Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo 10.01.2022
KESI namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: : : Mheshimiwa Jaji Upande wa Jamhuri tupo Kama tulivyo kuwa awali
Jaji baada ya Kukubaliana Pande zote Mbili Tumekubaliana Kuhairisha Shauri hili Mpaka Tarehe 10 January
NDIPO TULIPO ISHIA TAREHE 20 DECEMBER 2021
Nyimbo za Chadema zinaimbwa
Chadema Chadema Chadema, Tanzania Tanzania People’s Power
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 kamili
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: : : Mheshimiwa Jaji naomba kuwatambulisha
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: : Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala.
Naomba kuwatambulisha
Nashon Nkungu
John Malya
Dickson Matata
Seleman Matauka
Sisty Aloyce
Faraji Mangula
Michael Mwangasa
Gaston Garubindi
Maria Mushi
Jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: : : Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo, Tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: : nasi pia tupo tayari Kupokea Uamuzi na Kuendelea
Anainama
Jaji anainama na Kuandika Kidogo
Mahakama ipo kimya.
Jaji: Ni kweli Shauri hili. Lina kuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo
Kama ambavyo Mahakama Ilihairisha Mwaka Jana
Uamuzi huu Unatokana na kupigwa kwa kupokelewa vielelezo ambavyo vilikuwa vimetolewa na ASP Jumanne
Na Kwamba aliomba Kutoa Vielelezo baada ya Kufanya Upekuzi na Kwamba Upekuzi huo Ulifanyika Mbele ya Mwenye Nyumba Mariam Juma na Mjumbe wa Nyumba kumi pamoja na Mke wa Mshtakiwa
[Na Kwamba alijaza Certificate of Seizure Kwa mlolomgo wa mali ambazo alizo kamata kama ambavyo nimeziorodhesha
Na Kwamba Baada ya Kufanya Upekuzi huo alizo weka alama X/ HD
Na baadaa akamkabidhi Mtunza Vielelezo Kituo cha Polisi Kati
Na Kwamba alivichukua na Kwenda Kutunza Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam Tarehe 17 December 2021
Notebook Nyekundu hakutoa Hapa Mahakamani, na Kwamba Baada ya yeye Kupitia na Kugundua haina Uhusiano na Kesi hii alicha Kuitoa hapa Mahakamani
Na alikuwa anavitaja Vielelezo Kwa Kutumia Alama ya X/HD
Alipokuwa anavitoa hapa Mahakamani alipingwa na Mawakili wa Utetezi
Wote Walipinga Vielelezo Vyote vilivyokiwa vinaombwa Kutolewa hapa Mahakamani
Hata hivyo Kila Wakili akisimama na Kutoa Hoja zake
Kwa Maana hiyo Mahakama haitaenda kwa Kila Wakili Bali kwa Hoja Moja moja
Mapingamizi haya yalijikita Maeneo Mawili:
- Chain of Custody
- Competence ya Vielelezo Vyenyewe na Shahidi aliyekuwa anaomba Kutoa Mahakamani
Si Jambo Jipya hapa Mahakamani
Mahakama hii kwa kutumia Experience ya huko Nyuma
Sheria Inaelezea Kwamba Upokelewaji wa Vielelezo Mahakamani Kupitia Sheria Kesi ya SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER, CHARLES GAZILABO AND THE OTHER THREE,
Katika Mashauri yote Mawili Mahakama imeeleza Kwamba Vielelezo Inaweza Kupokelewa Baada ya Vitu Vitatu
Kutumia Criteria ya Competence, Mahakama ili eleza Kuwa test ipo katika Mambo Matatu ya naitwa Authentication
Lazima atambue unique features
Unique features ya Kielelezo hicho
Atambue Chain of Custody
Kwa Maana hiyo Mapingamizi yaliyoletwa yameltwa kwa Jambo Moja la Competence
Mhakama Ita adopt namna ambavyo Mapingamizi yameletwa kwa Chain of Custody na Competence
Ishu ya Chain of Custody imeelezwa na Mawakili Wote wa Utetezi
Nitaamua kwa Kufuata Ishu kama ambavyo zime letwa na Mawakili Wa Utetezi
Maelezo ya jumla yanaeleza Chain of Custody ni nini.? Na Wakili Nashon Nkungu: Alieleza nini Maana ya Chain Of Custody
Mahakama ina kubaliana kwamba ni namna ambavyo kielelezo kilikamatwa na kikitunzwa wapi kam ambapo kilikuwa mahakamani
Kielelezo Ambacho Kilikuwa kimelengwa Kuletwa hapa Mahakamani Kilichezewa na Kwamba hii inaonyesha kwamba Vielelezo Vilikuwa Pamoja ndiyo Maana Notebook Nyekundu Imetolewa
Kwa Upande wa Utetezi walikuja na Hoja Kadhaa
Kwa Mujibu wa Sheria Vielelezo ambavyo vimekamatwa kwamba vielelezo ambavyov imekuwa Commited vinatakiwa kuja vyote Mahakama Kuu
Kwa sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 inataka afisa wa polisi ambaye anataka kutoa kielelezo mahakamani anatakiwa anarudishe kwa amtu aliyepata kwake
Inaonyesha kuwa shahidi Namba nane hakutoa Hoja zake kwanini Kielelezo Hicho Hakikuletwa Mahakamani
Kama hajarudisha inaonyesha kielelezo hicho kimechezewa
Waliendelea kuikimbusha mahakama kwamba PGO 229 Afisa wa Polisi anatakiwa kushika kielelezo hicho mpaka atakapo kitoa mahakamani
Na kwamba wakati anakamatwa aliamini kina husika ndiyo maana alikikamata, hivyo sisSawa kutokutoa hapa mahakamani
Wakili Malya: alisema Kwamba haieleweki Huenda Kwamba Kielelezo hicho Kilikuwa kinamnufaisha Mashitakiwa namba Moja
Kwa hoja wakasema kwamba \wanaomba mahakama ione kwamba kielelezo kimechezewa
Kwa sababu Vielelezo hivi Vingine vilikamatwa na notebook nyekundu basi mahakama ione kuwa vielelezo hivyo vimechezewa.
Kwa Upande wa Mawakili Wa Mashitaka Walisema Kwamba Mawakili Wa Utetezi wametafsiri vibaya
Kwamba upande wa mashitaka awalazimishwi kutoa vielelezo vyote mbele ya mahakama
Shahidi aliona kwamba kielelezo hicho hakihusiki hapa mahakamani
Kwa maelezo hayo waliendelea kusema kielelezo kipokelewe mahakamani kama ambavyo Vilikamatwa
Sasa hapa mahakamani, mahakama ni kweli inaona kwamba kielelezo hicho hakikutolewa hapa mahakamani.
Kutokana na shahidi namba 8 alisema kwamba hakutoa kielelezo hicho hapa mahakamani kwa sababu aliona kwamba haihusiani na kesi hapa mahakamani.
Kwa upande wa utetezi, wanamaoni kuwa vielelezo vyote ambavyo vimekuwa commited vinatakiwa kuja mbele ya Mahakama Kuu na kama siyo basi mchakato wa kurudisha kielelezo hicho ulipaswa uwe umefuatwa.
Kwa namna hiyo, waliomba mahakama ikatae vielelezo vyote.
Ukisoma pande zote mbili, ni wazi kuwa kielelezo hiki kwa kutolewa kwake kimekiuka sheria ukizingatia kuwa kilikuwa tayari imekuwa commited.
Hakuna sheria inayosema kwamba kila kielelezo ambacho kimekuwa commited kinatakiwa lazima kiletwa mahakamani
Kifungu cha 246 CPA na kanuni ya 8 ya mwaka 2016 inasema kuwa vielelezo vyote ambavyo vimekuwa commited kutoka kwenye a Mahakama ya Hakimu Mkazi ni vile ambavyo Mkurugenzi wa mashitaka atataka kuvitumia
Ni wazi atakuwa amepitia kielelezo hicho kuona kama kinatemgeeza kesi au akitengenezi kesi
Siyo lazima kwa ushahidi au shahidi ambao umekuwa commited anatakiwa lazima aje kutoa ushahidi mahakamani
Kama Kifungu cha 110 na 114 cha CPA pamoja na sheria ya ushahidi kifungu cha 1,3 na 4 katika mazingira hayo basi Mahakama Inaona kwamba Pingamizi hili limekosewa
Mahakama inaona pingamizi hili halina msingi na kutupilia mbali.
