Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ.
Mwenendo wa leo Novemba 4, 2021 wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili
Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi.
Jaji ameshaingia mahakamani na kesi imeanza kwa kutajwa namba yake. Mawakili wa upande wa Jamhuri wanajitambulisha.
- Robert Kidando
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka
- Tulimanywa Majige
Mawakili wa upande wa utetezi nao wanatambulishwa na wakili Peter Kibatala.
- John Malya
- Fredrick Kiwhero
- Dickson Matata
- Idd Msawanga
- Nashon Nkungu
- Maria Mushi
- Hadija Aron
Kesi inatajwa. Ni namba 16 ya mwaka 2021 inayomhusu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe.
Kesi inatajwa. Ni namba 16 ya mwaka 2021 inayomhusu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe.
JAJI: mshtakiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu wa nne?
Washitakiwa wote wanaitika kuonyesha kwamba wapo.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, shauri linakuja kwa ajili ya kusikilizwa, na leo tuna shahidi mmoja. Tupo tayari kuendelea.
JAJI: Upande wa utetezi?
Kibatala: Na sisi pia tupo tayari kuendelea.
JAJI: Shahidi wenu?
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji ameenda kufuatwa.
(Shahidi anaingia akiwa amevaa kaunda suti).
Majina yako?
SHAHIDI: SSP Sébastian Madembwe.
JAJI: Umri?
SHAHIDI: Miaka 46.
JAJI: Kabila lako?
SHAHIDI: Mhehe.
JAJI: Shughuli zako?
SHAHIDI: Afisa wa Polisi.
JajiL Dini yako?
SHAHIDI: Mkristo.
SHAHIDI: Mimi SSP Sebastian Madenge naapa kwamba ushahidi nitakaotoa ni kweli tupu, Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, Shahidi ataongozwa na wakili wa Serikali Pius Hilla.
WAKILI WA SERIKALI: Shahidi umesema majina yako kwa ukamilifu ni nani?
SHAHIDI: SSP Sebastian Madenge.
WAKILI WA SERIKALI: Unaishi wapi?
SHAHIDI: Iyumbu kule Dodoma.
WAKILI WA SERIKALI: Mkazi wa Dodoma tangu lini?
SHAHIDI: Mwezi wa nane mwaka 2020.
WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya hapo ulikuwa unaishi wapi?
SHAHIDI: Nilikuwa naishi Muongo la Ndege Ukonga, nikiwa ofisa wa Polisi Makao Makuu, iliyokuwa Makao Makuu Dar es Salaam.
WAKILI WA SERIKALI: Uliajiriwa lini kama polisi?
SHAHIDI: Tarehe mbili mwezi wa tisa mwaka 1999.
WAKILI WA SERIKALI: Katika Jeshi la Polisi uop kamisheni gani?
SHAHIDI: Nipo kamisheni ya upelelezi wa makosa ya jinai.
WAKILI WA SERIKALI: Kitengo gani?
SHAHIDI: Udhibiti na usajili wa silaha.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa Kizungu mnaitaje?
SHAHIDI: Arms Management and Registration Unit.
WAKILI WA SERIKALI: Kitengo hicho kinahusika na nini?
SHAHIDI: Usajili wa silaha za raia, utoaji wa leseni za kumiliki silaha, vibali vya kuingiza silaha nchini, vibali vya usafirishaji wa silaha na risasi hapa nchini, vibali vya upotoshaji wa silaha zinazoenda nchi mbalimbali kupitia kwetu. Tunatoa vibali vya uuzaji wa silaha na risasi. Yote yanahusiana na usajili wa silaha. Tunahusika pia na nchi Mbalimbali katika udhibiti wa silaha katika kutekeleza mikataba ya kikanda na kimataifa.
WAKILI WA SERIKALI: Umesema usajili wa kiraia. Je, unamaanisha nini?
SHAHIDI: Ni zile silaha zilizoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria namba 02 ya mwaka 1995. Sheria imetaja silaha zinazoruhusiwa ni pistol, riffles, short gun na silaha yoyote ambayo Bodi ya Udhibiti wa Silaha itapendekeza iingie miongoni msilaha za kiraia. Samahani Mheshimiwa Jaji, silaha nyingine ni gobole.
WAKILI WA SERIKALI: Silaha ndogo na nyepesi. Fafanua hapo.
SHAHIDI: Udhibiti wa silaha hizi tunazomiliki za kiraia, silaha ndogo ndogo ni zile ambazo mtumiaji ni mtu mmoja. Kwa mfano AK47 ni (si) silaha ndogo. Lakini silaha nyepesi, yaani Light Weapon ni Ile ambayo inatumika kwa urahisi.
WAKILI WA SERIKALI: Kwenye kitengo wewe ni nani?
SHAHIDI: Ni mrajisi wa leseni za bunduki.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa Kizungu?
SHAHIDI: Ni CEO wa Arms Register.
WAKILI WA SERIKALI: Majukumu yako wewe ni yapi?
SHAHIDI: Ni kuhakikisha kwamba napokea maombi yote ya waombaji wanaotaka kumiliki silaha. Yaliyopitishwa na Kamati za Ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya mtaa ambako mwombaji anaishi, kata, wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
WAKILI WA SERIKALI: Jukumu la pili?
SHAHIDI: Kuyakagua maombi hayo niliyoyapokea ili kuona kama yana vigezo kwa mujibu wa sheria, licha ya kwamba maombi hayo yatakuwa yamepitishwa kwenye kamati nilizozitaja. Na kwamba maombi yalikidhi vigezo huendelea kuyashughulikia ngazi inayofuata.
SHAHIDI: Na Maombi yaliyokidhi vigezo nayarudisha yalikotoka. Jukumu lingine ni kutoa vibali vya uuzaji wa silaha hapa nchini, kibali cha usafirishaji wa silaha hapa nchini na upitishaji vibali kwenda nchi jirani hasa wanatumia bandari yetu. Tunatoa vibali vya kutunza silaha (Warehouse Lisence). Tunatoa silaha Gunsmith Lisence (Kibali Cha Kufanyia Matengenezo) silaha kwa raia endapo itapata hitilafu. Na pia kutoa leseni kwa wale waonataka kumiliki silaha. Tunatunza kumbukumbu ya silaha na wamiliki wote ambao wamesajiliwa. La mwisho ni kupokea maombi ya kiuchunguzi pale silaha Inapookotwa ili tuweze kuangalia kwenye Data Base kama silaha hiyo imesajiliwa au la.
WAKILI WA SERIKALI: Mbali na maombi hayo, maombi mengine huja kwa namna gani?
SHAHIDI: Ninapozumgumzia uchunguzi ni uchunguzi wa taarifa yoyote inayohitajika kwa ajili ya shughuli ya kiupelelezi. Ni kitengo kinacho- support upelelezi katika masuala ya silaha.
WAKILI WA SERIKALI: Moja ya majukumu yako umesema ni kutoa vibali au leseni za umiliki wa silaha. Je, mchakato ukoje. Utaratibu wa mpaka mtu apewe leseni.
SHAHIDI: Wa kwanza ni kupokea maombi ambayo yamepitishwa katika Kamati za Ulinzi na Usalama.
WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya hilo anaanza na jambo gani?
SHAHIDI: Ni kununua silaha. Anaweza kununua katika vyanzo vitatu.
