Kesi ya Mbowe: Shahidi wa 13 apingana na shahidi wa 12

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe Februari 2022.

Jaji Tiganga ameshaingia mahakamani tayari kusikiliza kesi.

Saa 4:01 asubuhi kesi namba 16 ya Mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, ikikupendeza mimi naitwa Robert Kidando na nipo na wakili

 1. Pius Hilla
 2. Abdallah Chavula
 3. Jenitreza Kitali
 4. Nassoro Katuga
 5. Esther Martin
 6. Tulimanywa Majige
 7. Ignasi Mwinuka

Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala na nipo pamoja na wakili

 1. Nashon Nkungu
 2. John Mallya
 3. Dickson Matata
 4. Seleman Matauka
 5. Fredrick Kihwelo

(Jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika kuwa wapo).

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo tuna shahidi mmoja ambaye alishaanza kutoa ushahidi wake. Tupo tayari kuendelea.

KIBATALA: Na sisi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari kuendelea.

JAJI: Shahidi nakukumbusha kuwa Ijumaa ulikula kiapo, na leo utaendelea kuwa chini ya kiapo.

SHAHIDI: Sawa Mheshimiwa.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Sasa Inspekta Swila, siku ile tulikomea tarehe 27 Oktoba 2020 wakati unampatia DC Goodluck bastola.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hapo ulifanya shughuli gani nyingine?

SHAHIDI: Niliweza kupokea taarifa ya uchunguzi na silaha … tarehe 27 Novemba 2020. Nilipokea kutoka kwa Koplo Azizi wa kitengo cha silaha na milipuko. Nilipokea silaha, bastola aina ya Luger A5340, risasi moja, maganda mawili ya risasi pamoja na vichwa viwili vya risasi.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unapokea taarifa ya risasi moja pamoja na maganda mawili, ni wapi ulipokea?

SHAHIDI: Katika kitengo cha uchunguzi wa silaha na milipuko.

WAKILI WA SERIKALI: Uliwezaje kujua kama ndiyo silaha uliyopeleka?

SHAHIDI: Niliweza kuangalia serial number ya silaha, nikakuta ni A5340 na silaha aina ya Luger.

WAKILI WA SERIKALI: Vipi kuhusiana na risasi zenyenwe zilikuwa na hali gani?

SHAHIDI: Risasi niliyopokea ilikuwa ni moja, ilikuwa haijatumika. Ilikuwa na alama ‘A3’ na risasi ambazo zimetumika nilikuta zimepewa alama ya ‘T1’ na ‘T2’.

WAKILI WA SERIKALI: Nani aliweka alama katika vielelezo hivyo?

SHAHIDI: Mchunguzi wa vielelezo hivyo.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuwa umepokea ripoti na vielelezo ulifanya nini?

SHAHIDI: Vielelezo nilipeleka kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na kwenda kuvikabidhi.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani hicho ulienda kukabidhi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam?

SHAHIDI: Nilienda kukabidhi silaha bastola aina ya Luger A5340 na risasi moja, maganda mawili pamoja na vichwa vyake.

WAKILI WA SERIKALI: Na ripoti ulifanyia nini?

SHAHIDI: Ripoti niliihifadhi na kufungia katika kabati langu la chuma.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya tarehe 27 Novemba 2020, nataka kukurudisha kwanza hapo ambapo unasema ulikabidhi risasi moja, maganda mawili na silaha. Je, ulimkabidhi nani?

SHAHIDI: Nilimkabidhi Sajenti Nuru, ambaye yupo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Ni mtunza vielelezo katika ghala la kutunzia silaha.

WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya kwenda katika Shughuli nyingine za upelelezi, ni wakati gani tena uliweza kushughulika na vielelezo hivyo?

SHAHIDI: Nilishughulika tena wakati wa kutoa Mahakamani kwa ajili ya ushahidi, ambapo nilimkabidhi Koplo Hafidh Kwa ajili ya kuja kutoa ushahidi Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Turudi tena katika upelelezi baada ya tarehe 27 Novemba 2020. Kitu gani kiliendelea wakati wa kesi hiyo?

SHAHIDI: Niliweza kupokea taarifa kutoka kwa Mrajisi wa silaha siku ya tarehe 18 Machi 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Hiyo taarifa Ilikuwa inahusu nini?

SHAHIDI: Ilikuwa inahusu mmiliki wa silaha yenye serial number A5340 aina ya Luger.

WAKILI WA SERIKALI: Na ripoti hiyo ilisemaje?

SHAHIDI: Ripoti hiyo ilionyesha kuwa silaha hiyo haina usajili wowote katika ofisi ya Mrajisi wa Silaha hapa nchini.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kingine kiliendelea baada ya hiyo tarehe 18 Machi 2021?

SHAHIDI: Tarehe 30 Machi 2021 niliweza kupokea taarifa ya maabara ya sayansi kutoka kitengo cha uchunguzi wa maandishi, kutoka kwa Koplo Khamis wa kitengo cha uchunguzi wa maandishi.

SHAHIDI: Niliweza kusoma ripoti hiyo ambapo ilionyesha kuwa sampuli za maandishi yaliyochukuliwa kutoka kwa mtuhumiwa Khalfani Bwire Hassan ni sawa sawa na maandishi yaliyokuwepo katika daftari nililoambatanisha katika uchunguzi ule.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuwa umesoma, ukafanya nini?

SHAHIDI: Niliweza kuhifadhi katika jalada langu la kesi na kufungia katika kabati langu la chuma.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya tarehe hiyo kitu gani kingine ulifanya kuhusu kesi hiyo?

SHAHIDI: Mnamo tarehe 10 Julai 2021 niliweza kupokea taarifa ya simu zile nane kutoka kwenye maabara ya kisayansi kitengo cha uchunguzi wa makosa ya mtandao.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipokea kutoka kwa nani?

SHAHIDI: Nilipokea kutoka kwa Inspekta Ndowo wa kitengo cha uchunguzi wa makosa ya kimtandao wa maabara ya kisayansi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya uchunguzi wa taarifa hiyo nini kilitokea?

SHAHIDI: Alijulishwa DC Goodluck ambaye haikuwepo Dar es Salaam. Alinijulisha kuwa uchunguzi umekamilika. Ndipo nilipoenda kuchukua taarifa hiyo.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikabidhiwa kwa utaratibu upi?

SHAHIDI: Kwa kusaini katika kitabu cha kitengo cha uchunguzi wa makosa ya mtandao.

WAKILI WA SERIKALI: Mwanzoni ulisema kwamba ulipeleka simu, sasa unakabidhiwa ripoti. Vipi kuhusu zile simu?

SHAHIDI: Pia Nilikabidhiwa simu nane ambazo niliziandikia barua.

WAKILI WA SERIKALI: Ulijuaje kama ndiyo simu ulizopeleka?

SHAHIDI: Niliweza kuzikagua wakati nakabidhiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Ulifanyia nini hiyo ripoti baada ya kukabidhiwa?

SHAHIDI: Simu nane nilipeleka katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Nilimkabidhi Koplo Charles ambaye ni mtunza vielelezo katika chumba cha kuhifadhia vielelezo katika kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Na ile ripoti ulifanyia nini?

SHAHIDI: Ripoti ya uchunguzi niliweza kusoma na kuhifadhi katika jalada la kesi, kisha kuweka katika kabati langu la chuma.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa ripoti hiyo kwa sababu wewe ndiye uliyeomba uchunguzi, ni vitu gani uliweza kupata kutoka katika hiyo ripoti?

SHAHIDI: Katika ripoti hiyo niliweza kugundua vitu vifuatavyo: Niliweza kugundua kuwa palikuwa na mawasiliano kati ya shahidi Luteni Dennis Urio na mtuhumiwa Freeman Mbowe ambayo yalifanyika katika mtandao wa Telegram. Pia kupitia maelezo ya shahidi Luteni Dennis Urio, aliweza kusema kuwa alitumiwa pesa kutoka kwa mtuhumiwa Freeman Mbowe ambapo tarehe 20 Julai 2020 namba 0719-933 386 ambayo ni ya mtuhumiwa Freeman Mbowe ilituma kiasi cha 500,000/- kwenda kwa namba ya shahidi Luteni Dennis Leo Urio ambayo ni 0787-555 200. Pia tarehe 22 mwezi huo huo wa Julai 2020 ilionyesha kuwa shahidi Luteni Dennis Urio kupitia namba yake ya 0787-555 200 ilipokea kiasi cha 199,000/- kutoka kwenye namba ya wakala kama alivyoeleza Luteni Dennis Urio.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hapo nini kiliendelea?

SHAHIDI: Tuliendelea kuandika taarifa mbalimbali na kupitia ripoti hiyo niliweza kujiridhisha kuwa ni kweli mtuhumiwa Freeman Mbowe aliweza kutuma hizo fedha kwa Luteni Dennis Urio.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea baada ya hapo?