Kuhusiana na chain of custody imeelezwa kwamba kielelezo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mahakama lazima itazame sana
Endapo mnyororo wa kielelezo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine Inapokuwa umevunjika basi upande wa mashitaka wanakuwa wamekuwa wameshindwa
(c)
Hakuna maelezo yaliyotolewa na shahidi namba 8 kwamba aliwezake kutoa kielelezo hicho kutoka kwa Sargeant Johnson. PGO Hiyo inasema kwamba funguo ya chumba cha vielelezo inatakiwa itajwe ni nani alikuwa anatunza
Kwa kushindwa kueleza hilo wa naona kwamba chain of custody imevunjika
Bwana kidando nayeye alitoa maelezo yake kwamba pingamizi hili limekosa substance kwamba PGO ya 229 4(a) inavyotakiwa
Kidando alieleza namna ambavyo shahidi namba 08 aliviepeleka kwa Sarjent Johnson na kwenda kuchukua tarehe 17 December 2021 na kwamba shahidi ajahojiwa kuona ambavyo ushahidi wake unavyotetereka
Akaendelea kusema kwa kina kuwa shahidi alieleza kwa kina namna ambavyo alitunza kielelezo hicho hapa mahakamani
Akaomba mahakama Itumie sheria kesi ya IGNATUS MKOKA
Kesi namba 245 ya mwaka 2013
Pia akaomba Mahakama Itumie sheria kesi ya KENNEDY SHAYO 84 ya 2017 ukurasa wa 31 na 34
Na akaendelea kusema kwamba Shahidi anaeleza mahakama vile vielelezo ambayo alivi kamata na kuvitunza kwa sarjent Johnson
Upande wa utetezi walisema kwamba utunzaji wa vielelezo katika sheria Imetungwa kulinda vielelezo visichezewe
Na kwamba sheria inasema kwamba polisi anatakiwa kuwa na notebook namna ambavyo alikuwa anaviorodhesha
Na kwamba shahidi hakuonyesha paper trade na vithibitisho vya paper havikuonyeshw akama ambavyo inatakiwa
Wakaomba kutumia kesi ya ILUMINATUS MKOKA pamoja na kesi ya MAYALA MBITI 177 ya 2015.
Kuhusiana na kesi ya KENNEDY SHAYO wakaomba kwamba kesi hiyo I inaunga mkono hoja za utetezi, kwa sababu Bunge liliona kuwa kielelezo ambacho ni nguo kina what za kuchezewa na kwamba mnyororo huo unakuwa umevunjika
Na kuhusiana kupokelewe kwa vielelezo hivyo kuwa vitaathiri washtakiwa au lah
Walisema kuwa bunge kinapotunga sheria na sheria hiyo inapokuwa haifuatwi basi washtakiwa wanakuwa wameathirika
Kwenye suala hili ni seme ni kweli kwamba suala la upokelewaji wa vielelezo limeelezwa
Na suala zima la upokelewaji wa vielelezo Inategemea ambavyo vielelezo vimetunzwa
Na chronological paper trade inaonyesha namna ambavyo kielelezo kilikuwa kimekamatwa mpaka kutunzwa
Suala zima la upokelewaji wa vielelezo na chain of custody limeelezwa na sheria kwa kifungu cha 38 cha CPA, sura ya 322, sheria ya polisi na polisi wasaidizi, PGO ya 229
Suala la kufuatwa kwa mnyororo wa kielelezo kuna vipingili vingi.
Unapokuwa unaangalia kipingili kimoja likiwa kimekatika kimoja basi mnyororo huo unakuwa umekatika
Katika kushughulika na vielelezo hivyo kuwa vipo namba ambavyo vimakatwa mpaka vinagika mahakamani.
Siyo sahihi shahidi mmoja tuh anapotoka ushahidi kueleza kwa niaba ya wengine kuhusiana na mnyororo kuvunjia au kutovunjika
Kwenye kesi ya CHARLES GAZILABO, mahakama ilitoa uamuzi kwamba Mahakama ya Rufani inaamini uthibishwaji wa utunzaji wa mnyororo hauwezi kuthibitishwa na shahidi mmoja, kwamba mahakama Itaweza kuona baada ya ushahidi wote kutolewa.
Katika kesi ya CHRISTINA Vs JAMHURI, ukurasa wa 5 na 7 kufuatia mfano huu Mahakama Ya Rufani inasisitiza kuwa kama hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba mnyororo ulichezewa
Na kwamba kama upande wa Jamhuri hawatoleta mashahidi wengine kuthibitisha mnyororo huo basi mahakama inaweza kusema mnyororo huo haujathibitishw kwenye kesi ya ABASI KONDO Vs JAMHURI kesi 472 ya 2017
Pia Mahakama Ya Rufani imetoa malekezo kwemye kesi ya ANANIA Vs JAMHURI mahakama Iliyoketi Dar es Salaam
Hizo authorities nilizo sema hapo juu ni authorities ambazo zimetolewa na Mahakama Ya Rufani
Kwa maana hiyo mahakama ya chini inapotoa maamuzi lazima izingatie maamuzi hayo ya juu
Katika mazingira hayo basi kwa kutizama shahidi ambaye amekuja kutoa ushahidi hapa mahakamani kwamba vielelezo ambavyo alivikamata hakubaki navyo bali alimkabidhi sarjent Johnson
Kwakuwa bado upande wa jamhuri awajashindwa kumuita sarjent johnson ajaitwa mahakamani kutoa ushahidi at uwezi kusema kuwa shahidi aliyepo mahakamani ameshindwa kutoa mnyororo wa ushahidi
Kuhusiana na mwaliko niliopata kutumia kesi ya MKOKA NA MAYALA MBITI nakubalina na upande wa utetezi kuwa kanuni zilizotumika katika mashauri hayo ni mzuri lakini ikumbukwe maamuzi hayo yalifanyika baada ya ushahidi huo kutolewa
Naona hoja za utetezi zimeletwa kabla ya wakati labda kama ingeletwa wakati wa final submission
Kwa sababu hiyo mahakama hsiwezi kuzingatia na kwa sababu hiyo pingamizi hili nalitupilia mbali
Ikumbukwe pia shahidi aliyopo mahakamani, yeye ndiye aliye fanya search na alizikamata
Hoja za kwamba shahidi amethibitisha kwamba mali ambazo zinatolewa mahakamani ni mali ya JWTZ wakati hakuna mahala aliyothibitisha kuwa vielelezo hivyo ni mali ya JWTZ na pia hakuna mahali ambapo JWTZ walikuja kuthibitisha kuwa ni mali yao
Aliendelea kusema wakili JOHN Malya: kuwa shahidi alishindwa kutaka vizuri hapa mahakamani, ikumbukwe ni vifaa vya kijeshi na vina majina yake ya kijeshi
Akatoa mfano kuwa shahidi amesema kuwa kielelezo ni PONJOL wakati ni sleeping bag
Akaendelea kuomba mahakama kwamba shahidi ameshindwa kuvitambua vielelezo hivyo
Na kwamba vielelezo ambavyo vilikuwa vinatolewa hakuna sleeping bag na akaomba kwa kusema shahidi hana knowledge ya kutosha
Shahidi alisema vielelezo ni mali ya JWTZ na JKT wakati shahidi hajawahi kufanya kazi JKT wala JWTZ
Kwa sababu vielelezo hivyo ni vya jeshi na shahidi hana knowledge basi mahakama isipokee vielelezo hivyo kwa sababu shahidi siyo competent
Kwa upande wa mashitaka walikuja kusema kwamba likuka kutoa ushahidi wa kile ambacho alikikamata
Na kwamba kwa hatua ya sasa siyo sawa kutoa ushahidi wa kitaalamu
Shahidi alieleza kwa kina kuwa aliweka alama hiyo baada ya kuvikamata
Aliomba Mahakama ione kwamba shahidi huyo ameweza kutambua vielelezo hiyo
Mr Malya: hajaonyesha pia kuwa yeye alivitambua je hapa mahakamani
Kwa sasa mahakama inatazama kama vinaweza kupokelewa na siyo kuthibitisha kuwa ni mali ya jeshi au siyo mali ya jeshi
Wakasema kuwa imeelezwa kwenye kesi ya Jamuhuri Vs CHARLES GAZILABO
Kwamba mahakama ishughulike na kuvipokea
Kuhusu alama aliyo weka aliomba kusema kwamba mahakama ione kuwa vielelezo hivyo vilishughulikiwa vizuri
Katika rejoinder walieleza upande wa utetezi ni kwamba kwakuwa shahidi alitaja kwa majina vielelezo hivyo basi alionyesha kuwa anavitambua
Upande wa mashitaka wanasema kwamba swala la utalaam siyo suala la sasa
Maelezo ambayo yameletwa pande zote mbili kuwa kukosekana kwa uelewa kuhusu vielelezo hivyo inatosha kum disqualifie
Katika kesi ya SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER VS DPP I asema kwamba katika ushahidi kuna identification ikifanyika inatosha
Utambuzi kwa kuangalia features pekeee
Utambuzi kwa kuangalia unique futures
Kwa alama ambayo shahidi maeiweka yeye mwenyewe, ambayo nimeweka hapo juu kuwa kielelezo kinaweza kutambuliwa kwa unique features
Lakini features ambayo ni X/HD ilikuwa inatosha
Features ambayo ni mabaka inapatikana katika vielelezo vyote
Nafahamu maelezo ambayo ya inasema kuwa features X /HD siyo features ya kisheria
Mahakama inaona hoja hii itashughulika nayo katika hoja inayofuata
Hoja ya utaalamu tuta shughulika nayo baadae siyo kwa sasa
Hoja ya kidaftari cha five star, kuhusu kikaratasi ambacho kilikuwa ndani yake,
Kuwa hakikufuata mchakato wa sheria juu ya kuongeza kielelezo
Upande wa mashitaka awajafuata utaratibu wa kisheria kutumia kifungu cha 289 cha CPA sura ya 20 juu ya kutaarifu mahakama katika kuingiza kielelezo ambacho halikuwa commited
Vielelezo ambavyo havikuwa commited katika trial court
Kidando wakati anajibu alieleza mahakama kuwa swala zima la commital limeelezwa katika kanuni ya 8(2) ya 2019 GN ya 277
Katika Ukurasa wa 32,33 wa commital proceedings, inaonyesha kuwa ilisha tajwa
Katika hali hiyo waliomba mahakama ipokee kielelezo hicho
Katika hali hiyo waliomba mahakama ipokee kielelezo hicho
Katika Kesi ya RONJINO walisema Kwamba Hai hausiki na urodheshwaji wa vielelezo
Wakaomba mahakama kuwa katika certificate of seizure kuna vingine vimetwajwa
Upande wa utetezi wakasema kuwa kielelezo ambacho kinatajwa hakikupokelewa
Kwa kuangalia kwa ujumla naona kuwa ni kweli
Vielelezo vinavyolengwa kutolewa hapa mahakamani havikutolewa hapa mahakamani haviku orodheshwa wakati wa commital
Kifungu cha 246 linataka kuwa kielelezo au ushahidi wowote unapotakiwa kupokelewa mahakamani unatakiwa uwe umekuwa commited mahakamani
Nikisona Kanuni ya 8 (2) ya mahakama hii inataka mahakama hii kusoma maelezo kwa lugha wanayo ufahamu, kusoma ushahidi wanaoshtakiwa nao, nyaraka za ushahidi unalotarajiwa kutolewa mbele ya mahakama
Kinachotakiwa kufanywa na mahakama husika ni kusoma mashitaka, kusoma ushahidi lakini pia kusoma nyaraka zinzo contain substance ya ushahidi unapotakiwa kusomwa mahakamani
Kinachotakiwa kufanywa ni kungaliwa kama ni kweli kilisomwa.?
