Kesi ya Mbowe: Shahidi mtaalamu wa silaha achanganya maelezo

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 29.Oktoba 2021.

Saa 3:50 asubuhi Jaji anaingia mahakamani.

Kesi namba 16 ya mwaka 2021 inasomwa. Ni Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anasimama. Anawatambulisha mawakili wenzake.

  1. Robert Kidando
  2. Nassoro Katuga
  3. Ignas Mwanuka
  4. Esther Martin
  5. Tulumanywa Majige
  6. Jenitreza Kitali
  7. Abdallah Chavula

Wakili Peter Kibatala anasimama na kuwatambulisha wenzake wa upande wa utetezi.

  1. John Malya
  2. Jonathan Mndeme
  3. Nashon Nkungu
  4. Dickson Matata
  5. Allex Massaba
  6. Seleman Matauka
  7. Evaresta Kisanga
  8. Maria Mushi

Jaji anawaita washitakiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa nne. Wanaitika kuonyesha uwepo wao.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo tuna shahidi mmoja. Tupo tayari kuendelea.

JAJI: Upande wa utetezi?

Wakili Peter KIBATALA: Na sisi tupo tayari kuendelea.

(Jaji anaandika)

JAJI: Na anakuwa shahidi namba ngapi?

WAKILI WA SERIKALI: Namba tatu.

JAJI: Apande [kizimbani].

JAJI: Majina?

SHAHIDI: Namba F 5914 D Koplo Hafidh Abdallah Mohamed.

JAJI: Umri?

SHAHIDI: Miaka 38.

JAJI: Kazi.

SHAHIDI: Askari Polisi.

JAJI: Dini?

SHAHIDI: Muislamu.

Mimi namba F5914 Koplo Hafidh, naapa kuwa kwa ushahidi huu nitakaotoa utakuwa wa kweli. Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie.

JAJI: Kiapo kiko sawa? Asaidiwe.

SHAHIDI: Mimi Koplo Hafidh nathibitisha kuwa ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, kweli mtupu, Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie.

WAKILI WA SERIKALI: Nitakuuliza maswali utajibu kwa sauti.

WAKILI WA SERIKALI: Itaje kazi yako.

SHAHIDI: Ni askari Polisi. Nafanya Makao Makuu Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Askari polisi tangu lini?

SHAHIDI: Tangu mwaka 2013.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama tukufu kituo chako cha kazi ni wapi.

SHAHIDI: Forensic Bureau Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Forensic Bureau ni kitu gani?

SHAHIDI: Ni maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

WAKILI WA SERIKALI: Upo kitengo gani?

SHAHIDI: Silaha na milipuko.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kitengo chako kinahusika na nini (ballistic and explosion).

SHAHIDI: Uchunguzi wa silaha na milipuko.

WAKILI WA SERIKALI: Upo tangu lini?

SHAHIDI: Tangu mwaka 2014.

WAKILI WA SERIKALI: Umesema kitengo chako kinahusika kuchunguza silaha. Eleza majukumu yako ya msingi ni yapi.

SHAHIDI: Kuchunguza silaha zinazotumiwa kufanya uhalifu.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Kuchunguza risasi ambazo zinatuhumiwa kufanya uhalifu.

WAKILI WA SERIKALI: Jingine?

SHAHIDI: Kuchunguza maganda ya risasi.

WAKILI WA SERIKALI: Jingine?

SHAHIDI: Kuchunguza kitako cha risasi.

WAKILI WA SERIKALI: Jingine?

SHAHIDI: Kwenda eneo la tulio kwa uchunguzi.

WAKILI WA SERIKALI: Jingine?

SHAHIDI: Kuandaa report baada ya kuchunguza ballistic and explosion report.

WAKILI WA SERIKALI: Jingine?

SHAHIDI: Kutoa ushahidi mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kama una jukumu lingine.

SHAHIDI: Hakuna.

WAKILI WA SERIKALI: Kuna uchunguzi wa silaha wa aina ngapi?

SHAHIDI: Aina mbili.

WAKILI WA SERIKALI: Aina ya kwanza?

SHAHIDI: Physical examination.

WAKILI WA SERIKALI: Mnafanya mambo gani?

SHAHIDI: Kupokea silaha mbalimbali zinazofanya uhalifu. Je, hii silaha inafanya kazi? Hii silaha ni nzima? Hii sasa ni Physical Examination.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa mnafanya nini?

SHAHIDI: Tunafanya Visual Examination.

WAKILI WA SERIKALI: Ni kitu gani hapo?

SHAHIDI: Hii bunduki ni nzima? Ina koki? Ina magazine? Je, magazine ni nzima? Kama inagonga vizuri kama nyundo? Ina nguvu? Nita ikoki katika upande wa mitambo kama inafanya vizuri. Je, fine pin inafanya kazi?

JAJI: Fine pin ni nini?

SHAHIDI: Kiwashio cha risasi.

SHAHIDI: Nitaangalia ndani ya bao (mtutu) internal ballistic.

SHAHIDI: Nitaangalia ni safi? Nitaikoki kama inafanya vizuri. Ni hayo tu.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa uchunguzi wa aina ya pili ni upi?

SHAHIDI: Nimepokea pistol au SMG.

WAKILI WA SERIKALI: Unaitwaje huu uchunguzi wa pili?

SHAHIDI: Comparison Examination.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kinafanyika?

SHAHIDI: Nachukua ganda nililoletewa na mteja kisha napeleka kwenye mitambo maalumu.

WAKILI WA SERIKALI: Unafanya hii comparison kubaini nini?

SHAHIDI: Je, hii risasi ina sifa hii?

WAKILI WA SERIKALI: Mnatumia mitambo maalumu?

SHAHIDI: Unaitwa Computer Microscope and Digital Camera Forensic Machine LAECA 2004.

WAKILI WA SERIKALI: Umeeleza za vyema kuhusu uchunguzi wa silaha. Kwenye risasi unafanya kitu gani?

SHAHIDI: Kitaalamu inaitwa live ammunition. Nitaangalia kiwashio. Je kimegongwa? Kama kimegongwa hiyo siyo nzima. Hiyo tunasema miss-fired. Kwamba ilipigwa na haikulipuka. It was miss-fired.

WAKILI WA SERIKALI: Na hiyo miss-fired ieleze Mahakama. Je, live ammunition ikiwa miss-fired maana yake ni nini?

SHAHIDI: Ni mbovu sababu ulipiga haikulipuka.

WAKILI WA SERIKALI: Fafanua sasa Mahakamani endapo haijagongwa ni vipi?

SHAHIDI: Kama haijagongwa ni nzima.

WAKILI WA SERIKALI: Tofauti na kugomgwa na kutokugongwa mnafanya kitu gani?

SHAHIDI: Tunaangalia gun powder resolutions.

WAKILI WA SERIKALI: Mnaangalia kitu gani?

SHAHIDI: Kwemye risasi kuna powder. Tunaangalia je, powder yako imeganda au nzima?

WAKILI WA SERIKALI: Sasa tunataka kwenye risasi. Mnasema mnachunguza maganda ya risasi?

SHAHIDI: Tunachunguza pin impression (mapigo ya bunduki). Je, yanalingana?

WAKILI WA SERIKALI: Ulisema mnachunguza vichwa vya risasi?

SHAHIDI: Yani bullets cartridge. Tunaangalia michirizo, yaani Internal Ballistics. Hizo alama za kipekee tunasema proved.

WAKILI WA SERIKALI: Mnafanyaje?

SHAHIDI: Tunaangalia kitu kinaitwa Twist. Twist silaha/risasi kuna twist right na twist left. Naangalia counts inasema twist right na left. Nyingine unapopiga kuna counts mbili unapopiga mpaka kumdhuru mtu.

WAKILI WA SERIKALI: Katika uchunguzi inatusaidiaje?

SHAHIDI: Inatusaidia silaha kugundua mbalimbali zinazoweza kufanya uhalifu.

WAKILI WA SERIKALI: Tumalizie kwenye mlipuko unachunguza nini?

SHAHIDI: Inapotokea mlipuko wowote. Sisi tunakwenda kwenye eneo la tukio. Wanaenda askari wa awali. Halafu tunaenda sisi wataalamu kuangalia kama kilichotokea ni Local Explosive au ni Industrial Explosive.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe una utalaamu gani sasa?

SHAHIDI: Mimi ni mtaalamu kwa kufanya kozi mbalimbali.

WAKILI WA SERIKALI: Kozi ya kwanza?

SHAHIDI: Nilienda Ballistic kwa askari wabobezi kupata mafunzo.

WAKILI WA SERIKALI: Ulifanya kwa muda gani?

SHAHIDI: Kwa miaka miwili.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa miaka miwili ulikuwa unajifunza kitu gani?

SHAHIDI: Kuchunguza silaha mbalimbali ambazo zinatumika kwenye uhalifu.

WAKILI WA SERIKALI: Tofauti na kuchunguza nini kingine?

SHAHIDI: Kuchunguza maganda ya risasi mbalimbali?

WAKILI WA SERIKALI: Kingine tofauti ya kuchunguza?

SHAHIDI: Kuandaa riport za kitaalamu.

SHAHIDI: Kuandaa Ballistic and Explosion Report.

WAKILI WA SERIKALI: Kozi gani nyingine umefanya?

SHAHIDI: Kozi ya uchunguzi wa awali ya upelelezi, Basic CID Course.

