Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 17, Januari 2022.
Jaji ameingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa leo Jumatatu ya Tarehe 17 Januari 2022
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo Pamoja na
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka Wote Mawakili Wa Serikali Waandamizi
Pamoja na Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na Mawakili
Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Faraji Mangula
Dickson Matata
Seleman Matauka
Michael Mwangasa
Khadija Aaron
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja na tupo Tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Nasisi pia Tupo Tayari Kuendelea
Shahidi anakwenda kuitwa
Anakuja Kwa Mbali Shahidi Wa Kiume
Jaji: Majina
Shahidi: Inspector Innocent Ndowa
Jaji: Umri
Shahidi: 37
Jaji: Kabila
Shahidi: Mchaga
Shahidi: Mimi Inspector Innocent Ndowa Naapa Kuwa Ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu Nisaidie
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ataongonzwa na Wakili Pius Hilla
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Majina Yako Kamili ni nani
Shahidi: Naitwa Inspector Innocent Ndowa
Wakili wa Serikali: Unafanya Kazi gani
Shahidi: Mimi ni Askari Polisi
Wakili wa Serikali: Tangu lini Shahidi: Mwaka 2012
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kituo chako Cha Polisi cha Kwanza
Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Ya zamani
Wakili wa Serikali: Ulisema Ya Zamani Una manisha Nini
Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, posta Kabla hayajaamishiwa Dodoma
Wakili wa Serikali: Kazi yako ni Ipi huko Polisi
Shahidi: Wakati Naanza Kazi nilikuwa Katika Kamisheni ya TEHAMA Makao Makuu
Wakili wa Serikali: Ulifanya Kazi hadi lini
Shahidi: Mwaka 2014
Wakili wa Serikali: Mwaka 2014 kilitokea Kitu gani
Shahidi: Nikahamishiwa katika Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi
Wakili wa Serikali: Ipo wapi
Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Ya Zamani
Wakili wa Serikali: Kamisheni Ya Uchunguzi Wa Kisayansi upo Kitengo Gani
Shahidi: Nipo katika Uchunguzi Wa Makosa ya Kimtandao, Yaani Cyber Crime
Wakili wa Serikali: katika Hilo Kitengo Una Muda gani
Shahidi: Kwa sasa Nina Miaka 8
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Kitengo hicho cha Cyber Crime Kina husika na Nini hasa
Shahidi: Kina Husika na Uchunguzi Wa Vifaa Vya Ki Electronics Ambavyo vinadhaniwa Kutumika Katika Matukio Mbalimbali ya Kihalifu
Wakili wa Serikali: Sasa wewe ni nani Katika hicho Kitengo
Shahidi: Mimi ni Computer and Mobile phone Forensic Analyist
Wakili wa Serikali: Wewe Ukiwa kama Computer and Mobile phone Forensic analist Majukumu yako ni Yapi
Shahidi: Kupokea Vifaa Kama Computer na Simu ambavyo vinatuhumiwa Kuhusika katika Matukio Mbalimbali. Kazi ya Pili ni Kufanya Uchunguzi Mbalimbali Kufuatia Maombi Ya Taasisi Mbalimbali, Kuandaa Ushahidi
Wakili wa Serikali: Fafanua Hilo Jukumu la Kuandaa Ushahidi
Shahidi: Inapotokea Kifaa kimekuja, Kuna Utaratibu Wa Kuandaa Ushahidi Wa Namna Kifaa Kilivyo kuja, Jukumu hilo ni la Kwetu la Kiuchunguzi Jukumu lingine ni Kuandaa report ya Uchunguzi Jukumu lingine ni pale ninapohitajika Kutoa Ushahidi Basi naenda Kutoa Ushahidi
Wakili wa Serikali: Wewe Shahidi Ni Analyist, Sasa Ifahamishe Mahakama Unautaaluma gani
Shahidi: Kwaka 2009 nilihitimu Katika Chuo CHA usimamizi wa Fedha IFM katika… 2012 nilijiunga katika Jeshi la Polisi 2014 nilifanya Certificate in Ethical Hacking, Taasisi Ya Uingereza Ipo DSM, Upanga
August 2014 nilifanya Kozi inaitwa Penetration Testing, Chini ya Taasisi inaitwa ATU ikifanyika Dar es Salaam Chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania November 2014 ndiyo Niliingia Forensic bureau
Nilienda Kozi Nyingine India ambayo inaitwa Certificate course in Networking, ilifanyika katika Chuo kinaitwa UTL Technology Limited Mwaka 2016 June Nilifanya Training Nyingine Dar es Salaam inaitwa Identification and Seizure of Digital devices ambayo ilitolewa na Taasisi ya Chini ya Ubalozi wa Marekani ambayo inaitwa BUREAU OF DIPLOMATIC SECURITY July 2016 nilifanya Training Nyingine ambayo inaitwa Network Security administration Version 4 ambayo ilitolewa na Link Academy
Kozi Nyingine Chini ya Ubalozi wa Marekani ambayo inaitwa Terrorist Crimes Scene Investigation September 2016 nilikwenda Nchini Egypt kufanya Kozi inaitwa CRIMINAL INVESTIGATION AND CRIME SCENE
Shahidi: Mwaka huo huo November Chini ya Ubalozi Wa Marekani Nikifanya Kozi INAITWA DIGITAL LABORATORY FORENSIC MENTORSHIP PROGRAM. Mwaka 2018 March Nchini RWANDA nikafanya Kozi inaitwa CYBER CRIME INVESTIGATION
Mwezi may Mpaka June 2018 Nilienda Nchini Uganda Kufanya Kozi inaitwa CYBER SECURITY Mwaka 2021 nilifanya Kozi Nyingine Katika UNIT ACADEMY ambapo nilifanya Kozi ya Certificate of Hacking, Version 12
Wakili wa Serikali: Shahidi Umeeleza Vyema Kuhusu Ujuzi na Taaluma Yako, Eleza Mahakama Taratibu za Upokelewaji wa Vielelezo Vya Ki Electronics
Shahidi: Utaratibu wa Upokelewaji Wa Vielelezo Vya Ki Electronics Unaanza Katika Kitengo Chetu ambapo Pale Unakutana Na Mapokezi Ukiwa na Barua na Kielelezo Husika, Unamkabidhi Ofisa wa zamu
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama sasa Upo pale na Kielelezo Kimefika
Shahidi: Jukumu la Ofisa wa Zamu, Ni Kwanza Kukagua Kielelezo na Barua Husika
Wakili wa Serikali: Unakaguaje?