SHAHIDI: Siku ya tarehe 27 Julai 2021 watuhumiwa Justin Kaaya, Khalid na Gabriel Muhina walifutiwa shitaka lao baada ya kugundulika hawahusiki na chochote.

WAKILI WA SERIKALI: Turudi baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa kisayansi kuhusu simu. Baada ya hapo ulifanya nini?

SHAHIDI: Mnamo tarehe 18 Julai 2021 niliandika taarifa kwenda kwa Afande Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini kuwa kuna ushahidi wa uhusika wa mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe, na kuwezesha kumkamata.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa (Halafu anakaa kimyaaaa).

WAKILI WA SERIKALI: Mwanzoni wakati unatoa ushahidi wako ulizungumzia kuhusu kufungua majalada mawili. Je, ni jalada lipi ambalo wewe uliandikia taarifa?

SHAHIDI: Ni lile jalada la kesi tulilofungulia polisi, ambalo ni CD/IR/2097/2020 lenye njama za kutaka kufanya vitendo vya kigaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati wa kufungua jalada la kesi hili CD/IR/2097/2020 uKwamba usiandike jina la Freeman Mbowe kwa sababu kama ungeandika jina taarifa zingeweza kuvunja, na akasitisha mpango wake. Je, ulikuwa unamaanisha nini?

SHAHIDI: Nilikuwa namaanisha kuwa angeweza kusitisha kumtumia mtoa taarifa. Angeweza kutumia watu wengine ambapo Jeshi la Polisi lisingejua mahali wala muda, kitu ambacho kingesababisha Jeshi la Polisi kushindwa kuzuia uhalifu.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuandika taarifa kwenda kwa DCI, nini kiliendelea?

SHAHIDI: Nilipokea taarifa kutoka kwa afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi wa Polisi akinitaka nitunze jalada hilo na kwamba yeye anafanya jitihada za kumkamata mshitakiwa Freeman Aikael Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya DCI kukuambia hatua ambazo angechukua nini kilitokea sasa?

SHAHIDI: Tarehe 22 Julai 2021 nilipokea karatasi ya mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe kutoka kwa afande Jumanne Malangahe Mrakibu wa Polisi. Kimsingi nilipokea maelezo hayo ikionyesha mtuhumiwa amekataa kutoa maelezo yake Polisi.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa kipindi hicho ulifahamu huyo mtuhumiwa Freeman Mbowe amepatikanaje?

SHAHIDI: Nilifahamu kwamba amekamatwa Mwanza na kusafirishwa kuja Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Umekuwa ukizungumza majina ya watu kadhaa hapa Mahakamani akiwepo Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe. Hebu ieleze Mahakama kama watu hao wapo hapa Mahakamani.

SHAHIDI: Ndiyo. Watu hawa wapo hapa Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Hebu onyesha sasa.

SHAHIDI: Mtuhumiwa wa kwanza kutoka upande wa kulia ni Khalfani Bwire Hassan. Wa pili kutoka kulia kwangu ni Adam Hassan Kasekwa. Wa tatu kutoka kulia kwangu ni Mohammed Abdillah Ling’wenya na wa nne kutoka kulia Kwangu ni Freeman Aikael Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa mwanzoni wakati unatoa ushahidi wako ulizungumzia kuhusu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya walifikishwa Mahakamani tarehe 19 Agosti 2020. Mtuhumiwa Freeman Mbowe alifikishwa Mahakamani tarehe ipi?

SHAHIDI: Mtuhumiwa Freeman Mbowe alifikishwa Mahakamani tarehe 26 Julai 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Ni tofauti gani ipo kutokana na kufikishwa tarehe tofauti na wale watatu?

SHAHIDI: Utofauti unakuja kutokana na kusubiri kwa taarifa ya uchunguzi wa makosa ya mtandao, ambao kimsingi nilipokea tarehe 10 Julai 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa na upelelezi wa kesi inayowakabili, ni ushahidi gani ulipata kwamba walikula njama za kutenda matendo ya ugaidi?

SHAHIDI: Ni kupitia maelezo yao ya onyo ya mshitakiwa wa Pili Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya pamoja na mshitakiwa wa kwanza Khalfani Bwire Hassan.

SHAHIDI: Pia ushahidi mwingine ambao unaonyesha walikula njama ni kupitia maelezo ya shahidi Luteni Dennis Urio, maelezo ya askari waliowakamata, askari walioandika maelezo ya watuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Kuhusiana na pesa iliyotumwa uliweza kubaini nini?

SHAHIDI: Niliweza kubaini kuwa fedha hiyo ilitumwa kutoka kwa Freeman Mbowe kwenda kwa Luten Dennis Urio, ambapo fedha hiyo iliweza kuwawezesha watuhumiwa mshitakiwa wa pili na wa tatu pamoja na mwingine ambaye hajakamatwa kuweza kufika eneo la uhalifu ambalo lilikuwa eneo la Moshi. Niliweza kubaini kuwa fedha hiyo iliyotumwa iliwezesha watuhumiwa kufika eneo la utejelezaji wa uhalifu.

WAKILI WA SERIKALI: Unaposema kwamba mshitakiwa wa pili, wa tatu na mwingine hajakamatwa, vipi mtuhumiwa wa kwanza kuhusiana na fedha hii?

SHAHIDI: Kuhusu mshitakiwa wa kwanza inaonyesha pia aliweza kupokea pesa kutoka kwa Luteni Dennis Urio kwa ajili ya utekelezaji wa vitendo vya kigaidi.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji naomba kukomea hapo kwenye examination in chief.

(Anasimama Wakili Nashon).

NASHON: Shahidi habari za leo?

SHAHIDI: Njema.

NASHON: Shahidi umepona?

SHAHIDI: Bado.

NASHON: Umemeza dawa zako?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Nadhani shahidi unatambua ukubwa wa hii kesi.

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Kwamba ugaidi ni jambo serious kwa nchi na dunia.

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Kutokana na U- seriousness wa mashitaka, hata uchunguzi wako ulitakiwa uwe serious ku- match na makosa haya.

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Kupitia ushahidi wako uliotoa, unaweza kusimama kifua mbele kwamba ulitendea haki uchunguzi wa kesi hii?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Makosa ni vitu vinavyotengenezwa na sheria.

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Kwa hiyo kuna sheria ambazo zilikuwa zinawaongoza.

SHAHIDI: Ni sahihi.

SHAHIDI: Tutajie sheria zipi mlikuwa mnazitumia kuwa- guide.

SHAHIDI: Sheria mbalimbali.

NASHON: Nitajie sheria mbili mlizokuwa mnatumia.

SHAHIDI: Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

NASHON: Ni nani aliyeangalia sheria akatoa conclusion kwamba alisema kwa story hii, haya ni Makosa ya Ugaidi?

SHAHIDI: Ni Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi wa Polisi.

NASHON: Wewe huku- take part katika kujua haya ni makosa ya ugaidi?

SHAHIDI: Hata mimi mwenyewe pia nilikuwa najua haya ni makosa ni ya ugaidi.

NASHON: Una taaluma ya kung’amua kuwa haya ni makosa ya ugaidi?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Ulisomea wapi?

SHAHIDI: International Law EnforcementAcademy Botswana.

NASHON: Kozi gani?

SHAHIDI: First Breast Scene.

NASHON: Kwa hiyo walimu wako wakakuambia kwamba kozi hiyo inahusika na ugaidi?

SHAHIDI: Inahusika na milipuko.

NASHON: Shahidi ulisema kwamba mmoja ya watuhumiwa katika kesi hii ni Justin Kaaya?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Uliwahi kumwandikia Kaaya maelezo ya onyo?

SHAHIDI: Hapana.

NASHON: Je, unafahamu kwamba Kaaya alitumiwa pesa na Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Ni kweli.

NASHON: Uliwahi kumwandika Kaaya maelezo ya ushahidi?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Alikuambia kwamba aliwahi kutumiwa pesa na Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ni sahihi kwamba alitumiwa pesa kama watuhumiwa wengine hapa mbele (mahakamani)?

SHAHIDI: Hapana.

NASHON: Justine Kaaya na Khalfani Bwire wote walitumiwa pesa na Freeman Mbowe.

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Kwa hiyo wote hawa wametumiwa pesa na Freeman Mbowe?

SHAHIDI: Sahihi, lakini malengo ni tofauti.

NASHON: Malengo ya pesa ya Khalfani Bwire unayatoa wapi?

SHAHIDI: Katika maelezo ya mtuhumiwa.

NASHON: Maelezo ambayo washitakiwa wanakataa kwamba hawakuyatoa kwa hiari yao, bali kwa mateso ndiyo ushahidi wako wa pekee?

SHAHIDI: Na maelezo ya washitakiwa wengine.

NASHON: Je, unafahamu kwamba Kaaya alisema alikuwa anapewa pesa na Freeman Mbowe kwa ajili ya kutoa taarifa za Sabaya?

SHAHIDI: Lakini alikuwa hafahamu malengo.

