Kesi ya Mbowe: Rais Mwinyi atajwa, shahidi agoma maelezo yake kuingizwa kwenye kumbukumbu

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 13.01.2022.

Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 8

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naomba Kuwatambulisha:

Pius Hilla

Abdallah Chavula

Jenitreza Kitali

Nassoro Katuga

Esther Martin

Tulimanywa Majige

Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikupendeza naitwa Peter Kibatala, nipo pamoja na wakili:

Jeremiah Mtobesya

John Malya

Dickson Matata

Seleman Matauka

Faraji Mangula

Gaston Garubindi

Maria Mushi

Hadija Aron

Jaji anaita washitakiwa Wote wanne na wote wanne wanaitika kuwa wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo tuna Shahidi:  mmoja na sote tupo tayari kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari kuendelea

Jaji: Atakuwa ni Shahidi:  wa ngapi huyo..?

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Atakuwa Shahidi:  wa 9 Mheshimiwa Jaji

Shahidi:  anaingia ni mdada amevaa miwani mweupe na mrefu kidogo

Kavaa koti la blue

Jaji: Majina yako

Shahidi: : Gladys Fimbari

Jaji: Miaka?

Shahidi: 36

Jaji: Dini yako?

Shahidi: Mkristo

Jaj: Kazi yako?

Shahidi: Mwanasheria kampuni ya Airtel 

Shahidi:Naapa mbele ya mahakama hii kuwa uShahidi:  nitakao toa utakuwa ni kweli, kweli tupu

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi:  ataomgonzwa na Jenitreza Kitali

Wakili wa Serikali: Unafanya kazi wapi?

Shahidi:  Nafanya kazi Airtel Tanzania

Wakili wa Serikali: Unafanya kazi kama nani?

Shahidi:  Awali niliajikiwa kama afisa wa sheria

Wakili wa Serikali: Kama nani?

Shahidi:  Nafanya kazi Airtel  PLC

Baadae 2021 mwezi march nilibadilishwa cheo na kuwa meneja kitengo cha sheria

Wakili wa Serikali: Sasa hiyo Kampuni ya AIRTEL  PLC Inatoa hizo huduma kaa watu gani? 

Shahidi:  Ili Upate huduma kutoka Airtel  lazima uwe na simu handset na lazima uwe na sim card ya Airtel 

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama kampuni ya AIRTEL  PLC imajihusisha na nini

Shahidi:  Imajihusisha na mawasiliano ya kupiga na kupigiwa simu, huduma ya miamala ya fedha kupitia Airtel  Money

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi tueleze huyo mteja anapata je hiyo simu card ya Airtel 

Shahidi: Ili uweze kuwa mteja lazima ufike katika ofisi za Airtel au kwa mawakala wa Airtel  utanunua sim card lakini baada ya hapo lazima ufanyi we usajili wa ile line

Wakili wa Serikali: Sasa mteje amemumua sim card ya AIRTEL lazima afanye usajili, je usajili unafanyikaje?

Shahidi:  Lazima mteja awepo katika usajili, atajitambulisha majina yake yote, lazima awe na kitambulisho chake cha taifa yani NIDA card, anaye msajili atachukia hiyo namba na kuingiza katika mifumo yetu, kisha atatakiwa aweke dole gumba na kisha msajili wetu atafanya uhakiki (verification) kupitia mifumo ya NIDA ambayo imeunganishwa na mifumo yetu ya NIDA

Baada ya verification na uhakiki atapata namba ya NIDA kuhusiana na mifumo yetu, baada ya kupata uhakiki kutoka NIDA, Taarifa zote zitaifadhiwa katika mifumo yetu na baada ya hapo usajili utakuwa umekamilika

Wakili wa Serikali: Ifafanulie mahakama vizuri, umesema afisa usajili wa Airtel atafanya uhakiki kutoka NIDA, Je afisa wenu wa usajili anapataje taarifa kutoka NIDA?

Wakili Peter Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Huyu shahidi  ameingia akasema yeye ni mwanasheria hakuna mahala yoyote ameomgozwa kusema kama anautaalumu wa usajili….. Kwa maoni yetu hiyo ni “HEAR SAY”!

Shahidi:  Okey, ni kwamba mifumo yetu imeunganishwa………..

Wakili wa Serikali: Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ni mapema kwa wakili kuibua hiyo hoja kama ni hear say au lah!

Jaji: Kwa nini unasema ni hear say?

Kibatala: Kwa sababu yeye ajasema anafanya jukumu la usajili, Bali kasema kuwa yeye ni mwanasheria, hakuna mahala kasema ni jukumu lake kusajili

Jaji: Kwani Hear say ni nini?

Jaji: Mimi nafikiri ni mapema sana kusema ni hear say kwa sababu bado anaendelea kutoa ushahidi:  wake

Kibatala: Ni jambo lolote ambalo halitoli kwa shahidi:  bali kwa third party, ndiyo maana anasema juu ya afisa msajili ambaye siyo yeye

Jaji: Sasa Si Mtamu uliza Maswali Baadaye? Katika kumuuliza maswali, kwa sababu hatuwezi kusema tuukatae ushahidi wa namna hii, ni hatari kama kila shahidi akija tuukatae ushahidi:  kwa sababu hana knowledge ya kutosha

JEREMIAH MTOBESYA: Napata tabu Mheshimiwa Jaji kwa sababu shahidi msingi wake unajengwa na matukio, Hakuna mahala kasema kama alishawahi kupata training au lah, anachotoa ni opinion

Jaji: Nyinyi mtapata nafasi ya kumfanyia cross examination, tusubiri wakati huo!

JEREMIAH MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji ni hatari sana mbele ya sheria, tufuate sheria inasemaje

Wakili wa Serikali: Tuendelee Gladys

Wakili wa Serikali: Sasa ifahamishe mahakama majukumu yako katika kitengo chako cha sheria

Shahidi: Kama nilivyo eleza unapotoa majina yako, na kadi ya NIDA basi msajili anahakiki kwa mifumo yetu ambayo imeunganishwa na mifumo ya NIDA

Shahidi: majukumu yangu ni:

Kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali ya kisheria

Lakini pia kuandaa tathimini za kisheria

Kuandaa nyaraka za kisheria

Kufuatilia kesi zinazohusu kampuni ambazo zipo mahakamani

Pia natoa taarifa ninapoombwa, juu ya taarifa, za kiuchunguzi kwa taasisi za kiuchunguzi au baada ya kupokea amri ya mahakama

Shahidi: Nina shahada ya sheria, niliyopata mwaka 2006 chuo kikuu cha dar es salaam

Nina certificate ya basic skills za computer ambayo nimepata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UCC

Na pia nilipojiunga Airtel mwaka 2004 nilipata mafunzo ya ziada ya mifumo ninayo tumia katika majukumu yangu

Wakili wa Serikali: Ifahamishe mahakama una elimu gani ambayo inakuwezesha kutekeleza majukumu uliyo taja

Shahidi: Nilipata mafunzo ya mfumo wa Mobiquit Kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za mihamala ya fedha inayofanywa na mteja

Mafunzo hayo niliyaoata kwa muda wa wiki mbili Airtel 

Nilijifunzwa Mafunzo kuhusiana na Bussiness Intelligence, mfumo ambao unatunza mawasiliano ya mteja

Nilipofika mwaka 2018/2019 nilipata mafunzo ya mfumo unaitwa AGILE huu ni mfumo wa kutunza taarifa za usajili wa mteja wa Ki BIOMETRIC

Katika mifumo hiyo tunafundishwa mambo mbalimbali ikiwamo :

Jinsi taarifa inavyo chukuliwa na kuhifadhi wa katika mifumo hiyo

Usalama wa mifumo

Endapo kuna tolea tatizo la kimtandao au tatizo la kiteknolojia ni nini tunatakiwa kufanya na utuzanji wa zile taarifa 

Na hiyo Ndiyo Taarifa yangu Kwenye Maeneo hayo

Wakili wa Serikali: Sasa ieleze mahakama juu ya mfumo wa MOBIQUIT jinsi unavyofanya kazi katika utunzaji wa kumbukumbu za mihamala

Shahidi:  Kama nilivyo taja mfumo wa MOBIQUIT, mfumo huu unatunza taarifa za miamala pale ambapo mteja anatuma au kupokea pesa automatic, mfumo unachukua zile taarifa na kwenda kuzihifadhi kwenye sever na baada ya hapo, ilikuweza kuzifikia hizi taarifa unatumia mfumo

Wakili wa Serikali: VIpi kuhusiana na mfumo wa BUSSINESS INTELLIGENCE unafanyaje  kazi?

