Kesi ya Mbowe: Kibatala adai jibu la shahidi wa Jamhuri ‘limetoka kwa Mungu’

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 20 Januari 2022.

Jaji ameingia mahakamani muda huu saa 4 kasorobo
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali: Robert Kidando Mheshimiwa Jaji ikupendeza naitwa Robert Kidando nipo pamoja na Wakili wa Serikali: Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala: nipo Pamoja na wakili
Nashon Nkungu
Faraji Mangula
Fredrick Kihwelo
Seleman Matauka
Maria Mushi
Hadija Aron
Alex Massaba
Jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo mahakamani
Wakili wa Serikali: Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na tupo tayari kuendelea
Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasisi pia tupo tayari kuendelea
Jaji Shahidi: nakukumbusha bado upo chini ya kiapo
Wakili wa Serikali: Robert Kidando atamuongosha shahidi: kwenye Re Examination
Wakili wa Serikali: Shahidi jana uliulizwa kama ulidukua taarifa za mtu mwingine, ukasema jibu haiwezi kuwa ndiyo au hapana, ulikuwa unamaanisha nini
Shahidi: Ukisema hacking inategemea nia ya yule anaye fanya kile kitendo, kuna wakati inaweza kuwa nia ovu au hapana, ndiyo maana nikasema inategemea
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali pia kuhusiana na zoezi la extraction, kama zoezi ulilofanya ungeweza kubaini namba ya mtu anaitwa Bwire, ukasema uwezi, fafanua
Shahidi: Katika Extraction tunafanya zoezi la identification la ICCID namba, na ilikujia ni namba gani lazima urudi kwa mtoa huduma, ndiye atathibitisha ni namba gani
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali pia kuhusiana na wakati wa kufanya uchunguzi, kama kifaa kikiwa kina kina Internet Connection, inaweza kisababisha kifaa kuingiliwa, ukasema siyo kila wakati ila ni wakati fulani fulani
Shahidi: Mheshimiwa Jaji wakili alikuwa ananiuliza kifaa cha maabara ndiyo maana nikasema kama kitaunganishwa kina weza
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kama kifaa cha maabara wakati wa uchunguzi hakitakiwi kuwa na internet connection, kinatakiwa kuwa off, waka uliza kama kinaweza kuwa connected na infrared au bluetooth
Shahidi: Mheshimiwa Jaji hayo ni mambo tunazingatia maabara kwamba wakati wa zoezi tuna hakikisha hakuna connection either ya bluetooth au infrared
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu zoezi la analysis ukasema wakili kakunukuu vibaya ulikuwa unamaanisha nini
Shahidi: Wakati wa zoezi la analysis una tafuta content ulizopewa against zile content zote, ndiyo analysis
Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia akama kwa uchunguzi uliofanya kama ukiweza kubaini majina ya mmoja baada ya mwingine, kama wana husika na ugaidi ukasema mpelelezi ndiyo anaweza kubaini hilo
Shahidi: Role yangu kama mchunguzi, ni kumpa mpelelezi yale aliyo yaomba, mimi kama mchunguzi sihusiki kabila na hilo
Shahidi: Wakati Watu wawili wanaongoe kwenye mawasiliano kuna mtu anaunga nisha hapo, ambaye ni mtoa huduma, mimi siwezi
Wakili wa Serikali: Shahidi pia ulikuwa unaulizwa kuhusiana na data ambazo ulizo access katika zile simu, kama ukiweza kupata simu za kuongea ukasema wewe ulicho access ni call logs
Mangula: OBJECTION Mheshimiwa Jaji, JANA Wakati namuuliza shahidi alisema hawezi kuzungumza kuhusu sauti, alisema awezi kuzungumza sababu za kiusalama, naomba jibu liondolewe au tuoate nafasi ya kumuuliza tena
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji kuna tatizo hapa, hili swali aliulizwa nashon nkungu, ambapo shahidi: alisema haku access sauti bali call logs na hata jibu aliokuwa anatoa
Jaji: Kwamba kwanini haku access sauti
Mangula: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa OBJECTION sikutaja swali lilikuwa na nani
Jaji: Hayo hakuyatoa, isipokuwa nasema anayatoa haya kwenye ufafanuzi, je ni sawa..?
