Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ, leo tarehe 30 Novemba 2021.
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 12 ya Tarehe 30 November 2021
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
WAKILI PETER KIBATALA Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naomba Kuwatambulisha
John Malya
Nashon Nkungu
Fredrick Kihwelo
Paul Kaunda
Seleman Matauka
Michael Lugina
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa, Naomba tupatiwe Nyaraka ilikuweza Kuzikagau
Wamekabidhiwa Nyaraka na Kuanza Kukagua Moja baada ya Nyingine
Mahakama ipo Kimya Wakiendelea zoezi la Kukagua
Wakati wanakagua Leo Mahudhurio siyo Makubwa Sana, Huenda Sababu ya Hali ya hewa
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tunamapingamizi Kuhusiana na Upokelewaji Wa Nyaraka hizo Nne Zinazotaka Kutolewa na Shahidi Wa Pili
Mheshimiwa Jaji tumeandaa Mapingamizi ngamizi ifuatavyo
1.Mwenendo wa Kesi( Case Proceedings, Hati ya Mashitaka (Charge Sheet) pamoja na Barua inayo Daiwa Kuandikwa Kwa Hakimu wa Mahakama Mkazi Kisutu,
Nyaraka hizi haina Relevance Katika Shauri Linalo endelea Kuhusu Mshitakiwa Wa Tatu
Kwa hiyo Nyaraka hizi tunazipinga
Mheshimiwa Jaji Kuhusiana na Nyaraka nikizozitaja hapo Juu, Kuna Cha Kuongezea Kuhusiana na Hati Ya Mshitakiwa, Kwamba Kilicho letwa Mahakamani hapa ni Copy ya Hati ya Mashitaka, ambayo Kwa Mujibu wa Sheria Copy haiwezi Kupokelewa kabla ya Kukidhi Vigezo Vya Kisheria Kama Vilivyotakiwa katika Vifungu Vya 65, 66, na 67 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya Sita
Mheshimiwa Jaji Kuhusiana na Dispatch, Shahidi aliyepo Mahakamani siyo Competent Witness Kuweza Kuitoa hiyo Dispatch
Mheshimiwa Jaji sisi tupo tayari Kuendelea na Hizo Hoja zetu za Kisheria kwa Maana Kufanya Submission na ataanza Pius Hilla
JAJI: Kwa hiyo ni Mapingamizi Matatu
WAKILI WA SERIKALI Pius Hilla:
Mheshimiwa Jaji Nyaraka ambazo Wenzetu Wanataka Kutender Kwenye Ushahidi
JAJI: Hapo unamaanisha Dispatch
WAKILI WA SERIKALI Pius Hilla: KUHUSU RELEVANCE Nyaraka Wanazotaka Kitumbukiza Kwenye Ushahidi Barua, Proceedings, na Charge sheet
Ukizitazama Zinahusiana Criminal case namba 77 /2020 kuhusu Jamhuri Vs Lembrus MCHOME Kesi ambayo ilikuwa Mahakama Ya Kisutu
Mheshimiwa Jaji Hakuna Namna yoyote Ile, Nyaraka hizi zikahusiana na Shauri Lililopo Mbele yako
Hakuna Namna yoyote Ile Mheshimiwa Jaji Nyaraka hizi Kuhusiana na D/C Msemwa Ambaye ni Shahidi namba 3 wa Shauri Dogo Ndani ya Shauri kubwa
Nyaraka hazina Uhusiano wowote Ule na Hoja ya D/C Msemwa Kuwepo Central Police au Hatakuwepo Oysterbay Police
Nyaraka hazina Indicator Zozote zile kama D/C Msemwa aliwahi Kufanya Kazi Kituo cha Polisi Oysterbay kipindi cha Mwezi May 2020
Mheshimiwa Jaji Nyaraka hizi pia hazina Bearing yoyote ile za Ukamatwaji Wa Ling’wenya, Uandikaji wa Maelezo Ya Ling’wenya, Mambo ambayo Ndiyo Issue Iliyopo Mbele Yako
Nyaraka hizi pia Mheshimiwa Jaji hazina Bearing yoyote ile Kwamba Lembrus MCHOME (DW2) Kuwa amewahi Kukaa Kituo cha Police Oysterbay
Mheshimiwa Jaji Jaji Kwa Mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Kwamba Ushahidi Mheshimiwa Jaji, Utatolewa na Kupokelewa Mahakamani Kama Upo Relevant
Na wala Siyo Vinginevyo
Mheshimiwa Jaji Mahakama Yako hii inaongozwa na Sheria, Kwamba Kila Kinachofanyika Mahakamani lazima Kifanyike Kwa Mujibu wa Sheria
Kila kitakachopokelewa lazima Kiwe na connection (Uhusiano)
Mheshimiwa Jaji Kesi ya DPP VS SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHERS Criminal appeal namba 74 ya Mwaka 2016 katika Ukurasa Wa 6 Aya ya Mwisho
Mahakama Ya Rufaa Ilipata Kusema Kwamba, Ushahidi ambao ni Irrelevant ni inadmissible
Mheshimiwa Jaji Page ya 7 ya Hukumu hiyo paragraph Ya Kwanza
Mahakama Ya Rufani Inasema Kwamba fact inakuwa Relevant kama Inakusudia Ku Prove au Ku disaprove Ushahidi
Bila Kuzingatia hayo Mahakama Ingaletewa Mambo Mengi ya siyo Ya Msingi
Mheshimiwa Jaji Mahakama Inapaswa Kuletewa Mambo ambayo ni Relevant
Mheshimiwa Jaji Barua inayo taka Kuletwa Mahakamani inatoka TANAFRICA LAW imesainiwa na Wakili Peter Kibatala Imeelekezwa kwa Hakimu Mkazi Kisutu imenakiliwa kwa Lembrus MCHOME na Kwa Deputy Registar wa Mahakama hii Kuomba Proceedings
Haiongelei Ukamatwaji Wa Ling’wenya Wala Haiongelei Uandikaji wa Maelezo wa Ling’wenya
Kwamba Barua Mheshimiwa Jaji Haijaongelea Kwa Jambo Lote Lote lile Kuhusiana na Shauri Lililopo Mahakamani
PW2 Hajaongelea Kwa Namna Yoyote ile anahusiana na Ling’wenya
PW2 Hajaongelea lolote Kuhusiana na hii Barua Kama inahusiana na Ukamatwaji na Uandikaji wa Maelezo wa Ling’wenya
PW2 haja eleza Kwa namna gani, Barua hii, Proceedings na hata Charge Vinahusiana Vipi na Yeye Kuwepo pale Oysterbay Police
Mheshimiwa Jaji Charge Sheet na Proceedings Zinahusiana na Mashitaka, Publication of photographs
Shahidi aliyepo Mahakamani alikamatwa kwa Kupigwa Picha Fulani Kwa Kiongozi Fulani akashtakiwa Kwa Matumizi Mabovu ya Mtandao
Mheshimiwa Jaji Swali la Kujiuliza ni Je Shauri hili lina Uhusiano gani na Matumizi Mabovu ya Mtandao, Ya Uhusiano gani wa a Kupiga Picha Kiongozi Fulani au Taasisi fulani
Mashitaka haya ya Publication of Photograph Yana Uhusiano gani na D/C Msemwa Kuwepo Oysterbay police
Mheshimiwa Jaji Nyaraka zinatakiwa kujiongelea Zenyewe
Ni Wasilisho letu Kwamba Nyaraka hizi haziongelea Chochote Kuhusiana na Ishu iliyopo Mahakamani
Nyaraka zinaongelea Vitu Vingine kabisa
Nyaraka hazina Uhusiano na Ukamataji na Uchukuliwaji wa maelezo ya Ling’wenya
Na zaidi zaidi Nyaraka haziongelei kabisa Kuwepo Kwa Lembrus Oysterbay na Kuonana na D/C Msemwa
Mheshimiwa Jaji Tunawasilisha Kwamba Shahidi Ndiyo anaye Lay Foundation Juu ya Upokelewaji Wa Ushahidi Wake Mahakamani
Alitakiwa a ieleze Mahakama Yako Tukufu Kwenye Hizo Nyaraka Kuna Moja Mbili Tatu Kuhusiana na D/C Msemwa
Mheshimiwa Jaji Shahidi alijaribu Kueleza Mahakama Yako tukufu Kwamba alikaa na Msemwa Kwa Muda
Hicho siyo Kigezo Cha Kuleta Hizo Nyaraka
Nyaraka zilitakiwq zijitambukishe Zenyenwe na Shahidi aongee Kuzitambulisha
Kwa Kifupi pasipo Kuwa chosha Mahakama Yako tukufu Nyaraka hizi ni Irrelevant, Hazina Sifa za Ku pokelewa Nyaraka hizi
Kwamba Kitendo Cha Shahidi Kutokuongelea ni Kitu gani kwenye Nyaraka Kinahusiana na D/C Msemwa Inabainisha Kwamba Wala Hana Knowledge Ya Kile Kilichopo Katika hii Nyaraka
Mheshimiwa Jaji nizungumzie Sasa Kuhusiana na Charge Kuwa Nakala
Mheshimiwa Jaji Kinacho letwa Mbele Yako Hakuna Ubishi it’s a photo Copy
Tunasema Hakuna Ubishi Kwa Sababu Shahidi Mwenyewe Alianza Kwa Kusema Hivyo
Rules of Evidence zinademand Kufuatwa Kwa Procedures ili Kuleta Ushahidi
