Kesi ya Mbowe: Maswali ya mawakili na majibu ya mashahidi (2)

Anaripoti BJ mwandishi raia kutoka mahakamani. Tunaiweka bila kuihariri ili kutoharibu asili na vionjo vyake. Fuatana naye:

Leo tarehe 17. Septemba 2021, saa 6:00 mchana. Jaji hajaingia mahakamani. Mawakili wa Serikali hawajaingia mahakamani.

Saa 6:02, mawakili wa Serikali hao wanaingia chumba cha mahakama.

Watuhumiwa wanaingia na kukaa kwenye bechi kabla ya kupanda kizimbani.

Jaji naye anaingia mahakamani.

Jaji amekaa.

Kesi inatajwa. Ni kesi namba 16 ya 2021.

Watuhumiwa wanapanda kizimbani.

Wakili wa Serikali Robert Kidan anawatambulisha wenzake.

  1. Robert Kidando
  2. Nassoro Katuga
  3. Ignas Mwanuka
  4. Esther Martin
  5. Tulumanywa Majige na wengine

Wakili Peter Kibatala naye anawatambulisha mawakili wenzake. anawataja kwa majina:

  1. Adv Peter Kibatala
  2. Adv Jeremiah Mtobesya atajoin baadae
  3. Adv Jonathan Mndeme
  4. Adv John Malya
  5. Adv Evaresta Kisanga
  6. Adv Hadija Aron
  7. Adv Maria Mushi
  8. Adv Gaston Garubindi
  9. Adv Seleman Matauka
    10 .Adv Ferdinand Makore
  10. Adv Dickson Matata
  11. Adv Rita Ntagazwa
  12. Adv Alex Masaba
  13. Adv Michael Mwangasa
  14. Adv Deogratius Mahinyila
  15. Adv Nashon Nkungu
  16. Adv Fikiri Gabriel

Jaji ameinama, anaandika kitu. Mahakama iko kimyaaaaa.

Kibatala anasema “mawakili wote hawa wanamwakilisha mshitakiwa wa nne (Mbowe) isipokuwa Nashon Nkungu na Mtobesya watamwaklisha mshtakiwa wa kwanza.

Kibatala: Mshitakiwa wa pili atawakilishwa na John Malya. Mshitakiwa wa tatu atawakilishwa na Dickson Matata.

Wakili wa Serikali: Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa sisi tupo tayari … lakini kwa kuwa tumeona leo mawakili wa utetezi wamejitambulisha kwa kujitofautisha tungependa waielezee mahakama kwanini.

Kibatala: Itakumbukwa kuwa kesi ya msingi kabla ya Trial within Trial Bwana Kingai alitoa kielelezo/nyaraka ambayo yeye Kingai alisema ni Maelezo ya Onyo … Baada ya hapo sisi mawakili wote tuliweza kuapta nafasi ya kuangalia kwa undani.

Kibatala: Tukaona mle ndani mshtakiwa wa pili anaelekea kuwataja wenzake wa kwanza, wa pili na wa nne
… tukagundua kuwa katika mazingira ya kuelekea kutajana katika maelezo, kunatokea conflict of interest.

Kibatala: Kwa kuwa shahidi wa kwanza hayupo leo, kwa sababu haikigundulika mapema, ni maombi yetu kuwa tunaweza kulijibu kwa pamoja.

Kibatala” Kwa Mahakama kuachia mawakili mmoja mmoja iwapo wanakusudia kuiomba Mahakama imuite shahidi wa kwanza katila kesi ndogo katika kesi kubwa kwa sababu kila mshitakiwa anapaswa amhoji shahidi.

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: Tunaomba tujiridhishe katika column yako ya tarehe 15 kama wakili John Malya alikwepo.

Jaji anansoma orodha ya mawakili wote waliotajwa tarehe 15 na kusema John Malya alikuwapo katika orodha na jina lake liko namba 14.

Wakili wa Serikali: Basi tunaomba turidhie kwa maombi aliyoomba Wakili Kibatala. Sisi hatuna pingamizi kwa sababu suala hilo lipo wazi.

Wakili wa Serikali: Isipokuwa sehemu ya kuwawakilisha watuhumiwa tungeomba wakati wote wakiwa mahakamani wawe wanawashirikisha watuhumiwa.

Jaji: Sawa nashukuru.

Wakili Peter Kibatala anaomba ruhusa ya kushauriana na watuhumiwa.

Jaji: Endelea.

Kibatala anaenda kizimbami kuongea na watuhumiwa. Mahakama iko kimya inamsubiri amalize.

Ameongea na mtumiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu na sasa yupo kwa wanne.
Wakili Peter Kibatala anamshukuru Jaji.

Jaji anamwita wakili wa mtuhumiwa wa kwanza, Nashon Nkungu.

Nashon Nkungu: Baada ya jambo hili na baada ya kuzungumza na mteja wangu ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza sioni haja ya kumuita tena ACP Kingai.

Jaji: Nashukuru.

Jaji anamuita Wakili John Malya kwa niaba ya mshitakiwa wa pili.

John Malya: Na mimi pia sioni haja ya kuita tena ACP Kingai.

Jaji: Nashukuru.

Jaji anamuita Wakili Dickson Matata.

Wakili Dickson Matata anasema kwa niaba ya mshitakiwa wa tatu “sina nia ya kumuita shahidi wa kwanza kwa ajili ya kumhoji tena.”

Simu inaita kwa vibration kubwa upande wa mawakili wa Serikali.

Jaji anaonya simu ziwekwe silence zisisumbue Mahakama.

Jaji anamuuliza mshitakiwa wa kwanza kama amekubaliana na uamuzi wa wakili wake kwamba hana nia ya kumuita shahidi wa kwanza.

Mshitakiwa wa kwanza anasema anakubaliana na wakili wake.

Jaji anamuuliza pia mshitakiwa wa pili. Naye anasema anaomba waendelee na shahidi anayefuata.

