Kutoka mahakamani kama ilivyowasilishwa na ripota rais, BJ, leo tarehe 02 Novemba 2021.
Jaji ameingia Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe Imeshatajwa
Wakili wa Serikali Robert Kidando Anatambulisha
- Pius Hilla
2. Nassoro Katuga
3. Abdallah Chavula
4. Ester Martin
5. Jenitreza Kitali
6. Tulimanywa Majige
Kibatala anatambulisha Jopo lake
1. Michael Mwangasa
2.Seleman Matauka
3.Nashon Nkungu
4.Alex Massaba
5.Michael Lugina
6.Maria Mushi
7.Hadija Aron
8.Dickson Matata
9.Jonathan Mndeme
10.Fredrick Kihwelo
11. John Malya
Jaji Mashtakiwa 1,2,3 na 4 Wananyanyuka kuashiria uwepo wao
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tunashahidi Mmoja Kwa Leo Lakini Kabla ya Kuendelea Leo tuna ombi, Na Maombi yetu yatamuhusu Shahidi Wa Leo Mheshimiwa.
Jaji: Wakati wa Kufile Mashahidi tuliorodhesha Majina Kama Frank Kapala
Jaji: Ndiyo
Wakili wa Serikali: na Kule Kwenye Comito Proceedings Katika Ukusara wa 32 wa zile proceeding za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilitaja Kama Frank Kapala Lakin kama tulivyo leta information Barua ya 11 August 2021 Ndiyo alitaja kama Frank Kapala Mheshimiwa Jaji Kwa Usahihi ….Shahidi huyu anaitwa Frank kapara.
Wakili wa serikali: Kwa hiyo tunaomba Kumbukumbu sahihi za Mahakama zi-note kama Frank Kapara Kwa kifungu 264 Sura ya 20 cha CPA Rev Ya 2009 Na Kwa sababu Ushahidi wa Shahidi huyu ulisomwa wakati wa Comito Proceedings tunaomba turuhusiwe Kuendelea na Shahidi huyu.
Jaji: Kifungu gani?
Wakili wa Serikali: 264 Sura ya 20 kama Ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2009
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Maombi yetu ni hayo tu
Mtobesya: Tumesikia Maombi ya Upande wa Mashitaka na Kwa sababu Wanasema Substance ndiyo Iliyo contain Ushahidi Wake tangu Maelezo yake Polisi. Kwa Upande wetu hatuoni Kama inaathiri Haki za Mteja wetu, Hatupingi hilo Ombi Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Kwanza. Asante.
Wakili John Mallya: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili hatuna Pingamizi.
Wakili Fredrick Kihwelo: hatuna Pingamizi Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu.
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi Kwakuwa wameleta Maombi Rasmi.
Jaji: Samahani Kidogo, Unachotaka Kirekebishwe Unaweza Ku-Spell
Wakili wa Serikali: FREDY KAPALA
Jaji: Basi maombi ambayo yameletwa Kurekebisha Kumbukumbu za Mahakama Kuwa Shahidi alikuwa Frank Kampala na Sasa atafahamika kuwa ni FREDY Kapala Na hiyo ndiyo Itakuwa kumbukumbu Mpya ya Mahakama, NATOA AMRI. Mawakili wote Wananyuka na Kukubaliana na Jaji.
JAJI: Shahidi aletwe sasa
Wakili wa Serikali: Ameenda Kuitwa
Jaji: Anakuwa Shahidi Wa Ngapi huyo
Wakili wa Serikali: Shahidi 05
Jaji: Utetezi Ndiyo..?
Kibatala: Ndiyo
Jaji: Majina yako
Shahidi: Naitwa Afredy Kapala
Jaji: Umri
Shahidi: 38yr
Jaji: kabila
Shahidi: Mpare
Jaji: Shughuli yako
Shahidi: Nimeajiriwa na kampuni ya Tigo
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni Kweli, kweli tupu Eenheeeee Mwenyezi Mungu nisaidie.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakili Nasorro Katuga atamuongoza
Wakili wa Serikali Nasorro: Nitakuuliza Maswali
Wakili wa Serikali: Umesema Unashughulika na nini?
Shahidi: Nimeajiriwa na kampuni ya kibiashara inaitwa TIGO
Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema Kampuni ya kibiashara
Shahidi: Kwa sababu kampuni iliyosainiwa Brela ni MIC Tanzania
Wakili wa Serikali: Jina la Kibiashara ndiyo
Shahidi: Tigo
Wakili wa Serikali: Kampuni ya MIC Tanzania Ltd Inafanya Shughuli gani?
Shahidi: Mawasiliano ya Simu pamoja na Mihamala ya Kifedha
Wakili wa Serikali: Mwambie Mheshimiwa Jaji Umeajiriwa lini
Shahidi: March Mwaka 2012
Wakili wa Serikali: Umeajiriwa kama nani?
Shahidi: Kama Mwanasheria wa Tigo
Wakili wa Serikali: Katika Kitengo Kipi
Shahidi: Kitengo cha Sheria
Wakili wa Serikali: Umesema Kampuni yako inajishughulisha Kutoa Mawasiliano ya Simu na Mihamala ya kifedha Iambie Mahakama kwa nani?
Shahidi: Kwa Wateja Ambao wanamiliki line za Mitandao ya Simu
Wakili wa Serikali: Hawa wateja Wa Tigo Wanapatikana Vipi?
Shahidi: Wanapatikana Kwa Kununua line za Tigo na Wakaitumia basi Wanakuwa Wateja wetu. Na ili ifanye kazi lazima ifanyiwe Usajili.
Wakili wa Serikali: Kwenye Kusajili mnasajili Kitu gani?
Shahidi: Kwa mtu ambaye ana kitambukisho cha NIDA tunatumia NATIONAL IDENTIFICATION NUMBER. Mtu anaye sajili ataingiza Namba ya Kitambulisho Cha Taifa Itasoma Taarifa.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama process za Manunuzi ya Line kama zipo?
Shahidi: Mtu yoyote anaweza Kufika kwenye Duka au sehemu ambayo kuna Wakala anauza hizo line za Tigo akiwa na Kitambulisho Cha Taifa, Lakini pia Kuna Wageni ambao wanatakiwa kutumia passport….
Wakili wa Serikali: Mtu anaye jua atafanya nini?
Shahidi: Ataweke Kidole Kigumba, Zitasoma Taarifa zote ambazo zipo Kwenye NIDA, Kama Jina Na tarehe ya kuzaliwa Kwa hiyo Taarifa hiyo itachukuliwa Na kuhifadhiwa Kwenye Mfumo wa Tigo kama Taarifa za Owner au Mtumiaji wa hiyo line.
Wakili wa Serikali: Mtu asiyejua NIDA, unaposema Zinaenda Kutally na Taarifa za NIDA unamaanisha Nini?
Shahidi: NIDA nimfumo wa Usajili wa Vitambulisho Vya Taifa ambao unatunzwa na Authority
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama unaposema Taarifa zile zitachukukiwa na Kuhifadhiwa Tigo, Nani atazichukua
Shahidi: Tunasema Ki Electronic kuna Mfumo wetu ikizipata na Ikatally inatunza Kwetu, Kwa hiyo Mifumo inawasiliana
Wakili wa Serikali: Jinsi ya Kusajili line Taratibu ziko Vipi
Shahidi: Ukishanunua Laini na Kwamba wewe sasa Unawasiliana, Tuna kutumia Meseji Kuwa kama Unataka Kutumia huduma ya Mihamala ya Fedha, Ukisema Okey tunakupa Vigezo na Masharti.
Wakili wa Serikali: Hiko Kitendo Mnakiitaje?
Shahidi: Umejiregister Kwenye Huduma ya Tigopesa
Wakili wa Serikali: Nikurudiahe kwako sasa wewe Mwenyewe, Tigo Umeajiriwa kama Mwanasheria Je Majukumu yako ni Yapi
Shahidi: Kushauri Viongozi Maswala Yanayohusu Sheria, Kutengeneza Kusoma, kupitia na Kusaini Mikataba Kufuatilia, Kusimamia Kesi zote zinazohusiana na Tigo …Kumsaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama Katika Kupata Taarifa Mbalimbali Kutoka kwa Wateja zinapohitajika.
Wakili wa Serikali: Jingine, Baada ya kutoa hizo Taarifa
Shahidi: Kama Kuna Jinsi Yoyote Kusaidia Chombo chochote Katika Kutafuta Taarifa, Naweza Kusaidia Siyo VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama tu Bali hata Mtu Binafsi anaweza kupata Msaada wangu.
