Kesi ya Mbowe: Shahidi wa Jamhuri asema watuhumiwa hawakukutwa na msumeno

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 21 Januari 2022.

Jaji ameingia Mahakamani muda huu saa 4 na dakika 4
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka Mawakili was Serikali Waandamizi

Na Tulimanywa Majige Wakili wa Serikali
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili Peter Kibatala: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Peter Kibatala: nipo Pamoja na wakili
Nashon: Nkungu
John Malya
Fredrick Kihwelo
Michael Mwangasa
Michael Lugina
Hadija Aron
Maria Mushi
jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo mahakamani
Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna Shahidi: Mmoja
Tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Na sisi Pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kuendelea
Jaji aandika Kidogo
Shahidi: anaingia, ni kijana mrefu mweusi kidogo
Jaji: Jina Lako
Shahidi: Naitwa H 4347 Goodluck
Jaji: Umri
Shahidi: Miaka 32
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Jaji” kazi yako
Shahidi: Askari Polisi
Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Ataongozwa na Wakili wa Serikali: Pius Hilla
Shahidi: Mimi Askari Namba H 4347 Goodluck Naapa kuwa UShahidi: nitakao toa Mahakamani Utakuwa Wa Kweli na Kweli Mtupu, Eehee Mwenyezi Mungu Nisaidie
Wakili wa Serikali: Pius Hilla Shahidi: Unaitwa Nani
Wakili wa Serikali: Wewe ni Polisi tangu lini
Shahidi: Naitwa namba H 4347 Detective Afande Goodluck
Wakili wa Serikali: Kituo cha Kazi ni wapi
Shahidi: 2013
Shahidi: Nipo Central Arusha
Shahidi: Nina Cheo Cha Sarjent
Wakili wa Serikali: Una Cheo gani
Wakili wa Serikali: Ulikipata lini
Shahidi: Mwaka 2021 Mwezi wa Nane
Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama Huko Central Police Arusha una nafasi gani
Shahidi: Ni Mpelelezi Wa Makosa ya Jinai
Wakili wa Serikali: Ukiwa Kama Askari Polisi una Majukumu gani
Shahidi: Kukamata Wahalifu
Kuhoji, Kupekua, Kukamata Vielelezo Husika, na Kutekeleza Majukumu Mbalimbali ninayopewa na Wakubwa Zangu
Shahidi: Napeleleza Makosa Ya Jinai
Wakili wa Serikali: Unasema Unaeleleza Kitu gani Shahidi
Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama Tarehe 04 August 2020 ulikuwa wapi
Shahidi: Nakumbuka Nilikuwa Kazini Kituoni Central Arusha Nikiendelea na Majukumu Yangu ya Kazi
Wakili wa Serikali: Eleza Majira Ya Jioni Kitu gani Kilitokea
Shahidi: Majira ya Jioni nilipata Maelekezo Kutoka Kwa Afande Mahita Nilikuwa nahitajika Kwa Afande RCO
Wakili wa Serikali: Ulikuwa unahitajika wewe na nani
Shahidi: Mimi na Coplo Francis
Wakili wa Serikali: Afande Mahita ni nani hapo Kituoni
Wakili wa Serikali: Maelekezo hayo uliyatekeleza Kwa Namna gani
Shahidi: Ni Msaidizi Wa OC CID
Shahidi: Tuliondoka Mimi na Afande Mahita Tukaenda Kwa Afande RCO
Wakili wa Serikali: Mlienda Wapi
Shahidi: Mkoani, Makao Makuu ya Polisi
Wakili wa Serikali: Wakati huo RCO Mkoa wa Arusha alikuwa ni nani
Shahidi: Alikuwa Afande Ramadhan Kingai
Wakili wa Serikali: Malipo wasili Kwa RCO Kitu gani Kilitokea
Shahidi: Tulipo fika Kwa Afande RCO Afande alisema Kuna kazi inatakiwa Kufanywa Kwa hiyo tujiandae
Shahidi: Mimi na Afande Francis Tulienda Kituoni Tukachukua Silaha
Wakili wa Serikali: Maelezo Ya Kujiandaa na Kitu gani
Wakili wa Serikali: Wewe Ulichukua Silaha gani
Wakili wa Serikali: Na Mwenzio naye alichukua Silaha gani
Shahidi: Mimi nili chukua Silaha aina ya AK 47
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuchukua Silaha wewe Na Mwenzio Mlielekea Wapi
Shahidi: Na Yeye alichukua AK 47
Shahidi: Tulielekeq Kwa Afande RCO Mkoani
Wakili wa Serikali: Baada ya hapo
Shahidi: alituelekeza Tuelekee Kituo cha Polisi USA RIVER Wilaya Ya Arumeru
Shahidi: Majira ya Saa 12 Jioni
Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa Mida ya Saa ngapi
Wakili wa Serikali: Safari ya Kuelekea USA RIVER ilihusisha Watu gani
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika USA RIVER Kilikuwaje
Shahidi: Afande RCO mwenyewe, Mahita, Mimi Mwenyewe pamoja na Afande Francis
Shahidi: Tulielekea Kituoni Tukamkuta OC CID pale Kituoni
Wakili wa Serikali: ambaye alikuwa ni nani
Shahidi: alikuwa Afande JUMANNE
Wakili wa Serikali: Mlimkuta Eneo gani
Shahidi: Nje ya Kituo
Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo
Shahidi: Afande alitukaribisha Ofisini Kwake, Tukaingia Wote
Wakili wa Serikali: Mkiwa Ofisini Kitu gani Kilifanyika
Shahidi: afande RCO alituambia amepewa Jukumu la Kuandaa timu kwa ajili ya Kufanya kazi, ambayo alisema ni Kazi Maalum
Wakili wa Serikali: alisema amepewa Maelekezo na nani
Wakili wa Serikali: Ukiacha Jukumu la Kuandaa Kikosi Kitu gani Kingine aliwaeleza
Shahidi: Hakusema ameelekezwa na nani
Kikundi hicho Kina Watu ambao wapo Kilimanjaro Moshi
Shahidi: Afande RCO alisema amepata Taarifa Kuwepo Kwa Kikundi Cha Ugaidi ambacho Kimejiandaa Kufanya Matukio Sehemu mbalimbali
Akatuambia Kikundi hicho Kimepanga Kudhuru Viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya
Kikundi hicho kepanga Kufanya Maandamano hapa Nchini yasiyokuwa na Kikomo
Pia alituelekeza kuwa Kikundi hicho kinaratibiwa na Mkuu, Mwenyekiti Wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Jambo Jingine
Afande a Kingai alituelezq Pia Kikundi hicho pia Kilipanga Kuchoma Vituo Vya Mafuta na Kakata Miti na Magogo Kuweka Barabarani ili Kuleta Taharuki Kwa Wananchi, Nchi Kuonekana Haitawaliki
Shahidi: Afande Kingai alituambia Kwa Taarifa alizo nazo Kuna Wahalifu Wapo Moshi, Kwa hiyo tunatakiwa Kwenda Moshi Kwenda Kuzuia, Uhalifu huo Usifanyike
Wakili wa Serikali: Kuzuia Uhalifu Wa Namna gani Shahidi
Shahidi: Afande Kingai aliniambia tunatakiwa tukawakamate
Wakili wa Serikali: Kuna Kitu Kingine shahidi.?
