Majeshi yamgeuka Rais Magufuli, yamweka pabaya Bashite na watu wake “wasiojulikana”

Mabeyo na Dk. Kipilimba wamekerwa na rais kujaza Wanyarwanda katika idara ya usalama; Sirro naye anahaha kuondoa polisi kwenye mikoni michafu ya Bashite

Na Mwandishi Wetu

MAMBO si shwari kati ya Ikulu na vyombo vya dola. Kuna fukuto na uhusiano unaotia shaka kati ya vikosi vya ulinzi na usalama na Ikulu.  Sintofahamu hiyo imesababishwa na amri za rais zisizozingatia sheria, matumizi yaliyopitiliza ya majeshi katika siasa, na mihemko ya baadhi ya wasaidizi wake wanaoingilia na kutumia vibaya vyombo vya dola kuumiza wananchi na kuhatarisha usalama wa taifa, SAUTI KUBWA inaeleza.

Vyombo vyote hivi vinakubaliana kwamba katika miaka mitatu ya utawala wa Rais John Magufuli, amani ya nchi imetetereka, usalama wa taifa upo hatarini, licha ya mabavu yanayotumika kudhibiti wananchi kwa amri za rais. Wataalamu wa sosiolojia ndani ya vyombo hivyo wameridhika kwamba utawala wa kibabe na kikatili wa Rais Magufuli umesababisha chuki kubwa ya wananchi dhidi ya rais na serikali, na sasa hali hiyo inaanza kujenga uhasama wa wananchi dhidi ya majeshi.

Tafakuri yao imewafikisha mahali pa kubaini kwamba ingawa rais ndiye amiri jeshi mkuu na ndiye anateua wakuu wa vyombo hivyo, uendeshaji na usitawi wa vyombo hivyo haumtegemei rais bali weledi na uzalendo wa vyombo hivyo katika kutekeleza wajibu wao wa kikatiba. Viongozi wa vyombo hivyo wamepima pia athari za majeshi kubadilikabadilika kila mtawala mpya anapoingia wakati kanuni za jeshi hazijadadilika, na kwamba kijumla vyombo vya dola vimetumbukizwa katika siasa bila kujua.

Moja ya mambo yaliyokera vyombo hivyo ni hatua ya serikali kutumia nguvu nyingi dhidi ya maandamano hewa ya tarehe 26 Aprili 2018, huku ikichukua baadhi ya wanajeshi na kuwavalisha sare za polisi na kuwaweka barabarani kwa maagizo ya kuua waandamanaji. Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanasema kazi yao si kuua raia bali kulinda mipaka ya nchi.

Kinachowaumiza zaidi ni kwamba yule yule anayewatuma kufanya kazi isiyo yao, ndiye anaruhusu askari wa kigeni kufanya kazi inayopaswa kufanywa na askari wenyeji. “Yaani sisi tunaagizwa kuua ndugu zetu wanaoandamana kutetea haki zao na haki zetu, halafu sisi tunaingizwa barabarani tuwaue, huku mipaka yetu imeshavuja kwa kibali cha yule yule anayetutuma kazi kuua wanananchi wetu. Dhamiri inakataa,” kilisema chanzo kimoja kutoka JWTZ, kikaongeza: “Hata kama tulilipwa vizuri, hakuna pesa inaliyongana na damu ya Mtanzania mwenzangu.”

Hata hivyo, SAUTI KUBWA halikupata kujua iwapo wakuu wa vyombo hivi wamekutana kupeana mawaidha, na kujadili athari za majeshi kufanya siasa dhidi ya wananchi, au kama ni tafakuri na msukumo binafsi kwa kila chombo. Lililo dhahiri ni kwamba yote haya yametokea katika wakati mmoja wakati chuki ya wananchi dhidi ya rais na serikali ikiwa juu kuliko wakati mwingine wowote katika historia.

