Kesi ya Mbowe: Shahidi akana kujua kesi ya ugaidi dhidi ya mshitakiwa

Kama ilivyoripotiwa na ripota raia, BJ.

Mwenendo wa kesi ya Mbowe leo Januari 14, 2022

Jaji ameshaingia Mahakamani muda huu. Ni saa 4:06.

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inayomhusu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anajitambulisha: “Mheshimiwa Jaji, ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na:

  1. Pius Hilla
  2. Abdallah Chavula
  3. Jenitreza Kitali
  4. Esther Martin
  5. Nassoro Katuga
  6. Ignasi Mwinuka
  7. Tulimanywa Majige.

“Wote kwa pamoja tunawaikilisha Jamuhuri.”

Wakili Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji Ikipendeza Mahakama hii Tukufu Majina yangu naitwa Peter Kibatala na nipo pamoja na wakili:

  1. Jeremiah Mtobesya
  2. John Malya
  3. Dickson Matata
  4. Seleman Matauka
  5. Faraji Mangula
  6. Michael Lugina
  7. Gaston Garubindi
  8. Evaresta Kisanga
  9. Hadija Aron

JAJI: Shahidi unakumbuka kuwa wakati unaanza kutoa ushahidi wako uliapa na bado upo chini ya kiapo?

JAJI: Bwana Malya unaweza kuendelea.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naweza kukumbushwa nilipoishia jana?

JAJI: Ulikuwa unamaliza kueleza kielelezo namba 20, pale ambapo P and P inatumika na akajibu kuwa ni pale ambapo mteja kwa mteja na kwa agent.

MALLYA: Ni sahihi shahidi kuwa cash out ni kutoa pesa kwa wakala?

SHAHIDI: Ndiyo. Anapotoa pesa yake kwa wakala kwa namba yake.

MALLYA: Naomba kielelezo namba 15.

MALLYA: Je ni sahihi muamala umeandikwa cash out hapo kwenye kielelezo, kwamba mtu aliyetumiwa 500,000 akaenda 300,000?

SHAHIDI: Ndiyo. Sawasawa.

MALLYA: Inaonyesha kuwa hiyo 300,000 aliifanyia nini?

SHAHIDI: Haionekani.

MALLYA: Kuna uwezekano wa mtu kujiwekea pesa mwenyewe kupitia kwa wakala?

SHAHIDI: Naomba urudie tena.

MALLYA: Kwenye hiyo 500,000 ambayo inaonekana iliwekwa kwa wakala, je kuna uwezekano huyo mtu alijiwekea hiyo 500,000 mwenyewe?

SHAHIDI: Nakataa haijatoka kwa wakala.

MALLYA: Lakini ame- cash out kwa wakala.

SHAHIDI: Ndiyo, ame- cash out kwa wakala.

MALLYA: Inawezekana mtu kuitumia pesa yake kutoka namba yake ya TiGO kuja namba ya Airtel?

SHAHIDI: Ndiyo inawezekana.

MALLYA: Wewe ulitueleza kuwa hiyo namba ya Tigo ni ya nani?

SHAHIDI: Hapana sijaeleza.

MALLYA: Kuna record yoyote uliyoleta hapa Mahakamani inayoonyesha hiyo 80,000 baada ya hapo ilienda wapi?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Kwenye kielelezo namba 20, ulizungumzia muamala wa 199,000/- wa tarehe 22 Julai 2020.

SHAHIDI: Ndiyo nilizungumzia.

MALLYA: Ni Cash in au …?

SHAHIDI: Ndiyo. Imeandikwa cash in.

MALLYA: Line ya Airtel inauzwa shilingi ngapi?

SHAHIDI: Shilingi 500.

MALLYA: Kuna kanuni zinazohusu ku- handle sim card. Je, unazijua?

SHAHIDI: Ndiyo. Nazijua.

MALLYA: Je, kwa mujibu wa hiyo barua iliyoomba taarifa ulichukulia serious?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilichukulia serious.

MALLYA: Hiyo namba unayosema kuwa ni ya Khalfani Bwire imeuzwa kwa Godson Munuo

SHAHIDI: Mimi sifahamu.

MALLYA: Nyie mmeuza namba ya Khalfani Bwire kwa shilingi 500.

SHAHIDI: Sikujua kama wameuza.

MALLYA: Khalfani Bwire alicha pesa mle hatujui kuwa za ugaidi au lah. Je, anapata wapi pesa zake?

SHAHIDI: Pesa zake zinawekwa kwenye collection account.

MALLYA: Kwa hiyo Airtel mna collection account za kutunza pesa za ugaidi?

SHAHIDI: Hapana. Si kweli.

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Objection!! Mheshimiwa Jaji namna Wakili anavyouliza maswali kwa shahidi anaanza yeye kutoa ushahidi. Hakuna sehemu shahidi kasema kuwa kuna collection account ya ugaidi huko Airtel. Sitaki kuingilia Mahakama. Mimi nimesikia kuwa anasema kwenye collection account ya Airtel kuna pesa za ugaidi. Tunaomba wakili aelekezwe namna nzuri.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji, naamini Mahakama imerekodi vizuri.

JAJI: Nilishakuuliza Mahakamani mara kadhaa hapa mahakamani. Je, hayo mengine unayoyasema unayatoa wapi? Kuna wakati unaulizwa kwa wewe kwa kutoa maelezo. Sasa unakwenda mbali zaidi wakati unazungumzia na kuyasema hayo. Hayapo kabisa katika proceedings. Naomba uulize yale yaliyopo mahakamani tafadhali.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji nimesikia, ila nina haki ya kuuliza kuwa mimi nafahamu hivi. Je wewe unafahamu vipi?

JAJI: Kuna maswali ambayo umekuwa unaaimulia wewe. Ndiyo uwe unaulizwa maswali.

