Messi aondoka Barcelona

TOFAUTI na matarajio ya wengi, kilichodhaniwa kuwa hakiwezekani, hatimaye kimewezekana!

Leo hii majira ya jioni, klabu ya Barcelona imetangaza rasmi kuwa mshambuliaji wake mkongwe Leo Messi, hatarejea tena na ameondoka rasmi klabuni hapo.

Hii inatokea baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Barcelona na Messi kuzaa matunda na leo hii vyanzo mbalimbali vikubwa duniani viliripoti kuwa leo jioni Messi angemwaga wino kwenye mkataba mpya ya miaka mitano na klabu hiyo.

Tukio hili limekuwa tofauti na matarajio ya wengi na imethibitishwa kwamba uamuzi huu umefikiwa kati ya pande zote mbili kutokana na mdororo wa kiuchumi unaoikumba ligi ya La Liga hasa timu ya Barcelona.

Tamko kutoka klabuni hapo limesema:

“Licha ya klabu ya Barcelona na Leo Messi kuwa tumefikia makubaiano na kuwa na nia thabiti ya kuongeza mkataba mpya leo, azma hiyo imeshindikana kutokana na changamoto za kifedha (kanuni za ligi ya La Liga)_

“Kwa sababu hiyo, tunasikitika kutangaza kuwa Messi hataweza kusalia klabuni Barcelona na hivyo matakwa ya mchezaji na klabu hayataweza kutimia.

“Timu ya Barcelona inatoa heshima zake za dhati kwa Messi, kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa timu hii na tunamtakia mustakabali mwema, katika maisha yake ya kisoka na maisha yake binafsi. “

Like
1