MALYA: Adamoo na Ling’wenya mlipoachana Morogoro walikwenda wapi? SHAHIDI: Walikwenda Dar es Salaam. MALYA: Kielelezo D1, katika maelezo aliyoandika Kingai anasema alimuhoji Ling’wenya akakiri. Soma hapa. SHAHIDI: “Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi. MALYA: Na wewe umesema walipotoka kwako walikwenda wapi? SHAHIDI: Nimekwambia Dar es Salaam siyo Moshi. MALYA: Kwenye nauli uliwapa TSh ngapi? SHAHIDI: 199,000. MALYA: Hapo wao wameandika uliwapa shilingi ngapi? SHAHIDI: Nauli TSh 87,000. KIBATALA: Unaweza kutuisaidia kwanini Inspector Swila alifungua faili la kula njama tarehe 18 Julai 2020 wakati umekutana na hawa vijana tarehe 20 mpaka 24? SHAHIDI: Sijui sasa. KIBATALA: Je, wewe ulikula njama na Mbowe? SHAHIDI: Sijala njama na Mbowe. KIBATALA: Kwani shahidi suala hili kuna mtu zaidi yako alienda kutoa taarifa kwa DCI? SHAHIDI: Ni mimi peke yangu ndiye niliyemwambia DCI. KIBATALA: Kwani wewe ulimueleza Jaji kwamba Mbowe alikuwa tayari ana vijana wengine? SHAHIDI: Sikumwambia mheshimiwa jaji.
KIBATALA: Na ni simu ipi pia itaonyesha call records za simu ya Bwire tarehe 04 August 2020? SHAHIDI: Ni hiyo simu ya Samsung Duo.KIBATALA: Hivi ile simu yako ya jana uliikabidhi lini?SHAHIDI: Tarehe 11 August 2020. KIBATALA: Ulimfafanulia Jaji kwamba simu yako ina uwezo wa kukaa na chaji zaidi ya mwaka mmoja na nusu? SHAHIDI: Hapana. KIBATALA: Simu yako ilikuwa na kiasi gani cha charge wakati unamkabidhi? SHAHIDI: Ilikuwa chini kidogo ya nusu. KIBATALA: Ulimfafanulia Jaji kwanini simu hii ni tofauti na zile tatu, kwamba inakaa na chaji mwaka mmoja na nusu? SHAHIDI: Siku fafanua.
Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 28 Januari 2022.
Jaji ameingia mahakamani saa 4 na dakika 4
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili wa Serikali Waandamizi na
Tulimanywa Majige Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala: nipo Pamoja na wakili
Seleman Matauka
Alex Massaba
Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Maria Mushi
Evaresta Kisanga
Khadija Aron
Michael Lugina
Evaresta Kisanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Dickson Matata:
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea
Shahidi: anapanda Kizimbani, ana shati Jipya la Mikono Mirefu lenye weupe na Blue blue fulani ya mchongo..
Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa UShahidi: Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo
Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho
Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana…
Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje
Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi
Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum’ protect
Shahidi: Ni sahihi
Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?
Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26
Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem’ protect, Sasa Ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi
Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time
Malya: Kwa Kazi gani
Shahidi: Ulinzi Ndiyo
Malya: Je kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?
Shahidi: kwenye meseji hazipoMalyaJe kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?
Shahidi: kwenye meseji hazipo
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35
Hii ni Ile simu yake aliyowasha Jana ndugu homeboy.. M
Ni Kielelezo namba 34 kama sijasahau.. Mtanikumbusha wadau…
Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?
Shahidi: Imeandikwa FREE… Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe
Malya: Very Good Shahidi: umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa easha simu yako
Shahidi:anabonyeza simu, anasema tayari
MalyaUnasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram
Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram
Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume’ chat na Mbowe.. Je Hapa Kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group,, nafungua…
Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?
Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe
Malya: Je ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?
Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu
JajiUmeelewa Swali.? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani
ShahidiUfafanuzi huo sikutoa
Mahakama: Kichekooo
Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, Je Meseji zimeanza lini
Shahidi: Tarehe 20 July 2020
Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini
Shahidi: alikuwa ananipigia Simu
Malya: Alikuwa anakupigia Simu Kwa Njia ipi
ShahidiKwa Telegram
Malya: Je unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record
Shahidi: Sina Utaalamu huo
Malya: Je Jana Wakati wa UShahidi: Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe
Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu
Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi: hajasema hivyo
Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp l
Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram
Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa UShahidi: Wako?
Shahidi: Sikuonyesha
Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu
Shahidi: Sikuonyesha
Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..
Malyasitaki sababu hapa
Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu
Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu
Jaji: Shahidi sililiza swali ndiyo ujibu
Malya: Naomba Kielelezo Namba 28
Malya: Anam kabidhi shahidi
Malya: Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu
Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka
Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka
Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote
Malya: Kama Kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa UShahidi: Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa
sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi
Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane
Shahidi: Washa wewe
Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako
Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji
Malyawewe Ndiyo Mwenye Simu
Shahidibasi hayo Mengine ni Maoni
Malya: Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe
Shahidi: Sikuonyesha
Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha
ShahidiSikuonyesha, Sababu sikuulizwa
Malya: Je Jana Ulionyesha Meseji za Ling’wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke
Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona
Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne
Shahidi: Ndiyo
Malya: Soma hapa
Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu
MalyaSasa Kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini
Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire
Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza
Shahidi: Ndiyo
Malya: Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?
Shahidi: Mimi sifahamu anafahamu Mbowe
Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe
Malya: Shahidi: Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi
Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua
Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako
Shahidi: Ndiyo
Malya: Je Ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Nilifika Kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao
Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?
Shahidi: Sikueleza
Malya: Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?
ShahidiMimi sifahamu
Malya: Je unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi
Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi
Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia
Shahidi: Hakuniambia
Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi
Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine
Malya: Bwire alikuja Nyuma yako
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini
Shahidi: 2010
Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora
Shahidi: Hapana
Malya: Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki
Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu
Malya: Ulipewa award gani
Shahidi: Sikupewa Award
Malya: Lakini wewe Ulifuzu
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?
Shahidi: Ni sahihi
Malya: na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi
Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa
Shahidi: Ni Afisa
Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling’wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani
Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye
Malya: Shahidi: Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?
Shahidi: Hapana
Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Una kwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa Coplo
Shahidi: Ni sahihi
Malya: na Kwenye Jeshi Coplo siyo Afisa
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Shahidi: ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi
Shahidi: amekuuliza Coplo ni Afisa siyo Afisa
Shahidi: Ni Afisa
Malya: Wakati Una kwenda Darfur ulikuwa na Ling’wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani
Shahidi: Sija kana, Siwezi Kukumbuka kama. Nilikuwa naye
Malya: Shahidi: Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree.?
Shahidi: Hapana
Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Malya: Adamoo na Ling’wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi
Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo D 1
Ambapo ni Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling’wenya akakiri, Soma hapa.
Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi
Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi
Shahidi: Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi
Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi
Shahidi: TSh 199,000
Malya: hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi
Shahidi: Nauli TSh 87,000
Ndivyo walivyo andika wao
Malya: Ulielezea Shahidi: Kwenye UShahidi: Wako namba Uliyotumia Kuwasiliana na Bwire ni Namba gani
Shahidi: Sikueleza
Malya: Je Wakati Mnaenda Kuonana na Swila Mara ya Kwanza Ilikuwa lini
Shahidi: Tarehe 11 August 2020
Malya: Ndiyo Siku hiyo hiyo ulitoa Maelezo Yako
Shahidi: Ndiyo
Malya: nimesikia Siku Unakutana na DCI Mlikutana baadae akaja Kingai
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Ulielezea Kwamba Kuna mtu Yoyote alikuja Kuwa Join Baadae
Shahidi: Kuwa Join Kwenye Nini
Malya: Kwenye Kikao cha Siku hiyo na DCI na Kingai
Shahidi: Hakuna Mtu yoyote alikuja Kutujoin Siku hiyo
Malya: Kwenye Meseji ya Mwisho ambayo Mbowe alikutumia, Ukasema Hukueleza, ni kwanimi hukutuma Meseji Nyingine Kuuliza Unamaana gani
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Baada ya Kupita Muda Hakuna Mawasiliano, Nilimuuliza Bwire Boss wako anajua, Sasa ningejibu Meseji ya Nini
Malya: Na ni UShahidi: Wako Kwamba Ofisi za Swila ni Ghorofa ya Nane Makao Makuu
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Mheshimiwa nafikiri Sina Swali la Ziada kwa Shahidi: huyu
Sasa anaingia wakili Dickson Matata:
Anasimama Wakili Dickson Matata:
Matata: Shahidi: nitakuuliza Maswali Machache naomba Ushirikiano Wako Kuokoa muda
Matata: Nikumbushe Ulionana na Mbowe Tarehe ngapi
Shahidi: Mwezi Wa Saba, 2020 Sikumbuki Tarehe gani
Matata: Na Ulipo Onana naye ndiyo alikwambia anahitaji Vijana Wa Kuambatana naye wa Kuchukua dola
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa Maelezo yako Ndiyo alikwambia anahitaji Vijana hao Vijana Kwa ajili ya Kumsaidia Kuwashambulia Viongozi ambao hawaupendi Upinzani
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Ndipo alipokwambia Kwamba anataka Kuhakikisha amachoma Masoko na Vituo Vya Mafuta
Shahidi: Naomba Nilifresh alisema Kwamba ataleta Taharuki Kwa Kufanya hayo Uliyo niambia
Matata: Majuzi Ulisema Kwamba Ulifanya Kitu kinaitwa Tactical appreciation, na Mimi Leo nataka tufanye Tactical appreciation ya Kisheria
Wakati anakwambia Mlikuwa Wawili
Shahidi: Ndiyo
Matata: Kwa Lugha Nyingine Hapakwepo na Watu wengine
Shahidi: Sahihi
Matata: tofauti na Siku hiyo, Kuna Siku yoyote aliwahi Kukwambia Jambo hilo au kukuandikia Barua
Shahidi: Hakuna
Matata: Kwa hiyo kwa Tafsiri Nyingine hatutopata UShahidi: Wa Maandishi au Wa Sauti au Meseji unaweza Kuthibitisha Kuwa alikwambia hayo Maneno
Shahidi: Hakuna Sauti.
