Kesi ya Mbowe: Shahidi aibua utata kuhusu IMEI za simu za watuhumiwa

Kama ilivyowasilishwa na maripota raia BJ na LS leo 18, Januari 2022.

Jaji ameingia Mahakamani, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na

wakili wa Serikali Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala: Mahakama hii Tukufu ikipendezwa, Majina yangu naitwa Peter Kibatala, Nipo Pamoja na;

Michael Lugina
Michael Mwangasa
Faraji Mangula
Nashon Nkungu
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Alex Massaba
Khadija Aaron
Maria Mushi

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Shahidi tukiyekuwa naye Jana, Amefika na yupo Tayari Kuendelea

Shahidi: anapanda Kizimbani

Jaji: Utetezi

Kibatala: tupo tayari kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha tangu Jana Uliapa na Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo hicho

Wakili wa SerikaliPius Hilla: Mheshimiwa Jaji naomba Kukumbushwa tulipoishia Jana

Jaji: uliishia ambapo alisema Kuwa Mihamala ambayo ilihusika ni Kuanzia Tarehe 1 June 2020 Mpaka 31 July 2020

Na akasema aliringanisha report yake na Ile aliyopata Kutoka kwa Service Provider

Wakili wa Serikali: Shahidi Eleza report Yako Kwenda kwa wapelelezi iliambatana na Vitu gani

Shahidi: Vielelezo pamoja na Cover letter

Shahidi: Kutoka Forensic Beaural kwenda Kule ambapo Kesi Imetoka

Wakili wa Serikali: Cover letter inaandaliwa na nani

Shahidi: Inaandaliwa na Kamishna wa Uchunguzi, Kama hayupo inaandaliwa na kusainiwa na Wasaidizi Wake Kwa Niaba

Wakili wa Serikali: Madhumuni ya Barua hiyo, Covering Letter ni nini?

Shahidi: Ni Kutambulisha ile kazi niliyofanya kama Imetoka Kwa Kamishina Wa Forensic Beaural

Wakili wa Serikali: Shahidi Nikuulize, Katika zile Extraction Report ambazo Uliandaa, Unasema Zinatokana na Vielelezo Vipi

Shahidi: Vielelezo Vilivyo kuja Maabara ambazo ni Simu zilikuwa Ni Nane, Kwa Maana ya Vielelezo Vyenye Positive Results ni Simu Nne ambazo Ndiyo niliandalia report

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama kati ya hizo su Nane, hizi Nne unazo Sema ni zipi

Shahidi: Simu ya Kwanza Nilikuwa Nimeipa Alama “E” Ilikuwa Stika Ya Rangi Ya Kijani ambayo tunatumia Maabara Ku label Vielelezo, Juu Nimeandika Kwa Mwandiko wangu, Ilikuwa ni simu aina ya Tecno

Wakili wa Serikali: Simu Nyingine Shahidi

Shahidi: Simu Nyingine Miliipa Alama “F” na Pia ni Stika ya Kijani, Niliandika Mimi Mwenyewe Kwa Mkono Wangu

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Simu ya aina Gani

Shahidi: Ilikuwa ni Simu aina ya Itel

Wakili wa Serikali: Simu ya tatu Shahidi,

Shahidi: Niliipa Alama “G” na Yenyewe Ni Stika ya Kijani na Niliandika hiyo Herufi Kwa Mkono Wangu Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Ni simu ya aina gani?

Shahidi: Ni simu aina ya Tecno

Wakili wa Serikali: Simu ya Nne Shahidi

Shahidi: Simu ya Nne Niliipa Alama “H” Pia ipo katika Stika ya Kijani na Niliandika Kwa Mkono Wangu Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Ni simu ya aina gani

Shahidi: Ni Tecno pia

Wakili wa Serikali: Alama hizi ulikuwa unaziweka Sehemu gani?

Shahidi: Nilikuwa naweka Upande wa Nyuma ya Simu na Kwa zile Zenye Cover nilikuwa naweka Upande wa Nyuma na Kwenye Cover la Simu

Wakili wa Serikali: Kwanini kuwa unaweka alama hizo

Shahidi: Kwa ajili ya Utambuzi Wangu Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Barua uliyoambatanisha na Vielelezo Utaweza Kuitambua

Shahidi: Ndiyo itakuwa na Sahihi yangu

Wakili wa Serikali: Nasemea Barua, Sisemei report Senior assistant Commissioner Of police NAFTALI JOSEPH

Wakili wa Serikali: Kitu Kingine

Shahidi: Pia itakuwa na Muhuri Kwa Niaba ya Kamishina

Wakili wa Serikali: Twende kwenye Nyaraka Nyingine, Report yako uliyotuletea wewe Mwenyewe, Ukiona Leo hii utaitambuaje

Shahidi: Ina Logo ya Jeshi la Police, Ina Majina Yangu, Ina sahihi Ya Kwangu, Ina Muhuri Ambao Umeandikwa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Itakuwa na Kumbukumbu ya Maabara ambayo ni FB/CYBER /2020 /LAB/ 479

Wakili wa Serikali: Namna Nyingine ya Kutambua Report yako

Shahidi: Pia itakuwa na namba ya Kesi ambayo ni CD/IR/2027/2020

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Hizo ndiyo Features Kuu

Wakili wa Serikali: Twende Katika zile Extraction Report, Ieleze Mahakama Je Extraction Riport ya Simu Yenye alama E Ukiona Leo hii Utaitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Kwa sababu Nakumbuka Baadhi ya IMEI

Wakili wa Serikali: Unakumbukaje

Shahidi: Kwanza Naomba Mahakama Inielewe Kuwa IMEI ni 14 Mpaka 16 Digits Kwa hiyo siyo Rahisi Kushika namba zote, Kwa hiyo Nilichofanya ni Kushika Namba za Mwanzoni na Mwishoni Kwa baadhi ya Vielelezo

