Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 24 Januari 2022.
Jaji ameingia Mahakamani saa 4 na dakika 55
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Peter Kibatala Wakili wa Mshtakiwa wa Nne, Nipo Pamoja na Wakili
Nashon Nkungu
Faraji Mangula
Dickson Matata
Michael Mwangasa
Idd Msawanga
Sisty Aloyce
Seleman Matauka
Jaji: anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo tayari Kuendelea
Jaji: Wakili wa Utetezi
Wakili Peter Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji
Jaji: Shahidi Nakukumbusha Siku ya Ijumaa Uliapa, Na Leo Utaendelea Kutoa Ushahidi Wako Chini ya Kiapo
Wakili Dickson Matata ananyanyuka na Kuendelea
Matata: Shahidi Habari
Shahidi: Salama
Matata: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulisema Wakati Mnafanya Ukamataji We Ulikuwa Detective Coplo
Shahidi: Siyo Sahihi
Matata: Ulikuwa nani
Shahidi: Detective
Matata: Utakubaliana na Mimi Kwamba Kwa nafasi hiyo Ulikuwa Unatakiwa Kufuatilia Vyombo Vya Habari na Bunge Ilikupata Taarifa za Ndani na Nje ya Nchi
Shahidi: Kufuatilia Habari ni Jambo la Kawaida Kabisa Kama Unataka Kufuatilia
Matata: Kama Ulikuwa Unafuatilia Uliwahi Kusikia Habari Ya Mtu Kupigwa Risasi Mkoani Dodoma anaitwa Tundu Antiphas Lissu
Shahidi: Ndiyo Niliwahi Kusikia
Matata: Unafahamu Kwamba Tundu Antipas Lissu ni Kiongozi za Chadema
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Matata: Na Kwamba alipigwa Risasi akiwa Kwenye Shughuli za Bunge, Dodoma
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Matata: Je Ulifuatilia Kuhusu Report ya Tukio hilo kutoka
Shahidi: Sijawahi Kufuatilia
Matata: pia Ushawahi Kusikia Kuvamiwa na Kuulizwa Kwa Freeman Mbowe Dodoma
Shahidi: Nishawahi Kusikia
Matata: Na Je Unafahamu Kwamba Freeman Mbowe ni Kiongozi wa Chadema
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Matata: Kwa hiyo Unathibitisha Kwamba Tundu Lissu na Freeman Mbowe ni Viongozi wa Chadema?
Shahidi: Ndiyo ni Viongozi Wa Chadema
Matata: Sasa Shahidi Kwa Ufahamu Wako Baada Ya Mtu Kama Tundu Lissu Kupigwa Risasi 16 anaruhusiwa Kuwa na Ulinzi au hatakiwi
Shahidi: Suala la Ulinzi ni La Mtu Binafsi, akiamua anakuwa na Ulinzi
Matata: Je unafahamu Kwamba Mmoja ya mtu Mliye Mkamata Rau Madukani ni Mlinzi Wa Mbowe?
Shahidi: Sifahamu
Matata: Kwani Tukio la Rau Madukani lilifanyika lini?
Shahidi: Tarehe 05 August 2020
Matata: Je Kipi Kilianza Kati ya Tukio la Lissu na Rau Madukani
Shahidi: Sifahamu
Matata: Je unafahamu Kwamba Washtakiwa Wanashtakiwa kwa Kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Matata: Moja ya shutuma pia, Ni kutaka Kumdhuru Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya
Shahidi: Ndiyo
Matata: Kwa kuwa Ole Sabaya alikuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Je Freeman Mbowe alikuwa mbunge wa wapi?
Shahidi: Sifahamu alikuwa mbunge wa wapi, sijui kati ya SIHA au MOSHI ila najua alikuwa mbunge tu..
Matata: Je, hjawahi kusikia kiwa Freeman Mbowe alikuwa mbunge wa jimbo la Hai?
Shahidi: Ndiyo maana nimesema nilikuwa sifahamu ni SIHA au wapi ila najua ni Machame…
Matata: Uliwahi Kusikia Kwenye Vyombo Vya Habari Kuwa SABAYA alisema 2020 Freeman Mbowe hawezi Kushinda Ubunge Hai.?
Shahidi: Sijui
Matata: Kazi Maalum Maana Yake ni nini, Uliposema Kwenye Ushahidi Wako Juzi
Shahidi: Haina Utofauti na kazi za Kawaida
Matata: Kwakuwa Umekiri Kuwa Kazi Maalum haina Utofauti na kazi za kawaida, kwanini wewe na Wenzako Mlipokuwa Mnakuja Hapa Mnasema kazi Maalum
Shahidi: Kwa Nature ya kesi, ilikuwa ni Kuzuia Uhalifu
Matata: Sasa Shahidi Nikisema Kwamba Kazi Maalum Ilikuwa Ni Kumdhoofisha Mbowe kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 ili asiweze Kushinda Ubunge
Shahidi: Si Kweli, Ndiyo Maana Walikamatwa Wenyewe
Matata: Kwani Unaposema Walikamatwa Wenyewe, Hapa Mahakamani Hayupo na Mbowe?
Shahidi: Mheshimiwa Mbowe naye Yupo
Matata: Wakati Unatoa Ushahidi Ulisema Wanataka Kufanya Ugaidi Kiongozi wao alikuwa Freeman Mbowe
Shahidi: Hapana Siyo Kiongozi Wao, Nilisema anayeratibu alikuwa Freeman Mbowe
Matata: Na Taarifa Za Kwamba anaratibu Ulizifahamu Mapema
Shahidi: Nilifahamu Tarehe 04 August 2020
Matata: Kama ulizipata, Je kwa Kawaida Mtu anayeratibu ni Mtuhumiwa au siyo Mtuhumiwa
Shahidi: Ni Mtuhumiwa
Matata: Kama ni Mtuhumiwa Ikumbushe Mahakama Mbowe alikamatwa lini
Shahidi: Sikumbuki Lini, ila ni 2021
Matata: Tukihesabu Tangu umezifahamu hizo Taarifa, Mpaka anakamatwa 2021 imepita angalau Miezi Mitano?
