Kesi ya Mbowe: Shahidi Kaaya aongopa mahakamani kuhusu uanachama wake CCM

Wanaharakati waibua picha zake akiwa na sare ya CCM na viongozi wa CCM. Afuta akaunti yake Facebook kuficha utambulisho. Wamwambia ‘umechelewa, tayari tunazo.

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 27 Oktoba 2021.

Saa 3:42 asubuhi Jaji ameingia mahakamani. Kazi inaanza.

Kesi imetajwa. Ni namba 16 ya mwaka 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji.

WAKILI WA SERIKALI: Ikikupendeza Mheshimiwa Jaji, naitwa Robert Kidando nimeongozana na
Chris, Abdallah Chavula, Jenitreza Akitali, Ester Martin, Ignas Mwinuka, Tulimanywa Majige ….

Peter KIBATALA: Ikukupendeza Mheshimiwa Jaji, mimi naitwa Peter Kibatala, nipo pamoja na Alex Massaba, Seleman Matauka, Sisty Aloyce, Dickson Matata, Michael Mwangasa, Jonathan Mndeme, Hadija Aron, Evaresta Kisanga, Maria Mushi, Idd Msawanga, John Malya.

JAJI: Mshitakiwa namba moja, mbili, tatu na nne?

Washitakiwa wanaonuka, kila mmoja anatoa ishara kwamba yupo mahakamani.

JAJI: Upande wa Jamuhuri?

WAKILI WA SERIKALI: Shauri limekuja kwa ajili ya re-examination kwa shahidi wa kwanza. Yupop na tupo tayari kuendelea.

JAJI: Upande wa utetezi?

KIBATALA: Na sisi tupo tayari Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Umesema kwa niaba ya wenzako, siyo?

KIBATALA: Ndiyo Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Shahidi, jana ulihojiwa maswali ya dodoso na upande wa utetezi. Leo tukasema utakuja kwa ajili ya re-examination. Nakukumbusha upo chini ya kiapo bado.

WAKILI WA SERIKALI: Jana Mtobesya alikuuliza wakati gani jalada la uchunguzi lilifunguliwa na wakati gani jalada la kesi lilifunguliwa?

SHAHIDI: Jalada la uchunguzi tulikuwa tumefungua baada ya kukutana na Luteni Denis Urio katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

WAKILI WA SERIKALI: Na jalada la kesi?

SHAHIDI: Nilifungua baada ya mimi kupata taarifa kuwa vijana walipokuwa wanatafutwa na Luteni Urio kwa amri ya Mbowe ndipo tulifungua jalada.

KIBATALA: Objection. Swali lilikuwa kwamba suala la kumtafuta Moses Lijenje. Je ulimuhoji mshitakiwa wa pili?

JAJI: Wakili wa Serikali?

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa sijauliza alichofanya cross-examination yeye, nipo kwa Mtobesya.

JAJI: Uliza tena.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusu kuwa na taarifa za Moses Lijenje wakati unamhoji mshitakiwa wa pili. Je, ulijua taarifa hizo kabla au baada?

JAJI: kibatala umesikia swali?

KIBATALA: Nimesikia lakini kaniondoa mimi sasa ni eneo la Mtobesya.

SHAHIDI: Nilipata taarifa kuwa Freeman Mbowe alikuwa anatafuta kundi la wahalifu.

Wakili MTOBESYA: Hakufika huko. Tt’s something a new alisema alikuwa anatafuta vijana.

JAJI: Ndiyo na mimi nimesikia hivyo jana ulisema alikuwa anatafuta vijana siyo kundi la wahalifu.

SHAHIDI: Ndiyo nilipata taarifa kuwa Freeman Mbowe alikuwa anatafuta kundi la vijana walioachishwa kazi jeshini kwa dhumuni la kudhuru viongozi wa Serikali na pia mpango wa maandamano ya kushinikiza viongozi yasiyokuwa na kikomo na kwamba lengo la kufanya hivyo ni nchi isitawalike na ionekane imefeli kuelekea Uchaguzi Mkuu.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa hapa jana kuwa wakati mshitakiwa wa pili kama ulikuwa umempa onyo mshitakiwa wa pili kuhusiana na ukamataji. Wewe ukasema ulikuwa umeshampa haki zake. Haki zake zipi?

SHAHIDI: Haki zake ni pamoja na kumfahamisha na kosa alilokuwa anashitakiwa nalo na kwamba halazimishwi Kusema lolote ila jambo analozungumza linaweza kutumika kama ushahidi dhidi yake Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kwamba matukio ya kula njama yalifanyika kati ya Mei 10, 2020 na tarehe tano Agosti mwka 2020 lakini katika ushahidi wako ulisema kula njama huku kulifanyika tarehe 25 Julai 2020 hadi tarehe moja Agosti 2020 huko Aishi Hotel. Unasemeje juu ya ushahidi wako kupingana na hati ya mashitaka?

SHAHIDI: Naomba kuona hiyo hati ya mashitaka.

JAJI: Utetezi mapingamizi juu ya hilo?

MTOBESYA: Hapana. Hakuna pingamizi. Apewe tu.

SHAHIDI: Mie naona hakuna utofauti bado. Ipo in between bado.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusiana na maelezo ya mshitakiwa wa kwanza kwamba yaliandikwa Chang’ombe ukasema ndiyo. Ni kweli? Na maelezo mshitakiwa wa pili na watatu yalichukuliwa Central Dar es Salaam. Eleza kwanini uliamuru maelezo ya mtuhumiwa wa kwanza yachukuliwe Chang’ombe.

SHAHIDI: Kwanza Chang’ombe ni Dar es Salaam. Pili huwezi kufananisha na Moshi. Halafu nilikuwa pia naangalia masaa manne.

MTOBESYA: Objection! Mheshimiwa Jaji wamuelekeze shahidi wao vizuri. Hatutaki kila saa kusimamasimama.

JAJI: Jamuhuri?

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi eleza sababu tu kwanini uliamuru maelezo ya mshitakiwa wa kwanza yachukuliwe Chang’ombe.

SHAHIDI: Baada ya mshitakiwa kudanganya kuhusu makazi yake.

MTOBESYA: Objection Mheshimiwa Jaji. Hayo ya kudanganya ni mapya. Sheria ya ushahidi ipo wazi. Haupaswi kuongea mambo mapya.

JAJI: Nafikiri shida ipo kwenye neno kudanganywa. Hata mimi sikusikia neno “Kudanganywa”. Ondoa hilo neno uendelee.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea kwanini uliamuru maelezo ya mshitakiwa wa kwanza yachukuliwe Chang’ombe.

SHAHIDI: Kwanza ni kituo cha karibu cha Polisi lakini pia tulikuwa bado hatujajua makazi yake.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kwamba mshitakiwa wa pili uliomuonya kuhusu kula njama ya kutenda matendo ya ugaidi. Kwanini hukumuonya na makosa mengine?

KIBATALA: Objection! Hayo niliuliza mimi sikumuuliza kwanini hukumuonya kila shitaka. Nilikuwa nauliza kwa kila kosa. Kama mnataka twende hivyo tutaomba kumuhoji tena.

JAJI: Unasemaje Wakili wa Serikali?

WAKILI WA SERIKALI: Nitarudia swali Mheshimiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusiana na kuamini na kutoamini hasa kwenye sababu ya wakili.

SHAHIDI: Nilikuwa siamini kwamba Mkuu wa Wilaya anaweza kushusha bendera lakini pia ndiyo iwe sababu ya kumdhuru kiongozi wa Serikali. Lakini _statement_niliamini sababu alitoa yeye.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kupatiwa kielelezo P1.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi chukua karatasi hii (anampatia). Nitakuuliza maeneo ambayo ulihojiwa na mawakili wa utetezi.

WAKILI WA SERIKALI: Tafuta eneo ulikohojiwa kuhusiana na kumfikisha mheshimiwa Mikocheni. Ukipata nitakuuliza swali.

Shahidi anatafuta wakati mahakama iko kimya kumsubiri.

Shahidi hajaona anachokitafuta hadi wakili wa Serikali anaingilia na kumuuliza:

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kufika Dar es Salaam na kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni, hujaona?

JAJI: Labda uchukue kwanza wewe usome halafu umuonyeshe.

WAKILI WA SERIKALI: Kama hawatokuwa na pingamizi.

KIBATALA: Hatuna [pingamizi] Mheshimiwa Jaji.

WAKILI WA SERIKALI: Soma hapa.

SHAHIDI: Baada ya kufika Dar es Salaam na kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni mimi na Mohammed tulipewa laki mbili mbili baada ya kesho yake kuwa annakuja Lissu na kumpokea.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuwa huyo mheshimiwa ni nani ukasema. Sasa ieleze Mahakama huyo mheshimiwa ni nani.