Hayo ndiyo masharti ambayo yapo kifungu 289 (1) hakuna shahidi atakaye itwa kama ushahidi wake haukusomwa wakati wa commital, shahidi ataitwa endapo kama ushahidi wake ulisomwa na ushahidi huo ulienda upande wa mashitaka
Katika haki hiyo basi kumbe kinachomatazwa ni shahidi kuitwa bila kutolewa notisi upande wa utetezi, kama kuna nia ya kumuita shahidi huyo na mahakama ita angalia notisi hiyo ni toahelezi au siyo toahelezi
Hakuna takwa la kisheria kuwa kuna takwa la kuleta kielelezo ambacho
Ni physical.
Kwa maelezo hayo naona hakuna sheria ambayo imevunjwa
Na upande wa utetezi waliomba kwamba ili kusudi tukubali au kupokea kielelezo chochote lazima pawe na sheria inayokataza
Kama hakuna sheria wala sheria kesi mahakama hii itakuwa inafanya makosa kukataa kielelezo
Vielelezo vyote ambavyo vinalengwa kutumika hapa mahakamani, hakuna sheria ambayo imevunjwa
Kwa upande wa mashitaka hawalazimishwi kusoma kielelezo ambacho ni physical
Na sheria ambayo zimeorodheshwa hazikatazi
Kwa maana hiyo naitupilia mbali hoja hii
Lakini pia Suala la Mr. Malya: aliomba mahakama kuwa kidaftari ambacho kilikuwa commited siyo kilicho letwa hapa mahakamani
Mahakama imeona kilikuwa commited na kiliorodheshwa na karatasi zimo ambazo zinamichoro michoro
Kwa Hoja hiyo ya Malya: Pia siyo ya Msingi
Mr Malya: ni kama alitaka ku impeachment kumbukumbu za mahakama, na mahakama inaona hoja aliyoleta haina msingi
Katika mazingira hayo basi mahakama hii imeona hoja yake haina msingi
Kuhusiana na kibali cha kufanya seizure of certificate kwamba baada ya kukamata vielelezo hivyo vitakiwa kupelekwa kwa hakimu
Kesi ya NESTORY Vs Maryland Jaji Masabo alisema kuwa pale ambapo kuna hoja ya kutaka kuwa na wasiwasi na kumbukumbu za mahakama ushahidi unatakiwa kuwa wakutosha
Hoja za kupinga za Bwana Kidando PGO 226 (2)c kwamba afisa wa upelelezi alikuwa anahusika na kukamata na kuhifadhi
Kesi ya Mbowe Vs DPP ya 420/2018 Mahakama ya Rufani ilisema kwamba kutokutolewa Kwa Taarifa kwa Hakimu haizuii Ushahidi Kupokelewa
Utetezi Wao walisema kwamba hakuna ushahidi kwamba vielelezo vilienda kuthibitishwa kwa hakimu
Mahakama ione kuwa kutofuatwa kwa utaratibu wa kuvalidate search
Kuhusiana na Kesi ya Mbowe Waliomba mahakama ione kuwa kesi hiyo siyo relevant
Nakubalina na utetezi kuwa search inatakiwa kuwa validated na hakimu kama ambavyo PGO 226 (2)c na kifungu cha 38 (2) kwamba kama hukupata kibali cha search basi unatakiwa kupeleka vielelezo kwa hakimu kwa ajili ya ku validate
Nakubalina na utetezi kuwa kesi ya Mbowe ni distinguishable
Nakubakina kuwa hakimu anatakiwa kutoa kibali cha ku validate search
VUYO Vs DPP ya 334 ya 2016
Lakini ikumbukwe kuwa kesi hiyo ilielekeza kuwa ipo kesi nyingine
Kutokana na maamuzi hayo ya Mahakama ya Rufani kuwa siyo automatic kuwa kielelezo hicho kisipokelewe mahakamani
Bali kitaangaliwa kuwa kielelezo hicho kupokelewa kwake kuna muathiri mshitakiwa
Ndipo inapoweza kuoekana kuwa kutofuatwa kwa kifungu hicho kumeathiri mshitakiwa
Katika mazingira hayo mahakama inaona pia pingamizi hilo halina msingi
Katika hoja nyingine ya vielelezo ambavyo vinalengwa kutolewa mahakamani vinatakiwa kuwa lebeled kwa kufuata sheria na mahakama iliombwa kungalia PGO 229 (10) inaeleza namna ya kuweka alama katika nguo kama lebel ya kielelezo
Na Lebel ya X / HD siyo moja ya lebel ambayo inatajwa katika sheria
Imeelezwa kuwa kilicho fanyika siyo lebeling bali ni kuharibu kielelezo
Kanuni zinasisitiza kuwa alama inayowekwa ni kwa ajili ya kutofautisha
Ikumbukwe kuwa jambo hili limefanyika bila kuwepo kwa mashahidi wakiokwepo
Kukiuka masharti ya PGO hii ni kukiuka sheria hii
Kwenye hoja hii wakili wa serikali alisema kuwa vielelezo ambavyo vinalengwa kutolewa hapa mahakamani, zilikuwa lebeled na kumsaidia shahidi kukumbuka vielelezo hivyo
Na wakaomba kuwa hoja hii haina msingi na mahakama itupilie mbali
Kwamba vielelezo ambavyo vinatolewa hapa mahakamani lebeling ilikuwa sahihi
Katika mazingira hayo mahakama imeelekezwa katika PGO 229 (8) kwamba askari anatakiwa kuweka lebel katika ushahidi unaingia katika mikono yake
Eneo la ku lebel limeelezwa vizuri
Katika PGO hii imelekeza vielelezo ambavyo ni nguo vinatakiwa kuwa lebeled, mahakama imeelezwa kuwa inatakiwa akuwekwa lebel kwa kamba ambayo itapita katika vishikizo na ining’inie
Na exhibit ambayo inatakiwa kulebel inatakiwa kuwa paper pin
PGO 229 (8) I eleza kuwa lebel hiyo inatakiwa kuwa ni minor number, na vingine
Kutokana na malekezo hayo ya kisheria yakiyoelezwa katika PGO hiyo ni wazi kuwa alama iliyiwekwa siyo alama ambayo PGO 229 Imeitambua na kuelekeza
Hata kama alama hiyo ingekuwa imevumiliwa basi kama ingekuwa alama hiyo iliwekwa mbele ya mashahidi hao basi ingevumilia
Katika utaratibu huo mahakama ina maoni kwamba alama hiyo iliyiwekwa imekiuka PGO 229 kwa maana hiyo inaathiri afya ya kielelezo hicho na kuathiri competence
Na nikutafute matakwa ya adminsibility kuwa polisi ofisa alitakiwa kutoa risiti ya ku acknowledge kukamata vielelezo hivyo
Katika hoja hiyo upande wa utetezi wanasema kuwa mtu yoyote ambaye anafanya upekuzi lazima atoe risiti baada ya upekuzi kama ambavyo sheria inalekeza
Wakasema kuwa shahidi namba 08 ajasema kuwa ametoa risiti wala ajatoa nakala yoyote mahakamani kama alitoa risiti
Kwa namna hiyo wakialika kuwa kutokutoa risiti kulikiuka sheria
Bwana Kidando anasema kwa kufanya upekuzi na kukamata mali, shahidi namba 08 alitoa seizure certificate
Upende wa mashitaka wakasema kuwa kwa kutolewa seizure certificate ambayo ina content sawa na risiti wakaomba mahakama wa one kuwa seizure certificate ionekane kama risiti
