Kesi ya Mbowe: Maswali ya mawakili na majibu ya shahidi (1)

Kama ilivyoripotiwa na mwandishi raia BJ, JUMATANO, SEPTEMBA 15, 2021. Endelea.


Mawakili wa Serikali ndio wameingia na magari mawili aina ya Land Cruiser Prado Tx

 1. Robert Kidando yupo
 2. Nassoro Katuga yupo
 3. Ignas Mwanuka yupo
 4. Esther Martin yupo
 5. Tulumanywa Majigo yupo

Uwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya, wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani, Canada, Uingereza na Sweden wako hapa mahakamani. Wanaingia kwenye chumba cha mahakama.

 1. Peter Kibatala (amejitambulisha mwenyewe kisha akawatabmulisha wengine)
 2. Jonathan Mndeme
 3. Boniface Mwabukusi
 4. Gaston Garubindi
 5. Dickson Matata
 6. Alex Masaba
 7. Sisti Aloyce
 8. Seleman Matauka
 9. Evaresta Kisanga
 10. Maria Mushi
 11. Deogratius Mahenyila
 12. Jeremiah Mtobesya
 13. Nashon Nkungu
 14. Saraha Aginga

Kibatala anasema Wakili John Malya ataungana nao baadaye.

Wakili wa Serikali anaomba kuendelea kwa upande wa mashahidi.

Jaji anauliza kama Kibatala yupo tayari.

Kibatala anasema wapo tayari.

Jaji anauliza anamuuliza Kibatala kama washtakiwa wanataka wakumbushwe mashtaka yao. Kibatala anasema waendelee.

Wakili wa Serikali anaulizwa, Je, washitakiwa wakumbushwe mashitaka yao? Mawakili hao wanasema washtakiwa wasomewe tena mashtaka yao.

Jaji anauliza “Kuna ulazima wa kisheria…?” Mawakili wa serikali wanakaa kimya.

Jaji anasema “Sawa. Acha wasomewe tena mashtaka yao.” Jaji anasema Kibatala asome hayo mashitaka, anayo hayo mamlaka ya kumteua yeyote asome hayo mashitaka.

Kibatala anaomba kwa Jaji kuw apamoja na heshima hiyo anaomba asisome yeye mashitaka. Jaji anauliza washitakiwa je, “mtaridhika wakili wenu akisoma mashtaka?”

Wote wanaitikia NDIYOOOOOOO.

Jaji anawaambia serikali wasome mashitaka.

Serikali wanauliza “Kwa Kiswahili au kwa Kiingereza?”

Jaji anasema kwa sababu ya uharaka wasome tu kwa Kingereza kama yalivyoandikwa.

Mashtaka yanasomwa na Serikali.

Hati ya mashtaka inasomwa upya kabla ya kesi kuendelea. Mashitaka yote 6 yamesomwa.

Mshitakiwa wa anasema SI KWELI
Mshitakiwa wa pili anasema SI KWELI
Mshitakiwa wa tatu anasema SI KWELI
Mshitakiwa wa nne anasema SI KWELI

Wote wamekana mashtaka.

Shtaka la pili linasomwa. Wanaulizwa.
Mshitakiwa wa kwanza SI KWELI
Mshitakiwa wa pili SI KWELI
Mshitakiwa wa tatu SI KWELI
Mshitakiwa wa nne SI KWELI

Shtaka la tatu linasomwa. Wanaulizwa tena shitaka la tatu, linamhusu mshtakiwa wa nne tu (Mbowe)

Mshtakiwa wa nne (Mbowe) anasema si kweli.

Shitaka la nne linasomwa.

Mshitakiwa wa kwanza anasema SI KWELI
Mshitakiwa wa pili anasema SI KWELI
Mshitakiwa wa tatu anasema SI KWELI
Mshitakiwa wa nne anasema SI KWELI.

Linasomwa shtaka la tano ambalo linamhusu mshtakiwa wa pili peke yake. Mshtakiwa anakana shtaka na anasema SI KWELI.

Linasomwa shtaka la sita na la mwisho ambalo linamhusu mshtakiwa wa kwanza peke yake. Yeye anakana anasema SI KWELI.

Wakili mmoja wa Serikali anatoka kumuita shahidi. Jaji anasema shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri aitwe apande kizimbani. Wakili mwingine wa Serikali anasema shahidi huyo ameenda kuitwa.

Sasa shahidi kapanda kizimbani tayari kutoa ushahidi. Jaji anamwambia anaweza kujitambulisha.

Shahidi anajitambulisha. Anasema anaitwa ACP Ramadhani Kingai. Huyu ni polisi.

Jaji anauliza “huyu ni shahidi namba ngapi?” Wakili wa Serikali anasema ni shahidi namba mbili.

Unapita muda mahakama imetulia kimya. Halafu Jaji anauliza “Dini…?” Shahidi anajibu “Muislamu.” Jaji anamwambia “thibitishisha.”

Shaidi anasema “Wallah, billah, subillah nathibitisha ushahidi nitakaotoa utakuwa ni wa kweli.”

Wakili wa Serikali anasimama. Jaji anawauliza akina Kibatala “Utetezi mpo tayari?”

Wakili wa Serikali anamwambia shahidi “…nitakuuliza maswali na utaenda kwa utaratibu sababu Jaji ataandika.”

Wakili wa Serikali anamuuliza shahidi “umejitambulisha ACP Ramadhani Kingai. Wewe unafanya kazi gani?”

Shahidi: Ni afisa polisi

Wakili wa Serikali: upo kituo gani cha kazi?

Shahidi: Nipo ofisi ya RPC Kinondoni iliyopo Oysterbay

Jaji: Je tunamskia wote shahidi?

Kibatala anamtaka shahidi aongeze sauti kwa sababu hasikiki vizuri

Wakili wa Serikali: Je unaweza kusema ukiwa akamanda wa Polisi majukumu yako ni nini?

SHAHIDI: Nikiwa akamanda wa Polisi Kinondoni jukumu langu ni kulinda watu na mali zao, pili ni kuzuia uhalifu

WAKILI WA SERIKALI: Una muda gani tangu ukiwa kamanda wa Polisi Kinondoni?

SHAHIDI: Nina miezi 10 tangu nihamie kutoka Arusha

JAJI: Na Arusha ulikuwa RPC

SHAHIDI: Hapana. Arusha nilikuwa RCO

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa RCO kwa muda gani?

SHAHIDI: Tangu 2018 mpaka mwaka jana Novemba

WAKILI WA SERIKALI: Elezea Denis Urio unamfahamu vipi?

SHAHIDI: Ni Luteni wa JWTZ

WAKILI WA SERIKALI: Ulimfahamu tangu lini?

SHAHIDI: Mwaka jana nikiwa Oysterbay kikazi nilipigiwa simu na afande aliyekuwa Kamishina wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai, aliyekuwa Kamishina wa Polisi Robert Boazi

SHAIDI: Alinipigia Simi akitaka niende Ofisini kwake. Kwamba Niende Kuna Maelekezo ya kazi. Nilipoenda ofisini Kwake ndipo nilipo Mkuta Luten Deni Urio

WAKILI WA SERIKALI: Wakili wa Serikali Ofisi hiyo Ipo wapi?

SHAIDI: Ofisi ipo Mtaa wa Ohio hapa Dar es salaam

WAKILI WA SERIKALI: Elezea baada ya kufika.

SHAIDI: Baada ya kufika kwa Afande Boazi, aliniambia Kuwa Denis alikuwa na taarifa ya kihalifu. Alimuomba Denis Urio ambaye ni Luteni wa JWTZ aanze kutuelezea kwa Pamoja Mimi na DCI

JAJI: Endeleaaaaa

SHAIDI: Alitueleza kuwa Kuna Kundi la Kiharifu ambalo linaandaliwa na Freeman Mbowe. Ambalo kundi hilo lilikuwa na Lengo la kudhuru viongozi wa Serikali. Kundi hilo pia lilikuwa nimejipanga kufanya vitendo ya akuchoma Vituo vya amafuta,alitumia kulipua vitu…

Shahidi anaeleza kuwa Mbowe alikuwa anamwambia kwa vyovyote vile lazima achukue mamlaka ya nchi na kumwambia Denis kwa kuwa yeye ni Homeboy wake, angempa mamlaka makubwa pale ambapo angekuwa amepata mamlaka ya nchi.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi elezea ni kwa nini Mbowe alimwambia Luteni Deni na si mtu mwingine.