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa Hiyo Kwa Muda wote huo alikuwa hajakamatwa
Shahidi: Ndiyo alikuwa hajakamatwa
Matata: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulieleza ni Kwanini Mtu anayeratibu Ugaidi, ni kwa nini alikaa Miezi zaidi ya Mitano Bila Kufikishiwa Kwenye Vyombo Vya Dola
Shahidi: Sikueleza
Matata: Baada ya hilo Jibu lako bado Unakataa suala la Kuwakamata Walinzi Wa Mbowe haikuwa Kumdhoofisha Mbowe Wakati Wa Uchaguzi Mkuu wa 2020
Shahidi: Haikuwa hivyo
Matata: Wewe ni Polisi Wa Kituo Gani
Shahidi: Central Arusha
Matata: Wakati Unawakamata Ulikuwa na Cheo gani
Shahidi: Constable Wa Polisi
Matata: Wakati Mpo Central Arusha na mkaenda Kuwakamata Watuhumiwa Rau Madukani Mkoa Mwingine Wa Kilimanjaro
Shahidi: Ni sahihi
Matata/ Na Kwa Mujibu wa Utaratibu Wa Kipolisi, Polisi anapokuwa anaenda Mkoa Mwingine anatakiwa Kuwa na MOVEMENT ORDER
Shahidi: Ndiyo ni sahihi
Matata: Na Hiyo Movement Order Ndiyo inaonyesha Umetoka Mkoa Wako Kwenda Mkoa Mwingine Kufanya kazi fulani
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Ukikosa hiyo Movement Order Unakuwa unaenda Kufanya Kinyume na Taratibu
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Je Shahidi Wewe Umeleta Movement Order Hapa Mahakamani
Shahidi: Sijaja nayo
Matata: Baada ya Kufanya Mliyofanya Moshi Mkaelekea Dar es Salaam ambapo ni Mkoa Mwingine
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulileta Movement Order Kwamba Umekuja Dar es Salaam
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Matata: Ulisema Kwamba Ulikuwepo Kwenye Ukamataji pale Rau Madukani
Shahidi: Ni kweli
Matata: ulisema katika Ukamataji Ule Watuhumiwa walikuwa watatu, Ila Mmoja aliweza Kutoroka, ambaye anaitwa Moses Lijenje
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Je Umezungumzia Katika Ushahidi Wako Kwa Yoyote Kuendelea Kumtafuta Moses Lijenje
Shahidi: Sijazungumzia
Matata: Mpaka Mnaleta Kesi Mahakamani, Upelelezi Ulikuwa Umekamilika
Shahidi: Mimi sifahamu kwa sababu Siyo Mpelelezi
Matata: una taarifa zozote za Moses Lijenje
Shahidi: Sina Taarifa
Matata: anatafutwa au hatafutwi?
Shahidi: Taarifa za kuwa anatafutwa zipo na nazifahamu
Matata: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulieleza Mahakama Kwamba anaendelea Kutafutwa?
Shahidi: Nilieleza za Kwamba anaendelea Kutafutwa
Matata: Kwa Maelezo yako akikamatwa atakuja kuunganishwa Kwenye hii Kesi
Shahidi: Mpaka akamatwe
Matata: Je Shahidi Unafahamu Kwamba Makosa ya Ugaidi ni Makosa Makubwa Sana
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Matata: Na Je Unafahamu Kwamba suala la Ugaidi ni la kidunia
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Matata: Je unafahamu Kwamba Mtu anayetuhumiwa kwa Ugaidi ni Hatari Sana
Shahidi: Mpaka Mahakama ithibitishe
Matata: Je kati ya Mtu anayetuhumiwa kwa Kuiba Kuku na Mtu anayetuhumiwa Kwa Kufanya Ugaidi, nani ni Mtu hatari
Shahidi: Yote ni Makosa na Wote wanaweza Kuwa Hatari
Matata: Wakati unahojiwa na Wakili hapa, Ulizungumzia chochote Juu ya Moses Lijenje Kwamba Uchunguzi unaendelea, ikiwa kumtangaza Kwenye Gazeti ili Raia wema wasaidie?
Shahidi: Sijazungumzia
Matata: Kuhusu kumtangaza Kwenye Tv
Shahidi: Sijazungumzia
Matata: Kwakuwa Moses Lijenje alikuwa Mwanajeshi Ulizungumzia Chochote Kuhusu Kushirikiana na Jeshi liweze Kusaidia
Shahidi: Sija +zungumzia
Matata: Ulizungumzia kuhusu kushirikiana na Interpol Ili Kumkamata
Shahidi: Sijazungumzia
Matata: Ulizungumzia Kuhusu Kuongea na Vyombo Vya Kimataifa kama BBC ili Kuweza Kumkamata Moses Lijenje
Shahidi: Sijazungumzia
Matata: Ulizungumzia Kuhusiana Kuongea na Ofisi za mabalozi kuhusu Kumkamata Moses Lijenje
Shahidi: Sija zungumzia
Matata: Kuhusu Vyombo Vingine Vya Kimataifa Vya kupambana na Ugaidi
Shahidi: Sijazungumzia
Matata: Nilisikia Kwamba Mlipofika Central Police Moshi Mahita na Jumanne Ndiyo Walishuka
Shahidi: Ndiyo
Matata: Na Kwamba Mahita na Jumanne, Walipo rudi ndiyo Mkaenda Kumtafuta Moses Lijenje
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Wakati Mpo Central Police Moshi, Je Mlikuwa na Mashahidi huru
Shahidi: Walikuwa Kwenye Gari Nyingine
Matata: Je Ulisema lolote Kwamba Mashahidi huru Walishuka kwenda Kuandika Maelezo
Shahidi: Walikuwa Kwenye Gari Nyingine
Matata: Je Ulieleza Mahakama kwamba uliwaona Mashahidi huru Wakishuka Central Moshi Kuandika Maelezo
Shahidi: Hiyo Sikueleza
Matata: Nikumbushe Mkiwa pale Rau Madukani Mlimkamata nini na wewe Ulimkabidhiwa nini
Shahidi: Tulimkamata Simu, Madawa ya Kulevya, Silaha na Risasi
Matata: Wewe Ulimkabidhiwa Vitu gani
Shahidi: Silaha na Simu
Matata: Wewe Ulijaza Hati za Kukamatia Mali?
