Kesi ya Mbowe: Jamhuri yafunga ushahidi kesi ndogo, utetezi waanza

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ leo tarehe 25 Novemba 2021.

Jaji ameingia

Kesi namba 16/2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

WS Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Idd Msawanga
Seleman Matauka
Maria Mushi
Khadija Aron
Evaresta Kisanga

Jaji anaita washtakiwa wote 4 na wanaitika wapo

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa, upande wetu baada ya kupitia Sheria ya ushahidi, baada ya Shahidi wa 4, tumeamua Kufunga ushahidi wetu katika kesi hii ndogo katika kesi kubwa.

Wakili wa Serikali: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji..

Jaji: anaandika Kidogo

Jaji: Mna lolote la kusema upande wa Utetezi

Wakili Peter Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji

Jaji: anaandika Kidogo.

Jaji: baada ya Maombi ya Upande wa Mashtaka ambayo yamewasilishwa Muda siyo Mrefu, Mahakama Inafunga Ushahidi wa Upande wa Utetezi na Kwa Sababu hiyo nawakaribisha Upande wa Utetezi.

Wakili Fredrick Kihwelo: Kwa Niaba ya Mshitakiwa Wa Tatu tupo tayari Kujitetea na Sababu hiyo basi ataanza Wakili Dickson Matata kumuongoza Shahidi

Jaji: Mshitakiwa namba 3

Mshitakiwa namba 03 anaenda Kizimbani Kama shahidi Upande wa Utetezi.

Jaji: Majina yako

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling’wenya

Jaji: Umri

Shahidi: 35yrs

Jaji: Kabila

Shahidi: Mmakonde

Jaji: Dini yako

Shahidi: Muislamu

Shahidi: Wallah wabillah watallah Nathibitisha Mbele ya Mahakama hii, Kuwa Ushahidi nitakao toa Utakuwa ni kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu nisaidie

Jaji: Karibu Mr. MATATA

Wakili Dickson Matata: Asante Mheshimiwa Jaji

Matata: Shahidi Ieleze Mahakama Unaitwa nani Unatokea Wapi

Shahidi: Mohammed Abdilah Ling’wenya, Naishi Kimara, King’ong’o

Matata: Shahidi Ulikuwa unafanya Kazi Gani?

Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi, na Baada Ya Kuacha kazi nikawa napambana Kupata Kazi kwa Freeman Mbowe

Matata: Kazi ya Jeshi Umeacha lini?

Shahidi: Mwaka 2017

Matata: Baada Ya Kuacha kazi Mwaka 2007 ukawa unaishi wapi?

Shahidi: Nilikuwa naishi Shinyanga

Matata: Baada ya Kuishi Shinyanga Ukaishi Wapi

Shahidi: Nikaipata Kazi Mtwara

Matata: Ulikuwa umepata kazi gani?

Shahidi: Kampuni ya Muhindi Ya kusaga Kokoto, DOT

Matata: Kwanini Uliacha kazi?

Shahidi: Nakumbuka Nilipigiwa simu na Denis Urio Kwamba Kuna kazi Ya VIP protection

Matata: ilikuwa ni Kipindi gani ambapo Denis Urio alikwambia Mbowe alikuwa anahitaji VIP Protection

WS ROBERT Kidando: OBJECTION

Matata: Ngoja Nibadili Swali

Matata: Unakumbuka Tarehe 05 August 2020 ulipokea kuwa wapi

Shahidi: Nakumbuka nilikuwa Moshi, Rau Madukani, nikavamiwa na Polisi na Kupelekwa Central Polisi

Matata: Unasema Central Polisi, ya wapi.?

Shahidi: Moshi

Matata: Unasema Kwamba Ulivamiwa na Polisi Walikuwa wangapi

Shahidi: Walikuwa zaidi ya Nane, Hatukujua ni Polisi Kwa sababu Hawakujitambulisha, Baada Ya kutukamata na kutoa Amri tupelekwe Polisi ndiyo tukajua hawa ni Polisi

Matata: Baada Kufikisha Central Polisi Moshi

Shahidi: Moja kwa Moja nipelekwa mahabusu, Chumba ambacho Kina Watu wengi

Matata: chumba ambacho Ulipelekwa Kilikuwa eneo gani

Shahidi: palepale Central

Matata: Unaweza Kuwatambua Baadhi ya watu Waliokuwa katika hicho Chumba

Matata: Unasema mlikamatwa, Je ulikamatwa na nani

Shahidi: Adam Hassan Kasekwa

Matata: Unaweza Kuwakumbuka baadhi au Wote waliokuvamia na Kuwakamata

Shahidi: Nawakumbuka Baadhi Goodluck, Francis, Mahita, Ramadhan Kingai na Jumanne ndiyo namna a kumbuka Kwa Majina

Matata: Unaweza Kuwatambua Baadhi ya watu Waliokuwa katika hicho Chumba

Shahidi: Siwakumbuki Zaidi ya wale niliowataja Mwanzo, nikakuta wapo na Camera zao, wamenizunguka na Kuanza Kuhojiwa kwamba nini kilicho Kuleta Moshi

Matata: alikuwa anakuhoji ni nani

Shahidi: Ni Jumanne na wakati Mwingine ni Mahita alikuwa anadakia Kunihoji, Wakati Nawajibu Kwa Nimekuja Kufanya VIP protection Kwa Mheshimiwa Mbowe walikuwa wanajibu kuwa sisi tunajua Kilichokuketa huku wala usitudanganye..

Matata: ni hasa aliyekwambia Hayo Maneno Kwamba “Sisi tunajua Kilichokuketa, Wala usitudanganye”

Shahidi: Ni Jimanne

Shahidi: Wakati huo Nilikuwa nimefungwa Pingu, Mahita akasema Kwamba huyu si hataki Kusema, akachukua Bomba akalipitisha Katikati ya Miguu na Mikono, akalinyanyua Juu, nikabinuka, Wakati huo Nyayo zikawa Juu, Mahita akasema huyu si hataki kusema, atasema yote tu..

Matata: Baada Kuinuliwa juu na kuweka nyayo Juu nini Kilifuata?

Shahidi: Mahita akaanza kunipiga sana..

Matata: zoezi hilo lilichukua muda gani?

Shahidi: Lilichukua nusu saa..

Matata: Nini kilifuata sasa

Shahidi: Kilichofuata Kilikuwa ni Kilimo tu, Hata Kuongea nilikuwa siwezi tena, Nikasikia Sauti ya Askari Mmoja akasema Msimpige Muacheni jamani..

Matata: Baada Ya hapo Nini Kilifuata

Shahidi: Nilishushwa Kwenye Bomba, Wakaniweka Chini Kisha wakanirudisha tena Ndani.

Matata: Wakati huo Adamoo Ulimuachia wapi?

Shahidi: Nilimuacha selo ya ndani

Matata: Sasa Umesema Ulirudishwa selo, Je ni lini tena Ulitolewa selo?

Shahidi: Nilikuja Kutoka Kesho yake Tarehe 06 August 2020 nikiwa nimefungwa Kitambaa Kizito nikapandishwa Kwenye gari..

Matata: Unaweza Kukumbuka ulikuwa ni Muda gani?