Jaji: Lakini mshitakiwa wa pili statement ndiye inayemuhusu. Akisema hahitaji kumhoji shahidi anamaanisha nini? Maana yale ya kwanza tunayaondoa.

wakili Kibatala anasimama

Jaji: Kama wanafanya tena mashauriano wafanye, maana mwanzo Kibatala alisema anamwakilisha mshtakiwa wa wanne. Je huyu mshitakiwa wa pili ambaye cross examination imefanyika akisema hana nia ya kumhoji shahidi wa kwanza maana yake tunafuta mahojiano ya kwanza?

Jaji: Niwape muda mzuri mjipange? Hatuna muda wa haraka.

Kibatala: Sioni tatizo.

Jaji: Upande wa Serikali?

Wakili wa Serikali: Sisi tunaona upande wa utetezi wana tatizo kwenye suala la utaratibu. Mwanzo yeye ni wakili wa mshitakiwa wa nne. Ndiye aliyeweka pingamizi na ndiye aliyefanya mahojiano kwa niaba ya mshitakiwa wa nne.

Wakili wa Serikali: Sisi inatuchanganya na mahakama inapata mkwamo. Inawezekana vipi wakili wa mshitakiwa wa nne anakuwa ndiye wa mshitakiwa pili? … Sisi ni mtizamo wetu mshitakiwa wa pili hajaongozwa sawasawa.

Wakili wa Serikali: Sisi tunaona rai ya mahakama wakae watulie tunaona sawasawa … Wao wakae sawasawa na sisi tukae sawasawa.Tukikosea hapa haya yote yatatolewa kwenye records … upo wajibu wa kukaa kujitafakari. Asante sana.

Jaji: Kibatala?

Wakili wa Serikali: Wakili Peter Kibatala kwa bahati mbaya ameongea too dramatic kwa sababu hakuwa kwenye briefing. Laiti angekuwapo asingeongea aliyoyaongea … sisi tuliitwa na mahakama na kuombwa kuisaidia Mahakama kwenda mbele ndiyo maana hata Mahakama ilichelewa kuanza.

Kibatala: Sisi tunasaidia kutibu tatizo la tarehe 15. Mimi ni wakili wa mshitakiwa wa nne kuanzia leo na si kuanzia tarehe 15.

Jaji: Wakili Malya?

Mallya: Haki za mshitakiwa wa pili kumwakilisha imeanza leo. Siku ya tarehe 15 sisi sote tulikuwa tunamwakilisha yeye.

Jaji: Unafikiri ni lazima kumhosji mshitakiwa?

Malya: Sioni ulazima. Labda kama Mahakama itaona ni busara.

Jaji: Nitamuhoji mshitakiwa halafu nitatolea maelekezo.

Jaji: Mashtakiwa wa tatu?

Mshitakiwa wa tatu anasema ameridhia alichosema wakili wake

Jaji: Sawa. Kimsingi hapa tunajihusisha na haki za watu.

Jaji: Na leo mtaona walivyojitambulisha ni tofauti. Kabla ya leo walikuwa wote kwa pamoja walikuwa wanamwakilisha mshitakiwa wa pili … jambo hili linapata tafakuri, kuwa kama Mshitakiwa wa pili amepata nafasi sawasawa ya kumuhojo au kumsikia shahidi wa kwanza … nafikiri siyo busara kukimbia harakaharaka. Nahitaji muda wa kutafakari kwa dakika 15 ofisni kwangu kisha nitarejea.

Jaji: Ninaahirisha kesi kwa dakika 15 kisha nitarejea.

Jaji anasimama na kuondoka.

Mahakama imesharejea. Jaji ameshaingia mahakamani.

Kesi imeanza kusomwa.

Mafaili yanapelekwa kwa Jaji.


Jaji: Kabla hatuja break kwa muda mfupi, niliwahoji washitakiwa lakini sikuwa nimemhoji mshtakiwa wa nne. Namhoji sasa mshtakiwa wa nne … Kauli yako ni nini?

Freeman Mbowe: Tuendelee Mheshimiwa Jaji.

Jaji: Sawa. Sasa na mimi nimepata nafasi ya kutafakari. Nilianza kwenye hoja iliyoibuliwa na Wakili wa Serikali nami aliyeitoa. Kumbukumbu za Mahakama zinaonyesha Kibatala alisema kwa niaba ya mawakili wote na kwa niaba ya washtakiwa wote. Siku hiyo ya 15.09.2020 uwakilishi ilikuwa kwa mawakili wote na kwa niaba ya washitakiwa wote … hivyo utenganisho inaanza leo. Ni maamuzi yangu kuwa mahojiano yaliyofanywa na Wakili Kibatala na Wakili Mtobesya kwa niaba ya mawakili wote na washitakiwa wote … hivyo basi sioni sababu ya kumuita tena shahidi wa kwanza … Hivyo naangiza Kuendelea na swa pili aitwe sasa tuweze kuendelea.

Jaji: Katika mwenendo wa Mahakama nimeondoa kuwa Kibatala ni kwa mshitakiwa wa nne kwa siku ya tarehe hiyo ya 15 Kibatala aliwawakilisha washitakiwa wote kwa niaba ya mawakili wote.

Jaji anamuita shahidi. Shahidi anaingia anajikwaa.

Jaji: Pole sana

Shahidi: Naitwa Inspector Mahita

Jaji: We ni dini gani?

Shahidi: Muislamu

Jaji: Unaweza kuapa.

Shaidi” Wallah Wabillah nathibitisha

Jaji: Upande wa Jamhuri nani utamwongoza shahidi.

Wakili wa Serikali:Shahidi ieleze Mahakama wewe ni Mkazi wa wapi

Shahidi: Mkazi wa Morogoro.

Wakili wa Serikali: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Polisi

Wakili wa Serikali: Kabla ya 2021 leo ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa Msaidizi Ofisi ya Upelelezi Arusha.

Wakili wa Serikali: Umenza lini kazi ya upolisi?

Shahidi: 2010.

Wakili wa Serikali: Katika Idara ya Upelelezi huko Polisi upo tangu lini?

Shahidi: Takribani Miaka minane.

Wakili wa Serikali: Ukiwa Msaidizi wa Upelelezi Majukumu yako ni yapi?

Shahidi: upelelezi wa Makosa ya jinai, ukamataji wa
watuhumiwa, Kusimamia Askari ambao wapo chini yangu, Kupokea Maelekezo ya Viongozi wangu, kufanya upekuzi, kufanya escort za watuhumiwa, lengo la msingi kuzia na kupambana na uhalifu.