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Baada ya Kukwambia Ukaona Inafaa ukatoe Taarifa, Ukaenda kwa DCI, Kwanza Ulimpigia Simu alafu akakupa appointment
Matata: Na Kwamba Baada ya Kumueleza akamuita Kingai
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Utakubaliana na Mimi Kwamba DCI ni Mtu Mwenye Ujuzi Katika Upelelezi
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kingai alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Unafahamu Kwamba anakuwa na uzoefu wa Upelelezi
Shahidi: Kwanza Nilikuwa sijui kuwa ni Mpelelezi
Matata: Mtu akiwa Mpelelezi Wa Mkoa anauzoefu au hana Uzoefu
Shahidi: anakuwa na Uzoefu
Matata: Wewe Kama Komamdo, Katika Kikao hicho na Baada ya Hapo, Hukuona wewe au DCI na Kingai, Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu kuwa Msiridhike Kile ambacho umesema, Je Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu Wa Kurekodi Voice Notes
Shahidi: Mamlaka labda Ndiyo haikuona Umuhimu,
Matata: Wewe Uliona Kuna Umuhimu au Hakuna Umuhimu, Kwamba Usiridhike na Maneno Utengeneze Voice Record
Shahidi: Niliona Kuna Umuhimu
Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita Sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko
Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudi
Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita Sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko
Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti
Matata: Mbowe akikataa Leo Hakusema, Ni UShahidi: gani Unao Mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe Alisema hayo Maneno
Shahidi: Ni UShahidi: Wa Meseji ya Kusema “Muda Umeisha”
Matata: hiyo Meseji inayosema Muda Umeisha Inasehemu Inasema Kulipua Masoko
Shahidi: Hakuna Mahali inasema
Matata: hiyo Meseji Inasehemu Inasema Kushambulia Viongozi ambao awapendi Upinzani
Shahidi: Hakuna Mahali inasema hivyo
Matata: Hiyo Meseji Kuna sehemu inasema Kulipua Vituo Vya Mafuta
Shahidi: Hakuna Mahali inasema hivyo
Matata: Tutoke hapo, Unasema Ulienda Kwa DCI na Kabla ya kwenda Ulimpigia Simu,
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulielezea Mahakama Kwamba Ulikuwa Unafahamiana na DCI
Shahidi: Nilieleza, Kuna Mtu aliuliza Kama Nilienda Ofisi ya DCI Mara ngapi
Matata: Sitaki Habari ya Kwenda Ofisini, DCI Anabadirika, nakuuliza Kama Ulielezea Kwamba Unafahamiana na DCI
Shahidi: Sikueleza
Matata: Ulieleza Mahakamani hapa Kwamba Namba Yake Ulipata Wapi
Shahidi: Sikueleza
Matata: Hata hiyo namba yenyewe Ulitaja
Shahidi: Sikutaja
Matata: UShahidi: gani Unathibitisha Kwamba Ulimpigia Simu
Shahidi: UShahidi: ninao kwa sababu nina namba zake na Nilifika Ofisini Kwake
Shahidi: Je ulivitaja hivyo Vitu Wakati Unahojiwa na Upande wa Mashitaka
Shahidi: Siku vitaja.
Matata: Unasema Kwamba Ulienda Kesho Ukasema Una Appointment naye Ukakutama na Secretary Wake
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa Maana hiyo Ulifuata Utaratibu wa Umma Wa Jinsi ya Kuingia Ofisi Fulani
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulisema Kwamba Ulipofika Ulifuata taratibu za Ofisi za Umma
Shahidi: Nilieleza Kwamba, Nilionyesha Kitambulisho kama Askari
Matata: Ulisema Kwamba Askari apaswi Kufuata Utaratibu Wa Kuingia Ofisi Za Umma
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mimi Nilieleza Kuwa ni Askari, yeye Ndiye alitakiwa aniambie Kufuata Utaratibu
Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, Ulisema Kwamba Nyie Askari hamfuati Utaratibu
Shahidi: Sikueleza
Matata: Ulileta Visitors Book Kuonyesha Kweli Ulienda Ofisi Za DCI
Shahidi: Hapana Siku leta
Matata: Shahidi Wewe ni Mwanajeshi, Ulitakiwa Kufuata Taratibu zote za Kijeshi
Shahidi: Ni sahihi.
Matata: Unapotoka Mkoa Mmoja Kwenda Mkoa Mwingine, unatakiwa Kuwa na Movement Order
Shahidi: Inategemea na Siku Ngapi, Kama Chini ya Siku Tatu unaweza Kwenda bila Movement Order kama zaidi ya Siku Nne Unatakiwa Kuwa na Movement Order
Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili Abdallah Chavula Ukiyasema hayo
Shahidi: Sikuyasema
Matata: Unapokuwa Askari Unapoenda Ofisi za Umma si lazima Uwe na Pass
Shahidi: Ni kwenye Kitabu Unachotaka,
Matata: si lazima uonyeshe Pass
Shahidi: Ndiyo ni lazima
Matata: Umeleta Mahakamani hapa Pass Kwamba Umeruhusiwa Kutoka kazini Kwako
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Sijaleta Sikujua I nahitajika Mahakamani.
Matata: Tarehe 11 ulienda kwa Inspector Swila na Tarehe 12 Ulimpelekea Simu
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulileta Mahakamani Hapa Pass za Umeruhusiwa
Shahidi: Siku leta, Sikupewa Maelezo
Matata: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 20
Matata: Naomba Nikuonyesha Kielelezo namba 20 ambacho Kina Mihamala yako ya namba ya Airtel
Matata: Jana Wakati a Unahojiwa ulisema Freeman Mbowe alikurushia Kwa Mara ya Kwanza TSh 500,000
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Ukatoa TSh 499,000
Shahidi: Kweli
Jaji Umeelewa Swali.? Anasema Umetumiwa TSh 500,000, Swali Ukatoa kwenye hiyo Fedha kiasi gani
Shahidi: Ni TSh 499,000
Matata: Kwa Mantiki Nyingine Hukutoa yote Kwa sababu Kuna Makato kidogo
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa hiyo Ulichukua TSh 500,000 Ukatoa TSh 499,000 Je Makato TSh ngapi
Shahidi: TSh 1000
Matata: Naomba Nikuonyesha Kwa Siku hiyo,
Mheshimiwa Jaji Namuonyesha Mhamala Wa Siku hiyo ambapo anasema alitoa Mhamala Wa TSh 499,000
Matata: Sasa Shahidi: angalia Tarehe 20 July 2020, Kwenye Mhamala sehemu ambayo Umeenda Kwa Wakala Ukatoa TSh 499,000
Jaji a nakuuliza Hapo Hapo hapo Kwenye hiyo Nyaraka
Shahidi: Hapa Kwenye Mhamala Haipo hiyo 499,000
Matata: Mheshimiwa Jaji naomba ni Muonyeshe Hapo hapo, Kuna. Majedwali ambayo Yana onyesha Receiver Balance kabla ya a kutumiwa TSh 500,000 kutoka Kwa Mbowe.
