Kesi ya Mbowe: Shahidi ajichanganya, adai ana tatizo la kukumbuka

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, kutoka mahakamani leo tarehe 01 Novemba 2021.

Mawakili,watuhumiwa na Mawakili wa Serikali wameshaingia Mahakamani

Muda wowote Kesi itaanza

Jaji ameingia sasa Saa 4 na Dakika 06

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa.

Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo lake

WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando anawatambulisha,

Pius Hilla
Abdallah Chavula,
Jenitreza Kitali,
Nasorro Katuga,
Esther Martin,
Ignasi Mwinuka na Tulimanywa Majige

WAKILI PETER KIBATALA Nawatambulisha Mawakili Wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
Michael Mwangasa
Seleman Matauka
Nashon Nkungu
Alex Massaba
Michael Lugina
Maria Mushi
Hadija Aron
Dickson Matata
Jonathan Mndeme
Fredrick Kihwelo
John Malya

Jaji awaita Washitakiwa 1,2,3 na 4.
Wanasimama Kuitikia

WAKILI WA SERIKALI: Kwa Upande wetu tuna shahidi Mmoja kwa Leo na tupo tayari Kuendelea Kwa Upande wetu tupo tayari kuendelea

Mahakama Ipo Kimya Kidogo

Shahidi anapita ni Mdada Kajitamda Buibui na Kavaa Baraka Kubwa sana Kumziba Sura,
JAJI: Majina Yako

SHAHIDI: Anita Varelian Mtali
JAJI: Umri?

SHAHIDI: 45yrs

JAJI: Kabila?

SHAHIDI: Mchaga

JAJI: Shughuli Zako?

SHAHIDI: Nafanya Biashara

JAJI: Dini yako?

SHAHIDI: R. C

Shahidi Naapa Mbele ya Mahakama hii Kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni kweli, kweli tupu Eeeh Mungu nisaidie.

Wakili wa Serikali Robert Kidando Shahidi Ataongozwa na Wakili Esther Martin

WAKILI WA SERIKALI Esther: Ikumbushe Mahakama Majina yako?

SHAHIDI: Anita Varelian Mtali

WAKILI WA SERIKALI: Unaishi Wapi?

JAJI: Jina lako la Tatu sijalipata Vizuri ni Mtali.?
SHAHIDI: Moshi, RAU madukani

SHAHIDI: Mtaro

WAKILI WA SERIKALI: Umeishi kwa Muda gani Rau?
SHAHIDI: Miaka 08

WAKILI WA SERIKALI: Unafanya Shughuli gani?

WAKILI WA SERIKALI: Ulianza lini Biashara yako ya Mbege?

SHAHIDI: Nafanya Biashara ya Kuuza Mbege

SHAHIDI: Miaka 08 nayo

WAKILI WA SERIKALI: Mbali na Biashara yako ya Mbege unabishara gani Nyingine?

SHAHIDI: Kuna Grocery, Stationary, Banda la Tigo Pesa na Kuna Sehemu ya Kutolea Muvi

WAKILI WA SERIKALI: Iambie Mahakama 05 Mwezi 08 2020 ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Sehemu yangu ya Biashara Nikifanya Usafi

WAKILI WA SERIKALI: Saa ngapi?

SHAHIDI: Saa Saba Kasoro

WAKILI WA SERIKALI: Ya Muda gani?

SHAHIDI: Ya Mchana

SHAHIDI: Nilikuwa Nimetoka Nyumbani Nikaenda Saloon Kutosha Nywele

WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya Kufika eneo lako la Biashara ulikuwa umetoka wapi? Na Ulipotoka Saloon kuelekea sehemu yako Kufanya Usafi

SHAHIDI: nilikuta Wakaka Watatu walikuwa wamekaa Mbele Yangu walikuwa wanakunywa na Kusajili Laini

WAKILI WA SERIKALI: Walikuwa wanakunywa nini?

SHAHIDI: Walikuwa wanakunywa Bia

WAKILI WA SERIKALI: Hizo laini walikuwa wanasajili wapi?

SHAHIDI: Kuna Vijana wanapitaga Mitaani Kusajili Laini

WAKILI WA SERIKALI: Ukiwa unafanya Usafi kitu gani Kingine ulishuhudia?

SHAHIDI: Kuna wakaka wawili walikuwa wanapitapita waki ongea na simu. Wanaenda wanarudi waki ongea na Simu

WAKILI WA SERIKALI: Hao wanaopita ni tofauti na wale uliposema walikuwa wanakunywa Bia?

SHAHIDI: Hapana ni walewale

WAKILI WA SERIKALI: Kutoka Kwako Unapofanyia Kazi Mpaka Glocery ni Umbali gani?

SHAHIDI: Kama Hatua 10

WAKILI wa SERIKALI Hapo katikati sasa Kati ya Glocery na ulipo pana kitu gani?

SHAHIDI: Pana uwazi

WAKILI WA SERIKALI: wa Serikali Baada ya Muda kitu gani kilitokea?

SHAHIDI: wakati wanaongea na Simu Walitokea watu wawili wa Kaongea kwa sauati kali “Mpo chini ya Ulinzi Mnahusika na Mambo ya Kigaidi, chuchumaa Chini Mikono Juu”

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani Kingine ulisikia?

SHAHIDI: Chuchumaa Chini Mnahusika na Mambo ya Kigaidi

WAKILI WA SERIKALI: Ni watu gani sasa hao?

SHAHIDI: Ni Askari

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa unafanya nini wakati huo?

SHAHIDI: Nafanya Usafi

WAKILI WA SERIKALI: Pana umbali gani kutoka Walipo Mpaka Ulipokuwa unafanya Usafi?

SHAHIDI: Hatua 05

WAKILI WA SERIKALI: ulisikia nini Kingine?

SHAHIDI: Sikusikia Kingine zaidi ya Chuchumaa Chini Nyoosha Mikono Juu

WAKILI WA SERIKALI: Walikuwa Askari wangapi?

SHAHIDI: Wawili

WAKILI WA SERIKALI: Hali ya Pale ilikuwaje

SHAHIDI: Ilikuwa ni Utulivu

WAKILI WA SERULALI: Nini Kilifuata?

SHAHIDI: Walitokea Askari Wengine watatu wakawa wamefika eneo la Tukio

WAKILI WA SERIKALI: Ongeza Sauti

SHAHIDI: Baada ya Kuwa Askari watano alitokea Mmoja akaniambia anaomba nisogee anahitaji Kuwafanyia Upekuzi

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani Kiliendelea?

WAKILI wa SERIKALI: Ni Askari gani huyo

SHAHIDI: alinitambulisha anaitwa Askari Polisi Jumanne

WAKILI WA SERIKALI: Ulifanya nini kujiridhisha?

SHAHIDI: Alitoa Kitambulisho Akanionyesha

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hapo nini kilifanyika? Kabla ya Kumsimamisha..?

SHAHIDI: Alimsimamisha Mmoja

SHAHIDI: Afande Jumanne alijipekua kuanzia Kifuani akatoa Mifuko Nje

WAKILI WA SERIKALI: We ulikuwa na nani wakati huo?

SHAHIDI: Dada Mmoja anaitwa Esther

WAKILI WA SERIKALI: Kutoka Eneo la walioambiwa Wachuchumae Chini, palikuwa na Umbali gani?

SHAHIDI: Kama Hatua Mbili

WAKILI WA SERIKALI: Kuna Kitu gani Kingine

WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya Raia Kusogea eneo hilo palikuwa na hali gani?

SHAHIDI: Raia walikuwa wamekuja

WAKILI WA SERIKALI: Aahaa ahaaa yani hali ya pale ilikuwaje?

SHAHIDI: Palikuwa na jua

SHAHIDI: Palikuwa pametulia

WAKILI WA SERIKALI: Ikaendelea nini?

SHAHIDI: Alimsimamisha Mmoja akamuuliza Unaitwa nani

WAKILI WA SERIKALI: Akajibu anaitwa nani?akamwambia nini?

SHAHIDI: Adam Kasekwa?

SHAHIDI: Akiwa amenyoosha Mikono Juu akamwambia Geuka, akageuka

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya Kugeuka?

SHAHIDI: Askari Jumanne alianza Kumpekua Kuanzia Kichwani, Mabegani, Alipofika Kiunoni alikuta Kitu kigumu

WAKILI WA SERIKALI: alikikuta Upande gani?

SHAHIDI: Kushoto

WAKILI WA SERIKALI: Maeneo Gani?

SHAHIDI:kushoto.Niliona ni Bastola

WAKILI WA SERIKALI: Ulijuaje kama ni Bastola?

SHAHIDI: Afande Jummane alituambia ni Bastola

WAKILI WA SERIKALI: Halafu?

SHAHIDI: Akatuonyesha namba

WAKILI WA SERIKALI: Zilikuwa ni namba gani.?

SHAHIDI: A5340

WAKILI WA SERIKALI: Zilikuwa kwenye nini?

SHAHIDI: Kwenye Bastola

WAKILI WA SERIKALI: i wakati anakuonyesha Bastola Adam alikuwa wapi?

SHAHIDI: Alikuwa amesimama

WAKILI WA SERIKALI: Ukaona na nini Kingine? nini kiliendelea

SHAHIDI: Risasi 03

SHAHIDI: Akaendelea na Upekuzi

SHAHIDI: Alipofika Upande wa Kulia akakuta Vitu vidogo vidogo Kwenye Karatasi ya Nailon akasema inasadikiwa na a Madawa ya Kulevya ila itajulikana Mbele

WAKILI WA SERIKALI Zilikuwa ngapi?

SHAHIDI: 58

WAKILI WA SERIKALI: Ikawaje?

SHAHIDI: Aliendelea Kumpekua akamkuta na Simu Ndogo aina ya Itel

WAKILI WA SERIKALI: hiyo simu akaifanyeje

SHAHIDI: itel, akatoa laini akakuta namba akaziandika

WAKILI WA SERIKALI: baada ya hapo aliendelea na nini?