WAKILI WA SERIKALI: Ulifanya mwaka gani na wapi?

SHAHIDI: Mwaka 2004 kwenye Polisi College Zanzibar.

WAKILI WA SERIKALI: Ulijifunza nini huko Zanzibar?

SHAHIDI: Nilijifunza mambo mbalimbali ya kiupelelezi. Nilijifunza bunduki kupiga, kuchukua alama za vidole, kutafuta finger prints.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Ku- lift finger prints, baada ya kuchunguza finger prints na kuhamisha.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Kufungua na kuirudishia bunduki.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Nimejifunza chunguzi za silaha mbalimbali. Nilipata elimu ya awali juu ya ku- collect ushahidi katika crime scenes.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kama ulipata kozi nyingine.

SHAHIDI: Baada ya kurudi ofisni nilihitajika kwenda kozi nyingine Moshi, mwaka 2006.

WAKILI WA SERIKALI: Ulijifunza kitu gani?

SHAHIDI: Techniques, Protocol in Fire arms Evidence.

WAKILI WA SERIKALI: Fafanua.

SHAHIDI: Kufungua silaha, vifaa vyake na kuirudishia, na kutengeneza kama inawezekana.

WAKILI WA SERIKALI: Na kozi nyingine kama ipo.

SHAHIDI: Nilifanya Polisi College Dar es Salaam ambayo inaitwa Ballistic Tools.

JAJI: Rudia jina la kozi.

SHAHIDI: Fire arms, tools and ballistic materials testing. Mwaka 2007.

WAKILI WA SERIKALI: Kozi nyingine.

SHAHIDI: To determine and examine fire arms.

JAJI: Jina la kozi rudia.

SHAHIDI: To determine and examination of fire arms.

WAKILI WA SERIKALI: Wapi?

SHAHIDI: Botswana Police College mwaka 2010.

WAKILI WA SERIKALI: Nyingine.

SHAHIDI: Mwaka 2015 inaitwa a Forensic in General.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwa mwaka gani?

SHAHIDI: 2015?

WAKILI WA SERIKALI: Ulijifunza nini?

SHAHIDI: _Ballistic Woundage. Vidonda.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Mtu amepigwa bastola amekufa naangalia shooter alikuwa upande gani.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kutokana na mafunzo lini ulianza kuanza kuchunguza rasmi?

SHAHIDI: Mwaka 2010 nilianza rasmi kuchunguza kesi.

WAKILI WA SERIKALI: Ofisini kwako unapofanyia kazi, ifahamishe Mahakama silaha au mlipuko inatokea wapi?

SHAHIDI: Vituo vya Polisi na hata TANAPA kuja kufanya uchunguzi.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama utaratibu wa kupokelewa vitu vya kufanyia kazi ukoje.

SHAHIDI: Kwanza mteja awe na barua.

WAKILI WA SERIKALI: Kwenye barua kuna kuwa na nini?

SHAHIDI: Barua ionyeshe kosa.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Aeleze nini anaomba tumfanyie.

WAKILI WA SERIKALI: Tofauti na barua anakuwa na nini?

SHAHIDI: Aje na hivyo vielelezo husika sasa.

WAKILI WA SERIKALI: Barua pamoja na vielelezo hupokelewa eneo gani na nani anapokea?

SHAHIDI: Anakuwa afisa wa zamu anayetupangia. Leo utakuwa zamu na kupokea vielelezo. Tunakuwa wawili.

WAKILI WA SERIKALI: Mkishapokea kama afisa wa zamu unafanya nini?

SHAHIDI: Tunapokea barua na kielelezo. Nafungua kujiridhisha kama alivyovileta vipo sahihi.

WAKILI WA SERIKALI: Ukishajiridhisha?

SHAHIDI: Lazima niangalie safety (usalama) kabla haijaingia laboratory (maabara).

WAKILI WA SERIKALI: Umeshajiridhisha vielelezo na usalama. Sasa unatakiwa ufanye kitu gani?

SHAHIDI: Natakiwa kuingia laboratory nitai- register.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa kufanya nini?

SHAHIDI: Nitaandika Exibit K1 nitaweka FStroke ya mwaka gani.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kusajili vielelezo hupelekwa wapi?

SHAHIDI: Nitapeleka sehemu ya kuhifadhia silaha.

WAKILI WA SERIKALI: Barua utaipekeleka wapi?

SHAHIDI: Kwa officer in charge.

WAKILI WA SERIKALI: Inapelekwa kwa officer in charge kwa madhumuni gani?

SHAHIDI: Lazima atambue ni silaha gani. Na atampa mtu kuchunguza hii kesi.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama mnamo tarehe 25 November unakumbuka ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa ofisini kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Kwenye dawati la kupokea vielelezo mbalimbali.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipokea vielelezo vipi siku hiyo?

SHAHIDI: Nilipokea vielelezo kutoka Ofisi ya DCI ambavyo ni pistol yenye namba A5340 caliber 9mm ikiwa na magazine yenye rangi nyeusi na nikapokea risasi tatu.

WAKILI WA SERIKALI: Za silaha gani?

SHAHIDI: Za _pistol caliber 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Vielelezo hivyo viliambatana na nini?

SHAHIDI: Kwanza alivileta PC Goodluck kutoka Ofisi ya DCI.

WAKILI WA SERIKALI: Goodluck aliwasilisha nini?

SHAHIDI: Barua.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kupokea vielelezo hivi na barua ieleze Mahakama ulifanya nini.

SHAHIDI: Nilivi- label kama nilivyosema awali. Pistol niliipa alama Exhibit K1 … Ni kosa ili kwa FB /BALL/LAB 158/2020.

WAKILI WA SERIKALI: Na hizi risasi tatu?

SHAHIDI: Nilizipa alama ya K2 K3 na K4.

WAKILI WA SERIKALI: Risasi hizi ulizipa usajili upi?

SHAHIDI: 158 kama pistol.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukamilisha usajili wa vielelezo ulichukua hatua gani?

SHAHIDI: Nikarudi kwenye barua kujiridhisha wanataka nini wafanyiwe.

WAKILI WA SERIKALI: Sawa. Ukibaini wanataka kitu gani?

SHAHIDI: Kufanya uchunguzi wa kuutambua hiyo bunduki na risasi ni nzima K2, K3 na K4.

WAKILI WA SERIKALI: Na kuhusu vielelezo pistol na risasi ukafanya nini?

SHAHIDI: Kwanza ile pistol niliipima.

WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya kupima, tupo kwenye hatua ya upokeaji.

SHAHIDI: Nika- minutes kumpelekea Boss.

WAKILI WA SERIKALI: Vielelezo ukapeleka wapi?

SHAHIDI: Nilipeleka chumba cha kuhifadhia silaha.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama nani aliteuliwa kufanya uchunguzi.

SHAHIDI: Mimi mmojawapo.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwa ni lini ulipolewa jukumu hilo?

SHAHIDI: Ilikuwa tarehe 25 Novemba mwaka 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Katika uchunguzi huo ulifanya lini?

SHAHIDI: Nilianza kufanya tarehe 25 uchunguzi wa awali.

WAKILI WA SERIKALI: Katika uchunguzi wako ulifanya nini kulingana na mahitaji?

SHAHIDI: Hatua ya kwanza.

WAKILI WA SERIKALI: Mteja alikuwa anataka nini?

SHAHIDI: Mteja alikuwa anataka kujua ile pistol na risasi zilifanya kazi?

WAKILI WA SERIKALI: Sasa wewe ulifanya nini?

SHAHIDI: Kwanza Ile bastola nilipima na kifaa kinaitwa Gun Barrow Gauge. Hapo nilikuwa napima kwenye barrow, yaani mtutu, kwamba ile caliber ni kweli 9mm. Nikaona ni kweli ipo sahihi ni 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Nikatoa magazine. Kumbuka ilikuwa na magazine inaitwa Magazine Release. Naangalia magazine yake ile bastola ni ya kwake? Nikaona OK, magazine ni ya kwake.

WAKILI WA SERIKALI: Jingine?

SHAHIDI: Ndani ya magazine kuna spring ambayo ukiweka risasi inashuka chini. Yenyewe inapandisha risasi juu. Nikaona ni nzima. Nikaangalia nyundo, hummer, kama ni nzima. Sometime inakuwa loose. Nikabaini ni nzima.

SHAHIDI: Nikaangalia triger kwa kutumia triger pull kama inafika kwenye 100, nikabaini ni nzima. Nikai- koki ili nijiridhishe kama inaenda vizuri. Nikaona inaenda vizuri kwenye njia zake na inaenda intact. Nikaenda ndani ya barrow nikatumia mdeki kuangalia kama ilikuwa Safi au chafu kupoteza ubora wake. Nikabaini _barrow lipo vizuri halina vumbi, hakuna mchanga maana yake barrow lipo safi. Lolote linaweza kufanya. Baada ya hapo nikaikoki kungalia firing pin mechanism kama ipo. Nilibaini ipo. Kwa hatua hiyo niliishia hapo.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa aina za uchunguzi ulizotutajia huu ni uchunguzi wa aina gani?

SHAHIDI: Ni Visual Examination.

WAKILI WA SERIKALI: Kwenye zile risasi tatu ulichunguza nini?

SHAHIDI: Pale niliingia sana kwenye pin impresion kwa maana primer au Kiswahili chake ni kiwashio au kitako cha risasi.

WAKILI WA SERIKALI: Ulibaini nini?