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Letu kuwa Nyaraka hii Imeletwa kwenye Violation
Ni Violation ya kifungu cha 63 Mpaka 66 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6
Kwamba Kwakuwa Walifahamu Kwamba Nyaraka ni Photocopy (Secondary) Walitakiwa Mheshimiwa Jaji Wa Comply na Masharti
Mheshimiwa Jaji Ushahidi Ambao ni Photocopy (Secondary) it’s a General Rule Kuwa ni Adminsible
Mheshimiwa Jaji baada ya Kusema hayo naomba Wakili Mwenzangu Abdallah Chavula aendelee pale Nilipo Ishia, ata Kuja kwa Swala la Dispatch
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji ni Kama alivyo tangu Lia a Kusema Mwenzangu
Nitaanzia Hapa Alipoishia Yeye
Na Yeye Aliishia Kwamba hii Hati ya Mashitaka Imekiuka Kifungu namba 63 Mpaka 66
Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 63 kimatoa Ruhusa kwa Nyaraka kwa namna mbili
Kwa primary Evidence na Secondary Evidence
Na Kifungu ha 64 limeweka Bayana Kwamba Primary ni Documents
Mheshimiwa Jaji Shahidi akaweka Bayana kwamba alipewa Photocopy
Kwa hiyo siyo Primary Evidence, Kwa Maana hiyo anataka Kuijulisha Mahakama Hii ni secondary Evidence
Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 65 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, kinasema kwamba
ANASOMA
(a), (b) (C), (d), na (e)
changed this group’s settings to allow only admins to send messages to this group
Mheshimiwa Jaji Katika Ushahidi Wake haja eleza Mahakama Kwamba Nyaraka hii Imekuwa Certified na Ukatazama Nyaraka Yenyewe Pia Hazijawa Certified
Shahidi ajieleza Mahakama Kwamba Nyaraka hii Imetengenezwa Kutoka Kwenye Nyaraka
Hajaileleza Mahakama Mheshimiwa Jaji Kwamba Baada Ya Kufanyiwa Photocopy Wali ringanisha Kujiridhisha Kwamba Kilichopo humu ndiyo Kipo kwa Original Charge Sheet
Vilevile Haja elezea Kwa mdomo Kwamba hii ni sehemu ya Ile Original Document
Mheshimiwa Jaji Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi huyu wakati wa Kuomba Kutoa Nyaraka Hajakidhi Matakwa ya Kifungu cha 65
Twende Mbele zaidi, Fungu la 67 Kinaweka Masharti Kwamba Secondary Evidence Inatapaswa Kutolewa Mahakamani
Ni Maoni yetu Siye kwa Madai Ya Kwamba Eti Kule Mahakamani Kisutu Kwamba walielezwa Nyaraka Ya Mashataka ipo Moja tuh
Kwa Bahati Mbayo siyo Sababu Iliyo Tajwa Kisheria Kuleta Nyaraka hiyo
Ni Maoni yetu Vigezo Vilivyomo Katika Kifungu cha 65 vinakosekana kwa Ushahidi na Shahidi Mwenyewei
Na hii ya Kupewa Photocopy Haikamiilishi Kifungu
Kifungu Cha 68 Kinachotaka Wao Kufanya Ku Introduce hiyo Documen na Wao hawakufanya
Na Kwa Sababu Hawa Kutumi hiyo nafasi, Basi Maombi yao ya nakuwa Batili Mbele ya Mahakama hii
Mheshimiwa Jaji naomba tuelekee Kwenye Pingamizi La Dispatch
Mheshimiwa Jaji ni Msimamo Wa Sheria na Katika Nyakati tofauti Tofauti
Tumekuwa tulielekeza Mahakama Yako Kwenye Shauri la JAMHURI Vs CHARLES GAZILABO NA WENZAKE Katika Ukurasa Wa 12, Na Pia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI
Mahakama ili weka Vigezo na Vigezo Hivyo Ni knowledge na Kama Ushahidi Ulishawahi Kuwa kwenye Himaya Yake
NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji Kuna Kesi Zinatajwa hapa Kama Rejea Naomba Nasisi Tungapatiwa
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji alikuwa afuatilii Kwa Sababu nilikuwa nasema tuh Kuhusu hizo Kesi, ila pia tuliwapa
Nashukuru Kaka Yangu Kibatala anasema aniendelee
Mheshimiwa Jaji hapa Kuna Swala la Knowledge
Ilikuwa ni Lazima Kuonyesha Mahakama Kwamba alishawahi Kumiliki Kielelezo hiki
Sisi ni Maoni yetu Kwamba Kuna Eneo Muhimu Sana ambalo tunaona ni lazima Mahakama itambue
Wakati anaeleza Kuhusu Barua, alieleza Barua ile Ina Reference namba, Mheshimiwa Jaji Shahidi a Kwenda Mbele na Kutuambia hizo Reference Nmab ni zipi Ni Maoni yetu Kwamba Shahidi ameshindwa Kunukuu Reference namba za Barua ambazo yeye Anada Kwamba hazikamiliki
Ni Maoni yetu Kwamba Shahidi hana Knowledge ya Kielelezo ambacho anataka Kukitoa
Na Vilevile Kwamba Kielelezo hicho Hakina Uhusiano na Kesi iliyopo Mahakamani
NASHON NKUNGU: OBJECTION Mheshimiwa Jaji tungejikita na P. O zile tatu naona hii ni P. O Mpya
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Shahidi alieleza Mahakama Kwamba Dispatch Hii Ililetwa na Msaidizi Wa TANAFRICA LAW naye Baada ya Kuleta Barua, na haya ya Kupeleka Barua yakifanywa na Mtu anaitwa FAITH kwa Mujibu wa Ushahidi Wake
Na Yalifanyika Tarehe 23 November Mwaka huu, na Yeye alikuja Tarehe 24 November 2021, Hakuna Sehemu alitaka Kwamba FAITH Alimkabidhi Dispatch
Lakini hajaileleza Mahakama Kwa Namna alivyo Kihifadhi Kielelezo Hicho
Haja eleza Mahakama Kwamba Mpaka anafika hapa Kielelezo hicho Kilivyo kuwa wapi na Kilikuwa kinatunza kwa namna gani
Naomba Nielekee Mahakama Yako Kwenye Kesi Ya DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN na Wenzake
WAKILI JOHN MALYA: OBJECTION naona Wakili analeta Jambo Jipya, Sababu Hapa P. O ilikuwa ni Kuhusu Competence ya Shahidi Juu ya Kielelezo
WAKILI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji nafikiri Wakili angetukia kwanza anisikilize na Mahakama Yako iniachie nafasi Nionyeshe Natokea wapi
WAKILI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Ilitakiwa Ionyeshwe Kwamba Kielelezo Kile akijachezewa Mpaka Kuja Mahakamani
Katika hili hili Kesi ya DPP VS SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER Ishu Ilikuwa ni Shahidi Wa Jamhuri Kuonyesha Chasis Namba ya Gari na Kwa Bahati Mbaya Shahidi alishindwa Kufungua Bonet ilioneshe Ushahidi Wake
Na Wakati Wa Ushahidi Wale alisema Anatokea Himo wakati Gari Ipo Moshi Ndiyo zikatokea Hizo Ishu
Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Shahidi Ilikuonyesha Kwamba Alilioata wapi Kielelezo na alikaa nacho ilikuweza kukileta Kielelezo
Hilo Haku fanya na wala Hakuileza Mahakama Hiki Kielelezo alikabidhiwa na nani
Ni Hoja yetu Kwamba Kukosekana Kwa Ushahidi huo
Kwa hayo tuliyoyaeleza ni Maoni yetu Kwamba Kielelezo Hiki (Dispatch) haiwezi Kupokelewa
Mheshimiwa Jaji naomba Kumalizia Kwa Kurejea kwenye Hati ya Mashitaka,
Hati ya Mashitaka I akin ana na Ushahidi Wa shahidi
Pale anaposema alikamatwa na Kufunguliwa Mashitaka kwa Makosa aliyo fanya Wilaya ya Mwanga
Hati anayotaka Kuleta Yeye inaongelea Makosa Yaliyofanyika Dar es Salaam
Hakuna Sehemu aliyo weza Kulinganisha Kosa akilofanya Wilaya ya Mwanga na Makosa aliyoshtakiwa Dar es Salaam
Haya yote Kwa Ujumla hayana Sifa Ya Kupokelewa na Mahakama hii, Ni Maoni yetu Kwamba Katika Mazingira haya Tunaomba Mahakama Isipokee Vielelezo hivyo
Ni Hayo tuh Mheshimiwa Jaji
JAJI: Mmemaliza..?