Wakili wa Serikali: Ni Vipi Mtu Binafsi, Mtu X anaweza kupata Taarifa za Mtu Y
Shahidi: Mtu Mmoja Kupata Taarifa za mtu Mwingine HAIWEZEKANI
Wakili wa Serikali: Kwa mujukumu hayo uliyoyataja, Unamajukumu gani au Ujuzi gani inayo Kusaidia katika Kutekeleza Majukumu yako
Shahidi: Kama Mwanasheria wa kampuni Nina Digrii ya Sheria, Nimesomea India JSS law college. Under MYSORI University, Ambayo niliipata 2009 Nilisoma Pia Advanced Computer Course, MYSORI University India 2007. Nilisoma Pia Advanced Diploma in Practice Nilimaliza Mwaka 2012 Baada ya hapo Kuna Training mbalimbali ambazo Nimezipata Nikiwa kazini 2012 nilipoanza Kazi
Wakili wa Serikali: Zitaje Training gani
Shahidi: Nilipopata kazi ilikuwa ni Majukumu yangu Nilikuwa nimeingia Kampuni ya Telecom Nilipata Training Ya Mwezi na nusu
Wakili wa Serikali: Ulisomea nini ktk hiyo Training
Shahidi: Mifumo ya Kujifunza Kutumia, ilikupata Taarifa Wa kwanza ni oracle Wa Kusaidia Kupata Taarifa mbalimbali zilizopo Sehemu za Kazi.
Shahidi: Kuna system Nyingine ambayo CONVIVER iliyokuwa Inasaidia Kupata Mihamala Yote ni soft ware BILL QUERY Iilikuwq Inasaidia Kujua matumizi Mbalimbali ya Mteja Upande wa Vocha Na SMAP ni Mfumo Sawa QUERY Kwa hiyo nilikuwa nasaidia VYOMBO Vya Ulinzi Na Usalama Kupata …Information.
Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka Ulikuwa unafanyiwa na nani
Shahidi: Ofisini na Mtu anaitwa Mr…..
Wakili wa Serikali: Ofisi za Tigo ziko wapi
Shahidi: Ofisi za Tigo Zipo Makumbusho DERM COMPLEX
Wakili wa Serikali: Unakumbuka Training Nyingine
Shahidi: 2015 palikuwa na Training Nyingine Baada ya Mifumo Kubadilika Baada ya oracle ikaja SQL Server CONVIVER ikaja Kubadirishwa Ikaja TELVIVER IKAJA ENVIVER ambayo sasa Ikaja Information Mbayo Ukiingia Unaona Matumizi …na Kila Kitu. Wanakufundisha Kule Unakoenda Kuchukua zile Information Siyo Kila amtu anaruhusiwa Kwenda Kuchukua Unafundishwa Jinsi gani ya Kuzilinda.
Wakili wa Serikali: Baada ya Mifumo Kubadilika sasa
Shahidi: Ikabidi tupate Training, Jinsi zinavyofanya kazi na Tabia zake
Wakili wa Serikali: Katika Training zako ulipata Lolote Kuhusiana na Information ambazo unaenda kufanyia Kazi
Shahidi: Wanakufundisha General Overview
Wakili wa Serikali: Umetaja Training za 2012 na 2015 Je una Training Nyingine
Shahidi: Zipo Nyingine hizo ni Major Kila Siku Dunia Ikileta System Mpya tutaambiwa tu Kuna Training za Kila Siku Katika Majukumu ya kazi
Wakili wa Serikali: Nikurudishe Nyuma Wakati Unataja Majukumu Yako Unasema Unasaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama. Je Ni VYOMBO gani
Shahidi: VYOMBO Vyote Vya Usalama Ukijumlisha Polisi, Jeshi, Kama ni Anga kama ni Ardhi na VYOMBO Vyote Vinavyofanya Uchunguzi wa Kisayansi. 2.Taarifa za Mihamala ya Fedha, Kutuma na Kupokea fedha 3. Kuna Recharge ya Vocha na Kutumia pamoja na Matumizi yake 4. Taarifa za Usajili 5. Taarifa Nyingine zote zinazoambatana Kama NIDA, LOCATIONS, BILL MBALIMBALI ANAZOLIPA
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama sasa Unawasaidia Kuwapa Taarifa, Je ni Taarifa zipi Mnawapa, ulikuwa unatumia Neno zinazoruhusiwa Kisheria
Shahidi: Zozote ambazo zitakuwa zinahitajika sisi tunazo 1.Kuna Kupiga na Kupokea Simu, Za wateja wetu zinaitwa Call Details …
Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Hizo Taarifa wewe unazitoa wapi
Shahidi: (Tigo) Taarifa zote za kampuni pamoja na Wateja wake Zinakuwa Stored Kwenye Server
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Nani anaitoa Taarifa kwenye Server
Shahidi: (Tigo) Taarifa zote Zinakuwa Served Automatically Mtu anapo piga Simu Mnara Unasima na Taarifa zinashuka na Zina switch kwenda Automatically Kwenda Kwenye Server Kuwa stored. Lakini pia Kuna watu ambao ni Observers wa kungalia na Ku Audit kazi Nzima ya Server
Wakili wa Serikali: hizo Taarifa unazozitoa Unasema Zinakuwa self Generated, Je kiuadilifu kuwa hizi ni zile zilizojitengeneza, Uadilifu wake kwenye Server?
Shahidi: (Tigo) Kama kampuni ina Mifumo ya tofauti ilitengenezwa Mahususi Kulinda hizi Server na The Whole System
Wakili wa Serikali: Unaweza kuwa unaijua hiyo Mifumo
Shahidi: (Tigo) Yeah Naweza kukujibu Kuna Mfumo Obeservit, Server au Kutoka Kwenye Switch yanyewe inakuwa na Catalist Na Kuna HUAWEI pia
Wakili wa Serikali: Unajishughulisha na nini na unafanyaje kazi?
Shahidi: (Tigo) ni software ambayo kazi yake ni Kucheki Kama Kuna Mtu au kitu kili Intend Kuingia. Kuna Firewall ni Mfumo wa kuulinzi Pale kwetu wanatumia SISQO Kuchuja kinachoingia Na Kutoka Kwenda kwenye ….
Shahidi: (Tigo) Kuna Kitu Kinaitwa AUDIT Kuangalia nani na nani Kachukua nini na Kapita wapi Kingine kuna VAPT Volumeability Acess And Penetration Test Hizi Test zinafanywa na Watu ambao ni Very Profesional lakini ni Independent Office ambapo Mnawapa Kazi Ya Kuingia …. Kwenye Mifumo yenu So It’s the test Ukitaka Unamleta Unamwambia Vunja Mifumo yako Akijaribu anakwambia Wapi pana Udhaifu na wapi Mtu anaweza Kupita Inabidi Kufanya Test Mara kwa mara ili Ujue.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Ili Usitujaze sana, Wewe Umeyajuaje
Shahidi: (Tigo) Training niliyopata, Kazi nilizofanya, uzoefu niliyopata, na Matatizo ya kila Siku (Challenge).
Wakili wa Serikali: Unaiambia Mahakama ndiyo yaliyokupa Ujuzi
SHAHIDI: (Tigo) Training, Experience ya 9yrs na Matatizo Computer nitakayopewa, nitapewa Acess kwa kuombewa Access Kwamba Mtu tuliyemuajiri anahitaji Kupata Access ili utendaji wake wa Kazi uwe Rahisi
Wakili Wa Serikali: Iambie Mahakama wewe Kwakuisaidia VYOMBO Pelelezi au VYOMBO Vya Ulinzi wewe Unafanyeje
Shahidi: (Tigo) Ukipata Kazi tuh, Kwa Maana ya kuajiriwa Kuna Vitendea Kazi kama Computer na simu ya Kwanza, Ni Vitu Vinavyo Configure Namaanisha Simu nitakayopewa na ..
Wakili wa Serikali: Unapoombewa Acess Unapewa Vitu gani?
Shahidi: (Tigo) wakati Unapewa Access Kuna SERVICE NOW system ambayo inampa Ruhusa Boss wako Ruhusa ya kuthibitisha kwamba unakuja Kufanya Kazi Fulani Kuna watu ambao ni IT security wanatakiwa kuangalia. Naingia Mara ya Kwanza Kwa Laptop lakini Kuna System Nyingine itaniambia Kama tunataka Password Yako Kuverify Either Inipigie Simu au Itumie sms, itatuma Alafu itatuma sasa Code ili niweze Kufungua Sasa Kwenye System.
