Maalim Seif aivaa benki kuu, aitaka irejeshe milioni 76 za CUF

CHAMA cha Wananchi (CUF), kupitia kwa Katibu Mkuu Maalim Seif Shariff Hamad, kimeitaka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kurejesha Sh. 76 milioni kwa chama hicho.

Kwa mujibu wa Salum Bimani, Mkurugenzi wa Habari wa CUF, chama kinataka benki kuu irejeshe fedha zake ambazo zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti za chama kinyume cha sheria na taratibu.

Benki kuu iliamuru fedha hizo zichukuliwe kutoka akaunti za CUF katika kile ambacho Bimani anaita “utatu mchafu” wa msajili wa vyama vya siasa, vyombo vya dola na taasisi za fedha, na Profesa Ibrahim Lipumba.

Barua hiyo inasema kuwa hatua hiyo ya benki ni moja ya njama za serikali kuhujumu demokrasia na utawala wa sheria.

Nakala ya barua inapatikana hapa.

Like
1
1 Comment
  1. Jovent Johansen Mushwaimi 6 years ago
    Reply

    Naaam hujuma dhidi ya CUF ni mkakati mzito ambao umeratibiwa kwa muda mrefu tu.

    0

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.