MALLYA: Kwa hiyo mnasema kwamba zile pesa za Khalfani Bwire zipo kwenye Collection Account?

SHAHIDI: Nitaomba kuelezea.

MALLYA: Utaelezea baadaye. Hapa jibu swali.

MALLYA: Sasa wewe ulipokea barua kuwa hawa watu wanachunguzwa. Je, hiyo siyo exception ya kuzuia hiyo namba?

SHAHIDI: Sikujua kama wanachunguzwa.

MALLYA: Soma barua ya uchunguzi wa kisayansi walisema nini.

SHAHIDI: Wanaomba taarifa kwa uchunguzi zaidi.

MALLYA: Kwa hiyo nyie mkauza ushahidi wa Khalfani Bwire kwa shilingi 500?

SHAHIDI: Atazikuta zimewekwa.

MALLYA: Je, mteja wangu akitaka kujitetea so itabidi ampokonye huyo Godson Mnuru?

SHAHIDI: Taarifa zake zipo lakini.

MALLYA: Ulitoa ufafanuzi huo?

SHAHIDI: Sikuulizwa.

MALLYA: Jibu swali.

SHAHIDI: Sikuulizwa.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali langu.

JAJI: Umeelewa swali?

SHAHIDI: Sikutoa ufafanuzi.

MALLYA: Kwenye hiyo barua yako soma paragraph ya mwisho.

SHAHIDI: Tupo tayari kuendelea kutoa ushirikiano zaidi.

MALLYA: Sasa kwenye muamala wa 300,000/- ulijisumbua kujua wakala aliwa nani?

SHAHIDI: Sikufuatilia.

MALLYA: Kwa hiyo unasema namba inakuwa dormant kwa siku ngapi kuwa deactivated?

SHAHIDI: Siku 90.

MALLYA: Mshitakiwa namba moja kizimbani Khalfani Bwire alikamatwa tarehe 9 Agosti 2020. Je, wewe uliombwa lini taarifa za hiyo namba?

SHAHIDI: Tarehe 1 Julai 2021.

MALLYA: Ni miezi mingapi ilikuwa imepita?

SHAHIDI: Kama 10 au 11.

MALLYA: Kwa hiyo ni zaidi ya miezi 3 ya kisheria kuwa namba inakuwa deactivated?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Sasa tangu yule bwana amekamatwa mpaka wewe unaombwa taarifa tayari namba ilikuwa deactivated?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Sasa Bwana Godson Mnuru anasema kuwa alinunua hiyo line mwezi Januari 2021. Ni sahihi kwamba KYC ya hii namba ingesoma namba yake siyo Khalfani Bwire.

SHAHIDI: Hakuna record yoyote. Kwa hiyo siwezi kutoa jibu.

MALLYA: Katika hali ya kawaida kwa miezi 10 namba ya Bwire ingekuwa deactivated au isingekuwa deactivated?

SHAHIDI: Ingekuwa deactivated.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji sina Swali lingine.

(Sasa anaingia Wakili Dickson Matata).

Matata: Mheshimiwa Jaji sina swali kwa niaba ya mshitakiwa wa tatu.

Anaingia Wakili Peter Kibatala.

KIBATALA: Shahidi, gazeti la The Citizen la tarehe 12 Januari 2019, Serikali kupitia Waziri Kabudi, serikali Ilifanya mazungumzo na kampuni ya BALT iliongeza hisa kutoka 40% mpaka 49%.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kwa hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania ni maboss zako?

SHAHIDI: Si kweli.

KIBATALA: Je, unafahamu kuwa Serikali ya Jamhuri Wa Muungano wa Tanzania ina- nominate wakurugenzi kuingia katika kusimamia kampuni ya AIRTEL?

SHAHIDI: Ndiyo. Nafahamu.

KIBATALA: Je, hao ni wakurugenzi mabosi wako au siyo mabosi zako?

SHAHIDI: Siyo mabosi zangu.

KIBATALA: Kwa hiyo wewe uliripoti kwa Bodi ya Wakurugenzi iwe direct au siyo direct?

SHAHIDI: Siyo mabosi zangu.

KIBATALA: Kwa hiyo wewe Legal Menager unaripoti wapi?

SHAHIDI: Kwa Managing Director.

KIBATALA: Ambaye yeye anaripoti kwa nani?

SHAHIDI: Kwenye Bodi.

KIBATALA: Kwa hiyo Bodi wakitoa malekezo Managing Director akufukuze kazi with regard ya Labour Law, utafukuzwa au hautafukuzwa?

SHAHIDI: Ushasema Labour Law.

KIBATALA: Nataka kujua wana uwezo wa kuagiza au hawana?

SHAHIDI: Wana uwezo wa kuagiza.

KIBATALA: Kwenu nyinyi Airtel kipi ni paramount?

SHAHIDI: Mteja ni mtu muhimu kwetu na tunaangalia sana taarifa zake lakini pale panapohitajika kisheria ku- comply na sheria tunafuata sheria.

KIBATALA: Kama mteja hataki data zake ziwe released, wakati enforcing organ wanataka data zake, wewe kama mwanasheria unaishauri nini Body of Directors?

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Objection Mheshimiwa Jaji! Law enforcement wanahitaji taarifa, swali limejengewa premises wanataka kumtengenezea kesi. Yeye aseme tu polisi wanataka taarifa.

KIBATALA: Kwa heshima Mheshimiwa Jaji, sitamjibu kwa kuokoa muda.

SHAHIDI: Sitajui, sababu ni opinion.

KIBATALA: Je, unafahamu kuwa Freeman Mbowe ni kiongozi wa Chadema au hufahamu?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Unafahamu kuwa Mbowe amekuwa na kesi mbalimbali na law enforcement organ?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Je, unafahamu mpaka hapa unakuja kutoa ushahidi anashitakiwa kwa kesi gani?