Wakili wa Serikali: Nitakuuliza mnamo tareje 4 Mwezi nane 2020 tarehe hiyo ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa kituoni natekeleza Majukumu yangu kama kawaida

Wakili wa Serikali: Kituo gani?

Shahidi: Kituo cha Kati.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama tarehe 04 Mwezi 08 2020 jioni ilikuwaje

Shahidi: Siku hiyo nilipigiwa simu na afande wangu ACP Ra…

Shahidi: Aliniambia niandae Askari wengine. Nikaanda Afande Goodluck na wengine … tuliaanza safari tukiwa Dereva a wake Constable Azizi.

Wakili wa Serikali: Mlisiamam wapi?

Shahidi: Kituo cha Polisi Arumeru, wilaya ya Usa River.

Wakili wa Serikali: Mkaelekea wapi?

Shahidi: Tulikuwa tunaelekea Kilimanjaro tukasimamama kituo cha USA River Wilaya ya Arumeru.

Jaji: Mwanzo umeongea tofauti, umechanganya.

Wakili wa Serikali: Hebu rudia vizuri.

Shahidi: Kituo cha Usa River.

Wakili wa Serikali: Elezea Kituo cha Polisi Usa river kilitokea nini

Shahidi: Tulishika wote tukiwa na Afande Kingai tukapata a briefing ya kazi

Wakili wa Serikali: Briefing uliyopewa ilikuwa inahusu kazi gani?

Shahidi: Briefing niliyopewa ninkwamba kuna kikundi kinapanga kufanya matukio ya kigaidi.

Shahidi: Briefing niliyopewa ninkwamba kuna kikundi kinapanga kufanya matukio ya kigaidi.maeneo mbalimbali Nchini ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza. Na pia Kikundi hicho kilikuwa na nia ya kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Ole Sabaya.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa mkafanyeje?

Shahidi: Tuliambiwa kwakuwa ni mpango twende tukawakamate tuwazuie kabla haija
fanyika.

Wakili wa Serikali: Sasa mkafanyeje?

Shahidi: Kwa kuwa kikundi hicho kilikuwa Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Moshi Mjini kwemda kuwamakata.

Wakili wa Serikali: Na baada ya briefing kitu gani kiliendelea?

Shahidi: Tuliendelea na safari tulifika majira ya saa mbili usiku. Tukaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Mliendelea na upelelezi mpaka muda gani?

Shahidi: Ilipofika majira ya saa sita tukiwa tumewakosa ikabidi tubreak.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa tarehe 05 Mwezi wa 8 2020 mlifanya nini?

Shahidi: Ilikuwa muda wa asubuhi tuliendelea kusubiri taarifa ambazo afande alikuwa akizopokea na olipofika saa sita akaniambia kuwa watuhumiwa tuliokuwa tunawatafuta wameonekana maeneo ya RAU MOSHI.

Wakili wa Serikali: Rau ipo maeneo gani?

Shahidi: Ipo kama unaelekea Keys Hotel.

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama hatua mlizo chukua ni zipi?

Shahidi: Kwanza tuliuliza afande hao tunaoenda kuwakamata mwonekano wao ukoje. Afande akasema mmoja alikuwa amevaa shati, mmoja alikuwa mevaa kama kitenge na mtuhumiwa wa tatu alikuwa amevaa jezi ya mpira.

Wakili wa Serikali: Watu mliotakiwa kuwakamata ni wangapi?

Shahidi: Watatu kwa mujibu wa afande.

Wakili wa Serikali: Na baada ya hapo..?

Shahidi: Tulifika maeneo ambayo walikwepo tukiwa na gari yetu yenye tinted, tuka Drop Section ya kwanza ambayo alioongoza Afande Kingai. Section ya pili nili Drop mimi na Afande Francis na gari.

Shahidi: Timu ya kwanza ilikuwa inaelekea kwa watuhumiwa. Watuhumiwa walikuwa wameiona, watuhumiwa wawili walianza kutoka wakielekea nilipo mimi.

Wakili wa Serikali: Eleza uliwatambuaje?

Shahidi: Section ya kwanza ya Afande Kingai ilivyotoka iliwafanya watake kukimbia, ilibidi kuwasimamisha kutaka kujiridhisha.

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama kwa namna gani uliwasimamisha.

Shahidi: Nilipowasimamisha kwa sauti kali “Simama hapo chini ya ulinzi”

Wakili wa Serikali: Baada ya response yako hiyo walifanya nini?

Shahidi: Walisimama. Wakaamriwa kuweka mikono juu. Wakatii.

Wakili wa Serikali: Kitu gani kilifuata?

Shahidi: Nilijitambulisha naitwa Inspector Mahita natokea Central Arusha nafanya kazi kwenye Kikosi Maalumu.

Wakili wa Serikali: Baada ya kuwatambulisha?

Shahidi: Niliwaonya wakiwa wawili kuwa wanatuhumiwa kula njama za kutenda matendo ya ugaidi

Wakili wa Serikali: Wenzenu wakina Kingai wakati huo walikuwa wapi?

Shahidi: Walikuwa wanakuja,Sababu walikuwa umbali mrefu. Kingai akatoa order kwa Jumanne wapekuliwe

Wakili wa Serikali: Shahidi sasa ieleze Mahakama Jumanne alitekeleza vipi maelekezo ya Kingai?

Shahidi: Alitekeleza. Kuna mama mmoja alikuwa anashuhudia pale. Aliwaambia wasogee karibu washuhudie anachokifanya. Mama mmoja alikuwa anauza supu akasogea.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama taratibu za upekuzi.

Shahidi: Mmoja aliamriwa asimame juu ambaye baadaye nikaja kumtambua alikuwa anaitwa Adamoo Adama Kasekwa.

Wakili wa Serikali: Wakati huo ulikuwa unafanya nini?

Shahidi: Nilikuwa na Afande Jumanne.

Wakili wa Serikali: Ikawaje?

