Soka duniani: Klabu zapanda na kushuka dau kusajili nyota msimu ujao

MANCHESTER City watalazimika kupanda dau la Euro miloni 40 zaidi ili kufikisha dau la Euro milioni 160, lililowekwa na Spurs kama bei ya mshambuliaji wake nyota, Harry Kane 27. (Star)

Klabu ya Chelsea haijakata tama na ina matumaini ya kuinasa saini ya mshambuliaji raia wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, 28, anayekipiga kwenye klabu ya Inter Milan. (Athletic)

Barcelona wanajiandaa kutangaza rasmi Messi 34, kutia saini kwenye kandarasi yake mpya klabuni hapo itakayodumu kwa miaka mitano. (Sport)

Newcastle United wameulizia juu ya upatikanaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Wales na klabu ya Juventus, Aaron Ramsey 30. (Goal)

Klabu ya Manchester United, ina miezi 12 ya kumshawishi mshambuliaji kinda wa Norway na klabu ya Dortmund Erling Braut Haaland kuwa wao ndo timu sahihi kwake. Kinda huyo aambaye nanyatiwa na timu ya Chelsea, anatarajiwa kuwa atasalia klabuni kwake mpaka mwishoni mwa msimu wa 2022, na bei yake itakuwa ni Euro milioni 75, kama kandarasi yake inavyoeleza. (Manchester Evening News)

Timu ya Aston Villa, imetuma dau la pili baada ya dau lau la kwanza (Euro milioni 25) kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Southampton na timu ya taifa ya Uingereza, James Ward Prowse kukataliwa. (Mail)

Klabu za Leicester City, Leeds United ma Everton zinapigana vikumbo katika juhudi za kumnasa winga wa Uhispania na klabu ya Real Madrid, Marco Asensio, 25. (Fichajes)

Atletico Madrid wanajiandaa kumuuza beki wao Kieran Trippier 30, kwenda Manchester United na wanamnyatia beki wa As Roma Alessandro Florenzi, 30 kama mbadala wake. (AS)

Sheffield United wapo kwenye mazungumzo ya usajili na mshambuliaji Ronaldo Vieira, 23, anayekipiga Sampdoria. (Mail)

Kalbu ya Chelsea itapaswa kumuuza mchezaji wake ili iweze kuinasa sainini ya beki wa Sevilla Jules Kounde 22. (Express)

Like