Kesi ya Mbowe: Mawakili wanyukana kwa pingamizi, jaji aahirisha uamuzi hadi kesho

Jaji: “natazama muda, naona kama sitaweza kufanya maamuzi muda huu. Kwa maana hiyo, naomba tuahirishe mpaka kesho asubuhi.”

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 08 Novemba 2021.

Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa 

Jaji: Ndiyo. 

Wakili wa Serikali Robert Kidando anasimama Wakili Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo  na Abdallah Chavula, Jenitreza Kitali, Pius Hilla, Nassoro Katuga, Esther Martin, Tulimanywa Majige, Ignasi Mwinuka. Wote tunaiwakilisha Jamuhuri.

Wakili Peter Kibatala na Yeye amesimama na Kuanza Kuwatambulisha: Maria Mushi, Evarista Kisanga, Hadija Aron, Alex Massaba, Idd Msawanga, Seleman Matauka, Dickson Matata, Nashon Nkungu, Fredrick Kihwelo, John Mallya, Peter Kibatala.

Jaji anaita Washitakiwa wote Wanne
 Maria MushiEvaresta KisangaHadija AronAlex MassabaIdd MsawangaSeleman MataukaDickson MatataNashon NkunguFredrick KihweloJohn Malya
Na wote wanne wanaitika Wapo
 Wakili wa Serikali Shauri hili lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna Shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea 

Wakili Peter Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji
 Wakili wa Serikali Mmoja anaenda Kumfuata Shahidi
 Shahidi anapita
 JAJI yupo kimyaaaa anaandika
 Wakili Peter Kibatala anaomba radhi kwa kuchelewa kidogo.

Jaji: Shahidi wa ngapi huyo? Wakili wa Serikali: Shahidi wa nane 
 Jaji: Majina yako?
 Shahidi: Superitendent Jumanne Malangahe

Jaji :Umri?
 Shahidi : Miaka 46 

Jaji: Kabila
 Shahidi: Msukuma
 Jaji Shughuli yako
 Shahidi: Afisa wa Polisi

Jaji: Dini yako?