Utakubaliana na Mimi Kwenye akaunti yako palikuwa na TSh 49646
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Baada ya Kuweka TSh 500,000 balance Ikawa TSh 549,646
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Tarehe hiyo hiyo Ukatoa TSh 300,000
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Balance Yako Ikabakia 243,646
Ni sahihi
Matata: hebu chukua salio uliokuwa nalo la 549,646 Kutoa 300,000 ukabaki na 243,646 tuone Makato ni TSh ngapi
Wakili wa Serikali Robert Kidando: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Naona Hajajengewa Misingi Kwamba wakili anauliza ikiwa hayo Makato yapo au hayapo
Matata: Mheshimiwa Jaji Mimi Lengo langu nikutaka Kujua Kama kwanini atoe TSh 499,000 akatwe TSh 1000 na atoe TSh 300,000 akatwe Elfu Sita na.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hicho ndicho alichopaswa Kuulizwa
Matata: Je Shahidi: Utakubaliana na Mimi Kwamba Ukitoa TSh 300,000 ikibakia TSh 243,646 Je Elfu 6 inaenda Wapi
Shahidi: Siwezi Kujua Kama ni Makato au imeenda wapi..
Matata: Kwani hiyo Tsh 1000 Mwanzo Ulijuaje Kama ni Makato
Jaji Swali lako la Mwisho kinasema Je Kwani, Kuhusu Elfu 6 nimesharekodi
Wakili John Malya: anasaidiana Kufafanua Kidogo
Matata: Shahidi: Ulitoa Maelezo hii TSh 1000 Ilienda wapi
Shahidi: Sijawahi Kutoa
Matata: Shahidi: Sasa ulitoa…. Sorry Mheshimiwa Jaji Kidogo
Wakili Matata: anapekua Nyaraka
Matata: Shahidi: Umesema Freeman Aikael Mbowe alikuwa na Mpango Wa Kulipua Vituo Vya Mafuta, Je Wakati Unahojiwa ulitaja Majina ya Vituo Vya Mafuta
Shahidi: Hakuniambia Vituo Vya mafuta anavyoenda Kulipua Bali alitaja Mikoa tuh
Matata: Kwa hiyo ukiulizwa Alitaka Kulipua Vituo gani Morogoro hutakuwa na Majibu
Shahidi: Sitokuwa na Majibu
Matata: Tukisema Utaje Vituo Vya Mafuta alivyo taka Kulipua Mkoa wa Mwanza Utakuwa na Majibu au hutakuwa na Majibu
Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu atakuwa nayo Freeman Mbowe
Matata: Ukiulizwa pia Kuhusu Mkoa wa Dar es Salaam Vituo Vipi Vya Mafuta alitaka Kulipua
Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu anayo Freeman Mbowe, Mimi anilificha
Matata: Ukiulizwa ni eneo gani alipanga Kukata Miti kati ya Mkoa wa Morogoro na Iringa
Shahidi: Hakuniambia ni Eneo gani
Matata: Ukiulizwa Swali Kwamba, Ukiachana Na Sabaya ni Viongozi gani wengine Walipanga Kuwashambulia
Shahidi: Sikutaja Jina la Kiongozi Yoyote, Hakuniambia Kiongozi Yupi
Matata: Mpaka anakushirikisha bila Shaka alikuwa anakuamini
Shahidi: Ndiyo
Matata: Ukiachana na Swala la Kumtafutia Vijana, Je alikueleza Kuhusu Kumtafutia Vilipuzi
Shahidi: Hakunieleza
Matata: Kukwambia Kuhusu Kumtafutia Silaha za Kuwashambulia Viongozi
Shahidi: Hakunieleza
Matata: Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh
Matata: Naomba Kurudisha Kielelezo
Naomba Pia Kurudisha na Kielelezo Cha simu
Malya: Mheshimiwa Jaji Samahani, lakini hata hivyo haiwaki
Kibatala: Shahidi: Nikikuita baba kareem ni sawa.?
Shahidi: Ni sawa
Kibatala: Baba Junior
Shahidi: Ni Sawa
Kibatala: Baba Jackson
Shahidi: Nisawa
Kibatala: Jackson amezaliwa Lini
Shahidi: 17 December 2020
Kibatala: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali Ya Mkoa Morogoro
Kibatala: Nani na nani alikwepo
Shahidi: Mke wangu na Jirani
Kibatala: Wewe ni Mkristo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: nasali Kanisa lipi
Shahidi: Parokia Ya Ngerengere, Kigango cha Kizuka
Kibatala: Paroko wako Unamfahamu
Shahidi: Sikumbuki.
Kibatala: Kwani Kanisani Umeenda Mara ya Mwisho lini
Shahidi: Juzi juzi
Kibatala: Paroko anayehudumu Ngerengere Unamfahamu
Shahidi: Simfahamu
Kibatala: Katekista anaye Msadia Paroko
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: narudia tena Mara ya Mwisho Kanisani Umeenda Lini
Shahidi: Sikumbuki Kusema Kweli
Kibatala: Una Gari ya silver
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Aina gani
Shahidi: Rav 4
Kibatala: Namba zake zipi
Shahidi: T 114 DHL
Kibatala: Toka Mwaka 16 August 2020 hiyo Gari ipo Wapi
Shahidi: Kazini Kwangu Ngerengere
Kibatala: Toka Tarehe 16 August 2020 Gari hii ilikuwa parked Wapi
Shahidi: Nilikuwa natumia, Kila Nilipo ipo
Kibatala: Baada Tarehe 16 August 2020 Gari hii umeitumia
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Umekuja Kutoka Morogoro Kuja kwenye Kutoa UShahidi: Kwenye Hii Kesi , Na Kwamba Umetoka Moja kwa Moja Kuja Hapa na kwamba siyo Kutoka Kambi fulani ya Jeshi ulikokuwa umetekwa
Shahidi: Mheshimiwa Jaji.
Kibatala: Shahidi: Relax.
Wakili wa Serikali Robert KidandoMheshimiwa Jaji Mawakili Uliwakataza Kutoa Mawazo yao Bali Kuulizwa maswal
Kibatala: Shahidi: hiyo Gari Ipo wapi
Shahidi: Kambini Kizuka
Kibatala: Umepeleka lini hiyo Gari
Shahidi: Ijumaa Wiki Iliyopita
Kibatala: Utaratibu gani Umetumika kupark hiyo gari
Shahidi: Park at Your Own Risk
Kibatala: Kwa hiyo wewe Ka afisa wa Jeshi unataka Kuniambia Kuwa Unapark Gari at Owner’s Risk Kambini, Upo serious
Shahidi: Lipo Katika Parking ya Staff
Kibatala: Bado Kwamba Unaendelea Kusema Gari ipo Parking Owner’s Risk
Shahidi: Hapana Nimeliondoa jibu la Owner’s Risk
Kibatala: Jibu lako la. Kwanza kwamba Ulipark Chini ya Owner’s Risk Ulilitoa Chini ya Kiapo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: haya, Turudi tena Kwamba Gari Umeipark Kwa Utaratibu gan
Shahidi: Pale Hakuna Ku Register, Nilitoka Kwenye
Oparation Ni kaambiwa Nije
kutoa Ushahidi
Kibatala: hapo Maana yake ni Owner’s Risk
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: si Ndiyo umeliondoa hilo Jibu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Naiachia Mahakama Twende Eneo Lingine
Kibatala: Mwanzo Ulisema Ulikuwa unapanda Tax huna Gari
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Basi Ujue kwanini Nimekuuliza Kuhusu gar.
Kibatala: Shahidi: Fungua Yohana Sura ya 8, Mstari wa 31 Mpaka 39
Shahidi
aliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Abrahamu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wowote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. 37Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu. 38Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.
Yesu na Abrahamu
39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Abrahamu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu
Kibatala: Unafahamu Maan ya hilo Neno
Shahidi: Ndiyo Nafahamu
Kibatala: Maana yake ni nini
Shahidi: Tusiogope, Tuseme Kweli
Kibatala: Soma pia Waefeso Sura ya 4 Mstari Wa 25 Mpaka 32
Shahidi
Waefeso 4:25-32 BHN
Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo. Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima. Msimpe Ibilisi nafasi. Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini. Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu. Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni. Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu! Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.
Kibatala: Je unafahamu Maana ya hilo Neno
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Maama Yake ni nini
Shahidi: Tusiseme Uongo na Tupend.
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: lakini Ukaenda Kumshirikisha nani
Shahidi: DCI na Kingai
Kibatala: Mwingine Je.?