SHAHIDI: Nafahamu.

KIBATALA: Sasa umekuja kutoa ushahidi kuhusu kesi gani inayomkabili mteja wako?

SHAHIDI: Economic Crime.

KIBATALA: Unafahamu ni kesi ya ugaidi?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Kabla ya kuwa The Guardians.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kabla ya hapo ulikuwa kampuni gani ya mawakili?

SHAHIDI: Hallmark.

KIBATALA: Nilisikia unazungumzia kuhusu summons, je, ile summons inasema wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi?

SHAHIDI: Mpaka nitazame tena.

KIBATALA: Jana ulitaja namba 3 kwa kumbukumbu zako?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ila kuhusu summons hukumbuki?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Barua imekufikia tarehe ngapi mwezi gani na mwaka gani?

SHAHIDI: Tarehe 2 Julai 2021.

KIBATALA: Na wewe umejibu tarehe ngapi?

SHAHIDI: Tarehe 2 Julai 2021.

KIBATALA: Ni sahihi kusema ilijibu siku ileile?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Wakati unafanyia kazi ulijua unafanyia kazi namba ya Freeman Aikael Mbowe?

SHAHIDI: Ndiyo. Niliona kwenye KYC kwenye picha.

KIBATALA: Iambie Mahakama na mteja wako Freeman Mbowe, je, ni juhudi gani ulichukua kulinda taarifa za mteja wako?

SHAHIDI: Niliombwa na chombo cha uchunguzi.

KIBATALA: Hilo jibu ni zuri ila si la swali langu. Swali ni kwa namna gani ulijaribu kulinda taarifa za mteja wako kama ulijibu siku hiyo hiyo.

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji nimeelewa swali. ila chombo kilichoniomba kinaruhusiwa kisheria.

KIBATALA: Kwa hiyo unasema kuwa ulijibu ile barua kwa sababu imetoka Polisi?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Kwa hiyo tutaona wapi kama Airtel wali- balance kati ya mteja wao na Polisi?

SHAHIDI: Huwezi kuona.

KIBATALA: Jana mawakili walitaja hapa Sheria ya Makosa ya Mtandao, wewe ukataja Sheria ya Electronic and Post Communication Act. Je, unafahamu regulations ya Proctection of Consumers?

SHAHIDI: Naweza kupata nijikumbushe.

KIBATALA: Ngoja mawakili wako wa Serikali wajiridhishe kwanza.

KIBATALA: Sasa tusomee Rule 6(2)d.

SHAHIDI: Inasema 6(2) The Collection and Maintenance of Information on Individual’s Consumer…

Anaendelea kusoma.

KIBATALA: Je, ni kweli nyiye kama licencee mnatakiwa ku- balance haki zingine za mteja?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ni sahihi hizo haki ni pamoja na privacy?

SHAHIDI: Hapo itabidi tuangalie kwenye interpretation.

KIBATALA: Unafikiri utaweza kuona? Ngoja nikuonyeshe.

SHAHIDI: Ni kweli haijasema.

KIBATALA: Nilijua haijasema. Sasa unasemaje?

SHAHIDI: Ni kweli inajumuisha haki ya privacy.

KIBATALA: Katika Sheria hii kuna sehemu inaonyesha mteja haki zake zitupwe kapuni for the name of compliance?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Je, unafahamu kuwa kuna Judicial Review?

SHAHIDI: Ndiyo. Nafahamu.

KIBATALA: Iambie Mahakama nyiye kama Airtel mnaweza kufungua Judicial Review pale mnapopewa amri.

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Je, kuna sheria inakataza nyiye Airtel ku- challenge order ya kutoa taarifa za mteja wenu?

SHAHIDI: Hakuna sheria hiyo.

KIBATALA: Je, mwambie Mheshimiwa Jaji Airtel ilienda mahakamani ku- challenge haki ya mteja wake.

SHAHIDI: Hapana. Haikwenda.

KIBATALA: Je, uliwaandikia barua Polisi kuwa wawape _details_kutaka kujua nini kinafanyika?

SHAHIDI: Hapana. Hatukuwaandikia.

KIBATALA: Je, hakuna jambo lolote liliwazuia kufanya hivyo kisheria?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Shahidi, nakuonyesha kielelezo P16 cha Requisition Letter. Mwambie Mheshimiwa Jaji ni wapi barua hiyo iliwaharakisha nyie Airtel muwape hizo taarifa.

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Kwa hiyo hakuna kwenye barua mahala ambapo pameonyesha palikuwa na haraka katika kujibu barua.

SHAHIDI: Hakuna.

KIBATALA: Na jana hukusema kabisa kama ulifanya kwa haraka kwa sababu gani.

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji zaidi ya kungalia barua yenyewe kuna hatua gani ulichukua ku- authenticate.

SHAHIDI: Hakuna kingine nilichofanya zaidi ya kuangalia barua.

KIBATALA: Huyo aliyesaini barua unamfahamu?

SHAHIDI: Simfahamu.

KIBATALA: Mpaka leo hujawahi kumwona?

Shahidi Gladys

SHAHIDI: Sijawahi kumwona.

KIBATALA: Kwenye hiyo barua kuna namba za simu?

SHAHIDI: Ndiyo. Kuna namba za simu.

KIBATALA: Ulizitumia hizo namba za simu?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Badala yake baada ya wiki moja ukaenda kutoa maelezo yako kwa Inspector Swila?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Je, ulichukua hatua kuchunguza kama anayekuhoji alitoka Cyber?

SHAHIDI: Sikuchunguza.

KIBATALA: Na wala hukuchunguza mpaka leo kuwa Swila alikuwa anapeleleza makosa ya ugaidi na siyo Cyber?

SHAHIDI: Sikuchunguza.

