Kesi ya Mbowe: Shahidi akiri kuwa maelezo yake yana dosari kubwa

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 31 Januari 2022.

…………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………..

Katika maswali 401 yaliyoulizwa na Wakili Peter Kibatala, shahidi Luteni Dennis Urio amejibu maswali 360 tu. Na miongoni mwa hayo 360, maswali 32 amesema SIFAHAMU, maswali 50 amesema ANAFAHAMU, 32 akisema NI SAHIHI na sita amesema HAKUMBUKI. Mengine amejibu NDIYO na mengine HAPANA

Kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamuhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa mahakamani mbele ya Jaji Tiganga.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

 1. Pius Hilla,
 2. Abdallah Chavula
 3. Jenitreza Kitali
 4. Nassoro Katuga
 5. Esther Martin
 6. Ignasi Mwinuka
 7. Tulimanywa Majige

Wakili Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo pamoja na wakili

 1. Michael Mwangasa
 2. Sisty Aloyce
 3. Gaston Garubindi
 4. Idd Msawang
 5. Maria Mushi
 6. Nashon Nkungu
 7. John Malya
 8. Dickson Matata

(Jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika kuwa wapo mahakamani)

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na tutaendelea na shahidi. Tupo tayari kuendelea.

Shahidi anaingia kutoka nje.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji nasi pia tupo tayari kuendelea.

JAJI: Nakukumbusha kwamba tarehe 28 ulikuwa upo chini ya kiapo na leo utaendelea kutoa ushahidi wako chini ya kiapo.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba sababu ya kelele za jenereta tufunge madirisha.

KIBATALA: Mr Urio, how are you?

SHAHIDI: I’m fine.

KIBATALA: Did you have a nice weekend?

SHAHIDI: Like … speak again.

KIBATALA: Did you have a nice weekend?

SHAHIDI: Like that.

KIBATALA: Shahidi umeshawahi kukutana na mazingira ya kuambiwa maneno mazito unayosema ya ugaidi?

SHAHIDI: Sijawahi kukutana nayo.

KIBATALA: Umesema hauna tatizo la kumbukumbu?

SHAHIDI: Sina tatizo la kumbukumbu.

KIBATALA: Iweje usikumbuke tarehe mbili muhimu za wewe kukutana na Mbowe na kwenda ofisini kwa DCI ukizingatia wewe ni mwanajeshi, na luteni wa Jeshi?

SHAHIDI: Kwanza Mheshimiwa Jaji Mheshimiwa Mbowe alikuwa ni ndugu yangu. Nilikuwa sijui kuwa ni kweli au si kweli mpaka nikaona kuwa kumbe ni serious.

KIBATALA: Wewe Luteni unaona umejibu swali langu la inawezekana vipi usikumbuke tarehe?

SHAHIDI: Sijawahi kusikia maneno mazito ndiyo maana nikaenda kutoa riport Polisi wafanye uchunguzi.

KIBATALA: Swali langu inawezekana vipi ushindwe kukumbuka tarehe ya matukio kama hayo?

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji mimi naona kama limejibiwa.

JAJI: Swali lilikuwa inawezekanaje kuwa asahau tarehe za mambo muhimu?

SHAHIDI: Ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kutoka kwa Mheshimiwa Mbowe. Sikuwa nategemea.

KIBATALA: Vipi kuhusu tarehe ya kwenda kwa DCI na yenyewe ulikuwa shocked?

SHAHIDI: Siyo duty yangu mimi kukumbuka. Kazi yangu ilikuwa kutoa ripori tu.

KIBATALA: Kwa kuwa unaomekana kujivua duty ya record ya tarehe, unaweza kutuisaidia kwanini na yeye DCI hakumbuki tarehe uliyokwenda ofisini kwake?

SHAHIDI: Sifahamu. Siwezi kumjibia.

KIBATALA: Siku unakwenda kwa DCI Kingai alikuwa summoned akaja. Unaweza kutuisaidia kwanini huyu Kingai mtu wa tatu na yeye hakumbuki ni tarehe ipi mlimkutana?

SHAHIDI: Siwezi kujua ni kwanini.

KIBATALA: Ni kwanini hata Inspector Swila ambaye ndiyo Afisa wa Upelelezi aliyefungua faili tarehe 18 Julai 2020, hakumbuki tarehe hiyo?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Je, kwa wewe kama Luteni wa Jeshi unaona ni sahihi kwa nyinyi watu wote hamkumbuki tarehe?

SHAHIDI: Siwezi kujibia.

KIBATALA: Umeshawahi kusikia msemo “The lights are on but no body at home”?

SHAHIDI: Hapana. Sijawahi kusikia.

KIBATALA: Kwanini tarehe 11 Agosti 2020 ndiyo maelezo yako yaandikwe mtoa taarifa ambaye ndiyo ulisababisha faili kufunguliwa tarehe 18 Julai 2020?

SHAHIDI: Hapana. Sifahamu.

KIBATALA: Wewe ni Luteni wa TPDF. Huoni kwamba inategemewa maelezo ya mtoa taarifa kuandikwa mapema kadiri inavyowezekana?

SHAHIDI: Siwezi kuijibia Polisi kwa sababu wao wana utaratibu wao wa kazi na mimi nina utaratibu wangu wa kazi.

KIBATALA: DCI alikufafanulia kwamba kwanini maelezo yako hayawezi kuchukuliwa siku ambayo wewe umeenda kuripoti?

SHAHIDI: Hawakufafanua chochote.

KIBATALA: Tarehe 11 Agosti 2020, kwa ushahidi wako ndiyo ulikwenda kutoa maelezo ya ushahidi wako kwa Inspector Swila.

KIBATALA: Inspector Swila alikufafanulia kwanini alisubiri mpaka mwezi mmoja baadaye?

SHAHIDI: Hakunifafanulia.

KIBATALA: Tukisema kuwa mliitunga kesi mapema kisha baadaye ndipo mkaanza kutafuta watuhumiwa nitakuwa nakosea kwa facts hizo?

SHAHIDI: Utakuwa unakosea.

KIBATALA: Unafahamu dhana ya infiltration?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Maana yake?

SHAHIDI: Kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa siri.

KIBATALA: Ni sahihi pia maana yake pana ni kutuma mtu kwenda kwenye kambi ya upinzani ili kupata taarifa kamili?

SHAHIDI: Hapana. Tactics inasema kwamba ni kitendo cha kutuma mtu kwa siri.

KIBATALA: Nikumbushe tena elimu yako.

SHAHIDI: Form Four.

KIBATALA: Unafahamu decoy?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Luteni wa Jeshi hufahamu decoy?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Mlijadili kwa pamoja kumpeleka mtu kwa Mbowe akiwa na vifaa aweze kupeleleza na kurekodi ushahidi?

SHAHIDI: Hatujawahi kujadili.

KIBATALA: Ni kweli katika ushahidi wako kwamba Mheshimiwa Mbowe alikuambia atachukua dola kwa namna yoyote, je, uchaguzi ulitajwa?

SHAHIDI: Nafahamu uchaguzi ulitajwa.

KIBATALA: Bado Jeshi lilikuwa halina role to play kwamba wewe ni mwanajeshi uliye kazini na Mbowe anataka ex-commandos, bado Jeshi lilikuwa halina sababu ya kupewa taarifa?

SHAHIDI: Ni taarifa ambazo hazina ushahidi. Bado Jeshi litapeleka kule kule kwa Polisi.

KIBATALA: Unamfahamu aliyekuwa Chief of Staff Luteni Generali A. Shimbo?

SHAHIDI: Namfahamu.

KIBATALA: Akiwa katika majukumu yake ulikuwa Jeshini?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Namnukuu. Tarehe 13/10/2010 (alisema) “Katika Uchunguzi huu, Jeshi limejipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na utulivu.” Uliwahi kusikia?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Bado unasisitiza kwamba mambo ya kiuchaguzi Jeshi halihusiki?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Huoni kwamba kwa kutoa kwako taarifa Jeshi lingefanikisha kuweka decoy (mamluki) wa kwenda kukusanya taarifa ambazo ni sahihi?

SHAHIDI: The issue ni kwamba mtu anaitwa Freeman Mbowe hapokei simu za kawaida. Anasema nitumie picha na profile yake ili ajiridhishe kwamba bado wapo katika service. Kwa hiyo endapo tumgetuma mtu ambaye bado yupo katika service angehundua.

KIBATALA: Kwa hiyo tactical appreciation yako ilikuambia kwamba Mheshimiwa Mbowe ana uwezo wa kujua profile zao?

SHAHIDI: Ndiyo. Unafikiri kwanini alitaka picture na profile zao?

KIBATALA: Katika ushahidi wako wote kuna mahala popote ulisema kwamba Mbowe alikuabmia kwamba ana access ya mtu mwingine Jeshini?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Tujadili kuhusu Tactical Appreciation. Ni sahihi kwamba kamanda anakutana na mazingira fulani ambayo kamanda anapanga vikosi vyake kukabiliana na mazingira hayo kwa muda kwa kupanga mkakati.