SHAHIDI: 1. kwenye duka ambalo wamepewa leseni ya kuuza silaha (Lisenced Dealer)
- Kwa kununua kwa mtu aliyekuwa anamiliki hiyo silaha kihalali kwa kuandikishiana mkataba wa kisheria. Na Kama silaha ya mirathi basi kikao cha ndugu wa marehemu kitakaa chini ya mwenyekiti ambaye atakuwa amepitishwa na Mahakama kwamba ni msimamizi wa mirathi kwamba ni nani wa kuirithi silaha hiyo. Endapo wataamua basi mrithi anaweza kumiliki mwenyewe kwa utaratibu wa kisheria au kuuza. Lakini mrithi atahakikisha kwamba mteja anayemuuzia anamkabidhi nyaraka zote za mirathi pamoja na mkataba walioandikishana kisheria. Muombaji anaeleza kununua nje ya nchi kwa kuomba kibali cha kuingiza hiyo silaha nchini (Import Lisence) iwe bandarini au uwanja wa ndege. TASAKI ndiye atahusika ku-clear hiyo silaha na kuhifadhi wakati mhusika ataendelea na taratibu za kuomba kumiliki silaha hiyo. Kwa hiyo katika vyanzo vyote vitatu silaha itatakiwa kuwa kwenye ghala, yeye atakuwa na nyaraka za mauziano ili ziweze kumsaidia kama attachments katika maombi yake.
SHAHIDI: Zipo fomu za umiliki wa Silaha kwa mujibu wa sheria na kanuni zinaitwa Fomu A. Mwombaji hupaswa kuzijaza na kuambatisha nyaraka zote zinazoomyesha chanzo cha silaha hiyo. Ata- attach fomu za silaha hiyo, kama mfanyabiashara basi leseni ya biashara, kitambulisho cha Taifa na nyaraka yoyote ile itakayothibitisha kutokana na kazi anayofanya.
WAKILI WA SERIKALI: Inaambatana na nini hiyo fomu?
SHAHIDI: Ni lazima kuwa na muhtasari kuanzia ngazi ya mtaa, kata, wilaya na mkoa.
WAKILI WA SERIKALI: Kingine?
SHAHIDI: Hati ya tabia njema inayotolewa na Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha……
Kibatala: Samahani Mheshimiwa Jaji. Naomba kwanza kumwombea Wakili Jeremiah Mtobesya aweze kuingia kwenye orodha yetu, ambaye amechelewa kwa sababu nilizotoa mwanzoni. Baada ya hayo nitaomba sasa wakili Mtobesya aweze kusema alichotaka.
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, shahidi hana maelezo katika kifurushi cha committal.
MTOBESYA: Kwa hiyo ushahidi wake hauwezi kuingia kwa mujibu wa kifungu cha 246 cha CPA. Hakuna maelezo yake, na nimeulizana na wenzangu kama upande wa mashitaka uliomba mwanzoni ombi lolote. Nimeambiwa hapana.
(Mahakama inakaa kimya).
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, tutaomba pia maelekezo endapo wenzetu watafanya kwa usahihi, vipi kuhusu ushahidi ambao shahidi ameshaanza kuutoa hapa mahakamani.
MTOBESYA: Na ninataatifiwa hapa na kaka yangu kwamba shahidi anatakiwa aondoke na ushahidi wake tuendelee na ushahidi mwingine kwa sababu hawawezi kupata faida baada ya sisi kusema kama wao hawakuomba mwanzoni.
(Mawakili wa Serikali wananong’onezana jambo).
(Jaji naye ameinama anaandika kidogo).
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, ombi hilo halina mashiko yoyote ya kisheria.
JAJI: Maombi au pingamizi?
WAKILI WA SERIKALI: Ahaaa! Pingamizi halina mashiko yoyote ya kisheria kwa sababu limeletwa katikati ya ushahidi wa PW6 kinyume na sheria. Na kama wangekuwa na hoja hiyo walitakiwa kufuatilia mapema. Lakini kwa wakili ambaye hakufuatilia tangu mapema proceedings hizi … Hoja yetu ya pili ni kwamba shahidi huyu aliorodheshwa tangu kipindi cha commital proceedings na anasomeka kama shahidi namba 23 tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Na hata katika barua yetu ya 11 Agosti 2021.
JAJI: Ukurasa wa ngapi?
WAKILI WA SERIKALI: Ukurasa wa 32 na jina lake linaonekana namba 23.
WAKILI WA SERIKALI: Labda lile neno S liondoke isomeke Sebastian. Lakini substance ilikuwa committed na ilisomwa katika mwenendo wa shauri hilo katika proceedings za tarehe 23 mwezi wa nane siku ambazo commital proceedings zilifanyika. Na jina lake limeandikwa Sebastian Madembwe SSP.
WAKILI WA SERIKALI: Lakini pia katika ile list ya exhibit katika ukurasa wa 33 nyaraka inayokuja kuzungumzia imekuwa listed pale namba 18 ambayo pia imesainiwa na Sebastian Madembwe SSP nilikuwa committed na substance yake ilisomwa. Kwa hiyo kwa namna yoyote ile hatukutakiwa kuleta ombi kupitia kifungu cha 289 cha CPA ili shahidi huyu aweze kutoa ushahidi wake.
WAKILI WA SERIKALI: Na tunasema pia matakwa ya Rule 8 Sub 2 ya The Economic and Organized Crime (Corruption and Procedure Rules ya 2016) takwa hili la kisheria lilitekelezwa na Mahakama. Iwe jina ama substance ya ushahidi anaotoa leo hii hakuna kitu kipya kama ambavyo wakili anajaribu kuonyesha Mahakama yako tukufu.
WAKILI WA SERIKALI: Na kama hali iko hivyo hakuna haja ya kutoa amri yoyote ile kutokana na ushahidi ambao umetolewa na shahidi kwa sababu shahidi yupo sahihi kwa mujibu wa sheria. Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba hilo pingamizi ulitupilie mbali ili shahidi wetu aweze kuendelea na ushahidi wake.
(Jaji anaandika kidogo).
MTOBESYA: Kwanza kabisa wenzangu wameni- attack personally. Sikuwapo kwenye proceedings tangu mwanzo. Mimi kuchelewa kufika sidhani kunaweza kuathiri. Sisi tunachofanya hapa ni kuisaidia Mahakama Kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria. Nimesema kwenye commital documents hakuna ushahidi wa shahidi huyu.
MTOBESYA: Substance inaongelea mambo matatu. Kwanza ni majina, ingawa yamekosea hatuna shida na hilo, pili cheti atakachotoa na tatu hakuna kile ambacho “ataongea nini mbele ya Mahakama”. Tumeongea mara nyingi kuhusu hili kuwa kuna sababu ipo ya kumpatia mtu nyaraka za ushahidi kupitia commital. Na wasipokuwa wamefanya (hivyo) upo mlango mwingine wa wao kuomba kupitia kifungu cha 289 cha Criminal Procedure Act.
WAKILI WA SERIKALI: Kama namwelewa Mtobesya anazumgumzia sasa kwamba documents kutosomwa.
JAJI: Kama nimekuelewa umesema haipo kwenye Commital Bundle.
MTOBESYA: Nimesema haipo kwenye Commital Bundle, na kwa maana hiyo haijakidhi matakwa hayo ya kwenye 246 CPA.
JAJI: Umeridhika na line yake ya argument sasa?
WAKILI WA SERIKALI: Hapana! Sikubaliani na Mtobesya. Yeye ana- argue kwamba haijasomwa. Maana akianza kujielekeza kwenye mengine na mengine inakuwa siyo sawa.
JAJI: Hoja yao ni kwamba u- argue kwa namna ambayo umeletea pingamizi.