SHAHIDI: Nilikuwa naangalia risasi nilizoletewa ni nzima. Nilibaini ni nzima.

WAKILI WA SERIKALI: Hatua gani ikafuata?

SHAHIDI: Hatua ya pili ya uchunguzi wa pili.

WAKILI WA SERIKALI: Kivipi?

SHAHIDI: Nilichukua risasi mbili ya zile nilizoletewa calibre yake ni 9mm. Nikaenda kwenye chumba maalumu. Kwenye chumba kuna sehemu ya kupigia silaha mbalimbali.

WAKILI WA SERIKALI: Ulienda na kitu gani?

SHAHIDI: Nilikuwa na Pistol na risasi tatu.

WAKILI WA SERIKALI: Ulienda kufanya kitu gani hasa?

SHAHIDI: Kuna kifaa kinaitwa Tank Water Recovered Bullets.

WAKILI WA SERIKALI: Kiswahili ni nini?

SHAHIDI: Ni tanki la maji tunalotumia kupata risasi. Mle kwenye tanki kuna nyavu na kisha tunajaza maji, na unalifunga na kisha anaenda kupiga risasi yako.

WAKILI WA SERIKALI: Kwanini sasa mnapiga risasi kwenye tanki la maji?

SHAHIDI: Ili kupata maganda ya risasi na vichwa vyake.

WAKILI WA SERIKALI: Kwanini sasa mnapiga vile vielelezo?

SHAHIDI: Najiridhisha sasa. Je. ni kweli zile risasi ni nzima? Nakwenda kupiga sasa.

WAKILI WA SERIKALI: Nini matokeo ya uchunguzi wa kina?

SHAHIDI: Nikichukua risasi mbili nikaweka kwenye magazine. Nikaweka kwenye ile bastola nikapiga sasa. Nikapata maganda na vichwa vya risasi. Nikafanya hivyo tena kwa risasi ya pili. Nikapiga.

WAKILI WA SERIKALI: Risasi zako zilikuwa na alama. Je, risasi za alama zipi ambazo ulipiga?

SHAHIDI: K2 na K4

WAKILI WA SERIKALI: Ulifanya nini sasa kuhusiana na yale maganda?

SHAHIDI: Nilienda kuya- label yale maganda yangu mawili.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa kuyapa alama gani?

SHAHIDI: T1 na T2. T1 ilikuwa K2 na T2 iliyokuwa K4.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya labelling ni kitu gani sasa kingine kilifuata?

SHAHIDI: Nikaenda kuandaa riport yangu (Ballistic Examination Report).

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuandaa ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilisaini.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Nilipiga muhuri.

WAKILI WA SERIKALI: Muhuri gani?

SHAHIDI: Forensic Bureau Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Kuhusiana sasa na silaha yenyewe.

SHAHIDI: Baada ya hatua zote zote hizo nikafunga kwenye mfuko na nikafunga seal, nikasaini na kuandika tarehe.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kusaini ukapeleka wapi?

SHAHIDI: Chumba cha kutunzia silaha.

WAKILI WA SERIKALI: Na report yako sasa?

SHAHIDI: Niliweka kwenye bahasa na nikairudisha kwenye File Book. Baada ya hapo nikiwa nasubiri wenyewe waje kuchukua vielelezo vyao.

WAKILI WA SERIKALI: Vielelezo vyao vilikuwa vilichukuliwa siku gani?

SHAHIDI: Tarehe 27 Novemba 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Nani alikuja kuchukua vielelezo hivyo?

SHAHIDI: Afande Swila kutoka ofisi ya DCI.

WAKILI WA SERIKALI: Nani aliyemkabidhi afande Swila hivyo vielelezo?

SHAHIDI: Mimi mwenyewe.

WAKILI WA SERIKALI: Ulimkabidhi Swila vitu gani?

SHAHIDI: Riport yangu ya kiuchunguzi Ballistic Examination Report. Nikamkabidhi pistol moja ambayo ni Exibit K1 Calibre A5340 9mm. Model yake CZ 41 rangi nyeusi ikiwa na magazine yake. Pia nikamkabidhi risasi moja nzima iliyobaki ambayo nilii- label K3. Nikamkabidhi maganda mawili na bullets zake. Yale maganda niliya- label kama T1 na T2.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kwamba tangu ulivyomkabidhi Swila ni lini tena ulipata kuviona tena vielelezo?

SHAHIDI: Jana.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa jambo lipi?

SHAHIDI: Ili aniletee vielelezo kwa ajili ya ushahidi Mahakamani hii leo.

WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama hii report yako ya kiuchunguzi uliyoiandaa ni kitu gani kitakutambulisha?

SHAHIDI: Kwanza kwa nembo ya ofisi, nembo ya Polisi. Force namba zangu F5914 na majina yangu ya Koplo Hafidh Abdallah.

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Na signature yangu. Na muhuri wa ofisi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji shahidi anaonyesha anaweza akutambua nyaraka aliyofanyia kazi kwa ruhusa ya Mahakama. Tunaomba kumuonyesha.

(Shahidi anakabidhiwa)

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi litizame hilo kabrasha ndogo sasa uimbie Mahakama nilichokupatia ni kitu gani.

SHAHIDI: Ni report yangu niliyoindaa kuhusiana na uchunguzi wa silaha na risasi.

WAKILI WA SERIKALI: Ifahamishe Mahakama vitu gani vinaonyesha wewe ndiyo uliandaa.

SHAHIDI: Kuna nembo ya polisi, Force Namba, signature yangu. Kuna muhuri wa ofisi. Kwa hiyo ripoti hii ni ya kwangu.

WAKILI WA SERIKALI: Unaiomba nini Mahakama hii?

SHAHIDI: Naomba Mahakama hii Ipokee ripoti yangu kama sehemu ya ushahidi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji shahidi anaomba ipokelewa Ballistic Examination Report.

(Wakili wa Serikali anaipeleka upande wa mawakili wa utetezi).

WAKILI NASHON NKUNGU: Kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza sina pingamizi.

Wakili John MALLYA: Kwa niaba ya mshitakiwa wa pili sina pingamizi.

WAKILI DICKSON MATATA: Kwa niaba ya mshitakiwa wa tatu pia hatuna pingamizi.

WAKILI PETER KIBATALA: Kwa niaba ya mashitakiwa wa nne pia hatuna pingamizi.

(Jaji anapelekewa nyaraka).

(Mahakama bado imekaa kimya kidogo wakati Jaji akiandika).

JAJI: Mahakama imepokea nyaraka hii yenye kichwa cha habari Ballistic Report.

JAJI: Mahakama imepokea nyaraka hii ambayo iliandaliwa tarehe 26 Novemba 2020. Napokea kama kielelezo namba 02.

JAJI: Nakuomba shahidi usaidie kuisoma.

(Shahidi anapewa aisome)

SHAHIDI: Forensic Bureau Ballistic Laboratory DSM/F ya tarehe 26 Novemba 2020.

(Kisha shahidi anaisoma upya yote).

(Shahidi amemaliza Kusoma Riport yote ambayo ndiyo yale aliyokuwa anaieleza mahakama, lakini sheria inataka aisome upya Mahakamani.)

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa taarifa hiyo ulikuwa unachunguza silaha ya aina gani?

SHAHIDI: Pistol A5340 ya caliber 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa uchunguzi wako ulibaini nini kuhusu bastola?

SHAHIDI: Ni nzima.

WAKILI WA SERIKALI: Unamaanisha nini kusema ni nzima?

SHAHIDI: Ukiweka risasi inalipua.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa taarifa yako ulifanyia uchunguzi risasi tatu, je, ni za silaha gani?

SHAHIDI: Za pistol caliber 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa taarifa yako, functioning test ikoje?

SHAHIDI: Risasi ni nzima.

WAKILI WA SERIKALI: Zinatumika kwenye caliber gani?

SHAHIDI: Risasi za pistol ni za caliber 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Uhusiano wake risasi na bunduki ukoje?

SHAHIDI: Ni za kwake, kwa maana zimeingia na ikapiga.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa taarifa yako umesema unaambatanisha K1, K2, K3 na K4 was attached. Sasa elezea kwanini kwenye taarifa yako umeandika tena K4 wakati unasema ulishailipua.

SHAHIDI: Nimekosea Mheshimiwa Jaji. Ni typing error kwa sababu nilishailipua.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo attachments zitakuwa ni nini?

SHAHIDI: K1 ambayo ni bastola na K3.

WAKILI WA SERIKALI: Ukionyeshwa utavitambuaje?

SHAHIDI: Nimeweka kwenye bahasha. Nimesaini nikaandika na tarehe.

WAKILI WA SERIKALI: Mbali na hivyo silaha ina vitu gani vingine vitakavyokufanya uitambue?

SHAHIDI: Kwanza ni serial number, labelling ya forensic ambayo ni K1 FB /BALL /LAB 158 of 2020.

SHAHIDI: Maganda niliya- label kwa T1 na T2. Na vilevile nika- label FB /BALL /LAB 158 of 2020, na bullets nili- label kwa maganda yake.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, shahidi ameonyesha uwezo wa kuvitambua. Kwa ruhusa ya Mahakama naomba kumuonyesha.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi tazama mfuko mmoja baada ya mwingime.

(Shahidi anatazama mifuko ya nailoni ambayo anayoonyeshwa).

WAKILI WA SERIKALI: Huo mfuko ni nini?