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Sasa wewe palikuwa na several unknown. Nimekuuliza kama Mbowe alikuwa na access Jeshini ukasema hujui. Sasa huoni kwamba tactical appreciation yako ilikuwa si sahihi?

SHAHIDI: Huyu bwana ningemwambia kuwa sitaki angemtumia nani? Ndiyo maana nilifanya Tactical Appreciation na kwenda kuripoti kwa DCI.

KIBATALA: Unakubaliana na mimi kwamba katika hali hiyo kuna mambo kadhaa wa kadhaa ulikuwa huyafahamu, ndiyo maana ukasema kwamba ulikuwa hujui kama alikuwa ameshaongea na watu wengine?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilikuwa sina uhakika kama Mbowe ana option A, B na C.

KIBATALA: Sasa jambo hilo linaendana na Tactical Appreciation?

SHAHIDI: Ndiyo linaendana.

KIBATALA: Kazi yangu ni kuuliza maswali.

KIBATALA: Wewe umesema kuwa ulikuwa huna uhakika kama Mbowe alikuwa na option A, B na C. Je ulijihakikishia kwa kumuhoji?

SHAHIDI: Sikumuhoji.

KIBATALA: Na unathibitisha kwamba alikuwa na trust yako yote?

SHAHIDI: Sijui kwa yeye sasa.

KIBATALA: Nakuuliza wewe.

SHAHIDI: Je, ni mimi peke yangu anayeniamini?

KIBATALA: Na hakuna mahala uliposema kwamba Mbowe alikutishia wewe au familia yako.

SHAHIDI: Sijasema.

KIBATALA: Na kwamba Mbowe alikuhaidi cheo kama incentive (motisha) yako.

SHAHIDI: Mbowe hawezi kunipa cheo Jeshini.

KIBATALA: Kwa hiyo Mbowe alikuwa hawezi kukuhaidi cheo kwa sababu alikuwa Mbunge tu?

SHAHIDI: Sahihi. Hawezi.

KIBATALA: Nashukuru kwa jibu lako zuri.

KIBATALA: Wakati Mbowe anakupa maombi yake, ulimkubalia au moyoni ulimkatalia?

SHAHIDI: Ilikuwa issue ya Tactical Appreciation. Ile kwamba nitachoma vituo vya mafuta, kuchoma masoko….

KIBATALA: Na kumdhuru Sabaya pia ulikuwa unachakata?

SHAHIDI: Sijawahi kumtaja Sabaya mimi. Nilitaja viongozi. Kwa hiyo baada ya kuchakata yote hayo nikaenda kwa DCI.

KIBATALA: Akili ya kawaida ya Luteni haikuwa na zaidi ya kumchimba kwamba anataka kulipua vituo gani, kukata miti sehemu gani?

SHAHIDI: Hata ingekuwa ni mimi, ukishaanza kunidodosa nakosa trust na wewe.

KIBATALA: Wakati mnakutana kupanga matendo ya uhalifu, hasa ugaidi, Mahakama itakapopima, itapima maneno yako dhidi ya maneno ya Mbowe kwa sababu hakuna sauti nyingine wala decoy?

SHAHIDI: Ndiyo maana nikatuma vijana.

KIBATALA: Kwani vijana hawa si washtakiwa? Wa ni wapelelezi wako?

SHAHIDI: Ni washitakiwa.

KIBATALA: Unakubaliana na mimi sasa mahakama itabidi ipime neno lako dhidi ya Mbowe kwa sababu hapakuwa na mtu mwingine pale?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Unakumbuka wakati wa utekelezaji wa majukumu yako, namna ulipompata Ling’wenya?

SHAHIDI: Nakumbuka.

KIBATALA: Unakumbuka uliongea na baba yake Ling’wenya?

SHAHIDI: Nakumbuka.

KIBATALA: Unakumbuka kwamba uliongea naye tarehe ngapi?

SHAHIDI: Sikumbuki.

KIBATALA: Unakumbuka uliongea naye majira gani?

SHAHIDI: Sikumbuki.

KIBATALA: Unafahamu kwamba Mzee Ling’wenya alikukatalia kumtoa mwanawe kwa sababu ya mambo yaliyomtokea mwanawe Jeshini?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba yeye alishamtafutia mwanawe Kazi ya kokoto?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba huyu Mzee (Baba yake Ling’wenya) ni Mwenyekiti wa Kijiji fulani huko Kusini?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Baba yake alipokutafuta baada ya kusikia mwanawe kakamatwa unakumbuka ulimjibu nini?

SHAHIDI: Sikumbuki. Ila niliwambia kuwa amuulize bosi wao.

KIBATALA: Kwani bosi wao ndiye aliyempigia kumwombea ruhusa kwamba kuna kazi?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Ulimwambia Mzee Ling’wenya kwamba kuna kazi kwa Mbowe lakini nataka akafanye mipango ya ugaidi?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Unafahamu maana ya entrapment?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Maana ya kumtoa mtu kafara?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Unakumbuka kwamba nilikuuliza unasali wapi kwa sababu gani?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Umeapa kwa Biblia. Je, unafahamu kuhusu Daniel?

SHAHIDI: Nafahamu kuwa walitupwa kwenye tundu la simba.

KIBATALA: Wewe kuna tofauti na walichomfanyia Daniel na Ling’wenya Mkristo mwenzangu?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Kwamba Ling’wenya alikuwa na kazi yake ya kubonda kokoto, wewe wa kikao chenu na DCI ukamtafuta kumwimgiza kwenye matatizo?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Wakati baba yake Ling’wenya anakutafuta kukuuliza kwamba mwanawe yupo wapi ukajibu “ongea na bosi wake”. Ni kweli?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Unafahamu kwamba Mzee Ling’wenya alistaafu bila doa lolote Serikalini?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba kama mzazi, anaumia kama iliyokuwa kwa Mama Maria kumuona mwanawe anateseka msalabani wakati hajafanya kitu chochote?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Je, inawezekana kwa mafunzo yako wewe yanaruhusu kiongozi wa askari wa chini, awaache askari wake wa chini wakati wa hatari?

SHAHIDI: Inategemea na mazingira.

KIBATALA: Je, ni mazingira gani kwa mafunzo yako wewe yanaruhusu kiongozi wa askari wa chini awaache askari wake wa chini wakati wa hatari?

KIBATALA: Unafahamu kwamba kwanini kwenye Platoon kiongozi anakuwa mbele, hata katika Biblia?

SHAHIDI: Sifahamu. Sijawahi kuona.

KIBATALA: Unafahamu kwamba Adam Kasekwa alipatwa na Battle Traumatic Fatique?

SHAHIDI: Mimi sifahamu. Sijawahi kusikia ana historia hiyo.

KIBATALA: Je, unafahamu kwamba katika maelezo ya onyo ambayo mnasema alikiri, nyinyi ndio mmem- record hivyo?

KIBATALA: Ni sahihi kwamba ulisema kwamba ulienda kwenye ofisi ya Admin Officer ukasoma
mafaili yao?

SHAHIDI: Siyo mafaili ya taarifa individual, bali taarifa za matukio tangu siku natoka.

KIBATALA: Je, ni sahihi kwamba hujui sababu ipi ambayo ilipelekea Adam Kasekwa kufukuzwa Jeshini?

SHAHIDI: Sijui zaidi ya utovu wa nidhamu.

KIBATALA: Unafahamu ni maeneo gani mahususi ambayo walitembelea kwa ajili ya kumdhuru Sabaya?

SHAHIDI: Bwire hakuniambia.

KIBATALA: Katika ushahidi wako hujui wala hujazungumzia kuhusu Milestone, Kokoriko na Triple B?

SHAHIDI: Sijazungumzia.

KIBATALA: Je, unafahamu kwamba walikamatwa kwa tuhuma za kupanga kufanya uhalifu wa kumdhuru Sabaya?

SHAHIDI: Ndiyo. Nafahamu.

KIBATALA: Wewe ukiwa katika kazi maalumu, hukuona sababu ya kuuliza kwa Bwire ni wapi walipanga kufanya uhalifu?

SHAHIDI: Kwanza mimi siyo kazi maalumu.

KIBATALA: Kwani aliyewatafuta hawa vijana ni Polisi au ni wewe?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Mbowe aliomba Polisi wamtafutie hawa vijana?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Ni kweli kwamba uliwatafuta vijana kwa ajili ya kufanya ukamataji kabla ya uhalifu haujatokea?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Bado hukuona sababu ya kumuuliza Bwire?

SHAHIDI: Polisi walitakiwa wafanye uchunguzi wao.

KIBATALA: Kwani nani aliyemafuta Adamoo?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Kwani nani alikuwa anaaminiwa na Adamoo kati yako na Polisi?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Kuna taarifa kwamba siku za Adamoo na Ling’wenya wanakamatwa walikuwa wanapokea taarifa kutoka kwa msiri wao. Je huyo msiri ni wewe?