MTOBESYA: Kwa sababu haipo, ina maana haijasomwa, na kwa sababu haijasomwa, inakiuka sheria aliyosoma kaka yangu Kidando ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2016. Kingine kaka yangu anasema P. O imeletwa kinyume na sheria kwa sababu ilishapitwa. Hiyo siyo sawa. Jambo lolote linaweza kuibuliwa pale tu tunapoona tunaenda kinyume cha Sheria. Tunalo hilo jukumu kama wawakilishi wa wateja wetu na pia kama maafisa wa Mahakama.
MTOBESYA: Kwa hiyo kama ilivyoombwa mwanzoni Mahakama itoe maelekezo na kukidhi matakwa ya Sheria. Na pia Mahakama ielekeze uwepo wa shahidi huyu. Sisi tunasema aondoke. Ni hayo tu kwa sasa Mheshimiwa Jaji.
(Jaji anainama na kuandika kidogo. Kisha ananyanyua kichwa na kusema).
JAJI: Nimesikia hoja zote. Naomba nipate muda na mimi.
JAJI: Nitapitia Sheria zote ambazo mmezitaja. Tutarudi tena saa tano na robo.
Jaji ananyanyuka na kuondoka.
Saa 5:57 Jaji anaingia mahakamani. Kesi inatajwa tena. Wakili wa Serikali anasema upande wa Jamhuri wapo tayari na hakuna mabadiliko kwa upande wao.
Wakili Kibatala anasema nao upande wao wako tayari kuendelea na kesi.
JAJI: Tuli- break kwa muda kwa nia ya kuandika maamuzi madogo, maamuzi yanalenga kutatua mgogoro wakati shahidi namba 6 anatoa ushahidi.
JAJI: Mtobesya aliieleza mahakama kuwa shahidi huyo anakiuka sheria kwa kutoa ushahidi wakati ushahidi wake haukuwa umesomwa kwenye commital Mahakama ya Kisutu. Na akaeleza kuwa hiyo inakiuka kifungu 246 cha Sheria 8 Sub ya CPA Sura ya 20. Na pia GN 267/2017 na kifungu cha 63 cha CPA na Sheria ya Uhujumu Uchumi. Hivyo inakiuka haki ya washitakiwa na wao kama wawakilishi wa washitakiwa kutokuona nyaraka hiyo na pia kwamba haikusomwa. Anaiomba Mahakama imkatae shahidi na ushahidi wake utupwe. Upande wa Serikali walikuwa na hoja mbili. Kwanza, haina mashiko kwa sababu pingamizi limekuja kwa kuchelewa na pili ushahidi wa shahidi huyo (Substance) ni sehemu ya ushahidi tu, Mahakama ijeielekeze ukurasa wa 33 ambapo inaonyesha ushahidi wake ulisomwa Mahakamani. Akaongeza kuwa ushahidi ambao anakuja kutoleta Mahakamani unakuwa umesomwa basi Shahidi anatakiwa kuendelea kutoa ushahidi wake, na kwamba kanuni zilifuatwa kama ambavyo imefanyika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mtobesya kwenye kuhitimisha kwamba hoja ya serikali ya kuchelewa haina mashiko yoyote na kwamba pingamizi linaweza kuletwa wakati wote wote. Ni Jukumu la upande wa mashitaka kutoa nyaraka mapema na orodha ya watu wanaopangwa kufanya ushahidi mahakamani.
JAJI: (Mtobesya) anaiomba Mahakama itamke shahidi amefika kinyume cha sheria na ushahidi alitoa upo kinyume cha sheria, na kwamba disclosure ni kwamba Mahakama itumie hiyo kama msimamo wake. Sasa katika hukumu nitatumia sheria zilizotaja hapo juu. Pande mbili wanakubaliana kuwa malengo mahususi ni kwamba ushahidi unaokuja kutolewa unajulikana mapema. Ushahidi wote unaotakiwa kuja Mahakama Kuu unatakiwa kujulikana, moja kwa kusomwa na kuandaliwa kwa mfumo wa kitabu na kukabidhiwa. Majukumu haya yanafanywa na upande wa mashitaka kusambazani kazi ya Mahakama. Pingamizi lolote linaweza kuja wakati wowote. Mr. Mtobesya yupo sahihi.
JAJI: Pale anapogundua kuwa kuna mapungufu anaweza kuleta Mahakamani. Ni msimamo wa sheria kuwa pale ambapo ushahidi unakuwa haujasomwa basi hauwezi kupokelewa mahakamani labda kama wataomba kama ilivyoelezwa na Wakili Mtobesya Kwenye Kifungu cha 289 CPA. Jambo linalobishaniwa ni kwamba ushahidi haukusomwa hapa Mahakamani. Mahakama inayo jukumu la kukagua kama ushahidi ulisomwa au haukusomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakati wa commital Inasoma.
JAJI: Mahakama wakati ina- examine records imeona kwenye ukurasa wa 21 kwamba maneno yafuatayo kwamba ushahidi na mashahidi yamesomwa kwa washitakiwa. Akasema Hakimu Simba tarehe 23 mwezi wa nane mwaka 2021. Akaorodhesha mashahidi 21 na jina la shahidi namba sita linaonekana katika ukurasa wa 31. Na kwamba mashahidi hao waliorodheshwa na maelezo yao yalisomwa mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Huo ndio msimamo na kumbukumbu za Mahakama, kwamba maelezo yote yalisomwa na kwamba ushahidi huo ulisomwa na Mahakama haikuishia hapo, kama nilivyosema katika ku- examine. Mahakama ikaona kuna maelezo Ya shahidi namba sita. Kumbe yalisomwa na kwamba tatizo maelezo hayo hayakuunganishwa katika kifurushi cha commital proceedings.
JAJI: Kutokwemo katika kifurushi haimaanishi kwamba ushahidi wa shahidi namba sita haukusomwa. Hivyo Mahakama inaona pingamizi halina mashiko. Lengo la pingamizi ilikuwa ku- impeach record za Mahakama. Maelezo yaliyopo Mahakamani yanaonyesha kwamba ushahidi ulisomwa, hivyo naelekeza sasa shahidi aendelee.
(Mawakili wote wananyanyuka kuonyesha ishara ya kukubaliana na jaji).
Jaji: Mara ya mwisho alisema huyo mwombaji lazima awe na cheti cha tabia njema kutoka Jeshi la Polisi.
WAKILI WA SERIKALI: Ieleze mahakama iwapo zipo nyaraka zingine zinaambatanishwa na maombi.
SHAHIDI: Zile zinazoonyesha mwombaji kuwa upo imuhimu wa yeye kumiliki silaha. Vielelezo anavyoweza kuambatanisha ni Ile kazi anayofanya.
WAKILI WA SERIKALI: Maombi ya kishawakilishwa?
SHAHIDI: Yakishawasilishwa kwangu nayakagua ili kujiridhisha kama yanakidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria.
WAKILI WA SERIKALI: Kama maombi hayajakidhi vigezo nini hufanyika?
SHAHIDI: Mambo mawili hufanyika. Moja, yanaweza kurudihswa kwenye mkoa husika Ili kukamilisha vigezo vinavyokosekana, pili, endapo itaonekana mwombaji hana sifa zilizoainishwa kisheria na kwamba hata akirekebisba vigezo vinavyopungua basi maombi hayo hubaki Makao Makuu na mkoa unaohusika hujulishwa kuwa mwombaji hana sifa.
WAKILI WA SERIKALI: Maombi yanayokidhi vigezo? Nini hufanyika?