SHAHIDI: Denis alieleza kuwa Mbowe amemuomba kuwa amtafutie watu wa kutekeleza mambo hayo, wawe makomandoo wastaafu au waliofuluzwa kazi.

WAKILI WA SERIKALI: Makomandoo kutoka wapi?

SHAHIDI: Makomandoo kutoka Tanzania

WAKILI WA SERIKALI: Wawe wastaafu wapi?

SHAHIDI: Kutoka JWTZ.

WAKILI WA SERIKALI: Ulimulekeza Swila afungue Uchunguzi kuhusu swala gani

SHAHIDI: Uchunguzi ulikuwa upelelezi mipango iliyokuwa inataka Kufanyika

JAJI: Huyu Swila ni nani..?

SHAHIDI: Swila ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi

Kisha shahidi anaendelea kutoa ushahidi wake. Anasema baada ya hapo alikuwa anaendelea kuwasiliana na Luteni Denis Urio na kwamba ameshatumiwa nauli katika Kipindi hicho walikuwa wameshapatikana Vijana wawili.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea Kama hao Vijana wawili walikuwa na sifa hizo alizoelekezwa

KIBATALA: Objection your honor, Wakili anamfundisha shahidi.

JAJI: Rudia swali au jibu objection (ya Kibatala)

WAKILI WA SERIKALI: (anarudia swali)

WAKILI WA SERIKALI: Elezea hao vijana ni akina nani?

SHAHIDI: Denis alinieleza kuwa Mbowe amefamya kijana mmoja Khalfan Bwire kuwa mlinzi wake. Huyu alikuwa Komandoo alifukuzwa kazi kutokana wizi wa mafuta wa Standard Gauge

WAKILI WA SERIKALI: Ilifunguliwa wapi?

SHAHIDI: Police Central Dar es Salaam

JAJI: Ulifungua kesi gani..?

SHAHIDI: Kula Njama ya kutenda vitendo vya kigaidi

WAKILI WA SERIKALI: ACP Kingai unasema ulimueleleza Inspector Swila kufingua jalada la kesi ya kula njama ya kutekeleza matendo ya kigaidi. Kwanini.?

SHAHIDI: Ni kwa Sababu ya nature ya makosa yenyewe,mama yangeweza kufanywa yangeweza kuleta madhara kwa Watanzania hasa katika kipindi kile tulichokwepo.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kutoa maelekezo hayo nini kilifutia?

SHAHIDI: Tarehe 04 Agosti mwaka 2020 nilienda Kukutana na Luteni Denis Urio. Aliniambia kwamba alishapata tena vijana wawili na amewaunganisha na Freeman Mbowe. Akanitajia vijana hao ni Adama Kasekwa alimaarufu Adamoo na Mohammed A Ng’wenya

JAJI: Endelea.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Kupata taarifa Kitu gani kiliendelea

SHAHIDI: Alinieleza tayari vijana hao walishafika Moshi

JAJI: Eleza ni vijana wapi. Wote wanne au wawili wa mwisho?

SHAHIDI: Asante Mheshimiwa, aliniambia Vijana watati kati ya hao wa Nne

WAKILI WA SERIKALI: Eleza walikuwa wamefikia kwa madhumuni gani

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Kupolea raarifa hiyo ulichukua hatua gani

SHAHIDI: Niliwasiliana na DCI nikamfahamisha na baada ya kumfahamisha alielekeza niunde timu itakayofanya ufuatiliaji na hatimaye kuwakamata watu hao kabla awajafanya madhara yoyote kwa wahusika. Baada ya maelezo haya nilimtafuta Assitan Superintendent wa Polisi ambaye kwa Sasa ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Jumanne. Na mwingie Inspector Mahita, Detective Coplo Francis, Detective Constable Goodluck na Dereva wangu Constable Azizi. Tulianza kuweka miundombinu ya kuwakamata watuhumiwa kabla awajafanya madhara yoyote.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea shughuli gani alifanya baada ya ufuatiliaji.

SHAHIDI: Siku ya Jumanne nilieleka Moshi, ambapo hao watuhumiwa walikuwa, na kwamba jioni Ileile tulianza ufuatiliaji wa hao watuhumiwa kwa ajili ya kuwa kamata. Lakini siku hiyo taarifa hazikuwa zimekaa sawasawa. Tarehe 04 hatukufanikiwa kuwakamata. Baada ya mawasiliano na wasiri wetu tulihairisha zoezi na usiku ule tukawa tumelala Moshi. Asubuhi Agosti 5, 2020 tuliamka na kuweka miundombinu na wasiri wetu kwa ajili ya ufuatiliaji. Ufuatiliaji tulipata taarifa Kuwa watuhumiwa wapo maeneo ya ya Rau Mjini Moshi

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kupata taarifa hiyo ulichukua hatua gani?

SHAHIDI: Tulifuatilia eneo hilo na tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili, Adam Kasekwa na Mohammed Ling’wenya. Wakati tumewakamata, tumewaweka chini ya ulinzi nilimuelekeza ACP Jumanne awapekue Maungoni. Adama Kasekwa alivyopekuliwa alipatikata maungoni akiwa na Pisto moja aina ya Ruvern iliyokuwa na namba 53A 5340

SHAHIDI: Pia alikutwa na risasi tatu. Alikuwa na kete 58 za heroine, madawa ya kulevya. Mohammed Kingwenya alikuwa na kete 25 za madawa ya kulevya.

WAKILI WA SERIKALI: Eleza upelelezi huu ulifanyika mbele ya nani?

Shahidi: Ulifanyifanyika palepale mbele ya mashahidi.

Wakili wa Serikali anamuuliza shahidi kama anawakumbuka hao mashahidi. Alisema anakumbuka wawili wanaitwa Anita na mwingine anaitwa Esther.

SHAIDI: Baada ya kujaza hati ya kuchukua vitu, tuliwachukua watuhumiwa na wale mashahidi hadi Kituo cha Polisi Mjini Kati kwani eneo la Rau lilikuwa siyo rafiki kwa kuandika maelezo yao pale.

Anaulizwa kwanini eneo la Rau halikuwa rafiki? Anajibu ni kwa sababu lilikuwa na fujofujo.

JAJI: Spellings za hilo eneo?

SHAHIDI: RAO

JAJI: Mwanzo tulikuwa tunasikia ni RAU. Kwa hiyo ni RAU au ni RAO?

SHAIDI: Ni RAO.

SHAHIDI: Ni RAO Madukani

Kisha shahidi anaendelea: Baada ya kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro nilimwachia Jummane aendelee kufanaya mahojiano.

SHAHIDI: Wakati huohuo tukawa tunaendelea sisi na watuhumiwa kumtafuta Moses Lijenje kwa sababu hatukuwa tumemkamata na wenzake.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea ufuatiliaji wa Moses Lijenje ulifanyikaje?

SHAHIDI: Wakati huo mchana, tulitoka na watuhumiwa mle ambapo wwanapiga na Moses lakini zoezi lile lilituchukua mpaka usiku. Tulipofika usiku tuliamua kupumzika na kulala tena, na kuendelea kesho yake Tarehe 6 Agosti.

Wakili wa Serikali: Kwa ile tarehe 5 mlipokuwa mmekamata Adam na Lingwenya ni nani aliyekuwa anawaelekeza kumleta Moses?

SHAHIDI: Ni Watuhumiwa wenyewe

WAKILI WA SERIKALI: Maeneo gani mliyokuwa mnapita?

SHAHIDI: Boma Ng’ombe, Machame na Arusha.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea ikawaje?

SHAHIDSI: Mpaka mwaka jana mwezo wa tisa tulikuwa hatujafanikiwa kumpata Moses Lijenje.

WAKILI WA SERIKALI: Ufuatiliaji wa tarehe 6 ikawaje?

SHAHIDI: Ulikuwa na ugumu wa kumpata tena baada ya ufuatiliaji na kupita maeneo mengi.

Wakili wa Serikali: Naomba kukurudisha nyuma kidogo … Siku ya tarehe 5 watuhumiwa uliwapeleka wapi?

SHAHIDI: Central Station Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Saa ngapi?

SHAHIDI: Sikumbuki … zaidi ya saa nne na nusu.

WAKILI WA SERIKALI: Yale maeneo mliyokuwa mnamtafuta Moses Lijenje Moshi Boma Ng’ombe ni maeneo gani?

SHAHIDI: Ni maeneo waliyokuwa wanamtafuta Ole Sabaya.

WAKILI MTOBESYA: Objection. Naona kama anaongea mambo ambayo bado shahidi hajaongea.