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula: Ndiyo
JAJI: Nakukumbusha Wakili Nashon Nkungu Kwemye Sababu Zako Za a Kuunga Mkono Usijibu Hoja ambazo zimetolewa na Upande Wa Mashitaka
NASHON NKUNGU: Sawa Mheshimiwa Jaji, Ingawa napata Ugumu, Naomba Mahakama Univumilie naona Hoja Nyingi Zinakuwa against na Hoja zao
JAJ: I Ndiyo Changa Moto tunazopata Eneo hili
WAKILI wa SERIKALI Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Naomba Kuwakumbusha Kwamba Siyo Haki yao Kujibu
Huyu siyo Mtu aliye leta Motion
Jaji Nakukumbusha Mr. Hila Kwamba Hilo siyo Jambo Jipya, nimemkumbusha Kwa sababu Hakwepo Mahakamani
NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji Naunga Mkono Upokelewaji wa Vithibiti hivi Kwa Pamoja kwa sababu Nimeona vimekidhi Matakwa Makubwa Matatu ambayo ni RELEVANCE, MTERIAL na COMPETENCE
Sijaenda Kwa Haraka Haraka kwenye Proceedings Za Mahakama hii
Lakini niliona ina Case Namba, Ina jina la Mshitakiwa
JAJI: Hiyo ni Nyaraka gani
WAKILI NASHON NKUNGU: Court Proceedings
NASHON NKUNGU: Pia Nikihamia Kwenye Charge sheet, Sitoenda Kwenye Content nitajikita Hasa yake Maeneo alisema ni Copy, Nimeona kweli ni Copy Nimeona namba ya Kesi namba 77 ya 2020 na Relevance InaKuja Kwa sababu akishatueleza Kwamba alipelekewa Oysterbay na Kwa kutumia Charg Sheet hii alipelekewa Mahakama ya Kisutu
Kwa Swala la Relevance Kwa Mujibu Wa Kifungu cha
WAKILI WA SERIKALI: OBJECTION Mheshimiwa Jaji anachokifanya Wakili anajibu
JAJI: Mr. Hila anachokisema Unaenda Ndani Sana
NASHON NKUNGU: , Sawa Mheshimiwa Jaji, Kingine Kinachoifanya niunge Mkono ni Kesi ya DPP VS MIZIRAHI Ukurasa wa 8
JAJI: We Unayo hiyo Nakala ya MIZIRAHI Kwa Maana Nakumbuka Ina chukuliwa a kutoka. Kwenye kesi ya ABEL GAZILABO
NASHON NKUNGU: Mimi ninayo tutawapatia pia, neona Kwenye kesi hii Inasisitiza Knowledge Wala Siyo Sufficient Knowledge
Kwa hayo Machache, Naomba Sababu za Kuunga Mkono Zichukuliwe
WAKILI JOHN MALYA: Mheshimiwa Jaji Nita ongea akwa Kifupi Sana na Kwa Bahati Nzuri sikuwa nawasikikiza Upande wa Mashitaka
Swala la Kwanza la Barua ni, Naona Lazima Barua Isomwe na Charge Sheet na Proceedings kwa hiyo Barua ni Relevant
Zaidi Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 8 cha Sheria Ya Ushahidi, Kwamba Matters ambazo zipo Connected at anytime zinaweza kuibuliwa
Shahidi alieleza Ni Muda gani Kila Nyaraka aliiimiliki, kwa Madhumuni gani na alishughulikia Vipi, kwa Hiyo naona ni Shahidi Competent
Kwa sababu hiyo tunaomba Nyaraka aza Shahidi Zipokelewe Bila Wasiwasi wowote
WAKILI PETER KIBATALA: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Nne tunafunga Mkono, Kupokea Kwa Set Ya Nyaraka zote Nne, Kwa Maana Nyaraka zote zimekidhi Vigezo Vya Msingi
Na Yeye Mwenyewe ameweza Kutengeneza Misingi ya hizo Nyaraka
Ameeleza Kwa namna alivyokaa na Vielelezo Vyote kuanzia alipokabidhiwa
Na sisi Washitakiwa wanne tunasubiria Kujanakuzijaribu Velacity yake Mbele ya Safari wakati wa Cross Examination
WAKILI FREDRICK KIHWELO: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa tatu ataanza Wakili Matata Na Baadae nitafuata Mimi
WAKILI DICKSON MATATA:, ASANTE Mheshimiwa Jaji
Upande wa Jamhuri waliweka Mapingamizi Matatu, Moja ikiwa kwa Nyaraka ambazo Shahidi anaomba Kuingiza a Mahakamani kwa Maana Barua, Charge sheet, Proceedings na Dispatch hazina Relevant
La Pili Ni kwamba Hati Ya Mashitaka ni Photocopy na Kwamba haijakidhi Kifungu Cha 66 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6
Na Pingamizi la Tatu Kwamba Dispatch, Shahidi Siyo Competent Kuweza Kutender Dispatch
Mheshimiwa Jaji nitajibu Kwa Ujumla na Wakili Mwenzangu atakuja Kujibu pale Nitakapo Ishia
Mheshimiwa Jaji nianze na Swala la Relevance
Mheshimiwa Jaji ipo katika Kumbukumbu Za Mahakama hii Kupitia Shahidi Kwamba Jana alieleza Mahakama Kwamba alipata Taarifa za Shahidi D/C Msemwa ambaye alikuwa Shahidi Wa Jamhuri Katika Shauri Dogo
Kwamba alikuja kutoa Ushahidi, Ambao Ushahidi Ule Kimsingi Ulionyesha Kwamba D/C Msemwa Wakati Mtuhumiwa Namba 3 anakamatwa na Kuletwa Dar es Salaam alikuwa Central Police Dar es Salaam
SHAHIDI: anasema hiyo Hakuwa Kweli Kwasababu yeye Mwaka Jana Tarehe 14 May 2020 baada ya Kukamatwa Mwanga na Kuletwa Dar es Salaam alipokelewa na D/C Msemwa
Sitaki Kuzuia ngumza Sana Kuhusu D/C Msemwa Pale Oysterbay, Itoshe Kusema Kwamba a baada ya Kuongea Sababu hiyo na Kwamba Kwa Sababu anajua D/C Msemwa alikuwa Oysterbay aliamua Kuja Kujitolea Kuja Kutoa Ushahidi Ili Kuja Ku Disaprove alichokisema D/C Msemwa
Na akasema ili Kudhibitisha Hayo, aliwasilina na Wakili wake (Peter Kibatala) alisema Kwamba Ni Wakili aliye husika Kutetea Mwaka Jana Kwamba ni Kesi namba 77 ya Mwaka 2020 ambayo ni Jamhuri Vs Lembrus MCHOME ambayo ilikuwa Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu
Aliwasilina na Wakili wake ili aweze Kupata Charge sheet na Proceedings Za Kesi hiyo na Alisema Kwamba Sababu ya Kuomba Nyaraka hizo
Ilikuwa ni Kuthibitisha Kwamba aliwahi Kufika Kituo cha Polisi Oysterbay Na Baada ya Hapo Ndiyo alipelekewa KwabHakimu Mkazi Kisutu
Na Kwamba a alipokuwa Kituo cha Polisi Oysterbay Ndiponalipokutana na D/C Msemwa
Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Ni Wasilisho letu Kwamba Nyaraka hizi ni Relevant na Kwasababu Malengo ya Nyaraka hizo ni Kutaka Ku Disprove Kile alichokisema D/C Msemwa
Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Pingamizi walilileta Upande wa Serikali Kwamba Nyaraka hizi siyo Relevant, Tunaona ni Pingamizi ambalo halina Mashiko
Kwa Sababu Hakuna Namna D/C Msemwa angeweza a kuwa Oysterbay na wakati huo huo akawa Polisi Central Dar es Salaam Wakati ni Vituo tofauti
Na Mheshimiwa Jaji Bila hata Kuingia Kwenye Barua yenyewe, ilikuwa ni Barua ya Kuomba Nyaraka Kuja kutumika Kwenye Kesi hii
Mheshimiwa Jaji nije kwenye Swala la Photocopy, ni Pingamizi la JAMHURI Kwamba Hati ya Mashitaka ni Photocopy na Kwamba Imekiuka Kifungu cha 66 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2019
Na Wamesema Kwamba Imekiuka Kifungu Cha 65,66,67 na 68
Mheshimiwa Jaji Nianze Kwa Kusema Kwamba Shahidi Alianza Kwa Kulay Foundation Vizuri kwa kuieleza Mahakama ni Kwanini amekuja na Photocopy
Ni Maelezo ya Shahidi Kwamba Yeye Mwenyewe akiwa na Dada anayeitwa FAITH
Baada ya Kukabidhiwa Barua Kama Nyaraka Walizooomba Mahakama Ya Kisutu
Kwamba alienda Kisutu akiwa na FAITH na Alipofika Alikutana na Mmama Kwenye Chumba ambacho alikitaja
Na Kwamba Baada ya Kufika alimkabidhi Barua aliyopewa na Peter Kibatala ya Kuomba Nyaraka hizo, na Kwamba Yule Mama baada ya Kujiridhisha inafana na Barua iliyopo Pale Mahakamani
Alimpitia Lembrus MCHOME Court Proceedings na akampa Photocopy ya Charge sheet
Shahidi akauliza mbona nimeomba Certified Copy, Mama akajibu Kwamba hii Ndiyo tuliyonayo
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Fault ya Kupewa Photocopy haijatokana na Mteja wetu ni Fault Ya Mahakama
Sisi tunaona Pingamizi Halina Mashiko
Kwa sababu Kifungu cha 67 ya Sheria ya ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019 Inaruhusu Kutumiwa Kwa Photocopy pale ambapo Kuna Mazingira kama Yaliyotokea Kwenye kesi hii
Naomba Nikisome
67(a)Secondary Evidence May be given…………………
ANAENDELEA KUSOMA
11/30/21, 10:29 – Irene Lema: Naomba Kusisitiza 67(c) When the Parties Offers Evidence of its contents not for other Reason……………
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho la Upande wa Jamhuri Kwamba tulitakiwa Kuomba Notice to Produce Chinese ni ya kifungu cha 68
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Letu Kwamba Kifungu Hiki awajakitazama kwa usahihi, Katika Mazingira ya kesi yetu
Ilikifumgu cha 68 ya Sheria ya Shahidi Kiweze Kutumika ni pale ambapo Masharti Yaliyowekwa Katika Kifungu (a) Mheshimiwa Jaji naomba kukisoma
Mheshimiwa Jaji Kwa Kifupi Kifungu cha 68 kina Sema Kwamba Uwezi Kutumia Evidence ambayo ni Secondary Kama Inaangukia Kwenye Kifungu 67(a)
Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Kielelezo Kinacho Ombwa Kuingia Mahakamani Kipo sahihi na akija Kosa Sifa yoyote ya Sheria Ya Ushahidi
Mheshimiwa Jaji Kwa namna Nyingine Kwamba, Tufanye Kweli Tulitakiwa Kutoa Notice to Produce Kitu ambacho nakipinga Kwa Nguvu zote
Lakini Bado Mahakama Inayo Uwezo Wa Kupokea Secondary Evidence Kwa Kutumia Kifungu hicho hicho cha 68 68(g)
Mheshimiwa Jaji Kwa kuzingatia Kwamba Photocopy hii alipewa na Mahakama na Kwa Kuzingatia tupo Kwenye Ndogo inayohitaji Uharaka
Na Kwa kuzingatia Kipengele (g) Mahakama Inayo Mamlaka ya Kukipokea
Ni Wasilisho letu Kwamba Pingamizi hilo halina Mashiko na litupiliwe Mbali
Mheshimiwa Jaji nije kwenye Swala la Competence
Na specifically nitazungumzia Kuhusu Dispatch
Mheshimiwa Jaji Ni Submission ya Shahidi Kwamba alipofika Dar es Salaam alienda Kuonana na Wakili wake Peter Kibatala
Na Baada Kuonana na Wakili wake, Wakili wake alimkabidhi Barua na Dispatch akiwa yeye Shahidi Na Mtu anaitwa FAITH
Na Kwamba Baada ya Kukabidhiwa yeye na FAITH waliongozana Kwenda Mahakama Ya Kisutu Wakiwa na hiyo Barua na Dispatch
Na ni Ushahidi Wake Kwamba kwanza Alipopewa Dispatch na Barua alijirodhisha Kama Dispatch na Barua Zinahusiana na Kesi namba 77 ya 2020
Na Kwamba waliofika Mahakamani Walienda Kuonana na Mmama Katika Chumba ambacho alikitaja yeye Shahidi akiwa na Barua na Dispatch
Na Kwamba waliofika Mahakamani Walienda Kuonana na Mmama Katika Chumba ambacho alikitaja yeye Shahidi akiwa na Barua na Dispatch
WAKILI WA SERIKALI Pius Hilla :Mheshimiwa Jaji tumevumilia Sana Lakini Sasa Wakili asitoe Ushahidi, Hakuna Sehemu Shahidi alisema alienda akiwa na Dispatch alisema alienda na Barua
WAKILI DICKSON MATATA: Naomba Mahakama itukumbushe, Mimi Nilisikia Kwamba Walienda na Barua pamoja na Dispatch
Jaji napekua Faili lake
Jaji anasoma ila Hakuna Sehemu Jaji Kaandika Kuhusu Dispatch
Kumbukumbu za Jaji Hakuna Sehemu Dispatch imetajwa
JAJI: Mimi Niliandika Kwamba alikabidhiwa Barua sioni sehemu ya Dispatch
WAKILI PETER KIBATALA: Kuna Mahala Tunalinganisha Hapa KWAMBA, Paonyesha majibu ya Wakili na Shahidi
Kibatala ANASOMA
JAJI: Unalinganisha Wapi Kwenye Live..?
Mahakama kichekoooooo
KIBATALA: Sawa lakini Kama Mahakama Haiku andika atuwezi Kufanya lolote
Kwamba Hakusema Swala la Dispatch
JAJI: Mbeleni Mpaka Wanafika Mahakamani hapa Walikuwa na Dispatch Ila sijaona sehemu Kwamba FAITH Alimkabidhi Barua na Dispatch, Ila Baadae alikuwa na Dispatch
WAKILI WA SERIKALI Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Kwa Hiyo Dispatch ipo au Haipo
JAJI: Dispatch ipo kwa Sababu Mbeleni huku naona Kuna sehemu alisema Kwamba awalipo fika hapa walikuwa na Dispatch
WAKILI WA SERIKALI: Lakini haionyeshi Dispatch alipata wapi na Ilikuwa Kwenye Custody yake tangu saa ngapi?