SHAHIDI: Ni kumjulisha mwombaji kwamba amekubaliwa. Kumjulisha kwa barua na huambatanisha Kwa fomu ya maombi aliyoombea.
WAKILI WA SERIKALI: Kwenye barua hii husika mhisika anatakiwa nini?
SHAHIDI: Mwombaji anajulishwa kuwa maombi yake yamekubaliwa anatakiwa kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kwenda kukamilisha malipo. Na baada ya kukamilisha malipo arudi katika ofisi ya mrajisi. Akiwa na barua aliyopewa ya kumjulisha kuwa ameruhusiwa kumiliki silaha kutoka ofisi ya mrajisi ikiwa imeambatanishwa na risiti ya malipo ambapo malipo hayo hufanyika kwa mkuu wa polisi wilaya.
WAKILI WA SERIKALI: Nini tena hufanyika?
SHAHIDI: Kama amekamilisha malipo, kinachofuata ni hatua ya usajili.
WAKILI WA SERIKALI: Unakamilishwaje?
SHAHIDI: Kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuipa silaha husika Registration Number, Central Arm Register Number, kwa kifupi tunaita CAA number.
SHAHIDI: Ambapo kitabu hicho chenye CAA namba kitaandikwa mambo yafuatayo. Maelezo ya silaha ambayo mhusika ameomba.
WAKILI WA SERIKALI: Yanapatikana wapi.
SHAHIDI: Kwenye ukurasa wa kwanza kwenye hicho kitabu.
WAKILI WA SERIKALI: Unayapata wapi mambo ya kujaza?
SHAHIDI: Ile barua ya kumjulisha mwombaji inakuwa na maelezo yote. Pamoja na maelezo ya mhusika yanaingizwa kwenye kitabu, na kisha kuandika picha kwenye kitabu hicho chenye CAA number. Nitafungua faili na kuingiza document kwenye faili. Na juu ya faili nitaandika Registration Number, yaani CAA namba kwa ajili ya kumbukumbu.
SHAHIDI: Nikishamilisha sasa kusajili katika mfumo wa makaratasi namwingiza sasa katika Electronic Data Base.
WAKILI WA SERIKALI: Kwenye mfumo ni taarifa zipi unazoingiza?
SHAHIDI: Mfumo utanitaka kuingiza kwanza CAR number. Mfumo utanitaka niingize aina ya silaha, mtengenezaji kwa maana ya kampuni iliyotengemeza na Serial Number ambayo mtengemezaji ameigonga kwenye silaha husika.
SHAHIDI: Kuna parameters za nyongeza kama nchi ambayo silaha hiyo imetengenezwa, model number pamoja na Calibre Size. Hizi parameters nilizotaja mwishoni si za umuhimu sana bali ni za nyongeza katika kusaidia utambuzi.
WAKILI WA SERIKALI: Ulizungumzia particulars za mhusika. Ni kitu gani?
SHAHIDI: Kwa ruhusa ya Mheshimiwa Jaji, pia tunaingiza idadi ya risasi ambazo mmiliki anaruhusiwa kuzimiliki kwa wakati mmoja, idadi ya risasi anaruhusiwa kumiliki katika kipindi cha uhai wa leseni.
WAKILI WA SERIKALI: Twende sasa katika particulars za mmiliki.
SHAHIDI: Tunakuja katika particular za mmiliki. Tunaingiza kama vile fomu inayotakiwa kujazwa. Majina, uraia wake, jinsia yake, kazi yake, namba ya kitambulisho cha Taifa au mpiga kura kwa wale ambao hawana cha Taifa, makazi yake, tukiingiza kuanzia mtaa, kata anayotaka mwombaji, tarafa, wilaya na mkoa.
WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama kama kuna taarifa zingine mnazoingiza kwa simu.
SHAHIDI: Namba ya simu, anuani ya barua pepe, chanzo cha silaha kama ameinunua.
WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama ukiishakamilisha kuingiza taarifa zote kwenye mfumo kinachofuata ni nini?
SHAHIDI: Kinachofuata ni ku- save, na baada ya kubonyeza button ya ku- save hakuna chochote kitakachokuwa amended.
WAKILI WA SERIKALI: Una- save ili nini?
SHAHIDI: Kuweka kumbukumbu, kurejea kumbukumbu endapo silaha itakuwa inatafutwa. Pengine imepatikana katika tukio la uhalifu ili kujua inaweza Ikawa miongoni mwa silaha zilizosajiliwa.
WAKILI WA SERIKALI: Nyaraka zipi sasa mhusika hupewa?
SHAHIDI: Kwa mujibu wa sheria Udhibiti wa Silaha ya mwaka 2015 na kanuni zake za 2016, mmiliki anachokabidhiwa ni kile kitabu.
wa Serikali: Shahidi, sasa umesema kumbukumbu za umiliki kwa maana Hard Copy na Soft Copy, na madhumuni ni kwa maombi ya uchunguzi wa silaha yatafanyika, je, ni watu gani huleta maombi?
SHAHIDI: Sisi hupokea maombi kutoka kwenye ofisi inayopeleleza kwenye shauri husika.
WAKILI WA SERIKALI: Pengine ni wapi?
SHAHIDI: Kwenye taasisi zinazosimamia utekelezaji wa sheria mbalimbali. Mfano tumepokea maombi kutoka PCCB au kutoka taasisi inayodhibiti Madawa ya Kukevya.
WAKILI WA SERIKALI: Maombi ya uchunguzi wa silaha yanatakiwa kuwa na nini?
SHAHIDI: Yawe na taarifa tatu za msingi. Taarifa za lazima au zile za ziada. Taarifa ya kwanza iwe ni aina ya silaha. Kingine ni jila mtengenezaji (Makers name au Manufacturer name), namba zilizochongwa na mtengenezaji (Manufactural serial number) itatuwezsha kujua hii silaha imesajiliwa au haikusajiliwa.
WAKILI WA SERIKALI: Unapopokea maombi kama hayo unafanyia nini?
SHAHIDI: Kwanza tunagonga muhuri kwamba tumepokea. Baada ya hapo tunaanza kufanyia kazi.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa namna gani?
SHAHIDI: Kwa kuingiza parameters ya yale maombi katika mfumo. Sababu Parameters ni unique hata kama silaha zimetemgezwa na mmiliki huyo huyo bado panakuwa hakuna coalition.
WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kinafanya kuwa na unique Serial Number.
SHAHIDI: Hawa watengenezaji wanakutana kupeana kuhusu Serial number na kuhakikisha namba haziingiliani.
WAKILI WA SERIKALI: Mkishaingiza kwenye parameter kwenye mifumo?
SHAHIDI: Na- click OK. Kama silaha imesajiliwa italeta amatokeo chanya na ninaweza sasa kwenda kwenye Hard Copy.
SHAHIDI: Endapo marokeo yatakuwa hasi, hatutakuwa na printout yoyote.
WAKILI WA SERIKALI: Matokeo hasi ni yapi?
SHAHIDI: Nilipoingiza parameters na mfumo kutafuta nakubaini hakuna kumbukumbu zozote katika mfumo huo.
WAKILI WA SERIKALI: Mwisho wa siku unafanya nini?
SHAHIDI: Kama matokeo chanya nafanya mambo mawili kwenye taasisi iliyooomba uchunguzi ufanyike. Nita- print out mfumo umetueleza hivi na itakuwa kiambatisho katika barua yangu. Kama matokeo yatakuwa hasi itaandikwa barua na hapatakuwa na na printout yoyote.
WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama tarehe 25 Novemba 2020 ni kitu gani kilitokea?
SHAHIDI: Nikiwa ofisini kwangu makao makuu Dodoma nilipokea barua ya kufanyia uchunguzi silaha aina ya bastola.
WAKILI WA SERIKALI: Ilitoka wapi?
Shahidi:Makao Makuu madogo Police Dar es Salaam.
WAKILI WA SERIKALI: Idara gani?
SHAHIDI: Idara ya Upelelezi Makosa ya Jinai. Barua ilinitaka kufanya uchunguzi wa aina ya silaha bastola, mtengenezaji ni Luger na Serial Number A5340.
WAKILI WA SERIKALI: Maombi hayo uliyafanyia kazi kwa namna gani?
SHAHIDI: Kama ifuatavyo: Kwanza nilijiridha matokeo ya silaha yanaweza kunifanya niendelee. Nikaingiza parameter kwenye mfumo. Na matokeo yakawa silaha hiyo haijawahi kusajiliwa.
WAKILI WA SERIKALI: Baada ya matokeo hayo?
SHAHIDI: Niliandika barua ya matokeo ya uchunguzi.
WAKILI WA SERIKALI: Uliandika kwenda kwa nani?
SHAHIDI: Kwa mwombaji aliyeomba uchunguzi kufanyika.
WAKILI WA SERIKALI: Ulimweleza kitu gani?
SHAHIDI: Nilieleza kwamba kufuatia uchunguzi uliofanyika, sihala haijawahi kusajiliwa.
WAKILI WA SERIKALI: Barua yako uliyoandika ukiiona utaweza kuitambua?
SHAHIDI: Nikiletewa naweza kuiona na kuitambua.
WAKILI WA SERIKALI: Utaitambuaje?
SHAHIDI: Nitaitambua kwa kuangalia majina yangu pamoja na sahihi, yani siganture.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji shahidi anaonyesha uwezo wa kuutambua kwa ridhaa ya mahakama naomba kumuonyesha.
WAKILI WA SERIKALI: Tazama nyaraka hii ninayokuonyesha.
SHAHIDI: Nimeiona.
WAKILI WA SERIKALI: Mweleze Jaji nyaraka hiyo ni kitu gani?
SHAHIDI: Barua niliyoandika kuonyesha sahihi yangu mwenyewe.
WAKILI WA SERIKALI: Kingine?
SHAHIDI: Kuna majina yangu pamoja na wadhifa nilionao.
WAKILI WA SERIKALI: Unaiomba nini Mahakama?
SHAHIDI: Naiomba Mahakama kwamba barua hii inayoonyesha taarifa ya kiuchunguzi ipokelewe na Mahakama kama ushahidi.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji shahidi anaomba nyaraka hii Ipokelewe.
(Wanapelekewa mawakili wa utetezi).
Mtobesya:Hatuna pingamizi.
MALLYA: Hatuna pingamizi.
Fredrick Kiwhelo: Hatuna pingamizi.
Kibatala: Hatuna pingamizi.
(Sasa anapelekwa Jaji).
JAJI: Basi tunaipokea barua hii inayoelekezwa kwa ASP Msangi kama kielelezo namba 10.
JAJI: Shahidi naomba utusomee.
SHAHIDI: Barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai CID HQ CAR C12 VOL VII, kwenda kwa Msangi. Yahusu kupatiwa taarifa ya bastola Leuven A5340. Rejea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai CID HQ CAR C12 VOL VII Kwenda kwa Msangi. Ofisi imefanya uchunguzi wa silaha aina ya Luger A5340 haikusajiliwa na ofisi hii.
WAKILI WA SERIKALI: Barua yako ni ya tarehe ngapi?
SHAHIDI: 15/03/2021.
WAKILI WA SERIKALI: Unahusu nini?
SHAHIDI: Kufanya uchunguzi wa silaha Luger namba A 5340.
WAKILI WA SERIKALI: Uchunguzi ulikuwa unataka kubaini jambo gani?
SHAHIDI: Kubaini taarifa ya silaha niliyoitaja endapo inamilikiwa na mtu yoyote.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa kielelezo cha Mahakama namba 10 (barua yako) matokeo ya uchunguzi wako ni nini?
SHAHIDI: Kumbukumbu za silaha aina ya bastola yenye kumbukumbu namba A 5340 haijawahi kusajiliwa.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa barua yako kwenye “Yahusu”, mojawapo ya vitu ulivyoandika jalada ndani ukirejea kumbukumbu namba za barua ya aliyekuleta no ya 15 Novemba 2020, eleza Mahakama namba sahihi hapo ni ipi?
SHAHIDI: Barua ambayo tuliletewa maombi ya kufanya uchunguzi ilionyesha kumbukumbu ya jalada husika, ili kumsaidia aliyeomba taarifa hiyo, kwamba inahusiana na kile alichokiomba. Kwenye barua hii ambayo tuliipokea ni ya tarehe 15 CID HQ SO. 63 VOL XI / 41/25, Novemba 2020. Ukija kumbukumbu ya jalada ni CD /IR /2097 /2021.
SHAHIDI: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji nilichobaini hapa kwa haraka haraka palikuwa na mistake ya kiuandishi. Naomba msamaha Mheshimiwa Jaji kwa mapungufu ya yalijitokeza.
MTOBESYA: Objection! Anachokifanya shahidi hakiruhusiwi. Document inatakiwa kujieleza yenyewe na wenzetu wanajua hicho cha kumwomba msahama Jaji hakiruhusiwi.
Kibatala: Kwa kuongeza hapo, kifungu 63 ya Sheria ya Ushahidi na 64 (1) ya Sheria ya Ushahidi inazuia hapo.
WAKILI WA SERIKALI: Pamoja na vifungu walivyorejea vya Sheria ya Ushahidi hakuna mahala popote ambapo shahidi anazuiwa kufafanua ushahidi wake, na shahidi yupo kizimbani na yupo chini na mwongozaji wa dodoso nafikiri wamesoma vifungu bila kujipa muda.
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji sidhani kama tunatakiwa kujiingiza kwenye mambo yaliyo wazi. Basi tupewe muda tulete nyaraka. Hayo ni mambo yapo wazi tangu tupo shule.
JAJI: Nafikiri kifungu kipo wazi kwamba documents haiwezi kufanyiwa marekebisho.
JAJI: Lakini anachokifanya yeye anafafanua, hafanyi marekebisho. Sasa kwenye maamuzi ya Mahakama itarejea hivyo vifungu ulivyotaja.
MTOBESYA: Nina mtazamo tofauti. Prove ya documents wakati huu ambapo Mahakama imeshapokea, ndiyo tunasema sheria inakataza.
JAJI: Ndiyo sasa hiyo itafanyika wakati wa Maamuzi ya Mahakama.
JAJI: Labda kama una wasowaso Mahakama haitatafsiri sheria vizuri.
MTOBESYA: Hapana.
JAJI: Basi iachie Mahakama.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa hiyo shahidi ulikuwa unasema kumbukumbu ya jalada?
SHAHIDI: Kumbukumbu ya jalada iliyopo kwenye taarifa CD IR 2097 2021 na ilipaswa kusomeka CD IR 2097 2020.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kuwasilisha.
Kibatala: Mheshimiwa Jaji kabla hujamwalika mshitakiwa wa kwanza … Kwa kuwa sisi sote wawakilishi wa washitakiwa. VIfurushi vya commital, hatuna statement ya shahidi ili tuweze kutumia wakati wa cross-examination. Na tunatumia maombi haya chini ya kifungu cha 264 cha Sheria ya Ushahidi.