MTOBESYA: Objection! Mheshimiwa Jaji. Kifungu cha 61 cha Sheria ya Ushahidi kinasema nyaraka isitafsiriwe bali nyaraka ijieleze yenyewe. Hapo shahidi anaulizwa tafsiri.

WAKILI WA SERIKALI: Naona hiyo objection haina mashiko kwa sababu tutakuwa hatuna cha kufanya.

JAJI: Nafikiri Mtobesya hoja yako inahusu thamani ya nyaraka. Sasa Mahakama itaangalia hicho anachokisema kipo kwenye nyaraka?

MTOBESYA: Sawa Mheshimiwa Jaji.

SHAHIDI: Ni Mheshimiwa Mbowe. Kwa sababu mheshimiwa aliyetajwa kwenye statement hii ni Mheshimiwa Mbowe na Mbowe mwenyewe anaishi Mikocheni.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia kuhusiana na kupewa laki mbili mimi na Mohammed. Huyu Mohamed ni nani?

SHAHIDI: Ni Ling’wenya kwa sababu huko juu tulikuwa tunazungumzia Mohamed Ling’wenya na statement hii alikuwa anatoa mwenyewe.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kama kwenye statement hiyo kama alivyoelezea yeye kama mshitakiwa wa pili kama alimfuatilia Sabaya katika maeneo aliyokuwa akienda Arusha. Uliulizwa swali wewe ukasema HAPANA. Sasa nitakupeleka kwenye statement halafu utafafanua.

MTOBESYA: Objection! Samahani Mheshimiwa Jaji. Labda kwa maelekezo yako nitakubali maelekezo ya Mahakama. Anachoulizwa shahidi alishajibu kuwa hakuwa Arusha. Anaulizwaje jambo hilo hilo tena?

JAJI: Nafikiri ngoja tusubiri swali lake.

KIBATALA: Jaji naomba umuangalie shahidi vizuri. Kuna zoezi linaendelea pale na dawati la jirani. Tuna- suspect anapewa information na watu wa pembeni yake.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa utaratibu wa Mahakama Kibatala anapaswa aongee kwa ushahidi kama kuna kitu kweli umekiona kitolee ushahidi, siyo kuja na neno una- suspect. Nani kafanya na kitu gani kimefanywa?

JAJI: Kibatala ulikusudia nimuonye, na tunachukulia una taarifa za kiintelijensia kwamba tumuonye shahidi kwa intelijensia yako?

KIBATALA: Mimi nimesema Mahakama imuangalie.

JAJI: Basi kwa sababu mimi sijaona naomba upande wa Jamhuri waendelee kuuliza maswali.

SHAHIDI: Katika kufuatilia nyendo za Sabaya tulienda Club Kokoriko lakini hatukumpata Mheshimiwa Sabaya siku hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Eleza sasa kwenye statement hii kama mshitakiwa alifika Club Kokoriko.

SHAHIDI: Alifika.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia swali kuhusiana na kama kuna sehemu yoyote kama mshitakiwa wa pili amechukuliwa finger prints katika statement hii. Ni kwanini katika statement hii hakuna maelezo ya kuchukuliwa finger print?

SHAHIDI: Mimi kama mchunguzi nilishaona hakuna haja ya kuchukua finger prints.

SHAHIDI: Haihitaji la kuchukua finger prints. Ilikuwa ni baada ya kumpekua mshtakiwa namba moja na baada kukuta kijitabu ikabidi sasa kuchukua finger prints. Wakati nachukua maelezo mshitakiwa wa pili ilikuwa tarehe saba Agosti mwaka 2020 kabla ya kupata kijitabu hicho.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kama ulichukua sampuli za finger prints za pistol inavyodaiwa kukutwa na mshitakiwa wa pili. Sasa wewe kama mchunguzi ni kwanini hukuchukua finger prints na sampuli za DNA?

SHAHIDI: Mimi sikuona haja ya kuchukua finger prints kwa sababu mshitakiwa tulikuwa naye. Tunafanya finger prints kama mshitakiwa amevunja na hayupo. Sisi hatukua na hitaji hilo kama alivyouliza wakili.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuwa kwa kipindi chote baada ya kupata nia ya uhalifu, kama ulimtaarifu kiongozi aliyelengwa Ole Sabaya kama ulimpatia, ukasema hukumpatia na wala Kamati ya Ulinzi ya mkoa wa Kilimanjaro. Ni kwanini sasa?

SHAHIDI: Tulikuwa na uhakika wa taarifa zetu. Hatukuwa na sababu za kuwaambia watu wengine kwa kuwa tunge- create pressure.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa wakati mtuhumiwa wa kwanza anakamatwa palikuwa na askari jeshi na ukasema hakukuwa na askari jeshi.

SHAHIDI: Hapakuwa na askari jeshi kwa sababu mimi ndiyo nilikuwa Arresting Officer na nikisaidiwa na Inspector Mahita pamoja na ASP Mahita.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusiana na maandamano ukasema ni sheria inaruhusu lakini kwa kufuata taratibu. Eleza una maana gani?

SHAHIDI: Ni kweli Sheria inaruhusu maandamano lakini kuna sheria zingine pia zinaweka taratibu kuwa kabla ya Kufanya maandamano awe amepata kibali.

WAKILI WA SERIKALI: Kibali gani?

SHAHIDI: Cha Polisi.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusiana na Sheria ya Ushahidi wakati wa onyo kuwa section one na two hukuweka, ukasema hiyo ni curable. Ulikuwa unamaanisha nini?

SHAHIDI: Haiwezi kuathiri maelezo ya kuonywa.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusiana na mtu wa pili katika maelezo yake kuwa mtu mmoja anaitwa Kakobe. Ukasema ukabaini kuwa mtu anaitwa Kakobe ndiyo Moses Lijenje. Eleza ni wakati gani ulibaini?

SHAHIDI: Wakati tunawakamata watuhumiwa walikuwa wawili lakini tulikuwa tuna taarifa wapo watatu. Tuliwauliza yupo wapi mwenzenu? Wakasema anaitwa Kakobe ambaye ndiyo Lijenje.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tunaomba tukomee hapa.

JAJI: Kama tumekukwaza, kwa niaba ya Mahakama naomba radhi. Naomba radhi kwa niaba ya utetezi na ninakushukuru kwa ushahidi wako.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tuna shahidi mwingine lakini kabla ya kuendelea naye tunaomba ahirisho fupi. Ikiwezekana tuweze ku- resume saa tano na nusu.

JAJI: Upande wa Utetezi?

KIBATALA: Mheshimiwa tumekubaliana kuwa hatuna pingamizi lolote.

JAJI: Maombi yanakubaliwa. Tutarudi mahakamani saa tano na nusu.

Jaji ananyanyuka kutoka kwenye kiti chake na anaondoka mahakamani.

Saa 5:39 Mahakama imerejea.

Wakili wa Serikali Kidando anasema wako tayari kuendelea na mashahidi.

JAJI: Upande wa utetezi mpo tayari?

KIBATALA: Tupo tayari kwa ruhusa yako mheshimiwa.

JAJI: Shahidi wa pili?

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi amefuatwa.

Mahakama imetulia kimya ikimsubiri shahidi aingie mahakamani na kupanda kizimbani.

Shahidi ameshaingia mahakamani.

JAJI: Shaihdi, majina yako?

SHAHIDI: Justine Eliya. Umri miaka 31, kabila ni Mmeru.

SHAHIDI: Dini ni Mkristo. Shughuli ni mkulima. Naapa mbele ya Mahakama hii kuwa ushahidi nitakaotoa utakuwa ni kweli, na kweli tupu. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.

WAKILI WA SERIKALI: Ataongozwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula.

JAJI: Karibu.

WAKILI WA SERIKALI: Nitakuwa nakuhoji maswali utakuwa unajibu kwa kuelekea kwa Mheshimiwa Jaji

WAKILI WA SERIKALI: Majina yako yapi?

SHAHIDI: Justine Eliya Kaaya.

WAKILI WA SERIKALI: Bwana Kaaya kwa sasa shughuli zako ni zipi?

SHAHIDI: Kilimo na biashara.

WAKILI WA SERIKALI: Kilimo cha aina gani?

SHAHIDI: Cha mboga mboga na nafaka.

WAKILI WA SERIKALI: Unamaanisha nini?

SHAHIDI: Mboga mboga, nyanya, vitunguu, karoti. Nafaka namaanisha mahindi na maharage.

WAKILI WA SERIKALI: Shughuli hizi unazifanyia wapi?

SHAHIDI: Arumeru mkoani Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Wateja wako hasa wanunuzi wa haya mazao ni akina nani?

SHAHIDI: Ni watu tofauti Watanzania na wageni wanaokuja mkoa wa Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Unazifanyia wapi?

SHAHIDI: Mkoani Arusha, Wilaya ya Arumeru, Longido na Wilaya ya Arusha Mjini.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama mwaka 2017 wewe maskani yako yalikuwa ni wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa naishi Longido.