NASHON: Je, tangu ugundue hakuwa na nia mbaya ilikuwa ni muda gani baada ya kumkamata?

SHAHIDI: Zaidi ya miezi kumi.

NASHON: Ulimkamata lini?

SHAHIDI: September 2020.

NASHON: Ukaja kumwachia lini?

SHAHIDI: Julai 2021.

NASHON: Baada ya mwaka mmoja ndiyo ukajua hakuwa na malengo mabaya?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Ni sahihi kwamba taarifa za Sabaya Freeman Mbowe alizitoa kwa Kaaya?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Na kwamba alilipwa kwa kazi hiyo?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Na wewe hukuona kosa?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Na kwamba alikuwa anakaa kikao na Mbowe kutoa taarifa hiyo?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Kwa kushiriki kikao hicho Kaaya alikuwa anashiriki kikao cha kigaidi?

SHAHIDI: Alikuwa hajui dhumuni la kikao, kwa hiyo hajashiriki kikao cha kigaidi.

NASHON: Lakini katika kikao hicho hicho Mbowe alishiriki kikao cha ugaidi?

SHAHIDI: Ndiyo.

(Wasikilizaji wanaangua kicheko mahakamani).

NASHON: Je, ni wakati gani ulipokea bastola?

SHAHIDI: Baada ya kutoka maabara.

NASHON: Wewe ulii- lebel?

SHAHIDI: Sikui- lebel.

NASHON: Lakini simu za mshitakiwa wa kwanza ndiyo ulizi- lebel.

SHAHIDI: Hapana. Siku- lebel.

NASHON: Wewe uli- lebel simu za nani?

SHAHIDI: Luteni Dennis Urio.

NASHON: Na uli- lebel lini?

SHAHIDI: Tarehe 11 na 13 Agosti 2020.

NASHON: Je, ni sahihi kwamba ulichukua bastola ya A5340 pamoja na risasi kutoka kwa Koplo Hafidh?

SHAHIDI: Nilipokea silaha A5340 aina ya Luger kutoka kwa Hafidh ikiwa na risasi moja, maganda mawili.

NASHON: Kwa hiyo ulipokea vielelezo kutoka kwa Kolpo Hafidh?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Naomba sasa upokeee simu. Mheshimiwa Jaji ni kutoka katika kielelezo P28.

NASHON: Hii aina au dizaini la ku- lebel unaitolea wapi?

SHAHIDI: Kipo kwenye sheria.

NASHON: Sheria ambayo unaitumia ni sheria gani?

SHAHIDI: Ni PGO.

NASHON: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ulijaza makabidhiano wakati wa makabidhiano.

SHAHIDI: Humu sijaandika.

NASHON: Unafahamu kwamba katika kielelezo, lebel ya kielelezo pale unapoambatanisha namba ambayo unaambatanisha inatakiwa iwe namba ya jalada la kesi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Unafahamu kwamba unatakiwa pia uwe na exhibit serial number?

SHAHIDI: Siyo lazima kwa sababu hivi vielelezo vilikuwa kwenye mfuko kwa hiyo exhibit serial number inakuwa kwenye mfuko.

NASHON: Hiyo PGO unayosema ulitumia inataka uwe na mahala, namba na tarehe mnayokabidhiana?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Lakini hapa hakuna hata moja.

SHAHIDI: Ndiyo. Hapo hakuna.

SHAHIDI: Samahani Mheshimiwa Jaji, naomba niende washroom (kujisaidia).

(Shahidi amesharejea kizimbani).

NASHON: Nipo interested na shahidi ambaye alikuwa mtuhumiwa akaachiwa. Je, ni sahihi katika maelezo uliyomwandika wewe, aliandika kuwa aliwahi kuwa msaidizi wa katibu wa CCM Wilaya ya Meru?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Pamoja na kwamba kapokea fedha, na kashiriki vikao ila akaachiwa.

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Nani ni mwamuzi ambaye aliamua kuwa pesa hizo siyo za ugaidi?

SHAHIDI: Ni upelelezi.

NASHON: Ni nani hasa?

SHAHIDI: Mchakato wa upelelezi.

NASHON: Ni sahihi kwamba uliwahi kuandika maelezo yake Agosti 6, 2020?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ni sahihi kuwa katika maelezo yako uliwahi kusema kuwa Mbowe ameshiriki vikao vya kigaidi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Na katika maelezo yako ulisema kuwa, kuthibitisha hilo ni kupitia maelezo ya ONYO ya washitakiwa wenzake?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ni sahihi kwamba wewe na wapelelezi wenzio hamkuwahi kushuhudia Mbowe akiwa katika kikao cha ugaidi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ni sahihi kwamba wewe na wapelelezi wenzio hamkuwahi kushuhudia Mbowe akiwa katika kikao Mbeya au Arusha?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ni sahihi kwamba pia nyie kama wapelelezi wa kesi hii hamna CCtv camera?

SHAHIDI: Hatuna.

NASHON: Ni sahihi kwamba wewe na wapelelezi wenzio hamna hata sauti ya Mbowe akipanga ugaidi?

SHAHIDI: Ni sahihi. Hatuna.

NASHON: Ni sahihi kwamba Jeshi la Polisi lina vifaa vya kurekodi sauti?

SHAHIDI: Siwezi kuzungumzia hilo.

NASHON: Lakini unafahamu kwamba simu inaweza kurekodi sauti?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Na Jeshi la Polisi hamkatazwi kutumia simu kurekodi sauti.

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Na unajua kuwa Mahakama inaruhusu kutumia video na sauti katika ushahidi?

SHAHIDI: Sifahamu.

NASHON: Nikumbushe cheo chako huko Polisi.

SHAHIDI: Inspekta wa Polisi.

NASHON: Na Inspekta wa Polisi hujui kuwa Mahakama inatumika video na sauti katika ushahidi?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Ndiyo maana hamkuleta video wala sauti mahakamani kwa sababu hufahamu kama inatumika Mahakamani kama ushahidi?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Nionyeshe sasa sehemu ambayo Mahakama itaona Mbowe alikaa vikao vya kigaidi.

SHAHIDI: Ilikuwa kwenye gari. Ukisoma maelezo utaona.

NASHON: Naomba sasa Mahakama ikupatie hizo meseji.

SHAHIDI: Nimeona meseji ya tarehe 22 Julai 2020 muda wa waa 7:49. “Kutakuwa na safari ya kwenda Hai, leo usiku au asubuhi.”

(Wasikilizaji mahakamani wanaangua kicheko).

SHAHIDI: Hii inaelezea sasa kwamba kutakuwa kuna kikao.

NASHON: Katika hiyo meseji wataje wanaokutana.

SHAHIDI: Mtuhumiwa wa kwanza, wa pili, na wanne.

NASHON: Kwa hiyo mtu akisoma hiyo meseji ataona kwamba kuna kikao cha ugaidi?

SHAHIDI: Ushahidi ni kuunganisha dots.

NASHON: Kwa hiyo nikisoma meseji ipi nitaona nani na nani wametajwa, saa ngapi na wapi?

SHAHIDI: Kwenye meseji huwezi kuona, ila kwa kuunganisha dots.

(Wasikilizaji mahakamani wanaangua tena kicheko).

NASHON: Tutoke hapo. Umeshasema hatutaona meseji. Twende kwingine. Ni kweli kwamba mlikuwa na msiri wenu Dennis Urio?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Baada ya kuona hiyo meseji kwamba wanaenda Hai, nyie hamkufuatilia?

SHAHIDI: Hatukufutilia.

NASHON: Mnafahamu kuwa Aishi Hotel ina CCtv cameras?

SHAHIDI: Sifahamu.

NASHON: Na hufahamu kwa sababu hujawahi kufika Aishi Hotel. Sasa ulifanya juhudi zozote za kwenda pale Aishi Hotel kama mpelelezi ambaye yupo serious, labda kuandaa warranty, CCtv camera, kuangalia _list ya wageni?

SHAHIDI: Sikuwahi kufanya hivyo.

NASHON: Kwa ujasiri kabisa mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa uliwezaje kuwaleta watuhumiwa Mahakamani kwamba wamekutana sehemu fulani ambayo wewe na polisi wengine hamjawahi kufika.

SHAHIDI: Mimi nilikuwa sehemu ya upelelezi tu, kuna wengine ambao walikuwa Arusha na Kilimanjaro.

NASHON: Kwa hiyo wewe kwa sababu upo Dar es Salaam hukuona sababu?

SHAHIDI: Hapakuwa na ulazima.

NASHON: Sasa pale Aishi walifanyia nje au ndani?

SHAHIDI: Nje.

NASHON: Nje sehemu gani?

SHAHIDI: Kwenye garden.

NASHON: Garden ya upande upi?

SHAHIDI: Sifahamu. Sijawahi kufika.

NASHON: Katika ushahidi wako nimekusikia mahala kwamba unasema ulikuwa unapokea vielelezo na kuvitunza. Je, hapa Mahakamani umewahi kusema kuwa uliwahi kuwa Forensic Beaural?