Wakili wa Serikali: Sasa Umeshakuwa Approved Kwamba Huyu Mtu anafaa, Iambie Mahakama sasa Vitu gani Unakabidhiwa
Shahidi: (Tigo) Laptop Ukishapewa na Simu Kuna Vitu Vinakuwa vinawekwa ndani ya Laptop ambapo Kuna System Nyingine itaniruhusu Mimi Kuingia Mimi kwenye hiyo Computer.
Wakili wa Serikali: Code Unapewa Mara Moja unapo ajiriwa.?
Shahidi: (Tigo) Kila Ninapotaka Kuingia
Wakili wa Serikali: Nini Kitafuata
Shahidi: (Tigo) ndiyo nitakuwa na Uwezo wa Ku Access Emails, Kufungua Systems yoyote ile
Wakili wa Serikali: Nataka Kujua Sasa Jinsi ya Kuingia Kwenye Server
Shahidi: (Tigo) Kuna Mifumo sasa Nilitaja Mfumo wa SQL Itanisaidia ku-Commicate Kupata Taarifa mbalimbali
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaweza Je Kujua hapa umezipata na Utafanya nini
Shahidi: (Tigo) nikishaingia na kama nimezipata Kuna Button ya ku-Execute itazileta Kwenye Screen ya Laptop Yangu Kwamba naziona lakini siwezi ku-editi (READ ONLY) Kwamba naweza Kuziona tu ..nikitaka itaniruhusu Kuzi Print.
Wakili wa Serikali: Ishu ya kuvisaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama Utaratibu Ukoje
Shahidi: (Tigo) Kila Chombo Cha Ulinzi Kinahitaji Kuwa na Hizo Document iwe Amri au Ombi lazima iwe In Writing
Wakili wa Serikali: In Writing Unamaanisha nini?
Shahidi: (Tigo) iwe na Proper heading, naIwe na Nini wanataka
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo ni Barua, lazima iwe hivyo
Shahidi: (Tigo) NI Barua au Order ya Mahakama
Wakili wa Serikali: Kwa kumbukumbu zako Mnamo tarehe 02 Mwezi 07 2021 ulikuwa wapi
Shahidi: (Tigo) nilipata Barua Mbalimbali za Maombi, Katika Barua hizo Kuna Barua ilitoka Kwa Kamishina wa Upelelezi wa Kisayansi Ikihitaji Taarifa za Namba ya mteja.
Wakili wa Serikali: Ulisema kuna aina Mbili Za Maombi kuwa kuna Maombi na Amri. Je hiyo ilikuwa nini?
Shahidi: (Tigo) Ilikuwa ni Requeast
Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka Ilikuja kwa Maombi Ya Kuomba Taarifa fulani za Namba fulani, Je unaweza Kukumbuka.? Hiyo namba uliyoombewa Kwenye Hiyo barua
Shahidi: (Tigo) Baada ya Kuifikiria Sana anaitaja 0719933386
Wakili wa Serikali: hilo Ombi lilikuwa ni Maombi Mangapi
Shahidi: (Tigo) yalikuwa Maombi ya Mihamala ya Fedha na KYC
Wakili wa Serikali: KYC unamaanisha nini
Shahidi: (Tigo) Usajili.
Wakili wa Serikali: baada ya Kupokea Sasa, Nini Ulifanya Kuhusiana na Ombi hilo
Shahidi: (Tigo) nilipopokea ombi Kutoka kwa kamishina, Niliingia Kwenye Computer yangu Nikaweka Credentials Zangu Nikafunga Screen Server Nikaingiza namba ya Simu kwenye Procedure Ambayo…Inaniruhusu Kupata Tigo Pesa.
Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa ni wakati gani?
Shahidi: (Tigo) walitaka Taarifa za mihamala ya Fedha kutoka 01 June ya 2020 Mpaka 31 June ya 2020 Nikaingia Kwenye Computer Nikaziona
Wakili wa Serikali: Baada Ya Kuziona
Shahidi: (Tigo): Nikaziprint
Wakili wa Serikali: Kabla ya kuziprint
Shahidi (Tigo): nili-execute Kuona Ni Yenyewe Nikaingiza Namba sehemu ambayo itanipa Usajili. Server yenyewe ilitoa Majibu Ambapo Taarifa Inapokaa iliweza Kutoa hiyo Taarifa ambayo niliweza Kuiomba.
Wakili wa Serikali: Na huko Unatumia Mfumo gani?
Shahidi(Tigo): SQL server
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Utendaji kazi wa Siku hiyo Ulikuwaje
Shahidi (Tigo): Laptop yangu ilikuwa Kwenye condition Nzuri Inafanya kazi Kawaida SQL sever ilikuwa Inafanya kazi Vizuri ….
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama hicho ulichokifanya, watu wapi wa Kitengo gani wanaweza Kuwa na Access ya Server kama wapo?
Shahidi: (Tigo) kila Mtu anapata Access Kutokana na Kazi anayoifanya ambapo Kuna watu wanaangalia ile server Kama Inapata Moto Kila wakati ili iweze Kufanya kazi yake
Wakili wa Serikali: Kama watu gani?
Shahidi (Tigo): Kama Legal Department Ambapo tulipaswa Kuwa na Access Ya Kuingia Kutokana na Order za Mahakama ni watu tunaoweza Kufanyia Kazi Haraka Kuna watu Wanaitwa Order Audit, Watu wa IT security Kuna watu pia wa Data warehouse …
Wakili wa Serikali: Nyinyi Legal Department Mnapewa Access ya Kufanyaje
Shahidi (Tigo): Kusaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama na lazima Muhuri wa MIC Tanzania Ltd
Wakili wa Serikali: Turudi Kwenye namba uliyotaja, Baada ya kuprint Ukafanya nini?
Shahidi (Tigo): Niliandika Barua kumjibu Kamishina wa Makosa ya kisayansi alichokuwa anakitafuta, nikamrudishia Katika Barua nilisha Print lazima Nigonge Muhuri na Signature yangu ….
Wakili wa Serikali: Ukiambatanisha na nini hiyo Barua?
Shahidi (Tigo): Cover later, Barua ya kamishina, Mihamala ya kifedha na KYC
Wakili wa Serikali: Ukafanya nini?
Shahidi (Tigo): Nikazipeleka Ofisi ya Cyber
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Leo hii Ukionyeshwa hiyo Barua na Hizo Print Out kama utaweza Kuzikumbuka.
Shahidi (Tigo): naweza Kuzimbuka kwa Barua yangu ambapo Cover later ipo kwenye headed Paper. Cover later Ya Tigo Nimesaini Nimegonga na Muhuri
Wakili wa Serikali: Barua Ukiona Utakumbuka
Shahidi (Tigo): Nitakumbuka kwa namba Niliyofanyia Kazi
Wakili wa Serikali: Namba ngapi
Shahidi (Tigo): Nimesahau
Wakili wa Serikali: Tarehe?
Shahidi (Tigo): Nimesahau ila ni 2020
Wakili wa Serikali: ambapo ulisema hiyo namba ni ngapi
Shahidi (Tigo): 0719933386
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi (Tigo): Mihamala ya Fedha pia ninaweza kutambua Kwa sababu niligonga Muhuri wa MIC Tanzania Ltd
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa ridhaa ya Mahakama naomba nimuonyeshe Shahidi Documents fulani Kama anaweza Kuzitambua.