Shahidi: Muislamu
Jaji: Karibu

Wakili wa Serikali Asante
 Shahidi Wallah wabillah taala nathibitisha kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie
 Shahidi Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha
 Wakili wa Serikali Kitambulisho Bwa Jummane Unafanya Kazi gani
 Wakili wa Serikali Majukumu yako ni nini
 Shahidi Kuzuia uhalifuKukamata UhalifuKupeleleza Makosa ya JinaiKuwaongoza Askari Waliochini yangu ktk Shughuli ya Upelelezi
 Shahidi Alikuwa afande ACP Ramadhan Kingai
 Wakili wa Serikali Ukiwa Mkuu Wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Je Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha Mwaka 2020 alikuwa ni nani
 Wakili wa Serikali Katika Majukumu yako ya Upelelezi na Kusimamia Askari waliopo Chini yako no Shughuli gani katika Upelelezi hufanyika
 Pamoja na Kuku Sanya Vielelezo  namambo Mengine kutokana Aina ya tukio
 Shahidi Baada ya Shauri Kufunguliwa, ndipo Upelelezi Unapoanza kwa kuwakamata wa husika, Kupelele Shauri na Kukagua eneo la Tukio
 Shahidi 04 August 2020 nilikwepo katika Kituo Changi cha Kazi, Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Nikiwa Ofisni Kwangu nilipigiwa Simu na Afande Kingai
 Wakili wa Serikali Elezea hapa Mahakamani Tarehe 04 Mwezi August 2020 ulikuwa wapi
 Wakili wa Serikali ilikuwa Muda gani wakati anakupigia Simu
 Shahidi Ilikuwa Muda wa Saa 12 na Kitu
 Akinitaarifu kuna Safari Ni jiandae Ya Kwenda Kufanya Moshi, Mkoani Kilimanjaro
 Wakili wa Serikali ya Muda gani
 Shahidi Ya Jioni
 Wakili wa Serikali Wakati Kingai anafika, Yeye alikuwa na nani
 Wakili wa Serikali Nini kiliendelea Kutokana na alichokutaarifu
 Shahidi Nilijiandaa na Saa 1 kasoro aliwasili nikiwa Ndani nikasikia Muungurumo wa Gari, nikampokea na Kwenda Ofisini Kwangu Kisha tukaketi
 Wakili wa Serikali Wakati Kingai anaingia Ofisini Kwako hawa wenyewe walikuwa wapi
 Shahidi Alifika na Askari Jumla walikuwa watano akiwemo yeye Mwenyewe, Insp Mahita, Detective Coplo Francis, Detective Coplo Goodluck pamoja na Dereva wa Gari Detective Constable Azizi
 Wakili wa Serikali Elezea sasa baada ya Kuingia Ofisini nini Kiliendelea
 Shahidi Wali ingia Wote Ofisini Kwangu
 Ambayo ni Kulipua Vituo Vya Kuzuia Mafuta, Kuanzisha Vurugu na Maandamano, Kukata Miti na Magogo na Kuyaweka katika Barabara Kuzia Magari Kupita pamoja na Kuwadhuru Viongozi wa Serikali Akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole sabaya
 Shahidi Afande Kingai Alianza Kutoa Taarifa Kwamba Kipo Kikundi Cha Kihalifu ambacho kinatarajia Kufanya Matukio ya Kihalifu hapa Nchini
 Na hivyo Miongoni Mwa Wahalifu hao watatu walikuwa wameshawasili Moshi kwa jili ya kutekeleza Uhalifu huo
 Na Kwamba Baadhi yao walikuwa wamwahawasili Moshi Mkoani Kilimanjaro, na Kwamba Kikundi hicho kinaratibiwa na Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa Chadema
 Baada ya Kumalizia a kutoa Maelekezo hayo ilikuwa ni Takribani saa Moja
 Akasema Jukumu letu ni Kuzuia Uhalifu huo Kutendeka na Kuhakikisha Wahalifu hao tunawakamata
 Tukianza Safari ya Kuelekea Moshi
 Pale Moshi Mlifika Saa ngapi
 Shahidi Saa 2 Usiku
Shahidi Afande Kingai akasema anaendelea Kupokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wake Kutoka Kwa Msiri wake
 Wakili wa Serikali Mlikuwa mnategemea Kuwakamata Wahalifu wangapi
Shahidi Wahalifu watatu[11/8, 08:52] +255 768 464 712: Wakili wa Serikali Nini kiliendelea wakati anaendelea Kupokea Taarifa hizo
 Shahidi tuliondoka pale tukaendelea akuzunguka Maeneo Mbalimbali pale Moshi
Alikuwa anaongea na Simu
 Akasema halinhaijaka Sawa ya kuweza Kuwakamata hawa Wahalifu
Wakili wa Serikali Nani aliomgea hivyo
Shahidi Afande Kingai
 Muda huo ikiwa Takribani Saa Sita Usiku alielekeza tukapumzike
 Tukaenda Kupumzika Mpka Kesho yake Asubuhi
 Wakili wa Serikali Elezea Sasa Kesho yake Asubuhi nini Kiliendelea
 Shahidi Tulikutana Kituo cha Mjini Kati pale Moshi akasema, Tuendelee Kupokea Taarifa Mpaka atakapojiridhissha Mazingira Yamekaaje
 Wakili Ilikuwa Tarehe ngapi
 Shahidi Tarehe 08 August 2020
 Wakili wa Serikali Nini kiliendelea
 Shahidi Tuliendelea Kuwepo Maeneo yake Mpaka Takribani Saa 6 Mchana Afande Kingai akatuita tena
 Akatuambia amepata Taarifa wale Wahalifu Wapo Maeneo ya RAU Madukani
 Wakili wa Serikali Rau Madukani ni wapi
 Shahidi ni Moshi
 Wakili wa Serikali aliwaambia Wahalifu ni wa ngapi
 Shahidi Walikuwa watatu na akatuelekeza Mwonekano wao na aina ya Nguo walizo vaa
 Wakili wa Serikali Kuhusiana na hicho alichowaambia Kingai Kuhusiana na Mwonekano wa Nguo ulikuwaje
 Shahidi Alisema Wawili Kati yao Wanamaumbo Madogo Madogo lakini wa mevaa Masharti Mekundu
Kati ya wale wawili Mmoja Amevaa Shati la  Maua Mekundu Mekundu, Mmoja amevaa Shati la  Maua Maua ya Kijani iliyopauka
 Na Watatu alivaa Jezi ya Mpira ya Taifa Stars ambayo ilikuwa na Rangi ya Blue
Wakili wa Serikali baada ya Kuwa eleza Mwonekano wao.?
 Shahidi Alituambia sasa tuelekee katika Eneo hilo Haraka ili tuweze Kufanya Ukamataji, Ndipo tuliondoka Kuelekea Eneo la Ray Madukani
 Wakili wa Serikali Mlioondoka kuelekea Rau Madukani mlikuwa nani na nni
 Shahidi Ramadhan KingaiMimi MwenyeweInspector MahitaGOODLUCKFRNCISNa Dereva wa Gari Azizi
 Wakili wa Serikali Mlifika Saa ngapi
 Shahidi Mchana Takribani Saa Saba
 Tukaelekea Gari ambapo Afande RCO alikuwa ameelekezwa Eneo ambalo Wahalifu Wamekaa
 Alisema Kwenye Glocery
 Wakili wa Serikali: Glocery ilikuwa wapi?
 Shahidi :Palepale Rau Madukani, Ambapo Kwenye Kona ya Barabara, Yenyewe ipo Lando kabisa ya hiyo Barabara
 Wakili wa Serikali: Wakati Mmefika Rau Madukani nini kilifanyika?[11/8, 08:58] +255 768 464 712: Shahidi Tuliegesha Gari yetu, Ndipo Afande RCO akamtuma Kwanza Inspector Mahita Kwenda Kujiridhisha Kama Watu wenye Mavazi na Mwonekano huo wapo
 Wakili wa Serikali Mahita alifanya nini
 Shahidi alishuka Kwenye gari, a Kapita Kwenye lile eneo na baada ya Muda Mfupi akarudi Wakili wa Serikali Baada Ya Kurudi Majibu yalikuwa nini
 Shahidi Amewaona wamekaa Katika Kibanda
 Wakili wa Serikali Walikuwa wa ngapi
 Shahidi Watatu
 Wakili wa Serikali Nini kilofuata
 Shahidi Afande RCO katuamuru tushuke kwenye gari, Akatugawa. Akundi Mawili Moja lilikuwa Kingai, Mimi na Goodluck
 Wakili wa Serikali Kundi lingine..? Mgawanyiko huo sasa Mkafanya nini Shahidi mahita na Coplo Francis Wakili serikali alitoaa nn?
 Shahidi Alitoa Maelezo Kwamba Mahita Aelekee Upande wa Kushoto na Sisi tuelekee Upande wa Kulia
 Wakili wa Serikali Elezea ilikuwa imeakaaje kaaje
 Shahidi Mwonekano wa Eneo hilo ni kama hivi, Hapa Bara Bara imepita, Kuna Uwazi, Hapa pembeni Kuna Uwazi, na Ndipo Maduka Yanatizana Babarabarani, Kuna Banda lipo ambapo Lenyewe kuna uwazi Katikati na Limepakana na hiyo Glocery ( ANAELEKEZA KWA ISHARA ZA MIKONO) Vilevile Kwenye Banda Kuna Uwazi wa Kuingilia, na Kwenye haya Maduka Kuna Choo
 Wakili wa Serikali Sasa Ulisema Mpangilio wenu ulikuwa Mgawanyiko mara mbili, Je akina nani walipata Kushoto na akina nani walipata Kulia[11/8, 09:01] +255 768 464 712: Shahidi: Inspector Mahita na Coplo Francis Walipitia Upande wa Kushoto Mimi na Afande Kingai na Goodluck tulipitia Upande wa Kulia ambapo Kuna Banda hilo lililopakana na Glocery[11/8, 09:04] +255 768 464 712: Shahidi Tuliegesha Gari yetu, Ndipo Afande RCO akamtuma Kwanza Inspector Mahita Kwenda Kujiridhisha Kama Watu wenye Mavazi na Mwonekano huo wapo
 Wakili wa Serikali Mahita alifanya nini
 Shahidi alishuka Kwenye gari, a Kapita Kwenye lile eneo na baada ya Muda Mfupi akarudi
 Wakili wa Serikali Baada Ya Kurudi Majibu yalikuwa nini
 Shahidi Amewaona wamekaa Katika Kibanda
 Wakili wa Serikali Walikuwa wa ngapi
 Shahidi Watatu
 Wakili wa Serikali Nini kilofuata
 Shahidi Afande RCO katuamuru tushuke kwenye gari, Akatugawa. Akundi Mawili
 Moja lilikuwa Kingai, Mimi na Goodluck
 Wakili wa Serikali Kundi lingine..?
 Shahidi mahita na Coplo Francis
 Wakili wa Serikali Baada ya Mgawanyiko huo sasa Mkafanya nini
 Shahidi Alitoa Maelezo Kwamba Mahita Aelekee Upande wa Kushoto na Sisi tuelekee Upande wa Kulia
 Wakili wa Serikali Elezea ilikuwa imeakaaje kaaje
 Shahidi Mwonekano wa Eneo hilo ni kama hivi, Hapa Bara Bara imepita, Kuna Uwazi, Hapa pembeni Kuna Uwazi, na Ndipo Maduka Yanatizana Babarabarani, Kuna Banda lipo ambapo Lenyewe kuna uwazi Katikati na
 Wakili wa Serikali Kwa Mujibu wa ile Taarifa aliyowapatia Mahita, Elezea ni wapi walikuwa watu hao
 Shahidi Walikuwa ndani ya eneo hili, Walikuwa wamekaa Glocery
 Wakili wa Serikali Baada ya Kuwa Mmegawanyika Katika Makumdi Mawili Nini Kilifanyika
 Shahidi Tukianza Kuelekea Katika Maeneo hayo Mawili Kama ambavyo Afande RCO alikuwa anaelekeza
 Wakili wa Serikali RCO ndiyo nani
 Shahidi Afande Mahita
 Shahidi Na pale tuliokuwa tunaenda watu walipokuwa karibu ni Coplo Francis na Inspector Mahita
 Sisi wakati tunaelekea Kwenye hilo Eneo hayuluina Watu, lakini tulipotaka Kuingia Kwenye huo Uchochoro hayuluina Watu
 Ghafla tukasikia Sauti, ambayo ilikuwa Sauti ya Inspector Mahita
 Wakili wa Serikali Ukisikia Mahita akisema nini
 Shahidi “KAA CHINI, UPO CHINI YA ULINZI” kwa Sauti ya Juu
 Wakili wa Serikali Baada ya Sauti hiyo
 Shahidi tulitembea Kwa Haraka Kuelekea Kwemye hilo Eneo ambapo tuliwakuta
 Wakili wa Serikali Mliwakuta walifanya Nini
 Shahidi Watu wawili walikuwa wamekaa chini
 Kibatala OBJECTION hiyo ni Leading
Shahidi Coplo Francis alikuwa na silaha
 Wakili wa Serikali Silaha ya aina gani
 Shahidi SMG[11/8, 09:05] +255 768 464 712:

Wakili wa Serikali; Kwa Upande wenu je?
 Shahidi alikuwa nayo Goodluck
 Wakili wa Serikali: Wakati mmesikia Amri ya a kukaa Chini Kitu gani Kingine alichofanya?
 Shahidi :Tulikutana anamalizia Kuwaambia Kwa Sauti kwamba wanatuhumiwa Kula Njama za Kufanya Vitendo Vya Kigaidi
 Wakili wa Serikali Elezea Mlipofika Pale nini Kiliendelea pale?
 Shahidi :Baada ya Kufika Pale ACP Ramadhan Kingai aliwaukiza Majina Yao.

Nao walijitambulisha kwa Majina ya Adam Hassan Kasekwa na Mwingine Mohammed Ling’wenya
 Wakili wa Serikali: Mwanzoni Mlisema Mlikuwa Mnaenda Kukamata watu watatu Je Mwingine Yupo wapi?
 Shahidi: Mtu wa tatu pale hakuonekana.

Mpaka Afande Kingai aliulizwa Pale Mwingine Yupo wapi
 Wakili wa Serikali Alikuwa anamuuliza nani
 Shahidi Aliwauliza Watuhumiwa
 Wakili wa Serikali Wakasemaje
 Shahidi hawakujibu Kitu wakati ule
Lakini Afande Kingai akasema ndiyo wenyewe

Na baada ya hapo a kawaambia kuwa Wanatuhumiwa Kula Njama kutenda Makosa ya Kigaidi
 Baada ya Maelezo hayo aliniamuru Mimi Kufanya Upekuzi wa Maungoni
 Wakili wa Serikali Ukisema Upekuzi wa Maungoni Unamaanisha Nini
 Shahidi Kupekua Ndani ya Nguo na Sehemu za Maungo yao
 Wakili wa Serikali baada ya hapo Ulifanya nini
 Shahidi Nikamwambia Afande Kingai kuwa Ngoja Nikaite Watu kwa ajili ya kushuhudia
 Wakili wa Serikali Ukawafuata wapi
 Shahidi Palikuwa na Maduka na Mabanda kwa hiyo niliamini kuna watu wanaoendelea na Shughuli zao
 Na hapo watu watu walikuwa Wamesha Anza Kusogea
Wakili wa Serikali Eneo lipi walikuwa wamewekwa Chini ya Ulinzi Katika Eneo hilo.

Shahidi Hatua Kidogo Katika Banda, Katikati ya hayo Maduka na Pembeni Kidogo Kuna hayo Maduka
 Wakili wa Serikali Zoezi la Kutafuta Mashahidi lilifanyikaje
 Shahidi Nili angalia Maeneo Kadhaa Nikaenda Kwenye Banda, Ni kauliza nani anaye husika hapa, Kwamba Kwakuwa Kukikuwa wazi basi Kuna Shughuli zilikuwa zinaendelea
 Baada ya Kuuliza hivyo alijitokeza Dada Mmoja kwa Jina la Anita Mtaro
 Wakili wa Serikali yeye alikuwa wapi
 Shahidi ikiwa amesimama Mbele ya Banda lake Kidogo
 Wakili wa Serikali Kuna Umbali gani Kutoka Watuhumiwa walipowekwa Chini ya Ulinzi
 Shahidi Hapakuwa mbali sana Takribani kama Hatua 5
 Wakili wa Serikali Nini kiliendelea.

Shahidi Nilijitambulisha Kwake kwamba Mimi ni Afisa wa Polisi na baada ya hivyo nilimuomba asogee kuja Kushuhudia
Wakili wa Serikali Endelea
 Shahidi Yule Dada alisita Kidogo, akaniuliza ataamini Vipi Kama Mimi ni Afisa wa Polisi
 Nikamtolea Kitambulisho Changu Cha kazi  ambacho ni Chekundu
 Akakubali
 Nikaenda pia pale Glocery nikamkuta Dada Mmoja anaitwa Esther Nduhulu.

Shahidi Nikiwa uliza tena Majina watuhumiwa ambao walikuwa bado wamekaa Chini
 Wakajitambulisha tena kwamba ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Ling’wenya
 Na Mimi Nikajitambulisha kwao kwamba naitwa ASP Jumanne Malangahe.

Wakili wa Serikali Kwa Esther Pia nini kiliendelea
 Shahidi Pia nikijambulisha kuwa Mimi ni Afisa wa Polisi nikamuonyesha Kitambulisho Changu akakubali Kusogea
 Wakili wa Serikali palikuwa na Hatua ngapi au Umbali gani
 Shahidi Hatua Sita au Saba
 Wakili wa Serikali Baada ya Kupata Mashahidi nini Kiliendelea. Nikawaambia Wanatuhumiwa Kwa Vitendo Vya kula Njama ya Kutenda Makosa ya Ugaidi na hivyo nahitaji kuwapekua katika Maungo yao.

Wakili wa Serikali: Wakati huo Anita Mtaro na Esther Nduhulu walikuwa wapi
Shahidi: Walikuwa palepale Wakishuhudia
Shahidi: nikatoa Vitu vyangu na Kunyoosha Mikono yangu
Nikamwambia Mtuhumiwa wa Kwanza asimame,
Wakili wa Serikali: Ambaye ni Nani
Shahidi: Adam Kasekwa. Nikawaambia Wanatuhumiwa Kwa Vitendo Vya kula Njama ya Kutenda Makosa ya Ugaidi 
Wakili wa Serikali Wakati huo Anita Mtaro na Esther Nduhulu walikuwa wapi
 Shahidi Walikuwa palepale Wakishuhudia
 Shahidi nikatoa Vitu vyangu na Kunyoosha Mikono yangu
 Nikamwambia Mtuhumiwa wa Kwanza asimame,
 Wakili wa Serikali Ambaye ni Nani
 Shahidi Adam Kasekwa
 Wakili wa Serikali Baada ya Kusimama 

Shahidi Nilimwambia ageuke  Nyuma, Anyooshe Mikono Juu
 Shahidi alitii na nilianza Kimpapasa JKuanzia Kichwani, Shingoni, Kifuani na Nilipo fika Sehemu ya Kiunoni nilihisi Kitu kigumu Upande wa Kushoto
 Nilipitisha Mkono wangu nikishika  kitu Kigumu na Kukichomoa, kilikuwa ni silaha
 Wakili wa Serikali Ilikuwa ni sehemu gani
 Shahidi Kwenye Mkanda au Pindo la Silaha
 Wakili wa Serikali Ikafuata nini
 Shahidi Nikaichomoa na Kuonyesha hii ni salaha, Ni Bastola na Nichomoa Magazine, ilikuwa na Magazine na Ndani ya Magazine Ilikuwa na Risasi tatu