SHAHIDI: Sijawahi kusema.

NASHON: Wewe ulikaa na vielelezo vipi ambavyo uliviandaa kwa ajili ya ushahidi?

SHAHIDI: Simu za Urio.

NASHON: Simu za Urio tu?

SHAHIDI: Simu zote nane.

NASHON: Za kwanza?

SHAHIDI: Nilipokea tarehe 7 Agosti 2020 mpaka tarehe 13 Agosti 2020.

NASHON: Tukumbushe nani alivileta Mahakamani.

SHAHIDI: Hivyo vielelezo nilimpa Inspekta Ndowo.

NASHON: Lini?

SHAHIDI: Sikumbuki.

NASHON: Kwa sababu hamkuandikishana.

SHAHIDI: Tuliandikishana.

: Lakini tukiangalia katika PF145 hatuoni sehemu mliyokabidhiana.

SHAHIDI: Ni sahihi. Hakuna.

NASHON: Ulikuwa unafahamu kuwa sheria inataka uonyeshe katika PF145?

SHAHIDI: Nilikuwa nafahamu.

NASHON: Ila ukaamua kupuuza sheria?

SHAHIDI: Hapana.

NASHON: Ni sahihi kwamba uliondoka pale Head Quarter Agosti 2021?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ni sahihi kwamba hujaieleza Mahakama baada ya kuondoka ofisini kwako vielelezo ulimuachia nani?

SHAHIDI: Usipotoshe Mahakama. Nilisema kwamba vielelezo vyote nilikuwa nimepeleka kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

NASHON: Unakumbuka muda ambao ulikaa na vielelezo amavyo vilienda Polisi Kati Dar es Salaam na kukaa navyo katika kabati la chuma?

SHAHIDI: Kwa nani …

NASHON: Je, ni sahihi kwamba ulichukua vielelezo kutoka kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam? YES or NO?

SHAHIDI: Yes.

NASHON: Kwanini sasa unapoteza muda wa Mahakama?

NASHON: Baada ya uchunguzi ulikaa navyo au ulipitiliza Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam?

SHAHIDI: Nilipeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

NASHON: Kwa hiyo ni sahihi kwamba ulikuwa umekaa na vielelezo katika kabati lako wakati wewe si mtunza vielelezo?

SHAHIDI: Nilikaa navyo kwa ajili ya kuviandikia barua kwa sababu ya upelelezi.

NASHON: Ilikuwa inashindikana kwa wewe kuandika barua vielelezo vikiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam?

SHAHIDI: Ilikuwa haiwezekani.

NASHON: Unafahamu kwamba OC Forensic Bureau ndiye anayehusika katika kuandaa na kutunza vielelezo kabla ya kwenda kufanyiwa uchunguzi?

SHAHIDI: OC wa Forensic Bureau anapelekewa na mpelelezi.

NASHON: Je, unafahamu kwamba OC Forensic Bureau ndiye anayehusika katika kutunza, kuandaa na kupeleka kwa expert examination?

JAJI: Sijui mimi ndiyo sielewi! Naomba wakili unisaidie.

Wakili Fredrick Kihwelo: Swali lake linahusu custodian wa kutunza kabla ya kwenda kwa expert examination.

SHAHIDI: Sifahamu.

NASHON: Katika ushahidi wako kuna sehemu ulisema kwamba DCI alikuambia pamoja na OC Forensic Bureau ndiyo mtunza kielelezo, lakini wewe kaa navyo?

SHAHIDI: Sikueleza hayo.

NASHON: Kwakuwa umeibuka mjadala hapo, na kwa kuwa Mheshimiwa Jaji shahidi alisema anaifahamu PGO, naomba nimwonyeshe shahidi PGO hii ambayo alikuwa anaitumia wakati wa kufanya kazi. PGO ya 8 paragraph ya 9.

(Shahidi anasoma PGO ya nane aya ya 9).

(Shahidi anasoma kwa sauti ya chini).

JAJI: Rudia na uongeze sauti.

NASHON: Soma Kipengele cha ‘E’.

JAJI: Samahani kidogo. Hapa OC anahusika baada ya OC kuwa ameletewa vielelezo. Hapa sheria inasema kwamba OC Forensic Bureau, ndani ya forensic baada ya kuvipokea. Nataka sasa kufahamu premise ya swali lako naandikaje. Inawezekana una hoja ila namna ya ulivyoliweka ndiyo unanichanganya.

NASHON: Labda kwako Mheshimiwa Jaji. Lakini najua siyo sawasawa.

JOHN MALLYA: Mheshimiwa Jaji, kwa kuokoa muda, wakili aende kwenye eneo lingine baadaye ndiyo arudi kuunganisha hapo.

JAJI: Sawa.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, hata sisi tunapata tabu kwa sababu shahidi alishasema siyo utaratibu. Nilifikiri kuanzia pale ndiyo tuelezwe.

JAJI: Ndiyo maana wanasema watarudi baadaye.

NASHON: Shahidi, ni sahihi kwamba wewe ndiyo ulimwandika maelezo Luteni Dennis Urio?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Na wakati wote unapomchukua mtu maelezo, akigusa unatakiwa umuonye?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Je, hukuona kosa pale ambapo Luteni Dennis Urio aliposema kwamba “Milimkubalia kwa kwenda kutafuta watu wa kufanya vitendo vya kigaidi” alikuwa anatenda kosa?

SHAHIDI: Soma yote ndiyo utaona siyo kosa.

Wakili Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji, naomba hapa kuweka sawa. Shahidi anaitwa kwa sheria tofauti na kifungu tofauti. Sasa anapoelekea wakili akatazwe. Shahidi hawezi kuwa mtuhumiwa.

NASHON: Mheshimiwa Jaji, kumsitiri kaka yangu Abdallah Chavula, PGO 236 paragraph 8 ambapo inasema _during police officers, during taking statement …

WAKILI WA SERIKALI: (Abdallah Chavula) Mheshimiwa Jaji nafikiri aendelee.

NASHON: Shahidi, nimekuuliza kwa uelewa wako wewe kama Police Officer kukubali kwenda kutafuta vijana hukuona ni kosa?

SHAHIDI: Sikuona kama ni kosa.

NASHON: Kwa ufahamu wako, kumtafutia mhalifu wahalifu wa kwenda kutimiza uhalifu siyo kosa?

SHAHIDI: Inategemea.

NASHON: Huyu Luteni Dennis Urio alikuwa ni askari Polisi?

SHAHIDI: Hakuwa askari Polisi. Siyo mimi niliyepokea taarifa zake. Mara ya kwanza alitoa taarifa kwa DCI.

NASHON: Kwani huyu Luteni Dennis Urio alikuwa na taaluma ya upelelezi?

SHAHIDI: Siyo mimi niliyepokea taarifa.

NASHON: Kwani Luteni Dennis Urio mlimfundisha kuhusu kufanyia watu upelelezi?

SHAHIDI: Mimi sikuwahi kumwona Luteni Dennis Urio kabla.

NASHON: Umesikiliza ushahidi wa Luteni Dennis Urio?

SHAHIDI: Wapi?

NASHON: Alipokuwa hapa Mahakamani.

SHAHIDI: Sikuwepo Mahakamani.

NASHON: Sawa. Ngoja nikwambie sasa. Urio ndiye aliwatafuta watuhumiwa lakini hawakuwa wanajua kuwa wanaenda kufanya ugaidi.

NASHON: Je, muda gani sasa Khalfani Bwire alipata guilty mind?

SHAHIDI: Anafahamu mwenyewe.

NASHON: Je, ni muda gani Adam Kasekwa alipata guilty mind?

SHAHIDI: Anajua yeye mwenyewe.

NASHON: Je, ni muda gani Mohammed Ling’wenya alipata guilty mind?

SHAHIDI: Sifahamu.

NASHON: Katika ushahidi wako ulisema uliitwa tarehe 14 Julai 2020 kwa Mkurugenzi. Je, ni sahihi?

SHAHIDI: Siyo sahihi.

(Wakili anasoma).

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Kwa hiyo tarehe 14 Julai 2020 taarifa zimekuja tayari kuna kundi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Unafahamu kwamba pesa zimeanza kutumwa tarehe 20 Julai 2020?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Je, hilo kundi lilikuwapo kabla halijakutana tarehe 20 Julai 2020?

SHAHIDI: Lilikuwapo kabla.

NASHON: Je, unafahamu kwamba kundi lilianza kutengenezwa na Luteni Dennis Urio tarehe 20 Julai (2020)?

SHAHIDI: Kundi lilikuwepo mara baada ya Luteni Dennis Urio kukutana na Freeman Mbowe.

NASHON: Kwani hilo kundi ni hili au kundi lingine?

SHAHIDI: Ni hili.

NASHON: Kwa hiyo wewe na Luteni Dennis Urio Mahakama iangalie nani anasema kweli?