Wakili wa Serikali: Anamkabidhi Makaratasi
Wakili wa Serikali: Nakupa hii Nyaraka Ishike iangalie Moja badala ya Nyingine
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Kama umeweza Kuitambua
Shahidi (Tigo): nimetambua Barua ya juu ambayo ni Cover later ambapo ina later Head ya Tigo
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi (Tigo): Nimeona Muhuri Niliogonga na namba ambavyo Nililetewa kwenye Barua ya kamishina
Wakili wa Serikali: na KYC
Shahidi (Tigo): Same same Ina namba na pia nimegonga Muhuri za Usajili wa namba hiyo, Ziwe Kielelezo katika Kesi hii
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Sasa Unaiomba nini Mahakama
Shahidi (Tigo): Naomba Mahakama hii Ipokee Barua niliyoandika kwa kamishina Uchunguzi wa Kisayansi, Barua iliyokuwa inahitaji Taarifa alizokuwa akihitaji Mihamala ya Fedha ya namba iliyokuwa anaiombea na Taarifa …
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza hatuna Pingamizi
Malya: kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili hatuna Pingamizi
Fredrick Kihwelo: hatuna Pingamizi Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu
Peter Kibatala: na sisi pia kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne hatuna Pingamizi
Jaji: tunaweza Kukiita Kielelezo namba ngapi
Wakili wa Serikali: Namba 05 Mheshimiwa jaji
Mahakama ipo Kimya kwa Dakika 10 Sasa
Jaji: Mahakama Imepokea Barua ilivyoandikwa Kutaka Taarifa ya Uchunguzi wa Kisayansi kama Kielelezo namba 06 Napokea Barua ya Tigo, Majibu yao Kama Kielelezo namba 07 Napokea Print Out Kama Kielelezo namba 08 Na Mwisho Nyaraka ya KYC kama Kielelezo Namba 09.
Jaji: Sasa Naomba Shahidi utusomee Kila Kielelezo
Shahidi (Tigo): anasoma Barua ya Ombi la Kupatiwa Uchunguzi wa Kisayansi
Shahidi (Tigo): anasoma Barua ya majibu yao Kwa Kamishina wa Upelelezi wa Kisayansi Kwa niaba ya MIC Tanzania Ltd Ni matumaini Yangu Taarifa tuliyowapatia Itawasaidia
Shahidi (Tigo): anasoma Taarifa ya Mihamala ya Kifedha.
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji nafikiri Shahidi (Tigo) hawezi Kusoma hiyo Nyaraka yote tutakesha hapa Wao Wamuongoze na Kisha Tukubaliane kuwa Nyaraka ilisomwa.
Jaji: upande wa serikali
Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali:Shahidi tufafanulie Maneno Ya Juu kama Sender Maana yake nini
Shahidi (Tigo): Send My Op namba 0719933386 Receiver 0787555200 Miamala wa Tarehe 20 Kiasi 500,0000 Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 21na Balance Ilikuwa 2.3M
Wakili wa Serikali: Twende kwenye hii KYC Kielelezo namba 09
Shahidi (Tigo): Imeanza na namba pale Juu Jina la Kwanza Jina la Katika, Taifa, Jenda na Vitu Vinginevyo Mstari unaofuata 0719933386 Jina Freeman Last name Mbowe Nationality Tanzanian From Kilimanjaro
Shahidi (Tigo): Kuna namba ya Tigo ya O719933386 imetuma kiasi cha fedha Tsh 500,000 kwenda kwa namba ya Airtel namba 0787555200
Wakili wa Serikali: IOP Maana Yake nini?
Shahidi (Tigo): Kitu Kimetumwa kutoka Namba hiyo
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa hayo ndiyo maeneo ambayo tulikuwa tunaomba Shahidi ayasome
Wakili wa Serikali:Kielelezo namba 7 iambie Mahakama ni nini?
Shahidi (Tigo): Barua iliyotoka kwa Kamishina Ikiwa inataka taarifa za mteja
Wakili wa Serikali: Tarehe 20.7.2020 inaonekana nini.
Wakili wa Serikali: Sender City maana yake nini?
Shahidi: Mnara wa mtu aliyetuma Pesa alikuwa wapi?
Wakili wa Serikali: Fafanua Sender One Mikocheni
Shahidi: aliyetuma fedha alikuwa Mikocheni na alikuwa Kinondoni
Wakili wa Serikali: Fafanua hapo Kwamba Mikocheni ipo Kinondoni
Shahidi (Tigo): hapana, MIKOCHENI ni KITONGOJI
Wakili wa Serikali: Kielelezo namba 9 Kuna Kitu Umesema First name na Middle name Na ulianzana namba
Shahidi: 0719933386 ni namba ya Tigo
Shahidi: First name Freeman, Middle name Aikael, Last name Mbowe
Wakili wa Serikali: Maana yake
Shahidi (Tigo): namba inamilikiwa na Mtu anaitwa Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: chini ni nini
Shahidi (Tigo): Tarehe ya kuzaliwa
Wakili wa Serikali: ID proof Maana yake nini?
Shahidi (Tigo): Kitambulisho kilichotumika Kusajilia namba
WS: Mwenye namba hii alisajili kwa alama za Vidole tarehe ngapi?
Shahidi (Tigo): 16.9.2019
Wakili wa Serikali: hizi Null Null Null fafanua kidogo
Shahidi (Tigo): System haipati Taarifa za Usajili wa wakati Ule wa zamani
Shahidi (Tigo): Nilienda Kutoa Maelezo yangu katika Taarifa nilizozitoa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu, Namuacha Mikononi Mwa Mahakama
Shahidi (Tigo): alinipigia Simu Kwamba yeye ni Askari Polisi na Kwamba nahitaji kutoa Maelezo
Wakili wa Serikali: Alikuambia nini?
Shahidi (Tigo): aliniambia Kuhusiana na Taarifa zako ambazo Ulizotoa
Wakili wa Serikali: Wewe Ukafanya Nini
Wakili wa Serikali:Tarehe 08 July 2021 Unakumbuka nini?
Shahidi (Tigo): Nikitakiwa kutoa Maelezo kituoni, kituo cha Polisi Central, Si kuandika Maelezo
Wakili wa Serikali: Ulitakiwa na nani?
Shahidi (Tigo): Kuna Inspector wa Polisi alinitafuta
Wakili wa Serikali: alikutafutaje
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kabla hatujaanza maswali ya dodoso nilikuwa naomba Mahakama itambue uwepo wa wakili mwenzangu Nashon Nkungu
Jaji anaandika Kidogo..
Mtobesya: Nilikuwa naongea na wenzangu kama Tutapata mapumziko ya Afya lakini naomba Niulize mimi Japo kwa nusu saa tu baada ya Hapa Nina kesi mahakama ya Rufani nitaacha wenzangu waendelee
Jaji: itakuwa vizuri ukitumia dakika 20
Mtobesya: Shahidi Wakati naongozwa na wakili wa serikali ulielezea kwa urefu sana namna ambavyo mnafanya kulinda mfumo wenu Pamoja na Server. Je Ni sahihi?
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Lakini Hukuiambia Mahakama Mpaka Wakati Unatoa Taarifa hapakuwa pamefanyika Audit ya namna gani na Kwamba System Ilikuwa Vizuri.
Shahidi: Sahihi
Mtobesya: Sikusikia Ukisema Kwamba Servers zinaweza kuingiliwa na Mahakama?
Shahidi (Tigo): Sahihi
Mtobesya: Wakati Jaji akiandika elezea HACKERS ni Watu gani
Shahidi (Tigo): Ni Wataalamu wa mitandao ambao wanasoma mfumo au wanakuwa wanaufahamu mfumo na wanatabia ya kujaribu kuingia kwenye mfumo, kuchukua ama kuharibu taarifa ama mfumo Wenyewe.
Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema wakati unaongozwa na wakili wa serikali hukusema kama palikuwa na possibility ya hackers kuingia kwenye mfumo?
Shahidi (Tigo): Ndiyo Sikusema
Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema hackers wana uwezo wa kuingia na kucheza na taarifa za READ ONLY kama alivyokuwa anakuongoza wakili wa serikali?
Shahidi (Tigo): Ndiyo uwezekano upo
Mtobesya: Ofisi ya Tigo ulisema ni nini
Shahidi (Tigo): Jina la Kibiashara
Mtobesya: Ofisini kwenu kuna wanasheria Wangapi?
Shahidi (Tigo): Kwa Ujumla au Legal Department.?
Mtobesya: Legal Department
Shahidi (Tigo): Watatu
Mtobesya: Nilisikia Ulisema wanaweza Kuingia Kwenye Mfumo ni watu wa Mantainance na Audit, Je Kuna lolote Umetoa lenye Jina lako kwamba wewe ndiyo ulishughulikia Taarifa hizi?
Shahidi (Tigo): Mbali na Barua kwa kweli Hakuna
Mtobesya: na Barua pia haina Jina?
Shahidi (Tigo): Ndiyo haina Jina
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Barua ithibitishe hiyo
Mtobesya: Nitakuwa sahihi Nikisema Kwenye Taarifa ya KYC (KNOW YOUR CLIENT) haihitaji Barua za Utambulisho kama Serikali za Mitaa?
