Kesi ya Mbowe: Jaji Tiganga atupilia mbali pingamizi la mawakili wa utetezi

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ leo asubuhi tarehe 09 Novemba 2021.

Saa 3:35 asubuhi ya Novemba 9, 2021, Jaji ameshaingia mahakamani. Wakati wowote kesi itaanza.

Kesi inasomwa. Ni kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha wenzake kwa kuanza na yeye mwenyewe:

  1. Robert Kidando
  2. Pius Hilla
  3. Abdallah Chavula
  4. Jenitreza kitali
  5. Nassoro Katuga
  6. Esther Martin
  7. Ignasi Mwinuka
  8. Tulimanywa Majige

Peter Kibatala anatambulisha mawakili wa utetezi:

  1. Maria Mushi
  2. Evaresta Kisanga
  3. Hadija Aron
  4. Alex Massaba
  5. Idd Msawanga
  6. Seleman Matauka
  7. Dickson Matata
  8. Nashon Nkungu
  9. Fredrick Kihwelo
  10. John Malya

Jaji anawaita washitakiwa wote wanne—mshtakiwa wa kwanza, mshtakiwa wa pili, mshtakiwa wa tatu, mshtakiwa wa nne—wote wanaitika kuwa wapo

Wakili wa Serikali Robert Kidando anasema shauri limekuja kwa jili ya kusikiliza uamuzi wa Mahakama na wapo tayari kwa ajili ya yote.

JAJI: Utetezi?

PETER KIBATALA: Na sisi tupo tayari kwa ajili ya ruling.

JAJI: Jana Mahakama iliahirisha shauri hili na maamuzi yapo tayari. Maamuzi haya madogo yamekuja baada ya upande wa utetezi kupinga kielelezo cha Hati ya Kukamata Mali ambapo ASP Jumanne aliyekuwa kwenye timu ya kuwakamata washitakiwa huko Rau Madukani, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, na alikuwa anatoa ushahidi. Katikati ya ushahidi wake aliomba kutoa kielelezo cha Hati ya Kukamata Mali, na mawakili wa utetezi wakapinga.

JAJI: Kwa kuanzia na Wakili Nashon Nkungu na wengine wote hoja zao ilikuwa kwamba kielelezo ambacho kilikuwa kinaenda kutolewa hapa Mahakamani na kilikuwa tayari kimeshafanyiwa utambuzi. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa ni kwamba hakuna kifungu cha 38 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2018 na kwamba hatuna Sheria hiyo, na kwamba kifungu namba 38 (3) ndiyo kinaelekeza namna ya kuchukua mali, na kwamba Hati hiyo ni ya kisheria na lazima sheria ifuatwe, na kwamba upande wa mashitaka hawakuomba nafasi ya kutibu mapungufu.

JAJI: Na kesi ya Mwenderosi katika Mahakama ya Rufaa, kwamba Overriding Principle haitaji kuachiwa kwa kuwa itaharibu kabisa mwenendo wa kesi. Wakaomba Mahakama itumie maamuzi ya Mahakama Kuu kutupilia mbali. Na kwamba kesi nyingine ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Malimbe yapo maamuzi kwamba kutokurejea vizuri vifungu vya sheria kunaathiri kesi. Na Kwamba tutupilie mbali kwa kutumia kanuni ya Overriding Principle.

JAJI: Hizo ndizo zilikuwa hoja in chief kwa upande wa utetezi. Kwa upande wa mashitaka walikawakilishwa na Robert Kidando na Pius Hila. Hoja zao ilikuwa wanaomba Mahakama iongozwe na Sheria ya Tafsiri ya Sheria chini ya kifungu cha 20 (1) kwamba mtu anaweza kurejea kwa kifupi … Mtu anaweza kurejea mwaka au namba ya sheria. Au anaweza kurejea sura ya sheria hiyo kama inavyoonekana katika sheria hiyo. Wao wanasema kielelezo kimekidhi kigezo cha sheria hiyo kwa sababu imetajwa jina la Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Wametaja Mwaka. Wametaja Sura. Na kwa mujibu wa sheria wamekiri ni kweli hakuna marekebisho ya sheria hiyo. Hapakuwa na marekebisho ya kifungu hicho mwaka 2018. Na pamoja na kutorekebishwa Kwa kifungu hicho lakini sheria yenyewe iliwahi kurekebishwa.

JAJI: Maamuzi yaloyorejewa kwa upande wa kesi ya Mwenderosi haishabihiani na kesi iliyopo Mahakamani kwa kuwa Kesi ya Mwenderosi ilikuwa ni juu ya kukosekana kwa barua iliyokuwa kwenye kesi hiyo wakati nyaraka hiyo ilikuwa ni ya lazima na kwamba kesi hiyo ni tofauti na kesi hii. Kuhusu kesi ya John Marco na Malimbe ni kwamba kesi hiyo ilikuwa inahusu maombi ya nyaraka ya kesi iliyopo Mahakamani wakati kesi hii kinachozungumzwa ni kurejewa tofauti kwa sheria tofauti. Kwa maana hiyo Mahakama itupilie mbali pingamizi hilo.

JAJI: Na kwa namna hiyo wameomba Mahakama irejee kesi ya Athuman Sharif iliyoketi katika Mahakama ya Rufani ambapo kesi hiyo ilitaja kanuni tatu za kufuata. Na kwamba wameomba kielelezo hicho kichukuliwe kama shahidi ni Admissive, kielelezo ni competence na kwamba kielelezo ni relevance. Kwa mambo hayo, pingamizi, halijaonyesha kwamba kielelezo hicho kimekosa sifa hizo. Na kwa sababu hiyo kielelezo kinatupeleka kupokelewa. Na kwamba siyo sheria moja tu ambayo imetejewa katika kielelezo bali pia kuna sheria ya The Police Force and Auxiliary Act. Na kwamba Mahakama itupilie mbali pingamizi. Kwa upande wa utetezi walikuja na ufafanuzi wa kifungu hicho cha sheria.

JAJI: Wao hawapingi kifungu cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria. Na kwamba kifungu hicho kipo upande wao. Na kwamba wao marejeo yao hayarejei kurejea kwa ukamilifu kama sheria inavyotaka. Na Kwamba wamesahau kwa makusudi kusoma kifungu cha 20 (3,) kwamba sheria inapaswa kurejewa kama ambavyo imepigwa na Mpiga Chapa wa Serikali.

JAJI: Mahakama inafahamu kwamba kifungu cha 35 kuwa inapaswa kusomwa kwa pamoja kifungu cha 38 na kwamba vifungu hivyo vinafanya kazi kwa pamoja. Na kwamba kukosewa kwa sheria moja hakuifanyi nyaraka hiyo kuwa hai. Hawakuomba Mahakama irekebishe kabla, na kwamba kurekebisha wakati nyaraka ipo Mahakamani haikubaliki hata kidogo. Kwamba wanatumia namba na sura. Hawanjaeleza kwamba wametumia short title. Kwamba walicholeta ni marejeo ya kesi kwa ujumla. Kesi ya Mwenderosi inatoa kanuni ambayo Mahakama hii naiomba kuitumia. Na kwa sababu ilitakiwa irejee kwa mujibu wa sheria ambayo ilitakiwa kuwa ipo.

JAJI: Basi wa naomba Mahakama ikatae nyaraka hiyo. Kimsingi hizo ndizo hoja za pamoja. Nimejitahidi kufupisha. Kwa pamoja kuna hoja ambayo haina ubishi. Pingamizi lilikuwa la moja kwa moja, kwamba nyaraka haikunukuu sheria kwa ukamilifu. Na wameitambua wakati wa kutaka kuingizwa.

JAJI: Mambo waliyoongea kwa upande mashita ni mambo ya statutory na siyo hoja ya msingi iliyopo mbele yake. Niwapomgeze mawakili wote ambao wameisaidia Mahakama kufika maamuzi yake. Na kwa sababu hiyo nitajitahidi kwenda kwenye hoja ambazo zinahusu pingamizi na hoja ambazo sijazitumia. Sijazipuuza. Hapana.