SHAHIDI: Mahakama ndiyo itajua.

NASHON: Shahidi, ni sahihi ulisema kwamba hamkuandikisha jina la Freeman Mbowe kwa sababu taarifa zingevuja?

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Kwa hiyo kuna askari siyo waaminifu?

SHAHIDI: Tulihofia kwamba kile kitabu kinasomwa na kubadilishana taarifa kwa Polisi.

NASHON: Kwani wewe unafahamu sheria yoyote inayoruhusu kufungua kwa balada bila kujaza jina?

SHAHIDI: Hakuna.

NASHON: Lakini unafahamu sheria ambayo inaelekeza majina yajazwe.

SHAHIDI: Nafahamu.

NASHON: Shahidi, wakati unaenda kule Coco Beach kumtafuta Khalfani Bwire, hukuona haja ya kuwachukua watuhumiwa wenzake kwenda pamoja kumtafuta Khalfani Bwire kwa sababu wangemtambua hata kama kawapa mgongo?

SHAHIDI: Hapakuwa na haja hiyo.

NASHON: Shahidi nakuuliza kuhusu kidaftari. Ulisema kuna kidaftari.

SHAHIDI: Ni sahihi.

NASHON: Ulisema kile kidaftari kina michoro ya ramani?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Kwani wewe una taaluma ya ramani?

SHAHIDI: Hapana, ila naweza kusoma ramani.

NASHON: Kwani nikochora duara utajua ni kisima?

SHAHIDI: Hapana. Mle waliandika majina ya barabara na mishale ya kuingia na kutoka.

NASHON: Kwani kwenye hiyo ramani walitaja mikoa?

SHAHIDI: Hapana.

NASHON: Unaona GBP na Bigbon?

SHAHIDI: Sahihi.

NASHON: Kilichokufanya ujue ni Kariakoo na Morocco uliyokwenda wewe ni ipi?

SHAHIDI: Sababu palikuwa na majina ya barabara.

NASHON: Kwani hakuna majina ya barabara yanayofanana kama Morocco zipo mbili Kinondoni?

SHAHIDI: Nafahamu zipo mbili.

NASHON: Hicho kidaftari kipo hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Hapana.

NASHON: Ulisema kwamba Khalfani Bwire alikataa sampuli ya maandishi?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Unafahamu kwamba unapokuwa unamhoji mtuhumiwa kuna haki zake ikiwemo kuandika maelezo ya onyo?

SHAHIDI: Nafahamu.

NASHON: Maelezo ya kukataa hapa Mahakamani yapo wapi?

SHAHIDI: Hakuna.

NASHON: Unasema ulikuwa unawatoa watuhumiwa mahabusu kuwachukua sampuli. Je, huo muda ulifanyika kisheria?

SHAHIDI: Ndiyo.

NASHON: Umeleta Detention Register ambayo inaonyesha walitoka saa ngapi na kurudi saa ngapi?

SHAHIDI: Hapana.

NASHON: Nikikataa kuwa hukuwatoa kisheria una ushahidi gani?

SHAHIDI: Maelezo yangu.

NASHON: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapa kwa shahidi huyu.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji, nina maswali kadhaa. Ila naona muda wa health break umefika. Naomba tuahirishe kwa sasa.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, kwa dakika 45.

JAJI: Naahirisha mpaka saa 7:45.

Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama.

Saa 8:23 alasiri Jaji anaerea Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa. Quorumyetu iko kama awali na tupo tayari kuendelea.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo kama awali na tupo tayari kuendelea.

JAJI: Bwana Mallya karibu.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo …

MALLYA: Ile namba ya kesi CD/IR/2097/2020 ipo sahihi?

SHAHIDI: Sahihi

MALLYA: Ina maana yoyote hapa?

SHAHIDI: Inafanya reference kwenye kesi ambayo ipo Mahakamani.

SHAHIDI: Ni mtiririko wa kesi zilizopo.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba 39.

MALLYA: By the way Mheshimiwa Kielelezo kimeandikwa namba 29 nafikiri ni makosa ya karani wa Mahakama. Ilitakiwa kuwa kielelezo namba 39.

MALLYA: Shahidi namba hii ndiyo tunayoiona hapa?

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Kwa hiyo hakuna namba nyingine ambayo inafanana na hii namba hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Na hizi features zote ni za muhimu katika kuandika namba ya kesi katika hili faili?

MALLYA: Naomba mheshimiwa kielelezo namba P37.

MALLYA: Tazama katika karatasi hii. Je ni sahihi hakuna mkwaju?

SHAHIDI: Ni sahihi hakuna mkwaju katika kielelezo namba 37.

JAJI: Huo mkwaju una- miss wapi?

(Wakili John Mallya anamwelekeza Jaji).

MALLYA: Wakati mnakabidhiana simu na Dennis Urio ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Ofisi ndogo ya Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai.

MALLYA: Ni sahihi kwamba ofisi ile ndiyo ofisi kubwa ya upelelezi kuliko zote kwa Dar es Salaam?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Je, ofisi ya DCI Dar es Salaam ina uhaba wa vifaa?

SHAHIDI: Inategemea.

MALLYA: Wakati wa shauri kubwa kama la kesi ya ugaidi, utakubali kuvunja sheria au utasubiri vifaa?

SHAHIDI: Nitasubiri vifaa.

MALLYA: Sasa hii fomu hapa iliyojazwa hivi, ni just for cosmetics au inatakiwa kujazwa kama inavyotakiwa?

SHAHIDI: Inatakiwa ijazwe kama inavyotakiwa.

MALLYA: Hizo features zilitakiwa zijazwe au zisijazwe?

SHAHIDI: Zilitakiwa zijazwe.

MALLYA: Ni sahihi hizo fomu mlitakiwa mkabidhiane askari Polisi kwa askari Polisi?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Sasa wewe ulikabidhiana kwa fomu hiyo na askari?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Je, Dennis Urio alikuwa ni askari Polisi?

SHAHIDI: Hapana. Kwa sababu yeye ni shahidi.

MALLYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji akisoma wapi atajua yeye ni shahidi?

SHAHIDI: Hapa haionyeshi.

MALLYA: Fomu yenyewe inajieleza kuwa anayekabidhi, jina na sahihi ya anaye kabidhi.

SHAHIDI: Mtu anaye kabidhi hakuna jina.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe kielelezo D4, maelezo ya Bwana Dennis Urio.

MALLYA: Shahidi tumeulizana habari ya jina kujiridhisha kama kweli huyo mtu alikuwa ni Urio. Je, katika signature ya Dennis Urio kuna features zipi ambazo zinaonyesha?

SHAHIDI: Anayeweza kuitambua hii ni mtaalamu wa maandishi.

MALLYA: Kwa hiyo huwezi kuitambua?

SHAHIDI: Anayeweza kuitambua hii ni Luteni Dennis Urio.

MALLYA: Sijauliza kama unavitambua au huvitambui.

SHAHIDI: Kuna mkorogo tu. Anayeweza kuitambua hii ni mtaalamu wa maandishi.

MALLYA: Sasa hapa pia nina maelezo ya Dennis Urio, yana signature pia. Je kwa macho yako zinafanana au hazifanani?

SHAHIDI: Zinafanana.

MALLYA: Sawa. Nenda pale kwa ruhusa ya Mheshimiwa Jaji. Muonyeshe zinavyofanana.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe kielelezo P30. `

“(Mallya anapatiwa kielelezo).“`

MALLYA: Je, shahidi katika simu ya Bwire wewe ndiye uliyeandika exhibit label?

SHAHIDI: Nilijibu siyo mimi.

MALLYA: Maana ya kuhamisha faili maana yake ni nini?

SHAHIDI: Namba ya faili inabakia vilevile.

MALLYA: Je, unasema kwamba shughuli zinafanyikia wapi?

SHAHIDI: Inategemea.

MALLYA: Ulielezea kwa Mheshimiwa Jaji?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Bwire alikamatwa wapi?

SHAHIDI: Chang’ombe.

MALLYA: Unajua aliyejaza simu za za Bwire alijaza wapi?

SHAHIDI: Sijui.

MALLYA: Wakati wa Kingai na Goodluck wamemkamata Bwire wewe si ulikuwa Central?

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Hii simu ambayo nimeshika ni ya Bwire. Je, ilijaziwa wapi?

SHAHIDI: Sijui.

MALLYA: Lakini Kingai na Goodluck walikukuta Central.

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Msomee Mheshimiwa Jaji sehemu iliyoandikwa Station.

SHAHIDI: Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

MALLYA: Na simu ya Urio ulichukua wapi?

SHAHIDI: Ofisi ya DCI.

MALLYA: Shahidi nakuonyesha kielelezo P28. Simu ya Urio imeandikwa wapi? Kielelezo P29 msomee Mheshimiwa Jaji sehemu ya Station.

SHAHIDI: Polisi Kati Dar es Salaam.