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Msemo wa Kwamba Askari awezi Kuwa Raia ila Raia anaweza Kuwa Askari Maan yake nini
Shahidi: Kwamba Ukishakuwa Askari Uwezi kuwa Raia, Ila Raia anaweza Kwenda kujifunza Kuwa Askari
Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Mnafundishwa Kuwa Jeshi la Polisi ni Jeshi Kweli au si Kweli
Shahidi: Kweli
Kibatala: Raia Akiona Uhalifu unatendeka anaweza Kuzuia Uhalifu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwamba Mwajeshi Akiona Uhalifu Unatendeka anaweza Kuzuia au anaacha utokee alafu anariport Taarifa Polisi
Shahidi: Anazuia Uhalifu
Kibatala: ila wewe Ulikuwa na Mbowe anakwambia Mambo ya Kigaidi ukamuacha
Shahidi: Ndiyo Maana Nilienda Kuriport Polisi
Kibatala: Kwani Jeshini si Kuna sehemu ya kwenda Kutoa Taarifa za Kihalifu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Kuna Kitengo Kina shughulika na Ugaidi
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kuna Jeshi la Navy ambalo kazi yao Ni Kushughulika na Ugaidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: na bado wewe ni Luteni wa Jeshi kabisa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwani kwa ufahamu wako wewe Jeshi halishirikiani na Jeshi la Polisi
Shahidi: Kama ikihitajika
Kibatala: Kwani Shahidi: Kwa Mfano Mbowe amgelipua Kituo cha Mafuta Puma pale Mwenge, Jeshi Pale Jirani Wamgedhurika au Wasingedhurika
Shahidi: Wangedhurika
Kibatala: Bado Ukaona Usiwaambie Jeshi
Kibatala: unasema Kwamba Mbowe alikwambia Kukata Miti wapi
Shahidi: Kukata Miti Kwenye Barabara zote zinazo ingia Mjini
Kibatala: Kwa Hiyo Unafahamu Kwamba Maisha ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya yapo Mikononi Mwako
Shahidi: Ndiyo najua
Kibatala: na Ulisema Kwamba Mara Ya Kwanza Ulikutana na Mbowe Lini
Shahidi: JULY 2020
Kibatala: Tarehe Ngapi
Shahidi: Sikumbuki ni Tarehe za Kati kati
Kibatala: zipi hizo
Shahidi: Tarehe 10 Mpaka 15
Kibatala: Hizo ndiyo Tarehe za Katikati
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: na wewe ni. Luten wa Jeshi la Wananchi Tanzania tunaolipemda wote
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Elimu yako ni Form Four
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulipata Divisheni Ngapi
Shahidi: Three ya Point 25
Kibatala: unajua Division Four Inaanza point ngapi
Shahidi: Point 28 ila Sikumbuki Vizuri
Kibatala: Kwa hiyo Unakumbuka au Ukumbuki
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Umesoma wapi.?
Shahidi: King’ori Sekondari
Kibatala: Headmaster Wako ni nani
Shahidi: Simkumbuki
Kibatala: Graduation Mlifanya lini
Shahidi: Hatukufanya Graduation
Kibatala: Ukimaliza Form Four lini
Shahidi: Mwaka 1999
Kibatala: Yule Mchungaji Wako anayefundisha Mzumbe Mara ya Mwisho Kuwasiliana naye ni Lini
Shahidi: Sina Mchungaji
Kibatala: Na Nabii Tito anayefundisha Mzumbe Umeacha Kusali Kwake lini
Shahidi: Simfahamu
Kibatala: Habari Nzito ya Mbowe Ulimshirikisha Paroko au Mchungaji
Shahidi: Sikumshirikisha Mtu
Kibatala: lakini Ulishindwa kulala.
Kibatala: pale Kambi ya Jeshi Lugalo Kuna Barabara ya Kuingia Mjini au Hakuna
Shahidi: Ipo
Kibatala: Kama Wangekata Miti pale Barabara ya Lugalo Jeshi lingedhurika au lisingedhurika
Shahidi: Lingedhurika
Kibatala: Lakini Bado wewe Ukaona Usiwaambie Jeshi
Shahidi: Nilipeleka Taarifa Polisi Kwa sababu wao Wana husika na Uchunguzi
Kibatala: Kati ya Wewe Ulipo pale Mgulani Kambini na Ofisi za DCI, Wapi Ilikuwa Rahisi Kwako Kuriport
Shahidi: Kambini Mgulani
Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa Logic na Common sense
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: haya pale kwa DCI umesema Kwamba Kuna Scanner, Umejitambulisha Kuwa wewe ni Luteni na ukafanyeje
Shahidi: Nikatoa Kitambulisho
Kibatala: Baada ya Pale Ulimwambia Jaji Kwamba Jina lako liliingizwa Kwenye Register
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba sisi tumefika Kwa DCI Mara ngapi
Shahidi: Hapa Sijui
Kibatala: Nikikukwambia Kwamba pale kwa DCI Nilifika Kimsindikiza Lowasa Mwaka 2017
Shahidi: Ndiyo nitakubali
Kibatala: Unafahamu Kuwa DCI ni Mwanajeshi
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Kuna Mtu alipiga Simu Kwanza Kuhakiki appointment Yako
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba Wanajeshi hasa DCI ambaye ndiye Kama. WAZIRI Mkuu wa Jeshi la Polisi ni watu wa tahadhari kwa sababu ni Watu naodili na Uhalifu Nchi Nzima
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Umemwambia Jaji Kwamba Kuna Kitambulisho Ulipewa cha Kuvaa
Shahidi: Si kumwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwa DCI Kuna Askari Kwa ajili ya Kimsindikiza Wanaenda Kwa DCI
Shahidi: Sikumwambia Jaji
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Askari Wa Kukusindikoza Mpaka Kwa PS wa DCI
Shahidi: Si kumwambia
Kibatala: Waiting Area ya Ofisi za DCI Makochi ni Rangi gani
Shahidi: Ya Brown
Kibatala: Unauhakika Kwamba Siyo Mekundu
Kibatala: Ukifika kwenye Ofisi za DCI PS anakuwa Upande Upi
Shahidi: Upande huu, (anaonyesha Kushoto)
Kibatala: Umebadilsha Sasa hivi.
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: lakini Ukaenda Kumshirikisha nani
Shahidi: DCI na Kingai
Kibatala: Mwingine Je.?
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Msemo wa Kwamba Askari awezi Kuwa Raia ila Raia anaweza Kuwa Askari Maan yake nini
Shahidi: Kwamba Ukishakuwa Askari Uwezi kuwa Raia, Ila Raia anaweza Kwenda kujifunza Kuwa Askari
Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Mnafundishwa Kuwa Jeshi la Polisi ni Jeshi Kweli au si Kweli
Shahidi: Kweli
Kibatala: Raia Akiona Uhalifu unatendeka anaweza Kuzuia Uhalifu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwamba Mwajeshi Akiona Uhalifu Unatendeka anaweza Kuzuia au anaacha utokee alafu anariport Taarifa Polisi
Shahidi: Anazuia Uhalifu
Kibatala: ila wewe Ulikuwa na Mbowe anakwambia Mambo ya Kigaidi ukamuacha
Shahidi: Ndiyo Maana Nilienda Kuriport Polisi
Kibatala: Kwani Jeshini si Kuna sehemu ya kwenda Kutoa Taarifa za Kihalifu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Kuna Kitengo Kina shughulika na Ugaidi
Shahidi: Hapana.