WAKILI WA SERIKALI: Wilaya ya Longido ipo mkoa gani?

SHAHIDI: Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Hapo wilaya ya Longido ulikuwa unajishughulisha na shughuli zipi?

SHAHIDI: Kupiga picha na kilimo katika wilaya ya Arumeru.

WAKILI WA SERIKALI: Mwaka 2017 ulikuwa unajishughulisha na kilimo cha aina gani?

SHAHIDI: Nilikuwa nalima karoti.

WAKILI WA SERIKALI: Wateja wako walikuwa ni akina nani?

SHAHIDI: Waliotoka sokoni na baadhi ya watu wa pale Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Tueleze sasa hivi shughuli ya kupiga picha nayo. Ni shughuli gani?

SHAHIDI: Picha za mnato kwa kutumia camera na simu.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa ukiwapiga akina nani?

SHAHIDI: Viongozi wa Serikali na viongozi wa kisiasa.

WAKILI WA SERIKALI: Unaweza ukatuambia ni akina nani hasa?

SHAHIDI: Dk Steven Kemomo Kiruswa mbunge wa Longido.

WAKILI WA SERIKALI: Mwingine?

SHAHIDI: Mrisho Mashaka Gambo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Gabriel Daqaro aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini na wengine wengi.

WAKILI WA SERIKALI: Hao umewataja wa kiserikali. Je, wa kisiasa?

SHAHIDI: Lengai Ole Sabaya.

WAKILI WA SERIKALI: Huyu Lengai Ole Sabaya ulikutana naye wapi kwa mara ya kwanza?

SHAHIDI: Mwaka 2017 uchaguzi mdogo wa marudio Jimbo la Longido.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilijiri wakati huo baina yako wewe na yeye?

SHAHIDI: Alikuwa diwani wa Kata ya Kisambasha, Wilaya ya Arumeru. Alivutiwa na upigaji wangu wa picha. Akanitaka nikamsaidie kupiga picha katika shughuli zake zingine mbalimbali.

WAKILI WA SERIKALI: Alikutaka ukamsaidie wapi?

SHAHIDI: Katika kata yake ya Kisambasha, Wilayani Arumeru.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipokea vipi ombi hilo?

SHAHIDI: Nilimkubalia kwa kuwa ilikuwa ni fursa kwangu.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama baada kukubali lile ombi utaratibu wa ufanyaji kazi wenu ulikuwaje.

SHAHIDI: Longido ni mbali. Hivyo ilinipasa nikahama Longido na kuhamia Arusha nyumbani kwa Lengai Ole Sabaya sehemu inaitwa Kibanda Maziwa, Sakina.

WAKILI WA SERIKALI: Kwenye hiyo nyumba ya Ole Sabaya ulikuwa ukiishi na nani?

SHAHIDI: Yeye mwenyewe Sabaya na mke wake Jesca.

WAKILI WA SERIKALI: Ulifanya kazi na Ole Sabaya na kuishi kwenye nyumba yake kwa muda gani?

SHAHIDI: Mimi mwaka 2017 mpaka mwaka 2018 Julai alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulienda kuishi wapi baada ya kuteuliwa?

SHAHIDI: Nilikwenda kuishi naye Hai mkoani Kilimanjaro katika makazi ya Mkuu wa Wilaya.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipokuwa ukiishi naye wewe hasa ulikuwa ukifanya shughuli zipi?

SHAHIDI: Kufanya shughuli zake ndogo ndogo ikiwemo kumpelekea nguo zake dry cleaner. Ikiwemo kumpelekea chai na chakula ofisini kila siku.

WAKILI WA SERIKALI: Katika hiyo nyumba ya Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya, ulikuwa ukiishi na nani?

SHAHIDI: Nilikuwa nikiishi naye yeye mwenyewe na mke wake.

WAKILI WA SERIKALI: Umeishi pale kwa muda gani?

SHAHIDI: Kutoka Julai 2018 mpaka mwezi wa kumi mwaka 2018.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea?

SHAHIDI: Niliamua kurudi Longido kuendelea na shughuli zangu nyingine sababu niliacha mchumba na kutaka Kusimamia shughuli zangu zingine za kilimo.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama sasa mwaka 2018 uliporudi Longido unaweza kukumbuka watu gani katika medani za kisiasa? Ulianza kufanya nao mawasiliano?

KIBATALA: Objection! Quite leading kwa kutaka kuuliza ni watu gani wa kisiasa ulifanya mawasiliano nao.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi hebu tuambie ulifanya mawasiliano na watu gani?

SHAHIDI: Siku moja nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwenye simu yangu Airtel 0693-006 700 kutoka kwenye namba ya Airtel 0784-779 944 na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Freeman Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Akakawambia kitu gani?

SHAHIDI: Nilishtuka sana akaniuliza hujambo? Nikamwambia sijambo. Akasema ana shida ya kuniona.

WAKILI WA SERIKALI: Ukafanyeje?

SHAHIDI: Nikamuuliza uko wapi? Akajibu yupo Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Ukajibu kitu gani?

SHAHIDI: Nikamwambia nipo Longido kwa sasa siwezi kuja kwa sababu ya changamoto ya usafiri.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kikatokea?

SHAHIDI: Akaniambia chukua gari Noah gaharama nitakuja kulipa ukifika Arusha. Kwa sababu ya ile hofu nikamwambia siwezi kuja.

WAKILI WA SERIKALI: Hofu ya nini?

SHAHIDI: Kwanza ni kiongozi mkubwa lakini pia sina ukaribu naye.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumweleza hayo nini kilitokea?

SHAHIDI: Aliniambia subiri nakupigia. Akakata simu.

SHAHIDI: Baada ya muda akaniambia nipo njiani nakufuata Longido.

WAKILI WA SERIKALI: Muitikio wako ulikuwaje?

SHAHIDI: Kwa kuwa alisema yupo njiani anakuja nikasema wacha nisubiri nisingeweza kumzuia.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama nini kilitokea.

SHAHIDI: Baada ya dakika 40 alinipigia simu kuwa njoo hapa uwanja wa mpira.

WAKILI WA SERIKALI: Uwanja wa mpira wa wapi?

SHAHIDI: Ndani ya mji mdogo wa Longido.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumweleza hayo ulichukua hatua zipi?

SHAHIDI: Nilichukua bodaboda na kwenda.

WAKILI WA SERIKALI: Tuambie yaliyojiri.

SHAHIDI: Alikuja akanichukua bodaboda nikaenda mpaka uwanja wa mpira na kukuta gari inaunguruma.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwa ni majira ya muda gani?

SHAHIDI: Saa tatu usiku.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukuta gari?

SHAHIDI: Akaniambia sogea hapa kwenye gari kwa namba ile ile ya 0784-779 944.

SHAHIDI: Akaniambia ingia kwenye gari chief. Acha kuogopa.

WAKILI WA SERIKALI: Huko kwenye gari kuna watu wangapi?

SHAHIDI: Nilimkuta yeye na dereva na nyuma ya upande wa dereva palikuwa na mwanamke.

WAKILI WA SERIKALI: Alikuambia dhumuni lake lilikuwa na ujumbe gani?

SHAHIDI: Akaniambia kuwa Lengai anamsumbua sana.

WAKILI WA SERIKALI: Lengai ni nani?

SHAHIDI: Mkuu wa Wilaya ya Hai.

WAKILI WA SERIKALI: Endelea.

SHAHIDI: Akataka nimpatie taarifa na shughuli anazofanya pamoja na watu anaofanya nao kazi pale Hai.

SHAHIDI: Nikamwambia haitawezekana kwa sababu mimi sipo tena kwa Sabaya.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipomueleza haya yeye alifanya nini?

SHAHIDI: Akaniambia yeye ni kiongozi mkuu wa chama cha upinzani kwenye nchi hii. Hivyo atafanya vyovyote vile anavyoweza ili nirudi kwa Sabaya kuendelea na kazi.

WAKILI WA SERIKALI: Muitikio wako ulikuwa ni upi?

SHAHIDI: Nikamwambia haitawezekana kwa sababu nimechagua kufanya shughuli zangu binafsi.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea?

SHAHIDI: Akaniambia samahani kwa usumbufu wa kunisumbua na akanipa shilingi laki tatu (300,000).

WAKILI WA SERIKALI: Nini kikaendelea?

SHAHIDI: Akaniambia ni za usumbufu. Tutawasiliana.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea?

SHAHIDI: Tuliagana na aliondoka.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya yeye kuondoka wewe ulielekea wapi?

SHAHIDI: Baada ya kushuka kwenye gari nilimpigia Ole Sabaya simu lakini hakupokea simu.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulienda wapi sasa?