Nikampatia Goodluck Nikaendelea kupapasa zaidi nikaingiza Mifukoni Mwake
 Shahidi Baada ya Kuuliza Mikono Mifukoni Mwake, Upande wa Kushoto sikuoata Kitu, Ila Upande wa Kulia Niliingiza nikatoa Simu Ndogo aina ya Itel
 Ila Pia nikatoa Kinailoni baada ya Kukitoa, ambacho kilionekana kimeviringishwa nikakitoa nikakinyoosha ambacho Kilikuwa ni Kirefu
 Na Kilikuwa na Vitu Mfano wa Karanga
 Wakili wa Serikali Vilikuwa ni Vitu gani
 Wakili wa Serikali Vilikuwa Vingapi
 Shahidi Nili Sogea kwa  Mtuhumiwa Nikaanza Kuhesabu 

Nilihesabu Zikawa 58
 Ndani ya Simu palikuwa na Line Mbili
 Nilituma Goodluck aende  kwenye Kuchukua Fomu ya Hati ya Kuchukulia Mali. Nilianza Kujaza kwa akuitambua Ile Silaha
 Ambayo ilikuwa a imeandikwa Luger A5340 na namba hizo zilikuwa zimeandikwa Upande wa Kulia
 Na pia niliorodhesha Risasi Tatu ndani ya hiyo Magazine
 Pamoja na Simu
 Na laini zake
 Wakili wa Serikali Ulikuwa unaorodhesha wapi
 Shahidi Katika fomu hiyo, Hati ya Kukamatia Mali
 Lakini Pia Nilijaza fomu Nyingine ambapo Nilijaza hizo Kete za Huo Unga ambao nilihisi ni Madawa ya Kulevya
 Wakili wa Serikali Ulifanya nini kwenye hiyo Fomu.

Shahidi: Nilimuonyesha Mtuhumiwa akaangalia akasaini na Anita na Esther na wao wakasaini katika fomu zote Mbili
 Wakili wa Serikali: Ulifanya nini Kuhusu Mtuhumiwa Mohammed Ling’wenya? 

Shahidi: Kwanza baada ya Kumalizia Kujaza nilitoa Carbon Nakala ya Ile Fomu nikampa Adam Kasekwa ambaye nilimwambia akae Chini
 Nikamsimamisha Mtuhumiwa wa Pili na Yeye Nikamwambia ageuke
 Naye hivyo hivyo nilianza Kumpekua Kichwani Na Kiwili wili chake sikuona kitu
 Nikaanza Kuingiza Mikono yangu Mifukoni Mwake
 Nikakutana na Simu, Simu Kubwa aina ya Techno
 Na Yeye pia nilimkuta na Vikaratasi
 Ambayo nilihisi ni Madawa ya  Kulevya, nikavihesabu Mbele ya Mashahidi ambapo Vilikuwa 25
 Vilevile nilifungua ile simu Nikaikuta ina line Mbili, za Hallotel na Airtel niliwaonyesha Mashahidi na Kuendelea Kuteremka Sehemu za Miguu lakini sikuona Kitu.

Baada ya Kumalisha nilimpa Nakala mbili Nakala niliyojaza simu na Nakala ya fomu niliyojaza kete
 Mtuhumiwa aliviona karidhika akasaini na Mashahidi wakasaini nikampa Nakala zake
 Wakili wa Serikali: na Hivi Vitu ambavyo unasema Ukijaza eneo la Rau Baada ya hapo ulivipeleka wapi? 

Shahidi: Nilimkabidhi Goodluck ambaye nilikuwa namkabidhi tangu Mwanzo, na Pia Nika chukua fomu nikajaza na Kumkabidhi
 Wakili wa Serikali: Leo hii ukiiona ile Pistol Unaweza Kuitambuaje?
 Shahidi Kwa Serial Namba
 Shahidi :Na Jina lake lililoandikwa
 Wakili wa Serikali: ambalo ni Jina Gani?
 Shahidi: Luger
 Wakili wa Serikali: Naomba Kupatiwa exhibit P3
 Mahakama inampatia Wakili wa Serikali Robert Kidando
Wakili wa Serikali: Robert Kidando anaifungua.

Wakili wa Serikali angalia Kielelezo hiki kama unakitambua, na Ukikitambua Utasema Ka unakitambua
Shahidi Nakitambua
Wakili wa Serikali: Unakitambuaje?
 Wakili wa Serikali: Unakitambuaje?
 Shahidi A5340
 Wakili wa Serikali: Ipo wapi?
 Shahidi: ANAONYESHA KWA KIDOLE
 Wakili wa Serikali; Luger imeiona wapi?
 Shahidi Luger Ipo Kushoto

 Kibatala OBJECTION naomba hilo Jibu liondolewe Kwenye Kumbukumbu za Mahakama
 Shahidi  aKusema Kwenye Kielelezo Kuna Neno Luger
 Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi hatuoni tatizo, na Pingamizi Halina Mashiko
 Kibatala: Nasema hivi Shahidi aliulizwa kabla haja Shika Kielelezo na akaulizwa Utatambuaje akasema Kwa Serial number
 Na hapa akaulizwa Umeitambuaje akasema Kwa Kuona Serial namba.

Wakili akasema Luger Ipo wapi Kitu ambacho Shahidi a kutaja, Ndiyo nasema huko nikumlisha Majibu Shahidi
 Anasimama Wakili Pius Hilla
 Kibatala Hana haki Kusimama, Nimeweka a Pingamizi, Amejibu Wakili Robert Kidando na Nimejibi tena huyu anasimama Kufanya nini
 JAJI Ngoja tuh tumsikilize
 Wakili Pius Hilla  Baada ya Kutaja Na Kuonyesha Serial Namba, Wakili akauliza Neno  Luger lipo wapi, Ni swali tuh ambalo Shahidi anatakiwa Kujibu kuwa Neno Luger lipo wapi, Kwa Maelezo Hayo ni swali Genuine
 Na Kama litazuiliwa haiwezi Kuwa sawa
 Jaji Shahidi aliulizwa Vigezo ambavyo anaweza Kutambua Kielelezo, Kwa Serial Namba na Mahala ya hiyo serial Namba na Baada ya Hapo Wakili akauliza hilo Neno Luger Lipo wapi akasema hili hapa
 Ndiyo alichlsema
 Kwa namna ambavyo Bwana Kibatala ameweka a hoja yake nakubalina na Kibatala na hili Jibu  naliondoa Kwenye Record
 Labda Urudie Upya Swali
 Wakili wa Serikali Shahidi Unakitu gani Kingine Unachiweza Kutambua Silaha hiyo
 Shahidi Kwa Serial number zake, A5340 NA Kwa Jina la Silaha hiyo lipo Upande wa Kushoto Luger
 Wakili wa Serikali Sasa wakati Unatoa Ushahidi Wako Ukasema Baada ya Kuoata Pistol hii kutoka Kwa Mtuhumiwa Adam kasekwa na Ukapata Risasi tatu, Onyesha Risasi hizo Umetoa wapi
 Shahidi Nilipata kwenye Magazine
 Shahidi Magazine hiyo Ipo wapi 

