Messi atua rasmi PSG

Jumapili iliyopita, Messi alionekana akimwaga machozi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari na kukiri kuwa haikuwa nia yake kuondoka klabuni Barcelona, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, imembidi aondoke.

MWANASOKA mahiri wa zama hizi, Lionel Messi, alikwisha kubaliana na Barcelona kutia saini kwenye kandarasi mpya ya miaka 5, ambayo ingemfanya akatwe asilimia 50 ya jumla ya mshahara wake wa awali ili kusalia klabuni hapo.

Hata hivyo, dili hilo halikufanikiwa katika hatua za mwisho kwani hata kwa kufanya hivyo, bado Barcelona wangekuwa wanakiuka sheria ya kiwango cha mishahara ya wachezaji kwenye ligi ya La Liga.

“Alikuwa akipokea Euro milioni 140 kwa mwaka akiwa Barcelon, Baada ya kukubali kusalia klabuni hapo, aliridhia kupunguza msahahara wake kwa asilimia 50. Ili kumbakisha Messi, Barcelona walipaswa kupunguza mshahara wa Messi hadi asilimia 0, jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani. Hii ni kutokana na deni la Euro bilioni 1 linalowakabili,” alisema Guillem Balague katika mahojiano na BBC Radio 5.

Kwanini Messi ameondoka Barcelona?

Kuhakikisha Messi anasalia kblabuni Barcelona ndo kilikuwa kipaumbele cha Rais mpya wa klabu hiyo, Joan Laporta. Lakini majaribio ya kuhakikisha jambo hilolinafanikiwa yalikumbwa na changamoto kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikumba timu hiyo kwa sasa.

Messi alikuwa mchezaji huru tangu tarehe 1 mwezi Julai, lakini hakukuwa na shaka juu ya mustakabali wake klabuni hapo. Hi indo ilikuwa imani ya kila mtu mpaka Barcelona walipotoa tamko kwamba Leo Messi ataondoka klabuni hapo kutokana na matatizo ya kifedha na kimfumo yanayoikumba timu yao.

Safu hatari zaidi ya ushambuliaji?

Kwa mara ya pili, Messi anaenda kukutana na Neymar, waliowahi kucheza pamoja Barcelona. Wawili hawa watashirikiana na kinda nyota Kylian Mbappe ambaye wengi wanamtabiria kama mrithi wa Messi na Ronaldo. Kwa safu hii, tutegemee makubwa!

Takwimu za Messi

Messi anadhaniwa kuwa mchezaji bora wa soka kuwahi kutokea duniani, amepachika mabao 672 kwenye michezo 778 aliyoicheza akiwa na Barcelona toka alipojiunga na timu hiyo akiwa na miaka 13. Ametwaa tuzo ya mchezaji bora duniani (Ballon d”Or) mara sita, na ametwaa mataji 35 akiwa na Barcelona.

Ukurasa Mpya

Sasa Messi ametua rasmi PSG, Ufaransa. Baada ya kusajiliwa na PSG, Lionel Messi,34, alisema: “ Nimefurahi sana kuanza ukurasa wangu mpya na Paris St-Germain. Kila kitu kinachoihusu timu hii, kinaendana na malengo niliyonayo.

Ninao ufahamu jinsi klabu hii ilivyo na vipaji vikubwa, kuanzia kwa wachezaji mpaka kwenye benchi la ufundi na hivyo nimedhamiria kusaidia katika ujenzi wa jambo kubwa kwa ajili ya timu na mashabiki. Ni shauku yangu kubwa kuwa mwenyeji wa dimba la Parc des Princes.”

Like