Mabeyo akerwa na Wanyarwanda wa Ikulu na Mererani

SAUTI KUBWA ina taarifa za uhakika kuwa JWTZ, Jeshi la Polisi, na Idara ya Usalama ni miongoni mwa vyombo vya dola ambavyo katika siku za hivi karibuni vimetikiswa, navyo sasa vimeamua kutikisa watawala kimya kimya. “Tunafanya haya kwa uangalifu mkubwa. Tunajua siri nyingi za nchi. Tunatambua hatari inayoweza kutupata baadhi yetu kutokana na hatua hii. Lakini tunajua kuwa sisi ndio wataalamu wa masuala tunayosimamia. Wanasiasa wanakuja na kuondoka, wanatuteua, lakini sisi ndio tunaowalinda,” kilisema chanzo chetu.

Ndani ya mwezi mmoja uliopita, uhusiano kati ya Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa majeshi, na Rais Magufuli, umeingia dosari kwa sababu ya ushauri wa jeshi ambao rais hakufurahishwa nao, na kwa majibu ambayo rais alitoa, na jeshi halikufurahishwa nayo. Habari zinasema kuwa baadhi ya maofisa wa JWTZ hawafurahishwi na ubaguzi wa unaofanywa na rais dhidi ya jeshi hilo, kuwapatia askari wa Rwanda jukumu la ulinzi wa maeneo nyeti ya taifa. Moja ya maeneo hayo ni ukuta uliojengwa majuzi mkoani Arusha kuzunguka eneo la mgodi wa Mererani yanakochimbwa madini adimu ya Tanzanite. Ukuta huo unalindwa na “majasusi” kutoka Rwanda.

Chanzo chetu kiliiambia SAUTI KUBWA: “Badhi ya maofisa waandamizi jeshini hawapendi mambo haya. Walimuomba Mabeyo azungumze na Rais Magufuli, amuulize kwani haamini jeshi letu mpaka alete Wanyarwanda kulinda mali yetu. Walimtaka ameweleze rais kuwa sisi tupo tayari, na tuna uwezo wa kujilinda.” Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mabeyo alipofikisha ujumbe huo, rais alimjibu: “Mimi ndiye najua nani nafaa kulinda raslimali za nchi.”

Majibu haya hayakumfurahisha Mabeyo, na alipowaeleza waliomtuma hawakufurahishwa na majibu ya rais. Maofisa hao wa jeshi wanasema ni majibu ya dharau kwa jeshi letu. Chanzo chetu kinasema: “Mabeyo analalamika kwamba wanajeshi wapo, polisi wapo, usalama wa taifa wapo, kwanini rais atumie Wanyarwanda?

Taarifa zinasema Rais Magufuli anadai kuwa haamini wanajeshi wetu kwa kuwa “mambo mengi yanayopangwa yanavuja kama ilivyokuwa wakati wa Rais Kikwete.” Chanzo hicho kinaongeza: “rais anaongoza nchi kama familia yake. Kuna mambo mengine ya hovyo ambayo inabidi yakomeshwe ili kurudisha nchi hii mstarini… ni vema naye atambue kuwa jeshi ni la wananchi, si la rais.”

Dk. Kipilimba ametengwa kwa miaka miwili mfululizo

Katika Idara ya Usalama nako mambo si shwari. Kwa miaka miwili mfululizo, kumekuwa na manung’uniko kuwa rais amekuwa anamtenga Dk. Modest Kipilimba, mkurugenzi mkuu, huku akifanya kazi nzito kwa karibu na kutoa maelekezo ya moja kwa Robert Msalika Makungu, aliyekuwa makamu wa Dk Kipilimba.

Makungu na Paul Makonda (Daudi Albert Bashite) ndio wamekuwa “watoto wapendwa wa rais,” na wanahusishwa na usimamizi wa moja kwa moja wa kikosi cha operesheni maalumu, ambacho baadhi ya maofisa wake hutokana na vikosi cha ulinzi wa rais, usalama wa taifa, JWTZ na polisi.