Wakili wa Serikali: Ni Vyema Je Kwa Simu ya Alama E Ikoje

Shahidi: Ilikuwa ni simu ya TECNO nitataja Moja ambayo ni 35 na Namba Mbili za Mwisho ni 15

Wakili wa Serikali: Kigezo Cha Pili cha Kutambua Extraction Report ni Kipi

Shahidi: Ni Kutokana na Taarifa zilizopo Katika Report ambazo ni Kwanza Lazima Report itakuwa na Sahihi Ya Kwangu na Itakuwa na Muhuri Wa Tanzania, Forensic Beaural, Dar es Salaam, Itakuwa na Laboratory Namba

Wakili wa Serikali: Lab Namba Ngapi

Shahidi: LAB CYBER /2020 /479

Wakili wa Serikali: Kigezo Kingine katika simu hii

Shahidi: itakuwa na Majina yangu pia Kwa Maana ya Mchunguzi.. Kwa kuwa zile Documents Zinatokana na Mashine ya CELEBRITE, pia Itakuwa na Maneno CELEBRITE

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Report ya Simu uliyoipa alama F,

Shahidi: Niliona naweza Kuitambua Kwa Alama za IMEI, ambayo ni 35 na Inaishia na 05

Wakili wa Serikali: Kigezo Kingine Cha Kutambua Extraction Report ya Simu F

Shahidi: Ni sahihi ya Kwangu, Muhuri Wa Polisi Tanzania, Forensic Beaural Dar es Salaam, Itakuwa na Laboratory Namba

Wakili wa Serikali: Lab Namba Ngapi

Shahidi: LAB/CYBER /2020, 479 Wakili wa Serikali_ Kigezo Kingine

Shahidi: Itakuwa na Majina Yangu, Na Kutoka Imetoka na Mashine ya CELEBRITE itakuwa na Maneno CELEBRITE

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Report ya Simu uliyoipa alama G Shahidi: Report hii niliona Nitaitambua Kwa IMEI namba Mbili za Mwanzo no 35 na Mwisho Zilikuwa ni 40 Wakili wa Serikali: Namna Nyingine ya Kutambua Report yako

Shahidi: Kupitia sahihi ya Kwangu, Muhuri Wa Tanzania Police, Forensic Beaural Dar es Salaam, Kuwa na Laboratory Namba ambayo ni FB/CYBER/2020/479 Kwa kuwa Imetoka na Mashine ya CELEBRITE Itakuwa na Maneno CELEBRITE

Wakili wa Serikali: Na Extraction report ya Simu uliyoipa alama F Utaitambuaje

Shahidi: Kupitia IMEI namba ya 35 na Mbili za Mwisho ni 27

Wakili wa Serikali: Vigezo Vingine

Shahidi:,.Itakuwa na Sahihi yangu, Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam

Shahidi: Itakuwa na Majina yangu, itakuwa na Neno CELEBRITE sababu Imetoka kwenye Mashine ya CELEBRITE

Wakili wa Serikali: Elezea Mahakamani Uhalisia Wa Taarifa zilizopo Katika Report

Shahidi: Uhalisia wa Taarifa Zipo kama ambavyo zimetoka Katika Mashine, Kwa sababu Ya Mifumo ya Vifaa Vya Uchunguzi Inaruhusu Ku Read tu na siyo Tu kutoruhusu Bali ina Teknolojia ya WRITE BROCA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesema anao uwezo wa Kutambua Nyaraka

Wakili wa Serikali anakusanya Nyaraka

Wakili wa Serikali: Shahidi Naomba utazame Nyaraka hizi

Shahidi anazichambua Moja Moja

Shahidi: Kwanza Ina Muhuri Kwa Niaba ya Kamishina Wa Uchunguzi wa Kisayansi, Ina sahihi Ya Kimishna Msaidizi wa Polisi NAFTALI JOSEPH, Ina Kumbukumbu ya Maabara, Ambayo ni FB /HQ/CYBER/R. 38/2021/VOLUME 21/300,

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Taarifa Yako

Shahidi: Ina Logo ya Police, Ina Kumbukumbu namba Kwa Maana ni Laboratory Namba ambayo ni FB/CYBER/LAB /479, Pamoja na Kesi namba CD IR 2097 2020, Ina Muhuri Wa Tanzania Police, Forensic Beaural Dar es Salaam, Pia Ina Majina Yangu Pamoja na Sahihi Yangu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwa Ujumla Wake ni Kitu gani

Shahidi: Nyaraka hizi Mheshimiwa Ni Nyaraka ambazo niliziandaa Mwenyewe na Ninazitambua

Wakili wa Serikali: Kwa Jina La Jumla Unaziitaje

Shahidi: Report Ya Uchunguzi Niliofanya

Wakili wa Serikali: Katika Report hiyo Kuna Nyaraka zipi

Shahidi: Kuna Taarifa ambayo niliyoiandaa, Kuna Extraction Report ya Simu Nne Kama Nilivyo Eleza

Wakili wa Serikali: Jana Ulielezea Viambatanisho Katika Taarifa Yako Je ni Viambatanisho Vipi ambavyo havipo hapo

Shahidi: Taarifa Ya Airtel na Taarifa Ya Tigo

Wakili wa Serikali: Vipo wapi

Shahidi: Jana Vilitolewa Mahakamani Hapa

Wakili wa Serikali: Kwenye hizi Nyaraka ambazo zipo Mbele Yako, Covering Letter Umeitambuaje

Shahidi: Kwanza Ina Muhuri Kwa Niaba ya Kamishina Wa Uchunguzi wa Kisayansi, Ina sahihi Ya Kimishna Msaidizi wa Polisi NAFTALI JOSEPH, Ina Kumbukumbu ya Maabara, Ambayo ni FB /HQ/CYBER/R. 38/2021/VOLUME 21/300,