Shahidi: Baada ya Taarifa hiyo na Kupata Malekezo Tuliondoka Pale Kituoni na Kuelekea Moshi
Wakili wa Serikali: Safari ya Kuelekea Moshi ilihusisha Wakina nani
Na Jumanne pia
Shahidi: Ilihusisha Afande KINGAI,Inspector Mahita, Afande Francis, Mimi na DC Azizi ambaye ni Dereva
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya akiwa Mmefika Moshi, Mambo gani Yalifanywa
Wakili wa Serikali: Mambo gani Mlifanya Siku hiyo
Shahidi: Baada ya Kufika Central Moshi, Afande a Kingai alikuwa amesha fanya Mawasiliano, Tukazunguka Maeneo Mbalimbali pale Mjini kuweza Kuwakamata Wahalifu hao
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama, Kwakuwa Lengo ni Kukamata Wahalifu, Je Kazi yenu Kwa Siku hiyo Ilikuwaje
Wakili wa Serikali: Unasema Mlizunguka Moshi Maeneo Mbalimbali, aje ieleze Mahakama mlifanya hivyo hadi Saa ngapi
Shahidi: Kazi yetu kwa Siku hiyo ilikuwa ni Kuwatafuta Wahalifu, Lakini hatukuwa kamata
Shahidi: Baada ya Kuzunguka Maeneo Mbalimbali bila ya Kuwa kamata, ilipo fika Majira ya Saa Tano Kuelekea Saa Sita Afande alisema tukapumzike tutaendelea Kesho yake
Wakili wa Serikali: Kesho yake ilikuwaje
Shahidi: Nakumbuka Afande Kingai alikuwa anaendelea Kupokea Taarifa, ilipo fika Saa 6 Kuelekea Saa 7, Afande Kingai alipokea Taarifa kuwa a watu hao wameonekana Rau Madukani
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Taarifa hiyo ilikuwaje
Wakili wa Serikali: Kwa Maana Watuhumiwa Walikuwa Wangapi
Shahidi: Walikuwa watatu
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuelezwa walivyo Vaa nini Kilifuata
Shahidi: Tulielekea Maeneo ya RAU Madukani Kwa ajili ya kuwakamata
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Ikawaje
Shahidi: Tulifika Rau Madukani, Afande Kingai akatoa Maelekezo Afande Mahita ashuke Kwenye Gari aende Kuangalia Eneo ambalo Watuhumiwa Wapo
Wakili wa Serikali: Baada ya Hayo Maelekezo Kilifutia nini
Shahidi: Afande Mahita alishuka Kwenye Gari akaenda Kufanya Surveillance
Wakili wa Serikali: Elezea Mahakama ilichujuq amuda gani Kufanya Jukumu hilo
Shahidi: Haikuchukua Muda Mrefu Afande Mahita alirudi na akisema ameona Watu Watatu ambao tulikuwa tunawatafuta
Wakili wa Serikali: Aliona watu watatu Wakiwa wamekaa wapi
Wakili wa Serikali: Baada ya Taarifa hiyo ya Afande Mahita, Hatua gani ilichukuliwa
Shahidi: Wakiwa wamekaa Kwenye Glocery
Shahidi: Afande Kingai alitutaka tushuke Kwenye gari, Aligawa timu Mbili, Moja aliingoza Afande Kingai Mimi na Afande Jumanne lakini Nyingine aliongoza Afande Mahita na Francis, Dereva alibaki kwenye Gari
Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini Kilifuata
Wakili wa Serikali: Mkaelekea Wapi
Shahidi: Baada ya Afande Mahita Kurudi alisema akuna uchochoro, alipendekeza tujigawe, Mimi na Afande Kingai timu yetu ilipita Kulia, Mahita na Afande Francis wakapita Kushoto
Shahidi: Baada ya Kugawa timu Mbili, Mlielekea Wapi
Shahidi: Kwenye Hiyo Glocery, na Kabla hatuja fika Eneo la Tukio sisi tulisikoa Afande Mahita akisema “CHINI YA ULINZI”
Wakili wa Serikali: Shahidi: Sasa Umesikia Sauti ya Mahita akisema Chini ya Ulinzi nini Kilifuata
Shahidi: Tulifika Eneo la Tukio, Tukamkuta Afande Mahita na Afande Francis Wameweka Watu Chini ya ulinzi, Na sisi tukajumuika
Wakili wa Serikali: Shahidi: Sasa Baada ya Kufika pale kingai alichukua Jukumu gani
Shahidi: Afande Kingai alijitambulisha Kwanza, aliwauliza Watuhumiwa Majina yao,
Wakili wa Serikali: Watuhumiwa Walikitambulisha kwa Majina yapi
Shahidi: Adam Kasekwa na Mwengine kwa Mohammed Ling’wenya
Wakili wa Serikali: Baada ya Utambulisho huo, Kingai alifanya nini
Shahidi: Kingai Alimpa Maelekezo Afande Jumanne ya kuwapekua Watuhumiwa
Shahidi: Afande Jumanne aliwaita Mashahidi
Wakili wa Serikali: Afande Jumanne alitekeleza Vipi Jukumu la Kuwapekua Washtakiwa
Wakili wa Serikali: aliwatoa wapi
Shahidi: Mmoja alikuwa kwenye Glocery, na Mwingine alikuwa Kwenye Banda
Shahidi: Mmoja anaitwa Esther na Mmoja anaitwa Anita
Wakili wa Serikali: Baada ya MaShahidi: Kufika nini kilifuata
Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Wa Kwanza aliye Anza Kupekuliwa ni nani
Shahidi: Afande Jumanne alijitambulisha Kwa Mtuhumiwa Wa Kwanza,baada ya Kujitambulisha alimuamuru ainuke akaanza Kumpekua
Wakili wa Serikali: alimpekua Kwa Namna gani
Shahidi: Ni Adam Kasekwa
Shahidi: Alimuamuru ainuke, ageuke na akaanza Kumpapasa Kuanzia Kichwani, alipofika Kiunoni akatoa Bastola
Shahidi: Upande wa Kushoto
Wakili wa Serikali: Kiunoni alitoa Bastola Upande Upi.?
Wakili wa Serikali: Jumanne alifanya nini baada ya Kutoa Bastola
Shahidi: Baada ya Kutoa Bastola alionyesha Juu kwa Mashahidi, Akasoma Namba A5340, alisoma Jina la ile Silaha, akasema ni LUGER
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine alifanya
Shahidi: Alitoa Magazine, akahesabu Risasi zilizo kuwa ndani ya magazime
Wakili wa Serikali: Alitoa Risasi ngapi
Shahidi: alizi Hesabu ni tatu
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine alichofanya
Shahidi: Baada ya hapo aliendelea Kumpekua Mtuhumiwa, akatoa Karatasi ambacho Kilikuwa na Kete za Madawa Ya Kulevya 58
Wakili wa Serikali: Alitoa Wapi hicho Kikaratasi
Shahidi: Kwenye Mfuko wa Suruali
Wakili wa Serikali: Wakati unasema Kete zinazodhaniwa Dawa za Kulevya
Jaji: Miye Nimeandika zinazo dhaniwa, labda Neno Kete ndiyo sijasikia
Wakili wa Serikali: Ikawaje
Kibatala: Kwa sababu wewe Ndiyo Mkuu wacha tukubali
Shahidi: akanipa nishike Bastola na Kete
Wakili wa Serikali: Nini Kikaendelea
Shahidi: Aliendelea Kumpekua Mtuhumiwa, akamkuta na simu
Wakili wa Serikali: Simu ilikuwa wapi
Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa ni simu gani
Shahidi: Kwenye Mfuko wa Suruali Wa Adam Kasekwa
Shahidi: Ilikuwa ni Simu Ndogo aina ya Itel
Wakili wa Serikali: Kafanya nini
Shahidi: Alitoa Betri akatoa Line akasoma IMEI namba ya Ile simu, pia alisoma namba za Zile line
Wakili wa Serikali: Baada ya Kusoma zile namba alifanya nini
Shahidi: Alimuamuru Mtuhumiwa akae Chini
Wakili wa Serikali: Aliweka Wapi hiyo Simu
Shahidi: alinipa Nishike
Wakili wa Serikali: Vitu Ulipokuwa navyo Wewe, Nini Kilifanyika
Shahidi: Afande Jumanne aliniambia niende Kwenye Gari Kuchukua Bahasha Ya Kuweka Vitu hivyo, Kwa sababu Gari alikuwa imeshasogea eneo la Tukio Nikaenda Kuchukua
Wakili wa Serikali: ulienda Umbali gani Kutoka eneo la Tukio
Ni kachukua Hiyo Bahasha afande Jumanne
Shahidi: Gari ilikuwa imesogea Karibu na Eneo la Tukio, MaShahidi: Is alikuwa wananiona na Watuhumiwa Walikuwa wananiona
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumkabidhi hiyo Bahasha afande Jumanne alifanya nini
Shahidi: Baada ya kumkabidhi hiyo Bahasha afande Jumanne alitoa Karatasi akaanza Kujaza Kwenye Zile Karatasi Vile Vielelezo
Shahidi: Za Kukamatia mali
Wakili wa Serikali: Karatasi zipi
Shahidi: Zilikuwa Mbili
Wakili wa Serikali: Unakumbuka zilikuwa ni Hati ngapi
Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema Mbili
Shahidi: Hati ya Kwanza alijaza Silaha pamoja na zile simu na Hati Nyingine alijaza Madawa yanayo zaniwa ya Kulevya
Shahidi: Alimsimamisha Mtuhumiwa Wa Pili
Wakili wa Serikali: Alipokamililisha Kujaza Vielelezo alifanya nini
Wakili wa Serikali: Na baada ya Kujaza hizo Hati alifanyeje
Shahidi: alisaini Afande Jumanne, MaShahidi: pamoja na Mtuhumiwa
Wakili wa Serikali: Kilicho fuata Kilikuwa ni nini
Shahidi: Alimuamuru Mtuhumiwa akae Chini, akamuamuru Mtuhumiwa Wa pili asimame
Shahidi: Mtuhumiwa wa pili ni nani
Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Wa Pili ni nani
Shahidi: Mtuhumiwa wapili ni Mohammed Ling’wenya
Wakili wa Serikali: Ikawaje
Shahidi: Alimuamuru ainuke, ageuke, akaanza Kumpapasa kuanzia Kichwani, akatoa Kete zinazozaniwa ni Madawa ya Kulevya
Shahidi: Kwemye Mfuko wa Suruali
Wakili wa Serikali: Zilikuwa kwenye nini
Wakili wa Serikali: Na Kete zilikuwa kwenye Nini
Shahidi: Kimfuko kama Vile Vya Karanga, Baada ya kuhesabu Vilikuwa 25
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha alifanya nini
Shahidi: alivihesabu Mbele ya Mashahidi, Baada ya Hapo alinipa Nivishike
Wakili wa Serikali: aliendelea Kufanya kitu gani
Shahidi: Aliendelea Kumpekua Mtuhumiwa alimkuta na Simu Moja aina ya Techno
Wakili wa Serikali: Ilipatikama wapi hiyo simu
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuitoa alifanya nini..?