SHAHIDI: Mfuko wa kuwekea vielelezo mbalimbali.

WAKILI WA SERIKALI: Unauhusiano gani na wewe shahidi?

SHAHIDI: Ndiyo nilitumia kuweka bastola.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kinachombulisha kuwa wewe ndiye uliweka silaha?

SHAHIDI: Nilisaini nikaweka na tarehe 26 Novemba 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Unasema kwenye mfuko huo kuna kitu gani?

SHAHIDI: Bastola yenye serial number A5340 caliber 9mm CZ 100 nyeusi.

WAKILI WA SERIKALI: Mfuko wa kwanza?

SHAHIDI: Una risasi, na nika- label na nikafunga kwa seal.

WAKILI WA SERIKALI: Kinachokutambulisha kuwa wewe ndiye uliweka?

SHAHIDI: Nilisaini na nikaweka tarehe.

SHAHIDI: Ina alama Exhibit K3.

WAKILI WA SERIKALI: Tumalizie mfuko wa mwisho.

SHAHIDI: Niliweka maganda T1 na T3 na bullets zake.

WAKILI WA SERIKALI: Unaiomba nini Mahakama?

SHAHIDI: Naomba Mahakama hii ipokee vielelezo hivi kwenye kesi husika.

WAKILI WA SERIKALI: Ipokee nini?

SHAHIDI: Bastola yenye serial number A5340 caliber 9mm ikiwa na magazine nyeusi kwa rangi yake, Model ni CZ 100.

WAKILI WA SERIKALI: Kwenye hiyo mifuko mingine?

SHAHIDI: Naomba Mahakama ipokee risasi ya pistol ya caliber 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Uliipa alama gani?

SHAHIDI: K3.

WAKILI WA SERIKALI: Mfuko wa mwisho Mahakama ipokee?

SHAHIDI: Maganda mawili ya risasi ambayo nimeyapa alama ya T1 na T2 na bullets mbili.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, shahidi ameomba vielelezo ambavyo amevitaja vipokelewe na mahakama.

(Wakili wa Serikali wanaipeleka mifuko mitatu kwa mawakili wa utetezi).

(Mawakili wa utetezi wanazingira kwa kuzunguka vielelezo kwa lengo la kuvikagua kila kimoja baada ya kingine).

WAKILI NASHON NKUNGU: Kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza hatuna pingamizi dhidi ya vielelezo hivi vyote kwa pamoja.

WAKILI JOHN MALYA: Hatuna pingamizi kwa niaba ya mshtakiwa wa pili.

WAKILI DICKSON MATATA: Hatuna Pingamizi kwa vielelezo vyote.

Wakili Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji nasi pia hatuna pingamizi.

(Jaji anainama anaandika).

(Jaji anawakumbusha kuwa Mahakama ya Rufani imesema kuwa vielelezo havipaswi kupokelewa kwa pamoja)

JAJI: Kwa hiyo kwa namba nitavipokea kwa tofauti tofauti.

JAJI: Basi Mahakama inapokea silaha moja ya moto aina ya Pistol aina ya A5340 kama kielelezo.

Mahakama inapokea maganda mawili ya risasi ambayo yametumika kama T1 na T3.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba sasa shahidi akate mifuko ili aweze kutuelezea.

(Shahidi anachana mifuko ya nailoni. Mahakama iko kimyaa kusubiri kitendo hicho kikamilike).

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi hiyo unasema ni silaha ya aina gani?

SHAHIDI: Pistol.

(Wakili wa Serikali anaishika na yeye hiyo pistol iliyotolewa kwenye mfuko wa nailoni).

JAJI: Wakili wa Serikali nakutahadharisha ulivyoibeba naona unamuelekezea Jaji.

(Mahakama inaangua kicheko).

WAKILI WA SERIKALI: Hii ni pistol ya aina gani?

SHAHIDI: Luger ya 2005.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea uliyokuwa unaelezea hii pistol.

SHAHIDI: Hiki ni kifunguo cha magazine. Ukiminya unaruhusu magazine Itoke. Magazine hii ina uwezo wa kuchukua risasi nane.

WAKILI WA SERIKALI: Unasema uli- test magazine?

SHAHIDI: Ukibonyeza spiring nilipima kama ina nguvu ya kusukuma risasi. Na hiii ni Box Magazine. Na magazine hii ni nzima.

WAKILI WA SERIKALI: Na ulisema barrow ndiyo ipi?

SHAHIDI: Ndiyo hii. Kwa Kiswahili ni mtutu. Nilipima kwa kuchukua barrow gauge nikatoa kwenye barrow, Je hii ni 9mm ikaniambia ni yenyewe.

WAKILI WA SERIKALI: Ulisema triger. Triger eleze triger ipo wapi.

SHAHIDI: Nilipima triger kwa kuiminya hivi (anaonyesha alivyoiminya). Nikaona ikafika kwenye 100.

WAKILI WA SERIKALI: Kwenye 100 ikafika hapa? Hebu onyesha Mahakamani firing yake na uwezo wake.

SHAHIDI: Hapa naikoki. Hii ni pini na hapa nikikoki panakuwa na risasi inaenda chemba. Nikaikoki nika- fire nikaona nyundo inagonga vizuri.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kingine ulifanya?

SHAHIDI: Nilipima barrow. Kupima kama ni safi. Nikaona barrow ipo safi. Hii ina serial number. Hawa Luger wanaweka Serial Number hapa na hapa (anaonyesha).

WAKILI WA SERIKALI: Ni ipi?

SHAHIDI: Imesajiliwa A5340. Kama haijagongwa serial number sijajua imeingia vipi nchini. Hii pia ni risasi niliipa K3.

WAKILI WA SERIKALI: Ulichunguza nini kwenye hii risasi?

SHAHIDI: Nilichunguza kiwashio, hapa ukiwa na chuma ukigonga inalipuka.

WAKILI WA SERIKALI: Kiwashio cha hiyo risasi kikoje?

SHAHIDI: Ni kizima.

WAKILI WA SERIKALI: Twende kielelezo cha mwisho.

SHAHIDI: Haya ni maganda. Kama ulienda Marekani wanakuandika 9mm Pass 50, kwamba kutoka kwenye base hadi kwenye kichwa ni pass 50. Hizi mbili ni bullets nimezipata baada ya kupiga kwenye tanki la maji, kwa maana hazikudhuru mtu. Wanaita Terminal Firing.

(Shahidi anarudishia vielelezo kwenye mifuko yake)

WAKILI WA SERIKALI: Mwisho kwa ufupi nini ugunduzi wako?

SHAHIDI: Kwamba vyote kuanzia bastola na hizo risasi tatu ni vizima na vinafanya kazi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.

JAJI: Upande wa utetezi?

KIBATALA: Naomba kwa ruhusa yako nimtambulishe Jeremiah Mtobesya ambaye alichelewa kwa sababu alikuwa Mahakama ya Rufaa. Na ninamatambulisha kwa sababu yeye ndiye ataanza maswali kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza.

(Jaji anainama na kuandika kidogo).

JAJI: Naliingiza jina lako kwenye orodha ya mawakili … Nitaruhusu watu wapumzike kidogo kunyoosha miguu na kupata maji mpaka saa saba na nusu. Naomba tujitahidi kutunza muda.

(Kisha Jaji ananyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kuondoka katika chumba cha mahakama).

Tumerejea mahakamani.

Saa 7:40 mchana Jaji ameingia Mahakamani

Mawakili wote wako kwenye nafasi zao.

Pande zote mbili zinasema wapo tayari kuendelea na kesi.

Jaji anaandika.

Anaanza Wakili Mtobesya kumhoji shahidi.

Mtobesya anamfuata shahidi.

Mtobesya: Shahidi unafahamu kitu kinaitwa Exibit Lebel?

SHAHIDI: Sifahamu.

Mtobesya: Wewe kama polisi nitakuwa sahihi nikisema Exhibit Lebel ni fomu namba ngapi?

SHAHIDI: Siyo fomu ni label. Siyo Fomu. Sisi ballistic tuna ya kwetu. Siyo fomu.

Mtobesya: Mweleze Mheshimiwa Jaji kama unajua Polisi Fomu Namba 145.

SHAHIDI: Siijui.

Mtobesya: Unaelewa kwamba ni matakwa ya kisheria kuhusu movements za exhibit kwamba Polisi yenyote anayehamisha kielelezo, hasa Polisi kuweka kumbukumbu ya jina lake na cheo chake anataka kufanyia nini?

SHAHIDI: Hakuna kitu kama hicho. Sisi tunasaini. Huweki jina wala cheo.

Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema kwenye mdomo wa silaha huwa kuna vitu ambavyo risasi ikitoka inaacha? Inaacha groove ambayo ni unique kwa kila silaha?

SHAHIDI: Hapana. Wewe unazungumzia gun powder.

Mtobesya: Sasa ndiyo nasema bullets ikitoka inaacha groove?

SHAHIDI: Hapana.

Mtobesya: Hizo impressions za grooves zinatoka wapi?

SHAHIDI: Hapana. Wewe unasema gun powder.

Mtobesya: Sasa tuokoe muda wa Mahakama. Wewe unajua grooves ni nini?

SHAHIDI: Ni michirizi baada ya kutoka risasi.

Mtobesya: Kwa hiyo grooves inapatikana kwenye nini?

SHAHIDI: Baada ya risasi kutoka kwenye silaha.