Nakubaliana na upande wa utetezi kama ambavyo wameieleza mahakama kuwa panapokuwa oamefanyika upekuzi katika nyumba, box au eneo afisa ambaye amekamatwa mali anatakiwa kutoa risiti juu ya mali alizokamata
Wakaomba mahakama izingatie sehemu ya pili katika sehemu A ya CPA, 2 (a) D mahakama ione kuwa kuwepo kwa seizure certificate ni sawa na kutolewa risiti
Nanukuu kifungu cha 38 (3) ya CPA
Kifungu pia cha 22(3)d cha sheria ya uhujumu uchumi inasema pia kuwa ni lazima. kutoa risiti
Kifungu kingine kinachohusika kutolewa na risiti ni kifungu cha 35(3) ya sheria ya polisi na polisi wasaidizi sura ya 322
Lakini pia PGO ya 226 (2,5) na yenyewe inasema kuhusiana na utolewaji wa risiti
Anasoma……. kwa kingereza
Na mwisho guidelines ya mahakama chapter 05 paragraph ya 5 (f) inasema kuwa inatakiwa kutolewa risiti ya mali zilizokuwa zinakamatwa
Hakuna sehemu inayosema kuwa pale mahala ambapo risiti haijatolewa basi seizure certificate itumie kama mbadala wa risiti
Kwa upande wa utetezi walikataa mwaliko huo kwa kuomba mahakama ikatae mwaliko huo kwamba risiti na seizure certificate ni nyaraka mbili tofauti
Katika eneo hilo mahakama inamaoni kuwa suala la risiti mahakama imewekwa wazi na ni muhimu itumike
Mahakama ilipo itwa kuona kuwa risiti itumike mbadala wa certificate of seizure ilisema kuwa
Swala la seizure certificate kutumika badala ya risiti kuna maamuzi ya Mahakama Ya Rufani ya ANDREA AGUSTINO na wenzake ikiwa imeamliwa huko Tanga katika Rufani ya Jinai
Basi ni wazi kuwa a Mahakamani ya Rufani ilisha ona kuwa jambo hili no vitu viwili tofauti na mahakama inaona kuwa kutokutolewa kwa risiti ni mambo mawili tofauti
Baada ya kuwa tumeona kutokutolewa kwa risiti kuna athari, mahakama ya rufani iliyoketi iringa na ilikuwa aime quote with approval katika kesi ya PATRICK JEREMIAH Vs JAMHURI 34 / 2016
Kwa sababu hiyo mahakama hii inaona kuwa kushindwa kutoa kwa risiti ni fatal na jambo hili lina athiri admissibility
Katika hali ya kawaida mahakama ilitakiwa kuishia hapa, lakini kuna mwaliko wa Kibatala kuwa mahakama izingatie kuwa unatafuta nini kila inapokuwa sheria inakiukwa lakini wanapewa nafasi upande wa mashitaka
Nimeona hakuna cha ku reconcile katika maamuzi ambayo nimeshayatoa, maamuzi yote niliyo yatoa ni maamuzi halali hivyo mahakama inaona hoja hiyo halikuwa na mashiko na naitupilia mbali
Mahakama inaona hoja zote zilizo letwa na upande wa utetezi haya kuwa na mashiko isipokuwa mapingamizi mawili ya lebeling na kutokutoa risiti
Na Kwa Mapingamizi haya Mahakama Inaona Yana Merit na Sababu nilizo toa Mahakamani Nakataaa Vielelezo Hivyo NINATOA AMRI!
Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia
Wakili wa Serikali Robert Kidando: : tuna shahidi mmoja namba 08 aliyekuwa anatoa ushahidi wake, tupo tayari kuendelea
Wakili Peter Kibatala: : Na sisi Pia tupo tayari Kuendelea
Shahidi anapanda Upya Kizimbani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: : Shahidi nini kilichofuata baada ya hapo
Shahidi: Shughuli niliyo fanya ilikuwa ni kufuatilia taarifa au michoro ambao ni kuwa nimeona kwenye kidaftari
Wakili Peter Kibatala: :: OBJCECTION shahidi anazungumzia kielelezo ambacho kimekataliww mahakamani, naona wanaongoza kwa mlango wa nyuma
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji mimi sioni kama kuna sheria inakataza juu ya swali hilo
Kibatala: Sija object swali bali majibu ya shahidi, anazungumzia kidaftari ambacho kimeshakatazwa na mahakama
Jaji: Mimi sioni kama kuna tatizo na hilo kama anaongelea jambo ambalo. limekatazwa mahakama itaona mbeleni
Shahidi: nimefuatilia baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yamechorwa na taarifa za a baadhi ya maeneo uhalifu ulikuwa umepangwa
Wakili wa Serikali: Lini na Wapi?
Shahidi: Tarehe 24 August 2020 nilifika eneo moja ambalo lilikuwa kwenye mchoro ambalo lilikuwa limeandikwa sokoni Kilombero.
Kwa Kulifuatilia eneo hilo nililitembelea ni Soko ambalo lipo Mkoani Arusha ambapo Lipo Uhuru Road
Kati kati ya kesi chupa ya soda inandoka na kesi inasimama, jaji anaomba kilicho lia kitafutwe kimtokea wapi
Kina kutwa ni chupa ya fanta chini ya miguu ya mawakili wa serikali
Jaji anaagiza kuwa chup ya soda ni silaha, isiingie tena mahakamani na kuanzia kesho ukaguzi uimarishwe
Shahidi : Tarehe 25 August 2020 anakamatwa Mtuhumiwa mwingine anayeitwa justin kaaya ambaye alikuja kuachiwa baaadae
Jaji: tuendelee
Wakili wa Serikali: Kwanini Justin Kaaya aliachiwa?
Shahidi: Aliachiwa baada ya ushahidi kuonyesha hausiki na tuhuma tuliokuwa tunampeleleza
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine Ulifanya
Shahidi: Upelelezi uliendelea katika kutafuta taarifa za watuhumiwa wengine tuliokuwa tunawataufa
Ambapo Tarehe 10 September 2020 tulimkamata mtuhumiwa mwingine aliyekuwa anaitwa Khalid Ally Athuman ambaye na yeye aliachiliwa baada ya upelelezi kufanyika
Wakili wa Serikali: Kwanini Khalid Ally Athuman alikamatwa
Shahidi: Alikamatwa kama mtuhumiwa ambaye alikuwa analemgwa kushiriki kwemye kikundi, pia aliwahi kuwa ni mwanajeshi wa kikosi cha 92 KJ alimakatwa hapa Dar es Salaam eneo la Kinondoni
Wakili wa Serikali: Baada ya ukamatwaji Khalid Ally Athuman kitu gani kingine ulifanya?
Shahidi Tarehe 19 September 2020 Tulimkamata Gabriel Muhina huko Tabora, aliwahi kuwa Mwanejeshi wa JWTZ katika kikosi Cha KJ 92
Wakili wa Serikali: :Mlimkamata kwa Tuhuma gani
Shahidi: Kwa tuhuma za a kutaka kwenda kushiriki vitendo vya kigaidi vilivyokiwa vinataka kutendwa hapa nchini
Wakili wa Serikali: :Gabriel Muhina sasa hivi Yupo wapi?
Shahidi: Aliwahi Pia kuwa Mwanajeshi wa JWTZ Kikosi cha 92 KJ
Nikiwa Mwanza nilitembelea maeneo ya Mabatini Mwanza na BOT kwa kufatisha mchoro uliokuwa kwenye kidaftari
MALIMA BURONGO Tulimkamata maeneo ya Pasiansi
Wakili wa Serikali: Baada ya hapo kitu gani kiliendelea?