SHAHIDI: Nilibakia palepale kwenye uwanja na kumpigia Dk Steven Kiruswa na kumweleza kilichotokea.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe sasa ulienda wapi?

SHAHIDI: Nilirudi nyumbani kwangu.

WAKILI WA SERIKALI: Ulirudi vipi nyumbani kwako?

SHAHIDI: Niliita bodaboda nikarudi nyumbani kwangu.

WAKILI WA SERIKALI: Ni wakati gani tena ulikuja kuwasiliana na mtu uliyemtaja kuwa ni Freeman Mbowe pale uwanjani?

SHAHIDI: Mwaka 2020 mwanzoni alinipigia simu kupitia WhatsApp.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa namba ipi?

SHAHIDI: Kwa namba ileile ya 0784-779 944.

WAKILI WA SERIKALI: Alikuwa na ujumbe gani?

SHAHIDI: Akasema tumepotezana sana chief.

WAKILI WA SERIKALI: Alikupa ujumbe gani?

SHAHIDI: Akasema anataka tuonane.

WAKILI WA SERIKALI: Wapi?

SHAHIDI: Moshi. Wakati huo nilikuwa Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ukasemaje?

SHAHIDI: Ngoja nimalizie kumwagilizia shambani huku nikishamaliza nitakuja.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea kutokana na ahadi yenu?

SHAHIDI: Baada ya kumalizia shughuli zangu nilipanda Coaster na kumpigia simu kwamba naenda.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipanda Coaster kuelekea wapi?

SHAHIDI: Moshi Kilimanjaro.

WAKILI WA SERIKALI: Iambie Mahakama ulifika hadi wapi?

SHAHIDI: Baada ya kumpa taarifa kuwa nipo kwenye gari akasema nishuke Machame Road.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa namba ipi?

SHAHIDI: Ileile ya 0784-779 944.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipomueleza akakupa maelekezo yapi?

SHAHIDI: Akaniambia nishuke Machame Road.

WAKILI WA SERIKALI: Ipo wapi?

SHAHIDI: Ipo Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

WAKILI WA SERIKALI: Tueleze sasa baada ya kupewa maelekezo hayo nini kilitokea?

SHAHIDI: Nilishuka kwenye gari nikapiga tena simu.

WAKILI WA SERIKALI: Simu ipi?

SHAHIDI: Namba yake ile ile ya 0784-779 944.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipompigia simu nini kilitokea?

SHAHIDI: Akaniambia nisubiri hapo nakuja.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilijiri?

SHAHIDI: Baada ya muda akinipigia simu kuniambia umefika umekaa upande upi? Akaniambia vuka, kaa upande wa kulia.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulikutana na nini?

SHAHIDI: Palikuwa na barabara ya kwenda Machame na nyingine kwenye Arusha na nyingine Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kikatokea?

SHAHIDI: Ilikuja gari aina ya Land Cruiser V8 yenye mlingoni na bendera ya bunge ikiwa na plate namba zilizoandikwa KUB.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea?

SHAHIDI: Ilisimama upande wangu. Ikashusha kioo upande wa abiria. Nikamwona Mwenyekiti akaniambia panda.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuambiwa upande nini kilitokea?

SHAHIDI: Alishuka mtu kutoka siti ya nyuma akaniambia “pita”. Nikaingia kwenye gari.

WAKILI WA SERIKALI: Eheee!

SHAHIDI: Ile gari ilienda mwelekeo wa kwenda Machame. Baadae tukaingia sehemu ambayo nilikuja kugundua ni Hotel ya Aishi.

WAKILI WA SERIKALI: Palikuwa na watu gani kwenye gari?

SHAHIDI: Palikuwa na dereva na huyo mlinzi wake aliyenipisha nikaingia kwenye gari.

WAKILI WA SERIKALI: Mahusiano yenu na dereva na huyo mlinzi kabla ya siku hiyo yalikuwaje?

SHAHIDI: Tulikuwa hatufahamiani.

WAKILI WA SERIKALI: Ulijuaje aliyekupisha kuwa ni mlinzi wake?

SHAHIDI: Baada ya yeye kunitambulisha kuwa ni mlinzi lakini pia ni diwani wa Kata ya Kibororoni.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya dakika nane mlifika wapi vile?

SHAHIDI: Hotel ya Aishi Machame.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulitambuaje?

SHAHIDI: Sababu ya kibao kilichoandikwa Aishi Hotel.

WAKILI WA SERIKALI: Tueleze sasa yaliyotokea?

SHAHIDI: Baada ya kushuka a kwenye gari mimi, yeye na yule mlinzi wake.

WAKILI WA SERIKALI: Mlivyoshuka nini kiliendelea?

SHAHIDI: Tulielekea upande wa mgawaha.

WAKILI WA SERIKALI: Umekuwa ukielezea yeye na mlinzi wake. Mlinzi wake nani? Yeye nani?

SHAHIDI: Freeman Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kushuka kwenye mgahawa akasema tuongee kidogo sababu ana mikutano kwenye jimbo lake. Akaniambia niagize chakula.

WAKILI WA SERIKALI: Muda huo? Ilikuwa saa ngapi?

SHAHIDI: Saa saba mchana.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati anakutaka mkutane Moshi ilikuwa ni saa ngapi?

SHAHIDI: Saa Mbili asubuhi.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe safari yako kuelekea Moshi ulianza saa ngapi?

SHAHIDI: Saa tano kasoro.

WAKILI WA SERIKALI: Ulianzia wapi hiyo saa tano kasoro.

SHAHIDI: Sehemu inaitwa Kilala wilaya ya Arumeru.

WAKILI WA SERIKALI: Alikwambia nini sasa?

SHAHIDI: Akauliza mna mpango gani juu ya mikutano inayoendelea jimboni.

WAKILI WA SERIKALI: Jambo gani lingine alikuambia?

SHAHIDI: Akaomba nimtajie wale wasaidizi wa Sabaya aliokuwa anatembea nao.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulimwambia nini?

SHAHIDI: Nilimwambia sina taarifa yoyote ya kumwambia kwa wakati ule.

WAKILI WA SERIKALI: Nataka kuhusu hayo majina.

SHAHIDI: Nikimtajia majina na yule diwani akawa anaandika kwenye kikaratasi.

  1. Japhet Rwendela
  2. Vedastus sibula
  3. Mtoto wa Mkulima
  4. Sylvester Nyegu
  5. Binti wa kichaga
  6. Mwalimu Doreen
  7. Watson Malimumgu

JAJI: Mtoto wa Mkulima na Binti wa Kichaga ni majina?

SHAHIDI: Ndiyo. Majina nilivyokuwa nayafahamu wanayatumia kwenye mitandao.

WAKILI WA SERIKALI: Kipi kingine alikueleza?

SHAHIDI: Nilitoa hizo namba kwenye simu niliwatajia wakaziandika.

WAKILI WA SERIKALI: Lipi lingine alikueleza?

SHAHIDI: Akasema atashughulika nao. Tutawasiliana wewe na mimi baadaye.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea baina yako wewe na yeye?

SHAHIDI: Akaniaga akasema atanitumia chochote jioni.

WAKILI WA SERIKALI: Ukisema chochote umaanisha nini?

SHAHIDI: Gharama zangu za nauli.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwaje baada ya hiyo ahadi?

SHAHIDI: Hakutimiza hiyo ahadi na pia hakunitafuta baada ya pale.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya makutano yenu pale Aishi Hotel wewe ukielekea wapi?

SHAHIDI: Nilirudi Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Ni wakati gani mwingine uliwasiliana na Mbowe?

SHAHIDI: Mwezi saba mwaka 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Tarehe ngapi?

SHAHIDI: Sikumbuki tarehe.

WAKILI WA SERIKALI: Alikutafuta kwa namna gani?

SHAHIDI: Alinipigia kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa namba ipi?

SHAHIDI: 0784-779 944.

WAKILI WA SERIKALI: Ujumbe wake ulikuwa nini?

SHAHIDI: Nipo Dar es Salaam nakuja Moshi. Naomba tuonane. Nina jambo la kuzungumza na wewe.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati huo wewe ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Shambani kwangu Maji ya Chai.

WAKILI WA SERIKALI: Majira ya saa ngapi?

SHAHIDI: Mchana wa saa nane.

WAKILI WA SERIKALI: Ulichukua hatua zipi baada ya ujumbe huo?

SHAHIDI: Nilifanya shughuli zangu nikaanza safari ya kwenda Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Na ulienda Moshi kwa aina gani ya usafiri?

SHAHIDI: Nilipanda basi la Kilimanjaro kutokea Singida.

WAKILI WA SERIKALI: Ahadi ilikuwa mkutane majira gani?

SHAHIDI: Alisema saa moja atakuwa amefika Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kupanda basi la Kilimanjaro ulifikia wapi?

SHAHIDI: Moshi stendi.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unashuka ilikuwa majira gani?

