Lissu atetea wafugaji. Awaahidi ukombozi

Kwenye viwanja vya Mnada wa Ng’ombe Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, Mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi mkuu. Mheshimiwa Tundu Lissu akihutubia maelfu ya wananchi wa Bariadi..

Nilikuja hapa bariadi miezi miwili iliyopita kuja Kuomba Udhamini, lakini Léo nimekuja kuomba kura kwa ajili ya madiwan wote halmashauri ya Bariadi ili Chadema tuchukue Halmashauri, nimekuja kuomba kura kwa ajili ya Mbunge wetu Maendeleo. Nimekuja kuomba kura kwa ajili yangu mnichague niwe raisi.

Ndugu zangu Bariadi Chadema ilani yetu inasema mambo makubwa matatu nayo ni Uhuru, Haki na maendeleo ya watu. Nchi yetu imeminywa uhuru wa watu, uhuru wakuhoji, Uhuru wa vyombo vya habari. (Ananukuu maneno ya Mwalimu Nyerere “Kama hakuna uhuru wa watu basi hakuna maendeleo ya watu.”)
Imekuwa shida nchi hii ukimsema Magufuli hata kwa ukweli basi utashgulikiwa na watu wasiojulikana au polisi. Wabunge mnachagua wamefungwa midomo, Wakisema wanapigwa. Bunge likikaa kimya basi wananchi Wanapigwa.

Simiyu ni wafugaji, lakini miaka mitano hii mmenyanyaswa sana wafugaji wameuliwa sababu wanachunga mifugo karibu nahifadhi, serikali Ya CCM imewanyang’anya mifugo na imethubutu mpaka kuwapiga risasi mifugo yenu.

Simiyu mnalima Pamba lakini wanaotajilika ni CCM. Mnalima kwa pesa zenu lakini mnalazimishwa muwakopeshe maCCM kwa pesa wanazotaka wao. Na haya yote yanafanyika sababu tumekosa uhuru wakuyakataa haya. Wananchi hamna uhuru, wakijisikia mara changia mwenge, mara nini Ilimradi tu.

Bariadi ngoja tuongee kuhusu vitambulisho vya utapeli vilivyotolewa na ofisi ya raisi, Vitambulisho havina jina, picha, anwani wala sahihi sasa vinamtambulishaje. Vimetolewa nchi nzima bila risiti, sasa nawaambia pesa za vitambulisho ndo wanatumia kwenye kampeni. Anazunguka nchi nzima na msururu wa magari ambao pesa zote nizakitambulisho. Tulipoanza kumsema Magufuli akasema kwanza sio lazima, tukamwambia kama sio lazima basi rudisha pesa za watu wote. Yote haya yanatokea sababu hakuna uhuru wakusema.

Mauaji ya wavuvi kwenye maziwa yote nchi nzima.

Maslahi kwa watumishi wa umma, Serikali ya CCM haijaongeza mishahara kwa miaka mitano. Wakati katiba yetu inasema kila mwaka kuwe na ongezeko la mshahara ili kumudu hali ya maisha.

Sasa watu wa Bariadi tarehe 28 mkapige kura kwa ajili yenu, tukapige kura kumuondoa Magufuli ili iwe nchi huru. Bariadi nawaomba muipe dhamana Chadema ili itekeleze agenda ya uhuru, haki na maendeleo ya watu. Chagueni madiwani wote wa Chadema ili wawatetee kwenye halmashauri, chagueni wabunge wa Chadema wakawatete Bungeni. Bariadi nichagueni Tundu Lissu nikawe raisi atakaye wafariji nakuwatendea haki. Tarehe 28 mkapige kura kwa wingi nakulinda kura.

Ahsante Bariadi na Simiyu kwa ujumla.

Like