Kikosi hiki kimekuwa kimekuwa kinatuhumiwa kwa kuhusika na matukio ya hatari ya kuumiza, kuteka na hata “kupoteza” wananchi, hasa waliodhaniwa kuwa wapinzani au wakosoaji wa rais au serikali, walio katika taasisi mbalimbali nchini. Hata yule mtu ambaye serikali imesema “hajulikani” aliyechomoa bastola hadharani kumtisha Nape Nnauye, mbunge wa Mtama mwezi Machi 2017, alibainika kuwa mmoja wa maofisa wa kikosi cha ulinzi wa rais. Kikosi hicho hicho ndipo pia kilivamia ofisi za Clouds FM usiku Machi 2017 kikimsindikiza Bashite.

Matukio yote haya yalitokea chini ya “baraka za rais,” na ndiyo maana Bashite hakuchukuliwa hatua zozote, na Nape alipounda tume ya kuchunguza tukio hilo, akiwa waziri wa habari, sanaa na michezo, rais alimfukuza kazi, ili kuua nguvu ya matokeo ya tume yake na kumlinda Bashite.

Vyanzo vyetu ndani ya usalama vinasema idara hiyo imekuwa inakerwa na mwenendo wa watu kuteswa na kuuawa hovyo hovyo. Vinasema heshima ya idara imeathirika, na usalama wa nchi umekuwa hatarini katika kipindi ambacho rais na vijana wake wameachiwa kufanya mambo jinsi watakavyo.

Baada ya hisia za wanajeshi na usalama kuvuja, katika siku za karibuni kumekuwa na mzozo wa chini chini ukichochewa na Makungu na Bashite dhidi ya Dk. Kipilimba.  Bashite amekuwa anahaha kutafuta jinsi ya kuzuia wakubwa kumchukulia hatua. Mbali na kujilinda dhidi ya “wakubwa,” Bashite na Makungu, ambao wamekuwa wanatuhumiwa kuongoza kikosi maalumu, wamekuwa wanafanya kila wawezalo kusababisha Dk. Kipilimba aondolewe ili wao wawe salama, na Makungu ateuliwe kushika nafasi ya bosi wake.

Chanzo kimeiambia SAUTI KUBWA: “Wakabuni njia ya kushawishi bwana mkubwa. Kwa msaada wa watu kadhaa wa Kolomije walio ndani ya NIDA (Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa), wakapata habari na nyaraka kuwa zimechukuliwa dola milioni tano na kuhamishiwa kwenye akaunti ya mtoto wa kigogo wa kitengo anayesoma nje ya nchi.

“Bila kujua undani wa fedha hizo, wakampa bwana mkubwa dili hiyo wakimshtaki bosi wa kitengo. Kumbe bwana mkubwa alikuwa anajua ishu hiyo, kwa sababu ulikuwa ni mpango wake wa siri alioufanya na mtu wake ili kutunisha mfuko wa CCM katika uchaguzi 2020. Bwana mkubwa akachukia kuona Bashite na Makungu wameingilia anga zake. Kilichofuata ni boss wa kitengo naye kingilia na kumwambia bwana mkubwa achague kati yake na Makungu.

“Hicho ndicho kisa cha Makungu kupelekwa Tabora kuwa afisa tawala chini ya uangalizi. Bashite naye anachunguzwa na tume mbili mfululizo. Tume moja inaongozwa na bosi wa kitengo, na wiki hii bosi amemhoji mwenyewe Bashite. Taifa linajaribiwa kwa kitengo kunajisiwa.”

Mbali na sababu hiyo iliyotajwa hapo juu, taarifa zinasema pia kuwa Makungu alihusishwa na kutoa ushauri mbaya kwa rais kuhusu upotevu wa shilingi trilioni 1.5 zilizokosa maelezo  katika taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG). Baada ya ripoti kukabidhiwa kwa rais, kabla haijapelekwa bungeni, wasaidizi wa rais walipewa jukumu la “kuondoa kona” ambazo zingeleta taswira ya ufisadi wa serikali.

