Kwanini Kabudi ameongopea Bunge?

WIKI hii, Profesa Palamagamba Kabudi, aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania katika serikali ya awamu ya tano, ametaja bungeni baadhi ya nchi ambazo, kwa kauli yake, haziruhusu uraia pacha. Alizitaja nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani, Uholanzi, Denmark na Saudi Arabia.

Takwimu zifuatazo zinaonyesha kuwa Profesa Kabudi hakusema kweli. Hali halisi iko hivi:

Ujerumani: wanaruhusu uraia pacha.

Kuanzia January 1, 2000, Ujerumani iliingiza haki ya udongo ( jus soli) kwenye sheria yake ya uraia

Kuanzia tarehe 1 January 2000, mtoto aliyezaliwa ujerumani na wazazi wasio wajerumani, anapata uraia wa kuzaliwa kama mmoja wa wazazi ametimiza masharti ya ukazi.
ii) Mmoja wa wazazi awe ameishi kihalali Ujerumani
kwa miaka 8.au
ii) Mmoja wa wazazi amekuwa na kibali cha ukazi miaka 3 kabla ya mtoto kuzaliwa.

Kabla raia wa Kijerumani hajajipatia uraia wa nchi nyingine ya kigeni ambayo siyo mwanachama wa EU au Switzerland, atatakiwa kuomba ruhusa ya kubaki na uraia wake wa ujerumani – Section 25(1) ya sheria ya uraia.

Kuanzia tarehe 28 August 2007 Raia wa nchi wanachama wa EU na Switzerland wanaruhusiwa kuwa raia wa kuandikishwa wa ujerumani bila kulazimishwa kukana uraia wa nchi zao.

Raia wa kuzaliwa wa Ujerumani anaweza kujipatia uraia wa nchi nyingine mwanachama wa EU pamoja na Switzerland bila kupoteza uraia wa Ujerumani.

Mtoto anayezaliwa kati ya raia wa ujerumani na mmarekani, anakuwa na uraia pacha maisha yake yote.

Sheria mpya ya ujerumani inayofanyiwa kazi sasa hivi, itaruhusu raia wa kuandikishwa kutoka nchi zisizo wanachama wa EU kukaa na uraia wa nchi zao za asili pindi wapatapo uraia wa ujerumani.

Uholanzi: Wanaruhusu uraia pacha.

*Mholanzi mwenye uraia wa nchi mbili hapotezi uraia wa nchi yake isipokuwa akikaa nchi ya kigeni kwa miaka zaidi ya 13 mfukulizo bila kuomba kubadilisha passport ya uholanzi au kuomba kitambulisho chochote cha taifa. Hii ni kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria ya April 1 2022. Ibara ya 15 ya sheria ya uraia.

Mgeni mwenye ndoa na muholanzi upata uraia na kubaki na uraia wa nchi yake ya asili.

*Wakimbizi upata uraia na kubaki na uraia wao wa asili.

Denmark: Inaruhusu uraia pacha.

Kuanzia September 1, 2015 sheria mpya ya uraia inaruhusu raia wa Denmark kujipatia uraia wa nchi ya pili bila kupoteza uraia wa Denmark. Vile vile raia wa kigeni wanapata uraia wa Denmark bila kutakiwa kukana uraia wa nchi zao za asili.

Watoto wenye asili ya Denmark waliozaliwa nje ya nchi wanatakiwa kufanya maombi ya kubaki na uraia wao wa Denmark wanapokuwa na umri kati ya miaka 21 na 22.

Austria: Inaruhusu uraia pacha.

Raia wa Austria kabla ya kujipatia uraia wa nchi nyingine, inabidi atume maombi ya kubaki na uraia wake wa asili. Hii ni sawa na sheria ya uraia ya Africa Kusini.

Mtoto wa Kiaustria aliyezaliwa na uraia wa nchi mbili hatakiwi kuchagua nchi moja kati ya nchi hizo mbili hatimizapo umri wa mtu mzima. Anakuwa na uraia pacha maisha yake yote. Hii ni kwa mujibu wa section ya 7 ya sheria ya uraia.

Raia wa kigeni aliyepewa uraia wa Austria kwa sababu ya kiuwekezaji ( ibara ya 10(6) ya sheria ya uraia) halazimiki kukana uraia wa nchi yake ya asili.

Saudi Arabia:

* Mwanamke wa Kisaudia, hapotezi uraia kwa kuchukua uraia wa nchi ya mume wake wa kigeni, isipokuwa kama nchi hiyo ya kigeni hairuhusu uraia pacha.

Asilimia ya kubalika kwa uraia pacha duniani:

Wakati Prof Kabudi alidai kuwa utafiti aliofanya yeye unaonyesha kuwa asilimia ya nchi zinazokubali uraia pacha duniani ni 49, ukweli ni kwamba asilimia ya kukubalika kwa uraia pacha duniani kote ni 76. Kwa mabara, takwimu zinaonyesha hali ifuatayo:

Marekani 91%
Oceania 93%
Ulaya 80%
Africa 70%
Asia 65%

Kwanini Kabudi ameongopea Bunge? Bunge liombwe hotuba ya Prof Kabudi ifutwe kwenye kumbukumbu zake.

Like
3