Jaji anawataka mawakili wa Serikali wamjibu Wakili Mtobesya ambaye ni mmoja wa mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake.

WAKILI WA SERIKALI: Mimi nimemuuliza Shahidi ACP Kiingai, unasema umemfuatilia Moses Moshi, Boma Ng’ombe na Machame. Je ni maeneo gani haswa?

Jaji anamuuliza Wakili Mtobesya “kuna tatizo na hilo swali?”

WAKILI MTOBESYWA: Nimefanya Objection kwenye line wakili wa Serikali aliyokuwa anaelekea. Shahidi amevuka mipaka kwa shahidi anayoelekeza kuhusu Fact. Ukisoma Section 6 ya Evidence Act.

Jaji anauliza je, pana sababu ya msingi ya kuendelea na objection?

WAKILI MTOBESYA: Tunaondoa Objection baada ya ushauri na wenzangu.

JAJI: Taja maeneo shahidi.

SHAIDI: Moshi Mjini.

JAJI: Hayo tumeshayasikia

SHAIDI: Maeneo mengine ni yale waliyokuwa wamefikia wao wakati wanatoka Dar es Salaam. Na maeneno mengine waliyokuwa wanamfuatilia Ole sabaya.

JAJI: We Wakili wa Serikali … hayo yanatusaidia nini?

WAKILI WA SERIKALI: Unasema ulienda Machame. Ulienda eneo gani?

SHAIDI: Kuna Hotel inaitwa aishi Ambayo ni Mali ya Freeman Mbowe

WAKILI WA SERIKALI: Na Boma Ng’ombe ….

SHAIDI: Ni Hapohapo Boma Ng’ombe

WAKILI WA SERIKALI: Nitaenda kwenye swali lingine baada ya tarehe 06 baada ya kurudisha taarifa kwa DCI ni hatua gani iliyokuwa umechukua?

SHAIDI: Tulielekea Dar es Salaam kwa ajili ya ufuatiliaji na hatua nyngine ya upelelezi na ambapo Dar es Salaam ndipo Center ya jalada lilipofunguliwa.

WAKILI WA SERIKALI: Safari ya Dar es Salaam alianzia wapi?

SHAIDI: Ilianzia Moshi tarehe 7 Agosti 2020 saa 11 alfajiri ndiyo tulipofika Central Police Station.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea Adama kwa wajio wake.

SHAHIDI: Adam Hassa Kasekwa ni yule pale wa pili. Si mrefu sana wala mfupi sana.

SHAHIDI: Na Mohammed ni mtumuhiwa aliyekaa wa tatu kutoka kushoto kwa Khalifan.

Shaidi anaruhusiwa kwenda walipo akawaonyeshe pale pale walipo. Shaidi anamshika Adam Kasekwa, kisha anamshika Mohammed Lingwenywa.

Amemaliza sasa anarudi anarudi kizimbani.

Jaji anauliza. Mlioguswa na shahidi ni sahihi? Adam anasema ni sahihi. Mohamed naye anasema ni sahihi.

WAKILI WA SERIKALI: Mlipofika Central Police alfajiri, nini kilifanyika?

SHAIDI: Tuliwaweka mahabusu. Sisi tukaenda kupiga mswaki na kunawa.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea?

SHAIDI: Nilimuhoji Adam Kasekwa kwa njia ya onyo.

WAKILI WA SERIKALI: Mahojiano hayo uliyafanyia wapi?

SHAIDI: Central Police Station Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa sababu ulimkamatia Moshi, ni sababu gani iliyopelekea ukafanya mahojiano Dar es Salaam?

SHAIDI: Dar es Salaam ni sehemu kesi ilipofunguliwa. Pia palikuwa na taarifa watuhumiwa wengine wapo Dar es Salaam.

SHAHIDI: Na Kwamba ndipo sehemu sahihi ya watuhumiwa kuhojiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea ni taratibu gani ambazo ulizitumia.

SHAIDI: Kwanza nilimfahamisha mtuhumiwa haki zake. Haki hizo ni pamoja na mimi kujitambulisha kwake.

SHAHIDI: Lakini pia kumueleza kosa lake.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa sheria gani?

SHAHIDI: (Badala ya kutaja sheria, shahidi anaendelea kusema) Nilimuonya halazimishwi kusema lolote.

SHAHIDI: Alinijibu kuwa yupo radhi kuandika maelezo akiwa peke yake.

SHAHIDI: Haya yote nilikuwa nayaongea nikiwa naandika na mwisho akawa tayari kusaini maelezo yake akiwa mbele yangu.

WAKILI WA SERIKALI: Ulisema ulimfahamisha kosa lake na Sheria?

SHAIDI: Kosa la kula njama na kutenda vitendo vya ugaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Kumuonya na Kuandika Maelezo ulifanya nini?

SHAIDI: Niliandika maelezo yake, baada ya maelezo hayo nilimpa akayasoma. Nikampa yeye mwenyewe kwa uthibitisho wake akasema yapo sawasawa na akayasaini.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya yeye kusaini wewe ulifanya nini?

SHAIDI: Niliyafunga muda wa saa 3 asubuhi.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa unasema kayasaini, kasaini kwa namna gani?

SHAIDI: Kwa saini ya kalamu na dole gumba.

JAJI: Aina gani ya kalamu?

SHAIDI: Kalamu kwa maana ya peni.

WAKILI WA SERIKALI: Baada sasa kumaliza kuandika maelezo yake ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilitengeneza jalada la kesi.

WAKILI WA SERIKALI: Unayatambuaje maelezo yako?

SHAIDI: Nayatambua kwa mwandiko wangu, sahihi ya Adam na sahihi yangu.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kumkabidhi karatasi hii aione.

SHAIDI: Natambua haya ni maelezo niliyoandika kwa mwandiko wangu, na sahihi yangu na mtuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Ungependa statement hii itumike Mahakamani kama ushahidi?

SHAHIDI: Ndiyo naomba itumike kama sehemu ya ushahidi.

Kuna mapumziko ya dakika mbili sasa. Mawakili wa utetezi, akina Kibatala, wamepewa kupitia hati ya maelezo aliyoyatoa Shahidi ACP Kingai.

Tayari mawakili wa utetezi wamesimama kuielezea hati hiyo na maelezo yaliyotolewa.

Wakili Kibatala anaanza.

Kibatala anasema hiyo hati ina matatizo.

Kibatala anasema maelezo ya hati hiyo yamechukuliwa nje ya muda wa kisheria.

Kibatala anasema maelezo yamechukuliwa zaidi ya saa 4 tangu mshtakiwa atiwe kizuizini.

Anasema ni zaidi ya saa nne tangu mtuhumiwa atiwe chini ya ulinzi huko RAU, Moshi na kwa kuwa kifungu husika kimeweka masharti ya lazima, kwa kuwa yamechukuliwa nje ya muda hayawezi kupokelewa mahakamani.

Kibatala anasema kabla na wakati maelezo yanachukuliwa kwa mashitakiwa Adama Kasekwa aliteswa (Tortured) na zoezi hilo la kumtesa lilisimamiwa na Shaidi namba moja ACP Kingai na maafisa wengine wa Polisi.

Kibatala anasema: “Ssehemu ya kwanza ya pingamizi letu kuhusu ushaidi wetu ni kuhusu jambo la sheria na sehemu ya pili ni namna ushaidi ulivyopatikana.”

KIBATALA: “Naiomba Mahakama ifanye kesi ndogo katika kesi kubwa.”

JAJI: “Kwa maana hiyo tutoe hukumu sehemu ya kwanza? Au tufanye hukumu kwa zote mbili?

KIBATALA: “Tutoe hukumu sehemu ya kwanza kisha tufanye kesi ndani ya kesi.”

JAJI: “Unafikiri inawezekana utaratibu zote na uchukuaji wa ushaidi unaweza kuwa sehemu ya kesi ndogo?”

KIBATALA: “Ndiyo. Inawezekana kwa sababu sisi tunataka tuzingatie kifungu 169 CPA.”

MTOBESYA: (Anamtazama jaji halafu anasema) “Ukisoma Kifungu cha 151 kinaruhusu kuondoa muda pale mtuhumiwa anakuwa anaendelea na upelelezi, lakini kwa ushaidi wa Shaidi wa Kwanza awali waliwakamata tarehe 5 na waliwaweka lock up … tarehe 6 walikuwa nao wote na akasafiri kuja Dar es Salaam na wakafika tarehe 7 alfajiri.”