Mangula: Siyo sawa, ndiyo hoja yetu ipo hapo
Jaji: Suala la sauti ipo kwa services provider haya kutolewa jana, ndiyo maana anataka jibu liondolewe
Wakili wa Serikali: Inspector Ndowo kila ulipoulizwa kuhusu kufanya extraction ya sauti, na ulisema hamku access, bali wewe ulifanya ku access call logs
Wakili wa Serikali: Shahidi uliulizwa swali pia kama wakati unafanya extraction, kama hivyo vifaa uliyotumia vinaweza kubaini simu ni original au feki
Shahidi: Mheshimiwa kwa sababu mnapowasiliana, kinacho bali katika vifaa vyao ni call logs, kwa maana tarehe fulani siku fulani mtu fulani alipiga simu kwa mfu fulani
Shahidi: Kazi ya mtambo ule siyo kubaini simu ni feki au original, bali ni ku extract kilichopo ndani ya simu
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali pia Kuhusiana na Vitu Viwili Pia Kuhusu DECORDING na Analysis ya Data
Shahidi: Ni Vitu Viwili Tofauti, DECORDING ni Wakati Wa Mchakato Wa Physical Analyser inapo analyse Data Wakati ili Vitu hivyo viweze Kuonekana Ina fanyika DISCRIPTION
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusu Reporting Na Uchunguzi
Shahidi: Riporting ni Automatic Process, Mpangilio unapangwa na Mfumo wenyewe
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusiana na Kama Kazi ya Physical Analyser Kama kazi yake ni Kupanga Mafaili kwa Logical Sequence, Ukasema Siyo Wakati Wote Inafanya hivyo
Shahidi: Mpangilio Wa Data, Unategemea na Kazi Iliyo fanyika, Ulifanya Kwa File itafanya Katika Mfumo huo na Ulifanya Physical Itakuwa katika Namna tofauti
Wakili wa Serikali: Kingine Uliambiwa Kuwa Ulinganifu Wake ni sawa tuh Na screen Shots za Kwenye Simu, Ukasema Siyo hivyo
Shahidi: Mfumo Umetengenezwa katika Namba ya Kupata Taarifa Kama Imefutwa au Ipo, Katika Kile Kifaa, Tofauti na Screen Shots Hauwezi Kuona Kama Taarifa Imefutwa
Wakili wa Serikali: Ulizwa Maswali Kuhusiana na Vielelezo Katika Extraction Riport, Hasa Kielelezo namba 24,25,26 na 27 kuhusu Cable zilizotumika, Ukasema Cable namba 100 ilitumika Katika Kielelezo 24,na 26 Kwingine Ukasema haionekani
Shahidi: Taarifa Kuhusiana na Identification Katika hivyo Vifaa Inategemea na…….
Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Hayo so tuh Majibu Mapya, Hata tulipo Muuliza Hakusema
Jaji: Swali halijapingwa, Bali Shahidi: alicho eleza Leo Jana Hakuyaeleza
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona tupo Sahihi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Purpose ya Re Examination ni Kupata Ufafanuzi, Sisi tunaona tupo Sawa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Msingi wa jibu la Shahidi, alisema alituma Cable ya aina Moja, Bila Kujua na pelekwa Wapi, Na baadae tukaenda kwa Moja Moja
Aendelee kama Sisi tutapewa nafasi Ya a Kuuliza Maswali zaidi, na Kwa Nini aendelee Wakati Sheria inakataza
Jaji anasema Kwamba Kwa Mtazamo wake Na wao Waje Wapate nafasi ya Kuuliza
MaWakili wa Serikali: Wanakutana na Kujadiliana Kama Kikundi
Wakili wa Serikali: Ni sawa Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nimewasiliana na Wenzangu tunaomba tuliache hilo Swali
Wakili wa Serikali: Shahidi: Uliulizwa hapa Kama Unachunguza Tuhuma Za Jinai, Ukasema Wewe Unachaguza Vifaa Vilivyohusishwa na Jinai, Maana yake nini
Shahidi: Sisi Kazi Yetu ni Kutoa Taarifa Kwa Wapelelezi Ambao wa naleta Kazi za Uchunguzi Forensic Beaural, Kwa hiyo Sisi Mwisho Wa Kazi yetu ni Kutoa Taarifa akama Vile ambavyo Wameomba
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Pia ni Lini haswa, Vile Vielelezo Vilirudishwa Kwa DCI Ukasema Vilikuja Kuchukuliwa Tarehe 10 July 2021 wakati Wakili Pius Hilla anakuongoza Ulisema Tarehe 06 August 2021
Unasemaje kuhusu hiyo Tofauti
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naomba Mahakama Yako ichukue Tarehe 10 July 2021
Shahidi: Features zote ni Automated Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Kielelezo namba 27 kama aina simu ilitajwa Katika Kielelezo hicho kama Katika Vielelezo Vingine, Hebu Ifafanulie Mahakama
Shahidi: Mazingira kama hayo yanatokea Pale ambapo Property ya Kifaa Husika Haipo Katika Kifaa Husika, Tunatumia Chipset….
Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hiyo ni Fact Mpya, Concept anayojemga Sasa hivi Hakuulizwa Swali, Ali Volunteer yeye Mwenyewe, Mimi nikasema Jibu lako limetoka Kwa Mungu, Re examination purposes yake ni Kufikia Mashimo ya Maswali, Siyo Kwa Kitu ambacho hakuulizwa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji OBJECTION Yake haina Mashiko, Kwanza ana admits kabisa kama lilijitokeza, Kwanza Jana alikuwa Shahidi: akitaka Ufafanuzi anasema Miye sitaki Ufafanuzi, Swali letu lipo Kutaka Kupata Majibu
Jaji Suala la Kwamba aliulizwa au Ali Volunteer siyo Sahihi, process ilikuwa ni Cross examination
Suala ni Information inayo letwa Haiku letwa hapo awali
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Ngoja Niulize Kwa tofauti
Shahidi: Kwamba Kuna Simu Haijatajwa, Elezea hapo Kwa Kuji Confine
Shahidi: Kwa sababu ilitumika kwa Chipset
Wakili Kibatala: Kinachofanyika ni Kile Kile tuh Kwa Njia Mpya
Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa Kugundua Kuwa Suala la Chipset au Simu Card halikuingia Mahakamani, wanataka Kuingiza UShahidi: Mpya Kwa Njia ya Nyuma, Naungana na Kaka Yangu Kibatala
Jaji: Swali nafikiri halina Shida
Wao wanasema Katika Majibu ni UShahidi: Mpya, Je Nyie Mnasemaje
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba niliondoe hilo Swali
Wakili wa Serikali: Shahidi: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Service Provider, Ukasema ni TTCL Ukaulizwa Kama anaweza Kuwa access Data Ukasema si Kweli, Ni Kwanini Ulisema hivyo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Ni kweli TTCL Anatupa internet ila Control ya Data ni Sisi wenyewe
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana na Kielelezo namba P35 ambapo Wewe Uliandika Kama Kielelezo namba H, ambapo Juu imeandikwa “IMEI namba Imefutwa” Ukaulizwa Kama Kwenye Riport yako Uliandika, Ukasema hukuandika
Je ni Kwanini
Shahidi: Kwa sababu celebrite ina Access na Ku Extract IMEI namba
Wakili Kibatala: It’s a New Fact, Hakuna Mahala Popote ambapo alisema Kuwa Celebrite Ina Extract IMEI namba
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji OBJECTION Yake haina Mashiko, Kwa sababu Shahidi: amesha Sema a kuwa Taarifa ni Automatic generated
Jaji: Nakumbuka Alisema Kuwa Taarifa za IMEI namba inaweza Kuonekana Kwa Ile iliyopo Wazi au ambayo ipo Ndani, na alisema Barua Ilikuwa Na IMEI namba
Kibatala: Kuhusu Barua Hakuna Tatizo, Lakini Kwamba Celebrite Kuwa Inaweza Kutoa kama End Product kuwa ni IMEI
Jaji: alisema Kuwa IMEI namba inaweza Kupatikana ndani ya Simu
Kibatala: Hilo Kweli alisema ila tunapinga Kuwa Ali Extract Kwa kutumia Celebrite Mashine, Hilo tunapinga
Wakili wa Serikali: Shahidi: aliulizwa Kama Kwenye Riport alisema, akasema Hakusema, Sisi tunataka Kujua kwanini Hakusema Kwenye Riport
