Kesi ya Mbowe na wenzake awamu ya pili: Maswali ya mawakili na majibu ya shahidi ACP Kingai

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ leo Jumanne 26.10.2021

Saa 4:16 Jaji anaingia Mahakamani

Wakili wa Serikali, Robert Kidando, anatambulisha jopo la mawakili wa Serikali.

 1. Robert Kidando
 2. Nassoro Katuga
 3. Ignas Mwanuka
 4. Esther Martin
 5. Tulumanywa Majigo
 6. Jenitreza Kitali

Wakili Peter Kibatala anawatambulisha mawakili wa upande wa utetezi kwa kuanza na yeye mwenyewe.

 1. Jeremiah Mtobesya
 2. Michael Mwangasa
 3. Nashon Nkungu
 4. Dickson Matata
 5. Alex Massaba
 6. Jonathan Mndeme
 7. Hadija Aron
 8. Idd Msawanga

Jaji anaomba kuwaona washitakiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa nne.

Washtakiwa wanainuka kwa namba zilivyotajwa.

Wakili wa Serikali anaomba kesi kuendelea na kwamba shahidi yupo tayari. Lakini kabla ya kuendelea anaomba kufuatilia kuhusiana mabadiliko yaliyosababisha hadi kuletwa jaji mwingine kwa mujibu ya kifungu cha 299 CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai).

JAJI: Upande wa utetezi?

PETER KIBATALA: Hatatumia haki ya kumwita tena shahidi kwa kesi Inayoendelea hapa.

Jaji anaandika

JAJI: Wote mnafahamu na mlikwepo siku ya tarehe 20 mhuu na alielekeza jaji mwingine atakuja kuendelea na kesi hii. Na Jaji mwingine ndiyo mimi.

JAJI: Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 kifungu cha 299, kwamba upande wa utetezi mna haki ya kumuita tena shahidi kwa kuwa mmesema hamna nia nitawaruhusu upande wa Jamuhuri kumwita sasa shahidi wao tuweze kuendelea.

Mawakili wote wanainuka ishara ya kukubaliana na uamuzi wa Jaji na kupokea maelekezo ya mahakama.

Wakili wa Serikali anakwenda kumwita shahidi.

ACP Kingai anaingia chumba cha mahakama na kupanda kizimbani.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anamtaarifu Jaji kwamba shahidi amefika.

JAJI: Majina yako tafadhali!

SHAHIDI: Naita ACP Ramadhan Kingai.

JAJI: Unakumbuka uliwahi kufika mahakamani, ukaapishwa kutoa ushahidi. Mahakama inakukumbusha upo chini ya kiapo hicho.

SHAHIDI: sawa Mheshimiwa.

JAJI: Mtakumbuka mawakili kuwa siku ya tarehe 20 Jaji alipokea kielelezo. Baada ya kupokelewa kinatakiwa kusomwa Mahakamani? Naomba kuanzia hapo shahidi akabidhiwe kielelezo aweze kusoma kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Soma sasa kielelezo kuanzia ukurasa wa kwanza.

SHAHIDI: Adama Kasekwa anaishi Chalinze. Maelezo ya Onyo chini kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20. Mimi Kingai nakuonya wewe Adam Kasekwa. Hulazimishwi kusema lolote. Pia unaweza kualika ndugu, jamaa au mwanasheria kushuhudia utiaji saini wako maelezo. Mtuhumiwa akasaini na mimi nikasaini Majibu ya Onyo. Mimi Adam Kasekwa anaonywa na Kingai chini ya Kifungu cha 24 cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai, silazimishwi na yoyote kutoa maelezo yangu. Je, upo tayari kutoa maelezo yako? Jibu, Ndiyo nipo tayari. Maelezo yamechukuliwa katika Ofisi ya RCO Ilala. Mimi Adam Kasekwa nimezaliwa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Ileje. Mwaka 2011 nilijiunga na Recruiting Makutopora. Nikachaguliwa kujiunga na mafunzo ya ukomando 92KJ.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Mwaka 2014 niliteukiwa kwenda Kituo cha Msangani kujifunza Ulinzi wa Amani na nikachaguliwa kwenda DR Congo. Mwaka 2017 nilimaliza mkataba na kurejea . Nilipata malipo na kumwoa mke wangu Lilian ambaye naishi naye mpaka leo. Nimepata naye mtoto mmoja. Nilirudi nikaa miezi sita kazini. Nikaugua ugonjwa wa akili. Nikaachishwa kazi na kulipwa mafao ya millioni nne na laki sita. Je, unamfahamu Luteni Dennis? Ndiyo.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Niliporudi nikaambiwa mwenzangu ananitafuta. Niliporudi nyumbani nilimpigia simu mwenzangu Mohammed Ling’wenya kwamba kuna kazi ya VIP Protection. Akaniambia inabidi twende Morogoro kumwona Luteni Urio. Tulipoenda akatuambia kuna kazi ya VIP Protection ya kumlinda Mbowe. Akatupatia TSh 21,000 nauli ya Kwenda Moshi.

Kingai anaendelea kusoma.

SHAHIDI: Siku hiyo hiyo tulirudi Chalinze na kuanza safari ya kwenda Moshi. Tulipokelewa na dereva wake anayeitwa Willy. Alitupokea na Pick Up nyeupe yenye maandishi ya M4C. Tukaenda mpaka kwenye Hotel ya Mheshimiwa Mbowe. Huko tulimkuta Khalfani Bwire aliyetutambulisha kwa Mbowe kuwa mkuu wale vijana tuliowaagiza ndio hawa hapa. Mbowe akatueleza kuwa Sabaya anamvuruga sana na anamvurugia wapiga kura, na Kwamba anawatisha wapiga kura wake kiasi cha kuhatarisha kurudi kwake. Na Kwamba akatuelekeza tumdhuru kwa njia yoyote. Akatuelekeza maeneo yake ya Moshi na Arusha. Tulipanga kumdhuru kwa spray. Spray ya sumu alitafuta Mohammed Ling’wenya.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Siku inayofuata tulikuwa mimi na Mohammed na wanachana wawili siwakumbuki majina. Baada ya kufika Dar es Salaam tulimfikisha Mheshimiwa Mbowe nyumbani. Akatukabidhi TSh 200,000 za kununua nguo kwa sababu Kesho yake tulikuwa tunampokea Mheshimiwa Lissu. Na siku ya tarehe 27 Julai alitutumia kila moja TSh 78,000 nauli ya kwenda Moshi. Siku ya tarehe moja Agosti tulienda Moshi tukamkuta Mbowe akiwa na Khalfani Bwire.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Akatuelekeza kuwa tufanye ile kazi yake haraka. Akatuelekeza maeneo anayokaa Sabaya kama vile Milestone. Akatuelekeza tuje Dar es Salaam pia kuchoma vituo vya mafuta. Kwamba yeye anatachochea maandamano ili Serikali ionekane imeshindwa kuandaa Uchaguzi.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Tulienda maeneo ya Boma Ng’ombe njia ya a kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kumfuatilia. Siku ya terehe tatu tulienda maeneo ya Rau Madukani kwa ajili ya kubana matumizi. Kwa sababu Mheshimiwa alitiachia pesa 150,000/- kwa ajili ya kukaa isingetosha.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Tulienda kkwa dada yake kwa ajili ya kubana matumizi. Suala la kupanga ugaidi ni la kweli na suala suala la kukutwa na silaha ni la kweli. Wakati Polisi wananikamata pia walinikuta na heroine. Baada ya kuchukua vitu hivyo askari walisaini na mimi nikasaini na Polisi walichukua vitu hivyo kwenda Central.

Kingai anaendelea kusoma maelezo:

SHAHIDI: Alikiri kupewa maelekezo ya kazi kutoka kwa Mheshimiwa Mbowe. Alikiri pia alipewa maelekezo ya kazi kutoka akwa Mbowe kupitia kwa Luteni Dennis Urio. Alikiri pia kuwapo Moshi tarehe 24 mwezi wa saba mwaka 2020. Alikiri pia kuwapo Moshi na wenzake Mohammed Ling’wenya na mwenzake aliyemtaja kwa jina la Kakobe. Baada ya ufutailiaji tukamfahamu ni Moses Lijenje. Alikiri pia kufanya mkutano yeye na wenzake wanne—yeye mwenyewe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya, Moses Lijenje (aliyemtaja kwa jina la Kakobe) Khalfani Bwire na Freeman Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa mkutano huo nini kiliendelea?

SHAHIDI: Mbowe alitoa maelezo kuwa Sabaya anamfanyia vurugu.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kingine alikueleza?

SHAHIDI: Mtuhumiwa alikiri kupewa pesa 150,000/= kukidhi mahita kipindi watakapokuwa hapo Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Tuelezee shahidi kuhusiana na kilichofuata.