SHAHIDI: Siyo mimi.

KIBATALA: Je, kwa ufahamu wako palikuwa na mtu mwingine aliyekuwa anatoa taarifa kwa DCI na Kingai?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Kwa ufahamu wako wewe kuna mtu mwingine ambaye alikuwa anawajua Adamoo na Ling’wenya?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Unafahamu kwamba Adamoo na Ling’wenya siku wanakamatwa pale Rau Madukani walikuwa wanafanya nini?

SHAHIDI: Wala sijui kama walikamatwa Rau Madukani.

KIBATALA: Unafahamu kwamba pale Rau Madukani Mohammed Ling’wenya alikuwa na dada yake anaitwa Athima?

SHAHIDI: Sifahamu. Hakuwahi kuniambia.

KIBATALA: Wewe hukumuuliza Bwire?

SHAHIDI: Sikumuuliza.

KIBATALA: Ulikuwa unafahamu kwamba Moses Lijenje ana dada yake anaishi Arusha?

SHAHIDI: Hapana. Sijui.

KIBATALA: Na wala msiri wao unasema siyo wewe?

SHAHIDI: Siyo mimi.

KIBATALA: Kuna sehemu katika maelezo yako uliandika “Nilimpatia ACP Kingai namba za Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya aweze Kuwa fuatilia”. Ni sahihi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Suala la kwamba ACP Kingai alikuwa namba za watu watatu mpaka siku wanakamatwa, je, uliliongelea?

SHAHIDI: Sikuongelea.

KIBATALA: Suala la kuwapa namba za simu ni suala la muhimu au siyo la muhimu?

SHAHIDI: Ni suala la muhimu.

KIBATALA: Unafahamu kwanini Kingai wala mtu mwingine yeyote hakuna anayezungumzia suala la wewe kuwapa namba za simu kabla?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba suala la Kingai kuwa na namba za simu za watu hawa zina implication gani katika uchunguzi?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba mashahidi ambao wamekutangulia, walikuwa wanamtafuta Lijenje manually wakati wana namba zao za simu?

SHAHIDI: Hapana. Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba hata baada ya watu hawa kukamatwa Kingai hakufanya chochote katika kuwafahamisha wapendwa wao?

SHAHIDI: Hapana. Sifahamu.

KIBATALA: Wakati wa tarehe 12 Agosti 2020 ulisema ulimkabidhi Inspector Swila na kuandikishwa ID 02?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Mwanzo ukasema kwamba wakati unamkabidhi simu yako ulitoa line ya VodaCom ambayo ilikuwa na mawasiliano yako na watu wengine?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Kwa hiyo wewe ulimkabidhi Inspector Swila simu bila sim card?

SHAHIDI: Nilitoa ya VodaCom nikabakisha moja.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba sim card ya VodaCom ulirudisha lini?

SHAHIDI: Nilisema kwamba nilirudisha tarehe 12 Agosti 2020.

KIBATALA: Ni katika nyaraka ipi tukiangalia tutaona mlikabidhiana Sim Card ya VodaCom na Inspector Swila?

SHAHIDI: Ipo.

KIBATALA: Ipo hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Hapana. Hapa Mahakamani haipo.

KIBATALA: Ipo wapi?

SHAHIDI: Sikujua kama inahitajika mahakamani.

KIBATALA: Ile simu ya Techno uliyowasha hapa (mahakamani) ina sim card ndani?

SHAHIDI: Sikukagua kama ina sim card ndani.

KIBATALA: Aliyesema kwamba ile simu ina sim card ndani ni nani?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Nikuombee (kwa jaji) utuonyeshe sim card?

SHAHIDI: Vyovyote vile itakayokuwa.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P 34.

KIBATALA: Haya! Fungua utuonyeshe humo ndani kuna sim card ya mtandao gani.

(Shahidi anafungua simu yake kuangalia sim card).

SHAHIDI: Hakuna LINE hata moja.

KIBATALA: Unafahamu thamani ya kiapo chako?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba una wajibu wa kulinda hadhi ya Jeshi la Wananchi Tanzania?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba ukweli na uongo wako unapimwa katika vitu vidogo vidogo kama hivyo?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Nakuuliza tena. Wakati unamkabidhi Inspector Swila simu ilikuwa na sim card au haina sim card?

SHAHIDI: Ilikuwa na sim card.

KIBATALA: Unafahamu kwamba Sim Card imepelekwa wapi?

SHAHIDI: Ilikuwa na line ya Airtel iliyobakia. Sifahamu ipo wapi.

KIBATALA: Ile sim card ya VodaCom na zile simu zingine tatu, katika maelezo yako ya tarehe 12 Agosti 2020 ulizungumzia katika maelezo yako?

SHAHIDI: Sikuandika katika maelezo yangu.

KIBATALA: Sisi tunathibitisha wapi kwamba ulikabidhi hizo simu tatu wakati hazipo katika maelezo yako wala hakuna hati ya makabidhiano?

SHAHIDI: Lakini zipo hapa Mahakamani.

KIBATALA: Ungekuwa Polisi nimgekuuliza unafahamu _Chain of Custody_wewe? Ila wewe afisa wa Jeshi nitakuonea. Unafahamu Kwamba hizo simu tatu zina uhusiano na kesi hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Je, ulimwambia Jaji kwamba zile simu zingine mbili kule Morogoro ulimwachia nani na zilikuwa chini ya uangalizi wa nani?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Wala hukumwambia Jaji kama huko ulipoziacha zina password au hazina.

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Je, unafahamu kwanini yule aliyekuambia ulete simu tatu kesho yake hajazungumzia chochote kuhusu hizo simu tatu?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unafahamu au hufahamu kwamba Freeman Mbowe alikuwa na kaka wa damu, Jeenerali ambaye katika kifo cha huyo Jenerali Rais Magufuli alikwenda kwa Mbowe kumpa pole?

SHAHIDI: Nilisikia.

KIBATALA: Na unataka tukubali sisi watu wazima kuwa aliacha ndugu yake wa damu aliyenyonya naye ziwa moja akutafute wewe?

SHAHIDI: Yule si alishastaafu?

KIBATALA: Alistaafu lini?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Kati ya wewe luteni uliye kazini na Jenerali ambaye amestaafu nani anawafahamu watu wengi Jeshini waliopo na waliotangulia?

SHAHIDI: Ni Jenerali.

KIBATALA: Unasema siku ya kwanza Mbowe alikutafuta siku ya kwanza ukashangaa?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Je, unafahamu kwamba kitendo cha mtu wa kukupigia simu bila ridhaa yako unaweza kutolea taarifa?

SHAHIDI: Rudia swali.

KIBATALA: Je, unafahamu kwamba kitendo cha mtu wa kukupigia simu mtu muhimu kama wewe bila ridhaa yako unaweza kutolea taarifa?

SHAHIDI: Kwanza mimi siyo mtu muhimu.

KIBATALA: Wacha Jaji aandike kuwa wewe siyo mtu muhimu.

KIBATALA: Je, unafahamu kwamba kitendo cha mtu wa kukupigia simu bila ridhaa yako unaweza kutolea taarifa?

SHAHIDI: Siyo utamaduni wetu.

KIBATALA: Je, ulitoa taarifa Jeshini kwamba kiongozi wa chama cha upinzani Chadema kakutafuta?

SHAHIDI: Sikutoa.

KIBATALA: Kwenye maelezo yako ulisema kuwa mliendelea kuwasiliana naye kwa sababu wewe na yeye wote ni kabila moja.

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Kwa hiyo hili la ukabila ndiyo lilikufanya uendelee kuwasiliana na Mbowe?

SHAHIDI: Hapana. Ni mawasiliano.

KIBATALA: Si ndiyo mawasiliano na Mwenyekiti wa Chadema wakati wewe umesema hamfumgamani na chama chochote.

SHAHIDI: Mbowe ni Mbowe na Chadema ni Chadema.

KIBATALA: Kwanini katika maelezo yako unasema “Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema”?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Hapo ulimtenganisha Mbowe na Chadema?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Shahidi, ushahidi wako unasema kwamba 500,000/- ulitoa 300,000/- ikabakia 200,000/-. Ukawapa Adamoo Ling’wenya 199,000/-?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Katika maelezo yako uliandika kwamba Mheshimiwa Mbowe alikukumbushia kuhusu vijana, ukamwambia kuwa wamepatikana vijana wawili. Kwa hiyo wewe kwa maelezo yako ulisema tarehe 20 Julai 2020 alinitumia 500,000/- nikatoa 300,000/- ikabaki 200,000/- kwenye simu?

KIBATALA: Ni sahihi kwamba katika maelezo hakuna mahala ulisema ulibakisha 200,000/- kwenye simu?

SHAHIDI: Hakuna nilipoandika.

