Messi na PSG: Avutia mashabiki juu ya taswira yake halisi kwa vitendo

LIONEL Messi, gwiji wa soka katika zama hizi, alianza kwa kusuasua katika klabu yake mpya ya Paris Saint-Germain (PSG), lakini baada ya kuwa amesoma mchezo, sasa mambo yameanza kubadilika na amekuwa gumzo la mashabiki na wachezaji wenzake kuhusu anavyojitoa kwa timu yake mpya, hasa kwa jitihada alizoweka ili kusaidia PSG iibuke na ushindi dhidi ya Manchester City.

Timu hiyo ya Ufaransa ilipata ushindi wa 2-0 kwenye Ligi ya Mabingwa wakati Messi akiifunga bao lake la kwanza kwa kilabu na kumaliza vizuri kwa kupata alama hizo tatu.

Wakati huo wa miujiza ulikuwa hatua kubwa ya kuongelewa wakati wote, ni tukio lingine linalohusu nahodha huyo wa Argentina lilovutia ulimwengu wa mpira.

PSG walikuwa wakitetea ushindi wao wa mabao mawili kuelekea mwisho wa mechi wakati City walipojaribu kurudi kwenye mchezo dakika za mwisho.

Messi alionyesha utayari wa fikra (kujiunga na kikosi cha kwanza) wakati alijilaza chini kujiunga na wenzake kuweka ukuta wakati wa mpira wa adhabu uliokuwa upigwe na Mahrez kuelekea lango la PSG.

Mshambuliaji huyo anaweza asiwe na mwanzo mzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa hayuko tayari kuvuta soksi zake na kufanya kazi ya ziada kwa timu yake hiyo.

Like