Shahidi: Muda siwezi Kukumbuka ila Ilikuwa tayari ni Jioni kwa Sababu Kajua Kalikuwa kameanza Kuzama.

Matata: Kuna Shahidi Hapa amesema Siku hiyo alipowatoa Central Mlianza Kuzunguka Maeneo mbalimbali

Shahidi: Huo ni Uongo Sijawahi Kuzungushwa eneo lolote Moshi kwanza Mimi nilikuwa Mgeni Moshi, nilitoka na Kuanza Safari

Matata: hiyo Safari ulikuwa Unaelekea Wapi

Shahidi: Sifahamu nilikuwa naelekea Wapi ila Nimekuja Kugundua tumeshafika Dar es Salaam

Matata: Kwa Kukadiria ilikuwa Saa ngapi

Shahidi: Sikumbuki Saa ila Safari Ilianza Jioni na Tukafika Alfajiri

Matata: Unakumbuka Katika hiyo Gari palikuwa na nani na nani

Shahidi: Nakumbuka Wakati kabla sijapigwa Kitambaa Kwenye Gari Palikuwa na Mahita, Goodluck na Jumanne.. Wengine Siwakumbuki

Matata: Hawa ilikuwa je ukawa fahamu Majina

Shahidi: Hawa Ndiyo waliotukamata Tangu Siku ya kwanza, Walikuwa Wanaitana Majina Kwa hiyo nikawa nimesha wakariri…

Matata: Ukiwa Njiani unaweza Kueleza Mahakama Mlisimama wapi

WS: Robert Kidando, OBJECTION. Hilo ni Leading Question

Matata: Njiani Unakumbuka Ilitokea nini na nini

Shahidi: Nakumbuka ilikuwa nikitaka Kuinua Shingo nakandamizwa Chini Mpaka Dar es Salaam Hakuna Kunyanyua Kichwa Hakuna Sehemu Gari imesimama hata Kukojoa..

Matata: Wakati wamekufunga Kitambaa Usoni na Pingu Mkononi ulihisi Jambo gani

Shahidi: Tayari nilikuwa mateka wao, Nilikuwa siwezi Kufanya lolote kwa Kitambaa na Pingu nilikuwa Chini ya Himaya yao

Matata: Ulipofika Dar es Salaam Ulijuaje Kama Umefika Dar es Salaam

Shahidi: Walipokuwa wanatushusha, Nilisikia Milango Ya Gari inafunguka na Watu Wanashuka, Wakaja Kwenye Mlango wa Nyuma Kunishusha Mimi, Wakanishusha na Kunipeleka sello

Shahidi: Waliponifikisha Wakanifungia selo, na Kufungua Kitambaa Cha Usoni, baada ya walionileta Pale mahabusu Kuondoka Nikajivuta Mpaka Kwenye Mlango wa Cello yangu Nikaona watu wengine..

Matata: hao watu wengine Ni akina nani

Shahidi: Mahabusu

Matata: Ikawaje sasa

Shahidi: Nikawauliza kwanza hapa Wapi? Wakaniambia kwamba hapa ni Kituo cha Polisi TAZARA wakati Unashushwa pale Nje Tumekuona… Wenzangu sello yao inaona mbele mie niliweka selo ninayoona kwa nyuma

Matata: Endelea

Shahidi: Wakaniuliza Kwani Una makosa gani, Maana hapa wanaletwa Watu wenye Makosa ya Ugaidi, NikawaJibu Kwamba Mimi nilikuwa Askari, Je akaniuliza Kutokea Wapi Ni kawaambia nilikuwa 92KJ

Jaji: 92 ni nini

Shahidi: 92 ni Kikosi Cha Makomandoo

Shahidi: Na yule niliyekuwa naongea naye pale Mahabusu ya TAZARA akasema, “Mimi pia ni Mwanajeshi nipo kambi ya Twalipo, Hakuna anayejua Kama nipo hapa” Wakati naongea alisogea Mwingine Ambaye alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Manyara.. Alinieleza hayo kwa Mdomo wake.. Walikuwa Wana muita sergeant Kidume

Matata: Sasa ulijuaje pale ni Tazara

Shahidi: sergeant Kidume Wakati namlilia shida, Maana Ndani Kuna sehemu ya Haja Ndogo tu, nikawa namuuliza Sasa Shida zangu ni Mueleze nani na hapa ni Kituoni, Kanijibu Waulize Wenzio hapa Ndiyo TAZARA.

Matata: Ukiondoa hao waliokwambia kwamba Upo Tazara, Je Ulijuaje tena

Shahidi: Nilitambua Kwa sababu Kuna Askari alikiwa ananiita Sana, Nilikuwa namlilia shida Kama Vile Mswaki na Mahitaji Mengine.. Akajibu Kwamba Wewe sijakuleta Mimi, Umeletwa Kwa Maelekezo, Mahabusu Wengine Walikuwa Wana muita sergeant Kidume

Matata: Sasa ulijuaje pale ni Tazara

Shahidi: sergeant Kidume Wakati namlilia shida, Maana Ndani Kuna sehemu ya Haja Ndogo tu, nikawa namuuliza Sasa Shida zangu ni Mueleze nani na hapa ni Kituoni, Kanijibu Waulize Wenzio hapa Ndiyo TAZARA.

Matata: Kitu gani Kingine Kilikufanya Ujue pale TAZARA

Shahidi: Baada ya Muda Nilitolewa na Kupelekwa Juu Pale kituoni, Kwenda Nikawakuta ALEX AHADI na CHUMA CHUGULU Walikuwa ni Madepo Wenzangu na nimeshafanya nao Kazi 92 KJ…Mara paaap! wanaingia Wakina Mahita……

Matata: TARATIBU JAJI ANAANDIKA

Matata: Ukasema Kidume alikwambia kuwa Upo wapi

Shahidi: sergeant Kidume aliniambia Hapa ni Tazara na Alex Ahadi akaniambia Usiwe na Wasi Wasi hapa ni Tazara..

Matata: Siku wanayokupandisha ilikuwa tarehe ngapi

Shahidi: Ilikuwa Tarehe 07 August 2020 Mchana

Matata: Walipokupandisha huko Juu ilikuwaje

Shahidi: Walinisogelea na Kuniuliza Nini Kinaendelea, Nikasema Safi tu, Wakaniambia Wamekuja kusikiliza Kinachoendelea

Shahidi: Walikuwa wananihoji Kwamba nini Nilichofuata Moshi, Jinsi Nilivyompata Freeman Mbowe na Nani aliyeniunganisha na Freeman Mbowe..

Matata: Je ni wote au nani alikuwa nakuhoji

Shahidi: pale ni Omary Mahita

Matata: Baada ya Kuingia Kwenye Kile Chumba Kule Juu nini Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuingia Wakina Mahita, Goodluck na Kingai aliingia Mtu na Video Camera akiwa ameielezea Kwangu

Matata: Nini Kilikuwa Kinaendelea

Shahidi: Walikuwa wananihoji Kwamba nini Nilichofuata Moshi, Jinsi Nilivyompata Freeman Mbowe na Nani aliyeniunganisha na Freeman Mbowe..