Shahidi: ilikuwa Mfukoni
Shahidi: Alianza Kusoma IMEI namba na Baada ya hapo alijaza Hati ya Ukamataji
Shahidi: Alijaza Hati ya Kukamatia Mali, Certificate of Seizure
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama, Unasema alijaza Je alijaza Kitu Gani
Wakili wa Serikali: Alijaza Hati ngapi
Shahidi: Alijaza Hati Mbili, Ya Kwanza Ya Madawa ya kulevya na Hati Ya Pili alijaza Simu
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Vielelezo, Jumanne alifanya nini
Shahidi: Jumanne alisaini, MaShahidi: walisaini Pamoja na Mtuhumiwa alisaini
Wakili wa Serikali: Nani alikabidhiwa Vielelezo Vilivyokamatwa
Shahidi: Afande Jumanne Baada ya Kukamilisha Kujaza Vielelezo, aliweka Kwenye Bahasha akanikabidhi Mimi
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Kwamba Upekuzi na Ujazaji wa Zile Hati zimekamilika nini Kilifuata
Shahidi: Afande Kingai alitoa Maelekezo Twende kwenye Gari Pamoja na Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Wakati huo Gari Ilikuwa wapi
Shahidi: Gari ilikuwa aimepaki Pembeni ya Barabara ambapo ni Karibu na Eneo la Tukio
Wakili wa Serikali: Baada ya a Kufika Kwenye Gari Kitu gani Kilifanyika
Shahidi: Baada ya Kufika kwenye Gari Afande Jumanne alini kabidhi Hati ya Makabidhiano ambayo aliandaa Yeye Afande Jumanne
Wakili wa Serikali: Hati ya Makabidhiano ilikuwa inahusiana na Vielelezo Vipi
Shahidi: alini kabidhi Hati ya Silaha Pamoja na Simu
Hati za Madawa alibaki nazo
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Hati Mliyo kabidhi ana Silaha na Jumanne Utaitambuaje
Shahidi: Ina Jina Langu, Ina Namba yangu H 4347 ina Jina la Afande Jumanne, Ina Vielelezo ambavyo Nimekabidhiwa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi: anaomyesha Uwezo Wa Kutambua, Naomba Kielelezo namba P 12
Wakili wa Serikali: Angalia Nyaraka hiyo, Ni nini
Shahidi: Hati ya Makabidhiano ambayo Afande Jumanne alini kabidhi
Shahidi: Kuna Majina yangu, namba yangu, Tarehe Niliyokabidhiwa na Vielelezo Nilivyo kabidhiwa
Wakili wa Serikali: kuna Vitu Gani
Wakili wa Serikali: Hati hiyo ni ya Tarehe ngapi
Shahidi: 05 August 2020
Wakili wa Serikali: anaye kabidhi ni nani na anayekabidhiwa ni nani
Shahidi: anaye kabidhi ni Afande Jumanne na ninaye Kabidhiwa ni Mimi Goodluck
Wakili wa Serikali: Unamkabidhiwa Vitu gani
Shahidi: Pistol namba A5340 aina ya Luger, pamoja na Risasi 3 ndani ya Magazime
Shahidi: Tulifanya Ndani ya Gari Baada Ya Kuni kabidhi Zile Documents
Wakili wa Serikali: Makabidhiano hayo Yalifanyika Wapi
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Hati hivi Vitu Vimekamatiwa Wapi
Wakili wa Serikali: kutoka Kwa nani
Shahidi: Kwa Mujibu wa Hati Vitu Vimekamatiwa RAU Madukani Moshi
Wakili wa Serikali: akuna Kumbukumbu namba hapo, inasomekaje
Shahidi: Kwa Adam Kasekwa
Shahidi: CD/IR /2097 /2020
Wakili wa Serikali: Naomba Kurudisha Kielelezo Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Baada ya Zoezi la Makabidhiano, ni Kitu gani Kilichofuatia
Shahidi: Tulielekea Kituo Cha Polisi Moshi
Wakili wa Serikali: Wakina nani Mliolekea Kituo cha Polisi Moshi
Shahidi: Ani Afande Kingai, Jumanne, Mahita, Francis, Dereva na Mimi pamoja Watuhumiwa Wawili
Wakili wa Serikali: Watuhumiwa Wawili akina nani
Shahidi: Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya
Wakili wa Serikali: Kwenye Gari Mnasema alikuwa Wewe Kingai, Mahita na Jumanne Mlikuwa Kwenye gari ipi
Shahidi: Gari ya RCO
Wakili wa Serikali: Coplo Francis alipanda Gari ipi
Shahidi: Kwenye Gari Nyingine ambayo alipanda yeye na Mashahidi,
Wakili wa Serikali: MaShahidi: Gani
Shahidi: Ni Anita Pamoja na Esther
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Mlivyofika Kituo cha Polisi Central Moshi, Mambo gani Yalifanyika
Shahidi: Tulipofika Kituoni Afande Kingai aliwauliza Kwa Taarifa Tulizo nazo Mlikuwa Watatu, Mmoja Yupo wapi

Kwa hiyo Tulipofika Kituoni Afande Jumanne na Mahita Walishuka kwenye Gari
Mimi, Afande Kingai, na Dereva Hatukushuka Kwenye Gari Pamoja na Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Ni kwanini Hamkushuka Kwenye Gari
Shahidi: Ni Kwa sababu Afande Kingai alisema tunatakiwa turudi Kumtafuta yule Mtuhumiwa Mmoja, ambaye ni Mtuhumiwa Wa tatu
Wakili wa Serikali: Ilichukua muda gani
Shahidi: Baada ya Muda Afande Mahita na Jumanne Walirejea Kwenye Gari, Walipo rejea ndiyo tuliondoka Kituoni
Wakili wa Serikali: Mliondoka Kuelekea Wapi
Shahidi: Kulekea Sehemu tuliyokamata Watuhumiwa, Ambapo Watuhumiwa Walisema Kuwa Yule Mwenzao alibaki pale
Wakili wa Serikali: Nini Matokeo ya kazi yenu
Shahidi: Ni Kumkamata Mtuhumiwa Wa tatu ambaye alikuwa pamoja na Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Dhumuni la Kurudi kule lilikuwa ni nini?
Shahidi: Tulikuwa tunazunguka Maeneo ambayo Watuhumiwa walikuwa wanatupitisha ili Kumkamata Mtuhumiwa Wa tatu
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuelezwa hivyo Mlichukua Hatua gani
Shahidi: Baada ya Kufika Eneo la tukio hatukumpata, Afande Kingai akawauliza tutampataje, Wakatuonyesha Maeneo ambayo tungempata Mtuhumiwa wa tatu ambaye Walikuwa naye
Wakili wa Serikali: Ufutailiaji Wa Mtuhumiwa Wa Tatu, Umesema Walimtaja Kwa Jina gani
Shahidi: Walimtaja Kwa Jina la Kakobe
Wakili wa Serikali: Ilikuwaje Ufutailiaji wake
Shahidi: Ufutailiaji Wa Siku hiyo hatukumkamata
Wakili wa Serikali: Baada ya KumKosa Mtuhumiwa, Ilikuwaje
Shahidi: Tulienda Kituoni Watuhumiwa Walifikishwa Charge Room ambapo Mahita na Afande Jumanne ndiyo Walishuka
Wakili wa Serikali: Afande Kingai alielekeza Tuwarudishe Watuhumiwa Kituoni
Wakili wa Serikali: Utejelezaji huo huo huo Ulifanyikaje
Shahidi: Tulifika Hotelini ambapo Mimi na Afande Kingai Tulishuka na Mahita na Jumanne Walibaki Kwenye Gari
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwaweka Mahabusu Ilikuwaje
Shahidi: Tulirudi na Kuendelea na ufutiliaji
Wakili wa Serikali: Ikawaje
Shahidi: Ilikuwa Majira ya Saa 11 Asubuhi, Tulifika Kituoni Central Pale Moshi, Tuliwa chukua Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Sasa Siku iliyofuata Tarehe 06 August 2020 Nini Kilifuata
Shahidi: Tulirudi na Kuendelea na ufutiliaji
Wakili wa Serikali: Kwa Madhumuni gani
Shahidi: Kwa Madhumuni Ya Kwenda Kumtafuta Mtuhumiwa Wa tatu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Matokeo Ya Utafutajinwa Mtuhumiwa Wa tatu Ilikuwaje pale moshi
Shahidi: Matokeo Ya Kumtafuta Mtuhumiwa Wa tatu, Hatukufanikiwa Kumpata
Wakili wa Serikali: Mlifanya Utafutaji Maeneo Gani
Shahidi: Tulienda Moshi Mjini, Aishi, Boma. Ng’ombe, na Baadae Sakina Arusha
Wakili wa Serikali: Ufutailiaji Wenu wa Tarehe Sita Mlifanya hivyo Hadi Saa ngapi
Shahidi: Tulifanya Ufutailiaji Mpaka Saa 12 Jioni, Baada ya Kutoka Arusha Tulirudi Moshi Mjini
Wakili wa Serikali, Ni Kitu gani Kilitokea Hiyo Majira ya Saa 12 Jioni
Shahidi: Tulirudi Moshi Pale Polisi Central, Afande Kingai alikuwa anafanya al Mawasiliano, Baada ya Hapo Afande Kingai alirudi Kwenye Gari akasema Watuhumiwa Wanatakiwa Kupelekwa Dar es Salaam
Wakili: Baada ya Maelekezo hayo Ikawaje
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Mlifika lini
Shahidi: Baada ya Kufika Central Moshi, Tulifika pale Njia panda Himo, Gari iliharibika, na Afande a Kingai akafanya Mawasiliano ilikupata Gari Nyingine Kuelekea Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Hapo Njia panda Himo Kitu gani Kingine Mlifanya
Wakili wa Serikali: Gari ilitoka wapi
Shahidi: Ilitoka Moshi, Gari ya Afande RPC
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba Mlifika lini Dar es Salaam
Shahidi: Baada ya Gari ya RPC Kufika tulianza Safari ambapo tulifika Tarehe 07 August 2020