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Taarifa Yako

Shahidi: Ina Logo ya Police, Ina Kumbukumbu namba Kwa Maana ni Laboratory Namba ambayo ni FB/CYBER/LAB /479, Pamoja na Kesi namba CD IR 2097 2020, Ina Muhuri Wa Tanzania Police, Forensic Beaural Dar es Salaam, Pia Ina Majina Yangu Pamoja na Sahihi Yangu

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Riport ya Simu uliyoipa alama E

Shahidi: Ni IMEI 335 KWA Maan ya 35 na Mwisho ni 45

Wakili wa Serikali: Vigezo Vingine,

Shahidi: Ina Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam Ina Sahihi Yangu, Majina Yangu, Laboratory Namba

Wakili wa Serikali: Lab Namba Ngapi

Shahidi: FB/CYBER /2020 /LAB /479

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Riport ya Simu uliyoipa alama F

Shahidi: Ni hii hapa na part ya IMEI namba ni 35 na Mbili za Mwisho ni 05

Ina signature ya Kwangu, Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam, Ina Majina Yangu, Ina laboratory Namba ambayo ni FB /CYBER /2020 /LAB /479

Wakili wa Serikali: ina kitu gani Kingine

Shahidi: Neno CELEBRITE

Wakili wa Serikali: Linaonekana Sehemu gani

Shahidi: Kulia juu

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Riport ya Simu uliyoipa alama G

Shahidi: Ni hii hapa na Ina Features za IMEI namba za Mwanzoni ni 35 na Mwishoni ni 40

Wakili wa Serikali: Vigezo Vingine

Shahidi: ina sahihi ya Kwangu, Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam na Majina yangu, Sahihi Yangu na Lab Namba FB/CYBER /2020 /LAB /479

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Taarifa Nyingine

Shahidi: Ni hii Extraction Report ya Simu niliyoipa alama G

Wakili Peter Kibatala: MHESHIMIWA JAJI, Nimewanong’oneza mawakili wa serikali lakini naona Wa naendelea tu, Shahidi anasoma content za ndani ya nyaraka badala ya utambuzi

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji labda Kama Wakili afuatilii

Kibatala: Inawezekana Kweli Nilisinzia, Lakini Mheshimiwa Jaji Ndiyo Shahidi anasoma na Kumbukumbu namba na Lab Namba Kweli? ndiyo Utaratibu huo?

WS Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji naelewa Concern Yake, Lakini Nature ya Content katika hili linataka ataje alama ambazo ni Namba

Kama Lab Namba na IMEI namba, Hii ni description Ya Nyaraka hizi, Mheshimiwa Jaji Ukiangalia Kwa Maana hii siyo Content, Kwa Kutaja Namba za IMEI za Kwanza na Mwisho sidhani kama ina Violates na Kuzuia Admission ya Vielelezo

Jaji: Namna nzuri ya kwenda Ni Kwamba anachokisema ni Kile alichosema Wakati wa Identification, Kitu ambacho Mahakama Ingekuwa Karibu angeonyesha..Kilichopo katika Documents ni Reference Ya Kile alichokitaja..

Kibatala: Kwa Ruhusa Yako Wacha tu aendelee

Jaji: Kama naona Sawa Sawa alikuwa anaelekea Kwenye Kielelezo Cha Mwisho

Wakili wa Serikali: Shahidi Tulikuwa kwenye Nyaraka ya Mwisho, na Vigezo Uliyotumia Kutambua

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Unaiomba Kufanya Nini katika hizi Nyaraka ulizotambua

Jaji: Nyaraka zipo Ngapi

Wakili wa Serikali: Zipo Sita

Jaji: H bado hajaitambua

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Kwamba Sasa Extraction Report ya Simu uliyoipa alama H Kama Ipo

Shahidi: Ndiyo ipo

Wakili wa Serikali: Unaitambuaje

Shahidi: Part ya IMEI namba zipo hapa Kwa Maana ya 35 Mwanzoni Pamoja na 27 Pia kuna sahihi ya Kwangu, Kuna Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam, ina Majina yangu, Ina Lab Namba FB/CYBER /2020 /LAB /479

Kingine ni Mwonekano wa CELEBRITE

Wakili wa Serikali: baada ya Utambuzi wa Nyaraka hizi Unaiomba nini Mahakama

Shahidi: Naomba Nyaraka hizi zipokelewe Kama USHAHIDI wangu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kukabidhi Vielelezo Shahidi amenyoosha Mkono wake

Jaji: Ndiyooo

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilinyoosha Mkono, Naomba Kwenda Chooni

Kibatala: Mhe Jaji Hatuna Pingamizi Kwa hilo ni katika hali ya Ubinadamu, ila kwa kuwa Yupo Katika Kizimba naomba asindikizwe na Askari Polisi Pamoja na Magereza

Jaji: Sawa Nenda Lakini Utasikindikizwa na Askari Magereza, pamoja ni Inspector lakini ni Inspector ambaye ni Shahidi

Wakati huo Jopo la mawakili wa utetezi wameizunguka nyaraka zilizotolewa na shahidi… Wanazikagua.

Shahidi amesharejea kutoka chooni na sasa amepanda tena kizimbani tena

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa kwanza Sina Pingamizi Wakili

John Mallya: Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Pili sina Pingamizi

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Sina Pingamizi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne hatuna Pingamizi Nyaraka zinachukuliwa na Makarani na Kupandishwa Kwa Jaji

Jaji: tuliishia Kielelezo Namba Ngapi? 21 siyo?

Jaji: Kwenye hizi Report, Nitumie IMEI namba au nini Sababu hizo Mark za E au F zina Appear Kwenye hizi report?