KIBATALA: Alikuambia Inspector Swila maana ya haya maelezo?

SHAHIDI: Hakuniambia.

KIBATALA: Baada ya siku chache wakapatikana vijana wawili nikawapatia 195,000/-?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Maelezo yako na unachosema kwenye kizimba vinafanana au vinatofautiana?

SHAHIDI: Vinatofautiana.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba P1 na P13.

KIBATALA: Nimeshika hapa maelezo ya onyo ya Adam Kasekwa ambayo wenzetu wanasema alikiri. Sasa wewe katika ushahidi wako unasema kwamba uliwapa 195,000/- katika 199,000/- uliyotumiwa. Je, ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba 4,000/- ilienda wapi?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Kwa hiyo 4,000/- ya ugaidi hujasema iko wapi?

SHAHIDI: Siyo ya UGAIDI, bali ni ya kuwasafirisha.

KIBATALA: Kwa hiyo wenzetu wanasema yote 199,000/- ilitumika kwenye UGAIDI. Kumbe siyo ugaidi? Maelezo haya yanasema kuwa alipokea 87,000/- kila mmoja. Je, ni kweli au si kweli?

SHAHIDI: Sikumpatia mtu mmoja mmoja. Niliwapa kwa pamoja.

KIBATALA: Kama Adam Kasekwa kasema walipewa 87,000/- atakuwa kasema uongo?

SHAHIDI: Atakuwa kasema uongo.

KIBATALA: Unakubaliana kuwa 87,000 x 2 = 174,000? Unakubali unakataa?

SHAHIDI: Amount hiyo mimi sijui.

KIBATALA: Nakuuliza kimahesabu 87,000×2=174,000.

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Adam Kasekwa anasema kwamba jumla Uliwapa 174,000/-. Wewe unasema 195,000/-.Je. inatofautiana?

SHAHIDI: Inatofautiana.

KIBATALA: Na Adam Kasekwa anasema kwamba fedha hiyo uliyotumiwa na Mbowe ilikuwa ni kuwarejeshea (refund). Ni sahihi au si sahihi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji naomba na sisi tuwe tunaangalia kama maelezo yapo sahihi.

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Mheshimiwa Jaji pia awe anasoma kile ambacho kimeandikwa. Kwa mfano hakuna sehemu imeandikwa 174,000/- lakini kuna 87,000/-.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, sasa kwa majibu kuhusu majibu ya kielelezo P1 yaondoke.

KIBATALA: Ni sawa. Tufute mstari mmoja halafu tuanze upya.

KIBATALA: Sasa nilikuwa nakuuliza awali shahidi kuhusu maelezo yako yanasema hivi, “Baada ya siku mbili waliopatikana vijana wawili Adamoo na Ling’wenya ambao niliwapatia 195,000/-, tulipokutana eneo la Msavu…”

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Kwa hiyo ni sahihi kwamba hiyo 195,000/-, kwamba uliwapatia kama gharama ya nauli zao kutoka walipotoka kuja Morogoro?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Walipokuja Morogoro kutoka walikotoka uliwapa 195,000/- kwa ujumla au la?

SHAHIDI: Niliwapa kwa ujumla.

KIBATALA: Adam Kasekwa anasema walikuja na Ling’wenya. Anasema “kwa kutumia simu ya mke wangu, alinipigia kuna kazi ya VIP Protection, maelezo sahihi anayo Luteni Urio.”

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Na kwamba anasema “alitupatia kila mmoja 87,000/-” kwa maelezo ya Ling’wenya.

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Ni sahihi kwamba fedha zote hizo ilikuwa kwa ajili ya refund (kuwafidia)?

SHAHIDI: Ilikuwa kwa ajili ya kuwafidia.

KIBATALA: Safi sana.

KIBATALA: Na unakumbuka kwamba ulisema kwamba uliwapa nauli ya kwenda wapi Adamoo na Ling’wenya kutoka Morogoro?

Shahidi:Niliwapa keshi 195,000/-, ila sikumbuki niliwapa tena shilingi ngapi.

KIBATALA: Ni sahihi kwamba ile 199,000/- iliyotumwa baadae ndiyo uliwapa nauli ili waende kwa Mbowe?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Unafahamu katika maelezo yake Adam Kasekwa, katika ukurasa wa nne mstari ya mwisho, ili mtu kufika Moshi … Wewe unasema walikwenda Dar es Salaam kukutana na Mbowe. Je, statement hii inafanana au inatofautiana?

SHAHIDI: Inatofautiana.

KIBATALA: Nimeshika maelezo ya Mohammed Ling’wenya kielelezo namba P13, anasema kuwa “Baada ya mazungumzo Luteni Urio aliniuliza kuwa mshahara wa Mtwara ni shilingi ngapi, nikajibu ni posho ya 15,000/- kwa siku, basi Luteni Urio akanishauri mshahara uwe kuanzia 800,000/-.” Je, ni sahihi kwamba ulimshauri kuhusu mshahara?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Anaendelea kusema kuwa “alitupatia shilingi 190,000 za nauli ya kwenda Moshi.” Je, ni sawa au zinatofautiana na maelezo yako?

SHAHIDI: Tofauti. Pia tofauti hata na ile ya Adamoo.

KIBATALA: You’re very smart.

KIBATALA: Ling’wenya anazungumzia 190,000/-, wewe unazungumzia 199,000/-. Kuna tofauti ya 9,000/-.

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Unakubaliana na mimi kuwa wapokeaji wa hizi pesa wanasema kuwa matumizi yake yalikuwa siyo UGAIDI bali ni nauli?

SHAHIDI: Sikubaliani na wewe.

KIBATALA: Kwani wewe umesikia wao wanasema kwamba ile fedha ilikuwa kwa ajili ya nini? Adama Kasekwa si kwa ajili ya refund na Mohamed Ling’wenya ilikuwa kwa ajili ya kwenda Moshi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Hapa walikuwa wamekutana na Mbowe?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Walikuwa bado hawajafanya UGAIDI?

SHAHIDI: Walikuwa ndiyo hawajafanya UGAIDI.

KIBATALA: Unafahamu kwamba wenzio wanasema hizo 199,000?- Mbowe zilifadhili UGAIDI?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Kumbe wenzako wamekuficha?

KIBATALA: Ling’wenya nasema pia alipewa pesa akanunue mavazi. Ni kweli?

SHAHIDI: Si kweli.

KIBATALA: Kwamba wewe unasema Ling’wenya alipewa pesa ya kwenda Dar es Salaam, yeye anasema kwenda Moshi. Mmetofautiana?

SHAHIDI: Ni sahihi tumetofautiana.

KIBATALA: Eneo lingine mlilotofautiana Ling’wenya anasema alipewa pesa ya kurejeshwe nauli wewe unasema nauli ya kwenda Dar es Salaam.

SHAHIDI: Sahihi.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba nipewe kielelezo Namba P26.

SHAHIDI: Tayari.

KIBATALA: Ni kweli kwamba Mbowe alikuambia umtafutie ex commandos bila kikomo?

SHAHIDI: Hakuniambia idadi. Yeye alisema wao waje tu.

KIBATALA: Kwenye kielelezo P26, ni sahihi kwamba kwa mujibu wa tarehe 20 Julai 2020 saa 1:39 yeye Mbowe anasemaje?

SHAHIDI: Kaka, wale mtu tatu au nne ni muhimu sana.

SHAHIDI: Lakini kabla ya hiyo meseji kuna mawasiliano ya simu.

KIBATALA: Yako wapi?

SHAHIDI: Hayapo hapo.

KIBATALA: Wewe soma kama ilivyo. Kwa mujibu wa meseji hiyo Mbowe anauliza watu wangapi?

SHAHIDI: Kaka wale mtu tatu au nne ni muhimu.

KIBATALA: Kwa hiyo namba hapo ni 3 au 4?

SHAHIDI: Ndiyo waliopatikana.

KIBATALA: Nenda kwenye meseji ya tarehe 20 Julai 2020 saa 2:03:30. Nani katuma hiyo meseji?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Unaifahamu hiyo namba hapo?

SHAHIDI: Naona meseji kwenda kwa Mbowe tu.

KIBATALA: Kwani meseji hiyo uliyotuma kwenda kwa Mbowe, Je ni namba ipi ya simu?

SHAHIDI: Nilitumia mtandao wa Telegram.

KIBATALA: Mtandao wa Telegram ambao unapotumia unahitaji mtandao?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Namba uliyotumia mtandao huo wa Telegram ni namba ipi?

(Shahidi anacheka).

KIBATALA: Shahidi usicheke. Ndiyo maana nilikuambia The truth shall set you free. Mwambie Mheshimiwa Jaji namba yako ipo au haipo?

SHAHIDI: Haipo.

KIBATALA: Soma katika extraction report hapo wanasema namba gani hiyo?

SHAHIDI: 1130138344 Dennis Owner.

KIBATALA: Namba hiyo unaifahamu au huifahamu?