Shahidi: Alijaza Afande Jumanne
Matata: alijaza Ngapi
Shahidi: Alijaza Mbili Mbili kwa Kila Mtuhumiwa
Matata: Wewe Ulishuhudia
Shahidi: Niliona, sikushuhudia
Matata: tulianza na Hati ya Kukamatia Mali za Adamoo, Je Hati ya Kwanza Ilikuwa na Nini na Nini
Shahidi: Ya Kwanza Ilikuwa na Simu na Silaha
Matata: Ya Pili ilikuwa na Nini
Shahidi: Ya Pili ilikuwa na Madawa ya Kulevya
Matata: Twende Kwa Mshitakiwa Wa Tatu Mohammed Ling’wenya, Ya Kwanza Ilikuwa na nini
Shahidi: Ya Kwanza Ilikuwa na Simu na Ya Pili ilikuwa na Madawa ya Kulevya
Matata: Sasa Shahidi Wakati unatoa Ushahidi Wako, Ulielezea Kwanini ziliandikwa zilitofautishwa kwa sababu ipi
Shahidi: Sikueleza
Matata: Shahidi Wewe Sasa Ulitoka na Vitu gani Mpaka Ukaja navyo Dar es Salaam
Shahidi: Simu na Silaha
Matata: Na Ulipofika Dar es Salaam Uliambiwa Ukabidhi Vielelezo Pale Central Polisi
Shahidi: Ndiyo
Matata: Na pale Ulimkabidhi Vitu gani Afande Nuru
Shahidi: Silaha na Risasi
Matata: Kwa hiyo Nuru Ndiyo Mtunza Vielelezo Pale Central polisi
Shahidi: Sahihi
Matata: Ukasema Simu Ulimkabidhi Afande Swila
Shahidi: Sahihi
Matata: Ulielezea Hapa Mahakamani Kwanini Simu alipewa Swila na siyo Mtunza Vielelezo
Shahidi: Hapana Sikueleza
Matata: Mheshimiwa Jaji ni Hayo tu
Kibatala: una elimu gani?
Shahidi: Degree
Kibatala: Chuo gani?
Shahidi: Open University
Kibatala: degree gani?
Shahidi: Sociology
Kibatala: advance umesomea wapi?
Shahidi: Karatu
Kibatala: ulipata divisheni ngapi
Shahidi: Divisheni 3
Kibatala: Point ngapi?
Shahidi: 21
Kibatala: nikisema kwamba majibu yako yaendane na digrii nitakuwa nakukosea?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Msingi wa upelelezi unatakiwa uwe ProActive siyo mpaka ipate maelezo?
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Uwe umeshika silaha hujashika silaha wewe ni mpelelezi
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ukasema Mahita alikwambia Kwamba Unaitwa na RCO ukachukua Silaha
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Katika Ushahidi Wako Kuna Mahala Yoyote ulisema Kwamba Kuna Kiongozi Yoyote alikwambia Majukumu yako ya Upelelezi yapo Suspended
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Nilisikia Wakili amakueleza hapa Kuwa SMG ni Function au siyo Function
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je inategemewa Afisa wa Juu wa Polisi asema Kwamba Kuna Silaha inaitwa AK47 au SMG
Shahidi: Inategemea
Kibatala: Kwa hiyo Kinacho tofautisha Silaha ni Jina na siyo Function
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je hii Bunduki aina ya Luger ni A5340.?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ndiyo ilikamatwa kwa Adam Kasekwa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Wakati una wa Describe wale Watu Mahakamani, Kuna Mahala Kwenye Ushahidi Wako pia alijitambulisha kwenu la Adamoo
Shahidi: Hapana
Kibatala: Wala Hukusema Kwamba Adam Kasekwa pia ni Adamoo
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Pia Hukusema Kwamba Mohammed Ling’wenya ndiye DOYI
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Ulimtaja Kakobe wala Siyo Moses Lijenje
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Moses Lijenje Katika Ushahidi Wako hukumtaja
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa Ushahidi Wako wewe Mlikuwa mnatafuta Kakobe
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Bunduki aina ya Luger A5340 Je ni Moja wapo ya silaha inayotolewa kwa maafisa wa Juu
Shahidi: Sijawahi kuona zaidi ya ile
Kibatala: Je Maafisa wa Juu anapewa bastola za aina gani
Shahidi: Chinese Pistol
Kibatala: Hakuna bastola zinaitwa Chinese Pistol,
Kibatala: Brand name yake ni nini
Shahidi: Sifahamu, mie najua zinaitwa Chinese Pistol
Kibatala: Je Unafahamu kwamba Bidhaa kama Simu ya Samsung Inaweza kutengenezwa Nchi Nyingine Kama Brazil kwa Makubaliano
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Baada ya Zoezi la Kukamata Silaha, Ukaenda Kuchukua Seizure Certificate kwenye Gari
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je ni kweli ulipokwenda kwenye Gari hukuambatana nao Kwenda kwenye Gari.?
Shahidi: Sikuambatana nao
Kibatala: Na Wakati unaenda Kwenye Gari hukuambatana na Washitakiwa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: na Ulipo rudi ulipatia tena Jumanne hiyo Bunduki
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: kwa hiyo Mmebadirishana na Jumanne Mara Mbili
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa mlisaini Hati ya Kukabidhiana na Jumanne Mara ngapi
Shahidi: Mara Moja tu
Kibatala: Mlisaini Hati ya Makabidhiano Baada ya Yeye kuKupatia, Mwanzo au Baada ya Kusaini Seizure Certificate?
Shahidi: Baada ya Kusaini Seizure Certificate
Kibatala: Kwa hiyo Mwanzo alipokupa Uende kwenye gari Hukusaini Makabidhiano?
Shahidi: Ndiyo alikuwa amenipa tu
Kibatala: Je Mshitakiwa Adam Kasekwa, alipewa nafasi ya Kurekodi namba ya Ile Silaha
Shahidi: alisomewa, Hakuandika
Kibatala: Je Wala Mashahidi huru Walipata nafasi ya Kurekodi ile namba ya silaha
Shahidi: Walisomewa, Kama Kuishika Kichwani inategemea Uwezo wao
Kibatala: Katika ile Seizure Certificate Je yaliwekwa Maneno CZ 100
Shahidi: Sikushuhudia
Kibatala: Je Kama Hukushuhudia Kilicho andikwa Pale Rau Madukani kwenye Seizure Certificate, Details zilizowekwa Kwenye Seizure Certificate Pale Rau Madukani ndiyo Details hizo hizo mlizokabidhiana na Nuru
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Naomba Kielelezo Namba 36
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo mahala popote kama kuna majina Adam Kasekwa maarufu kama Adamoo, kwenye hiyo kielelezo namba 36
Shahidi: Hakuna majina
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Upekuzi Uliopelekea Kukamatwa kwa hiyo Silaha Umefanyika Kwa nani kwenye Kielelezo namba 11
Shahidi: Kwa Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo
Kibatala: Na Wewe Ukisema hujawahi Kusikia Neno Adamoo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unafahamu Kwamba Nuru uliye Mkabidhi Vielelezo ina description ya CALLIBRE 9, CZ 100
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu kwamba description ya kielelezo kinatakiwa kuwa vilevile kama Ilivyokatwa
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala Kama Nuru kaweka Maneno CZ 100 Ndiyo anajua Maneno haya ya ziada yaliyoongezwa?