KIBATALA: Na Swila hakukuambia kuwa anaandika maelezo kuhusu makosa ya ugaidi?

SHAHIDI: Hakuniambia.

KIBATALA: Wewe ulijua anakuhoji maelezo kwa makosa gani?

SHAHIDI: Barua inasema kuwa walikuwa wanaomba taarifa kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za jinai.

KIBATALA: Hizo tuhuma za jinai wakati unajibu ulikuwa unazifahamu au huzifahamu?

SHAHIDI: Nilikuwa sifahamu.

KIBATALA: Hii barua ya P16 inasema kuwa iliandaliwa chini ya kifungu cha 34 cha sheria gani?

SHAHIDI: Ilikuwa inataka taarifa kwa kutumia Sheria ya Makosa ya Mtandao.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji hii barua ilikuwa addressed kwa nani.

SHAHIDI: Ilikuwa addressed kwa mwanasheria.

KIBATALA: Kwa hiyo wigo uliokuwa nao wa kushughulika na hiyo barua ni uanasheria wako?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na hiyo barua haikuelekezwa kwa HR, wala mfagiaji?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Wewe kama mwanasheria wa miaka minane, je, ni wapi katika barua, kielelezo namba 15, ni wapi Mheshimiwa Jaji akiangalia ataona iliandikwa na wewe Gladdys au mwanasheria?

SHAHIDI: Neno Mwanasheria halipo.

KIBATALA: Tukitaka tujue kuwa aimejibiwa na mwanasheria tunaangalia wapi?

SHAHIDI: Hakuna … Lakini Gladdys ni nani?

KIBATALA: Sitaki maswali.

KIBATALA: Ombi limeletwa kisheria, kwa watu wanaotegemewa kutoka Jeshi la Polisi … Na kwa terms of reference, je ni sahihi kwamba na wewe ulitakiwa kujibu kwa kufuata terms of reference?

SHAHIDI: Ni kweli.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa barua iliomba taarifa namba ngapi.

SHAHIDI: Namba tatu.

KIBATALA: Na wewe ukapeleka majibu ya taarifa za namba ngapi?

SHAHIDI: Namba mbili.

KIBATALA: Zinaoana au zipo tofauti?

SHAHIDI: Zipo tofauti.

KIBATALA: Jana ulisema kuwa barua ilipokelewa wapi?

SHAHIDI: Reception.

KIBATALA: Baada ya hapo ikawaje?

SHAHIDI: Waka- minutes kuja kitengo cha sheria.

KIBATALA: Wewe kama mwanasheria wa Airtel, miaka minane unafahamu kitu kinaitwa Chain of Custody?

SHAHIDI: Hapana. Sifahamu.

KIBATALA: Na ni mwanasheria miaka minane?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: OK. Tuendelee. Ni wapi barua hiyo Mheshimiwa Jaji akiangalia ataona kuwa ilipokelewa mapokezi Airtel?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Barua hiyo inaonyesha kuwa ilifika Kitengo cha Sheria?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Katika maelezo yako ulizungumzia kuhusu dispatch au register?

SHAHIDI: Ndiyo. Nilizungumzia.

KIBATALA: Hiyo register kwa Mwanasheria Mkuu wa Airtel ungetaka kuja nayo ungenyimwa?

SHAHIDI: Hapana. Nisingenyimwa.

KIBATALA: Register hiyo uliileta Mahakamani?

SHAHIDI: Hapana. Sikuleta.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba register hiyo ilipotea au ipo mbali?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Ulimwambia Jaji kuwa mpaka wewe unaleta barua hapa Mahakamani ulimwambia Jaji uliitoa wapi hiyo barua?

SHAHIDI: Sikueleza hayo unayoyasema.

KIBATALA: Ulimwambia Jaji kuwa barua kama hizo zilizotoka Polisi zinahifadhiwa wapi pale Airtel?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba barua hiyo uliyotoa inalingana na nakala ya barua iliyopo Jeshi la Polisi?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuwa barua ilifika vipi Polisi?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Wewe unafanya kazi masijala ya Polisi?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba barua uliyotoa jana na uliyopeleka Jeshi la Polisi zinafanana content?

SHAHIDI: Hapana. Sikumwambia.

KIBATALA: Ndiyo maana nilikuuliza hapa unajua maana ya Chain of Custody?

SHAHIDI: Nilijibu sifahamu.

KIBATALA: Twende eneo lingine. Ni kweli taarifa unazoleta zinaonyesha zipo uncorrupted?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Nianze na kielelezo namba 17,19 na 20. Je, ile taarifa ulivyopokea uli- print au ulimtaarifu bosi wako?

SHAHIDI: Nili- print tu.

KIBATALA: Mpaka unatoa taarifa hii Mahakamani Airtel wanafahamu kuwa ulitoa taarifa hii?

SHAHIDI: Ndiyo. Wanafahamu.

KIBATALA: Je, ulimwambia sasa Mheshimiwa Jaji kuwa uliwataarifu mabosi zako kuwa uliingia katika mfumo ukatoa taarifa?

SHAHIDI: Hapana. Sijamwambia.

KIBATALA: Ni kitengo gani pale Airtel kinahusika na statutory liability, consumers liability?

SHAHIDI: Sisi pale vitengo vinashirikiana. Kitengo cha Sheria ndiyo kina mamlaka ya kushughulika na mambo yote ya kisheria.

KIBATALA: Ni lini ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba baada ya kutoa taarifa, ulimtaarifu MD au bosi wako?

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji ananiuliza utaratibu ambao sisi hatuna.

KIBATALA: Je, ni kweli au si kweli kwamba kabrasha la sheria lazima lipelekwe Body of Directors?

SHAHIDI: Ni kweli.