Shahidi:  Pale ambapo mteja anafanya mawasiliano, akiwa karibu na mnara, automatically yake mawasiliano yake yana chukuliwa kupitia mifumo na kwenda kutunza kwenye sever, baada ya hapo unapotoa kuzifikia hizi taarifa ndipo unatumia mfumo wa BUSSINESS INTELLIGENCE

Wakili wa Serikali: Ifahamishe mahakama ni mawasiliano ya namna gani mfumo huu ndiyo unafanya kazi 

Shahidi:  Anapopiga simu, anapo tuma ujumbe mfupi, anapo pokea Simu na anapotaka huduma za internet, inakuwa captured kwenye mfumo wetu

Wakili wa Serikali: Shahidi:  Umetaja Mfumo Mwingine Wa AGILE Ifahamishe Sasa Mahakama ni Kitu gani 

Shahidi:  Kama Nilivyo eleza Kuwa Mfumo wa AGILE unafanya kazi mteja anapotaka kwenda kusajili line yake, anapotaja namba ya utambulisho wa NIDA msajili anaingia namba za NIDA kwenye mfumo, na baada ya taarifa hizi mteja kuweka kidole gumba zinakwenda kuhakikiwa NIDA na majibu yatakurudi kisha taarifa hizo zinaenda kuhifadhi wa katika mfumo wetu wa AGILE

Wakili wa Serikali: Ifahamishe mahakama, kama wewe ni mtumiaji wa hii mifumo ni kwa muda gani umetuma hii mifumo? 

Shahidi:  Kwa upande wa MOBIQUIT na BUSSINESS Intelligence niliweza kutumia mifumo hii tangu nipo jiumga na Airtel  mwaka 2004 na kwa upande wa AGILE ni tangu mwaka 2019 mpaka sasa

Wakili wa Serikali: Sasa wakati wa ushahidi umeeleza mahakama majukumu yako, na moja ya majukumu yako ni kutoa taarifa chunguzi kwa vyombo vya uchunguzi, ifahamishe mahakama taarifa  unazotoa  ni kwa vipi na zipi?

Shahidi:  Kwanza nikianza, tunatoa kwa Jeshi la Polisi, Tume ya Kupambana na Kuzia Rushwa PCCB, Tume  ya Kupambana na Madawa ya Kulevya, Mamlaka ya Mawasiliano na Financial Intelligence, na  pale mteja anapo hitaji kupewa taarifa zake anaruhusiwa kupewa

Wakili wa Serikali: Ni taarifa ya namna gani? 

Shahidi: Kila taasisi zinaomba taarifa za mawasiliano kwa ujumla nikimaanisha kupiga na kupokea simu, mihamala ya fedha na pia usajili wa line

Wakili wa Serikali: Ifahamishe mahakama utaratibu wa maombi huwa unafanyikaje

Shahidi:  Taratibu kubwa ni chombo chunguzi kuleta barua ya maombi ya taarifa, na maombi haya yanawasilishwa airtel kupitia upande wetu wa mapokezi ya kisha pokelewa yanaratibiwa katika register yetu na kupelekwa kwenye kitengo cha sheria kufanyiwa kazi na baada ya hapo mkuu wa kitengo cha sheria anatoa ruhusa kwa muhusika juu ya kufanyia kazi maombi hayo

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi barua ya maombi imeshafika na mkuu wa idara ameshasaini, sasa huyu aliye na barua anafanya nini kazi? 

Shahidi:  Lazima afanye kazi barua kwa kujiridhisha kwanza, juu ya anuani ya taasisi kama barua hiyo imeelekezwa kwa Airtel? , Je barua hiyo ina nembo ya taaaisi husika..? , Taarifa hizo ni za kiuchunguzi..? Na kama siyo za kiuchunguzi haiwezi kufanyia kazi, lakini pia iwe na sahihi na muhuri wa taaaisi husika

Wakili wa Serikali: Umesema afisa anahakiki vitu vyote ikiwemo kama taarifa ya kiuchunguzi, Je nini unaangalia kujua kama. ya kiuchunguzi au siyo?

Shahidi: Barua zote za kiuchunguzi zinataja kosa ua kuna ambazo zinataja jalada namba ili kuonyesha kwamba kuna kesi inaendelea

Wakili wa Serikali: Ni watu gani hasa sasa wanao fanyia kazi maombi?

Shahidi:  Ni watu wa kitengo cha sheria

Wakili wa Serikali: Ieleze mahakama sasa kitengo ha sheria ni watu wangapi wanashughulikia hizo kazi?

Shahidi:  Ni watu wa wili ambapo ni mimi na mwenzangu

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi assignment imefika mezani kwako na maombi yote umepangwa yamefuata utaratibu

Na kila mfumo ni credentials zangu za kuniruhusu kuingia kwa kila ninapo ingia

Shahidi: Ofisini kwangu kumuanganishwa na mifumo niliyo taja kupitia computer yangu yangu MOBIQUIT, BUSSINESS INTELLIGENCE NA AGILE

Wakili wa Serikali: USER name unapata wapi? 

Shahidi: Kitengo cha IT ambapo ni mimi mwenyewe na kitengo cha it hakuna mwingine anayefahamu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuingiza hizo Credentials Kitu gani kinafuata?

Shahidi:  Mfumo wenyewe unakuletea sasa sehemu ya kuingiza namba ya simu ya mteja lakini pia muda ambao unataka zile taarifa

Na automatically mfumo wenyewe unachakata zile taarifa na kuleta katika computer yako

Wakili wa Serikali: Taarifa zinachakatwa na zinakuja kwenye page yako (computer yako) je zinakuwa zimehifadhiwa wapi? 

Shahidi:  Zinakuwa zimehifadhiwa katika saver, zinahifadhiwa na mfumo

Shahidi:  Baada ya hapo ni uhakika wa taarifa ukitoka ktk mfumo na taarifa husika kama ni namba husika, je ni sahihi na kama vile unavyotaka

Kisha Nina-print taarifa 

Shahidi:  Nilisha print inafanya tena uhakiki

Wakili wa Serikali: Uhakiki wa Namna gani?

Shahidi:  Kwa kulinganisha na barua ya maombi, nagomga muhuri na kusaini pamoja na kuweka tarehe, kisha naandaa cover later kwa ajili ya kuambatanisha taarifa hizo

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umeshasema ulisha aandaa na kuweka cover later, nini kinafuata? 

Shahidi:  Ni naweka Vizuri na Kuiwasilisha Kwenye Mamlaka husika

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umesema hapa mahakamani kwamba wewe huwa unapewa credentials na watu wengine kuwezesha kuingia katika mifumo, je ni watu gani wengine katika taasisi yenu? 

Shahidi:  Kuna watu wa aina mbili, watu wa call centers watu wa customer care hawa ndiyo wenye uwezo wa kuona, kama nilivyosema kwa ajili ya kuhudumia wateja kwa ajili ya kuona mihamala kama imekosewa au lah. na watu wengine ni watu wa ku extract zile taarifa, huyu ni mtu pekee kutoka kitengo cha sharia. 

Kundi la pili ni kitengo cha sheria sasa, sisi tumepewa uwezo wa kuona na ku print lakini pia hatuna uwezo wa kufanya chochote katika ile taarifa, na sisi pia inakuja kwa  mfumo wa read only.

Mifumo hiyo pia inafanyiwa SYSTEM AUDIT mara kwa mara kuangalia uimara wake

Lakini si kila mtu ana access ya hii mifumo, ni baadhi ya watu ambao wamepewa credentials ambazo zinawaruhusu kuingia katika mifumo

Wakili wa Serikali: Sasa huyu mtu aliyepewa uwezo wa kuingia na kuona zile taarifa, ni kitu gani kingine anaweza kufanya katika taarifa?

Shahidi:  Huyu aliyepewa access ya kuona hana uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kuona, kwani taarifa hizo zinakuwa katika mfumo wa read only (kuweza kusoma tuh)

Wakili wa Serikali: Hawa watu wenye uwezo wa kuona tuh ni watu wa idara zipi? Shahidi:  Ni watu wa customer service pamoja na Call Center, na wale ambao wapo kwenye kitengo Cha IT

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umeeleza mahakama juu ya mifumo, Je umadhubuti wa hiyo mifumo ikoje?