SHAHIDI: Akamwambia Naomba fomu, akaleta fomu

WAKILI WA SERIKALI: Fomu ngapi?

SHAHIDI: Zilikuwa Mbili

WAKILI WA SERIKALI: akafamya nini sasa Kwenye ile Fomu?

SHAHIDI: Akaandika Vitu alivyokuwa amempekua

WAKILI WA SERIKALI: Umesema palikuwa na fomu Mbili, fomu ya kwanza akijaza nini?

SHAHIDI: Fomu ya kwanza alijaza Bastola, Risasi na Laini

WAKILI WA SERIKALI: Zilikuwa ni laini gani?

SHAHIDI: Laini ya Voda na Airtel

WAKILI WA SERIKALI: baada ya Kumalizia fomu ya kwanza? Kabla ya Kujaza Fomu Nyingine?

SHAHIDI: Alichukua fomu Nyingine. alipo maliza Kujaza akampa akasaini na Baadae akasaini yeye alipo maliza Kusaini…

WAKILI WA SERIKALI: alimpa nani?

SHAHIDI: Alimpa Adam

WAKILI WA SERIKALI: baada ya fomu ya kwanza nini kiliendelea?

SHAHIDI: alichukua Fomu Nyingine

WAKILI WA SERIKALI: alijaza nini?

l SHAHIDI: Alijaza vile Vikete vidogo Vidogo

WAKILI WA SERIKALI: Vingapi Vilikuwa Vingapi?

SHAHIDI: Vilikuwa 58

WAKILI WA SERIKALI: baada ya hapo?

SHAHIDI: Akampa Adam asome alafu asaini na sisi akamtupa tusaini

WAKILI WA SERIKALI: Wewe na nani..?

SHAHIDI: Mimi na Dada Esther

WAKILI WA SERIKALI: Baada Kumalizia nini kilifuata

WAKILI WA SERIKALI: Huyo Mwingine anaitwa nani?

SHAHIDI: Akamuita Mwingine

SHAHIDI: Mohamed Abdulahi Ling’wenya

WAKILI WA SERIKALI: akamwambia nini?

SHAHIDI: asimame ageuke. Baada ya kugeuka akaanza Kumpekua

WAKILI WA SERIKALI: alianzaje Kumpekua?

SHAHIDI: Kichwani Mikononi

WAKILI WA SERIKALI ilikuwaje?

SHAHIDI: Upande wa Kulia alikuta na Vikete Vidogo Vidogo

WAKILI WA SERIKALI: Vilikuwa vingapi? akafanyeje?

SHAHIDI: 25. Akavishika Akaendelea Kumpekua

WAKILI WA SERIKALI: alikuta Vitu gani pia?

SHAHIDI: alikuta Simu aina ya Tecno

WAKILI WA SERIKALI: Rangi gani?

SHAHIDI: Nyeusi

WAKILI WA SERIKALI: akafanya nini?

SHAHIDI: akapekua akakuta kuna laini

WAKILI WA SERIKALI Laini gani?

SHAHIDI: halotel

WAKILI WA SERIKALI: baada ya Kupata simu akafanyeje?

SHAHIDI: Akazitoa zile Laini,akampa yule Mwingine akazishika,akaendelea na Upekuzi

WAKILI WA SERIKALI: Na Yeye Akaendelea na nini? hizo laini alikuwa anafanya nazo nini?

SHAHIDI: Alimpa Askari wa Pembeni akazishika

WAKILI WA SERIKALI: baada ya Upekuzi?

SHAHIDI: aliendelea na Upekuzi lakini hakukuta kitu Kingine

SHAHIDI: aliomba fomu Mbili

WAKILI WA SERIKALI: fomu ya Kwanza alijaza nini?

SHAHIDI: alijaza vile Vikete Vidogo Vidogo

WAKILI WA SERIKALI: Vilikuwa Vingapi?

SHAHIDI: 25

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hapo?

SHAHIDI: Alimpa akasema asaini

WAKILI WA SERIKALI: Nani Yeye afande Jumanne?

SHAHIDI: Ndiyo na Baadae Mohamed

WAKILI WA SERIKALI: na baadae

SHAHIDI: tukasaini sisi

WAKILI WA SERIKALI: Wewe na nani? Baada ya hapo?

SHAHIDI: Mimi na Dada Esther

SHAHIDI: Ile fomu Nyingine akajaza Simu na laini Nyingine

WAKILI WA SERIKALI: Za Mtandao gani?

SHAHIDI: Airtel na Hallotel

WAKILI WA SERIKALI baada ya hapo?

SHAHIDI: Alimpa Mohamed asome kisha akasaini

WAKILI WA SERIKALI: baada ya hapo?

SHAHIDI: afande Jumanne alituomba na sisi tusome Kisha tusaini

WAKILI WA SERIKALI: Wewe na nani?

SHAHIDI: Mimi na Dada Esther

WAKILI WA SERIKALI: baada ya Upekuzi?

SHAHIDI: walivalishwa Pingu

SHAHIDI: afande Jumanne akatuomba tuelekee Kituoni

WAKILI WA SERIKALI: baada ya hapo?

WAKILI WA SERIKALI: Hao walivalishwa Pingu walikuwa ni akina nani?

SHAHIDI: Adam na Mohamed

WAKILI WA SERIKALI: baada ya kuvalishwa Pingu..?

SHAHIDI: wakielekea kwenye Magari Barabarani

WAKILI WA SERIKALI: palikuwa na Askari wangapi?

SHAHIDI: watano

WAKILI WA SERIKALI: Walikuwa wamebeba nini?

SHAHIDI: walikuwa wamebeba bunduki

WAKILI WA SERIKALI Hali ya hewa eneo lile ilikuwaje?

SHAHIDI: ilikuwa imetulia. Kilikuwa na Jua na Mwanga

WAKILI WA SERIKALI: Mlichukua Muda gani kwenye lile eneo Mpaka Mnamaliza Zoezi

SHAHIDI: Kama Dakika 45

WAKILI WA SERIKALI: sasa bada ya Kumalizia Mkaelekea kituoni, kituo gani..?

SHAHIDI: Central Moshi

WAKILI WA SERIKALI: baada ya a Kufika police central?

SHAHIDI: Tuliandika Maelezo

WAKILI WA SERIKALI: Sasa fomu ukiziona hapa utaweza Kuzitambua?

WAKILI WA SERIKALI: baada ya Kufanya Upekuzi Kuna Vitu Vilipatikana na Kwamba Kuna fomu zilijazwa

WAKILI WA SERIKALI: Tukianza na fomu ya Adam utaitambuaje

SHAHIDI: Kwa vitu vilivyoa andikwa, Jina langu na sahihi yangu

WAKILI WA SERIKALI: Kukikuwa na nini Kingine Bastola

WAKILI WA SERIKALI: Kingine?

SHAHIDI: Palikuwa na Risasi

WAKILI WA Serikali namba gani?

SHAHIDI: A5340

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba nimpe fomu aweze Kuitambua

WAKILI WAa SERIKALI: Shika hii Karatasi iangalie kwa Makini

SHAHIDI: Ndiyo yenyewe

WAKILI WA SERIKALI: Yenyewe nini

SHAHIDI Fomu niliyo saini

WAKILI WA SERIKALI: Umeitambuaje?

SHAHIDI: Kwa Jina langu na Sehemu niliyosaini

WAKILI WA SERIKALI: Jina lipo wapi, Ni Jina gani?

SHAHIDI: Anita Valerian Mtaro

WAKILI PETER KIBATALA: ALICHOKIFANYA DADA YANGU ESTHER HAIRUHUSIWI, ANAKWEMDA KWENYE DETAILS

WAKILI WA SERIKALI: Ungependa hii fomu ipokelewe Mahakamani

WAKILI WA SERIKALI: Sawa naondoa hilo swali

SHAHIDI: Ndiyo

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba Fomu ipokelewe

JAJI: Wakili wa Mshtakiwa wa kwanza

MTOBESYA:HATUNA PINGAMIZI?

MALLYA: Hatuna Pingamizi

FREDRICK KIWHERO: kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu hatunapingamizi

PETER KIBATALA: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne hatuna Pingamizi

JAJI: anaandika Kidogo

JAJI: Mahakama inaipokea kwa ID 1
Tuanze na Bastola

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi pia ulisema kwenye huo Upekuzi pana Bastola na Risasi unaweza hapa Mahakamani ukavitambua

SHAHIDI: Ndiyo nitavitambua

SHAHIDI: Kwa Namba A5340

WAKILI WA SERIKALI: Bastola unazitambuaje

WAKILI WA SERIKALI: na Kwa Upande wa Risasi

SHAHIDI: namtambua zilikuwa na Rangi ya Dhahabu

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji Naona Exibit nimuonyeshe Shahidi

Afisa Wa Mahakama a nafungua Baasha ya Kaki,Anamkabidhi WAKILI WA SERIKALI.

WAKILI WA SERIKALI: Hebu Kingalie hiki kitu hapa, Iambie Mahakama ni nini

Shahidi anaingilia bila Kushika

SHAHIDI: ni Bastola

WAKILI WA SERIKALI: ambayo Imetoka wapi?
SHAHIDI: Imetoka Kwa Adam

WAKILI WA SERIKALI: Uliona wapi?

SHAHIDI: iliyotoka kwa Adam

WAKILI WA SERIKALI: ni Kitu gani Kilichokufanya ukagundua

SHAHIDI: kwa namba

WAKILI WA SERIKALI: Namba gani?

SHAHIDI: A5340

WAKILI WA SERIKALI: Umeeleza pia ulishuhudia Upekuzi wa watu wa wili ambao kwa Majina yao ni Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya, Je ukiwaona unaweza Kuwatambua?

SHAHIDI: Naweza Kuwatambua

SHAHIDI: Wapo hapa Mahakamani

WAKILI WA SERIKALI: Wapo hapa Mahakamani?