Shahidi: Hapana

Jaji: Kila Moja tunapata Namba Yake atuwezi Ku admits as a group

Wakili wa Serikali: Kwa IMEI Mheshimiwa Jaji

Jaji: Samahani Shahidi Naomba Usogee hapa

Shahidi: anaenda Mezani Kwa Jaji na Kushika Nyaraka

Jaji: Tuanze na E

Shahidi: E Ilikuwa 35 na 40 Mwisho

Jaji: ya F?

Shahidi: ilikuwa 35348.. 05

Shahidi: G ilikuwa 35……..

Shahidi: na H ni 35…..27

Naona kama sauti hazitoki kwa Ufasaha Zoezi halisikiki kwa uzuri, Kidogo pana Ugumu Jaji na Shahidi Wapo Pale Mbele Mezani Kwa Jaji wanaseana IMEI namba huku Mbele Hatusikii Chochote… Tunaendelea kusubiri..

Shahidi amemaliza zoezi aliloitiwa Kwa Jaji anashuka Kutoka Mbele Mezani anarejea kizimbani

Jaji: Kuna Karatasi Hapa, Tusaidie Ipo kwenye Nyaraka ipi? Shahidi anatoka Kizimbani anaenda Mezani Kwa Jaji Kuchambua Makaratasi Amemaliza na kurudi, Karani anabana na stapler

Jaji: Baada ya Kusikiliza Pande zote Mbili, Nyaraka zinapokelewa kama ifuatavyo Report ya Uchunguzi Kutoka Forensic Beaural ni Kielelezo namba 22 Report ya Uchunguzi Kielelezo namba 23 Extraction Report ya Simu IMEI 365029115930845 Kielelezo namba 24

Extraction Report ya SIMU IMEI 353487133305 Kielelezo namba 25 Extraction Report ya SIMU IMEI namba 358821101132040 Kielelezo namba 26 Extraction Report ya SIMU IMEI namba 352386071165127 Kielelezo 27

Shahidi anasoma sasa Nyaraka zote Kama Ulivyo Utaratibu Wa Mahakama Kupitia Sheria ya Ushahidi

Jaji: Kwa sababu ya Muda mnaonaje asome sehemu pekee ambazo aliomba na Barua badala ya Kusoma kila kitu?

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shahidi Umesikia Maelezo ya jaji?

Jaji: Soma kwenye reference za Barua

Shahidi: Nikiwa nasoma Mawasiliano yaliyokuwa yanaingia na kutoka

Je ni some yote au in summary?

Jaji: Soma in summary

Shahidi amemaliza kusoma Kielelezo namba 26 bado kielelezo kimoja..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tupumzike, maana ni saa saba sasa

Jaji: Mnasemaje

Kibatala: Kibatala ni bora tuvumilie, tu’ break Kwa ajili ya Cross Examination baadae..

Jaji: Basi amalizie kielelezo namba 27

Shahidi amemaliza sasa kusoma kielelezo cha 27, na amemaliza kusoma vielelezo vyote

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji naomba tuhairishe turudi kuendelea baadae

Jaji: turudi saa ngapi?

Kibatala: turudi saa 1:55

Jaji: basi tunaenda break ya dakika 45 na tutarejea saa saba na dakika 55

=======

Jaji amerejea Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Quorum ya Uoande wa Serikali Ipo Kama awali

Wakili Kibatala: Mhe Jaji sisi tupo Kama tulivyo kuwa hapo awali na tupo tayari Kuendelea

Jaji: Kwa Mara Nyingine tena nakukumbusha upo chini ya kiapo

Wakili wa Serikali: Shahidi nitaendelea Kukuuliza Maswali.. Zile simu kabla ya Kurejesha Kwa Mpelelezi ililiwaje

Shahidi: Nili hifadhi Kwenye Roka Langu

Wakili wa Serikali: Ulihifadhi Kwenye Kiwango gani

Shahidi: Nili hifadhi Kwenye plastic Bag, Na kuseal, Kwa Juu nikaandika Majina yangu na Tarehe

Wakili wa Serikali: uli Seal Kwa Kutumia nini.?

Shahidi: Kwa Kutumia Tape

Wakili wa Serikali: Kwanini Uli seal, Elezea Mahakama

Shahidi: Nilitaka ziwe Intact (Salama)

Wakili wa Serikali: Jana pia Ulielezea Kuwa Ulihifadhi, Je ni lini tena Ulikuja Kuziona

Shahidi: Nilikuja Kuziona Siku ya Jana Tarehe 17

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Ilikuwaje

Shahidi: Ijumaa wiki iliyopita nilipigiwa simu na Inspector Swila, Kwamba nahitajika kuja Kutoa Ushahidi, Kutokana na Uchunguzi niliofanya, Na Baadae Katika Kumuuliza ni Uchunguzi unaotokana na Lab Namba Ngapi akaniambia 479 ya 2020

Wakili wa Serikali: baada ya kukutajia namba Ukafanya nini

Shahidi: Nilienda Kuangalia kwenye Register Ya Maabara Kuhusu Kesi Inayo toka Kwa DCI Baadae simu ya Jumatatu, nikawasiliana naye akawa kaniletea Vielelezo

Wakili wa Serikali: alikuletea Vielelezo wapi

Shahidi: Forensic Beaural

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama sasa hiyo Jumatatu ya Jana Swila alikuletea Vielelezo Vipi

Shahidi: Ni simu

Wakili wa Serikali: Simu Ngapi

Shahidi: Simu Nane

Wakili wa Serikali: Uliweza Kuvionaje

Shahidi: Sababu niliweka Kwenye Bag ambalo Transparent

Shahidi: Niliangalia Zile Stika na Attachment Fomu yake ambayo ni PF 109

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhiwa na Swila Ulifanya nini

Shahidi: Nili hifadhi Kisha Nikaja navyo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Hali ya seal Ilikuwaje

Shahidi: Ilikuwa kama Nilivyo weka, Niliona Majina yangu Bado yapo pamoja na Tarehe, Niliona Pia Maandishi yaliyoongezwa Juu ya Bahasha Yameandikwa Kwa Maker pen