WAKILI DICKSON MATATA: Mheshimiwa Jaji Shahidi aliweza Kusema Kwamba alikabidhiwa Barua na Dispatch na Aliweza Kutaja Kuwa Ilikuwa na Rangi ya Pinki, Juu Imeandikwa Classic Dispatch Book
Inamaneno yameandikwa COURT 2
Ndani yake ina
anuani ya Mahakama
Kwa Maoni yetu shahidi aliweza Kusema Kwamba alipata wapi na alikaa nayo, Ni Ushahidi Wetu Kwamba Shahidi ni Competent
Kwa sababu Pingamizi lao Lilikuwa linahusiana na Competence na siyo Swala la Chain of Custody
Tunaiomba Mahakama Inapokuwa inatoa Maamuzi Juu ya Competence
Ijielekeze kwenye Kile Kilicho amriwa Katika Kesi Ya DPP VS MIZIRAHI na wenzake Watatu Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, Criminal appeal namba 293 ya Mwaka 2016, Ukurasa wa Saba na Nane aya ya kwanza
Iliposema posseser anaweza Ku tender Document
Inasema…….. ANASOMA
Shahidi alionyesha ana hiyo Knowledge na aliposess Nyaraka hiyo tunaomba Mahakama Imuone ni Competent na Tunaomba Mahakama Itupile mbali Pingamizi hilo
Mheshimiwa Jaji naomba Wakili Mwenzangu amalizie
WAKILI FREDRICK KIHWELO: Mheshimiwa Jaji Mimi nitakuwa na Jambo Moja
Mheshimiwa Jaji Wakili Wa Serikali Wakati anazungumzia Swala la Dispatch , alisema Kutoka Kutajwa kwa Reference namba kwenye Dispatch
Kwa Maoni yangu Mheshimiwa Jaji alikuwa anazungumzia Authentication ya Dispatch hiyo
Mheshimiwa Jaji Wakati Shahidi anatoa Ushahidi Wake, Alizumgumzia Kidogo Kuhusu Dispatch hiyo kwa Kutaja Features Mbalimbali kama Rangi, Jina Lililopo Juu Kwa Maana Classic Dispatch Book na COURT 2
Naalikwenda Mbali Kwamba Ndani palikuwa na Tarehe, Anuani ya Barua na Sahihi ya Mpokeaji
Kwa Maoni yangu Kwamba aliweza Ku authenticate
Mheshimiwa Jaji Pia naomba nizungumzie Kuhusu Swala la Hati ya Mashitaka
Kwamba Shahidi Ameleta Nakala Na Shahidi alieleza kwamba Kwanini alileta Nakala
Kwakuwa Shahidi amesema Kwanini Shahidi Ameleta Nakala, Ni Submission Yetu Kwamba Ushahidi Wa Shahidi Unapaswa Kuchukuliwa akwa Uzito unaostahili
Na hilo pia lipo Katika Sheria Kesi Ya GOODLUCK KYANDO Vs REPUBLIC Criminal appeal 118, ya 2003 ipo kwenye Tanzania Law Report Kwenye Ukurasa wa 363 na Specifically 367
Mheshimiwa Jaji Kwa hili na yake ambayo yemezungukzwa na Wakili Mwenzangu Dickson Matata Naomba, Itupilie Mbali Mapingamizi na Ikubali Vielelezo Vilivyoletwa Mbele Yako
Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
JAJI: Jamhuri
WAKILI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Kwa Ufupi sana Naanza na Hoja ya Wakili Msomi Dickson Matata
Alianza Kujibu Hoja ya Relevance
Wakati anazungumzia Hoja ya Relevance
Ni kweli Shahidi alieleza hayo, lakini Hoja yetu ya Msingi ni Hayo aliyiyasema alipaswa aoanishe kwenye Hizo Nyarak
Tunaimbaia Mahakama Kwamba Vitu anavyosisema Vilipaswa Pia Kwa al Kuangalia hizo Nyaraka utayakuta
Kwa Ushahidi Mwingine sasa Yeye Kuunganisha
Yeye anasema Hakuna Uwezekano wa DC Msemwa Kupatikana Oysterbay na Mwaka huo huo Kuwa Central Police Dar es Salaam
Ingelikiwa anasema Kwa Siku hiyohiyo Sisi tuna Isingewezekana kwa Swala hili sisi tunasema hakuna Muunganiko
Akaenda ambali akasema Kwamba Nyaraka zile zimelenga Katika Kuthibitisha Kwamba DC Msemwa Hakuwa Kuwa Central Police Dar es Salaam
Walitakiwa Sasa Kuonyesha Nyaraka ambazo Ndani yake Ukizisoma Zina onyesha Kwamba DC Msemwa alikuwa Oysterbay Police
Sasa Kwakuwa Nyaraka hizo Kwa Hati ya Mashitaka na Proceedings zinaonyesha Mashitaka Ya phonograph
WAKILI PETER KIBATALA: OBJECTION Wakili anaruhusiwa Kwenda Ndani tena ya Proceedings
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Eneo Lingine Mwenzetu aligusia Swala la Secondary Evidence
Mwenzetu alielekeza Mahakama Kifungu cha 67 1(c) na aakaisomea Mahakama Kwa Ufasaha
Katika Hiki Kifungu, Wenzetu hawawezi Kupata Hifadhi hapa
Walitakiwa Kuieleza Mahakama Kati haya Matatu, Nyaraka Halisi either Imepokea, ama Nyaraka halisi imeharibika, ama kwa Sababu ambazo hazitokani na wao Wameshindwa Kuleta Nyaraka hiyo Ndani ya wakati
Sasa Kusema Pekee Kwamba aliyetuhudumia akituambia Kwamba hii Ndiyo Nyaraka pekee, haitoshi kwa Kusema
Badala yake Walipaswa Waonyeshe Jitihada Walifanya Nini Baada ya Kuambiwa Hivyo
Badala yake wanaitupi Mahakama Lawama Badala ya Kusema Walifanya nini
Kwa Maoni yetu siyo Sahihi
Vilevile Mheshimiwa Jaji Mwenzetu anaomba Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo kwa kutumia Kifungu Cha 68(g)
Huu siyo Wakati wake,
Alipaswa aiombe Mahakama Kabla hatuja weka Mapingamizi
KWA hiyo Kitendo cha Kuomba Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo Wakati wa Mapingamizi, Kwa Maoni yetu Siyo Sahihi
Mwenzetu Hakusema kwamba Nyaraka hii Kwa Mujibu kwa Kifungu cha 65 ni Secondary Evidence
Kitendo Cha Kuto Jibu Maana yake Wenzetu wamekubali na hawana Kipingamizi nalo
Vilevile Wenzetu Wamezungumzia Kuhusiana Na Swala la Competence Ya Dispatch
Wamezungumzia Competence Ya Shahidi Yenye Connection Na Dispatch
Mheshimiwa Jaji hapa tunaona Wenzetu wakichanganya Mambo mawili Kwa Wakati Mmoja
Wenzetu Wanasema Kwamba Kwa Sababu Shahidi ameweza Ku Identity Unique Features basi ana Knowledge
Mheshimiwa Jaji Utambuzi wa Nyaraka na Kilichopo ndani ya Nyaraka Ni Vitu Viwili tofauti
Kutambua Nyaraka Peke yake Haitoshi
Kwa Maoni yetu Kutambua Nyaraka Na Kujua Kilichopo ndani ya Nyaraka Ni Tofauti
Ugomvi wetu ni Kwamba Shahidi hajaweza Kutuambi Kilichopo Ndani ya Nyaraka ni nini
Sisi tunasema Hakuna Ushahidi Wa Shahidi Unaonyesha Kwamba FAITH Ali transfer Dispatch Kwa Shahidi
Connection hii inakosekana
Wenzetu Walitakiwa Wajibu Hoja yetu Katika Misingi huu, Kitu ambacho hawajafanya
Mwisho Wenzetu Wameielekeza Mahakama Katika Kesi Ya GOODLUCK KYANDO, Kitu ambacho sisi tunasema Principle hii haiwezi Kutumika hapa Kwenye kesi hii Wanaongelea Kielelezo ambacho Kipo Kwenye Kumbukumbu za Mahakama
Sisi tunasema Hoja za Wenzetu hazijajibu Hoja zetu
Sisi tunaomba Mahakama Isizingatie Hoja zao Kwa Sababu Hazina Nguvu Kisheria
Mheshimiwa Jaji Samahani, Walizungumza Pia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI
Kwamba Ku possess Kukikuwa Kunatosha Kuonyesha Kwamba Kiliwwza Kuwa Kwenye Miliki yake
Sisi hatuja kataa, Bali tunasema Hicho anachotaka Kukitoa Ndiyo cha Faith
Kwa Hiyo Kesi zote Mbili hazina Connection na Kesi hii
Maombi yetu ni Vielelezo Hivi visipokelewe na Hoja za Wenzetu Kuhusu Mapingamizi zisitiliwe Mkazo
Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Jaji anaandika Kidogo, Wakati pande zote mbili Wamemaliza Kuwasilisha Hoja zao
JAJI: nimewasikia Pande zote mbili kwa Hoja zote mbili nahitaji Ku digest
Nahitaji Muda wa Dakika 45 kama naweza Kuwaita Mapema nitawaiteni
Tutarudi Saa Nane na Dakika 25
Jaji anatoka
Jaji amerejea Mahakamani Muda huu Saa 9 na Dakika 17
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Mahakamani
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando:Upande wa Jamhuri Quorum ipo vile vile na tupo tayari
WAKILI PETER KIBATALA: na sisi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari na Quorum ipo Vilevile haijabadirika
JAJI: Muda Mfupi Uliopita kabla Mahakama Kupumzika
Niilisikiliza Hoja za Pande zote mbili
Sasa Uamuzi ni Kama Ufutavyo
Shahidi Wakati anatoa Ushahidi Wake ambapo ni Barua Kutoka Kwa Wakili Wake Peter Kibatala Kwenda Mahakama Ya Hakimu Mkazi, Dispatch na Mwenendo Wa Kesi pamona na Hati ya Mashitaka Kutaka Kuingia Kama Kielelezo
Jambo ambalo lilipingwa na Mawakili wa Serikali Kwamba Moja Nyaraka hizo hazina Uhusiano na Kesi (Relevance)
Na Pia Kwamba Hati Ya Mashitaka Ilikuwa ni Nakala na siyo Nakala Halisi
Tatu ilikuwa Kwamba Shahidi ajaonyesha Kwamba anaifahamu Dispatch
Mahakama Kwa kuzingatia Hoja zote za pande Mbili
Na Mahakama Ikazingatia Kwamba Nyaraka hizi Zinazoombwa Kuingia zitaishia Kwenye kesi hii Ndogo
Pia Kwamba Shahidi ana tatizo la kina Ki Afya
Na Kwamba Ni Kweli Kwamba Nyaraka zinatumika Kuuliza Maswali lakini Mahakama Inayo Muda wa Kuzichunguza
Kwa Sababu hiyo Mahakama Imeona izipokee Nyaraka kuzingatia Uamuzi Wake autaokuja Kutoa Mbele
Mahakama Inapokea Barua Kwenda Kwa Hakimu Mkazi Kisutu kama Kielelezo Namba 1
Mahakama Inapokea Dispatch Kama Kielelezo Namba 2
Mahakama Inapokea Nakala ya Hati Ya Mashitaka ambayo ilikuwa imefunguliwa Mahakama ya Kisutu Jamhuri Vs Lembrus MCHOME
Mahakama Inapokea Pia Mwenendo Wa Kesi hiyo namba 77 ya Mwaka 2020.