JAJI: Kwa kuanza, pande zote mbili wanakubaliana kuwa kifungu 20(1) cha Sheria ya Tafsiri Ya Sheria kinatoa namna ambavyo sheria za nchi yetu zinaweza kutafsiriwa. Na kifungu cha 38 na kifungu cha 35 ndivyo vinatoa namna ya kuchukua mali kwa mtuhumiwa.

JAJI: Kifungu cha 38 (3) kinatoa umuhimu wa kuchukua hati ya kukamata mali. Lakini haijapingwa kwamba ni takwa la kisheria kwamba fomu hiyo ni lazima ikidhi kisheria, ambapo pande zote mbili wamekubalina. Na mimi naona hivyo. Niende moja kwa moja kwenye pingamizi.

JAJI: Pingamizi hili linaonyesha kwamba sheria ambayo imenukuliwa na kwamba imekosewa kurejewa. Nimeona Mahakama iende moja kwa moja kwenye fomu hiyo. Kama ambavyo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, imeandikwa Hati ya Kuchukua Mali, na kwamba imetolewa kwa kifungu cha 38 na kifungu cha 35 cha Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi iliyorekebishwa mwaka 2018, kwamba ndiyo imeleta ubishi mbele ya Mahakama.

JAJI: Imetumika kama sheria ambayo imerekebishwa mwaka 2018. Maana halisi ya iliyorekebishwa mwaka 2018 halikuwa limeelezwa linamaanisha nini. Mahakama ikaona ni vizuri kama kweli sheria hii ilirekebishwa mwaka 2018. Mahakama ikasema iendelee na hii sintofahamu? Mahakama ikaona ni hapana. Ishughulike na neno hili.

JAJI: Mahakama ikapata kamusi ya Kiswahili TUKI toleo la University of Dar es Salaam la mwaka 2001. Rekebishwa siyo jina wala kitenzi ambacho kinaweza kusimama peke yake. Kitu ambacho nimepata kwenye kamusi hiyo ni neno REKEBISHA, kwamba ni adjusted or amended.

JAJI: Which was Adjusted or was amended. Hivyo kwamba kilichopo mbele ya Mahakama siyo iliyorekebishwa mwaka 2018. Mahakama inaona kifungu hicho cha 38 hakikuwahi kurekebisha mwaka 2018 bali kuna ushahidi wa kutosha ambapo sheria hiyo ilirekebishwa mwaka 1993. Na wote tunakubaliana kwamba imekosewa kurejewa kimakosa. Sasa baada ya kurejea Sheria hiyo kimakosa nini kinafuatia?

JAJI: Ni wazi kwamba sheria inapokuwa imekosewa kurejewa katika kesi ya Malimbe kwamba nyaraka ambayo imekosewa inakuwa DEFECTIVE. Inakosa nguvu za kisheria.

JAJI: Nakubaliana kwa pamoja na maamuzi ya John Marco na kwamba huo ndio msimamo wa sheria, na kwamba kanuni hiyo kwamba kukosa nguvu kwa n yaraka inafanya ife. Maamuzi hayo hayaingii kote bali kuna sehemu mbalimbali. Mahakama imeona kwamba yapo maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwamba kukosewa kurejea sheria mbalimbali kunifanya Mahakama kutoa nafuu kwenye kesi hiyo na kutoa maagizo juu ya mamlaka. Maombi kama haya yalirejewa katika maombi ya jinai namba 3 ya mwaka 2012. Imeelezwa kwamba pale ambapo kunakosewa kurejea sheria vizuri kunaifanya na kuinyima Mahakama kufanya maombi Mahakama. Nyaraka yoyote ambayo inafanya motion ya kuomba Mahakama ifanye maamuzi inafanya Mahakama ifanye maamuzi. Na kwamba nyaraka iliyopo Mahakamani siyo nyaraka inayofanya maombi Mahakamani. Mazingira haya ni tofauti na mazingira niliyotaja hapo juu.

JAJI: Yametajwa vizuri kwenye rejea ya kesi ya Saidi Kindamba dhidi ya Jamuhuri na maamuzi ya Seleman Abdallah dhidi ya Jamuhuri, ambapo kote walieleza kwamba dhumuni la nyaraka ni CERTIFICATE OF SEIZURE. Ni malengo yanayotofautiana. Kwa mana hiyo nakubaliana na upande wa mashitaka kwa mazingira ya kesi ya John Marco ni tofauti kabisa na kesi iliyopo mbele yetu. Mahakama inapofanya maamuzi iangalie haki zaidi.

JAJI: Mahakama imeamua kuangalia mapungufu yanayokuja na masuala ya kisheria ambapo imekuja na kanuni kwamba sheria kunukuliwa vibaya haitoshi kwamba kutorejea kwa sheria hiyo kunafanya nyaraka hiyo iwe imekufa. Lazima aeleze ni kwa namna gani kwa kukosewa kwa kesi hiyo kunafanya nyaraka hiyo kuwa imekufa.

JAJI: Mahakama ya Rufani iliona kwamba kuna makosa na ikasema maneno yafuatayo: Majaji katika maamuzi hayo hayo walisema maamuzi ya Charles Mwinyichande dhidi ya Jamuhuri na Said Ally dhidi ya Jamuhuri wakasema kwa sasa Mahakama imekuwa na maamuzi tofauti na kwamba kwa sasa lazima mtu aeleze mtu kwamba kutokurejewa kwa sheria vizuri kumemuathiri vipi. Kwa mtazamo huo huo nitaona kwamba Mahakama Kuu kuwa kutokurejewa vizuri kwa mashitaka kama hakutoonyesha kumeathiri vipi, Mahakama hii inakubali mambo yafuatayo.

JAJI: Kwamba hakuna ubishi kwamba kukosewa kwa kurejea kwa sheria kwa nyaraka ambayo inaleta maombi Mahakamani kunafanana na Seizure Certificate. Katika mazingira hayo ni wazi kwamba kwa kanuni hiyo ambayo nyaraka ambazo zinahimiza kesi Mahakamani lazima zifuate utaratibu huu. Katika hali hiyo basi Mahakama inaona katika shauri hili kwamba kuwapo kwa mwaka 2018 kimakosa hakujaelezwa kwamba kunaathiri vipi upande wao.

JAJI: Kwa namna hiyo basi natupilia mbali pingamizi na Mahakama inapokea kielelezo cha Seizure Certificate

JAJI: Shahidi wenu yupo wapi? Upande wa mashitaka?

JAJI: Naomba Sasa shahidi apokee nyaraka hiyo na aisome Mahakamani.

SHAHIDI: (Anasoma) Jeshi la Polisi Tanzania. Hati ya Kuchukulia …

JAJI: Bado upo chini ya kiapo.

SHAHIDI: Imetolewa chini ya kifungu cha 38(3) Sura ya 20 Sheria ya mwaka 1985 iliyorekebishwa mwaka 2018 na kifungu cha 35 cha Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi. Hii ni kuthibitisha kwamba leo tarehe tano Agosti mwaka 2020, muda wa saa saba … Kutokana na upekuzi uliofanyika Adam Kasekwa alimaarufu Adamoo … Vitu vifuatavyo hapa chini vimechukuliwa kama vielelezo. Pistol aina ya Luger, magazine na risasi tatu, simu, Vodacom Simcard, Airtel Sim Card, afisa aliye chukua mali (ni) ASP Jumanne Shaban Mahangale. Sahihi ya shahidi Anita. Sahihi ya shahidi Esther. Mwisho wa kusoma Mheshimiwa Jaji.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi, kwa mujibu wa fomu hiyo, Hati ya Kukamatia Mali ilikuwa inamuhusu nani?

SHAHIDI: Adam Kasekwa, alimaarufu Adamoo.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unatoa ushahidi wako mwanzoni ulisema unampekua mtu anaitwa Adam Kasekwa. Je, Adamoo inatoka wapi?

SHAHIDI: Shahidi wakati najaza fomu hii kwa ukamilifu ndipo alinitajia majina yake, alimaarufu Adamoo.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati unajitambukisha mwanzoni unajitambulisha ASP Jumanne Malangahe?

SHAHIDI: Kwa ukamilifu naitwa ASP Jumanne Shaban Malangahe.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa kielelezo hicho hebu elezea vitu ulivyovikamata kwa Adam Kasekwa.