WAKILI WA SERIKALI: Wapo wapi?

WAKILI WA SERIKALI: Mohammed amevaa Tshirt ya Amevaa Meupe Kijani na Nyeusi

SHAHIDI: hapa Mbele

WAKILI WA SERIKALI: na Adam yupo wapi?

SHAHIDI: amevaa Shati lenye Rangi Nyeupe Nyeupe

WAKILI WA SERIKALI: Yupo wapi hapa Mahakamani

SHAHIDI: Yupo pale

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu

JAJI: upande wa Utetezi

MTOBESYA: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

MTOBESYA: naomba Nipatiwe ID 1

MTOBESYA: Shahidi umeomba Mahakama Ipokee Kielelezo hiki
Mahakama Inampatia
Onyesha Sehemu ipo saini

SHAHIDI: Nimesaini hapa

MTOBESYA: Kwa Ushahidi wako Unasema ulisaini Nyaraka ngapi

SHAHIDI: Nne

MTOBESYA: na Ushahidi wako kwamba Sahihi zako Lote zinafanana

MTOBESYA: Naomba kwa Kifungu 75(1) Sheria ya Ushahidi, Shahidi asaini tena sehemu Nyingine ili Mahakama iweE Kufananisha Saini zake

JAJI: unaweza Kutusomea.?

JAJI: hicho Kifungu kinaitaka Mahakama shahidi asaini ili iweze Kufanya ufafananisho

MTOBESYA: anasoma Kifungu cha 75(1) cha Sheria ya Ushahidi

MTOBESYA: Ndiyo ili Mahakama iweze kufananisha, kwa sababu tuna Nyaraka Nyingine inadaini yake tofauti

JAJI: lakini hiyo Nyaraka itakuwa imetengenezwa hapa
Utakuwa aumeiiingiza Mhakama Kwenye Kutafuta Ushahidi
Unaingiza Mahakama Kwenye Jukumu la Ku Collect Ushahidi

JAJI: Bwana Matata unajambo la Ku she a na sisi
Labda Utumie hiyo Nyaraka Nyingine kama Upande wa Pili watatu Object Tutaona. Matata Sheria Anayosoma Wakili Mtobesya Ni Sheria inasema kuwa Shahidi anaweza kuandika sehemu tuh 75(2) Mahakama inaweza Kuagiza Mtu yoyote Mahakamani Kulingananisha

JAJI: Je hiyo inahusiana na Mahakama kumuelekeza Shahidi asaini
Matata ni tafisi yangu kuwa Mahakama Inaweza Kuruhusu Shahidi Kuandika ili Kufananisha Kama alichokiandika ni sawa

Wakili Mallya: pale kwenye 75(2) inasema any Documents aijambana wapi kwahiyo anaweza Kusaini popote (any documents) ili Mahakama ifanye Uamuzi iwe imepata kwa Usahihi wake

JAJI: upande wa Mashitaka

WAKILI WA SERIKALI: Maombi ya Mtobesya Pamoja na Kuegemea kutoka kifungu 75 cha Sheria ya Ushahidi tunaona amekimbia Sana na siyo wakati wake.
Lakini pangekuwa na Nyaraka Nyingine ambayo Ndiyo Ingekuwa imekuja Rasmi Mahakamani ndipo angetumia kwa usahihi Kifungu cha 75 lakini siyo kwa Kumtaka Shahidi aandike
Najiuliza kama Njia yako ya Kutaka shahidi Asaini Ni sahihi?

JAJI: Kwa tafsiri yangu Mamlaka iliyopewa Mahakama 75(2) ni naona Mahakama inayo Mamlaka kumuelekeza Mtu yoyote Kufanya Mlinganisho wa Maneno au Namba kwa Nia ya Kuiwezesha Mahakama Kufanya Ulinganisho, ila huyu Mtu aliye na amaarifa Kuliko Mahakama Yenyewe.
Ka watapinga tuta Shughulikia Kupinga huko wakati huo

MTOBESYA: Kifungu cha 47 cha Sheria ya Ushahidi ndiyo kinaruhusu Maoni ya Kitaalamu katika Ushahidi
Lakini Kifungu cha 48 au 49 Sikumbuki Vizuri kinaruhusu hata mtu asiye Mbobezi Kufanya Maoni yake
Hili Kifungu cha 75 chenye we Kinataka Mahakama Kufanya Ulinganisho
Leo nilikuwa na Avoid Upande wa Utetezi Kutuzuia Kutumia Nyaraka hii ambayo sisi tumeipata kwenye Comito

JAJI: Na Mimi na kubaliana na wewe
Lakini kwenye Document uliyonayo hatujui baada ya Kumkabidhi Karatasi at asaini Sahihi gani kati ya hizo Mbili

JAJI: Ndiyo nasema wewe endelea na Jukumu lako kama Walitokea Wakapinga tuta Shughulikia Pingamizi hilo wakati huo

Mtobesya: Asante Mheshimiwa Jaji

MTOBESYA: naomba nikabidhi we Nyaraka Original ya Hati ya Kuchukua Mali iliyosainiwa tarehe 25 2020 inayomhusu Mohamed Ling’wenya
Kwa sababu sisi tunayo Moja

JAJI: chini ya Sheria Gani
Kifungu cha 246 na 146 ya Makosa ya Jinai na Sheria ya Ushahidi wa Kifungu cha 75.
Vyote Vinafanya washitakiwa Kupewa Nyaraka zinazokusudiwa Kutumika dhidi yao kwenye Makosa Makubwa Kama haya kupitia Comito. Kwa hiyo watupatie

JAJI: Jamani Mmelewa?

WAKILI WA SERIKALI: Sisi Haija yetu ni Swala la Procedure
Hakuna mahala popote ambapo Mteja wake anaweza Kuwa na haki ya kutumia Nyaraka hizo.

Ni kweli Tulianika Ushahidi Tutaokuja kutumia Mahakamani lakini ieleweka Kuwa Ushahidi hi ni Wa Kwetu.
Angetoa basi Maombi Rasmi lakini hata kama no Original haiwezi kuitumia kwa wakati huu
Haki yake ya Kuhoji aendelee nayo na anaweza Kuitumia hata sasa.
Sisi tuna tatizo na Procedure jinsi gani Ushahidi huu unataka Kuletwa Mahakamani
Mheshimiwa Jaji tunatakiwa tuzingatie Mfumo wetu wa Utoaji haki, Mahakama kwa Kutimiza Wajibu wake anakuwa ni refa na siyo kwa kukaribishwa Kutaka Kufanya Uchunguzi
Zoezi kama hilo ni Kuingiza Mahakama katika riski ambazo zinaweza Kuepukika

KESI YA buying wa John dhidi ya Jamuhuri criminal appeal namba 450 ya Mwaka 2017 Mahakama iliyoketi Shinyanga Katika Ukurusa wa 11 paragraph ya Mwisho ya a Ukurasa huo wa 11
Ambapo swala Lililojitokeza tangu wakati wa Trial Court na Kesi Ilikuwa ni ya Ubakaji

Ubishi ulikuwa kama Mshitakiwa Alikuwa ametahiriwa au haja tahiriwa
Mahakama ya Rufani ikasema kuwa Hilo no Kubwa sana Kwake na Isingeweza Kujiingiza katika Risk
Kwa kesi hii basi Kama anataka Mahakama Ijiridhishe
Swala ni Kama Nyaraka hiyo imepokelewa na Kama imekubali imeandikwa na Mtu huyu
. Na pia kama Nyaraka hiyo Nyingine kama Ingekuwa hapa angekuwa na Haki
Sisi tunaona ni Kukiuka Procedure na a Maombi hayo tunaomba uyakate Mheshimiwa jaji

Na sijui ni wakati gani tena sisi tutapata Kuwa na wasaa wa kuwa na Shahidi huyu

Nashon Nkungu Naona nisaidie Mahakama kama Afisa wa Mahakama alichosema Wakili Robert Kidando Amejieleza Kwenye Kifungu cha 76 tuh asemi kwa nini kuna Haki ya Kukabidhi wa Nyaraka za Comito
Na Hilo Ndiyo Dhumuni la Comito Trial kwamba Mshitakiwa ajue anachokuja akujitetea nacho
Na Kingine Kifungu 30 cha Sheria inasema tupewe Copy siyo Photocopy na hapa swala la Copy kwa Washitakiwa halijazungumziwa wakati ni Haki kwa Mshitakiwa Kupatiwa Hiyo Nyaraka

MTOBESYA: naam Mheshimiwa Jaji

JAJI: hoja zako ulizijenga katika Mazingira Matatu
1.Haki za Mahakama Jinai hasa akatika Mahakama Kuu, amtu anasomewa na Kukabidhi wa Nyaraka,
Ambapo wewe Umegundua Sahihi Katika Nyaraka hizo na Zilizopo hapa Mahakamani Sahihi zinatofautiana. Kwamba wewe Unataarifa Kwamba zipo Nyaraka wanazolemga kuzitumia Kama Ushahidi Wao. Kwa Maana hiyo Ukaomba Mahakama ikupatia Nakala halisi

JAJI: Jambo la Pili Kwakuwa wanasema Ushahidi huo watautumia basi Waurumie Mapema ili uweze Kuutumia

MTOBESYA: Mahakama I kisha fanya Mlinganisho naurejesha Miye nataka Mahakama I nukuu Kama Palikuwa na Mlinganisho na Kwamba Mahakama Iamue kwa Kuzingatia Mlinganisho huo Jaji: nafikiri Niwape nafasi ili niweze Kurekodi mnachozungumza ili niweze kutoa Maamuzi

MTOBESYA: Mheshimiwa nilikuwa naomba Mashauriano na Mahakama ilitusiiipe Mahakama Mzigo wa a kuandika Rulling

JAJI: mnasemaje Jamuhuri?

