Kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi Kaaya avuruga ushahidi wake

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo Alhamisi tarehe 28 Oktoba 2022.

Kwa ufupi

Shahidi wa Jamhuri Justine Kaaya jana alisema kuwa alikutana na Mbowe kupanga ugaidi Januari 2020 Longido. Lakini Januari 2020 Mbowe alikwa jela, Segerea, Dar es Salaam.

Shahidi huyo alipoulizwa tena leo na wakili wa utetezi, akasema alikutana na Mbowe kupanga ugaidi Septemba 2020. Lakini Septemba 2020 shahidi mwenyewe alikuwa jela, Ukonga Dar es Salaam; ameachiwa mwaka huu.

Wakili wa serikali akaomba pumzikofupi. Mahakama iliporejea, shahidi akaongozwa na wakili wa serikali, akaema kuwa alikosea kutaja tarehe. Akataja tarehe mpya, kuwa alikutana na Mbowe Januari 2018..

hahidi huyo akasema kuwa alipokutana na Mbowe, alikua na gari lenye number za KUB (Kiongozi ya Upinzani Bungeni). Lakini Mbowe alinyang’anya gari la KUB mwaka 2017. ENDELEA:

Mawakili wa Serikali ndiyo wameingia muda huu mahakamani.

Jaji ameingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Inatajwa ya Khalfani Bwire na wenzake

Wakili wa Serikali Robert Kidando anawatambulisha Abdallah Chavula, Jenitreza Kitali, Nasorro Katuga, Esther Martin, Ignasi Mwinuka na Tulimanywa Majige

Kibatala anawatambilisha

Peter Kibatala
Bonifasia Mapunda
Seleman Matauka
Sisty Aloyce
Dickson Matata
Michael Mwangasa
Jonathan Mndeme
Hadija Aron
Evaresta Kisanga
Maria Mushi
Idd Msawanga
John Malya

Wakili wa Serikali Shauri linalopaswa limekuja kwa a ajili ya Ushahidi na Shahidi namba mbili anaendelea

Jaji; Jana tuliishia kwa Mawakili wa Mshitakiwa wa Kwanza wa Pili, Naomba tuendelee na Wakili wa tatu Mshitakiwa
na nakukumbusha Shahidi upo chini ya Kiapo, Naomba sasa Wakili aendelee JAJI Wakili wa Mshtakiwa wa Nne

MATATA; Kwa Niaba ya Mshtakiwa watatu sisi hatuna Maswali

Kibatala; kwa Ruhusa yako Mheshimiwa Jaji naomba Kuuliza Maswali yakibakia nitaomba Michael Mwangasa amalizie

Kibatala; Shahidi unakumbuka Jana wakati wa Ushahidi wako ulitaja namba zako za Simu

Shahidi; Ndiyo

Kibatala Unaweza kunitajia

Shahidi. 0693006700
0754916666

Shahidi; sijui Kesi Nzito, Najua Nimekuja kutoa Ushahidi tuh

Kibatala; Unajua kuwa Umekuja Kutoa Ushahidi Kwenye kesi Nzito..?

Kibatala ; Unakumbuka wakati Unaandika Maelezo yako kwa Inspector Swila ulitoa namba zako za Simu

Shahidi; Hapana sikutoa

Kibatala; kwa Ruhusa ya Mahakama Unaweza Kusoma Hapa

Shahidi 0754 216170

Kibatala Je unasemaje kuhusu hizo namba
Shahidi; sijui sasa

Kibatala; Je iambie Mahakama chini ya Kiapo hizi namba sasa Inspector Swila kazitoa wapi

Shahid;i Sijui
Swali lake lipo chini

Kibatala; Shahidi unaweza kutuambia aliyethibitisha Maelezo ya Inspector Swila kuwa Maelezo ni sahihi ni nani

Shahidi; Ni mimi

Shahidi; Shahidi tuambie wakati Unatoa namba za Simu hapa Mahakamani Umetoa Ushahidi au Kielelezo kama usajili kwamba ni namba za kwako
Shahidi; Hapana

Kibatala; Unamfahamu Inspector Swila kwa kumuona
Shahidi; Ndiyo

Kibatala; ni Mmoja ya aliyekuwa anawalinda Mahakamani wakati wa kesi

Shahidi; Hapana

Shahidi; Jana wakati Unatoa Ushahidi ulisema ujawahi kuwa Mwanachama wa Chama chochote cha siasa

Shahidi; Sijawahi
Shahidi;Ndiyo

Kibatala; ujawahi Kushiriki Kura za Maoni kata ya Pili.?