Shahidi: Kwa kufanya Identification, Barua Ka Ina Kifaa kama Simu lazima Iwe namba Kama IMEI namba, Unakagua kama Ipo
Shahidi: Baada ya Identification Ofisa Amejiridhisha Wajibu wake ni Kuvipa Usajili Wa Maabara
Wakili wa Serikali: Usajili Unafanyikaje
Shahidi: Unafanyika Kwa Mwaka Husika, Kwa Reference namba ya Barua, Useme Imetoka Himaya ya nani, Tarehe iliyofika Kwako na Vielelezo Vilivyofika kwako
Wakili wa Serikali: Una sajili Kwenye nini
Shahidi: Kwenye Kitabu Cha Maabara Kutoa Lab Namba
Wakili wa Serikali: Hiyo Lab Namba Inapatikanaje
Shahidi: Inatolewa In sequencial Series Pale ambapo Mwaka Unaanza unasajili namba moja
Wakili wa Serikali: Hatua Inayofuata ni nini
Shahidi: Hatua Inayofuata ni Kifungua Jalada
Wakili wa Serikali: Jalada linafunguliwa kwa Madhumuni gani
Shahidi: Kwa Kuangalia Vielelezo na Kutunza Vielelezo, na Kama Kazi Ifanyika
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kinafanyika
Shahidi: Kielelezo Chenyewe Kinatakiwa Kutunza Kwenye Roka lake, Kwa ajili ya Kutunza Kielelezo, na Baadae Jalada lina enda kwa Commanding Officer na Baadae kwa Kamishina Kwa ajili ya Kutolea Maelekezo na Kupanga kazi
Na Baadae ndipo linarudi Kwa ajili ya Kufanya Kazi na Kuchukua Vielelezo hivyo..
Shahidi: Ni Kufanya Uchunguzi, Kwa Mujibu wa Ratiba yake, Wajibu wake ni Kutunza na Kufanya Kazi ya Uchunguzi
Shahidi: Ni Kufanya Uchunguzi, Kwa Mujibu wa Ratiba yake, Wajibu wake ni Kutunza na Kufanya Kazi ya Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Tuongelee Uchunguzi Wa Hivi Vifaa, Uchunguzi wa hivi Vifaa Vya Ki Electronics vinachunguzwa Vipi, Kwa Kifupi
Shahidi: Uchunguzi wa hivi Vifaa Unafanyika Kwa Hatua tatu
Wakili wa Serikali: Hatua zipi
Shahidi: Ya Kwanza ni Aquirezation Maana yake Unafanya Extraction ya Kifaa Husika
Wakili wa Serikali: Una Extract nini
Shahidi: Taarifa zinazotokana na Kielelezo
Shahidi: Hatua ya Pili Unafanya Analysis Hatua ya Tatu Unafanya Reporting
Wakili wa Serikali: Hivi Vielelezo ni Vielelezo Vya Namna Gani ambavyo Vinafanyiwa hizi Hatua
Shahidi: Vielelezo Vya Electronics, Mobile Phone, Gard Disk, Flash Disk, Sim Card, Memory Card, na Vifaa Vingine Vyenye Asili Kama hiyo
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Uchunguzi Wa Vifaa Vya Namna hii Unafanyika Kwa Vifaa gani
Shahidi: Kwa Kutumia Vifaa Vya Uchunguzi wa Kimaabara kwa Vifaa Vinaitwa CELEBRITE MACHINE
Wakili wa Serikali: hiyo CELEBRITE MACHINE Inafanyaje kazi
Shahidi: Inakuwa na Kifaa Kinaitwa LAGADIZZED ambacho ni Computer ambayo inakuwa na Windows ndani yake ambayo ni UNIVERSAL FORENSIC EXTRACTION DEVICE (UPC)
Wakili wa Serikali: Mbali na hicho, Kingine ni nini
Shahidi: Forensic Cables pamoja na Adapter Pia Kuna Kifaa Kingine Kinaitwa CELEBRITE PHYSICAL ANALYISER
Wakili wa Serikali: Software ambazo mnazotumia ni nini
Shahidi: Ni CELEBRITE PHYSICAL ANALYISER NA UPC unakuwa na Kifaa Kinaitwa DONGLE license kwa ajili ya Kufanyia Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Hujaielezea Mahakama Extractions Zinafanyika Vipi
Shahidi: Extraction inafanyika Kwa Kufanya Kifaa Husika Kama ni simu au kingine, kinaunganishwa na Mashine ya Uchunguzi Kwa Kutumia Forensic Cables
Wakili wa Serikali: Ili hicho Kilichopo kwenye Kielelezo ili kiweze Kuchukuliwa ni Nini Kinafanyika
Shahidi: Kwanza Ile UPC lazima Ui run kwenye Mashine, Ukiwa tayari umesha connect Device Yako Kwenye ile Mashine kile Software Ina Detect Kile Kifaa
Wakili wa Serikali: Kwa sababu gani
Shahidi: Kwa sababu Architecture ya Kile Kifaa Kinaundwa na Software mbalimbali za Zile Devices
Wakili wa Serikali: Inapo Detect Kuwa Umeunganisha Devices na Kifaa Je Ni taarifa ipi Inatoa
Shahidi: Ina Tegemea Na Kifaa Ulicho tumia, Itakuoa aina ya Extraction ambayo Inaweza Kufanya Katika hicho Kifaa
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Kikubwa ni hicho.