WAKILI WA SERIKALI: Ni Sawa Mheshimiwa

JAJI: Basi tuta Break kwa Dakika 10,tukutane pande zote pale Ofisini
Jaji anatoka

Watu wamayanyuka saa 5 na Dakika 48 tutarudi na Dakika 58.

BAADA YA BREAK

Jaji ameingia tena Saa 6 NA Dakika 24

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 natajwa tena Ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe

Kisha Mahakama Kimyaaaaaa

JAJI: Muda Mfupi Uliopita Tulibreak kwa Nia ya Kuweka Sawa Mambo ya Kitaaluma.

Baada ya Kuyaweka Sawa na Kualika Sasa Mtobesya Kuendelea

MTOBESYA: Wakati Unaongozwa na Dada Yangu Esther Ulisema Uliandika Maelezo?

SHAHIDI: Niliandika Tarehe 05 Mwezi 08 2020
MTOBESYA: aliyeandika Maelezo yako?

SHAHIDI: anaitwa Jumanne

SHAHIDI: Sijui Jina lake

MTOBESYA: Ulishawahi Kukutana na Askari anaitwa Detective Coplo Francis.?

SHAHIDI: Sikumbuki Kukutana naye

MTOBESYA: Lakini walikupa Maelezo Ukayioma na Ukaona sasa Kisha Ukasoma?

SHAHIDI: ndiyo

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji naomba Nipewe Statement (Handwritten Statement)
Naomba Chini ya Kifungu Cha 164 (1h) cha Sheria ya Ushahidi

Wakili wa Serikali Wapo Kimya Jaji anawasubiri

WAKILI WA SERIKALI Robert Kidando: Hatuna Pingamizi la Kumpatia hii Nyaraka

JAJI: Pokea

MTOBESYA: Shahidi Unajua Kusoma na Kuandika?

SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: Shika Karatasi zipo Mbili, Soma kama Ndiyo Uliyosoma Ukasaini na Kama Kuna Majina yako na Askari aliye andika. Ihakiki Kwanza

SHAHIDI: Anaipekua, anaikazia Macho anafunua funua mara Nyingiyingi

Mtobesya Ndiyo hiyo.?

SHAHIDI Kimyaaaa anatizama tena ile Karatasi, anaipekua

SHAHIDI: Ndiyo Yenyewe

MTOBESYA: Soma Kuanzia Juu Kwa Sauti
SHAHIDI: Mimi Ndiyo Mwenye Majina na anuani takwa hapo Juu, Mkazi Wa Kilimanjaro.Familia ya watoro
Nimezaliwa Mwaka 1979
Watoto 10
Ninawatoto 10
Na baada ya Kumalizia nilieleza Sehemu yangu ya Biashara Kufanya Usafi
Nilikuwa naelekea Saloon Rau Madukani
Mbele Kuna Bar. Na Kukikuwa na Vijana walikuwa wanakunywa Pale
Kwa Maana walikuwa ni wageni
Sikuwa nawafahamu

MTOBESYA: Soma Kote

SHAHIDI: Kwa Muda Mwingi walikuwa wanaongea na simu Sikuwafahamu kwa Maana walikuwa ni Wageni wa maeneo haya.
Baada ya Muda walikuja watu watano na a Kuwafuata wale Vijana
Na wakawaambia wapo Chini ya Ulinzi Askari hao walitaka Kufanya Upekuzi ndipo walipokuka Kuni….

Kamyamaza Kidogo

Askari hao walihitaji Kufanya Upekuzi ndipo walikuja……Akaniomba niwe Shahidi huru
[ Kwangu Afande Mmoja akajitambulisha Jina Afande Jumanne
Ambapo nilishuhudia Kufanya Upekuzi
Pia alikutwa na Kete 58 za Madawa ya Kulevya
Kwenye Kupekuliwa Kijana Mmoja alikuwa na Bastola Zenye nmabaA A 5340
Adam Kasekwa mbaye nilimfahamu Jina baada ya Kuulizwa Jina lake baada ya Upekuzi
Na huyo Mwingine aliyekuwa naye alitaka anaitwa Mohammed Ling’wenya ambaye pia kwenye Upekuzi alikutwa na Simu Moja ya Smartphone
Yenye Line ya Airtel na Hallotel na Kete 21 za Madawa ya Kulevya
Watu hawa wawili nilikuwa siwafahamu Majina wala Sura niliwafahamu baada ya Kutajwa Majina yao
Baada ya Kukamatwa na Polisi, Askari wale nilikuwa siwafahamu
Na Kiongozi wao aliyekuwa anafanya
upekuzi aliwatambulisha kwangu ASP Jumanne
Baada ya Majina hayo Nilijaza Hati ya Upekuzi
Na Kuzuia Mali
Walisaini wote na Watu tulioshuhudia
Na Afande Jumanne
Na baada ya Upekuzi Nilijaza Hati ambayo inaonyesha Upekuzi umefanyika Ambapo tukisaini wote na tulioshuhudia
Haya Ndiyo Maelezo Yangu Sahihi Kama Nilivyoyatoa

MTOBESYA: Nitakurudisha Kwemye baadhi ya Maeneo kama Ulivyosoma?

SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: Ni sahihi Katika Ushahidi wako ulisema Askari wawili walifika wakawaambia Mpo chini ya Ulinzi na Wakawatajia Makosa yao? Kwenye Maelezo yako hapo hayo Maneno Yapo au hayapo?

SHAHIDI: Hayapo

MTOBESYA: Nilikusikia Unasema hawa Vijana waliokamatwa wao walikuwa wanakunywa wakati wewe unafanya usafi katika Eneo lako la Biashara?

SHAHIDI: Sahihi

MTOBESYA: Kwenye Maelezo yako hiyo Taarifa ipo?

SHAHIDI: haipo

MTOBESYA: Nilikusikia Ulisema Kwamba afande Jumanne alikuja kwako akatoa Kitambulisho?

SHAHIDI: Ndiyo alitoa Kitambulisho

MTOBESYA: Hayo Maelezo ya a kutoa Kitambulisho yapo kwenye Statement yako?

SHAHIDI: Hayapo

MTOBESYA: kwenye Maelezo yako nilikusikia watuhumiwa Walipo simamishwa kabla ya Upekuzi walijitambulisha Majina yao kwa Polisi aliyekuwa anafanya Upekuzi?
Nitakuwa sahihi nikisema Statement Yako inasema Uliwajua Majina Baada ya Upekuzi?

SHAHIDI: Niliwajua Majina kabla ya Upekuzi

MTOBESYA: Soma sehemu inayosema nilishuduia wakipekuliwa…….. Mpa inaisha Jina la Afande Jumanne, Soma kwa Sauti

SHAHIDI: Nilishuhudia Kupekuliwa kwa Vijana hao, na Kupekuliwa Mmoja wao alikutwa na Bastola yenye namba A5340 pamoja na Magazine yanye Risasi 3 pia alikuwa na Madawa ya Kulevya

Ambae nilimfahamu Jina baada ya Kuulizwa baada ya
Upekuzi

MTOBESYA: Kwa hiyo Statement Ulifahamu Kabla au Baada?

SHAHIDI: Baada ya Kupekuliwa

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi kwenye Ushahidi wako ulielezea ulisaini Nyaraka Nne za Kushuhudia Upekuzi?

SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: Nenda Sasa baada Upekuzi huo, Nilijaza Hati ya Upekuzi na Hati ya Kuzuia Mali ili onyesha Upekuzi Umefanyika, ambao tukisaini wote tulioshuhudia pale

MTOBESYA: ishia pale, Nitakuwa sahihi nikisema Nyaraka hiyo Uliyosoma inaonyesha ulisaini Nyaraka Moja..? Na siyo Nne kama Ulivyosema Asubuhi ya Leo

SHAHIDI: kwa Mujibu wa Mstari huu ni Kweli

MTOBESYA: Soma baada ya Neno Watuhumiwa wale wawili, isaidie Mahakama sehemu nataka Usome Kwa Sauti

SHAHIDI: Baada ya Upekuzi huo NA Kusaini Hati ya Kuzuia Mali ambapo tukisaini wote

SHAHIDI: Nilisema ni Afande ambaye sikujua Kwa Jina

MTOBESYA: Wakati Wakili Wa Serikali Esther anakuongoza Ulisema aliyekuongoza hapo ni Jumanne, Ipo Kwenye Rekodi Jaji ataona?

MTOBESYA: Ungependa hayo Maelezo Yawe sehemu ya Ushahidi Wako Siku ya Leo?

SHAHIDI: Ndiyo ningependa yawe Ushahidi Wangu Siku ya Leo

WAKILI WA SERIKALI: Hatuna Pingamizi

JAJI: Mahakama imeyapokea Maelezo hayo Kama Kielelezo namba 02 kwa Upande wa Utetezi

MTOBESYA: Kwa Ruhusa yako Mheshimiwa naomba Kuendelea

MTOBESYA: Ulielezea Mahakama Ulisaini Nyaraka za Uzuiajinwa Mali zaidi ya Nne?

SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: ieleze Mahakama Hati hizo zilijazwa na nani Mpka Nyie Mkasaini?

SHAHIDI: Zilijazwa na Askari Jumanne

MTOBESYA: na wewe Unakumbuka ulisaini kwenye Hati zote?

SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: Unaweza Kumsaidia Mahakama Ulisaini Upande gani?

SHAHIDI: Pale Mwisho Kwa Pembeni

MTOBESYA: Naomba Nimuonyeshe Shahidi ID 1.
Nitakuwa Sahihi Nikisema Nyaraka zote Nne ulisaini hapa Kwenye Jina lako?

SHAHIDI: Siyo zote sehemu hii. Zingine Nilisaini Upande wa Kushoto na Zingine Upande wa Kulia

MTOBESYA: Unaweza Kutuambia Ulizosaini Upande wa Kushoto zinaruhusu nani na Kwaajili ya Vifaa Vipi?
Hizo Ulisaini Upande wa Kushoto

SHAHIDI: Nilizo Saini Upande wa Kushoto zilikuwa zinamhusu Adam

MTOBESYA: na Zilizomuhusi Mohammed Ulisaini Upande gani?