SHAHIDI: Siifahamu.

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Mheshimiwa Jaji, shahidi apewe nafasi ya kutoa ufafanuzi.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, wakili (wa Serikali) anataka kufanya submission muda huu. Asubiri kwenye re examination. Swali langu ni je, shahidi anaifahamu namba au haifahamu?

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Mheshimiwa Jaji, kama anataka kuuliza namba, ni vizuri shahidi akafafanua.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, mimi naona kuna tatizo na line.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji wametoa objections (nami) nime- rebuttle. Wao wafanye rejoinder siyo Mr. Kidando atoe hoja mpya.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, kwenye rekodi za Mahakama aliyetoa kielelezo hicho ni Inspector Ndowo. Hatuoni haki kwa shahidi kuulizwa kielelezo hicho. Si sawa kuzuiwa kutoa maelezo.

JAJI: Kama nimesikia vizuri Mr. Kibatala alikuwa anauliza kuwa shahidi anaifahamu au haifahamu hiyo namba? Mimi sijasikia akijibu hilo swali. Alipotaka kufanya kufafanua ndipo Mr Kibatala akakataa akasema hayo atamueleza wakili wake. Ni sahihi kwa shahidi kujibu maswali anayoulizwa na wakili tu.

KIBATALA: Shahidi, hiyo namba unaifahamu au huifahamu?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Wakati wa ushahidi wako kuna wakili yoyote alikuambia fafanua?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Unafahamu juu ya application inaitwa Free SMS.

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Ni application ambayo unatuma meseji halafu pia unatuma kwa namba yako na kuweka ya mtu unayemtumia.

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Kuna wakili yeyote aliyekuuliza kuhusu Free SMS?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Na hakuna wakili yeyote amekuongoza kuitambua hiyo Free SMS ili kuondoa hiyo dhana?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Soma hapo. Kuna maelezo unasema simu siyo salama sana. Niwezeshe ili tuweze kukutana.

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Kuna sehemu yoyote katika kielelezo namba P34 ambayo Freeman Mbowe amekueleza wewe kwamba mtumie njia ya mawasiliano mbadala kwa sababu simu si salama?

SHAHIDI: Meseji ya mwisho.

KIBATALA: Haya tusomee.

SHAHIDI: Hellow bro! Nilishindwa kupokea simu yako sababu – – – – – (desh).

KIBATALA: Kwa hiyo kwa tafsiri yako ndiyo kasema kuwa simu siyo salama?

SHAHIDI: Ndiyo nilivyotafsiri.

KIBATALA: Katika hiyo meseji ya mwisho kuna neno simu siyo salama?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Taja namba ya Mbowe katika hiyo meseji ya mwisho.

SHAHIDI: 0713-933 386.

KIBATALA: Soma sasa katika kielelezo kama hizo meseji zinafanana au tofauti.

SHAHIDI: Zinafanana.

KIBATALA: Sasa soma namba ambayo ipo katika kielelezo namba P26 meseji hiyo hiyo.

SHAHIDI: Inatoka katika namba 729414989.

KIBATALA: Ambayo ni namba ya nani?

SHAHIDI: FREE.

KIBATALA: Je, namba uliyosoma mwanzo na sasa hivi zinafanana?

SHAHIDI: Hapana hazifanani.

KIBATALA: Kuna tofauti eeehh!!!!?

SHAHIDI: Ndiyo. Kuna tofauti.

KIBATALA: Kubwa au ndogo?

SHAHIDI: Kubwa.

KIBATALA: Uliongozwa kufafanua hiyo tofauti?

SHAHIDI: Sikuongozwa.

KIBATALA: Tafuta meseji ya tarehe 20 Julai 2020, saa 2:15 na sekunde 54.

SHAHIDI: Naomba nitumie nauli ya ku- mobilise nikutane nao Morogoro.

KIBATALA: Nani alikuwa anaomba nauli?

SHAHIDI: Mimi ndiye niliyekuwa naomba nauli.

KIBATALA: Kwa hiyo [Luteni] Dennis Urio ndiye aliyeomba nauli kwa ajili ya kuwa- mobilise?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Baada ya wewe kuomba nauli ndiyo Mbowe sasa akatuma 500,000/-?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Nitafutie meseji yoyote ambayo Mbowe anatoa wazo yeye la kutuma 500,000/-.

(Shahidi anachukua zaidi ya dakika kutafuta).

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Ni nani kwa mujibu wa kielelezo namba P34 (Simu) aliye- propose kuwa pesa ya ku- mobilise iwe 500,000/-?

SHAHIDI: Ni mimi Denis Urio.

KIBATALA: Kwa mujibu wa meseji ya tarehe ngapi na mwezi wa ngapi ambayo wewe ndiyo mtoa wazo?

SHAHIDI: Meseji ya tarehe 20 Julai 2020 saa 2:19 na sekunde 53.

KIBATALA: Ambayo meseji hiyo wewe ulituma kutoka kwenye namba gani ya kwako?

SHAHIDI: Haionekani namba.

KIBATALA: Ongeza sauti.

SHAHIDI: Haionekani namba.

KIBATALA: Tafuta meseji ya tarehe 20 Julai 2020 saa 2:24 na sekunde mbili.

SHAHIDI: Usiwe unatumia namba yako kutuma pesa. Tumia wasaidizi wako au wakala kutuma.

KIBATALA: Ni nani aliyetuma meseji hii?

SHAHIDI: Mimi Dennis Urio.

KIBATALA: Nikumbushe kule kwa DCI na Kingai uliambiwa jambo gani vile?

SHAHIDI: Kuwapeleka watu.

KIBATALA: Ni sahihi katika maelezo yako uliyoandika, uliambiwa uendelee na kazi ya kumtufutia vijana na kukusanya ushahidi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Hao wasaidizi wa Mbowe washawahi kukutumia pesa?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Katika mawasiliano yako na Mbowe uliwahi kutajiwa au kupitia fedha au kufanya muamala na mtu anaitwa Willy kijana wa Mbowe? Na Willy alikutumia shilingi ngapi?

SHAHIDI: 199,000/-.

KIBATALA: Ndiyo fedha ambazo uliwapa Adamoo na Ling’wenya?

SHAHIDI: Ndiyo hiyo.

KIBATALA: Swali la mwisho kabla ya lunch.

KIBATALA: Hiyo namba ya Willy ambayo ilituma hiyo fedha 199,000/- uliwapa akina DCI na Kingai?

SHAHIDI: Haikuja namba. Alinitumia namba baadaye.

KIBATALA: Hiyo namba hata kama ulipewa baadaye, ulimpa DCI au Kingai?

SHAHIDI: Sikumpa.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba kama wenzangu wataridhia tupate Health Break. Baadaye tuendelee na cross examination. Naomba pia nirudishe vielelezo.

JAJI: Naahirisha kwa dakika 45 mpaka saa 7:45 ambapo shahidi ataendelea kutoa ushahidi.

Jaji anaondoka kwenye chumba cha Mahakamani.

Saa 8:01 Jaji amesharejea mahakamani.

Inasomwa kesi namba 16 ya mwaka 2021 ambayo ni Jamuhuri dhidi ya washtakiwa wanne ambao ni Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Kama ikupendeze Mheshimiwa Jaji quorum ya upande wa Jamhuri ipo kama ilivyokuwa mwanzoni. Sasa tupo tayari kuendelea.

Wakili Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji na sisi kwa upande wetu quorum yetu ipo kama iliuvyokuwa awali. Tupo tayari kuendelea Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Shahidi nakukumbusha tena kuhusu kiapo chako. Utaendelea kutoa ushahidi chini ya kiapo.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba kwa hisani tukumbushwe jibu la mwisho.

JAJI: Kama alimpa DCI na Kingai namba ya Willy.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba kumpa shahidi kielelezo namba P34.

(Shahidi anapewa kielelezo ambacho ni simu).

SHAHIDI: Tayari.

KIBATALA: Shahidi ni sahihi kwamba meseji ya tarehe 22 Julai 2020 saa 3:19 sekunde 30 inasema “namba ya dereva wangu anaitwa Willy. Wamtafute yeye?”

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Ni sahihi kwamba kielelezo namba P26 saa 9:30 sekunde 45 ulipokea hiyo namba?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Na wewe saa 9:36 na sekunde 39 ukasema “Nimepata namba. Nitawapa”?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Hao unaosema utawapa ndiyo akina Khalfani?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Nionyeshe meseji ambayo inaonyesha kwamba Mbowe alituma namba peke yake kama meseji.

SHAHIDI: Alituma lakini hapa haipo.

KIBATALA: Ipo wapi?

SHAHIDI: Sikumbuki ipo wapi.

KIBATALA: Kama nakumbuka vizuri wewe hujawahi kukutana na Willy.

SHAHIDI: Sijawahi kukutana naye.

KIBATALA: Tu- assume kama mambo yalivyotokea, je, Freeman Mbowe alikuomba umtafutie walinzi au magaidi?