Shahidi: Wakati afande anampekua upande wa kushoto wa suruali yake alikuta aina Luvern Pistol A5340

Wakili wa Serikali: Kitu gani kingine?

Shahidi: Aliendelea kumkagua mifukoni akamakuta na kete 58 ambazo baadae zilijulikana ni madawa ya kulevya.

Wakili wa Serikali: Kitu gani kingine?

Shahidi: Alikuwa na simu yake.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ndani ya pistol palikuwa na kitu gani?

Shahidi: Ndani ya magazine palikuwa na risasi 3.

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Sikumbuki kwa sasa.

Wakili wa Serikali: Baada ya upekuzi nini kilifuata?

Shahidi: Upekuzi uliofuatia ulikuwa wa Adam Lingwenya. Yeye wakati anapelekuliwa alikuwa na kete 25

Wakili wa Serikali: Mbali na kete ni kitu gani kingine?

Shahidi: Na simu yake.

Wakili wa Serikali: Kingine unachokumbuka?

Shahidi: Hapana kwa sasa.

Wakili wa Serikali: Kama mashahidi walikuwapo unawakumbuka, ieleze Mahakama majina yao.

Shahidi: Nakumbukaajina yao ya kwanza ya Anita na Esther

Wakili wa Serikali: Baada ya upekuzi nini kulifuata?

Shahidi: Naona…… (halafu anakaa kimya).

Shahidi anakatizwa na Kibatala.

Kibatala: Objection. Aseme ni hear say au anakijua

Jaji: Mmeelewa?

Wakili wa Serikali: Ndiyo.

Shahidi: Baada ya upekuzi tuliaanza kujaza Certificate of Seizure ilijazwa.

Wakili wa Serikali: Baada ya kusaini kilifuata nini?

Kibatala: Objection. Hajasema ilisainiwa.

Jaji: Ni kweli ajasema wakili wa Serikali.

Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji.

Shahidi:: Baada ya kujaza Certificate of Seizure ilisainiwa na watuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Nini kulifuata?

Shahidi: Yalikuja magari mawili tukapanda.

Wakili wa Serikali: Mkaelekea wapi?

Shahidi: Tukaelekea kituo cha kati Moshi.

Wakili wa Serikali: Wakati mnaelekea Moshi kitu gani kulifuata?

Shahidi: Afande Kingai aliwauliza kwa taarifa alizo nazo walikuwa watatu, je watatu Moses Lijenje yupo wapi?

Wakili wa Serikali: Majibu yao yalikuwa ni yapi?

*Shahidi: Walisema kweli walikuwa naye na wakakubali kutuonyesha alipokuwa kwani walikuwa naye palepale wakati tunawakamata.

Wakili wa Serikali: Mlipofika kituoni nini kikifanyika?

Shahidi: Afande Kingai alitoa maelekezo Afande Francis aendelee kuwachukua maelezo. Sisi tukiokuwa kwenye gari jeupe na Afande Kingai pamoja na Jummane tukawa tumerudi RAU Madukani kumtafuta mtuhumiwa mwingine Moses.

Wakili wa Serikali: Nini sasa mlichofanya?

Shahidi: Baada ya kurudi tulimkosa. Lakini Adam na Lingwenya wenyewe wakasema huyu kuna vijiwe vyake tulivyokuwa tunazunguka wote Moshi.

Wakili wa Serikali: Baada ya kutoka Rau mkaelekea wapi?

Shahidi: Tukawa tunazunguka maeneo mbalimbali.

Shahidi: Tulizunguka maeneo mbalimbali ndani ya Moshi Mjini, KCMC, Majengo yani vijiwe vijiwe. Baadaye tukaenda mpaka Boma Ng’ombe na Aishi.

Jaji: Hebu rudia maeneo mliyozunguka ndani ya Moshi.

Shahidi anarudia.

Wakili wa Serikali: Kwanini mlikuwa mnazunguka maeneo hayo?

Shahidi: Watuhumiwa wenyewe walikuwa wanatuongoza.

Wakili wa Serikali: Ikawaje?

Shahidi: Tulimaliza saa nne au saa tano usiku.

Shahidi: Tulikaa pale Boma kwa sababu tulijua atapanda vibasi hadi saa 2 asubuhi. Tulikaa Boma Mg’ombe tukafanya kikao cha Kipolisi asubuhi kwenye saa mbili mpaka saa tatu … Tukaelekea Kituo cha Kati.

Wakili wa Serikali: Mlielekea Kituo cha Kati kufanya nini?

Shahidi: Kuwaweka watuhumiwa mahabusu.

Wakili wa Serikali: Siku inayofuata nini kilifanyika.

Shahidi: Saa 11 kuelekea saa mbili kwenda kuwafuata watuhumiwa mahabusu, kwa afande alisema tuelekee Stand Kuu. Tulienda na watuhumiwa kwa sababu wao ndio wanamfahamu, na tulikaa Stand tukijua anaweza kuwa anataka kwenda kusafiri. Tulikaa stendi bila mafanikio.

Wakili wa Serikali: Nini kilifuata?

Shahidi: Tukielekea maeneo ya palepale stendi sisi na watuhumiwa tukaenda kupata chai.

Wakili wa Serikali: Baada ya ya kupata chai nini kilifuata?

Shahidi: Hoja iliibuka kwa watuhumiwa kuwa Moses ana dada yake Arusha.

Wakili wa Serikali: Baada ya hoja hiyo nini kilifuata?

Shahdi: Afande Kingai alisema tupite kwanza kwenye vijiwe tulivyopata Jana anaweza kuwa amejifificha na baadae tukaeleka Sakina Arusha.

Wakili wa Serikali: Ifahamishe kama mlifika Arusha. Huko Arusha mlipita maeneo gani?

Shahidi: Kwa kuwa tulikuwa kwenye leading investigation moja kwa moja tulienda Sakina na hatukumkuta tukaona wanatupotezea muda.

Wakili wa Serikali: Baada ya ya kuwakosa mlielekea wapi?

Shahidi: Tukielekea Moshi na Afande Kingai akatoa malekezo kuwa kwakuwa kesi tunayoifuatilia imefunguliwa Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Unasema alitakiwa kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya nini?