KIBATALA: Twende eneo lingine. Jana nilisikia unasema mojawapo ya mambo uliyoyataja ulitaja System kama AGILE, BUSSINESS INTELLIGENCE na MOBIQUIT. Sasa mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa AGILE ni nini.

SHAHIDI: Ni mfumo wa kungalia taarifa za mteja.

KIBATALA: Na ukiwa chini ya kiapo unasema AGILE unasema ni mfumo, na siyo utaratibu wa kuangalia mauzo, idadi ya wateja ili kuongeza ufanisi wa kampuni?

SHAHIDI: AGILE ni mfumo.

KIBATALA: Unatengenezwa na nani?

SHAHIDI: Sikumbuki.

KIBATALA: Na nani ana hakimiliki ya Trademark ya AGILE?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Jana nani hapo alisimama kusema kwamba alienda training?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Twende kwenye Business Intelligence. Na yenyewe ni software?

SHAHIDI: Ndiyo. Ni software.

KIBATALA: Inatengenezwa na nani?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Ina versions ngapi?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Nani jana alileta habari za Bussiness Intelligence?

SHAHIDI: Ni mimi.

KIBATALA: Wakati jana unatoa ushahidi kuhusu Business Intelligence, ulitolewa ushahidi ku- impress kuwa unafahamu au ulijua kuwa ni authentication.

SHAHIDI: Nilitaja kutoa ushahidi.

KIBATALA: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa kweli Business INtelligence ina Exists inahusiana vipi na vielelezo 17, 18, 19 na 20.

SHAHIDI: Haihusiani.

KIBATALA: Ya tatu inaitwa nini?

SHAHIDI: MOBIQUIT.

KIBATALA: Unafahamu kweli?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Airtel wame- install lini hiyo MOBIQUIT?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Ina versions ngapi?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Ipi version ni safety and latest of MOBIQUIT?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Ni lini ulifahamu kuwa kuna MOBIQUIT na inafanya kazi?

SHAHIDI: Nimeajiriwa Airtel nimekuta inafanya kazi.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba MOBIQUIT ilikuwa upgraded lini?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Ulimwambia weaknesses za MOBIQUIT kama kweli ina Exists.

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Ulimwambia ina tofauti gani na softwares zingine?

SHAHIDI: Hapana. Sikumwambia.

KIBATALA: Hizi data zinakuwa stored kwenye severs?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Unafahamu kuna aina mbalimbali za sever?

SHAHIDI: Hapana. Sifahamu.

KIBATALA: Kama hufahamu hata aina ya sever ya Airtel bado unataka tuamini kuwa hizi data haijachezewa?

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba sever ya Airtel ni ya aina fulani?

SHAHIDI: Hapana. Sikumwambia.

KIBATALA: Je, ulimwambia kuwa hizo severs zinakuwa upgraded lini?

SHAHIDI: Sikusema.

KIBATALA: Twende eneo lingine. Hizi systems zote kuna watu wanazi- maintain pamoja na kuzifanyia auditing?

SHAHIDI: Sahihi.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba kuna internal auditors?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Nyie mna external auditors au hamna?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Nilisikia unazungumzia kuhusu firewalls, kama ukuta for protection.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Zipo aina nyingi sana za firewalls.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na ulitaja ili kuonyesha taarifa zipo salama?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuhusu aina ya firewall wanazotumia Airtel?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Ulitoa sababu yoyote kwa Jaji kuwa huwezi kutaja aina ya firewalls mnazotumia kwa ajili ya industrial secrets?

SHAHIDI: Hapana. Sikumwambia.

KIBATALA: Ni kweli kuna aina mbalimbali za firewalls?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na ni kweli zinatofautiana ubora?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Twende eneo lingine.

KIBATALA: Uliwahi kupokea barua ya Jeshi la Polisi kuwa muifanyie uangalizi miamala ya Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Nyiye kama Airtel mlifahamu kuwa Mbowe anafanyiwa uchunguzi wa Makosa ya Ugaidi?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Baada ya tarehe 2 Julai 2020 aliendelea kuwa uraiani na kuendelea kutumia namba zake. Je, nyie kama Airtel mlishawahi kuwa na wasiwasi na miamala ya Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Nyie si reporting authority?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Moja ya majukumu yenu kama Reporting Authority si mngelitaarifu Jeshi la Polisi kama kuna miamala yenye mashaka?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Katika wakati wote hamkuwahi kupata kengele ya kiusalama kuhusu kiwango cha pesa kama sehemu ya kigezo chenu cha kutilia mashaka namba ya Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Namba yake haikuwahi kupiga kengele ya kutilia mashaka.

KIBATALA: Miamala ya tarehe 20 Julai 2020 inahusisha namba gani na namba gani?

SHAHIDI: Ni 780900174 ambayo ituma kwenda 787555200.

KIBATALA: Kwa hiyo hizo namba zinaanza na 7 na siyo SIFURI?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Namba ambazo zipo katika kielelezo cha Polisi na hizo ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba ndiyo namba hiyo hiyo.

SHAHIDI: Sikutolea ufafanuzi.

KIBATALA: Unakubaliana na mimi kuwa kuna utofauti katika kielelezo P20 hizo namba hazianzi na sifuri lakini katika barua ya maombi zinaanza na sifuri.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Ambapo tunasema hukumfafanulia Mheshimiwa Jaji?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Nilisikia mnasema kuwa kuna Collection Account au Wallet sijui nini.

SHAHIDI: Unaweza kuiita Wallet.

KIBATALA: Ni ya kampuni gani?

SHAHIDI: Ni wallet ya TiGO.

KIBATALA: Wewe ni mtu sahihi kuzungumzia Wallet ya TiGO?

SHAHIDI: Ndiyo. Naweza kuzungumzia.

KIBATALA: Kati yako wewe na mtu wa TiGO nani yupo competent kuzungumzia originating namba ya TiGO?