Kibatala; Kama Nikileta Ushahidi ulishiriki
Shahidi; walete Mahakamani

Kibatala; tutarudi hapo baadae

Shahidi; Ndiyo

Kibatala; nimesikia umesema kuwa Umeishi na Sabaya na Ukasema ulikuwa unaishi naye akiwa na Mke wake

Kibatala; Je ulitutajia Jina la Mke wa Sabaya

Shahidi; Nilitaja Jina Moja la Jesca

Kibatala; Je Uliishi na Sabaya Kwa Muda gani akiwa Mkuu wa wilaya

Shahidi; Miezi Mitatu

Kibatala ;Unafahamu Mahala anapoishi Mkuu wa Wilaya ni Mahala Nyeti
Shahidi; Sahihi

Kibatala; Unafahamu Makazi ya Mkuu wa Wilaya ni Ikuku Ndogo ya Hilo eneo
Shahidi; sahihi

Kibatala; Unafahamu Kuwa kuna Baadhi ya Vikao Vya Kiusalama vinafanyika kwa Mkuu wa Wilaya

Shahid;i Sahihi

Kibatala; Je wewe ulifanyiwa Vetting na Tasisi yoyote..?

Shahidi; Hapana

Shahidi; Sahihi

Kibatala; na Ulikuwa na Access ya Kuachiwa Nyumba na kukaa ngia popote kwa a Mkuu wa wilaya

Kibatala; Nimeona pia unajina lingine la Power Kaaya, umelitoa wapi

Shahidi; Tangu nikiwa Nyumbani

Kibatala; nitakuwa sahihi nikisema Umepewa hilo Jina baada ya Kufanya uhalifu sana Maeneo ya Longido na Arusha..?

Shahidi; Hapana si Kweli

Kibatala; nitarudi eneo hilo baadae

Kibatala Je unafahamu wakati Unakutana na Freeman Mbowe ulikuwa unafahamu ni Mwalifu

Shahidi; Ndiyo

Kibatala; Wakati unampq Majina ulitambua kuwa yanakwenda kutendewa Uhalifu

Shahidi; Ndiyo nilijua kuwa kuna halufu ya uhalifu

Kibatala; Wakati Unakutana na Mbowe ulikuwa unajiskia Amani Kukutana naye pekeyako..?

Shahidi; Ndiyo,

Kibatala; una Elimu gani

Shahidi; Kidati Cha nne

Kibatala; kwa hiyo uliona Uhalifu wa Madawa ya a Kulevya unatolea Taarifa wapi

Shahidi; Polisi

Kibatala; Ukiona uhalifu wa Wizi unatolea Taarifa wapi

Kibatala; Je Wakati Mbowe anakupatia pesa TSh Laki Mbili ulijua ilikuwa kwa ajili ya Uhalifu.?

Shahid;i Hapana alisema ilikuwa ni ya Usumbufu

Kibatala; we Uliamini kuwa ni ya usumbufu..?

Shahidi; Ndiyo

Shahidi;Ndiyo

Kibatala; ulisema baada ya Kukutana na Mbowe ulimpigia simu Mbunge na Sabaya

Kibatala Mwambie Mheshimiwa Jaji Je uliriport polisi..?

Shahidi; Hapana

Shahidi;Ndiyo wao ni watunga Sheria

Kibatala; Je Kazi ya Mbunge ni Kushughulika na uhalifu

Kibatala; Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji baada ya kutoa Taarifa kwa Mbunge ulifuatilia kama amefanyia kazi Taarifa hiyo
Shahidi ;Hapana sikufuatilia

Kibatala; Shika Maelezo yako haya Kielelezo D1 uliyoyatoa kwa Inspector Swila kama Ulimwambia Mambo ya Kihalifu aliyokwambia Mbowe

Shahidi; Haipo

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Taarifa yako ya Jana ya Laki Mbili ulitolea Maelezo kwa Inspector Swila

Shahidi; Haipo

Shahidi Hakuna

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa ulitolea Maelezo kwa Tasisi yoyote ya Kiuchunguzi kuhusu uhalifu wa Mbowe