SHAHIDI: Ni silaha aina ya Luger ikiwa na magazine yenye risasi tatu, yenye namba A5340. Lakini pia alikuwa na simu ndogo ya Itel aina ya 2160

SHAHIDI: Ni Itel aina ya 2160 yenye IMEI namba 353736289120265/353736289120273. Kulikuwa na laini ya Vodacom, ICC ID 89255044105294533187. Kulikuwa na Airtel sim card yenye ICC ID namba 89250509095499322. Inaishia hapo.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa kwa mujibu wa nyaraka hiyo mashahidi walikuwa wakina nani?

SHAHIDI: Anita Mtaro wa Rau Madukani. Wapili ni Esther Daughter of Nduhulu wa Rau Madukani

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi, unazungumzia kuhusiana na kukamata simu ya Itel pamoja na Vodacom na Airtel. Elezea kwa pamoja.

SHAHIDI: Simu na laini za simu ni sababu ya kufuatilia na kupata ushahidi wa mawasiliano ya miamala ya fedha au mawasiliano ya ujumbe wa simu ambao ungeweza kusaidia katika upelelezi.

WAKILI WA SERIKALI: Na upekuzi huo ulifanya kwa sheria gani?

SHAHIDI: Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 iliyorekebishwa mwaka 2018, na chini ya Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

WAKILI WA SERIKALI: Swali moja ya mwisho kwenye fomu hiyo. Ilikuwaje mashahidi hawa Anita na Esther wakapatikana?

SHAHIDI: Sehemu tuliyopata watuhumiwa hawa wawili. Kwani majengo yale yalikuwa wazi. Ni wazi wangeweza kuona ni nini kinafanyika.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kufanya upekuzi huo wa Adam Kasekwa, vipi kuhusu vile vitu?

SHAHIDI: Nilisogea kwenye gari nikaandaa Hati ya Makabidhiano na Goodluck ambaye nilikuwa nampa tangu mwanzo.

WAKILI WA SERIKALI: Leo hii hiyo Hati ya Makabidhiano ukiiona unaweza kuitambuaje?

SHAHIDI: Naweza kuitambua kwa mwandiko wangu, majina yangu na sahihi yangu pamoja na jina la askari niliyemkabidhi. Katika makabidhiano hayo niliandaa hati mbili tofauti.

WAKILI WA SERIKALI: Utofauti wake ni nini?

SHAHIDI: Niliandaa fomu ya kumkabidhi silaha, pamoja na magazine na pia fomu ya kumkabidhi simu na laini.

WAKILI WA SERIKALI: Hiyo fomu na risasi tatu ukiiona utaitambuaje?

SHAHIDI: Kwa majina yangu pamoja na sahihi yangu.

SHAHIDI: Pamoja na jina la askari niliyekuwa namkabidhi.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kumuonyesha kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Angalia kama umeitambua.

SHAHIDI: Nimeitambua ni hati ya makabidhiano baina yangu na askari Detective Constable Goodluck.

WAKILI WA SERIKALI: Umeitambuaje?

SHAHIDI: Kwa majina yangu, sahihi yangu pamoja na askari niliyemkabidhi.

WAKILI WA SERIKALI: Ungependa Mahakama ifanye nini katika hiyo nyaraka?

SHAHIDI: Ningependa Mahakama ipokee kama sehemu ya ushahidi wangu.

(Wakili wa Serikali anaipeleka nyaraka kwa mawakili wa upande wa utetezi. Wote wanainamia na kuikagua pamoja).

(Mawakili wa utetezi wanaisoma kwa kuigeuza geuza na kujadiliana).

NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji, kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza hatuna objection na hati hii.

JOHN MALLYA: Sisi pia hatuna objection.

WAKILI FREDRICK: Kwa niaba ya mshitakiwa wa tatu hatuna objection.

PETER KIBATALA: Kwa niaba ya mshitakiwa wa nne hatuna objection.

(Mahakama inaipokea nyaraka, kisha Jaji anaandika kidogo).

JAJI: Basi Mahakama inaipokea na inakuwa kielelezo namba 12 cha upande wa mashitaka.

JAJI: Tusomee.

(Shahidi anasoma upya).

SHAHIDI: Hati ya Makabidhiano. Mimi ASP Jumanne Malangahe wa CID Arumeru namkabidhi Detective Goodluck vitu ambavyo vilikamatwa Moshi eneo la Rau Madukani saa saba mchana kutoka kwa mtuhumiwa Adam Kasekwa anayetuhumiwa kwa kosa kula njama za kutenda vitendo vya kigaidi.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa mujibu wa hati hiyo ya makabidhiano, ni nani uliyemkabidhi vitu ulivyovikamata kwa Adam kasekwa?

SHAHIDI: H4347 Detective Constable Goodluck.

WAKILI WA SERIKALI: Na ulimkabidhi nini?

SHAHIDI: Pistol yenye namba A5340 aina ya Luger pamoja na risasi tatu ndani ya magazine.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi ulifanya nini vitu ulivyokamata kwa Adam Ling’wenya?

WAKILI WA SERIKALI: Vitu ulivyokamata kutoka kwa Mohammed Ling’wenya ulivipeleka wapi?

SHAHIDI: Nilimkabidhi Constable Goodluck simu pamoja na laini. Kete sikumkabidhi.

WAKILI WA SERIKALI: Zile kete ulipeleka wapi?

SHAHIDI: Nilienda moja kwa moja kwa mtunza vielelezo pale kituo cha Polisi Kati Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa baada ya kukamilisha upekuzi kwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya nini kilifanyika baada ya upekuzi huo?

SHAHIDI: Tuliondoka na watuhumiwa kwenda Kituo cha Mjini kati Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Muda gani?

SHAHIDI: Muda huo huo na dakika kadhaa zilikuwa zimepita.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea Mahakamani zoezi la ukamataji na upekuzi mpaka mmakamilisha linaweza kuwa muda gani?

SHAHIDI: Linaweza kuwa limepita saa saba na dakika 45 kuelekea saa nane mchana kuelekea Kituo cha Polisi Kati Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilitokea Kituo cha Polisi Kati Moshi?

SHAHIDI: Sisi na Afande RCO tuliingia kwenye gari yetu na watuhumiwa.

SHAHIDI: Na mashahidi wakapanda gari ambayo ACP Kingai aliagiza kutoka kituoni. Tulipokuwa njiani nilimuuliza Adam Kasekwa kama ana nyaraka yoyote kuhusiana na hiyo silaha. Akasema hana. Mimi nilienda kukabidhi zile kete za unga ambazo nilidhani ni madawa ya kulevya.

SHAHIDI: Wakati nakabidhi kete zile niliandika draft la kukamata ili tufungue kesi kwa unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya. Tukiwa kwenye gari Afande ACP aliwauliza mwenzenu wa tatu yupo wapi? Wakajibu yule Kakobe hatujui kwenye lile eneo ameondokaje.

WAKILI WA SERIKALI: Nani alijibu?

SHAHIDI: Wote walijibu.

WAKILI WA SERIKALI: Kwamba….

SHAHIDI: Kwamba hawajui yule wa tatu aliondokaje.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea huyo mtuhumiwa wa tatu kama unamfahamu.

SHAHIDI: Watuhumiwa wenzake walisema majina yake ni Moses Lijenje. Maarufu Kama Kakobe.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilifanyika na huyu mtuhumiwa mmoja?

SHAHIDI: ACP Ramadhani Kingai aliwauliza mnaweza kutusaidia kumpata huyu mtuhumiwa?

SHAHIDI: Wakasema wapo tayari kuonyesha maeneo waliyoamini kwamba anaweza kupatikana.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea?

SHAHIDI: Tulianza zoezi la kuanza kumtafuta.

WAKILI WA SERIKALI: Zoezi la kuanza kumtafuta lilianza wapi?

SHAHIDI: Lilianza Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwa saa ngapi?

SHAHIDI: Saa nane dakika 20 mpaka 30.

WAKILI WA SERIKALI: Mlianzia wapi?