SHAHIDI: Kwa hao nilikuwa namtafuta watu wa kwenda kufanya kazi ya ulinzi.

KIBATALA: Yeye Mbowe alitaja walinzi au hakutaja?

SHAHIDI: Alitaja walinzi.

KIBATALA: Ndiyo maana wewe uliwatafuta watu wa kwenda kufanya ulinzi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Mbowe alikuambia ukionana nao uwaambie hivi na vile?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Aliyewaambia kuwa mnaenda kufanya kazi ya ulinzi ni wewe?

SHAHIDI: Ndiyo ni mimi.

KIBATALA: Akina Inspector Swila walikuambia kuwa actually unatakiwa uwe mshitakiwa namba moja au namba mbili?

SHAHIDI: Hawajawahi kuniambia.

KIBATALA: DCI au Kingai walikuambia kuwa watakupatia kinga dhidi ya mashitaka?

SHAHIDI: Hawajawahi kuniambia.

KIBATALA: Tarehe 22 Julai 2020 saa 6:27 na sekunde 23 soma.

SHAHIDI: Kama ikikupendeza uwe unanitumia pesa ya kutosha kwa ajili ya kuwa- mobilise kwa ajili ya kuwafanyia vetting.

KIBATALA: Nani katuma hiyo meseji?

SHAHIDI: Ni mimi Dennis Urio.

KIBATALA: Wakati unatuma meseji hii, Khalfani Bwire na Moses Lijenje walikuwa wameshakwenda kwa Mbowe?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Katika kukamilisha zoezi la kutafuta vijana hao ambao hakutaja kikomo (Kibatala anasoma maelezo ya Luteni Urio), “Freeman Mbowe alinitumia 500,000/-, ambapo nilizitoa,” Je, kwa maelezo haya si ni kwamba ulitoa 500,000/- kwa mkupuo wa pamoja?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Maelezo yako ya ushahidi wako na maelezo yako ya statement vinapishana au vinaendana?

SHAHIDI: Vinaona ila tofauti kwenye tafsiri tu.

KIBATALA: Nakurudisha kwenye meseji. Ni sahihi kwa meseji hii ulikuwa unaomba pesa za ziada (kutoka) kwa Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Ni sahihi ili kufanya mambo kwa urahisi.

KIBATALA: Ulikuwa unaomba pesa za ziada kwa mtu ambaye bila shaka ambaye unafahamu kwamba ana mipango ya UGAIDI?

SHAHIDI: Ndiyo. Nafahamu. Kwa kuwawezesha watu aliokuwa anawahitaji.

KIBATALA: Si ndiyo watu ambao alikuwa anataka kuwatoa kwa ugaidi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Unafahamu kuhusu neno solicit?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Kwa clarity wakati unatuma meseji kwamba awe anatuma pesa za kutosha so ulikuwa umeshapokea 500,000/-?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kwa hiyo awe anatuma pesa zaidi ya 500,000/- sasa?

SHAHIDI: Ni sahihi kwa kadiri itakavyompendeza.

KIBATALA: Ulisema kwamba kila ulichopata ulikuwa unamfahamisha Kingai?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Katika simu hiyo kuna meseji za kumtaarifu Kingai kuhusu kutumiwaa 500,000/-?

SHAHIDI: Hakuna. Nilikuwa naongea naye kwa simu.

KIBATALA: Je, kuna meseji ya muamala wa 500,000/- ulimtumia Kingai kwenye njia ya meseji kumwonyesha Kingai kama ushahidi?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Tarehe hiyo hapo ulimsalimia mtuhumiwa wa ugaidi “Shikamoo Mkuu.” Ni sahihi?

SHAHIDI: Sikuwa na ugomvi naye.

KIBATALA: Mtu akiwa adui wa nchi yako si ni adui yako?

SHAHIDI: Sikuwa na ugomvi naye.

KIBATALA: Unasema tarehe 4 Agosti 2020 Khalfani Bwire alikupigia kuwa Adamoo na Ling’wenya wapo Moshi kumdhuru Sabaya?

SHAHIDI: Tuweke vizuri. Mimi ndiye niliyempigia kisha akanipigia.

KIBATALA: Kwa maelezo yako Khalfani Bwire alikuwa Dar es Salaam au Moshi?

SHAHIDI: Alisema kwamba wale madogo wapo Moshi. Sikujua yeye yupo wapi.

KIBATALA: Kwa maelezo yako wewe kama Luteni wa Jeshi, maelezo yako ya wale madogo wapo Moshi uliitafsiri kuwa Bwire hayupo Moshi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Katika maelezo yako kuna maelezo wale madogo wapo Moshi?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Na maelezo “mnamo tarehe 4 Agosti 2020 Khalfani Bwire alinijulisha wapo Moshi kumdhuru Sabaya, kwani tarehe 12 Agosti 2020 wanatakiwa kurudi Dar es Salaam,” Je Bwire bado yupo Dar es Salaam?

SHAHIDI: Kwa mtazamo wangu mimi.

KIBATALA: Katika statement hii kuna mahala popote umeandika kwamba Bwire yupo Dar es Salaam?

SHAHIDI: Sikuandika.

KIBATALA: Kwanini hukuandika kwamba Bwire alikuwa yupo Dar es Salaam?

SHAHIDI: Hakunitajia location.

KIBATALA: Katika Maelezo yako mstari wa kwanza, unasema “Nakumbuka mwaka 2008 nilikutana na Freeman Mbowe, kwa kuwa wote ni kabila moja, mimi na Freeman Mbowe tumekutana tena CASA Motel kwa maongezi.” Je, neno kukutana naye tena, ni mara ya kwanza?

SHAHIDI: Miye ndiyo nilikutana naye kwa mara ya kwanza.

KIBATALA: Lakini haya maelezo yako uliyosoma na kuyathibitisha? Ni sahihi kwamba kabla ya kukutana naye ana kwa ana alikuwa anakutakia Heri za Sikukuu na event mbalimbali? Ni sahihi kwamba moja ya njia ambayo Freeman Mbowe mlikuwa mnawasiliana alikutumia pongezi za maonyesho ya Sherehe ya Muungano?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Mtu ambaye anatuma ujumbe wa pongezi kwa niaba ya JWTZ, kutokana na maonyesho ya Muungano ni mzalendo au jahili?

SHAHIDI: Kwa kipindi Kile nilimwona mzalendo.

KIBATALA: Katika ushahidi wako uliotoa katika kizimba ulisema kwamba Freeman Mbowe ndiye alikutafuta mara iliyopelekea kukutana katika mambo ya ugaidi.

SHAHIDI: Yeye ndiye alinitafuta.

KIBATALA: Alikutafuta kwa njia ipi?

SHAHIDI: Kupitia Kwa namba za watu wengine.

KIBATALA: Namba ambazo alikuwa anazitumia uliwapa DCI na Kingai?

SHAHIDI: Sikuwapa.

KIBATALA: Ulizitolea maelezo ambazo huzijui?

SHAHIDI: Sikutoa kwa sababu nilikuwa sizijui.

KIBATALA: Mpaka unaenda kuonana na Mbowe akakuambia issues za ugaidi, nani alimtafuta mwenzie?

SHAHIDI: Mimi Ndiye nilimtafuta. Akakuta missed call akanirudia jioni.

KIBATALA: Kwa hiyo ambaye ali- prompt kuonana, siyo wewe ni simu ya Mbowe? Nani aliyeandika kwamba mwezi Julai tarehe za katikati nilimtafuta ili tuweze kuonana. Nani kasaini haya maelezo?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Rudia tena kusoma. Kuna eneo lolote ambalo palikuwa na missed call na baadaye uka- return call?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Je, kuna tofauti kati ya maelezo na unachosema kizimbani?

SHAHIDI: Ndiyo. Tofauti zipo.

KIBATALA: Katika maelezo yako, kuna maelezo yoyote kwamba ulipompigia DCI ulimpigia simu, kuna maelezo kwamba ulijitambulisha kwake in fully?

SHAHIDI: Nilijitambulisha.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, kama wenzangu hawatakuwa na pingamizi, naomba wanipe nimwonyesha shahidi maelezo yake. Kama ni foundation nimefanya hivyo kwa zaidi ya masaa mawili.

KIBATALA: Shika hayo maelezo kwa dakika mbili au tatu uonyeshe kwamba ulipompigia simu DCI ulimpigia na kujitambulisha kuwa wewe ni Afisa wa Jeshi na maelezo yako yote.

JAJI: Kanuni zinasemaje kabla hajatafuta?

KIBATALA: Sawa Mheshimiwa Jaji Asante. Shahidi si unaifahamu hiyo statement?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Sasa shika hayo maelezo kwa dakika mbili au tatu kwamba ulipompigia simu DCI ulimpigia na kujitambulisha kuwa wewe ni Afisa wa Jeshi na maelezo yako yote.