Wakili wa Serikali: Ulihifadhi Kwenye nini

Shahidi: Bag langu

Wakili wa Serikali: Kwa nini kwenye Begi lako

Shahidi: Ili viwe Kwenye Possession yangu

Wakili wa Serikali: Ukaenda navyo wapi

Shahidi: Ni kaja navyo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Kwa Makusudi ya kutolea Ushahidi

Wakili wa Serikali: Ilikuwaje sasa hiyo Jana

Shahidi: Kutokana na Changamoto za Ki Afya Zoezi halikukamilika

Wakili wa Serikali: Baada ya Zoezi Kutokamilila ilikuwaje

Shahidi: Nilirudi navyo Ofisni nikavihifadhi kwenye Roka Langu

Wakili wa Serikali: Ofisini Wapi

Shahidi: Forensic Beaural, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam Kitengo Cha Cyber Crime

Wakili wa Serikali: Ulihifadhi Mpaka Lini

Shahidi: Mpaka Leo Asubuhi ambapo Nilivichukua wakati Nakuja Mahakamani

Wakili wa Serikali: Hivi sasa Vielelezo hivyo Vipo wapi

Shahidi: Ni navyo Kwenye Begi langu

Wakili wa Serikali: Begi lipo wapi

Shahidi: Begi ninalo hapa

Wakili wa Serikali: Endapo Utatoa Vielelezo Kutoka Kwenye Begi lako vitakuwa na Alama zipi

Shahidi: Zitakuwa na Alama A, B, C, D, E, F, G, na H

Wakili wa Serikali: Alama hizo ni za Namna gani

Shahidi: Alama ambazo zipo Kwenye Stika ya Kijani ambapo Niliandika Kwa Mkono Wangu

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama endapo Unakumbuka Ni simu za aina gani

Shahidi: Techno zilikuwa Nne, Itel Mbili, Samsung Moja na Moja ni Bundy

Wakili wa Serikali: Kwenye Kila simu Ala ulizo weka wewe ni zipi

Shahidi: zilikuwa na Kikaratasi Kilichoandikwa PF 145

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Shahidi apewe Begi lake aweze Kutuonyesha Vielelezo

Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama Parcel Unayo Fungua ni Vitu gani

Shahidi: Hizi ni simu mbalimbali

Wakili wa Serikali: Nini kinachokutambulisha

Shahidi: Kuna Majina Yangu Sehemu ambayo Imeandikwa” SEALED BY” Na Tarehe, 09 July 2021

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine

Shahidi: Ni Vile Vikaratasi ambavyo vilikwepo tangu Siku ya Kwanza PF 145 ambapo Vina namba ya Kesi, Vyote Vilikuwa na namba ya Kesi CD IR 2097 2020

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji Samahani, Hebu turudi Nyuma Kama Kuna sehemu alitaja Kwa Kifupi hiyo Kumbukumbu namba ya Kwenye stika

Jaji: Wewe Kumbukumbu zake Zinasemaje

Kibatala: alitaja zote full FB/CYBER /2020 /LAB..

Jaji: Kama nimesikia Vizuri amezungumzia Kwenye Ile Green Label Aliandika tena hiyo LAB Namba Kwa Ufupi, Hoja Yangu sasa Je Wakati anafanya Identification alitaja hiyo Kwa Kifupi?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji shahidi anatoa simu nane VIELELEZO (SIMU) zinakwenda kwenye Jopo la mawakili wa utetezi kuziangalia vizuri Jopo la mawakili wa utetezi wamezunguka vielelezo kwa pamoja

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Unaiomba nini Mahakama Kuhusiana na Vielelezo Hivi

Shahidi: Naiomba Mahakama Kwamba Hivi Ndiyo Vielelezo Nilivyo fanyia kazi na Taarifa niliyotoa Imetokana na Vielelezo Hivi, Naomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi Wangu

Wakili Nashon Nkungu: Kwa Niaba ya Mshtakiwa Wa Kwanza Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi

Wakili John Mallya: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili Hakuna Pingamizi

Wakili Fredrick Kihwelo: Kwa Niaba ya Mshtakiwa wa tatu Hatuna Pingamizi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Nne hatuna Pingamizi

Karani anachukua Kifurushi cha Simu Kwenda Mezani Kwa Jaji

Jaji: tunapokea Jaji anamuita shahidi Kwenda Mezani Kwake Kuviorodhesha

Shahidi anamueleza Jaji Kuwa vielelezo vina seal Karani wa mahakama amekuja na mkasi, Wanakata Seal na kumkabidhi shahidi Vielelezo vyake

Jaji: Mahakama inapokea simu aina ya Tecno yenye stika ya Green A Kama Kielelezo Namba 28 Simu aina ya Samsung yenye Green B Kama Kielelezo namba 29 Simu aina ya Bundy Green C Kama Kielelezo namba 30 Simu ya Itel yenye Green D Ka Kielelezo namba 31

Simu aina ya Techno Yenye Stika ya Green E Kama Kielelezo namba 32 Simu aina ya Itel yenye Stika green F kama Kielelezo namba 33 Simu aina ya Techno Yenye Stika ya Green G kama Kielelezo namba 34

Simu aina ya Techno Yenye Stika ya Green H kama Kielelezo namba 35 Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji sina Swali zaidi Kwa Upande wangu

=======

Nashon Nkungu: Shahidi Nilikusikia Sawasawa Kwamba Unamiaka 37. Kwani Jeshi la Polisi Una Staafu Ukiwa na Miaka Mingapi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Wewe ni Mstaafu wa Jeshi la Polisi

Shahidi: Hapana

Nashon: Juzi Ijumaa Tuliambiwa wewe Shahidi Unayefuata ni Mstaafu na Unamuuguza Mzazi wako Handeni

Shahidi: Si Za Kweli

Nashon: Je wewe Ndiyo Utakuwa Ulitoa Taarifa za Uongo?