Kwa sababu matukio yalikuwa yafanyike sehemu mbalimbali ikabidi twende Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama chakula cha mchana mlipata wapi?

Kibatala: Objection! Anafundisha cha kuongea.

Jaji: Objection izingatiwe.

Wakili wa Serikali: Nimesikia Mheshimiwa Jaji.

Wakili wa Serikali: Baada ya ya kuelekea Dar es Salaam nini kilifuata?

Shahidi: Tukiwa Njia Panda ya Himo gari yetu ilipata break down. Afande akaita gari nyingine na pale pana kuwa papo bize chakula cha usiku ilibidi tupate pale.

Wakili wa Serikali: Kwa kuwa unasema mlipata break down ni majira gani mliondoka pale?

Shahidi: Tuliondoka mya saa mbili usiku na kufika Dar es Salaam majira ya saa 11 alfajiri siku ya tarehe saba.

Jaji: Mlifika Dar es Salaam saa ngapi?

Shahidi: Saa 11 alfajiri.

Wakili wa Serikali: Nakurudisha nyuma mlipokuwa Njia Panda Himo unasema mlikula je ni akina nani hao?

Shahidi: Sisi na convoy yetu pamoja na watuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Baada ya kufika Central nini kilifuata hiyo saa 11?

Shahidi: Afande Kingai alitupatia break akatuambia saa moja turudi pale Central.

Wakili wa Serikali: Saa moja kitu gani kilifanyika?

Shahidi: Afande alitupa maelekezo tutoke pale kituoni pale Central na Goodluck na Ass Inspector Swila kuendelea na upelelezi.

Jaji: Mlipewa maelekezo gani?

Shahidi: Afande Kingai alitupala maelekezo tutoke tuendelee kufanya upelelezi kuhusiana na watuhumiwa ambao bado hawajakamatwa.

Wakili wa Serikali: Shahidi ieleze mahakama sasa muda wote mlipokuwa mnatoka na watuhumiwa, wakati huo walikuwa kwenye ulinzi wa nani?

Shahidi: Wakati huo mimi ndiyo nilikuwa nasimamia ulinzi.

Wakili wa Serikali: kwakuwa wewe ndiyo ulikuwa na watuhumiwa wakati wote ieleze Mahakama walikuwa na hali gani?

Shahidi: Walikuwa na hali nzuri.

Wakili wa Serikali: Sawa.

Shahidi anasita anasita tena kisha Jaji anaingilia kati.

Jaji: Endeleeni wewe na anayekuongoza. NI suala lenu.

Shahidi: Niliitwa tarehe nane Agosti mwaka 2020 Kituo cha Central na nilipofika nilikutana na Afande Kingai na Jopo zima la timu.

Shahidi: Na nilipewa malekezo kuwa watuhukiwa wale wote tuwatie Central pale Rock (… au) tuwapeleke Kituo cha Mbweni. Sababu ya msingi ni kwamba watuhumiwa kwa mafunzo waliyopitia inapaswa tuwapeleka kituo kingine.

Jaji: Rudia sababu iliyowafanya muwatoe Central.

Shahidi: Afande Kingai alisema kutoka watuhumiwa wenyewe mafunzo yao na makomandoo, walikuwa ni makomandoo wa JWTZ na kwamba complexity ya upelelezi wenyewe sababu watuhumiwa wengine tulikuwa bado hatujawapata … kwamba tuwapeleke Kituo cha Mbweni kwa sababu kuna information tulikuwa hatujazimalizia.

Wakili wa Serikali: Kituo cha Mbweni kipo wapi?

Shahidi: Kipo Wilaya ya Kinondoni.

Wakili wa Serikali: Mliowapeleka tofauti na wewe mlikuwa na akina nani?

Shahidi: ASP Jumamne, Ass Inspector Swila, Detective Constable Goodluck

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa majira gani?

Shahidi: Saa nne kuelekea saa tano.

Jaji: Kama unaweza kufafanua ilikuwa ya asubuhi au jioni?

Shahidi: Ilikuwa asubuhi.

Wakili wa Serikali: Shahidi yapo malalamiko kuwa watu hawa waliteswa.

Shahidi: Hapana hawakuteswa.

Wakili wa Serikali: Walipata treatment gani?

Shahidi: Walipata treatment ya dignity na respect.

Wakili wa Serikali: Ni hayo tu mheshimiwa.

Jaji: Utetezi!? Je, mpo tayari kuendelea?

Kibatala: Naomba kwanza tushauriane na wakili wa mshitakiwa ili aanze.

Mahakama kimyaaaaaaaaaa!

Wakili Nkungu: Unakumbuka tarehe nane ulitoa maelezo Central Police?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Nkungu: (Anampelekea shahidi maelezo hayo ili ayasome).

Bado anayasoma

Shahidi anayakana maelezo hayo kuwa si ya kwake kwa sababu hajayasaini.

Wakili Nashon: Anamuomba sasa Jaji apewe rasmi maelezo hayo Mahakamani ambayo shahidi wa pili aliyoyatoa kwa RCO Ilala.

Shahidi anatazamana na Wakili wa Serikali.

Wakili wa Serikali: (Anamuomba Jaji kuwa wakili aanze kwanza kusema anachotaka kabla ya maelezo).

Jaji: Maelezo yapo au hayapo.?

Mawakili wa Serikali wanakubali maelezo yapo mahakamani.

Jaji: Endelea kutengeneza msingi kisha uyatumie.

Wakili Nashoni: Shahidi, Je, ni kweli maelezo aliyoyatoa katika Statement yako ya RCO Ilala kuwa kulikuwa kuna kazi anaenda kuifanya Moshi baada ya kupigiwa na Afande Kingai na kuwa alikuwa hufahamu anaenda wapi tofauti na ulichosema kwenye statement yako?

Shahidi: Ni kweli sikuwa najua Mpaka nilipofika Arumeru.

Wakili Nashon: Je, shahidi unaweza kueleza upande ambao mshitakiwa aliposachiwa alitolewa hiyo pistol kwa demonstration?

Shahidi: (Anasimama anaonyesha kwa kitendo).

Wakili Nashon: Kati yako na Kingai nani alikuwa na nafasi nzuri ya kuwaona watuhumiwa.