Makungu ni miongoni mwa watu ambao walimhakikishia rais kwamba rasimu ya mwisho ya ripoti hiyo waliyokubaliana nayo haikuwa na ubaya wowote; kwamba “sasa serikali ipo salama, rais yupo salama.”  Mara baada ya Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Mjini, kuibua ufisadi huo bungeni na kwa vyombo vya habari, ufisadi mkubwa ambao haujawahi kutokea katika awamu zote za serikali, rais alikasirika na kuhoji umakini wa Makungu, akisema: “kumbe naweza kupinduliwa nawe uko hapa unaniambia mambo yako sawa?” Baada ya siku chache Rais Magufuli alimpangia Makungu kazi nyingine, ambayo kwa tafsiri yoyote ile ni kumshusha cheo.

Wakuu ndani ya idara ya usalama wanadai kwamba hatua ya Makungu kuondolewa ni fursa ya kusuka upya chombo chao ili kisipoteze weledi, kwani kwa miaka miwili kimetekwa na rais na vijana wake, na kimechafuka mbele ya umma.

Sirro naye aibuka na maagizo nyeti kuzuia mauaji ya kisiasa

Wakati Mabeyo na Dk. Kipilimba wakihaha kunusuru vyombo wanavyoongoza visitumiwe hovyo na vijana wa Ikulu, Simon Sirro, Inspekta Jenerali wa Polisi, naye ameibuka na waraka kwa wakuu wa polisi katika mikoa yote nchini, akiwataka kusimamia weledi na kuepuka kutumwa na wahuni ndani ya serikali wanaotesa na kuua wapinzani.

Waraka huo, ambao kwa mujibu wa vyanzo vyetu una shabaha ya kuzuia polisi kutumiwa hovyo na Bashite na vijana wake walio katika “sistimu,” umetoka wiki hii, na umeshawafikia makamanda wote wa mikoa. Baadhi yao wameshafanya vikao na kamati za ulinzi na usalama kujulisha polisi wote kuwa nchi sasa imeanza kuchafuka kimataifa kwa sababu ya vitendo vyao hivyo vibaya dhidi ya raia

Sirro anasema baadhi ya vitendo vimesukumwa na “mabifu” binafsi ya baadhi ya viongozi na watu kadhaa, na vimehatarisha zaidi ya amani na usalama wa nchi. Anasema vitendo vya akina Bashite, vimesababisha hata yeye kulaumiwa binafsi kwani polisi wamehusika katika vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu bila sababu za msingi.

Katika hali isiyo ya kawaida, chanzo chetu kinasema Sirro ametoa agizo kwa polisi mkoani Pwani wafanye vyovyote inavyowezekana wamsake na kumpata akiwa hai Azory Gwanda, mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi aliyetekwa na “watu wasiojulikana” tangu Novemba 21, 2017. Azory alitekwa akiwa anakamilisha kuandika habari za mauaji ya raia na polisi katika eneo la Kibiti, Mkuranga, mkaoni Pwani. Wanaotuhumiwa kwa mauji hayo ya Kibiti ni wale wale “watu wasiojulikana” wa Bashite na wenzake.

Moja ya mambo ambayo watu wa karibu na Sirro wanasema yamekera jeshi ni habari za matukio yanayopangwa kuvuja kupitia Twitter na Instagram za “watu walio nje ya nchi,” na kuaibisha jeshi la polisi.