SHAHIDI: Alikiri kuwa siku ya tarehe moja mwezi wa nane saa 11 alfajiri kabla ya safari ya kuja Dar es Salaam aliwaelekeza wamdhuru Ole Sabaya. Akawaonyesha picha ya Ole Sabaya kupitia simu yake ya mkononi. Aliwapa maelekezo ya kufanya kazi hiyo na kwamba baada ya hapo atawataka warudi Dar es Salaam. Alipanga kuwapa kazi ya kwenda kulipua vituo vya mafuta. Alipanga kufanya vurugu kwenye masoko.

WAKILI MTOBESYA: Objection! naomba shahidi ajielekeze kwenye kikichoandikwa kwenye statement. Mambo ya kituo cha mafuta na masoko havijatajwa.

JAJI: Kwa hiyo asome?

WAKILI MTOBESYA: Ajielekeze kilichoandikwa hata kama anarudia kuelezea. Sheria inasema statement itajielezea yenyewe.

JAJI: Upande wa Mashitaka?

WAKILI WA SERIKALI: Sahihi Mheshimiwa tutarekebisha.

WAKILI WA SERIKALI: Alikueleza lengo ilikuwa ni nini?

SHAHIDI: Lengo ni Serikal ionekane imefeli. Alikiri pia kukamatwa na Polisi siku ya tarehe tano mwezi wa nane mwaka 2020 akiwa Rau Madukani. Alikiri pia kukamatwa na pistol aina ya Ruvern ikiwa na risasi tatu (3). Alikiri kukamatwa na kete 58 za madawa aina ya Heroine.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuwa umeandika maelezo hayo, yeye ulimpeleka wapi kwa siku hiyo?

SHAHIDI: Ilikuwa siku ya tarehe sabba mwezi wa nane mwaka 2020 nilimrudisha mahabusu.

WAKILI WA SERIKALI: Shughuli gani nyingine iliendelea baada ya shughuli hii?

SHAHIDI: Tuliendelea na upelelezi kwa kutafuta watuhumiwa wengine. Maeneo ya Chang’ombe tulimkamata Khalfani Bwire.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa tuhuma gani?

SHAHIDI: Kwa tuhuma hizi hizi za kula njama kutenda matendo ya ugaidi.

WAKILI WA SERIKALI: nini kiliendelea?

SHAHIDI: Nilimtaka Khalfani Bwire aandike maelezo yake.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea kuhusu kumkamata kwake.

SHAHIDI: Baada ya a kuwasiliana na askari aliyekuwa kwenye pointi akiwa kwenye gari, tukielekeza gari iingie Kituo cha Polisi Chang’ombe. Tukawa tumeingia pale na Inspector Mahita na ASP Jumamne.

JAJI: ASP nani?

SHAHIDI: Jumanne.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumkamata mlimpeleka wapi?

SHAHIDI: Tuliekeza Superintendent Lukangira wa hapo hapo Chang’ombe. Hii ni baada ya mtuhumiwa kutuelekeza hana makazi hapa Dar es Salaam na ni mkazi wa Ngerengere.

WAKILI WA SERIKALI: Nia ya kuuliza kwake wapi ilikuwa ni ya nini?

SHAHIDI: Nia ilikuwa kufanikisha shughuli za kiupepelezi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Lukagingira kuandika maelezo yake nini kilifuata?

SHAHIDI: Tukawa tunaendelea kufuatilia makazi yake tofauti na taarifa aliyokuwa ametoa yeye kwa kuwa tulijua haiwezekani awe kila siku anaenda Ngerengere.

WAKILI WA SERIKALI: Nia ilikuwa nini?

SHAHIDI: Ilikuwa kufuatilia movements zake.

WAKILI WA SERIKALI: Katika ufutailiaji wa makazi yake mlipata nini?

SHAHIDI: Tulipata taarifa ana makazi Temeke. Tukaelekea ku- stop kwanza uchukuaji wa maelezo yake ili kukamilisha upelelezi na kuja kuandika tena.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unapata taarifa ana makazi Wilaya ya Temeke elezea sasa maelezo yalikuwa yanaandikiwa wapi.

SHAHIDI: Maelezo yalikuwa yanachukuliwa Kituo cha Polisi Chang’ombe na mimi niliweka base Central Police (Ilala).

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kutoa maelezo hatua ya kuchukua maelezo ikasimama. Nini kilifuata?

SHAHIDI: Tulipata taarifa mtuhumiwa anakaa Temeke Makangarawe. Tuliungana na Detective John wa Temeke na RCO kwa ajili ya kwenda kumpekua makazi yake.

WAKILI WA SERIKALI: Mlienda sehemu ipi haswa huko Mkangarawe?

SHAHIDI: Ule mtaa jina limenitoka.

WAKILI WA SERIKALI: Uliwezaje kuutambua sasa?

SHAHIDI: Tulielekea na watu hadi nyumba aliyokuwa amepanga mtuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea sasa hiyo shughuli ilifanyikaje na Khalfani Bwire alikuwa wapi.

SHAHIDI: Tuliongozana na mtuhumiwa. Tukamtafuta mwenyekiti wa ule mtaa. Tukamkuta na mwenye nyumba aliyempangisha Khalfani Bwire na hata mke wake alikuwapo.

WAKILI WA SERIKALI: Huyu mwenyekiti ni wa nini?

SHAHIDI: Ni mwenyekiti wa mtaa.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilifuata?

SHAHIDI: Nilimuelekeza ASP Jumanne kwa kushirikiana na Detective John kutoka Ofisi ya RCO Temeke na kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa na hata mke wake.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea sasa katika upekuzi huo mlikuta nini.

SHAHIDI: Vitu mbalimbali vilipatikana kama uniforms za JWTZ, masharti ya JWTZ, T-shirt za JWZT, ….

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kupata uniforms na vifaa mbalimbali nini kilifanyika baada ya kupata vitu hivyo?

SHAHIDI: Viliorodheshwa katika Hati ya Uchukuaji Mali. Wakati wa upekuzi tulimkuta na kidaftari kilichokuwa na ramani na majina ya vituo vya mafuta.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuorodhesha kitu gani kilifanyika?

SHAHIDI: Baada ya kuwa viliorodheshwa yaliandikwa na majina ya walioshuhudia upekuzi huo. Lakini pia wakasaini Hati ya Uchukuaji Mali. Mtuhumiwa pia alisaini Hati ya Uchukuaji Mali na aliyepekua alisaini hati hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukamilisha Hati ya Uchukuaji Mali, kitu gani kiliendelea?

SHAHIDI: Nilikuwa nimeelekeza mashahidi walioshuhudia waandikwe maelezo palepale.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukamilisha?

SHAHIDI: Tulichukua vitu tulivyoorodhesha na mtuhumiwa tukamrudisha kituo cha Polisi.

WAKILI WA SERIKALI: Kituo gani cha Polisi?

SHAHIDI: Chang’ombe.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumrudisha Kituo cha Polisi Chang’ombe kitu gani pia kiliendelea?

SHAHIDI: Mtuhumiwa tulimkamata na kidaftari chenye ramani ya vituo vya mafuta Dar es Salaam, Soko la Kilombero Arusha. Tukachukua sampuli za miandiko ya watuhumiwa wote.

SHAHIDI: Lakini pia tuliendelea na hatua ya kuwatafuta watuhumiwa wengine.

WAKILI WA SERIKALI: Watuhumiwa gani wengine mlikuwa mnawatafuta?

SHAHIDI: Watuhumiwa wengine tuliokuwa tunawafutilia ni mtu alikuwa anaitwa Gabriel, Lijenje, Malima, Khalid na jamaa mmoja anaitwa Kaaya.

WAKILI WA SERIKALI: Nini hatima ya hao mliokuwa mnawafuatilia?

SHAHIDI: Ukimwondoa mtu mmoja anaitwa Malima, watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Vipi kuhusu huyu Moses Lijenje?

WAKILI WA SERIKALI: Hapa Mahakamani kuna washitakiwa wanne, inakuwaje hao wengine hawapo Mahakamani kama walifunguliwa mashtaka?

SHAHIDI: Walifutiwa mashitaka baada ya kuonekana ushahidi haukuwa wakutosha ukilinganisha na wenzao.

WAKILI WA SERIKALI: ACP Kingai katika ushahidi wako tangu mwanzoni umezungumzia kukamatwa Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Khalfani Bwire, vipi ukamatwaji wake mshitakiwa wa nne?

SHAHIDI: Freeman Mbowe alikamatwa tarehe 21 Julai mwaka 2020 akiwa Mwanza.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa tuhuma gani?

SHAHIDI: Kwa tuhuma hizi hizi.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unatoa ushahidi wako ulizungumzia kukamatwa hawa wengine mwaka 2020 na huyu 2021. Elezea Ilikuwaje hapa Mahakamani.