MALLYA: Shahidi, tarehe 11 Agosti 2020 ndiyo Urio alikuja ofisini kwako, akakuachia simu moja.

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Wewe ni mpelelezi wa aina gani? Anayejipanga au kukurupuka?

SHAHIDI: Anayejipanga.

MALLYA: Kama anayejipanga, Urio alipokuambia kesho anakuja, ulikuwa umejipanga au hukuwa umepanga?

SHAHIDI: Za makabidhiano nilikuwa nazo, ila PF145 sikuwa nazo.

MALLYA: Kwa hiyo ulijipanga kuwa na fomu za makabidhiano ila za PF145 hukuwa nazo?

SHAHIDI: Ndivyo nilivyoeleza.

MALLYA: Haya. Shahidi msomee Mheshimiwa Jaji sehemu ya station imeandikwaje.

SHAHIDI: Polisi Kati Dar es Salaam.

MALLYA: Shahidi umeeleza wewe ulikuwa mjumbe wa Kikosi X. Je, wajumbe wa Kikosi X wanafamika na Jamii?

SHAHIDI: Wanafahamika.

MALLYA: Jumanne alikuwa katika kitengo hicho?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Kingai?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Goodluck?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Mahita?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Mwenzako wa Kitengo X alikuwa nani?

SHAHIDI: Afande Msangi.

MALLYA: Mwingine nani?

SHAHIDI: Ni huyo tu.

MALLYA: Kumtukana Rais mtandaoni ni kuhatarisha usalama wa nchi?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Ugaidi ni kuhatarisha usalama wa nchi?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Kwa sasa upo ofisi ya RCO Temeke?

MALLYA: Ni sahihi kwa mlalamikaji kuteua mpelelezi wangu?

SHAHIDI: Hapana.

[MALLYA: Katika kesi hii mlalamikaji ni nani?

SHAHIDI: Afande DCI.

MALLYA: Wewe alikuteua nani?

SHAHIDI: Afande DCI.

MALLYA: Kwa hiyo sisi haturuhusiwi kuchagua mpelelezi ila kwa DCI analalamika na kuteua wapelelezi?

SHAHIDI: Kwa hili mazingira ni tofauti.

MALLYA: Ulimweleza Mheshimiwa Jaji hayo mazingira tofauti?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Nilisikia umeandika barua kwa DCI wakati huo Wambura tarehe 18 Julai 2021.

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Wakati unatoa ripoti kwa DCI ulikuwa unamdanganya au ulikuwa serious?

SHAHIDI: Nilikuwa nipo serious.

MALLYA: Wakati unaandika ripoti kwa DCI watuhumiwa wengine walikuwa tayari upelelezi wao tayari au bado?

SHAHIDI: Ilikuwa tayari katika ripoti hiyo hiyo.

MALLYA: Wakati unaandika ripoti hiyo ya kutaka sasa Mbowe akamatwe ulikuwa na ushahidi au ulikuwa unataka Mbowe akae ndani kidogo?

SHAHIDI: Nilikuwa na ushahidi wa kutosha.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo D1.

MALLYA: Tarehe 18 Julai 2021 umemwandikia DCI una ushahidi wa kutosha?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Ni sahihi kwamba maelezo ya Justine Kaaya uliyachukua tarehe 30 Julai 2021 kuhusu ugaidi wa Mbowe wakati huo umeshamkamata Mbowe tayari?

SHAHIDI: Ndiyo. Lakini huo ni ushahidi wa ziada.

MALLYA: Unataarifa mwaka huu kuna masoko yameungua?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Na Moshi na kwingine kote masoko yameungua?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Yameungua wakati hawa wapo ndani, mnasema kwamba walipanga kuchoma masoko. Je, nikisema yanaungua sababu ya laana ya kumsingizia Mbowe nitakuwa nakosea?

SHAHIDI: Ni uongo. Hilo ni kosa moja, lakini wanashitakiwa na makosa ya kukata miti barabarani, kupanga njama za ugaidi, kutaka kudhuru viongozi.

MALLYA: Wakati unaandika taarifa ya kwenda maabara ya kisayansi, simu ya Kaaya na wenzake ulikuwa nazo?

SHAHIDI: Nilikuwa nazo.

MALLYA: Uliambatanisha katika maombi ya uchunguzi?

SHAHIDI: Hapana. Walikamatwa baada ya kuwapeleka hawa Mahakamani. Nilipeleka simu za watu watatu tofauti.

MALLYA: Wakati wa ushahidi wako ulizungumzia hilo? Kkatika maelezo ya Kaaya, Kaaya anasema alikuwa anapigiwa simu na Mbowe.

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Je, finding za Kaaya zipo hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Ushahidi wa utaalamu wa uchaguzi wa simu ya Kaaya mnayo Jeshi la Polisi?

SHAHIDI: Taarifa zimeanza kufanya tarehe 10 Agosti 2020.

MALLYA: Kwa hiyo Mbowe na Kaaya waliwasiliana baada ya hawa mabwana kukamatwa?

SHAHIDI: Hakuendelea kuwasiliana naye.

MALLYA: Sawa. Hiyo conclusion naiachia Mahakama.

MALLYA: Kuna simu ulipewa na IMEI namba yake ilikuwa Imefutika.

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Ulipewa katika hali gani?

SHAHIDI: Ikiwa imezimwa na ukiwasha inakuwa katika flight mode.

MALLYA: Simu ya nani hiyo?

SHAHIDI: Mohamed Abdillah Ling’wenya.

MALLYA: Wakati unakabidhwa ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikabidhiwa nikiwa katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

MALLYA: Umepewa simu ukaambiwa IMEI namba zake zimefutika, wakati unapewa simu ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa ofisi ndogo ya DCI.

MALLYA: Ulikuwa na nani aliyeshuhudia?

SHAHIDI: DC Goodluck.

MALLYA: Mohammed Ling’wenya alikuwapo?

SHAHIDI: Hakuwepo.

MALLYA: Anita Mtaro?

SHAHIDI: Hakuwepo.

MALLYA: Esther Nduguhuru?

SHAHIDI: Hakuwepo.

MALLYA: Na ukasema ukabonyeza namba fulani fulani ukapata taarifa uliyokuwa unatafuta katika ile simu?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Turudi tena pale Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Ni sahihi ulisema kwamba siku ya tarehe 7 Agosti 2020 ulipigiwa simu kuwa uje kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Ni sahihi ulikabidhiwa simu?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Baada ya hapo mlitoka kwenda Sinza na Coco Beach?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Mpaka hapo hukusema zile simu ulihifadhi wapi.

SHAHIDI: Nilirudisha.

MALLYA: Uliyasema hayo wakati anakuongoza kaka yangu Kidando?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Vifaa simu na computer vilivyokamatwa kuhusu kesi hii vilikuwa vinakuja kwako?

SHAHIDI: Siyo sahihi.

MALLYA: Unafahamu kwamba computer, router za watoto na mke wake vilikamatwa?

SHAHIDI: Ninachofahamu mimi, mtuhumiwa alikamatwa na simu na laptop.

MALLYA: Simu ngapi?

SHAHIDI: Si zaidi ya moja.

MALLYA: Aina gani ya simu?

SHAHIDI: Sikumbuki.

MALLYA: Computer?

SHAHIDI: Zaidi ya moja.

MALLYA: Angalau zilikuwa mbili.

SHAHIDI: Sikumbuki.

MALLYA: Vitu hivi ulipeleka wewe maabara ya uchunguzi?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Wakati Wakili wa Serikali Robert Kidando anakuongoza ulitoa ushahidi huo wa kupeleka vifaa hivyo?

SHAHIDI: Hapana. Sikusema.

MALLYA: Uchunguzi huo unasemaje?

SHAHIDI: Leo ndiyo nimejulishwa kuwa matokeo ya uchunguzi yamekamilika.

MALLYA: Kwa hiyo leo ndiyo upelelezi wa kesi ya Mbowe umekamilika?

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Kuna tuhuma hapa. Line za simu za Dennis Urio hazifahamiki zilipo. Je, umepeleka wapi?

SHAHIDI: Zipo katika simu zake.

MALLYA: Dennis Urio alikuja hapa akawasha simu zake akasema hazioni line zake. Kwa hiyo Jaji atapima maelezo yako wewe na Dennis Urio.

MALLYA: Ni sahihi kwamba madawa ya kulevya yanaongeza hali ya uhalifu?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Je, Mbowe anaweza kuwapa hawa vijana madawa ya kulevya ili wakafanye uhalifu?

SHAHIDI: Inategemea.

MALLYA: Shahidi, je tuhuma za ugaidi na madawa ya kulevya yanaunganika?

SHAHIDI: Inategemea.

MALLYA: Ni sahihi kwamba kukutwa kwa madawa ya kulevya kungeweza kuongeza hali ya wao kutenda ugaidi sasa?

SHAHIDI: Madawa ya kulevya hayahusiani na ugaidi kwa sababu ugaidi ni kesi nyingine na madawa ni kesi nyingine.