Kikimnukuu Sirro, chanzo chetu kimesema: “Unakuta jambo limepangwa sasa hivi katika kikao cha siri, halafu baada ya muda mfupi tunalisoma kwenye akaunti ya Twitter au Instagram, ya mtu yuko nje ya nchi, na ni la kweli…maana yake sisi wenyewe tunasalitiana, na hii inachafua sura ya nchi, hasa jeshi letu, kwa mambo ya siasa….Ole wake nimpate anayevusha siri hizi… Na yote haya yanatokea kwa sababu jeshi limetumiwa mno na wanasiasa. Tumeliruhusu kwa muda mrefu kutumiwa na wanasiasa, tukavuruga misingi ya kitaaluma jeshini, na amani ya nchi, na kibaya zaidi, mambo yanapokuwa yameharibika, wanaobeba lawama za moja kwa moja ni sisi vyombo vya dola badala ya wanasiasa wanaosababisha maovu hayo.”

Uamuzi huu wa ghafla wa Sirro, ambaye amekuwa anaendeshwa na Bashite katika operesheni kadhaa, umetokana, pamoja na mambo mengine, na shinikizo la kimataifa na kelele za wadau wa demokrasia walio nchini na nje ya nchi. Wabunge, hasa Zitto, Nape, John Heche (Tarime Mjini), na Hussein Bashe (Nzega), wamezungumzia kadhia hii bungeni hata Bashe akaandaa hoja binafsi ambayo spika wa bunge hakutaka iwasilishwe.

Umoja wa Ulaya na Serikali ya Marekani, kwa nyakati tofauti wamepiga kelele dhidi ya ukatili wa serikali ya Magufuli. Maaskofu wa madhehebu mbalimbali nchini wamepiga kelele katika nyaraka na mahubiri wakihimiza amani. Asasi za kiraia hapa nchini, zimeshinikiza serikali ichukue hatua dhidi ya “watu wasiojulikana” na kuitaka iandae mazingira ya kurejesha maridhiano ya kitaifa, suala ambalo hata Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) limesisitiza katika taarifa yake kwa rais siku ya maadhimisho ya Uhuru ya Vyombo vya Habari Duniani, Mei 3, 2018 yaliyofanyika Dodoma.

Wiki hii, asasi za kiraia 65 zinazotetea haki za binadamu duniani kote, zimeandika waraka wa pamoja kwa Rais Magufuli kumtaka arejeshe nchi katika mstari kwa kudhibiti siasa za kikatili zinazozuia watu kutoa maoni yanayotofautiana na ya kwake au serikali, ambazo zimeumiza watu na kupoteza baadhi yao wakiwemo waandishi wa habari, wanasiasa, wanaharakati, na hata watendaji wa serikali, wakiwemo polisi.

Kimsingi, uamuzi huu wa majeshi unakinzana na hulka, tabia, na matamko ya Rais Magufuli ambaye katika miaka takribani mitatu ya utawala wake amekuwa akitoa matamko makali mara kwa mara dhidi ya wapinzani na wakosiaji wake akisema, “nitawavunja miguu.” Sijaribiwi.” “Jeshi la polisi msitishwe na kitu, msibabaishwe na kitu. Yale mnayoyaamua amueni, na mimi nawasapoti…” Kauli hizi zimewapa jeuri polisi kutumia silaha za moto dhidi ya raia bila woga wa kuchukuliwa hatua.

Akizungumzia wananchi wanaompinga, ambao yeye anawaita wasaliti, tarehe 7 Septemba, 2017 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam, majira ya saa tano asubuhi, Rais Magufuli alisema: “…na saa nyingine mtu anapowasaliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari huwa wanajua kazi yao huwa wanafanya nini… huwezi kuwa msaliti halafu uka-survive.” Saa takribani mbili na nusu baadaye, “watu wasiojulikana” walimpiga risasi Tundu Lissu, mbunge wa Singida Mashariki, mbele ya nyumba yake mjini Dodoma, akiwa anatoka katika kikao cha asubuhi cha Bunge. Hadi leo, hakuna aliyekamatwa, na polisi wamegoma kuchunguza tukio hilo. Lissu amekuwa mpinzani kinara katika kumkosoa Rais Magufuli, na ndiye alimwita “dikteta uchwara.” Kabla ya serikali aliikuwa amekamatwa na kuwekwa ndani zaidi ya mara sita, huku akikabiliwa na kesi kadhaa za uchochezi.