Shahidi hii hapa (ANAONYESHA KWA KIDOLE)
 Wakili wa Serikali na Risasi 3  zilikuwa wapi
 Shahidi Zilikuwa ndani ya hii Magazine
 Kibatala Mshitakiwa wa kwanza anaomba Kwenye Uwani kidogo
 Jaji kwenda kwake akutasimamisha Shughuli za Mahakama
 Kibatala swala la Kukubaliana tuh
Nashon Kwakuwa wakili wake nipo naomba Mahakama eindelee wakati anaenda Uwani
Wakili wa Serikali Mheshimiwa Jaji naomba niendelee
 Wakili wa Serikali Kuna haitaji la Kisheria 196 cha CPA wakati Ushahidi Unachukuliwa, Mshitakiwa Anatakiwa awepo
 Jaji katika Mazingira anamwakilisha na ameridhia Kama wakili wake yupo inatosha, Je unahisi bado Kuna ulazima
 Wakili wa Serikali Tunaomba Guidance yako Mheshimiwa
 Jaji Kwanza  Kwa stahaOmbi Lenyewe la Kwenda Uwani, Records haiwezi Kuonyesha Kwenye records zangu
 Kwanza amesha ingia
 Wakili wa Serikali Shahidi Umesema Wakati unampekua Mtuhumiwa Adam kasekwa Ukijaza Hati ya Kukamatia Mali, Je Leo Mahakamani Ukiiona unaweza Kuitambuaje
 Shahidi Kwa Mwandiko wako
 Majina yangu
 Sahihi yangu na Vitu Nilivyo Orodhesha Hapa
 Pamoja na Saini za Walioshuhudia Wakati wa Upekuzi na Majina yao.

Wakili wa Serikali Mheshimiwa tunaweza Kupatikana Exhibit IP1
 Mahakama inampatia
 Wakili wa Serikali Shahidi hebu Shika Nyaraka hiyo na uoangalie na uweze Kuiambia Mahakama
Kama Umeitambua
 Shahidi ANASOMA
 Shahidi nimeitambua ni Hati ya Vielelezo Nilivyo Pata kwa Mshitakiwa Adam Kasekwa
Wakili wa Serikali Umeitambuaje
 Shahidi Kwa Majina YanguSahihi yanguMwandiko wanguNa Majina ya mashahidi YapoLakini pia Mtuhumiwa Mwenyewe Majina yake Niliandika ambayo yamo pamoja na Sahihi yake
 Wakili wa Serikali Ungependa Mahakama ifanye nini hiyo Hati ya Kukamatia Mali
 Shahidi ningeomba Mahakama Ipokee Hati ya Kukamatia Mali kama Sehemu ya Ushahidi wangu
HATI INAPELEKWA KWA MAWAKILI WA UTETEZI

Wanaipitia Kwa Pamoja, Wanainamia Wote Kuikagua
 Bado wanaijadili
 Wanaifananisha na Nyaraka zao
 Wanaigeuza geuza Kidogo
 Wanapekua Vitabu Vya Sheria
 Nashon Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa Kwanza tunapinga Uchukiliwaji wa Nyaraka hii
 Na Msingi wetu ni Kwamba Nyaraka hii imendaliwa kwa Sheria ambayo Haipo kwenye Nchi yetu
Hii siyo Nyaraka ya Kawaida, Bali Msingi wake ni Sheria tuh
 Lakini Nyaraka  hii imenukuu Kifungu cha Sheria  38(3) Sura ya 20 ya Mwaka 1985 iliyorekebishwa Mwaka 2005  ambayo haijulikani naomba is Ipokelewe sababu Haijulikani Sheria hiyo
 Nashon anakaa Chini baada ya Kumuomba Mheshimiwa Jaji asipokee
 Mallya Kwa Niaba ya Mshitakiwa Wa Pili tunapinga Kupokelewa kwa Nyaraka hii  kwa Mawasilisho aliyo Sema Wakili Nashoni
Na Kuongezea tuh Hakuna Marejeo ya Sheria hii Mwaka  2018 na Hakuna Mapitio ya Sheria hii ya 38 imefanyiwa Marekebisho Mwaka 2019
 Na hatuwezi Kujua kwamba WalimanIsha Kwamba ni 2019 na Mara ya Mwisho Kifungu cha 38 kimefanyiwa Mwaka 1993 baada ya hapo Hakuna
 Kama Kielelezo kinahusu Mahakama lakini siyo Ya Tanzania Ambayo Kwa MAHAKAMA yako Tukufu haina Sheria hii yenye Marejeo ya Mwaka 2018

 Ni hayo tuh
 Fredrick Kihwelo kwa niaba ya Mshitakiwa namba 03 tunapinga pia Kielelezo Kwa Njia ileile ya Kupinga kwa sababu Nyaraka imeletwa kwa Sheria ambayo Haipo kwenye Vitabu Vya Sheria zetu Tanzania
 Fredrick anakaa
 Kibatala Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne Tunaunga Mkono Pingamizi la wakili wa Mshitakiwa Wa kwanza
 Kwa ufafanuzi ni kwamba
 Nyaraka hii imeundwa Chini ya msingi wa Kisheria ndiyo Maana yenyewe inasema IMETOLEWA CHINI YA KIFUNGU….. inaonyesha wenyewe wanajua kuwa haiwezi Kusimama bila Sheria
 Na Sidhani kama Wenzetu watabisha kwamba Kuna Marekebisho ya Sheria hii ya Mwaka 2018
 Hii ni Nyaraka I siyo halali kwa Maana hiyo haiwezi kuishi Katika Nyaraka za Mahakama
 Na Mallya amesema hapa Kwamba hata hawakuomba kama Kuna Marekebisho tunaomba Upitie
Ciliv Appeal ya Mwenderosi VS Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ilisema Kwamba Overriding Objective haikuletwa Mahakamani Dhidi ya wadawa.

Na Kuhusu Madhara ya Kuleta Nyaraka iliyonukuliwa a Kinyume na Sheria usome
 Kesi ya Ardhi ya  John Marco VS Joshua Malimbe ni Uamuzi wa Mahakama Kuu, lakini Mahakama Ilirejea Mashauri Kashaa
 Maamuzi hayo Robert VS Shibeshi Abebe
 Na akarejea Mahakama ya Rufaa ya Mgonja Dhidi ya….. Na Kesi ya Antony Tesha VS Anita Tesha ya Mahakama Ya Rufaa
 Nisikuchoshe Mheshimiwa Jaji
 Ni hayo tuh Na Nyaraka hii isipokelewe
 Jaji upande wa Serikali
 Wakili wa Serikali Kutokana na Pingamizi hilo na Wamerejea Mashauri Kadhaa, kusuport Hoja zao
 Tunaomba Hairisho fupi tuweze Kulipitia
 Ilituweze Kujibu na pia tunaomba Nakala ya Kesi hizo.

Tukipata Hairisho la Saa Moja Linatosha
Jaji Utetezi
 Kibatala Kwakuwa ni haki yao sisi hatuwezi Kuwapinga
 Kibatala Kuhusu Kuwapa hizo kesi, Tumetoa kwenye Tanzii ambayo ni Kifaa Kazi ila tunaweza Kuwasaidia wao Kupata
 Jaji sahihi
 Wakili wa Serikali Kama zote zipo Tanzii haina shida tutazipata
Jaji anaandika Kidogo
 Jaji Kufuatia Maombi ya Wakili wa Serikali Robert Kidando Mhakama I nahairiswa Mpaka saa 7 na Dakika 20
 Jaji anatoka.

Mahakama imerejea.

Jaji Kaingia
 Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe
Inatajwa Upya
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Kolamu yetu ipo Kawaida kama iliyokuwa Mwanzoni, Tupo tayari Kujibu Hoja za Pingamizi
Wakili Peter Kibatala Nasiye pia tupo tayari MheshimiwaJaji
Jaji anaandika Kidogo.