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Ushahidi wako na hayo maelezo katika hilo eneo kunatofautiana au hapatofautiani?

SHAHIDI: Kwenye hilo eneo ni tofauti.

KIBATALA: Kwenye maelezo yako ukisoma hapo, kuhusu pongezi ya JWTZ?

SHAHIDI: Ni meseji ya pongezi.

KIBATALA: Kwa maelezo hayo yanatofautiana au hayatofautiani?

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, kanuni inasema kwamba isomwe kwanza.

KIBATALA: Baada ya maelekezo ya Mahakama tafadhali soma hiyo statement yote kwa sauti.

(Sasa shahidi anasoma statement)

KIBATALA: Unakumbuka nilikuuliza kwamba unaishi wapi ukasema Ngerengere?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa Ngerengere na Kihonda kuna umbali kiasi gani.

SHAHIDI: Ni mbali sana.

KIBATALA: Rejea katika maelezo yako hapo juu. Address yako unaishi wapi?

SHAHIDI: Kihonda.

KIBATALA: Je, ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuhusu tofauti hiyo?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Nani alikuwa ana- propose kuwa msitumie simu kwa sababu simu siyo salama?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Katika statement yako unasema kwamba Mbowe alikuambia kuwa Telegram ndiyo salama?

SHAHIDI: Ndiyo,

KIBATALA: Kwenye meseji kuna sehemu tumeona Mbowe kasema hivyo?

(Shahidi, kimya).

KIBATALA: Shahidi haya si maelezo yako?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Una tatizo tukimpa haya maelezo Jaji ayatumie katika kutenda haki?

SHAHIDI: Hakuna tatizo.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, shahidi kama alivyoomba, tunaomba iingie kama kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi.

JAJI: Ni kielelezo namba ngapi?

KIBATALA: Kama kielelezo namba D4.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, tunaomba tujikumbushe ni kielelezo namba ngapi.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, ni sahihi kuwa ni D4.

JAJI: Nayapokea maelezo haya kama kielelezo namba D4.

(Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia.)

KIBATALA: Shahidi nilikuuliza kuhusu ile meseji ya saa 12:27 na sekunde 23 mchana kwa ajili ya kuwa- mobilise na kuwafanyia vetting na kuwaleta Dar es Salaam.

SHAHIDI: Nimeona.

KIBATALA: Focus yangu ilikuwa katika kuwafanyia vetting, ni vetting ya nini hasa?

SHAHIDI: Kuwa- brief kwamba mnaenda katika kazi ya ulinzi na mkikuta vitu kinyume mnitaarifu.

KIBATALA: Ndiyo maana ya vetting?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Hiyo meseji kaandika nani hapo?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Kwani Mbowe alikuwa anajua kuwa vetting yako ilikuwa inafanyika vipi?

SHAHIDI: Vetting kama kufanyia orientation.

KIBATALA: Vetting siyo kumuangalia background na kumuangalia sifa zake kama za kweli au za uongo?

SHAHIDI: Sikuwa na tafsiri hiyo mimi.

KIBATALA: Kwa hiyo kuna kitu gani ukitaka kufanya mpaka ukatala pesa zaidi?

SHAHIDI: Ni hiyo. Kuwa- orient tu.

KIBATALA: Bwire na Lijenje uliwa- orient au hukuwa- orient?

SHAHIDI: Niliwa- orient.

KIBATALA: Sasa Bwire na Lijenje kuna mahala walisema kwamba pesa haiwatoshi mpaka upate pesa za ziada?

SHAHIDI: Pesa ya awali ilishakuwa consumed tayari.

KIBATALA: Pesa ya awali iliyokuwa consumed ni shilingi ngapi?

SHAHIDI: Ni shilingi 500,000.

KIBATALA: Shahidi nataka kujua bado kwanini kwenye meseji kuna nyongeza ya vetting.

SHAHIDI: Ilikuwa kuwafanyia orientation.

KIBATALA: Kwa hiyo ni pesa ya Mbowe ndiyo imefadhili ugaidi halafu pia ukatoa mafunzo kuwa wasifanye ugaidi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Tarehe 22 Julai 2020 saa 8:03 na sekunde 53, soma hiyo meseji.

SHAHIDI: “Lakini wewe usitume kwa namba yako.”

KIBATALA: Nani alituma hiyo meseji?

SHAHIDI: Mimi Denins Urio.

KIBATALA: Kwanini ulimtumia Mbowe taarifa hiyo?

SHAHIDI: Ilikuwa kuongeza trust.

KIBATALA: Lakini wewe una maagizo ya DCI ya kukusanya ushahidi kwa kadri ya uwezo wako.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Tarehe 22 Julai 2020 saa 7:51 na sekunde 4?

SHAHIDI: Nimeona.

KIBATALA: Soma.

(Shahidi anasoma).

SHAHIDI: Pamoja na pesa ya kula tuma shilingi 200,000/-.

KIBATALA: Ilikuwa pesa ya nini?

SHAHIDI: Nauli pamoja na kula.

KIBATALA: Tafuta meseji ya tarehe 22 Julai 2020 saa 5:59 na sekunde 31.

SHAHIDI: Nimeona.

KIBATALA: Soma.

(Shahidi anasoma)

SHAHIDI: Pamoja na mambo mengine kuna suala la mishahara.

KIBATALA: Mishahara uliyokuwa unazungumzia ilikuwa ya kazi gani?

SHAHIDI: Kufanya uhalifu.

KIBATALA: Unafahamu kwamba kutolipa mishahara ni kosa la jinai?

SHAHIDI: Sifahamu sheria.

KIBATALA: Pale kuna sehemu umasema kuwa kuna masuala ya utawala wanauliza na mishahara. Je, utawala unamanisha nini?

SHAHIDI: Utawala ni masuala ya chakula.

KIBATALA: Utawala ni chakula tu?

SHAHIDI: Pamoja na maradhi.

KIBATALA: Watu wanaokwenda katika uhalifu wanatakiwa kuwa na Administration Obligation?

SHAHIDI: Ndiyo. Kwani hawali? Hawavai?

KIBATALA: Sawa shahidi. Twende taratibu.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba P20.

KIBATALA: Kuna mahala ulikuwa unasema kwamba ulikuwa unawasiliana na Khalfani Bwire kupitia namba 0782 237 913. Sasa nakuonyesha kielelezo namba P20.

KIBATALA: Ni kweli shahidi au si kweli kwamba ulituma kiasi cha 190,000/- kutoka 0787 555200 kwenda kwenye namba 0782 237913?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Ulituma shilingi ngapi?

SHAHIDI: Shilingi 200,000.

KIBATALA: Sasa ulisema kwamba Khalfani Bwire ulimpa shilingi 300,000, je, ulitolea maelezo kwa Jaji?

SHAHIDI: Transactions hiyo ya Bwire sikumbuki na sijatolea maelezo.

KIBATALA: Kuna mahala fulani ambapo inasemekana Mbowe, kama sehemu ya kutekeleza mpango huo alitakiwa kupata mabomu kutoka Ngerengere?

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Mheshimiwa Jaji samahani. Sina hakika kama kuna mahala popote ambapo imesemwa hilo.

KIBATALA: Wacha wanisaidie kutafuta. Nitarudi baadaye.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji hilo suala halipo hata akitafuta.

KIBATALA: Kwani shahidi unaweza kulipua bila ya kuwa na material ya kulipua?

SHAHIDI: Huwezi.

KIBATALA: Ni kweli kwamba Mbowe alishawahi kukushirikisha kutafuta material ya kulipua?

SHAHIDI: Hajawahi kunishirikisha.

KIBATALA: Je, katika ushahidi wako uliwahi kusema kwamba Khalfani Bwire, Mohammed Ling’wenya na Adam Kasekwa walikuwa na access ya kupata milipuko kutoka 92 KJ?

SHAHIDI: Sijawahi kusema.

KIBATALA: Je, umewahi kuzungumzia kuhusu bunduki aina ya bastola aina ya Luger A5340 kuwa ni standard bunduki za makomandoo?

SHAHIDI: Sijawahi kusema.

KIBATALA: Ulisema kwamba Mohammed Ling’wenya baada ya kufika kwa Mbowe tarehe 24 hujawahi kuzungumza naye?

SHAHIDI: Hapana. Nilimtafuta bila mafanikio.

KIBATALA: Je, unasema kwamba Mbowe aliacha kuwasiliana na wewe tarehe ngapi?

SHAHIDI: Tarehe 24 Julai 2020.

KIBATALA: Kwa hiyo kwenye kielelezo namba P34 kuna meseji ambazo ulimtumia Mbowe hakukujibu?

SHAHIDI: Zipo.

KIBATALA: Meseji hizo ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji ambazo hazikujibiwa na Mbowe kwa kuongozwa na mawakili wa Serikali?

SHAHIDI: Sikuonyesha.

KIBATALA: Vipi kuhusu calls? Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Kwenye hii meseji Mbowe anasema kuwa “sikuona simu yako kwa sababu deshi deshi, l hope umenielewa.”