Wakili wa Serikali: Nimekuuliza Information ambazo Zinakuwa Detected na zile simu ni zipi
Shahidi: Kama IMEI namba na Mobile Phone Namba
Wakili wa Serikali: Kina Kuwa ni Kielelezo gani
Shahidi: Kwanza lazima Ufanye Isolation, Kwa kutumia Flight Mode au Faraeay Forensic
Wakili wa Serikali: Kwanini Iwe hivyo Shahidi: Kwa sababu ya Forensic principles ili Ku’ mantain Data zilizopo Ndani, na Ushahidi Utakaotoa uweze Ku’ Sound
Wakili wa Serikali: Na Kifaa unachotumia Kufanya Uchunguzi Kinatakiwa Kuwa Katika hali gani
Shahidi: Kwanza Kinatakiwa Kuwa na Software ambazo zipo Updates kwa Maana ya Windows pamoja na Severs, Pamoja pia na Physical analyser, Lazima Wakati wote Kifaa Kisiwe na Any Connection ya Internet Wakati wote wa Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Kwanini Shahidi?
Shahidi: Ili Kuzuia kwa namna yoyote ile Mtu ambaye hayupo Physical asiweze Ku’ access Kile Kifaa
Wakili wa Serikali: Baada ya Ku’ Extract Vitu Vyote Unaviweka wapi Shahidi
Shahidi: Unaviweka Katika Storage ambayo Inakuwa Ndani ya Computer
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ambapo Extraction inakuwa Imekwisha
Shahidi: Pale ambapo Mashine inakwambia Imemaliza, Una accept YES
Wakili wa Serikali: Unasema Inafanya Storage Ndani
Shahidi: Ndiyo ni Kifaa kinachokuwa na Hard Disk Ndani, Kwahiyo Unachagua Kuweka katika Partition Baada ya Kufanya Kazi yake
Shahidi: Hatua inayo fuata ni analysis ya Extracted Data Analysis Inafanyika kwa Kutumia CELEBRATE PHYSICAL ANALYISER Mfumo huu una kazi Kuu tatu, KAZI ya Kwanza ni Kufanya RECORDING, ANALYISIS kwa Kufanya Advanced Search ya Stored Data na ya Tatu ni DECORDING
Wakili wa Serikali: unaposema DECORDING ina maana gani
Shahidi: Huwa tunapata Extraction ambazo kwa Jicho la Kawaida huwezi Kuziona, Sasa Mfumo unafanya Kuona Taarifa kwa Usahihi Kabisa, Process Nzima Ndiyo tunaita DECORDING
Wakili wa Serikali: Unaposema Search katika Uchunguzi Wenu Maana yake ni Nini?
Shahidi: Tunapo fanya Uchunguzi Maana yake Tunatafuta Ushahidi, Kwa Mfano Kwenye terms of reference Unapata Unachotafuta na inakuletea Majibu
Shahidi: Hizo nazipata Katika Barua
Wakili wa Serikali: Barua Ipi
Shahidi: Ya Mpelelezi ambaye ameomba Uchunguzi Wa Kisayansi ufanyike
Wakili wa Serikali: Elezea Vizuri Madhumuni ya hiyo search ni Kitu gani
Shahidi: Ni Kusaidia Uchunguzi, Kwa kuwa tuna simu ambazo Zina hifadhi Data Nyingi, Kama GB 200 Sasa yenyewe Inakusaidia Kwenda Direct katika Kitu unachokitafuta Unaenda Moja Kwa Moja kwenye Text Meseji, Mult Media,
Wakili wa Serikali: Pia Ulitaja Advanced Search, Je hiki ni Kitu gani
Shahidi: Inafanya Indepths Diving Hiden, Pale ambapo Kitu ambacho unatafuta Kina Kuwa Hiden au Kimekuwa Deleted, Sasa Yenyewe inatafuta ili Kuleta Majibu
Wakili wa Serikali: Na hii Madhumuni yake ni Nini
Shahidi: Kutafuta Ushahidi Ulipo
Wakili wa Serikali: Hapo Mwanzoni Ulisema Kuwa Mashine Ulisha connect kupitia Forensic Cables kupitia Profile yake, Je Kama Hakuna Profile Yake
Shahidi: Kama Profile ya Kifaa Haipo, Manufacturer amekupa Option Ya Kufanya Extraction Ku’ base Kwa Operating System au Kwa Chip Search ya Simu
Wakili wa Serikali: Tuongelee sasa reporting, Je inafanyikaje?