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: na hapa katika seizure certificate Chini Kuna Maneno Yamesema kwamba silaha Iliyochukuliwa kutoka Adam Kasekwa kama kuna Maneno CZ 100
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Na Silaha hiyo Ndiyo inamuunganisha Adam Kasekwa na hii Kesi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nilikusikia Katika Ushahidi Wako Ulisema kuhusu Silaha AK 47
Shahidi: sahihi
Kibatala: Je hii Silaha Ina Uhusiano wa Moja kwa Moja Kuhusu Kuwalinda Washtakiwa
Shahidi: Ina Umuhimu katika Ushahidi
Kibatala: Silaha inatolewa Je Kwa Utaratibu au Kama Pipi
Shahidi: Unachukua Kwa Kuandika Pale Chumba Cha Silaha
Kibatala: Je Hapa Mahakamani Umekuja na Makaratasi ya hiyo Silaha Hapa Mahakamani
Shahidi: Kwa Leo Sijaja nayo, Yakihtajika nitakuja nayo
Kibatala: Je Baada ya Kuja Dar es Salaam Kukabidhi Silaha, Ujawahi Kukabidhi popote
Shahidi: Ndiyo unaenda nayo hadi Nyumbani
Kibatala: Ndiyo Mafunzo Mliyopewa CCP
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Wakati Watuhumiwa Wanafika DAR ilikuwa Saa Ngapi
Shahidi: Saa 12 kasoro
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba nini Kilikufanya Usikabidhi Kielelezo Saa 12 Kasorobo
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Katika Ushahidi Wako tunaona Ukienda Kunawa Uso Ukiwa na Vidhibiti
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Katika Ushahidi wako Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulimkabidhi Saa ngapi hiyo Silaha Siku ya Tarehe 07 August 2020
Shahidi Nilimwambia
Kibatala: Katika Kielelezo namba 36 Kuna Muda Unaomekana kwamba Mlikabidhiana Saa ngapi?
Shahidi: Hapana Muda hauonekani
Kibatala: Wewe huoni sasa Kwamba Kwa Kwenda Kuzurula na Silaha ambayo ni Kidhibiti, Imepelekea Nuru Kuongeza Maneno Mengine ya CZ 100?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Umwambia Jaji Kwamba Wakati wa Makabidhiano, Risasi zilitolewa Katika magazine mkahesabu
Shahidi: Hapana Sikusema
Kibatala: Kwamba Kuna Risasi Tatu Ndani ya magazine ulimwambia Wewe?
Shahidi: Hapana aliona yeye, Kwa Sababu ya Kuna Vitabu Vingine Vya kujaza,
Kibatala: Vitaje vitabu Vingine ni Vipi
Shahidi: anavijua Mtunza Kielelezo
Kibatala: Vitaje hivyo Vielelezo
Shahidi: Kuna Kitabu Kinaitwa PF 16
Kibatala: Je Ulionyeshwa kwenye Extract ya PF16 Kwamba Ndicho Kile Kilicho andikwa kwenye Seizure Certificate
Shahidi: Hapana Sikuonyeshwa
Kibatala: Wakati Upo Rau Madukani, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Afande Jumanne alitoa namba za Zile Risasi akawasomea Mashahidi huru
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: aje unafahamu kwamba Katika Uchunguzi wa Ballistic, Makabaki ya Risasi Mbili Kwenye kitako zina namba
Shahidi: Hapana Sifahamu
Kibatala: Wakati Mpo Rau Madukani ukisikia Maneno Kati ya Kingai, Jumanne au Mahita Kwamba Adam Kasekwa ana haki ya Kuita , Ndugu, Jamaa au Rafiki
Shahidi: Hapana
Kibatala: Ndiyo Maana Katika Kielelezo namba 11 sehemu ya Adamoo Kuweka Mashahidi Wake Pako wazi
Shahidi Pako wazi
Kibatala: Mnasema Wale Mashahidi walikuwa Mashahidi huru
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwamba Mmoja alikuwa Mmiliki wa ile Grocery
Shahidi: Hapana Siyo Mmiliki
Kibatala: Ulisema Kwamba Wakati Afande Kingai Alimtuma Mahita Kuangalia Kama Watuhumiwa Walikiwepo, Ulisema aliwakuta wapi Vile?
Shahidi: Kwenye Grocery
Kibatala: Na bado hapo hapo huyo Mwenye Grocery Mnasema Shahidi Huru?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: unajua maana ya shahidi huru?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je unafahamu kuwa shahidi huru hatakiwi kuwa mtu mwenye mahusiano na mtuhumiwa kwa namna yoyote?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Vipi kama Adamoo alipishana kauli na kugombana na mwenye Grocery, Je atakuwa shahidi huru huyo?
Shahidi: Hakunaaaaaaaa Bhanaaaaaaaa..