Mtobesya: Nitakuwa sahihi sasa nikisema kila bullets inapotoka inaacha grooves ambayo ni unique kwa kila silaha?

SHAHIDI: Sahihi.

Mtobesya: Nitakuwa sahihi ili utambue kuwa risasi hii imetoka kwenye silaha gani ni lazima nifafanishe barrow na grooves kujua imetoka kwenye silaha gani?

SHAHIDI: Hapana.

Mtobesya: Ni kwanini nikitaka kujua kuwa risasi imetoka kwenye silaha hii imetoka kwenye silaha fulani ni lazima nipigie (fire) na kwenda kulazimisha?

SHAHIDI: Lazima uwe na specimen ambayo ina standard fulani ili kuweza ku- compare. Kwa hiyo mimi ni lazima nitapiga kwenye bullets water tank kufanya mlinganisho.

Mtobesya: Kwa hiyo ili ujue ni lazima kulinganisha grooves?

SHAHIDI: Ndiyo.

Mtobesya: Kwa hiyo wakati unaonyesha vielelezo ulituonyesha hizi grooves ndiyo zilizofanana?

SHAHIDI: Nilionyesha bullets.

Mtobesya: Ulionyesha grooves?

SHAHIDI: Nilionyesha Pin Impresion.

Mtobesya: Ulionyesha grooves hukuonyesha?

SHAHIDI: Nilionyesha pin impresion.

Mtobesya: Kuna tofauti gani kati ya 9mm na 9mm Luger?

SHAHIDI: 9mm ni aina ya risasi na Luger ni aina ya bunduki.

Mtobesya: Ni ushahidi wako kwamba Luger siyo aina fulani ya bastola?

SHAHIDI: Luger ni aina ya bastola.

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa maana ya CZ 100.

SHAHIDI: Maana yake ni Zcheck Republic. Ni majina yake.

Mtobesya: Kwa hiyo unakumbuka wakati Goodluck anakupatia silaha alikuambia ni silaha ya aina gani?

SHAHIDI: Ile ni ofisi tunaenda kwa documents siyo lala lalala lala. Tunaenda kwa documents bhana!

Mtobesya: Wakati anakukabidhi alikukabidhi nini?

SHAHIDI: Pistol yenye serial number A 5340 Caliber 9mm black in colour.

Mtobesya: Unaweza kuiambia Mahakama kama kuna sehemu yoyote mliandikishana wakati mnakabidhiana?

SHAHIDI: Niliandika kwenye PF113.

Mtobesya: Aliweka model number?

SHAHIDI: Ndiyo. Aliweka CZ 100.

Mtobesya: Baada ya wewe kumalizia ulimrudishia nani?

SHAHIDI: Afande Swila.

Mtobesya: Mliandikishana pia?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilimkabidhi kwa documents.

Mtobesya: Na kwenye makabidhiano uliandika model number?

SHAHIDI: Ndiyo. Niliandika model number, aina ya silaha, Calibre yake na namba za risasi.

Mtobesya: Wakati wewe mmeletewa silaha kwa ajili ya kuangalia kama ni nzima, je, mlifanya finger prints kuangalia hiyo silaha?

SHAHIDI: Sikufanya.

Mtobesya: Kwa upande wa mhitakiwa namba moja naomba kuishia hapo.

Anaingia Wakili John Mallya.

MALLYA: Shahidi nitakuuliza mambo machache. Ni sahihi nikisema ni maabara iliyosheheni vifaa vya kisasa?

SHAHIDI: Of course!

MALLYA: Ni sahihi ina uwezo wa kufanya uchunguzi wa masuala yote unayoyafanya?

SHAHIDI: Inafanya yote.

MALLYA: Ni sahihi kwamba mnafanya uchunguzi kwa mujibu wa barua?

SHAHIDI: Ni sahihi kwamba nafuata maelekezo ya barua.

MALLYA: Naomba kielelezo Mheshimiwa Jaji.

(Wakili Mallya anamwambia shahidi soma paragraph ya kwanza hapa)

SHAHIDI: “I F5914 Hafidh Abdallah Mohamed Coplo wa Police Force States That(s) have been engaged in Examination of Fire Arms, Catridge, suspected…. “

MALLYA: Kwa maelezo yako ulitumwa na barua kufanya nini?

SHAHIDI: Nilitumwa kuchunguza bunduki, risasi na maganda ya risasi.

MALLYA: We uliletewa vitu gani uchunguze?

SHAHIDI: Risasi tatu na bunduki.

MALLYA: Maganda yalikuwapo?

SHAHIDI: Sikuletewa.

MALLYA: Vichwa vya risasi uliletewa?

SHAHIDI: Sikuletewa.

MALLYA: “I have been Engaged” maana yake nini?

SHAHIDI: Maana yake “nimefanya uchunguzi.”

(Mahakama inaangua kicheko).

MALLYA: Uliletewa maganda ya risasi?

SHAHIDI: Nililetewa risasi.

MALLYA: Uliletewa?

SHAHIDI: Sikuletewa.

MALLYA: Kwenye maandishi yako umeandika “and tools”, vifaa ambavyo hapa hujatuletea.

SHAHIDI: Sikuletewa vifaa.

MALLYA: Soma hapa (anamwonyesha pa kusoma).

SHAHIDI: …And tools. Vifaa mbalimbali.

Malya: Eheee! Halafu wewe hujatuletea hivyo vifaa.

JAJI: Asome sentence yote tuelewe.

(Shahidi anasoma, na mwishowe anasema “…and tools”).

Malya: Kwa hiyo hizo tools ziko wapi?

SHAHIDI: Tools siyo kwa kesi hii tu.

Malya: Kwa hiyo mwambie Jaji report yako siyo ya kesi hii tu.

SHAHIDI: Mimi Sikuletewa vifaa kwa kesi hii.

Malya: Riport hiyo kwa ushahidi wako inahusiana na kesi hii na inazungumzia uzoefu wako wa kazi.

SHAHIDI: Ndiyo. Ndiyo Maana nimeweka hapa.

[Malya: Mwambie Mheshimiwa Jaji.

MALLYA: Ulisema umeanza kazi mwaka 2013. Ni sahihi?

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Kutoka mwaka 2013 mpaka sasa ni miaka mingapi?

SHAHIDI: Miaka 18.

MALLYA: Haya. Katika ripoti yako unasema una uzoefu wa miaka 18. je, umetoa wapi miaka 18?

SHAHIDI: Siyo kwamba tangu nianze kazi yangu. Nikiwa nasoma.

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors. Je kuna errors ngapi?

SHAHIDI: Hiyo hiyo moja.

MALLYA: Shahidi, maana ya terrorist ni nini?

SHAHIDI: Ni ugaidi.

MALLYA: Terrorism maana yake nini?

SHAHIDI: Ni masuala ya utalii.

(Mahakama inaangua kicheko kirefu).

Malya: Narudia tena. Terrorist umesema ni Ugaidi, na terrorism maana yake nini?

SHAHIDI: Ni masuala ya UTALII.

MALLYA: Msomee Mheshimiwa Jaji hapo ulipoandika kuhusu “conspiracy” na ‘terrorist.’

(Shahidi anasoma kwa spelling zake C. O. N. S. P. I. R. A.C. Y.

MALLYA: Na hapo?

SHAHIDI: T.E.R.R.O.R.I.S.T.

MALLYA: Ulikuwa unajua kuwa unafanyia uchunguzi silaha zilizotoka wapi?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Kwa hiyo ulikuja kujua muda gani kuwa silaha zinahusika na ugaidi?

SHAHIDI: Nilijua baada ya kufungua barua.

MALLYA: Kwa hiyo wewe ulijua wakati gani kwamba silaha ulizoletewa zinahusika na ugaidi?

SHAHIDI: Ni baada ya kufungua barua.

MALLYA: Je, kati ya barua na silaha ulianza kupokea nini?

SHAHIDI: Nilipokea vyote kwa pamoja.

MALLYA: Kabla ya kesi hii ulishawahi kufanya uchunguzi juu ya mabomu au bunduki?

SHAHIDI: Ndiyo. Niliwahi kufanya.

MALLYA: Kwa hiyo unafahamu kwamba makosa ya ugaidi ni makosa serious au ni makosa mepesi?

SHAHIDI: Mimi niulizie kuhusu bunduki na risasi tu. Mambo ya ugaidi siyajui mimi. Nitaeleza facts kuhusu risasi na bunduki.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji, aambiwe ajibu swali langu.

SHAHIDI: Sijui kama ni makosa serious au mepesi.

MALLYA: Wakati unaelezea ushahidi wako ulitueleza kwamba wakati unapokea ulivaa gloves na vifaa vingine.

SHAHIDI: Hayo ni mambo ya kawaida sana. Siwezi kueleza kila kitu hapa kwamba nilivaa miwani, gloves na hijabu.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji, naomba ajibu swali langu.

SHAHIDI: Sikueleza.

MALLYA: Ulielezea hapa kwamba waliokuletea bunduki na risasi walikuwa wamevaa gloves?

SHAHIDI: Sikueleza.

MALLYA: Je, mtu alikuwa na bunduki haijasajiliwa na haimiliki kihalali. Je, inamaanisha ameifanyia uhalifu?

SHAHIDI: Jibu linategemea.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba nipewe risasi.

(Wakili Mallya anapewa risasi, naye anamkabidhi shahidi kizimbani).