JAJI: Upande wa Serikali? Mna pingamizi na hilo?
WAKILI WA SERIKALI: Hapana.
JAJI: Tukubaliane tuna- break kwa muda gani?
Kibatala: Tumekubaliana tu- break kwa dadika 45. Turudi hapa saa nane na robo.
JAJI: Tunahairisha kwa muda mpaka saa nane ne robo. Naelekeza maofisa wangu wawapatie hizo nyaraka.
Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama.
Saa 8:22 Jaji ameingia Mahakamani. Kesi inatajwa. Ni kesi namba 16 ya Mwaka 2021 ambayo ni Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire na wenzake.
WAKILI WA SERIKALI: Tupo tayari kuendelea.
JAJI: Upande wa utetezi?
Kibatala: Kwa ruhusa yako tupo tayari kuendelea.
JAJI: Sawa. Wakili wa mshtakiwa wa kwanza?
Mtobesya Ananyanyuka.
MTOBESYA: Shahidi, unakumbuka ulishawahi kuandika maelezo Polisi?
SHAHIDI: Nakumbuka.
MTOBESYA: Unakumbuka uliyasoma maelezo yako na ukahakikisha kwamba ni sahihi? Unakumbuka uliandika siku gani ya tarehe ngapi mwezi na mwaka?
SHAHIDI: Tarehe 20 mwezi wa tatu mwaka 2021.
MTOBESYA: Kuanzia wakati huo mpaka sasa ni muda gani umepita?
SHAHIDI: Miezi saba.
MTOBESYA: Nitakuwa sahihi nikisema wakati unaandika memory yako ilikuwa sahihi wakati unaandika maelezo Nitakuwa sahihi wakati unaandika maelezo yako ulikuwa umeshaandika barua Iliyopokelewa kama kielelezo namba 10?
SHAHIDI: Sahihi.
MTOBESYA: Uliongelea pia kuhusu hiyo barua?
SHAHIDI: Rudia swali.
MTOBESYA: Kwemye maelezo yako unakumbuka uliongelea barua uliyoitoa? Lakini hukukumbuka Machi wakati ule kama ulikosea jalada namba umekuja kukumbuka leo?
SHAHIDI: Kwenye maelezo yangu nilikuwa nimesimamia kazi ya kile nilichokifanya kuhusu uchunguzi … eeehh … eeeeeh….
MTOBESYA: Malizie hiyo eeeeeh!!
MTOBESYA: Barua yenye matatizo ya kiuandishi ndiyo hiyo hiyo ulikuwa unaielezea?
SHAHIDI: Tatizo la kiuandishi lilikuwa kwenye jalada.
MTOBESYA: Ndiyo nakuuliza sasa barua yenye matatizo ya kiuandishi ndiyo hiyo hiyo uliyoifanyia uchunguzi?
SHAHIDI: Sahihi.
MTOBESYA: Ulitaja Sasa mapungufu ya barua yako?
SHAHIDI: Sikumbuki kama nilitaja.
MTOBESYA: Mheshimiwa naomba original statement ya shahidi aweze ku- refresh memory.
(Mawakili wa Serikali wanaitafuta).
(Mtobesya anampatia shahidi).
MTOBESYA: Angalia kama haya ndiyo maelezo ya kwako uliyoyaandika polisi kama ni ya kwako kwa mujibu wa kesi hii.
SHAHIDI: Ndiyo yenyewe.
MTOBESYA: Soma yote kwa sauti ili tuone kama kuna sehemu uliomba kurekebishwa.
JAJI: Sorry, kwani alisema yeye aliandika?
MTOBESYA: Alisema hakumbuki. Nimemwambia asome tusikie kama alisema.
MTOBESYA: Unless kama Mahakama ina maoni tofauti aseme hakuna tuishie hapo.
JAJI: Anaposema hakumbuki, naona ungem- lead labda. Kusema asome statement yote naona mmh! Sijui lakini.
SHAHIDI: Kwenye maelezo CD IR 2097 2020.
MTOBESYA: Unasoma wapi?
SHAHIDI: Juu kabisa.
MTOBESYA: Tupo chini hapo ndiyo kwenye content yako.
SHAHIDI: Hakuna sehemu niliyoandika.
MTOBESYA: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji kwamba katika maelezo yako hiyo kumbukumbu namba.
SHAHIDI: Nakumbuka ilikuwa 15 Machi 2021 baadae nikaja kuandika maelezo, kwa hiyo makosa ya kibinadamu tu.
MTOBESYA: Kwa hiyo kipengele hicho kwenye maelezo yako kipo au hakipo?
SHAHIDI: Hakipo.
MTOBESYA: Mheshimiwa narudisha kielelezo.
MTOBESYA: Umesema ulifanya kazi kwa kutumia mfumo, Je, uliweza ku- demonstrate namna huo mfumo unafanya kazi?
SHAHIDI: Issue ya kuwaita watu ili waweze kushuhudia ninachokifanya ni suala lingine.
MTOBESYA: Je, uliwahi kufanya?
SHAHIDI: Ndiyo. Mara yangu ya kwanza.
JAJI: Kuna sehemu hamwelewani naona.
MTOBESYA: Labda nirudie swali.
MTOBESYA: Ulionyesha wakati unalekezwa na wakili wa Serikali namna mfumo unavyofanya kazi?
SHAHIDI: Sikuonyesha.
MTOBESYA: Naomba kuishia hapo.
JAJI: Mallya?
MALLYA: Dhumuni la usajili wa silaha ni kudhibiti silaha isifanye uhalifu?
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Kwa hiyo wewe ulipewa silaha kuchunguza ni rahisi kujua kama ilifanya uhalifu?
SHAHIDI: Mimi naletewe kuchunguza silaha ni ya nani.
MALLYA: Majibu negative unatazamaje kujua kama ni negative?
SHAHIDI: Kwenye results inasema ‘No Records’.
MALLYA: Kwa hiyo ‘No Records’ ndiyo results?
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Sasa ulisema hapa mahakamani leo kuwa results ni ‘No Records’?
(Shahidi anakaa kimya bila kujibu)
MALLYA: Mheshimiwa Jaji nasubiri jibu.
SHAHIDI: Nilicho- present leo ndiyo kilichokuwapo.
MALLYA: Kwa hiyo umeleta au hujakileta?
SHAHIDI: Hakipo.
MALLYA: Umeingia polisi ukiwa na miaka 24?
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Kwa hiyo una uzoefu wa miaka zaidi ya 20.
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Hicho kitengo una muda nacho gani?
SHAHIDI: Miaka 20.
MALLYA: Ulipata kujua hiyo silaha imepatikana wapi?
SHAHIDI: Hiyo siyo kazi yangu.
MALLYA: Kwa hiyo wewe unatolea majibu ya uchunguzi silaha iliyosajiwa tu?
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Ulizungumzia ufanisi wa huo mfumo wakati unaongozwa?
SHAHIDI: Data base ipo vizuri na ina speed.
MALLYA: Ulizungumzia hilo suala?
SHAHIDI: Sikuzungumzia.
MALLYA: Nilikusikia kwamba ukibonyeza ‘save’, huwezi kufuta bila ruhusa ya admn.
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Je, kama hukueleza Admin ndiyo mwenye mandate vipi kama admin alibadilisha umiliki wa silaha ya Kingai aweze kumbambikia mtu?
SHAHIDI: Adimn hana mandate ya moja kwa moja.
