Ronaldo arejea Manchester United

KLABU ya soka ya Manchester United imetoa tamko rasmi la kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo, 36. Kupitia ukurasa wake, timu ya Manchester United imethibitisha;_

“Manchester United inayofuraha kuthibtisha kwamba klabu imefikia makubaliano na timu ya Juventus juu ya usajili wa Cristiano Ronaldo, kilichosalia ni makubaliano binafsi ya mkataba kati ya timu na mchezaji, visa na vipimo vya afya.

Cristiano Ronaldo ambaye ametwaa tuzo za mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or) mara tano na ametwaa mataji makubwa 30, katika maisha yake kisoka, ikiwemo mataji 5 ya klabu bingwa Ulaya, mataji 4 ya FIFA kwa ngazi ya vilabu, makombe 7 ya ligi kuu ya Uingereza, Uhispania na Italia pamoja na kombe la Ulaya akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno.

Katika kipindi chake akiwa na Manchester United, alipachika mabao 118 katika michezo 292. Kila mfuasi wa United, anayo furaha kumkaribisha Cristiano tena klabuni hapa”.

Karibu nyumbani Cristiano Ronaldo! 

Like
4