Shahidi: Sijawahi Kutoa Taarifa za Namna hiyo

Nashon: Ulisoma Kitu gani IFM

Shahidi: Advanced Diploma in Computer Since

Nashon: Ni sahihi Kuwa Umesomea Hacking

Shahidi: Mimesomea Ethical Hacking

Nashon: Ulitaja Jina la Uliposomea Hacking

Shahidi: Nilitaja

Shahidi: Nitakuwa Sahihi nikisema Hacking ni Udukuaji wa Taarifa Za Mtu Mwingine

Shahidi: Kwa Maneno Yako

Nashon: Jibu ni yes au No

Shahidi: Jibu siyo Yes au No inategemea

Nashon: Je ni Kweli Hacker anaweza Kuingilia Taarifa na Kuzibadili,

Nashon: Je Hacker anaweza Kuingilia Kifaa hata Kama Kina Password

Shahidi: Possible

Nashon: Je inawezekana Kifaa hicho kikawa Kina Version ambayo ni latest

Shahidi: Sijaelewa Swali

Nashon: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji ulinzi wa kile chumba?

Shahidi: Hapana

Nashon: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba kifaa hata kikiwa na Password unaweza kupata Access na ukaingia

Shahidi: hapana

Nashon: Ni sahihi kuwa ulikaa na taarifa hadi 2.7.2021 ndipo ukaaanza kufanyia uchuguzi?

Shahidi: sikusema hivyo

Nashoni: Kwa majibu wa Ushahidi wako ulipopokea 13.8.2020 ukaweka kwenye locker lako hadi 1.7.2021?

Shahidi: sio kweli

Nashoni: Kutokana na Ushahidi kuacha 1.7.2021 ambayo ndio ulijibiwa barua ni kitu gani ulifanya hapo katikati?

Shahidi: Mheshimiwa 1.7.2021 ndio nilianza kuomba taarifa

Nashoni: Ni muda gani tangu umepokea taarifa?

Shahidi: miezi 10

Nashon: Kwanini hukutoa taarifa ya kutofanyia kaz hivyo vifaa?

Shahidi: nilitoa

Nashon: Unajua kutofanyia kazi kwa muda wote inasababisha Vielelezo kuwa na mashaka?

Shahidi: Sifahamu

Nashoni: Hatua ya kwanza kuchukua ni kuomba data.. ilifanyika tarehe 1 majibu yakaja tarehe 2 kaz ilifanyika siku moja?

Shahidi: tarehe 1 na mbili nilifanya kazi

Nashoni: Ni kawaida Upelelezi kufanyika ndani ya siku1?

Shahidi: Uchunguzi wa nini?

Nashon: wa kile mlichokua mnachunguza

Shahidi: kimya

Nashon: wewe ni Askari unafahamu PGO?

Shahidi: HAPANA

Nashon: unafahamu PGO imeweka utaratibu wa ku label Vielelezo?

Shahidi: Nafahamu

Nashon: PGO imeweka utaratibu wa ku’ label Vielelezo kutoka afisa mmoja kwenda mwingine?

Shahidi: sahihi

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba package ya Exhibit from 28_33

Nashon: Shahidi unafamu PF 135

Shahidi: nafahamu kwa kuona

Nashon: Mheshimiwa jaji naomba iingie KWENYE recod

Nashon: Unatakiwa kuonyesha mtiririko tangu ulipovichukua unatakiwa uonyeshe mtiriko wa chain of Custody kama ulivichukua kwa mtu Mwingine kuja kwako..

Shahidi: mimi sifahamu

Nashon: ulisema wakati wa uchunguzi kifaa kinatakiwa kisiwe na internet sahihi?

Shahidi: mpaka maabara tu

Nashon: kifaa kinaweza kuingiliwa hata kama hujawasha internet possiblity ipo?

Shahidi: sahihi

Nashon: kifaa kinaweza kuingiliwa na infrared or blooth or WiFi

Shahidi: hakuna uwezekano

Nashon: vifaa unavyotumia maabara Kuna computer?

Shahidi: ndio

Nashon: Ina WiFi na Bluetooth?

Shahidi: ndio

Nashon: ulimwambia jaji ulizima WiFi na Bluetooth

Shahidi: nisahihishe

Nashon: nilikuuliza ukiacha internet connection ulisema ulizima Wi-Fi na Bluetooth?

Shahidi: hapana sio sawasawa

Mahakama: Kicheko

Nashon: shahidi ulisema katika Extraction process unachukua taarifa zote na kupeleka storage nyingine?

Shahidi: sio sahihi

Nashon: kabla hujachukua taarifa hapa kupeleka kwingine ulikagua kuwa kuna data gan?

Shahidi: hapana

Nashon: ulimwambia kwenye ushahidi wako kwamba extraction process ilichukua muda gani?

Shahidi: hapana

Nashon: ulimwambia mh jaji ule ushahidi wako extraction process inapofanyika inachukua muda mpaka itakapokuambia yes kwamba imekamilika

Shahidi: hapana

Nashon: ulimwambia mh jaji wakati extraction inafanyika hakuna mtu anaweza kuingilia process mpaka utakapokamilika?

Shahidi: hapana

Nashon: ulimwambia mh jaji uchunguzi wako unachukua siku ngapi

Shahidi: hapana

Nashon: siku zote hizi data zlikua mkononi mwako?

Shahidi: nilikua nazo mimi

Nashon: tangu umekua na Vielelezo mwaka mzima hujamueleza jaji nani alikua na access kwenye office katika kutunza hivi vielelezo

Shahidi: rudia Mheshimiwa

Nashon: hukumbuki swali?

Shahidi: sikumbuki

Nashon: ulieleza lengo la uchunguzi wako?