SHAHIDI: Tulikuwa tunajiridhisha haswa uhusika wake. Tulikuwa bado tunaendelea kufuatilia mawasiliano.

SHAHIDI: Na uchunguzi wa forensic ambao ulikuwa unahusiana na shauri hili.

WAKILI WA SERIKALI: Sababu ukamataji ulifanyika 21 Julai mwaka 2020 ni lini taarifa zilifahamika rasmi?

SHAHIDI: Zilifahamika mwanzoni Julai 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati anakamatwa upelelezi ulikuwa umefikia hatua gani?

SHAHIDI: Upelelezi wetu kwa muda huo tunamkamata ulikuwa umekamilika.

WAKILI WA SERIKALI: Upelelezi wa aina gani ulikuwa unaendelea wa mshitakiwa nne?

SHAHIDI: Tulifanya forensic na devices za kieletronic tuliokuwa tunafuatilia kujiridhisha dhidi yake na tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unatoa ushahidi wako mwanzoni ulisema ulielezea kuwa umeelekeza kufungua jalada la tuhuma za kigaidi.

SHAHIDI: Kulingana na taarifa ambazo tulikuwa tumezioata kwa Luteni Urio na aina ya vitendo vilivyokuwa vimepangwa na watuhumiwa. Ilikuwa ni kudhuru viongozi wa Serikali, kufanya vurugu sehemu zenye watu wengi, kulipua vituo vya mafuta, hata miti kwenye highway kukatwa kuzuiwa magari yasipite, hasa katika Barabara ya Morogoro kwenda Iringa.

WAKILI WA SERIKALI: Ukatafsiri ni vitendo gani?

SHAHIDI: Vitendo vyenye kuleta hofu kwa wananchi kujiona hawapo salama. Ni vitendo vinavyoleta tafsiri la shitaka la ugaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Ulisema katika taarifa ya Luteni Urio ulisema walipanga kuonyesha kuwa nchi haitawaliki.

WAKILI MTOBESYA: Objection! Kaka yangu Wakili Msomi ajielekeze kwenye fact siyo kwenye opinion, maana huyo ni shahidi wa fact, He’sdoing too much sasa maana mwanzo tulijua ameteleza.

WAKILI WA SERIKALI: Sawa Mheshimiwa Jaji nitaomba njielekeze sawa sasa.

WAKILI WA SERIKALI: Vitendo hivi vilipangwa vifanyike wapi?

SHAHIDI: Mwanza, Moshi, Dar es Salaam na Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Vilikuwa vifanyike lini?

SHAHIDI: Kabla ya Uchaguzi wa mwaka jana.

WAKILI WA SERIKALI: Ni hayo tu kwa sasa Mheshimiwa Jaji.

WAKILI MTOBESYA: Asante Mheshimiwa Jaji. Nitaomba niendelee kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza.

WAKILI MTOBESYA: Ni sahihi shahidi wewe ulikuwa ni sehemu ya waliokuwa wanahusika na upelelezi wa kesi hii?

SHAHIDI: Ni sahihi.

WAKILI MTOBESYA: Ni sahihi kuwa baada ya kupokea maelezo kwa DCI Boaz mkafungua jalada?

SHAHIDI: Ni sahihi.

WAKILI MTOBESYA: Mweleze Mheshimiwa Jaji ni lini mlifungua jalada.

SHAHIDI: Yalikuwa majalada mawili. La upelelezi na kesi.

WAKILI MTOBESYA: Mweleze Mheshimiwa Jaji.

SHAHIDI: Lilifunguliwa jalada la uchunguzi.

WAKILI MTOBESYA: Uchunguzi au upelelezi?

SHAHIDI: Yote ni yaleyele. Labda useme unataka jalada gani.

WAKILI MTOBESYA: Wewe ndiye unayetoa ushahidi.

SHAHIDI: Sawa. Mwanzo lilifunguliwa jalada la uchunguzi wa kula njama. Ilikuwa Julai mwaka jana.

WAKILI MTOBESYA: Yote mawili mlifungua kwa pamoja au tofauti?

SHAHIDI: Kuna utaratibu wa kiupelelezi. Labda kwa sababu hujawa mpelelezi ndiyo maana unahangaika. Kuna jalada la awali la uchunguzi lakini unapopata taarifa unafungua jalada la kesi ya kula njama lilifunguliwa na Mkaguzi wa Polisi Msaidizi anaitwa Swila.

WAKILI MTOBESYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kabla hujawakamata watuhumiwa mlikuwa mmekusanya taarifa zipi kwa wakati huo.

SHAHIDI: Taarifa za kutaka kuwadhuru viongozi wa Serikali, kufanya maandamano yasiyo na kikomo, taarifa za kukata miti na kufanya uporaji, magari yasipite na kutaka nchi isitawalike.

WAKILI MTOBESYA: Kwa hiyo hizo taarifa ndiyo zilitengeneza kosa la kula njama?

SHAHIDI: Sahihi.

WAKILI MTOBESYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji hizo taarifa mlizipata kabla au baada ya kumchukua maelezo mshitakiwa wa pili.

SHAHIDI: Kabla.

WAKILI MTOBESYA: Kabla ya kesi ndogo unakumbuka ulisema Urio aliwapatia taarifa kuwa vijana wamepatikana? Unakumbuka ulisema tarehe ngapi?

SHAHIDI: Ilikuwa tarehe nne mwezi wa saba mwaka jana (2020).

WAKILI MTOBESYA: Wakati unaelezea (kusoma) unakumbuka kielelezo ulipata wasaa wa kujua Urio alishiriki vipi katika suala hili?

SHAHIDI: Sijaelewa vizuri.

WAKILI MTOBESYA: Statement hii ambayo unasema uliandika unakumbuka Urio alishiriki namna gani?

SHAHIDI: Naomba Jaji anisomee anapo parejea.

JAJI: Labda tuwekee ushiriki wa Urio ulikuwa vipi.

SHAHIDI: Urio ameshiriki kwa kuwatafuta vijana, ameshiriki kuwapatia nauli na ameshiriki kutafuta vijana waliofukuzwa Jeshi.

WAKILI MTOBESYA: Umesema kwenye maelezo alifanya hayo tarehe ngapi?

SHAHIDI: Sikumbuki tarehe.

WAKILI MTOBESYA: Sasa nije kwenye maelezo uliyoyachukua. Kwa ajili ya kumbukumbu unakubaliana na mimi kuwa kuna namna tatu za kuchukuliwa maelezo? Kwa anateyetaka kuchukuliwa maelezo kuomba karatasi na kalamu na kuandika mwenyewe. Pili kwa anayehojiwa kuongozwa. Tatu kwa njia ya maswali na majibu.

SHAHIDI: Mimi nilitumia maswali na majibu.

WAKILI MTOBESYA: Naomba niishie hapa.

Anaingia Wakili Johna Mallya.

WAKILI MALLYA: Naomba kielelezo (statement).

Mahakama inampatia John Mallya

WAKILI MALLYA: Una simu ya mkononi?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Unaweza kututajia IMEI namba ya simu yako?

SHAHIDI: Hapana. Siwezi.

WAKILI MALLYA: Kwanini?

SHAHIDI: Sijaamua kuishika (kuuikariri).

WAKILI MALLYA: Una ya mtu yeyote wa karibu yako unayoikumbuka?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI MALLYA: Sasa katika maelezo ya Adam alikutajia IMEI namba kutoka wapi?

SHAHIDI: Alikuwa na kikaratasi.

WAKILI MALLYA: Ulizungumza kwamba mshtakiwa alikuwa na kikaratasi?

SHAHIDI: Sikuzungumza.

WAKILI MALLYA: Ni sahihi unapoandika maelezo unaandika kwa usahihi kabisa?

SHAHIDI: Sahihi kabisa.

WAKILI MALLYA: Kwa uelewa wako unapotaka sheria mbele mwaka unatajwa. Maana ya kuwa na miaka katika Sheria.

SHAHIDI: Mimi siyo mwanasheria.

WAKILI MALLYA: Nafahamu wewe siyo mwanasheria ila umeandika mwenyewe vifungu vya Sheria ili mtu ajue haki yake.

Ndiyo: Nafahamu. Sasa unatoa somo?

WAKILI MALLYA: Kwa hiyo wewe unaweza kuandika mwaka wowote tu?

SHAHIDI: Am not aware of it.

WAKILI MALLYA: Kwa hiyo wewe unaweza kuandika Sheria na mwaka ukaweka wowote tu?

SHAHIDI: Hapana. Naweka na Sheria.

WAKILI MALLYA: Na mwaka kama imefanyika amendment zake? Sasa kwa maelezo hayo uliyoshika tusomee hapa…

SHAHIDI: Cap 20 REV 2018.

