Bukoba yavamiwa: Bashiru aangukia pua kwa Meya Chifu Karumuna

Karumuna (katikati) akiwa katika moja ya matukio ya kijamii, Bukoba

SAUTI KUBWA inakuletea MCHAPO wa kisiasa kutoka Dodoma katika ofisi ya waziri wa fedha na mipango, ambaye majuzi alimpigia simu Meya wa Bukoba, Chifu Karumuna, akamwita kwa dharura aende Dodoma kwa mazungumzo ya kikazi. Manispaa ya Bukoba inaongozwa na CHADEMA. Iilikuwa hivi:

Chifu Karumuna akapokea simu toka Waziri Mpango, akaitwa Dodoma. Akaenda.

Kufika ofisi ya Waziri, akakutana na Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkuu wa Wilaya Bukoba.

Wakaanza kumbembeleza kuwa ameitwa kupewa hela ya miradi ya Stendi mpya na Soko.

Walipoingia ndani wakamkuta Bashiru. Waziri Mpango akaanza. Tumetenga hela kwa ajili ya miradi muhimu ya Bukoba. Akamsifia Chifu jinsi alivyo mtu makini. Ndipo Bashiru akaanza kuwa Mh Rais ana imani kubwa na Chifu. Kwamba anamuomba akubali kuunga mkono juhudi.

Kwamba njia ya kuwa waziri ni nyeupe. Miradi hiyo mikubwa fedha tayari. Akiingia CCM, wote wanaotangaza nia watanyamazishwa mara moja. Balozi Khamisi Kagasheki atafukuzwa kwenye chama kwa sababu ni mpinzani. Chifu akadakia, sisi wapinzani hatumtambui kuwa ni mwenzetu. Bashiru akasema, “Balozi ni wa ACT.”

RC na DC wakapiga magoti mbele ya Chifu kumsihi aunge mkono juhudi. Bashiru  akataka kupiga magoti Chifu akamzuia. Ndipo Chifu akawaambia kuwa hawezi kufanya hicho kitu. Akawaambia yeye ni mseminari na anaheshimu viapo. Akawapa ofa, kuwa yuko tayari aache siasa kuliko kuunga mkono juhudi.

Bashiru akasema Bukoba ni kwao na amehakikisha fedha inatengwa lakini sasa Chifu amewaangusha wana Bukoba.

Mkutano ukavunjika. RC na DC wakachukia kweli. 

Awali, katika maandalizi, walikuwa wameshirikisha wabunge wote wa CCM kutoka Kagera. Anna Tibaijuka wa Muleba Kusini na Diodorus Kamala wa Nkenge waligoma. Charles Mwijage wa Muleba Kaskazini hakuwepo Dodoma wakati Chifu anafika. Innocent Bashungwa wa Karagwe alishiriki mipangi lakini hakuhudhuria kikao cha Dodoma.

Msione watu wanajidai, msione wabunge na madiwani wa CHADEMA wanapukutika. Mipango inaanzia mbali.

Kumbe ndio mradi wa Bashiru alioufanya Mbeya, Ujiji, Iringa na kwingineko. Chifu anaandamwa sana kuelekea Oktoba 2020. Mlindeni!

Like
1

Leave a Comment

Your email address will not be published.