Mahakama: Kichekoo
Kibatala: Tutoke Kwenye Bunduki Twende Kwenye Simu
Kibatala: Kwanza Ulisikia kutoka kwa Kingai, Jumanne au Mahita Kuitwa kwa Viongozi Wa Serikali ya mtaa pale
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Seizure Certificate ni Nakala tatu
Shahidi: Nafahamu ni Nakala Mbili
Kibatala: Je Ulishawahi Kushuhudia Adam Kasekwa akipewa Nakala yake ya Seizure Certificate
Shahidi: Ndiyo niliona
Kibatala: Nakala Nyingine Kabaki nayo nani
Shahidi: Ikabaki Kwenye Vielelezo Kwa Afande Jumanne
Kibatala: Wale Mashahidi Hawakupewa
Shahidi: Hawakupewa
Kibatala: Wewe ulipoenda Kwenye Gari Ulimkabidhiwa ngapi
Shahidi: Nilipewa Kwenye Bahasha, Si kuweza Kufahamu
Kibatala: Aliyekabidhi wa Kituo cha Polisi zile Seizure Certificate ni nani
Shahidi: Sijui nilizikuta Kwenye Gari
Kibatala: Ulizikagua Ulipoitoa Kwenye Gari
Shahidi: Si Kukagua
Kibatala: Kwahiyo Ka zilishajazwa Hujui
Shahidi: Hazikujazwa
Kibatala: zilijazwa Seizure Certificate ngapi kuhusu Madawa ya Kulevya
Shahidi: ilijazwa Moja na Nakala yake
Kibatala: Ile copy Ilienda Wapi
Shahidi: Alipewa Mtuhumiwa
Kibatala: Mtuhumiwa alisaini wapi Kwamba kapewa Seizure Certificate
Shahidi: Hakuna anaposaini
Kibatala: Hebu tuchoree Jiographia ya Pale
Shahidi: Barabara ya Lami, Kuna Glocery alafu Kuna Uchochoro
Kibatala: Mahala mlipo waweka Watuhumiwa Palikuwa na uchochoro
Shahidi: Ndiyo palikuwa na Uchochoro
Kibatala: Gari Mliyoenda nayo ilikuwa ya Namba Gani
Shahidi: Toyota Land Cruiser
Kibatala: Ilikuwa na Vioo Vya giza au Hakuna
Shahidi: ilikuwa navyo
Kibatala Twende Kwenye Simu sasa, Unasema Ulimkabidhi Inspector Ndowo lini
Shahidi Nilikabidhi 07 August 2020
Kibatala: Ulimkabidhi nani
Shahidi: Swila
Kibatala: Kwa Hati ya Makabidhiano
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: hiyo Hati ya Makabidhiano ipo hapa Mahakamani
Shahidi: Haipo Hapa Mahakamani
Kibatala: Hati ya Makabidhiano ndiyo ingeonyesha sasa IMEI namba
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hati hiyo ya Makabidhiano ndiyo Ingekuwa na IMEI namba za Simu na IC CID
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Na wewe hapa Mahakamani hujataja IMEI namba
Shahidi: Sijataja
Kibatala: na SimCard mlizokabidhiana Haijataja ICCID namba
Shahidi: Sijataja namba
Kibatala: Wala unasema kwa Mheshimiwa Jaji Kwamba 07 August 2020 Kama Kweli Mlikabidhiana na Inspector Swila tulimtegemea tuone IMEI NAMBA na ICCID wakati wa Makabidhiano Tarehe 13 August 2020
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Na wala hujamwambia Jaji Kwamba Ulilinganisha
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: Umeleta Hati ya Makabidhiano ya Barua iliyofungua Uchunguzi pale Forensic Beaural?
Shahidi: Hapana Sijaleta
Kibatala: Baada ya Kufika Pale Forensic Beaural, Kwa Inspector Ndowo Ilikuwaje Makabidhiano
Shahidi: Tulikabidhiana kwa Hati ya Makabidhiano
Kibatala: Umeleta Hati ya Makabidhiano ya wewe na Ndowo
Shahidi: Hapana Sijaona Hapa Mahakamani
Kibatala: Inspector Ndowo anasema aliingiza Vielelezo Kwenye Kitabu Cha Register na siyo Hati ya Makabidhiano, Tusaidie Sasa mlijaza nini pale
Shahidi: Tulijaza Hati ya Makabidhiano na Kwenye Register
Kibatala: Je Register Ambayo Inspector Ndowo alijaza Kuhusu Vielelezo, Je Umeonyeshwa hapa Mahakamani
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwanini hizo Hati tatu za Makabidhiano ujazileta Mahakamani
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwanini Ujaleta Register Mahakamani
Shahidi: Sijamwambia Mheshimiwa Jaji
Kibatala: Na wala hujamwambia Jaji Kwamba mlibadilishana Namba na Inspector Ndowo
Shahidi: Hapana Sija Mwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Siku Moja Ulipiga Siku Kwamba Umepata Dharula, badala yake aMkabidhi inspector Swila
Shahidi: Hapana Sija Mwambia
Kibatala: Wala hujamwambia Kwamba ni nani aliyetoa Maelekezo Kwamba akachukue Inspector Swila
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: na wala hujamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Baada ya pale Swila Kupokea Vielelezo ulilinganisha Hati za Makabidhiano
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: Na wala hujamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba ni lini Uliacha wala Kusimamia Majukumu Yako ya Kutunza Vielelezo, na akapewa Inspector Swila
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: Shahidi nakuonyesha maelezo yako yaliyochapwa soma KWA SAUTI
Shahidi: ANASOMA
Lakini kama anashtuka Mwenyewe hivi na kuhamaki..
Shahidi: Sikumbuki Kama Niliandika hivi,
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kupata maelezo yake halisi
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ilishawahi kujitokeza na ikatolewa ruling kwenye proceedings hizi hizi
Kibatala: Mhe Jaji Tumekuwa too Much Technical, Kama hawana siyo tatizo la Mahakama wala letu
Jaji: Haipo Kwenye Possession Yao Bali ipo Upande wa Mahakama
Kibatala: nitaendelea, Wakati wa Break nitaomba wenzangu waifuate
Kibatala: Twende Kwenye simu na SimCard za Bwire
Kibatala: Nilisikia sahihi Kwamba Simu za Bwire zilichukuliwa na Kingai
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Seizure Certificate ya simu za Bwire Ulishawahi kuiona
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Simu na Simu Card Ulikabidhiwa kwa Makabidhiano
Shahidi: Hapana Nilipewa nizishike tu
Kibatala: kutoka Chang’ombe Mpaka Central Dar es Salaam ulikuwa Umezishika tu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulikuwa na Mashahidi huru Wakati wote Ukiwa Njiani kutoka Chang’ombe Mpaka Central
Shahidi: Hapana Sikuwa na Mashahidi huru
Kibatala: Ulikuwa na Bwire
Shahidi: Hapana
Kibatala: Wakati Unamkabidhi Swila, Bila Seizure Certificate alipata nafasi ya kulinganisha
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Swila Alihifadhi wapi hizo Simu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Akaja Kukukabidhi tena simu na SimCard Tarehe 13 August 2020
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: umepewa Simu 8 na Swila 13.8.2020, Kuna Simu zilizo katwa Rau Madukani Tarehe 05 August 2020, na Zile za BWIRE zilizo Kamatwa za Bwire Siku ya Tarehe 10 August 2020
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: kwa hiyo Uwezi Kujua Kama Simu na Sim Card za Simu mbili ni Zenyewe au Siyo
Shahidi: Ndiyo siwezi Kufahamu
Kibatala: Turudi tena Moshi Kidogo
Kibatala: Mlipofika Central Police Station Moshi, nyie mlibaki ndani ya Gari
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ni wakati gani Mliwauliza kuhusu Mwenzao
Shahidi: Tulipo kuwa tunakaribia Kituoni
Kibatala: ulisikia Mtu yoyote ndani ya Gari a kwamba Nawauliza Lakini Mkijibu inaweza Kuchukuliwa ni sehemu ya Maelezo yao
Shahidi: Hapana Hakuna aliyesema
Kibatala: Je, unafahamu Kwamba Mtu ana haki zake Za Kujulishwa Makosa na Kumwambia Haki ya kunyamaza wakati wa Mahojiano?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Kabla ya Mahita na Jumanne Kushuka Kwenye Gari, Mlikuwa Mmeshaaamua Kurudi Kumtafuta Kakobe au Bado hamjaamua?