SHAHIDI: Ni mtu wa TiGO.

KIBATALA: Katika barua yako ya tarehe 2 Julai 2020 hukutoa maelezo yoyote?

SHAHIDI: Ni kweli sikutoa.

KIBATALA: Transaction ya chini yake umesema ni namba ya agent. Je, unamfahamu?

SHAHIDI: Hapana. Simfahamu.

KIBATALA: Airtel mnasajili namba za agents na mna- file lake. Je, ni kweli?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Je, hilo file lipo hapa Mahakamani ili tujue kama ana uhusiano na Mbowe?

SHAHIDI: Hapana. Halipo Mahakamani.

KIBATALA: Katika barua yako ya tarehe 2 Julai 2020 uliwaambia Polisi juu ya huyu wakala?

SHAHIDI: Sikumwambia.

KIBATALA: Nikitumia namba yangu ya Airtel siwezi kumtuma house girl, akifika kwa wakala anitumie namba niweze kutoa fedha hiyo?

SHAHIDI: Haiwezekani.

KIBATALA: Kwa hiyo nikimtuma amtu aende kwa wakala wangu kutoa pesa na nikatoa bila mimi kuwepo pale siwezi kutoa pesa, haya niambie kwa sheria gani inayokataza?

SHAHIDI: Sifahamu.

KIBATALA: Angalia katika taarifa ya namba ya Mbowe, tarehe 20 Julai 2020, mnasema kuwa alituma shilingi 500,000 kwa Denis Urio?

SHAHIDI: Hakuna muamala humu wa hiyo shilingi 500,000.

KIBATALA: Twendew kielelezo namba 20. Nitafutie tarehe 22 Julai 2020. Kuna miamala miwili ambayo namba ya Freeman Mbowe ilituma pesa kwenda kwa Denis Urio au Khalfani Bwire, either shilingi 190,000 au 199,000.

SHAHIDI: Hakuna miamala hiyo.

(Ghafla simu inaita Mahakamani na kusababisha kesi kusimama. Mawakili wa Serikali wanataka mwenye simu awe chini ya ulinzi kwa tuhuma za kurekodi proceedings za mahakama kwa njia ya sauti. Ananyang’anywa simu yake na anatolewa kupelekwa mahabusu. Kibatala anasema hakuna sheria wala kanuni ya kinachofanyika kwa sababu mahakama Ilikamata diary na ilishatoa ruling.)

Kesi sasa inaendelea.

KIBATALA: Primary source ya taarifa za mteja ambazo zinakuwa reflected katika KYC zipo NIDA ndiyo maana mna retrieve kutoka NIDA?

SHAHIDI: Sawasawa.

KIBATALA: Na wewe hufanyi kazi NIDA.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Na wewe hukutoa chochote kutoka NIDA.

SHAHIDI: Ndiyo

KIBATALA: Nilisikia kuwa uliitwa Polisi ukaandike maelezo yako.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Kama uliyaandika kwa nia njema, na yalikuwa ya kweli, kwanini hutaki kuyatoa Mahakamani?

SHAHIDI: Siyo kwamba sitaki kuyatoa.

KIBATALA: Ndiyo sasa nakuuliza kwa nia njema kama kweli uliyaandika chini ya Mungu, kwanini usitoe?

SHAHIDI: Jana kuna uamuzi ulitoka kuwa nisitoe.

JAJI: Mr Kibatala jJana Mtobesya alisema kuwa mlikubaliana kama jopo mna- withdraw.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, kwa heshima na taadhima ni kweli wakili mwingine alifanya Cross Examination. Mimi siruhusiwi kuhoji hilo jambo?

JAJI: Yeye alisema kuwa mlikubaliana “sisi ni jopo” na kwa bahati mbaya hayupo.

KIBATALA: Kama ikiwezekana naomba utusomee ulichorekodi.

JAJI: Hapana. Sisomi. Kwani wewe jana hukusikia?

KIBATALA: Basi Mheshimiwa Jaji sitaki kubishana na Mahakama, na nitaomba kuishia hapo.

Kibatala anakwenda kukaa

(Wakili wa Serikali Jenitreza Kitali anasimama na kufanya re examination)

WAKILI WA SERIKALI: Jana uliulizwa kuhusu taarifa ya KYC, taarifa za msajili hazionekani katika hiyo taarifa. Ni kwanini labda?

SHAHIDI: Ni kweli haionekani lakini hizo taarifa zipo na zikihitajika zinaweza kuletwa Mahakamani.

MALLYA: Objection! Taarifa kuwa zipo katika mfumo wa usajili zikihitajika zinaweza kuletwa Mahakamani si sawa na ni taarifa mpya.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa maoni yetu ni explanation na kwa upande wetu sisi hatuwezi kuzuia shahidi kueleza jambo.

JAJI: Basi eleza katika namna ambayo hataleta jambo jipya.

WAKILI WA SERIKALI: Jana shahidi uliulizwa kwamba katika taarifa yako msajili haionekani. Kwa nini ipo hivyo?

SHAHIDI: Mfumo ndivyo ulivyo lakini endapo zitahitajika zitaletwa.

WAKILI WA SERIKALI: Umeulizwa kuhusu namba ya Simu ikiwa dormant, haitumiki na kwamba Airtel wamemuuzia mtu mwingine anaitwa Godson Mnuru, ukasema huwezi kueleza mpaka uone nyaraka.

SHAHIDI: Ni kweli nilitaka nithibitishe jina, kwa sababu nisingeweza kujibu kabla sijathibitisha.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusu wakala kuwa hukutoa details za wakala aliyefanya huo muamala wa shilingi 300 000. Kwanini ilijitokeza?