MALLYA: Sasa unabadili ushahidi wako?
SHAHIDI: Hapana kuna mambo sikuulizwa.
MALLYA: Je, ulielezea namna Admin anavyotoa ruhusa?
SHAHIDI: Sikueleza.
MALLYA: Ulisema pia kuna taarifa unazitumia, je, ulipata mazingira ya serial number kufuta na wahalifu?
SHAHIDI: Ni sahihi.
MALLYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji sasa namna kama hiyo inaweza kujitokeza.
SHAHIDI: Endapo parameters zimefutwa tunashirikiana na watu wa ballistics.
MALLYA: Kwa hiyo tunakubaliana parameters zako siyo kitu pekee cha kutambua silaha.
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Kwa hiyo ulielezea wakati unaulizwa?
SHAHIDI: Hapana. Sikueleza.
MALLYA: Umewahi kupata mazingira ambapo namba imefojiwa kutoka namba 04 kwenda namba 07?
SHAHIDI: Unajua kwa mazingira yangu.
MALLYA: Jibu swali shahidi.
SHAHIDI: Issue za kutempa hatujazishuhudia.
MALLYA: Ulieleza kwamba uliletewa barua tu siyo bastola.
SHAHIDI: Ndiyo.
MALLYA: Kwa hiyo hujajisumbua kama namba ulizoletewa zilikuwa tempered?
SHAHIDI: Siyo jukumu langu.
MALLYA: Unafanya kazi siku ngapi katika wiki?
SHAHIDI: Maasa 24 kwa siku saba.
FREDRICK: Ni kweli tarehe 25 ulipokea barua kutoka kwa ASP Msangi?
SHAHIDI: Ndiyo nilipokea.
FREDRICK: Mpo wa ngapi kwenye hicho kitengo?
SHAHIDI: Tupo 20.
FREDRICK: Barua ya ASP Msangi Ilikuwa inakutaka ufanye nini?
SHAHIDI: Kutoa majibu ya umiliki.
FREDRICK: Wewe ulitoa taarifa ya umiliki au uchunguzi?
SHAHIDI: Nilifanya uchunguzi nikatoa taarifa ya umiliki.
FREDRICK: Barua yako ya majinu ni ya uchunguzi au umiliki?
SHAHIDI: Umiliki.
FREDRICK: Ni sahihi kwamba mnafanyia uchunguzi siku hiyo hiyo mnapopokea barua?
SHAHIDI: Ndiyo.
FREDRICK: Wewe ulipokea barua siku gani?
SHAHIDI: 25 /11/2020.
FREDRICK: Ukatoa majibu lini?
SHAHIDI: Tarehe 15 Machi 2021.
FREDRICK: Ni muda gani umepita?
SHAHIDI: Miezi mitano.
FREDRICK: Je, katika majukumu yako ulitaja jukumu lako la kutaja umiliki?
SHAHIDI: Hapana.
FREDRICK: Ni kweli kuna njia mbili za kumiliki silaha?
SHAHIDI: Swali sijaelewa.
FREDRICK: Katika maelezo yako ulisema mtu anaweza kumiliki silaha kwa njia ya kuingiza ndani ya nchi, kununua ndani ya nchi na kama amerithi. Sasa nakuuliza je, kuna namna mbili tu za kumiliki silaha?
SHAHIDI: Si kweli.
Kibatala: Kielelezo cha mashtaka namba 10 umetaja barua ya tarehe 25 Novemba mwaka 2020, je, ni sahihi Kwamba barua hii ndiyo chanzo chote cha wewe kuandika barua?
SHAHIDI: Sahihi.
Kibatala: Ni sahihi kwamba bila barua hiyo wewe usingeandika hiyo barua?
SHAHIDI: Ndiyo sahihi kabisa.
Kibatala: Siyo kawaida yako kuandika tu barua?
SHAHIDI: Itakuwa kinyume…
Kibatala: Je, hiyo barua iliyokufanya uandike barua umekuja nayo?
SHAHIDI: Sikuja nayo.
Kibatala: Kwa ufahamu wako wewe ni muhimu au siyo muhimu?
SHAHIDI: Kwa Upande wangu sikuona umuhimu wa kuja nayo.
Kibatala: Na kwa hiyo barua ndimo ambapo tungepata details za hiyo bunduki ambayo wewe ulipswa uifanyie uchunguzi?
SHAHIDI: Sahihi kabisa.
Kibatala: Na ndiyo humo tungeona namba CZ 100, Calibre 9mm. Hatuwezi kuona popote zaidi ya hiyo barua.
SHAHIDI: Sahihi kabisa.
Kibatala: Hujazunhumza kabisa kuhusu CZ 100 9MM za uliyokuwa unachunguza kwenye hiyo barua uliyoandikiwa.
SHAHIDI: Sahihi kabisa.
Kibatala: Na ni sahihi kabisa hujazunhumza kuhusu CZ 100, calibre 09mm.
SHAHIDI: Sahihi sikuzungumzia.
Kibatala: Na kuhusu Electronic Data Base ulizungumza kuhusu mmiliki wa risasi.
SHAHIDI: Kwenye electronic data base inaonyesha kuwa idadi ya risasi za kutumia wakati wa uhai wa leseni.
Kibatala: Je, katika huo mfumo wa usajili wa bunduki na risasi ni kitu kimoja au tofauti?
SHAHIDI: Ni kitu kimoja.
Kibatala: Kwa hiyo nikishasajiliwa bunduki naona na risasi zizlizopo? Mfano TRA umiliki wa gari unaonyesha na kiasi cha mafuta kilichomo?
SHAHIDI: Hapana.
Kibatala: Kwa hiyo mfano niondoe.
SHAHIDI: Ndiyo.
Kibatala: Je, risasi zinasajiliwa?
SHAHIDI: Hazisajiliwi.
Kibatala: Na hujazungumza kuhusu risasi.
SHAHIDI: Sijazungumzia.
Kibatala: Na wala kwenye barua p10 hujazungumzia kuhusu risasi.
SHAHIDI: Ni sahihi kabisa.
Kibatala: Kuna swali umeulizwa kuhusu umiliki (Possession), Je mtu aki- import bunduki inakwenda wapi?
SHAHIDI: Lisenced Warehouse.
Kibatala: Wewe katika system yako muda huo inasomeka nini?
Shahidi” Muda huo inakuwa haijaingizwa kwenye mfumo.
Kibatala: Ulisema chochote a kuwa inawezekana bastola ile inaweza kuwa imetoka Licensed Warehouse?
SHAHIDI: Sikusema chochote.
Kibatala: Ulisema hiyo possibility kwenye hiyo barua yako?
SHAHIDI: Sikusema.
Kibatala: Ulitaka Jaji akusemehe kwa makosa ya kumbukumbu namba, je, ni sahihi kwamba ili tukusamehe ni lazima marekebisho yako tuangalie kwenye barua (mama) ambayo yenyewe ndiyo ina mwaka na sahihi?
SHAHIDI: Sahihi kabisa.
Kibatala: Na barua hiyo hujaitoa Mahakamani.
SHAHIDI: Ni sahihi kabisa.
Kibatala: Kwa hiyo sasa msamaha wako unaelea Henry Ani kwa sababu hatuna control.
SHAHIDI: Ni sahihi kabisa.
Kibatala: Hii barua yako inaonekana ulikuwa unaipeleka kwa ASP H. MSANGI, je, kuna mtu anaitwa Inspector Swila. Je, ulimtaja?
SHAHIDI: Sikumtaja.