Shahidi:  Mheshimiwa Jaji taarifa zetu ni automatic generator designated, hakuna mtu anayeweza kuzalisha taarifa za hiyo mifumo, mifumo hiyo pia inalindwa kwa kuwekwa software za usalama (firewalls)  kwa kulinda usalama wa mifumo na taarifa endapo imetokea muingilio wa aina yoyote

Lakini mifumo hii imeunganishwa na Airtel Kwa maana hauwezi kuwa mahala popote kuingia katika mifumo hii 

Lakini pia Uwezi Kutumia Kifaa Chochote Kuingia Katika Mifumo yetu

Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Sababu ya Kutoingia Ukiwa popote? Shahidi: Kwenye mifumo hii lazima uwe na hivyo vifaa ambavyo vimeunganishwa na Airtel  na siyo kila mtu anaweza kuingia katika mifumo

Wakili wa Serikali: Unaposema kifaaa/ vifaa ni vya namna gani? 

Shahidi:  Namaanisha computer yaani desktop au laptop

Wakili wa Serikali: Ulikuwa unaelezea umadhubuti wa hiyo mifumo, je ni kitu gani kingine?

Wakili wa Serikali: Hiyo Mifumo inausalama gani Kuhakikisha nyie watumiaji na Mliyotumia ni Salama?

Shahidi:  Kwanza kuna software ambazo ni firewall ambazo zitatambua a endapo kuna mtu anajaribu kutaka kuingia, na lakini pia endapo patakuwa na tatizo la kimtandao zile taarifa haziathiriwi kwa namna yoyote

Wakili wa Serikali: Na je utendaji kazi wa huu mfumo ukoje?

Shahidi:  Mfumo wetu ni madhubuti na hauna hitirafu yoyote, na inapotokea pale unapoingiza credentials, kuwa kuna tatizo na uwezi kuzifikia taarifa za mteja

Wakili wa Serikali: Nini kinatoa endapo network inakuwa chini kwa taarifa mnazotunza? 

Shahidi: Network inapokuwa down haiathiri vile vilivyomo ndani, pale ambapo imerekebishika unaweza kupata taarifa

Wakili wa Serikali: Nakurudisha nyuma, ulisema wakati wa usajili mteja anaweka dole gumba katika kifaa je hilo kifaa kinaitwaje? 

Shahidi:  Msajili anakuwa na vifaa viwili, handset na kifaa cha dole gumba ambapo airtel  tunatumia kifaa kinaitwa FALOPO 

Wakili wa Serikali: Intergrity ya  vifaa mnavyotumia ofisini ukoje?

Shahidi:  Mfumo wetu sisi ni automatic generated, hakuna taarifa ya ziada ya kuongeza, mifumo yetu inafanya kazi vizuri, tuna vifaa (software) ili kusaidia usalama wa hiyo mifumo

Wakili wa Serikali: Ieleze mahakama sasa hiyo mifumo ni mifumo ipi?

Shahidi:  Tunatumia desktop au laptop, ambapo vifaa hivi vimeunganishwa na mifumo ya Airtel. Na uwezi kufanya lolote, vifaa hivi vimeunganishwa na mifumo ambayo inatoa ALERT pale ambapo unafanya kinyume.

Shahidi:  Mifumo ya kuweza kupata taarifa za miamala ni MOBIQUIT kama nilivyo eleza ni mfumo wa kuchukua taarifa na kuhifadhi mihamala

Mfumo mwingine ni AGILE ambapo mteja anapofika dukani na kufanya usajili, basi uhakiki wa taarifa hizo, zile taarifa zinaenda kuhifadhi wa kwenye mfumo wa AGILE. Na kupitia mfumo huo unaweza kuzipitia taarifa hizo

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi ieleze mahakama mnamo tarehe 02 July 2021 ulikuwa wapi?

Shahidi:  Mnamo tarehe 02 July 2021 nikiwa ofisi za Airtel Morocco nikiwa nafanya majukumu yangu 

Wakili wa Serikali: Ieleze mahakama Morocco ipo maeneo gani? 

Shahidi:  Ofisi za Airtel zipo Morocco hapa hapa Dar es Salaam ambapo ndipo kitengo cha sheria kilipo

Wakili wa Serikali: Sasa wakati upo ofisini kwako kilitokea kitu gani? 

Shahidi:  Wakati naendelea na majukumu yangu ya sheria, Mkuu wetu wa Idara a lini assign kushughulikia maombi ya taarifa

Wakili wa Serikali: Maombi hayo yalitaka nini?

Shahidi:  Kushughulika na maombi ya miamala ya fedha ya namba 0782 237913,0787555200, 0784789944 pamoja na taarifa za mihamala iliomba pia na taarifa za usajili

Wakili wa Serikali: Baada ya kupokea maombi hayo ulifanya kitu gani?

Shahidi:  Nilihakiki ile barua kama imetoka kwenye taasisi husika, ya uchunguzi wa kisayansi, Ile barua ilikuwa inaongelea taarifa ya kiuchunguzi na pia niliangalia taarifa gani inayoombwa, nilihakiki kama imegongwa muhuri wa taaaisi husika

Wakili wa Serikali: Taarifa inayihusiana na nini? 

Shahidi:  Taarifa ambayo nimeomba kuhusiana na zile namba tatu nilizo zitaja awali

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo kitu gani kilifuata?

Shahidi:  Baada ya kujiridhisha niliingia kwenye kifaa changu cha kazi ambacho ni computer, kisha ni kaingia kwenye mfumo wa AGILE, na mfumo huo ulifanya kazi vizuri ni kaingiza namba moja ya simu ambayo imeombewa taarifa, na kisha ikanitolea taarifa husika baada ya kuchakata

Wakili wa Serikali: Kwemye barua iliombwa taarifa za mihamala ya fedha na usajili, hapa unaomgelea kuingia kwenye mfumo wa AGILE Je ulipata taarifa ipi? Shahidi:  Nilipata taarifa za usajili wa namba

Wakili wa Serikali: VIpi kuhusu namba zingine?

Shahidi:  Hiyo ilikuwa kwa namba 0784789944 ni kafanya kwa namba ya pili 0782 237913 na ni kafanya vilevile kwa namba ya tatu 0787 555200 ambapo zote nilipata usajili wa namba hizo nika print

Wakili wa Serikali: Kitu gani ulifanya baada ya kupata hizi nyaraka?

Shahidi:  Niliingia tena katika mfumo wa MOBIQUIT ambapo ni lazima uingize namba na muda, tofauti na ule mfumo wa AGILE 

Shahidi:  Nilipo ingia namba na muda, window yangu ya computer ikaniletea zile taarifa,.

Wakili wa Serikali: Muda unamaanisha nini.? 

Shahidi:  Labda nikurudishe katika barua, barua iliomba taarifa ya mihamala kutoka tarehe 01 June 2020 mpaka 31 July 2020

Ambapo nilifanya hivyo kwa namba ya kwanza 0787 555200 ni kaingiza namba na muda

Wakili wa Serikali: Sasa kwa namba hiyo uliyotaja unasema iimgiza namba na muda, endelea 

Shahidi:  Nikifanya hivyo hivyo kwa namba iliyofuata ya 0784789944 ni kaingiza namba na muda, na system ikaniletea taarifa kama nilivyoomba

Wakili wa Serikali: Baada ya taarifa hizo kuja nini ulifanya?

Shahidi:  Nilihakiki tena, ile namba ambayo imeombewa taarifa, na baada ya kujiridhisha nili print na nikaendelea kwa namba nyingine

Wakili wa Serikali: Endelea

Shahidi:  Nilihakiki na nikaendelea kuprint baada ya kujiridhisha

Shahidi:  Baada ya kuprint kwanza niligonga muhuri wa Airtel katika nyaraka zote, kisha nikaweka sahihi pamoja na tarehe 

Wakili wa Serikali: baada ya kuletewa hizo taarifa?