SHAHIDI: Sikuwa nimeombwa taarifa hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusiana jukumu lako kutoa taarifa kuhusiana na kutoa taarifa, lakini pia kuna kifungu cha wewe kukataa kutoa taarifa, ukamtaka mtoa taarifa aende Mahakamani, Ukasema ni kweli vifungu unavijua ila hukutaka kufanya hilo.

SHAHIDI: Kuna vitu vingi tunaangalia katika kutoa taarifa. Kuna sheria zinaniruhusu kufanya hivyo na Sheria siyo moja, kwa hiyo sheria inaniruhusu kufanya hivyo pale ninapotakiwa kutoa taarifa.

WAKILI WA SERIKALI: Pia jana kuna taarifa kwenye kielelezo namba 17 kuhusu neno “kanda”. Kimoja kina neno hilo kanda, kimoja hakina. Ieleze Mahakama kwanini ilijitokeza hivyo.

SHAHIDI: Kama nilivyosema hiki kimetolewa katika mfumo wakati mteja taarifa zake zinatolewa katika mfumo wa NIDA hivyo Taarifa nilizowasilisha ndiyo zilivyoletwa.

WAKILI WA SERIKALI: (Jenitreza Kitali) Mheshimiwa Jaji, ya kwangu yameisha. Naomba nimkaribishe mwenzangu kwa maswali.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Gladdys jana umeulizwa maswali kuhusiana na kielelezo namba 20, ambayo ilikuwa na taarifa ya miamala ya namba 0787 555200 na ukasema taarifa za muamala mwingine ya 19 namba za Airtel, ukaulizwa umechukua hatua gani kulinda taarifa za wateja wengine 19 ambazo hazikuwa zimeombewa lakini zinasomekana. Je, ulimaanisha nini?

SHAHIDI: Kwanza taarifa za wateja ziliombwa kupitia utaratibu wa kisheria, katika taarifa hizi tunaona mtumiaji anafanya miamala na namba zingine. Hatuna uwezo wa kufanya changes zozote kwenye taarifa hizo.

MALLYA: Hizo ni facts mpya.

JAJI: alisema jana kuwa wana- extract na ku- print, haiwezi kuzichanganua.

MALLYA: Sawa Mheshimiwa Jaji.

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji nina maswali na majibu ya Mtobesya ya jana.

JAJI: Umesoma wapi?

Wakili Nashon Nkungu: Wenzangu walikuwa wamerekodi.

JAJI: Umetoa wapi? Naona una- refer kwenye simu, wala huna karatasi.

Nashon: Basi Mheshimiwa Jaji naomba nikae.

JAJI: Inavyoonekana kuna source nyingine, maana proceedings bado sija- certify sasa huyo ana- refer kwenye simu.

JAJI: Inaonekana kuna source nyingine kwenye simu zaidi yangu.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji. technology imekuwa kubwa pia. Maana hata sisi mawakili tuna Group la WhatsApp na tunashea taarifa na nyaraka humo.

JAJI: Ndiyo nimeona yeye kashika simu na ninachojua Mtobesya atakuwa kaondoka na simu yake. Sasa yeye anatoa wapi au ana source nyingine?

KIBATALA: Jaji naona tusifungue mambo mengine. Itoshe kusema hakuna wakili atavunja kanuni za Mahakama wala kwenda nje ya taaluma yake. Mengine ni mambo ya kibanadamu.

JAJI: Tuendelee.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuwa wakati unaomba taarifa hizi, za usajili na miamala kama ulijua zilikuwa taarifa za Freeman Mbowe ukasema hufahamu. Ukasema ulijua baada kuingia kwenye mifumo. Ni kwanini ulisema hivyo?

SHAHIDI: Baada ya kupata taarifa, ndiyo nilifahamu lakini niliwasilisha kama nilivyoombwa kwenye barua.

WAKILI WA SERIKALI: Ulirejewa hapa kuhusu sheria ya Electronics na Regulation kuhusu Protection of Consumers Rights, ukasema kwamba hazisema kwamba haki za mteja zinatupwa kapuni.

SHAHIDI: Ukiangalia kifungu hicho kinatoa exception pale unapoombwa taarifa, paramount ni mteja lakini ukienda mbele sheria inatoa exception kwenye hilo suala.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kwamba mara baada ya kupokea barua kutoka Kamisheni ya uchunguzi, kwamba waliomba taarifa hizo kupitia Cyber Act, ukasema kweli waliomba ila ukasema hukuona maelezo zaidi. Labda kwa nini?

SHAHIDI: Hapakuwa na uwezekano wa kuomba taarifa za ziada, Vile ambavyo tumeomba ni Kwa utaratibu wa sheria na tulifuata sheria.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuwa tarehe 2 Julai 2021 uliombwa taarifa, ukajibu tarehe 2 July.

KIBATALA: Mheshimiwa, marekebisho barua ilipokelewa tarehe 1 Julai na ikajibiwa tarehe 2 Julai.

WAKILI WA SERIKALI: Sawa. Labda kwanini ulijibu siku hiyo hiyo?

SHAHIDI: Ni kazi niliyokuwa assigned siku hiyo hiyo. Ni sababu palikuwa na volume kubwa ya kazi,

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji tunaomba neno volume lisiingie.

WAKILI WA SERIKALI: Hatuoni sababu, Ni sawa na kuzuia shahidi kutoa ushahidi.

JAJI: Hoja yake neno ‘Volume’ ya kazi hakulisema mwanzo na lisiingie.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusu ku- authenticate barua hiyo. Wewe ukasema barua hiyo ilikuwa imejitosheleza. Ni kwanini ulisema hivyo?

SHAHIDI: Sikuwa na haja ya kuona vitu vingine sababu niliona vingine vimetimia katika Ile barua.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusu barua iliyotoka Polisi ambayo ni kielelezo namba 16 kuwa palikuwa na namba za simu pale na Fax, lakini hukuhakiki kama kweli Ile barua Ilikuwa inahitaji mambo hayo.