MALLYA: Je, shahidi, kuna uwezekano hii ambayo hujaipiga hatujui kama inafanya kazi?

SHAHIDI: Hii nimeiacha.

MALLYA: Si kuna uwezekano ukapiga risasi halafu isilipuke?

SHAHIDI: Ndiyo kama kumefanyika mishandling.

MALLYA: Kwa hiyo hata hii inawezekana iwe nzima.

SHAHIDI: Ndiyo, lakini nilipiga mbili nikabakisha moja.

MALLYA: Katika maabara yenu kuna vifaa vya kupima finger prints?

SHAHIDI: Kwa ofisi yetu?

MALLYA: Ndiyo.

SHAHIDI: Ipo lakini ni upande wa mtu mwingine.

Malya: Na wewe hukujisumbua kutaka kujua kama hii bunduki imetoka kwa binadamu au kwa ng’ombe Hukujisumbua kufanya hivyo?

SHAHIDI: Mie nacheza na barua kwa sababu inataka nifanye nini. Nafanya hicho tu.

MALLYA: Soma tena hapa. (Anamwonyesha pa kusoma).

SHAHIDI: “I have been engaged in identification.”

Malya: Mnapo- identify silaha mnafanya nini?

SHAHIDI: Kungalia Serial Number. Kuangalia magazine. Tunaangalia silaha kwa ujumla. Tunaangalia fire arms, firing pin, pin impression, hammer, barrow, aina ya silaha, Serial Number yake, model yake.

MALLYA: Hapo hapo. Kuna mahali umeandika Examination Report Page Number 02. Mwambie Mheshimiwa Jaji kama orodha ya vyote kama umevionyesha ama ku- identify katika hiyo report yako.

SHAHIDI: Sikuvionyesha.

Malya: Mheshimiwa Jaji, ya kwangu ni hayo tu.

Anaingia Wakili Dickson Matata.

Matata: Kwa ajili ya mmshtakiwa wa tatu sitafanya cross-examination.

JAJI: Wakili wa mshitakiwa wa nne?

Anaingia Wakili Peter Kibatala.

KIBATALA: Naomba nipatiwe Kielelezo P3, P4 na P5, halafu nipewe dakika moja.

JAJI: Umevaa gloves?

(Mahakama inaangua kicheko)

KIBATALA: Sijavaa gloves.

KIBATALA: Nipo tayari Mheshimiwa Jaji. Nimeomba Kielelezo namba 04 Live Amunition.

KIBATALA: Umesema hizi risasi zina uhusiano na Luger. Nakuonyesha usome kwenye kitako.

(Shahidi anaonyeshwa na anasoma “9mm”)

KIBATALA: Kuna sehemu imeandikwa Luger?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Kuna sehemu yoyote umefafanua kwa Jaji kwamba katika kielelezo namba nne utaona 9mm lakini hakuna maneno Luger?

SHAHIDI: Sikufanya hivyo.

KIBATALA: Nauonyesha risasi nyingine. Soma kwenye kitako iwapo maneno 75 kama ilivyokuwa kwenye kielele namba nne.

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Je, ulifafanua kwa Mheshimiwa Jaji kwamba kuna utofauti wa namna hiyo?

SHAHIDI: Sikueleza.

KIBATALA: Ushahidi wako katika Mahakama kwamba hakuna neno Luger kwenye risasi na Mheshimiwa Jaji atumie kupima ukweli na uongo wako.

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji hii ni bunduki au risasi.

SHAHIDI: Risasi. Ganda la risasi.

KIBATALA: Hakuna neno Luger chini ya kitako.

SHAHIDI: Sioni. Naona tu 9mm.

KIBATALA: Naomba Mheshimiwa Jaji upatiwe uone.

KIBATALA: Nakuuliza tena chini ya kiapo. Usichezee Mahakama.

SHAHIDI: Maneno Luger yapo.

KIBATALA: Bado unataka Mahakama ikuchukulie wewe ni shahidi serious kabisa na ni afisa wa Polisi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Je, kielelezo hicho kina maneno 75?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umesema wewe moja ya kazi zako ni kufanya Comparison Analysis.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kuna tofauti au hakuna?

SHAHIDI: Upo.

KIBATALA: Kwa hiyo wewe unasisitiza wewe ni shahidi wa ukweli kabisa?

SHAHIDI: Ni sahihi pamoja na haya uliyoyasema.

KIBATALA: Kazi yangu ni kuuliza maswali tu. Analysis watafanya watu wengine.

KIBATALA: Uwepo wa utofauti wa maneno Luger na hii 75 hukufafanua kwa Jaji.

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Na kwenye report hiyo tofauti haipo?

SHAHIDI: Haipo ndiyo.

KIBATALA: Kwenye report umesema wewe ni mtaalamu wa miaka mingapi?

SHAHIDI: 11.

KIBATALA: Umesema kilichokufanya ufanye uchunguzi ilikuwa ni barua kutoka kwa nani?

SHAHIDI: DCI.

KIBATALA: Na barua hii ni nyenzo muhimu sana?

SHAHIDI: Ndiyo sababu inasema nini nifanye.

KIBATALA: Na kwamba ripoti yako haiwezi kuwepo bila barua?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na kwamba wewe ndiyo ulipokea barua kutoka kwa DCI?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo hiyo barua umetoa kama kielelezo.

SHAHIDI: Sikuitoa.

KIBATALA: Sema kwa Mheshimiwa Jaji iwapo uliitambua kuwa barua hiyo ni hii hapa hata kama hujatoa kama kielelezo.

SHAHIDI: Haipo hapa.

KIBATALA: Kwa hiyo hujaitambua.

SHAHIDI: Niliitambua ofisni.

KIBATALA: Kwani hapa ni ofisini?

SHAHIDI: Hapa Mahakamani.

KIBATALA: Uliitambua?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Barua inaonyesha bunduki na risasi zimetoka kwa nani?

SHAHIDI: Haupo sahihi inaonyesha makosa tu.

KIBATALA: Kwa hiyo wewe yale makosa kwenye ripoti yako yametoka kwenye ile barua?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ambapo hiyo barua hapa mahakamani haipo.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kwa pamoja ulishughulikia bunduki na risasi na uka- register?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ulitoa hapa Mahakamani hiyo register?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Umeonyeshwa hapa Mahakamani kwamba ile register ndiyo hii?

SHAHIDI: Ile ipo ofisini.

KIBATALA: Kwa hiyo hukuitambua Mahakamani.

SHAHIDI: Haipo hapa.

KIBATALA: Ulitoa ufafanuzi kuhusu hiyo barua kutoka kwa DCI?

SHAHIDI: Sikutoa.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwanini uliitwa kutoa register Mahakamani leo?

SHAHIDI: Sikuulizwa.

KIBATALA: Ulisema ulienda kuhifadhi hiyo silaha armoury?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ulimueleza Jaji kwamba wewe ndiyo In charge wa armoury?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Ni sahihi kwamba armoury huingizi vitu kama nyumbani kwako? Je kuna register ya armoury?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ulitoa hapa Mahakamani hiyo register ya armoury?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Wakati wa makabidhiano na Kopplo Goodluck mlikabidhiana silaha kwa hati ya makabidhiano?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kwa ruhusa ya Mahakama nitakuletea uweze kuitambua hiyo hati ya makabidhiano.

(Kibatala anamwoshesha shahidi hiyo hati na kumuuliza ndiyo yenyewe?)

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Naomba Mheshimiwa Jaji wenzetu wa nikabidhi original hati ya makabidhiano siyo hii copy.

(Mawakili wa Serikali wanaendelea kupekua).

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Tunaomba atupatie hiyo copy ya hati ya makabidhiano.

(Mahakama imekaa kimya).

(Mawakili wa Serikali wanaendelea kupekua).

KIBATALA: Kama wenzetu hawana, kuokoa muda wa Mahakama tuendelee na maeneo mengine.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Hapana Mheshimiwa Jaji. Kama wenzetu kwanza wanataka kutumia wafanye maombi hapa Mahakamani.

KIBATALA: Basi Mheshimiwa Jaji kama hawana wacha niitumie hiyo hiyo copy yangu.

WAKILI WA SERIKALI: Hapana Mheshimiwa Jaji. Sisi tunasema asitumie kabisa kwa sababu ilikuwa ni ushahidi wetu.

JAJI: Hoja halikuwa hiyo. Hoja ilikuwa muwape pia.

WAKILI WA SERIKALI: Hapana. Hatuwapi. Atuletee ombi kwa mujibu wa Sheria.

JAJI: Kwa nini sasa?

WAKILI WA SERIKALI: Ndiyo msimamo wetu.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, ili kuokoa muda Wakili Mtobesya ataendelea kunitafutia.

KIBATALA: Naomba Mahakama inisaidie Kielelezo p2.

KIBATALA: Wakati unatoa ushahidi ulisema uliletewa vielelezo vya bunduki na anatoka Ofisi ya DCI.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na Katika maelezo yako hukusema D. Koplo Goodluck anatoka Ofisi ya Upelelezi Dar es Salaam.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na Hukusema D. Koplo Goodluck anatoka CID Arusha.

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Barua inasema D. Koplo Goodluck anatoka wapi?

SHAHIDI: Ofisi ya DCI.

KIBATALA: Shahidi una uhakika na hilo? Nakukumbusha upo chini ya kiapo.

SHAHIDI: Sahihi.