WAKILI MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, kuna muda hapa haujaelezewa. Ukisoma ushahidi wa shahidi wa kwanza anasema hawa watu walihifadhiwa majira ya saa 4 usiku. Ukiangalia sioni sababu kuna nini kiliwazuia wasichukue maelezo. Labda kama pangekuwa na ushahidi mbeye yako yanayo onyesha pana sababu iliyosababisha wasichukue maelezo … Ukisoma hukumu mbalimbali za Mahakama Kuu, zinaeleza kuwa labda kama palikuwa na mazingira yakiyopelekea msichukue maelezo wakati wanafanya maelezo.

JAJI: Je, unaona unahitaji kesi ndogo ndani ya kesi hii kama Wakili Kibatala alivyosema kwa kifungu cha 169 cha CPA?

WAKILI MTOBESYA: Vifungu vya ushaidi vinamtaka shahidi yeye ndiyo aeleze. Tukienda upande wa pili wa kesi ndogo inampa shahidi kuelewa ambayo hajayaleza.

JAJI: Je mshatakiwa wa pili alitoa hayo maelezo au hajayatoa? Je, washitakiwa walitoa maelezo au hawajatoa iwe kwa mateso au la?

WAKILI MTOBESYWA: Maelezo yaliyochukuliwa kinyume na sheria hayawezi kuwa maelezo halali.
WAKILI MTOBESYWA: Mheshimiwa Jaji baada ya kujiridhisha kama walifuatisha vifungu vya sheria ndiyo twende kwenye kesi ndani ya kesi ya msingi.

WAKILI WA SERIKALI: Tumesikia mapingamizi yote.

WAKILI MTOBESYWA: Kwa maoni yetu, mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na upande wa utetezi yanaweza kutolewa baada ya mahakama hii kufanya kesi ndogo ndani ya kesi … Ni baada ya Wakili Kibatala sehemu ya pili kulalamikia ukiukwaji wa taratibu za kisheria wakati wa kuchukua maelezo … Na hata sehemu ya kwanza ya maelezo ya kwanza ya Wakili Kibataka pia inauhusiano na kesi kubwa.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa sisi tunaona pingamizi la kwanza lina uhusiano na pingamizi la pili. Mahakama ijielekeze kwenye kesi ndogo katika kesi ya msingi … Jambo lingine hata wakati Wakili Mtobesywa alikuwa anaelezea anashindwa kujitenganisha na ushahidi.

WAKILI WA PILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji. Ni msimamo wetu kuwa mapingamizi haya yasikilizwe kupitia kesi ndogo, Baada ya ushaidi … Mahakama ituruhusu kuwasilisha … Kibatala alisema Shaidi na maafisa wengine wa polisi waliwatesa washitakiwa. Atusaidie kuwataja pasipo kutuacha. Je, ni wakina nani?

WAKILI KIBATALA: Tunaomba tupate ruhusa ya mahakama twende kwenye kesi ndogo katika kesi ya msingi (Trial within a trial). Mapingamizi ni mawili:

 1. Maelezo ya watuhumiwa kuchukuliwa nje ya muda
 2. Maelezo ya watuhumiwa kutolewa kwa kuteswa

JAJI: Kimsingi pingamizi la kwanza likuwa linaweza kutatuliwa bila kuwa na kesi ndogo katika kesi ya msingi. Lakini kwa pingamizi la pili linataka Mahakama ihairishe kusikiliza kesi ya msingi, tusikilize kwanza kesi kuhusu pingamizi la pili kuhusu watuhumiwa kama waliteswa au la … Nakubaliana na mawakili wa upande wa utetezi kusimamisha kesi kuu ya msingi kwanza na kuanza kusikiliza kesi ndogo.

JAJI: Nahairisha kesi hii ya msingi hadi saa nane tuanze kesi ya kusikiliza kesi ndogo.”

Ananyanyuka kwenye kiti. Anatoka kwenye chumba cha mahakama.

Jaji anaingia na wote wanasimama. Sasa wote tunakaa.

Kesi inatajwa kwa mara nyingine tena. Washtakiwa wanahamia kizimbani kutoka kwenye mabenchi waliyokalia.

Mawakili wa Serikali wakiongozwa na Robert Kidando wanajitambulisha tena kwa mara nyingine. Wamejipanga kama walivyokuwa wamejipanga asubuhi.

Kwa upande wa utetezi Wakili Peter Kibatala anatambulisha mawakili wenzake. Sasa hivi ameongezeka Wakili John Malya ambaye asubuhi hakuwapo mahakamani.

Anatambulishwa pia Wakili Pacience Mlowe. Sasa jumla ya mawakili wa utetezi ni 16 baada ya kuongezeka Mallya na Mlowe.

Wakili wa Serikali anaanza kuzungumza.

Anasema: Mheshimiwa Jaji, katika shauri hili dogo tunategemea kuwa na mashaidi saba na leo tuna shahidi mmoja.

Jaji anamtaka shahidi arudie kujitambulisha. Anasema: “Naitwa ACP Ramadhani Kingai”

JAJI: Utetezi kabla hatujaendelea. Palikuwa na concern kuhusu chakula cha washitakiwa. Je, leo wamekula?

WAKILI KIBATALA: Kwa leo tutumie diplomasia tuendelee ingawa hawajapewa achakula. Magereza wamesema kuna hatua wanachukua. Kesho wanaweza kuwa tayari.

JAJI: Shaidi Kingai we ni Muislamu?

SHAHIDI: Ndiyo

JAJI: Thibitisha

SHAHIDI: Wallah, Wabillah nathibitisha

Wakili wa Serikali: Kingai umesema wewe ni ACP?

WAKILI WA SERIKALI: Unafanya Shughuli gani

SHAHIDI: Ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni

WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya kuwa Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, katika shughuli zako ulikuwa kituo gani?

SHAIDI: Nilikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha

JAJI: Sijasikia Vizuri

Kinagai anarudia tena

Wakili wa Serikali: Ulifanya kwa muda gani?

SHAIDI: Nitalifanya kwa mwaka mmoja na miezi minne

WAKILI WA SERIKALI: Elezea majukumu yako ulipokuwa Mkoa wa Arusha

SHAHIDI: Nilikuwa napeleleza makosa ya jinai. Nasimamia nidhamu ya askari, ukamataji wa watuhumiwa na kufanya mahojiano na matuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea tarehe 5 mwezi wa nane mwaka 2020 ukiwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha ulikuwa una shughuli gani.

SHAIDI: Tarehe tano mwezi wa nane mwaka 2000 nilikuwa katika mji wa Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Ulienda akufanya nini?

SHAHIDI: Nilienda mahususi kwa nia ya ukamataji wa watuhumiwa wa kesi ya kula njama ya kutenda vitendo vya kigaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Hao watu ulienda kwa kuwakamata ni akina nani?

SHAIDI: Adsama Kasekwa, maarufu kama Adamoo, Mohammed Ling’wemya na Mose Likenja … Kwa taarifa tulizokuwa tumezipata, tulienda kwa dhumuni la kuwakamata

WAKILI WA SERIKALI: Elezea ulivyowakamata.

SHAIDI: Siku ya tarehe sita mwezi wa nane mwaka 2020 tulipata taarifa kupitia kwa wasiri wetu kuwa watuhumiwa tunaowafuatilia wapo eneo la RAO madukani.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya taarifa hiyo ulichukua hatua gani?

SHAIDI: Nikiwa na timu yangu ACP Jumanne, OC CID Arumeru, Detective Goodluck CID Arusha, Detective Constable Azizi tulienda kuwafuatilia watuhumiwa ambao tuliwakamata.

WAKILI WA SERIKALI: ikawaje?

SHAHIDI: Tulifanikiwa kuwakamata wawili kati ya watatu tuliokuwa tunawafuatilia. Tulimkamata Mohammed A Ling’wenya na Adam Kasekwa.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuwakamata nini kilifuata?

SHAIDI: Tulimuamuru ACP Jumanne aawapekue Maungoni, ili kujiridhisha.

SHAHIDI: Tulijiridhisha kuna usalama katika kuwapeleka sehemu tulizokuwa tunawapeleka.

JAJI: Maungoni unamaanisha nini?

SHAHIDI: Search in person.