Matata: Je ni wote au nani alikuwa nakuhoji

Shahidi: pale ni Omary Mahita

Matata: Na wewe ulikuwa una wajibu nini

Shahidi: Niliwajibu kwamba aliyeniunganisha na Freeman Mbowe ni Luteni Denis Urio ambaye ni Luteni wa Jeshi 92KJ na Kazi aliyokuwa amenitafutia ni VIP Protection

Matata: walikuhoji Kwa Muda gani

Shahidi: Kama Dakika 30

Shahidi: Waliponiuliza Sababu Ya kwenda Moshi nikiwajibu BOSS alikuwa huko, Tulienda Kuelewana naye

Matata: Baada ya Kukuhoji nini Kiliendelea

Shahidi: Walinihoji Mambo Mengi, Umri, Dini kabila Mpaka Nilipoacha kazi huku wananichukua Video, Baada ya hapo Wakanirudisha Cello

Matata: Baada Ya Kukurudisha mahabusu nini Kilifuatia

Shahidi: ilikuwa Mwisho Wa Kunitoa Nje kwa Siku ile, Ila Kwa Siku ya Tarehe 8 Watu Waliokuwa mahabusu ya Mbele Walinishtua Kwamba Wale Jamaa wamefika, Nikiwa attention hawakufika kwenye chumba changu ila walikuwa wakiongea na Simu Wakaenda nyuma kwenye Magari Mabovu..

Matata: Ilikuwa tarehe ngapi

Shahidi: Siku ya 08 August 2020

Matata: Sasa wewe uliwajuaje

Shahidi: Niliwaona akina Goodluck, Chuma Chugulu na baada ya muda nilisikia mtu akiwa analia kule nyuma kwenye magari mabovu, na baada ya muda nilimtambua aliyekuwa analia Kule Nyuma kwenye magari mabovu kuwa ni DENIS URIO

Matata: Ulimtambuaje DENIS URIO

Shahidi: Namfahamu, Ni Mwalimu wangu, nilishawahi KUFANYA naye Kazi 92 KJ

Matata: Walikuwa Wanafanya naye nini

Shahidi: Sikuona Walichokuwa wanafanya, Ila Nilimuona wakati wanamtoa analia, kwa ufahamu wangu nikajua alikuwa anapigwa

Matata: Ulisema Kule Central Police Moshi, ulikuwa na Adamoo, Je Mlikuja Kuonana wapi tena

Shahidi: Safari zetu na Adamoo zilikuwa za Kupigiwa Kitambaa, Tulikuwa hatuonani Mpaka tunapofikishwa sello. Ndiyo Maana Askari wanakwambia Mwenzao yupo Chumba hicho..

Matata: Umesema Kuna Askari alikwambia Mwenzao yupo hapa unaweza Kumfahamu Majina

Shahidi: Hapana Utakuwa hujanisikia, nimesema Mahabusu Wenzangu ndiyo walioniambia Kwamba Mwenzao yupo Chumba hicho, Nikawa namuita kwa Sauti anaitikia.

Matata: Ukiachana na Sauti Kitu Gani Kingine Kilikufanya Uamini kuwa huyu ni Adamoo

Shahidi: Wakati nipo Moshi Alipitishwa akiwa ameinamishwa Kichwa niliona akiwa na Suruali yake aliyovaa na Shati lake

Matata: tuje sasa Safari ya 9/8/2020, Je ilikuwa ni Safari ya Kuelekea Wapi

Shahidi: Sifahamu Kuwa tulikuwa tunaelekea Wapi, walifungua Milango wakanipandisha Nikiwa Nimewekwa Katikati, Goodluck akiwa ananigusa na Bastola akisema Kwamba Nikileta Ujanja Ujanja watanipoteza.

Shahidi: Baada ya Kufika Wao walitangulia kushuka, Mimi nikiwa Ndani ya Gari, baada ya Muda nikasikia Sauti Mshushe huyo, Baada Kuingia Ndani nikafahamu kwamba Tupo Kituoni, Aliyekuwa amenikamata Suruali nilikuwa Namfahamu, Akaja Jumanne akanipa kikataratasi

MATATA: twende taratibu

Shahidi: Alikuja Jumanne hadi nilipo, Akanipa kikaratasi akaniambia kuanzia leo wewe utaitwa JOHNSON JOHN

Matata: Ile Safari ya kwenda Mpaka Kwenye Kile Kituo Mlikuwa Watu wangapi

Shahidi: Shahidi Siwezi Kukumbuka watu wangapi ila najua Mahita aliyekuwa amenishika, Jumanne aliyeniletea Kikaratasi..

Matata: Baada ya Hapo

Shahidi: Alikuja Kuniambia Askari Mmoja Baada ya akimuuliza Hapa ni wapi? Akasema Kwamba hupajui Enhe, Utapajua tu na utasema yote mbona.. Baada ya Muda Mfupi alirudi kaanza Kuniuliza particular zangu, naitwa nani na natokea wapi..

Shahidi: Nikiwa Kituoni walikuja Wote kwenye sello Yangu Goodluck, Mahita, Jumanne na Kingai

Matata: Baadae Ulikuja Kufahamu ni Kituo gani Cha Polisi

Shahidi: Baadae nilikuja Kufahamu Kwamba Pale ni Kituo cha Polisi Mbweni

Shahidi: Nikawa naongea naye pia Nikamwambia kwamba nilikuwa Mwanajeshi Kutoka 92KJ

Matata: Ukisema 92 unamaanisha nini

Shahidi: Kikosi cha Jeshi 92. Kikosi cha Makomandoo hicho

Matata: Akasemaje

Shahidi: Kama wewe ni Komando basi Mmeshafika watatu hapa

Matata: Akaendelea Kusemaje

Shahidi: Akasema Mmoja Umekuja naye wewe na Mmoja kaletwa Muda Mrefu, Nimeongea naye kasema ni Luteni wa jeshi Kutoka KJ92 Komandoo..

Matata: eh!

Shahidi: Akasema Kwamba kuna Mwingine pale nimempita pale yeye hanisemeshi kakaaa tu Pembeni, Nikamwambia kwamba waambie Mimi nipo hapa.. Akarudi akasema sawa ila Denis Urio anasema kwamba aliwatafutia kazi kwa nia njema tu haya mengine hayajui yametokea wapi

Shahidi: Tukawa tunapeana Salamu Kila Siku Asubuhi.

Matata: Ujumbe wa Salamu Ulikuwa Kwa Njia gani

Shahidi: Kwa Nia ya Sauti, Ila Urio nilikuwa sipigi naye Kelele, Niliyekuwa napiga naye kelele ni Adamoo.

Matata: Baada ya kubadilishwa Jina Kwamba Utaitwa Johnson John, ilikuwaje

Shahidi: Nakumbuka Ilikuwa tarehe 10 August 2020 alilita Mkuu wa Kituo Cha Mbweni ni Mwanamke akaniuliza Majina Nikamwambia naitwa Johnson John

Matata: Ikawaje

Shahidi: Nikaanza Kumueleza Jinsi Nilivyo kamatwa, Nilipotoka, Kazini nilipokuwepo akaniambia nitajie Jina lako la Ukweli Nikamtajia Mohammed Abdilah Ling’wenya

Matata: Baada ya Kumtajia Majina yako Halisi

Shahidi: Alinihaidi kwamba Ngoja tukusaidie, akaondoka Ilikuwa Asubuhi

Matata: Baada ya hapo Nini Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Muda Mfupi Kuondoka yeye, alikuja Goodluck, Mahita na Kingai kisha Nikawaona Alex Ahadi na Chuma Chungulu, Nikapishana nao wakina Chuma Chungulu nikiwa napelekwa Kwenye Chumba baada ya Kutolewa mahabusu

Shahidi: Mbele Kidogo Upande wa Kulia nikakuta Mlango, nikaingia Kwenye Ule Mlango ndani nikamkuta Chumba Kimeandikwa Ofisi ya Upelelezi, ila Mimi niliishia Kwenye hichi cha Mwanzo..