Kibatala: Kuna Jeshi la Navy ambalo kazi yao Ni Kushughulika na Ugaidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: na bado wewe ni Luteni wa Jeshi kabisa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwani kwa ufahamu wako wewe Jeshi halishirikiani na Jeshi la Polisi
Shahidi: Kama ikihitajika
Kibatala: Kwani Shahidi: Kwa Mfano Mbowe amgelipua Kituo cha Mafuta Puma pale Mwenge, Jeshi Pale Jirani Wamgedhurika au Wasingedhurika
Shahidi: Wangedhurika
Kibatala: Bado Ukaona Usiwaambie Jeshi
Kibatala: unasema Kwamba Mbowe alikwambia Kukata Miti wapi
Shahidi: Kukata Miti Kwenye Barabara zote zinazo ingia Mjini
[1/28, 1:03 PM] Cdm Lucy ShayoKibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba niilipokuwa Ulipokuwa wait Area Kwa DCI iwapo Body Guard Wake Ukiwa Una subiri Kuingia
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Jana wakati wa UShahidi: Ulizungumzia Meza na Viti, Je Ulizungumzia DCI kuwa Ni Mnene, Mfupi, Mwembamba au Lah
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ukaona ni Muhimu tufahamu Viti na Meza na siyo DCI ambaye Ulimfuata
Shahidi: DCI SI anajulikana
Kibatala: anajulikana na nani
Shahidi: na Watanzania wote
Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba Utaratibu gani Ulitumia Kutoka
Shahidi: Sija Mwambia
Kibatala: Ulimwambia Jaji Kuwa Ulipokuwa Unatoka Ulisaini Out
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unasema Ulifika Ofisi ya DCI Saa ngapi
Shahidi: Nimefika Majira ya Saa Mbili au Saa Tatu
Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Huo Ndiyo Muda wa Kufika DCI
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Kwamba Chini ya Kiapo hapo Luteni Kwamba Siku hiyo DCI alipanda Ngazi Kwa Mguu Mpaka Ghorofa Ya Saba
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kwa hiyo ufahamu Kwamba DCI alikuwa na Umri Miaka zaidi ya 50 na Sasa amestaafu Kwamba alipanda Ngazi
Shahidi: Sifahamu alifika Je Juu
Kibatala: kwa hiyo Wewe Unasema Kwamba Jeshi la Polisi Kwa DCI Kiongozi Wao Kama. Waziri Mkuu, Kuwa Lift yake Ilikuwabovu
Shahidi: Hapana Sifahamu
Kibatala: Jana Ulionyeshwa Simu zako, na Moja ilikuwa na Display ya Mke Wako
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Wakati Simu zako zote Nne Umepewa, Je Ni wakati gani Uliomba nafasi ya Kungalia Simu yako Namba ya Kingai Kama. Kweli uliwasiliana naye
Shahidi: Hapana Siku Mwambia jaji
Kibatala: Je Kwa DCI pia Ilimuomba Jaji nafasi ya Kungalia namba ya DCI Kwenye Simu yako
Shahidi: Hapana
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sasa Ni saa Saba Kamili, Kama Wenzetu wataridhia Twende Health Break na naomba Niependekeza Kwako Dakika 45
Wakili wa Serikali Robert Kidand: oMheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi
Jaji: Kwa Maana hiyo tutabreak Kwa Muda wa Dakika 45 na Saa Saba na Dakika 45 tutarudi
Jaji anatoka Mahakamani
Jaji Amerejea mahakamani muda huu saa 8 na dakika 8
Kibatala: Unafahamu Kwamba Utambulisho Wa su Moja dhidi ya Nyingine ni IMEI, Je unafahamu
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Wakati Unaongozwa na Mawakili Wenzetu wa MSomi walikuongoza Kutoa Nyaraka fulani hivi?
Shahidi: Ndiyo Nakumbuka
Kibatala: Kwahiyo Nyaraka Ile Ilikuwa ni Kuthibitisha Kuwa palikuwa na Makabidhiano kati yako wewe na Inspector Swila?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Inaitwa Techno nini Vile?
Shahidi: Techno CAMMO
Kibatala: Niambie Kama wakati Unaonyeshwa Simu zako zote Nne, Je ulitambua Simu Moja Moja Kwa kutumia IMEI namba?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kwa hiyo Ka tuna Simu Nne, Tatu hukuzitambua kwa IMEI namba ya Simu Moja Moja Nilitambua Moja tuh?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatalakwa hiyo hii Techno CAMMO ulitambua Kwa IMEI namba
ShahidiNdio
Kibatal: Kwa UShahidi: Wako wote hapa umesema Kwamba Unaishi Ngerengere, Je Kuna sehemu Umesema Kwamba unaishi kihonda?
Shahidi: Nilisema Nina makazi mawili ngerengere na Kihonda
Kibatala: Je Ulisema Jana na Leo Kabla Sijakuuliza?
Shahidi: Sikusema
KibatalaJe Kuna Mahala Popote Ulitambua Maneno CAMMO Kama Yapo?
ShahidiHakuna
KibatalaKuna Maneno gani badala yake?
ShahidiTechno tuh
KibatalaJe Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji Kwamba hiyo Techno ndiyo
Techno CAMMO?
ShahidiSiku fafanua
KibatalaWakati Wa UShahidi: Wako Wote Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula, Kama Uliongozwa na kutoa Betri na Kusoma IMEI namba na Kumwambia Mheshimiwa Jaji Kama IMEI zinafafana na Inspector Swila Wakati wa Makabidhiano?
ShahidiSikumwambia
KibatalaSoma Hapa Pameandikwa Kwamba wewe Luteni Urio unaishi Wapi?
ShahidiKihonda
KibatalaJe Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwenye Kielelezo Kuwa wewe Luteni Urio Unaishi Kihonda
Shahidi: Anatingisha Kichwa
Kibatala: Hapa Mahakamani, Usijibu kwa Kichwa
Shahidi: Sikumwambia Mheshimiwa Jaji
Kibatala: Soma hapa
Shahidi: CD/IR /2097 /2020
Kibatala: Ni nini hiyo
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je Ulifafanua ni nini hicho
Shahidi: Siku fafanua
Kibatala: Kuna IMEI namba Ngapi hapo
Shahidi: ameshuka Kielelezo Cha Karatasi Moja anatetemeka Balaaaa
Shahidi: Sijui ni IMEI namba ngapi
Kibatala: Unafahamu Inspector Swila alikozitoa hizi IMEI namba au Ufahamu
Shahidi: Kwenye Simu yangu
Kibatala: Je Zipo ngapi hizo IMEI namba zipo ngapi
Shahidi: Sifaham
Kibatala: Hiyo ni Standard Form Document
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Soma Hapo Chini
Shahidi: Jina na Sahihi ya anayekabidhiwa
Kibatala: Wakati unatoa UShahidi: Jana Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba hiyo ni sahihi yako
Shahidi: Niliwambia.
Kibatala: Soma Hapo Chini ya Mstari Uliochapwa
Shahidi: 11 August 2020 Imeandaliwa Chini ya
Kibatala: ulifafanua Kuwa Kwanini hayo Maelezo Yapo Chini ya Nyaraka
Shahidi: Siku fafanua
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Nyaraka hii inasema Mimi Luteni Denis Urio Wa Kihonda Morogoro, Na mkabidhi Vitu ambavyo Vimekamatiwa Tarehe Deshi, Kutoka Kwa Mtuhumiwa Deshi, Vitu aina ya Deshi
Kibatala: Sasa Kwa UShahidi: Wako wewe Tukiangalia hapo Kwenye Deshi tunaweza Kujua ni nini
ahidi Sijui ni nini
Kibatala: Mkumbushe Mheshimiwa Jaji Ulisema Simu yako wewe Ulikabidhi sababu ya
Shahidi: Uchunguzi
Kibatala: ambapo Wewe Unaamini ilikuwa Mawasiliano ya wewe na nani
Shahidi: Mheshimiwa Mbowe
Kibatala: Tuache Simu, Turudi Ofisini Kwa DCI
Kibatala: Lengo la Kutaja Meza na Viti Kwa DCI Lengo ilikuwa Kuonyesha Kwamba Ulifika kwa DCI, Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Ulimwambia kuwa Meza ni ya Rangi gani
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Kwakuwa Lengo lako lilikuwa Kuonyesha Unaifahamu Ofisini ya DCI Je Ulisema Juu Palikuwa na nakshi gani
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Kwakuwa Lengo lako lilikuwa Kuonyesha Unaifahamu Ofisini ya DCI Je Ulisema Juu ya Rangi ya Viti
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Je Umwambia Jaji Details zingine Kuhusu ile Ofisi
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Kama Ofisi Ya DCI Kuna Bendera ya Taifa
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Sasa Ulimwambia Detail hiyo Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba Ofisini Kwa DCI kuwa Kuna Picha ambazo zinaonyesha Matukio Mbalimbali ya Utejelezaji Wa Majukumu Yake
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusu hilo
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ofisini Kwa DCI Kuna kalenda zaidi ya Tatu
Shahidi: Niliona Moja
Kibatala: Ulimwambia Kuhusu hiyo Kalenda Moja
Shahidi: Sikumwambia, na pembeni ya Kiti Chake Pia Kuna Kiti Kingine pia Sikumwambia Mheshimiwa Jaji
Mahakama Kichekoooooo
Kibatala: Asante kwa Taarifa
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Ofisini Kuwa Kuna Beseni la Kunawa Mikono
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ofisini Kwa DCI palikuwa na Askari Wangapi Wa zamu
Shahidi: Walikuwa wawili Ila Sikumwambia
Kibatala: Kwamba Pale Reception Kuna Magari ya ya Viongozi Mazuri Mazuri, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Pale Nje Kuna Gari ya Rapid Response, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Umeliona
Shahidi: Sikumwambia, Ila siku hiyo halikuwepo
Kibatala: Unakumbuka Juu ya somo letu la TRUTH SHALL SET YOU FREE
Shahidi: Ndiyo nalikumbuka
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwanini ulishindwa Kuweka Mheshimiwa Mbowe Chini ya Ulinzi
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Ni nini cha Ziada Kilicho ongezeka kutoka Tarehe July 2020 Mpaka Leo hapa Mahakamani
Shahidi: Tuna Amani tuh Tanzania
Kibatala: Tarehe Katikati ya July 2020, Toka Kipindi Kile Mpaka Leo ni zaidi Ya Mwaka sasa, Je Kuna Kitu cha Ziada ambacho wewe Binafsi Moyoni Mwako ulipata Taarifa ya ziada
Wakili wa Serikali Robert KidandoMheshimiwa Jaji Swali hilo lime Ulizwa na kujibiwa Amani
Kibatala: Twende Eneo Lingine, Unasema Baada ya Kupata Taarifa hizo za Freeman Mbowe Kupanga Uhalifu, Bado Unasa Ukumbuki Tarehe
Kibatala: Swila anasa Kwamba alifungua Faili lake Tarehe 18 July 2020, Je Unaweza Kukumbuka Siku Uliyo enda Kwa DCI
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: sisi shida yetu ilikuwa ni Kutaka Kujua Kama Ulifika kwa DCI lini . Tujue kuwa Faili lilitungwa au lah
Shahidi: Siwezi Kukumbuka Tarehe.