Shahidi; Sikuzitaja

Kibatala; ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa ulimpigia Sabaya Simu, Je ulitaja namba za Simu za Sabaya

Kibatala; Ulimbia Jaji Kuwa Baada ya Kumkosa Sabaya Ulifanya Jitihada za kumtafuta Sabaya

Shahidi ;sikumwambia

Kibatala; ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Baada ya kumkosa Sabaya ulimtafuta Mke wa Sabaya huyo Jesca kwamba Kuna Taarifa Mbaya ya Sabaya

Shahidi ;Sikusema

Kibatala; Uliowataja Jana ni Walinzi wa Sabaya

Shahidi; Hapana ni Marafiki zake

Kibatala; hao uliokuwa umewataja Jana ulikuwa umefahamiana nao kwa muda mrefu au Mfupi

Shahidi; Muda Mfupi

Kibatala; Je uliwataarifu hao Marafiki wa Sabaya

Shahidi; Hapana

Kibatala; Wakati Unakutana na Freeman Mbowe ulihisi uhalifu gani unataka kufanyika

Shahid;i Sikuwa nafahamu

Kibatala; Mkutano wa kwanza unaosema mlikutana na Mbowe, Kama Kweli ilikuwa Lini

Shahidi; 2020 Mwezi wa Kumi, sikumbuki tarehe

Kibatala; nilisikia kuwa Umesema walikufuata na Gari, Je gari ya KUB..?

Shahidi; ilikuwa gari ya Kiraia

Shahidi Ndiyo

Kibatala; unasema alikuwa anaendesha Mwanamke..?

: Kibatala; Angalia Maelezo yako hapo, Je umeeleza kuhusu huyo Mwanamke

Kibatala; Je Ulifahamu kuwa Mbowe alikuwa anakwambia Mambo ya Kihalifu ila ukaenda Kuonana naye

Shahidi; Sikutoa

Kibatala ;Ulipokamatwa 20 08 2020 ulihifadhiwa Gereza gani..?

Shahidi; Ukongo
Lakini Ulikutana na Mbowe Longido 0ctober 2020

Kibatala; Okeeeey Kazi yangu Kuuliza Maswali

Kibatala; haya Mara ya Pili Mlikutana na Mbowe Wapi na lini

Shahidi; Mwanzoni Mwaka 2020

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji ni wapi katika Statement ataona Khalfani Bwire alikwepo Katika Kikao Moshi

Shahidi; Khalfani Bwire alikuwa katika Kikao cha tatu

Shahidi; Hakuna

Kibatala; Sawa Mwambie sasa Katika hayo Maelezo yako ni wapi ulimwambia Inspector Swila kuwa Khalfani Bwire alikwepo..?

Kibatala; Nini kilitangulia kati ya Maelezo yako na Ushahidi wako Mahakamani

Shahidi; Kilitangulia Maelezo

Kibatala ;Je wewe ulitambua Bwire wapi.?

Shahidi; Kabla ya Mahakamani

Kibatala; kwa hiyo kumtambua Bwire umefanya Jana Hapa Mahakamani

Shahidi; Nilimwambia Kabla

Kibatala; Hapo Kwenye maelezo ipo sehemu Umemtaja Bwire.?

Shahidi; Hapana

Kibatala;kwa hiyo sisi tunaona umefanya hivyo kwa mara ya kwanza Jana

Kibatala; uliwahi Kuwa nao Pamoja jela
Shahidi ;Ndiyo

Kibatala; mliongea nini

Shahidi ;wao ndiyo walikuwa wananielezea walivyokuwa wanamtafuta Sabaya,Wakakurupushwa, wakahisi ni mimi

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji Mambo mazito kama hayo katika Statement hiyo atayaona Ukurasa wa ngapi

Shahidi; Hayapo

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Mambo Mazito kama hayo ulisema a kuwa a
uliriport Mambo mazito kama hayo kwa Mkuu wa Gereza

Shahidi; Sikusema

Kibatala; inawezekana wewe na Inspector Swila Mlipitiwa sasa Mwambie Mheshimiwa Jaji kama uliriport Matukio kama hayo popote

Shahidi ;Sikusema

Kibatala; Je a Ulizungumzia Ulikamatiwa wakati unapelekea pesa benki

Shahidi; Ndiyo

Shahidi Sahihi

Kibatala; Ukasema ulikuwa na Dollar na Euro
Ukasema ulikuwa unafanya Biashara na Hotel na Hotel gani ,Je ulitoa kielelezo Chochote kama Ulilipwa fedha hizo