SHAHIDI: Kituo cha Polisi Kati Moshi tukarudi tena eneo la Rau Madukani, tukaenda eneo la KCMC, Majengo, Pasua. Tulikwenda mpaka Hotel ya Aishi ambayo ipo Machame. Tulikwenda mpaka Boma.

SHAHIDI: Lakini kote huko hatukuweza kufanikiwa kumpata Moses Lijenje.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kiliwafanya mwende kwenye hayo maeneo mliyoyataja?

SHAHIDI: Washitakiwa walisema ni maeneo ambayo walikuwa wanapenda kwenda, kupata chakula au kinywaji na eneo kama la Aishi walieleza waliwahi hata kukaaa.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea zoezi hili la kumtafuta siku hiyo ilikuwaje.

SHAHIDI: Zoezi hilo la tarehe tano Agosti 2020 liliisha kwenye majira ya saa nne kwenda saa tano, tukarudi kituo cha Polisi Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Mlirudi kufanya nini.

SHAHIDI: Kuwarudisha watuhumiwa na kuweza kupumzika ili kesho tuendelee na zoezi.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea hapa Mahakamani kama walipata huduma ya chakula.

KIBATALA: Objection! Tunapinga hilo swali.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati ufutailiaji unaendelea nini kilitokea?

SHAHIDI: Tukiwa tunatoka Boma tuliagiza chakula, sisi tukiwa nje ya gari na watuhumiwa wakiwa kwenye gari.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati mmerudi kituo cha Polisi pale Moshi ni nani iliwakabidhi watuhumiwa?

SHAHIDI: Tukiwa kituoni tulimkabidhi Afande Mahita awakabidhi watuhumiwa pale kituoni.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati mnakabidhi ule unga uliodhani kuwa ni madawa ya kulevya watuhumiwa walikuwa wapi?

SHAHIDI: Walikuwa ndani ya gari bado wanasubiri kwemda kumtafuta Moses Lijenje. Alfajiri ya tarehe sita Agosti mwaka 2020 tulikwenda Kituo cha Kati Moshi.

SHAHIDI: Mimi na Mahita tulikwenda ndani wakati ACP Kingai alibaki nje. Nilikwenda kuwatoa watuhumiwa wote wawili.

WAKILI WA SERIKALI: Uliwatoa kwa madhumuni gani?

SHAHIDI: Tuliwatoa kwa madhumuni ya kwenda kutusaidia kwenda stendi kumtafuta mtuhumiwa wa tatu.

WAKILI WA SERIKALI: Mlikuwa nani na nani?

SHAHIDI: Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na Detective Coplo Aziz ambaye alikuwa ni dereva.

WAKILI WA SERIKALI: Mkiwa Stendi nini kiliendelea?

SHAHIDI: Tulijaribu kuangalia mabasi yanayoenda mikoa mbalimbali kama Morogoro, Dar es Salaam au Arusha, na maeneo ambayo tulikuwa tunaingiza na watuhumiwa ambao tulikuwa tumewakamata.

WAKILI WA SERIKALI: Zoezi hili liliendelea kwa muda gani?

SHAHIDI: Hatukuweza kumpata Moses Lijenje.

SHAHIDI: Tuliendelea kumfuatilia katika maeneo ambayo jana yake tulipitia tukiwa tunamfuatilia ambayo ni Majengo, Rau Madukani, KCMC maeneo ya Pasua. Lakini tuliondoka kuelekea maeneo ya Aishi Hotel. Lakini maeneo yote hayo tuliyopita bado hatukufanikiwa kumwona Moses Lijenje. Lakini watuhumiwa waliweza kusema kwamba Arusha, Sakina mtuhumiwa Moses Lijenje ana dada yake.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilifanyika?

SHAHIDI: Ikiwa muda wa mchana kwenye saa nane tuliamua kuondoka kuelekea Arusha kumtafuta Moses Lijenje.

WAKILI WA SERIKALI: Ni akina nani hao walienda Arusha?

SHAHIDI: Mimi mwenyewe, Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck, Detective Coplo Aziz.

SHAHIDI: Tulifika kule na kufuatilia maeneo hayo kadri ambavyo watuhumiwa walikuwa wakituongoza lakini hawakuwa na uhakika na nyumba anayoishi dada yake Lijenje. Baada ya kushindwa kumpata tuliamua kurudi.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa muda gani?

SHAHIDI: Muda huo ulikuwa saa kumi ambapo tulifika kwenye saa 12 jioni.

WAKILI WA SERIKALI: Mlirudi wapi?

SHAHIDI: Moshi.

WAKILI WA SERIKALI: Mlifika wapi?

SHAHIDI: Mpaka kituo cha polisi pale Moshi. Afande Kingai alionekana kuendelea kupokea taarifa kwa mtu ambaye anamuita msiri. Ikaonekana kuna ugumu wa kumpata Moses Lijenje.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea?

SHAHIDI: Baada ya kushindwa kumpata, Afande Kingai alisema amepokea maelekezo kutoka kwa DCI wakati huo Robert Boaz, na kwamba shauri la kula njama za kutenda matendo ya ugaidi lilikuwa limefunguliwa katika Kituo cha Mjini kati Dar es Salaam.

SHAHIDI: Tulianza safari ya kuelekea Dar es Salaam na watuhumiwa wawili. Tulikuwa na Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na Detective Coplo Aziz. Tulikuwa tunatumia gari ya Afande RCO ambayo ni Toyota Landcruiser.

WAKILI WA SERIKALI: Safari ya a kuelekea Dar es Salaam ilianzia wapi?

SHAHIDI: Ilianzia Moshi, ambapo Njia Panda Himo gari yetu ilikuwa na tatizo kwenye mfumo wa umeme, dereva alitueleza.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea?

SHAHIDI: Afande Kingai aliomba gari kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, na baadaye akaletewa gari. Wakati tunasubiria gari tuliteremka na kuagiza chakula.

WAKILI WA SERIKALI: Hapo Himo umesema gari ilipata tatizo la mfumo wa umeme. Mlikaa hadi saa ngapi?

SHAHIDI: Hatukukaa sana. Saa mbili au saa tatu gari ililetwa aina ya FOTON na Detective Coplo Aziz tukimuacha na mafundi.

WAKILI WA SERIKALI: Mlikuwa na nani kwenye hiyo safari?

SHAHIDI: Mimi, Afande Kingai, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck na dereva wa ile gari ya Moshi PC Wembo.

WAKILI WA SERIKALI: Ukaaji katika ile gari ya FOTON ulikuwaje?

SHAHIDI: Mbele kushoto alikaa Afande Kingai.

SHAHIDI: Na mlango unaofuata kushoto nilikaa mimi, mtuhumiwa Adam Kasekwa katikati na kulia ni Inspector Mahita na Nyuma alikaa Constable Goodluck na Mohammed Ling’wenya.

WAKILI WA SERIKALI: Hali ilikuwaje?

SHAHIDI: Ilikuwa safi. Hakukuwa na shida yoyote.

WAKILI WA SERIKALI: Dar es Salaam mlifika lini?

SHAHIDI: Tarehe saba Agosti 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Saa ngapi?

SHAHIDI: Alfajiri.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea baada ya kufika Dar es Salaam?

SHAHIDI: Tulifika Kituo cha Polisi pale Mjini Kati Dar es Salaam. Niliwakabidhi watuhumiwa pale.

WAKILI WA SERIKALI: Saa ngapi?

SHAHIDI: Ilikuwa imeshapita saa 12 asubuhi.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kuwakabidhi watuhumiwa?

SHAHIDI: Afande Kingai alielekeza kwenda kupata refreshments angalau maji na akasema tukutane saa moja pale Central.

WAKILI WA SERIKALI: Saa moja ya majira gani?

SHAHIDI: Ya asubuhi, ya Tarehe saba Agosti 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Hebu elezea ni wakati gani tena mlikutana.

SHAHIDI: Saa moja tulikutana. Alikuwapo Afande Kingai na Inspector Swila. Swila alikuwa anatokea ofisi ya DCI.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulipewa majukumu gani?

SHAHIDI: Nilipewa jukumu la kumhoji mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling’wenya.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe kama askari Polisi ni wakati gani mtuhumiwa anatakiwa kuhojiwa?