Lakini pia niliandaa barua (cover later) ambayo niliambatanishia taarifa

Wakili wa Serikali: Nini Kilifanyika Baada ya Zoezi hilo 

Shahidi:  Niliandaa na cover later niliyo andaa ilikuwa na logo ya Airtel, zile taarifa, katika cover later hiyo kuna jina langu , sahihi yangu na muhuri Wa Airtel 

Wakili wa Serikali: Sasa ieleze mahakama hali ya hiyo mifumo uliyo tumia siku hiyo kama i kuwa inafanya kazi vizuri

Shahidi: Mifumo Hiyo Ilikuwa Inafanya Kazi Vizuri, Hapakuwa na Tatizo la Kimtandao na Halikuwa na Changamoto yoyote Wakati na Print hizo Taarifa

Wakili wa Serikali: Vipi kuhusiana na kile kifaa kazi ambacho ulikuwa unakitumia?

Shahidi: Kifaa kilikuwa katika hali nzuri na halikuwa na tatizo lolote wala changamoto yoyote na endapo kingekuwa na tatizo lolote basi pale ambapo unaingiza credentials zingakukatalia na kukutaarifu kuna tatizo, lakini katika kifaa changu hapakuwa na tatizo hilo siku hiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuandaa hizo Taarifa na Kuweka Cover Later nini Kilifuata

Shahidi:  Baada ya hapo niliwasilisha taarifa hizo ofisi ya uchunguzi

Wakili wa Serikali: Hizo Nyaraka Ukiziona Hapa Mahakamani Unaweza Kuzikumbuka?

Shahidi:  Ndiyo

Wakili wa Serikali: Eleza utajuaje?

Shahidi: Katika cover later hiyo niliambatanishia barua ya  maombi kutoka ofisi ya uchunguzi ya tarehe ya  01 July 2021 ambayo inaonyesha jalada namba  ilikuwa ni CD/ IR / 2097/ 2020 lakini pia ina namba 3 ambazo ziliombewa taarifa ambazo 0787 555200, 0782 237913, 0784779944

Wakili wa Serikali: VIpi kuhusiana na zile taarifa za usajili wa namba za simu. kitu gani kitakufanya ukiziona uzikumbuke?

Shahidi: Taarifa hizo zina namba ya simu, majina yangu na signature yangu na nimegonga muhuri kwa barua zote pamoja na tarehe

Wakili wa Serikali: Taarifa ya Kwanza ambayo utaweza kuitambua ni ya namba ipi?

Shahidi: Taarifa ya kwanza ni 0787 555200 

Ya pili ni 0782 237913

Namba ya mwisho ni 0784789944

Wakili wa Serikali: VIpi kuhusu taarifa za mihamala?

Shahidi: Kuna taarifa ya mihamala ina jina langu, sahihi yangu, muhuri wa kampuni na tarehe

Wakili wa Serikali: Angalia hiyo nyaraka na uniambie ni kitu gani 

Shahidi: Nyaraka mkononi mwangu ni cover later ambapo inaonyesha anuani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kumuonyesha shahidi wetu nyaraka hizo

Wakili wa Serikali: Angalia kama nyaraka hizo unazitambua au huzitambui

Shahidi: Cover later hii naweza kuitambua kwa sababu zifuatazo kwa sababu ina nanani ya kampuni ya Airtel, ina namba ambazo zomeombewa taarifa, ina jina langu, na muhuri wa  Airtel

Nyaraka inayofuata ni barua kutoka ofisi ya uchunguzi wa kisayansi, na nimeitambua sababu, ina namba ya jalada niliyo taja, ina muhuri wa Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi

Lakini pia hakuna taarifa za usajili ambazo zina namba iliyo ombewa taarifa, ina muhuri wa kampuni, sahihi ambayo ni ya kwangu na tarehe

Wakili wa Serikali: Unasema kuna namba ambayo umetaja mwanzoni, ni ipi?

Shahidi: Ni 0784789944

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje? 

Shahidi Kutokana na hiyo namba lakini pia ina muhuri wa kampuni, sahihi ambayo ni ya kwangu na tarehe

Kuna taarifa ya usajili pia wa namba 0782 237913

Kuna taarifa pia ya usajili wa namba 0787 555200 ambayo ina muhuri wa kampuni, sahihi yangu na tarehe

Wakili wa Serikali: Na Nyaraka Inayofuata?

Shahidi: Ni ya mihamala ya fedha ya namba 0787 555200 ambayo ina muhuri wa kampuni, sahihi yangu na tarehe 

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi unaiomba nini mahakama kuhusiana na nyaraka zote hizo hapa mahakamani?

Shahidi: Naiomba Ipokee Kama Vielelezo

NYARAKA ZINA PELEKWA UPANDE WA UTETEZI

Jopo la Mawakili Wa Utetezi Wanazizunguka na Kuzichambua

Waliozingira Nyaraka hizo ni Wakili Peter Kibatala: 

Wakili Jeremiah Mtobesya

Wakili John Malya

Wakili Dickson Matata

Wakili Faraji Mangula

Wakili seleman Matauka

Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza hatuna pingamizi kwa kuzingatia haki ya kufanya cross examination

Wakili John Malya: Kwa upande wangu sina OBJECTION

Wakili Peter Kibatala:  Kwa niaba ya mshitakiwa wa nne hatuna pingamizi

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji kwa upande wangu sina pingamizi

Jaji anazitizama moja moja

NYARAKA ZINATOKA UPANDE WA UTETEZI ZINAENDA JUU KWA MHESHIMIWA JAJI KUPITIA WASAIDIZI WAKE

Mahakama bado ipo kimyaaaa

Jaji: tuliishia kielelezo namba 14, si ndiyo?

Mawakili wote wanaitika NDIYO!

Bado mahakama ipo kimya, nyaraka zote zipo pale juu kwa Jaji anazipitia na kuandika andika hivi

Jaji: Kwa maana riport za transactions ni namba mbili siyo tatu, si ndiyo?

Wakili Peter Kibatala:  Na sisi tumeona Mbili

Kibatala:  kwa maana print out au barua kutoka Airtel.?

Jaji: Kwa hiyo kwenye registration ni namba 3 ila kwenye transactions ni namba 2

Jaji: Basi mahakama inapokea vielelezo kama ifuiatavyo:

Barua ya kwenda ofisi ya uchunguzi no kielelezo namba 15

Barua ya kuomba taarifa ni kielelezo 16

Taarifa ya usajili ya namba 0782 237913 ni kielelezo namba 18

Taarifa usajili ya 0784789944 ni kielelezo namba 17

Taarifa ya usajili ya namba 0797555200 ni kielelezo namba 19

Taarifa ya mihamala ya namba ,0787555200 ni kielelezo namba 20

Taarifa ya mihamala ya namba 0784789944 ni kielelezo namba 21

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi jaji na kusimama. na kuinama kidogo

Jaji: Sasa Taarifa zote zisomwe na shahidi kama ulivyo utaratibu

Shahidi ameanza kusoma barua ya Airtel kwemda ofisi ya uchunguzi wa kisayansi

Shahidi anasoma sasa barua kutoka Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi Maombi ya Taarifa

Shahidi anasoma Taarifa ya Usajili wa namba ya Usajili wa Namba  0784789944

Shahidi anasoma taarifa ya usajili wa namba 0782 237913

Shahidi anasoma taarifa ya usajili wa namba 0787 555200 namba ya Luten  Denis Urio

Wakili wa Serikali: Kwa mujibu wa kielelezo kinachofuata cha mihamala ya namba 0787 555200, tusomee mihamala ya tarehe 20 July 2020

Shahidi: Muamala  wa kwanza wa tarehe 20 July 2020 namba ya muamala , namba iliyotuma ni 0784789944, receiver ni 0787 555200 kiasi kilichotumwa ni Tsh 500,000

Wakili wa Serikali: Naomba utusomee muamala  wa 22 July 2020

Shahidi: Kuna mihamala mitatu

Wakili wa Serikali: Naomba utusomee muamala  wa pili wa 22 July 2020

Shahidi: Transactions:

Muamala  umetoka 0780900244 ametumiwa tsh 199,000 akawa na jumla ya Tsh 300, 000 kwenda kwa 0787555200

Wakili wa Serikali: Tusomee muamala  wa mwisho

Shahidi: Muamala  wa 31 July 2020 kutoka 0784789944 kwenda  0782 237913, kiasi kilicho tumwa kilikuwa Tsh 80,000

,

Wakili wa Serikali: Hebu angalia kielelezo namba 17, ambapo ni taarifa ya usajili kielelezo nmab 17 cha mahakama 

Shahidi: Kilikuwa kielelezo cha taarifa ya usajili wa namba 0784789944

Wakili wa Serikali: Kwa Taarifa yako namba hiyo ilikuwa imesajiliwa kwa majina gani?