WAKILI MALLYA: Sasa hiyo Sheria hakuna. Wewe umechukua maelezo ya Onyo kwa Sheria ambayo haipo.

WAKILI MALLYA: Unasemaje kwa hilo?

SHAHIDI: Hiyo ni typing error. Kwa sababu imechapwa. Ile niliyoandika kwa mkono wangu huenda sikuandika hivi.

WAKILI MALLYA: Wakati unaisoma hapa mahakamani ulisema hapa kwamba hii siyo au ulikariri ukawa unaisoma tu hapa?

SHAHIDI: Kwenye eneo hili Onyo chini ya Kifungu Cap Rev 2002 badala ya kusomeka 2018.

WAKILI MALLYA: Kwa hiyo ulipaswa kusomeka vinginevyo siyo hiyo?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Ushawahi kusikia kiongozi wa Polisi Liberatus Barrow aliuwawa?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Aliuawa?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Waliomuua walikamatwa. Ndiyo?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Walishitakiwa na makosa gani?

SHAHIDI: Mauaji.

WAKILI MALLYA: Lakini kumdhuru Sabaya ni ugaidi?

SHAHIDI: Kuleta vurugu kwenye masoko, kukata miti barabarani, kuzia magari yasipite ni vitendo vingeleta hofu na wasiwasi. Vitendo hivi vinaashiria ni vitendo vya ugaidi.

WAKILI MALLYA: Umerudi viongozi sana. Ukimtoa Lengai Ole Sabaya, kiongozi mwingine nani?

SHAHIDI: Ni maelezo ya Adam Kasekwa, siyo ya kwangu.

WAKILI MALLYA: Ulipomkamatia Adamoo Moshi na kilichokufanya usichukue maelezo Moshi ni sababu zipi?

SHAHIDI: Sababu za kiupelelezi.

WAKILI MALLYA: Wakati unatoka Moshi ulipitia njia ipi? Ya Chalinze au Bagamoyo?

SHAHIDI: Msata.

WAKILI MALLYA: Ukitoka Msata kwenda Central kuna Mbweni na Oysterbay. Kwanini uliamua kwenda Central?

SHAHIDI: Sababu za maelezo na pili ndipo kesi ilipofunguliwa.

WAKILI MALLYA: Wewe kwa sasa ni RPC Kinondoni. Je unafahamu kuwa Kinondoni inajitegemea?

SHAHIDI: Ndiyo. Zikiwa chini ya Kanda Maalumu Dar es Salaam.

WAKILI MALLYA: Ulieleza Mahakama kwanini huyu achukuliwe maelezo Temeke mkoa mwingine wa Kipolisi na kwanini hakusafirishwa kama wenzie kuja Mkoa wa Ilala?

SHAHIDI: Hapana. Sikueleza.

WAKILI MALLYA: Umesema yalifunguliwa majalada mawili?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Nani alifungua hayo majalada?

SHAHIDI: Inspector Swila.

WAKILI MALLYA: Umemtaja Sabaya. Alikuwa Mkuu wa Wilaya wa wapi vile?

SHAHIDI: Hai.

WAKILI MALLYA: Je, pale Hai pana Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Je, Kilimanjaro kuna Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MALLYA: Ni hayo tu.

Jaji anaomba BREAK ya saa moja. Mahakama itarejea saa 7:20

Saa 7:38 alasiri Mahakama imesharejea. Kila mmoja amekaa mahali pake. Wakili Robert Kidando anaomba kumtambulisha Wakili Nasorro Katuga.

JAJI: Nilipo- break tulikuwa tumemaliza maswali ya dodoso ya wakili wa mshitakiwa wa pili. Nipo sahihi?

Mawakili wa pande zote mbili wanasema ‘NDIYO.’

JAJI: Namruhusu wakili wa mshtakiwa wa tatu aendelee.

Anaingia Wakili Matata.

WAKILI MATATA: Shahidi ni sahihi kwamba maagizo ya kushughulika na kesi hii ulipewa na DCI?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MATATA: Ni kweli kwamba Urio ndiye aliyekupa taarifa kuwa kuna makomandoo ametafuta kuwapeleka kwa Mbowe kwa kusaidiana naye kutenda uhalifu?

SHAHIDI: Kweli.

WAKILI MATATA: Urio huyo huyo ndiye alikupa taarifa kwamba alikuwa anatoa fedha za kuwezesha makomandoo?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MATATA: Na ukasema mambo hayo yote yakifanyika mwaka jana kuanzia mwezi wa saba?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MATATA: Nnitakosea nikisema Mbowe kuwapa fedha makomandoo yalifanyika mwaka jana?

SHAHIDI: Kweli.

WAKILI MATATA: Utakubaliana na mimi Mbowe amekamatwa mwaka huu mwezi wa saba?

SHAHIDI: Kweli.

WAKILI MATATA: Amekamatwa akiwa Mwanza.

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MATATA: Mbowe alishiriki uchaguzi mwaka jana akigombea Jimbo la Hai?

SHAHIDI: Kweli.

WAKILI MATATA: Kwa nyakati tofauti Mbowe amekuwa nchini?

SHAHIDI: Kweli.

WAKILI MATATA: Leo umeieleza Mahakama kwamba hamkumkamata kwa sababu mlikuwa mnafanya upelelezi na uchunguzi wa ki- forensic?

SHAHIDI: Kweli.

WAKILI MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba huo uchunguzi umeisha lini?

SHAHIDI: Nimeeleza Mahakama.

WAKILI MATATA: Utakubaliana na mimi Kwamba huo uchunguzi wa ki- forensic ulikuwa unahusu nini?

SHAHIDI: Nimeeleza.

WAKILI MATATA: Wakati unahojiwa na wakili umeeleza huo uchunguzi wa ki- forensic ulihusisha nini?

SHAHIDI: Nilieleza kwamba ni vifaa vya electronics.

WAKILI MATATA: Nikisema Mbowe mmemkamata Mwanza Julai 21, 2020 kwa sababu la kutaka kufanya kongamano la Katiba nitakuwa nimekosea?

SHAHIDI: Si kweli. Utakuwa umekosea.

WAKILI MATATA: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.

JAJI: Wakili wa mshtakiwa wa nne?

Anaingia Kibatala

PETER KIBATALA: Asante Mheshimiwa Jaji.

WAKILI KIBATALA: Shahidi katika statement uliyosoma kuna mambo yanamgusa mshtakiwa wa nne?

SHAHIDI: Ni sahihi.

WAKILI KIBATALA: Kwanini huwa tunataka kifungu mahususi kinachompa haki zake mshitakiwa katika Caution Statement?

SHAHIDI: Ni takwa la kisheria.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo unafahamu kuwa kuna matakwa yake ili zoezi likamilike kuwa la kisheria?

SHAHIDI: Ni sahihi.

WAKILI KIBATALA: Unafahamu kuwa unapokosea kifungu cha Sheria jambo lote linakufa?

SHAHIDI: Inategemea.

WAKILI KIBATALA: Ukikosea Sheria yenyewe?

SHAHIDI: Inaweza kuwa fatal.

WAKILI KIBATALA: Sheria katika kielelezo P1 imepatiwa au imekosewa?

SHAHIDI: Slip of the pen.

WAKILI KIBATALA: Hiyo slip of the pen mpaka mawakili wanakuongoza kwa mujibu wa “Oxygen Principle” kwamba turekebishe hata kwa pen?

JAJI: Fafanua hiyo “Oxygen Principle” aweze kuelewa.

WAKILI KIBATALA: Je, ukishawahi kuiomba Mahakama kwamba kuna kuteleza kwa pen turekebishe?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Unafahamu kuwa kukiri kwa mshitakiwa kunapaswa kuongozane na vitu vingine?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Je, umetaja hapa Mahakamani vielelezo gani vingine kama vinaunga mkono kukiri kwa mshtakiwa wa pili?

SHAHIDI: Maelezo yake.

WAKILI KIBATALA: Ndiyo hayo maelezo yanatakiwa yafungwe mkono na premises zingine. Tuorodhesheee.

SHAHIDI: Maelezo ya Luteni Denis kuhusu kukata miti na kutaka kufanya vurugu.

WAKILI KIBATALA: Umemweleza Jaji sehemu yoyote kwamba ulienda huko Morogoro mpaka Iringa kuona miti uliyotakiwa kukatwa?

SHAHIDI: Hapana. Wala sijaenda.

WAKILI KIBATALA: Umetaja maandamano yalitakiwa kufanyika wapi hadi wapi?

SHAHIDI: Hapana. Sijasema.

WAKILI KIBATALA: Kuhusu Mwanza pia maandamano yalitakiwa yaanze point gani hadi point gani tarehe fulani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

WAKILI KIBATALA: Kuhusu Kilimanjaro ulitaja sehemu yoyote?