Shahidi (Tigo): Hapana haihitaji
Mtobesya: tuweke Record sawa kwa hiyo hata Photocopy Ya Kitambulisho Cha NIDA haihitajiki
Shahidi: NI Scanned ID
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi nikisema KYC inatakiwa iambatane na hiyo Image ya Kitambulisho Cha NIDA
Shahidi (Tigo): Siyo lazima
Mtobesya: Nitakuwa sasa Kwenye Kielelezo namba 09 Cha Mtu Uliye Sema ni Freeman Mbowe Taarifa zake Hazipo Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 09
Mtobesya: Nionyeshe Jina la Mtumishi aliyesajili
Shahidi (Tigo): Siyo Mtumishi ni Mtu Mwenye Device
Mtobesya: Ndiyo huyo huyo Nionyeshe Jina lake
Shahidi (Tigo): Halipo
Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema hata Mtu aliye sajili haionekani alisajilia wapi?
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Shahidi (Tigo): Legal Department
Mallya: Ulitaja Department Zingine Kwenye Ushahidi wako
Shahidi (Tigo): Ndiyo Kama IT Security
Mallya: Kazi zake?
Shahidi (Tigo): Ulinzi wa Taarifa za Mfumo na Taarifa zote zinazoshughulika na wateja
Mallya: Shahidi wewe ni Wakili siyo
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Umekuwa admitted kwenye bar mwaka gani?
Shahidi (Tigo): 2013
Mallya: Tigo Umeajiriwa lini
Shahidi (Tigo): 2012
Mallya: na Uliajiriwa department gani?
Mallya: Hiyo Department ya Security Bwana Yahaya Zahoro ndiye anayeshughulikia taarifa kama hizi?
Shahidi (Tigo): Yeye ni Internal Investgation Officer
Mallya: yeye ndiye anaye Shughulikia Maswala kama haya
Shahidi (Tigo): Siyo haya
Mallya: Upi Ulianza
Shahidi (Tigo): Ulianza CONVIVER Ukaja Telepin
Mallya: kwanini waliondoa CONVIVER
Shahidi (Tigo): Kwa sababu ya Mabadiliko ya muda na Technology
Mallya: kuna Department inayoshughulika na Masuala External Investigation
Shahidi (Tigo): hatuna, hiyo labda ni Polisi na Serikali
Mallya: Ulizungumza lolote kuhusu Telepin
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Ulisema ni nini
Shahidi (Tigo): Mfumo Mmoja Ulikuja Kure place Mwingine
Mallya: Wakati Unatoa Exhibit P8 suala la Miamala ya Fedha Ulielezea Mahakama Kwamba Ulizungumza Kutoka Kwenye Software gani?
Shahidi: Screen Server
Mallya: Wakati Unaona hizi Taarifa Ulisema Umetumia Mechanism Gani Kugenerate hii Print Out
Shahidi: Nilichagua Option ya Kuprint
Mallya: Kwanini Ulichagua Kwanini Uliacha Option Ya Screenshort ukaamua Kuprint?
Shahidi (Tigo) Ilikuwa ishu ya Choice tu
Mallya: Kuhusiana na Jina lako Mwanzoni palikuwa na Maombi ya Kubadili Kutoka Frank Kwenda FREDY,
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mallya: Je Kapala ni R au L Mwishoni
Shahidi (Tigo): NI L Mwisho
Mallya: Kwa hiyo huyu Kapara siyo wewe
Shahidi (Tigo): Inaweza Kuwa wamechanganya
Mallya: Wewe ni Wakili unajua Madhara ya kukosewa Jina
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Life cycle ya Simu Card unaweza Kupata Wapi?
Shahidi (Tigo): SQL server
Mallya: Mimi ninao Ushahidi inapatikana Kwenye SMAP
Shahidi (Tigo): Ndiyo inapatikana pia
Mallya: Unababilisha Jibu eeh!
Shahidi (Tigo): Hapana Kote unaweza Kupata Kote
Mallya: Taarifa uliyoileta KYC ni Taarifa Accuracy?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Unataka Mahakama Ikueleweje ukisema Accuracy?
Shahidi: Nimezipata Kwa Njia iliyokamilika sina Wasiwasi nazo
Mallya: Hapo Kuna Mpangilio wa Taarifa Je umeelezea Sababu Ya Kupanga hivi?
Shahidi: Hapana
Mallya: Kuna City imeandikwa Kilimanjaro Je Ulimwambia Jaji hiyo Kilimanjaro City Unaifahamu
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: Hiyo Kilimanjaro City unaifahamu
Shahidi (Tigo): Hakuna Kilimanjaro City
Mallya: Kuna District inaitwa Kinondoni, Je huko Kilimanjaro inaweza kuwa District ya Kinondoni?
Shahidi (Tigo): SAMAHANI KIDOGO
Mallya: NISHAKUSAMEHE
Shahidi (Tigo): RUDIA SWALI
Mallya: Kuna City ya Kilimanjaro, kuna District ya Kinondoni
Shahidi (Tigo): Hakuna
Mallya: Kuna sehemu hapo imeandikwa Region, Region gani?
Shahidi (Tigo): Kimyaaaaaaaaaa
Mallya: Je huko Dodoma Kuna Sehemu Inaitwa Kilimanjaro City?
Shahidi (Tigo): Hakuna
Mallya: Unasemaje Kuhusu hizo Taarifa?
Shahidi (Tigo): Kuna Taarifa ambazo zipo NIDA so Ukiweka Kidogo Nauliza Mfumo wa NIDA, Mtu Mwenye Jina hili na Fingerprints hizi Zina Match Zinasoma anaitwa nani, na Taarifa zake zote zinakuja,Kama hazipo zinakuja Kuhuishwa siyo Za NIDA Kama hazipo ni za kwetu sisi.
Mallya: kama Taarifa hakuna Je Freeman Mbowe alijisajili Mwenyewe?
Shahidi: Nahisi Wakili hatuelewani katika hili, Nilisha Sema Kama Taarifa zilizotakiwa Kuchukuliwa NIDA kama Hawana Sisi tulipaswa kuchukua NIDA
Mallya: Kielelezo 09 kimetoka kwenu au NIDA?
Shahidi: kwetu
Mallya: Kwa hiyo Hiyo Mitambo ya kuprint ipo NIDA au Ofisini Kwenu?
Shahidi (Tigo): Ofisini Kwetu
Mallya: Aliyemsajili Mbowe nani kama Kweli Mbowe ana namba ya Tigo?
Shahidi (Tigo): Simjui
Mallya: Kwanini humjui?
Shahidi (Tigo): Sababu Kwenye Taarifa hiyo Sijamuona
Mallya: Nitakuwa sahihi Nikisema Taarifa Yenu Haipo Kamili nitakuwa Sahihi?
Shahidi (Tigo): Haupo Sahihi
Mallya: Pale Ofisini Kuna Department ya Tigo Pesa
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Ulizungumzia kuhusu Tigo Pesa Department.?
Shahidi (Tigo): Sikuzungumzia.
Mallya: Mimi siijui kama namba ni ya Freeman Mbowe au Lah, lakini hebu niambie Pale Kwenu Kuna Kitengo cha Business to Business kama Post paid?
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Mallya: Ulizungumzia Hiyo?
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: Hii namna ya Kujibu Mabarua ni Standard Form au Kila Barua na namna yake?
Shahidi (Tigo): NI Standard Form
Mallya: Lengo la Kuweka ENEO la Kujaza Kosa la Mteja wenu wanalomchunguza nalo?
Shahidi (Tigo): NI Format ya Kuweka Kosa wanalo mchunguza nalo
Mallya: Je Polisi Wakitaka Uwape Taarifa ya kuchunguza Girl Friend wake we utatoa taarifa?
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: Je wewe Ulipata Kuuliza Wana mtuhumu Kwa Makosa gani?
Shahidi (Tigo): Hapana Sikuuliza
Shahidi (Tigo): Siyo lazima pawe na kosa la Jinai, Kazi yangu ni kuona Kama Wamekidhi vigezo
Mallya: Ni Mara yako ya Kwanza Kupata Barua Kutoka Forensic Bureau?
Shahidi (Tigo): Hapana
Mallya: Kwa hiyo wewe Ukatoa Taarifa hata kama Mtu anataka Kujua anamtumia pesa Mpenzi wake
Shahidi (Tigo): Siyo Utaratibu wangu wa Kazi
Mallya: Kwa hiyo nyie Tigo mnataka Kutuambia Kuwa Polisi Wakitaka Taarifa hata kama hawana Kosa la Kuchunguza Mtawapa?