MALLYA: Kesi ya madawa iko wapi?

SHAHIDI: Ilifunguliwa Moshi.

MALLYA: Inaanza lini ili kama wakili wake Adamoo nijiandae?

SHAHIDI: Siwezi kufahamu.

MALLYA: Wakati DC Goodluck anakukabidhi vielelezo alikuambia anatoka wapi?

SHAHIDI: Alisema anatoka Moshi.

MALLYA: Kwamba alienda nazo kwa mama Ntilie kunywa supu na kupiga mswaki hakukwambia?

SHAHIDI: Hakuniambia.

MALLYA: Hivi malalamiko kuja Kitengo X yalikuwa ofisi za DCI ila wewe ukaenda kufungua kesi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam?

SHAHIDI: Malalamiko yalianzia kwa DCI.

MALLYA: Nani alisema ukafungue kesi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam?

SHAHIDI: Ni Kingai.

MALLYA: Alikuambia kwanini hakukwambia ukafungue Kituo cha Temeke au Oysterbay?

SHAHIDI: Hakuniambia.

MALLYA: Je, angekuambia ukafungue Oysterbay ingekuwa tofauti?

SHAHIDI: Kwa nature ya kesi yenyewe isingewezekana kwa sababu kuna mikoa inahusika.

MALLYA: Kwa nini hamkufungua Moshi, Kilimanjaro?

SHAHIDI: Kwa nature ya offense yenyewe.

MALLYA: Kwani makao ya nchi ni Dodoma au yalisharudi Dar es Salaam?

SHAHIDI: Ni Dodoma.

MALLYA: Polisi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ni wambea kwamba wangetoa taarifa?

SHAHIDI: Hapana. Si kweli.

MALLYA: Je, Kitengo X kinaweza kutoa amri kwa polisi wa mkoa wa fulani wamkamate mtu fulani?

SHAHIDI: Inawezekana.

MALLYA: Tarehe 14 Julai 2020 (Wakili wa Serikali) Kidando alitoa wapi hii tarehe?

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, mimi nilikuwa namwongoza shahidi. Sasa sijui wakili ana lengo gani.

MALLYA: Sawa. Nitarudia swali. Je, tarehe 14 Julai 2020 aliyokuwa anakuuliza alitoa wapi?

SHAHIDI: Alitoa kwangu.

MALLYA: Maelezo yako ninayo hapa. Hakuna sehemu umeandika kuhusu tarehe 14 Julai 2020.

SHAHIDI: Ni sahihi. Hakuna tarehe 14 Julai 2020.

MALLYA: Huyu mtu alitoa wapi sasa hii tarehe 14 Julai 2020?

SHAHIDI: Mimi ndiyo nimetoa wakati wa kukumbushia maelezo yake.

MALLYA: Wewe ulimweleza Mheshimiwa Jaji kuwa ulitoa wapi hizo memory?

SHAHIDI: Sikuumweleza.

MALLYA: Unasema tarehe 7 Agosti 2020 Kingai alikupigia simu kwamba wale watu weshapatikana?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Maelezo ya Kingai umeshawahi kuyaona?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Sasa …

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji naomba niende washroom.

(Shahidi amesharejea kizimbani.)

MALLYA: Je, shahidi unajua Kingai alipokuwa anapata taarifa?

SHAHIDI: Nilikuwa najua.

MALLYA: Na unaamini kuwa alikuwa hadanganyi na hamuonei Mbowe? Je, ulikuwa unafahamu kwamba simu ya nani ilikuwa ina- coordinate?

SHAHIDI: Simu ya Mbowe.

MALLYA: Kwenda kwa nani?

SHAHIDI: Kwa Luteni Dennis Urio.

MALLYA: Wale ambao sasa tarehe 14 mnaosema kuwa wale watu wamepatikana, je, hapa Mahakamani wapo?

SHAHIDI: Hawapo. Siku ambayo Luteni Dennis Urio alikutana na Freeman Mbowe ndiyo ukisoma Mbowe anasema kwamba mimi na chama changu Chadema kimedhamiria kuchukua nchi.

MALLYA: Kwa hiyo kundi lake mlilofungulia kesi ni chama chake?

SHAHIDI: Sijui sasa kama chama chake.

MALLYA: Kwa hiyo hao anaosema chama changu wewe huwajui?

SHAHIDI: Siwajui.

MALLYA: Unafahamu kwamba 2020 ulikuwa mwaka wa uchaguzi?

SHAHIDI: Nafahamu.

MALLYA: Unafahamu kwamba Mbowe na wenzake walikuwa wanagombea nafasi mbalimbali?

SHAHIDI: Nafahamu.

MALLYA: Je, unafahamu kwamba vyama vya siasa vimeundwa kwa dhumuni la kuchukua dola?

SHAHIDI: Ni sahihi kama utafuata sheria.

MALLYA: Ni sahihi kwamba vyama vingine vimeundwa kwa lengo la kushiriki uchaguzi kuchukua dola?

SHAHIDI: Lengo kubwa la chama ni kuchukua dola.

MALLYA: Unafahamu kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe ni kiongozi wa chama gani?

SHAHIDI: Chadema.

MALLYA: Chama cha Mheshimiwa Mbowe mwaka 2020 kilishiriki uchaguzi au hakikushiriki?

SHAHIDI: Kilishiriki.

MALLYA: Wewe kama mpelelezi uliwahi kumhoji Lengai Ole Sabaya?

SHAHIDI: Sijawahi.

MALLYA: Je, kama hiyo mipango ingetimia angedhurika?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Hata Kingai mwenyewe hajawahi kumhoji Sabaya.

SHAHIDI: Hajawahi.

MALLYA: Hujawahi kusikia kauli ya Afande Sirro kwamba kesi ya kupigwa risasi Lissu wanashindwa kufanya upelelezi kwa sababu wameshindwa kumhoji Lissu?

SHAHIDI: Sijawahi kusikia.

MALLYA: Haya. Sabaya sasa ambaye ni victim hajawahi kuhojiwa lakini upelelezi wake umekamilika. Je, hii si double standard?

SHAHIDI: Sabaya bado siyo victim.

MALLYA: Kuna mtu kapigwa risasi upelelezi wake haujakamilika, lakini kuna mtu hata hajaguswa na upelelezi umekamilika.

SHAHIDI: Siwezi kuzungumzia suala ambalo sijapeleleza.

MALLYA: Lengo la kwenda TiGO na Airtel ilikuwa kuleta Mahakamani kama ni kweli?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Sasa kilichokushinda kuandika barua kwenda EWURA kuthibitisha kwamba kweli kuna kituo cha mafuta pale Morocco?

SHAHIDI: Sikuona haja hiyo.

MALLYA: Je, ulithibitisha vipi kituo kama kinauza mafuta kweli? Ulinunua hata mafuta ya 5,000/-?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Haya. Ulienda kuthibitisha masoko katika vyama vya ushirika kwa kuandika barua?

SHAHIDI: Sikuona haja hiyo.

MALLYA: Mimi nikibisha kwamba hakuna hayo masoko sasa, utathibitisha kwa lipi?

SHAHIDI: Kwa ushahidi wangu.

MALLYA: Shahidi mnataka kujenga picha kwamba mlifahamu Mbowe alitaka kutenda ugaidi na nyie kumwezesha?

SHAHIDI: Si kweli.

MALLYA: Kufanya kikao cha ugaidi kosa siyo kosa?

SHAHIDI: Ni kosa.

MALLYA: Kama kukaa kikao cha ugaidi ni kosa, je, hao waliokaa kikao cha ugaidi walitoka wapi?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Hao watu ambao Mbowe anashitakiwa kufanya nao kikao chao, Mbowe aliwapata wapi?

SHAHIDI: Alitafutiwa kwa lengo la kukusanya taarifa.

MALLYA: Kwa hiyo wakati wanafanya kikao walikuwa wanafanya ugaidi au wanakusanya taarifa?

SHAHIDI: Walikuwa wameshawishiwa.

MALLYA: Kwani kikao cha ugaidi walikuwa wamekaa wapi na akina nani?

SHAHIDI: Washitakiwa wanne katika Hotel ya Aishi.

MALLYA: Kwani tarehe ngapi walikuwa wamebadilika kuwa magaidi?

SHAHIDI: Tarehe 25 Julai 2020.

MALLYA: Swali langu ni tarehe 20 Julai 2020 wakati wanatumiwa pesa walikuwa magaidi au siyo magaidi?

SHAHIDI: Hawakuwa magaidi.

MALLYA: Kama tarehe 20 Julai 2020 Mbowe anatuma pesa kwa wale watu zilikuwa safi au chafu?

SHAHIDI: Ilikuwa chafu kwa sababu Mbowe alikuwa anajua lengo.

MALLYA: Na mwamala wa tarehe 22 Julai 2020 zile pesa ambazo walitumiwa siku hiyo na zenyewe safi au chafu?