Shahidi: inafanyika pale ambapo Imetambulisha zoezi la Analysis, Kwenye Mfumo ambapo kisha funga Zoezi hilo inaenda Next Stage ambayo ni Reporting ambapo Inakuoa Fursa Mchunguzi Kuweka Details ambazo Zinahusiana na Kesi
Wakili wa Serikali: Reporting hizi zinfanyikia wapi
Shahidi: Zinafanyika kama Segment ndani ya Mfumo wa Physical analyser
Wakili wa Serikali: Inafanyikaje
Shahidi: Mchunguzi anaweka Jina la Mtuhumiwa, Namba ya Kesi, Taasisi ambayo Inafanya Uchunguzi, Majina yake, pamoja na namba ya Kesi, Lab Namba pia
Wakili wa Serikali: Tofauti na Taarifa hizo, Kwenye Segment ya Report Kuna Taarifa zipi Nyingine
Shahidi: Taarifa zingine ni zile zimekuwa generate katika Mfumo ambazo Zinahusiana na Mfumo
Wakili wa Serikali: Muda wote Extraction, na Reporting zile Data znazokuwa Katika Kielelezo Zinakuwa katika Hali gani
Shahidi: Wakati wote Wa Process inafanyika Mashine Ina Kitu Kinaitwa….ambacho Kina ruhusu Kutoa Taarifa lakini hakirihusu Manipulation ya Taarifa ya aina yoyote
Lakini Pia Lengo la analysis hatutaki Content yote ya kwenye simu, Mchunguzi anakuwa anahitaji Taarifa ambazo anazitaka kwa ajili ya Uchunguzi wake
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Mambo yote Yamefanyika, baada ya hapo ni Kitu gani Kinafuata
Shahidi: Baada Reporting Kufanyika Kama Content si Kubwa Unaweza Ku Print kama ni Kubwa Unaweza Kwenye Storage, Kama DVD, FLASH DISK kutegemeana na Ukubwa
Wakili wa Serikali: Kwa Content ambazo ni Chache Unasema Unaprint, Je Ulisha Print ni Kitu gani Kinafuata
Shahidi: Kama Ume’ print na Kulinganisha Taarifa Yako, verification Kuangalia Usahihi
Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo
Shahidi: Ni Kujiridhisha Kama Ulicho nacho na Kwenye Mfumo ni sawa
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama tofauti na print out, Vielelezo vinakuwaje
Shahidi: Kwanza Mtu wa Maabara Unatakiwa Uweke MARK Kwa ajili ya Utambuzi na Ndiyo utayotumia katika Report yako
Wakili wa Serikali: Baada ya hapo
Shahidi: Unaweka Muhuri Ambao Una Nembo ya Polisi na FORENSIC BEAURRIAL, unasaini
Wakili wa Serikali: Ile Report yako sasa Unayoandaa Inakuwaje
Shahidi: Ya Kwanza inakuwa na Extract ambazo tumezipata, Lazima iwe na Vielelezo Vyote ambavyo Vimeletwa Pale, lazima iwe na Majina ya Uchunguzi
Shahidi: Ya Kwanza inakuwa na Extract ambazo tumezipata, Lazima iwe na Vielelezo Vyote ambavyo Vimeletwa Pale, lazima iwe na Majina ya Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Kuhusiana na Uchunguzi wenyewe
Shahidi: Taarifa Yangu itajibu Maombi ya Taarifa iliyoomba
Wakili wa Serikali: Baada ya Kusaini kitu gani unafanya
Shahidi: Mchunguzi anakuwa na Jina lake, namba ya Simu, Tarehe ya Uchunguzi ambao Umefanyika Unaenda Kuzihifadhi katika Roka lako la Kuhifadhi Kazi za Uchunguzi zilizokamilika
Wakili wa Serikali: Kuhifadhi kwa Madhumuni gani
Shahidi: Kuhifadhi sababu wewe Ndiyo Responsible na Utatoa Siku Vinavyohitajika
Wakili wa Serikali: Tarehe 13 August 2020, Unakumbuka Siku hiyo ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa katika Kituo Changu Cha kazi Katika Maabara Ya Uchunguzi wa Kisayansi
Wakili wa Serikali: Siku hiyo ulitekeleza Majukumu yapi
Shahidi: Nilikuwa Ofisa wa Zamu Mapokezi
Wakili wa Serikali: Ofisa wa Zamu Mapokezi Wapi?
Shahidi: Katika Ofisi yetu ya Cyber Crime
Wakili wa Serikali: Majukumu yako yalikuwa yapi
Shahidi: Kupokea Kazi zinazo kuja Kwa ajili ya Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Siku hiyo ulipokea Kazi Ipi
Shahidi: Moja ya Kazi niliyopokea ilikuwa ni Kutoka Katika Ofisi ya DCI
Wakili wa Serikali: Siku hiyo Ulipokea Kazi gani
Shahidi: Nilipokea Barua na Simu ambazo ambazo zilikuwa zipo Nane
Simu hizo ziliambatana na Barua
Wakili wa Serikali: Barua Ilikuwa ina kazi gani
Shahidi: Barua Ilikuwa inaomba Kufanya Uchunguzi katika Vile Vielelezo, Maombi yalikuwa sehemu Kuu tatu
- Sehemu ya Kwanza ilikuwa inaomba Kuangalia Mawasiliano Kupitia Mitandao ya Kijamii Kama Telegram, WhatsApp, Mawasiliano ya Jumbe za Simu, Mawasiliano ya Miamala ya Fedha, Mawasiliano ya Kupiga na Kupigiwa, Kati ya Vielelezo Vyote Nane against kwa namba za simu Kadhaa ambapo sikumbuki zilikuwaje 2. iliomba Usajili Wa Namba Tajwa, 3. Taatifa zingine zozote zitakazo saidia Katika Upelelezi
Wakili wa Serikali: Ukiwa kama Afisa Wa Zamu Baada ya Kupokea Ulifanya Nini
Shahidi: Kwanza Nilikagua Kwa Maana ya Kufanya Verification Kama Kile Kilichopo Kwenye Barua Lipo sawasawa
Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo
Shahidi: Baada ya Verification na Kuona Vipo sahihi nilivisajili na Kuvipa Kumbukumbu namba ya Maabara ILIKUWA NO. FB/CYBER /2020/LAB/479
Wakili wa Serikali: Baada ya Usajili Kumalika Kitu gani Kilifuata
Shahidi: Ni lifungua Jalada, na Kwenda Kuhifadhi Katika Roka Langu
Wakili wa Serikali: Roka gani Shahidi Kila Mchunguzi ana Roka lake, Kwa hiyo Mimi peke yangu Ndiyo Nina Access na Roka. Langu
Shahidi: Kila Mchunguzi ana Roka lake, Kwa hiyo Mimi peke yangu Ndiyo Nina Access na Roka. Langu
Shahidi: Commanding Officer Wangu a lini assign Kufanya Ile kazi
Wakili wa Serikali: Nani alikuwa assigned
Shahidi: Mimi Assistant Inspector Innocent Ndowa
Wakili wa Serikali: Assistant Inspector Innocent Ndowa ni yupi
Shahidi: Ni Mimi hapa kabla Sijapanda Cheo ndiyo Nilikuwa naitwa Assistant Inspector
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuvisajili
Shahidi: Nili hifadho Katika Roka Langu
Wakili wa Serikali: Kingine?