Shahidi; mount Meru

Shahidi Sikutoa

Kibatala; ulifafanuq kwa Mheshimiwa Jaji kwamba Ulibadili pesa kwa Euro na Dollar kwenda fedha za kitanzania

Shahidi; Nili fafanua Jana Kuwa nilipewa pesa ambalimbali

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Ulitoa Nyaraka za Malipo za Mount Meru

Shahidi; Sikutoa

Kibatala; ulitaja Jina la Afisa aliyekulipa hizo pesa

Kibatala; Mount Meru hawanunui papo kwa papo wanafanya kazi kwa mkataba na Mzabuni

Shahidi; Sikutoa

Kibatala; Je ulitoa Mkataba kwa Jaji

Kibatala ;Ulitoa Risiti za TRA na Zingine kwamba Biashara ni halali

Shahid;i Sikutoa

Kibatala; Je unataka Mount Meru Hotel Leo wasikie wanapo fuatilia kesi hii wasikie luxury walikulipa Dollar 1000 cash

Shahidi; Sikutoa

Shahidi;Siyo Mount Meru Bali Mtu wa Mount Meru

Shahidi; Sikusema

Kibatala; ooohooo Ukiyasema hayo Jana

Kibatala;Karoti za fedha za hizo Nyingi sana, Je ulitoa Maelezo kuhusu Namna ulivyozipewa kwa usafiri gani na Risiti zake

Shahidi;Sikusema

Kibatala; Polisi walipokukamata Unawakumbuka.?

Shahidi; Siwakumbuki

Kibatala; unasema ulihojiwa na Inspector Mahita

Shahid; i Ndiyo Kuhusu tuhuma zote

Shahidi; Central Dar es Salaam

Kibatala; Mahojiano uliyafanyia wapi

Shahidi; Ndiyo nilirudishiwa

Kibatala ;Mashitaka yalifutwa na Ukakabidhiwa fedha zako

Kibatala; Walichukua hivi hivi au walikuandikisha na kukupa Karatasi

Shahidi; Walinipa Karatasi

Kibatala; Je Wakati Jana Mawakili wa Serikali waliokuongoza Jana walikuinyesha hapa Mahakamani hiyo karatasi

Shahidi ;Hapana hawakunionyesha

Kibatala;swala la pesa ni kubwa sana, Je ulionyesha Karatasi kwamba sasa wamenirudishia

Shahidi; Sikuonyesha

Shahidi;Sikumbuki

Kibatala; Unaweza Kutuambia huyo Wakili wa Serikali ambaye badala ya kukwambia uende kwa DPP badala yake akakawambia uende Central

Kibatala; Sisi tunasema kuwa hizo Euro au Dollar hujarudishiwa

Shahidi;Wamenirudishia

Kibatala ;Sisi tutaamini Vipi

Shahidi; nimesema Chini ya kiapo

Kibatala; Ingekuwa hivyo usingekuwa unahojiwa hapa

Kibatala; haya niambie sasa kuhusu Kukutana na Freeman Mbowe Je ulitoa Taarifa hapa Mahakamani kuwa Mlinzi wake sikuwa namfahamu Vizuri

Shahidi ;Hapana

Kibatala;Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji baada ya Kuombwa Majina mara ya Pili Ulichukua tahadhari za Kwenda polisi

Shahidi ;Sikusema

Kibatala; Je Ulimwambia Sabaya Mwenye Rafiki zake kuwa kuna Jambo Kinaendelea wachukue tahadhari

Shahidi;Sikusema

Kibatala; zile fedha ulizopokea ulizionaje za Kihalifu au fedha safi

Shahidi;Niliona Fedha safi

Kibatala; baada ya Kuona Siyo pesa Mbaya ndiyo Maana hukumu Mwambia Sabaya, Mke wa Sabaya, wala Marafiki zake

Shahidi; Hapana si kweli

Kibatala; Je Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji hayo Majina Yamo katika Statement..?

Shahidi;hayamo

Kibatala; Kibatala Namba zao Za Simu..?