SHAHIDI: Saa moja usiku.

WAKILI WA SERIKALI: Ikawaje?

SHAHIDI: Nilimpigia simu Freeman Mbowe kuwa nimefika.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa namba gani?

SHAHIDI: 0784-779 944.

WAKILI WA SERIKALI: Akasemaje?
[13:02, 10/27/2021] William Shao: SHAHIDI: Nichukie pikipiki nimfuate Keys Hotel.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya maelekezo hayo nini kilitokea?

SHAHIDI: Niliita bodaboda nikaenda hadi Keys Hotel na baada ya kufika Keys Hotel nikampigia Freeman Mbowe kwamba nimefika.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa namba ipi?

SHAHIDI: 0784-779 944. Nikamwambia nimefika. Akasema namtuma msaidizi wangu anifuate.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hapo nini kilitokea?

SHAHIDI: Alikuja dereva wake ambaye namtambua kwa Jina moja la Willy.

WAKILI WA SERIKALI: Nini hasa kilikufanya umtambue?

SHAHIDI: Siku nakutana naye kwa mara ya kwanza Machame ndiye aliyekuwa anamwendesha na alinitambulisha.

WAKILI WA SERIKALI: Kule nyuma ya Hotel ulipoenda nyuma ya swimming ulikutana na jambo gani?

SHAHIDI: Waliambia mheshimiwa yupo kwenye kikao. Tukae hapa tukiwa tunasubiria amalizie kikao.

WAKILI WA SERIKALI: Ukiacha wewe na dereva nani mwingine mlikaa naye?

SHAHIDI: Tulikaa na mlinzi wake alikuwa baunsa baunsa kidogo.

WAKILI WA SERIKALI: Ulifahamu vipi huyo _baunsa baunsa_ni mlinzi wake?

SHAHIDI: Willy aliniambia huyo ni mlinzi wa mheshimiwa usiwe na wasiwasi.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea hapo mlipokuwa mmekaa?

SHAHIDI: Tulikula. Baada ya kula mlinzi wake akaenda kule alipokuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, na baada ya muda alirudi na kusema tunaondoka.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe shahidi ulijuaje kuwa kule alipo mwenyekiti ndipo alikuwa mwenyekiti?

SHAHIDI: Ilikuwa ni sehemu ya wazi tulikuwa tumetenganishwa na swimming pool.

WAKILI WA SERIKALI: Tueleze wakati hayo yanatokea ilikuwa ni majira ya saa ngapi?

SHAHIDI: Saa tatu kasoro usiku.

WAKILI WA SERIKALI: Aliporudi na kuwaambia sasa mnaomdoka nini kilitokea?

SHAHIDI: Tulinyanyuka wote na kuelekea kule alipo Freeman Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Mlipoelekea huko alipokuwapo mwenyekiti nini kilitokea?

SHAHIDI: Akatuambia pole sana kwa kutuweka.

SHAHIDI: Baada ya muda mlinzi wake akatufungulia mlango wa gari. Naye mwenyekiti akaingia kwenye gari. Na nyuma ya dereva akaingia aliyekuwa mlinzi wa Chadema Joyce Mukya. Mimi nikakaa katikati na nyuma akakaa mlinzi wake.

WAKILI WA SERIKALI: Mlielekea wapi?

SHAHIDI: Tukitoka Keys Hotel tukaelekea mwelekeo wa Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Iliwafikisha wapi?

SHAHIDI: Aishi Hotel.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulijuaje kuwa mmefika Aishi Hotel?

SHAHIDI: Nilishafika pale. Haikuwa mara ya kwanza.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea?

SHAHIDI: Aliwaambia watangulie ndani sisi tuna kikao kifupi.

WAKILI WA SERIKALI: Kikao kifupi mlifanya nani na nani?

SHAHIDI: Freeman Mbowe, mlinzi wake. Na dereva alipotaka kujumuika akamwambia hiki kikao ni cha watu watatu.

WAKILI WA SERIKALI: Hebu tuambie sasa mahusiano yako na huyu mtu unayesema ni mlinzi kabla yalikuwaje?

SHAHIDI: Nilikuwa sifahamiani naye.

WAKILI WA SERIKALI: Kwenye hicho kikao mliongea masuala gani?

SHAHIDI: Alinitambulisha kwanza kuwa huyu ni mlinzi wake anaitwa Khalfani Bwire na msiri wake na hivyo niwe huru kuzungumza naye.

WAKILI WA SERIKALI: Yeye mlinzi alikuwa wapi?

SHAHIDI: Tulikuwa tumekaa naye upande wa kushoto.

WAKILI WA SERIKALI: Kikao chenu mlizungumza mambo gani?

SHAHIDI: Alikuwa ananiambia nitaje tena majina ya wale a vijana na namba zao za simu na kazi wanazozifanya kwa Sabaya.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe baada ya kukutaka ufanye hivyo ulichukua hatua gani?

SHAHIDI: Kabla ya kuanza kuwataja nilimtaka mlinzi wake akachukue kalamu na karatasi ili tuweze kuandika.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hayo maelekezo ikawaje?

SHAHIDI: Alirudi na kalamu na karatasi nikaanza kuandika.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe majina na namba za simu za hao watu wewe ulizitoa wapi?
[
SHAHIDI: Nilikuwa nawafahamu tangu nafanya kazi kwa Sabaya.

WAKILI WA SERIKALI: Hizo namba za simu ulizitoa wapi wewe?

SHAHIDI: Nilizito kwenye simu.

WAKILI WA SERIKALI: Majina ya akina nani?

SHAHIDI: Japhet Rwendela, Vedastus Sibula, Mtoto wa Mkulima, Sylvester Nyegu, Binti wa Kichaga, Mwalimu Doreen, Watson Malimumgu, Enock Kirigiti.

SHAHIDI: Baada ya pale aliniambia nimtajie sehemu anazopenda kutembele Mheshimiwa Sabaya.

WAKILI WA SERIKALI: Ulimtajia sehemu gani?

SHAHIDI: Cocoriko Annex iliyopo Arusha, Cocoriko ya Kijenge, The Don iko karibu na Tanzania Breweries. Nikamtajia Milestone Park iliyopo Sakina. Na hotel anazolala Sabaya ikiwemo SG Resort iliyopo Sakina Arusha, Golden Crest Hotel ipo Arusha pia.

WAKILI WA SERIKALI: Iieleze mahakama baada ya kuwa wewe umetoa taarifa hizi ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilimuuliza mwenyekiti haya majina na hizi sehemu unataka za nini? Akaniambia hilo niache mimi. Kazi yako hapa imeisha.

WAKILI WA SERIKALI: Lingine nini lilijotokeza baada ya mazungumzo yake?

SHAHIDI: Akaniambia nimkabidhi Khalfani Bwire yale majina. Khalfani Bwire akasema huyu Sabaya ni mtu mdogo sana. Nitamchezesha.

SHAHIDI: Baada ya pale mwenyekiti akaniambia kazi ndiyo inaanza rasmi kuanzia sasa hivi nitakuwa nakulipa mshahara.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwa ni majira ya saa ngapi?

SHAHIDI: Takribani saa nne usiku.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama wewe baada ya yale mazungumzo ulielekea wapi?

SHAHIDI: Alisema wewe utapewa chumba utalala hapa baada ya muda kuwa umekwenda.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Ilibidi nilale kwa sababu nisingepata usafiri wa kwenda Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilifuatia?

SHAHIDI: Kesho yake asubuhi alinipatia 200,000/- kwenye namba yangu ya 0754-916 666 kutoka Airtel Money yenye namba 0784-779 944.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hapo ulielekea wapi?

SHAHIDI: Nilirudi Arusha kuendelea na kazi zangu za shambani.

WAKILI WA SERIKALI: Ni wakati mwingine upi tena ulikuja kuwasiliana tena na mwenyekiti?

SHAHIDI: Hatukuwasiliana tena kwa sababu tarehe 25 Agosti 2020 nilikamatwa na askari wa Jeshi la Polisi.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikamatiwa wapi?

SHAHIDI: Makumira, Wilaya ya Arumeru nikiwa nakwenda CRDB USA RIVER.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa unapelekea CRDB pesa za nini?

SHAHIDI: Nimetoka kuuza mazao shambani.

WAKILI WA SERIKALI: Mazao gani?

SHAHIDI: Karoti.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa umewauzia watu gani?

SHAHIDI: Watu wa Mount Meru. Wao walikuwa wanapeleka Game Site huko Ngorongoro.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa na kiasi gani?

SHAHIDI: Dola za Kimarekani 1,100 na shilingi 1milioni moja laki moja na kumi na saba, na Euro 240.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukamatwa nini kilifuata?