SHAHIDI: Nilisaini Upande wa Kulia

SHAHIDI: Upande WA Kushoto

MTOBESYA: Ulisaini Baada au Kabla ya Jina lako?

SHAHIDI: Nilisaini baada ya Jina

MTOBESYA: Na Ni Ushahidi wako Mbele ya Mahakama zote Ulisaini wewe Mwenyewe na kwa Mwandiko wako?

SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: Na Kwa Ushahidi Wako Saini zako umesaini wewe Zikiwa zinafanana?

SHAHIDI: Kuna zingine zilikuwa hazifanani kwa sababu nilikuwa na Hali tofauti

MTOBESYA: Mweleze Mheshimiwa Jaji Sasa ni hali ipi Ulikuwa nayo ikapelekea Saini zako Kutofautiana

SHAHIDI: Kuna saa wakati wa Ukamataji Nilisaini wakati nimesimama na Zingine nimesaini wakati nimekaa kwenye Meza

MTOBESYA: Unaieleza Mahakama Ukisaini ukiwa aumesimama na Wakati Umekaa saini lazima zitofautiane
SHAHIDI: Ndiyo

MTOBESYA: Nilisikia wakati anakuongoza Dada Yangu Wakili wa Serikali Kuwa Mlisaini wakati Wa Tukio..

MTOBESYA: Ni Signature zipi sasa zinazofanana ukiwa Umekaa au Umesimama?

SHAHIDI: Nikiwa Nimekaa ndiyo zinafanana

MTOBESYA: Ukiwa Umekaa umesaini Mara Ngapi na. Nyaraka zipi?

MTOBESYA: Zote ambazo ulisaini Ukiwa Umekaa Zina fanana..?

SHAHIDI: Zile ambazo nilikuwa kituoni kutoa Maelezo

SHAHIDI; Hapana

MTOBESYA: Zote ulizo Saini Ukiwa Umesimama Zina fanana au hazifanani?

SHAHIDI: Zinafanana

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia Hapo

MTOBESYA: naomba Kurudisha Kielelezo

JAJI: Wakili Malya unahitaji Muda gani?

MALLYA: Nusu saa hivi

MALLYA: Bado unauza Mbege?

SHAHIDI: Ndiyo

MALLYA: Mbege unayouza wewe inalewesha?

SHAHIDI: Kuna Inayolewesha na Isiyolewesha

MALLYA: Una Ndugu au Mume ambaye ni Polisi

SHAHIDI: Hapana

MALLYA: Ulitambuaje kuwa hiki ni Kitambulisho cha Polisi?

SHAHIDI: niliona Chapa ya Taifa

MALLYA: Kitu gani Kingine Uliona?

SHAHIDI: Niliona Jina lake

MALLYA: Lilikuwa limeandikwaje

SHAHIDI: kwa kweli hapo Sikumbuki

MALLYA: Umesema Wakati Unafanya Shughuli zako za Usafi na Vijana walikuwa wanakunywa Bia?
Ni hatua ngapi?

SHAHIDI: Ni hatua 10

MALLYA: Napiga hatua Mahakamani. Hapa Kuna Hatua Saba tu, Umbali wa Hatua 10 Macho yako yanaona Vizuri?

SHAHIDI: Yanaona Vizuri

MALLYA: Je unataka Mahakama Iamini kwamba unaona Vizuri?

MALLYA: hapa Kuna Umbali Wa Hatua 7 tuh Unasema Mtu Amevaa Tshirt yenye Rangi Nyeusi wakati ni Dark Green

MALLYA: Siku ya Tukio ulikuwa Umbali wa Mita 10 Leo Mshitakiwa yupo hatua 10 tuh hakuna aliyevaa Tshirt Nyeusi, unataka Kumwambia Mheshimiwa Jaji unaona Vizuri?

SHAHIDI: Kimyaaaaaaaaaa

JAJI: umelielewa Swali?

SHAHIDI: Ndiyo

JAJI: Jibu Basi

SHAHIDI: Kuna saa Macho yanashida natumiaga Miwani, Sema Leo nimesahau Miwani

MALLYA: Ulielezea Kuwa sikubya Tukio ulivaa a Miwani?

SHAHIDI: hapana

MALLYA: Wakati Unatoa Maelezo Leo Uliomba Miwani uweze Kuangalia Vizuri.?

SHAHIDI: Sikuomba

MALLYA: Ni sahihi Kuwa Usajili wa Simu unafanya kwa Kitambulisho?

SHAHIDI: Ndiyo

MALLYA: na wewe Ukiwaona watu waliopo Mahakamani alikuwa wanasajili Line za simu?

Shahidi Ndiyo

MALLYA: Kwenye Maelezo Yako kuna sehemu umesema Wanasajili lini?

SHAHIDI: Hakuna

MALLYA: pale Rau Bia wa nauza au Bure

SHAHIDI: wanauza

MALLYA: Wakati mnawapekua Mliwakuta na Bastola na Siyo Pesa

SHAHIDI: Hakuwa na Pesa

JAJI: Watakuwa walishalipaaaaaa

MAHAKAMA kichekoooooo

MALLYA: zoezi la Kufanya Lili chukua muda gani?

SHAHIDI: Kwa muda wa Kufanya Usafi kama Dakika 10

MALLYA: Wakati Tukio linatoka Ulishamaliza Usafi au Ulikuwa unaendela?

SHAHIDI: nilikuwa na endelea ikabidi nia
Nisimame

MALLYA: Tukio la kukamatwa lilichukua Muda gani?

SHAHIDI: Rudia swali

MALLYA: Kitendo Cha Kukamatwa hawa watu Mpaka anaitwa kushuhudia ilichukua muda gani?

SHAHIDI: kama Dakika 03

MALLYA: Kwa hiyo tukijumlisha Dakika 10 za Usafi na Dakika 3 wakakuita wewe, Zoezi la Kusachiwa lilidumu kwa
muda gani?

SHAHIDI: Kwa Dakika 45

MALLYA: Saa Nane ilikuwa imefika

SHAHIDI: Kama saa Nane Kasoro

MALLYA: Kwa Maelezo Yako wewe yalitolewa Umesaini Ukiwa polisi saa 7 kamili Je tukuamini wewe au?

SHAHIDI: Muamini Maneno Yangu

MALLYA: Tuchukue Yote.?

SHAHIDI: Ndiyo

MALLYA: Kabla ya kwenda Kwenye Tukio Siku hiyo ulikuwa wapi na wapi?

SHAHIDI: Nilitoka a Nyumbani baada ya Usafi, Nikaenda Kwa Mgonjwa na Baadae Saloon

MALLYA: Umeulizwa aliyekuchukua maelezo Yako ni nani?

SHAHIDI: Simfahamu Kwa Majina

MALLYA; Hakukuonyesha Kitambulisho ndiyo Maana Humkumbuki?

SHAHIDI: Hapana alinitajia nimemsahau

MALLYA: Kwa akutazama Kwa Macho yako sahihi yako uliyosaini Hapa na Hapa Kwenye Exibit 02 zinafanana?

SHAHIDI: Hazifanani lakini ni sahihi zangu

MALLYA: Kwenye Maelezo Yako umeeeleza Mahali Kiongozi wao Afande nani?

SHAHIDI: Afande Jumanne

MALLYA: akitokea Mtu akisema yeye ndiyo Kiongozi alikwepo atakuwa Muongo?

SHAHIDI: ndiyo

MALLYA: Unamfahamu Kingai?

SHAHIDI: Hapana

MALLYA: na Ulisema Mapolisi walikuja kujitambulisha kwako.?

SHAHIDI: alikuja Mmoja

MALLYA: Askari waliowakamata watuhumiwa waliku wangapi?

SHAHIDI: walikuwa watano

MALLYA: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu

JAJI: Mnasemaje Tubreak au tuendelee?

WAKILI WA SERIKALI: Tubreak

JAJI: kwa Muda gani?

PETER KIBATALA: Kwa Sababu tulisha Kaa Dakika 30 tupumzike Kwa Dakika 45

JAJI: Mnasemaje Serikali?

WAKILI WA SERIKALI: Sawa

JAJI: Shahidi Tunapumzika tunywe Maji tutarudi baadae Kidogo

Jaji tutarudi Saa 8 na Robo

BAADA YA BREAK

Saa 8 na Dakika 21
Jaji Kaingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa

Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe

Jaji anaandika Kidogo

WAKILI WA SERIKALI: Kwa Upande wa Jamuhuri na Upande Wa Utetezi tupo tayari Kuendelea

MATATA :Shahidi nitakuhoji Maswali Machache utajibu kwa Sauti, Umesema wewe ni Mwenyeji Wa Miaka 08 pale Rau Madukani?

SHAHIDI: Katika Biashara

MATATA: Lakini pia Umesema Unaishi Palepale?

SHAHIDI: Ndiyo

MATATA: Umesema Pale Rau Madukani ni Kata, Kijiji au Kitongoji?

SHAHIDI: Kata ya RAU Madukani

MATATA: Utakubaliana na Mimi Hukusema Pale ni Kata ya RAU Madukani?

MATATA: Utakubaliana na Mimi Ujatutajia Unatoka Mtaa Gani hiyo Kata Ya Rau?

SHAHIDI: Sikuulizwa

MATATA: Ujatutajia Hata Mwenye Kiti wa Mtaa wako?

SHAHIDI: Sijaulizwa

SHAHIDI: Si kuulizwa

MATATA: Ujatuambia pia Kuwa unaishi kwenye Nyumba yako au Nyumba ya Kupanga?

MATATA: Unaishi Nyumba yako au Umepanga?

SHAHIDI: Nimepangisha

SHAHIDI: Sikuleta

MATATA: Kuna Mkataba Ulileta hapa Kwamba wewe Umehamia Rau, umetutajia Umepanga Nyumba ya Nani?