SHAHIDI: Hapana. Sijamwambia.

WAKILI KIBATALA: Umemtajia Mheshimiwa Jaji maandamano yalitakiwa kuanzia wapi hadi wapi na ajenda ya maandamano?

SHAHIDI: Nilisema ni ili kuonekana nchi haitawaliki.

WAKILI KIBATALA: Kuna sehemu umemwambia Jaji tarehe ya maandamano?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Umezungumzia kuwa Aliplan kuwepo yeye personally?

SHAHIDI: Sikusema.

WAKILI KIBATALA: Ulitaja vituo vilivyotakiwa kuchomwa?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilivitaja.

WAKILI KIBATALA: Ndiyo mwambie Mheshimiwa Jaji ulitaja wapi na wapi.

SHAHIDI: Nakumbuka nilitaja Big Bon Kariakoo, Big Bon Sinza na Total Morroco.

WAKILI KIBATALA: Unakumbuka upo chini ya kiapo? Maana kazi yangu ni kuuliza maswali. Suala la uongo au la wanajua watu wengine.

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Je, baada ya planning huko Moshi, washitakiwa walifanikiwa kuja Dar es Salaam kuja kutekeleza hilo?

SHAHIDI: Walikuwa baada ya kuwakamata.

WAKILI KIBATALA: Nauliza mshitakiwa wa nne alitoa maagizo Moshi akaja Dar es Salaam kuja kutekeleza hayo maagizo?

SHAHIDI: Dar es Salaam tuliwakamata kabla hawajatekeleza.

WAKILI KIBATALA: Mliwakamata na nini ambacho mtu anaweza kukihusisha na ulipuaji wa vituo vya mafuta?

SHAHIDI: Kwa upande wa kuchoma vituo vya mafuta sikuwakamata na kitu chochote.

WAKILI KIBATALA: Uliwakamata na kifaa gani kinachohusisha kukata miti?

SHAHIDI: Sikuwakamata na kifaa chochote.

WAKILI KIBATALA: Mshitakiwa wangu wa nne ulimkamata na kipeperushi cha maandamano?

SHAHIDI: Hapana.
WAKILI KIBATALA: Wewe ni polisi mzoefu wa miaka 18 ya upelelezi kazini. Najua siyo mwanasheria ila unasimamia Sheria. Je, unafahamu mtu anapokiri anatakiwa kukiri kila kipemgele anachoshitakiwa?

SHAHIDI: Ndiyo. Nafahamu.

WAKILI KIBATALA: Ulizungumza chochote kuhusu mshitakiwa Mbowe kuwapo Morogoro kati ya tarehe moja Mei na 20 Agosti 2020?

SHAHIDI: Sikuzungumza.

WAKILI KIBATALA: Ulizungumza katika ya tarehe moja Mei 2020 na 20 Agosti 2020 kuwa washitakiwa watatu walikuwa Arusha?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilizungumza ila siyo leo.

WAKILI KIBATALA: Kwa ufahamu wako kama mpelelezi mkuu umewahi kugundua kuwa Freeman Mbowe na watuhumiwa wenzake Mkoani Morogoro?

SHAHIDI: Na Mbowe. Hapana.

WAKILI KIBATALA: Waliwahi kukutana mkoa wa Arusha?

SHAHIDI: Sijafahamu.

WAKILI KIBATALA: Waliwahi kukutana mkoani Dar es Salaam?

SHAHIDI: Walikuja Dar es Salaam walikuwa pamoja. Tarehe 26 Julai 2020.

WAKILI KIBATALA: Hayo yapo katika maelezo ya kukiri uliyoyasoma?

SHAHIDI: Yapo. Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Naomba Mahakama nimkabidhi P1 anitafutie eneo hilo.

JAJI: Tutajie ukurasa.

SHAHIDI: “Kesho yake tulirudi Dar es Salaam, tukiwa na Mheshimiwa Mbowe na wanachana wengine ambao sikuwafahamu”. That means walikutana.

WAKILI KIBATALA: Sitaki tafsiri yako. Tusomee ambao mshtakiwa amesema walikutana.

JAJI: Nafikiri kuna sehemu hamkutani. Nafikiri anatafsiri kuwa kuna wakati walikuwa wote Dar es Salaam. We unamaanisha nini?

WAKILI KIBATALA: Hati ya Mashitaka inasema walikuwa wamekaa kikao. Nitafutie alipokiri kuwa walikaa kikao.

SHAHIDI: Hiyo specifically kikao sikueleza.

WAKILI KIBATALA: Ohoo! Sasa umeelewa!

WAKILI KIBATALA: Sheria inayounda shitaka unatakiwa kuitamka kikamilifu ili haki za mshitakiwa ziwe zimekamilika. Unafahamu?

SHAHIDI: Ndiyo nafahamu.

WAKILI KIBATALA: Je, unafahamu sub section mbili zote zinazozungumzia hilo?

SHAHIDI: Hiyo ni mpaka niperuzi.

WAKILI KIBATALA: Ahaaa! Sawa ngoja nimpatie sheria.

Jaji anatabasamu halafu anamuuliza Kibatala “Sasa atafahamu vipi kuwa ni yenyewe?”

WAKILI KIBATALA: Nawapa kwanza kaka zangu mawakili wa Serikali waithibitishe.

Wakili wa Serikali anasema ndiyo yenyewe.

WAKILI KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo maelezo ya onyo ulitaja kifungu cha sheria cha kwanza na cha pili (subsections).

SHAHIDI: Subsection sikutaja.

WAKILI KIBATALA: Kwa ufahamu wako wewe kutokutaja subsection zinakuja zimeathirika au azijaathirika?

SHAHIDI: Hiyo ni curable irregularity.

WAKILI KIBATALA: Ulitoa ufafanuzi huo kwa Jaji ili afanye hiyo cure?

SHAHIDI: Sikutoa.

WAKILI KIBATALA: Hawa washitakiwa wawili wanashitakiwa kushiriki vitendo. Mkutano wa kuongea vitendo vya kigaidi. Ndiyo hati ya mashitaka inavyosema.

SHAHIDI: Sahamani naomba niione.

WAKILI KIBATALA: Ahaaaa! Sawa. Hii hapa.

Kimya Kinatawala wakati shahidi anasoma.

Wakili wa Serikali: Sahamani Mheshimiwa Jaji na sisi kabla hajajibu tunaomba tuione.

WAKILI KIBATALA: Ohooo! Sawa Mheshimiwa Jaji. Wana haki hiyo.

Wakili wa Serikali: Ndiyo yenyewe Mheshimiwa Jaji.

SHAHIDI: Ndiyo yenyewe.

WAKILI KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa iwapo alishiriki mkutano ugaidi ilikuwa sehemu ya maelezo yako ya onyo.

SHAHIDI: Nilimuonya kwa vitendo.

WAKILI KIBATALA: Ulimuonya kwa meeting au hukuonya?

SHAHIDI: Sikumuona.

WAKILI KIBATALA: Terrorists Meeting ni shitaka namba ngapi?

SHAHIDI: Namba nne.

WAKILI KIBATALA: Ndilo ambalo hukumuonya Adamoo?

SHAHIDI: Ndiyo sikumuonya.

WAKILI KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ulimuonya kwa kupatikana na mali.

SHAHIDI: Kwa vitendo vya kigaidi.

WAKILI KIBATALA: Twende shitaka la tano kwa kupatikana kwa hiyo mali. Si bado tunakubaliana kuwa kunapaswa kuungama na mambo mengine? Si tuna kubaliana?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ulifanya forensic ya DNA au finger prints kuwa ni kweli ilikuwa chini ya umiliki wake.

SHAHIDI: Hapo unazungumzia kumiliki?

WAKILI KIBATALA: Ulizungumzia kuhusu kwamba umefanya uchunguzi wa finger prints?

SHAHIDI: Hapana. Sikufanya finger prints.

WAKILI KIBATALA: Hii Kesi tangu ni lini ianze kuanzia kuwakamata na muanze upelelezi?

SHAHIDI: Miezi nane.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo kwa miezi minane hamjawahi kufanya finger prints?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Unakubaliana na mimi kuwa DNA ni njia ya kisasa ya kuthibitisha umiliki, na jinai?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Umezungumzia chochote Kuhusu DNA analysis?

SHAHIDI: Hapana Mheshimiwa.

WAKILI KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Jaji kuwa Adamoo amepata wapi hii bunduki?

SHAHIDI: Adamoo hakusema.

WAKILI KIBATALA: Nikiangalia kielelezo cha mahojiano nitaona hilo swali?

SHAHIDI: Hapana. Nilimuuliza kama mimi tu.