KIBATALA: Katika riopti yako hii hakuna mahala popote. Hakuna mahala umezungumzia bunduki aina ya Luger.

SHAHIDI: Sikuweka. Nimeweka model na number.

KIBATALA: Shahidi, CZ100 ulitoa wapi?

SHAHIDI: Kwenye bunduki.

KIBATALA: Hukutoa katika nyaraka za makabidhiano wala katika barua iliyotoka kwa DCI?

SHAHIDI: Ilikuwapo.

KIBATALA: Je, katika Hati ya Makabidhiano hii Model CZ 100 ilikuwapo au haikuwapo?

SHAHIDI: Ilikuwapo.

KIBATALA: Kupitia Kielelezo P2 unasema ulipokea K2 mpaka K4. Mwambie Mheshimiwa jaji kama maelezo hayo yapo au hayapo.

SHAHIDI: Sikuweka.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji pia kuwa maelezo ya ufafanuzi tuliyoyaona katika Live Catridge hapa hayapo.

SHAHIDI: Sikuweka.

KIBATALA: Unafahamu kwamba ripoti kama hii haiongezewi nyama kutoka kwenye kizimba. Inatakiwa ijiongelee yenyewe. Unafahamu hilo au hufahamu?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Ni sahihi nikisema wewe Kingereza unakifahamu ndiyo maana taarifa umeandika kwa Kingereza?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Nini maana ya DCI.

SHAHIDI: Director Criminal of Investigation.

KIBATALA: Na ukasema Goodluck ametokea Ofisi gani DCI?

(Kibatala namwonyesha hshahidi mahali pa kusoma na kumwambia “Soma hapa”).

SHAHIDI: D/C Goodluck from Criminal Investigation Office.

KIBATALA: Nilipokuuliza ulisema hivyo?

SHAHIDI: Sikusema hivyo.

KIBATALA: Kwa hiyo kuna utofauti ulichoandika na ulichosema kwenye kizimba.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Shahidi, kwa mujibu wa kielelezo namba P2 ulipewa risasi tatu ambazo ni live, ambazo sisi ndiyo vidhibiti vyetu. Umeviona hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Havipo. Nilivipiga.

KIBATALA: Sijkuuiza kuhusu kuvipiga.

KIBATALA: Ulicholeta wewe ni risasi moja na maganda mawili ambayo hata hivyo vinatofautiana.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji ili kuzadhimu kutimiza vidhibiti kwamba katika ofisi ile palikuwa hakuna risasi nyingine mbadala ililazimu nitumie hivyo.

SHAHIDI: Sikusema hivyo.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo kuna mahala popote ulipata idhini ya kutumia vidhibiti kutoka kwa in charge wako kwa kesi ya ugaidi kubwa kama hii.

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Kwani barua upo mstari unasema unaweza kutumia risasi kupiga kwenye water tank?

SHAHIDI: Upo.

KIBATALA: Ikija tuotaona? Lakini Mahakamani pia hukusema.

SHAHIDI: Ndiyo sikusema.

KIBATALA: Rangi ni kitu ambacho unaweza kujua kwa visual examination au Ballistic Examination?

SHAHIDI: Kwa Visual Examination.

KIBATALA: Na kuonyesha kidhibiti kama ukiweka rangi wakati unapokea?

SHAHIDI: Sikuweka rangi. Kwenye visual niliweka rangi.

KIBATALA: Wakati unapokea?

SHAHIDI: Sikuweka rangi.

KIBATALA: Pamoja na rangi unaona kwa kuangalia tu, ila wewe hukuweka rangi baada ya kupokea.

SHAHIDI: Sikuweka rangi.

KIBATALA: Kwa kuwa hukuweka rangi huku ukaweka rangi, kuna utofauti au hakuna utofauti?

SHAHIDI: Kuna utofauti.

KIBATALA: Barua iliyokuja hilo kosa ambalo limeandikwa huko liliandikwa hivyo Conspiracy to Commit Terrorist?

SHAHIDI: Iliandika kwa Kiswahili kuhusisha na ugaidi.

KIBATALA: Wewe sasa Kiingereza chake ndiyo ukatafsiri kuwa “Conspiracy to Commit Terrorist”?

SHAHIDI: Ndiyo nimetafsiri hivyo.

KIBATALA: Kuna mahala popote umemwambia Jaji kuwa wewe ni Gazzeted Officer?

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Umetaja Serial Number. Je, umemwambia Jaji kuwa ile Serial Number ya bunduki kielelezo P3 inapatikana kwenye bunduki moja tu hapa duniani? Ulimwambia hivyo?

SHAHIDI: Sikumwambia hivyo.

KIBATALA: Wakati wa ushahidi wako nilisikia umesema mwaka wa kutengeneza bunduki ilikuwa mwaka gani?

SHAHIDI: Mwaka 1995.

KIBATALA: Ulielezea hivyo?

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Nimesikia ulisema bunduki hiyo ina uwezo wa kubeba risasi nane ila wewe ulipewa risasi tatu.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo ulisema lolote la kiuchuchunguzi iwapo risasi nyingine tano katika bunduki hiyo ilipiga kwa muda mfupi uliopita.

SHAHIDI: Sikuzungumzia.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kwamba ni utaratibu wa kawaida kila bunduki inapokuja kwenye uchunguzi lazima nitumie vielelezo vilevile kupiga katika water tank.

SHAHIDI: Nilimwambia.

KIBATALA: Shahidi, katika ushahidi wako wote kuna mahala popote umesema kuna nyaraka ilikuonyesha kwamba kuna uhusiano na mtu anayeitwa Adam Kasekwa?

SHAHIDI: Sikukwambia.

KIBATALA: Katika barua iliyoletwa majina hayo yalikuwapo au hayakuwapo?

SHAHIDI: Hayakuwapo.

KIBATALA: Katika hati ya makabidhiano majina hayo yalikuwapo au hayakuwapo?

SHAHIDI: Hayakuwapo.

KIBATALA: Katika hati ya makabidhiano Goodluck alikukabidhi wewe vidhibiti, je 9mm iliandikwa?

SHAHIDI: Haikuandikwa.

KIBATALA: Ulishawahi kumwambia Mheshimiwa Jaji kwamba hiyo Caliber 9mm…?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Pamoja na Hati ya Makabidhiano na barua kutokutaja Calibre 9mm, katika kidhibiti K1 bastola ametaja Calibre 9mm kabla ya uchunguzi?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilijaza kabla ya uchunguzi.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, kuhusiana zoezi nililositisha kuhusiana tulichozungumza asubuhi, nasubiria sasa.

JAJI: Nawaomba mawakili wa pande zote mbili ofisini kwangu.

Jaji anaahirisha kwa dakika kumi.

Saa 10:05 jioni Jaji amesharejea na kesi imeshatajwa tena.

JAJI: Muda uliopita wakili aliomba jambo Mahakama. Sasa tunaweza kuendelea.

KIBATALA: Unakumbuka kila kitu D/Coplo Goodluck alikutambulisha anatoka ofisi ya DCI?

SHAHIDI: Sikusema anatoka Arusha.

KIBATALA: Ni ushahidi wako katika Makabidhiano kwamba D/Coplo Goodluck anatoka kwa DCI au CID Arusha.

SHAHIDI: CID Arusha.

KIBATALA: Na Nyaraka hii ni nyaraka ya kisheria.

SHAHIDI: Zoezi rasmi la kisheria.

KIBATALA: Unafahamu madhara ya utofauti wa ushahidi wako na yaliyopo kwenye nyaraka?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Ni sahihi katika hati hii ya Makabidhiano inasema vitu fulani, kutoka sehemu fulani na ina sehemu ya kutaja majina?

SHAHIDI: Haina sehemu hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Objection!

(Wakili Kibatala ananyanyua nyaraka juu na kuuliza “maana yake nini”)

JAJI: Kwa hiyo tatizo kunyanyua?

KIBATALA: Nitaweka chini basi.

KIBATALA: Kwa hiyo shahidi nyaraka hii haina sehemu ya kujaza majina?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Hakuna sehemu unayotakiwa kujaza aina ya vifaa unavyokabidhiwa?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Nyaraka hii pia ina sehemu ya nafasi ya kuweka majina. Ipo au haipo?

SHAHIDI: Haipo.

KIBATALA: Na sehemu ya kujaza aina ya mashitaka kwamba anatuhumiwa kwa makosa … ipo au haipo?

SHAHIDI: Haipo.

KIBATALA: Je, katika hii Hati ya Makabidhiano kuna mahali inasema jina la fulani na mkabidhi mtu fulani katika fomu hii?

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Ina sehemu ya kuweka saini?

SHAHIDI: Ipo. Nimeweka Force Namba na saini yangu.

KIBATALA: Ndiyo Ushahidi wako huo?

KIBATALA: Nilikusikia sahihi una ujuzi na utalamu wa kutosha kuhusu masuala ya bunduki nchini Tanzania.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Katika ushahidi wako wote uliwahi kumwambia Mheshimiwa Jaji kuwa aina ya bunduki CZ100 Luger ni mojawapo ya bunduki kutoka Jeshi la Wanachi Tanzania?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Swali la mwisho kwako. Kuna mahala popote ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuhusu ulinganifu kati ya Ofisi ya CO Arusha DCI?

SHAHIDI: Sikumwambia.

(Jaji anaandika)

JAJI: Re-examination?