SHAHIDI: Sijaulizwa

MATATA: Umesema Unafanya Shughuli Ya Kuuza Mbege?

SHAHIDI: Ndiyo

MATATA: Ujasema akama Mbege Una nunua au Unaitengeneza

[SHAHIDI: sikuulizwa

MATATA: Umesema Pale Rau Una eneo la Biashara?

SHAHIDI: Hapana

MATATA: Unaonyesha Hati wala Kataba wa Pango
Ni sahihi lakini sasa….
Umesema Wakati wa Maelezo Yako Una Glocery, Stationary, Kibanda Cha Simu, Ujatutajia Mtu Yoyote zaidi ya Huyo Esther ambaye ni Shahidi?

SHAHIDI: Sijataja

SHAHIDI: Sijaulizwa

MATATA: Ujatutajia Hat Saloon au Mtu aliyekuosha Hizo Nywele

MATATA: Wakati Ukiwa eneo lako la Biashara Ukiona Vijan wa ngapi wakiwa wanakunywa Bia?

SHAHIDI: Niliona watatu

MATATA: Ukasema Walikuwa wanasajili laini za Simu?

SHAHIDI: ndiyo

MATATA: Wakati Unahojiwa na Wakili Mallya Ukasema hawasajili laini?

SHAHIDI: walikuwa wamekaa Meza Moja na Kijana anayesajili laini

MATATA: Mahakama Ichukue Lipi walikuwa Wanakunywa Bia, Wanasajili Laini au Walikuwa Mekaa Mezani?

SHAHIDI: Ichukue Yote kwa sababu yalikuwa yanafanyika kwa Pamoja

MATATA: Mtu anaweza Kuwa anakunywa Bia, anasajili Line na wakati huo huo a kaa mezani..?

SHAHIDI: ndiyo

MATATA: ulielezea Mahakama Kwamba Mlifika Saa ngapi Polisi?

SHAHIDI: Hapana Sikuulizwa

MATATA: Shika Maelezo Yako

MATATA: naomba Exhibit P2
Wakati Unaulizwa na Wakili ulisema aliyekuwa anashuhudia ni wewe na Esther Sasa Iambie Mahakama Katika Maelezo yako ni wapi Esther ametajwa?

MATATA: Mheshimiwa ni hayo tu

SHAHIDI: Hajaandikwa

KIBATALA: Shahidi saa hizi ni Saa ngapi

SHAHIDI: Saa 9 Kasoro

SHAHIDI: Kwenye Saa

KIBATALA: umeona wapi?

KIBATALA: unaona yake Magari pale Nje

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Rangi gani?

SHAHIDI: Ni Pink, Nyeupe na Blue

KIBATALA: na Hapo Ujavaa Miwani?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Mallya alipokuuliza kwa sababu ya kutomtambua Mshitakiwa Ukasema Unatatizo la Macho na Sababu Ujavaa a Miwani. Ila Kwa Sasa wakati nakuuliza Ujava Miwani?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: na wala Ujamuomba Mheshimiwa Jaji Uvae Miwani?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Umekuja Hapa ukitokea wapi?

SHAHIDI: Gesti

KIBATALA: mara ya Mwisho Kuwa Rau Madukani ni lini?

SHAHIDI: Ijumaa

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Ulikuwa Unaendelea na Kuuza Mbege Rau..?

KIBATALA: aliyekuuzia Mbege Mwezi wa 05 ni nani

SHAHIDI: Mama kazi Moto na Mmoja anaitwa Paulo

KIBATALA: Wewe Majina Mengine ni Mama Pendo..?

SHAHIDI: Ni kweli

KIBATALA; na Ni kweli usimami wewe Peke yako kuna Mtu anakusaidia

SHAHIDI: Wakati upi?

KIBATALA: Ni Kipindi Kipi Binti yako alikuwa anauza pale

SHAHIDI: Alianza Juzi Jumamosi

Shahidi anayoosha Kidole

KIBATALA: Unataka Kurekebisha Jibu
anaitwa Nani?

SHAHIDI: Kuna Binti yangu ananisaidiaga Usafi

SHAHIDI: Naitwa Pendo

KIBATALA: katika Ushahidi wako Ulizungumza Lolote kuhusu huyu Pendo

SHAHIDI: sikumzungumza

KIBATALA: pale Rau Madukani Karibu na Tukio lilipotokea kuna Mtu anaduka la Vipodozi?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Kuna Mtu ana Duka la Jumla

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: na Mtu huyo Mwenye Duka la Jumla Ndiyo mwenye flemu za Vipodozi?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Na Pana Flemu 4 kwa Upande Mmoja?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Anayeuza Duka la Vipodozi anaitwa Athima?

KIBATALA: na Upande wa Pili ndiyo wa nauza Vinywaji ila Unajua ni Mmama au Mdada?

SHAHIDI: Sijui Jina lake

KIBATALA: na ndiyo unakaa Mbele ya Duka lake?

SHAHIDI: Ndiyo

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Picha hii tunayo zungumza ulimcholea Jaji hiyo Picha?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Unajua kuwa kwanini unajua kwanini Ujamchorea Jaji?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Ni Kwa sababu wewe Ni Shahidi wa Kupanga

SHAHIDI: Hapana Kabisa

JAJI: Naliondoa hilo Swali

KIBATALA: Twende kwenye Bastola.Ulikuwa unampekua?

SHAHIDI: hapana

KIBATALA: ulijuaje Kuwa kulikuwa na Vitu vigumu?

SHAHIDI: Baada ya kutoa kwenye mfuko

KIBATALA: na Ulishuhudia MADAWA ya Kulevya?

SHAHIDI: ndiyo

KIBATALA: Unga ni kitu kigumu

SHAHIDI: Kitu kilaini

KIBATALA: Kuna sehemu uliona namba za Bastola CZ 100?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Mpaka unamaliza Zoezi la Kuulizwa na Serikali hakuna aliyekutajia hizo namba?

SHAHIDI: ndiyo

KIBATALA: Unakumbuka ulisema zilipatikana Risasi tatu na Magazine, hapa Mahakamani Umeonyeshwa hizo Risasi?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: kwa hiyo ujamsaidia Mheshimiwa Jaji Kuwa kumtambua Risasi?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Umesema Kuhusu Magazini, unajua magazine unakaa wapi kwenye Bastola

SHAHIDI: upende wa Chini

KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Jaji Kwa Kufafanua Kuwa Magazine inakaa hapana

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Wakati Umetoa maelezo yako ambayo yapo katika D2 kwamba Kuna Afisa Wa Askari Alichomoa Magazine Ukaona Risasi 03

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji Naomba Kielelezo Namba D2

SHAHIDI: Nilisema

KIBATALA: Nionyeshe ni wapi

SHAHIDI: hakuna sehemu kama hiyo

KIBATALA: Kwa hiyo tunakubaliana Jibu la Kwanza ni Uongo?

SHAHIDI: Hapana siyo Uongo, Makosa ya Mwandishi

KIBATALA: Nichukie lipi sasa?

SHAHIDI: Chukua Yote

KIBATALA: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuna Kitu hapa Mwandishi amekiacha ambacho Mimi nilikisema, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji?

KIBATALA: Eneo LA Batola Nitarudi Baadae Kidogo

KIBATALA: Ni sahihi Kuwa Kielelezo D2 haitaji Jina la Askari yoyote isipokuwa Jumanne

Shahidi Ni sahihi

KIBATALA: kwa sababu walijitambulisha ukajisahau

SHAHIDI: Ndiyo walijitambulisha Nikasahau

KIBATALA: Unatatizo la Kumbukumbu?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Soma Kuanzia Neno baada ya Upekuzi huo

SHAHIDI: Ndiyo

SHAHIDI: Nilishuhudia na a Kusaini Fomu za Upekuzi

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji hapa kwenye watu wawili Umefafanua
Pia Mlisaini Wote Ulifafanua Neno Watu wote?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Wakati yanaandikiwa Uliambiwa ni Maelezo ya Kisheria au Mapambo?

SHAHIDI: niliambiwa ni Maelezo Yangu

KIBATALA: Kwa Mujibu wa a maelezo haya Adam Kasekwa Ulifahamu Jina Lake Baada ya Upekuzi?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Unakubali Hakuna Sehemu ukiyotaja Adamoo?

SHAHIDI: Ndiyo Sikutaja

SHAHIDI: Hakuna Adamoo

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni kweli au siyo Kweli Kwamba Katika Kielelezo ukichosha hapo Hakuna Adamoo

KIBATALA: Unakubaliana na Mimi Kwamba Unatakiwa Kusema Ukweli ndiyo Maana Unaapishwa

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Soma hapa na Jaji akupime Ukweli au Uongo wako kwa hilo

SHAHIDI: Adam Kasekwa Adamoo

KIBATALA: awali ulisema ipo au haipo?

SHAHIDI Nilisema Haipo

KIBATALA: Sasa wewe ni Muongo au Mkweli?

OBJECTION Pius Hilla Swala la Kweli au Uongo aiachie mahakama

JAJI: Naona Shahidi anaweza Kujibu yeye ni Mkweli au Muongo

WAKILI WA SERIKALI: Sawa Mheshimiwa

KIBATALA: Swali langu lipo palepale Kutokana na Mgongano wa Majibu Mwanzoni Ulisema Adamoo Haipo na baadae tukasema Kwa pamoja Ukaona Ipo, Wewe ni Shaidi wa Ukweli au Uongo?

SHAHIDI: Mimi ni Shahidi wa Ukweli

KIBATALA: Unakumbuka ulisema uligundua namba ya Bastola..?

SHAHIDI: afande Jumanne

KIBATALA: Na ndiyo Unavyosema Katika Maelezo yako

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Hakuna mahala Umesema Kuwa “Mimi ndiye niliyesoma na Kugundua Namba za Bastola”?