Shahidi: Sikufanya Lolote zaidi ya Kuhifadhi Mpaka Siku nafanyia Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Katika Kutekeleza Uchunguzi wa Vielelezo hivi Vitu gani Ulifanya. Je Maelekezo Ya Kupata KYC na Miamala ya Simu Ulifanyeje Kutekeleza?
Shahidi: Taarifa za KYC na Miamala hazipo Katika Himaya yangu niliwajibika Kuomba kutoka kwa Watoa Huduma
Wakili wa Serikali: Je, ni Watoa huduma wapi hao
Shahidi: Niliandika Barua kwenda Tigo pamoja na Airtel
Wakili wa Serikali: Kwa Watoa huduma uliomba nini na Nini Shahidi: Niliomba KYC Kwa Maana (KNOW YOUR CUSTOMER) na Miamala Ya simu
Shahidi: Nakumbuka Ilikuwa Tarehe 01 July 2021, NILIOMBA kwa kutumia namba ya Kesi. Nakumbuka CD IR /2027/ 2020
Wakili wa Serikali: Hiyo namba ni ya Kitu Gani
Shahidi: Namba ya Kesi Kutoka Kwa Mpelelezi
Wakili wa Serikali: Madhumuni ya ku Indicates hiyo namba ni nini
Shahidi: Ku verify Kuwa kweli Pana Jinai Kuhusiana na Kesi namba hiyo, Kwa Chochote kama atahitaji Na Yeye Kuhakiki
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama sasa ni lini Ulipata Majibu Kutoka kwa hao Watoa huduma Shahidi: Majibu nilipata Tarehe 02 July 2021
Wakili wa Serikali: Kitu Gani Kingine Sasa Ulifanya
Shahidi: Kwanza Nilitaka Kuthibitisha hicho, nikawa nimehifadhi
Wakili wa Serikali: Jambo Jingine ulilofanya.?
Shahidi_ Baada ya Kupata hizo Taarifa Nikaanza Kufanya Uchunguzi Wa Vile Vielelezo
Wakili wa Serikali: Vielelezo gani
Shahidi: ambazo zilikuwa Ni simu nane
Wakili wa Serikali: Ulifanya Uchunguzi Kwa Kufanya nini
Shahidi: Nilitoa Vielelezo Vyangu Kutoka Kwenye Roka, nikaweka Mark
Wakili wa Serikali: Eleza Jinsi Ulivyo weka Mark
Shahidi: zilikuja Zikiwa na Mark, lakini Bado nikazipa Alama za Kimaabara kwa kuzipa A Mpaka H Pembeni Nikazipa Maneno LAB 479
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine Kilifuata
Shahidi: Kwa Maana ya Identification nilizipa Mark Nikianza kwanza Kwa Kuandaa Vitendea Kazi Mashine Kama CELEBRITE
Wakili wa Serikali: Hiyo Mashine Uliyotumia ya CELEBRITE Ukitumia ina Namba gani
Shahidi: ilikuwa U face for PC 7:4:4 lakini namba Nyingine Sizikumbuki
Wakili wa Serikali: Version Ya Mwaka gani
Shahidi: Ya 2021
Wakili wa Serikali: Wakati Unafanya Uchunguzi Software Zilikuwa za Mwaka gani
Shahidi: Kwa ajili ya Kufanyia Uchunguzi ilikuwa ni 7:4:4 ya Mwaka 2021 na Kufanyia Extraction ni 7:4:0 WS: Umadhubuti Wa Vifaa hivyo ulikuwaje
Shahidi: Vifaa Vile vinatumia Genuine Windows, za LICENSED SOFTWARE kutoka Microsoft
Wakati Mwingine wa zoezi Zima tulikuwa tunafanya Updates…
Wakili wa Serikali: Mara ya Mwisho Kufanyia Updates ilikuwa ni lini
Shahidi: Kwa Upande wa CELEBRITE Ilikuwa NI Mwezi July
Wakili wa Serikali: Jambo Jingine?
Shahidi: tuna Install Mashine, Pia Vifaa hivi Vina Rights Broke Hakuna any internet Connection,
Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo Shahidi: Unachukua Cable na Ile simu, Unaunganisha kwenye ile simu
Wakili wa Serikali: simu 8 ulizokuw nazo zilikuwa simu za aina gani
Shahidi: Tecno zilikuwa Nne, Itel zilikuwa Mbili, Samsung Ilikuwa Moja na Simu Moja inaitwa BUNDI
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Kila simu Ilkuwa Connected, Je kwenye Extraction ya kila simu ilikuwa Wapi
Shahidi: Kila simu Destination ilikuwa Kwemye Mashine (Computer)
Wakili wa Serikali: Hali ya Hizo Simu zilikuwaje
Shahidi: Kila simu Ilikuwa katika Flight Mode
Wakili wa Serikali: Fafanua Flight Mode Unamaanisha Nini
Shahidi: Ni Mode ambayo Simu haiwezi Kupata Communication
Wakili wa Serikali: Intergrity ya Vifaa ilikuwaje
Shahidi: inaposoma Hakuna Uwezo Kuongeza au Kupunguza Kufuatia Uwepo Right Broke
Wakili wa Serikali: Mashine yako ili Detect Kwa Kusema nini Shahidi Baadhi ya su ili Detect lakini baadhi ya Simu Ili Detect kupitia Sim Card, Na OS yake
Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Mpelelezi anataka Kubaini Mawasiliano, Kwenye analysis sasa Katika simu zote Nane analysis yako ili baini Kitu Gani
Shahidi: Katika analysis Simu ambazo zilikuwa na Majibu Positive tulibaini Simu Nne ambapo tulibaini kupitia Mitandao ya Kijamii
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Kwenye Process ya analysis ulibaini nini
Shahidi: Software Zote Zina fanya katika Same Technology
Wakili wa Serikali: Kwenye Baadhi ya Simu Ulipata nini
Shahidi: Mawasilisho ya Mitandao ya Kijamii Kama WhatsApp, Telegram, Facebook, Call Logs, call za social Network..
Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa analysis ushakamilisha, Je Kitu Ulifanya?
Shahidi: Katika zile simu Nne Zenye Majibu, Nilienda Kwenye Reporting, unaweka Details na Baadae Nika print Taarifa
Wakili wa Serikali: Taarifa ya Simu Ngapi Shahidi Ya Simu Nne
Wakili wa Serikali: Baada ya Ku Print Ukafanya nini
Shahidi: Nilipata Muda wa Kuandaa Taarifa yangu ya findings zangu
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Lini
Shahidi: Ilikuwa ni Tarehe 09 July 2021
Wakili wa Serikali: Report Ilikuwa ni Kuhusu nini
Shahidi: Kuelezea Uchunguzi Niliofanya
Wakili wa Serikali: Baada ya kumaliza kuanda report ulifanya nini
Shahidi: Nikajiridhisha Kama zipo Sahihi, nikagonga Muhuri
Wakili wa Serikali: Muhuri gani
Shahidi: Wa Forensic Beaural, Tanzania, Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Je Vielelezo Vyenyewe Ikawaje
Shahidi: Baada ya Kukamilisha, Vile Vielelezo nikaviweka Seal ya Plastic Bag ambapo ilikuwa na Majina yangu, Tarehe na Sahihi na Kwenda Kuhifadhi Katika Roka Langu
Wakili wa Serikali: Ukasema Umehifadhi Kwenye Roka, Je Kwa Madhumuni gani
Shahidi: Kuhakiksha Vipo Salama na Kwa Ajili ya Usalama Wake Kuwa Hivi Ndiyo Nilivyo Viacha
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba ni Lini sasa, Hiyo Taarifa ilichukuliwa
Shahidi: Tarehe 06 August 2021
Wakili wa Serikali: Ni nani uliye Mkabidhi
Shahidi: Anaitwa Inspector Swila
Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Vitu gani
Shahidi: Vielelezo Vyote Nane, Taarifa ya Vifaa Kwa Maana Simu Nne, Nilimkabidhi Taarifa yangu ya Findings
Nilimkabidhi Taarifa Nne kutoka kwenye zile Simu Nne Zenye Ushahidi Nilimkabidhi Taarifa kutoka kwa Watoa Huduma
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumkabidhi Uliendelea na Jambo gani
Shahidi: Niliendelea na Mambo yangu Sababu nilikuwa Nimeshamaliza
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Hairisho, Sasa ni saa Saba Kasoro 4
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Inategemea Kabakisha Kiasi gani, ila amekuwa anarudia sana Maswali Mpaka Shahidi anamkumbusha Kama nilivyosema..
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Hairisho Bado sana
Jaji: Kwa Muda Gani
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Naomba Hairisho la Lisaa Moja
Kibatala: Tulikubaliana na Wakili wake Kiongozi Dakika 45 sijui 1hr anatoa wapi
Jaji aandika Kidogo
Jaji: Dakika 45 zinatosha tutarudi hapa Saa Nane Kasorobo
Jaji anatoka…
Jaji amerudi Mahakamani
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa, Quorum ipo Kama awali
Kibatala: Mhe Jaji Kama utakumbuka Niliomba Wakili Nashon Nkungu atakapofika nitamtambulisha na Kwamba Anabadilishana na Wakili Mtobesya ambaye ameitwa na Rais wa TLS
Jaji: Shahidi nakukumbusha Bado Upo chini ya Kiapo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: kwenye Ku access ile Mashine PALE LAB ikoje
Shahidi: Kila User ana akaunti Password za ku-log in kuweza Ku access
Wakili wa Serikali: Akaunti Zina nini
Shahidi: User name na Password
Wakili wa Serikali: Nani anaye Create Password
Shahidi: Unapokuwa Unaingia mara ya kwanza Ofisi Ina Utaratibu Wa Kutengeneza User akaunti Pale ambapo Mashine imenunuliwa
Wakili wa Serikali: Password Inatengenezwa na nani
Shahidi: Wewe Mwenyewe unayetumia ile Mashine
Wakili wa Serikali: USER name yako ni nani
Shahidi: Nina Reserve Sababu za Kiofisi
Wakili wa Serikali: Shahidi Tumeshaongea Vitu Vingi baada ya Kutengeneza Taarifa na attachments Kutoka Tigo na Airtel ina Vitu gani
Shahidi: Kwanza Itakuwa na Barua niliyo tumia Kuomba Taarifa, Itakuwa na Barua Kutoka Ofisi ya Uchunguzi Kwenda Tigo ambayo imesainiwa na Ofisa anaitwa NAFTALI JOSEPH kwa Niaba ya Kamishina, itakuwa na Kumbukumbu namba
Wakili wa Serikali: Ile Barua ya Kutoka Tigo inakuwa na Vitu gani
Shahidi: Inakuja Barua ina Nyaraka ya KYC na Miamala ya Fedha
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Taarifa hizo ziliwasilishwa Zikiwa na Kitu gani
Shahidi: Barua ambayo Imetoka Kampuni ya Tigo
Wakili wa Serikali: Report Kutoka Tigo ambayo Umeletewa, Unaweza Kuitambua Kwa Vipi
Shahidi: Kwanza Ina Nembo Kutoka Tigo, Muhuri umeandikwa MIC Tanzania
Wakili wa Serikali: Nyaraka ambayo imegongwa Muhuri Unakumbuka ni zipi
Shahidi: KYC na Miamala ya Fedha
Wakili wa Serikali: Report Kutoka Airtel Utaitambuaje
Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa JAJI tunapata taabh sana, Tangu Asubuhi Hatusikii kabisa labda kwa sababu Shahidi amesogeleana na Wakili.