Kama nilivyosema Kwamba Mahakama Itatoa Uamuzi Juu ya Nyaraka hizi wakati Maamuzi wa Kesi Ndogo
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando; Naomba Kwa Record Juu ya Namba, Kuna Kielelezo Cha Goodluck
JAJI: Basi naomba Kubadirisha Namba,
Barua itakuwa D2
Dispatch Itakuwa D3
Hati ya Mashitaka ni D4
Na Mwenendo ni D5
JAJI: naomba Sasa Shahidi akabidhiwe aweze Kusoma
JAJI: Shahidi Nikikumbushe Kwamba Uliapa, na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo
WAKILI FREDRICK: Isome Barua hiyo
Shahidi… ANASOMA BARUA Kutoka TANAFRICA LAW kwenda kwa Hakimu Mkazi Kisutu
Shahidi anasoma kwa Kingereza kile cha Ndani Ndani kabisa (BBC ENGLISH)
Mahakama Imetulia Vizuri Kabisa inasikilizwa Kingereza Kinachovuti Kwa Namna anavyotamka Maneno Ya Kingereza (Pronunciation)
Nafikiri ni Mpare Wa Pili Kumsikia Kuongea Kingereza kizuri baada ya Waziri Mkuu Cleopa Msuya
Jaji Soma na Dispatch Book
Shahidi anasoma Dispatch Book.
WAKILI FREDRICK: naKukabidhi Hati ya Mashitaka Shahidi
Shahidianasoma Hati ya Mashitaka pia Kwa Kingereza
WAKILI FREDRICK: Nitakukabidhi Mwenendo Wa Kesi na nitataka Usome Page ya Kwanza na Ya Mwisho
Shahidi anasoma Pia Case Proceedings Kwa Kingereza Pia
Anasoma Page ya Mwisho Sasa….!!!
Shahidi amemaliza Kusoma Vielelezo Vyote, Lakini Mawakili wa Serikali Wanamshangaa Mwonekano kano wake na Kingereza chake ni Vitu Viwili
WAKILI Fredrick KIHWELO: Shahidi Ulisema Kwamba Oysterbay Ulikaa Siku 14 Je Ulimaanisha nini?
SHAHIDI: Nikipofikishwa Oysterbay Mara ta Kwanza Nilikaa Siku Tano Kuanzia Tarehe 14 May Mpaka Tarehe 15 May 2020
Nilipo pelekwa Kisutu
WAKILI FREDRICK: Baada ya Hapo, Nikisomewa Kesi Na Kunyimwa Dhamana Nakutakia kwenda Magereza nikarudi Shwa Oysterbay Siku 14
Ilikuwaje Ukarudi Shwa Oysterbay
SHAHIDI: Baada ya Kukosa Dhamana, Hakimu alisema Nipelekwe Keko, Lakini Wakati Ule Palikuwa na Corona Siku pelekwa Magereza Badala Yake nikapekwa Oysterbay tena
WAKILI FREDRICK: Kwanini Sasa Hawakukupeleka Magereza Kama Hakimu alivyosema?
SHAHIDI: Kwa Uelewa Wangu Sababu ya Corona
WAKILI FREDRICK: Ulipimwa lini Corona
11/30/21, 13:41 – Irene Lema: Shahidi Siku ya Tarehe 19 May 2020
lini tena Ulipima Corona?
SHAHIDI: Hakuna zaidi Ya Kusubiri Majibu ya Corona
WAKILI FREDRICK: lini Ulirudishwa tena Mahakamani
SHAHIDI: Siku ya Tarehe 19 ambapo Hakimu alikataa Kunipokea Kwa Sababu Nilikuwa Nimtokea Polisi na siyo Magereza kama alivyoagiza
WAKILI FREDRICK: Siku ya Tarehe 03 nini Kilitokea
SHAHIDI: Siku niliyopelekwa Magereza
WAKILI FREDRICK: Na Siku ya Tarehe 05 June nini Kilitokea
SHAHIDI: Nilisomewa Mashitaka Kwa Njia Ya Mtandao na Hakimu akasema Kwamba Naweza Kupata Dhamana
WAKILI FREDRICK: Na Tarehe 08 June, Nini Kilitokea Siku ambayo nilipata Dhamana Maana Siku ya Tarehe 05 June sikukamlisha Masharti ya Dhamana
Umetaja Tarehe Nyingi Nyingi Je zote zipo Kwenye Mwenendo Wa Kesi
SHAHIDI: Ndiyo zote zipo
Tarehe 03 Mwezi Wa Sita Utaipata Ukurasa wa Ngapi
SHAHIDI: Ukurasa wa Tano
WAKILI FREDRICK: Tarehe 08 June 2020 Utaipata Ukurasa Upi?
SHAHIDI: Kwenye Ukurasa Wa Sita
WAKILI FREDRICK:
Nini Kilitokea Mwezi wa 10 August 2020
SHAHIDI: Hakimu aliniachia Kwa kifungu 225 baada Ya Upelelezi Kutokamilika
WAKILI FREDRICK: Nini Kilitokea tena
SHAHIDI: Nili kamatwa na kurudishwa tena Oysterbay
WAKILI FREDRICK: Uliwakuta Askari Gani
SHAHIDI: Mkuu wa zamu alikuwa Afande Msemwa, Hadija na Sam
WAKILI FREDRICK: Umekuwa Ulimtaja Afande Msemwa wa Oysterbay
SHAHIDI: Mwonekano kano wake ni Mweusi Kidogo kwangu, Anamwili kunizidi Kidogo.
Kitu Kingine ni Namba Yake
WAKILI FREDRICK: Namba gani?
SHAHIDI: Namba Yake Ya ajira
WAKILI FREDRICK: ambayo ni namba Ngapi?
SHAHIDI: H4323
WAKILI : Wakati Unajitambulisha Umesema Wewe Ni Mkulima, Ukiachana na Kilimo unafanya Shughuli Gani Nyingine
SHAHIDI: Najihusisha na siasa
WAKILI FREDRICK: Kule Mwanga Ulihojiwa Kwa Kosa gani
SHAHIDI: Kwa Makosa ya Kupiga Picha Gari ya Kiongozi Fulani wa Taasisi Fulani Tanzania
WAKILI FREDRICK: Ukashtakiwa kwa Makosa gani?
SHAHIDI: Kwa Makosa ya Kimtandao, Kitu ambacho Kilinishangaza
WAKILI FREDRICK: Unasema Ulitambua Afande Msemwa Kwa Namba Yake, Je Ilikuwa sehemu gani
SHAHIDI: Upande wa Kulia Kifuani
WAKILI FREDRICK: Wakati Unahojiwa hapa ulisema Kwamba Mwanga huku andika Jina Popote na Ulipokuwa Moshi pia Huku andikwa Popote
SHAHIDI: Watu wengi wana fikishwa Vituo Vya Polisi bila Kuandikwa Mahali Popote
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hayo ni Maoni yake
WAKILI FREDRICK KIHWELO: Naondoa Mheshimiwa Jaji
Na huo utakuwa Mwisho Wangu
WAKILI NASHON NKUNGU: Shahidi Ulisema Kwamba Askari walikuja Nyumbani Kwako Kukukamata, Je Walikuja nyesha Arrest Warrant.?
.
SHAHIDI: Hapana
NASHON NKUNGU: Nilisikia Pia Unasema Waliruka Geti
SHAHIDI: Ndiyo
NASHON NKUNGU: Je Walikuja na Kiongozi yoyote Wa Mtaani Kwako
SHAHIDI: Hapana
NASHON NKUNGU: Nilisikia Unasema Ulishtakiwa Kwa Matumizi Mabaya Ya Mtandao
SHAHIDI: Ndiyo
Nilisikia Ulikamatwa Kwa a Kupiga Picha Kiongozi Fulani Mkuu wa Taasisi Fulani hapa Nchini
SHAHIDI: Ndiyo
NASHON NKUNGU: Nilisikia Unasema Kuhusu Askari Msemwa hapa Mahakamani, Je Mnaugomvi
SHAHIDI: Hatujawahi Kuwa na Ugomvi
NASHON NKUNGU: Nilisikia Pia Kwamba Uliletewa Dar es Salaam Tarehe 14 May 2020
SHAHIDI: Ni sahihi
NASHON NKUNGU: Ulimuona Afande Msemwa Siku hiyo
SHAHIDI: Ndiyo
NASHON NKUNGU: Alikuwa Wapi
SHAHIDI: Mapokezi Oysterbay
NASHON NKUNGU: Ulikuwa Unapata Huduma Za Kibinadamu
SHAHIDI: Ndiyo
NASHON NKUNGU: kama Nini
SHAHIDI: Kama Chakula na Maji
NASHON NKUNGU: Nani alikuwa anakuhudumia Chakula
SHAHIDI,: Mimi nilikuwa Simfahamu Kwa sababu Nilinyimwa Kuonana Na Ndugu zangu
NASHON NKUNGU: Askari gani alikuwa anakuhudumia Kule Mahabusu
SHAHIDI: Askari wengi akiwemo Msemwa
NASHON NKUNGU: Asante Mheshimiwa Jaji
WAKILI MALYA:
Sasa Umesema Wewe Mwanasiasa Je Wa Chama Gani?