Mallya: Kwani Forensic Bureau Wanahusika na masuala ya ndoa na matunzo ya watoto?
Shahidi (Tigo): Mimi naangalia namba na kutoa taarifa
Mallya: Hukuona umuhimu wa kujua kosa..?
Shahidi ( Tigo): Siyo kazi yangu kujua makosa
Mallya: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Jaji; anaandika Kidogo
Jaji; Tutaenda break Dakika Ngapi?
Kibatala: Ngoja tushauriane
Jaji; Sawa Wakili wa Serikali; Tumekubaliana na Wenzetu Tubreak Kwa Dakika 40 turudi saa 08 kamili
Jaji; basi tunabreaka kwa Dakika 40 tutarudi Saa 08 kamili, Naomba tutunze Muda
Jaji ameingia tena Kesi inatajwa tena.
Kibatala: Naomba Wakili Dickson Matata Kwa Ruhusa yako aingizwe Katika column Nilimuombea Ruhusa Kwamba atachelelewa na Kwa Sasa ameshafika Namualika Wakili wa Mshtakiwa wa 03 aweze Kuuliza Maswali ya Dodoso
Matata: Nilikusikia Kwamba Kwenye Kitengo Cha Sheria Mpo watatu
Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili wa Serikali Ukusema nani Mkuu wa Idara Yenu
Matata: Na Hukusema Wewe licha ya Kuwa Mwanasheria Ni Mkuu wa Idara, Kweli siyo kweli
Shahidi: (Tigo) +/ Siyo Kweli
Matata: licha ya Kuwa Wewe Mwanasheria Hukusema Wewe unanafasi gani Nyingine
Shahidi: Siyo Kweli Matata Ikae hivyo hivyo Mheshimiwa Jaji
Matata: Wewe Ndiyo umepokea Barua, wewe Ndiyo umeprint Taarifa, na Wewe Ndiyo Umepeleka Majibu Polisi
Shahidi (Tigo): Sijaelewa
Matata: Wewe Ndiyo ulipokea Barua
Shahidi (Tigo): Sahihi
Matata: wewe Ndiyo uliandika Barua
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Nitakuwa sahihi nikisema wewe Ulifanya Kila Kitu Kwa Niaba ya Tigo
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Ulielezea mahakama kwamba kwanini wenzio 3 hawakushiriki katika hiyo kazi?
Shahidi (Tigo): Siyo kweli
Matata: Kampuni yenu mnasera ya Usiri?
Shahidi (Tigo): Upo sahihi
Matata: ambapo Mawasiliano ya mteja yanakuja ni Siri kati ya Mteja na Nyinyi
Shahidi (Tigo): Sahihi
Matata: Kwamba nitakusa sahihi nikisema Moja ya Sababu Ya Kuvunja Usiri ni endapo panahitajika Kufanya Uchunguzi Kwa VYOMBO Vya Uchunguzi
Shahidi (Tigo) Sahihi
Matata: Na Utoaji huo Wa Taarifa unalindwa na Sheria
Matata: Na wewe ni Mwanasheria
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Na Mimi nimekusikia Mtatoa Taarifa Endapo Mtaombwa au Kwa Amri ya mahakama
Shahidi (Tigo): Sahihi
Matata: Kwa kuzingatia Umuhimu wa Usiri wa mteja Nisomee Kifungu cha 34 cha Sheria Ya Makosa ya Mtandao
Shahidi (Tigo): 34(i) Disclosure of Data………
Matata: Utakubaliana na Mimi kwamba Pale panapohitajika Taarifa Ya Uchunguzi Police ambaye ni Ofisa anaweza Kuomba Taarifa Kwenu?
Shahidi (Tigo): Hapo anaongelea Ongoing Trafficking Data siyo Stored Data
Matata: Mh Jaji naomba Kielelezo
Matata: hiyo Barua Wametumia Kifungu gani?
Matata: Kwa Mujibu wa Maelezo yako walitaka Uwapo Data Trafficking Ya Siku hiyo Siyo Stored Data
Matata: Naomba Unisomee hapa
Shahidi kutoka( Tigo_TZ ) Anasoma kwa sauti sheria tajwa
Shahidi (Tigo): Kifungu cha 34 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao
Matata: Na Mimi nimekuuliza Usome Kifungu gani?
Shahidi (Tigo): Kifungu hicho hicho cha 34
Matata: Kwa hiyo utakubaliana na Mimi wewe Umeombwa Kitu Kingine na wewe Ukatoa Kitu Kingine
Matata: Utakubaliana na Mimi kwamba Kama Mtu ameombwa Taarifa na akakataa na Yule Police Officer alitakiwa kwenda Mahakamani Kuomba Court Order
Shahidi (Tigo): NI sahihi
Matata: Naomba Unionyeshe Kwenye hii Barua ni wapi Pameonyeshwa Kosa Kwenye hiyo Barua ambapo hiyo namba Inatuhumiwa kwenye Kosa la Jinai
Shahidi: Hakuna
Matata: Kuna Kosa Umeandika hapa Wakati Unajibu Barua hii Kuhusiana na Uchunguzi
Shahidi (Tigo): Kuna Dash Hakuna Kosa
Shahidi (Tigo): Hapakuwa na Haja hiyo
Matata: Kwa hiyo Polisi Wakikuandikia Barua ya Kutaka Taarifa Bila Kukutajia Makosa
Shahidi (Tigo): Nitampa
Matata: Kwenye kampuni yenu haitaji la Kutuma Meseji au Kupiga Simu Kwenu ni Kosa?
Shahidi (Tigo): Hapana Siyo Kosa
Matata: Kwa hiyo Hakuna Kosa
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Matata: Pamoja na Barua kuja Bila Kutaja Kosa na Wewe Ukatoa Taarifa hiyo bila Kutaja Kosa kama Inavyosema katika Kifungu 34 Je Hukuona hilo ni Jambo lisilostahili ili uwakatalie Waende Mahakamani Kulinda Usiri wa wateja wenu?
Jaji: wakili wa mshtakiwa namba 4
Kibatala: Nyie Kama (Tigo_TZ) MIC Tanzania Ltd Priority ni nini, USIRI wa MTEJA au Kufuata MASHARTI ya POLISI?
Shahidi (Tigo): Tuseme COMPLIANCE na SIRI za MTEJA
Kibatala: Sawa tuweke hivyo Kwenu Kipaumbele ni nini?
Shahidi (Tigo): COMPLIANCE
Kibatala: Unafahamu Kuwa Mtu uliyemtolea Ushahidi Kama Freeman Mbowe Kuwa ni Kiongozi wa CHADEMA kama Kiongozi wa Chama Cha Upinzani
Shahidi (Tigo): Simfahamu
Kibatala: Umekuwa Wakili tangu lini?
Shahidi (Tigo): 2013
Kibatala: Bado unataka tukubali kuwa humfahamu Freeman Mbowe kama Kiongozi wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani Tanzania?
Shahidi (Tigo): Ndiyo sifahamu, Wapo wengi
Kibatala: Barua ilisema Kwamba iwe ni Siri sana Mteja asijue?
Shahidi (Tigo): Haikusema hivyo
Kibatala: Ulimtaarifu Mteja Mwenyewe kwamba Kuna Taarifa zako za Kiuchunguzi zinahitajika?
Shahidi: Hapana.
Kibatala: Kama Kampuni Mlichukua Hatua yoyote ya Kumlinda Mteja Kwa kwenda Mahakamani Kupinga au Kuandika Barua kwenda TCRA, Mlichukua hatua kama hiyo?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Hakuna Polisi Wana abuse power zao
Shahidi (Tigo): Sifahamu
Kibatala: mlichukua hatua gani kumlinda mteja?
Shahidi (Tigo): Hiyo siyo kazi yetu, Hakuna hatua tuliyoichukua kumlinda mteja
Kibatala: Mnafahamu Angalau kuwa Kuna Tasisi Mbili angalau zinahusika Kulinda Maslahi ya Mteja
Shahidi (Tigo): Ndiyo nazifahamu
Kibatala: Zitaje
Shahidi (Tigo): TCRA na FCC
Kibatala: Barua Yako uliyoitoa Mahakamani, Je Mahakama Ikitaka Kujua Kuwa nini wewe Mmiliki wa Barua, Ina angalia Wapi?