Shahidi: Tarehe 22 July 2021 usiku aliletwa mtuhumiwa namba nne ambaye ni Freeman Aikael Mbowe ili nimhoji
Baada ya kuletwa mbele yangu na yeye kunipatia majina particular zake zote
Ndipo nilimuonya kwa makosa ya kula njama kutenda ugaidi
Chini ya sheria ya kuzia ugaidi
Wakili wa Serikali: Baada ya kumuona..?
Shahidi: Alipomaliza kutaja majina yake, wakili wake fredrick kihwelo hakwepo na hakuwezi kupatikana wakili wake
Hivyo mpaka kesho yake tarehe 22 July 2021 hiyohiyo ndipo alipatikana wakili wake
Siku fanikiwa kumuhoji mtuhumiwa, alisema mpka atakapo fika mahakamani ndipo atakapo toa maelezo yake
Wakili wa Serikali: Umekuwa ukieleza kuhusiana na Khalfani Bwire, hebu onyesha hapa mahakamani yupo sehemu gani
Shahidi: Ni yule aliye vaa tshirt yenye maandishi ya njano
Wakili wa Serikali: Wakati unaandika seizure certificate uliandika HALIFANI BWIRE elezea jina hilo ulilipata wapi
Shahidi: Ni kutokana. na matamshi aliyokuwa anataka mwenyewe
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh kwa sasa katika examination in chief.
Wakili Peter Kibatala: : Mheshimiwa Jaji tunaoemdekeza tupate mapumziko kwa dakika 45 mpaka saa 7 na nusu turudi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi
Walikuwa wametushiriksha
Jaji: Basi tuna break kwa muda wa dakika 45, tutarudi saa saba na nusu
Jaji anatoka
Jaji amerejea saa 8 kamili mchana
Kesi namba 16 ya mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa mahakamani kwa mara nyingine
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji quorum yetu ipo kama awali, tupo tayari kuendelea.
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia quorum yetu ipo vilevile tupo tayari kuendelea.
Wakili NashonNkungu: Shahidi habari!
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Maswali yangu nitataka ujibu kwa sauti.
Shahidi: Ndiyo nitajibu
Wakili Nashon Nkungu: Kwamba ulihusika kukamata washitakiwa wa kwanza, pili na watatu
Shahidi: Sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Hata Mahita alieleza hivyo
Shahidi: Miye sijui Kama Mahita kasema hivyo
Wakili Nashon Nkungu: Na ulikuwa na Mahita
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Mahita anasema mlifika kituoni
Shahidi: Ndiyo kituoni tulifika
Wakili Nashon Nkungu: Mweleze Mheshimiwa Jaji kama ni muhimu kumuandikisha mtuhumiwa kwenye detention register mtuhumiwa anapo fikishwa kituo cha polisi
Shahidi: Kufikishiwa na kupokelewa ni vitu viwili tofauti
Wakili Nashon Nkungu: Unaweza kumfikisha mtuhumiwa na asipokelewe..?
Shahidi: Mtuhumiwa analokelewa Kituo cha Polisi ndiyo anarekodiwa
Wakili Nashon Nkungu: Mweleze Mheshimiwa Jaji kama ni kitu che pesi kwa askari kwa vitu anavyofanya kwa kutumia memory yake
Shahidi: Ni Vyepesi kwakuwa ni moja ya sifa ya askari
Wakili Nashon Nkungu: unafahamu kwamba PGO inasema kinyume kwamba askari ategemewi kutumia kumbukumbu zake
Shahidi: Miye sifahamu, ila nafahamu sifa ya askari ni kumbukumbu
Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo PGO Unaposema kuwa askari asitegemee memory yaje inadanganya
Shahidi: Haidanganyi
Wakili Nashon Nkungu: Mida ya kukamata, kusachi na kuchukua vielelezo ni mida sahihi au makadirio.?
Shahidi: Mida sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo mida yite mliyikuwa mna andika ilikuwa ni muda sahihi na siyo makadirio
Shahidi: Ni mida sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba 12 na 13
Nashon Nkungu Ulielezea kuwa mlifika Rau madukani saa saba kamili mchana
Ni kweli.?
Wakili Nashon Nkungu: Nilisema saa saba
Wakili Nashon Nkungu: Kwa kuwa hatukadirii tuambie ilikuwa Saa Saba na Dakika Ngapi..?
Shahidi: Nilikuwa siangalii Muda kuangalia dakika nakumbuka ni saa saba mchana tuh
Wakili Nashon Nkungu: sasa ulisema mlifika saa saba mchana Rau Madukani mkapaki gari
Shahidi: Ni Kweli
wakili nashon nkungu: na ukasema kingai akamtuma mahita kuangalia kama wale watu bado wapo
Shahidi: Sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Kisha Mahita akarudi?
Shahidi: Sahihi
Nashon Nkungu Sasa kwa kukadiria ulichukua dakika ngapi
Shahidi: Hatufanyi kazi kwa kukadiria
Wakili Nashon Nkungu: Nikisema ulichukua muda wa nusu saa nitakuwa sahihi
Shahidi: Wewe ndiyo umesema ila sisi hatufanyi kazi kwa kukadiria au kungalia muda wa kila kitendo
Wakili Nashon Nkungu: Alipo rudi akasema wale watu wapo?
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Nyinyi Sasa mkatelemka mkaanza kuji panga
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Kwa kukadiria mazoezi yite haya sita yalifanyika kwa muda gani?
Kama utaki kujibu ni ruksa pia unaweza kuiambia mahakama kwamba utaki kujibu
Shahidi: Vyote vili fanyika ndani ya saa moja
Shahidi: Ndiyo tuliwapekua..?
Wakili Nashon Nkungu: Baada ya matukio yote kufanyika, sasa mkawapekua wale watuhumiwa, ni sahihi.?
Shahidi: Ndiyo tuliwapekua..
Wakili Nashon Nkungu: Hapa nimeshika vielelezo P11 na P12 nakuletea karibu uvione na kuvitambua?
Shahidi: Ndiyo nimevitambua
Wakili Nashon Nkungu: Mwambie Mheshimiwa Jaji hii imeandikwa P ngapi
Shahidi: Imeandikwa P 12
Wakili Nashon Nkungu: Na hii Imeandikwa Ngapi Ukitizana?
Shahidi: Nimeona ni Exhibit P 11.
Wakili Nashon Nkungu: Sehemu za muda ambao upekuzi ulifanyika unasomeka saa ngapi..?
Shahidi Saa saba mchana
Wakili Nashon Nkungu: Hapo ndiyo panasomeka hivyo?
Shahidi: Ni 13:00 mchana
Wakili Nashon Nkungu: Sasa 00 si saa saba kamili mchana
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Sasa ni sahihi kwamba upekuzi (search) ikifanyika kabla hamjafika..?
Shahidi: Sasa si tulifika saa saba mchana
Mahakama Kichekoooooo
Wakili Nashon Nkungu: Sawa miye nitaishia hapo
Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kuwa nyie mlitembea na watuhumiwa na mkawarudisha kituoni, ingepata nguvu kama ungetuoa detention register ya moshi
Shahidi: Nguvu ni huu ushahidi ninaotoa hapa
Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi kuwa zaidi ya mara moja mlienda na watuhumiwa Moshi Police Central?
Shahidi: Ni kweli
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu kuwa detention register ni muhimu kama mtu alifika kituoni na kutoka
Shahidi: Ni muhimu kuonyesha kumbukumbu
Wakili Nashon Nkungu: Na pia ni ushahidi.?
Shahidi: Kama utaamua huo ndiyo ushahidi
Wakili Nashon Nkungu: Kutokwepo kwa nyaraka hakuna mtu mwingine kwa hakika ataeleza kuwa watu hawa walifikishwa Moshi
Shahidi: Sasa mimi si nipo hapa ndiyo nina uhakika
Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo nyaraka hizi ni urembo?
Wakili Nashon Nkungu: Ushahidi Wa Nyaraka Muhimu zinazoelezwa na Sheria hujatoa hapa Mahakamani?
Shahidi: Mimi sijaleta nyaraka hiyo
Wakili Nashon Nkungu: Wakati mpo Moshi Watuhumiwa walikuwa wanalala wapi..?
Shahidi: Sijui kama walilala maana yake walikaa kituo cha polisi
Wakili Nashon Nkungu: Kama kweli mlisafiri na kama kweli mlisafiri muda huo, si tungeona kwenye polisi log book?
Wakili Nashon Nkungu: Nyinyi safari yenu mlisafiri kwa gari ya polisi.?
Shahidi: Ndiyo Kwa Gari ya Polisi
Wakili Nashon Nkungu: Je unafahamu kuwa kama mnasafiri kwa gari ya polisi, kila safari kuna watu wanatoa vibali vya nyinyi kusafiri, je unafahamu.?