Jaji: Sasa Jibu lake lilikuwa Lina Jibu swali
Wakili wa Serikali: Naomba Kurudia Swali
Wakili wa Serikali: Kwanini Huku andika katika Riport yako Suala la IMEI namba
Shahidi: Nilipata Kwa andani
Kibatala: Anajibu Kitu Kilekile
Jaji: Nafikiri Shahidi: Ajibu swali, Kwanini Katika Riport Yako Ujaandika Suala la IMEI namba
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Katika Uchunguzi Wangu IMEI namba huwa naiona
Wakili wa Serikali: Shahidi: Uliulizwa Swali Kuhusiana na Ile Barua Iliyo andikwa Kwemda Kampuni ya Tigo, Kuwa haina Sahihi yako, Ukasema ni Kweli Signature yako haionekani, Je ni Kwanini
Shahidi: Ni Utaratibu Wa Ofisi kwa Cheo Changu siwezi Kusaini Barua zinazo enda Nje ya Ofisi.
Jaji: Nakumbuka Kuwa yeye alisema Kuwa Hakusaini Kwa Sababu Yeye Siyo Ofisa Mwenye Mamlaka Ya kusaini
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kukomea Hapa, Sina Swali Lingine la Ziada
Jaji: Shahidi tunakushukuru Kwa UShahidi: Wako Unaweza Kwenda Sasa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji baada ya Zoezi hilo, Hakuna Shahidi: Mwingine Kwa Leo, Tunaomba Hairisho Mpaka Kesho Tarehe 21 January 2022 ilituweze Kuendelea na Shahidi: Mwingine
Sababu Shahidi ambaye tulimtegemea angefika Jana, Hakufika, Ile Jioni tulivyotoka Hapa tulilazimika Kuita Shahidi: Mwingine, hivi Leo atafika, Tutafanya Maandalizi tuweze Kesho Kuendelea
Shahidi: tuliye Mtegemea Jana Si Mkazi wa Dar es Salaam na Shahidi: ambaye anakuja Leo Si Mkazi wa Dar es Salaam, Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Kibatala: Mheshimiwa Jaji ka ambavyo tulielekezwa na mahakama, sisi tupo na tupo tayari, kama tungejua mapema tungeweza kufanya mambo mengine
Naikumbusha mahakama kuhusu amri yake ya jana na juzi
Kuhusu Kukosekana na Shahidi, Ni Detrimental Kwetu
Nammukuu Dr.Nshala ” Siku za mwanadamu hauwezi kuzifidia zikipita”
Sisi tumekuwa waaminifu kwa mahakama kuzia kesi kuhairishwa, pamoja na changamoto nyingi
Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Jaji anaandika Kidogo
Mahakama ipo Kimya
Muda ni Saa 4 na Dakika 56
Bado Mahakama Ipo Kimyaaaaa
Jaji: ni kweli kwamba mahakama hii kwa amri ilitoa siku mbili ilieekeza jamhuri kuwa waleye shahidi, kwa jana ukweli hapakuwa na muda kwa namna shahidi: alikuwa anatoa ushahidi: wake ili chukua muda mwingi wa jana
Lakini ilitegemewa leo ushahidi: wake ungemalizika mapema na kuendelea na shahidi: mwingine
Upande wa mashitaka wamekuja kuwa shahidi: amekuwa nje ya Dar es Salaam
Upande wa utetezi nimesiliza concern zao
Kwa sababu hiyo naagiza upande wa mashitaka kesho walete shahidi: tuweze kuendelea
Na ka shahidi huyo mnaye muita atakuwa na dharula basi mfamye mapema kuita shahidi: mwingine
Kwa Maana hiyo nahairisha Shauri Mpka Kesho, Washitakiwa Wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Kamili Asubuhi
Jaji anatoka

Like