Kibatala; hilo gari la KUB uliona lini

Shahid;i Hazimo

[Shahidi; January 2020

Kibatala;unataka Mahakama ikuchukulie wewe ni shahidi Muhimu na Umetoka kwa Chumba wako kuja Kutoa Ushahidi

Shahidi; Ndiyo

Kibatala; Je unafahamu January 2020 Freeman Mbowe alikuwa Gerezani Segerea baada ya kufutiwa Dhamana Mahakama ya Kisutu

Shahidi; Sifahamu

Kibatala;Je Mtu akiwa Gerezani Segerea anaweza Kukutana na wewe Longido

Kibatala; umezungumzia Joyce Mukya Jana, Nieleze kwenye Statement hiyo Umeandika Wapi

Shahidi; Hapana Sifahamu

Shahidi ;Hakuna mahala nilipoandika

Kibatala; Je kuna Karatasi Umetoa hapa Mhakamani inayoinyesha Ushahidi a kwamba Namba hii ilimpigia namba hii, Je ulitoa Karatasi hiyo hapa Mahakamani

Kibatala; kwetu Muhimu sana sijui Kwa Mahakama

Shahidi;Hapana sikutoa

Shahidi; Ni sahihi

Kibatala;Ni kweli Freeman Mbowe ni Mtu Maarufu

Kibatala; kwa hiyo hata mtu wakawaida anaweza Kumfahamu Freeman Mbowe

Shahidi; Ndiyo

Kibatala; Sawa

Kibatala; Shahidi Jana Ulizungumzia kuwa wewe ni Mkulima

Shahidi Ndiyo

Je Mkulima analipa kodi..?

Kibatala; Sasa wewe Ulitoa Karatasi yoyote hapa Mahakamani Kwamba unalipa Kodi

Shahidi sikutoa

Kibatala; Jana Ulimtajia Majina ya Kina japhet na wenzake kwamba Je ni Viongozi wa Serikali

Shahidi Hapana

Kibatala; Je unafahamu Kuwa Sabaya kwa Mujibu wa sheria ni Muhalifu hapa tunavyoongea

Shahid;i Sifahamu

Shahidi; Ndiyo nimesikia

Kibatala;ila Unajua kuwa amefungwa Miaka 30

Kibatala;Umesikia kafungwa ila hujui kama ni Muhalifu na alifanya uhalifu Miaka ya 2018 Mpaka 2020

Shahid;i sifahamu

Kibatala; bila shaka ufahamu pia kwamba Freeman Mbowe aliwasiliana na IGP SIRRO Kumfahamisha Matendo ya Kihalifu aliyokuwa anatenda Sabaya

Shahidi;Sifahamu

Kibatala; bila Shaka ufahamu pia kuwa ni Wajibu wa Raia Mwema Kukusanya Taarifa na Kuzifikisha kwa Mamlaka husika

Kibatala; Mwanzoni ulisema kuwa Mbunge kazi yake ni Kushughulika na Uhalifu

Shahidi; Nilisema Kuwa Mbunge kazi yake ni Kutunga Sheria na anaweza Kushughulika na uhalifu

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa kuwa Wakati Mbowe anakuomba Taarifa alikuwa Mbunge

Shahidi; Alikuwa Mbunge wa Hai

Shahidi ;Nafahamu

Kibatala; Je unafahamu Mtu uliye mtajia Jina lake Sylvester Nyegu amehukuliwa Kifungu cha Miaka 30 na Sabaya Kwa a Makosa ya Ujambazi

Kibatala; Huyo ndiyo uliyempatia Freeman Mbowe Taarifa zake

Kibatala; na Umesema hujui kuwa ufahamu Mbowe alikuomba Taarifa zao

Shahidi; Ndiyo

[ Shahidi; Ndiyo sikuwa nafahamu

Shahidi sifahamu

Kibatala;na Ufahamu kuwa Hizo Taarifa alizishughulikia

Kibatala;Kama nakumbuka baada ya Kumpatia Mbowe Majina na Namba nimekunukuu Mbowe alisema “Wewe niache Mimi, miye nafahamu nitashughulika nao Vipi”

Kibatala;Na Hukusema kama Mbowe alikwambia kuwa anataka kumdhuru Sabaya wala Wenzie

Shahidi ;Ndiyo alisema hivyo

Shahidi ;Hakusema

Kibatala; Jana Katika Statement Yako umeeeleza kuwa ulimtongoza Helga Mchomvu

Kibatala ;Unafahamu Helga Mchomvu Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Ya Hai kuwa anamiaka Mingapi