Shahidi: Siwezi Kumsemea
Kibatala: Je Unakumbuka Tarehe Uliyokutana na Khalfani Bwire
Shahidi: Sikumbuki ila ilikuwa Mwenzi Wa Saba
Kibatala: Je Khalfani Bwire Uliwasiliana naye lini akiwa Tunduma
Shahidi: Sikumbuki ila Katikakati ya Mwezi Wa saba
Kibatala: Na Adam Kasekwa Uliwasiliana naye lini
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Kwa Mujibu Wa Mohammed Ling’wenya katika Maelezo Yake anasema Kwamba Tarehe 24 July 2020 Mkakutana Morogoro
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Si Siku Sita Tangu Inspector Swila aseme alifungua Faili Tarehe 18
Shahidi: Sijui
Kibatala: Si Ipihe Hesabu Kutoka Tarehe 18 July 2020 Mpaka 24 July 2020 ni Siku ngapi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Umeanza Kuwakusanya hawa baada ya Tarehe 20 July 2020
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Nawewe ndiyo Ulikuwa Unawafahu hawa wala Siyo Mbowe
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unaweza Ku tuisaidia Kuwa Kwanini Inspector Swila alifungua Faili la Kula Njama Tarehe 18 July 2020 Wakati Wakati Umekutana hawa Vijana Tarehe 20 Mpaka 24
Shahidi: Sijui sasa
Kibatala: Je wewe Ulikula Nja ma na Mbowe
Shahidi: Sijala Njama na Mbowe
Kibatala: Kwani Shahidi: Swala hili Kuna Mtu Zaidi Yako alienda Kutoa Taarifa Kwa DCI
Shahidi: Ni Mimi Peke Yangu ndiye niliye Mwambia DCI
Kibatala: Kwani wewe Ulimueleza Jaji Kwamba Mbowe alikuwa tayari anavijana Wengine
Shahidi: Sikumwambia Mheshimiwa Jaji
Kibatala: Baada ya Kutoka Kwa DCI ulienda Wapi
Shahidi: Morogoro
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulitumia Usafiri gani Kurudi Morogoro
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Baada ya Kutoka Kwa DCI Ulifika Nyumbani Kwako Usiku
Shahidi: Nilifika Jioni Jioni
Kibatala: Tuambie nani alikwepo Nyumbani Kwako ulimkuta Siku hiyo
Shahidi: Mke wangu
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba alikwepo Mtoto wako Careen Nyumbani kwako
Shahidi: alikwepo Mke wangu na Watoto
Kibatala: Inabdilisja Enheeeee
Kibatala: haya Ulitumia Basi gani Kurudi Morogoro
Shahidi: Abood bus Service
Kibatala: Je Unayo ticket
Shahidi: Hapana
Kibatalaimi na Malya: tunafahamu CASA Motel, na Kila Gari Inayoingia pale inasajiliwa
Shahidi: Sijui
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Gari yako Tax ile Ilisajiliwa pale Mlangoni
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba CASA Motel ni Nyumba ya Chini au Ghorofa
Shahidi: Ni Ghorofa
Kibatala: Ndiyo hiyo si Taarifa Muhimu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji sasa
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba mlilaa sehemu gani, Nje au Ndani
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba mlilaa kwenye Makochi ya namna gani
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ni UShahidi: Wako Kuwa Mbowe Mwenyekiti Wa Chadema Taifa, alikuwa CASA Motel Bila Dereva wala Mlinzi
Shahidi: Nilisema Kuwa Alitupokea Kijana Mmoja akasema Chairman Yule Pale
Kibatala: Sasa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba aliyekuwa anaye wahudumia ni Mwanamke au Mwanamme
Shahidi: Hapa Sikumwambia
Kibatala: Je wewe Luteni Wa Jeshi Moja ya ulichojifunza ni Kufanya kazi Katika High Pressure, Si Ndiyo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Moja ya Ulichojifunza ni Kuongeza umakini
Shahidi: Ndiyo.
Kibatala: Sasa Afisa wa Jeshi la Wananchi ambalo Miye Nimeamza Kulisoma tangu Wakati wa Willy Gamba , Luteni Unaitwa sehemu na Mtu ambaye umfahamu unaenda tuh
Shahidi: Nilikuwa Nasikia Kwenye Tv
Kibatala: Kwani Mtu akakupigia yeye ni Peter Kibatala: akakuita Goba Unakuja tuh
Shahidi: alikuwa a nawasiliana na Mimi Siku Nyingi
Kibatala: Ulipokuwa Pale Kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe, Nani alilipa Chakula
Shahidi: Freeman Mbowe
Kibatala: Nani alilipa Tax Yako
Shahidi: Freeman Mbowe
Kibatala: kwa hiyo Pamoja na Kukwambia Taarifa za Ugaidi bado Ukapokea Fadhila zake
Shahidi: Siyo Taarifa za Ugaidi, Ni Uhalifu tuh
Kibatala: Kwa hiyo Baada ya Kukwambia Mipango hiyo ya Uhalifu, Bado alilipia Tax Yako
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Wewe Kama Luten wa Jeshi, Ulimwambia Mtu yoyote Kuhusu Swala hilo
Shahidi: Nilimwambia CEO wangu
Kibatala: Ulimwambia lini
Shahidi: Tarehe 05 August 2020
Kibatala: hayo Mambo Uliyo enda Kumwambia CEO wako, Yapo Katika Maelezo Yako Uliyo andika Kwa Inspector Swila
Shahidi: Hayapo Katika Maelezo yangu
Kibatala: hayo Unayosema Kwamba Ulienda Kuriport Kwa CEO wako, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Sikumbuki Kama nilimwambia
Shahidi: No Sikumbuki nilitamka Kwenye situation gani.
Kibatala: Mlikaa na Mbowe pale CASA Motel akakwambia Maswala Kadhaa wa Kadhaa
Shahidi: CASA Motel Siyo Wakati wa hiyo Mipango, CASA Motel ni Wakati wa 2012
Kibatala: Baada ya Kujua Mbowe anamipango ya Kigaidi Uliendelea Kuwasiliana naye
Shahidi: Ndiyo nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye ili Kumtafutia Watu wa Kwenda Kutekeleza Mipango yake
Kibatala: Ni kweli Kwamba Ulishiriki Mipango ya Kigaidi
Shahidi: Sikushiriki
Kibatala: Nani aliyemuwezesha Mbowe Kupata hao Vijana Kutekeleza Mipango ya Kigaidi
Shahidi: Ni Mimi
Kibatala: Shahidi: Wewe ni Afisa Wa Jeshi, Je Unafahamu Sheria yoyote Inayoruhusu wewe Kutafuta Vijana Kutekeleza Mipango ya Kigaidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Wewe si Ulikuwa Darfur
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kilichokufanya Mpaka Muende Darfur ni Janja Weed na SPLM
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Ingewezekana Wewe Askari Umeenda Darfur Chini ya Chapter Seven Ukawa Unafanya Mawasiliano ya Simu na Kiongozi wa Janja Weed.?
Shahidi: Nisingeeleweka.