Matata: nani hasa alikuwa anakuongoza wewe kwenda

Shahidi: Goodluck

Matata: Hicho Chumba Kilikuwa Wapi

Shahidi: Nilitembeea Kwenye korido Nikaenda Kwenye selo zinazoangaliana nikakata Kulia nikapishana Na Denis Urio… Mbele Kidogo tena Nikakutana na Denis Urio

Matata: Baada ya Kuingia Kwenye Kile Chumba nini kiliendelea

Shahidi: Goodluck alienda kukaa Mlangoni akiwa na Bastola Mkononi, Jumanne akatoa Bahasha Ya Kaki na akatoa makaratasi akasema Hatutaki Usumbufu hapa..

Shahidi: Nikageuka Nyuma Nikamkuta Goodluck na Yeye anananiangalia Mimi akiwa na Bastola Yake anasema Ukileta Ujanja Ujanja wako Tutakufanya kama tulivyo Kufanya Moshi..

Matata: Baada ya Maneno hayo Ulifanya nini

Shahidi: Nilipatwa na Hofu, Uoga na wakati nafikiria Kusaini Adam Kasekwa akapitishwa.

Matata: Baada ya Jumanne Kutoa Karatasi Kwenye Bahasha Je Ulipata Kufahamu Makaratasi yalikuwa na nini

Shahidi: Sikufahamu kwa sababu hakutaka hata nisome zaidi ya Kusaini tuh, ananionyesha Saini hapa Saini hapa na baada ya Kusaini Goodluck kaichukua na Kunipeleka sello

Matata: Baada ya Kusaini nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya Kusaini, Nilirudi zangu sello Nikawa namuuliza Mkuu Wa Kituo kinachofuata, anasema tunaendelea Kufuatilia..

Shahidi: Mpaka Tarehe 19 August 2020 Nilitolewa sello nikapandishwa Gari ya wazi kisha akaja Adamoo tukasalimiana naye pale tukiwa tumekalishwa Chini, Askari Mmoja akasema Leo Mmeokoka mnaenda Mahakamani lakini Siyo kati ya wale waliokuwa wanakuja siku zote..

Matata: Tangu unazungumza sijasikia Ukisema Mmekula

Shahidi: Tarehe 5/8/2020 Moshi Hatukula,

Matata: Safarini?

Shahidi: Hatukupata Chakula

Matata: Tazara Je?

Shahidi: Pale tulipata Ugali na Mboga za Majani

Matata: Jioni Mlikula Nini

Shahidi: Hatukula tena Mpaka tunaondoka

Matata: na Mlipokuwa Mbweni

Shahidi: Nilikuwa napata Chakula siyo Cha Resheni Bali Yule Askari alikuwa ananiletea Biscuit

Matata: Mahakamani

Shahidi: Kabla hatujaingizwa Mahakamani pale Kisutu, Tulikuwa kwenye Mahabusu ya Pale Goodluck alituletea Wali Dagaaa

Matata: Unasema Mbweni Ulikuwa Unapata Chakula gani

Shahidi: Mbweni Sijawahi Kupata Chakula cha Mahabusu zaidi ya yule Askari aliyekuwa ananiletea

Matata: Unafikiri kwanini Yule Askari alikuwa anakuletea Chakula

WS Robert Kidando: OBJECTION. it’s a Leading Question

Matata: Shahidi Tangu unakamatwa, Ukiondoa Mahabusu Ulipokuwa Unakutana nao, Je Mtu gani uliwahi Kuwasiliana naye Shahidi Sikuwahi Kuwasiliana naye

Shahidi: Kwa Ufahamu wangu Mimi……..

Matata: Ni kwanini Hukuwahi Kuwasiliana na Mtu yoyote

Shahidi: Ilikuwa Kila Nikiomba wanajibu Kwamba wewe Hautuhusu

Matata: Sasa Shahidi Wa Pili katika kesi hii akiwa CRO Central Police Dar es Salaam anasema aliwapokea Mkitokea Moshi

Shahidi: Sijawahi Kufikishwa Central Polisi Dar es Salaam, Mimi ilikuwa Ni Tazara na Mbweni tu…

Shahidi: Na Kila nilipokuwa nafikishwa Mimi Sijawahi Kusimama popote Kujaza Taarifa zangu popote..

Matata: Sasa wewe baada ya Kusikia hivyo Ulichukua hatua gani

Shahidi: Siku ileile ilipofika Gerezani,

Matata: TARATIBU JAJI ANAANDIKA

Shahidi: Ni kaomba…….Movement Order ya Kutoka Central Kwenda Oysterbay na pia

Matata: T A R A T I B U

Shahidi: Na pia nipate Kujua OB na aithibitishie Mahakama Kwamba alinipokea Mimi, na Kujaza kwenye Matukio ya Siku hiyo na pia Niliomba Stationery Diary

Matata: hii Central anayosema central, central ni Central ipi

Shahidi: ni Central Police DSM

Matata: Unasema Uliongea na Wakili akusaidie Je akusaidie nini

Shahidi: Nilimuomba Wakili wangu aandike Barua kwenda kwa RPC wa Ilala, Kwamba ili nipate Uthibitisho, Basi nipate alipewa Silaha gani na alitoka Muda gani zamu yake..

Matata: Sasa Mawakili wako waliandika?

Shahidi: Ndiyo baada ya Kuongea na Fredrick Kihwelo, aliniambia atawasiliana na Wakili Kibatala Kiongozi wa Jopo la Utetezi..

Matata: Shahidi OB unafahamu ni Kitu gani

Shahidi: Ni ya Matukio ya pale Kituoni Kujaza Askari aliingia lini na alitoka lini

Matata: Na Station Diary ni Kitu gani

Shahidi: Stationery Diary kwa Upande wa Jeshi ndiyo Roaster ambayo inaonyesha Kwamba Askari aliipangiwa wapi,

Matata: Je aliyeandika ni nani

Shahidi: Nimeona Nakala ya Barua Leo, aliyeandika ni Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi

Matata: Sasa Umejuaje kama Kaandika Kibatala

Shahidi: Tangu kesi inaanza ndiye alikuwa wakili wa Washtakiwa wote tangu tupo Kisutu, na ndiye aliyekuwa anatuandikia Mabarua yetu kwenda sehemu mbali mbali.

Matata: hiyo Barua Ukiiona utaitambuaje?