Shahidi: hapana

Nashon: Sasa turudi kwenye hii term of request ni sahihi uliletewa kuchunguza njama za ugaidi?

Shahidi: kuchunguza mawasiliano

Nashon: ulisoma barua ulizopeleka tiGo?

Shahidi: kuomba miamala ya pesa

Nashon: kwa hyo hizi Meseji zako sio irrelevant kwa ushahidi wako

Shahidi: sijui

Nashon: ulimuonyesha mh jaji barua ambayo ilikuomba uchunguze

Shahidi: barua ililetwa

Nashon: wewe katika utaalam wako niliona kuwa umesema unauelewa wa masuala ya ugaidi

Shahidi: hapana

Nashon: atleast una fahamu elements or ingredients za masuala ya ugaidi?

Shahidi: hapana

Nashon: katika uchunguzi wako wa mawasiliano uligundua mawasiliano yoyote yanayohusu ugaidi?

Shahidi: Mimi siwezi kujibu hilo swali

Nashon: Sasa katika uchunguzi wako uliofanya uligundua kwamba Katika data zote ukizipitia kuna ingredients za ugaidi katika mawasiliano ya huyo Alphani Bwire???

Shahidi: Mheshimiwa nimesema siwezi kujibu

Nashon: huna jibu hujagundua au hufahamu?

Shahidi anajiuma umama hapa..

Nashon: uligundua kwa mshtakiwa wa pili katika uchunguzi wako kwa Adamoo Kuna ingredients za ugaid? Kwa kuwa wewe ndio ulingilia mawasiliano yao

Shahidi: hata huyo Adamoo simfahamu

Nashon: Je katika uchunguzi wako uligundua element hizo kwa Ling’wenya?

Shahidi: Simjui labda unionyeshe

Nashon: Je uligundua kwa Freeman??

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Nashon: ni ngumu kujua kifaa ni cha nani??

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Nashon: terms zipi za reference ulitumia

Shahidi: namba

Nashon: kwa hiyo wewe ukujihusisha kabisa kwenye masuala ya Ugaidi ili nisikuulize tena?

Shahidi: naomba niseme nilichunguza nilichoombwa

Nashon: Sasa shahidi ulipoingia kwenye meseji call details uligundua kitu kinachoitwa watuhumiwa walikula njama za ugaidi.. ulipata vitu vinahusiana na Ugaidi??

Shahidi: nilipata vitu barua ilivyoomba tu.

Nashon: uliingia kwenye calls

Shahidi: hapana

Nashon: kwanini

Shahidi: call unaingia wapi sasa?

Nashon: lakini umeleta sasa hizo call

Shahidi: call note, ndiyo.

Nashon: unafaham utaratibu wa kuchukua kifaa kutoka kwa mtuhumiwa

Shahidi: nafahamu

Nashon: Unafahamu kuwa Uko Bounded na PGO?

Shahidi: Ndiyo

Nashon: kwa hiyo Seizure certificate unaifaham?

Shahidi: Sifahamu

Nashon: mteja wangu anasema vifaa vyake vilichukuliwa kinyume Cha sheria wewe unasemaje

Shahidi anapata kigugumizi

Nashoni: Shahidi unaifahamu PF 145 kuwa msingi wake ni PGO?

Shahidi: Nafahamu

Nashon: Unaweza kusema ni PGO ngapi?

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Unafahamu maana ya hii PF 145 Ni ku Establish Chain of custody?

Shahidi: Siwezi kueleza kwa sababu siyo Mimi nimeweka

Nashon: Unafahamu kuwa unatakiwa kuonesha mtiririko kutoka Ulipovichukua hivi vielelezo mpaka vinafika hapa?

Shahidi: Nafahamu

Nashon: kimsingi hapa Mahakama wewe hauna documents ya makabidhiano ya Nyaraka hizi?

Shahidi: Mimi sifahamu kuhusiana na kielelezo kwa staili hiyo

Shahidi: nilisaini Dispatch

Nashon: hiyo dispatch umeitoa hapa Mahakamani?

Shahidi: sijaitoa

Nashoni: ni sahihi kuwa uliletewa tuhuma za ugaidi?

Shahidi : sikuletewa kuchunguza tuhuma za Ugaidi nililetewa kichunguza simu

Nashoni: wakati unachunguza ulikuwa Unafahamu tuhuma za hizo vifaa ?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Nashon : Unafahamu utaratibu wa kuchukua kitu kwa mtu?

Nashon: Kwa hiyo Unafahamu kitu kinaitwa Seizure certificate?

Nashoni: Wala hapa Mahakama hujaleta karatasi yeyote inayotambua uchukuaji wa vifaa hivi kisheria?

Shahidi: hapana

Shahidi: Mh Jaji Naomba kwenda Short Call (haja Ndogo) Anaruhusiwa…

WS Pius Hilla: Mh Jaji sielewi kwanini Shahidi wetu kila akienda Toilet anasindikizwa na Askari magereza..

Jaji anatoa ufafanuzi kuwa yeye ndo ameagiza hivyo kwa sababu za kiusalama kwa kuwa yeye ni sehemu ya Mahakama na kwa kuwa hajamaliza ushahidi wake

Shahidi anarejea Anasimama

Wakili Msomi Peter Kibatala.. Kumbe alikuwa anajinyoosha tu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji wala hata sikutaka kumjibu Mr Hila..

Sasa anasima Wakili Msomi John Malya

Mallya: Shahidi Askari anatakiwa Awe mwizi?

Shahidi: Hapana

Mallya: kabla ya kuwa kitengo cha Forensic ulikuwa kitengo Gani?