Shahidi: Tulikuwa tumeshaamua
Kibatala: Kuhusu ile Bahasha Kwenye Seizure Certificate, unajua ilitoka wapi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kamati anayejua Kuhusu ile Bahasha ni Afande Jumanne
Shahidi: Sifahamu
Kibatala’ Kabla ya kuanza Safari, Mlienda Aishi Machame Hotel
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Na kule Rau Madukani aliyeshuka pale ni Kingai au Mahita
Shahidi: Ni Mahita
Kibatala: Wakati Unatoa Maelezo yako Mwanzo a Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Unatoka CID ARUSHA
Shahidi: Hapana Sikumwambia
Kibatala: Katika Kielelezo namba 36 unasema umetoka wapi
Shahidi: CID ARUSHA
Kibatala: Uliongozwa Ukatoa Kielelezo namba 36, pamoja na kwamba wakati wa Utambulisho wako wewe ni Mpelelezi, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba CID ARUSHA ni nini
Shahidi: Sikufafanua
Kibatala: Uliwahi kusikia kuwepo Kwa njama zozote Sabaya akiwa Arusha?
Shahidi: Ndiyo Tarehe 04 August 2020
Kibatala: kabla ya Tarehe 04 August 2020
Shahidi: Sijawahi kusikia
Kibatala: Ulishawahi kusikia njama za kumdhuru Sabaya ukiwa CID Ausha?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je uliwahi kusikia intelijensia kama mpelelezi njama za kufanya maandamano ya siyo na kikomo?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Ulishawahi kusikia njama za kuchoma bituo vya mafuta Arusha ukiwa kama mpelelezi?
Shahidi: Hapana, SIJAWAHI KUSIKIA
Kibatala: Na kama ungesikia unge’ report na kufanyia Kazi kwa sababu hayo ndiyo mambo ya kufanya Askari apandishwe cheo
Shahidi Hapana sijawahi kusikia
Kibatala: Ulishawahi kusikia kwamba Freeman Mbowe alikuwa anapanga njama za matendo ya kigaidi
Shahidi: Hapana… Sijawahi kusikia
Kibatala: Unafahamu kuhusu kamati za ulinzi za wilaya na mkoa?
Shahidi: ndiyo
Kibatala: Je Ulishawahi kusikia malalamiko Kutoka kamati za ulinzi za wilaya na mkoa kuhusu njama za Freeman Mbowe na matendo ya kigaidi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Unafahamu kwamba Sabaya alikuwa Ndiyo mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Hai?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je Sabaya alishawahi kuwalalamikia Kuhusu njama za kutaka kudhurika?
Shahidi: Hapana sijawahi kusikia
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naona saa saba Imefika, naomba kutoa hoja ya kuhairisha kwa muda
Wakili wa serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kukumbushia kidogo kuhusu ombi letu la maelezo ya shahidi
Jaji nahairisha mpaka Saa 7 na dakika 45
Jaji anatoka
Jaji ameingia Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: kwa Upande wa Mawakili Wa Jamhuri tupo Kama Awali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu tupo Kama Awali, Isipokuwa Wakili Seleman Matauka amepata Dharula Kidogo
Jaji anaandika Kidogo palee
Mahakama ilikuwa kimya kwa muda..
Shahidi amerejea kizimbani, amekaa kwa unyonge sana.. Sio kama Asubuhi alivyokuwa na bashasha
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Hisani ya Mahakama hii Tukufu Nikumbushwe Nilipo Ishia
Jaji: Kama alifahamu Jinsi ambavyo Sabaya angedhuriwa, akasema Hapana
…….
Kibatala: Wewe upo Arusha, Mnabadilishana Taarifa na Arusha na Mikoa Mingine ya Kipolisi
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ulishawahi Kupata Taarifa Kabla ya Tarehe 04.8.2020 ulisikia chochote kutoka kwa wapelelezi Wenzako wa Moshi Kuhusiana na Kikundi kinachopanga kufanya ugaidi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je uliwahi kufahamu wewe na wapelelezi wenzio kuhusu kikao huko Moshi ikiwa ajenda ni kupanga matendo ya Ugaidi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je uliwahi kusikia Aishi Hotel na mmiliki wake kuwekwa chini ya uangalizi na nyendo za pale sababu ya Ugaidi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: hata baada ya tarehe 04 August 2020 ulishawahi kupata taarifa kwamba kuna kazi ya kufuatilia nyendo za Hotel na watu wa pale kuhusu Hotel yao kufanya ugaidi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Baada ya Timu yenu Kuundwa, Na Baada ya Pale Kutoka Moshi hujawahi Kushughulika na Ile hotel tena?
Shahidi: Sijawahi
Kibatala: Na Hata Wenzako hujawahi Kusikia Wakishughulika na Ile Hotel tena?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Timu yenu ya watu Sita akiwemo Dereva, Kuna Taarifa Nyingine ambazo Walikuwa wanazifahamu Kingai na Jumanne tu au Mlikuwa mazifahamu wote
Shahidi: Tulikuwa tunafahamu Taarifa zote kwa Pamoja
Kibatala: na Ungeshangaa Kama Kama Kuna wengine Wangekuwa wanawaficha Taarifa??
Shahidi: Tulikuwa tunafanya Kazi wote Kwa Pomoja
Kibatala: Je task force yenu Ilishawahi Kumuweka Freeman Mbowe chini ya uangalizi wakati wote kwa tuhuma za ugaidi?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je uliwahi kufahamu kwamba kuna Polisi wengine walimuweka Freeman Mbowe chini ya Surveillance kwa niaba yenu?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je Uliwahi kusikia kwamba washtakiwa wamepanga ku’ block barabara?