Shahidi: Wote.

Wakili Nashoni: Kwa hiyo ni sahihi nikisema kuwa alichokiona Kingai ndicho ulichokiona wewe?

Shahidi: Kama nilivyosema mimi nilitokea kwa mbele.

Wakili Nashoni: Ieleze Mahakama kuwa kati ya wewe na Kingai nani anaidanganya mahakama. Sababu Kingai anasema mliwakamata wakati wanakunywa supu wewe unasema wakati wanatembea.

Shahidi: Miye sijui Kingai katoa ushahidi gani. Sikwepo.

Wakili Nashon: Je, shahidi unamfahamu Bwire?

Shahidi: Siwezi kujibu.

Jaji: Unapswa kujibu.

Shahidi: Sikuwa namfahamu kwa tarehe hiyo.

Wakili Nashon: Unaifahamu Police Notebook?

Shahidi: Nafahamu.

Wakili Nashon: Je, unajua kuwa ulitakiwa kuna nayo mahakamani?

Shahidi: Ile ni taarifa ya siri ni nafsi ya polisi.

Wakili Nashon: (Anaenda kukaa. Anamkaribisha Wakili John Malya aendelee kumhoji shahidi).

Wakili Malya: Shahidi, ni sahihi Polisi wanapima afya mara kwa mara?

Shahidi: Hiyo ni jambo binafsi.

Shahidi jibu tafadhali kama unafahamu au hujui.

Wakili Malya: Umefanya kazi na Kingai kwa muda gani?

Shahidi: Kwa miaka mitatu au miwili.

Wakili Malya: Kwa hiyo nikisema Kingai ana matatizo ya kusahau au kupoteza kumbukumbu ni sahihi?

Shahidi: Siwezi kujibu.

Jaji: Jibu swali.

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Malya: Kwa hiyo nikisema Kingai ana kumbukumbu nzuri napatia?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili Malya: Umeeleza katika msafara wenu mlianzia Moshi. Je, akija mtu akisema mlianzia Boma Ng’ombe atakuwa ni mwongo?

Shahidi: Sifahamu.

wakili Malya: Unapswa ujue kwa sababu ulikuwepo kwenye msafara.

Shahidi: Ndiyo. Atakuwa anasema uongo.

Wakili Malya: Umesema kuwa mliwapa chakula watuhumiwa ila hukutaja aina ya chakula wala kiasi cha chakula.

Shahidi: Ndiyo.

Wakili Malya: Umezungumzia kuhusu kituo cha Polisi Central.

Shahidi: Ndiyo.

Wakili Malya: Pale Central kuna polisi wengi kuliko kituo cha polisi.

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Malya: Kuna ya RP ILALA?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Malya: Kuna ZCO?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Malya: Kuna Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Malya: Je hawa polisi wote tuliowataja kule Mbweni wapo?

Shahidi: Mheshimiwa naomba arudie swali lake.

Jaji: Swali lake rahisi sana nitakusaidia kukuelewesha. Umetaja Ofisi za ZCO, RPC Ilala. Je Kule Mbweni Ofisi zipo au hazipo?

Shahidi: Mheshimiwa naomba nimjibu wakili.

Wakili Malya: Jibu ofisi zipo au hazipo?

Shahidi: Hazipo.

Wakili Malya: Hilo ndilo Jibu.

Jaji: Kwa sababu ya afya zetu naahirisha shauri hili kwa dakika 10 tu halafu tutarejea.


Jaji ameingia

Kesi inatajwa tena

Mafaili yana pandishwa kwa jaji

Kila mtu yuko kwenye eneo lake.

Upande wa utetezi na upande wa mashitaka wako tayari. Shahidi Inspector Mahita yupo palepale kizimbani.

Jaji anauliza Kama Wakili Malya amamemaliza.

Jaji anauliza Wakili Dickson Matata kama yupo tayari kuendelea.

Jaji anamwomba Wakili Dickson Matata amkumbushe majina yake.

Shahidi anamkumbusha Jaji majina yake. “Naitwa Inspector Mahita Omary Mahita.”

Wakili Matata: Nitakuwa sahihi nikisema wewe ni mtoto wa IGP mstaafu Omary Mahita?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Matata: Wakati baba yako akiwa IGP wewe ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa Chuo Kikuu.

Wakili Matata: Kwa hiyo wakati baba yako alikuwa IGP ulikuwa na akili timamu?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili Matata: Unakumbuka kuhusu kauli ya baba yako kuhusu kuwakuta CUF na visu kkuleta vurugu nchini?

Wakili wa Serikali: Objection.

Wakili Matata: Naondoa swali langu.

Wakili Matata: Kituo cha kwanza m2010 ulianzia kazi wapi?

Shahidi: Zanzibar.

Wakili Matata: Baada ya hapo ulikwenda wapi?

Shahidi: Mkoa wa Arusha kuwa Msaidizi wa Upelelezi wilaya ya Arusha.

Wakili Matata: Nitakuwa sahihi nikisema unawajibika kulokea maagizo yoyote kutoka kwa kiongozi wako?

Shahidi: Nkupolea maelekezo yoyote kutoka kwa kiongozi wangu.

Wakili Matata: Wakati mnawakamata watuhumiwa mlisema mlikuwa na Kikosi Maalumu?

Shahidi: Kweli

Wakili Matata: Unakubaliana na nini unapotoka keneo lako la kazi unapaswa kuwa na Movement Order?

Shahidi: Kweli.

Wakili Matata: Na unapotoka Arusha kwenda Moshi ni Mkoa mwingine?

Shahidi: Kweli.

Wakili Matata: Na unapofika mkoa mwingine unapswa uriporti kwanza Kwa mamlaka ya Mkoa huo?

Shahidi: Kweli.

Wakili Matata: Katika maelezo yako hakuna uliposema imeripoti popote.

Shahidi: Lakini………

Wakili Matata: Jibu ndiyo au siyo.

Wakili Matata: Umeeeleza Mahakama umeripoti kwa nani?

Shahidi: Sikuileza Mahakama.

Wakili Matata: Kuna sehemu umetoa ushahidi kuwa umeripoti Moshi.

Shahidi: Sijaja nao.