SHAHIDI: Adama alikutwa na bastola aina ya Rivern A53 5340 ikiwa na risasi 3. Pia alikuwa akiwa na kete 58 za madawa ya kulevya. Baada ya uthibitisho kuwa yalikuwa ni Heroine. Mohamed Ling’wenya alikutwa na kete 25 za madawa ya kulevya baada ya kuthibitisha kuwa nayo ni Heroine … Baada ya upekuzi huo, iliandaliwa hati ya upekuzi … Sorry upekuzi huo ulifanyika mbele ya mashaidi. Mmoja anaitwa Anita na mmoja anaitwa Esther.

JAJI: Esther na nani?

Kingai anarudia.

SHAHIDI: Baada ya upekuzi huo iliandaliwa hati ya uchukuaji wa vitu kutoka kwa watuhukiwa.

SHAHIDI: Hati hiyo baada ya kujazwa ilisainiwa na watuhumiwa wenyewe pamoja na mashaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kujaza hati hiyo ni hatua gani ilifuata?

SHAHIDI: Niliwachukua watuhumiwa kuelekea Central Moshi. Na kuwapeleka mashaidi walioshuhudia upekuzi kwa ajili ya kuandika maelezo yao.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa uliwapeleka pale watuhumiwa na mashaidi kuwachukua maelezo ni hatua gani ilifuata?

SHAHIDI: Tuliwachukua na gari kuwapeleka Central Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Hilo ushalisema.

JAJI: Detective Coplo Francis mlimuacha anafanya nini?

SHAHIDI: Alikuwa anachukua maelezo ya mashaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumwacha Coplo Francis we ulifanya nini?

SHAHIDI: Tulienda tena pale RAO Madukani kumtafuta Moses Lijenje. Watuhumiwa walisema Moses alikuwepo kwenye timu yao lakini muda ule hawakuwa naye. Na walitoa uwezekano wa maeneo ambayo tunaweza kumpata.

SHAHIDI: Kwa hiyo tulitembea maeneo mbalimbali ya Moshi kumtafuta huyu Lijenje … Kwa ushirikiano wa watuhumiwa wetu tulipita maeneo mbalimbali ya Msoshi na kule Boma Ng’ombe kumtafuta Moses Lijenje mpaka usiku bila mafanikio.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kutofanikiwa kumpata Moses Lijenje hadi usiku ulichukua hatua gani?

SHAHIDI: Niliwachukua kuwarudisha watuhumiwa mpaka Moshi muda ule usiku kwa kuwa walikuwa wamechoka na Kusinzia.

WAKILI WA SERIKALI: Muda gani?

SHAIDI: zaidi ya saa nne usiku.

JAJI: Endelea

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kufika Polisi uliwapeleka wapi watuhumiwa?

SHAIDI: Niliwaweka mahabusu.

WAKILI WA SERIKALI: Kule wakati mnawakamata hawa watuhumiwa wawili, ukamataji huu ulikuwa kuwaje?

SHAHIDI: Ukamataji haukuwa na shida. Tulitegema kwa kuwa watuhumiwa ni askari pengine wangeleta shida lakini hapakuwa na shida.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea tarehe tano?

SHAIDI: Tuliendelea na nia kutaka kumakamata Moses Lijenje, mpaka asubuhi yake tulikuwa na nia hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Asubuhi muda gani alianza na wapi?

SHAHIDI: Tulianzia stendi ya mabasi, Manispaa ya Moshi asubuhi ya tarehe sita mwezi wa nane mwaka 2020 tukifikiri anaweza kusafiri.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa na nani?

SHAHIDI: Na Timu yangu ASP Jumanne, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck, Detective Constable Azizi tukiwa na watuhumiwa kwa ajili ya utambuzi wa Moses Lijenje.

WAKILI WA SERIKALI: Ufuatiliaji huu uliendelea kwa muda gani?

SHAHIDI: Mchana hadi usiku kwa maeneo mbalimbali kama nilivyosema. Lakini hatukufanikiwa kumpata Moses Lijenje … Tulipofika majira ya saa 2 usiku niliwasiliana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Kamishina Boaz kuhusiana na uwa kumpata Lijenje.

SHAHIDI: Akaelekeza tuondoke Moshi kuelekea Dar es Salaam ambako kesi imefunguliwa lakini pia kwa hatua zingime za kiupelelezi

WAKILI WA SERIKALI: Elezea uliondoka Moshi tarehe ngapi na saa ngapi.

SHAHIDI: Tuliondokoa Moshi Saa 2 usiku nikiwa na timu yangu

SHAHIDI: Tulipofika Njia Panda ya Himo gari yetu aina ya LX Land Cruiser ilizima tamaa ikabidi tufanye mawasiliano kwa ajili ya kupata gari nyingine … Baada ya mawasiliano tulipata gari nyingine. Tukawasiliana na RPC ikabidi Detective Coplo Azizi Abaki pale stunaendelea na Safari

WAKILI WA SERIKALI: Dar es Salaam mlifika majira gani?

SHAHIDI: Tarehe 07 saa 11 alfajiri … Tulienda moja kwa moja hadi Central Police Dar es Salaam … Na muda mfupi tuliwaweka mahabusu kwa ajili ya kupiga mswaki na kunawa.

WAKILI WA SERIKALI: Baadaye nini kiliendelea?

SHAHIDI: Majira kati ya saa moja na nusu na saa tatu siku hiyo hiyo tarehe saba mwezi wa nane nilimhoji mtuhumiwa Adam Kasekwa kwa njia ya onyo.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea sasa shughuli hiyo ulifanyika wapi?

SHAHIDI: Central Police Dar es Salaam. Kabla ya kuandika maelezo nilimfahamisha haki zake.

WAKILI WA SERIKALI: Tuambie hizo haki unazosema ulimfahamisha.

SHAHIDI: Nilijitambulisha kwake, nilimtaarifu kosa.

WAKILI WA SERIKALI: Kosa gani..?

SHAHIDI: Kula njama ya kufanya vitendo vya kigaidi. Nilimoinya ni kwa hiari kutoa maelezo yake kwangu na kwamba chochote atakachonieleza kinaweza kutumika mahakamani kama ushahidi dhidi yake.

SHAHIDI: Haki zingine nilikwambia iwapo anaweza kutoa peke yake mwenyewe au kumsaidia kupata ndugu, jama au rafiki au mwanasheria.

WAKILI WA SERIKALI: Yeye alijibu nini?

SHAHIDI: Alisema yupo tayari kutoa maelezo yake akiwa peke yake. Na haya yote nilikuwa nayaandika … Akatoa maelezo yake na kuweka sahihi yake.

WAKILI WA SERIKALI: Aliwela sahihi kwa kutumia njia gani?

SHAHIDI: Aliweka sahihi kwa kutumia kalamu ya wino na dole gumba.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipomuangalia alikuwa katika hali gani?

SHAHIDI: Alikuwa katika hali nzuri. Niliandika maelezo yake kama ambavyo alikuwa anayatoa.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumuandika maelezo ilikuwaje?

SHAHIDI: Nilimpatia Adamu kwa ajili ya kuyaona ili aone kama kuna nilicho ongeza au kupungiza.

WAKILI WA SERIKALI: Yeye alikwambia nini?

SHAHIDI: Aliniambia hakuna kilichopungua. Yapo kama alivyo yatoa yeye. Maneno ya kwamba hakuna kilicho ongeza wala kupungua aliyathibitisha kwa kaandika kwa mkono wake, na akasaini kwa kalamu ya wino na baadaye akaweka dole gumba.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya yeye kuandika maelezo yake mama alivyoeleza…

Wakili Kibatala anamkatiza Wakili wa Serikali.

WAKILI KIBATALA: Objection!

JAJI: Wakiliwa Serikali..

WAKILI KIBATALA: Sawa kama ana- rephrase.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuandika kuthibitisha maelezo yake wewe ulifanya nini?

SHAHIDI: Niliandika maelezo hayo kuashiria kumaliza kuandika statement.
WAKILI WA SERIKALI: Uliandika maelezo hayo muda gani?

SHAHIDI: Saa moja na nusu mpaka saa tatu na nusu.

WAKILI WA SERIKALI: Ukiyaona maelezo hayo unaweza kuyatambua?

SHAHIDI: Naweza kuyatambua.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa sababu gani?

SHAHIDI: Niliandika kwa mwandiko wangu mwenyewe, saini yangu pia na hata saini ya mtuhumiwa naikumbuka.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa jaji naomba kumkabidhi kama anaitambua.

SHAHIDI: Mheshimiwa nayatambua kutokana na mwandiko wangu, sahihi ni ya kwangu. Naukumbuka mwandiko wa mtuhumiwa na pia nakumbuka sahihi ya mtuhumiwa pia.