Shahidi: Sijawahi kusikia
Kibatala: Je umewahi kusikia Kingai au Jumanne wakizungumzia kwamba washtakiwa walipanga ku’ block barabara fulani fulani?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Katika Mambo yote haya, Adam Kasekwa aliwahi Kuwaambia Ile Bastola Ile Luger A5340 alipata Kwa nani
Shahidi: hajawahi kutuambia
Kibatala: Je Kingai?
Shahidi: Sijasikia
Kibatala: ufahamu wala kusikia ni namna gani alipanga kutumia bastola hiyo katika kutekeleza yale wanayoshtakiwa nayo na washtakiwa wenzie?
Shahidi: Sijawahi kusikia
Kibatala: Je Unafahamu kuwa katika vitu Ulivyotaja kuwa mlikamata kwa Bwire, kama uniform za Jeshi zilikataliwa hapa mahakamani
Shahidi: Hapana sifahamu
Kibatala: Shahidi Mlikabidhiana Na Stafff Sarjent Nuru, Je Ulieleza Lolote kuhusu Saini zako wewe na Nuru
Shahidi Hapana
Kibatala: Je Kuna Saini Zako wewe na Nuru
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ipo wapi
Shahidi: H4347
Kibatala: Soma Hapo Juu
Shahidi: Jina na Sahihi ya anayekabidhi
Lakini hii Ndiyo signature ya Kijeshi
Kibatala: ulimueleza Jaji hivyo
Shahidi: sikumueleza.
Kibatala: Kielelezo namba P 37 na Yenyewe haina Saini yako
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: na yenyewe Ulimfafanulia Jaji Kuhusu hiyo Saini ya Kijeshi
Shahidi: Hapana Sikutoa Ufafanuzi
Kibatala: Katika Kielelezo hicho Kuna sehemu anayetuhumiwa Kuna Deshi na Makosa Deshi
Ukasema Majina hayapo Kwa Sababu Kuna File namba, Je unafahamu Kuwa Kesi hii Ina Washitakiwa Wanne, na wote wanashea Kesi namba Moja
Shahidi: Kama wote wanatumiwa Kwa Kosa Moja Lazima Majina yawe yote
Kibatala: hiyo Kumbukumbu namba si lazima niende Kwenye Faili
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa hilo Kesi lipo wapi Hapa Mahakamani
Shahidi: Sijaliona
Kibatala: Mlikabidhiana Bastola na Risasi Wewe na Nuru Mara Mbili
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Tarehe 25 November 2020 kabla ya Kukabidhiwa Bastola na Nuru, Kwamba Mli Cross check Kwa Pamoja Kuona Kama Risasi zinafanana, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji?
Shahidi: sikumwambia
Kibatala: Je ulimwambia mheshimiwa Jaji kwamba tarehe 25 November 2020 kwa pamoja na kulinganisha, magazine na risasi?
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: Ile Seizure Certificate Pale Rau Madukani, Unafahamu Alianza Kusaini nani akafuata nani?
Shahidi: Hapana Sifahamu
Kibatala: Rau Madukani, Mnasema Kulikuwa na Mashahidi huru, Je Kuna mtu aliye Muuliza Huyu Dada aliye toka Grocery, Je Kuna Yoyote kati yenu aliye Muuliza huyu Dada Kuhusiana na Mmoja aliyetoroka?
Shahidi: sifahamu
Kibatala: Majukumu ya Ulinzi Ulipewa wapi
Shahidi: Pale Rau Madukani
Kibatala: Ni nani aliyeambiwa na Kingai Kwamba Wewe Utakuwa Mpelelezi?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Hati ya Makabidhiano ya Bunduki Kwa Ushahidi Wako Ilijazwa Kwenye Gari
Shahidi Mie Nilisaini Kwenye Gari
Kibatala: Je unafahamu alijaza wapi
Shahidi: Kwenye Gari
Kibatala: Mlikabidhiana Kwenye Gari?
Shahidi: Tulikabidhiana Chini, Tukasaini Kwenye Gari, Shahidi aliweka Afande jumanne
Kibatala: Je aliweka Lebel Kwenye Vielelezo Vipi
Shahidi: Aliweka Kwenye Simu tu siyo Silaha
Kibatala: Hizo Lebel Zina Rangi gani
Shahidi: Sizikumbuki
Kibatala: Ulionyeshwa hizo Simu Hapa Mahakamani
Shahidi: Ndiyo nilionyeshwa na Mheshimiwa Malya
Kibatala: Malya Ni Wakili Wa Serikali
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Vielelezo (dhibiti) Vinavyokamatwa palepale Vinawekwa Label
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: wewe Ulijiridjisha Kama Vielelezo Vyote Vina Label
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je ulifafanua Kwa Mheshimiwa Jaji kwanini Jumanne hakuweka Label Kwenye Silaha
Shahidi: Hapana Sikufafanua
Kibatala: aliye wakamata Watuhumiwa na Kuwaambia wapo Chini ya Ulinzi ni nani
Shahidi: alikuwa ni Afande Mahita
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji ile Gari ya Pili ilifika Saa ngapi
Shahidi: Nilieleza
Kibatala: Ulielezea Nani alikuwa anaendesha Gari ya pili
Shahidi: Hapana Sikueleza
Kibatala: aje Uliwahi kuhudhuria kozi yoyote ya kuhusu viashiria vya ugaidi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Wapi
Shahidi: CCP Moshi
Kibatala: nitajie viashiria vitatu
Shahidi: Kuhusu Kula Njama, State of Mind
Kibatala: ambapo wewe hukuona popote
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ya Pili
Shahidi: Nimesahau
Kibatala: Ya tatu
Shahidi: Nimesahau
Kibatala: Seizure Certificate Afande Jumanne alikuwa anajaza kwenye Nini Meza au Mkono?
Shahidi: Aliweka Mguu kwenye Jiwe akawa anaandika Kwenye Diary Juu
Kibatala: Seizure Certificate Afande Jumanne alikuwa anajaza kwenye Nini Meza au Mkono?
Shahidi: Aliweka Mguu kwenye Jiwe akawa anaandika Kwenye Diary Juu
Kibatala: Je Unafahamu Afisa wa Polisi ambaye aliwakabidhisha hawa Polisi
Shahidi: Sikumbuki, Nilikuwa Nje
Kibatala: Je Ulishuhudia Sasa?
Shahidi: Niliona lakini sikushuhudia
Kibatala: Na Mbweni Je?