Wakili Matata: Nyinyi mlipowakamata watuhumiwa ndiyo mliwasafirisha mpaka Dar es Salaam.

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Matata: Malya kakuuliza kuhusu Central sitaki kurudia huko.

Shahidi: Nilishamjibu wakili.

Wakili Matata: Unapaswa unijibu mimi.

Jaji: Anapswa anijibu mimi.

Wakili Matata: Mheshimiwa Jaji mimi ndiye ninayetaka jibu.

Jaji: Nakuelewa.

Wakili Matata: Katika maelezo yako hakuna sehemu uliyozungumza kuwa nyie baada ya kufika Dar es Salaam mlifanya yote na kwenda kote huko hakuna ulipozungumza kuwa umengozana na askari gani wa Dar es Salaam.

Shahidi: Rudia swali.

Wakili Matata: (Anarudia swali…….)

Shahidi: Nilieleza kuwa tarehe nane ya mwezi wa nane kuwa nilipoitwa na ACP Kingai tukukakutana Central.

Wakili Matata: Katika maelezo yako umezungumzia kuhusu watuhumiwa kupelekwa Mbweni. Je, umewahi kusikia Pale Central kuna mtuhumiwa alishwahi kutoroka?

Shahidi: Watuhumiwa wanatoroka.

Jaji: Mbona swali rahisi? Labda walishawahi kutoroka au hujui?

Shahidi: Mimi sijui.

Wakili Matata: Kati ya Central Police Dar es Salaam na Mbweni Police Station wapi pana usalama zaidi?

Shahidi: Kama nilivyoeleza kuwa kutokana na viongozi kusema watuhumiwa wapelekwe Mbweni kwa usalama.

Wakili Matata: Nakuuliza wewe siyo viongozi wako.

Shahidi: Kama nilivyosema Mbweni ndiyo sehemu sahihi ya kuwapeleka watuhumiwa hao na pana usalama zaidi.

Wakili Matata: Utakubaliana na mimi wakati mnasema amlifika Dar es Salaam haujasema mliripoti kwa nani?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Wakili Matata: Tutoke huko turudi kwenye ukamataji. Ni sahihi hjazungumza kuwa kabla ya kuwasachi watuhumiwa kuwa nyie mlisachiwa na nani kwa mujibu wa sheria?

Shahidi: Ni kweli sijazungumza hilo.

Wakili Matata: Katika mazungumzo yako yote hujazungumza kuwa ni wakati gani walichukuliwa maelezo.

Shahidi: Ni sahihi sijazungumza.

Wakili Matata: Shahidi ulisema ulikuwa kwenye kikosi kazi na kuwasafirisha kutoka Dar es Salaam. Utakubaliana na mimi kuwa wakati yanafanyika yote wewe ulikuwa sehemu ya kikosi kazi?

Shahidi: Hauko sahihi mheshimiwa.

Wakili Matata: Usahihi ni upi?

Shahidi: Kuna wakati sisi tulikuwa tunaendelea na kazi zingine za Mahakama na nilishaeleza.

Wakili Matata: Umeeeleza kuwa watuhumiwa walikuwa ni makomandoo?

Shahidi: Kweli.

Wakili Matata: Makomandoo ni watu ambao wana mafunzo ya kijeshi. Utakubaliana na mimi wanahitaji security zaidi ni kweli?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Matata: Wakati mnazungumzia kuwakamata haujazungumzia kuwafuga pingu.

Shahidi: Si kweli.

Wakili Dickson Matata amemaliza na anamshukuru Jaji. Anakwenda kukaa.

Sasa ni zamu ya Wakili Peter Kibatala.

Kibatala: Nauliza swali ninaloulizaga watu wote. Je, unafahamu kuwa kazi ninayoifanya siyo personal?

Shahidi: Kweli.

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kilichokufanya ushindwe kuja jana ni kwa sababu ulikuwa unaprocess kibali cha kijeshi.

Shahidi: Si kweli …

Kibatala: Umepata wapi taarifa?

Shahidi: Nilipata jana asubuhi.

Kibatala: Wapi?

Shahidi: Kwa Afande Kingai.

Kibatala: Ooohhh! Mwambie Jaji kuwa umewasiliana na Afande Kingai jana saa tatu asubuhi.

Shahidi: Lakiiiiiiiiini…..

Kibatala:* Jibu kulinda heshima yako.

Shahidi: Ndiyo niliwasiliana na Kingai.

Kibatala:* Je unafahamu kuwa Kingai alikuwa Shaidi kwenye kesi hii?

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala:* Uliona wapi?

Shahidi: niliona kwenye mitandao ya kijamii.

Kibatala: Kwenye mtandao gani?

Shahidi: Tweeter.

Kibatala:* Umeona proceedings za maswali na majibu pia?

Shahidi: Hapana.

Kibatala:* Nani ka kakwambia uje kuzungumzia masuala ya chakula Moshi na Himo?

Shahidi: Ni jambo la wazi. Ndiyo uhalisia.

Kibatala: Nani alikwambia ujje kuzungumza masuala ya chakula?

Shahidi: Hakuna. Ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu kula.

Kibatala: Unafahamu leo umekuja kwa ajili ya kesi ndogo katika kesi kubwa na mojawapo ya Mahakama inachokiangalia ni mambo mliyowatendea watuhumiwa ya kuwatesa?

Shahidi: Hilo nafahamu.

Sauti ya Adhana inasikika. Kibatala anamuomba Jaji kupisha adhana.

Jaji anaruhusu zoezi Kusimama kidogo. Mahakama inakuwa kimya.

Jaji anamshukuru wakili. Kisha anaendelea.

Kibatala: Kama nimekufuatilia wewe ndio ulikuwa arresting officer.

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Kazi ya Kingai ilikuwa ni nini?

Shahidi: Mkuu wa msafara.

Kibatala: Adamo pale Boma Ng’ombe alikula chakula gani?

Shahidi: Woteeeeee.

Kibatala: Sitaki wote. Jibu Adamoo.

Shahidi: Alikula nyama choma na Mo energy.

Kibatala: Nani alilipia hicho chakula?

Shahidi: Afande Kingai.