Shahidi: Kielelezo namba p6
Kibatala: Msaidie Mheshimiwa Jaji akiangalia Wapi ataona Barua hii Umesaini wewe FREDY Kapala
Kibatala: Je Uliongozwa na Wakili wa Serikali Kutoa Nyaraka Nyingine Kufanya Ulinganifu kwamba hii ni Saini yako?
Shahidi (Tigo): Sikuyatoa
Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa Hatuna sehemu ya Kulinganisha Signature Yako
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Tuchukulie Kwamba Barua Iliandikwa na Polisi na wewe hii ni Saini Yako, Je ni wapi Mheshimiwa Jaji akiangalia anaweza Kuona Barua hii Ilipita kwa Wengine Tigo kwamba Ufanye kama kwa Ku’ minute
Shahidi (Tigo): Sijaelewa
Kibatala: Unafahamu Kuwa baadhi ya Ofisi Barua inatembea na kupelekwa kwa Mhusika baada ya Kupita kwa wengine Ulimwambia Jaji kama Nyie Tigo hamna Utaratibu huu?
Shahidi (Tigo) Ningeweza Kujibu Lolote
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unakubaliana Barua Yako ya Tarehe 02 Haielei hewani Ndiyo Maana Inaviambatanishi?
Kibatala: Ni sahihi kwamba Jalada ulilonukuu wewe ni tofauti ambalo hata polisi wamekuletea?
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Ulitoa ufafanuzi wakati unaongozwa na wakili wa serikali kwamba umeulizwa barua kwa Jalada A wewe ukajibu Jalada B
Shahidi (Tigo): Hapana Sikusema
Kibatala: Twende eneo lingine, umetoa kielelezo namba P6 ni KYC. Nimesikia mnaulizana rekodi za NIDA Vs Tigo_TZ Kwa kuwa Taarifa za Freeman Mbowe zipo NIDA, ni sahihi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: kwa hiyo kimsingi NIDA ndiyo Primary Source za Freeman Mbowe
Shahidi: Haupo sahihi
Kibatala: Basi niambie Uhusiano wa Tigo na NIDA katika KYC
Shahidi (Tigo): Kwa sababu sisi tuna chukua Data Kwao kimtandao
Kibatala: Kwa hiyo utakubaliana na Mimi NIDA ni Primary Source
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Usajili wa Tigo unaweza kutambulika bila Mtu Kusajiliwa NIDA?
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Katika Ushahidi wako umezungumzia Lolote Kuhusu wewe Kusomea Mambo ya Data za NIDA
Shahidi (Tigo): Hapana Sikuzungumzia
Kibatala: Wewe unaweza Kuzungumzia suala la Server ya NIDA Kama siyo Administrator wa NIDA?
Shahidi (Tigo): Hapana
Kibatala: Kuna aina Ngapi za Server?
Shahidi (Tigo): Email Based, Data Based Server
Kibatala: Nikisema LINU server unaelewa
Shahidi (Tigo): Ndiyo naifahamu
Kibatala: Ni nini?
Shahidi (Tigo): Maelezo yake sifahamu
Kibatala: Ni Lenox au Linux
Shahidi (Tigo): Linux
Kibatala: Huku Taja Window Server
Shahidi (Tigo): Sikusema
Kibatala: SQL Server Foft ware
Shahidi (Tigo): Fost ware
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Server ni Software au Hardware
Shahidi (Tigo): Hard Ware
Kibatala: Kuna Version kadhaa za SQL Software
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Tutajie The Latest SQL version Shahidi
(Tigo): Siwezi Kujua Kwa kweli
Kibatala: Sasa aliyemtajia Jaji Mambo ya SQL fotware ulilenga nini?
Shahidi (Tigo): Kumuonyesha Jaji ni wapi nilipata Hizo Nyaraka
Kibatala: Wewe Hukutaka kabisa Jaji ajue Uimara, Uadilifu na Uimara wa hizo Software
Shahidi (Tigo): Sikumwambia
Kibatala: Je unajua The SQL Software 2019 ndiyo The best wewe utakataa?
Shahidi: SIWEZI KUJUA NDIYO MAANA NIMESEMA SIWEZI KUELEZEA HIYO
Kibatala: Kwa Maelezo yako SQL Server Mnayotumia ni ya 2015
Shahidi: Nilisema ile ndiyo nilisoma Kozi ya introduction, tume update juzi
Kibatala: Sasa ulimwambia Mheshimiwa Jaji..?
Shahidi (Tigo): Siku Mwambia Exactly
Kibatala: Hatuna Kumwambia Exactly Wanasheria
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Umeupdate Juzi?
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: VAPT ni nini?
Shahidi: NI Watu wakujaribu Umadhubuti wa mifumo
Kibatala: Kutokana na Umuhimu huo ndiyo Maana Mkawafuata Ernest & Young Taasisi Kubwa, Mmechukua Kwa ajili ya Ulinzi wa Mifumo?
Kibatala: Unafahamu DB2 software
Shahidi (Tigo): Siifahamu
Kibatala: Kwa hiyo wewe nikikwambia DB2 ndiyo madhubuti duniani kwa uwezo wake, huwezi kujua?
Shahidi (Tigo): Siwezi Kujua Kwa kweli
Kibatala: Na Unajua Kuwa SQL ni moja software ya bei rahisi duniani?
Shahidi (Tigo): Inayoweza Kununulika (affordable)
Kibatala: Unafahamu Kwamba Tigo ni Reportimg Institution
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Mlishawahi Ku’ report Mambo yasiyofahaa Kuhusu Hiyo namba za simu
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Unafahamu Kuwa PEGASUS ni SoftWare Hatari sana Duniani Kwa ajili ya Kuingilia Mawasiliano wa mtu?
Shahidi (Tigo): Hilo sifahamu
Kibatala: Makao Makuu ya Tigo yapo Karibu kabisa na Eneo la Usalama wa Taifa
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Unafahamu Kuna Pesa Za Mteja Zimeibwa Kwenye huduma ya Kibubu ya tigo, Na Mwanasheria Pacience Mlowe ameleta Demand Notes kwenu?
Shahidi (Tigo): Hapana Sifahamu
Kibatala: Nakupeleka Kwenye Detail ya Miamala ya pesa
Kibatala: Kuna Originating Number na Terminating Namba
Shahidi (Tigo): Ndiyo
Kibatala: Wewe Ulionyeshwa hapa Mahakamani Kwamba hii Ndiyo Terminating Namba.?
Shahidi (Tigo): Sikuonyeshwa
Kibatala: Unafahamu kuwa kuna Huduma ya Kurudisha Miamala?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa hiyo hatuwezi Kusema Details za kuanzia Tarehe 01.8.2020 kama tunazo hapa?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa hiyo hatujui Kama Pesa hiyo huenda mbele Ilirudishwa, Si Ndiyo
Shahidi: Ndiyo Hatujui
Kibatala kamaliza kuuliza maswali ya Dodoso.. Anasimama sasa Wakili wa Serikali Kwa ajili ya Re examination..
Wakili wa Serikali: Nitakuuliza Kwa ufafanuzi na Pole Kwa Maswali.
Wakili wa Serikali: Wakati Unaulizwa Maswali na Mawakili wasomi hasa Mtobesya kama umeiambia Mahakama kuhusiana na Watu Wanaitwa Hackers, na akakuuliza servers zinaweza Kuingiliwa na Hackers Ukajibu ni sahihi Na wakati Ulikuwa una generate Data Kama Mfumo ulikuwa Umeingiliwa
Shahidi (Tigo): Mantiki ya kuwa na Mifumo ya kulinda na Kutoa Taarifa, ni ili Mfumo wa kila wakati unapotumika Uwe Salama
Mallya: OBJECTION ni swali Jipya
Wakili wa Serikali: Nimetoa katika Maswali Mengi Labda Kama Mtobesya Mwenyewe angekuwepo
Jaji: Shida siyo Maswali shida ni Majibu
Shahidi: Wakati nafanya system hizo zilikuwa Inplace na zinalindwa na Mfumo kwa wakati wote
Wakili wa Serikali: Kama nilikuelewa Vizuri Ulikuwa Unaulizwa Kama Barua ya Polisi Ilikutaja, na Ofisi inachunguza nini
Shahidi: Kuhusiana na Tuhuma za Jinai
Wakili wa Serikali: Ambayo ni Kumbukumbu ya Nini hiyo?
Shahidi: Kumbukumbu ya Jalada
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Ulikuwa unamaanisha nini Katika kutokubadili Mfumo?