SHAHIDI: Ndani ya masaa manne kuanzia unapomkamata.

WAKILI WA SERIKALI: Sasa Mohammed Ling’wenya alikamatwa tarehe tano Agosti 2020 pale Moshi. Nini kilikupeleka uje uchukue maelezo tarehe saba Agosti 2020?

SHAHIDI: Ni baada ya kukosekana kwa muda, kwa sababu tulikuwa tunaendelea kumtafuta mtuhumiwa wa tatu.

WAKILI WA SERIKALI: Ni lini hiyo mlimtafuta mtuhumiwa wa tatu?

SHAHIDI: Kuanzia tarehe tano mpaka tarehe saba Agosti 2020.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kupewa sasa maelekezo ya kumwandika maelezo Mohammed Ling’wenya?

SHAHIDI: Tulikwenda kwa Mkuu wa Kituo cha Mjini Kati Dar es Salaam ili nipate chumba cha kuweza kukaa.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea sasa baada ya kufika.

SHAHIDI: Alikuwa hajafika na baada ya muda akafika na kwenye saa mbili na dakika ishirni asubuhi nilianza kumhoji Mohammed A Ling’wenya.

WAKILI WA SERIKALI: Kabla ya kuandika maelezo, asubuhi hiyo ulimpata wapi?

SHAHIDI: Nilienda kwenye chumba cha mashitaka nikaenda kumwomba, nikapewa na kwenda naye kwenye chumba cha mahojiano.

WAKILI WA SERIKALI: Taratibu zipi sasa ulizochukua kwenye chumba cha mahojiano?

SHAHIDI: Nilijitambulisha kwake kwamba mimi naitwa ASP Jumanne Malangahe.

SHAHIDI: Nilimuonya mtuhumiwa anatuhumiwa kwa kosa la kupanga njama za kutenda matendo ya ugaidi na hivyo halazimishwi kusema lolote isipokuwa kwa hiari yake mwenyewe chini ya kifungu cha 24 cha Sheria ya Kupambama na Ugaidi. Na lolote atakalolisema basi litaandikwa hapo chini na litaweza kutumika kama ushahidi Mahakamani. Pia nilimweleza anayo haki ya kuwapo mwanasheria wake, ndugu, rafiki au jamaa wakati wa kuandika maelezo haya.

WAKILI WA SERIKALI: Yote hayo unavyosema wewe kwamba ulimfahamisha, ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilisaini kwenye hilo onyo na mtuhumiwa akasaini.

WAKILI WA SERIKALI: Hilo onyo lipo wapi?

SHAHIDI: Lilikuwa chini baada kuandika particulars zote na kumuonya chini yake.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumfahamisha hizo haki alifanya nini?

SHAHIDI: Yeye alijibu kuwa ameelewa nimemuonya kwa kosa la kula njama za kutenda ugaidi na kwamba katika tuhuma hizo halazimishwi kusema lolote isipokuwa kwa hiari yake na lolote atakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi Mahakamani. Baada ya kusema hivyo alisaini na mimi mwenyewe nikasaini.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hatua hizi, kitu gani kingine kilichoendelea?

SHAHIDI: Nilimhoji je, upo tayari kutoa maelezo yako? Akajibu YES! Yupo tayari. Nikamuuliza tena nani awepo wakati wa kutoa maelezo yako? Akajibu ni yeye mwenyewe.

WAKILI WA SERIKALI: Kitu gani kinaonyesha alibubali mwenyewe?

SHAHIDI: Kwanza kwa yeye akusaini, mimi kusaini, kukubali kuhojiwa bila wakili, ndugu wala rafiki.

SHAHIDI: Muda wake wa kuandika maelezo ulikuwa ni saa mbili na dakika 20 asubuhi.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kilifanyika katika kuandika maelezo haya?

SHAHIDI: Nilianza kuandika tuhuma aliokuwa anatuhumiwa nazo, ambazo alinisimulia yeye mwenyewe na alikiri kuhusika na tuhuma hizo. Wakati ananieleza mimi nilikuwa naandika maelezo yake.

WAKILI WA SERIKALI: Kuanzia hapo saa mbili na dakika 20 mliendelea mpaka saa ngapi?

SHAHIDI: Mpaka saa tano na dakika mbili asubuhi ambapo niliandika uthibitisho akayasoma mwenyewe, nikayasaini na yeye akayasaini. Sasa ilikuwa imeshafika saa tano na dakika zake asubuhi.

WAKILI WA SERIKALI: Kwanini ulimpa yale maelezo baada ya kuandika ili ayasome?

SHAHIDI: Nilimpa maelezo hayo ayasome ili kujiridhisha maelezo hayo yapo sawasawa kama angehitaji kufanya marekebisho angeweza kunieleza.

WAKILI WA SERIKALI: Baada sasa ya kumalizia kuandika maelezo haya kwa siku ile ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilimchukua na kumrejeaha pale chumba cha mashitaka.

WAKILI WA SERIKALI: Wakati anaandika maelezo yeye alijitambulishaje?

SHAHIDI: Kwa majina matatu ya Mohammed Abdilah Ling’wenya na Jina lake alimaarufu kama Doyi.

WAKILI WA SERIKALI: Maelezo uliyoandika yalikuwa ni ya nini?

SHAHIDI: Maelezo ya onyo.

WAKILI WA SERIKALI: Unamuona hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Namuona hapa Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa ruhusa ya Mheshimiwa Jaji unaweza kupita na kwenda kumwonyesha.

SHAHIDI: Mohamed Abdilah Ling’wenya ni huyu hapa mwenye tshirt nyeupe (Anamwonyesha kwa kumgusa kwa kidole mkono wa kulia).

WAKILI WA SERIKALI: ASP Jumanne ulisema wakati wa briefing pale Arumeru kwamba uliambiwa kikundi hiki cha uhalifu kinaratibiwa na Freeman Mbowe?

KIBATALA: Objection! Sijasikia akisema hivyo.

WAKILI WA SERIKALI: Taarifa uliyopewa na Ramadhan Kingai Kwamba kikundi hicho kinaratibiwa na Freeman Mbowe hatua gani zilichukuliwa dhidi yake?

SHAHIDI: Pamoja na kupewa briefing pale ofisni kwangu Arumeru kwamba Freeman Aikael Mbowe ndiye aliyekuwa anaratibu kundi lile, kwamba watu wanaoratibu wana mafunzo ya kijeshi, yaani makomandoo, hatukuwa tayari tumemkamata.

WAKILI WA SERIKALI: Kwa sababu gani?

SHAHIDI: Kwa sababu za kiupelelezi zingine zilizokuwa zinaendelea ili kujiridhisha.

WAKILI WA SERIKALI: Mambo gani mlikuwa mkifuatilia?

SHAHIDI: Mambo ya forensic, yaani uchunguzi wa kisayansi tukiwa tumefanya kuelekea kuwakamata watuhumiwa hawa.

WAKILI WA SERIKALI: Ni wakati gani sasa yeye alikamatwa?

SHAHIDI: Tarehe 21 mwezi Julai mwaka 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulihusika vipi baada ya kukamatwa kwake?

SHAHIDI: Nilitakiwa kuandika maelezo yake ya onyo.

WAKILI WA SERIKALI: Lini?

SHAHIDI: Tarehe 22 Julai 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Ilikuwa saa ngapi?

SHAHIDI: Saa sita usiku.

SHAHIDI: Saa sita na dakika 51.

WAKILI WA SERIKALI: Ulipofika Central ikawaje?

KIBATALA: Objection! Hakuna mahala shahidi amesema alifika Central.

JAJI: Si ndiyo anatoa ushahidi wake sasa? Wewe ulitaka umsikie wapi?

KIBATALA: Ninachosema hiyo ni leading question.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji labda usome swali la mwisho.

JAJI: Nilijaribu kumuhoji saa sita na dakika 51 usiku.

KIBATALA: Wapi sasa kataja Central?

JAJI: Hakuna.

WAKILI WA SERIKALI: Ngoja nibadili swali.

WAKILI WA SERIKALI: Ukifika lini Dar?

SHAHIDI: Tarehe 21 mwezi Julai mwaka 2021.

