambao hutoa mafuta ya doria na maofisa wao.”

Kamanda Sokoro amesema pia kuwa wavuvi haramu wamekuwa hawakamatiki kutokana na boti moja aina ya Fiber waliyonayo ambayo tayari wavuvi wanaijua. Jeshi la Polisi wanapokuwa katika doria wavuvi hukimbia na kutelekeza nyenzo zao kama vile nyavu/makokoro na boti wanazozitumia.  

Mwaka huu 2023, jeshi hilo limewakamata watuhumiwa wawili tu wa uvuvi haramu na kuwafikisha mahakamani.

“Katka matukio hayo mawili kuna kesi moja Mahakama ya Mwanzo Kigambon na nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zote zikiwa za matukio tofauti katika uvuvi haramu wao.

Kila kesi ina mtuhumiwa mmoja. .moja alitiwa kizuini na kutuhumiwa kwa kuvua samaki kwa baruti na mwingine alikutwa na nyavu zilizo chini ya inchi tatu, yaani makokoro.

Maofisa Uvuvi wanena 

Maofisa uvuvi katika Soko la Kimataifa La Feri – Kivukoni na Halmashauri ya Kinondoni, nao wamekiri kuwapo kwa uvuvi haramu hasa wa kutumia nyavu zilizo chini ya inchi tatu ambazo huitwa makokoro.

Ofisa Uvuvi Soko la Kimataifa La Feri Ramadhani Mtabika anasema upo uvuvi haramu wa aina nyingi ingawaje ulioshamiri ni ule wa makokoro ambazo zinatum,ika katika kina kifupi.

“Kisheria nyavu zinazotakiwa kutumika kuvua dagaa ni zenye kuanzia inchi tatu ambazo uvuvi wake unafanyika katika kina kirefu … lakini wavuvi haramu hutumia nyavu zilizo chini ya kiwango hicho,” anasema 

 Snasema uvuvi mwingine haramu ni ule wa kuvua kwa mkuki uitwao (mchinji) ambao hutumika kumchoma samaki na kumtoa majini.

Pia anasema upo uvuvi wa baruti au mabomu ambapo samaki aliyevuliwa hivyo huonekana ana damu katika macho na mbavu.

Samaki wenye dalili hizo, baada ya kukamatwa  hupelekwa kwa mkemia mkuu ili kuchunguzwa na hatua zaidi huchukuliwa.

Anasisitiza: “Mwaka huu Februari 2023 tuliikamata boti/fibre iliyotelekezwa na nyavu/ makokoro maeneo ya Masaki jijini walipokuwa wakivua dagaa kwenye mazalia ya samaki … hatukufanikiwa kuwakamata wavuvi. Walikimbia.

“Kazi yetu kutwa tuliotakiwa kuifanya ni kukamata hiyo boti na samaki na dagaa kisha kuwapeleka kwa mkemia mkuu kuchunguzwa … na hatua zaidi kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Mtabika anasema kuwa  idara yao ndiyo hupeleka ripoti ya shughuli za uvuvi miezi mitatu mitatu kwa Bodi ya Soko hilo.

“Ripoti ya miezi mitatu ya Mei, Juni, Julai mwaka huu 2023 inaonyesha kuwapo kwa uvuvi haramu mkubwa. Mwezi  Mei tulikamata ngalawa/mitumbwi mitatu, kokoro moja na fiber/boti moja. Juni tulikamata makokoro manne huku, mwezi Julai tulikamata makokoro matatu na mitumba mitatu”

“Pia wawvuvi hawa wamekuwa na tabia ya kujitengenezea makokoro yao wao wenyewe kwa kupunguza nyavu zilizo halali na kuweka zisizo halali ili kufanya kqzi haramu yao,” anasema.

Kwa mujibu wa Mtabika, katika kukabiliana uvuvi haramu, wameweka mikakati ya muda mfupi na  mrefu ya kukabiliana na uvuvi haramu ambao Soko limepanga kuendeleza doria ya kushitukiza kwa kutumia boti/fiber ya manispaa ama ya polisi wa kitengo cha majini.

Pia anasema soko hilo mara kwa mara huandaa bajeti kwa ajili ya kutoa elimu/ mafunzo kwa wavuvi kuhusu sheria za uvuvi na madhara ya uvuvi haramu.

Naye Ofisa Mahusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Aquilinus Shiduki anasema kuwa Halmashauri hiyo ina mialo/fukwe sita ambazo Kunduchi, Ununio, Kawe, Masasani, Bweni na Mbezi Beach.