WAKILI WA SERIKALI: Maelezo hayo tukisema tuyatumie kama sehemu ya ushaidi wako tutakuwa tunakosea?

SHAHIDI: Ndiyo mheshimiwa naomba tuyatumie kama sehemu ya ushaidi.

JAJI: Kwa upande wa utetezi kuna objection..?

WAKILI KIBATALA: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

JAJI: Maelezo yanapolekewa.

WAKILI WA SERIKALI: (Anasimama) kisha anasema: “Kingai elezea ni ukurasa wa ngapi ulimfahamisha Adam Kasekwa haki zake.”

WAKILI KIBATALA: Mheshimiwa Jaji anachofanya Wakili wa Serikali si sahihi. Maelezo yaliyopokelewa ni ID anamuelekeza shaidi kujadili content (yaliyomo).

JAJI: Fafanua…

WAKILI KIBATALA: Hiyo Hati ya Maelezo imepokelewa tu Kama kielelezo. Anachofanya ni kujadili content ya kilichopo kwenye maelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Hofu tu Mheshimiwa Jaji. Mie sifanyi anachosema.

JAJI: Naomba muwe mnavumiliana Mahakamani. Mniachie Jukumu la kuamua tu.

JAJI: Wakili Kibatala..

WAKILI KIBATALA: Anachofanya Wakili wa Serikali anataka kuingiza maelezo ya ziada kwa mlango wa nyuma. Yeye alishakuwa na muda wa kutosha na kueleza.

Wakili wa Serikali unachotaka kuuliza unakusudia nini?

WAKILI WA SERIKALI: Sifanyi lolote nataka nitumie alichosema shahidi.

Jaji anakubaliana na Kibatala. Anamwambia Wakili wa Serikali “ondoa hilo swali lako. Tumepokea for Identification hatuna haja ya kujua kilichopo ndani.

WAKILI WA SERIKALI: Sawa Mheshimiwa. Shaidi wakati anachukua maelezo ya mtuhumiwa Adam Mazingira yalikuwaje..?

SHAHDI: Palikuwa na mazingira mazuri na tulivu na alikuwa vizuri kiafya.

WAKILI WA SERIKALI: Ulimkamatia Adam Moshi, elezea kwanini ulikuja kumchukua maelezo Dar es Salaam.

SHAHIDI: Kwanza kesi ilifunguliwa Dar es Salaam … Pia palikuwa ni sehemu sahihi. Na Dar es salaam palikuwa na hatua zingine za kiupelelezi

WAKILI WA SERIKALI: Hatua gani za kiupelelezi zilizokuwa zikiendelea kule Moshi?

SHAHIDI: Kule Moshi paliendelea na hatua za kumtafuta Moses Lijenje. Hasa kwa msaada wa watuhumiwa tuliokuwa tumewakamata.

WAKILI WA SERIKALI: Mshitakiwa Wa pili Adam analalamila kuwa alikuwa anateswa kabla na wakati anachukuliwa maelezo yake, aliteswa na wewe pamoja na maaskari ambao uliwalekeza wewe.

SHAHIDI: Si kweli, hatukumtesa kwa sababu hatukuwa na sababu. Kwa sababu hapakuwa hata na resistance wakati wa ukamataji wao.

WAKILI WA SERIKALI: Ennheeeee!!! Ni eneo gani ulichukulia maelezo yake ya onyo?

SHAHIDI: Kwenye Ofisi ya RCO Ilala.

JAJI: Umesema ukiwa kwenye kituo kipi?

SHAIDI: Central Station, ofisi ya RCO Ilala.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa kwa sababu kuna malalamiko ya kuteswa ili kuchukuliwa maelezo, hebu tueleze palikuwa na mazingira gani wakati wa ukamataji.

SHAHIDI: Kwanza hapakuwa na resistance wakati wa ukamataji. Hata wakati tunasubiri nao hawakutuletea shida ya aina yoyote ile. Lakini hata wakati naandika maelezo hapakuwa na shida ya aina yoyote au kuonekana akiwa na shida ya aina yoyote. Aliyatoa maelezo akiwa free na kwa kupenda mwenyewe.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa sababu anasema wakati anateswa palikuwa na askari wengine uliowaelekeza,Je akina nani ulikuwa nao.
SHAHIDI: Hapakuwa na mtu. Tulikuwa mimi na yeye.

WAKILI WA SERIKALI: Kule Moshi wakati unawakamata palikuwa ni eneo gani?

SHAIDI: Iilikuwa ni eneo la kibiashara. Kuna maduka na migahawa. Sina hakika maduka ya jumla. Grocery ya kuuza pombe na kuna vibanda umiza, moja ya huko kibanda cha supu ndipo tulipomkuta.

SHAHIDI: (Eneo) lipo bize na kuna watu wengi.

WAKILI WA SERIKALI: Yale maeneo mengine mliyopita Moshi na Boma Ng’ombe na Machame kumtafuta Moses yenyewe yalikuwaje?

SHAHIDI: Kote tulikopita ni maeneo waliyokuwa wanapita kula au kunywa. Arusha Sakina tuliambiwa kuwa ana ndugu yake, lakini hatukufanikiwa Kumpata.

WAKILI WA SERIKALI: Vipi pale mlipokuwa gari yenu umepata hitilafu, eneo likoje?

SHAHIDI: Eneo ambalo lipo bize na watu wengi. Kibiashara na wengine wanageuzia magari

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa jaji ni hayo tu.

Kisha Wakili wa Serikali anakaa chini huku shahidi akiwa bado amesimama kizimbani.

Jaji anaita mawakili wa utetezi kumhoji shahidi.

WAKILI PETER KIBALATA: Utakasirika nikiluita ni kaka yangu?

SHAHDI: Ni sahihi sababu nimekuzidi umri.

WAKILI KIBATALA: Bila shaka hutakasirika nikiwatetea wateja wangu.

Halafu Kibatala anamkabidhi shahidi (ni polisi) Kitabu cha PGO.

Anaulizwa hicho ndicho kitabu chenyewe cha kazi za polisi? Shahidi anasema ndiyo chennyewe.

Jaji anamsisitiza shahidi kukiangalia vizuri kitabu hicho na ajitidhishe.

KIBATALA: Ni chenyewe?

SHAHIDI: Ndiyo yenyewe.

KIBATALA: (Anamuonyesha shahidi ukurasa wa kwanza kwamba IGP wa wakati huo Saidi Mwema alisema kila mshiriki akisome).

Kibatala anaendelea kumweleza shahidi kwamba mshiriki ni polisi na awe na maadili na ajue miiko ya Polisi.

Shahidi anaitika kwa kichwa.

Jaji anasema anamwambia asiitike kwa kichwa

KIBATALA: Kila member wa Polisi muda wote anatakiwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na Watu wa Zanzibar.

SHAHIDI: Ni sahihi

KIBATALA: Sasa tuanze vizuri

KIBATALA: Unapomkamata mtuhumiwa unatakiwa pale pale umwambie kuwa wewe ni nani na unamkamata kwa makosa gani. Je ni sahihi?

KIBATALA: Je ni sahihi kwa mujibu wa PGO unatakiwa kuandika katika Notebook, na kwa mujibu wa NoteBook ni kifaa kazi chako wewe?

SHAHIDI: Ni sahihi

KIBATALA: Ni sahihi shahidi kufunga safari kutoka Arusha mpaka Moshi mkoa mwingine ukiwa unajua mtuhumiwa Adamoo anatuhuma za ugaidi?

SHAHIDI: Nilikuwa nafahamu

KIBATALA: Na Mawakili wa Serikali wameku Brief kuwa ushahidi wa sasa ni tofauti na ushaidi wa asubuhi. Hilo unafahamu?

SHAHIDI: Ndiyo nafahamu.

KIBATALA: Unafahamu bila shaka Mahakama haikuwepo wakati hayo yanatokea. Mahakama inatakiwa kuunganisha Vidot vidogo vidogo kujua nini kilitokea?

SHAHIDI: Sijalewa.

KIBATALA: Unafahamu ushahidi mdogo mdogo ndio unaunda ufahamu kwa Mahakama kufanya maamuzi?

JAJI: Adamo ni mshitakiwa wa kwanza au wa pili?

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kulipokuwa eneo la RAO huko Moshi kama ulimwambia Mheshimiwa Jaji ulifuatisha tataribu kwa mujibu wa PGO.

SHAHIDI: PGO gani inasema hivyo?

KIBATALA: Huko tushatoka jibu ninalokuuliza.