Kibatala: Kwa hiyo akisema Inspector Swila kuwa yeye ndiyo aliyeandika hiyo barua atakuwa anasema ni uongo?
SHAHIDI: Mimi nilipewa na ASP H. Msangi.
Kibatala: ASP H. Msangi hukumu- address kwa bahati mbaya? Ni kwa sababu yeye ndiye alikuandikia barua mama, akija Inspector Swila kasema ulimpelekea majibu ya uchunguzi atakuwa mwongo?
SHAHIDI: Mimi najua ASP H. Msangi.
Kibatala: Wakati unaandika barua ofisi yako ilikuwa chini ya Mkurugenzi ya Makosa ya Jinai?
SHAHIDI: Ndiyo.
Kibatala: Ni sahihi wewe na Msangi mlikuwa mpo wote chini ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai?
SHAHIDI: Ndiyo.
Kibatala: Kama serial number ikichezewa ikafutwa, je, hilo ni jukumu la nani?
SHAHIDI: Jukumu la ballistic.
Kibatala: Umesema ulipokea barua ukagonga barua na utaratibu wa kupokea barua lazima pawe na kitabu ili isajiliwe kuingia ofisini kwenu.
SHAHIDI: Ikihitajia nitaileta.
Kibatala: Lakini hapa hujaitoa.
SHAHIDI: Hapa sijaitoa.
Kibatala: Ulitoa maelezo kwa jaji kwanini hiyo register hukuleta kama sababu ni nzito au kubwa?
SHAHIDI: Sababu sikutoa.
Kibatala: Ulisema kwamba result ni negative?
Shahidi” Ndiyo.
Kibatala: Je, ulifafanua kwa Jaji kwanini hukuleta hiyo negative results?
SHAHIDI: Sikufafanua.
Kibatala: Unafahamu kwamba ushahidi wako lazima upitie sehemu kadhaa? Mahakama lazima ipime ushahidi wako?
SHAHIDI: Hiyo nafahamu.
Kibatala: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji kama ulifafanua kwanini ulishindwa kuleta extract ya negative results.
SHAHIDI: Sikufafanua.
Kibatala: Nilisikia kwamba kuna typing error kwenye P10.
SHAHIDI: Ndiyo.
Kibatala: Sasa Mahakama itajuaje kama hakuna tena makosa ya kibinadamu humu?
SHAHIDI: Ni jukumu la Mahakama sasa kupima.
Kibatala: Kuna sheria yoyote au kanuni yoyote ambayo inasema usilete barua mama, report iwe inajitegemea?
SHAHIDI: Hakuna.
Kibatala: Ni wewe tu uliamua? Swali langu la mwisho. Unakubaliana na mimi kuwa hakuna kosa linajitegemea kumiliki silaha bila kibali?
SHAHIDI: Ndiyo.
Kibatala: Sheria inaitwaje?
SHAHIDI: Inaitwa Sheria ya Umiliki na Udhibiti wa silaha kifungu cha 20.
Kibatala: Mheshimiwa Jaji sina mengine.
WAKILI WA SERIKALI: Shahidi umeulizwa maswali mengi kuhusiana na barua mama. Ieleze Mahakama uliposema hukuona umuhimu ulimaanisha nini.
SHAHIDI: Ile ilikuwa inaonyesha guidance ya uchunguzi ninaopaswa kufanya. Baada ya kukamilisha kwangu sikuona kama kuna ulazima wa kuleta ile barua.
WAKILI WA SERIKALI: Uliona umuhimu kitu gani.
SHAHIDI: Taarifa ya uchunguzi.
WAKILI WA SERIKALI: Ieleze Mahakama ulifanyia kazi jambo gani?
SHAHIDI: Particulars nilizozitumia kutoka kwenye barua mama, ndiyo key Issues katika uchunguzi wa umiliki wa silaha.
WAKILI WA SERIKALI: Elezea kuhusu tukio la uhalifu.
Kibatala: Objection! Hayo ni mambo mapya.
SHAHIDI: Tunapopokea taarifa hizo na majibu kwamba ni chanya, Data Base Inaonyesha silaha inamilikiwa na mtu fulani tuna Command Button, kisha report Inatoka.
MALLYA: Objection! Hiyo ni fact mpya tunapinga.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji sijui lakini ni maoni yetu kwamba cross examination ndiyo imeibua extract kuhusu negative results. Ameulizwa hiyo, shahidi aachwe aeleze. Kama wakili angeona siyo issue sana alipaswa asiibue. Ni hayo tu. Tunaomba shahidi ajibu.
Kibatala: Wakili hakatai those are new matters anajaribu ku- exclude new matters.
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji sahamani. Halafu hakuongelea Printability ya negative results.
JAJI: Hoja mmelewa ya upande wa utetezi? Hapa anakuja na ufafanuzi kwamba sikuweza kucommand. Ila print na mimi nakubaliana nao kwamba hilo ni jambo jipya ambalo hakuzungumza na sasa anataka kuzungumza.
WAKILI WA SERIKALI: Shahidi nitakuuliza suala hilo hiyo kama majibu yakiwa negative uwezi kuprint, kwanini sasa?
SHAHIDI: Uki- command ina- print ..
MALLYA: Objection!
Kibatala: Objection!
MTOBESYA: Objection!
JAJI: Nafikiri unaweza kwenda kwa njia nyingine.
WAKILI WA SERIKALI: Nilisikia umeulizwa kuhusu Inspector Swila kwamba ile barua mama kaandika nani.
SHAHIDI: ASP H. Msangi.
WAKILI WA SERIKALI: Kwamba ile barua mliandikiana wenyewe? Hebu fafanua.
SHAHIDI: Ni sahihi kabisa kwamba vitengo vyote vipo kwa DCI. Yeye kazi yake ni kuhakikisha je, tuna mfumo? Lakini inapokuja suala la kiuchunguzi yeye hahusiki tena. Ofisi yangu ya mrajisi kama mtaalamu wa kufanya uchunguzi ni kufanya uchunguzi bila kuingilia na naamuzi au msukuko wowote wa mkurugenzi wa makosa ya jinai.
WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa kuhusu forgery, elezea Mahakama ulichunguza nini?
SHAHIDI: Mimi sikuletewa silaha, nilichunguza barua na particulars zilizokwepo kwenye zile barua zilikuwa ni Key Parameters zillizoniwezesha mimi kufanya uchunguzi.
WAKILI WA SERIKALI: Uliulizwa pia kuhusiana na silaha inayoingizwa nchini kutoka nje. Wewe maelezo yako hayajaondoa possibility.
SHAHIDI: Mfumo wetu wa silaha na usajili, mfumo wetu unamuimgiza mwishoni kabisa baada ya silaha Imeshaingia nchini au kukamilisha utaratibu wa malilo. Silaha itakuwapo kwenye Lisenced Private Warehouse.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji mimi naishi hapo kama kuna wenzangu waendelee. Wenzangu na wao hawana.
JAJI: Shahidi tunakushukuru. Unaweza kuendelea.
WAKILI WA SERIKALI: Ndiye Shahidi tuliyekuwa naye leo. Tunaomba ahirisho hadi kesho tuweze kuendelea na shahidi mwingine.
JAJI: Upande wa utetezi?
Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi.
(Jaji anaandika kidogo).
JAJI: Basi maombi yakiyoletwa na mashitaka mahakama inakubali mpaka kesho saa tatu asubuhi. Upande wa mashitaka mnaelekezwa kuleta mashahidi washitakiwa wataendelea kuwa chini ya magereza mpaka kesho