WAKILI KIBATALA: Wakati anakamatwa Adamoo alikuambia walikuwa na Moses Lijenje. Je, alikuambia wakati wa mahojiano ya kisheria au nje ya kisheria?

SHAHIDI: Kivipi?

WAKILI KIBATALA: Uliipata baada ya kumhoji Adamoo?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Ulimuhoji kwa mdomo wa kwa maandishi?

SHAHIDI: Kwa mdomo.

WAKILI KIBATALA: Unakubaliana na mimi kwamba hicho kitendo cha kumuhoji Adamoo hutakiwi kukifanya kwa mujibu wa sheria?

SHAHIDI: Nilikuwa namhoji kupata upelelezi.

WAKILI KIBATALA: Ndiyo unakubaliana na mimi kwa mujibu PGO ulipaswa kwanza umpe haki zake mshitakiwa wa pili wakati mpo Moshi?

SHAHIDI: Usichanganye vitu. Miye namuhoji unachosema wewe.

WAKILI KIBATALA: Kwamba unakubaliana nami kuwa kuna mahojiano yalifanyika Moshi?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilifanya mahojiano ya mdomo.

WAKILI KIBATALA: Lakini mliwasafirisha kutoka Moshi kuja Dar es Salaam kuja kuwahoji?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Ilikuwa muda gani?

SHAHIDI: Muda ule ule.

WAKILI KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji pia kama ulimhoji Mohammed Ling’wenya akiwa Moshi kuhusu Moses Lijenje.

SHAHIDI: Ndiyo. Nilimhoji pia na maelezo ni yale yale.

WAKILI KIBATALA: Nimesikia kuwa leo umemtaja Kakobe kuwa ndiyo Moses Lijenje.

SHAHIDI: Kwa maelezo yao ndiyo wamesema hivyo.

WAKILI KIBATALA: Shahidi nakukabidhi maelezo hayo ya kielelezo cha P1 kuwa Adamoo anasema Kakobe ndiyo Moses Lijenje.

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji sikumbuki kama niliandika.

JAJI: Kibatala umemwambia atumie muda mwingi uwezekanavyo kutafuta hilo. Nakukumbusha muda ni wa Mahakama.

WAKILI KIBATALA: Mheshimiwa Jaji samahani sana nilipitiwa. Kama ningekuwa mwangalifu nimgesema kwa ruhusa ya Mahakama.

WAKILI KIBATALA: Nitafutie sehemu katika maelezo kuwa mshitakiwa wa pili kuwa amekiri bastola ni ya kwake.

SHAHIDI: Hakuna Mheshimiwa Jaji.

WAKILI KIBATALA: Nitafutie katika maelezo ambayo mshtakiwa amekiri kuwa bastola hiyo alitaka kutumia kumdhuru Sabaya, kutumia kwenye maandamano au kutumia kukata miti.

SHAHIDI: Hilo Mheshimiwa Jaji hakuna.

WAKILI KIBATALA: Nitafutie mstari au aya yoyote ambayo mashtakiwa wa pili anasema kuwa uniform za JWTZ walitaka kuzitumia kwa ajili ya ugaidi.

SHAHIDI: Hakuna kwa sababu mshitakiwa sikumkuta na uniforms. Uliza maswali sensible bhana!

Mawakili wa utetezi wote wananyanyuka.

WAKILI KIBATALA: No! No! No! No! Kaeni. Mwacheni!

WAKILI KIBATALA: Nataka ukama ksehemu katika maelezo kuna sehemu umesema kuhusu uniform.

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Nina swali la Lijenje la kijinga ila nivumilie. Je kuna sehemu kuna maelezo ya nyongeza kuhusu kuchukua sampuli za miandiko?

SHAHIDI: Hatukuwa na haja hiyo.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo mshitakiwa wa pili hakuna anapozungumza kuhusu mwandiko.

SHAHIDI: Hakuna.

WAKILI KIBATALA: Unaona umeokoa muda sasa?

WAKILI KIBATALA: Iliwachukua amuda gani kuwashitaki wakina Malima mpaka mkagundua kuwa hakuwa na ushahidi wa kutosha?

SHAHIDI: Tuliwashitaki mwisho mwa mwaka jana.

WAKILI KIBATALA: Ndiyo mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa ulichukua muda gani kuwa mliwakamata mpaka mkaja mkagundua kuwa mmekosea kuwashitaki kwa ugaidi.

SHAHIDI: Ulichukua miezi nane.

WAKILI KIBATALA: Ikumbushe Mahakama mteja wangu tangu mumkamate ana muda gani vile?

SHAHIDI: Kama miezi minne.

WAKILI KIBATALA: Fedha zilitumwa katika ushahidi wa mshitakiwa wa nne kwenda kwa watu wengine.

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Na rekodi za SMS za mshitakiwa zipo sehemu ya ushahidi? Nazungumzia mshitakiwa wa nne.

SHAHIDI: Hapana. Hakuna.

WAKILI KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa ulichukua devices za watoto wa Mheshimiwa Mbowe.

SHAHIDI: Ndiyo nilichukua.

WAKILI KIBATALA: Mpaka leo unazo?

SHAHIDI: Waliziadai nikatoa maelekezo.

WAKILI KIBATALA: Mpaka leo unaongea wamerudishiwa au bado?

SHAHIDI: Sijui. Nilitoa maelekezo.

WAKILI KIBATALA: Lakini wewe ndiyo mkuu wa uangalizi.

Shahidi anakasirika na anasema “SIYO MWANGALIZI”

WAKILI KIBATALA: Umeeleza m,akarani kuhusu kumtaarifu Sabaya?

SHAHIDI: Hiyo sikusema.

WAKILI KIBATALA: Je, hapa Mahakamani umetoa taarifa kuwa uliwapa taarifa kuwa kuna jambo zito kama hilo kwenye Kamati za Ulinzi na Usalama?

SHAHIDI: Hapana. Sikuwapa.

WAKILI KIBATALA: Je, wewe binafsi umeshawahi kumuhabarisha Rais Samia Suluhu kuhusu kesi hii?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Je, una taarifa kwamba washitakiwa wameshafungwa na kuchukuliwa hata kabla ya kesi kuanza?

SHAHIDI: Una maana gani kuuliza swali kama hilo?

WAKILI KIBATALA: Maana najua mimi. Wewe jibu swali.

SHAHIDI: Sijui.

WAKILI KIBATALA: Umeongelea hapa kuhusu ya Battle Confusion.

SHAHIDI: Mimi siyo practioner.

WAKILI KIBATALA: Wewe Mpaka unamhoji mshitakiwa ambaye na rekodi ya kuumwa ugonjwa kama huo?

SHAHIDI: Alikuwa ananijibu vizuri na kwamba alikuwa ameshapona.

WAKILI KIBATALA: Umesema akiwa anaondoka Chalinze yeye akijua anaenda Moshi kufanya VIP Protection?

SHAHIDI: Mheshimiwa labda sasa tusomewe.

Kibatala anasoma “Nilienda hadi nyumbani nikaambiwa kuna kazi ya VIP Protection, ambayo anajua zaidi Luteni Urio.”

SHAHIDI: Ndiyo, lakini siyo maelezo yote.

WAKILI KIBATALA: Tafuta katika statement hiyo mshtakiwa anaposema kuwa Urio alikuwa anamtafuta kwa vitendo vya ugaidi.

SHAHIDI: Hakuna sambayo Adamoo amesema hayo.

WAKILI KIBATALA: Hata huko mbele kuna sehemu amesema Urio alimtafuta kwa ajili ya kutenda vitendo vya ugaidi?

SHAHIDI: Hapana, lakini walikutana na Mbowe.

WAKILI KIBATALA: Sijkuuiza kuhusu Mbowe. Nimekuuliza kuhusu Urio.
SHAHIDI: Sasa usinibane kuniuliza maswali ambayo siwezi kutoa maelezo. Alikuwa anaficha ficha.

WAKILI KIBATALA: Wewe ndiye umesema Urio alikuwa willing informer. Leo amekuwa mtu wa kufichaficha tena?

SHAHIDI: Usiniulize kuhusu URio mimi.

WAKILI KIBATALA: Kwanini sasa nisikuulize kuhusu Urio? Wewe ndiye umemleta Urio Mahakamani.

JAJI: Kibatala unamchanganya sana shahidi. Kumleta amana pia kumbeba.

WAKILI KIBATALA: Sahamani Mheshimiwa Jaji kama kaelewa hivyo.

WAKILI KIBATALA: Unakubaliana mpaka wanaenda Moshi mlinzi wa Mheshimiwa Mbowe alikuwa ni Willy?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Mshitakiwa wa pili mpaka anaenda Moshi Julai 26, 2020, wakati mashitaka yenu yanasema tangu mwezi wa tano alikuwa ameshiriki vitendo vya ugaidi?