Shahidi: Kwa Kuona Majina na Sahihi ya Kibatala kwa Sababu Kaniandikia Barua Nyingi sana sahihi yake naifahamu

Matata: ina nini Kingine

Shahidi: Muhuri wa Naibu Msajili

Matata: Naibu Msajili wa wapi

Shahidi: Mahakama ya Divisheni

Jaji: Nina Wasiwasi kuna watu wanamsaidia shahidi kutoa majibu

Matata: shahidi ikijibu muangalie Jaji kumtoa wasiwasi wa majibu yako

Matata: Kingine Kuna Jina langu Mohammed Abdilah Ling’wenya

WS Pius Hilla: OBJECTION. Hakusema Jina

Jaji: alisema Kuna Jina langu ila hakulitaja.

Matata: Kingine Kuna nini

Shahidi: Kuna Sahihi Ya Kibatala

Matata: ulisema Kwamba Pia Kuna Muhuri wa Mahakama

Matata: nani alikuonyesha Barua hiyo Leo

Shahidi: Wakili Fredrick Kihwelo na Peter Kibatala

Matata: Nikikuonyesha Utaitambua

Shahidi: Ndiyo

Matata: Naomba Nikuonyesha hiyo Barua, ndiyo yenyewe..?

Shahidi: Ndiyo Nimeona Kei Namba ya 16 ya Mwaka 2021

Shahidi: Ndiyo Upo hapa umeandikwa

WS Abdallah Chavula: OBJECTION asiende Kwenye Kusoma

Matata: Je Ungependa Mahakama ifanyie nini hiyo Barua

Shahidi: ningeommba Mahakama Ipokee Barua hii Kama Kielelezo Barua imezungukwa na Mawakili wa Serikali wote wanaikagua, Wanaigeuza

Anasimama Wakili wa Serikali Robert Kidando.. Anasema, Mheshimiwa Jaji Tunapingamizi dhidi ya Kupokelewa Kielelezo hichi Na Sababu ya Kwanza ni suala Zima la Competence, Shahidi aliyepo Mahakamani siyo Competent lakini Vilevile Kielelezo anachotaka Kukitoa Siyo Competent.

Na Pingamizi letu la pili ni s.uala La zima la kuto’ Kuestablish Chain Of Custody.. Na suala la tatu ni Barua hii inakosa Relevance Na Jambo la Nne Mheshimiwa Jaji Kwamba Shahidi hajajenga Misingi kabla kabla hajaomba Barua kuwa Kielelezo..

Na Mheshimiwa Jaji Tunaomba Hairisho la Muda Mfupi ili tukija Kufanya Wasilisho letu tuje na Rejea Mahususi (Relevant Authorities) Jaji: upande wa Utetezi Mnasemaje

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kuna Mambo Mawili, Kwanza tunapinga kabisa Kuhairisha Kesi Kwa sababu, kabla Ya yote lazima tujue nani kaja saa ngapi hapa mahakamani, Kesi Imeanza Saa ngapi, Mtu hawezi kutoa Ombi wakati kachelewa mwenyewe..

Kibatala: Pili, Kabla ya kupewa hiyo Barua Ilipaswa na sisi Mawakili Mmoja Mmoja Tuulizwe Kama tunapinga hiyo Barua

Jaji: Basi Sawa

Wakili Wa mshtakiwa Wa Kwanza, Tunakubaliana na Barua ya hii Kupokelewa Mahakamani, Na Sababu ya Kwanza Kukubali ni Kwa sababu Shahidi ameonyesha

WS Abdallah Chavula: OBJECTION. Mheshimiwa Jaji Tunakatakaa kabisa huu Mwenendo, tangu lini Mtu anakubali halafu anatoa Sababu Yeye akubali akae au apinge atoe Sababu..

Mtobesya: Mhe Jaji hii ni tabia ya ajabu sana, Sijaona ni wapi Sheria inasema Kwamba nakatazwa Kutoa Sababu!

Wakili wa Serikali: Motion ya Kuomba Kuwasilisha Kielelezo Imetoka Kwa Upande wa Utetezi, Mheshimiwa Jaji ikija Wasilisho kutoka Upande Mwingine ni lazima Itoke Upande Mwingine, Lakini Ukisema kwamba afanye Wasilisho tunaona Siyo Sahihi ni Maoni yetu Kwamba tunaomba ulingalie Vizuri Jambo hilo

Jaji: baadae nitakupa nafasi ya Kutoa Sababu zako

Mtobesya: Hapana hapa Nafanya Highlights tu

Jaji: Sawa nitakupa baadae nafasi ya Kusema sababu

Mtobesya: Basi Mheshimiwa Jaji naomba iingie Kwenye Rekodi kwamba Nakubalina na Barua pamoja na Sababu nitakazo toa

Kibatala: Siyo Mtu anasimama hapa anatoa Maoni yake Binafsi anataka Kutuburuza bila Kutuambia Sheria gani inakataza..

Jaji: Mimi sijasema Kweli Kwamba Sheria gani inakataza, Miye nilicho Sema Kwamba Sitaki Marudio..

Jaji: Sasa wewe mjibu tu Mr Hilla

Peter Kibatala: Hatari ninayoona hapa Kwamba Kuna watu wanajiona wao ni bora Kuliko Wengine, Kesi Ya Mtobesya Vs DPP hawa waendesha Mashtaka Walishapewa Agizo kuwa sisi wote ni Mawakili hakuna aliye Juu Mahakamani..

Kibatala: Mahakama hapa Imeshatoa Rulling ndiyo Maana Hapa Mtobesya ameacha Kufanya Submission kwa Maelekezo Yako, halafu anasimama Mtu Mbele yako akijua Kuna Amri ya Mahakama na Kuanza Kuku’ challenge wewe wakati Mahakama Yako ipo Funtus Officio..

Mtobesya: Wanachokifanya Hapa Kaka Yangu Hilla na Chavula It’s Their Logic Siyo Sheria..

WS Pius Hilla: Kuweka Record Sawa, Nilisimama Kama Afisa wa Mahakama Kwamba hizi ni Rekodi, Je Hata kama Mahakama Imesema Lakini TUNAJIELEKEZA vizuri..

Wakili wa Serikali: Mtu yupo Upande wa Utetezi hakuleta Motion, Lakini yeye anataka pia awe Part ya Submission

Jaji: ni nakubalina kwamba hizi ni Proceedings na Kwamba Kila Proceedings Za Mahakama Zina Taratibu zake, Sikuwa nimesahau Kuwapa Nafasi kila Upande Kusimama na Kusikilizwa

Jaji: Nitachotaka Kusema Hapa Ni kwamba Iwe wa wanapinga au hawapingi, Hoja wanazozitoa Mahakama itachambua kisha itatoa Maamuzi ili Mradi Hoja haivunji Sheria.. Naomba Sasa Wakili wa Mshtakiwa wa pili

Mallya: pia Naunga Mkono Kupokelewa kwa Kielelezo hicho Kwa Sababu ambazo na Mimi pia nitazitoa

Kibatala: Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Nne Naunga Mkono Ombi la Shahidi Kutoa Kielelezo Kwa namna ambayo Mahakama Itaelekeza

Jaji: Hoja ambayo ipo Mahakamani Sasa ni Ombi la Hairisho,

Jaji: Naamini ni Ombi la Kibatala Kwa niaba ya Mawakili wa Utetezi wote kwamba Nyie ndiyo Mliosababisha Mahakama Kuchelewa Kuanza,

WS Robert Kidando: Hiyo Objection ni quite Unprofessional

Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji naomba aondoe hilo Neno Unprofessional

Jaji: ameshaliondoa

Kibatala: Kama ameshaliondoa Sawa

Jaji: Tuta’ break Kwa Nusu Saa Kutoka Saa Mpaka Saa 9 na Dakika 10


Jaji amerejea Mahakamami Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Hapa Muda huu Wa Saa 9 na Dakika 24

WS Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji Upande wa Jamhuri Quorum ipo Vilevile na Tupo tayari kuanza Kuwasilisha Hoja zetu na ataanza Abdallah Chavula

Jaji: Utetezi Mpo tayari..?