Shahidi Majina Ya kwanza Freeman, majina mengine Aikael Mbiwe

Wakili wa Serikali: Angalia Kielelezo 18  Cha Usajili wa Mahakama Namba gani 

Shahidi: Kilikuwa kielelezo cha usajili wa namba 0782 237913

Wakili wa Serikali: Kwa mujibu wa taarifa yako ilikuwa imesajiliwa kwa  namba gani? 

Shahidi: Kwa majina ya Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Kielelezo namba 19 no kielelezo cha usajili wa namba gani?

Shahidi: Ni usajili wa namba 0787 555200

Wakili wa Serikali: Ambayo ni ya nani?

Shahidi: Ni ya Denis Urio

Wakili wa Serikali: Kielelezo namba 20 ni kielelezo cha namna gani? 

Shahidi: Ni prin- out ya 0787 555200

Wakili wa Serikali: Nenda sasa katika muamala  wa tarehe 20 July 2020, ulifanyika muamala  wa Tsh ngapi?

Shahidi: Siku ya tarehe 20 July 2020 kwa namba 0780 900174 ilituma kiasi cha tsh 500, 000 kwenda kwa namba 0787 555200

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa taarifa hiyo tuambie namba iliyotuma fedha ni namba ya  mtandao gani

Shahidi: Ni namba ya mtandao wa Tigo

Wakili Mtobesya: Mheshimiwa Jaji yeye aseme yanayuhusu mambo ya AIRTEL ila mambo ya Tigo aachane nayo

Wakili wa Serikali: Sisi hatuoni tatizo kwa sababu hiyo taarifa imeletwa na shahidi

Jaji: Kuna pingamizi hapo?

Wakili Mtobesya: Tutaanza kumuuliza alijuaje kuwa ni namba ya tigo, na usajili wake aliujuaje

Jaji: Naona hapa hoja ni transactions tuh, mambo ya kampuni gani au ya nani siyo muhimu

Wakili Mtobesya: Mheshimiwa Jaji samahani, kaka yangu anaanza kusema hatukukataa taarifa, hakusema kuwa hiyo namba ni ya Tigo, sisi tunasisitiza kuwa anachokifanya shahidi anaenda OVERBOARD

Wakili Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji nafikiri wangemuacha amalize kwa sababu shahidi  ndiye aliye andaa taarifa na wao hawakupinga taarifa hiyo kuingia mahakamani

Palikuwa na Shahidi Wa Tigo hapa hakusema, watafute shahidi mwingine, tuache ku snick inn ushahidi kwa njia tofauti zisizo za kisheria

Jaji: Si ndiyo kazi yenu hiyo? Wakati wa cross examination, ukifika wakati huo ndiyo utaiuliza mahakama, lakini kama document imeshaingia mahakamani alafu tumwambia shahidi kuwa kuna vitu hatakiwi kuviongea

Wakili Mtobesya: Kwa kifungu cha 61 ndicho kinacho katazwa hapo, kwamba ushahidi wa nyaraka usiongezewe kwa mdomo, hakuna sehemu kwenye kifungu cha 61 kuwa aliweka ushahidi wa mdomo katika nyaraka tutahojinkwemye cross examination, akija mtu mwingine hatoona kwamba tukisimama. na wewe ukatuambia kuwa tutahoji kwemye cross examination

Jaji: Nafikiri hoja yako ni kuongeza maneno kuwa ni namba ya Tigo. Mh?

Wakili Mtobesya: Sahihi Mheshimiwa Jaji

Wakili Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji samahani mahakama yako tukufu, kwa maslahi ya muda na maslahi ya haki, tunaachana na hilo swali

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi kwa mujibu wa wa hiyo taarifa kuwa namba 0787 555200 ulisema hiyo namba ulipokea fedha kutoka wapi?

Shahidi: Tarehe 20 July 2020 namba 0787 555200 ulipokea fedha kutoka namba 0780900174

Wakili wa Serikali: Hiyo namba ya mtu gani au ni ya nini..?

Wakili PETER KIBATALA:  Mheshimiwa Jaji sisi wote watu wazima, walisema waondoa swali, ila naona wanafanya kile kile kwa mlango wa nyuma, ili siku ya mwisho ionekane ni namba ya Tigo

Jaji: Rudia hilo swali lako vizuri

Wakili wa Serikali: Asante Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Ulisema mnafanya kazi ya mihamala ya kifedha, je kampuni yenu inafanya kazi na makampuni gani?

Shahidi: Mteja wa Airtel anaweza kupokea Pesa Kutoka Vodacom, Tigo, Zantel na Hallotel hii ni kutokana na mikataba baina yetu na makampuni ya mitandao tofauti

Wakili wa Serikali: Nini kinatokea pale ambapo mteja ambaye siyo wa Airtel anatuma pesa kuja kwa mteja ambaye ayupo Airtel?

Shahidi: Endapo mtu atatuma muamala  kutoka mitandao mwingine tofauti, riport zetu zitaonyesha collection akaunti namba ya ule mtandao husika

Wakili wa Serikali: Na unaposema kuwa ni collection akaunti una maana gani?

Shahidi: Mteja anapopokea au kutuma pesa kwenda kwenye mtandao tofauti, fedha zinaimgia kwanza kwenye collection akaunti ya mtandao husika, kisha mtandao husika unasambasa ( disburse) kule unakktakiwa kwenda

Kwa hiyo taarifa yetu ya mtandao unaonyesha collection akaunti namba ya mtandao husikla 

Na hivyo hivyo kwa mteja wetu anapotaka kutuma kwenda kwa mtandao mwingine husika, mtandao ule tofauti anapokea ujumbe wa ela  kutoka kwenye collection akaunti

Wakili wa Serikali: Unaposema mtandao husika unamanisha nini?

Wakili wa Serikali: Ifahamishe mahakama kuwa unatambuaje kuwa ni collection akaunti ya mtandao tofauti?

Shahidi: Kwa sababu tumezioa namba tofauti, kwa mfano Airtel tumezipa 0787 na 780 kutokana na mteja anapo tuma au kupokea

Wakili wa Serikali: Ifahamishe mahakama kwamba kitu gani kinaomekana pale ambapo mtu wa mtandao mwingine anapotima kuja kwenye mtandao wa Airtel

Shahidi: Sisi tunatambua kutokana na collection akaunti namba

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo namba inayo onekana kutoka kwenye muamala  wa tarehe 20 July 2020 ni nini kinachoonekana? 

Shahidi: Hii pia ni collection akaunti namba, pale ambapo mteja anatuma kutoka airtel kwemda airtel namba itaonekana ya airtel lakini kama namba ya mtandao mwingine itaonyesha collection akaunti namba

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi kufuatia muamala wa 20 July 2020 hebu ifahamishe mahakama, ni collection akaunti ya kampuni gani?

Wakili Mtobesya: Mheshimiwa Jaji hatujalala, tuna fuatilia kinachoendelea, hilo swala la mahakama ishatoa maelekezo

Wakili wa Serikali: Basi tusomee Hizo Namba

Shahidi: CI200720. 0821.B.24154 Muamala  wa tarehe 20 July 2020, kutoka namba 0780 900174 kwenda 0787 555200 kiasi kilicho tumwa 500,000 muhusika mwenye namba ya airtel alikuwa na salio la TSh 49,646  baada ya hapo akawa na salio la  Tsh 549,646

Kinachofuata Ni aina ya Muamala, na Mwisho Inaonyesha Transactions Successfully

Wakili wa Serikali: Tusomee muamala  wa tarehe 22 July 2020

Shahidi: Transactions ID CI 200722.1528.A80515

Muamala  wa tarehe 22 July 2020 kutoka namba 0780900244 kwenda namba 0787 555200 jumla ya pesa iliyotuma ni 199,000 muhusika alikuwa na  salio 121, 296, jumla akawa na kiasi cha TSh 320,296 baada ya cash na muamala  ilikuwa successfully

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye kielelezo namba 21 cha mahakama, tusomee muamala  wa mwisho

Shahidi: Muamala  namba PP 200731.0041. B77783 muamala  wa tarehe 31 July 2020  Kutoka namba 0784779944 kwenda kwenye namba 0782 237913  kiasi kilikuwa Tsh 80,000 salio lilikuwa ni Tsh104,284 baada ya kutuma alibaki wa na TSh 23,684 natransaction ilikuwa successfully

Wakili wa Serikali: Kitu gani tena ulichokifanya baada ya kutuma hizo taarifa? 