Shahidi: TEHAMA

Malya: Uaskari wako ulienda kusomea pele Moshi

Shahidi: ndiyo

Mallya: Alikuja Shahidi Mmoja Ambaye mteja wangu amesema amemuibia simu Anaitwa Ramadhani Kingai

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Mheshimiwa Mallya akumbushwe jukumu la wakili, kwenye Cross-examination

Mallya: Shahidi nakupa Exhibit P1, Maelezo ya Adamoo, Yasome unieleze kama kuna Imei number aliyoileta hapa Kingai ambayo inafanana na uliyofanyia uchunguzi Shahidi Anasoma ili kutafuta ulinganishi

Shahidi: naona IMEI Number 1, na nyingine Digital siioni, Nyingine kuna Digiti mbili Zina miss.. 35373628912065 kwangu ni Kielelezo D

Mallya: simu Moja unaweza kuwa na IMEI Number Mbili si Ndiyo? 3537282920273 kwako ni inatofautiana na kwangu

Mallya: je ulieleza hiyo tofauti?

Wakili wa Serikali: mh Jaji Shahidi Amesema ameiona hiyo Nyaraka kwa Mara ya kwanza leo kwa hiyo hawezi kuulizwa jambo hilo

Mallya: mh Jaji bado nasisitiza swali langu , Je Ameeleza hiyo tofauti hapa Mahakamani au?

Jaji: hiyo rekebisha

Malya: sawa mh Jaji

Mallya: Kingai alikuletea hiyo simu Uichunguze?

Shahidi:hapana

Mallya: Umewahi kuchunguza simu hii yenye hizi IMEI number Mbili? Na je ni sahihi IMEI Number ni Unique?

Shahidi: ndiyo

Mallya: Kwa hiyo tunakubaliana kuwa simu hii ina IMEI number Mbili zinazokinzana?

Mallya: Shahidi nisomee hapa

WS Pius Hilla: Mh Jaji sidhani kama ni sahihi Shahidi huyu kuwa subjected kusoma kielelezo ambacho amekiona hapa na Amekutana nacho hapa Mahakamani Bila kuwa na Foundation yeyote ili Shahidi awe na Knowledge ya kutosha kwenye hicho kielelezo

Jaji: nakuelewa mr Hilla Shahidi yupo kwenye Position ya kutoa ushahidi hivyo asome kisha kama hajaelewa ndo tutajua hilo

Mallya: Shahidi wakati watuhumiwa walikamatwa walisema walikutwa na Madawa ya Kulevya na Simu kisha simu Ikatajwa kuwa ni Tecno na ina IMEI number fulani, je Simu yenye IMEI number hiyo uliletewa?

Shahidi: simu yenye Imei Number hiyo sikuifanyia kazi

Mallya: Sasa unasema uliyoifanyia Kazi ni hiyo “B” na IMEI zipo Mbili na ni sahihi kuwa hakuna Possibility ya IMEI number kufanana?

Shahidi: kwa ufahamu wangu ni sahihi!

Malya: ni sahihi Awali ulisema kuwa ukishindwa kutaja Imei zote kwakuwa zipo 14 na 15 so ni nyingi sana!

Shahidi: Ndiyo

Mallya: uliambiwa Kwenye content hii uliambiwa utafute mawasiliano Kati ya hiyo! Lazima upewe kwa usahihi taarifa zote? Na zikiwa kikamilifu?

Shahidi: Angalau kukiwa na simu Moja tunaweza kupata taarifa za Mwingine

Mallya: kwa simu Number je?

Shahidi: ni Angalau unatakiwa kuwa na Number za unayetaka kumfuatilia

Mallya: Mh naomba nipatiwe Exhibit 15,16,17

Mallya: Shahidi wewe unadai Uliandika Barua kwenda Airtel, nikitazama hii Barua nitaona wapi Uliandika wewe Bwana NDOWO

Shahidi: Content yote niliandika mimi ila sijasaini Mimi na ni kwa mujibu wa taratibu za kiofisi

Mallya: kuna Majina yako?

Shahidi: hakuna Majina yangu

Mallya: ukisoma hiyo Barua ilikuwa inaomba miamala ya Number ngapi?

Shahidi : Number Tatu

Mallya: wakati unajibiwa ulipewa Number ngapi

Shahidi: Mbili

Mallya: Ulitoa Ufafanuzi wa hilo?

Shahidi: hapana

Mallya: wakati unatoa ushahidi wako ulisema wakati unafanya Extraction ulisema uliweka taarifa yako kwenye Storage ( Hard Disc) ya computer yako

Shahidi; Ndiyo

Mallya: Uliwahi kusema Developer wa hiyo Storage ni Nani?

Shahidi : nilisema ni Microsoft

Mallya: Shahidi Ulieleza hapa Mahakamani kuwa Physical condition ya hizi simu

Shahidi: Sijaeleza!

Mallya: Ulisema case 145 ilibandikwa Muda gani

Shahidi: Nilisema Ilikuja nayo Tayari

Mallya: Ulisoma hujajua ni kitu Gani?

Shahidi: sikuzingatia sana niliona Number ya Kesi tu

Mallya: nitakuonesha Simu Uliyoileta hapa Imeandikwa Polisi Kati/08/09/2020 hivyo vimetangulia kabla ya Taarifa ya Kesi ni Kweli?

Shahidi: ndiyo

Mallya: Mh Jaji Naomba Mahakama Ikiridhia Tuahirishe Mpaka Kesho nina maswali kadhaa Kwa Shahidi

Wakili wa Serikali: Mh Jaji Hatuna Pingamizi

Jaji: Tukubaliane Kibatala namna ya ku’ manage time na haswa mnaweza Kesho mkamaliza saa ngapi

Kibatala: Mh Jaji nafikiri tukianza saa 4 Asubuhi tutamaliza saa 7 mchana Jaji anaandika Kidogo

Jaji: Maombi yamekubaliwa Na Kesi itaahirishwa mpaka Kesho 19/01/2022 saa Tatu Asubuhi na Upande wa JAMHURI mjitahidi Kesho kama mnaweza kuja na Shahidi mwingine ili tukimaliza tuendelee na huyo Mwingine.

Like