Peter Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji

Jaji: Mr. Chavula Karibu

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Kabla ya yote, Naomba Mahakama Yako inipatie Kielelezo ambacho Wenzetu wanataka Kukitoa Mheshimiwa Jaji Shahidi Wa Kwanza Upande wa Utetezi Katika Shauri Dogo la Shauri Kubwa aliomba Mahakama Ipokee Nyaraka katika Ushahidi Wake, ambayo ni Barua ambayo aliyodai yeye Kwamba Kwa Kupitia Wakili wa Mshtakiwa Wa Nne Katika Shauri hili alimuomba aandike Barua hiyo Kwenda Kwa Kamanda Wa Polisi, wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Dar es Salaam, Alitaka Kamanda huyo wa Polisi Wa Mkoa ampatie taarifa fulani fulani

Mheshimiwa Jaji Siye Tuliweka Mapingamizi Dhidi ya Upokelewaji wa Kielelezo hicho..Na Mapingamizi Yetu yalijielekeza Kwenye Maeneo yafuatayo: 1.Competence : na Katika Eneo hili tulisema (a) Comptence kwa shahidi Mwenyewe (b) Na Kielelezo Chenyewe

  1. Tulisema The Chain of Custody ya Nyaraka Yenyewe, 3.Tukasema Relevance Ya Ushahidi Wenyewe 4.Tukasema ni Foundation (Misingi) Mheshimiwa Jaji Naomba Kuunga Mkono Sababu zetu Kwa kuanzia na Hoja ya Competence Kwa Shahid

Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi Aliyepo Mbele ya Mahakama, Hana Uwezo au Hana Sifa za Kutoa Kielelezo Hiki na Mahakama Yako Kukipokea (Nyaraka hii).. Mheshimiwa Jaji Hakuna Ubishi Kwamba Shahidi huyu, Hayupo Huru, Yupo Mahabusu Ya Magereza, Shahidi huyu kwa kuwa hayupo Chini ya Mahabusu au Uangalizi wa Magereza,

Upo Utaratibu Wa Kumfikia na Kama ni Kumfikia Kwa Lengo la Kumkabidhi Nyaraka Kuna Utaratibu Wa akufuatwa Mpaka Nyaraka hiyo imfikie Sheria ya Jeshi LA Magereza, Pamoja na Prisons General Orders Zimewekwa Utaratibu Wa Nyaraka Kumfikia Mahabusu

WS: Nyaraka Yoyote ili Imfikie Mahabusu ni lazima Ipitie Kwa Mkuu wa Magereza, (Bwana Jela) Na ikapitia kwa Bwana Jela, Lazima iwe na Acknowledgement au Endorsement ya Bwana jela. Mheshimiwa Jaji Tunaamini kwamba Mshitakiwa au Mtuhumiwa anayo Haki ya kuwasiliana na Wakili wake.

Lakini Haki hiyo ina Utaratibu wake, Kama akiwa Chini ya Uangalizi wa Magereza, Kama alivyo Shahidi huyu. Mheshimiwa Jaji Shahidi huyu wakati anajenga Msingi wa Kupokelewa Kwa Kielelezo hiki alieleza Mahakama Kwamba alionyeshwa Barua

Iliyokuwa na imeandikwa kwenda Kwa kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Wilaya ya Ilala, Kama Ilivyo onyesha awali kwamba Shahidi huyu yupo Chini ya Uangalizi wa Magereza, Zipo taratibu za Kuwa fikia salio Chini ya Magereza

Alionyeshwa Barua hiyo Wakati Yupo Chini ya Uangalizi Wa Askari Magereza, Wakati anaingia Mahakamani kabla Shughuli haijaanza, Haijaelezwa Kwamba alionyeshwa Barua hiyo Wakati amewekwa Mahabusu ya Mahakama..

Mheshimiwa Jaji Kwa Bahati Mbaya Sana Mahakama Yako haijaelezwa ni Wakati gani Kama ni kweli shahidi huyu alionyeshwa Barua hiyo, Alionyeshwa Barua hiyo Wakati Mahakama Imeshaanza Shughuli zake Asubuhi ya Leo hii..? Haijulikani..

Wakili wa Serikali: Haijaelezwa Barua hiyo alienda Kuonyeshwa Kule alipokuwa Magereza. Mheshimiwa Jaji Shahidi huyu awali alieleza Mahakama Kwamba aliwaelekeza Wakili wake yeye ambaye alitaja Kwa Jina la Fredrick pamoja na Wakili wa Mshtakiwa Wa Nne Bwana Kibatala Kwamba iandikwe Barua kwenda Kwa Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Ikidai au Kuomba Vitu Vifuatvyo naomba ninukuuu “aliwaelekeza Kamanda huyo wa Polisi Wampatie Station Diary, Aliwaelekeza Kwamba Kamanda huyo atoe OB,”

WS: Shahidi ajaonyesha Kwamba Barua aliyoonyeshwa( ambayo tunamashaka nayo kama alionyeshwa) kama inavitu vile alivyowaelekeza Awali. Mheshimiwa Jaji haonyesha kwamba Baada ya Kuonyeshwa Barua hiyo alibaki nayo hiyo Barua
Kwa hiyo hivi ndiyo Vitu aliwaelekeza Kwa Uchache Pamoja na Lile la Movement Order (Samahani Mheshimiwa Jaji).. Wakati wa Kujenga Misingi alieleza kwamba aliomba Kuonyeshwa Barua ya Kwenda Kwa Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala…

Lakini hajaileleza Mahakama Kama alibaki na hiyo Barua alifanya nini, ama aliifanyia nini, Mheshimiwa Jaji Ajaieleza Mahakama Kwamba Barua ile Aliyoonyeshwa ilikuwa ni Nakala yake yeye, Katika Maelezo ya awali alieleza Kwamba Nakala zilioelekwa Kwake yeye pamoja na Naibu Msajili

Wa Mahakama Kuu Division. Barua ambayo anaomba Mahakama Ipokee Kwa Mtizamo wake ina Mihuri Miwili.. Muhuri wa kwanza unaonekana kwenye Ukurasa wa Mbele, na Muhuri huo naomba nisome unamaandishi ya HIGH COURT OF TANZANIA, CORRUPTION AND ECONOMIC CRIMES OF TANZANIA,

Muhuri huo una Tarehe 25 November 2021. Na Muhuri wa pili umepigwa Kwenye Maandishi Yaliyopigwa ya TANAFRICA LAW CHAMBER. Sehemu hiyohiyo ya Pili inaonyesha Kuna watu wawili Waliopewa Nyaraka hizi.

WS: Mtu wa Kwanza ni Mr. Mohammed Abdilah Ling’wenya (Third Accused) na Mtu wa pili ni The Deputy Register, High court of Tanzania, Corruption and Economic Crimes Division, Dar es Salaam..