Hata hivyo, wapo baadhi ya wachambuzi wanaotilia shaka taarifa zinazosambaa kuhusu uhusiano mbaya kati ya rais na Bashite, wakisema zinaweza zikawa mbinu ya kujaribu kunusuru taswira iliyochafuka ya Rais Magufuli kwa kumtenga na kikosi hiki cha mateso na mauaji ya raia.

Hata hivyo, wanasisitiza kuwa kama ni kuchafuka, Rais Magufuli ameshachafuka, kwani matone ya damu hayasafishiki kirahisi, na hana pa kutokea, maana ndiye amekuwa msimamizi na mlinzi mkuu wa ukatili wa vikosi hivi kwa nia ya kutisha wapinzani na wakosoaji wake. Hata kesi za viongozi wa kisiasa, hasa Chadema, zinazoendelea, ni matokeo ya polisi kutaka kuridhisha matakwa ya rais ambaye alisema tangu Februari 2016 kwamba anataka kuongoza nchi bila upinzani.

Baada ya Lissu kupigwa risasi, anayelengwa zaidi kwa sasa ni Freeman Mbowe, katika jitihada za Rais Magufuli kutokomeza chama hicho kikuu cha upinzani, ili “kimpishe atawale vizuri,” kwani alishasema wazi kuwa mbinu yake ni “kupiga mchungaji ili kondoo watawanyike,” na amegundua – kupitia kwa viongozi wa Chadema waliokimbilia CCM – kuwa kwa miaka 14 iliyopita, nguvu ya upinzani kimkakati imeshikiliwa na Mbowe.

Iwapo hatua hizi za majeshi zitafanikiwa, utakuwa ushindi mkubwa kwa wananchi wote wapenda amani, uhuru, demokrasia, na usalama.

Like
232
37 Comments
  1. Bagder 6 years ago
    Reply

    Good analysis

    3

    2
    • ngoko wa ngoko 6 years ago
      Reply

      Dah very painful….story bt God z able?

      2

      2
    • Mwita 6 years ago
      Reply

      Mwandishi hana jipya….Yuko biased kuponda tu.

      1

      6
  2. Mutta L. AB 6 years ago
    Reply

    Hongera kwa uchambuzi mzuri.

    Tunashukuru kwa taarifa hizi.

    6

    3
  3. Mutta L. AB 6 years ago
    Reply

    Lakini pia nakupongeza kwa ubunifu wako wa kuanzisha gazeti mtandaoni.

    3

    1
  4. KATALA 6 years ago
    Reply

    Ikiwa maneno hayo yanaukweli ndani yake na polisi pamoja na majeshi wameona hayo matatizo basi ni hatua nzuri na ni furaha Kwa wananchi Ila msimamo uko pale pale Raisi Magufuli Hana budi kujiondoa MADARAKANI Kwa hiyari yake au Kwa nguvu ya wananchi viva wanajeshi viva POLISI viva @mangekimambi_???????????

    7

    1
  5. Tqey 6 years ago
    Reply

    ✊?

    1

    0
  6. Tunahangamia. Mungu turehemu. 6 years ago
    Reply

    Unafanya kazi njema, Mungu akutunze Ngurumo. Just me in your list

    4

    0
  7. Asante 6 years ago
    Reply

    Makubwa, madogo yana nafuu!