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Majira ya Saa ngapi
Shahidi: Ilikuwa Majira ya Alfajiri ya Saa 11
Wakili wa Serikali: Mlifika Wapi
Shahidi: Tulifika Dar es Salaam Central police, Baada ya Kufika Walikabidhiwa Charge Room
Wakili wa Serikali: Washitakiwa Walikabidhiwa Wapi
Shahidi: Charge Room ya Central Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Mmewakanidhi Watuhumiwa Charge Roo, Je Ni Shughuli zipi zingine Mlifanya Siku hiyo
Shahidi: Afande Kingai alitoa Break, Kwenda kunawa Uso
Tulienda Kunawa Uso Baadae Saa 1 Asubuhi Tulirudi Kituoni
Wakili wa Serikali: Baada ya Saa 1 Kurudi Mlipewa Maelezo gani
Shahidi: Afande Kingai aliniambia Nikabidhi Vielelezo Kwa Afisa Vielelezo Pale Central
Wakili wa Serikali: Ukitekeleza Vipi
Shahidi: Nilienda Kwa Mtunza Vielelezo, Nikamkabidhi Silaha
Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Silaha ipi
Shahidi: Nilimkabidhi Silaha iliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Adam Kasekwa Bastola A5340 aina ya Luger Pamoja na Risasi 3
Jaji: Rudia namba ya silaha iliyokabidhi
Shahidi: Ni A5340
Wakili wa Serikali: ambayo Ulimkabidhi Nani
Shahidi: Nilimkabidhi Staff Sargent Nuru
Wakili wa Serikali: Shahidi Silaha ilikamatwa Tarehe 05 August 2020, Ukaikabidhi Tarehe 08 August 2020, amuda wote Silaha ilikuwa Kwa nani
Shahidi: Muda wote Silaha nilikuwa nayo Mimi
Wakili wa Serikali: Shahidi: Baada ya kuwa Umemkabidhi Silaha, Ni Jukumu lipi lingine ulitekeleza
Shahidi: Nilikabidhi Simu
Wakili wa Serikali: Simu Ulimkabidhi Nani
Shahidi: Afande Swila
Wakili wa Serikali: Huyu Swila ni nani
Shahidi: Ni Askari Wa Hapa Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Simu zipi
Shahidi: Simu zilizokamatwa Kwa Watuhumiwa Kule Moshi ambazo ni Itel na Techno pamoja na Line
Wakili wa Serikali: Kwenye Makabidhiano ya Silaha, Risasi pamoja na Magazine, Mlikabidhiana Vipi
Shahidi: Afande Kingai alisema tuendelee na Ufutailiaji Wa Taarifa, akatuambia yeye Pamoja na Afande Jumanne Watabaki
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe Ngapi
Shahidi: Tarehe 07 August 2020
Wakili wa Serikali: Hati Uliyotumia Kukabidhi Silaha, Ukiona Utaitambuaje
Shahidi: Nilisaini Hati ya Makabidhiano na yeye akasaini
Shahidi: Naiomba Mahakama Ipokee Kama UShahidi: Wangu
Hati inapelekwa kwa jopo la mawakili wa utetezi
Mheshimiwa Jaji sisi akwa niaba Ya Mshitakiwa Wa Kwanza Hatuna OBJECTION
Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji Sisi kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Pili hatuna Pingamizi
Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu Sina Pingamizi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne pia Hatuna Pingamizi
Sasa Hati Inachukuliwa Kutoka Upande Wa Mawakili Wa Utetezi Kwenda Katika Meza ya Jaji
Jaji anapokea a kutoka Kwa Karani wa Mahakama anasoma na Kuanza Kuandika Kidogo
Mahakama ipo kimya, mvua imeacha kuonyesha hali ya mawingu kiasi na jua kwa mbali
Umeme unakatika kila Saa na Kurudi
Jaji: Tuliishia Kielelezo Namba, 35..! Basi Naipokea Na Itakuwa Kielelezo namba 36
Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia kidogo
Hati inapelekwa kwa shahidi Goodluck anatakiwa a some yote kwa sauti kama ambavyo sheria ya ushahidi inavyotaka
Wakili JOHN MALYA: Mheshimiwa Jaji naomba shahidi asome kama ilivyo andikwa kuna vitu anaviruka
Shahidi anaanza kusoma upya
Shahidi Anauliza kusoma karatasi ya a kurasa moja, hati ya makabidhiano
Wakili wa Serikali: Shahidi, hati hiyo ni ya tarehe ngapi
Shahidi: Tarehe 07 August 2020
Wakili wa Serikali: anayekabidhi ni nani
Shahidi: NI Mimi H 4347 DC Goodluck anayekabidhiwa ni D 7853 staff Sarjent Nuru
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Staff Sargent Nuru anakabidhiwa Kitu gani
Wakili wa Serikali: Vilikamatwa Lini?
Shahidi: Tarehe 05 August 2020
Wakili wa Serikali: Kumbukumbu namba zipi
Shahidi: CD/ IR /2097 /2020
Wakili wa Serikali: Hiyo Kumbukumbu namba Uliandika Kwa Madhumuni yapi?
Shahidi: Ndiyo namba ya kesi
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa fomu yako Hapa Kuna Maeneo Umeweka Deshi, Ujajaza… Kutoka Kwa Mtuhumiwa Deshi, anaye tuhumiwa kwa Makosa ya Deshi
Shahidi: Kwa sababu Kumbukumbu namba ya CD/IR /2097 /2020 ina Jina la Mtu aliye kamatwa nayo na Kosa lililo husika
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba Bastola hii ambayo Ulimkabidhi Kwa Sargent Nuru Ukiiona Leo hii Unaweza Kuitambua Kwa namna ipi
Shahidi: Naweza Kuitambua Kwa Sababu ina Serial number ambayo Ipo Kwenye mwili wa Silaha na Jina
Wakili wa Serikali: Ni namba Ngapi
Shahidi: A 5340
Wakili wa Serikali: Hilo Jina Lipo sehemu gani
Shahidi: Jina Lipo Upande Wa Kushoto, namba zipo Upande wa Kulia Kwenye mwili Wa Bunduki
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha Uwezo Wa Kutambua Kielelezo, Naomba Kielelezo namba P 3
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Kielelezo
Shahidi: Anakabidhiwa Mfuko wa nailoni Inayoonyesha Ndani (Transparent)
Shahidi: Hii ni Silaha aina ya Pistol, Niliyo Mkabidhi Sarjent Nuru, Niliyokamata Kwa Mtuhumiwa Adam Kasekwa
Wakili wa Serikali: Ilikatwa Kwa Mtuhumiwa Wapi na Lini
Shahidi: Tarehe 05 August 2020, Rau Madukani
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kina thibitisha Kwamba Ndiyo hiyo
Shahidi: aina Serial number A5340 ipo Upande wa Kulia na Jina la Luger
Wakili wa Serikali: Unasema Ulimkabidhi Sarjent Nuru Magazine, Ipo wapi
Shahidi: anaonyesha Chini ya kitako Cha Pistol
Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama, Mnamo tarehe 08 August 2020 Unakumbuka nini
Shahidi: Afande alitoa Maelekezo kuwa Watuhumiwa Wahamishwe Kutoka Central Dar es Salaam kwenda Kituo cha Polisi Mbweni
Wakili wa Serikali: Nani alitoa Maelekezo
Shahidi: aliniambia Afande Mahita kaambiwa na Afande Kingai
Wakili wa Serikali: Kituo Cha Polisi Mbweni kipo wapi
Shahidi: Kipo Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni majira ya saa ngapi
Shahidi: Ilikuwa ni Majira ya sa 5 asubuhi
Wakili wa Serikali: Mliwahamisha Watuhumiwa Wakina nani?
Shahidi: Tuliotoka nao Moshi Walikuwa ni Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya
Wakili wa Serikali: Mlioshiriki zoezi la Kuwatoa Central Kuwapeleka Mbweni Ni akina nani
Shahidi: Afande Jumanne, Mahita, Swila Pamoja na Mimi na Dereva
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya Kufika Mbweni akitu gani Kilifanyika
Shahidi: Baada ya Kufika. Mbweni Waliingia Charge Room Mimi nikabaki nJe
Wakili wa Serikali: Unaposema Charge Room unamaanisha nini
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhi Mlielekea Wapi
Shahidi: Baada ya Washitakiwa Kukabidhiwa Tuliondoka kituoni
Wakili wa Serikali: Mlienda Wapi
Shahidi: Kwenda Kutafuta Taarifa za Watuhumiwa mbalimbali
Wakili wa Serikali: Majira ya Jioni ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa Maeneo ya Temeke
Shahidi: Tulikuwa a Maeneo Mbalimbali hapa Dar es Salaam tukiwa tunafutailia wahalifu wengine
Wakili wa Serikali: Ikawaje
Shahidi: Nili fanikiwa Kumkamata Mtuhumiwa Mwingine ambaye Nilikuja Kufahamu anaitwa Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: Bwire alikatiwa Eneo gani
Shahidi: Maeneo ya Kituo cha Polisi Chang’ombe
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mazingira ya Ukamataji Wa Bwire Yalikuwaje
Shahidi: Alikuwa katika Gari ya Abiria, Kwa hiyo ile Gari ya Abiria ilielekezwa Kuingia Kituoni
Wakili wa Serikali: Gari ya Abiria ya aina gani
Shahidi: Daladala
Wakili wa Serikali: Ikawaje
Shahidi: IKaingia Kituo cha Polisi Chang’ombe
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamatwa.?