Mheshimiwa Jaji Kwa tulivyoelewa siye, Kwa Kuwa Barua hii imewekwa Muhuri Wa High Court Of Tanzania, Corruption and Economic Crimes Division Tafsiri tunayo ipata, Hii Barua ni Nakala Ya Acknowledgement Ya Kupokea Barua hii Kutoka Kwa Deputy Registrar..

Mheshimiwa Jaji anaomba Kuweka Lugha Sawa, Kwamba Barua hii Wenzetu Walimpelekea Naibu Msajili wa Mahakama ana yeye kuthibitisha Kwamba ni Kweli nimefikishiwa akaweka Muhuri Wake

WS: Mheshimiwa Jaji Ukitizana Barua hii na Ukitizana Barua hii ambayo Wenzetu wanataka Ipokelewe Mahakamani. Hakuna Mahali inaonyesha Shahidi alipatiwa Barua hii na akaipokea

Kama tulivyoileleza Mahakama Awali Kwa kuwa Shahidi huyu yupo Chini ya Uangalizi Wa Magereza, Hakuna linalo weza Kupita bila Kupita Kwenye Macho ya Magereza.

Na haijawekwa Bayana kwamba Barua hii Kwa namna gani ilimfikia Shahidi, Tunachoonyeshwa Mahakamani Kwamba Barua alionyeshwa Shahidi Ingawa Hatuambiwi Alionyeshwa Wapi

Mheshimiwa Jaji Wala hatujaambiwa Kwamba Hawa Wenye Jukumu la Kumtizama hawa Maafisa Wa Magereza Kwamba Walionyesha Barua hiyo, Wala Mahakama Yako haijaelezwa

Mheshimiwa Jaji Naomba tuielekeze Mahakama Yako Kwenye Shauri la JAMHURI Vs CHARLES ABEL GAZILABO Ama Jina Lingine ni CHARLES GAZILABO NA WENZAKE WATATU

Ni Shauri la Jinai ya Rufaa namba 358 ya Mwaka 2019 Mahakama ya Rufaa (Unreported) naomba nielekeze Mahakama Kwenye Ukurasa wa 12 Unao patikana katika Shauri Hili na Naomba Kunukuu Aya ya Kwanza Mstari wa Kwanza ANASOMA SASA (KWA KINGEREZA)

Pia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI na wenzake Watano ASOMA TENA K(KWA KINGEREZA) Tajwa la Kwanza na la Msingi Ni Ufahamu, Knowledge, Kwa Kutuambia alichoonyeshwa tu Bila Kutuambia alichoonyeshwa ni Kitu gani na Kina nini, Hatuwezi Kusema anaufahamu na hiki anachotaka Kutoa

WS: Vilevile Hakuna Ushahidi Kwamba lishamiliki (Possession) na Hiki anachokisema, Ushahidi Uliopo ni Wa Kuonyeshwa Na Hata Kielelezo Chenyewe Hakionyeshi Kwamba alishawahi Kupewa huyu..

Si yeye wala Siyo Kielelezo Kinachoonyesha Kwamba Kuna Wakati Kilikuwa Kwenye Himaya Yake. Kielelezo Alichokitoa Kinaonyesha Kinaenda Kwa Naibu Msajili Pia Mheshimiwa Jaji Hakuna Ushahidi Unaonyesha Kwamba yeye ndiye Mmiliki wa Hii Nyaraka, Yeye Ndiye Maker Wa Hii Nyaraka

Katika Nyaraka yeye Ni Third Party, Ni Maoni yetu Kwamba Matakwa Ya Kisheria Kwenye Competence hayajakidhi Vigezo wala hayaonyeshwa hivyo Kushindwa Kufanya hivyo Kunamuondolea Sifa

Ndiyo tunakuja Kusema Kwamba hana Sifa Za Kutoa Hiki Kielelezo. Mheshimiwa Jaji Kwa kigezo hicho tunaomba Mahakama Yako isipokee Kielelezo hicho

WS: ENEO la Pili Mheshimiwa Jaji ni Eneo la Competence ya Kielelezo Chenyewe Mheshimiwa Jaji Ni Kanuni ya Sheria, Competence ya Kielelezo inakuwa Established by showing That “its Really what is Claimed to be”

Imebainishwa Kwenye Shauri la DPP VS SHARIF MOHAMMED na wenzake, Shauri la 74 la Mwaka 2016 katika Mahakama Ya Rufaa( Unreported) katika Ukurasa wa Nane, Aya ya Kwanza Mstari wa Pili, Mahakama unaombwa Kwamba Ipokee Barua iliyopelekwa Kwa Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Ilala,

Barua inayoletewa Mahakama ni Barua iliyopelekwa Kwa Naibu Msajili Wa Mahakama Kuu ya Divisheni ya Rushwa na Makosa ya Uchumi. Na Tuna Pressume hivyo tu Kwa sababu ya Barua ya Naibu Msajili, Mh Jaji Tangazo la Serikali namba 493 ya Mwaka 2009 Serikali Ilitangaza Kipengele C 12

Kinacho patikana Katika Ukurasa wa 34 Kinahusiana na Acknowledgement.. Na kinasema hivi…. Nitasoma kwa Haraka.. ANASOMA KWELI (KWA KIINGEREZA) Mwisho Wa Kunukuu

WS: Na Hicho ndicho alichofanya Naibu Msajili Wa Mahakama Kuu, Ame acknowledge tuh, Kwakuwa Maombi yalikuwa ni Kuhusu Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Tulitegemea Barua hiyo Ingekuwa na Muhuri wa kamanda huyu au Acknowledgement ya kamanda huyu inatafakarisha Sana

Kwamba Hichi Kilicho letwa hapa Ndicho Kilichopelewa Kwa Kamanda huyo, Na ni Kweli Huyo Kamanda anaepelekewa Hiki.. Kama Shahidi anavyodai Kwamba alimuandikia Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Je Kwa Barua hii inatoa majibu..? Kwamba ni Kweli aliandikiwa Barua..

Kukosekana Majibu kuwa Kielelezo hiki Ndiyo Kilichopelekwa Kwa Kamanda wa Polisi Ilala.. Kukosekana kwa Ulinganisho Kwamba hiki Ndicho Alichopelekewa Kamanda Wa Polisi Wa Ilala. Inatia Shaka, Hatuwezi Kusema Hiki Kielelezo, Kwamba Ndiyo Kimepelekwa Kwa Kamanda wa Polisi Wa Ilala

WS: Lingine Mheshimiwa Jaji hata Kielelezo Chenyewe Ukikiangakia, Nacho Kichwa Cha Habari Chake Kilikuwa Kinaleta Mashaka Kwamba Ni Kweli Kilikuwa Kinamuhusu Mshtakiwa /Shahidi Mheshimiwa Jaji Mbele Yako,
Translate Tweet

Shauri Lililopo Mbele Yako ni Shauri La Jinai namba 16 Mwaka 2021 na Wahusika Katika Shauri hilo ni Jamhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Mshtakiwa Wa Pili ni Adam Hassan Kasekwa, Mshtakiwa Wa tatu ni Mohammed Abdilah Ling’wenya na Mshtakiwa Wa Nne ni Freeman Aikael Mbowe

CHa Kustaajabisha Barua inayodaiwa Yenye Kumuhusu, Shauri ambalo nimetaja au Wa husika Katika Shauri ni Jamhuri……..

