Kesi ya Mbowe: Shahidi wa Jamhuri ‘aingia mitini’

Kutoka mahakamani kama ilivyowasiishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 03 Novemba 2021.

Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe imetajwaMawakili wa Serikali:

Robert Kidando
Pius Hilla
Jenitreza Kitali
Nasoro Katuga
Ester Martin
Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala anatambulisha mawakili wa utetezi:
John Malya
Dickson Matata
Fredrick Kiwhero
Nashon Nkungu
Idd Msawanga
Hadija Aron
Maria Mushi
Evaresta Kisanga

Jaji: Mshitakiwa 1,2,3 na 4
Wote wanaitikia

Wakili wa Serikali: Shauri lina kuja kwa ajili ya kusikilizwa. Mpaka jana jioni tulipata shahidi ambaye tulipanga kuja naye leo.
Lakini ssubuhi amepata tatizo la kiafya lililosababisha ashindwe kuja mahakamani.

Kwa sababu hiyo tunaomba ahirisho mpaka kesho. Na kwamba kwa sababu hii ipo nje ya uwezo wetu pia tunaweza kupata shahidi mwingine.

Jaji: Wakili wa Utetezi

Kibatala: Kwa kufuata amri ya mahakama iliyokuwa imetolewa jana, sisi kwa upande wetu tulikuwa tumejiandaa vizuri.

Lakini kama wenzetu wanasema hivyo ndivyo ilivyo, tunaomba wenzetu kesho wajitahidi tuweze kuendelea, ili tuweze kumalizia kwa wakati.

Jaji: Umezungumzia kwa niaba ya wote au

Kibatal: Kwa niaba ya wote mheshimiwa.

Mahakama ipo kimya. Jaji anaandika.

Kila mtu sura yake ipo disappointed kimtindo.
Washitakiwa wanatabasamu na kunong’onezana jambo.

Jaji: Kwa kuzingatia maombi yalitolewa na wakili mwandamizi Robert Kidando, kufuatia shahidi kushindwa kufika mahakamani, na kwa kuzingatia ukweli kwamba maombi hayo hayajapingwa na utetezi,
Nahirisha shauri mpaka kesho saa tatu ambapo upande wa mashitaka mnaaelekezwa kuleta mashahidi.

Na washitakiwa wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa magereza mpaka kesho saa 3 asubuhi.

Jaji anamaliza kusoma na anatoka. Polisi anapiga kelele za High Cooooooooooooooourt!

Like