Shahidi: Baada ya hapo niliemdelea na kazi zangu zingine mpaka nilipo itwa kituo cha kati Central kwa ajili ya kutoa maelezo ya nyaraka ambazo niliziwasilisha

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji samahani narudisha kwenye muamala  wa kielelezo namba 20,aiambie mahakama nini kilitokea?

Shahidi Kwa hiyo tarehe 20 July muamala  mwingine ukiofanyika ulikuwa ni co 0200720.1803.c00390 tarehe ni  20 July 2020 namba 0787 555200 ilituma fedha kwenda 0785191954,  kiasi kilikuwa tsh Tsh 300,000 na Muhusika alikuwa na salio la Tsh 549,646 baada ya a kutuma akabakiwa  TSh 243, 646

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji kwa upande wetu ni hayo tu!

Kibatala: Mheshimiwa Jaji tulikuwa tunaongea na wenzetu tubreak kwa 45 minutes

Jaji: Kwa hiyo tuna rudi saa nane na nusu.?

Kibatala:  Ndiyo saa nane na nusu

Jaji:Tunaahirisha kesi kwa muda wa dakika 45,mpaka saa nane na nusu ambapo tutaendelea na upande wa utetezi!

Jaji amerejea mahakamani muda huu saa 8 na dakika 57

Kesi namba 16 ya mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa mahakamani muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji quorum ipo kama awali na tupo tayari kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia tupo tayari kuendelea

Jaji anaandika kidogo wakati mahakama ipo kimya

Anamruhusu Mtobesya kusimama na kuendelea

Mtobesya anatembea kumfuata shahidi kizimbani alipo na makabrasha

Mtobesya: : Shahidi nimekusikia kwenye ushahid wako ukieleza mahakama kuwa mfumo uliyotoa taarifa, mifumo yake ya ulinzi ni FIREWALL?

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Lakini nitakuwa sahihi nikisema hukusema ni mfumo upi wa firewall lakini hukusema mfumo upi wa firewall sababu ipo tofauti tofauti

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Nilisikia pia unasema kuwa mnafanyia audit hii mifumo?

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Na audit mnayofanya siyo ya ubora wa mifumo ya ulinzi?

Shahidi: Ni mifumo yote iliyo chini ya Airtel kuangalia ubora wake na uimara wake endapo itaingiliwa inaweza kutoa alert

Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema kuwa audit inafanyiwa na credited companies za audit?

Shahidi: Inategemea

Mtobesya: Kwa hiyo kwenu wanafanya wakina nani?

Shahidi: Watu wetu wa IT

Mtobesya: Kwani hapa mahakamani ulielezea kuwa ushawahi kufanya kazi za IT?

Shahidi: Hapana sikusema

Mtobesya: Kwani ulielezea mahakama kama taarifa za audit mnazipata kutoka kwa watu wenu wa IT?

Shahidi: Hapana sikueleza

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba 15 na  16

Mtobesya: Hiyo ni barua ukiyosema ulifanyia kazi?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji akimaliza msomee kifungu kilicho ku move wewe kutoa taarifa, kifungu namba ngapi na sheria ipi?

Shahidi: Imeandaliwa chini ya  kifungu cha 34 cha sheria ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015

Mtobesya: Katika shughuli zako ulishawahi kukutana na sheria ya  makosa ya mtandao?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Wakati unatoa taarifa zako ulipata nafasi ya kupitia hicho kifungu.?

Shahidi: Ndiyo nilipitia

Mtobesya: Wakati unasoma hiyo sheria, ulipata kusoma hicho kifungu cha 36?

Shahidi: Sikukiangalia

Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema kuwa  kifungu cha 34  aliye ombwa taarifa anaweza kukataa na yule anayeomba akaenda mahakamani kuomba order?

Shahidi: Ni kweli

Mtobesya: Huwa mnalimdaje siri (taarifa) za wateja wenu?

Shahidi: Mteja kwetu ni paramount, mtu ambaye tunamthamini na tuna hakikisha taarifa zake hazitolewi kiholela

Mtobesya: Kwa mfano mimi nikija kuomba taarifa ya mtu ambaye ni mteja wa Airtel mtanipa?

Shahidi: Hatuwezi kukupa, kwa sababu taarifa hizi tunatoa kwa miongozo

Mtobesya: Kama mlikuwa na nafasi ya kukataa kutoa taarifa za wateja wenu, ili anayetaka aende mahakamani akapewe Court Order, mkawapa tuh Mnalimdaje Taarifa Za Wateja Wenu?

Shahidi: Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao kifungu cha 34 kwa ujumla, nikikupelekq kwenye hiki kifungu kina sema 34(1)……. For the Purpose of investigation a Police Officer…….. ANASOMA

Mtobesya: Kisome Pia Kifungu cha 36

Shahidi: Kifungu cha 36 kinasema…….. ANASOMA

Mtobesya: Kwahiyo 36 unasemaje pale ambapo mtu anakuwa amenyimwa taarifa?

Shahidi: Atatakiwa kuja na Court Order

Mtobesya: Kwanini sasa kama kama mlikuwa na nafasi ya  kuzuia kutoa taarifa, mkachagua kutoa taarifa?

Shahidi: Mheshimiwa mimi naamini kuwa natenda majukumu yangu kwa kufuata sheria mbalimbali siyo moja tu

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji sasa barua yako waliomba taarifa kwa sheria gani?

Shahidi: Kwa sheria ya makosa ya mtandao

Mtobesya: Soma na barua ya taarifa mlizotoa

Shahidi: Nimepokea barua yako ya tarehe 1 July 2021 yenye kumbukumbu FB/CYBER /2021/71 Airtel imeambatanisha taarifa za mihamala ya tarehe 1 June 2020 mpaka 31 July 2020 pamoja na usajili wa namba 0784779944 na 0797555200

Mtobesya: Kwa hiyo hii ndiyo barua iliyotoka kwenu.?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa naomba sasa twende kwenye kielelezo namba 17

Wakati unatoa maelezo yako nilikusikia unazungumzia swala la msajili, msajili msajili. Je huyo msajili anaweza kuonekana kwenye taarifa ya usajili?

Shahidi: Hapana hawezi

Mtobesya: Kwa hiyo mtu anawezaje kujua kuwa taarifa hiyo ilisajiliwa na fulani?

Shahidi: Ili Kufahamu aliye sajili, Unaweza Kuomba

Mtobesya: Sasa kwenye taarifa hizi ambazo unasema ni za msajili tunafahamu vipi?

Shahidi: Kwenye taarifa hizo hakuna msajili

Mtobesya: Kwenye ushahidi wako ulisema kuwa hapa hakuna msajili lakini aliomba tapatikana 

Shahidi: Sikusema hivyo

Mtobesya: Kwa hiyo ulileta taarifa tatu za usajili na zote tatu haionyeshi msajili wa hizo namba?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Nilikusikia unazungumzia kwa umaridadi sana kuhusu usajili, Je ulimueleza Mheshimiwa Jaji kwamba ushawahi kuwa msajili? 

Shahidi: Hapana Sijamwambia

Mtobesya: Nitakuuliza swali kama una utaalamu nalo utasema ndiyo kama haufahamu utasema haufahamu, Je unafahamu juu ya watu wanaitwa Hackers katika mitandao? 

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Mtobesya: Je unafahamu kuwa hao hackers wanaweza kuingia katika mifumo wakaingia kwenye mifumo na wakabadili taarifa?

Shahidi: Kwa uelewa wako

Mtobesya: Wewe unafahamu nini?

Shahidi: Ni watu ambao wanaweza kuingilia mifumo na kubadili data

Mtobesya: Ikiwemo taarifa?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Wakati unaongozwa  kuhusu intergrity ya  mifumo yenu hapa ulisema kuwa kuna watu wanaoingilia mifumo?