WAKILI WA Seri5kali Robert Kidando:Hiyo sehemu ichukukiwe kwa makini.

KIBATALA: Sijaona Objection na Shahidi amejibu

JAJI: Mimi sijasikia Swali

KIBATALA: Wacha Nirudie tena

KIBATALA: Kuna Mahala Umesema wewe Ulisoma namba za Bastola?

SHAHIDI: Kwenye maelezo haijaandikwa
Shahidi Lipo

KIBATALA: Katika MAELEZO yako kuna Mahala Kuna sehemu Yoyote Kuna Jina Luger..?

SHAHIDI: Kwenye hiyo Fomu Hakuna

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo

MAHAKAMA kichekoooooo

KIBATALA: hii fomu alijaza nani?

SHAHIDI: afande Jumanne ndiyo alijaza

SHAHIDI: Hapana sikumfafanulia

KIBATALA: ukimfafanulia jaji tofauti ya Kielelezo Kimoja kina Luger na Kingine hakimo

KIBATALA: Katika Maelezo Yako E2 ulitaja Aina simu, Je Namba ya Simu Ukiweka Kwenye Kielelezo Chako

KIBATALA: na wala hiyo Tofauti hukufafanua

SHAHIDI; Hapana Sikuweka

SHAHIDI: Sikufafanua

KIBATALA: Shahidi Unafahamu IMEI namba za Simu ya Adama Kasekwa

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: na wala Ufahamu kuwa kuna IMEI Moja wala 02
SHAHIDI: Hapana Sifahamu

KIBATALA: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa a Serikal huku fafanua kuhusu IMEI Moja au Mbili kwa Mtu anayeitwa kasekwa

SHAHIDI: Hapana

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Wala Hukuomba Ujikumbushe labda kwa Sababu Namba ni Nyingi, Ulifanya hilo zoezi

KIBATALA: katika hiyo Karatasi Kuna Maneno kama CZ 100 ya Kufafanua hiyo Bastola

SHAHIDI: Hakuna

KIBATALA: Walikwambia Karatasi hii Ndiyo inatakiwa akumtia Hatia ni Mshitakiwa bila Kuacha Shaka yoyote

SHAHIDI: Niliambiwa

KIBATALA: Twende Simu Card ya Vodacom?

SHAHIDI: Sifahamu

KIBATALA: Unafahamu Kwanza hiyo ICCD namba

KIBATALA: Kwa hiyo Unakubaliana kwamba hizo ICCD Namba ambazo ndiyo Utambulisho katika Ushahidi wako hazijaingia

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: hata namba ya Adam Kasekwa ya Hallotel kuhusu ICCD namba, hukutaja hivyo?

SHAHIDI: Ndiyo

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: wala ahukufafanua

KIBATALA: wala Ujazizungumzia Kabisaaaa?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: katika Ushahidi wako ulitambua huyu kama nani?

SHAHIDI: Kama Mohammed Ling’wenya

KIBATALA: Katika Ushahidi Wako ulimtambua Mtu anaitwa Mohamed Abdilah Ling’wenya?

SHAHIDI: Hapana Sikutaja Ling’wenya

KIBATALA: Kwenye Statement D2 Ulimtaja huyu Kama nani?

KIBATALA: Unakubaliana tutakachokipata pia tukitumie?

SHAHIDI: ndiyo

KIBATALA: Naomba D2

KIBATALA: Taja huyo Mtu humo Umemtaja Kama Mohammed Abdalahi Ling’wenya

SHAHIDI: Ndiyo Mohamed Abdilah Ling’wenya

KIBATALA: Mwanzoni Umesema Halipo

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Ulifafanua Kuwa Katika Utambuzi hapa Mahakamani na ile Hati yako ya maelezo pamoja Na kutofautiana, Ulifafanua Kwa Jaji kwamba huyo ni Mtu Mmoja?

SHAHIDI: Shapana

KIBATALA: Katika Ushahidi Wako Kuna Mahala Popote umezungumzia Kuna Afisa Wa. Polisi anaitwa Ramadhan Kingai

SHAHIDI: Hapana

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Wakati Maafisa Wa Polisi wanajitambukisha ulikwepo

KIBATALA: Hakuna Mahala Umezungumzia Kuhusu kingai Kwamba alikwepo ila Ujamtaja

SHAHIDI: Sijazungumza hilo

KIBATALA: Wakati Unaulizwa Maswali na Mtobesya kuhusiana na Saini zako na Kuna Mazingira zinatofautiana na Kwamba Kuna fomu ulisaini Ukiwa Umesimama?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Je Wakati Jumanne anajaza hii fomu pia alikuwa amesimama

SHAHIDI: Ndiyo alikuwa amesimama

KIBATALA: mara zote wakati Unatoa Ushahidi wako Ulikuwa Unatoa Maneno “Glocery” Mwambie Mheshimiwa Jaji Katika Maelezo yako kuna Neno Glocery

SHAHIDI: hakuna

KIBATALA: Maneno gani uliyatumia

SHAHIDI: Bar

KIBATALA: Ulifafanua kwa Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulikuwa unalenga Kitu Kimoja hichohicho?

SHAHIDI: Sikufafanua

KIBATALA: Kati yako wewe na Flemu 4 za Jumla na Vipodozi na Upande wa Pili Ndiyo Glocery na Kwamba Sehemu yako ya Mbege ni Nyuma kabisa?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Unakubaliana na Mimi Kutoka Kwenye Flemu 4 Duka la Vipodozi hadi eneo la Tukio ni hatua ngapi?

Objection Shahidi ameshasema hamfahamu Athma

KIBATALA: kutoka a kwenye Flemu 4 Mpaka waliokamatwa hawa ni Kama Hatua ngapi?

SHAHIDI: Kama Hatua Ngapi

KIBATALA: Wakati wanakamatwa Flemu zilikuwa wazi?

KIBATALA: Bado Unasisitiza Ushahidi wako waliwaacha hawa wa kwenye Flemu hatua Tatu wakakufuata wewe wa Hatua 10

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Shahidi Unafahamu unafahamu au hufahamu Mmlilki wa hilo Duka la Jumla na Duka la Vipodozi ni Dada yake Ling’wenya.?

SHAHIDI: Sifahamu

KIBATALA: hilo eneo lina Kiongozi wa Mtaa

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Naitwa nani?

SHAHIDI: Sigfrid Malewa

KIBATALA: Katika hizi Hati hapa unaona Jina la Sigfrid Malewa?

SHAHIDI: Hakuna

KIBATALA: Msaidizi Wake anaitwa nani?

SHAHIDI: Namjua Kwa Jina Moja la Temba

KIBATALA: anaishi wapi na eneo hilo?

SHAHIDI: anaishi Mbali

KIBATALA: katika Kielelezo chako Namba 02 Mnamo tarehe 05 08 2020 nilikuwa naenda Saloon hapo Rau Madukani
Kwamba Saa 7 Kamili Mchana?

SHAHIDI: Ni kweli nilisema hivi

KIBATALA: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulitoa Ufafanuzi kwamba Ulikuwa ni Muda wa Makadirio?

SHAHIDI:sikusema

KIBATALA: Huko Saloon Ulikaa Muda gani?

SHAHIDI: Kama Robo Saa

KIBATALA: Na Ukamwambia Mallya Ukarudi Sehemu ya Biashara Kwa muda gani?

SHAHIDI: Kama Robo saa

KIBATALA: kwa hiyo kama Saa Saba Na Nusu?
Na Katika Kielelezo Chako D1 Maelezo uliyoyatoa Ulisema ni Saa Saba, Si Unaona kuna tatizo?

KIBATALA: Tatizo ambalo hukulitolea Ufafanuzi?

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Nani atutatulie hili tatizo?

SHAHIDI: Mimi Mwenyewe

KIBATALA: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali nilikusikia ulisema hawa washitakiwa wawili walipigwa Pingu, Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kama baada ya Kupigiwa Pingu nini Kiliwatokea

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Mlifika nda Kwa usafiri gani?

SHAHIDI: Watuhumiwa WALIENDA kwa Gari Nyingine na sisi tukaenda na Gari Lingine

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: na ukamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba na hilo gari lina Maofisa

KIBATALA: Aliwahi Kukwambia Kesi Mama ipo Dar es Salaam

SHAHIDI: Hakuwahi kuniambia

KIBATALA: Wewe ulikuwa unajua kesi na Kila kitu kipo Moshi

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: ukisikia hao Maaskari wanaongea na Mtu yoyote kuhusu washitakiwa Kukamatwa

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: ulisikia Maofisa Wa Askari Kwamba Yupo wapi Moses Lijenje

SHAHIDI: Nilisikia akiuliza Mwenzenu

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji huyo Mwenzao Katika Statement Yako D2 umeaungumza Walikuwa wa ngapi?

SHAHIDI: Watatu

KIBATALA: Maelezo yako chini ya Kiapo, Kielelezo D2 ulizungumzia kuhusu Vijana watatu?

KIBATALA: we Umezungumzia wangapi

SHAHIDI: Hapana

SHAHIDI: wawili

KIBATALA: “palikuwa na Vijana wawili wanakunywa pale*
Ndiyo ukivyosema

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji huyo Kijana wa tatu umezungumzia Nini Kilitokea huyo Kijana wa tatu.?

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: zoezi la Kusajili laini ya Simu uliona kwamba wanasajili Simu

SHAHIDI: Ndiyo niliona

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji walikuwa wanasajili Laini ya kampuni Gani?