SHAHIDI: Pesa chafu.

MALLYA: Tarehe 25 Julai 2020 kama wangekataa zile pesa wangekuwa na hatia?

SHAHIDI: Wasingekuwa na hatia.

MALLYA: Mbowe katika hicho kikao cha watu wanne angekuwa amekaa kikao cha ugaidi au siyo?

SHAHIDI: Angekuwa amekaa kikao cha ugaidi.

MALLYA: Je, shahidi kama upo ofisini kwako akasema anataka kwenda kuiba benki, utakuwa na wajibu wa kuzuia au utamwacha?

SHAHIDI: Hilo haliwezekani mhalifu akupe taarifa.

MALLYA: Nikija kwako kwamba nataka kuiba benki, je, utanizuia au utaniacha?

SHAHIDI: Nitakuzuia.

MALLYA: Sasa DCI kapata taarifa kutoka kwa Luteni Dennis Urio (msiri wake) kwamba Mbowe anataka kufanya uhalifu wa kigaidi, je, alikuwa ana wajibu wa kuzuia au la?

SHAHIDI: Ndiyo maana alizuia.

MALLYA: Vipi kikao kilifanyika au hakikufanyika?

SHAHIDI: Kilifanyika.

MALLYA: Sasa Luteni Dennis Urio anasema alimpatia DCI taarifa kwamba Mbowe anatafuta watu akae nao kikao cha kigaidi, lakini DCI hakufanya lolote. Kikao kikafanyika, DCI katika hili hakuwajibika.

SHAHIDI: Si kweli.

MALLYA: Unafahamu kwamba kuna njia ya kuweka mamluki ambao mtu anakuwa nao akidhani ni wenzake halafu kumbe wanatoa taarifa?

SHAHIDI: Nafahamu.

MALLYA: Je, katika ushahidi wako ulizungumzia kuhusu kuweka mamluki au kutokuweka?

SHAHIDI: Sikueleza.

MALLYA: Unasema kwamba Mbowe alikaa vikao kuanzia Mei mpaka Julai kula njama za kutenda ugaidi?

SHAHIDI: Sahihi.

MALLYA: Kuna sehemu umetaja vikao vilifanyika wapi?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Wewe ndiye ulikuwa mpelelezi katika hili shauri. Je, wewe uliwahi kumwambia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa kuna watu wameshafungwa katika shauri hili?

SHAHIDI: Sijawahi kumwambia. Na ndiyo nasikia leo.

MALLYA: Je, shahidi unafahamu kwamba wakati Mheshimiwa Mbowe anakamatwa alikuwa Mwanza katika Kongamano la Katiba?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Kuna tuhuma dhidi yako kwamba ulipokuwa Tazara ulishiriki kumpiga kwa kusema “mshusheni chini tumshughulikie.”

SHAHIDI: Si kweli. Mtuhumiwa nilikutana naye Chang’ombe Polisi.

MALLYA: Kwani Kituo cha Polisi Chang’ombe ni cha ghorofa?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Kwanini sasa useme “mshusheni chini tumshughulikie”?

SHAHIDI: Si kweli.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba P36.

MALLYA: Wakati unaulizwa maswali na wakili msomi Nashon Nkungu ulifanya reference katika hii.

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Soma tena.

SHAHIDI: (Anasoma) Watakuwa tena na safari ya kwenda Moshi leo au kesho asubuhi.”

MALLYA: Kuna meseji yoyote inasema kwamba wamefika Hai?

SHAHIDI: Hakuna.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe kielelezo P15, 16, na 17.

MALLYA: Nilikuuliza swali mwanzo kwamba wewe ni mpelelezi unayejipanga au kukurupuka? Ukasema unajipanga. Ni sahihi kwamba uliomba taarifa za namba tatu?

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Ni sahihi wakati Airtel wanajibu walijibu namba mbili.

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Namba ipi taarifa zake zina- miss?

SHAHIDI: Ni namba 0782 237913.

MALLYA: Unataka nikuulize miamala ya Dennis Urio. Wacha nikuulize shahidi.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji namuuliza extraction ya Dennis Urio, kielelezo namba P20. Muamala kutoka kwa wakala. Muamala wa tarehe 22 Julai 2020, shilinigi 199,000 imeingia.

SHAHIDI: Ni sahihi kuwa muamala wa shilingi 199,000 umeingia kwenye namba ya simu ya Luteni Dennis Urio.

MALLYA: Unafahamu hii namba ya chini muamala wa shilingi 7,000 alipewa nani kwenda namba 0787-000 027?

SHAHIDI: Sifahamu.

MALLYA: Shahidi ulisema kwamba ulimruhusu shahidi kutoa line kwa sababu hata ukitoa line ya simu mawasiliano yatabakia kwenye simu?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Unafahamu au ulikuwa unajiongeza?

SHAHIDI: Nilikuwa nafahamu.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo P22 mpaka kielelezo namba P27 nimpatie mtaalamu wa Telegram.

MALLYA: Nakuonyesha kielelezo namba P26, kielelezo ameleta Bwana Ndowo.

SHAHIDI: Nilichokuwa nasema mimi, kwamba hata ukitoa line kwenye simu bado extraction report ya simu na simu taarifa zitafanana.

MALLYA: Haya. Namba ya Bwana Dennis Urio katika report ya Bwana Ndowo hebu itaje sasa.

SHAHIDI: 1130138344

MALLYA: Ulitoa explanation wakati unaongozwa na Wakili Msomi Kidando kuhusu hii variation iliyopo katika simu na extraction report?

SHAHIDI: Sikutoa.

MALLYA: Wewe na Goodluck ndiyo mlibadilishana vielelezo. Je, ulitoa maelezo kuhusu mvunjiko vunjiko wa simu pembeni katika kielelezo namba 27 na 35?

SHAHIDI: Sikueleza.

MALLYA: Ulihifadhi hizi simu. Kuna simu iliwashwa ilikuwa na chaji na zingine hazikuwaka. Je, unaweza kueleza kwanini simu moja tu ya Dennis Urio iliweza kuwaka hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Siwezi kujua. Miye nilikabidhi siku nyingi.

MALLYA: Wewe lakini una tabia za kuchungulia simu za watu. Unakumbuka ulichungulia simu ya Ling’wenya?

SHAHIDI: Siyo kuchungulia, bali niliangalia IMEI namba.

MALLYA: Ni sahihi kwamba hii namba ya jalada la kesi ina washtakiwa zaidi ya hawa wanne?

SHAHIDI: Ndiyo.

MALLYA: Je, katika wingi huo naweza kutaja kitu cha mtu bila kufafanua?

SHAHIDI: Kama kuna jina au namba unaweza kujua.

MALLYA: Sasa katika maelezo yako kuna sehemu unasema pia uchunguzi wa cyber unaonyesha waziwazi na jinsi mtuhumiwa Freeman Mbowe aliwaelekeza wenzake jinsi ya kutekeleza mipango yake.

SHAHIDI: Ni sahihi.

MALLYA: Sasa umeonyesha Mahakamani wakati wa ushahidi wako kuwa hapa ndiyo alikuwa anawaelekeza watuhumiwa cha kufanya?

SHAHIDI: Ndiyo. Nimeonyesha.

MALLYA: Ulipata kujua sasa wakala aliyetuma pesa ni yupo wapi?

SHAHIDI: Hapana.

MALLYA: Umeeleza ni wakala wa mtandao gani?

SHAHIDI: Kama nilivyojibu awali. Sikueleza.

MALLYA: Kuhusiana na taarifa ya Ballistic. Ni kweli wewe ndiye uliyempa ruhusa Koplo Hafidh kuharibu zile risasi?

SHAHIDI: Hakuziharibu. Alizichunguza.

MALLYA: Ulipompelekea wewe Koplo Hafidh zile risasi, zilikuwa ngapi?

SHAHIDI: Zilikuwa tatu.

MALLYA: Zilikuwa na hali gani?

SHAHIDI: Zilikuwa moja ni nzima na mbili zilikuwa zimetumika.

MALLYA: Hizi mbili ambazo ulipeleka zilikuwa sawa na wakati unazipeleka?

SHAHIDI: Zilikuwa katika hali ya kutumika.

MALLYA: Mheshimiwa Jaji sina swali la ziada. Naomba kurudisha vielelezo.

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji, tumebakia na dakika tano. Kwa sababu ya muda tunaomba ahirisho kwa sababu hizo dakika hazitoshi.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi.

(Mahakama iko kimya wakati Jaji anaandika).

JAJI: Kufuatia maombi yaliyoletwa na wakili wa mshtakiwa wa tatu juu ya muda, naahirisha shauri hili mpaka kesho saa tatu asubuhi. Shahidi naomba kesho tarehe nane urudi kutoa ushahidi wako. Washitakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka kesho asubuhi saa tatu asubuhi.

Jaji anaondoka katika chumba cha Mahakama saa 11:02 jioni.

Like