SHAHIDI: Mie sijui hayo.

WAKILI KIBATALA: Unakubaliana na mimi kwamba mpaka mshitakiwa wa pili anaenda Moshi alikuwa hajui mambo ya ugaidi.

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Sehemu inayosema kwamba tulienda naye kwenye kikao cha chama wakarudi. Je, kuna sehemu inafafanua kuwa walirudi wapi?

SHAHIDI: Hapana. Hakuna, ila mwenye akili timamu anajua walirudi wapi.

WAKILI KIBATALA: Mimi sina akili timamu.

WAKILI KIBATALA: Kitendo cha Mkuu wa Wilaya kushusha bendera za Chadema inaruhusiwa kisheria?

SHAHIDI: Hapana. Hairuhusiwi.

WAKILI KIBATALA: Kwamba kufanya preventive measures kwa kuzuia mtu kushusha bendera za Chadema ni ugaidi huo?

SHAHIDI: Nimeshatoa maelezo kuwa jinai haiwezi kuzuiwa na jinai.

WAKILI KIBATALA: Jibu swali langu. Sasa swali langu halikuwa hivyo.

WAKILI KIBATALA: Je, kitendo cha kuzuia kwamba wasishushe mbele ya Mungu ni ugaidi?

SHAHIDI: Halikuwa hivyo.

WAKILI KIBATALA: Hapa kuna maelezo kuwa “Ametisha wapiga kura, amefanya hujuma na kuitisha wapiga kura, ikiwemo kuiba kura.” Haya umeyaandika wewe. Je, uliyaamini au huyaaamini haya maneno?

SHAHIDI: Mimi sijui. Sasa inaweza kuwa haijaamini.

WAKILI KIBATALA: Tutakuwa tunahoji wengine kama wewe uliyeandika maelezo huyaaamini. wao wametoa wapi nguvu ya kuleta Mahakamani?

WAKILI KIBATALA: Kuna sehemu imesema kuhusu spray ya sumu. Je, kwenye statement umezungumzia?

SHAHIDI: Mheshimiwa sijazungumzia.

WAKILI KIBATALA: Huyo ambaye alikuwa ampatie Ling’wenya spray ya sumu umemzungumzia hapa huyo mtu?

SHAHIDI: Sijamzungumzia. Lakini upelelezi unaendelea.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo kuna siku unaweza kutuletea mtuhumiwa mwingine?

SHAHIDI: Ndiyo. Inawezekana.

WAKILI KIBATALA: OK. Mwenye Mahakama anasikia unachosema.

WAKILI KIBATALA: Kuna sehemu inasehema “Baada ya kumfikisha Mheshimiwa nyumbani kwake” katika hiyo statement uliyorekodi ametajwa au hajatajwa?

SHAHIDI: Huyo atakuwa ni Mheshimiwa Mbowe.

WAKILI KIBATALA: Nakuuliza hapo kwenye statement hapo kwenye huyo Mheshimiwa ametajwa?

SHAHIDI: Hajatajwa.

WAKILI KIBATALA: Tulikuwa na Mohammed Je hapo kwenye statement Mohammed ametajwa kuwa ni Mohammed nani?

SHAHIDI: Sijataja.

WAKILI KIBATALA: Kitendo cha kwamba tulipewa pesa kwenda kununua nguo ili kumpokea Tundu Lissu, Je, kutumia hizo pesa kununua nguo ni kosa la jinai?

SHAHIDI: Lengo halikuwa hilo.

WAKILI KIBATALA: Mimi sitaki lengo. Nauliza mlichoandika hapa.

SHAHIDI: Lengo haswa lilikuwa ni kufanya uhalifu. Hii ilikuwa kama incentives.

WAKILI KIBATALA: Hiyo incentives ndiyo walipanga kununua nguo?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Kuna sehemu ambayo amekiri kwamba hiyo pesa ilikuwa kwa ajili ya kutenda ugaidi.

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: “Kesho tukaenda kumpokea Lissu. Mimi na Mohammed.” Je huyo Mohammed ametajwa ni nani?

SHAHIDI: Sikutaja ila atakuwa ni Mohammed Ling’wenya.

WAKILI KIBATALA: Ndiyo ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuwa uligundua kuwa Mohammed Ling’wenya?

SHAHIDI: Hapana sikusema.

WAKILI KIBATALA: Na hii 78,000 ya nauli inajumuishwa kama pesa ya kufadhili ugaidi?

SHAHIDI: Inawezekana ikawemo.

WAKILI KIBATALA: Wewe upelelezi wako uligundua nini?

SHAHIDI: Imo.

WAKILI KIBATALA: Kuna mahala mshitakiwa anasema pesa ilitumika kwenda kununua spray ya sumu.

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kuna mahala popote mshitakiwa wa pili anasema hiyo pesa alitumiwa na Mbowe kwa ajili ya kufadhili ugaidi?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kuna mahala popote mshitakiwa anasema alipewa pesa na Mbowe kwa ajili ya kufadhili maandamano?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kuna mahala popote mshitakiwa alikiri kuwa alifika Arusha?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kuna mahala popote kwamba mshitakiwa anakiri alipewa pesa kwenda kumdhuru Sabaya?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kuna mahala mshitakiwa wa pili amekiri kuwa alishawahi kwenda Arusha?

SHAHIDI: Kwenye maelezo haya hakuna sehemu kama hiyo.

WAKILI KIBATALA: Katika maelezo mshitakiwa alikuwa na kete za madawa ya kulevya 52. Je, yanatisha humu?

SHAHIDI: Sikutaja 52.

JAJI: tujielekeze katika hii kesi.

WAKILI KIBATALA: Katika hayo madawa DNA analysis ilifanyika?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Finger prints ilifanyika?

SHAHIDI: Haikufanyika.

WAKILI KIBATALA: Huyu Moses Lijenje yupo wapi tunapomzungumza leo?

SHAHIDI: Sifahamu.

WAKILI KIBATALA: Hata kama amekufa hufahamu?

SHAHIDI: Sifahamu.

WAKILI KIBATALA: Mpaka wakati huu unapozungumza hujawahi kuhangaika kujua yupo wapi?

Hapana: Sijahangaika.

WAKILI KIBATALA: Ulishawahi kuuliza Jeshi kuhusu uwepo wa Moses Lijenje?

SHAHIDI: Sasa mtu kafukuzwa Jeshi litajuaje?

WAKILI KIBATALA: Ndiyo nijibu swali langu hata kama la kijinga.

JAJI: Halipaswi kuwa swali la kijinga. Anaweza kullipuuza au mimi nisiandike nikijua la kijinga?

WAKILI KIBATALA: Asante Mheshimiwa Jaji. Ni la msingi.

WAKILI KIBATALA: Shahidi uliwashirikisha Jeshi kuhusu Lijenje?

SHAHIDI: Ndiyo. Tuliwashirikisha.

WAKILI KIBATALA: Nimeona umezungumzia kuhusu uniforms za Jeshi. Una utaalamu wa kujua uniform za Jeshi?

SHAHIDI: Hata nikiona naweza kujua hili Jeshi la wapi. Yemen, Nepal au India.

WAKILI KIBATALA: Je, unafahamu kuwa nguo za Jeshi zimetungiwa kanuni?

SHAHIDI: Hilo sifahamu.

WAKILI KIBATALA: Kama hufahamu kanuni unajua wapi mambo ya nguo za Jeshi?

SHAHIDI: Kwa kuona.

WAKILI KIBATALA: Kwa kuwa leo upo ngoja nikuulize. Je, unajua kuwa mtuhumiwa wa kwanza alitekwa kwenye daladala akiwa na maafisa wa zamani wa Jeshi, nyuma yake na mbele yake akawekwa mtu kati. Yeye akaomba wasimdhuru wala wasimpige wakayamalize Polisi?

SHAHIDI: Hayo ya kwako.

WAKILI KIBATALA: Umesema mara ya kwanza mshitakiwa wa kwanza alichukuliwa maelezo akiwa wapi?

SHAHIDI: Chang’ombe.

WAKILI KIBATALA: Unafahamu nini kuhusu kupeleka mshitakiwa Tazara?

SHAHIDI: Mie mambo ya Tazara siyajui.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo tukienda kwenye _Detention Register_tunaweza kukuta kuwa alikuwa Chang’ombe?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Unafahamu Detention Register ili iwe genuine inatakiwa ionekane vipi nje na ndani?

SHAHIDI: Hapana sifahamu.

WAKILI KIBATALA: Kwanini hufahamu na wewe ni afisa wa Polisi kwa muda wa miaka 18?

SHAHIDI: Kuna maswali unataka kunibana na mimi nakwepa.