Jaji: Shahidi Jitahidi Kutoa Sauti
Shahidi: Kutoka Airtel Nilipokea KYC na Mihamala ya Fedha ya Namba Mbili
Wakili wa Serikali: Nyaraka hizi zinaambatana na nini
Shahidi: Barua ya Airtel
Wakili wa Serikali: Taarifa kutoka Airtel Ukiona Utaitambua Kwa lipi
Shahidi: Logo ya Airtel, Sahihi Imesainiwa na Gladdys Fimbari, na zile namba Ambazo nikiwa Nimeomba Kwenye Barua. Lakini pia Kwenye Attachments Kuna Mihuri pamoja na Logo
Wakili wa Serikali: Shahidi Kamata Nyaraka hii, Tizama Mwanzo Mpaka Mwisho
Shahidi….. Anakagua Makaratasi
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Nyaraka Uliyo nayo hivi sasa ni Kitu gani Shahidi: Ni KYC na Miamala ya Fedha, pamoja na Barua ya Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Nyaraka hizo Unazikumbukaje
Shahidi: Kwanza Kuna namba ya Kesi Katika Barua hii
Wakili wa Serikali: Una Uhusiano gani nazo
Shahidi: Niliombea Taarifa Za Namba za Simu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Nyaraka hizo Zina namba zipi
Shahidi: Ni 0784779944, 0782237913, 0787555200
Wakili wa Serikali: Namba hizo Ulizitumia Kuombea Vitu gani
Shahidi: Kuomba KYC pamoja na Miamala Ya Fedha
Wakili wa Serikali: Lwa Mujibu wa Taarifa Ya Airtel, KYC holder ni akina nani
Shahidi: Namba ya 0784779944 ina Usajili wa Jina la Kwanza FREEMAN na Jina la Kati ni AIKAEL na Jina la Mwisho ni MBOWE
Wakili wa Serikali: Shahidi namba ya Pili KYC yake ina taarifa zipi
Shahidi: KYC ilikuwa ya Namba 0782237913 Ambayo ilikuwa na Usajili Jina la Kwanza ni KHALFANI Jina la Kati ni BWIRE na Jina LA Mwisho ni HASSAN
Wakili wa Serikali: KYC inayofuata
Shahidi: Ni ya namba 0797555200 ambayo ilikuwa na Jina LA Kwanza DENIS Jina la Kati LEO na Jina la Mwisho ni URIO
Wakili wa Serikali: Ulisema Taarifa Ya Airtel Ilikuwa ina Miamala, Ieleze Mahakama Miamala Ilikuwa ya Namna gani
Shahidi: Ilikuwa ni Miamala kuanzia 01 June 2020 Mpaka 31 July 2020
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa ile Barua Walitaka Kujua au Kupata kitu gani
Shahidi: Walitaka Kujua Miamala ya Namba za Simu
Wakili wa Serikali: Wewe Ulibaini nini
Shahidi: Nilisaini Kuna Baadhi ya Namba Ambazo zilikuwa zimeainishwa na Mpelelezi Zilikuwa na Miamala, Zimefanya Miamala (Transactions)
Wakili wa Serikali: Kama utakumbuka Elezea Mahakamani ni Nmab zipi au Mihamala ipi Uliyo baini
Shahidi: Kuna Muhamala wa Tarehe 31 July 2020 ambao Ulitoka Kwenye 0784779944 kwenda namba 0782237913
Wakili wa Serikali: Huo ulikuwa Muamala Wa Pesa Kiasi gani
Shahidi: TSh Elfu Themanini Wakili wa Serikali: Ulikuwa Unaenda Kwenye namba ipi
Shahidi: 0782237913
Wakili JOHN MALLYA: Mheshimiwa Jaji Kama Shahidi anasoma namba Kwa Vielelezo ambavyo Vipo Mahakamani Tunaomba asome kwa usahihi..
Wakili wa Serikali: Sema kutoka lnamba ipi kwenda Ipi
Shahidi: Kutoka 784779944 kwenda 782237944
Wakili wa Serikali: Namba hizo Zina Uhusiano gani na zile walizo Omba Wapelelezi
Shahidi: Ni namba Walizoomba Wapelelezi
Wakili wa Serikali: Je, Kuna Mihamaa Mingine?
Shahidi: Upo Tarehe 20 July 2020 Mumala Kutoka Namba ya Simu 780900174 kwenda 787555200
Wakili wa Serikali: Muamala Wa Pesa Kiasi gani
Shahidi: TSh 500,000 WS anaenda Kuteta Jambo na Jopo la Mawakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: Dakika Moja Mheshimiwa Jaji Jaji anaitikia kwa kichwa.