SHAHIDI: Hapo hakuniongoza.

KIBATALA: Ulizungumzia jibu la Adamoo kuwa uliliweka kwenye Notebook ambacho ni kifaa chako cha kazi?
SHAHIDI: Hilo silikulisema.

KIBATALA: Infact hiyo Notebook hukuitoa mahakamani, ambacho tumekubaliana ni kifaa kazi.

SHAHIDI: Sikuitoa.

KIBATALA: Tutoke Rau Madukani, Twende Police Station Moshi. Nilikusikia vizuri kuna wadada mliwachukulia maelezo pale Moshi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Tukumbushe kuwa Investigation file lipo Dar es Salaam.

SHAHIDI: Ndiyo ilikuwa Dar es Salaam.

KIBATALA: Jaji akiandika sema kwamba hukusema kwanini ulichukua maelezo ya wale wadada pale Moshi wakati Investigation file lipo Dar es Salaam.

SHAIDI: ….Sikuulizwa hilo.

KIBATALA: Jibu ninachokuuliza.

KIBATALA: Kwa ushahidi wako kuna upekuzi wa Adamoo ulifanyika mbele ya mashahidi pale RAO Moshi.

Jaji anaomba watu wanyamaze kupisha hadhana kidogo.

KIBATALA: Kuna mashahidi wawili walihojiwa Moshi wakati IR 5 imefunguliwa Dar es Salaam. Sasa mweleze Jaji kuwa kama ulifafanua kuwa kuna mazingira yoyote yaliyosababisha watoe maelezo Moshi na si Dar es Salaam.

SHAIDI: Nilieleza mazingira hayakuwa rndiyo maana tukaenda kurekodia pale Polisi.

KIBATALA: Maelezo kuwa shahidi anaweza kuhojiwa popote kwa mujibu wa kiapo chako hapa Mahakamani ulitoa hapa leo.

SHAHIDI: Hiyo sikusema.

KIBATALA: Ndicho nilichokuwa nataka. Muda mwingine pay attention.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni kifungu gani cha PGO kuwa IR 5 ikifunguliwa Dar es Salaam mshitakiwa anatakiwa asafirishwe kutoka Moshi hadi Dar es Salaam.

SHAHIDI: Hiyo ni Manifesto ya CPA. Sikumbuki kifungu gani.

KIBATALA: Ngoja nikupe CPA unitajie ni kifungu gani.

Shahidi anatikisa kichwa halafu Kibatala anamuuliza: “Hutaki tena CPA?”
SHAHIDI: Nisisumbue Mahakama. Nilisema mazingira gani yaliyosababisha niwalete Dar es Salaam.

KIBATALA: Tuambie kifungu cha sheriua chochote.

SHAHIDI: Sikumbuki kifungu cha sheria.

KIBATALA: Pale Moshi palikuwa na facility zote za kukuweza kuwahoji watuhumiwa pale Moshi. Kweli si kweli?

SHAHIDI: Upelelezi ulikuwa bado unaendelea na jesi Ilikuwa Dar es Salaam.

KIBATALA: Umenisaidia ila bado hujajibu swali la msingi.

KIBATALA: Jibu kuwa Moshi palikuwa na facility zote za kukuwezesha kumuhoji Adam kwa mujibu wa sheria.

SHAHIDI: Ndiyo zilikwepo.

KIBATALA: Ulisema mlitoka Moshi saa ngapi vile?

SHAHIDI: Saa mbili.

KIBATALA: Afisa wa Polisi Gooldluck alikwepo?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Alikuwa na silaha yake wakati mnatoka Moshi kuja Dar es Salaam?

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji nitakuwa nimesahau kila nilitaka timu yangu yote nilikuwa nayo.

KIBATALA: Let’s assume kuwa maelezo kuwa Adama alichukuliwa na wewe ulikuwa na Goodluck kwenye eneo lolote la Central kwa ku- exclude?

SHAHIDI: Alikuwepo wakati anachukua maelezo.

KIBATALA: Wakati wewe unaongea mwanzo hukumtoa?

SHAHIDI: Sikumtoa.

KIBATALA: Iambie Mahakama, na nakukumbusha upo chini ya kiapo. Tangu umemkamata Adamoo ni saa ngapi umemwambia Jaji kuwa ni wakati gani umemruhusu anywe maji na chakula?

SHAHIDI: La chakula sikulizungumzia.

KIBATALA: Kwa makadirio tangu umakamte Adamoo tangu tarehe tano mpaka unamuhoji tarehe saba ilikuwa ni masaa mangapi?

SHAHIDI: Mpaka nipige hesabu.

KIBATALA: Lakini utakumbuka kuwa zinapita siku mbili?

SHAHIDI: Ndiyo zinapita.

KIBATALA: Ulimhoji mtuhumiwa. Unafahamau au hufahamu kuwa Adam Kasekwa Komandoo wa zamani kuwa alikuwa na ugongwa wa akili akiwa Jeshini TBD Traumatic Battle Disorder?

SHAHIDI: Aliniambia.

KIBATALA: Hapa uliongea?

SHAHIDI: Sijaongea.

KIBATALA: Unafahamu kuwa ugonjwa wa Battle Fatic Mental Disorder ni ugonjwa wa kawaida kwenye majeshi?

SHAHIDI: Hayo mambo ya kitaalamu?

KIBATALA: We si umesema ulimhoji akiwa mzima wa afya?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Je unajua alipata ugonjwa huo akiwa anatumika nchi hii?

SHAHIDI: Sikufahamu.

KIBATALA: Afya mliyokuwa anaongea na Wakili Msomi haikuwa pamoja na afya ya kichwa?

SHAHIDI: Nilikuwa nazungumzia afya ya mwonekano.

KIBATALA: Sasa hiyo afya ya Jumla inajumuisha afya ya kichwa?

SHAHIDI: Ndiyo. Pamoja na kichwa.

KIBATALA: Unafahamu kuwa watu wanaoumwa Battle Fatic au wewe umeita stress kuwa wanatakiwa kubebwa kama yai?

SHAHIDI: Hayo sifahamu.

KIBATALA: Umefanya kazi ya upelelezi kwa muda gani?

SHAHIDI: Miaka 20.

KIBATALA: Shaidi unafahamu mtuhumiwa namba 2 ni Komandoo?

SHAHIDI: Ndiyo ninafahamu.

KIBATALA: Mshitakiwa unamwona hapa na kila akiletwa amefungwa pingu, na najua na wewe unafahamu kwa kuwa unakuja Mahakamani hapa kuimarisha ulinzi.

SHAHIDI: Nakujaga ila naakaga mbali.

KIBATALA: Sijakuuliza unaishiaga wapi. Sema ndiyo nakujaga wakati wa kesi hii au hapana.

Shahidi anasema “Ndiyo. Nakujaga wakati wa kesi.”

KIBATALA: Mpaka mnakuja naye Dar es Salaam, mtuhumiwa alikuwa anamfahamu kuwa siku ya mwisho atashitakiwa kwa ugaidi?

SHAHIDI: Ndiyo. Alikuwa anafahamu.

KIBATALA: Muda wote mlikuwa manzunguka na watuhumiwa mkiwa mnamtafuta Moses Lijenje mkiwa na silaha?

SHAHIDI: Ndiyo. Tulikuwa na SMG mbili na pistol.

KIBATALA: Ulimwambia Jaji hapa kuwa kuna mazingira ya upekee yaliyosabaisha kuzunguka na watuhumiwa kwenye gari yenu?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Mwambie Jaji kuwa ni kwanini taarifa walizowaambia watuhumiwa msiende wenyewe kumtafuta mtuhumiwa wa tatu mpaka mzunguke nao kwenye magari … nini kiliwazuia kwenda wenyewe?

SHAHIDI: Ishu yenyewe ni serious.

KIBATALA: Asingekwepo Adam Kasekwa mngetumia njia zipi kumpata mtuhumiwa wa tatu?

SHAHIDI: Tungetumia njia zozote.

KIBATALA: Safi. Ndicho nilichokuwa nahitaji.

KIBATALA: Ikumbushe Mahakama kuwa mlipotoka Moshi saa mbili usiku mlifika Dar es Salaam saa ngapi vile?

SHAHIDI: Saa 11 alfajiri.

KIBATALA: Kwa hivyo mlimuhoji kuchukua maelezo baada ya masaa mawili tu?

SHAHIDI: Baada ya masaa mawili ndiyo.

KIBATALA: Na umesema kuwa alikuwa na afya nzuri?