SHAHIDI: Nilikamatwa nikapakizwa kwenye gari nikapeleka kituo Kikuu cha Arusha. Baada ya lisaa limoja nilienda kupekuliwa nyumbani kwangu. Na baadaye kusafirisha kuletwa Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama zile pesa zako zilikuwa wapi?

SHAHIDI: Zilikuwa mikono mwa askari pamoja na simu zangu.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwaje hizo fedha?

SHAHIDI: Walinipekua kutoka katika mifuko yangu wakasema ni noti bandia.

WAKILI WA SERIKALI: Walipokukamata walikueleza wanakukamata kwa makosa gani?

SHAHIDI: Kwamba nina tuhuma za kujihusisha na kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Tueleze sasa ulipofikishwa Dar es Salaam nini kilikusibu?

SHAHIDI: Baada ya kufikishwa kituo cha polisi Dar es Salaam nilifanyiwa mahojiano na afande Mahita.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya mahojiano?

SHAHIDI: Niliweka lockup mpaka nilipofikishwa Mahakamani Kisutu.

WAKILI WA SERIKALI: Mahakamani Kisutu ulipofikishwa ulifikishwa kwa sababu zipi?

SHAHIDI: Nilifunguliwa mashitaka mbalimbali ikiwemo kushiriki vikao vya kutenda mambo ya kigaidi, kula njama za kutenda ugaidi, kesi ya utakatishaji wa fedha.

WAKILI WA SERIKALI: Mashitaka mengine?

SHAHIDI: Hapakuwa na zaidi. Nilifika nikaumganishwa na wenzangu wengine watatu waliokuwa gerezani.

WAKILI WA SERIKALI: Wanaitwa akina nani?

SHAHIDI: Khalfani Bwire, Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa.

WAKILI WA SERIKALI: Eleza Mahakama sasa kwa kuanza na Khalfani Bwire wewe ulikutana naye wapi kabla ya kuunganishwa naye?

SHAHIDI: Nilikutana naye akiwa Keys Hotel na Aishi Hotel akiwa na Freeman Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Vipi kuhusiana na Mohammed Ling’wenya?

SHAHIDI: Huyo sifahamu. Nilikutana naye mara ya kwanza gerezani.

WAKILI WA SERIKALI: Vipi kuhusiana na Adam Kasekwa?

SHAHIDI: Huyo simfahamu pia.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuwa umeunganishwa kwenye kesi hiyo Mahakama ya Kisutu ulipelekwa wapi?

SHAHIDI: Nilipelekwa Gereza la Ukonga.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa na akina nani?

SHAHIDI: Kila amtu alikuwa na wing yake. Nilikuwa na Khalfani Bwire na baadae kaongezeaka mtu anaitwa Khalid Athuman na baadaye akaongezeka Mohamed Ling’wenya akitokea Segerea.

WAKILI WA SERIKALI: Umekuwa kwenye kesi ile kwa muda gani?

SHAHIDI: Kwa miezi 11.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea?

SHAHIDI: Aliletwa Mheshimiwa Mbowe siku ya tarehe 26 Julai 2021. Alitukuta tukiwa na Khalfani Bwire, akasema poleni sana. Nimekuja kuwatoa.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kauli hiyo nini kilitokea?

SHAHIDI: Asubuhi watu wa Magereza walikuja kusema tujiandae tunaenda Mahakamani.

SHAHIDI: Kesho yake Julai 27 2021 tulipelekwa Kisutu mbele ya Hakimu Mzee Simba mimi, Khalid Athuman (mshtakiwa wa tano) na Gabriel Muhina (mshtakiwa wa sita). Mwanasheria akasema bada ya upelelezi kuwa sisi hatuhusiki kwa hiyo tumefutiwa mashitaka kwa kifungu kidogo. Baada ya pale niliondoka kutoka mahakamani kwenda kwa mdogo wake Kitunda. Kesho yake nikarudi mahakamani kwa Mwendesha Mashitaka kuuliza vitu vyangu.

JAJI: Ni sehemu ya ushahidi wenu kwamba alienda kwa mdogo?

WAKILI WA SERIKALI: Hapana Mheshimiwa.

SHAHIDI: Kesho yake nilipokwenda Kisutu kuuliza utaratibu wa fedha zangu wakanielekeza niende Central Police Dar es Salaam. Nikaenda kuonana na Inspector Swila akaniandika maelezo. Baada ya kuniandika maelezo akanipa vitu vyangu.

WAKILI WA SERIKALI: Umemtaja mtu anaitwa Freeman Mbowe, Khalfani Bwire, Mohamed Ling’wenya … Unaweza kuwatambua?

SHAHIDI: Ndiyo. Wapo hapa mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba sasa awatambue hapa mahakamani.

JAJI: Upande wa utetezi?

KIBATALA: Hatuna pingamizi.

Shahidi anakwenda walipo washitakiwa na kumtaja kila mmoja kwa jina lake.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji siye ni hayo tu.

JAJI: Upande wa utetezi? Mkizingatia ni muda wa mapumziko.

KIBATALA: Tunaweza za kushauriana nao?

JAJI: Ni sawa.

KIBATALA: Tuna pendekezo kwamba tukuombe tu- break kwa dakika 30.

JAJI: Saa nane na dakika 25 tutarudi tena kuendelea.

Mahakama imerejea.

Kesi esi namba 16 ya mwaka 2021 imeshatajwa. Pande zote mbili, Jamhuri na utetezi, ziko kama zilivyokuwa. Wakili Nashon Nkungu anatambulishwa kwa sababu alikuwa Mahakama Kuu kwenye kesi nyingine asubuhi ya leo.

JAJI: Sasa tulikuwa tumebakisha upande wa cross-examination na ningependa kuanza na wakili wa mshitakiwa namba moja.

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba katika ushahidi wako hukutoa uthibitisho wako kwamba ulikuwa ukifanya kazi kwa Ole Sabaya?

SHAHIDI: Siyo sahihi.

MTOBESYA: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji ni uthibitisho upi umetoa mbele ya mahakama hii.

SHAHIDI: Muulize Mheshimiwa Mbowe ndiyo atakwambia kama nilikuwa nafanya kazi.

JAJI: Mbowe siyo shahidi.

JAJI: Labda wakili urudie swali.

MTOBESYA: Ni sahihi kuwa umesema ulikuwa unafanya kazi na Ole Sabaya?

SHAHIDI: Sahihi.

MTOBESYA: Ni sahihi sasa kwamba hukutoa chochote mahakamani kuthibitisha?

SHAHIDI: Ndiyo. Sikutoa.

MTOBESYA: Umesema katika ushahidi wako kuwa ulikuwa unasafikiri kutoka a Longido kuja Moshi na kutoka Arusha kuja Moshi. Ulikuwa unatumia usafiri gani?

SHAHIDI: Usafiri wa umma.

MTOBESYA: Ni matumaini yangu kuwa ukipanda basi la umma unapewa tiketi. Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji kwamba wewe hukutoa tiketi.

SHAHIDI: Sikutoa tiketi kwa sababu nilipanda njiani.

MTOBESYA: Kwa hiyo nipo sahihi kwamba hukusafiri kwa sababu hukutoa tiketi wala uthibitisho wako wowote hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Siyo sahihi. Siyo lazima uwe na tiketi kuthibitisha.

MTOBESYA: OK. Tunashukuru. Tangu ukutane na Mbowe mpaka unakutana na Inspector Swila ni muda umepita?

SHAHIDI: Umeuliza swali siyo sahihi.

JAJI: Uliza na mawakili wa Serikali. Wamenyamaza na Mahakama haijaingilia ujue hilo swali ni sahihi. Utatakiwa ujibu.

SHAHIDI: Jibu sifahamu.

MTOBESYA: Tangu huyo unayemwita Mbowe mkutane ni muda gani umepita?

SHAHIDI: Mwaka moja na nusu.

MTOBESYA: Kuna lolote alikuachia afande Swila baada ya kukuandika maelezo?

SHAHIDI: Hakuna aliloniachia baada ya kuandika maelezo. Alinipa vitu vyangu nikaondoka.

MTOBESYA: Kwa hiyo Swila hakukuambia kwamba siku moja maelezo yako anayoandika yatatumika kama ushahidi?

SHAHIDI: Hakuniambia.

MTOBESYA: Alichokiandika alikupa ukakisoma?

SHAHIDI: Ndiyo. Alinipa nikasoma.

MTOBESYA: Ukajiridhisha kwamba ulichokisema ni sahihi?

SHAHIDI: Ni sahihi ndiyo.

MTOBESYA: Hakuna wakati alikuambia kuwa umwambie kila kitu unakijua?

SHAHIDI: Hapana.

MTOBESYA: Una uhakika ulichoandika ndicho ulichosema leo Mahakamani?

SHAHIDI: Ndiyo hicho hicho.