Shahidi: Ndiyo Nafahamu
Wakili Nashon Nkungu: Mweleze Mheshimiwa Jaji kama ulisema safari yenu ilikuwa authorized na nani
Shahidi: Sikusema
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu kuwa mnapo anza safari CRO officer anatakiwa kurekodi muda na dhumuni la safari kabla mjaanza safari
Shahidi: Inategemea safari inaanzia wapi
Wakili Nashon Nkungu: Unaweza kuwa recorded au siyo lazima?
Shahidi: Inategemea Siyo Lazima
Wakili Nashon Nkungu: Je unafahamu gari ya polisi inapoyoka nje ya mkoa inatakiwa kupata ruhusa ngapi?
Shahidi: Si Kweli
Wakili Nashon Nkungu: Je unafahamu kuwa mnapo pata hitilafu gari hiyo inatakiwa kuripotiqa kwenye kituo cha karibu?
Shahidi: Si kweli
Wakili Nashon Nkungu: Unaifahamu Police Form Fomu EMI?
Shahidi: Hapana siifahamu
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu kuwa gari ya polisi inatakiwa kuwa na motor vehicle logbook
Shahidi: Naifahamu
Wakili Nashon Nkungu: Basi hiyo Fomu EMI ndiyo logbook
Wakili Nashon Nkungu: Je umeitoa logbook hapa mahakamani?
Shahidi: Hapana sijaitoa
Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli kwamba gari zote za polisi zina registration namba
Shahidi: Ndiyo, zina registration namba
Wakili Nashon Nkungu: Na Kweli hapa mahakamani hukutoa registration ya gari yoyote ya polisi mliyotumia
Wakili Nashon Nkungu: Unakumbuka kuwa tarehe 9 mwezi august 2020 mliwapeleka watuhumiwa Mbweni?
Shahidi: Si kweli tarehe 09 august 2020 sikuwapeleka watuhumiwa Mbweni
Wakili Nashon Nkungu: Lakini unakumbuka kuwa uliwapeleka watuhumiwa Mbweni
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Sasa unakumbuka registration namba ya gari mliyotumia kuwapeleka watuhumiwa Mbweni?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili Nashon Nkungu: Lakini wewe ukisema hapa moja ya sifa ya polisi ni kuwa na kumbukumbu
Wakili Nashon Nkungu: Sasa hapa kuna kauli mbili za mashahidi, ni sahihi kwamba mlikuwa kwenye gari ya pamoja wewe na Mahita mkitoka pale Rau madukani?
Shahidi: Ni sahihi
[1/10, 14:42] +255 767 206 226: Wakili Nashon Nkungu: Na Watuhumiwa.?
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Na kwamba mlikuwa mkiwa uliza maswali mbalimbali
Shahidi: Hapana, siyo maswali mbalimbali.
Wakili Nashon Nkungu: Mahita anasema kwenye ushahidi wake kuwa aliwauliza kuhusu mwenzao wa tatu yupo wapi
Shahidi: Ndiyo hilo waliulizwa
Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kwamba ulisema waliibu kuwa hawajui kuwa aliondokaje ondokaje katika lile eneo?
Shahidi: Ni sahihi walijibu hivyo
Wakili Nashon Nkungu: Tuambie nani muongo kati yako wewe na Mahita aliyesema walijibu tumeamwacha pale Rau Madukani na wewe waliokujibu kuwa hatujui
Shahidi: Hakuna mwongo
Wakili Nashon Nkungu: Je shahidi unafahamu kuwa watuhumiwa wanakataa kuwa hakuna sehemu yoyote mliyozunguka nao
Shahidi: Miye nimeeleza ushahidi wangu
Wakili Nashon Nkungu: Na moja sehemu mliyo enda Aishi Hotel?
Shahidi: Ndiyo tulifika
Wakili Nashon Nkungu: Mlijua mnaenda Aishi Hote?l
Shahidi:Ndiyo kwa kuongozwa na watuhumiwa
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Unajua Kuwa Hotel ni Private Premises?
Shahidi: Sisi hatukuingia Ndani ya Hotel, kiongozi wetu alishuka akasogea maeneo yake ila haku ingia ndani
Wakili Nashon Nkungu: Bado upo serious unataka mahakama iamini mlienda Aishi Hotel kumtafuta mtuhumiwa?
Wakili Nashon Nkungu: Hiyo ndiyo sababu pekee iliyoawafanya mvunje sharia?
Shahidi? Hatukuvunja sheria
Wakili Nashon Nkungu: Mliwaandikisha maelezo ndani ya masaa manne
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Anita na Esther maelezo yao yaliandikwa wapi?
Shahidi: Yaliandikwa Moshi
Wakili Nashon Nkungu: Pamoja na kwamba kesi ilifunguliwa Dar es Salaam?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Wakati mnawaandika maelezo mlikuwa mnajua Mbowe na yeye mtuhumiwa
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Na mliwaandika maelezo bila. MBOWE kukamatwa?
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo kutokukamatwa suala la Mbowe Freeman halikukwamisha suala la kuandika maelezo wengine
Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli Mbowe ulimuandika saa 6 na dakika 51
Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo inawezekana kuandika maelezo usiku?
Shahidi: Ndiyo kutoka na upelelezi ulikuwa bado haujakamilika
Wakili Nashon Nkungu: Ni wewe ndiyo ulifanya upekuzi wa maungoni.?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Na ulipofika kiunoni ukahisi ni kitu kigumu?
Kuna maeneo matatu ambayo ndiyo ukaguliwa fingerprints
Shahidi Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kuwa finger inaweza kuonyesha possession ya bastola hiyo?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu kwamba PGO inasema kuwa possession ya bastola inathibitishwa na finger prints?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Je umeleta hapa mahakamani ushahidi wa finger prints kuonyesha possession ya hiyo bastola.?
Shahidi: Hapana siku leta kwasababu halikuwa na sababu
Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kwamba PGO inasema silaha (exhibit) kisiwe loaded?
Shahidi: Inategemea PGO
Wakili Nashon Nkungu: PGO ipi.?
Wakili Nashon Nkungu: Je wewe ulimweleza Sébastien Madembwe kwamba atakiwi. kufanya hiki na hiki?
Shahidi: Mimi sijaongea kuhusu Madembwe na katika ushahidi wangu sija taja Madembwe
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu kwamba madawa yakikamatwa yanatakiwa kupelekwa kituo cha karibu yakabidhiwe kwa officer incharge?
Shahidi: Inategemea
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu kuwa mtu (Mtuhumiwa) anapokiri anatakiwa afikishwe kwa hakimu?
Shahidi: Inatemea na mtu mwenyewe kama anahitaji
Wakili Nashon Nkungu: Je unafahamu huo ukiri wa mtu wa tatu unaongeza nguvu ya ushahidi?
Shahidi: Ndiyo ni hitaji la mtuhumiwa mwenyewe siwezi kulazimisha
Wakili Nashon Nkungu: Wakati wa adamoo anaandika ukiri kwa kushiriki kwake kuweka magogo na ugaidi hukuona haja ya kwenda kwa mlinzi wa amani
Shahidi: Mimi sikuandika maelezo ya Adamoo
Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu Inspector Mahita
Shahidi: ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Na ulisema ulikuwa naye mlipofika kwa Bwire?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli mlieleza kwenye ushahidi wako mlimkamata Bwire na simu mbili za techno na nyingine
Shahidi: Ndiyo
Wakili Nashon Nkungu: Je ulitoa hapa mahakamani simu hizo?
Shahidi: Hapana
Wakili Nashon Nkungu: Je ulisema zipo wapi simu hizo?
Shahidi: Zipo mahala salama
Wakili Nashon Nkungu: Ulizihusisha na Mashitaka haya?
Shahidi: Hapana
Wakili Nashon Nkungu: Nimesikia umrhojiwa Kuhusu HALIFAN BWIRE
Je ulisema hapa Mahakamani kuwa Mtu huyu ndiyo Khalfani Bwire?
Shahidi: Sijasema labda kuna mtu mwingine atakuja
Wakili Nashon Nkungu: Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Wakili John Malya
Malya: unajua Kuwa Mamlaka inayotoa Leseni ya Kufanya Biashara ya Mafuta?
Shahidi Hapana sifahamu
Malya: inaitwa EWURA Leo nitakufahamisha
Malya: Unafahamu kuwa masoko yanasajiliwa?
Shahidi: Hapana sijui
Malya: : Basi Masoko yanasajiliwa na mamlaka za serikali
Malya:Shahidi unajua kuwa wauzaji wa mafuta uliowataja wana leseni za biashara katika halmashauri husika?
Shahidi” Sijui kama wanapewa leseni
Malya: Mimi sasa nakubishi kuwa katika yale makutano jirani na BOT hakuna kituo cha mafuta, sasa ithibitishe mahakama kama kweli kuna kituo cha mafuta Shahidi: Kwenye ushahidi wangu nimesema hakuna
Wakili: Wewe unasajili vituo vya mafuta.?
