Tanzania kufungua ubalozi Israel kwa mara ya kwanza

TANZANIA na Israel, ambazo zimekuwa na uhusiano wa shaka tangu 1973, sasa zinajenga uhusiano mpya kwa kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia kwa vitendo.

Kuazia wiki ijayo, Tanzania inatarajiwa kufungua ubalozi wake nchini Israel katika Mtaa wa Silver, namba 12 Abba Hillel, eneo la Ramat Gan, jirani na Tel Aviv.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hizo, waziri wa mambo ya nje wa Tanzania atatembelea Israel. Tarehe iliyopangwa kwa ajili ya uzinduzi wa ubalozi huo ni Mei 8, 2018. Balozi Augustine Mahiga, ambaye ndiye waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, anatarajiwa kushiriki uzinduzi huo.

Tanzania haijawahi kuwa na ubalozi katika Israel. Hata uhusiano wa kidiplomasia uliokuwepo kati ya nchi hizo ulivurugika mwaka 1973, Tanzania ilipouvunja
kutokana na vita ya Yom Kippur.

Vita ya Yom Kippur, hujulikana pia kama vita ya Ramadhan, au vita ya Oktoba, au vita ya mwaka 1973 kati ya Waarabu na Waisrael.

Umoja wa nchi za kiarabu, ukiongozwa na Misri na Syria, ulipigana vita dhidi ya Israel tangu Oktoba 6 hadi 25, 1973.

Mwaka 1995 uhusiano ulirejeshwa, lakini Israel haikuwa na ubalozi Tanzania, bali shughuli zote za kibalozi zimekuwa zinafanyikia Nairobi, Kenya.

Mwaka jana ndipo Tanzania iliteua balozi wake wa kwanza kwenda Israel, Job Daudi Masima. Kabla yake, uwakilishi wa Tanzania nchini Israel ulifanywa kupitia Kasbian Nuriel Chirich, balozi wa heshima.

Uzinduzi wa ubalozi wa Tanzania umetangulia ule wa ubalozi wa Marekani ambao unatarajiwa kufunguliwa Jerusalem, mji mkuu wa Israel, tarehe 14 Mei 2018.

Like
2
2 Comments
  1. Prof. Abdul Sheriff 6 years ago
    Reply

    In 1973 MW. Nyerere had defined Tanzania’s moral stand: “The establishment of the state of Israel was an act of aggression against the Arab people … Israel must evacuate the areas … Without exception. We cannot condone aggression on any pretext, nor accept victory in war as a justification for the exploitation of other lands, or government over other people.” This was the moral stand of the Father of the Nation. What is our moral stand now regarding the Apartheid Israeli occupation of Palestine?

    6

    0
  2. Jema 6 years ago
    Reply

    Great comment

    0

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.