WAKILI WA SERIKALI: Ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa ofisini Arumeru nilipigiwa simu na DCI Afande Wambura akinitaka nifike Dar es Salaam kituo cha Polisi Kati. Ndipo akaniambia kuna mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe ataletwa mbele yangu niweze kuhojiana naye kuhusiana na shauri tuliokuwa tunapeleleza.

WAKILI WA SERIKALI: Shauri gani?

SHAHIDI: Shauri au tuhuma likiwa na kumbukumbu namba CD /IR/2097/2020.

WAKILI WA SERIKALI: Elezea sasa ni wakati gani Freeman Aikael Mbowe aliletwa mbele yako.

SHAHIDI: Ilipofika saa sita na dakika 51 ndipo Freeman Aikael Mbowe aliletwa mbele yangu na Inspector Machota.

WAKILI WA SERIKALI: Inspector Machota alikukuta eneo gani?

SHAHIDI: Alinikuta katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda ya Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Nini kiliendelea?

SHAHIDI: Nilijitambulisha kwake kwa majina yangu na cheo changu. Nilimueleza kwamba nataka kufanya naye mahojiano.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulimfahamuje sasa kama ni Freeman Aikael Mbowe?

SHAHIDI: Alijambulisha kwamba yeye ni Freeman Aikael Mbowe. Akaeleza particulars zake zote, mahala anapoishi na namba zake za simu.

WAKILI WA SERIKALI: Na wewe ukafanya nini?

SHAHIDI: Nilimuonya na yeye kwamba anatuhumiwa kwa kosa la kula njama za kupanga ugaidi kinyume na sheria namba 24 ya Kupambana na Ugaidi na kwamba halazimishwi kusema lolote kutokana tuhuma hizi isipokuwa kwa hiari yake mwenyewe, na lolote atakalosema litaweza kuletwa kama ushahidi Mahakamani.

SHAHIDI: Vilevile nilimweleza anayo haki ya kuwapo mwanasheria wake, ndugu yake, jamaa yake, au rafiki yake ili aweze kushuhudia wakati maelezo hayo yakiandikwa.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kumfahamisha hilo ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilisaini sehemu yangu na yeye akasaini sehemu yake, na akajibu onyo hilo.

SHAHIDI: Alijibu kwamba ameonywa kwamba anatuhumiwa kwa kosa la kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi kinyume na kifungu cha 24 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Ugaidi. Pia anayo haki ya kuwapo mwanasheria wake, ndugu yake, jamaa yake au rafiki yake ili aweze kushuhudia wakati maelezo yake yake yakiandikwa. Baada ya kujibu onyo hilo alisaini na mimi nikasaini. Hivyo nilimuuliza kama yupo tayari kutoa maelezo yake. Alijibu NDIYO.

SHAHIDI: Nilimuuliza angependa nani awepo wakati maelezo yake yakiandikwa? Akajibu kwamba angependa awepo mwanasheria wake wakati wa kuandika maelezo yake ambaye alimtaja kwa jina la Fredrick Kihwelo.

WAKILI WA SERIKALI: Baada ya kukueleza kwamba angehitaji mwanasheria wake, wewe ulifanya nini?

SHAHIDI: Nilisaini na yeye alisaini baada ya kumweleza. Nikamwita Inspector Machota ili waweze kumpata mwanasheria wake, na ufutailiaji ulifanyika na mwanasheria wake hakuweza kupatikana kwa usiku ule.

WAKILI WA SERIKALI: Ni nyakati gani sasa kama mlifanikiwa kumpata mwanasheria wake?

SHAHIDI: Kesho yake tarehe 22 Julai 2021 majira ya saa saba na dakika 51 mwanasheria wake Fredrick Kihwelo aliweza kufika.

JAJI: Saa saba ya muda gani?

SHAHIDI: Saa saba mchana. Shahidi ndipo alipofika mwanasheria wake.

WAKILI WA SERIKALI: Alifika wapi?

SHAHIDI: Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Dar es Salaam.

WAKILI WA SERIKALI: Wewe ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikwepo Kituo cha Polisi palepale kwa kuwa muda mfupi mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe alikuwa amefika na wakili alikuwa amefika.

WAKILI WA SERIKALI: Freeman Mbowe alikuwa amefika. Kutokea wapi?

SHAHIDI: Sikuweza kujua. Aliletwa tena mbele yangu na Inspector Machota.

SHAHIDI: Baada ya mwanasheria wake kufika nilirudia tena kujitambulisha mbele ya mwanasheria wake, na nikarejea kusoma tuhuma zilizokuwa zinamkabili mtuhumiwa na wakili wake akiwepo, kwamba anatuhumiwa kwa kosa la kula njama za kutenda ugaidi kinyume na kifungu cha 24. Nikamuuliza mtuhumiwa kwamba ataendelea sasa kutoa maelezo yake mbele ya mwanasheria kama alivyokuwa ameomba. Akajibu kuwa hayupo tayari kutoa maelezo yake mbele ya afisa wa Polisi. Baada ya maelezo hayo yeye alisaini. Mimi nilisaini na mwanasheria wake Fredrick Kihwelo alisaini. Tukawa tumeishia hapo.

WAKILI WA SERIKALI: Unasema mwanasheria wa Freeman alifika na ulirudia kusoma tuhuma zinazomkabili?

SHAHIDI: Mwanasheria wake pia alisaini katika maeneo yote kuanzia nilipomuonya, alipojibu onyo, mpaka utayarishaji wa kutoa maelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Leo ukiona hiyo nyaraka hapa Mahakamani unaweza kutambuaje?

SHAHIDI: Uwepo wa jina langu, uwepo wa saini yangu, mwandiko wangu na yote niliyoaandika kuhusiana na majibu ya mtuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kumwonyesha shahidi maelezo hayo.

WAKILI WA SERIKALI: Hebu angalia nyaraka hiyo kama umeitambua na umeitambuaje.

SHAHIDI: Nyaraka hii nimeitambua kwanza kwa mwandiko wangu, uwepo wa majina yangu, sahihi yangu, yale niliyoaandika ikiwemo majina ya mtuhumiwa.

WAKILI WA SERIKALI: Ungependa Mahakama ifanye nini katika hayo uliyoyatambua?

SHAHIDI: Mahakama iyapokee kwa utambuzi kama sehemu ya ushahidi wangu ninaotoa hapa mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Naipeleka nyaraka hiyo upande wa mawakili wa utetezi.

(Mawakili wa utetezi wanaikagua, wanaisoma, wanaipitia na kuigeuza geuza).

NASHON NKUNGU: Kwa upande wetu tunapinga kupokelewa kwa nyaraka hii.

JAJI: Spry faili ni kubwa sana … Nauliza mashitaka najaribu kujiuliza kama upande wa mashitaka kuna mambo mnayotaka kuthibitisha kupitia hii nyaraka.

(Mawakili wa Serikali wanaipekua).

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, kwa mujibu wa Ph mshitakiwa wa nne alikubali Personal Particulars kwamba ni Mwenyekiti wa Chadema na kwamba alikamatwa Ilemela, Mwanza.

JAJI: Kama nimemwelewa shahidi, hii nyaraka ina maoni kwamba hayupo tayari kuhojiwa na afisa Polisi na pia ina particular zake ambazo alizikubali.

JAJI: Kama mnahisi you … Eeeeeeeheeeee!!! You need … Enheeee!

WAKILI WA SERIKALI: Sawa Mheshimiwa. Tunaweza kupata muda tuweze kutafakari hiyo hoja yako na ku- respond.

JAJI: Turudi saa ngapi?

WAKILI WA SERIKALI: Saa nane Mheshimiwa Jaji.

JAJI: basi tunaahirisha mpaka hiyo saa nane.

(Jaji anatoka mahakamani).

Jaji ameingia Mahakamani na ameshakaa kwenye kiti chake. Kesi inatajwa. Ni kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe.

Wakili wa Serikali anasema column yake iko kama ilivyokuwa awali. Wakili Peter Kibatala naye ansema wako kama walivyokuwa mwanzo.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, wakati shahidi wa nane anatoa ushahidi alitoa “caution statement” ya mshitakiwa wa nne. Kwa kuzingatia ushahidi ambao umetolewa tunaondoa maombi yetu ili shahidi wetu aweze kuendelea na ushahidi mwingine.