Wakili FREDRICK kihwelo: Mheshimiwa Jaji tutapinga anachokifanya

WS: Mheshimiwa Jaji naongelea Kuhusu Competence ya Barua, Wanaogopa nini na wao Walikuwa wanafanya

Jaji: Nilisema Nini Kuhusu Content,

Mtobesya: Mahakama Ilisema Kwamba tunaweza Kuangalia Jina na Force Namba,

Mtobesya: Lakini Siyo Kwenda Kwenye Content

Jaji: Ninachokumbuka Wale waliokuwa wanaomba Kutoa Kielelezo, Walitaka Kwenda Kwenye Content Wakapingwa, Tukakubaliana hakuna namna ya Kuelezea Competence Bila kwenda Kwenye Content..

Wakili FREDRICK kihwelo: Mheshimiwa Jaji tutapinga anachokifanya

WS: Mheshimiwa Jaji naongelea Kuhusu Competence ya Barua, Wanaogopa nini na wao Walikuwa wanafanya

Jaji: Nilisema Nini Kuhusu Content,

Mtobesya: Mahakama Ilisema Kwamba tunaweza Kuangalia Jina na Force Namba,

Mtobesya: Ninachokumbuka Ulisema ni category ya Unique features, Siyo Content yenyewe..

Jaji: Kwa namna hiyo Basi naona Mr. Abdallah Chavula (WS) Usiende Ndani zaidi..

WS: Sawa Mheshimiwa Jaji lakini Kichwa Cha HABARI Kinasomeka JAMHURI Dhidi ya Freeman Aikael Mbowe

Mallya: anachokifanya amekatazwa Muda huu tu

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wanataka…..

Jaji: endelea tu, Nimesha andika hicho Ulichosema

WS Abdallah Chavula: Asante Mheshimiwa Jaji

WS: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesema Kwamba alimuelekeza Wakili Wa Mshtakiwa Wa Tatu, Wakili wa Mshtakiwa wa Nne akaalikwa na Wakili wake

WS: Akayatoa Yale ambayo alitaka Yafanywe na Wakili wake, Katika Hali ya Kustaajabisha, Katika Uandishi wa Barua ambayo yeye alielekeza Haikuandikwa na yeye wala Wakili wake Bwana Fredrick Kihwelo, Ikaenda Kuandikwa na Bw. Kibatala, Wakili wa Mshtakiwa Wa Nne

WS: Mheshimiwa Jaji Sote tunafahamu, Awali Kaka zetu na Dada zetu Wasomi MAWAKILI Walikuwa wanawatetea washtakiwa Wote wanne Kwa umoja wao, Waliacha Kuwatetea Washtakiwa wote kwa Umoja wao Baada ya Kuonekana Kuna Mgongano wa Kimaslahi..

Kwamba Hivyo hawawezi Kuwatetea Washtakiwa Wote Kwa Pamoja bila Kuacha Athari..

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Tunamuomba Kama ana meneno Mengine ya Kutumia atumie, Hicho anachokisema Siyo Jambo Letu….

Wakili Peter Kibatala: Kama ana submit Pingamizi Jipya hapo Lisajiliwe kuwa ni Pingamizi Jipya, kwa sababu Sisi tunaguswa Kama Upande wa Mshitakiwa Wa Nne….

WS: Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi Jipya Hapo, Na Amri ya Mahakama ipo wazi Kwamba palikuwa na Mgongano Wa Maslahi ya Haki za wateja

WS: Kwa Maana hiyo Barua hii imeandikwa na Wakili wa Mshtakiwa wa Nne, na Wakili wa Mshtakiwa wa Nne awezi Kuvaa Viatu Vya Mshitakiwa wa 3

Wakili Peter Kibatala: No! No! Mheshimiwa Jaji, Hilo hatuwezi Kukubali, Anachokifanya Wakili wa Serikali Pale tunakifahamu..
Jaji: lakini Barua imeandikwa hivyo

Kibatala: Hasemi hilo anasema Kwamba Kuna Mgongano Wa Kimaslahi kwa Kusema Kwamba Mshtakiwa Wanne hawezi Kuvaa Viatu Vya Mshtakiwa Wa 3, Sisi Hatuogopi wala hatumkatazi, ila tunakata Haki na sisi ya Kujibu anachokifanya sasa

Jaji: Unakumbuka Wamesimama wakati gani?

WS Abdallah Chavula: Nafahamu Mheshimiwa Jaji, Naomba Niondoe Maneno yangu nisipoteze Muda

WS: Basi Naondoa Maneno hayo ila Ifahamike Barua Kaandika wakili wa Mashitakiwa Wa Nne

Jaji: hiyo nilishaandika

WS: Vile Vile Mheshimiwa Jaji Hakuna Ushahidi Kwamba Kwanini Haku andika Barua hiyo wakili Fredrick Kihwelo

Jaji: Mnahoja Nne Na Bado Upo Hoja ya Kwanza..?

WS: Kama Swala la Barua imeandikwa na Wakili Wa Mshtakiwa Wa Nne nimeshaandika

WS: Mheshimiwa Jaji Kama alikuwa anataka Tusijddili hilo asingeandika Barua hiyi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Hicho anachokifanya ni nini

WS: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Jaji: Nawakumbusha Ikifika Saa 11 ni lazima Kuhairisha Kuheshimu Taratibu za Wenzetu..

WS Abdallah Chavula: Sawa Mheshimiwa Jaji

WS Abdallah Chavula: Mh Jaji Kwa Kuhitimisha Hoja yetu, Haujaletwa Ushahidi Mbele Yako Kwamba, Kuna Ushahidi Mwingine Unaonyesha Kwamba Barua hii alipelekewa na akakabidhiwa Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Itoshe Kusema Kwamba Barua hii imealikwa Kupokea Barua Au Kielelezo Kilichopelewa na Naibu Msajili Wa Mahakama

Ni Maoni yetu Kwamba Kielelezo Hiki ni Incompetent na Tunaomba Mahakama Isikipokee… Kwa Kuhitimisha, Kwa Hoja yetu ya Competence Wenzetu wameshindwa Kuwasilisha Competence Ya Shahidi Mwenyewe na Competence ya Kielelezo Chenyew

Hivyo tunaomba Mahakama ikatae Ushahidi Wa shahidi kuhusu Kielelezo hiki na Vilevile Mahakama isiruhusu Kuingia Kwa Kielelezo hiki Ikatae Kielelezo Hiki.. Mheshimiwa Jaji Tizama Muda sasa hivi, Tuna Mengi ya Kueleza Mahakama, Hivyo tunaomba Hairisho Mpaka Kesho

Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji. WS Abdallah Chavula anakaa chini

Jaji: Utetezi Mnasemaje?

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi Kuhusu Hairisho

Jaji: anaandika Kidogo

Jaji: Basi, Mahakama Inakubaliana na Maombi ya Hairisho, Kwa hiyo Kesho ni Saa 3 Asubuhi Kamili tunaanza, Shahidi Utaendelea Kukaa tena hapo Kesho, Tutaendelea tena Kesho Na Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho

Like