Kibatala: Bila shaka baada ya kutumia aliomba kurejeshewe pesa zake za kulipia watuhumiwa chakula.

Shahidi: Siwezi kumjibia.

Kibatala: Ulishawahi kushiriki zoezi la retirement za pesa za Kingai alizotumia?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Wewe chakula chako alilipia nani?

Shahidi: Afande Kingai.

Kibatala: Na hotel Dar es Salaam alilipia nani?

Shahidi: Afande Kingai.

Kibatala: Kuna sehemu umeongelea kumkabidhi Afande Kingai risiti za matumizi yako aweze kurejesha alipopewa pesa.

Kibatala: Moshi kuna kambi ndogo ya jeshi.

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Kwa hiyo pale Moshi Central walikaa siku mbili?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Na wakati mnawaweka Moshi Central walikuwa wana mafunzo ya kikomandoo?

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala: Kwa hiyo ni sababu zipi special zipo Mbweni na hazipo Central zilizopelekea kupeleka watuhumiwa Mbweni?

Shahidi: Kituo cha Mbweni ni Class A na Kituo cha Mbweni hakina watu wengi tukaamua kuwatenganisha kutoka Central kuwapeleka Mbweni sababu ya complexity na nature yao.

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ulizungumza chochote kuhusu two separates cells Moshi.

Shahidi: Sikuongelea.

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa jaji kama uliongea chochote kuhusu kuwatenganisha in two separate cars.

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Mwambie Jaji kama ulisema chochote kubusu kuwatenganisha two separate cells wakiwa Central.

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Mwambie Jaji kama umezungumza popote kuwa hujasema kuwa vituo vingine kama Selande havina hadhi ya kuwapeleka.

Shahidi: Sikusema.

Kibatala: Unajua Goodluck alikuwa Mbweni?

Shahidi: Ndiyo nafahamu.

Kibatala: Unafahamu details za uchukuliwaji wa maelezo?

Shahidi: Sifahamu. Sikwepo.

Kibatala: Umeulizwa kuhusu kuandika statement.

Shahidi: Sahihi kabisa.

Kibatala: Katika a maelezo yako uliyoyarekodi kama shahidi kuna sehemu umezungumzia washitakiwa walisimama ili wale.

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Katika maelezo ya maandishi yako kuna sehemu umezungumzia washitakiwa kuwa walishawahi kupelekwa Mbweni?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Je unafahamu kuwa katika PGO kama Afisa wa Polisi namba 236 (3) ix unapomkamata mshitakiwa unapaswa ujitambulishe wewe binafsi. Umuonye kwa maneno yafuatayo:

Jaji: Mpatie PGO.

Kibatala: Sawa. Ngoja nimepelekee. (Anampelekea)

Shahidi: Mheshimiwa Jajj ananionyesha kitu kingine.

Jaji: Muonyeshe taratibu. Mtakuwa mmeshamchanganya.

Kibatala: (Wakili Kibatala anasoma PGO 236 (3) ix).

Shahidi: (Anarudia kila neno).

Jaji anamwambia shahidi atulie sasa kidogo.

Kibatala: Namaliza kusoma.

Shahidi sasa ametulia.

Kibatala: Unakubali kuwa ulipolkuwa unafanya arrest (ukamataji) ulikuwa unafanya nje ya kituo chako cha kazi?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama leo umetamka haya maneno kama ulimwambia Adamoo.

Shahidi: Mheshimiwa anasoma nukuu tofauti kwenye PGO.

Jaji: Shahidi hebu tulia. Jibu unachoulizwa. Mnafikiri na mimi sitaisoma hiyo PGO?

Kibatala: Je ulisema kama ilivyoandikwa katika PGO.

Shahidi: Hapana. Sikusema akama ilivyoandikwa katika PGO.

Kibatala: Nasoma PGO 236(3) sehemu ya 10 sasa, kwamba inataka kurekodi jibu la Adamoo katika notebook yako.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nataka kumsaidia Wakili Kibatala PGO 272.

Jaji: Hiyo siyo kazi yako.

Kibatala: Sasa soma hapa kwenye PGO.

Shahidi anasoma PGO ya 26.

Kibatala: Ni sahibi au siyo sahihi kuwa misingi yote inayoainishwa katika ukamataji lazima ifuatwe kama rula?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Unafahamu notebook kuwa ni kifaa kazi katika ukamataji?

Shahidi: Kama nilivyoeleza kuwa ni kifaa changu binafsi.

Kibatala: Unafahamu kuwa unakuja kutoa ushahidi kuhusu statement ya Adam Kasekwa?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mwambie Jaji hujui kuwa ulikuja kutoa ushahidi kuhusu kesi ndogo katika kesi kubwa kuhusu malekezo ya Adamoo.

Shahidi: Hilo sifahamu.

Kibatala: OK. Kumbe tupo na shahidi ambaye hajui amekuja kufanya nini mahakamani.

Wakili wa Serikali: OBJECTION. Tunaomba maswali ya Kibatala yazingatie utu na kuacha udhalilishaji.

Jaji: Kama amabavyo tunazungumzia ukamataji na mambo ya utu kuzingatia naomba na hapa amahakamani tuzingatie mambo ya utu ya kumtendea mtu.

Jaji: Kama amabavyo tunazungumzia ukamataji na mambo ya utu kuzingatia naomba na hapa amahakamani tuzingatie mambo ya utu ya kumtendea mtu.

Kibatala: Naomba unisomee hapa katika PGO kuhusu notebook.

Shahidi: Inasema kuhusiana na kuwa na notebook lakini silazimishwi kama nakumbuka kila kitu Mahakamani.

Kibatala: Sihitaji tafsiri yako.

Jaji: (Anaingilia kati nakusema) Naona mmechoka.

Kibatala anataka irudiwe kusomwa sehemu ya saba. Panatokea mvutano kidogo wa kisheria.

Baada ya mvutano Jaji anatoa dakika 10 mawakili wapumzishe vichwa vyao kuhusu mabishano ya shahidi kusoma PGO.

Mawakili wa Serikali wanataka tafsiri ya PGO isitolewe hapa isomwe, tafsiri iachiwe Mahakama.

Jaji anatoka.

Like