Shahidi;Ndiyo Ni sahihi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala;Mimi Nakwambia Sasa Anamiaka 60,wewe Unamiaka Mingapi

Shahidi; Miaka 31

Kibatala ;na Ulimtongoza

Shahidi ;Ndiyo

Kibatala; Jana Katika ushahidi wako ulisema palikuwa na Diwani wa kibororni

Shahidi; Ndiyo

Kibatala; Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama ulitaja Jina lake

Shahid;i Sikutaja Jina lake

Kibatala;Je unafahamu Kuwa Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Hai alitekwa na kumizwa Vibaya

Shahidi; sifahamu

Kibatala;Kwa hiyo unafahamu kuwa Mbowe kama Mbunge alikuwa anafuatilia Taarifa za Uhalifu wa watu waliomdhuru Kiongozi wake

Shahidi ;Sifahamu

Kibatala; Jana ulitaja Majina ya SG hotel na Gold Crest Hotel

Shahidi Ndiyo

[Kibatala; Je unafahamu sehemu zote hizo Sabaya alikuwa awezi Kufika kwa sababu ya amadeni Makubwa ambayo alikuwa halipi

[Shahidi; Sifahamu

Kibatala; Umesema pia ulilala Aishi Hotel

Kibatala;Ulitaja Jina la Chumba Ulicho Lala..?

Shahidi; Ndiyo

Shahidi ;Hapana

Kibatala; ulitaja Aina Ya Chakula Ulicho kura pale

Shahidi; Hapana

Shahidi; Sahihi

Kibatala; Nilisikia mara zote ulikuwa unasafiri kwa kutumia public transport?

Kibatala; na Ni sahihi kukutoa risiti/Ticket yoyote ya Magari uliyokuwa unasafiri !

Shahidi; Sahihi

Kibatala; ni sahihi kwamba Ulikuwa unaendelea kuwasiliana na hao Marafiki wa Sabaya Mpaka Muda Unakutana na mbowe Mara ya Mwishi

Kibatala; na hukumwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa alikuwa mnawasiliana kwa Mambo Mema au Mabaya

Shahidi; Sikusema

Kibatala; Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

Kibatala; labda kama Mwenzangu atakuwa na Maswali

Michael; Mwangasa unatamani Mahakama Iamini kuwa Ushahidi wako ni wa kweli

Shahidi; Ndiyo natamani

Michael; Je Kuna Mahala yoyote Umesema Mbowe alishiriki Vikao Vya ugaidi

Shahidi; Hapana

Michael; Je kunasehemu yoyote Umesema kuwa uliwahi kushiriki Vikao Vya Ugaidi na Mheshimiwa Mbowe

Shahidi ;Sikusema

Shahidi; Nilieleza Vikao tuh

Michael; Je ukiiambia Mahakama Kwamba ukishiriki Vikao Vya ugaidi

Michael; Kwakuwa ulikuwa unafanya Vikao na Mbowe na kushitakiwa, kisha Kuachiwa huru

Shahidi; Nilisema nikishitakiwa nikaachiwa huru

Michael; Ulisema ulimpatia Mbowe namba za akina Japhet, Je ulitaja hizo namba hapa Mahakamani

Shahidi; Sikutaja

Michae;l Ulisema Ulimpa Taarifa Mbunge wa Longido Taarifa za Kiuhalifu

Michae;l ni sahihi ukusema hapa Mahakamani kuwa walikupa Mrejesho gani

Shahidi; hazikuwa Taarifa za Kiuhalifu, nilimwambia kuna mtu Mkubwa amekuja Longido kunifuata sikutegemea

Shahidi; ndiyo

Michael; nitakuwa sahihi nikisema walikupuuza.?

Shahidi;Sijui

Jaji; Re examination..?