Shahidi: Niliona Waliingia Kituoni lakini sikushuhudia
Kibatala: Kwa Maana hiyo huwezi Kufahamu Kwamba Seizure Certificate zake aliziandika katika PPR?
Shahidi: Sikuona, Sifahamu
Kibatala: lakini Unafahamu kwamba Mshtakiwa anatakiwa Kuandika Vitu Vyake katika PPR hata Seizure Certificate
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Timu yenu Ili kuwa Ina report kwa nani?
Shahidi: Kwa Afande DCI
Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako Wewe DCI anafahamu Kwamba Mlikabidhiana Simu za Bwire Bila Hati ya Makabidhiano??
Shahidi: Sifahamu kama anafahamu Lolote
Kibatala: Katika Maelezo yako Unakumbuka Ulisema chochote Kuhusu Wewe Kupewa Majukumu ya Ulinzi pale Rau Madukani
Shahidi: Ndiyo niliandika
Kibatala: na katika Maelezo yako Unakumbuka Ulisema ulifika Saa Ngapi Dar es Salaam Central police?
Shahidi: Saa 12 Kasorobo
Kibatala: Siyo Saa 12 kamili
Shahidi: Yote ndiyo yake Yale
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sina Swali zaidiMWISHO
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji nitauliza Maswalia Machache
Wakili wa Serikali: Shahidi Nakuuliza Maswali Kwa ajili ya Ufafanuzi
Wakili wa Serikali: Kuna Swali Uliulizwa Juzi Kuhusu Watuhumiwa Kuwekwa Kwenye Dr, Ukasema Ni sahihi, Ulikuwa Una maanisha Nini
Shahidi: unapopelekwa Kwenye Charge Room, lazima Uwekwe kwenye DR
Wakili wa Serikali Uliulizwa Swali Kuhusiana na Mtunza Vielelezo Ukasema Siyo lazima kumkabidhi
Shahidi: ndiyo siyo lazima Kwa sababu unaweza Kumkata Mtuhumiwa hapa Ukazipeleka kwa Mtunza Vielelezo Baadae
Wakili wa serikali: Uliulizwa Kuhusu Raiding Kwamba lazima Uwe Umetoa Taarifa Kituo cha karibu Ukasema Ndiyo,
Shahidi: Ndiyo sisi tulienda Kufanya arrest siyo Raiding
Wakili wa Serikali: Malya alikuuliza Kwamba Ulipotea Vielelezo, Ukasema Hapana, Tufafanulie
Shahidi: Si Kupoteza Vielelezo, + ulikuwa Unamaanisha nini
Shahidi: Si Kupoteza Vielelezo
Wakili wa serikali: Mallya alikuuza Kwamba Baada ya Kuwakamata Watuhumiwa Mlienda CCP Moshi Kuwatesa, Ukasema Kweli
Shahidi: Ni Kwa Sababu Hakuna Mahala Tumesema Watuhumiwa Walienda CCP kwenye Mateso
Wakili wa serikali: Leo Sasa Mahojiano na Kibatala, Kwamba Washtakiwa Ni Walinzi Wa Mbowe, ukasema Si Kweli
Shahidi: Hatukuwa kamata Sababu ni Walinzi Wa Mbowe
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Ndugu wa Mtuhumiwa Wakati Wa Mshtakiwa anakamatwa, akasema Eneo la Ndugu Lipo wazi
Shahidi: Sababu sehemu ya Kuchukulia Mali ina Sehemu anajaza Maafisa Wawili, Lakini Hapa Yupo Mmoja na Katajwa Namba Moja tu
Wakili wa Serikali: Kwenye Swali hilo hilo Uliulizwa kuhusu Ndugu kuhusika
Shahidi: Ni Matakwa ya Mtuhumiwa Mwenyewe
Wakili wa Serikali Robert Kidando: anaendelea
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusiana Kama Mshitakiwa Khalfani Bwire, Zaidi ya Kuwekwa Mahabusu ya Chang’ombe, Ukasema Ufahamu
Shahidi: Kwa sababu Baada ya Kukamatwa Siku Ile Chang’ombe, Tuliondoka Na Kilicho Endelea ni Kazi ya Mpelelezi
Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Hati namba 36 na 37 ambapo Sehemu ya Sahihi ilisoma. Namba yako ya Kijeshi badala ya Saini
Shahidi: Askari Wa Cheo Cha Chini Harusiwi kukoroga
Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Hayo ni Mambo Mapya, Sisi tulifafanua au Lah
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kweli alisema ali fafanua
Jaji: Mimi Nilisikia alitoa Ufafanuzi
Wakili wa Serikali: Robert Kidando Je ulitoa ufafanuzi gani
Shahidi: Nilitoa Ufafanuzi Kuwa H4347 DC Goodluck Ndiyo Sahihi yangu na Jina langu
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia Hapo
Jaji: tunakushukuru Shahidi Kwa Ushahidi Wako
Wakili wa serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji huyo ndiye shahidi tuliyekuwa naye kwa leo, Hivyo tunaomba hairisho la kesi hii mpaka tarehe 26 January mheshimiwa Jaji
Kwani shahidi ambaye tulikuwa tumempa taarifa, tulimtegemea awe amefika leo ili aweze kuendelea kesho,
Ametupa taarifa mchana huu kuwa amepata dharula.. Hivyo hajaweza kusafiri leo, atasafiri kesho Kuja Dar es Salaam…
Wakili wa serikali: Katika Mazingira hayo Mheshimiwa Jaji, Ilikutoipotezea Mahakama Muda, Tunaomba Iridhie shauri hili lihairishwe mpaka tarehe 26 January 2022 badala ya kesho
Kibatala: Mheshimiwa Jaji nawakumbusha wenzetu kuwa washtakiwa wanasubiri kujua hatima yao, wafikirie kama ingekuwa ni wao au ndugu zao, wangefanya hayo wanayofanya?
Jaji: Kuhusu maombi ya hairisho hujasema kitu
Kibatala: Naiachia mahakama Mheshimiwa Jaji
Jaji anaandika
Shahidi ameshuka kutoka kizimbani sasa, na ameketi katika pahali pa-Mawakili wa Serikali, ameloana Jasho Mgongoni kweli kweli, na sehemu za makwapani pia kuna jasho la kutosha..
Jaji: Naelekeza Jamhuri Kuleta mashahidi siku ya tarehe 26 January 2022
Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza
Jaji anatoka na kuondoka