    0

    0
  8. Juma Mirigo 6 years ago
    Reply

    Only God can help us

    3

    0
  9. Juma Mirigo 6 years ago
    Reply

    Mungu atakuwa upande wa tanzania

    1

    0
  10. Kennedy Gurusya 6 years ago
    Reply

    Acheni Uzushi Tanzania Jamani tele hatudanganyiki na uzushi wenu unaofadhiriwa na Mabeberu. Msituhalibie Nchi yetu tukufu kwasababu ya ubinafsi wako we Ngurumo na Kujifanya mkimbizi. Utajutia tu baadae kusaliti Nchi yako. Marazote Mabeberu hawana urafiki wa kudumu, mfano kina Saddam na wenzake wako wapi Hufai

    10

    28
    • Tassy 6 years ago
      Reply

      Jifunze kufikiri kama wakubwa wenzio, mtu akifanya uchambuzi kama huu inahusiana vipi na ufadhili wa mataifa ya nje? Tafakari tena ndio urudi humu

      7

      0
  11. Munguatosha 6 years ago
    Reply

    We thanks you and appreciate your imformation

    6

    2
  12. Yassin Sadik 6 years ago
    Reply

    No comments plz

    1

    2
  13. Joseph Mpyalimi 6 years ago
    Reply

    Tanzania nchi yangu….get back to where we were heading …?

    1

    0
  14. Mfalme Jeuri 6 years ago
    Reply

    Wakututetea sisi wanyonge ni Mungu tuu eeeh! Mungu tunakulilia

    1

    0
  15. Elly 6 years ago
    Reply

    Thank you for this good update. What I know is that a lot of Tanzanian we don’t have that real picture of what is going on in our government, and I thank you for been out eye opener to see this. Hope and believe you will get more support to bring out things that are unclean and ritual in this government and I believe freedom is soon to come. Love Tz.

    5

    0
    • Chesco 6 years ago
      Reply

      kama ndiyo hivyo NAJUA MTETEZI WANGU YU HAI

      2

      0
  16. Mzalendo 6 years ago
    Reply

    Watu wenye uthubutu wasipo mthibiti Magufuli nchi itaangamia tena vibaya Sana….

    6

    0
  17. STAFORD BUSUMBIRO 6 years ago
    Reply

    HUU NI UPUUZI UNAOLENGA MAMBO MAKUU MANNE
    1): KUMCHAFUA RAIS MBELEL YA WAPIGA KURA
    2): KUMKOSANISHA RAIS NA VYOMBO VYA USALAMA
    3): KUWAFICHA WATOA SIRI ZA SERIKALI AMBAO NAFASI ZAO ZINAWAPA NAFASI YA KUJUA SIRI ZA SERIKALI
    4): KUMKATISHA TAMAA RAIS KATIKA MIKAKATI YAKE.

    2

    10
  18. The Prodigy 6 years ago
    Reply

    Wanyarwanda walinde mali zetu ? Si wale wanaoiba dhahabu ya Kongo. Oh God save TZ

    0

    0
    • Amani 6 years ago
      Reply

      Hakuna mtu mwenye uhakika na Wanywaranda kulinda rasimali zetu,kama ni kweli daah inatisha maana ni hatari kwa usalama wetu,Kama kuna mtu anawaona hao Wanywaranda wapigwe picha zisambazwe mitaandaoni ili tuthibitishe maana Sisi Watanzania tunafamiana.Pia tunapend Jeshi letu likanushe hizi taarifaa za Wanyarwanda kulinda sehemu nyeti hapa sio siasa inahitajika utaifa,uzalndo na mshikamamno ambao unaleta mustakabali wa taifa letu

      3

      0
  19. Mti Mkavu 6 years ago
    Reply

    Asante kwa taarifa. Alishasema Ruge wa kuogopwa ni wawili tu Mungu na teknolojia. Unawezaje kuzuia utandawazi kwa kuzima vyombo vya habari? Tazama amezima ndani mafuriko yanapiga toka nje.

    1

    0
  20. ayubu yasini 6 years ago
    Reply

    Comment*

    1

    0
  21. ayubu yasini 6 years ago
    Reply

    mungu akuweke sana bro.