Michael; ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali; tutaendelea na Re Examination na ataanza Abdallah Chavula

Wakili wa Serikali; Kwa Ruhusa yako Mheshimiwa Jaji tungeomba tupatiwe Kielelezo E1

Wakili wa Serikali; Shahidi Umeulizwa Maswala Mengi sana kuhusiana na Karatasi ya Maelezo uliyoyatoa Polisi dhidi ya Maelezo uliyoyatoa hapa Mahakamani
Wakiwa wanataka Kuonyesha…

OBJECTION aende Straight kwenye Re examination, a najua kuwa hairuhusiwi na ni Principal State attorney, Akitaka aweke hayo kwenye final submission. ” Kibatala

Wakili wa Serikali; Sawa

Wakili wa Serikal; i kwanini Kwenye Statement Yako uliyoatoa Polisi haina Maelezo uliyoyatoa Jana Mahakamani

Jaji Wakili wa Serikali; Unasemaje

Wakili wa Serikali; Nita Kukabidhi sasa hii Karatasi ufafanue

Shahid; i Kwa sababu Jana ilikuwa na eleza kwa aurefu Nikichoandika kwenye Statement yangu polisi

Shahid; i hapa Nimeona Nimeeleza Kuhusu Kilimo, Nilikuwa nalima Viazi na Karoti

Shahidi; Jambo Lingine ni Mwandishi amekosea Mwaka nilioacha kazi kwa Sabaya

Jaji; hapo sasa Mnafanya nini Wakili wa Serikali

Shahidi; Nafafanua kilichopo

JAJI; afafanue Sasa

Wakili wa Serikali; Sawa

Shahidi; Swala lingine nilimtaja Yule Diwani

Wakili wa Serikali; Kwenye Ushahidi wako ulitaja Diwani wa wapi

Shahidi; Diwani wa Kiboboroni
Ambaye Mheshimiwa alinitambulisha kuwa ni Kiongozi wa Ulinzi Kanda ya kaskazini

OBJECTION hiyo ni fact Mpya kuhusu ni Kiongozi wa ulinzi Kanda ya kaskazini

Jaji; Mimi nilirekodi hivyo

Mallya; kama Mahakama ili Rekodi sina tatizo

Wakili wa Serikali; Kuhusiana na huyo Diwani ulisema nini

Shahidi; Sikutaja Jina la Diwani

Wakili wa Serikali; sasa Uliambia Mahakama Huyo anaitwa nani

Kibatal; a Sasa Ndiyo tunafanya nini

Jaji; Ngoja tuone swali lake Maana hata Mimi nimerekodi kuwa Hakutaja Jina la Diwani

Shahidi; ameshasema hakutaja Jina, yeye anataka Shahidi ajibu nini cha ziada.?

Wakili wa Serikali; Tueleze kuhusu Majina na Maeneo uliyoyatoa Jana hukutaja.?

Shahidi; Sikutaja

Shahidi; Nikichofanya nilifanya ufafanuzi kwa kutaja hayo Majina niliyo mtajia Mheshimiwa Mbowe bowe

Wakili wa Serikali; Tueleze sasa kwanini sasa Katika Maelezo Yako Polisi hukutaja na Jana Ukataja

Wakili wa Serikali; Umeulizwa Kuhusu Kukutana na Bwana Mbowe Ukasema ni Mwanzoni mwa October 2020 longido na Baadae Ukasema ni October 2018 fafanunua Mkanganyiko huo

Shahid; i kwa sababu Mawakili wa Upande wa Utetezi walikuwa wananiuliza kwa njia Isiyo sahihi, wakawa wananichanganya baadae nikakumbuka

Wakili wa Serikal; i Chavula Mheshimiwa Naomba Nimkaribishe Mwenzangu

Wakili wa Serikali Robert Kidando Nasimama

Wakili wa Serikali; kuna swali Uliulizwa na Wakili Kibatala Kwamba wapi Mbowe alikuwa wapi a kuanzia November 2019 Mpaka January 2020 Ukasema ufahamu habu tuambie

Wakili wa Serikali Robert; Asante mheshimiwa Jaji

Shahidi; Ninachofahamu yeye alinitafuta akiwa na Mikutano ya Jimbo

Wakili wa Serikali; Umeulizwa Kuhusu Vikao kama Vilikuwa Vya kigaidi Ukasema Hapana Sasa hoja ilikuwa ni nini

Shahidi; Hoja ilikuwa ni Kuomba Majina ya wale a Vijana wanaotembea na Sabaya na Namba zao za Simu

Wakili wa Serikali ; Ukaulizwa na Wakili Kibatala Kwamba Kama ulikuwa na hofu ya kiuhalifu Ukasema Hapana hebu fafanua

Wakili wa Serikali; Uliulizwa swali kuhusu Kule Longido baada ya Kumtafuta Sabaya ukampigia Mbunge na Hukuliport hata Polisi