Kibatala: Ni Kwa Sababu Yule alikuwa Mhalifu wa Amani
Shahidi: Ndiyo alikuwa Mhalifu Wa Amani
Kibatala: lakini huku Tanzania ulikuwa Unawasiliana na Freeman Mbowe
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Je Kule Darfur Ungemuita Kiongozi Wa Janja Weed Bro Ungeeleweka
Shahidi: Nisingeeleweka
Kibatala: Kwani Kule Darfur Si palikuwa na Askari Wengine Wa Chapter Six Wanaofanya Peace Keeping wapo armed na wanafanya Demining
Shahidi: Sijui
Kibatala: na Kwamba Wewe Kabla ya Tarehe 05 August 2020 Hakuna Uliyekuwa Umempa Taarifa Ndani ya Jeshi Kuwa Umepewa Kazi na DCI na Kingai
Shahidi: Sikumwambia Mtu
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba huyo Dogo Adam Kasekwa anajina lingine anaitwa Adamoo
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mohammed Ling’wenya anajina Lingine anaitwa DOYI
Shahidi: Siku Mwambia
Kibatala: Unafahamu Moses Lijenje Yupo wapi
Shahidi: Nilimkabidhi Kwa Freeman Mbowe
Kibatala: Moses Lijenje Yupo Hai au amekufa
Shahidi: Nilimkabidhi Freeman Mbowe
Kibatala: ulimkabidhi Wapi
Shahidi: Nilimpigia Simu akasema Kwamba ameshafika
Kibatala: Nikuonyesha Meseji zako Uyanionyesha sehemu ambayo inameseji Kuwa Mbowe anasema Umemkabidhi
Shahidi: Hakuna
Alinipigia Simu
Kibatala: Jana Ulionyeshwa Sauti zako za Kukabidhiama Kwa Mbowe Moses Lijenje
Shahidi: Hapana
Kibatala: Wewe Mpaka Unaonana na Moses Lijenje, alikuwa anafahamu Maswala ya Ugaidi
Shahidi: Hapana, Maswala ya Ulinzi
Kibatala: Wewe Ulionana Lini tena na Moses Lijenje Baada ya Tarehe 21 August 2020
Shahidi: Sikuonana naye tena
Kibatala: Walicho ongea Na Mbowe Huko Hai au Popote unakifahamu
Shahidi: Sikifahamu
Kibatala: Unaweza Kuonyesha Chochote Kile au Sauti Ukionyeshwa kwa Mheshimiwa Jaji Kwamba Freeman Mbowe alimwambia Lijenje Wakafanye Ugaidi
Shahidi: Sijawahi Kusiki.
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Hakuna Pesa iliyotoka Moja Kwa Moja kutoka kwa Mbowe Kwenda Kwa Moses Lijenje
Shahidi: Hakuna
Kibatala: badala yake Shahidi: Unasema Mbowe alituma Laki Tano ambayo Uliingia Kwenye Simu yako, alafu wewe Ukatoa ya kwako Mfukoni
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu Jinsi Fedha inavyotakatishwa
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ile Fedha ulimpa Moses Lijenje, ilikuwa ya Kwako Mfukoni au ulitoa Kwenye Simu Ukampa
Shahidi: Nilitoa Pesa Mfukoni Kwangu
Kibatala: Nakuuliza tena, Kuna Pesa unazo Mfukoni Mwako, na Mbowe katima. Pesa za Kwenye Simu
Je pesa uliyompa Moses Lijenje, ulitoa Kwa Wakala Ukampa au Ulitoa za Kwako Mfukoni
Shahidi: Nilitoa Laki 3 kwenye Mhamala, Nika Changanya na za Kwangu Mfukoni
Kibatala: Unasema Kwamba Moses Lijenje Ulikutana naye Morogoro Tarehe ngapi
Shahidi: Tarehe 21 August 2020
Kibatala: na hiyo Fedha Ulipokea Lini Kwenye Mhamala
Shahidi: Tarehe 20 August 2020
Kibatala: Na hiyo 500,000 ulipokea Kutoka Mbowe Moja kwa Moja.?
Shahidi: Hapana Kwa Wakala
Kibatala: Wewe Ulitumiwa TSh ngapi
Shahidi: 500,000
Kibatala: Kwa Wakala Ulitoa TSh Ngapi
Shahidi: TSh 300,000, na Mfukoni nilikuwa na 199,000
Kibatala: Lijenje na Khalfani Bwire Uliwapa TSh ngapi
Shahidi: Niliwapa hiyo Tsh 300,000, Wagawane
Kibatala: Ile Laki 499,000 sasa Ilitoka Wapi
Shahidi: Siwezi Kutoa Pesa yote, Nilikata TSh 1000 la. Makato
Kibatala: Kwa hiyo Wewe Ulimkata Mbowe TSh 1000 katika ile TSh 500,000
Shahidi: Ndiyo Mbowe alikatwa Juu Kwa Juu, TSh 1000 nilijikata Mimi
Kibatala: Ulijikata wewe Kwa Sababu ipi
Shahidi: Ilienda Katika Deposit Ya Kampuni.
Kibatala: Kwa hiyo Ile TSh 1000 Ujui Imeenda Wapi
Jaji Kuna sehemu Mnashindwa Kuelewana, Wewe Ulitumiwa TSh 500,000, Ukaenda Kutoa 300,000, na Mfukoni Kwako Ukatoa 199,000
Anzieni hapo
Kibatala: Swali langu hiyo 499,000 Imetoka Wapi, ambayo Ulimwambia Malya: Ni Ip
Shahidi: Na assume Kuwa ile Laki Tano haiwezi Kutoka Yote, Laki 3 nilitoa Kwa sababu Nilikuwa na Balance Yangu
Kibatala: Kwakuwa Mfukoni Kwako Ulikuwa na Laki 2 ni nani aliye Kata TSh 1000, Ni wewe au Wakala
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ile Laki 2 Iliyobakia katika Simu yako Ulitoa lini.?
Shahidi: Ni Wakala
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Nipewe Kielelezo namba 20
Shahidi: Nilitoa Walipo Kuja…… Sikumbuki
Wakili Tafuta Ile Laki Mbili ambayo ikibakia katika Su yako Ulitoa Tarehe Ngapi, Ukipata we tuambie
Shahidi ANATATUTA (Yupo Dirishani, Jua lina Mpiga Kwa Mgongoni, Shahidi: Natoka Jasho Sana).
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Shahidi: ile Nyaraka siyo yake, na Shahidi: hajajengewa uwezo Wa Kusoma Ile Nyaraka, Kuokoa Muda, Shahidi: aelekezwe Maeneo hayo wakil
Kibatala: Sawa Fair enough, Wacha Twende Kwa namna Nyingine
Kibatala: Shahidi Kwani Wewe Unakumbuka ulitoa lini hiyo pesa
Kibatala: anamfuata Shahidi, Na Kumueleza Kwenye Nyaraka ya Airtel, Ili Kuokoa muda
Shahidi anatuta tena
Shahidi: Kuna Laki Mbili na Nusu
Kibatala: Miye Nimekuuliza Laki Mbili
Shahidi: Laki 2 Hakuna
Kibatala: Baadae Unasema Freeman alikutumia Laki 2 na Tisini na Tisa Je Ilikuwa Tarehe Ngapi
Shahidi: Ilikuwa Tarehe 22 july 2020
Kibatala: Namba Iliyo Ingiza ni 0780900244
Hiyo namba ya nani
Shahidi: Sijui ya nani
Kibatala: Siyo namba ya Mbowe
Shahidi: Siyo Namba ya Mbowe
Kibatala: pesa Uliyompatia Ling’wenya na Adamoo ulitoa Mfukoni na yenyewe au Ulitoa kwa Wakala
Shahidi: Nilitoa Kwa Wakala
Kibatala: Ulitoa TSh Ngapi
Shahidi: TSh 170, 000
Kibatala: Tafuta Tarehe 24 July 2020 Mahala ambapo unasa Ulitoa TSh 170,000
Shahidi: Haipo Katika Kielelezo Namba 20
Kibatala: lakini wewe Unasisitiza ulitoa Kwa Wakala
Shahidi: Ndiyo Kwa sababu nilitoa Kwa Serial Namba
Kibatala: Lakini Haipo Katika Kielelezo namba 20.
Kibatala: Hiyo namba hapo 0782 237913 ni Namba ya nani
Shahidi: Siwezi Kukumbuka Mpaka niangalie Kwenye Note Book
Kibatala: Hiyo Notebook ipo wapi
Shahidi: Hotelini Kwangu
Kibatala: Hotel Yako Inaitwa Je Vile
Jaji Kuna ulazima Wa Kutaja Hotel aliyofikia.