Anasema fukwe hizo sita zinasimamiwa vikundi shirikishi ambavyo vinajulikana kwa Jina la Beach Managements Unit (BMU) ambao hao utoa taari zote kwa maofisa uvuvi kuhusu hali ya fukwe na uvuvi unaondelea.

Shiduki anasema pamoja na kusimamiwa na BMU uvuvi haramu upo  na matukio kwa mwaka fedha katika mwaka 2022 /2023 ni mengi kwa kukamata nyavu haram una mishipi na mitumbwi hata boti/fiber zinazofanya shughuli hizo.

“Mwaka wa Fedha 2022/2023 tumekamata nyavu za uvuvi haramu aina ya Juya 24, mishipi 120… matumizi ya vilipuzi /baruti idadi haiko sawa ila yanarudi kwa kasi ila yanadhibitiwa na BMu”.

“Uvuvi wa baruti si la manisaa bali serikali inakabiliana nalo…na wote wanaobainika kufanya vitendo hivyo ukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sharia”anasema 

Shiduki anasema kama manispaa wanakabiliana na uvuvi haramu kwa njia mbalimbali ikiwamo ya kutoa elimu kwa jamii na wavuvi juu ya  hasara ya kuua mazalia ya mayai na samaki ikolojia kwa namna wanavyotumia vilipunzi na makolokolo.

Anasema pia manispaa hiyo inatutoa elimu na kuimarisha mafunzo kwa BMU na kuweka doria kwa kutumia boti maalum/fiber.

Kuhusu ushuru katika fukwe hizo, Shiduki anasema tozoz inazokisanywa katika fukwe hizo ni za minada ya samaki, leseni za uvuvi na leseni za vyombo uvuvi.

Hivyo anasema katika mwaka 2022/2023 kwa pamoja zimepatikana shilingi 212, 028,150/= katika ushuru huo.

Kauli ya Meneja wa Soko la Kimataifa

Meneja wa Soko la Kimataifa la Feri Kivukoni- Kigamboni Selemani Abdallah Mfinanga anasema uvuvi haramu ni changamoto iliyopo hapo Feri ambayo hujitokeza mara kwa mara.

Mfinanga anasema katika ripoti ya robo mwaka, yaani miezi mitatu mitatu, matukio ya uvuvi haramu yanakuwamo kwa idadi mbalimbali. 

Anasema wanakabiliana na matukio hayo kwa kutenga fungu la pesa kwa ajili ya doria za kushtukiza mara moja kwa mwezi na mafunzo kwa wavuvi juu ya uvuvi haramu.

Akielezea kuhusu takwimu za uingiaji wa samaki katika soko hilo,  anasema linaingiza samaki kutoka katika fukwe mbalimbali zikiwamo za Kunduchi, Zanzibar, Mafia, Bagamoyo, Kawe, kutoka maziwa na katika Mabwawa yanayozalisha samaki wengi wa kuuzwa.

“Soko hilo huwa lina takwimu za miezi mitatu, mitatu ya samaki wanaoingizwa hivyo kati ya January hadi Machi wameingiza kilo 2, 918,770 na  waliouzwa kwa mnada sh. 3,359 kwa kilo moja  ambapo waliuzwa kwa gharama ya sh zaidi ya Bilioni 9”

“Katika fedha hizo, serikali ilichukua asilimia 3 ya kile kilichouzwa katika mnada huo … na mabadiliko ya takwimu hizo utokea kutoka na wingi au uchache wa samaki” anasema

Mfinanga anasema biashara ya samaki inaendana msimu ambapo kama wakati samaki ni kidogo na wakati mwingine wengi mfano mwaka huu soko limepokea zaidi ya tani 2000 wakati kwa mwezi Juni na Julai kupokea zaidi ya tani 1000.

Aidha anasema  upatikanaji wa samaki  unaweza mzuri hata kulipatia soko fedha kubwa ya ushuru lakini pia unaweza kupungua kwa kasi kubwa kutokana na hali ya hewa (mawimbi na upepo)

“Samaki wanaopatikana kwa wingi katika soko hilo ni dagaa mchele, vibua, saladin, ndolo, msusa, palawe na wengine wengi mchanganyiko.”

“Samaki hawa wanauzwa ndani na nje ya nchi katika nchi za Congo, Malawi, Burundi, Kenya Uganda na katika mataifa ya ulaya ila si sana”

“Changamoto zilizopo katika soko hili za utawala ni kwa upande wa wavuvi na wafanyabiashara za samaki kulalamikia tozo kubwa,” anasema 

 

Je, sera na sheria zinasimamiwa vizuri kiasi gani? Fuatana nami katika toleo lijalo.

Like