Wauaji wa Akwilina Akwiline, Daniel John watajwa

SAUTI KUBWA inakuletea habari za uhakika ikitaja majina ya baadhi ya askari waliotumwa kuteka, kutesa na kuua baadhi ya raia, viongozi wa upinzani, na wakosoaji wa Rais John Magufuli; na njama zinazofanywa kuwanusuru.

Vyanzo vyetu vimethibitishiwa kuwa mtu aliyerusha risasi iliyomuua Akwilina Akwiline, mwanafunzi wa chuo kikuu cha usafirishaji Dar es Salaam, ni Deo Siwalile, askari wa Jeshi la Wananchi ambaye alivalishwa sare za Kikosi cha Kutuliza Ghasia cha Jeshi la Polisi (FFU). Moja ya namba za simu anazotumia ni +255762644001.

Akwilina alipigwa risasi kichwani tarehe 16 Februari 2018 akiwa kwenye daladala. Siwalile ndiye askari aliyefyatua risasi hiyo wakati polisi wakidhibiti waandamanaji wa Chadema maeneo ya Kinondoni.

Taarifa zinasema mtu aliyekuwa amekusudiwa kuuawa ni Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema, ambaye baada ya mkutano wa hadhara alikuwa anaongoza maandamano kuelekea ofisi za mkurugenzi mtendaji wa Manispa ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wa Chadema. Mawakala hao walikuwa wamenyimwa viapo hivyo, kinyume cha utaratibu na kanuni za uchaguzi, hadi siku moja kabla ya uchaguzi, huku wenzao wa CCM wakiwa navyo kwa zaidi ya wiki moja.

Hata hivyo, kutokana na taharuki, mvurugano na mwingiliano wa waandamanaji baada ya polisi kuwatawanya, risasi hiyo ilitua kichwani mwa Akwilina ambaye wala hakuwa sehemu ya waandamanaji bali abiria kwenye daladala iliyokuwa inapita.

Wakubwa waliudhika mno kwa askari huyo kukosea shabaha, na kuua mwanafunzi badala ya Mbowe. Matokeo yake, kwa kutekeleza “maagizo kutoka juu,” polisi hawakukamata muuaji aliyefyatua risasi; badala yake wamefungua kesi ya hila dhidi ya Mbowe na wenzake kwa kuongoza maandamano hayo.

Vyanzo vyetu kutoka jeshini vinasema hata kesi yenyewe imeshinikizwa na wakubwa kisiasa; na kwa kuwa jukumu la polisi ni kutii mamlaka, wamelazimika kumbambikia Mbowe kesi hiyo “ili wakubwa wafurahi.”

Katika hatua nyingine, SAUTI KUBWA inaandika kwa uhakika kuwa miongoni mwa askari walioteka na kuua Daniel John, aliyekuwa katibu wa Chadema Kata ya Hananasif, Kinondoni, ni askari wawili wanaotajwa kwa majina ya Rajab Isike na Matiko Chacha.

Moja ya namba za simu zinazotumiwa na Isike ni +255713262275. Chacha ni ofisa wa usalama wa taifa anayetumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Daniel John alitekwa, akauawa na kutupwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi mahali pajulikanapo kama Coco Beach, Dar es Salaam, Februari 2018. Mbowe alipozungumza na vyombo vya habari, alitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kifo cha katibu huyo.

Mpango wa mauaji hayo uliratibiwa na baadhi ya maofisa wa CCM. Bila kujua kilichokuwa kinaendelea, jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kumtia mbaroni Isike.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, amri kutoka juu ilimwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro, amwachie huru askari huyo. Badala yake alishauriwa atengeneze mazingira ya kumhusisha Mbowe na mauaji hayo, ionekane kwamba Daniel John alikuwa na mpango wa kuhamia CCM akashtukiwa na wenzake.

Agizo hili, ambalo Sirro hakuweza kutekeleza, lililenga kumwondoa Mbowe uraiani, katika utekelezaji wa kile ambacho Rais Magufuli anaendelea kuratibu kwa kutumia vyombo vya dola kuteketeza upinzani, kama alivyojiapiza akiwa akiwa Singida Februari 2016 kwamba “nitapiga mchungaji ili kondoo watawanyike.”

Like
37

Leave a Comment

Your email address will not be published.