Shahidi: Hapana
Malya: ulijaribu hata Kununua Mafuta Lita 5
Shahidi: Hapana
Malya: Vipi kama ni road show tu?
Shahidi: Sijui sasa wewe
Malya: Umesema kuwa pale Arusha ulienda kwenye soko je ulimtaja hata kiongozi wa soko?
Shahidi: Hapana
Malya: Hata sanduku la posta la soko?
Shahidi: Sijui
Malya: Shahidi ushawahi kufanya kazi ofisi za DCI?
Shahidi: Ndiyo
Malya: Muda gani.?
Shahidi: Kwa miaka 7 ofisi ya utawala wa upelelezi
Malya: Unakumbuka kesi yoyote ambayo umesha wahi kupeleleza?
Shahidi: Ni nazo nyingi lakini siwezi kutaja hapa
Malya: Vipi Kuhusu Kesi ya Tito Magoti ambayo alikamatwa na ZCO na baadae kunyimwa dhamana na akatoka kwa kulipa pesa baadae, ushiriki wako ukoje
Shahidi: Siwezi kueleza hapa hilo
Malya: Wakati Unatoa ushahidi wako ulisema wewe ni Msukuma?
Shahidi: Ndiyo
Malya: Unafahamu Kuwa Boaz na yeye ni Msukuma?
Shahidi: Miye sijui
Malya: Unafahamu pia kuwa Makonda ni Msukuma?
Shahidi: Miye sijui
Malya: Vipi ushiriki wako katika kumkamata Eric Kabendera.?
Shahidi Si Kweli
Malya: Na wala hukwepo Wakati anachukuliwa maelezo?
Shahidi: Sijafanya sijafanya sijafanya!
Malya: Wakati ukiwa kwa DCI Dar es Salaam ulishiriki ana na Makonda mliwahi kumtuhumu Mbowe kwa akuuza madawa ya kulevya?
Shahidi: Si kweli
Malya: Washitakiwa wanasema hawakukamatwa na bali walitekwa
Shahidi: Sijui
Malya: Mshitakiwa Namba 4 alikuwa na msaidizi wake anaitwa Ben Saa Nane alikamatwa na mamlaka za serikali ukiwa ofisi ya DCI
Shahidi: Miye sijui lolote
Malya: Lakini ulisikia kuwa Ben Saa Nane amepotea..?
Shahidi: Nilisikia kwenye vyombo vya habari
Malya: Ukiwa ofisi ya DCI ulichukua hatua gani baada ya Ben Saa Nane kupotea ukiwa ofisi ya DCI?
Shahidi: Miye siyo jukumu langu,DCI anajua kazi yake
Malya: Mbowe wakati anatekwa Mwanza simu zake walimpeleka wapi?
Shahidi: Mimi sijui nilikutana naye tarehe 22 July 2021
Malya: Alisachiwa nyumbani kwake walikamatwa computer, rooter na nyaraka zingine pamoja na hizo simu mmepeleka wapi hapa mahakamani hakuna?
Shahidi: Wanajua waliovi kamata miye sijui lolote
Malya: Fomu ya kukamatia mali unajaza kitu chochote au kilichoandaliwa Mle?
Shahidi: Kilichoandaliwa Mle
Malya: Zile particular alizojaza ulijaza kabla ya kumpekua au baada ya kumpekua?
Shahidi: Alijaza mwenyewe
Malya: Alijaza baada ya kupiga makofi kidogo au kwa hiari yake?
Shahidi: Kwa hiyari yake
Malya: Wakati una mpekua alijibu anakaa wapi..?
Shahidi: Alijaza Chalinze
Malya: Kwa hiyo ukaamini anakaa Chalinze?
Shahidi: Anapokaa haikuwa muhimu
Malya: Jina lake muhimu?
Shahidi: Ndiyo
Malya: Address yake hukumuuliza?
Shahidi: Sikumuuliza
Malya: Maelezo hayo ya Chalinze ulitoa wapi?
Shahidi: Hata mwenzie alisema hivyo
Malya: Mheshimiwa Jaji atasoma hapo umeandika address ya wapi wala sikupi faida kukutajia
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo P 13
Malya: Kwemye maelezo haya kuna sehemu wamesema kuwa walikutana Morogoro kupanga ugaidi.?
Shahidi: Ndiyo walikutana kupanga ugaidi
Malya: Sawa chukua maelezo haya nionyeshe sehemu palipoandikwa walikaa kikao cha kupanga ugaidi
Shahidi anapekua Maelezo
Shahidi anasoma sasa
Shahidi anasoma na mahakama inacheka tena
Mallya Kuna sheria yoyote inakata kiongozi kuwa na mlinzi.?
Shahidi: Hapana sifahamu
Malya: Kuna sheria yoyote inakataza kuwa mlinzi ambaye ni mwanajeshi mstaafu au aliye acha kazi?
Shahidi: Hapana
Malya: Ukiwa ofisi ya DCI mwezi 9 2017 kiongozi mwenzake alishambuliwa na risasi
Shahidi: Kuhusu kumshambulia Nina taarifa ila kuhusu riport sifahamu
Malya: Na Watu waliomshambulia Tundu Lissu wanamafunzo ya kutumia hizo silaha
Shahidi: Hata wahalifu wanajua kutumia
Malya: Sasa mtu a naona mwenzake alishambuliwa na risasi, anatafuta watu waka kusaidia kukabiliana na uhalifu kam huo, we utaki ajilinde..?
Malya: Shahidi nitafutie kwenye Kielelezo P 13 sehemu ambayo Ling’wenya alikiri Kufanya Ugaidi kwenye Mikoa ya Mwanza na Mbeya
Shahidi anapekua
Shahidi: Kuna sehemu anapo sema nchi nzima, mikoa unayosema ipo kwenye nchi nzima
Malya: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji aandike sehemu inaposomeka kwamba watafanya maandamano nchi nzima ndiyo kupanga ugaidi Mwanza na Mbeya
Shahidi: Ndiyo
Malya: Kwenye hati ya kukamatia bastola sehemu zote umejaza adamoo ila hapa Umejaza Adamo, je ulisha wahi kueleza utofauti huu?
Shahidi: Hapana sijaelezea
Malya: Mheshimiwa Jaji yangu ni Hayo tu!
Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji nitakuwa na maswali machache sababu mengi washaukiza wenzangu
Shahidi nikikurudisha nyuma hapa, Malya: alikuuliza Swali kwamba kuna sheria inayokataza mtu aliye staafu jeshi au kuacha kazi ya jeshi kulinda mtu binafsi ukasema hakuna je nipo sahihi?
Shahidi: Ndiyo upo sahihi
Shahidi Aliitwa na Denis Urio Kuja Kufanya VIP protection
Matata: : Huko Kwingine hakunihusu jibu ni nacho kuuliza tuh
Matata: Kama aliitwa kwa vipi protection, alitumiwa nauli na pesa ya matumizi njiani?
Shahidi: Kama zinamalengo mazuri siyo kosa
Matata: Soma hapo
Shahidi: Baada ya hapo Mheshimiwa Mbowe alisema kuwa atarudi Dar es Salaam, ambapo kuna kazi kubwa ya kuweka magogo
Matata: Sasa kwenye hiyo sehemu uliyosoma kuna sehemu imesema au kutaja hivyo vituo vya mafuta vya kuchoma
Matata: Ukiachana na hapo Uliposema Kuna sehemu amekiri Kuwa ataweka Magogo Mkoa fulani au Barabara fulani
Shahidi: Hakuna sehemu iliyoa andikwa
Matata: Kuna sehemu specific ambapo wamesema kwamba kuna maandamano yatafanyika mkoa fulani na mkoa Fulani?
Shahidi: Hakuna specific ilipo tajwa mkoa
Matata: Kwa uelewa wako kufanya maandamano ni kosa kisheria au siyo kosa?
Shahidi: Inategemea Maandamano yamefanyikaje
Matata: Nilisikia unasema mtu akikiri ni hitajio lake kama ata hitaji kwenda kwa mlinzi wa amani
Shahidi: Ndiyo mpaka yeye atakapo hitaji
Matata: Kwa kifungu kipi cha sharia?
Shahidi: Sikumbuki
Matata: Kwa Sheria Ipi?
Shahidi: Sikumbuki Sheria ipi ila Kwa uzoefu wangu
Matata: ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Kibatala :Nafahamu wewe ni shaidi mzoefu
:Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unafahamu kuwa wanao fuatilia kesi hii wanafuatilia wajibu wa utendaji kazi wa jeshi la polisi?