Shahidi; nilipata hofu kwa sababu Yeye alikuwa Mbunge na Sabaya alikuwa Mkuu wa Wilaya, nikajiuliza kwanini atafuti kwa Kiongozi Mwenzie

Shahidi; ni Kwa sababu nilihisi wote ni Viongozi na atamwambia mwenzie nikawa nimeshafikisha ujumbe

Wakili wa Serikali; Uliulizwa Kwamba Neno Bwire ni Msiri na Mlinzi wa mbowe, Elezea Sasa Kule Polisi Ulimtaja kwa namna gani

Shahidi; Nilitaja kuwa alikuwa na Mlinzi hapa nikajakutoa ufafanuzi

Wakili wa Serikali; Hebu fafanua kuhusu Biashara yako na mount ilikuwa je hukuleta nyaraka za Malipo hapa Mahakamani

Shahidi; Kwasababu nilikwepo Muda mrefu Gerezani na Nyaraka hizo ni za Muda Mrefu

Shahid;i ni Kwa sababu Kuna watu wanakuja kwa wakulima kwa ajili ya Kupeleka Mazao Mount meru

Wakili wa Serikal;i Uliulizwa Kama Ulileta Nyaraka za Mount Meru Ukasema hujaileta, kwa sababu Ulifanya na mtu wao hebu tufafanulie

Wakili wa Serikali; Uliulizwa kuhusiana kutotaja watu wa Sabaya Pale Polisi

Wakili wa Serikali; Uliulizwa swali kuhusiana na Jina Power Kaaya kwamba linatokana na Matendo ya Kihalifu, tufafanulie kwanini unaitwa Power Kaaya

Shahidi; nili ulizwa Majina ya watu hao hapa Mahakamani Hapo kwenye maelezo Siku ya orodhesha

Shahidi; ni Jina langu Ndiyo Maana naitwa Power Kaaya hata kwenye Charge Sheet lipo, tangu kwenye ubatizo niliitwa Power

Wakili wa Serikali Uliulizwa swali kwamba Ulipewa Laki 2 ndiyo Maana Hukutoa Taarifa polisi
Shahidi; Sikuwa nimesema Kitu hicho

OBJECTION

Jaji; hata Mimi Siku Rekodi Jambo hilo

Wakili wa Serikali ; Kuhusiana na namba hiyo kwenye Statement ukasema siyo Namba yako, kwanini sasa unasema siyo Namba yako

Shahidi; Sijui Sasa Mwandishi aliyeandika

Wakili wa Serikali; Na Ukaulizwa kuhusiana namba zako mbili za Simu na Ukaulizwa kama Ulileta Uthibitisho Mahakamani, elezea Sasa kwanini unasema namba hizo ni zako

Shahidi; kwa sababu Namba hizo ndiyo nazitumia

Wakili wa Serikali; Umeulizwa Swali Kwamba Katika Dhamana ya Mbowe kuwa aliwahi kufutiwa Dhamana, je Ni kitu gani walichokuonyesha kuwa walikuwa na Kesi na aikafutwa Dhamana

Shahidi; Hawajanionyesha Kitu chochote

Shahidi; Kwasababu wakati wanakamatwa Mimi nilikuwa Gerezani

Wakili wa Serikali; Umeulizwa kuhusiana uhalifu wa Sylvester Nyegu na Ole Sabaya Ukasema Ufahamu, elezea kwanini ufahamu

JAJI ; Shahidi Tunashukuru kwa Ushahidi wako, una eza kwenda sasa

Wakili wa Serikali; Mheshimiwa Jaji huyo ndiyo Shahidi tuliyekuwa naye kwa Leo

Shahidi; Mwingine tuliyekuwa tumemuita hajafika
Hivyo tunaomba Hairisho hadi Kesho tarehe 29 Mwezi wa 10 ilituweze kuendelea na Shahidi Mwingine

Jaji; Upande wa Utetezi

Wakili Peter Kibatala; Mheshimiwa sisi hatuna Pingamizi tunaomba waweze Kujitahidi Kadri inavyowezekana ili kesho Waje na Shahidi

Jaji: anaandika Mahakama ipo Kimya Kidogo

Jaji; shauri linahairishwa mpka Kesho saa 3 Asubuhi

Upande wa Mashitaka unapewa Maelekezo ya kuleta shahidi

Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande hadi Kesho Asubuhi

JAJI ananyanyuka.

Like
3