Shahidi: Hapana sikusema

Mtobesya: Nilisikia unasema ulienda Central Police Dar es Salaam kutoa maelezo yako, je unaweza kukumbuka au nikuombee kwa Mheshimiwa Jaji?

Shahidi: Nafikiri itakuwa vizuri zaidi nikipewa

Mtobesya: Ikague kama ndiyo hiyo, kama ndiyo yenyewe soma kwa sauti

Shahidi: ……. ANASOMA

Mtobesya: Mweleze Mheshimiwa Jaji kwenye maelezo yako kama ulisema una utaalamu wa kuingia kwenye mifumo na kutoa taarifa

Shahidi: Hapana sikusema

Mtobesya: Asubuhi nilisikia kuwa unasema ulipata trainig ya kuingia katika mifumo?

Shahidi: Hapana sikueleza

Mtobesya: Nilisikia pia asubuhi ulisema kuwa wakati una print mifumo ilikuwa intact?

Shahidi: Nilielezea ku print tu

Mtobesya: Haukuelezea ubora wake?

Shahidi: Sikuelezea

Mtobesya: Kwamba mlikuwa na mikataba na makampuni mengine ya miamala ya fedha, ipo humo?

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Je ungependa maelezo yako yaingie katika kumbukumbu za mahakama?

Shahidi: Nikipata miongozo

Mtobesya: Nakuuliza wewe, si umesema ndiyo maelezo yako?

Shahidi: Nahitaji nafasi kidogo ya kutafakari

Shahidi: Nilisha wasilisha vielelezo vya awali, naomba hii isiingie

Mtobesya: Kwahiyo hutaki?

Shahidi: Sijasema kuwa sitaki, ila nishatoa vielelezo vya awali

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba niwe guided kuwa amekubali au amekataa 

Jaji: Kwani we umesikiaje 

Shahidi: Nishajibu swali

Mahakama kichekoooooo 

Jaji: Nafikiri tumpe muda wa kushauriana na mawakili wake

Mtobesya: Lakini hairuhusiwi hiyo, nimemuuliza shahidi kizimbani sitegemei afundishwe majibu

Jaji: Nyie upande wa serikali mnasemaje?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji nafikiri kashajibu swali

Jaji: Bado hajajibu swali

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Basi wakili aendelee na cross examination

Jaji: Kui-move mahakama au cross examination?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Vyovyote vile Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji sisi tunaomba kui-move mahakama kuwa tunaomba maelezo yake aliyoyatia Polisi yaingie katika taarifa za mahakama kwa kutumia kifungu cha  154 na pamoja na 164 (1)C ya sheria ya ushahidi

Mheshimiwa Jaji 154 ndiyo nimeanza nayo kutengeneza nayo misingi inasema……. WAKILI ANASOMA

Na 164 (1) C inasema kuwa……… WAKILI ANASOMA

Sasa nilianza hivyo kwa sababu wenzetu walishaleta kesi katika mahakama hii iliyokuwa inaeleza mahakama hii, kwamba kabla ya kuchanganya shahidi na kujichanganya apewe maelezo yake awesome ze kusoma ndiyo iweze kuingia katika mahakama hii

Material to the extent kwamba wakati mahakama inafanya maamuzi  yake, kwa mujibu wa kesi ya MENDEZ ione kuwa taarifa zilizo achwa na zile zilizo chukuliwa ione kwamba nini athari yake shahidi, ichukue ushahidi: wake au iache

Kwa bahati mbaya sijabeba kesi ya Alberto Mendez, lakini ipo katika website ya mahakama

Kwa kuogezea, nasisitiza kuwa substance yote ya ushahidi ni muhimu shahidi apewe aweze kujiandaa tena ipo katika commital bundle

Tena shahidi anafanya hivyo akiwa katika witness box

Ukisoma kifungu cha 246 cha CPA, kina sema mshitakiwa apewe The Whole Substance, there is a reason to that

Kwa Kusema hayo Mheshimiwa Jaji naomba Statement iweze kuingiza ili niweze kuitumia kui-contradict

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji samahani kidogo tuna discussion

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tumesikia maombi ya wakili msomi Mtobesya aliyoyaleta kifungu cha 154 na 164 (1) C ya Sheria ya Ushahidi

Mheshimiwa Jaji wakati tukiwa tunakubali na position ya kisheria, tunakubali msimamo wa kisheria kama alivyo rejea, lakini mazingira aliyoyatanguliza (premises) aliyojemga wakati anamuhoji shahidi, hai support alichokiomba hapa mahakamani

Kile alichodai kwamba ni contradiction haijafika kuwa kiwango cha kuwa contradiction

Mheshimiwa Jaji tafsiri ya what amount to contradiction kupitia internet kupitia cambridge dictionary inatafsiri what amount is contradiction

Na inasema the fact of something being the opposite of something else or very different from something else, so that one of them must be wrong

Na hiyo inaweza kuwa accessed kupitia www.cambridgedictionary.org

Mheshimiwa Jaji shahidi ameulizwa maswali manne kuhusiana na majibu yake yakiyitangikiwa na neno “sikusema” sasa swali la msingi la kujiuliza hapa kama hakusema je hiyo ni contradiction.? na je inakinzana na nini kam kwenye statement hakipo.?

Jibu ni kwamba hakuna inachikinzana nacho

Mheshimiwa Jaji cross examination ni eneo ambalo ni muhimu katika kukamilisha mahojiano na shahidi

Na ina masharti yake  kisheria

Kama Wakili msomi mwenzetu angejielekeza kinachotakiwa  kisheria asimgeshindwa kuona kuwa premises alizozijenga ameshindwa kufikia yeye mwenyewe kwa hicho alichokiita ni contradiction

Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaona ombi hilo kwa tafsiri ya 154 na 164 (1) C kwa purpose ya kuonyesha kuwa kuna inconsistency, basi inconsistency hiyo ameshindwa kuonyesha na ombi hilo halina mashiko kisheria

Sambamba na hiyo hoja yetu, tunasema kuwa ameshindwa kufikia kiwango hicho cha kuonyesha inconsistency, ndiyo maana anaomba sasa yeye statement hiyo shahidi: aitoe, sisi tunaona yeye emefeli kwasababu maneno hayo hayajatoka kwa shahidi

Mheshimiwa Jaji wakati akiwa anawasilisha hiyo hoja alikuwa vilevile analalamika swala la non disclosure, Mheshimiwa Jaji sisi tunaona hoja hii imekuwa misplaced

Wakati wa cross examination, tena wakati i atoka na failure yake yeye mwenyewe, hoja hiyo imeletwa akatika wakati ambao siyo sahihi na haiwezi kuwa intertained

Nasisitiza tena kuwa huu ni wakati wa cross examination, Wakili Msomi angejielekeza katika kuuliza maswali

Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba ombi hilo likataliwe na Wakili aelekezwe kuendelea na cross examination kwa mujibu wa sheria

Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji addition kidogo kwa Mr Kidando

Mheshimiwa Jaji inapokuwa swala la allegation kuwa kielelezo kimeji contradict, ni swala la evidence

Mheshimiwa Jaji kinachoombwa ni document na tumeshasubmit mara a kadhaa rules za kwenye kesi za SHARIF MOHAMMED na kesi ya GEZILAHABO

Wakili MTOBESYA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji sisi hatukufika huko

Jaji Sijaelewa Vizuri

Mtobesya: Wakili Msomi, Pius Hilla anaanza a Kusema Mambo ya Competence ya Shahidi

Jaji lakini Mna nafasi na Nyinyi ya Kusimama

Mtobesya: Sawa

Wakili wa Serikali Pius Hilla Mheshimiwa anaye Omba ni Wakili Mtobesya, Whether anayeomba no sosos au Nani, Rules ni zilezile Mheshimiwa Jaji

Mheshimiwa Jaji kielelezo kinataka kuingia mahakamani bila  kufuata procedure

Mheshimiwa Jaji ni ufahamu wetu kwamba itakuwa ni kinyume cha sheria wakili kutender kielelezo katika mazingira kama hayo

Vifungu alivyovisema Mheshimiwa havitumiki hivyo

Mheshimiwa Jaji Wakili Abdallah Chavula anaomba Kidogo tuh aeleze jambo

Wakili PETER KIBATALA Mheshimiwa Jaji tumeomba dakika moja kabla ya Wakili Abdallah Chavula

Wakili Jeremiah Mtobesya: nimeshauriwa na wenzangu sababu ya muda niondoe hoja yangu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji wao wajibu tuh, tumesjajibi zaidi ya asilimia 90 kwa nini waondoke hoja yao, wao wajibu

Wakili Mtobesya: Mheshimiwa Jaji siyo jibu kwa nman yoyote, watake au wasitake wao kama wanataka waendelee ila mimi sotojibu

Wakili Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji basi tumekubali waondoe hiyo hoja

Jaji Basi statement yao warudishie

Mtobesya: Mheshimiwa na rejea kwenye kielelezo namba 20 na 21

Mtobesya: Ni namba ya nani

Mtobesya: Au Transactions Za P20 ni za Namba zipi

Shahidi: Ni namba 0787 555200

Shahidi: Ni namba ya Denis Urio

Mtobesya: Rudi kwenye kielelezo namba 20, mwambie mheshimiwa jaji kuna namba ngapi za wateja wa Airtel zaidi ya hiyo

Shahidi: sawasawa

Mtobesya: Sasa mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa hizo namba zilikuwa zina fanya transactions za namba hiyo inayoishia na 200

Mtobesya: Mliwezaje kulinda taarifa ya hao 19 wakati taarifa zao hazijaombwa?