Kibatala: OBJECTION siyo Sawa wakili anachotaka kufanya
Wakili wa Serikali: Alitaka Kufafanua Maana ya convenience zile ambazo hazipo Kwenye Mfumo wa NIDA na huzipati
Wakili wa Serikali: Uliulizwa na Kibatala kuhusiana na Utambulisho Kwamba Usajili wenu Primary Source yenu ni Nida. Ukasema Kula NIDA ni ku verify
Shahidi: Ilipofika kutafuta Kitambulisho Cha Taifa sehemu Nyingi Zina Verify Taarifa za NIDA tu
Jaji: Unawasiwasi Mahakama Haijaelewa Kuhusu Conviniance?
Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Umeulizwa kwenye KYC Kuhusu Mbowe kama yuko Ukasema hayumo, ipe Mwanga Mahakama
Shahidi: Taarifa zinazoonekana zimepatika Kwenye Server Ya Tigo, information ambazo zimeandikwa Null ni zile ambazo hazipo Kwenye Mfumo wa NIDA
Wakili wa Serikali: Elezea alipokutaka Kuelezea Kuhusiana na Utofauti na Namba kumbukumbu hasa kwenye Miaka, Elezea Mahakama Haya yakijitokeza Vipi?
Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Wakati unaandika Exhibit P6 ulikuwa unajibu nini?
Shahidi: Nilikuwa na Barua Kutoka kwa kamishina
Wakili wa Serikali: alikuuliza Kibatala Endapo Kumfanyika Mfananisho wa Signature yako, Ukasema Hukuweka Ikumbushe Mahakama Uliweka Saini ya nani
Shahidi: Saini Yangu
Wakili wa Serikali:: ni wakati gani sahihi ufananishwa
Kibatala: OBJECTION swali hilo subiri wakati wa Submission
Wakili wa Serikali: Sawa
Shahidi (Tigo): Kutafuta Miamala Ya Fedha Kutoka June Mpaka July Wakati Kifungu cha 34 kinazungumzia interpretation
Matata: Mheshimiwa Jaji OBJECTION Kusema Kilikuwa Misquoted ni Fact Mpya, miye Nilisoma Barua tuh
Shahidi: Kifungu kimenukuliwa tofauti na kile ambacho Barua Imetoka Reqiest
Wakili wa Serikali: umelitoa wapi, exhibit gani hiyo
Shahidi: P07
Wakili wa Serikali: Ilikutaka Kufanya nini
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji, Naomba Wakili Chavula ana maswali Kadhaa ya kuuliza
Wakili wa Serikali:: Ulikuwa Unaulizwa Kuhusu Cyber Act Kuhusu Kifungu 34 na 36 Hii report yako Ilikuwa kwa ajili ya Trafficking, Fafanua sasa Relevance ya vile Vifungu kile Ulichoombwa Kufanya
Shahidi (Tigo) Niliombwa Kutoa taarifa ya Miamala Kutoka June Mpaka July nisingeweza Kwenda zaidi ya Hapo
Shahidi (Tigo): ni Kwa sababu NIDA hawana Majina ya Trama Leader na wala Watu wanaosajili kutoka kwetu
Wakili wa Serikali: Shahidi ieleze Mahakama kuhusu pesa hizo kama zilirudishwa kwa aliyetuma….. Kwani wewe Kwa Mujibu wa Kielelezo Cha Mahakama uliombwa Kufanya nini?
Wakili wa Serikali: Tufafanulie katika hicho Kielelezo Imejitokeza Kwamba KYC Hakutaja Jina la Aliyemsajili Freeman Mbowe
Shahidi: Sijaelewa Swali
Wakili wa Serikali:: Tufafanulie katika hicho Kielelezo Imejitokeza Kwamba KYC Hakutaja Jina la Aliyemsajili Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Maneno City Kuna Kilimanjaro, District Kinondoni na Region ni Dodoma hebu ifafanulie Mahakama
Shahidi (Tigo): NI Classification yetu sisi
Wakili Malya: OBJECTION hiyo ni New Fact
Wakili wa Serikali: Hatuoni hapo Kama Kuna Jambo Jipya
Wakili wa Serikali: Mimi kwa Uelewa Wangu Kitu kinachotakiwa Kuwa Objected ni Maswali tu siyo Majibu Shahidi anaweza Kuongea Kitu Jipya, hawezi Kuongea Maneno yaleyale
Wakili wa Serikali: Chavula Kwa kuongeza tutazame Kifungu Kidogo ha 147 cha Sheria ya Ushahidi Maswali yetu yakijielekeza Kwenye yaliyojili kwenye Cross examination Na kazi yetu nikufukia Mashimo yaliyojitokeza Kwenye Cross Examination Tunaomba Shahidi wetu apewe Nafasi ya Kufafanua
Jaji: Ninaona ni kitu Jipya kwa hiyo na kubaliana na Maoni ya wakili Malya Unaweza Ukalitengeneza Ukauliza Kivingine
Jaji: Wote tunakubaliana Hairuhusiwi Kufanya Mambo Mapya kwenye Re examination kwa sababu utatoa Fursa ya Upande wa pili Kurudi tena Ninachokiona mimi hapa tunabishana Kama Jambo ni Jipya au lilikuwa mwanzoni
Wakili wa Serikali: Kwenye City inaonekana Kilimanjaro na Kwenye Region panaonekana Dodoma na Kuna District Kinondoni
Shahidi (Tigo) Hizo ni Permanent Adress na Zingine ni Temporary Adress nadhanu niishie hapa
Wakili Malya: Mimi Siku uliza Mambo ya Adress anachokileta ni Kitu Kipya, aseme kama Ilivyo Kilimanjaro City
Jaji: Wote tunakubaliana ni Jukumu la Mahakama Ku’ Control Process Wote tunakubaliana Jambo la Kuleta Mashahidi
Wakili wa Serikali: Sheria haikudhamiria kubana shahidi kuongea Hapa, Lakini si kuzuia kuongelea masuala walioyaibua wao Mheshimiwa Jaji Kwa mfano hapa hakuna sehemu Kinondoni kwenye Kilimanjaro Sisi tunaona basi bora tunyimwe kabisa haki hii Ni hayo tu, lakini nakaa kwa hasira.
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naona Wenzetu Wameibua Malalamiko na wanaelekeza Kwa Mahakama Wakili wa Serikali Kwanza Aondoe hilo, Hakuna anayelalamika sisi tumeleta Hoja
Kibatala: hii Statue inatoa Jibu, imesema Question and Answers lakini kwenye hili wameita Re-examination
Jaji: Akielekeza Majibu ambayo hayaibui Maswali Mapya tunayapokea. Na Shahidi Mpaka Sasa Kajibu mambo Mengi. Na suala la Msingi hapa Shahidi ajielekeze Kwenye Kutoleta Mambo Mapya Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana Jaji.
Wakili wa Serikali: Chavula Mheshimiwa ni hayo tuh Sina Cha Ziada
Jaji: Eneo hili limeleta Maswali Mengi na Mkanganyiko
Wakili wa Serikali: Shahidi Kwanini Kwenye exhibit P9 kuna Kilimanjaro City huku hakuna Kilimanjaro City
Shahidi: Tuseme Kwa Urahisi Ndiyo Inavyo kuwa Lebelled Kwa Upande wa Kuandika hizo Data
Wakili wa Serikali: Na Kilimanjaro kuna Wilaya inaitwa Kinondoni lakini Kwenye Exhibit, Kuna Region Imeandikwa Dodoma
Shahidi (Tigo): NI sehemu Tatu Tofauti
Jaji: Nina swali Moja tuh Je hizi Taarifa ambazo Zimeleta Mkanganyiko Sorce yake ni wapi?
Shahidi (Tigo): NIDA
Jaji na wewe Sasa unaweza Kuzisemea
Shahidi (Tigo): Zikiwa Upande wetu, zinakuja Kwa Mteja kama Mmiliki baada ya Finger prints
Jaji: Nakushukuru Kwa Ushahidi Wako
Wakili wa Serikali, Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Hairisho Mpaka kesho tarehe 3 ilituweze kuendelea na usikilizwaji wa shauri hili
Jaji: Utetezi
Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi kwenye hili
Jaji anaendelea kuandika
Jaji: Maombi ya hairisho yamekubaliwa na Shauri linairishwa Mpaka kesho tarehe 3. Upande wa Mashitaka mnaamriwa Kuleta Mashahidi. Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande Mpaka Kesho saa 3 Asubuhi. Jaji anatoka.