Shahidi: Aliingizwa Mahabusu
Wakili wa Serikali: Kabla ya Kumuingiza mahabusu
Shahidi: Afande Kingai alimpekua

Wakili wa Serikali: alimpekua Sehemu gani
Shahidi: katika Maungo yake
Wakili wa Serikali: Alikutana na Nini
Shahidi: Kwenye Upekuzi alikuwa na Simu Mbili
Wakili wa Serikali: Simu gani Kama Unakumbuka
Shahidi: Simu aina ya Bundy na Simu aina ya Techno
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama hivi Vitu vilipayikana Sehemu gani
Shahidi: Vilipatikana Mfukoni
Wakili wa Serikali: Baada ya Upekuzi Ikawaje
Shahidi: Mtuhumiwa Aliingizwa Mahabusu Kituo cha Polisi Chang’ombe
Wakili wa Serikali: Wewe Ulieleka wapi
Shahidi: Tuliendelea na Ufutailiaji Wa Taarifa Nyingine zilizo kuwa zimetolewa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona no Saa Saba Kasoro, Naomba Hairisho tupate Health Break kwa DAKIKA 45 baada ya hapo tuendelee
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa hatujui kabakisha kiasi gani, Kama ni Dakika 20 tuvumilie kama ni zaidi ya hapo tuhairishe
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Bado Nina Muda zaidi nitaomba Hairisho
Wakili Peter Kibatala: Kwa Kesi hiyo hatuna Pingamizi
Jaji: Basi nahairisha mpaka saa saba na dakika 45
Jaji anatoka
Jaji amerejea mahakamani muda huu saa saba na dakika 54
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani tena
Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile kama awali tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea, Quorum yetu ipo Kama Mwanzo
Jaji: Shahidi nakukumbusha Ulikuwa unaendelea Kutoa UShahidi: wako, Ulikuwa Chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo
Mheshimiwa Jaji anaandika Kidogo
Wakili wa Serikali: zile simu alizokuwa nazo Bwire ziliemda wapi
[Shahidi: Afande Kingai alini kabidhi mimi
Wakili wa Serikali: Ukazipeleka Wapi
Shahidi: Nilipewa Maelezo Ya Kumkabidhi Afande Swila
Wakili wa Serikali: Ni Lini na Ni wapi
Shahidi: Baada ya Kurudi Polisi Central Dar es Salaam, Nilimkabidhi Afande Swila
Wakili wa Serikali: Tarehe 10 August 2020 Siku hiyo ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa bado naendelea na Zoezi la Ufutailiaji, Siku hiyo Afande Kingai alitoa Maelekezo ya Kwenda Kumpekua Bwire Nyumbani Kwake, Maeneo ya Yombo Kilakala
[Wakili wa Serikali: Yombo Kila Kala Ipo wapi
Shahidi: Ipo Maeneo ya Temeke
Wakili wa Serikali: Mbali na Nguo za Jeshi la Wananchi la Wananchi, Nini Kingine
Shahidi: Vitu Vingi zikiwemo Sare za Jeshi la Wananchi
Wakili wa Serikali: Kwenye huo Upekuzi Vilipatikana Vitu gani
Shahidi: Kidaftari cha 5star na Kisu cha JWTZ
Wakili wa Serikali: Baada ya Upekuzi Mlielekea Wapi
Shahidi: Tulielekea Kituo Cha Polisi Chang’ombe
Wakili wa Serikali: Tarehe 13 August 2020 Ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikabidhi wa Simu Kwa ajili ya Kwemda Kuzi kabidhi Makao Makuu Ndogo ya Polisi, Maabara Ya Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Alikukabidhi nani
Shahidi: Alini kabidhi Afande Swila
Wakili wa Serikali: Ulipewa Simu Ngapi
Shahidi: Nilipewa Simu nane
Wakili wa Serikali: Mbali na Simu ulipewa nini
Shahidi: Na Barua
Wakili wa Serikali: Vielelezo hivyo ulitakiwa Kupeleka Wapi
Shahidi: Makao Makuu Madogo ya Jeshi la Polisi, Kitengo Cha Cyber ambapo Afande Ndowa ndiyo alinipokea
Wakili wa Serikali: Ikawaje
Shahidi: Nilimkabidhi Afande Ndowo
Wakili wa Serikali: Tarehe 25 November 2020 ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa bado naendelea Kufuatilia Kuhusu Wahalifu Tuliokuwa tunawatafuta
Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi
Shahidi: Nilielekezwa a kwenda Kuchukua Silaha
Wakili wa Serikali: Silaha Ipi.?
Shahidi: Nilienda Kwa Sarjent Nuru, Nilichukia Silaha Nikaenda Makao Makuu Ndogo Ya Polisi Kwa Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Silaha aina gani ulilkadhiwa
Shahidi: Silaha aina ya Pistol A5340 aina Ya Luger ambayo ilikuwa na Magazine na Risasi 3
Wakili wa Serikali: Huyu Nuru Alikukabidhi Kwa namma gani
Shahidi: Tulisainishana Hati ya Makabidhiano
Wakili wa Serikali: Hati ya Makabidhiano uliona Leo Utaweza Kuitambuaje
Shahidi: Naweza Kuitambua Kwa Kuona Jina langu, Force Namba yangu, aina ya Silaha na Jina la aliye Nikabidhi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi: ameonyesha Uwezo wa Kuitambua
Wakili wa Serikali: Shahidi: Ieleze Mahakama Nyaraka Uliyo nayo ni Kitu gani
Shahidi: Ni Hati ya Makabidhiano
Wakili wa Serikali: Ina Kitu gani Kinacho weza Kuthibitisha Kuwa Unaifahamu
Shahidi: Ina namba la Silaha, Pistol namba A5340
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine
Shahidi: Kuna Risasi Tatu Ndani ya Magazime
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine
Shahidi: Ina Sahihi yangu, H 4347 DC Goodluck
Wakili wa Serikali: Kigezo Kingine
Shahidi: Ina Jina la aliye Nikabidhi
Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama Kuhusiana na Nyaraka hiyo
Shahidi: Naiomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi
Wanaipitia Kwa Pamoja
Nyaraka inaenda Kwenye Benchi la Mawakili Wa Utetezi
Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza Hatuna Pingamizi
Wakili John Malya: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili Sina Pingamizi
Wakili Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa tatu Sina Pingamizi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne pia Hatuna Pingamizi
Nyaraka Inapelekwa Kwenye Meza ya Jaji Kupitia Karani wa Mahakama
Jaji: Napokea akama Kielelezo Namba 37
Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo
Wakili wa Serikali: Shahidi: Soma Nyaraka Kwa Sauti
Shahidi ANASOMA KIELELEZO NAMBA 37 kama ambavyo Sheria ya UShahidi: inataka, pale ambapo Kielelezo Cha Nyaraka Kinapo pokelewa Kisomwe Chote na Shahidi anayekitoa
Malya: Mheshimiwa Jaji ameongeza Kitu ambacho hakijatajwa hapo
Shahidi anasoma upya
Wakili wa Serikali: Hati hiyo ni ya Tarehe Ngapi
Shahidi: Tarehe 25 November 2020
Wakili wa Serikali: Naye kabidhi nani na anakabidhiwa Nani
Shahidi: Anakabidhiwa DC Goodluck na anayekabidhi ni Sargent Nuru
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Hati hiyo Silaha hiyo ilikamatwa lini na wapi
Shahidi: Ilikamatwa Tarehe 05 August 2020 Rau Madukani
Wakili wa Serikali: Kumbukumbu namba ni Ipi
Shahidi: CD/IR /2097 /2020
Wakili hiyo ni Kumbukumbu namba ya Kitu gani
Shahidi: Ni Kumbukumbu ya Kesi
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tunapinga anachofanya Wakili Pius Hilla, aliye takiwa Kusema Ni Kumbukumbu ya Kesi ipi Ilitakiwa Kusema na Shahidi: Siyo Yeye Wakili
Jaji: Rudia Swali lako
Wakili wa Serikali: Shahidi Kumbukumbu namba Inayo Tajwa hapo ni Ya Nini
Shahidi: Ni kumbukumbu ya kesi inayohusiana na kesi ya kula njama ya kutenda matendo ya ugaidi
Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Umemkabidhi wa Pistol Luger na Magazine Yenye Risasi Tatu, Vitu hivyo ulivipelela Wapi
Shahidi: nilivipeleka Makao Makuu Madogo Jeshi la Polisi, Kitengo Cha Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Ulivipeleka Wapi
Shahidi: Makao Makuu Ya Jeshi la Polisi Kwa Uchunguzi zaidi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Ulimkabidhi nini
Shahidi: Nilikabidhi Silaha ambayo Nilichukia kwa Sargent Nuru
Wakili wa Serikali: Silaha gani
Shahidi: Ni Silaha aina ya Pistol A5340, Magazine Pamoja na Risasi
Wakili wa Serikali: Pamoja. A Vielelezo Hivyo Uliwasilisha na nini
Shahidi: Nili Wasilisha na Barua ambayo Ilikuwa na Maelekezo ya Nini cha Kufanya
Wakili wa Serikali: Shahidi: Sasa ieleze Mahakama, Vielelezo Hivyo Ulimkabidhi Kwa Utaratibu Upi
Shahidi: Baada ya Kufika Kituoni Makao Makuu Ya Polisi tulikabidhiana Kwa Hati Ya Makabidhiano
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Hati ya Makabidhiano Uliyotumia Kukabidhiana Ukiona Utaitambuaje
Shahidi: Nitaitambua Ina Jina Langu, Force Namba yangu, Jina la Ninaye mkabidhi, Kumbukumbu namba
Wakili wa Serikali: Kumbukumbu namba ipi.?
Shahidi: Ni CD /IR /2097 /2020
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi: ameonyesha Uwezo Wa Kuitambua
Wakili wa Serikali: Eleza Nyaraka hiyo ni Nini Shahidi
Shahidi: Ni Hati ya Makabidhiano ambayo Nilimkabidhi Coplo Hafidh
Wakili wa Serikali: Ina Vitu Gani ambavyo Vimekufanya Uitambue
Shahidi: Ina Jina Langu pamoja na Sahihi yangu
Wakili wa Serikali: Inasokaje
Shahidi: H 4347 DC Goodluck
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Ina Jina la Ninaye Mkabidhi, Eneo ambapo Vilikamatwa
Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama Kuhusiana na Nyaraka hiyo
Shahidi: Naiomba Mahakama Ipokee Kama UShahidi: wangu
Nyaraka Inapelekwa Kwenye Benchi La Mawakili Wa Utetezi
Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza Hatuna Pingamizi
Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili Sina Pingamizi
Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa tatu Sina Pingamizi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne Sina Pingamizi
Nyaraka Inatoka Upande wa Benchi la Mawakili wa Utetezi Kwenda Mezani Kwa Jaji
Jaji: Naipokea Kama Kielelezo namba 38
Jaji: Shahidi Usome Kwa Haraka Haraka
Shahidi anasoma kama ambavyo sheria ya ushahidi: inataka, shahidi: anapotoka kielelezo ambacho ni nyaraka kusoma mbele ya mahakama
Wakili wa Serikali: Ni Hati Ya Tarehe Ngapi
Shahidi: Tarehe 25 November 2020
Wakili wa Serikali: anayekabidhi nani na anayekabidhiwa nani
Shahidi: anakabidhiwa Detective Coplo Hafidh, Anayekabidhi ni mimi DC Goodluck
Wakili wa Serikali: Nyaraka Inakabidhiwa Wapi
Shahidi: Inakabidhiwa Forensic Beaural, Kwa Detective Coplo Hafidh
Wakili wa Serikali: Kuna Kumbukumbu Namba hapo, Ieleze Mahakama Inasomekaje
Shahidi: CD/IR /2097/2020
Wakili wa Serikali: Ni Kumbukumbu namba ya kitu Gani
Shahidi: Ni Kumbukumbu namba ya Kesi ya Kula Njama ya Kutenda Matendo Ya Ugaidi
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Malipo Kuwa Moshi Baada ya Kuwakamata Watuhumiwa Mpaka Kuwa leta DAR ES SALAAM nani alikuwa ana husika na Ulinzi Wao
Shahidi: Vielelezo Vilivyo kamatwa Siku hiyo
Wakili wa Serikali: Tarehe 5 August 2020 Malipo wa kamata Watuhumiwa hali zao Zilikuwaje Mpaka Mnafilisha Mahabusu
Shahidi: Hali zao zilikuwa nzuri Waka Hapakuwa na Malalamiko Yoyote
Wakili wa Serikali: Tarehe 06 August 2020 Washitakiwa Walikuwa na Hali gani
Shahidi: Pia walikuwa na Hali Nzuri
Wakili wa Serikali: Tarehe 07 August 2020 Siku mnayofika Dar es Salaam, Washtakiwa Walikuwa na Hali gani
Shahidi: Walikuwa na Hali Nzuri, Na tulikula pamoja
Wakili wa Serikali: Tarehe 08 August 2020 Siku Mnawapeka Mbweni Walikuwa na hali gani
Shahidi: Walikuwa katika hali Nzuri
Wakili wa Serikali: Je Watuhumiwa Uliowakata Tarehe 05 August 2020 na Tarehe 09 August 2020 Wapo Hapa Mahakamani.?