Shahidi: Hatuna Uwezo wa kutemper na taarifa za hawa watu wengine

Mtobesya: Kwa namna hiyo unaweza kusema ulilinda taarifa za hao watu..?

Shahidi: Hizo taarifa ziliombewa na ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi, taarifa hizi unapotoa unakosa access ya kufuta au edit taarifa

Mtobesya: Unakwepa swali je hao watu wengine walilindiwa taarifa zao?

Shahidi: Ndiyo kwa sababu tulipeleka kwenye taasisi ambazo zinahusika na uchunguzi

Mtobesya: Nilisikia unasema kuwa mnamikataba na makampuni ya mawasiliano juu ya biashara ya miamala, je ulitoa mikataba hapa mahakamani?

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Kwa taarifa hiyo ilivyo unaweza kutambua namba za wateja ambao siyo wa Airtel kwamba ni namba ya mtu Fulani?

Shahidi: Kwa Taarifa hiyo jinsi  Ilivyo uwezi kuitambua

Mtobesya: Kwa taarifa uliyotupatia hapa mahakamani ya miamala, je unaweza kutuambia kuwa mtu fulani alituma. pesa kwa  ajili gani?

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia hapo

Malya: Unafahamu Makosa wanayoshitakiwa hawa Watuhumiwa Wanne

Shahidi: Hapana

Malya: Basi miye nakufahamisha kuwa mshitakiwa wa nne, Bw. Freeman Mbowe anashitakiwa kwa akuwatumia hawa pesa ya  kufanyia ugaidi

Malya: Kwenye  hiyo barua uliombwa transactions za watu wangapi

Shahidi: Haija specify

Malya: Haija specify kuwa miaamala ya namba zipi?

Malya: Tunakubaliana kuwa umeombwa mihamala ya namba ngapi?

Shahidi: Tatu

Malya: we Umepeleka mingapi

Shahidi: Miwili

Malya: Kwa Nini

Shahidi: Oversight, (Kupitiwa )

Malya: Miye siamini kuwa ulipitiwa

Malya: Hebu nisomee mhamala wa mwisho kwenye kielelezo namba 20 una involve TSh 80,000.?

Shahidi: Ndiyo elfu 80,000

Malya: Namba hiyo uliombwa  kutoa miaamala yake?

Shahidi: Ndiyo

Malya: Nikisema unaleta makusudi muamala wa Khalfani Bwire ambao umeombwa, ila kwa sababu Khalfani Bwire alikuwa alikuwa anafanya ugaidi na kingai ukaona usilete mahakamani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji bado nasimamia jibu langu kuwa nilipitiwa

Malya: Kwemye miamala ya Khalfani Bwire unasema kuna kupitiwa, je sisi tutajua kuna kupitiwa mara ngapi?

Shahidi: Hatuwezi Kujua

Malya: Sasa kwenye miamala ya Khalfani Bwire, ina onyesha alikuwa anatumiwa Fedha na Waziri wa Ulinzi Kipindi Kile Ambaye sasa Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar, ila wewe ukaona ufiche tusione miamala hiyo

Malya: Kwa mtateja wetu Mheshimiwa Jaji

Jaji: Bwana Malya unatoa wapi maelezo hayo?

Jaji: Ilikuwa Chini ya Kiapo.?

Malya: Hapana lakini wateja wetu wanatupatia taarifa za kesi yao kila siku

Jaji: Nafikiri si vyema kutaja watu wasiopo mahakamani, au mnampango wa kumuita Rais Hussein Mwinyi?

Malya: Ndiyo Mheshimiwa Jaji tutamuita tukihitaji baada ya kupata miamala Ya Bwire

Jaji: Basi naomba watu ambao hawapo mahakamani na hawajajitokeza kwenye proceedings tusiwataje sababu wanaweza wasioate nafasi ya kuja mahakamani kujitetea

Malya: Sawa Mheshimiwa Jaji

Malya: Shahidi makosa yako ya kutokuleta muamala wa Bwire, je nani atakuja kurekebisha kosa hilo?

Shahidi: Sifahamu

Malya: Je taarifa zenu za usajili (format) zina fanana?

Shahidi: Ndiyo muundo au format unafanana

Malya: Sasa hapa usmesajili watu mmoja anaitwa Mbowe, Katika Kielelezo namba 18 Je unaweza kuona sehemu ya juu imeandikwa kanda, je kanda gani?

Shahidi: Morogoro

Malya: Ukitizama pia taarifa za Denis Urio, Sehemu ya kanda kwa denis urio, ipo au haipo?

Shahidi: Ipo kwa Denis Urio

Malya: Sasa angalia kielelezo namba 17 cha Freeman Mbowe kama kuna sehemu ya kanda au mnapendelea wanajeshi.. ukiona mwambie Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Haionekani

Shahidi: Haijaandikwa

Malya: Ni sahihi sasa kwa kuwa amtu anaitwa Freeman Mbowe, hain sehemu imeandikwa Kanda ni sahihi hizo Taarifa zipo Tofauti?

Shahidi: Ndiyo Neno Kanda halijaonekana

Malya: Ulitoa hiyo clarification wakati wa chief examination?

Shahidi: Sikuulizwa

Malya: Nakushauri jibu ulitoa au hukutoa

Shahidi: Nimeshajibu

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali langu sasa

Jaji: Umeelewa swali.?

Malya: kwenye kielelezo namba 20 mhamala wa tarehe 20 July 2020, ulisema P to P maana yake ni nini?

Shahidi: Airtel kwemda Airtel

Malya: Na hiyo cash in..?

Shahidi: Namba ya muhusika  ambayo imepokea

Malya: Ikitopokea kutola kwa  wakala itaandikaje..?

Shahidi: Zote zina onekana kama cash in, kama. mteja kwa mteja ni P to P?

Shahidi: Kuna ufafanuzi

Malya: Sasa mimi interest yangu ni tarehe 20 July 2020, cash in ni wakala

Malya: Ufafanuzi utampatia dada yangu Kitali, Miye nataka majibu

Malya: Katika hawa washitakiwa wanne kuna hata mmoja kasajiliwa kama wakala?

Shahidi: Miye sifahamu

Malya: Mheshimiwa Jaji nina maswali bado kwa shahidi wetu, na muda umetutupa mkono, ningeleta ombi kwako tuhairishe hadi kesho tuendelee na mahakama

Wakili wa Serikali Robert Kidando:  Ni kweli Mheshimiwa Jaji muda umetutupa tungeomba tuhairishe mpaka kesho

Wakili wa Serikali Robert Kidando:  Mheshimiwa Jaji inategemea sasa na availability na shahidi: ambaye tulikuwa tumemuandaa kwa sababu alikuwa anauguliwa na mama yake mzazi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji tulikuwa tunaomba kama wenzetu watakuwa na shahidi, wanaweza kuja naye hata kama tukianza naye kesho si mbaya

Jaji: Basi Shauri hili lina hairishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi

Shahidi kesho ataendelea kuwa mahakamani na upande wa mashitaka mjitahidi kuleta shahidi: mwingine kesho

Washitakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho asubuhi

Jaji anatoka.

Like
1