Mahakama ipo Kimya Kidogo
 Jaji: ndiyo
Wakili wa Serikali: Robert Kidando Mheshimiwa Jaji tumesikikiza Pingamizi zilizoletwa na Upande wa Utetezi
 Wakidai Kwamba Ile Hati ya Kukamatia Mali, (Seizure) iliyotolewa Mahakamani na Shahidi wa 08 Kwamba Imeandaliwa Kutoka na Sheria ambayo haipo.

Na walisema Kwamba Kinachoonekana Kwenye Nyaraka Hiyo ni Criminal Procedures ACT ya Mwaka 1985 iliyorekebishwa. Na wakasema ktk hoja zao Kwamba Kifungu kike cha 38(3) hakijafanyiwa Marekebisho Mwaka huo.

Na wakaenda Mbali kwakuwa Nyaraka ni ya Kisheria na In andaliwa Kisheria kuna Wrong Citation na Kwamba Nyaraka hiyo sipokelewe
 Naomba Kurejea Kifungu cha 20(1) paragraph A, B, na C cha Sheria ya Utafsiri wa Sheria (Interpretation of Lawa Act)
 Mheshimiwa Jaji Jibuetu ni kwamba Pingamizi hizo Zote haina Mashiko Kisheria Kutokana na Kifungu nilicho nukuu nilianza na Paragraph A ambacho Kina onyesha Jinsi gani Sheria inapaswa KutafsiriwaNi Mahususi kwa jili ya Tafsiri ya Sheria zetu zote, Ambapo inazungumzia Kwamba Sheria inaweza Kutaja Kwa Ufupi wake au Kwa Jinsi Sheria Mahususi imesema itakuwa inatamkwa Vipi
 Naomba Sasa Kurejea Kifungu Cha 1 cha CPA Kina Sema Kwamba Sheria hii itaitwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya JinaiKwa Mujibu wa Tafsiri wa 20(1) panapokwepo na Sheria kama inavyotamkwa kwa Sehemu ile AKwa Mujibu huo basi hata akama Ingeishia  Kutaja Jina tuh Ingekuwa Inatosha Kwa hiyo Utambulisho huo Pekee hata Kama Usinge endelea Mbele Unatambulika Kisheria
 Mheshimiwa Jaji Mwaka katika Nyaraka hiyo Upo Katika Sheria ya tafsiri inasema kwamba Hata chapter namba katika Sheria zilizofanyiwa Mapitio au Marekebisho InajitoshelezaNa Chapter namba kwa Kielelezo Kilichopo Mahakamani, inajitosheleza Kwa Maana Ipo Kama Vile ambavyo Wenzetu wamejaribu Kusema.
 Mheshimiwa Jaji katika Mazingira hayo kwa Uhakika Kabisa haiwezi kusemwa Kwamba Nyaraka hii Imetengenezwa Kupitia Sheria ambayo haipo Na Pengine kwa Msisitizo waliouonyesha Kwa Kuonekana kwa Mwaka 2018 katika Seizure Certificate walisema Kwamba Hakuna Revision ya Mwaka 2018 
 Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Hakuna Marejeo(Revision) ya Mwaka 2018 Na Kwa Mwaka huo pia ilikuwa Hoja yao kwamba Kifungu  38 cha CPA hakikufanyiwa Marekebisho.

Bila Kuongeza au Kupunguza ni kwamba Imeandikwa Kwamba 2018
 Tukichukua Maneno ya Mallya Kwamba Hakuna Amandment ya 2018 ni kweli kabisa  Kifungu 38 Kwa Mwaka huo Hakikufanyiwa Marekebisho Isipokuwa Vifungu Vingine Vilifanyika Marekebisho Mwaka huo huo.

Hivyo Mheshimiwa Jaji katika Mazingira kama Inavyoonekana P8 anayotaka Kuitoa hawezi Kuwa Sheria hiyo Haipo Katika Vitabu Vyetu Vya Sheria Hoja hiyo Haina mashiko Tuna Criminal Procedure Moja tuhKwa Upande wa Samahani
 Mheshimiwa jaji Wakili wa Serikali Robert Kidando anatafuta Kitu Kwenye Laptop yake hapa anainamia Wakili wa Serikali Jenitreza Kitali anamsaidia
 Wakili wa Serikali Robert Kidando Tunasheria Moja tuh ya Criminal Procedure Act kwa Upande wa
 Tanzania Main Land Mheshimiwa Jaji, Mawakili wasomi walirejea Mashauri Mawili Ku Support Hoja zao Tukianza na Ndorosi na Wenzake Wawili wa Village Council  dhidi ya Serikali
 Maazimio yalikuwa Katika Shauri hilo ni Tofauti kabisa, kwa Maana Ya Kwamba Kilichokuwa kinajadiliwa Kwenye Rufaa hiyoNi kukosekana kwa Barua
 Na Kwamba Barua hiyo ndiyo iliyokuwa inatoa Msingi Kwa Kutolewa Certificate of Delay, Sasa Kwa Sababu ya Barua hiyo halikuwa Included katika Nyaraka zao Sasa Certificate of Delay ilikuwa haiwezi Kusimama,Kwa sababu Ilikuwa Pia inakwenda Kuangalia Kama Rufaa hiyo Ipo sahihi Mbele ya Mahakama na Kama Mahakama ina Uwezo wa Kuisikikiza
Na Kwa Mazingira hayo hata Kama Wenzetu wataichukulia kuna Overriding Objective Ni sahihi kwamba Katika Mazingira Yale Palikuwa na Overriding Objective lakini Sasa Mazingira Yaliyopo Mbele Yako Mheshimiwa Jaji, Mazingira hayo hayapo
 Pia walirejea Shauri la John Marco.

Walirejea Kesi hiyo ya John Marco Dhidi ya Joshua Malimbe Wakisisitiza Swala la kunukui Kifungu kisicho Lakini tunarudia tena Kusema Kilichokuwa Mbele ya Mahakama Kuu ilikuwa ni Maombi ya Kuongezea Muda wa Kukata Rufaa Ndiyo Pakawa na hilo Pakawa na Tatizo la Kurejea Kifungu cha Sheria Ambacho akitumiki katika a Mazingira hayo
 Mheshimiwa Jaji tunarejea tena Kwamba Pamoja na Kukubalina na Hoja za Mahakama Katika Shauri hilo, lakini Kwa a Shauri hili Mazingira ni tofauti
 Mheshimiwa Jaji baada ya Kutofautisha Mazingira hayo Mawili, Hivyo tupo katika Hatua Kwamba Nyaraka hii inaweza Kupokelewa na Mahakama yako tukufu Sasa tukirejea Mapingamizi ya Mawakili Wasomi Upande wa Utetezi
 Hakuna hata Mmoja anayelalamikia Kwamba palikuwa na Ukiukwaji wa Sheria Non Compliance Kwenye Kupatikana kwa Nyaraka hii iwe Kwa Criminal Procedure Act au Kwa Sheria Nyingine yoyote
 Tunaomba Kurejea Shauri lIlilotamkwa Katika THE DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTION  VS SHARIF ATHUMAN AND SEVEN OTHERS Katika Mahakama Ya Rufaa
 Mheshimiwa Jaji Kanuni zinazoongoza Kupokelekwa kwa Nyaraka hizo, zipo wazi kabisa Katika Paragraph ya Mwisho Ukurasa wa Saba na Paragraph Ya Kwanza Ukurasa wa nane
 Wakili wa Serikali Robert Kidando ANAISOMA hizo Paragraph  Kwamba Kuna Mambo Matatu yametamkw akatika Shauri hilo niRELEVANCEREALITYAND COMPETENCE.