Shahidi: Ndiyo Wapo Hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Uliowakata Tarehe 05 August 2020 ni Yupi ni Yupi
Shahidi: aliye Vaa Tshirt yenye Mstari Kijani, Nyeupe na Nyeusi nilimkamata Tarehe 05 August 2020
Wakili wa Serikali: Mwingine
Shahidi: Aliyevaa Tshirt ya njano na Draft anaitwa Adam Kasekwa, Nilihusika Kumkamata Maeneo ya Rau Madukani
Shahidi: Mwingine Ni amevaa Kanzu Nyeupe na Baraka Shia, anaitwa Khalfani Bwire, Nilihusika Kumkata Dar es Salaam, Tarehe 09 August 2020
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Mwingine Kama Yupo
Shahidi: Hakuna Mwingine niliye husika Katika Ukamataji
Wakili wa Serikali: ambao ulihusika Katika Ukamataji Uliwa kamata kwa Tuhuma zipi
Shahidi: Kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Sitakuwa na Swali Lingine
Kutoka Jopo la Utetezi anaanza
Nashon: Nkungu: Shahidi, Ulijitambulisha Wewe ni Askari kutoka Jeshi la Polisi ni Sahihi
Shahidi: Sahihi
Nashon: Kwa hiyo Utatakiwa Kuwa na Uelewa Wa PGO
Shahidi: Ni sahihi
Shahidi: ni sahihi
Nashon: Na Utatakiwa Kufuata Masharti ya PGO
Shahidi: Ni sahihi
Nashon: Mlifanya Safari Kadhaa na Kwa kutumia Magari ni sahihi
Shahidi: Ni sahihi
Nashon: Magari haya yalikuwa ni Magari Ya Binafsi au Ya Jeshi la Polisi
Shahidi: Magari Ya Polisi
Nashon: Na Mlifanya Safari Mkoa hadi Mkoa
Shahidi: Ni sahihi
Nashon: Ni sahihi Kwamba Gari ya Polisi Inapotokea Mkoa hadi Mkoa, unahitaji Ruhusa Ya IGP
Shahidi: Siyo Kweli
Nashon: Nisomee PGO 197 Paragraph ya 4,
Shahidi……… Without a prior aprove of Inspector General
Nashon: Mheshimiwa Jaji inamaana gani
Shahidi: Hatukubadirishana Magari, Gari zilikuwa bado za Arusha
Nashon: Unafahamu STATION Diary
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Kwakuwa umeshasoma mbele ya mahakama , mahakama utaona maana halisi
Nashon: Unafahamu Kwamba Safari zote zinaanzia Polisi
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Je Unafahamu kwamba ni takwa la kisheria kabla yakuanza safari, CRO natakiwa kurekodi muda, takwa la safari
Shahidi: Mimi siyo dereva
Nashon: Je uliona wakati wote jambo hilo likifanywa
Shahidi: Sijaona
Nashon: Unafahamu Kwamba Gari hilo la Polisi Kinatakiwa Kuwa na MOTOR VEHICLE LOG BOOK
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Unafahamu Kwamba Safari zote Mlizofanya Hiyo Gari Ilitakiwa Kuwa na MOTOR VEHICLE LOG BOOK
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Unafahamu Kitu Kinaitwa Report Book
Shahidi: RB ndiyo Nafahamu
Nashon: Je Unafahamu Kwamba Baada ya Kufanya Raid Ndani ya Eneo la Kituo, Officer Incharge Wa Hiyo Raid anatakiwa Kure port Kwa Incharge Wa Hilo Eneo
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Na Hiyo Reporting Inatakiwa Kufanyika Kwenye Report Book
Shahidi: Siyo Lazima
Nashon: Soma PGO ya 359 paragraph ya 9(e)
Shahidi anasoma
Nashon: Nimeeleza concern ya kaka yangu msomi Wakili Pius Hilla
Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji, Wakili Anaonyesha Foundation Kuwa anataka Shahidi: asome Kwa Lipi
Ni kwamba Mtu anapotoka OBJECTION Ya Sheria, Yeye Ndiye anatakiwa atoe Kilicho sahihi
Wakili hajatoa Sheria ambayo ni Proper, PGO ambayo tunatumia tangu Mwanzo wa Kesi ni hii hii ambayo na wao wananitumia, Ukiondoa Kwamba Kuna amandments imefanyia Mwezi July Mwaka huu
Jaji: Swali hilo unaliondoa au Lah
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Ni sahihi Mheshimiwa Jaji ni Vizuri Shahidi: aonyeshwe ni PGO ya Toleo lipi
Jaji: Concern Yake Wakati Unampa asome PGO ya Wakati gani
Nashon: Mheshimiwa Jaji Mpaka Nakuja na PGO hii tayari nimejiridhisha
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tunaomba Dakika 2
Nashon: Nkungu: Shahidi: Unafahamu Kwamba Kuna amandments za PGO
Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili awezi Kuendelea na Mahakama Mpaka ajibu Hoja ya Mahakama
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Mr. Hilla Hoja yake Ilikuwa ni Foundational Concern
JAJI: Hoja yangu ni kwamba anaondoa swali au anaendelea na Swali
Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba kuliondoa hilo swali
Nashon: Shahidi: Unafahamu Kwamba Kuna Amandments za PGO zime fanyika July Mwaka huu
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Unafahamu kwamba Kabla kabla ya hapo palikuwa na PGO ambayo wewe Ulikuwa Unafanyia Kazi
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Mheshimiwa Jaji KWA Ruhusa Yako nitaomba Unisomee 309 Paragraph 9(e)
Shahidi anasoma
Nashon: Baada ya Kusoma Sheria Hii Bado Unasimamiasimamo wako Wa Awali
Shahidi: Kwamba?
Nashon: Ulisema Siyo Lazima Kwa Nyinyi Kutoa Riport Baada ya Raid Mliyo fanya Pale Rau Madukani
Shahidi: Ndiyo siyo lazima
Nashon: Unafahamu SMG
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: SMG ni Aina ya Bunduki au Function ya Bunduki
Shahidi: Ni Function ya Bunduki
Nashon: AK 47 inaweza Kuwa Sawa na SMG
Shahidi: Ndiyo inaweza Kuwa ni SMG
Nashon: Unaweza Kueleza Wale MaShahidi: Huru walipatikana Vipi
Shahidi: Ni Afande Jumanne
Nashon: Ni UShahidi: Wako Kwamba Afande Jumanne aliwaacha Watuhumiwa akaenda Kuwaita Mashahidi
Shahidi: Siyo mbali sana, bado unaweza kuona watuhumiwa
Nashon: Kama Hatua ngapi
Shahidi: Sikumbuki
Nashon: Ni sahihi Wewe Ulikuwa Mtu wa Kwanza Kupokea Bastola kutoka Kwa Afande Jumanne
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Na wewe Ndiyo Ulifanyia Lebeling Kielelezo
Shahidi: Hapana
Nashon: Kwa ufahamu wako nani alifanyoa lebeling
Shahidi: Afande Jumanne Baada ya Kukabidhiwa ndiyo alifanyia Lebeling
Jaji: Shika vizuri hiyo bastola, either unaonyesha chini au juu
Mahakama Kichekoooooo
Nashon: kwenye hii Bunduki Kuna Lebel Mbili, Unaweza Kutueleza nani alizi attach
Shahidi: Baada ya Mimi Kukabidhiwa Niliweka Kwenye Begi, Silaha Ilieda Kwa Mtunza Vielelezo Dar es Salaam, ila Miye sifahamu
Nashon: Je ni UShahidi Wako Silaha hii Haiku Lebel kutoka Rau Madukani Mpaka Unafika Dar es Salaam
Shahidi: Ndiyo Siku Lebel
Nashon: ana Je Unafahamu Kwamba Kielelezo Kinatakiwa Kuwa Lebeled Mara Baada tuh ya Kukamata Kielelezo
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Na Shahidi: Unafahamu Kwamba Kuto Lebel Kielelezo Ni Hatari inayo Pelekea Kuchanganyika kwa Kielelezo
Shahidi: Ndiyo Nafahamu
Nashon: Umesa Hapa, Kwamba Muda Wote Silaha ilikuwa a kwenye Begi lako, Je ulileta Hilo Begi Mahakamani Ili Mahakama Ione Uimara Waka hilo Begi
Shahidi: Sikuleta
Nashon: JE Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Begi hilo Lin Lock au Password Ambayo wewe tuh Unaweza Kufungua, au Lina zipu au Lipo wazi
Shahidi: Si kumwambia
Nashon: Kwaluwa ujafanya hayo, Ni sahihi Mahakama Haiwezi Kufahamu Umadhubuti Wa Hilo Begi kwa Sababu Mahakama haijaliona
Shahidi: Sivyo
Nashon: Je Shahidi: Unafahamu Kwamba Lebeling ya Kielelezo inatakiwa Kuambatana na FOMU YA PF 145
Shahidi: Ndiyo Nafahamu
Nashon: Ulisema Pia Kwenye UShahidi: wako Ulienda Pia AISHI HOTEL Saa Tano Usiku Kuendelea Kuwatafuta
Shahidi: Siyo Kweli
Nashon: Si Kweli Kwamba Mlienda Aishi Hotel katika Harakati za Kuwatafuta, Nyinyi Mkabaki Nje na Jumanne na Mahita Waka Kaingia ndani
Shahidi: Siyo kweli
Nashon: Kwamba hukutaja jina la hotel?