SHAHIDI: Sikutaka kufanya hivyo kwa sababu barua ilikuwa inajitosheleza kutoka katika Ofisi ya Uchunguzi.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali, wakati unaandika ile barua kama ulikuwa unajua kama tuhuma ambazo ulikuwa unachunguza zilikuwa zinahusiana na ugaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa swali kuhusu kuleta barua kutoka Legal Council ya Airtel kama kweli ulipewa idhini ya kujibu ile barua.

SHAHIDI: Sikuwa nimeombwa ushahidi huo.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusu barua yako ya majibu hakuna neno ‘mwanasheria’ wala majina yako. Ni Kwanini ipo hivyo?

SHAHIDI: Sikuwa nimeandika kwa sababu niliandika kwa niaba ya Airtel, na kuongeza sababu kitengo kinanitambua.

KIBATALA: Hayo ya kwamba kitengo kinamtambua yasiingie.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kama ile barua ya Airtel kwemda Polisi uliwasilisha wewe. Ukasema kweli, na ukasema hukulinganisha hizo barua ndiyo ile uliyoleta hapa Mahakamani,

SHAHIDI: Nilieleza ni barua ambayo niliandika.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kama baada ya kutoa taarifa ulirudi kuwataarifu ofisini Ukasema hukurudi. Kwanini?

SHAHIDI: Ni utaratibu wa ofisi. Unarudi pale tu unapokwama.

KIBATALA: Objection Mheshimiwa Jaji. Suala la utaratibu ni fact mpya.

WAKILI WA SERIKALI: Labda ni kwanini hukurudisha taarifa ofisini?

SHAHIDI: Sikuhifajika kufanya hivyo.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa hapa swali kama ulisema kuhusu tofauti ya software ya kuhifadhi kumbukumbu za miamala, ukasema hukusema.

SHAHIDI: Mifumo ya uhifadhi wa taarifa za kumbukumbu za miamala ni mmoja, kwa hiyo nisingeweza kutoa utofauti wakati ni moja.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kwanini baada ya kujibu maombi na baada ya kujua taarifa hii ya Freeman Mbowe, ukaulizwa kwanini hamkufanya surveillance, ukasema hamkufanya surveillance baada ya pale.

SHAHIDI: Barua haikututaka tufanye hivyo.
[13:42, 1/14/2022] William Shao: WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa maswali kuhusiana na suala la kama unaweza kuzungumzia collection account ukasema huwezi kuzungumzia originating namba iliyotuma pesa katika collection account, je, ni kwanini ulisema hivyo?

SHAHIDI: Kwa sababu ni namba ambayo originated na TiGO ambayo inatengenezwa kama reference ya Airtel.

WAKILI WA SERIKALI: Ulisema hapa kwamba katika kielelezo namba 20, tarehe 20 kama namba ya Freeman Mbowe ilituma muamala kwenda kwa Denis Urio ukasema hapana. Tufafanulie kwanini kielelezo hicho hakionyeshi.

SHAHIDI: Kielelezo hiki kina namba ya mteja 787555200 ambapo ukirudi kwenye KYC ni namba ya Denis Urio. Kuna muamwala wa kupokea shilingi 500,000 ambapo Denis alipokea kutoka kwenye TiGO Wallet na siyo kwa Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusiana na taarifa ambazo ni primary source kwenye KYC ambapo ukasema ni NIDA. Kwanini unasema primary source ni NIDA?

SHAHIDI: Airtel tuna mfumo wa kusajili kutoka NIDA ambao unatambulika kisheria.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapo. Naomba kurejesha vielelezo.

JAJI: Shahidi asante kwa ushahidi wako.

(Saa 7:51 mchana)

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, huyu ndiye shahidi tuliyekuwa naye kwa leo. Tunaomba ahirisho mpaka Jumatatu tarehe 17 Januari 2022. Shahidi tuliyemtegemea baada ya shahidi huyu alipata udhuru wa kuuguliwa na sababu ni askari mstaafu na alisharejea kwao, hakuwezi kufika. Tunaomba ahirisho mpaka Jumatatu. Mheshimiwa Jaji tunaomba jambo jingine ambalo lilijotokeza. Tunaomba suala la kisheria liweze kutatuliwa.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, kuna mmoja wa watu waliokuwa ni wasikikizaji wa kesi alionyesha kitendo cha kutotii mwenendo wa kesi hii.

JAJI: Tukubaliane tunaendaje. Kwanza tunayemjadili hayupo humu.

Fue

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, utaratibu upo kwa mtu simu inapoita hata mapolisi humu simu zao zimekuwa zinaita. Suala la kwamba kuna mtu alikuwa anarekodi proceedings twende chamber Mr Kidando apewe simu akague atuonyeshe hizo records kisha ndiyo tujadili.

JAJI: Basi tunaahirisha hili jambo kwa muda. Mawakili tukutane chamber, lakini pia mhusika naomba aitwe. Na kwa sababu ya mazingira ya chamber tupate wawakilishi wangapi?

KIBATALA: Mheshimiwa wawili wawili wanatosha.

Jaji anatoka

(Saa 9:02 alasiri)

Mahakama imerejea. Mawakili wa Serikali wanaanza kujitambulisha na pia wa upande wa utetezi wanajitambulisha.

JAJI: Niliahirisha kwa muda kwa ajili ya kile tulichowaeleza awali. Na tumeongozwa na busara tukaamua kama tulivyoamua. Na Bwana Fue (aliyebeba begi katika picha na mawakili hapo juu) tumem-subject kwenye maamuzi yetu yale ya awali. Hataruhusiwa kuingia. Na tunaahirisha shauri hili mpaka Jumatatu tarehe 17 Januari 2022.

Like