MTOBESYA: Kwa Bahati nzuri sisi mawakili wa utetezi tuna nafasi ya kupewa nyaraka za maelezo mliyoandika.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji naomba nipewe original document ya hii. Na msingi wangu wa kuomba ni kifungu cha 164 cha Sheria ya Ushahidi.

(Mawakili wa Serikali wanasema hawana pingamizi)

(Mtobesya anatembea kumfuata shahidi alipo)

Kimya kidogo kinatawala.

MTOBESYA: Pitia nyaraka hii kama ndiyo aliyoaandika Swila na kama ulikubali kuwa ni sahihi (anampatia asome).

SHAHIDI: Haya ndiyo maelezo yangu ya kwanza.

MTOBESYA: Unaweza kusoma?

SHAHIDI: Ndiyo.

MTOBESYA: Soma tarehe kisha soma mtu aliyeandika ni nani.

SHAHIDI: Ndiyo haya.

MTOBESYA: Naomba nikuulize kuhusu hii statement yako dhidi ya ulichokisema leo.

MTOBESYA: 1. Nionyeshe kwenye hiyo statement sehemu iliyoandikwa kwamba huyo uliyemuita Mheshimiwa Mbowe kuwa yule alikuwa mlinzi wake na msiri wake

WAKILI WA SERIKALI: Objection! Kwa mujibu wa kifungu cha 154 anatakiwa amwonyeshe shahidi hicho anachokisoma . Yeye amefanya vice versa.

MTOBESYA: Sijapata msingi wa objection ya ndugu yangu Robert Kidando.

MTOBESYA: Nilianza kutengeneza msingi kwa kuuliza, je, alichokisema hapa ndicho kilichopo kwenye statement? Sasa kama anataka twende hivyo tutaenda.

JAJI: Hapana.Tuwasaidie wateja wetu.

WAKILI WA SERIKALI: Provisory mstari wa nne ndiyo inakataza.

JAJI: Tueleze nyie mmelewa nini?

Wakili wa Serikali Chavula: Maamuzi ya kifungu hiki yametolewa uamuzi na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Lilian Otesi Vs Jamuhuri, namba 77 katika rufaa ya Jinai ya 251 Mwaka 2008 katika Mahakama ya Rufaa. Katika kesi hii ukurasa wa 25 Mahakama ilisema yafuatayo: “Kinachozungumzwa pale ni sawa na Kifungu namba 154 cha Sheria ya Ushahidi kama kilivyogawanyika maeneo mawili. Eneo la kwanza shahidi anaweza kudodoswa kupitia maelezo yake aliyoyaandika nyuma. Eneo la pili anaweza kuhojiwa kuhusu masuala yake hayo hayo bila kumwonyesha maelezo yake.

WAKILI WA SERIKALI: (Chavula) Lakini kama inadhamiriwa kumpima mkanganyiko wake shahidi kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa. Na hivyo kabla ya kuthibitisha amwelekeze kwanza. Tofauti na yeye kaenda na kumfuata.

MTOBESYA: Rafiki yangu anarejea vifungu viwili tofauti. Wakitaka hayo ningefika huko kwa sababu hata kesi ya Alberto Mendez imejadili hayo na mimi nilikuwa ni sehemu ya ile kesi. Kwa hiyo nafahamu ninachofanya.

WAKILI WA SERIKALI: Kifungu cha 164 hakisimami peke yake. Kusimama kwake kunategemea kifungu cha 154. Na huo ndio msimamo wa Mahakama.

MTOBESYA: Tusaidiane Mheshimiwa Jaji. Dhumuni la Kifungu cha 164 ni kumchanganya (contradict) shahidi. Mimi nilikuwa nimeanza kwenye kifungu cha 154. Sikuwa nimefika huko.

JAJI: Wao wanasema wana hukumu ambayo wanaweza za kutu- supply. Nafikiri ni vyema basi tuweze kuona tu.

MTOBESYA: Hili suala linaweza kuibuka tena mbeleni. Tunaomba liwe cleared kabisa na Mahakama.

WAKILI WA SERIKALI: Tunaomba dakika 15.

JAJI: Sawa. Tunaahirisha kwa dakika 15.

Jaji alisema anaahirisha kwa dakika 15, sasa iniakaribia dakika 40.

Mawikili wote sasa wamerudi. Mahakama itarejea hivi punde.

Saa 10:08 Jaji ameingia mahakamani.

Kesi inatajwa tena. Ni kesi namba 16 ya mwaka 2021.

Jopo la mawakili wa Serikali wakiongozwa na Robert Kidando limetimia kama lilivyokuwa na anasema wapo tayari kupokea maelekezo ya Mahakama.

JAJI: Muda mfupi wakati wa dodoso na upande wa utetezi, upande wa utetezi waliomba Mahakama iruhusu itoe maelezo yaweze kutumika kwa nakala halisi P4. Baada ya mawakili wa utetezi kusimama, upande wa Serikali walisimama na kusema utaratibu haukufuatwa. Baada ya hapo pande zote walisema kuna maamuzi. Nikaomba maamuzi hayo.

1 Nyaraka inatakiwa itolewe. Hilo limeshafanyika.

2 .Nyaraka hiyo inapaswa isomwe katika maeneo anayotaka kumuuliza maswali ili kum- contradict.

JAJI: Mahakama hii inasema kwa kuwa huo ndio utaratibu basi unatakiwa ufuatwe na kuendelea na shughuli.

Wakili wote wanasimama na kushukuru wakionyesha ishara ya kukubaliana uamuzi wa Jaji.

Wakili Mtobesya anarudi kwa shahidi na anaiomba Mahakama impatie tena nyaraka. Shahidi anaulizwa na anasema anaweza kuisoma.

SHAHIDI: Anaanza kuisoma.

Katika maelezo yake ansoma alishawahi kuwa msaidizi wa Katibu wa CCM Longido. Amesomea Hotel Management. Alishawahi kufanya kazi na Sabaya kama msaidizi wake na aliacha kazi kwa Sabaya kwa sababu alitaka kurudi Longido na alienda kwa ajili ya kumfuata mchumba wake. Anarudia kuwa alipigiwa simu na Freeman Mbowe na kwamba alifuatwa Longido.

Shahidi (akisoma): “Freeman aliniambia kuwa nilitumiwa 50,000 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Mama Helga na kumtomgoza. Nilishangaa sana kwamba alijuaje kwa sababu ilikuwa ni kweli nilimtongoza. Alinipigia simu tukutane Moshi. Alinipigia niende Keys Hotel. Na siku nyingine tulienda Aishi Hotel.

MTOBESYA: Soma eneo linalosema mimi nilikwenda kwa kutumia nauli yangu.

SHAHIDI: Mimi nilikwenda kwa kutumia nauli yangu, na nilipofika alikuja kunichukua.

MTOBESYA: Ieleze Mahakama kwamba huyo mlinzi alikuwa diwani wa Kiboriloni.

SHAHIDI: Nilisema.

MTOBESYA: Elezea sasa hapo katika maandishi yako humo kuna mlinzi anaitwa Bwire.

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji mimi leo nilikuwa nafafanua.

MTOBESYA: Hkuna mahala kwenye statement inaonyesha kuna mlinzi anaitwa Bwire.

SHAHIDI: _Statement haionyeshi.

MTOBESYA: Kwenye statement yako kuna sehemu inasema baada ya kukutana mara ya pili kwamba ulimtajia majina huyo Mbowe watu wanaotembea na Sabaya.

SHAHIDI: Majina hayajaandikwa hapa kwenye statement.

MTOBESYA: Ulipokutana mara ya tatu ulisema ulimtajia pia najina. Hayo majina yapo kwenye maelezo yako?

SHAHIDI: Hayapo.

MTOBESYA: Wakati unaongozwa na Wakili Wa Serikali na huyo uliyemuita Mbowe ulimpigia Sabaya na baadae Mbunge uliyemjulisha. Je, hayo yapo kwenye statement yako?

SHAHIDI: Hayapo.

MTOBESYA: Pia wakati wakili wa Serikali anakuongoza nilisikia majina ya Hotel na clubs ulizotaja kwa majina yake. Hizo taarifa zipo humo kwenye statement yako?

SHAHIDI: Hazipo.

MTOBESYA: Wakati Wakili wa Serikali anakuongoza huyo uliyesema Bwire alitamka kuwa Sabaya ni mtoto mdogo atamchezesha. Je yapo kwenye statement?

SHAHIDI: Hayapo.

MTOBESYA: Wakati Wakili wa Serikali anakuongoza umesema wewe unajishughulisha na kilimo na ukasema unavyofanya kilimo. Je, yapo hapo kwenye statement?

SHAHIDI: Hayapo.

MTOBESYA: Soma kwa Sauti kuanzia sehemu unayosema kuwa ulikuwa msaidizi wa Katibu wa CCM.

(Shahidi anasoma kuwa alikuwa msaidizi wa Katibu wa CCM na mwanaharakati wa CCM).