(Jaji anaandika)

JAJI: Utetezi mna cha kusema?

NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji, kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza nakubaliana na ombi lao.

FREDRICK: Hatuna pingamizi Mheshimiwa Jaji.

JOHN MALLYA: Mheshimiwa hatuna pingamizi.

PETER KIBATALA: Na sisi pia hatuna pingamizi Mheshimiwa.

(Jaji anainama na kuandika na Mahakama ipo kimya).

JAJI: Basi Mahakama imekubali request ya kutenda hivyo, ili shahidi aendelee na ushahidi

WAKILI WA SERIKALI: Umezungumzia huyu Freeman Aikael Mbowe. Hapa mahakamani umemwona?

SHAHIDI: Ndiyo. NImemwona hapa mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Yupo wapi?

SHAHIDI: Huyu aliyevaa tshirt ya mistari mistari meusi jirani na huyo askari.

WAKILI WA SERIKALI: Mwanzoni ulielezea kumpekua Adam Hassan Kasekwa. Yupo wapi hapa Mahakamani?

SHAHIDI: Mtu aliyevaa shati nyeusi wa tatu kutoka alipokaa Freeman Mbowe.

WAKILI WA SERIKALI: Ulisema kwamba mnamo tarehe saba mwezi wa nane 2020 uliandika maelezo ya Mohammed Abdilah Ling’wenya? Kama ukiona karatasi hiyo ya maelezo unaweza kuitambuaje?

SHAHIDI: Niliona naweza kuutambua kwanza kwa mwandiko wangu, majina yangu.

SHAHIDI: Uwepo wa majina ya mtuhumiwa na sahihi yake, pamoja na vitu nilivyoviandika humo ndani.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji naomba kumpatia shahidi karatasi ya maelezo aweze kuitimbua.

WAKILI WA SERIKALI: Angalia nyaraka hiyo kama unaweza kuitambua.

SHAHIDI: Naweza kuitambua kwa kuwa ndiyo imeandika maelezo ya Mohammed Abdilah Ling’wenya.

WAKILI WA SERIKALI: Unaitambuaje?

SHAHIDI: Uwepo wa majina yangu, sahihi yangu, uwepo wa majina ya mtuhumiwa na sahihi yake pamoja na vitu vilivyo humo ndani.

WAKILI WA SERIKALI: Ungependa Mahakama ifanye nini kuhusu nyaraka hii?

SHAHIDI: Naomba ipokee kama sehemu ya ushahidi ninaoutoa hapa Mahakamani.

(Wakili wa Serikali anaichukua nyaraka ile anaipeleka kwa mawakili wa upande wa utetezi. Nao wanainama kuikagua).

(Mawakili wa utetezi wanaigeuza tena. Wanatafuta vitabu vya sheria)

FREDRICK KIWHELO: Kwa niaba ya mshitakiwa wa tatu tunapinga kupokelewa kwa maelezo haya. Naomba nitaje sababu. KWANZA, Mshitakiwa wa tatu hajawahi kuwa katika Kituo cha Polisi Mjini Kati Dar es Salaam kwa tarehe tajwa wakati wa kurekodi maelezo tarehe saba Agosti mwaka 2020 au tarehe nyingine yoyote ile. PILI, mshitakiwa wa tatu aliteswa katika kutia sahihi yake katika maelezo ambayo hajawahi kuandika kwa maelezo yake huko Kituo cha Polisi Mbweni, na hakuruhusiwa kusoma. Mateso yalikuwa kwa vitisho. Vitisho vya kisaikolojia vilovyotolewa na D/C Goodluck Minja ambaye alikuwa amemshikia bastola na ASP Jumanne Malangahe ambaye alimtishia kwamba asipoweka sahihi yake, mateso yatafuatia kama alivyofanyiwa Kituo cha Polisi Mjini Kati Moshi. TATU, maelezo ya mshatakiwa wa tatu yamerekodiwa kinyume na sheria ya masaa manne kinyume na kifungu cha sheria 50(1) a & b cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA ) Sura 20 ya mwaka 2019. NNE, maelezo ya mshitakiwa wa tatu yamechukuliwa kwenye Sheria ambayo haipo ya kifungu cha 57(3) CAP 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018. Mshitakiwa wa tatu hakuonywa kwa mujibu wa taratibu kwa shahidi wa nane kushindwa kunukuu kifungu cha sheria cha 57(3). Ni hayo tu kwa mtuhumiwa wa tatu.

MALLYA: Mheshimiwa nitaongezea kwa ajili ya mshitakiwa wa pili. Asante Mheshimiwa Jaji. Mahakama hii imeshazungumza mara kadhaa kuhusu kupatiwa nyaraka kwenye commital. Kwenye makabrasha inaonekana statement ya Mohammed Abdilah Ling’wenya kwenye ile pre trial bundle Type inaonekana kifungu cha 24 wameomgeza kifungu cha 24 wakaweka kipengele cha pili. Kwenye maelezo halisi ambacho anataka kutuletea wanatudanganya kwa kuwa maelezo halisi hayana eneo lililoandika hivyo. Hivyo wanatudanganya. Kwa maneno sahihi wame- edit kwa maelezo yanayotakiwa leo kutaka kutolewa Mahakamani. Kwa maana hiyo wanatudanganya na wanaidanganya Mahakama yako. Tusingekuwa makini tusingejua kama ni nyaraka Iliyo- editiwa (haririwa). Uongo huu wa wazi ulitaka kuwapa faida. Washitakiwa ni kukataa hii statement isipolelewe kwa maana nyaraka Iliyowekwa Kisutu siyo nyaraka inayotakiwa kwa kesi hii. Wateja wetu wanateseka kwa uongo ambao Jamhuri wameutengeneza.

Pius Hila: (Wakili wa Serikali): Objection Mheshimiwa Jaji. Annatumia maneno makali sana na tuhuma nzito sana.

WAKILI WA SERIKALI: Maneno “UONGO wa Jamhuri” … Nyaraka ina mwandishi na Mahakama inaweza kuangalia. Lakini Mahakama ilisema imuachie aseme “waongo waongo”. Tutaomba Mahakama itake utaratibu mzuri. Na kama unataka kuipotezea sifa nyaraka ipo namna nzuri lakini siyo kututuhumu wote.

JAJI: Mallya?

(Wakili wa Serikali Robert Kidando anaamka kwenye kiti chake).

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando ) Mheshimiwa Jaji pamoja na taratibu ambazo zipo, maombi yanayoletwa na wakili msomi basi yawe ya kisheria. Yani wakili anaomba kwamba hata nyaraka za Committal Proceedings zibatilishwe leo? Jamani kweli leo tubatilishe?

MALLYA: Kwa kuwa hiki kilichopo leo sicho tulichopewa kwenye kitita cha nyaraka kwenye hatua ya commital, na mtu ambaye hasemi ukweli anaitwa mwongo…

JAJI: Namimi najua kweli anaitwa MWONGO, lakini kwa Mahakamani tumia lugha ambayo haitawaudhi. Mbele yako kuna nyaraka moja na wewe una nyaraka tayari. Leo hatufanyi kwenye examination ya committal.

JAJI: Zungumzia kuhusu nyaraka hiyo, na maneno yawe moderate (yasiwe makali).

