Badala ya babake Meghan, sasa Prince Charles ndiye atamkabidhi bibi harusi Meghan kwa Prince Harry siku ya harusi

FAMILIA ya kifalme ya Uingereza imetoa taarifa kwamba Prince Charles, baba mzazi wa bwana harusi mtarajiwa Prince Harry,  ndiye atakayemkabidhi bibi harusi mtarajiwa Meghan Markle kanisani kwa mumewe mtarajiwa siku ya harusi. Kwa kawaida baba mzazi wa bibi harusi ndiye humkabidhi binti yake kwa bwana harusi.

Uamuzi huo unatokana na wingu lililotanda juu ya afya ya Thomas Markle, baba mzazi wa Meghan. Awali, kulikuwa na taarifa kwamba mama yake Meghan angeweza kuchukua nafasi ya baba yake, lakini kutokana na uzoefu mkubwa alionao Prince Charles katika shughuli kubwa kama hizi imeonekana achukue nafasi hiyo.

Harusi ya Prince Harry na Meghan itafanyika kesho Jumamosi katka kanisa la St George’s Chapel, London. Haikumbukwi ni lini mara ya mwisho baba mzazi wa bwana harusi alichukua nafasi ya baba mzazi wa bibi harusi katika tukio kubwa kama hili, hasa linalohusisha familia ya kifalme.

Like
1

Leave a Comment

Your email address will not be published.