Katika Jambo hili hakuna hata sehemu Moja limegusa Ushahidi huu katika Eneo hilo
 Hivyo Mheshimiwa Jaji kwakuwa hakuna Jambo hilo
 Tunaona Kwamba Mapingamizi ya Wenzetu Yamekosa mashiko Katika Kuleta Changa Moto Hati ya Ukamataji Mali (Seizure Certificate)
 Hoja Nyingine Mheshimiwa Jaji Ukiangalia Certificate Of Seizure ya Shahidi wa Nane anayoitolea Ushahidi
 Inaonekana wazi Kabisa Kwamba
Kuna CPA na The Police force and auxiliary Act ambayo pia Inakufungu cha 35 ambayo inampa Mamlaka Askari Police Kufanya Upekuzi Kama Ilivyo Kwenye Kifungu cha 38 cha CPA
 Hivyo Mheshimiwa Jaji na rejea Vifungu hivyo viwili 38 na 35 Kuonyesha Kwamba Kule Kilichokuwa Kinalalamikiwa kuhusiana na Misingi ya Kisheria ambayo inatakiwa itangulie kabla ya Kupatikana kwa Ushahidi huu
 Inaonyesha Kwamba Sheria Iliyitajwa Mwanzoni CPA ipo, lakini pia Sheria ya Police force and auxiliary Act ipo na Inakufungu hicho
 Na Kwa Sababu Shahidi aliye fanya Zoezi hilo Yupo Mbele ya Mahakama
 Nyaraka hii haiwezi Kuwa Challenged kwa aina ya Mapingamizi yaliyowasilishwa na Mawakili Wa Utetezi
 Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba Pingamizi zote zilizowasiliahwa zituliliwe Mbali na Uweze Kupokea hiyo Seizure Certificate iliyotolewa na Shahidi Wa Nane
 Mheshimiwa Jaji kama Wakili analo la Kuongezea, Mimi naishi hapa
 Wakili wa Serikali Pius Hilla.

Mheshimiwa Jaji limezungumza swala la Wrong Citation ni Kwamba  Uhalali wa Kielelezo Mheshimiwa haiwi Covered na Vifungu ambavyo Vilitumika Kwenye Documents Uhalali unaongozwa na Kanuni ambazo Zipo Kisheria ambazo Mwenzangu ametamgulia Kuzisema
 Lakini pia Unaongozwa na Ushahidi wa Shahidi aliyepo Kizimbani Ambapo Shahidi Anapaswa Kutengenezea MisingiJe Shahidi anaufahamuJe Nyaraka ni halisi Na hiyo ya Relevance ambayo imefanyika Vizuri Haya Ndiyo Maswala Ya MsingiKwa Ushahidi uliotolewa na Shahidi Wa 08 zimekidhi KWAMBA Zimezingatiwa Kigezo Cha Uhalisia Shahidi Wa 08 amekidhi ndiyo Maana Wenzetu hawakutaka Kujieleza huko
 Mheshimiwa Kuleta hapa Maswala ya Kunukuu Kimakosa Kwenye Nyaraka Kama hii, Ambapo Kwa Nyaraka iliyokuja hakuna Kitu kama hicho Maswala ya Nukuu za Vifungu yanapaswa Kuletwa pale ambapo Mahakama inakuwa Moved in a Proper, pale ambapo Inakuwa ina Gurantee Orders Tofauti na Mazingira ya K Shahidi ndiye anapaswa Kutengeneza MisingiNa Maswala yote ambayo Shahidi anatemgemza Ushahidi yamekidhi MheshimiwaKwa hiyo Mheshimiwa Jaji tunailila Mahakama Yako Kwamba Ione Mapingamizi hayana Uwezo ya Kuzuia Seizure Certificate na tunaomba Mapingamizi Uyatupilie Mbali
 Wakili wa Serikali Pius Hilla anakaa Chini
 Nyaraka yao ya Mawasilisho yinapelekwa Kwa
 JajiJaji Kwa hiyo mmemaliza
 Wakili wa Serikali Ndiyo Mheshimiwa
 Jaji Nashon Mheshimiwa Jaji Kwa kuanza
Jaji Mmefanikiwa Kupata Nakala na nyinyi
 Nashon Hatujapewa nakala Nashon Mheshimiwa Jaji Ni sahihi Kabisa Kifungu 20 kiliwekwa Kwa Mazingira kadhaa wa Kadhaa bila Kututoa Nje ya Mazingira yetu
 Wakili wa Serikali Mheshimiwa Hatukufanikiwa Kutoa Copy Ukisoma Kifungu cha 20 Utaona Inazungumzia Mazingira tofautiA Mazingira tofautiB Mazingira tofautiNa C. Mazingira tofauti[11/8, 13:10] +255 768 464 712: Ukosoma Sheria hii  Kifungu  cha 14 Utaona Maana ya “Or “Ni Kwamba Inatumika Disjunctive Ukitaka Risk ya Kutoa Full Citation unakuwa Umetakiwa Ku Cite Kila Kitu Ukitake Risk ya Ku Cite Full Citation Uwezo Kuja Kudai Advantage hapa MahakamaniKwa sababu Utakuwa umetegenzea Mkanganyiko

 Ukitake Risk ya Kuweza Ku Cite Unatakiwa aku Cite kitu ambacho ni Proper la sivyo Utakuwa Unatengeneza ConfusionPia Mheshimiwa Washitakiwa kuhusu Haki yao, kwakuwa Washitakiwa walishapewa Nyaraka hizi na Kwamba walienda Kulitafuta na was Ione Sheria Hiyo utakuwa umewanyima Haki zaoSisi tunaona Kuna Swala la Kuwa Nyima Haki zaoPoa
 Kuna Hoja ya Wakili wa Serikali Robert Kidando Kwamba Hatukuonyesha Ukiukwaji wa Sheria, Hii mbona Inaenda Sawa Ka Isa na Ukiukwaji Wa Sheria za Nchi hii
 Kwamba ametuambia hapa Kesi ya DPP VS Athuman Sharif,
 Tunaomba Kumkumbusha Kwamba Moja ya aKanuni za Ushahidi ni kwamba Ushahidi Usiwe Umepatikana Kinyume na Sheria
Pius Hilla OBJECTION Mheshimiwa Jaji Wakili anaongelea Kwenye Maswala ya Uchukuaji wa Ushahidi Kinyume na Sheria, Ambapo Haupo kwenye Main yao wala Kwenye Majibu yetu
Jaji Mimi nimemuelewa
 Kwamba amesema Anaomba atukumbushe Kwamba Kuna Kanuni Nyingine Katika zile Principle zenu 3 ambayo ni Ushahidi Usiwe Umechukuliwa Kinyume na Sheria
 NASHON Kusema Kwamba Hakuna Hoja hata Moja ambayo haimo kwenye Sheria hii Sisi tulichofanya tumekataa Nyaraka kwa Sababu Siyo Competent[11/8, 13:25] +255 768 464 712: Na kwanini Siyo Competent ni Kwa sababu hii ni Nyaraka ya Kisheria siyo tuh Nyaraka ambayo unaweza Kutengeneza Vyovyote
 Alieleza  Pia Kuwa Shahidi Ndiye anabeba Comptence ya Nyaraka, Siyo Sahihi Sababu Kuna Nyaraka ambazo zinaweza Kuletwa Zenyenwe Bila Shahidi
 Kwa Hoja zetu hazi serve Porpose, Tunapinga Kwa Sababu hili ni Swala la Msingi Mahakama hii Izingatie Hoja zetu ambapo sisi tunaona Nyaraka hii ni Lile au Mfu, Tunaomba Mahakama Yako iweze Kubalance
 Mheshimiwa Jaji Kwa hayo Nahitimisha na Wasilisho langu la awali kwamba naomba Nyaraka hii is iingie Kama Kielelezo Cha Mahakama, Kwakuwa haina Sheria inayotambulika Rasmi