SHAHIDI: Wa Chadema
JOHN MALYA: Je Nikisema Wewe Mwanachama Umekuja Kusema Uongo Mahakamani Kumuokoa Mwenyekiti Wako Mahakamani?
Nitakuwa nasema Uongo.?
SHAHIDI: Uongo Mkubwa
JOHN MALYA: kwanini
SHAHIDI: Kwa sababu hata Ingekuwa Mtu wa CCM anatoa Ushahidi Wa Uongo ningekuwa Kuisaidia Mahakama
JOHN MALYA: Je Namba ya Msemwa Iko Kwemye Nini
SHAHIDI: Beji Kama Chuma Kifuani
WAKILI JOHN MALYA: Asante Mheshimiwa Jaji
WAKILI PETER KIBATALA: Shahidi Oysterbay ipo sehemu gani au Unakitu gani Kimepakana nacho?
SHAHIDI: Ubalozi Wa Marekani
KIBATALA: Asante Mheshimiwa Jaji sina Swali lingine
WAKILI WA SERIKALI Roberts Kidando: Shahidi Hebu tutajie Majina yako?
SHAHIDI: Lembrus Kapuya Mchome
WAKILI WA SERIKALI: Ulisikia Mtu anaitwa Mchome Je ni Ndugu yako
SHAHIDI Hapana, Utakuwa ni Ukoo labda
WAKILI WA SERIKALI: Kinachotofautisha MCHOME wewe na Wengine ni nini?
SHAHIDI: Maboma ya Kifamilia
WAKILI WA SERIKALI: Unamaanisha Nini
SHAHIDI: Ukoo Mkubwa au Kuna wachome Wengine Wala Hatufahamiani
WAKILI WA SERIKALI: Sasa Umetuambia Kwamba Ulikuwa Unafuatilia Mwenendo wa kesi Hii kwa Mtandao na Magazeti
SHAHIDI: Sahihi
WAKILI WA SERIKALI:
Ulimaanisha Mtandao ni Mitandao ya Kijamii
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Katika Social Media unatumia Mtandao Ipi
SHAHIDI: Twitter
WAKILI WA SERIKALI: Unatumia Majina gani?
SHAHIDI: Lembrus MCHOME
WAKILI WA SERIKALI: Umesema pia wewe ni Mwanasiasa
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Katika Sasa unanafasi gani?
SHAHIDI: Ni Katibu Wa Chadema Wilaya ya Mwanga na Pia Katibu Wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro
WAKILI WA SERIKALI: na utakuwa Mwanachama Hai,wa Chadema W
Kwa Muda gani?
SHAHIDI: Kwa Muda wa Miaka 11 Sasa hivi
WAKILI WA SERIKALI Katika Muda wote wa Kuwa Mwanachama Mwenyekiti Wako ni nani?
SHAHIDI: Ni Freeman Aikael Mbowe
WAKILI WA SERIKALI: Nitakuwa Sawa Nikisema Kwamba Kwenye Nyanja za Kisiasa Mnafahamiana Sana
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Unapendezwa na Uongozi wake
SHAHIDI: Sana
WAKILI WA SERIKALI: Kwenye Kesi hii, Ya Uhujumu Uchumi namba 16 ya 2021
Unafahamu alishitakiwa lini
SHAHIDI: Hapana Sikumbuki
WAKILI WA SERIKALI: ya Mwaka huu au Mwaka Jana
SHAHIDI: Mwaka huu
WAKILI WA SERIKALI: Wakati unashtakiwa Hati yako inasema Kwamba Unashtakiwa Kwa Publication of Ponograph
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Unasema Kwamba Kesi hiyo ili maliza Tarehe 10 Mwezi 08 2021
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Wakati Huo Freeman Mbowe ameshashrakiwa tayari
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Baada Ya Kuwa Umeshaaachiwa Je Ulifunguliwa Kesi Nyingine tena
SHAHIDI: Hapana
WAKILI WA SERIKALI: utakubaliana na Mimi Kwamba Kwa Kipindi hicho kabla ya Kufahamu
Kwanza Nikuulize Swali
Je Ni kweli Ulifahamu Msemwa alitoa Ushahidi Kupitia Mitandao
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Ni kweli Kwamba, Kabla ya Kuona Taarifa hizo na Ulichukulia Kwamba Shitaka lako limefutwa, Kabla ya Hapo Ulikuwa Ujawahi Kuomba Kupatiwa Mwenendo na Hati ya Mashitaka
SHAHIDI: Hapana
WAKILI WA SERIKALI: Katika Mitandao ya Kijamii Haswa Twitter Ambapo Unajulikana Kama Lembrus MCHOME
Namna ya Kutuma Ujumbe Unautengeneza Mwenyewe yani (User generator)
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Ukitaka Kuchukua Ujumbe wa Mtu Mwingine yani Retweet Unafahamu
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Kwenye Mtandao Wa Twitter, Kama Naelewa Utanifahamisha, Ni Information Ambazo Mtu anaweza Kuona zile ambazo umetweet na Kuziona
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Sasa na Mara Nyingine Umekuwa Uliandika Ujumbe Unaohusiana na Kesi hii Kule Twitter
SHAHIDI: Ndyo
WAKILI WA SERIKALI: Katika Moja wapo ya Vitu Ulivyotweet Ukasema “kesi Mikazo, Mashahidi wa Michongo” ulikuwa unamaanisha nini
SHAHIDI: Maana yake ni Mashahidi Wa Kuunga
WAKILI WA SERIKALI: Vipi Kuhusu Mawakili wa Serikali wa Michongo na Majaji wa Michingo
SHAHIDI: Kwasababu Mawakili wa Serikali Wanateta Mashahidi Wa Uongo
WAKILI WA SERIKALI: Na Vipi Kuhusu Majaji wa Michongo
SHAHIDI: Ndiyo Kuna Hukumu ambazo Wanatoa hazipo Sawasawa
Mahakama kichekoooooo
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo Unamalalamiko Kuhusu Kesi hii
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo wewe ni Shahidi Mwenye Malalamiko
SHAHIDI: Ninayo Malalamiko Kwa Sababu Mahakama inadanganywa
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe
SHAHIDI: Nataka Haki itendeke
Wakili wa Serikali Jibu swali Langu
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe
SHAHIDI: Ambao Watakuwa Wapo Sahihi Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Ni kweli Watu walikuwa wa nakupa Pole Kwenye Mitandao yako
Baada ya Kupata Ajali
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Walikuwa wa nakupa Moyo Kamanda Nenda Kapambane
SHAHIDI: Hiyo sijaona
WAKILI WA SERIKALI: Kitu Kilichokufanya Uje Kutoa Ushahidi, Unamfahamu linamuhusu Mshitakiwa Yupi?