Shahidi: Miye natimiza majukumu yangu kama shahidi, suala la watu wanasema nini huko, siyo kazi yangu
Kibatala:Unafahamu unatakiwa kuwa na adabu unapokuwa kwenye kizimba cha mahakama na mchakato huu?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Na unafahamu kuwa unapoambiwa uje mahakamani siku fulani lazima uje
Kibatala: Uliambiwa Kwamba Mheshimiwa Jaji Alitoa Amri katika Mahakama ya Wazi Kuwa 14 December 2021 alisema Ukija Tarehe 15 December 2021 kuwa Uje na Uthibitisho
Shahidi: Niliambiwa lakini nilikuwa Njiani
Kibatala: Haya iambie mahakama ulifanya hivyo ulipokuwa mahakamani kutoa uthibitisho kuwa ulikuwa unaumwa
Shahidi: Si Kufanya
Kibatala: Kuna siku yoyote ile ambayo ulinyoosha mkono kumwambia Mheshimiwa Jaji nafahamu kuna amri yako
Shahidi: Sikunyoosha mkono
Kibatala: Kwa hiyo tukuchukuliaje sasa, kwamba umeizoea sana mahakama?
Shahidi: Si kweli kwamba nimeizoea mahakama
Kibatala: Haya tulikuwa na likizo ya mahakama ya wiki mbili je ulishawahi kuandika barua kupitia mawakili wako kuwa unasababu Fulani?
Shahidi: Sikufanya
Kibatala: Umefanya kazi kwa miaka mingapi huko polisi
Shahidi: Miaka 20
Shahidi Miye mwanadamu, uwezi kunipiga kwa kukosea jambo moja
Kibatala: Wakati wa upelelezi ulikuwa ASP sasa hivi umepanda cheo, Je ulipanda cheo lini?
Shahidi: Mwaka jana mwezi sita
Kibatala: Ni sahihi umepandishwa cheo baada ya kufanya hizi shughuli ambazo ziliwapelekea hawa kupelekwa mahakamani?
Shahidi: Ni kweli matokea yalikuwa yameshatokea
Kibatala: na Sasa ni nani?
Shahidi: Ni ACP
Kibatala Kwenye mkoa alikuwa ni nani?
Shahidi: Mpelelezi wa mkoa
Kibatala: Mahita alikuwa nani?
Shahidi: Alikuwa assistant inspector
Kibatala: Nilisikia Mlikuwa Mnafanya kazi na Mahita
Shahidi: Ndiyo
Kibatala Sasa hivi anacheo gani
Shahidi: Inspector
Kibatala: Amepanda cheo au ameshuka cheo?
Shahidi: Amepanda cheo
Kibatala: na Goodluck na yeye alikuwa nani?
Shahidi: Alikuwa Constable
Kibatala: Na yeye ni nani sasa hivi?
Shahidi: Yupo kozi anasoma
Kibatala: Nilisikia unasema kuwa wakati Bwire anakamatwa ulikwepo?
Shahidi: Ndiyo nilikwepo
Kibatala: Kuna mtu yoyote anamawasiliano ya dereva?
Shahidi: Mimi si mchukua mawasiliano
Kibatala: Namba, zake, root yake, namba ya daladala
Shahidi : Hakuna Details
Kibatala: Nilisikia kuna askari ulisema aaliwekwa ku intercept ile daladala, je unataarifa za huyo traffic
Shahidi: Sina
[1/10, 16:31] +255 767 206 226: Kibatala: Je kazi aliyoifanya ilikuwa ya Msingi au Haikuwa Msingi
Shahidi: Alifanya shughuli ya muhimu
Kibatala: Kwa ushahidi wako wewe ukisema kwamba Bwire alipofanyiwa search alikutwa na simu mbili za techno na bundi
Shahidi Ndiyo nilizungumzia ila nikasema kuhusu disposal yake watakuwa kuzungumzia wengine
Kibatala: Wakati Manazichukua Palikuwa na Shahidi Huru Mwingine?
Shahidi: Hapakuwa na shahidi huru yoyote
Kibatala Ulimwambia mheshimiwa jaji kwanini hapaku a na shahidi huru.? Shahidi: Ila kwa Jambo hili hamkuina Umuhimu wa Shahidi Huru
Kibatala Nilisikia ulihusika kukamatwa na Muhina na Khalid, kwa ufahamu wako walikaa ndani wakiwa wamebebeshwa kesi ya ugaidi mpaka nyie mlipoamua muwaachie huru
Shahidi: Sikusema
Mimi sikushughulika na hizo simu
Kibatala Baada ya Upelelezi Kukamilika ndiyo Mkagundua kuwa hawakuwa na Kosa
Shahidi: Mwaka Mmoja
Shahidi: taratibu zinataka wakae ndani mpaka upelelezi unapokamilika
Kibatala: Jeshi La Polisi limepanga kuwafidia nini?
Shahidi: Miye siwezi Kuingolea hilo
Kibatala: Ushawahi kufuatilia juu ya afya zao hasa Muhina ambaye amepata stress disorder ambayo mlimsababishia nyie ukiongozwa na wewe
Shahidi Walikuwa ni wahalifu
Kibatala: Kama wahalifu kwanini mliwaachia
Shahidi: Kwa sababu hapo kuwa na ushahidi wa kutosha
Kibatala: Sasa watu ambao umekosa ushahidi unakwaita wahalifu?
Kibatala Kwanini mahakama isione kwamba wewe ni shahidi ambaye unamaslahi kama unawaita watu ambao hawajakuwa convicted kuwa ni wahalifu tena amewaaachia mwenyewe?
Kibatala: Nilisikia Unasema Kuwa mpango wa kulipua vituo vya mafuta na kupanga magogo barabarani
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Sasa ulisema lolote hapa mahakamani kwamba ulitoa taarifa kwa Ubalozi wa Uingereza waweze kuwakinga watu wao
Shahidi: Sikufanya
Kibatala: Ulitoa taarifa kwa Ubalozi wa Marekani
Shahidi: Sikutoa taarifa popote
Kibatala: Ubalozi wa Kenya?
Shahidi: Sikutoa taarifa
Kibatala: Hili soKo la Kilombero, Je Kuna sehemu yoyote umemwambia Mheshimiwa Jaji kuwa Soko la Kilombero kipo Arusha tuh
Kibatala: Maswala ya Ugaidi ni Global, Je kuna taasisi yoyote mliwataarifu kusaidiana kukabiliana na ugaidi?
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala Nimesikia mara kadhaa sheli, sheli sheli hivi sheli ndiyo nini?
Shahidi: Sheli kwa mtaani ni vituo vya kuuza mafuta
Kibatala: Miye nafahamu ROYAL Dutch Shell ni kampumi ya kuuza mafuta kama Puma au Bp
Shahidi: Miye sijui, nasikia watu wanasema sheli najua ni kituo cha mafuta
Kibatala: Zoezi la wakili wa serikali kuchukua hati ya mashitaka, kuhusu kuandika HALIFANI je uliongozwa kuhusu kulimhanisha majina
Shahidi: Si kuongozwa kuringanisha majina
Kibatala Wakati Ling’wenya anatoka Mtwara akasimama Chalinze na Kumchukua Mshitakiwa Wa Pili Kwenda Morogoro kwenda Kwa Urio Je walikuwa tayari Wana Nia Ovu au hawajui
Shahidi: Miye siwezi kufahamu kama walikuwa wana nia ovu
Kibatala: Wakati wanatoka Morogoro kwenda Moshi walikuwa wa nafahamu kuwa wanaenda kufanya matendo ya Ugaidi Moshi
Shahidi: Walikuwa wanafahamu
Kibatala: Nani aliye wa recruit kati ya mheshimiwa Mbowe au Urio
Shahidi: Aliye wafadhili
Kibatal: Nani aliye watongoza Ling’wenya na Adam pale Morogoro Kwenda kufanya Ugaidi, Ni Urio au Mbowe?
Shahidi Ni Urio
Kibatala: Urio ana umri gani?
Shahidi: Ni mtu mzima
Kibatala: Alitoka Mtu Mwanza akaniomba nimtafitie Watu wa Kumuua Mtu Mwanza Je, Mimi niliyewatafuta watu Kwa ajili ya Kwenda Kuua nitakuwa Nina tenda Kosa la Jinai au siyo
Shahidi: Inategemea
Mheshimiwa Jaji bado Nina Maswali Mengi, Naomba tuhairishe hadi kesho
Kibatala: Basi Kama nilivyokueleza mwanzo watu wangapi a weledi wako wewe na jeshi la polisi
Jaji anaandika Kidogo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hatuna pingamizi na Ombi lililo Wasilisha na Wakili Msomi Kibatala kwa sababu ule muda tuliokubaliana umesha fika
Jaji: kufuatia maombi yaliyoletwa na upande wa utetezi na kukubaliwa na upande wa mashitaka nina ahiirisha shauri hili hadi kesho saa 3 asubuhi
Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi
Shahidi namba 08 ataendelea Kuwa Kizimbani hapo Kesho