    1

    0
  22. Tanzania 6 years ago
    Reply

    Niliwahi kusema kuwa itafika mahali Nchi nzima tutaongea Lugha moja kama vile tunasali….Ni suala la Muda tu.

    Wenye Haki wataishi kwa IMANI!

    4

    0
  23. bonevira@gmail.com 6 years ago
    Reply

    Inasikitisha sana tena inaumiza sana, haina tofauti na mwanaume kuondolewa kitandani na mme mwenza na kushuhudia mkewe akilala naye, Watu wanatoka Ruanda na kuingia nchini kulinda rasilimali za Taifa na vyombo vya usalama vipo na vinakubaliana na ushenzi na dharau kama hiyo? Vyombo vyetu vya usalama vinatofauti gani na mwanaume anayeshuhudia mme anastarehe na mkewe?
    Ni mapema sana na muda unaruhusu kufanya mabadiliko, fukuzia mbali wanyaruanda hao akiwezekana wawazimishe kimya kimya tuu hapo mkuu atajifunza kitu.

    2

    0
  24. makaveli 6 years ago
    Reply

    The citzens of Tanzania are well aware of most of the things you mentioned.So for the majority of us this only saves as a reminder and bit of additional information. Everything is in black and white those who choose to ignore the facts are in a way involved in these barbaric acts .State sponsored killings and kidnappings directed at members of the opposition and those who dare to question the president and his government must stop and those responsible must be brought to justice.

    4

    0
  25. Sebba.Kee 6 years ago
    Reply

    Thanks for this special and eyes out ,,,before I wasn’t in a position of knowing all these rubbishes of Bashite…once again thanks very much.. The people united will never be defeated..

    0

    0
  26. Mpare1777 6 years ago
    Reply

    Umeunganisha matukio ukaandika tamthilia we kwel taaluma yako huijui cdhan kama unachokieleza ni kimya yashasemwa meng mitandaon…..ushaur wangu tafuta jembe ukalime mvua ndo hiz asa we unatueleza ivo cc tufanyeje???

    1

    6
    • Inkinkulenka Nkoba Sanga. 6 years ago
      Reply

      Mmmhhh

      0

      0
  27. Giant madebe 6 years ago
    Reply

    please God restore our country, now we are suffering many things are not in good order,thanks poster

    0

    0
  28. May Mosi 6 years ago
    Reply

    Mipango ya uwovu wanayopanga usiku na mchana dhidi ya faia wema wa taifa hili, haitafanikiwa na mwishowao ni aibu.

    0

    0
  29. Amani 6 years ago
    Reply

    1.Kwanini kila kitu Ruanda?
    2.Reli Ruanda
    3.Ulinzi wa sehemu nyeti eti Ruanda.
    Kagame is very intellegent,bright, creative kwa njia yyte ile ilimradi nchi yake ipate kipato ile nchi haina kitu milima tu,Hakuna kitu tunaweza faidi Ruanda zaidi ya yeye(kufaidi rasilimali zetu)JK alimuogopa sana huyu nadhani kwa kuwa alipitia jeshini kwa hiyo akapewa feedback ya PK akiwa TMA.Intelegensia ya PK ni ya kimafia(very focussed).Nashangaa kuna watu wanajibu majibu mepesi kwenye vitu vigumu(critical issues)JPM sio rais wa CCM ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. kwa hiyo akialikwa nje ya nchi ni rais wa Tanzania.

    4

    0
  30. Amani 6 years ago
    Reply

    Watu baaadhi wanaleta siasa kwenye mambo ya utaifa

    2

    0
  31. Okonkwo 6 years ago
    Reply

    Ukienda against serikali basi wewe unatumwa na mabeberu au si raia wa Tanzania hii ina maana;
    1. Elimu yetu haina nguvu ya kuzalisha watu wenye fikra huru kiasi cha kukosoa mfumo.
    2. Hakuna mtanzania mwenye nguvu na akili juu ya kuiwajibisha serikali yake.

    INASIKITISHA

    2

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.