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Nano
SHAHIDI: Katika Shitaka hili Dogo ni Mohammed Ling’wenya
WAKILI WA SERIKALI: Wakati Unaongozwa na Wakili Dickson Matata Na Fredrick Kihwelo Ni kweli Hukutoa Ushahidi huyu Mohammed Ling’wenya Mnafahamiana Lini na Wapi
WAKILI WA SERIKALI: Ni kweli Kwamba Wakili Peter Kibatala ambaye Ulimpa Maelekezo Kwamba aandike Barua Kwenda Kisutu, Yeye Siye anayemwakilisha Mohammed Ling’wenya
SHAHIDI: Ndiyo nafahamu
WAKILI WA SERIKALI; Kama unafahamu Sema sasa ni Lini sasa Ulifahamu Kwamba Peter Kibatala amuwakikishi Mohammed Ling’wenya
SHAHIDI: Kwenye VYOMBO Vya Habari
WAKILI WA SERIKALI: Na Unafahamu Kwamba Peter Kibatala Anamwakilisha Freeman Mbowe
SHAHIDI: Nafahamu Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Mwanzoni Nilikuuliza Kuhusiana na Jina Mchome, Turudi Sasa Kwa Jina la Msemwa
Je litakuwa na Watu wengi wanaoitwa hivyo
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Katika Ushahidi Wako Tangu Unaongozwa Jana Hukutoa Ushahidi Kwamba Kwa Jina hilo la Msemwa Wapo Watu Wengi Kwa jina la Msemwa
SHAHIDI: ndiyo
WAKILI WA SERIKALI Na Hukusema hawa watu wa Jina la Msemwa Wapo Wangapi Kwa Jeshi la Polisi
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Kwa Sababu Ulikuwa Ukifuatilia Kesi hii, Unafahamu Kwamba hii ni Kesi Ndogo Ya Pili
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Unafahamu pia Kwamba Katika Kesi Ndogo Ya Adam Kasekwa Msemwa alitoa Ushahidi
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Ulifahamu Lini Siku hiyo hiyo au
SHAHIDI: Sikumbuki
WAKILI WA SERIKALI: Sasa Shahidi Katika Ile Barua iliyopo lelewa Mahakamani ilivyoandikwa na Kibatala Kwenda Kisutu, Ni kweli Kwamba haina Jina la Mohammed Ling’wenya Popote pale
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Kutokana na Jinsi ilivyoandikwa ndiyo inaakisi Kile Ulicho Muelekeza Peter Kibatala
Shahidi Ndiyo
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI 6wa SERIKALI: Sasa Kwa Mazingira hayo hata Katika Ushahidi huu, Ni Mamubaliano Yako Kuja Baina yako na Peter Kibatala
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Wenzangu Waendelee
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula:
anasimama
WAKILI WA SERIKALI: Shahidi Naomba nianzie alipoishia Mwenzangu
Mheshimiwa jaji naomba ni Muonyeshe Shahidi Exhibit D2
Umeona Enheeeeeee
Nyaraka I naelekeza akwa nani
SHAHIDI: I naelekezwa Kwa Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu
WAKILI WA SERIKALI: Ni sahihi Ilimfikia huyo Hakimu Mkazi Kisutu
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Nyaraka hiyo Wamepewa nani na nani
SHAHIDI: Lembrus Mchome
Na Naibu Msajili Wa Mahakama hii
WAKILI WA SERIKALI: anapaitika Wapi
SHAHIDI: Mahakama hii
WAKILI WA SERIKALI: Yupo humu Ndani
SHAHIDI: Hapana
WAKILI WA SERIKALI: Nitakuwa Sahihi Kwamba Umekuja baada ya Kusikia, DC Msemwa Kusema Kwamba alimpokea Mohammed Ling’wenya Pale Kituo cha Polisi Central
WAKILI WA SERIKALI: Reference namba zinamuhusu Nani
SHAHIDI: Mbowe
WAKILI WA SERIKALI: Wakili Wako ni nani
SHAHIDI: Peter Kibatala
WAKILI WA SERIKALI: Anamwakilisha Nani katika hili Shauri
SHAHIDI: Freeman Mbowe
WAKILI WA SERIKALI: Nitakuwa Sahihi nikisema Freeman Mbowe anaitambua Barua hii
SHAHIDI: Hilo silijui
WAKILI WA SERIKALI: Ni kweli Kwamba Mohammed Ling’wenya atakuwa anajua Barua hiyo
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI DICKSON MATATA: Mheshimiwa Jaji Napinga Swali na Jibu sababu Lina Suggest Opinion
JAJI: Ngoja tumsikie
WAKILI WA SERIKALI: Swali langu Kwamba Hiyo Barua haionyeshi Kumfikia Bwana Mohammed Ling’wenya
JAJI: ni Wakati gani hapo Opinion,
WAKILI DICKSON MATATA: Kauliza Ni kweli Kwamba Mohammed Ling’wenya Ajui kuhusu Barua hiyo
JAJI: Basi Wakili wa Serikali Rudia Swali
WAKILI WA SERIKALI: Shahidi Ni kweli Kwamba Kwa Maudhui ya Barua hiyo haionyeshi Kumfikia Mohammed Ling’wenya
SHAHIDI: Hilo sijui
WAKILI WA SERIKALI: kuanzia Siku ya Jana Mpaka Leo Hii hakuna Sehemu yoyote Uliyo eleza Kwamba Uliwasiliana na Mohammed Ling’wenya
SHAHIDI: Ni sahihi
WAKILI WA SERIKALI: Ni sahihi Kwamba Mahakama Haijaonyesha Kwamba Mohammed anaufahamu wako wewe Kuwepo Mahakamani
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo nitakuwa nakosea Nikisema Wewe Umeletwa Kwa Madhumuni fulani fulani
SHAHIDI: Sana
JAJI: Shahidi Umesema
SHAHIDI: Sawa
WAKILI DICKSON MATATA: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ameshajibu
WAKILI WA SERIKALI: Hakuna Kurudia Swali
JAJI: Miye Mwanzo nimesikia Sana
WAKILI DICKSON MATATA: Namimi nimesikia Sana
JAJI: Wakili wa Serikali, Kwa Maslahi Ya Haki hebu rudia Swali
WAKILI WA SERIKALI: Habu Soma hii Nyaraka Paragraph Ya Pili
SHAHIDI: Shahidi anasoma Kwa Kingereza
WAKILI WA SERIKALI: Hebu ijibu Mahakama Mr. Freeman Aikael Mbowe ndiyo Mohammed Ling’wenya
SHAHIDI: Hapana
WAKILI WA SERIKALI: Hebu I ambie Mahakama Ni sehemu Gani imeandikwa Kwamba hizo Taarifa unazoomba Umelenga Kuthibitisha Kwamba Mr. MSEMWA Hakwepo Central
SHAHIDI: Hakuna
WAKILI WA SERIKALI: Katika hiyo Barua ni sehemu Gani Inaeleza Kwamba Ulikuwa Kituo Cha Polisi Oysterbay
SHAHIDI: Hakuna
WAKILI WA SERIKALI: Ni wapi Katika Barua hiyo Sehemu Inavyoonekana Kwamba Wakili anaye Mwakilisha Mohammed Ling’wenya Kwenye hiyo Barua
SHAHIDI: Hakuna
WAKILI WA SERIKALI: Ulisema Tarehe 14 Maya 2020, Wakati Umefikishwa Oysterbay Polisi, Miongoni Mwa Askari Aliyekuhudumia alikuwa na DC Msemwa
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Na Ulisikika Ukisema Kwamba ulimtambua DC. Msemwa kupitia Beji yake aliyo vaa
SHAHIDI: Hapana
WAKILI WA SERIKALI: Nitakuwa Sahihi Nikisema Kwamba Huyo DC Msemwa Uliyemtambua wewe alikuwa amevaa Uniform
SHAHIDI: ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo nitakuwa Sahihi Nikisema Ulimtambua DC Msemwa Baada ya Kuona Beji yake yenye namba yake 4323
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Toka Umeanza Kutoa Ushahidi Wako Siku ya Jana Mpaka Leo Hii Hakuna Mahala Umesema Kwamba alikwambia ni wakati Gani anaitwa DC Msemwa na Hukusema ni Wakati gani ulipata Kujua
SHAHIDI: Ndiyo
WAKILI WA SERIKALI: Kwa Kushindwa Kusema Ulijuaje anaitwa DC Msemwa, Mahakama ipo gizani
SHAHIDI: Si Kweli
WAKILI WA SERIKALI Abdallah Chavula: Kwa Ruhusa Yako tunaomba tuendelee Kesho Kwa sababu Muda hautoshi
WAKILI PETER KIBATALA Mheshimiwa Jaji Tulishaliomgea hilo Kwenye Briefing Kwamba Tumlimde Shahidi Haki yake ni Mtu aliye Pata Ajali
Na Kwamba tulimuomba Mpaka Kwa Wazazi wake, Shahidi Ni Magonjwa na Haki yake inaonekana
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Magereza Waliomba Asubuhi Kwamba tujitahidi tumalize Saa 11 ili Wapate Muda wa Kuwahi Kurudi Magereza
JAJI: ni Kweli Kwamba tulikaa pamoja Asubuhi Kwamba Kuna Jambo hilo la Hali ya Shahidi
Ni swala linahusu Haki
Haki Upande wa Mashitaka Kusikilizwa
Na Hali ya Shahidi Tunaona pia
Je Shahidi Unaweza Kesho kuwepo
Nikuombe Shahidi, Je Uwezi Kuja Kesho
SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji Haki yangu inaniwia Ngumu, Ila Kwa Sababu ni Ombi lako inanibidi nikubali
JAJI: jitahidi tuh, tuh ni Ombi kutoka kwa Jaji
Na hilo nimekuomba wewe Binafsi Siyo Kupitia Kwa Wakili
WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Hairisho Mpaka Kesho Tarehe 01 Mwezi wa 12 ilituweze Kuendelea na Cross Examination
JAJI: Upande Wa Utetezi Mnaye Shahidi Mwingine
WAKILI PETER KIBATALA: Tunaye Mmoja
JAJI: Shahidi Baada ya Kuwa Nimekuomba na Umenikubalia naomba Kesho Uje
Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi
Saa 3 Asubuhi
Basi nawatakia Jioni Njema
Jaji anatoka