WABUNGE WA CHADEMA WATEMBELEA SUGU NA MASONGA GEREZANI

WABUNGE 10 wa Chadema leo Jumamosi wametembelea gereza la Ruanda, Mbeya, kuwajulia hali Joseph Mbilinyi (Sugu), mbunge wa Mbeya Mjini, na Emmanuel Masonga, katibu wa Kanda ya Nyasa.

Wabunge hao ni Joseph Selasini (Rombo), Susan Mgonukulima (viti maalumu Iringa), Aida Khenan (viti maalumu Rukwa), Grace Kihwelo (viti maalum Kilimanjaro), Happy Mbilinyi (mke wa Sugu), Cecilia Paresso (viti maalumu Manyara), Conchesta Rwamlaza (viti maalumu Kagera) na Anna Gideria (viti maalumu Manyara).

Sugu na Masonga wanatumikia kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la “kumkashifu rais.”

Katika picha hii wabunge wapo na wanachama wengine wa Chadema mkoa wa Mbeya, na Happy Mbilinyi, mke wa Sugu, nje ya Ofisi za Kanda ya Nyasa mara baada ya kutoka gerezani.

Picha kwa hisani ya
Kanda ya Nyasa.

Like
1

Leave a Comment

Your email address will not be published.