SHAHIDI: (Anakaa kimyaaaaaaa).

KIBATALA: Ulipomkamata Adamoo na bunduki Moshi kule Rao, ni saa ngapi umezungumzia kumuonya kisheria kuhusiana kupatikana kupatikana na silaha kinyume cha sheria?

SHAHIDI: Onyo kuhusiana na bunduki sikutoa.

JAJI: Hebu rudia tena.

SHAHIDI: Sikumuonya specifically kuhusiana na kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.

KIBATALA: Mwambie pia mheshimiwa Jaji kama ulimuonya kuhusiana na madawa ya kulevya.

SHAHIDI: Mi binafsi sikumuonya kisheria.

KIBATALA: Unakubalaina na mimi bunduki na madawa ya kulevya na kula njama ilikuwa ni ukamataji mmoja?

SHAHIDI: Ndiyo. Ukamataji mmoja.

KIBATALA: Unakubaliana nami bunduki na madawa ya kulevya ni makosa makubwa sana hata yanaweza kusababisha mtu afungwe maisha?

SHAHIDI: Inategemea iasi cha madawa.

KIBATALA: Vipi kuhusu kete 58?

SHAHIDI: Sijuo uzito wake.

KIBATALA: Ulitaja maungo ya Adamoo ulikokuta kete za madawa ya kulevya.

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Ulisema maungo gani kuwa ulikuta bastola?

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Umesema hapa yale madawa ya kulevya ulithibitisha kutoka kwa mkemia. Je, unafahamu status ya kesi ya madawa ya kulevya status yake ikoje?

SHAHIDI: Siwezi kulizungumzia.

KIBATALA: Hutaki au hujui? Kama hutaki nitamwomba Jaji Mahakama ikulazimishe.

SHAHIDI: Status ya kesi ya madawa sifahamu.

KIBATALA: Unakifahamu Kituo cha Polisi Mbweni.?

SHAHIDI: Nakifahamu.

KIBATALA: Mara ya mwisho ni lini kufika Mbweni?

SHAHIDI: Hata juzi nilienda.

KIBATALA: Je Adamoo katika kukamatwa kwake alifika Mbweni?

SHAHIDI: Alifika.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuwa Adamoo alifika Mbweni Polisi kufanya nini?

SHAHIDI: Hilo sikusema.

KIBATALA: Unafahamu kuwa kutoka … mpaka ufike Ufike Mbweni kuna vituo vingapi vya polisi. Ni vingi zaidi ya sita mpaka ufike Mbweni ukianzia Selander Bridge Polisi Station.

SHAHIDI: Ndiyo. Vipo vingi.

KIBATALA: Goodluck uliyekuwa naye alifika pia Mbweni Polisi?

SHAHIDI: Ndiyo. Alifika.

KIBATALA: Afisa wa JWTZ Komandoo anaitwa Chuma alifika pia Mbweni?

SHAHIDI: Simkumbuki.

KIBATALA: Je, ni maafisa wangapi wa JWTZ makomandoo waliofika kituo cha Polisi Mbweni?

SHAHIDI: Sikumbuki.

KIBATALA: Hukumbuki au hujui?

SHAHIDI: Sina knowledge hiyo.

KIBATALA: Hujui?

SHAHIDI: Sikumbuki.

KIBATALA: Tuachane na hilo …

Kibatala anamfuata hahidi na kumkazia macho huku akimuuliza., Je, unafahamu kuwa mshitakiwa Adamoo anashitakiwa makosa matano na moja la kula njama za ugaidi?

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji mimi siye ninayeandaa mashtaka. Wanaoandaa ni Ofisi ya Mwendesha Mashitaka.

KIBATALA: Kwa statement yako kuwa wanashitakiwa kwa maelezo uliyowaonya..?
WAKILI WA SERIKALI: OBJECTION. Mheshimiwa Jaji Wakili anatoa speech sana.

JAJI: Jamani tumpatie shahidi hata dakika mbili jamani. Pale kizimbani siyo mchezo.

SHAHIDI: Kweli naomba niende haja kidogo.

JAJI: Uende lakini urudi.

JAJI: Mawakili mnaweza kunishauri kama tunaweza kubreak tuendelee kesho. Upande wa mashitaka mnasemaje?

Shaidi amerudi

KIBATALA: Mwambie Jaji kuwa Adamoo alishawahi kwa sababu yoyote ile kwenda Kituo cha Polisi Tazara.

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Gari mliyoitumia kutoka Himo kuja Dar es Salaam unakumbuka namba zake za usajili?

SHAHIDI: Sikumbuki.

KIBATALA: (Anaomba Wakili Mtobesya aendelee kumhoji shahidi).

Anaingia wakili Mtobesya.

MTOBESYA: Shaidi ieleze Mahakama kama unafahamu document ya Police inaitwa Detection Register.

SHAHIDI: Naifahamu.

MTOBESYA: Mweleze Jaji hiyo ni kitu gani.

SHAHIDI: Ni usajili wa mahabusu wanapoinga na wanapotoka.

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi kuwa hujatoa Detention Register ya Moshi, Dar Central wala Mbweni ulikosema mshitakiwa alienda?

SHAHIDI: Mimi sikutoa watatoa wenzangu.

MTOBESYA: Siyo swali langu. Swali ulitoka hapa mahakamani au hukutoa?

SHAHIDI: Sikutoa.

MTOBESYA: Nimesikia unasema ulimuhoji na mtuhumiwa akathibitisha maelezo yake

SHAHIDI: Ndiyo.

MTOBESYA: Ni sahihi kuwa uthibitisho wa mtu anayejua kusoma na asiyejua kusoma ni tofauti?

SHAHIDI: Inategemea.

MTOBESYA: Mwambie sasa Jaji inategemea nini?

JAJI: Nahisi shahidi haelewi anachoulizwa. Naona anajibu tofauti. Wakili msaidie ajue uthibitisho ni nini.

MTOBESYA: Kuna aina ngapi za uthibitisho?

SHAHIDI: Usthibitisho wa shahidi na mtuhumiwa.

JAJI: Ngoja. Twende pamoja. Wewe shahidi kuthibitisha ni tendo gani?

SHAHIDI: Kuthibitisha ni kukubali kuwa kitendo fulani kimefanyika.

JAJI: Wakili endelea.

MTOBESYA: Huo uthibitisho unaosema ni wa aina gani unatumika.

SHAHIDI: Kama unamuhoji mtuhumiwa sababu namuhoji chini ya onyo ni lazima urifae sect 53.

MTOBESYA: Wewe kwa zoezi ulilofanya ulitumia kifungu kipi?

SHAHIDI: Kifungu namba 57.

MTOBESYA: Kifungu kidogo cha 57 (3) kuna aina ngapi za uthibitisho?

JAJI: Tumsaidie. Tusimuulize masuala ya kisheria.

MTOBESYA: Mtuhumiwa alikuwa anajua kusoma na kuandika?

SHAHIDI: Alikuwa anajua kusoma na kuandika.

MTOBESYA: Mtu anayejua kusoma na kuandika anathibitisha vipi?

SHAHIDI: Kwa sahihi na dole gumba.

MTOBESYA: Ni sahihi nikisema mtu asiyejua kusoma ndiye yanayoweza kuandika sahihi na kuweka dole gumba?

SHAHIDI: Ile ni kuthibitisha tu. Finger print mtu hawezi kukwepa lakini sahihi mtu anaweza kusema siyo wa kwangu.

MTOBESYA: Isaidie mahakama hicho unachosema wewe ni sheria na kanuni zinavyotaka au ni uzoefu tu?

SHAHIDI: Ni uzoefi siyo sheria.

MTOBESYA: (Anakaa chini).

Jaji anawauliza upande wa mashtaka kama wana lolote. Wakili wa Serikali wanaomba kesi iahirishwe mpaka kesho.

Jaji anauliza upande wa utetezi wanasemaje. Wakili Kibatala anasema hatuna pingamizi. Anasema anafikiri iahirishwe hadi kesho.

Jaji anauliza leo tumefika saa ngapi na washitakiwa wamefika saa ngapi. Wakili wa Serikali anajibu saa tatu.

Jaji anauliza kesho tuanze saa 2 au saa 3? Wakili Kibatala anasema saa 3. Wakishindwa kuwahisha watuhumiwa tufanye saa nne.

Jaji anahairisha kesi hadi kesho saa nne asubuhi kuendelea na shauri dogo.

Jaji amegonga meza na kuondoka.

Like
2