MALLYA: Mahakamani tunatumia neno ita koleo ni koleo. Pale ambapo panakuwa na utofauti kati ya nyaraka ya committal na ya leo inayoletwa Mahakamani, jambo jema ni kukataa _document kwa sababu content ya nyaraka hiyo inamuingiza kila mmoja wetu. Hii document kwenye commital haikuja. Ndiyo inakuja leo. Lakini ni hoja nyingine ya jambo hilo hilo la hii nyaraka. Kwa mujibu wa kesi ya hii nyaraka, imetaja sheria iliyotumika kuchukua maelezo hayo kwamba ni ya 2018. Lakini kwemye kitika cha nyaraka cha committal nyaraka hii hii inaonekana kwamba imechukuliwa kwenye sheria ya mwaka 2019. Athari gani inapatwa na wateja wetu na mtu huyo huyo mmoja anayetaka sheria hii ipo na sheria hii haipo? Zoezi lililozaa hii nyaraka ni zoezi la kisheria. Nyaraka inapaswa kufuata misingi ya kisheria. Kunukuu sheria ambayo kwa Tanzania haipo ni kutokuzingatiwa kwa sheria. Swali lingine Mahakama itajiuliza kwamba nyaraka hii inai- move mahakama, anachokiomba anaomba order ili Mahakama itamke kwamba ni kielelezo fulani ili Mahakama ifanye hayo inapaswa ifuatwe kwa masharti yake. Ndiyo maana tunapinga nyaraka hii isipolelewe na tunaomba Mahakama yako tukufu itupilie mbali. Ya kwangu ni hayo tu.

KIBATALA: Kwa niaba ya mshitakiwa wa nne tunapinga nyaraka hii kupokelewa kwa sababu hizi. MOJA, maelezo ya onyo hayawezi kupokelewa bila onyo. Onyo linaonekana kupelekwa kwa Mohammed Ling’wenya maarufu kama Doyi chini ya kifungu cha 24. Kifungu cha 24(1) kinahusiana kula njama kutenda matendo ya kigaidi nje ya Tanzania wakati 24(2) inahusiana na kula njama kutenda matendo ya kigaidi ndani ya Tanzania. Kwa kutokutaja vifungu vidogo na kuishia 24 haionyeshi nini hasa onyo lililenga katika mambo hayo. PILI, hakuna sheria inaitwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi. Hiyo HAIPO. Sheria tuliyonayo ni Sheria ya Kuzuia Ugaidi. Hapo hakuna onyo kisheria kwa sababu hizo. Lakini pia Mheshimiwa Jaji, nyaraka hii siyo admissible kwa sababu onyo limetolewa kwa kifungu cha 57 au 58. Kwenye onyo kuna vifungu vya 57 na 58 na siyo 57 au 58 na vifungu hivi vina mtaumizi tofauti. Kesi ya Seko vs Samuel ilisema vifungu hivi vina matumizi tofauti. Kwa namna hiyo kwa niaba ya mshitakiwa wa nne tunapinga kupokelewa kwa maelezo hayo. Ni hayo tu Mheshimiwa.

NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji, kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza napinga vikali kwa nyaraka hii kuingia kama kielelezo kwenye kesi hii. Nyaraka haijafika kwenye viwango vya kukubalika kuitwa maelezo ya ONYO. Nyaraka hii inatakiwa kuchukuliwa kwa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na vifungu vya 57 na 58, na moja ya vigezo ni maelezo ya ONYO yana “kutubu.” Kuna mambo kadhaa yanahitajika. Kifungu cha 57(d) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai chapter 20. Mara tu mtu anayehojiwa anapoanza kutubu/kukubali kosa kuna ONYO lake tofauti, kwamba kutokana ana uzito unaofuatia, ndiyo panapokuwa umuhimu wa kumwita au kwenda kwa Justice of Peace mara tu linapoibuka suala la kukubali makosa au kutubu 57,2(d). Kinasema…… (anasoma sheria).

NASHON NKUNGU: (Anasoma) Kwamba pamoja na kwamba mtu anachukuliwa maelezo, mara tu anapotubu/kukubali kosa mtu huyo anatakiwa kuonywa tena. Kuhusiana na kilichofanyika kwa wateja wetu, moja ambalo linaonekana moja kwa moja ni kitu ambacho linaonekana ukurasa wa pili, naye akakubali kuonyeka kwa kifungu hicho hicho. Hayo ni madhara ya kwanza mteja wetu aliyapata. Katika mashauri mbalimbali ya … (Ananong’onezwa na mawakili wenzake) … Mheshimiwa Jaji kwa hayo tunaomba kielelezo kisipokelewe.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji nimesikia hoja za mapingamizi ambayo ni ya aina mbili. Moja, kwa maana kwamba kuna ambayo yanakijita kwenye kifungu cha 27 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6. PILI, kuna ambayo yanayojikita kwa kutokidhi matakwa ya Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai kwenye vifungu kadhaa kama walivyovirejea. Kiutaratibu Mheshimiwa Jaji aina hiyo ya mapingamizi yalitakiwa kutatuliwa kwa mawakili wa pande zote mbili kuelezea Mahakama na iweze kutoa maamuzi.

WAKILI WA SERIKALI: Na yale chini ya Sheria ya Ushahidi yanatakiwa yawe kwa kesi ndogo Katika kesi ya msingi. Lakini sasa kwa aina ya mapingamizi yaliyotolewa hasa yale ya kutokidhi sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai yanaingiliana na yale mengine ya Sheria ya Ushahidi. Kama utaridhia na wenzetu hawatakuwa na pingamizi, tuanze na kesi ndogo katika kesi ya msingi.

WAKILI WA SERIKALI: Na itakapokamilika ndiyo tufanye yale yanayotokana na Sheria. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

KIBATALA: Tunakubali mwongozo wa wenzetu lakini nitoe maangalizo kwamba mashahidi tutakaoleta hawatahusika na “pure points of law.”

KIBATALA: Na baada ya kesi ndogo ndiyo tuwe na “Pure Points of Law”.

KIBATALA: Je, tutumie njia gani kuyachambua?

WAKILI WA SERIKALI: Pamoja na angalizo la mwenzetu, kuna maneno alikuwa antumia kuwa mteja alikuwa ameathiriwa. Hata kama litatolewa ushahidi naona Mahakama itaona jinsi gani.

(Jaji anaandika).

JAJI: Ni lazima tukayachambua yapi yaangukia kwenye kifungu cha 27 na kisha tufanye ya kisheria. Mnaweza mkapata muda wa kukaa pamoja na kuchambua. Mimi pia nakubaliana tufanye kesi ndogo katika kesi ya msingi bila kutengeneza kesi katika kesi ndogo.

JAJI: Mkutane, tupeane muda. Mnatizama kipi kinaangukia wapi? Na mimi nitakaporudi hapa nitaona niwape dakika ngapi.

(Mallya amekwenda kushauriana na mawakili wa Serikali na kisha akarudi).

MALLYA: Mheshimiwa Jaji tumekubaliana kwa dakika 20.

JAJI: Sawa dakika 20. Basi tutarudi baada ya dakika 20 tuone mmefika wapi.

Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama.

Mahakama imesharejea. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 ambayo ni Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe imeshatajwa.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tupo tayari.

KIBATALA: Nasisi pia tupo tayari.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, tumepitia mapingamizi yale. Tumeona ambayo yanaweza kutuongoza katika _trial within trial (TwT) ni mapingamizi mawili yaliyoletwa na Wakili Fredrick Kihwelo. Pingamizi la kwanza na la pili.

WAKILI WA SERIKALI: Kwamba hakuwahi kuwa Polisi Central Dar es Salaam, hajawahi kuchukuliwa maelezo pale na kwamba mteja wake alilazimishwa kuandika maelezo kwa vitisho vya maneno, na vitisho vya kisaililojia. Mapingamizi mengine yote mengine ni ya kisheria.

WAKILI WA SERIKALI: Ambapo yanaweza kuwa adressed kwa pande zote mbili kuleta hoja za kisheria.

KIBATALA: Ni sahihi Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Mmekubaliana tutaanzana kesi ndogo katika kesi kubwa?

WAKILI WA SERIKALI: Sisi kwa upande wetu tunaomba kujiandaa, na kwa sababu sisi ndiyo tunaanza tunaomba kuanza kesho tarehe 10 Novemba saa tano asubuhi.

JAJI: Upande wa utetezi?

KIBATALA: Ni sawa Mheshimiwa Jaji

JAJI: Basi maombi ya ahirisho yamekubaliwa mpaka kesho tarehe 10 Novemba 2021 saa tano asubuhi.

JAJI: Upande wa mashitaka mnaelekezwa kuleta mashahidi. Washitakiwa wataendelea kuwa chini ya Magereza mpaka kesho asubuhi saa tano shauri litakaposikilizwa.

Jaji ananyanyuka na kuondoka chumba cha mahakama saa 10:19

Like