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea hizi Taarifa za Airtel unasema Ulifanya nini
Shahidi: Nili report kwenye Taarifa Yangu
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba p6
Wakili wa Serikali: Shahidi Kwa Ujumla Hizo Nyaraka Ni Kitu gani
Shahidi: Ni Taarifa za KYC kutoka Kampuni ya Tigo
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kimekutambulisha Kuwa hiyo ni Taarifa kutoka Tigo
Shahidi: Barua ina Nembo Kutoka Kampuni ya Tigo, Ina Muhuri, Sahihi ya Mwanasheria
Wakili wa Serikali: Ni zile za miamala pia
Shahidi: Na zenyewe Zina Muhuri Wa MIC Tanzania
Wakili wa Serikali: Nyaraka ya KYC inahusiana na namba zipi
Shahidi: Ina husiana na 0719933386
Wakili wa Serikali: Na kwa Mujibu wa KYC Namba hiyo inamuhusu Usajili wa nani
Shahidi: Unahusu Jina la Kwanza FREEMAN Middle namba AIKAEL na Last name MBOWE
Wakili wa Serikali: Kwenye Miamala Ulifanya Ukabiani ni Namba ipi
Shahidi: Nilbaini Muamala Wa Kiasi cha TSh Laki 5, Tarehe 20 July 2020
Shahidi: Muamala Unatoka namba % 255719933386 WS: Kwenda namba ipi
Shahidi: Namba 255787555200
Wakili wa Serikali: Na Kwamba Sasa Shahidi, Hiyo Nyaraka ya Miamala Ilikuwa ya Kipindi Gani
Shahidi: alikuwa Mihamala ya Fedha Kuanzia 01 June 2020 Mpaka 31 July 2020
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa Kwenye report yako Mbali na Taarifa za Tigo na Airtel Uliambatanisha Kitu gani
Shahidi: Niliambatanisha report Kutoka simu zile Nne Zenye Matokeo
Wakili wa Serikali: Simu hizo ni zipi
Shahidi: Tecno Tatu na Itel
SHAHIDI ana nyoosha mkono wake Juu anasema “SAMAHANI MHESHIMIWA JAJI, KICHWA KINANIGONGA NASHINDWA KUONGEA KWA SAUTI”
Jaji: Wakupe Maji?
Jaji: au uondoe kitambaa usoni (Barakoa)
Shahidi: Hapana sababu ya kiafya ibakie tu
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tuwasiliane Maana Shahidi Ndiyo Kaibua Concern Hapa
Jaji: Mmewasiliana naye?
Wakili wa Serikali: Hapana
Jaji: Wasiliana naye
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ananiambia Kichwa Kinamgonga sana na hayupo Kwenye Position ya Kuendelea na Ushahidi
Jaji: Unaposema Kichwa Kinamgonga Maana yake Kinamuuma, si Ndiyo?
Wakili wa Serikali: Ndiyo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji, inategemea suala la Shahidi mwenyewe, kama tunaweza Ku’ Break kidogo ni sawa, lakini kuhairisha ni Jambo la mwisho kabisaaaaaa
Jaji: Wasiliana naye Kama anaweza kuendelea Kidogo, Tu’ break Kwa muda aje tuendelee
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani Nilipoongea naye kasema Hayupo Kwenye Position ya Kuendelea Ila Sisi Kama Wenye Kesi Shahidi akisema anaumwa tunaona akiendelea anaweza Kutoa Ushahidi Wa Vitu visivyo..
Jaji: Haya Inspector Unasemaje
Shahidi: Mheshimiwa Jaji nimekuja Asubuhi Kichwa kikiwa kinanigonga, ila kadiri Muda Unapoendelea Kinauma zaidi ndiyo Maana Unaona Sauti Ipo Chini..
Jaji: Nafikiri tumpe Benefits of Doubt
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakati Shahidi akiendelea Kutoa Ushahidi Wake Mahakamani, Yeye Mwenyewe Ame raise Concerns Kuhusiana na Afya yake, Tumewasiliana naye Mheshimiwa Jaji na ametueleza Kuwa Kichwa kinamuuma.
Na Kwamba Kwa Jinsi anavyojisikia hayupo Kwenye nafasi ya Kuendelea Kutoa Ushahidi Kwa sasa.. Mheshimiwa Jaji ni Utaratibu kwamba ili Shahidi aendelee Kutoa Ushahidi anapaswa awe Sawa Ki Afya, na Kwakuwa Shahidi ameeleza Kichwa Kinauma na Kwakuwa amesema hayupo Kwenye nafasi ya Kuendelea Kutoa Ushahidi Kwa sasa ni Busara tuhairishe ili Shahidi aweze Kupata Medical attention ili aweze Kupata Matibabu Nachelea Kusema turudi lini sababu sijui atakuwa Sawa KiAfya Sawa lini..
Jaji: Tunaye Askofu Mahakamani baada ya hapa atamfanyia maombi na mimi nitakuombea shahidi Ili kesho shahidi uweze kuwa Mahakamani…
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwakuwa Shahidi amewasiliana na Mahakama Mwenyewe sisi hatuna Shida na hilo lakini Premises za kuhairisha ndiyo sijafahamu..
Mimi nafikiri Tuhairishe mpaka Kesho, MUDA ambao Mahakama Itapanga na Kama atakuwa bado sheria ya ushahidi inaruhusu kufanya
Deferment ya ushahidi wake, tuendelee na shahidi mwingine, alipo atakuja kuendelea Na shahidi mwingine
Jaji: Sijui kwanini nahisi kesho atakwepo (Shahidi) Mahakamani
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tutafanya hivyo Ingawa hatuombei hivyo, Ikitokea imeshindikana tutatafuta shahidi mwingine
Jaji anaandika Kidogo kwenye makbrasha yake..
Jaji: tunahairisha shauri kama ambavyo mashtaka wameomba na Mahakama ika observe. Tunahairisha mpaka kesho Saa 3 Asubuhi Upande wa Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Upande wa Jamhuri kama Itashindikana mtatakiwa mlete shahidi mwingine
Jaji anatoka