SHAHIDI: Sijui sasa

KIBATALA: Unafahamu Iwapo Ndiyo au Lah kwamba hii laini ya Hallotel au Airtel ndiyo zilikuwa zinadajikiwa Siku hiyo

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Mlivyofika pale Polisi Central Station Moshi Iwapo Ulimwambia Chochote Kuhusu Kushuhudia Vile Vifaa Vikiingizwa Kwenye Daftari rasmi

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Iwapo hawa washitakiwa wawili walikuwa na avitu kama Wallet au Kitu Kingine anavyobeba Kijana wa Kiume

KIBATALA: Wewe Kama shahidi Huru Kama Ulishuhudia MALI Binafsi za Washitakiwa Kuingiziwa kwenye Daftari Maalum pale Kituoni

SHAHIDI: Sijazungumzia

KIBATALA: nimesikia mara kadhaa unataja DADA Esther ulifafanua Kwa namna yoyote ile

SHAHIDI: Si kumwambia

Shahidi: Hapana

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba huyu Dada Esther Unamfahamu anaishi wapi?

SHAHIDI Hapana

KIBATALA: Unafahamu Watu wenye Biashara Ndogo Ndogo Kupewa Kitambulisho Maarufu Kama Kitambulisho cha Wamachinga

SHAHIDI: Ndiyo

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: aulimuonyesha Mheshimiwa Jaji ili ajue Kuwa Unakitambulisho

KIBATALA: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Biashara yako inaitwa je kama vile Mama Mbege

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: hata Kumwambia Mheshimiwa Jaji kwamba Umesahau kutaja Jina la Biashara yako ulisema

SHAHIDI: Sikusema

KIBATALA: ulisema hapa a kwamba Mohamed Abdilah Ling’wenya Alikuwa amevaa Nguo gani wakati anakamtwa

SHAHIDI: Sikusema

KIBATALA: na Adama Kasekwa ulisema amevaa Nguo gani

SHAHIDI: Sikusema

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulisema ulishuhudia kiellezo Namba Moja kilijazwa Kwenye Fomu tatu na Fomu Moja akapewa Adam kasekwa

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Ulisema Kwamba Ulisikia Afisa wa polisi akisema Unahaki ya kuoata afomu Moja ya Hati za Kuchukulia hiyo Bastola

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: unasema Ulifanya Kazi na Afisa wa Askari Wa a Polisi Jumanne, na baadae wakakuonyesha Afisa Mwingine wa Polisi aliyekuchukua maelezo Je ulitolea Ufafanuzi kwa Mheshimiwa Jaji

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: Leo umesema Kwamba Bastola Ina Rangi Nyeusi, Je katika Maelezo yako Kuna Sehemu Umetaja Rangi ya Bastola

SHAHIDI: hapana

KIBATALA kwa hiyo Rangi umetaja Leo

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Pamoja na Kwamba Wakati Ule ndiyo Ulikuwa na Kumbukumbu, Maana umesema wewe Tukio la Muda Mrefu Mpaka unasahau, Lakini wakati Ule Hukusema Rangi ya bastola

KIBATALA: ulifafanua Kwa Mheshimiwa Jaji kamba wewe kabla Ulikuwa Unaifahamu kabla

SHAHIDI: Hapana

KIBATALA: nimesikia umesema Vitu vinavyodhaniwa kuwa Madawa ya kulevya, Je kuna Mtu yoyote alimtuhumu baada ya Kupatikana kwa Madawa ya kukevya

KIBATALA: kwa Ushahidi wako wewe unasema Adam Kasekwa alipatikana na Madawa ya Kulevya, Sikufahamu hatima yake
Kibatala Kuhusu Saini ya D01 na D02 ulifafanua kabla ya Wakili Mtobesya Kuuliza maswali

SHAHIDI: Hapana Sikufafanua

PETER KIBATALA: Mheshimiwa Jaji Kwa Shahidi Huyu naomba Kuishia hapo

Jaji anaandika

WAKILI WA SERIKALI: Tunaomba Hairisho ilituweze Kumalizia Asubuhi

JAJI: Kuna Kama Dakika 50 hivi ilituweze Kuhitimisha Leo

WAKILI WA SERIKALI: Sawa Mheshimiwa Ngoja tuendelee

WAKILI WA SERIKALI: Esther Martin

WAKILI WA SERIKALI: Umeulizwa Mahakamani na Malya Kuhusiana na Rangi za Tshirt na akasema siyo Nyeusi Bali Rangi ya Dark Green
Wewe ulikuwa Unaona nini

SHAHIDI: Nyeupe, Kijani na nyeusi

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia Maswali Kwenye Kielelezo D2 ukaambiwa Vitu mbalimbali
Kwenye Maelezo hayo uliyoandika Polisi Watuhumiwa hawakujulishwa Makosa yao
Na Mengine Mengi fafanukia mahakama ni Vipi hayo yamejitokeza

SHAHIDI: Rudia Swali

Swala la Watuhumiwa baada ya Kuambiwa Kaa chini kama walijulishwa Makosa yao, Mahakamani umesema lakini humu hayapo

MTOBESYA: samahani Shahidi anaenda kujazia Statement

JAJI: tungemuacha ajibu kwanza

WAKILI WA SERIKALI: Nasema wakati wakili anamuuliza Maswali akakuuliza kuhusu Maswali Ambayo Hapa Mahakamani umesema aila Kwenye Maelezo Hakuna
Ni kwa vipi hayo yamejitokeza

SHAHIDI: Yamejitokeza kwa sababu ni uandishi tuh

WAKILI WA SERIKALI: Kivipi?

SHAHIDI: Katika Kutoa Maelezo niliyo andika na maelezo ya hapa mahakamani

SHAHIDI: Kimetokea tuh Lakini fomu zilikuwa Nne

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia Kuhusu Maelezo haya pia kwamba Fomu iliyosainiwa eneo la Tukio ni Moja lakini Mahakamani umesema Fomu nne

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kwamba Ulijuaje kwamba Ulichokiona ni Kitambulisho Cha Polisi
Ukasema Ukaona Chata ya Taifa

JAJI: Siyo Chata Bali Chapa

SHAHIDI: Nilikuwa namaanisha Chapa ya Kipolis

i WAKILI MALLYA: Tunaoinga hilo Jibu

JAJI: sahihi Hakujibu hivyo

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali Kama Ulionyesha CZ 100, Fafanunua Mahakamani wewe Uliona nini

SHAHIDI: Niliona A5340

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia Kwamba Kwenye Maelezo haya Uliyasoma na Uliyajua Majina Baada ya Upekuzi lakini Mahakamani Umesema Kabla ya Upekuzi

SHAHIDI: Niliyajua hayo Majina Kabla ya Upekuzi

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji Mimi nimemaliza namuachia Mwenzangu

WAKILI WA SERIKALI: Robert Kidando Uliulizwa Kama Vijana wawili pale Rau Ukiwaona Wakisajili laini na Baadae Ukasema Walikuwa na Kijana anayesajili laini

SHAHIDI: Mimi niliwaona na Kijana anayesajili Laini

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa Kwamba hao Vijana walikuwa wawili na Baadae Ukasema watatu

SHAHIDI: Wakiwa wanasajili laini

Wakati gani Ukiwaona wakiwa watatu

WAKILI WA SERIKALI: Wakati gani walikuwa wawili

SHAHIDI: Wakati wa Ukamatwaji

SHAHIDI: Nimelifahamu Leo

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa Kwenye Fomu kuhusiana na Neno Adamoo Kama Ulikuwa umelisema, Fafanua Hapa Mahakamani Jina la Adamoo Umelifahamu lini
[11/1, 16:26] +255 767 206 226: Objection Kibatala anasema Jina la Amelifahamu lini it’s a New fact

JAJI: hili swali limezungumza Kayika Mazingira Matatu
Kama alitaja, Kama ALIJAZA fomu na Kama alitaja kabla
Hili Jibu la Lini alimfahamu nafikiri siyo Fact Mpya

SHAHIDI: Iliandikwa namba A5340

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali Kuhusiana na Ukamataji kuhusiana na Lile Neno CZ100 Halipo, elezea Kilichoandikwa kwenye Hati hiyo ni nini

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia na Kuhusu Hati yako Kuhusu Glocery na Huku ni Bar, Kwa Mujibu wa Ushahidi wako walikuwa kwenye eneo lipi

SHAHIDI: walikuwa kwenye Glocery ya Dada Esther

SHAHIDI: eneo waliokamatwa ni Karibu na Sehemu yangu ya biashara

WAKILI WA SERIKALI: kwanini jina Sweetfred Malewa Halipo kwemye Hati ya Upekuzi?

SHAHIDI: Sikuulizwa

WAKILI WA SERIKALI: Kuhusu wewe Kufika kwemye eneo lako la Biashara, Muda gani ulienda Saloon na Muda wa Ukamataji kuwa saa Saba
Kilichotokea kilikuwa saa ngapi

SHAHIDI; ilikuwa majira ya Saa Saba Mchana

WAKILI WA SERIKALI Uliulizwa Kama uliona Watuhumiwa kama awalipo fikishwa Polisi Kama Ulishuhudia Uandikishwaji wa vitu vyao
Kwanini hukutoa Ushahidi huo?

SHAHIDI: Sikutoa sababu Sijaulizwa

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kwamba kama katika Ushahidi wako alikwepo Askari anayeitwa Kingai kama alikwepo. Askari yupi aliye husika Kwenye eneo la Ukamataji Kwa Siku hiyo?

SHAHIDI: sikumzungumzia kwa sababu Siku ulizwa ni Askari gani aliyekamata

JAJI: Jamani Mnasikia hukoooooo.?
Kwa Sauti ya Chini sana
Mahakama Hatusikiiiiiii

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba Tukomee hapa

JAJI: Shahidi Nashukuru kwa Ushahidi Wako

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tunaomba Hairisho Mpaka Kesho Saa 03 Asubuhi ambapo tutaendelea na Shahidi Mwingine Upande wa Mashitaka

KIBATALA: Mheshimiwa hatuna Pingamizi

Jaji anaandika Kidogo

JAJI: basi Maombi ya hairisho yanakubaliwa hadi Kesho saa 03 Asubuhi
Upande wa Mashitaka Maelekezo ni kwamba Mtatakikwa mlete shahidi

Na Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande Mpaka Kesho saa 3 Asubuhi.

Jaji anatoka

Like
1