Shahidi: Hotel ya kwenda kupumzika siyo unayo taja
Nashon: Unauthibitisho wowote wa risiti ya hotel?
Shahidi: Sijaleta
Nashon: Hukuona umuhimu wa kuleta risiti?
Shahidi: Mimi nilikuwa na viongozi wangu
Nashon: Shahidi ajibu swali unaloulizwa
Shahidi: Sikuona Umuhimu
Nashon: Uliambiwa Watu hawa pia Wana nuia Kuwadhuru Viongozi akiwemo Sabaya
Shahidi: Ni kweli
Nashon: Uliwataja sasa viongozi wengine
Shahidi: Hapana
Nashon: Je ulieleza kwamba mlimwambia Sabaya kuwa akuna Hatari Inakaribia
Shahidi: Sikueleza
Nashon: Unaweza kukumbuka zoezi la ukamataji na upekuzi, lilichukua muda gani
Shahidi: Siwezi kukumbuka muda
Nashon: Je Unafahamu Kwamba PGO inataka Urekodi Kila Tukio na Muda Kwenye Diary Yako
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Na wewe hukufuatisha Kama PGO Inavyotaka
Shahidi: Walikuwa wana Rekodi Viongozi Wangu
Nashon: Je Unafahamu kwamba PGO Inataka Kila Polisi Kurekodi Matukio na Muda Kwa Askari Wote
Shahidi: Ndiyo Nafahamu
Nashon: Ni sahihi Kwamba Umesema Ulmkamata Khalfani Bwire
Shahidi: Ni sahihi
Nashon: Na Ulimpeleka Kituo gani
Shahidi: Kituo cha Polisi Chang’ombe
Nashon: Kwa Ufahamu Wako unafahamu Kwamba alipelekwa Kituo Kingine Cha Polisi
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Na Hamkumpeleka Kituo Cha Polisi Tazara
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Shahidi: Unafahamu Kwamba Mtuhumiwa afikishwe Mahakamani Baada ya Muda gani
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Kwa hiyo unaweza Kukaa naye Milele
Shahidi: Huwezi kukaa anaye milele, upelelezi ukikamilika unampeleka
Nashon: Upelelezi Unaweza Kuchukua Muda gani
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Baada ya Kumkamata Bwire Mlimfikisha Mahakamani Tarehe ngapi
Shahidi: Hapana Sikumbuki
Nashon: Nikisema Kuwa aliandika Maelezo Chang’ombe nitakuwa sahihi
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Nisaidie Je Mtuhumiwa anaweza kuandikwa Maelezo Kituo chochote
Shahidi: Inategemea na mpelelezi, kama yupo mpelelezi anamuandika ndiyo
Nashon: Wakati Unamkabidhi Inspector Ndowo Simu, Je zilikuwa na Line zake
Shahidi: Zilikuwa Pamoja
Nashon: KWANI Shahidi: Nyie huwa Mnatumia Mali za Mtuhumiwa
Shahidi: Kwa matumizi binafsi?
Nashon: Ndiyo
Shahidi: Haiwezekani
Nashon: Nikikuonyesha Chini ya Kiapo Kuwa wewe Umetumia Mali ya Mtuhumiwa utakataa?
Shahidi: Sijawahi Kutumia Mali ya Mtuhumiwa
Nashon: Je Tarehe 10 December 2020 Uliandika Maelezo Polisi Kituo Cha Polisi Kati Dar es Salaam
Shahidi: Ndiyo ni Maelezo yangu
Nashon: Mheshimiwa Jaji Sasa Kwa Kutumia Kifungu cha 164 naomba
Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Kuondoa Hilo Ombi sababu ya Muda
Nashon: Je Shahidi: Unafahamu kwamba unatakiwa Kumkabidhi Tuh Vielelezo Mtunza Vielelezo
Shahidi: inategemea na Mazingira
Nashon: Je Utakubaliana na Mimi Kwamba, Hukutoa Sababu Kwanini Ulimkabidhi Vielelezo Afande Swila ambaye siyo Mtunza Vielelezo
Shahidi: Ndiyo sikutaja
Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kuchukua Mali Bila Certificate of Seizure ni Kinyume cha Sheria
Shahidi: Nilieleza Afande Kingai alikuwa na Certificate of Seizure
Nashon: Hizo Certificate of Seizure Zilikuwa za Vifaa gani
Shahidi: Ni simu
Nashon: Na ni UShahidi Wako Kwamba Umetoa hapa Mahakamani hiyo Certificate of Seizure
Shahidi: Sijatoa Mahakamani
Nashon: Na Unafahamu Kwamba Ungetoa Certificate of Seizure ingeonyesha Muda
Shahidi: Miye sifahamu
Nashon: Je Unafahamu Detention Register
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Ni sahihi Ujatoa Detention Register Ya Moshi
Shahidi: Ndiyo sijatoa
Nashon: alisema Siku Tarehe 7 August 2020 Mlipofika Central Mlipewa Break ya Kunawa Uso Kabla Ya Kutoa Vielelezo
Shahidi: Ni sahihi
Nashon: ana Muda wa Kuna wa Uso Ulikuwa Lisaa Limoja
Shahidi: Ndiyo
Nashon: wewe na Sargent Nuru Mlikabidhiana Bastola A5340
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Na Hiyo ndiyo Ilikuwa Discription ya hicho Kielelezo
Shahidi: Ndiyo
Nashon: kama Nuru alitaja Kielelezo kwa Namba Nyingine kitaku ni tofauti na Ulicho taja wewe
Shahidi: Awezi Kutaja Kingine
Nashon: Unaweza Kurudia Kwa namna Kila Mmoja alivyokuwa amevaa
Shahidi: Mohamed Ling’wenya alikuwa amevaa Nguo Nyekundu Nyekundu na Adam Kasekwa Alikuw amevaa Shati Jacket la Kijani
Nashon: Hukuona Umuhimu Wa Kuja na Hizo Nguo
Shahidi: Ni Nguo zao
Nashon: Hukuona umuhimu wa kuja na nyaraka yoyote ile ilikuthibitisha kama kweli mlizunguka nao
Shahidi: Hakuna
Nashon: Shahidi nashukuru kwa ushirikiano wako
Wakili John Malya anaingia
Malya: Katika wale watuhumiwa kuna mtuhumiwa anaitwa Deshi?
Shahidi: Hakuna
Malya: Sasa umetuletea ushahidi mahakamani, mahakama a ipokee ushahidi wako, mtuhumiwa na kosa?
Shahidi: Mtuhumiwa Deshi na Kosa Deshi
Malya: Hiyo ilikuwa Kielelezo 37 Sasa Namuonyesha 38 Baada ya Namba 2097 Kuna Mkwaju 2020
Shahidi: Ni sahihi Kabisa
Malya: Je Katika Kielelezo P38 Kuan Mkwaju.?
Malya: Ni sahihi Kwamba Huu Mkwaju umetenganisha 2097 na 2020
Shahidi: Hakuna Mkwaju Kuna Nafasi
Malya: Umesema katika Kumbukumbu namba Umesema kuna Majina ya Watuhumiwa
Shahidi: Ndiyo
Malya: Sasa Faili Umekuja nalo
Shahidi: Sijaja nalo Mimi siyo Mpelelezi
Malya: Tarehe 04 August 2020, Mahita alikufuata akakwambia Twende Kwa RCO, Ukaenda Kubebea Silaha
Shahidi: Ndiyo, Niliambiwa Kuna kazi ya kufanya
Malya: Ulikuwa unajua Unafanya kazi gani
Shahidi: Hapana
Malya: Kwenye Sehemu ya Kutunza silaha, Kuna Virungu?
Shahidi: Ndiyo havitumiki siku hizi
Malya: Kwenye store yenu ya Polisi Kuna Bastola
Shahidi: Ndiyo zipo, ila miye siyo polisi mdogo
Malya: Wewe ulibeba AK 47?
Shahidi: Ni sahihi
Malya: AK 47 ina Kama Kilo 3.4 hivi bila Magazine
Shahidi: sawasawa
Malya: Coplo Francis na yeye alikuwa na silaha na yeye?