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Alisema simu yako au simu zako?

SHAHIDI: Amesema simu yako.

KIBATALA: Kwa kuwa wewe ulikuwpo kwa DCI na Kingai, nimesikia kuwa Kingai aliteuliwa kama mpelelezi.

SHAHIDI: Hajawahi kuniambia kuwa ni mpelelezi. Alisema taarifa utampa Kingai.

KIBATALA: Katika maelezo yako uliwahi kufahamu kwamba Inspector Swila ndiyo mpelelezi wa kesi yako?

SHAHIDI: Hiyo sifahamu.

KIBATALA: Wala hufahamu kwamba baada ya Inspector Swila kufungua faili, DCI alimteua kuwa mpelelezi wa kesi?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unaweza kukumbuka kwamba Mohammed Ling’wenya alikuwa Sudani katika Peace Keeping?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Unasema ulirekodi maelezo yako tarehe 12 Agosti 2020?

KIBATALA: Unasema ulirekodi maelezo yako tarehe 12 Agosti 2020. Wakati unatoa ushahidi Kambi ya Makomando ipo Ngerengere au Kizuka?

SHAHIDI: Ipo Kizuka.

KIBATALA: Wakati wa maelezo yako ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba Kambi ya Komandoo ipo Kizuka?

SHAHIDI: Sikutoa maelezo.

KIBATALA: Ni sahihi kwamba wakati upo Sudani kwenye Peace Keeping kambi yenu ilikuwa inaitwa KAUBECHE?

SHAHIDI: Inaitwa Colabeche.

KIBATALA: Mlipokuwa Sudani, kiongozi wenu alikuwa Kanali Mbwilo?

SHAHIDI: Hapana ni Jenerali Mbwilo.

KIBATALA: Body Guard wa huyu Jenerali Mbwilo yupo hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Hayupo.

KIBATALA: Unamfahamu Luteni Omary ambaye alikuwa Sudani?

SHAHIDI: Namfahamu.

KIBATALA: Je, Luteni Msandawe?

SHAHIDI: By then namfahamu.

KIBATALA: Ijumaa nilikuuliza maswali kuhusu namba za Kingai mlizobadilishana kwa DCI.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ukasemaje?

SHAHIDI: Niliacha hotelini.

KIBATALA: Kwa hiyo baada ya kesi kuhairishwa utakuwa umekuja nayo leo diary yako?

SHAHIDI: Sikuja nayo. Sikuelekezwa na Mahakama.

KIBATALA: Majibu kuhusu pass pale Jeshini ilikuwaje?

SHAHIDI: Pass ya zaidi ya wiki moja napewa karatasi kwenda katika ofisi yoyote ninapokuwapo. Pass chini ya wiki naandika katika daftari pale kambini.

KIBATALA: Wewe uliulizwa ukasema Movement Order ipo wapi?

SHAHIDI: Ipo hotelini.

KIBATALA: Wakati unaitwa Mahakamani ulipewa summons au mabosi zako walikuambia unatakiwa kutoa ushahidi?

SHAHIDI: Nilitoka kwenye operesheni maalumu bsi wangu akaniambia karipoti kwa DCI.

KIBATALA: Bosi wako anaitwa nani?

SHAHIDI: Kenoth.

KIBATALA: Ulipo- surrender simu zako zote toka tarehe 12 Agosti 2020, ulifafanua kwa Jaji kuwa ulikuwa unatumia simu gani?

SHAHIDI: Hapana. Sikufafanua.

KIBATALA: Unaweza kutuambia kwanini wewe kama mtoa taarifa baada ya kuchukua simu zako hawajawahi kukupa simu zako mpaka unakutana nazo tena hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Waliniambia kuwa wanafanyia uchunguzi.

KIBATALA: Wamekwambia kuwa uchunguzi bado haujakamilika?

SHAHIDI: Ndiyo. Mara ya mwisho kama mwaka mmoja umepita nilienda kuulizia.

KIBATALA: Ungetumia utaratibu gani kudai simu zako?

SHAHIDI: Kwa documents walizonipa.

KIBATALA: Ambayo ni moja?

SHAHIDI: Hapa ninayo moja, lakini zingine ninazo nyumbani.

KIBATALA: Ukiangalia suala hili limeanza tangu Juni 2020 mpaka Agosti 2020.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Katika ushahidi wako ni kwamba Mbowe alikuwa anawasiliana na wewe kwenye Telegram kuanzia Agosti ili kuficha baadhi ya taarifa?

SHAHIDI: Ni sahihi.

KIBATALA: Kwa hiyo tukiangalia katika Telegram hatutaona mawasiliano yako wewe na Mbowe kabla ya tarehe 25 Juni?

SHAHIDI: Tulikuwa tunawasiliana kupitia WhatsApp.

KIBATALA: Mlikuwa mnawasiliana kabla ya kipindi cha hili tukio au ni wakati wa jambo hili tu? Tarehe 7 Agosti 2020 ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa nipo kazini Sanga Sanga.

Shahidi Nilkuwa Commander wa QRF (Quick Response Force)

KIBATALA: Zaidi ya kuandikishana kielelezo namba P36, ni ushahidi upi kwamba Inspector Swila aliingiza simu katika kitabu kisha wote wewe na yeye mkasaini kitabu?

SHAHIDI: Mimi sikusaini kitabu.

KIBATALA: Na yeye hukumuona akiandika chochote katika kitabu? Zaidi ya hand over document, je uliwahi kupewa risiti yoyote ya simu zako?

SHAHIDI: Sijawahi kupewa risiti.

KIBATALA: Je, wakati unamkabidhi simu ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba Inspector Swila alikuwa anabandika makaratasi katika simu (exhibit).

SHAHIDI: Sijawahi kuona.

KIBATALA: Katika maelezo ya ushahidi ulisema kwamba haukujisumbua tena kuhusiana na Bwire kwa sababu lengo lilikuwa limeshatimia?

SHAHIDI: Nakumbuka nilisema.

KIBATALA: Lilikuwa lengo lipi?

SHAHIDI: Baada ya wahalifu kukamatwa.

KIBATALA: Lengo lako lilikuwa kuhakikisha wahalifu wanakamatwa? Kwa hiyo lengo lako wewe lilikuwa kuhakikisha wahalifu wanakamatwa?

SHAHIDI: Nazuia uhalifu.

KIBATALA: Je, ilikuwa kazi yako au kazi ya Polisi?

SHAHIDI: Ilikuwa kazi ya Polisi.

KIBATALA: Mallya alikuuliza kwamba uliwanunulia akina Adamoo chakula?

SHAHIDI: Nililipa mimi lakini pesa nilipewa na Mbowe.

KIBATALA: Je, ulizungumzia katika ushahidi wako mkuu kuwa katika pesa niliyowapa Adamoo na Ling’wenya sehemu ya pesa ile walitumia palepale kulipa chakula?

KIBATALA: Kwa kuwa wewe ulikuwa na mawasiliano moja kwa moja na DCI na Kingai, uliwahi Kufahamu kwamba hakuna simu ya Mbowe hata moja iliyokamatwa?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Kwa maana hiyo hufahamu pia kwamba Polisi wameshindwa kuthibitisha mawasiliano yako wewe na Mbowe.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji nauliza swali la mwisho alafu nitatoa hoja

KIBATALA: Unakumbuka ulisema kuwa Bwire alikuambia wapo katika utejelezaji wa mpango?

SHAHIDI: Siyo mpango, alisema “samahani bro tumeshakengeuka, tumeshawishiwa na Freeman Mbowe, na vijana wapo Kilimanjaro katika utekelezaji.

KIBATALA: Wewe ulikuwa na mamlaka yoyote ya kiupelelezi zaidi ya kutoa taarifa?

SHAHIDI: Kila Mtanzania ni mpelelezi. Sina mamlaka nyingine ya kiupelelezi.

KIBATALA: Hoja yangu ulipata wapi power ya kuagiza waendelee na uhalifu?

SHAHIDI: Nilishatoa taarifa.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, bado nina maswali kadhaa. Naomba tuahirishe cross examination, mpaka kesho Februari 1 ili tuweze kuendelea. Ni hayo tu.

(Mahakamani Jaji alitangulia kutoa taarifa ya kuwa ifikapo saa 10 jioni kutakuwa na matengenezo ya jenereta).

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi, lakini tunaomba kesho tukiendelea mwenzetu ajielekeze katika maeneo ambayo bado hajayahoji.

JAJI: (Anamtaza Kibatala) Unasemaje?

KIBATALA: Hakuna neno Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Basi shauri hili limeahirishwa mpaka kesho tarehe 1 Februari 2022. Shahidi namba 12 ataendelea kuwa Mahakamani kuendelea kutoa ushahidi wake. Washitakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka kesho asubuhi saa tatu.

Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama saa 10:29 jioni.

Like
1