Mallya Mheshimiwa Jaji Mambo Mawili Muhimu Mahakama Ikayanote, Jambo la Kwanza Wakili wa Serikali Msomi Robert Kidando amekili  hakuna Sheria Uliyo fanyiwa amarekebisho Mwaka 2018
Jambo la Pili Amekiri Kwamba Tangu Mwaka 1993  Mpaka kesi hii inaanza Hakuna Marekebisho ya Kifungu cha 38
Tafsiri yangu ni Kwamba anaelewa Kwamba hiki kilicho andikwa Hapa Hakikidhi
Pia alirejea Sura ya Kwanza wa Tafsiri ya Sheria zetu ana akajiongoza Sehemu Ndogo Sana 20 (1)
Kuna Mahala Muhimu sana a kutaja Mahakama iangalie, Mimi Nitataka sasa Mahakama Ingakie  Kifungu 20(3)
Ukitaka Kurejea Sheria Unapaswa Usome pia Kifungu hiki, Mahakama iangalie Sasa Kwanini Wakili Kidando  amekimbia Kifungu hiki
Amasema tuangalie  kuhusu Kifungu cha 35 sasa asome Pale Juu Kwamba NYARAKA HII IMEANDALIWA KWA KIFUNGU CHA 38(2) NA KIFUNGU CHA 35
Mheshimiwa Jaji tafsiri yake Neno “NA” ni kwamba ukavisome kwa pamoja  Sasa Usijusumbue Mheshimiwa Jaji wala Vifungu hivyo havipo Kwenye hiyo Sheria ya 2018
Marejeo tushasema  ni Kifungu cha 20(3) Kwa Sheria za Utafsiri
Kaka yangu Kidando ajue Maana ya Heading
Hapa Hakuna Mahala ambapo Shahidi ametengenza Msingi, labda atuambia Kwanza Amechukuaje Mali za watu kwa Sheria ambazo hazipo Kisha ndiyo aje atuombe hapa
 Hapakuwa na Ufuatwaji wa  Sheria
 Aliwasainisha watu Kwa Sheria ambayo haipo
 Mheshimiwa Jaji yakwangu ni hayo tuh
 Fredrick Kabla Sijazungumza yale niliyopanga Kuzungumza naomba Nimuunge Mkono Wakili wa Serikali Robert Kidando Kwamba Kuna Criminal Procedure Act Moja tuh

 Ambapo nakubalina na Yeye kwamba ni CAP 20 na Marekebisho yake ya 2019 Hakuna ya Ziada
 Na Kwamba Sheria Inaweza Kutaja Kwa ufupi
Labda swali kitakuwa Tukirudi kwenye Kielelezo Je wametaja Sheria Kwa aufupi..?
Jibu n Hapana. Na Ka waliangalia Kwa Kutaja CAP  Namba Wasingeandika Mpaka Mwisho
 Alichotaka Kufanya ni Marekebisho Ya Kielelezo Chao IP 1
 Ambapo sisi tunaona siyo Sahihi
 Katika Mawasilisho Yao Mawakili wa Serikali hawajatoa Rejea ya a kesi yoyote ambayo inasema Kukosewa Kwa Rejea siyo Hoja
 Kwa hiyo NI Maombi yetu Nyaraka Isipolelewe kwakuwa wameleta Kinyume na Sheria
 Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
 Kibatala Mheshimiwa Jaji Nianze Na Kifungu cha 20 cha CAP 1 ambapo kama Wenzetu
 “Where a written Law feffred to………. “
 Kwa hiyo Neno ACT hayakutumika Kwa Bahati Mbaya

 Lakini tunasisitiza Kifungu C  hayo Maneno Hayakutumika Kwa Bahati Mbaya
Ndiyo hoja yetu unakuja kwamba Rejea Ilitakiwa CAP 20 ya 2019
 Compliance lazima Uwepo ambapo Chief Government Printer anaitaja Sheria husika
 Hakuna Upenyo Wa Kuingiza hapo
 Kama ambavyo Maamuzi Yakisha fanyika Kwenye Mahakama ya Ardhi
 Ndiyo Maana Kutumika  “Neno ” May
 Ukitake Risk kutaja Sheria Nzima Ujue Upaswi Kuchanganya
Kama ambavyo Mchapaji Mkuu anaitaja Sheria husika
 Kwanini Hiyo Documents Imwchukua Uamuzi wa Kurejea Sheria Yote na Je Nini Kiliwafanya Wachague  kuandika Sheri Yote
 Kwenye kesi Ya  Mwenderosi tunachokiangalia siyo Material Bali ni Kanuni hasa panapokuwa na Maswala la lazima ya Sheria
 Ukikosea unakuwa Umepoteza
 Kwenye Kesi Ya John Marco ni Hoja kwamba Wrong Citation is Facto, nashukuru Hawajapinga hilo
 Hoja yao Kwamba Nyaraka hii siyo Motion inayohitaji Kuzingatiwa Zaidi, Hiyo ni Fallacy Argument
 Kwa sababu Documents Unahitaji Competence ya Shahidi
 Na Relevance ya Document Yenyewe
 Na Tutaoa Mfano Miwili
 Kwa mfano Umetoa Nottice to Produce Kama Umetoa Ombi la Nyaraka wakati Umenukuu Sheria isiyo, Jibu ni Hapana
 Na Pia statutory Document na awajabisha Wenzetu kwamba ID1 Ni statutory Documents
Kwamba Power ambazo Zipo purported Zenyewe
 Na  kwenye kesi ya Athuman Sharif na Wenzake wamezungumzia hiyo Relevance na Materiality ambapo Shahidi anatakiwa awe Competence ana Shahidi Pia awe Competence
 Hata act anayosema Wakili wa Serikali Robert Kidando Yenyewe Inamatatizo tu
 Namaliza Kwamba Mapingamizi yetu ni ya Muhimu na halali
 Asante sana Mheshimiwa Jaji
 Kibatala anakaaa
 Jaji anaandika 

Jaji: naombeni ile document.

Jaji: “natazama muda, naona kama sitaweza kufanya maamuzi muda huu. Kwa maana hiyo, naomba tuahirishe mpaka kesho asubuhi.”

Mawakili Wa pande zote wanakubaliana
Jaji: Utetezi kuna nyaraka yangu nimewaazimisha naiomba
 Kibatala: Correct
 Jaji: Shahidi kesho utatakiwa kuwa tena mahakamani saa 3 asubuhi
 Na washitakiwa wataendelea kuwa chini ya magereza kpaka kesho asubuhi saa tatu. 

Jaji anatoka

ReplyForward
Like