Kibatala: Ndiyo Kwasababu Tangu Mwanzo Case Theory Yetu ni Kwamba Hatokei Nyumbani Wala Hotelini sababu amewekwa sehemu
jajiNdiyo Nauliza Kuna Ulazima Wa Kutaja Hotel ambayo anatoka Kuja Kutoa Ushahidi
Kibatala: Sawa Mheshimiwa Jaji acha niendelee
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Huo Mhamala unafahamu
Shahidi: Ndiyo lakini Sikumbuki
Kibatala: Hiyo namba Iliyotuma ni Ya Kwako
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Namba Unaye Mtumia Unaifahamu
Shahidi: Sifaham.
Kibatala: DCI alikwambia Umwambie Kingai Kila Kitu au Vingine Umfiche
Shahidi: Ni Mwambie Vyote
Kibatala: Taarifa Muhimu Ka hizo kwanini Hukumwambia Kingai
Shahidi: Taarifa za Muhimu Nilimwambia Kingai
Kibatala: Tarehe 11 August 2020 Ulikutana na Inspector Swila
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Jeshini Kule Kuna Mtu yoyote Ulimwambia Kuwa Bwire ame Confess
Shahidi: Sikumwambia Mtu , Sababu siyo Mahala Sahihi.
Kibatala: Kwa hiyo wewe ulimruhusu Bwire Waendelee na Mipango yao, Mipango ipi
Shahidi: Waendelee na Mipango yao ya Kumdhuru Sabaya, Kama Wakiweza
Kibatala: kwa hiyo Baada ya Kumdhuru Sabaya Walitakiwa Kuriport Kwako tena
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Kingai alikwambia Kuwa Bwire amekamatwa
Shahidi: Hakuniambia
Kibatala: Je Maelezo yako si Uliandika Tarehe 12 August 2020
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Katika Maelezo Yako Uliandika Kwamba Bwire Ali Confess
Kibatala: Mimi bado nipo Tarehe 11 na Tarehe 12 August 2020
Kibatala: Wakili alikwambia Wakatinakabidhiana Simu mlisainiana Makaratasi Ma ngapi
Shahidi: Makaratasi Manne
Kibatala: Jana Ulitoa Makaratasi Mangapi.
Shahidi: Nilitoa Karatasi Moja
Kibatala: Ulitoa Ufafanuzi Kuhusu Makaratasi Matatu
Shahidi: Siku toa kwa sababu Sikupewa
Kibatala: hukupewa na nani
Shahidi: Na Wakili ambaye alikuwa akiniongoza
Kibatala: Unakumbuka ulikuwa Unafanya Mawasiliano na Simu ipi Mara kwa Mara kwa Mara
Shahidi: Kwa Samsung ya Torch
Kibatala: Hiyo Samsung ya Torch ndiyo Sumsumg Duo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kuna Mahala Popote ambapo Umefafanua kwa Jaji Kuwa hiyo Samsung Duo
Shahidi: Hapana
Kibatala: Mara ya Mwisho Kufanya Mawasiliano na Kingai Ulifanya Mara ya Mwisho ni lini
Shahidi: 10 August 2020
Kibatala: Nikukuombea Upewe Samsung DUO utaweza Kuonyesha Call Record zako na Kingai
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Namba ya Kingai Unaifahamu
Shahidi: Mpaka Nisome Kwenye Notebook Yangu
Kibatala: Mbayo Ipo wapi
Shahidi: Ipo Hotelini
Kibatala: Sawa Nitakuombea Mahakamani Ruhusa Ya Kufuata Notebook yako
Kibatala: Je Unafahamu hata Basic za Intelligence
Shahidi: Ndiyo nafahamu.
Kibatala: Je Wakati Mbowe amajiachia Kuongea na wewe Kwenye simu Kuhusu Mipango hiyo ya Ugaidi
Kibatala: Na Ni simu ipi pia itaonyesha Call Record za Simu Ya Bwire Tarehe 04 August 2020
Shahidi: Ni hiyo Simu ya Samsung Duo
Kibatala: Hivi Ile simu Yako ya Jana Ulikabidhi Simu Lini
Shahidi: Tarehe 11 August 2020
Kibatala: Ulimfafanulia Jaji Kwamba Simu yako inauwezo Wa Kukaa na Chaji zaidi Ya Mwaka Mmoja na Nusu
Shahidi: Hapana
Kibatala: Simu Yako Ilikuwa na Kiasi gani Cha charge Wakati Unamkabidhi
Shahidi: Ilikuwa Chini Kidogo ya Nusu
Kibatala: Ulimfafanulia Jaji Kwanini Simu hii ni tofauti na zile Tatu Kwamba Ina Kaa Na Chaji Mwaka Mmoja na Nusu
Shahidi: Siku fafanua
Kibatala: Ulisema Kwamba Pia Mbowe alikuomba Makampuni yanayo Install Mawasiliano Ya Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hilo Ombi ni kwamba wewe Ulilichukuliaje, La Kawaida au
Shahidi: Niliona la kawaida
Kibatala: Hawa ni Watendaji Wa Chini
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: na wewe ni Afisa wa Juu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ni sahihi Kwa wewe Afisa Kuwa na Mahusiano na Mawasiliano na Watu Waliofukuzwa Jeshi Kwa Utovu Wa Nidhamu
Shahidi: Kuna Maisha Nje ya Jeshi, Siyo Hawa tuh wapo wengine Wengi tunaishi nao Mtaani
Kibatala: Kwa Kanuni za Kijeshi Inaruhusiwa Kuwa na Mahusiano na Junior officer kama haya ya kupeana pesa na Kumtafutiama kazi
Shahidi: Ukiwa Uraiani inaruhusiwa
Kibatala: Hawa Ka Wangekuwa Watu wabaya au Majambazi si usingekiwa na Mahusiano au Mawasiliano nao
Shahidi: Hawa siyo Majambazi, Ni watu Wazuri .
Kibatala: Baada ya Kubadilishana Pesa na Majunior Wako wewe Ka Prudent Officer, Ulikuwa na Jukumu la Kijeshi Kuriport hilo Jambo
Shahidi: Siku Riport Ila Kuna sehemu lilikuwa Lina fanyiwa Uchunguzi
Kibatala: Nilisikia Kuwa umefahamiana na Mbowe tangu 2008
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba wewe Ulishawahi Kutumiwa Pesa na Mbowe
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je ilikuwa Muhimu Kwa Jaji Kujua Kama Alikutumia au Haku kutumia
Shahidi: Haikuwa Muhimu
Kibatala: Hii Namba ya 0754612525 ni Namba ya nani
Shahidi: Ya kwangu
Kibatala: Walikwambia Upande wa Mashitaka Kwamba Riport inaonyesha Namba hii Katika Taarifa Ya Chunguzi
Shahidi: Sikuambiwa
Kibatala: Unasema Bwire Unamfahamu Vizuri, Je unajua Kuwa Bwire alishawahi Kuwa Body Guard Wa Kiongozi Fulani Jeshini
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: unasema Ulionana na. MBOWE sehemu Nyingine zaidi ya CASA Motel, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji hiyo sehemu Nyingine inaitwaje
Shahidi: Nilimwambia ni Mikocheni
Kibatala: Ni kweli Ulikuwa Ujui Identity ya Viongozi waliokuwa wanaenda Kuzuiwa
Shahidi: Nilikuwa siwajui
Kibatala: Hata Sabaya ulikuwa Umjui.
Shahidi: Nilikuwa simjui
Kibatala: Shahidi: CDF ni Kiongozi Wa Kitaifa au Siyo Kiongozi Wa Kitaifa
Shahidi: Kiongozi wa Kitaifa
Kibatala: lakini wewe Hukuona sababu Ya Kuriport Jeshini
Kibatala: Chief of staff Wa Jeshi ni Kiongozi Wa Kitaifa au siyo Kiongozi Wa Kitaifa
Shahidi: Ni Kiongozi Wa Kitaifa
Kibatala: Waziri Wa Ulinzi ni Kiongozi wa Kitaifa au Siyo
Shahidi: Ni Kiongozi Wa Kitaifa
Kibatala: Na Swala lake linaweza Kushughulikiwa M Jeshi.?
Shahidi: Ndiyo Linaweza Kushughulikiwa na Jeshi
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kuhairisha Cross Examination Sababu Ya amuda Nitaendelea Jumatatu Kama Wenzangu Wataridhia
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi
Jaji: Kufuatia Muda na Ombi la Wakili Kiongozi Wa Jopo LA Utetezi, Nahairisha Mpaka Jumatatu Tarehe 31 January ambapo Shahidi: Namba 12 ataendelea Kuwa Kizimbani Kutoa Ushahidi
Washitakiwa Wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Jumatatu Saa 3 Asubuhi
Jaji anatoka