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi, nitakuuliza Kwa ajili ya ufafanuzi kwa yale uliyoulizwa Mahakamani uweze kuelewa ushahidi wako. Uliulizwa maswali kwenye ripoti yako paragraph ya kwanza inapoanza “I have been engaged … Tools na maganda.

SHAHIDI: Paragraph ya kwanza inajielezea na inajielezea uchunguzi nilikuwa nafanya pale forensic kwa miaka kumi nikaweka bunduki, risasi (ammunition) maganda (spent catridges). Na nikarejea nimefanya uchunguzi huu kwa muda wa miaka kumi.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa tools ambayo havikuletwa kwako vifafanue hapo.

SHAHIDI: Sasa hao hawakuleta tools.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa Kwanini ukiviandika hapo?

SHAHIDI: Sababu ndiyo navichunguza pale forensic bureau.

WAKILI WA SERIKALI: Kuna maswali umeulizwa hapa ukasema ni masuala ya utalii. Unakumbuka?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilisema “Terrorist” nikasema na kasema spelling nikatamka. Nikasikia “Tourism”, Tourism ni masuala ya kitalii.

WAKILI WA SERIKALI: Lakini kilichopo kwenye ripoti yako ni kitu gani? Ni terrorist? Uliulizwa swali ukasema hapa firing pin, barrow na ukaulizwa ulionyesha Mahakama jinsi hivyo vitu vinavyofanya kazi.

SHAHIDI: Nilionyesha.

MALLYA: Objection! Mheshimiwa Jaji sikuuliza swali la namna hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Naulizana na wenzangu. Mheshimiwa Jaji nimeulizana na wenzangu jibu nikiwa sikuonyesha hilo katika ripoti yangu.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi kwanini sasa hukuweka?

SHAHIDI: Nilichoweka nilichoombwa na mteja tu.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa ulichoombwa ni nini?

SHAHIDI: Kuchunguza pistol, risasi na maganda ya risasi.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali ukasema kwenye ripoti yako hakuna neno “Luger”. Ieleze Mahakama kwanini hukuweka?

SHAHIDI: Bunduki ni Serial Number.

WAKILI WA SERIKALI: Kwanini unasema bunduki ni Serial Number?

SHAHIDI: Serial Number ni unique.

MALLYA: Objection! Hiyo ni new fact kwa sababu hakueleza kuwa Serial Number ni unique.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tukumbushwe.

JAJI: Ndiyo Kibatala alimuuliza kwamba, Je, serial number haiwezi kuonekana kwenye bunduki nyingine yoyote?

WAKILI WA SERIKALI: Hukueleza Mahakama kwanini Luger hukuweka kwenye ripoti?

KIBATALA: Objection! Tuliuliza Luger ipo au haipo? Jibu likasema haipo. Akijibu lolote ni New Fact. Labda turuhusiwe tena kumuhoji wakimaliza.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji sisi tunataka atoe sababu kwanini haipo.

JAJI: Hiyo itatupeleka kwenye new facts na sababu watatakiwa warudi pia kumuhoji upya.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tunashukru.

WAKILI WA SERIKALI: Ulimaanisha nini kusema vielelezo havipo Mahakamani?

SHAHIDI: Nilikuwa namaanisha kuwa havipo kwa sababu nimevitumia kupiga katika ile bastola.

WAKILI WA SERIKALI: Ilifuatiwa na swalui hukumwambia Mheshimiwa Jaji kuhusu kutoleta hivyo vielelezo.

SHAHIDI: Mimi nilifuata maelekezo ya barua, kwamba natakiwa kupiga nikapiga.

JAJI: Swali lilikuwa linahusu nini na alichokujibu ndiyo ulichouliza.

WAKILI WA SERIKALI: Kajibu tofauti. Nilikuwa nataka kujua shahidi ulikuwa unamaanisha nini kusema hukuwa na idhini.

(Shahidi anakaa kimya).

WAKILI WA SERIKALI: Naomba nitoke hapo Mheshimiwa kuokoa muda wa Mahakama. Katika Ushahidi wako unasema ulipokea kielelezo cha kupokea 9mm lakini kwenye barua hakuna.

SHAHIDI: Kwa sababu wale ni layman hawawezi kujua ni silaha ya namna gani. Mimi ndiyo mtaalamu nikajua ni Pistol Calliber 9mm.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba mwenzangu aendelee.

Anaingia Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi uliulizwa kama uliomba idhini kwa kiongozi wako ili utumie risasi hizo hizo. Hebu eleza ni kwanini hukuomba idhini.

KIBATALA: Objection! Tunarudi kulekule. Kama akitoa sababu itakuwa mpya. Anamwalika shahidi atoe sababu.

JAJI: Swali linasema….

WAKILI WA SERIKALI: Kwanini hakuomba idhini?

KIBATALA: Itakuwa ni new fact akijibu.

WAKILI WA SERIKALI: Tunaomba tupewe nafasi. Wao ndio walifanya cross-examination.

JAJI: Ngoja aendelee.

SHAHIDI: Kwanza ni mambo ya kiofisi siwezi kueleza hapa Mahakamani. Mie naangalia barua siwezi kuuliza Afande……

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali ni kwanini hukutumia risasi zilizokuwapo maabara kwa uchunguzi wako badala yake ukatumia zilezile zilizoletwa na wao.

SHAHIDI: Kutokana na barua yao walitaka kujua ni nzima? Ndiyo maana nikatoa nikapiga kwenye bunduki.

WAKILI WA SERIKALI: Uliletewa kielelezo ukatakiwa usome nyuma ya maganda. Ukasema ni tofauti. Elezea maana yake ni nini.

KIBATALA: Objection! Huko wanakoenda ni kupya.

JAJI: Naona kuna problem.

WAKILI WA SERIKALI: Sawa Mheshimiwa Jaji. Nita- rephrase.

SHAHIDI: Hakuna nilipoombwa kufafanua kwenye barua.

WAKILI WA SERIKALI: Kwani wewe uliombwa kufanya nini?

SHAHIDI: Waliniomba kufanya uchunguzi wa pistol na risasi ni nzima?

WAKILI WA SERIKALI: Katika uchunguzi wako hakuna sehemu umetumia neno Luger ukasema ni kweli hakuna ulipo tumia. Sasa uliandika kwa utambulisho upi?

SHAHIDI: Kwa Serial Number yake A5340 calibre 9mm, Cz100.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusiana na tarehe 21 Novemba 2020 vielelezo kwa ajili ya uchunguzi. Swali lao lilikuwa hukumtaja ofisa aliyekuwa Armory ni ofisa yupi. Kwanini hukusema?

SHAHIDI: Sikusema kwa sababu hayo mambo ni ya kiofisi.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kwamba katika ushahidi wako wote hujataja jina la silaha aliyekamatwa nazo. Kwanini hukutaja?

SHAHIDI: Kwanza simjui Adamoo.

JAJI: Mmeleta kitu kipya.

WAKILI WA SERIKALI: Asante.

WAKILI WA SERIKALI: Endelea kitu cha pili.

SHAHIDI: Barua haikutaja majina.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusu D/C Goodluck kwamba anatoka Ofisi ya DCI na baadae CID ofisi Arusha.

KIBATALA: We must object this. Sisi tulifika mbali tukamuuliza kama alifafanua utofauti wa DCI na CID Arusha Anachotaka ni maelezo mapya.

WAKILI WA SERIKALI: Basi naondoa swali Mheshimiwa Jaji.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kwamba barua halikuwa na maelezo ya silaha.

SHAHIDI: Mimi ndiyo nitaeleza kitaalamu wala sio wewe mteja.

WAKILI WA SERIKALI: Hafidh uliulizwa kuhusu bastola ambayo Kibatala alitaja CZ 100 ulisema ni standard ya JWTZ. Kwanini sasa hukusema?

SHAHIDI: Sijui. Mie sijui.

WAKILI WA SERIKALI: Hafidh uliulizwa swali moja kuwa kwenye ushahidi wako hakuna mahala popote ulipozungumzia kama silaha ilikuwa imepigwa kabla ya kuletwa Forensic Bureau.

SHAHIDI: Hawakuomba kufanya uchunguzi wa gun powder resolution.

WAKILI WA SERIKALI: Ambayo ni kitu gani?

SHAHIDI: Gun Powder. Ni baruti.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali na Wakili Msomi Mallya kama bastola ile iliwahi kuwa mbovu na naadaye ikatengenezwa.

SHAHIDI: Sikuweza kujua kama ingekuwa mbovu na vilevile sikuombwa nifanye.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali pia kuhusiana na grooves zinazotoka kwenye bullets kama zinalinganishwa kutoka kwenye mtutu ukasema hapana. Kwanini hauwezi kulinganisha?

SHAHIDI: Grooves unaweza kulinganisha endapo zinakuja mbili. Unachua Specimen Side A na Side B Kufanya mlinganisho.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu. Hatuna maswali mengine.

JAJI: Shahidi tunashukuru kwa ushahidi wako na unaweza kwenda.

JAJI: Upande wa Jamuhuri?

WAKILI WA SERIKALI: Robert Kidando:* Tunaomba ahirisho la shauri hili mpaka Jumatatu tarehe moja Novemba 2021 tuweze kuendelea na usikilizwaji.

KIBATALA: Hatuna objection Mheshimiwa.

Ombi la kuahirishwa limekubaliwa mpaka Jumatatu Novemba 1, 2021.

Saa 10:57 jioni, Jaji anasimama na anaondoka mahakamani.

Like