Shahidi: Ndiyo, Askari Alisha Kuwa na Silaha lazima awe Makini
Malya: Wakati Jumanne anafanya Upekuzi Ulieleza Kuwa Bunduki Uliweka Wapi
Shahidi: Sikueleza
Malya: ulimuuliza za Mheshimiwa Jaji aina ya Nguo ulizovaa
Shahidi: Si Kumueleza
Malya: Kwa hiyo Kama ilikuwa na Mifuko Michache au Mingi hatuwezi Kujua
Shahidi: Ndiyo
Malya: Pale Rau Mlimkamata Simu Ngapi
Shahidi: Simu Mbili
Malya: Mmekamata Simu Mbili na Madawa ya Kulevya, Ukakamata na Bunduki na AK 47 Yako
Shahidi: Ndiyo
Malya: Ulitumabia Kuwa Upande wa Dereva Upo Upande gani
Shahidi: Sijasema Hapa Mahakamani
Malya: Je Umetumbia Ka Uliapa Mgongo au Ukirudi Kinyume Nyuma Askari mahili
Shahidi: Hapana Sijasema
Malya: Je alituelezq kwamba ulishika akwa namna gani vielelezo wakati una AK 47 ya Kilo 3.4
Shahidi: Sikueleza
Malya: Je Ulitumabia Kuwa Ulipofika Kwenye Gari Ulishika Bahasha Kwa namna gani
Shahidi: Nilisema Kwamba Nilimwambia Azizi anipe Bahasha
Malya: Je Kuna sehemu ulitoa Utofauti wa Bastola zilizopo Kwenye Chumba Cha Kutunzia Silaha
Shahidi: Hapana Sikutoa
Malya: Je ulitoa Ufafanuzi Kuwa ulipo rudi nazo Wakati anajaza Ulikuwa unafanya Ulinganifu Mbele ya MaShahidi: Pale Rau Madukani
Shahidi: Hapana Sikutoa
Malya: Naomba Kielelezo Namba P3, na Risasi zake
Malya: Leo hapa Mahakamani Ukiongozwa na Kaka yangu Pius Hilla Hilla, umeonyeshwa hapa Mahakamani
Shahidi: Hapana sijaonyeshwa
Malya: Uliambiwa Kwamba Risasi Moja Bwana Hafidh kaivunja vunja
Shahidi: Sijaambiwa
Malya: Uliambiwa Utoa Risasi Kwenye Magazine, ukatuonyesha Magazine
Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Swali liwekwe Vizuri, Hakuambiwa Atoe Risasi tatu
Shahidi: Hapana Sikuonyesha
Malya: Ulituonyesha Risasi Tatu Mahakamani au Hukutuonyesha
Malya: Wewe Ndiyo Ulimkabidhi Bwana Ndowo Simu
Malya: Je ulitoa Mahakamani hiyo Hati ya Makabidhiano
Shahidi: Ndiyo
Malya: Nani sasa ataleta Hati ya Makabidhiano ya hizo Simu
Shahidi: Hapana
Malya: Sasa tutamuuliza maana kuna su zime vunjwa vunjwa
Shahidi: Miye nilimuachia Ndowo
Malya: Kaja hapa ajatuonyesha,mwenzio
Shahidi: Sijui
Malya: Wewe ulieleza kuwa kuna simu kama hii imevunjwa?
Shahidi: Hapana sijaeleza
Malya: Unafahamu Justine Kaaya
Shahidi: Ndiyo Namfahamu
Malya: Unamfahamu Gabriel Muhina
Shahidi: Ndiyo namfahamu
Malya: Kwa hiyo Kwenye Faili namba CD/IR 2097 /2020 Walikwepo Wote
Shahidi: Sifahamu
Malya: Kwani wakati faili linafumguliwa ulikwepo?
Shahidi: Hapana
Malya: Sasa Unaposema Jina Deshi Deshi lipo kwenye faili kwani unajua kuna majina mangapi kwenye faili?
Shahidi: Hapana Sifahamu
Malya: na Unaposema Bwana Jumanne alikukabidhi Vielelezo Pale Rau Madukani
Shahidi: Ndiyo
Malya: na MaShahidi: Wote Waliona pale Rau Madukani Moshi
Shahidi: Ndiyo Waliona
Malya: Enheeeee Jumanne alikwenda Kujazia Fomu ya Makabidhiano Wapi
Shahidi: Kwenye Gari
Malya: Wewe Unasema Ulimkabidhi Afande Ndowo Simu na Line zake, Yeye Kaja Hapa Mahakamani Kaleta Simu Peke yake…. Nani Kaiba Line za Wateja Wangu
Shahidi: Sijui Kwa Sababu Nilimkabidhi Simu zikiwa na Line zake
Malya: Je kuna uwezekano wewe ndiyo umepoteza?
Shahidi: Weeeee hapana, nilikabidhi vyote
Mahakama kichekoooooo
Malya: Sasa shahidi, kuna tuhuma hapa wewe na Afande Mahita ndiyo mlikuwa mnwapiga watuhumiwa kwa kushirikiana na kuwa piga kwenye nyayo
Shahidi: Hapana siyo kweli hakuna mtu aliye wapiga
Malya: Kuna Story Very Interesting, Mwanzo mlisema Kuwa Afande Mahita alifanya Doria akasema Kuwa Wapo watatu, Ila Baada ya Kuwakamata hawa na Kuwa Pekua Ndiyo Mkashtuka Mmoja hayupo, Kwanini Hamkushtuka palepale
Shahidi: Afande Kingai Eneo la Tukio aliwauliza Wakakaa Kimya
Malya: Je Wakati a Unaongozwa na Wakili Pius Hilla Ulisema hilo
Shahidi: Hapana
Malya: Sasa iweje Ghafla Kwenye Gari Waanze Kutaja, Si Kwa sababu Mliwapiga
Shahidi: Hapana walijitolewa wao wenyewe kusema yupo wapi
Malya: Wewe ulishuhudia Wakati anajaza Fomu
Shahidi: Nilikuwa karibu
Malya: Ulishuhudia.?
Shahidi: Nilisikia
Malya: Soma Kielelezo Hicho Majina yameandikwaje
Shahidi: Adam Hassan Kasekwa ADAMOO
Malya: We Ulikwepo Eneo la Tukio kweli
Shahidi: Ndiyo nilikwepo ila Afande Jumanne ndiyo kasikia Vizuri zaidi
Shahidi: Hakuna
Malya: Hati ya Makabidhiano Ya Simu, Hasa ya Adamoo Kutoka Kwa Afande Jumanne Kuja Kwako, Umetoa Mahakamani Leo
Shahidi: Hapana
Malya: Umeonyeshwa Fomu ya Kabidhiano ya Simu.?
Malya: Kwa ufahamu Wako wewe Mpelelezi Wa hii Kesi alikuwa ni nani
Malya: Kwenye Faili CD/IR /2097 /2020 Kuna tuhuma Ngapi
Shahidi: Sifahamu
Shahidi: Simfahamu, Zaidi ya Kula Njama
Malya: Kutoka USA Mlipotoka Kuelekea Kilimanjaro, Moshi Mjini si mlipita Wilaya Ya Hai?
Shahidi: Ndiyo
Malya: Mlipita Kwa a Mkuu wa Wilaya ya Hai oe Boma Ng’ombe Kumwambia Be Careful
Shahidi: Hapana
Malya: Nyumbani kwake ulikwenda?
Shahidi: Hapana
Malya: Ni sahihi Kwamba Sababu Ya Kuandika namba ya silaha kwenye Hati ya Makabidhiano, ilikuwa Kutofautisha hii Silaha na Nyingine
Shahidi: Ni sahihi
Malya: na Kwa Uzoefu wako wewe Mpaka Kushika A47 ni sahihi Bullets zinatofautiana
Shahidi: Ndiyo
Malya: Je wewe Kwenye Hati ya Makabidhiano, Umetoa tofafuti ya Bullets hizi na Zingine
Shahidi: Hapana Sijatoa
Malya: Kwa Sababu Zile namba za Bullets Huku andika Nikikupa Zile Bullets Utakumbuka
Shahidi: Hapana Siwezi Kukumbuka
Malya: haya Turudi Arusha Ndugu yangu, Ulipofika USA Nakuambiwa Kuwa kuna Ugaidi Wa Kulipua vituo Vya Mafuta Je Mliwakuta na kidumu cha Petrol.?
Shahidi: Hapana
Malya: Mliwakuta na Mabumo ya Kulipua.?
Shahidi: Hapana
Malya: Mliwakuta na Chain Saw ya kukatia Magogo?
Shahidi: Hapana
Malya: Je ni sahihi Afande Kingai kwa nafasi yake anaruhusiwa Kutembea na Bastola
Shahidi: Ndiyo
Malya: Je Jumamne Kwa nafasi yake anaruhusiwa Kutembea na Bastola
Shahidi: Ndiyo
Malya: Je Wakati Unatoa UShahidi: Wako hapa Ulisema Kwamba Siku hiyo Walikuwa nazo au Waliacha kwenye Gari
Shahidi: Hapana Sijatoa Maelezo
Malya: Mnasema Mlimkuta Adamoo na Itel, Je Ili mimi Nabisha Mlimsimgizia si ni lazima Twende Voda au Tigo na Ile Simu na Line, Wakaangalie Usajili
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Hii simu ya Bw. Khalfani Bwire, Ni sahihi alikukabidhi Simu Baadae
Shahidi: Hapana alinipa palepale
Malya: Lakini Taratibu za Kipolisi Zinataka anapokukabidhi aKukabidhi na Kikaratasi
Shahidi: Hapana Siyo Lazima
Malya: Kuhusiana na Kukamatwa Kwa Bwire, Je Kuna Dereva au Abiria aliye shuhudia Wakati Bwire anakamatwa
Shahidi: Hakuna
Malya: Wewe Umemfahamu Lini Bwire?
Shahidi: Nilikuwa simfahamu mpaka baada ya kumkamata
Malya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Ulikuwa Umjui
Shahidi: Mheshimiwa Jaji ilikuwa simjui
Malya: Je ulitoa Ufafanuzi Kwamba Ulijuaje Kwamba Yule Ndiyo Khalfani Bwire
Shahidi: Hapana Sikutoa, Ila aliyekuwa anajua ni Kingai
Malya: Mheshimiwa Jaji sina swali la ziada kwa shahidi: huyu na pia muda umefika
Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji kwa kuzingatia suala la muda na ukizingatia nina maswali mengi nilikuwa naomba hairisho
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi kuhusu hiyo hoja
Jaji Jumatatu itakuwa Tarehe Ngapi
Mawakili: Tarehe 24
Jaji: Shauri linahairishwa tena Mpaka Jumatatu Tarehe 24 January 2022 ambapo shahidi: ataendelea kuhoji wa na upande wa utetezi
Washitakiwa Wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Jumatatu Saa 3 Asubuhi
Jaji anatoka

Like