MTOBESYA: Wakati Wakili wa Serikali anakuongoza ulisema kuwa wewe ulishawahi msaidizi wa CCM?

SHAHIDI: Hapana.

MTOBESYA: Je, ungependa maelezo uliyoyaongea leo yaingie kwenye ushahidi wako?

SHAHIDI: Ndiyo kwa sababu nimeongea chini ya kiapo ningependa yaingie kama ushahidi.

JAJI: Upande wa Serikali?

WAKILI WA SERIKALI: Hatuna pingamizi mheshimiwa.

Jaji anaandika wakati mahakama iko kimya na Wakili Mtosebya amekwenda kukaa kwenye nafasi yake.

JAJI: Kwa sababu imeombwa na shahidi kuwa maelezo hayo hayajapingwa na Mahakama, na haijapingwa na upande wa mashitaka, basi Mahakama imepokea maelezo hayo kama kielelezo namba 1.

MTOBESYA: Naomba kuendelea Mheshimiwa Jaji.

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi nikisema kwa kipindi hicho mpaka unaandika statement ulikuwa unajishughulisha na siasa?

SHAHIDI: Siyo sahihi kwa sababu mimi ni mwandishi ninayepiga picha siyo mwanasiasa.

MTOBESYA: Kwa hiyo wewe siyo mwanachama?

SHAHIDI: Siyo mwanachama wa chama chochote.

MTOBESYA: Ni lini uliiacha kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi?

SHAHIDI: Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile.

MTOBESYA: Hujawahi kuwa karibu na viongozi wa kisiasa?

SHAHIDI: Nimesema kuwa nimekuwa karibu na viongozi wa Serikali na siasa.

MTOBESYA: Unaweza kumtajia Mheshimiwa Jaji ni akina nani uliwahi kuwa nao karibu?

SHAHIDI: Mrisho Gambo, Daqaro na Sabaya.

MTOBESYA: Hujawahi kuandika barua ukiwa gerezani kwa viongozi wa kisiasa wakusaidie kwenye kesi iliyokuweka jela?

SHAHIDI: Sijawahi.

MTOBESYA: Hujawahi kutembelewa na viongozi wa kisiasa ukiwa gerezani?

SHAHIDI: Sijawahi.

MTOBESYA: Ulikutana na mheshimiwa Mbowe gerezani tarehe ngapi?

SHAHIDI: Tarehe 26 Julai 2021.

MTOBESYA: Maelezo yako umeandika lini?

SHAHIDI: Siku mbili baada ya kutoka gerezani.

MTOBESYA: Na umesema wakati umefika Mahakamani Kisutu siku hiyo, mlielekezwa nini siku hiyo?

SHAHIDI: Baada ya upelelezi kukamilika tumeonekana hatuna hatia tena.

MTOBESYA: Unakumbuka namba ya kesi ulikuwa umeshitakiwa nayo?

SHAHIDI: Sikumbuki.

MTOBESYA: Naweza kusema Kesi namba 63 ya mwaka 2020.

SHAHIDI: Sahihi.

MTOBESYA: Unakumbuka mashitaka uliyoshitakiwa nayo wewe binafsi?

SHAHIDI: Kushiriki vikao. Kula njama za kutenda vitendo vya ugaidi na utakatishaji.

MTOBESYA: Kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza naomba tuishie hapa.

Anaingia Wakili John Mallya.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naitwa John Mallya. Nina maswali machache (anamtazama shahidi na kumwambia) Jibu kwa sauti.

MALLYA: Diwani analipwa shilingi ngapi?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Diwani analipwa posho shilingi ngapi?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Kwa ufahamu wako wewe Sabaya alikuwa anakulipa kutoka mfuko gani?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Kwa hiyo wewe hukutaka kabisa kujua kama anaiba au anatoa wapi?

SHAHIDI: Sikujua.

MALLYA: Alikuwa anakulipa shilingi ngapi?

SHAHIDI: 300,000/-.

MALLYA: Kwa picha au kwa mwezi?

SHAHIDI: Kwa mwezi.

MALLYA: Mheshimiwa naomba kielelezo namba D1.

MALLYA: Soma hapo mwanzoni.

SHAHIDI: Nilianza harakati za kisiasa na kuwa msaidizi wa Katibu wa CCM.

MALLYA: Umemtaja Mrisho Gambo alikuwa chama gani?

SHAHIDI: CCM.

MALLYA: Sabaya alikuwa chama gani?

SHAHIDI: CCM.

MALLYA: Daqaro Mkuu wa Wilaya alikuwa chama gani?

SHAHIDI: Mkuu wa wilaya hana chama.

MALLYA: Unasema Sabaya alikuwa diwani wa chama gani?

SHAHIDI: CCM.

MALLYA: Halafu Magufuli akamteua kuwa mkuu wa wilaya?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Mkuu wa Wilaya hana chama ila Magufuli alimteua Sabaya wa CCM.

SHAHIDI: Ndiyo alimteua akiwa CCM.

MALLYA: Hapa karibu umesikia kabla ya Sabaya kufunguwa miaka 30 aliomba Mahakama impunguzie adhabu sababu ana mchumba. Wewe umesema Sabaya alikuwa na mke?

SHAHIDI: Mimi najua Sabaya alikuwa na mke.

MALLYA: Kwa hiyo kule kadanganya Mahakama?

SHAHIDI: Sijui yeye sasa.

MALLYA: Nimesikia ulimtajia Mheshimiwa Freeman Mbowe, Sylvester Nyegu?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Umesikia kuwa Mahakama imemfunga kwa makosa ya ujambazi Arusha?

SHAHIDI: Ndiyo. Nimesikia.

MALLYA: Soma statement yako hapo mlipokuwa mwishoni mwa mwaka 2017.

(Shahidi anasoma).

MALLYA: Kwa hiyo kati ya hapo na hapa ulisema mwisho mwaka 2018 mahakama ichukue lipi?

SHAHIDI: Aliyeandika atakuwa amekosea.

MALLYA: Soma hapo juu.

SHAHIDI: Mimi nathibitisha kuwa maelezo haya ni sahihi.

MALLYA: Sasa wakati gani tujue upo sahihi? Hapo umethibitisha upo sahihi na leo unasema tuchukue ya leo. Kwamba uliacha kazi kwa Sabaya mwaka 2017 na leo unasema aliacha kazi 2018?

MALLYA: Hapo chini maelezo uliyosaini yana maana gani?

SHAHIDI: Yana maana ya uthibitisho.

MALLYA: Mkuu wa wilaya analipwa shilingi ngapi?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Sabaya alikuwa anakulipa shilingi ngapi?

SHAHIDI: 300,000/-.

MALLYA: Alikuwa anatoa wapi?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Umesema Sabaya alikuwa anaongozana na watu saba au wanane. Je, walikuwa wanalipwa na nani?

SHAHIDI: Sifahamu. Walikuwa ni marafiki zake.

MALLYA: Wakati unatoa majina mwaka 2017 na ukaja kuyatoa tena mwaka 2018 kwanini ulikuwa nayo?

SHAHIDI: Walikuwa marafiki zangu.

MALLYA: Ulipokamatwa Arusha alikuhoji Afande Mahita?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Hayo aliyokuhoji umeyatoa hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Je, umeshawahi kuyatoa hayo maelezo kwa maana karatasi kwa Mheshimiwa Jaji?

SHAHIDI: Siyo kazi yangu.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali langu.

JAJI: Je, aliyatoa lakini?

MALLYA: Nataka iingie kwenye rekodi za Mahakama.

MALLYA: Ulipokutana na Mbowe gerezani alikuambia nimekuja kuwatoa na kesho yake ukatoka kweli?

SHAHIDI: Ni sahihi. Nilitoka.

MALLYA: Baada ya Kututiwa kesi ulienda Central kufuata vitu vyako?

SHAHIDI: Ni sahihi. Nilienda Central kwa Inspector Swila nikatoa maelezo ndiyo nikapewa vitu vyangu.

MALLYA: Kwa hiyo Mahakama irekodi kuwa ulipewa vitu vyako baada ya kuandika maelezo?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Hujamuuliza kama alipotoka gerezani alienda kwa mchumba wake

Mahakama inaangua kicheko.

JAJI: Kesho si unaweza kumaliza mapema? Je, tunaweza kupata shahidi mwingine?

WAKILI WA SERIKALI: Bado hatuna uhakika. Tulikuwa tunahangaika kumpata.

JAJI: Basi jitahidi msijiandae kumkosa.

JAJI: basi naahirisha mpaka kesho ambapo upande wa utetezi watamalizia kuuliza maswali ya dodoso.

JAJI: Kisha upande wa mashitaka watarudi kwa ajili ya re-examination.

Jaji anaahirisha kesi hadi kesho saa tatu asubuhi.

Like
4