WAKILI KIBATALA: Mimi kazi yangu ni kuuliza maswali tu. Wenyewe wakikaa wataamua. Tumeambiwa tukuulize kila kitu kwa sababu hatuna uhakika kama utakuja tena.

SHAHIDI: Ndiyo basi unilishe maneno?

WAKILI KIBATALA: Wewe kwa uzoefu wako kuna kesi yoyote ile ambayo mna taarifa jambazai anataka kuvamia benki A, B, C na mkamuacha jambazi azurure mtaa? Ipo?

SHAHIDI: Ndiyo. Ipo.

WAKILI KIBATALA: Umeitolea ushahidi hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kabla ya kumkamata Mbowe katika Kongamano la Katiba Mwanza, mlikuwa mnajua kuwa Mbowe anasafiri nje ya nchi?

SHAHIDI: Ndiyo. Tulikuwa tunajua.

WAKILI KIBATALA: Wewe mtu mzima. Inaingia akilini mtu ana kesi ya ugaidi, mnamepeleleza, mkamruhusu asafiri mpaka arudi mwenyewe?

SHAHIDI: Ndiyo. Inawezekana. Tulikuwa tuna mpelelezi ndani na nje ya nchi.

WAKILI KIBATALA: Ulishawahi kuitaarifu mamlaka zingine nje ya nchi kuwa anayekuja ni gaidi?

SHAHIDI: Hapana. Hakuwa Flight Risk.

WAKILI KIBATALA: Umesikiliza mahojiano ya BBC na Rais Samia?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Rais wa nchi alipokuwa BBC alisema kuwa Freeman Mbowe alichelewa kukamatwa kwa sababu alikimbilia nje ya nchi.

SHAHIDI: Naomba Jaji aniruhusu kujibu hilo swali.

WAKILI KIBATALA: Mimi nahitaji hilo jibu. Labda Mahakama inizuie, lakini mimi nataka unijibu.

Wakili wa Serikali: Objection! Mheshimiwa Jaji naomba tuangalie sheria kama zinaruhusu au kutubana.

Wakili wa Pili wa Serikali: Majibu anayotaka ni kuhusu mahojiano. Aulizwe maswali ambayo yeye yanamhusu.

JAJI: Peter (Kibatala) kwa hoja hizo. Unasemaje?

WAKILI KIBATALA: Mheshimiwa Jaji samahani sana. Tulifungua kesi ya kikatiba namba 21 ya mwaka 2021. Walalamikiwa walikuwa DPP na Mwanasheria Mkuu. Jaji Mgeta akasema hivi: Mahakama yake inafungwa haiwezi kuingilia kesi hiyo, na kama kuna hoja anaomba ziwasiliahwa katika kesi ya jinai inayoendelea Katika Mahakama Kuu.

JAJI: Sasa huyu amekuja kama Executive Order au kama shahidi?

WAKILI KIBATALA: Ikumbukwe Mahakama ipo majaribuni pia kwamba sasa Rais ameshasema.

JAJI: Naona shahidi unam- treat kama shahidi anayekuja kuwakilisha muhimili wakati tuemwapisha kuja kutoa ushahidi kwenye jambo alilolifanya.

WAKILI KIBATALA: Kama hutojali umauzi ule tumekatia rufaa. Mimi ukiniambia hapa siyo mahali pake nilitumia hiyo Statement.

JAJI: Mengine yote unaweza kumuuliza, lakini tusimuilize swali ambalo kasema mtu mwingine.

WAKILI KIBATALA: Nauliza kama forum hapa ikifungwa tukienda kwingine wasiseme hatukuileta hapa.

WAKILI KIBATALA: Hatuwezi kusema kwa hii trial mlango pia umefungwa.

JAJI: Nafahamu kwamba mna mashahidi mnaweza kuwaleta kuwahoji kauli hizo.

WAKILI KIBATALA: Je, shahidi unafahamu kuwa Freeman Mbowe alikimbia nchi kwa kukwepa tuhuma za ugaidi?

SHAHIDI: Hilo sifahamu.

WAKILI KIBATALA: Unakubali kuwa ulikuwapo wakati mnampekua Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Mimi nilikuwa nje tu zoezi lilisimamiwa na Superitendent Mwakabonga.

WAKILI KIBATALA: Ilikuwa saa ngapi?

SHAHIDI: Ilikuwa saa tatu mpaka saa nne.

WAKILI KIBATALA: Kwa ufahamu wako sheria inasemaje kuhusu kupeluliwa usiku?

SHAHIDI: Nikuulize wewe.

WAKILI KIBATALA: Shahidi mbona swali lipo fair?

SHAHIDI: Tunaruhusiwa kupekua hata usiku.

WAKILI KIBATALA: Uliwahi kumkamata na kumpekua Mbowe kabla?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo ni mwaka mmoja.

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI KIBATALA: Unafahamu kuwa Mbowe alikamatwa akiwa ameenda kuendesha Kongamano la Kikatiba? Ile situation report ambayo makamanda wanabadilishana taarifa na makamanda wengine kipolisi inaitwaje?

SHAHIDI: Situational Report.

WAKILI KIBATALA: Sasa tuambie kuwa mpaka kamanda wa Mwanza anamkamata Mbowe.

SHAHIDI: Mimi sikuwapo nilikuwa busy. Sikuwa najua kilichotokea Mwanza.

WAKILI KIBATALA: Kwa hiyo Kibona hakukwambia lolote kuhusu tukio la Mwanza?

SHAHIDI: Kwanza sisi tuna report kwa IGP siwezi kujua kinachotokea kwa mkoa mwingine.

WAKILI KIBATALA: Maelezo hayo uliyoatoa kwenye ushahidi?

SHAHIDI: Hapana.

WAKILI KIBATALA: Kwanini ulimtamkia mshitakiwa Freeman Mbowe kuwa “wewe si unajifanya unajua sana Katiba Mpya? Sasa tunakupa kesi ya ugaidi. Safari hii hutoki?”

SHAHIDI: Hayo ni maneno wameyapanga kwa maslahi yao wenyewe kama unavyosema nipo chini ya kiapo, hapa pia Korani ipo.

WAKILI KIBATALA: Kiongozi gani mwingine wa upinzani ulishawahi kumkamata?

SHAHIDI: Sijawahi.

WAKILI KIBATALA: Lissu je?

SHAHIDI: Sijawahi kumkamata ila niliwahi kushughulika na kesi zake.

WAKILI KIBATALA: Ngapi?

SHAHIDI: Mbili.

WAKILI KIBATALA: Ni hayo tu Mheshimiwa

Anaingia Wakili Mndeme.

WAKILI MNDEME: Shahidi unafahamu kuna sheria ya Vyama vya Siasa?

SHAHIDI: Nafahamu.

WAKILI MNDEME: Unafahamu kuwa inaruhusu mkutano na maandamano?

SHAHIDI: Nafahamu.

WAKILI MNDEME: Unafahamu maandamano ni kosa au siyo kosa?

SHAHIDI: Yakiwa na kibali siyo kosa.

WAKILI MNDEME: Utakubaliana kutofautiana kisiasa siyo kosa la jinai?

WAKILI MNDEME: Shahidi unafahamu kuna Sheria ya Vyama vya siasa?

SHAHIDI: Nafahamu.

WAKILI MNDEME: Unafahamu kuwa inaruhusu mikutano na maandamano?

SHAHIDI: Nafahamu.

WAKILI MNDEME: Unafahamu maandamano ni kosa au si kosa?

SHAHIDI: Yakiwa na kibali siyo kosa.

WAKILI MNDEME: Utakubaliana kutofautiana kisiasa siyo kosa la jinai?

SHAHIDI: Ndiyo.

WAKILI MNDEME: Kutoipenda Serikali ni maoni ya kisiasa?

SHAHIDI: Ni Maoni ya mtu binafsi.

WAKILI MNDEME: Kwa hiyo hata kuichukia Serikali maoni binafsi?

SHAHIDI: Inategemea na mtu.

WAKILI MNDEME: Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji.

Wakili wa Serikali: Naomba tuhairishe hadi kesho asubuhi saa tatu ilituweze kumalizia.

JAJI: Upande wa utetezi mnasemaje?

WAKILI KIBATALA: Hatuna pingamizi lakini tunaomba kesho waje na shahidi mwingine kwa kuwa re-examination hata ikiwa ndefu haitazidi masaa mawili tukianza saaa tatu asubuhi.

JAJI: Sawa ikiwezekana mje na shahidi mwingine.

JAJI: Basi maombi ya ahirisho yamekubaliwa kama amabavyo yameombwa na upande wa Jamhuri na hayajapingwa na utetezi. Basi tunaahirisha mpaka kesho saa tatu tutakapoendelea na shahidi namba moja na baada ya shahidi namba moja tunategemea kuendelea na shahidi namba mbili.

Jaji anaondoka mahakamani.

Like